Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live

Wezi fedha za TASAF kikaangoni

$
0
0
SERIKALI imetoa siku 30 kukamatwa kwa watumishi waliosababisha matumizi mabaya ya fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) III, kwa kuingiza majina ya watu masikini wasiostahili ili kujipatia fedha za mradi huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akizungumza na baadhi ya wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi, jana alisema ni lazima watumishi wa umma waliohusika katika kuisababishia hasara Serikali wawajibishwe.

Februari mwaka huu, TASAF ilitekeleza maagizo ya Serikali na kufanya uhakiki wa kaya masikini ziliopo kwenye mpango wa kupata fedha na kuziondoa zile zilizokosa sifa na kuziondoa kaya 32,456.

“Katika msako huo tulibaini, waliokufa ni 7,819, viongozi waliojipachika 2,999, waliohama sehemu ambapo mpango haujaanza 3,948, wasiojitokeza au wasiofahamika 9,342 na wasiokuwa na sifa 8, 348,” alisema Simbachawene.

Aidha alisema kuwa, zoezi hilo ni endelevu na kwamba utaratibu wa kutoa taarifa za walengwa waliofariki au kuhama unapaswa kufanyika ili fedha za serikali zisitumike ovyo nje ya malengo yaliyokusudiwa.

Simbachawene alisema, kuingizwa kaya zisizo na sifa katika mpango huo na kuachwa kwa kaya ambazo ni maskini zaidi, kumetokana na baadhi ya watumishi wasio waadilifu ambao pia wamekuwa wakipunguza malipo ya walengwa.

Watu 6.5 milioni, katika kaya maskini na zinazoishi katika mazingira hatarishi wanatarajiwa kunufaika na mradi wa fedha za TASAF katika awamu ya sasa.

Hata hivyo, Simbachawene aliwashauri wakurugenzi wa halmashauri zote nchini pamoja na wakuu wa wilaya, kutoogopa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo kwani suala hilo litaepusha hasara na mianya ya wizi.

Mhandisi Evarist Ndikilo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, alimuahidi waziri Simbacahwene kuwa, hawatofumbia macho ubadhirifu katika halmashauri na kusema watazishauri, kuzikumbusha na hata kuingilia kati pale mambo yanapoenda ndivyo sivyo katika halmashauri.


Navy Kenzo: Ngoma yetu Mpya ina Hadhi ya Kuingia Kwenye Chati za Billboard

$
0
0
Kundi la wasanii wa Bongo Flava la Navy Kenzo linaloundwa na Nahreel na Aika, limesema single yao mpya ni shida!

Wamesema wimbo huo una vigezo vyote vya kuweza hata kuingia kwenye chati za Billboard.

“Tumekuwa tukifanya muziki mzuri na wa tofauti ili tuifikishe Bongo Flava mbali. Sasa kuna nyimbo inakuja watu wakae tayari kwa sababu tumewekeza sana kwenye production na kila kitu,” waliiambia XXL ya Clouds FM.

“Ni ngoma kali Sana kuanzia style na kila kitu. Pia album yetu ‘Above In a Minute’ inakuja na wnyimbo hiyo itakuwepo pia, tunataka tufanye vitu vikubwa ikiwemo kuzifikia chati za Billboard,” waliongeza.

Prof Lipumba:Sihusiki na Vurugu zilizotokea Katika Mkutano wa CUF

$
0
0
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba amesema hausiki na fujo wala vurugu zilizotokea ktk mkutano wa CUF na kuletea kusitishwa kwa mkutano huo.
Akijibu maswali kadhaa ya mwandishi wa Habari wa Azam Tv,Prof.Lipumba anasema ni kweli yeye kama mwenyekiti aliyejiudhuru hakualikwa wala hana vigezo vya kuingia ktk mkutano huo,lkn akiwa nyumbani alipata ujumbe wa simu ya mkononi kuwa anahitajika ukumbini na baadhi ya wanachama wanataka arudi katk nafasi yake.

Baada ya kupata ujumbe huo,Lipumba aliamua kuondoka nyumbani kwake na kwenda ukumbini,ambapo kimsingi kikatiba na kikanuni hakuwa na ruhusa ya kuingia,lkn kwa nafasi yake ktk chama alipaswa kuruhusiwa kuingia japo walinzi walimgomea wakisema haitajiki kwa muda huo,yeye alilazimika kuhakikisha anaingia ili kuweza kukidhi kiu ya wanachama waliomhitaji na wanaoona anafaa kurudia nafasi yake.

Prof Lipumba anasema hakuna mwana-CUF anayeijuwa CUF kama yeye na wala hakuna mwana-CUF toka Tz bara na hata visiwani ukitoa Maalim Seif aliyeweza kuwatetea Wazanzibar kama yeye,akitolea mfano wa kudai haki ya mwaka 2001 na harakati nyingine za kuwasemea na kuwatetea Wazanzibar.Lipumba anasema yeye ndiye kiongozi aliyezunguka Tz bara na visiwani na kufahamiana na viongozi wa ngazi zote na ndio hao wanaomtaka arudi ktk nafasi yake.

Akijibu swali la kuwa "anatumiwa na Watu kuivuruga CUF"...Prof Lipumba anasema hawezi kuihujumu CUF kwa sabbu yeye ndio sehemu ya waasisi wa chama hicho na amekipigania kwa miaka mingi ndani ya jasho na damu,hivyo kuwataka viongozi wa CUF Taifa kutumia hekima na kuacha maamuzi ya wanachama wanaotaka yeye arudi na kuchukuwa nafasi yake na kuendeleza harakati za kuindoa CCM madarakani kuelekea 2020.

Prof anasema bado ana imani kuwa wanachama wanataka yeye arudi na ndio maana hata baada ya kuwa yeye si sehemu ya mkutano kikatiba na kikanuni,bado kuna wanachama walimpigia simu afike ukumbini na kujuwa hatima yake ya kurudia nafasi yake.

Jeshi la Polisi: Mazoezi Yanayoendelea ni ya Kawaida, Hayalengi Kuzuia Shughuli zozote Halali

$
0
0
Taarifa ya Jeshi la Polisi Kwa Vyombo Vya Habari

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na mitazamo tofauti miongoni mwa jamii kufuatia kuonekana kwa askari polisi wakifanya mazoezi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini, linatumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la polisi

Aidha, jeshi la polisi linawataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba – Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP)
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi.

Asasi zinazotetea Ushoga zachunguzwa

$
0
0
SERIKALI inazichunguza asasi za kiraia zenye mwelekeo za kuunga mkono ushoga na ndoa za jinsia moja na zitakazobainika zitachukuliwa hatua kali.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe wakati akizungumza na uongozi wa asasi ya Mtandao wa Jinsia Nchini (TGNP) ofisini kwake Dar es Salaam.

Alizitaka asasi hizo kutokubali shinikizo kutoka kwa nchi zinazowapa misaada zenye nguvu kiuchumi za kutaka nchi zinazoendelea na asasi hizo zikubali ushoga na ndoa hizo za jinsia moja kama sehemu ya haki za binadamu ili kuendelea kupata misaada kutoka kwao.

“Nchi hizo zimekuwa zikitoa shinikizo kwa nchi zetu na hasa asasi nyingi zikizitaka zikubali ushoga na ndoa za jinsia moja, nazichunguza asasi zote za kiraia zenye mwelekeo huo na tukibaini mapungufu hayo tutazichukulia hatua kali za kisheria, uchafu na upuuzi huo wa wazungu, ubaki hukohuko kwao,” alisisitiza.

Waziri Mwakyembe alionya kuwa nchi ikilegeza kamba katika suala hili, “tutashinikizwa baadaye kufunga ndoa na wanyama wa kufungwa kwamba nayo ni sehemu ya haki za binadamu”.

Dk Mwakyembe amezitaka asasi hizo zisiyumbishwe na misaada kutoka nje yenye mwelekeo huo wa kukinzana na mila, desturi, utamaduni, imani za Watanzania, sheria na Katiba ya nchi.

Alisema serikali inaunga mkono juhudi za asasi mbalimbali za kiraia kama vile TGNP za kuelimisha jamii na kutetea haki za watoto, wazee, wanawake, walemavu na makundi mengine maalumu yanayostahili fursa na haki sawa katika jamii, lakini haitazivumilia asasi ambazo zinaenda kinyume na maadili na kukiuka sheria na taratibu ambazo nchi imejiwekea.

“Serikali inaunga mkono kazi zinazofanywa na asasi za kiraia nchini, lakini niweke wazi kuwa hatutazivumilia asasi za kiraia zinazoyumbishwa na misaada kutoka nje na kujihusisha na vitendo ambavyo vinakiuka maadili, taratibu na sheria za nchi ambazo zipo kwa mujibu wa sheria,” alisema.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Amon Mpanju, alisisitiza umuhimu wa asasi za kiraia kuisaidia serikali kwa kupeleka kwenye jamii ujumbe sahihi wenye mafundisho, badala ya kusubiri kukosoa tu na kuzitaka asasi za kiraia kuacha kuunga mkono hoja za ushoga kwa kishawishi cha fedha wanazopewa kutoka kwa wafadhili wao.

Mbunge kizimbani kwa maneno ya uchochezi

$
0
0
MBUNGE wa Jimbo la Tanga kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Mussa Mbarouk amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Tanga kujibu shitaka la kutoa maneno ya uchochezi.

Mbunge huyo alifikishwa mahakamani hapo saa 8.30 alasiri jana akiambatana na jopo la mawakili wake wakiongozwa na Warehema Kibaha.

Mbele ya Kaimu Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga, Hilda Lyatuu Wakili wa Serikali, Saraji Iboru alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Agosti 13, mwaka huu.

Iboru alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kutoa maneno ya uchochezi wakati akiwa katika mtaa wa Madina jijini Tanga majira ya saa 10 jioni alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara.

Wakili Siraji akiwa na mwanasheria mwenzake wa Serikali, Shose Naiman aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa katika mkutano huo, Mbunge huyo alisema Mapango ya Amboni yanatumika kwenda kuwaua vijana.

Mshitakiwa huyo alikana shitaka hilo na mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi leo ili kutoa nafasi kwa upande wa mashtaka na mshitakiwa kukamilisha taratibu za kupata watu watakaokidhi masharti ya dhamana ambayo yamewekwa na mahakama.

Hata hivyo, Mbunge Mbarouk pamoja na mambo mengine leo atatakiwa kuripoti mahakamani hapo akiwa ameambatana na watu wawili ambao ni watumishi wa serikali ambao ndio watakuwa na sifa ya kumdhamini katika shitaka hilo.

Video Mpya: Tekno Ameachia Hii Video Ppya ya ‘PANA’

$
0
0
Good news kwa mashabiki wa mkali wa hit song ya DURO, Tekno kutoka Nigeria ambao wamekua wakiisubiri kwa hamu video ya PANA ambayo audio yake inazidi kufanya vizuri kwenye radio kwa sasa. Nyimbo zake zimezidi kumuweka katika chati na kumuongezea mashabiki wengi Tanzania kutoka Duro, Wash, Where na sasa Pana.

Unaweza kuicheki hapa chini mtu wangu

Maneno ya Orijino Comedy kwa Jeshi la Polisi Kuhusiana na Kuvaa Sare za polisi

$
0
0
Hivi  karibuni kundi la sanaa ya uigizaji la Orijino komedi liliingia matatani baada ya Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam kuwahoji wasanii wanne wa kundi hilo kwa tuhuma za kuvaa sare za polisi kwenye harusi ya msanii Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja ambapo waliachiwa kwa dhamana.

August 22 2016 kupitia taarifa ya habari ya Azam, mmoja ya wachekeshaji hao Isaya Gidion ‘Wakuvanga’ amehojiwa na kusema…
‘mara zote huwa tunawasiliana nao kabla ya kufanya lakini kwa kipindi hiki tulisahau, na kwa kusahau kwetu ndio yakatoa yale lakini hatukuwa na maana mbaya kwamba tunadharau jeshi la polisi’
Video:

Lowassa Apigilia Msumari Oparesheni UKUTA, Asema Haiwezekani Mtu Mmoja Azuie Kila Kitu

$
0
0
Leo nimezunguka katika majimbo ya Mbeya Vijijini ,Vwawa na Tunduma nikiwaeleza kuhusu Operation UKUTA,

UKUTA si fujo , UKUTA si machafuko na hatuna haja ya kufanya fujo , tunapiga kelele dhidi ya uvunjwaji wa haki ya kidemokrasia na katiba ya nchi unaofanywa na utawala huu wa awamu ya tano .

CHADEMA ni nani wakapambane na polisi ,polisi ambao ni watoto wetu ,ndugu zetu na hata wake na waume zetu ila tuwahakikishie hatutorudi nyuma pale katiba na haki ya kidemokrasia ikichezewa au kuwa chini ya mtu fulani .

Najua polisi watapiga watu ,wataumiza watu na hata kuua ila niwahakikishie wao na walio na mamlaka wataishia katika mahakama ya Kimataifa .

Siasa ni mazungumzo ,lazima tuzungumze milango yetu iko wazi kufanya mazungumzo ila kwa kuwa hawahitaji na sisi hatutorudi nyuma September Mosi ,tumejiandaa vya kutosha na sasa tuko ngazi ya kaya na wajumbe wetu wanakamilisha kazi katika kaya ili tarehe mosi sauti ya kutosha ipazwe kwa maandamano na mikutano kama tulivyokubaliana katika kata zetu na majimbo nchi nzima .

Haiwezekani hata kidogo mtu mmoja azuie kila kitu ,nchi hii ni mali yetu sote na inaongozwa na Katiba na sheria.

Kamati kuu ilipoamua katika suala la UKUTA haikukurupuka , kamati kuu yetu inaundwa na mchanganyiko wa wasomi wa kada mbalimbali ,wazee wenye busara na vijana machachari kamwe hawawezi kukukurupuka na UKUTA ni haki ya watanzania wote.

Pili naomba niwape siri ya ushindi 2020 ndugu zangu na wanachama wenzangu , tutashinda uchaguzi Mkuu 2020 kama tutafanya yafuatayo na kuyasimamia
Kwanza; Umoja ndani ya Chama na wanachama ,tuheshimiane ,tusameheane na tuimarishe chama chetu
"chama ndani ya Chama , chama nje ya chama na chama ndani ya Umma "- LOWASSA

Makundi yayumbisha CCM

$
0
0
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jijini Arusha, Medest Meikoki amesema kuyumba kwa chama hicho katika Jiji la Arusha na kusababisha upinzani kuongoza kutokana na makundi yaliyopo ndani ya chama hicho.

Akizungumza mjini hapa jana, Meikoki alisema aliamua kustaafu siasa baada ya kusulubiwa na makundi hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yalikuwa na nguvu katika miaka ya 2000.

Alisema katika jiji hili kulikuwa na makundi mawili ya G7 na G13 ambayo yalikuwa na nguvu katika miaka hiyo.

Kada huyo, alisema bado baadhi ya wana CCM waliojeruhiwa na makundi hayo wana hasira dhidi ya chama chao na kuamua kukaa pembeni na kuacha wenye pesa wafanye watakavyo, lakini waliapa chama hakitachukua jimbo hilo kamwe.

Alisema hatua za ziada zinatakiwa kuchukuliwa na viongozi wa juu wa CCM wa kuwarudisha kundini waliojeruhiwa na makundi hayo bila ya sababu za msingi vinginevyo, upinzani utaendelea kuongoza.

Kada huyo aliendelea kusema kuwa makundi ya kisiasa ya G7 na G13 ndiyo yamekivuruga chama na kuifikisha siasa ya Arusha kuwa taabani kwani waliokuwa wakichaguliwa walikuwa ni viongozi wasiokuwa na sifa za kuongoza chama hicho.

Alisema, kundi la G7 lilikuwa kundi lenye uwezo mkubwa wa kifedha ambapo wafanyabiashara wakubwa wa Arusha, walikuwa katika kundi hilo na walikuwa wakiamua wanavyotaka na ukipingana nao unang’olewa.

Kada huyo alisema, kundi la G13 lilikuwa kundi la wanasiasa wenye kujua siasa za Arusha na nchi kwa ujumla na walikuwa wapambanaji lakini walikuwa ni watu wa kawaida tu wasiokuwa na fedha, lakini wenye mikakati ya kutaka chama kishike hatamu.

Alisema yeye aliwahi kushughulikiwa mwaka 2000 ndani ya chama na kundi la G7 kwani katika kura za maoni za ndani ya chama, alishinda lakini kundi hilo halikuridhika na likaamua kumtoa mwanaCCM na kumsimamisha upande wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) ili kupambana naye kwenye udiwani wa kata ya Darajambili.

Kada huyo alisema kundi hilo lilifanikiwa, kwani TLP ilishinda katika kiti cha udiwani katika kata hiyo na yeye kuanguka vibaya ingawa awali alishinda kwa kishindo katika kura za maoni ndani ya chama

Alisema baada ya kushughulikiwa mwaka 2000 aliamua kujikita katika kushauri badala ya kugombea na alipoamua kuingia tena kwenye siasa mwaka 2005, alishughulikiwa tena na akaamua kustaafu na kubakia kuwa mshauri hadi sasa.

Mwanamuziki Raymond Azawadiwa Gari Jipya na Uongozi Wake

$
0
0
Raymond na Diamond
Uongozi wa WCB umeendelea kumwaga zawadi ya magari kwa wasanii wake na sasa bahati imemuangukia Raymond.

Jana ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa msanii Raymond, uongozi wa WCB ukaamua kumfanyia sherehe msanii wao huyo kwenye ikulu ya Diamond iliyopo huko Madale lakini kubwa zaidi ni zawadi ya gari aliyopewa kwenye sherehe hiyo. Bosi wake, Diamond, ameweka kipande cha video kinachoonesha msanii huyo akikabidhiwa gari hilo aina ya Rav4 yenye rangi nyeusi.

Raymond anakuwa msanii wa pili kutoka WCB kukabidhiwa gari na uongozi huo baada ya mwezi Mei mwaka huu uongozi huo kumkabidhi Harmonize gari aina ya Mark X yenye rangi nyeusi. Rangi nyeusi imeonekana kutawala WCB kwani hata Diamond anamiliki BMW X6 yenye rangi nyeusi pia.

Wamebakia wasanii wawili ndani ya kundi hilo ambao bado hawajakabidhiwa magari swali, je ni nani atakuwa wakwanza kuipata zawadi hiyo kati ya Queen Darlin na Rich Mavoko? Tazama Video Hapa Chini:

Jeshi la Polisi Wamzuia Lowassa Kuingia Rukwa

$
0
0
Edward Lowassa
Msafara wa aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa umekwama kwenda Mikoa ya Rukwa na Katavi  baada ya polisi kuuzuia kwa hofu kwamba unaweza kuingilia ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anayetembelea mikoa hiyo.

Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alianzia ziara yake  mkoani hapa tangu Agosti 21 na juzi alifanya vikao vya ndani katika majimbo yanayoshikiliwa na wabunge wa chama chake  mkoani  Songwe wakati leo asubuhi alitarajiwa kwenda Katavi na Rukwa.

Katika Mikoa ya Rukwa na Katavi alitarajiwa kufanya mikutano ya ndani Majimbo ya  Nkasi Kaskazini na Kusini na Sumbawanga.

Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wanayoiita ‘Kanda ya Nyasa’, Frank Mwaisumbe  alisema  kwamba polisi walimpigia simu Lowassa juzi saa 1.00 jioni akiwa Tunduma  wakimtaka aahirishe ziara yake Mkoa wa Rukwa.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, Gorge Kyando alipoulizwa  kwa njia ya simu alisema waliwashauri viongozi wa Chadema wapange siku nyingine ya ziara kwa sababu  mkoa ulikuwa na ugeni mkubwa.

Kwa habari zaidi nunua gazeti kesho, kwa walio mbali wanaweza kujiunga epaper yetu kwa kubonyeza hapa

Taarifa kutoka ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kuhusu operesheni UKUTA

$
0
0
Ubalozi wa Marekani kwa Tanzania umewatahadharisha raia wa Marekani waishio nchini kuhusiana na Operesheni UKUTA iliyopangwa kufanyika septemba.

Taarifa kutoka ofisi za ubalozi huo zinaeleza kuwa kuna hofu ya maandamano hayo kudumu hata baada ya september mosi hivyo kuwataka raia wake kuwa makini na usalama wao.

Ubalozi umeeleza kuwa raia wa Marekani hawajawai kuwa wahanga wa maandamano yaliyopita ila umewataka raia wake kuwa makini juu ya usalama pamoja na kufuatilia vyombo vya habari vya ndani ili kujua kinachoendelea.

Ubalozi huo umesema ingawa maandamano yamedhamiriwa kuwa ya amani, kuna uwezekano wa kutotokea makabiliano yatakayoweza kusababisha machafuko hivyo kuwataka raia wake kuepuka maeneo yatakayokuwa na maandamano.

**************
Security Message: Nationwide Protests Scheduled for September 1, 2016

The U.S. Embassy in Dar es Salaam alerts U.S. citizens that opposition political leaders have called for a nationwide day of protest currently scheduled for September 1, 2016, but may continue for more than one day.

While U.S. citizens have not been specifically targeted in past demonstrations, we urge you to exercise caution and stay current with media coverage of local events.

Even demonstrations intended to be peaceful can turn confrontational and escalate into violence.  Avoid areas where demonstrations are taking place and exercise caution when in the vicinity of any large gatherings, protests, or demonstrations.

For further information:
See the State Department's travel website for the Worldwide Caution, Travel Warnings, Travel Alerts, and Country Specific Information for Tanzania.
Enroll in the Smart Traveler Enrollment Program (STEP) to receive security messages and make it easier to locate you in an emergency.
Contact the U.S. Embassy in Tanzania, located at 646 Old Bagamoyo Rd, Msasani, Dar es Salaam, at+255-22-229-4000 or e-mail at drsacs@state.gov, and is open Monday-Thursday, 7:30 a.m.-5:00 p.m and Friday 7:30 – 11:30 a.m. For after-hours emergencies, U.S. citizens should call +255-22-229-4000 and ask to speak with the duty officer.
Call 1-888-407-4747 toll-free in the United States and Canada or 1-202-501-4444 from other countries from 8:00 a.m. to 8:00 p.m. Eastern Standard Time, Monday through Friday (except U.S. federal holidays).
Follow us on Twitter and Facebook.

Ruby anamtukana mamba ingali hajauvuka mto?

$
0
0
Hakuna aliyeliona hili la Ruby na Clouds FM/THT kuja mapema kiasi hiki. La kwamba Ruby atakuja kuwashutumu waliomfikisha hapo alipo tena kwa mtindo uliowaacha mdomo wazi wengi – kumuingiza Lady Jaydee kwenye picha.

Hadi wiki mbili zilizopita, Ruby na Clouds walikuwa wakisafiri kwenye boti moja. Kama ilivyokuwa kwa wasanii waliopata ‘usajili’ wa kutumbuiza kwenye tamasha la thamani la Fiesta mwaka huu, Ruby naye alijimwaya mbele ya kadamnasi kuweka sahihi kwenye mkataba. Kushoto kwake B12, kulia kwake Hamza Balla mwakilishi wa Tigo, wadhamini wa tamasha hilo na kila mmoja tabasamu na bashasha zikiwa zimewajaa nyusoni – deal done!

Heee! Yametokea wapi tena ya Ruby kususia show hiyo licha ya kusaini mkataba? Ya kwamba Clouds walitoa ofa kiduchu isiyotosha hata kumwezesha kufanya maandalizi yake binafsi? Mkataba alikuja kuusoma baada ya kuusaini? Makubwaa!

Ruby kageuka mada mtandaoni, maneno yamemtoka akitupa shutuma nzito kwa uongozi wake wa THT kuwa haujali. “To be honest naumia sana sababu they don’t care,” alisema Ruby kwenye mahojiano na Tizneez.

“So if someone hakujali, what can you do? Tatizo ndio kama hilo unakuwa na management ambayo haijali maslahi yako kwenye maisha yako. Tunajikuta tunakuwa na management ambazo zinajali umabavu, zinaendesha wasanii kimabavu kuliko kiakili ya kutimiza malengo ya wasanii wao ambapo sisi wasanii wa kike tunaonewa sana. Unadhani kwanini Lady Jaydee wanamuita komando?” alihoji.

Mimi na wewe hatuna nafasi ya kujua kilichopo nyuma ya pazia. Maneno yawe ya ukweli ama yawe na chumvi kiasi, tunachoweza kunusa baada ya kauli nzito ya Ruby ni yale yanayoweza kujiri baadaye.

Kwa msanii mchanga kama Ruby kuingia kwenye vita na himaya ya Clouds Media ni sawa na panzi na ndege tai kuingia vitani – wajua tu nani ataweka silaha chini. Ruby amemtukana mamba ilhali hajaufikia hata robo mto anaojaribu kuuvuka.

Njia aliyoitumia kufikisha malalamiko yake inaweza kumponza kwa kiwango kisichoelezeka – iwapo hana back up ya kutosha. Ni kwasababu bado hajafika katika hatua ambayo hata kama vituo vya Clouds vikimweka kwenye ‘orodha nyeusi’ ataweza kuhimili kulisukuma gurudumu la muziki wake. Najua utasema ‘ahhh, mbona inawezakana’ – Ndiyo inawezekana, lakini labda uwe Lady Jaydee!

Sina mfano mwingine ninaoweza kuutaja wa mtu aliyewahi kupishana nao hao jamaa na akaendelea kuwika kwenye kila kona ya spika za redio zinazolia mtaani. Ruby ana kipaji, anaimba sana, ana sauti inayoweza kumtoa nyoka pangoni, lakini haina faida sana kuingia vitani na waliompandisha, zaidi tu, itamuumiza.

Na kiukweli, Ruby asingekuwa na walau jina hilo alilonalo sasa kama Clouds FM/TV isingetumia nguvu hiyo iliyotumia kumfanya awe ‘relevant.’ Unakumbuka kuna kipindi sauti ya Ruby ilikuwa inasikika mara kadhaa kila baada ya saa Clouds FM na TV, si tu kwa kucheza wimbo wake, bali jingles za station. Kiukweli mimi hadi ilinikera!

Ilitumika nguvu kubwa kuufanya ‘Na Yule’ uwe hit song hadi redio zingine zikaupokea na kuanza kuucheza pia. Leo hii kwa msanii kama huyu kuja kuongea maneno kama yale, inamfanya awe mkosaji zaidi hata kama akionesha huruma kiasi gani. Ni sawa na mzazi aliyejinyima mengi kumsomesha mwanae kwa tabu ili ampatie elimu itakayomsaidia katika maisha yake.

Ndio, anaweza kuwa amekosewa mno na uongozi wake, lakini kuna namna alitakiwa kuwasilisha nung’uniko lake na kuyamaliza kama ndugu. Kama tu vile ambavyo mzazi akimkosea mwanae!

Muziki wa leo kipaji pekee hakitoshi. Unahitaji nguvu nyingi za nyuma ya pazia na fitina nyingi. Na kwakweli, itamhitaji nguvu nyingi zaidi Ruby kuweza kufika katika daraja la wasanii kama Vanessa Mdee, Shaa na wengine akifanya kazi bila ya nyimbo zake kuchezwa na vituo vya Clouds. Bado hajafika hapo, ana safari ndefu sana.

Bila shaka wanaweza kuyamaliza.

Diamond: Nimenunua nyumba SA, nimechoka kuhangaika hotelini

$
0
0
Baada ya kudai kuwa ana nyumba Afrika Kusini na haoni sababu ya kununua nyumba nchini Marekani , Diamond amefunguka sababu iliyomfanya anunue nyumba nchini humo.

Mapema mwezi April mwaka huu, alipohojiwa kwenye Stori Tatu ya Planet Bongo, inayoruka kupitia EA Radio, Diamond alisema, “Sina sababu ya kusema ninunue nyumba Marekani. Ninunue nyumba Marekani kwa sababu gani? Kwanza sipapendi, uongozi unajua kabisa.”

Akiongea na Times FM, hitmaker huyo wa ‘Kidogo’ amesema kuwa sababu iliyomfanya yeye kununua nyuma Afrika Kusini ni kutokana na kuchoka kuhangaika kwenye hoteli kupanga wakati anapokuwa nchini humo.

“Mimi mwenyewe kwanza nipate urahisi wa makazi nikiwa kule, nimechoka kuhangaika mahotelini,” amesema Diamond. “Lakini familia yangu ipo kule, mwanangu Tiffah na mwingine ambaye anakaribia kuja kwahiyo nawawekea mazingira bora wasije kuona kwamba baba anazalisha tu.”

Mkakati Mzito Serikali na CCM Dhidi ya Ukuta Wavuja

$
0
0
Mbowe na Edward Lowassa
MAMBO hadharani. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya taarifa kutoka ndani ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kubainisha kuwa, wanahaha kuikabili Chadema, anaandika Charles William.

Vyanzo vyetu kutoka serikalini na CCM vinaeleza kuwa, miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na kuwatia hofu wafuasi wa Chadema wanaojipanga kujitokeza kwenye maandamano na mikutano inayoandaliwa kufanyika Septemba Mosi mwaka huu.

Mikutano na maandamano hayo yanafanywa chini ya mwamvuli wa operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta nchini (UKUTA), jambo ambalo linapingwa na Rais John Magufuli pamoja na Jeshi la Polisi.

Tayari utekelezwaji wa mkakati huo umeanza, ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema-Taifa hatohudhuria mikutano na maandamano hayo na atakimbilia nje ya nchi.

“Jambo la mikutano na maandamano lipo kikatiba na kiukweli kuzuia ni kukiuka Katiba, jambo linalofanyika ni kujaribu kuwagawa watu.

“Kibaya zaidi ni kuwa, rais kapiga marufuku jambo ambalo hakupaswa kufanya hivyo. Hapa ndipo ugumu unaonekana maana kuna katiba na kauli ya rais inayotoa maelekezo yanayopingana na Katiba,” kinaeleza chanzo hicho kutoka CCM.

Kwa sasa, taarifa zilizopo kwenye mitandao ya jamii zinamtuhumu Mbowe kutaka kutorokea nje ya nchi ili kukwepa kushiriki maandamano na mikutano ya Ukuta iliyopigwa marufuku na Rais Magufuli na polisi.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, Mbowe amepanga kusafiri nje ya nchi tarehe 28 Agosti mwaka huu ikiwa ni siku tatu kabla ya kufanyika kwa maandamano na mikutano hiyo.

Taarifa hizo zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii, zimeambatanishwa na kile kilichodaiwa kuwa ni tiketi ya safari hiyo zinadai kuwa, Mbowe anapanga kusafiri ili kukimbia vurugu zitakazotokea Septemba Mosi mwaka huu katika maandamano hayo.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa imeeleza kuwa, ujumbe huo hauna ukweli wowote na kwamba, sababu za kusambazwa kwa ujumbe huo ni nia ovu ya wanaopinga maandamano hayo.

“Mheshimiwa Mbowe yupo mstari wa mbele na anaendelea kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha maazimio ya Kamati Kuu juu ya uanzishwaji na utekelezaji wa operesheni ya Ukuta inafanyika kwa ufanisi.

“Mpaka sasa mwenyekiti anaendelea na vikao vya kimkakati ndani ya Kanda ya Kaskazini kama ilivyopangwa,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa, kile kinachoelezwa kama tiketi ya safari ya ndege ya Mbowe, kimetengenezwa kwa kutumia kompyuta na hakina uhalisia na kusisitiza kuwa Mbowe atashiriki kikamilifu.

Mbali na mkakati huo wa kutengeneza propaganda kuwa viongozi wa kitaifa wa Chadema hawatakuwepo nchini katika siku iliyopangwa kwaajili ya mikutano na maandamano hayo, Jeshi la Polisi kote nchini, linaendelea kukamata watu wote wanaovalia fulana zenye neno; ‘UKUTA’.

Jeshi hilo ambalo limesharipotiwa kukamata watu mbalimbali katika mikoa ya Morogoro, Dar es Salaam na Mwanza, limeanza pia mkakati wa kufanyisha mazoezi vikosi vyake na kuwaita wanahabari ili waonyeshe mazoezi hayo kwa lengo la kuwatisha wananchi ambao huenda wakashiriki maandamano hayo.

Vikosi vya kutuliza ghasia (FFU), vimekuwa vikialika wanahabari ili kuonyesha mazoezi yanayodaiwa ni ‘kujiweka tayari kukabili uvunjifu wa amani’, Polisi wanaamini kwa kufanya hivyo, wananchi wengi wataogopa kujitokeza katika maandamano ya UKUTA.

CCM pia, imetumia mbinu ya kuwataka vijana wa chama hicho (UVCCM) kutangaza kufanya maandamano nchi nzima, siku moja kabla ya maandamano ya Chadema ili Polisi watangaze kuzuia maandamano hayo na kutengeneza dhana kuwa polisi hawapendelei chama chochote!
Mbinu hii ilitumika pia mwezi Juni, mwaka huu baada ya Chadema kutangaza kufanya mikutano nchi nzima na kisha, Christopher Ole Sendeka, msemaji wa CCM kutangaza kuwa CCM pia itazunguka nchi nzima kufanya mikutano ya kuikabili Chadema.

Jeshi la Polisi lilitumia mwanya huo kudai kuwa, mikutano ya vyama hivyo (CCM na Chadema) itasababisha vurugu na uvunjifu wa amani na hatimaye kuipiga marufuku lakini lengo hasa likiwa ni kuzuia mikutano ya Chadema.

Chanzo:Mwanahalisi

Mpaka Sasa Chadema Wanaonekana Wameshinda Hata Wasipoandamana-Edo Kumwembe

$
0
0
"Ukitaka kuwazuia watu wasifanye siasa basi waruhusu wafanye siasa....Mpaka sasa Chadema wanaonekana wameshinda hata wasipoandamana kwa sababu hadithi yao ya UKUTA imekuwa maarufu katika media na public na imewapa uhai kama Chama....wangeruhusiwa kuendelea kufanya siasa zao kama zamani leo wasingekuwa katika kurasa za mbele kama hivi.....wametengenezewa ajenda nzuri ambayo hawakuwa nayo....just thinking"Edo Kumwembe

CHADEMA katika dhana ya kumtikisa Rais wa Tanzania

$
0
0
Msingi wa kichwa cha mada yangu ipo kwenye kitabu cha Uongozi Wetu Na Hatima ya Tanzania kilichoandikwa mwaka 1994 na Mwl. Nyerere wakati taifa letu lilikuwa linakabiliwa na changamoto kadhaa za kihistoria ambazo ndizo zilimfanya kuingilia kati na kuandika kijitabu hiki ambacho kilikuwa kama nasaha, onyo, na usia kwa Watanzania.

Mwl. Nyerere alisema, ‘’ huwezi kumtikisa Rais wa nchi bila kuitikisa nchi yenyewe. Ni vizuri jambo hili likatamkwa wazi wazi na likaeleweka sawa sawa’’.

Maneno ya Mwl.Nyerere yanatupeleka kwenye Sura ya Pili ya Katiba ya Tanzania 1977 Ibara ya 33(2) inayosema,‘’Rais atakuwa Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu’’.

Ukubwa na umuhimu wa madaraka ya Rais wa Tanzania umeelezwa kwa kirefu katika sura ya pili kuanzia Ibara ya 33 mpaka 46.

Akiandikia gazeti la “The London Observer” mwaka 1963, mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwa nafasi ya ‘Rais Mtendaji’ nchini, Mwl. Nyerere, aliwahi kukiri kuhusu madaraka makubwa ya Rais Kikatiba akisema: “Katiba yetu inatofautiana na ile ya Amerika kwa sababu inamwezesha Rais kutenda kazi bila kuulizwa ulizwa [wala kuwajibishwa] mara kwa mara...Matakwa yetu si kudhibiti mwendo wa mabadiliko ya kijamii.

“Tunataka kiongeza mwendo (Rais) chenye nguvu kuweza kuvunja umasikini na vizuizi vilivyo ndani ya jamii…kusema kweli, Katiba (hii) inanifanya dikteta kwa kigezo chochote kile cha kidemokrasia,” alisema Mwalimu Nyerere.

Pamoja na kuachana na Katiba ya 1962 na kuandika Katiba ya 1977 ambayo mpaka sasa ina mabadiliko 14 lakini mabadiliko hayo hayajaondoa ukweli kuwa Katiba bado ina msingi unaomfanya Rais wa Tanzania kuwa kiongeza mwendo chenye nguvu kuweza kuvunja umasikini na vizuizi vilivyo ndani ya jamii na pia nguzo kuu ya nchi . Kama ilivyo nguzo kuu ya nyumba, kumtikisa Rais wa Tanzania ni kuitikisa Tanzania.

Mikutano na maandamano ‘’yasiyo na kibali’’ yaliyopangwa na CHADEMA kufanyika nchi nzima ni kama kumtikisa Rais wa Tanzania kwa sababu yatafanyika kinyume cha kauli yake.

Rais Magufuli hawezi kubadilisha kauli yake. Historia ya utendaji wake inaonyesha si mmoja wa viongozi wanaobadilisha badilisha misimammo yao. Sina uhakika zaidi kuhusu CHADEMA kwa sababu historia inaonyesha hawaeleweki kwenye misimamo. Kumbuka dhana ya kubadili gear angani

Swali la kujiuliza, kwa kiwango gani Rais atatikisika siku ya Septemba mosi na mtikisiko huo utaitikisa Tanzania kwa kiwango gani?

Je, mtikisiko huo kama utatokea utajenga precedence gani katika mstakabali wa siasa za Tanzania?

Nini itakuwa hatima ya CHADEMA kisiasa kama wataufyata au kubadilisha gear angani?

Ninaamini wataalam wa Impact Analysis wanaweza kunielewa vizuri.

Nafasi za Kazi Tigo Tanzania, Apply Kabla ya Tarehe 27 Jul 2016

Alichokiandika Raymond wa WCB baada ya Kupewa zawadi ya Gari

$
0
0
Moja ya headline kwenye mitandao ya kijamii iliyochukua nafasi usiku wa August 22 2016 ni pamoja na tukio la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa staa wa bongo flava kutokea katika label ya WCB Raymond ambapo uongozi wake uliamua kumfanyia suprise ya zawadi ya gari aina ya Toyota Rav 4 yenye thamani ya milioni 20 za kitanzania.

Leo August 23 Raymond kupitia ukurasa wake wa instagram aliamua kuyatoa yake ya moyoni kwa kuandika…

’Kweli Nimeamini Mungu Hana upendeleo.nilikua mtu nilie jikatia tamaa ndani ya miaka takribani mi nne nilikua nikiangaika na muziki wangu nakushukuru sana sana‘
‘Kaka Lao Diamond Platnumz Umenifundisha vitu vingi saaaaaanaaa hadi leo naiona njia boss wangu Babu Tale ni mwaka wa tano sasa toka Umenijua umenivumilia kwa mengi hadi leo hii haujanichoka na unanisaidia kwa moyo mmoja’
‘Boss Sallam Sk Asante sana kwakupigania kila siku thamani ya muziki wangu nakuakikisha nafika sehemu nzuri Mkubwa Fella wewe ni zaidi ya mzazi maana umenilea nakunifundisha meeengi kwenye muziki‘
‘Madee Sitoacha kukushukuru kaka lao wewe nikioo naamini unafurahi kuniona mdogo wako hapa nilipo maana unanijua saaaaanaaaa‘
Viewing all 104747 articles
Browse latest View live




Latest Images