Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Maneno ya Sober House Kuhusu Ray C Kupost Instagram…..

0
0
Unaambiwa Ray C sasa ni chuma cha Reli Amerudi katika hali yake ya kawaida kabisa baada ya kukaa Sober House kwa ajili ya tatizo la dawa za kulevya....Ray c kwasasa ameanza kutumia mtandap wake wa Instagram baada ya kuacha muda mrefu,  mmiliki wa kituo hicho Nuru kayaongea haya kuhusiana na post mpya za msanii huyo kwenye mtandao wa instagram na mengineyo
Ray C mpaka sasa hivi anaendelea vizuri na kuhusiana na zile post zake kwenye instagram yeye ndio anahusika kuzipost kwani amerudi katika hali yake ya kawaida na vitu anavyopost ni kuhusiana na hali yake kwahiyo maendeleo yake sio mabaya’

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Agosti 24, Ikiwemo Chadema Watoa Masharti Usitishaji Operationi UKUTA

0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Agosti 24, Ikiwemo Chadema Watoa Masharti Usitishaji Operationi UKUTA

Utajiri wa Nay, Umaskini wa Mr. T-Touch

0
0
IKIWA humfahamu kwa sura mkali wa midundo Bongo, Thabith Mango ‘Mr. T-Touch’ ni lazima utakuwa unafahamu kazi zake hata kwa kuzisikia tu zikichezwa kwenye vituo mbalimbali vya redio au mitaani.

Baadhi ya kazi hizo ni Muziki Gani, Salamu, Akadumba zote alizofanya na Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Too Much ya Darasa, Angejua na Komela za Dyna Nyange, Chafu Pozi wa Bill Nas na Jike Shupa wa Nuh Mziwanda.

Mr. T-Touch alianza kufahamika zaidi kupitia Studio ya Sedactive kwa kutengeneza ngoma kali lakini umaarufu ulikolea zaidi baada ya kupiga kazi nyingi na mkali Nay wa Mitego zilizowafanya kuwa washikaji wakubwa waliotengeneza ‘chemistry’ kali katika Muziki wa Bongo Fleva.



Nay na Mr. T- Touch kwa sasa hawaivi, wamepata ‘ajali ya kisanaa’, katika makala haya T amefunguka mambo mengi kuhusu ugomvi wao:

BMM: Umeanza kufanya kazi na Nay wa Mitego lini?

Mr. T- Touch: Muda mrefu umepita, zaidi ya miaka mitano.

BMM: Nini hasa ilikuwa siri ya ushikaji wenu?

Mr. T-Touch: Nafikiri damu tu ziliendana hasa baada ya kuwa tunatengeneza chemistry nzuri kwenye kazi zetu. Unajua mimi ndiye nimemfanya Nay kufika hapo alipo japo sina kitu, nina mchango wa kama asilimia 80 kwenye mafanikio yake akatae ama akubali!

BMM: Unasema una mchango mkubwa kwenye mafanikio yake, vipi kuhusu mafanikio yako wewe tangu umeanza kufanya naye kazi, amewahi kukulipa?

Mr. T-Touch: Sina mafanikio kabisa zaidi ya kuwa na studio yangu mwenyewe. Mwanzoni nilipokuwa nafanya kazi na Nay tulikuwa tunafanya kazi kishikaji na hajawahi kunilipa hata shilingi 10. Makubaliano yalikuwa kulipana kwenye matamasha na mauzo ya nyimbo, lakini hilo hakuwahi kulitekeleza. Hata hivyo, sikuona shida kwa sababu nilikuwa naangalia fursa, kwamba kupitia kumng’arisha mshikaji ningeweza kufanya naye kazi zingine kama kuandaa matamasha yangu na yeye kunisapoti!

BMM: Umewahi kuandaa tamasha halafu ukaomba sapoti yake lakini hakufanya hivyo?

Mr. T-Touch: Ndiyo, tena juzikati tu hata miezi miwili haijamalizika. Niliandaa tamasha mkoani lililonigharimu kama milioni moja hivi, mshikaji tulikubaliana kwamba atatokea kwenye tamasha hilo lakini mwisho wa siku hakutokea. Nikapata hasara, nilipomuuliza kwa nini alinifanyia hivyo hakuwa na jibu lolote la kunipa!

BMM: Umesema umefungua studio yako mwenyewe iitwayo Touch Sound, studio uliyopewa na Nay kama zawadi (Free Nation) vipi mlipokosana ulirudisha kila kitu kwake?

Mr. T-Touch: Kama nilivyotangulia kusema awali, kila kitu mimi na Nay tulikuwa tunafanya kishikaji, kwa hiyo hata hiyo Studio ya Free Nation japo alijitapa kwenye media kuwa alinipa kama zawadi lakini ukweli ni kwamba ilikuwa ni yake na mimi ni kama nilikuwa namfanyia kazi yeye.

BMM: Lakini chini ya kapeti kwenye sababu za kutengana kwenu kuna mambo mengi yanatajwa, hebu funguka sababu hasa!

Mr. T-Touch: Tumeshindwa kwenda tu sawa kimasilahi, hakuna zaidi, nahitaji mafanikio kwa sasa.

BMM: Umewahi kugombana na Nay kwa ishu yoyote ile huko nyuma?

Mr. T-Touch: Yap, kuna kipindi alitaka kurekodi na mimi sikuwa sawa. Nilipomwambia akadai nimemdharau, tulizinguana kiasi kwamba akaamua kuchukua vifaa vyake vya studio, lakini baadaye tuliweka mambo sawa.

BMM: Kuna chochote unamdai baada ya kuondoka kwenye studio yake?

Mr. T-Touch: Kuhusu studio simdai chochote, lakini namdai pesa kama shilingi milioni moja kwa ishu zingine ambapo siwezi kuziweka wazi hapa.

BMM: Mara ya mwisho kuzungumza naye ni lini?

Mr. T-Touch: Nilipoondoka kwenye studio yake, Julai 30, mwaka huu.

Nay anasemaje?

Kwa upande wa Nay akimzungumzia Mr. Touch amenukuliwa akisema mshikaji huyo kwake ni kama mtoto anayetakiwa kutoka nyumbani na kwenda kujitafutia. Hana ubaya naye na ikitokea kukawepo na sababu ya kufanya kazi hakuna ubaya wowote

Chanzo:GPL

Sirro: Majambazi 14 Wameua Askari Wanne Dar es Salaam

0
0
Watu wanaoaminika kuwa ni majambazi usiku huu wamevamia Benki ya CRDB iliyopo Mbande wilayani Temeke mjini hapa na kuua askari kisha kupora silaha na kutokomea kusikojulikana.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alipoulizwa kuhusu tukio hilo, amesema hawezi kuzungumza chochote kwa maelezo kuwa yuko eneo la tukio na amesema atafutwe kesho.

Uhalifu huo umetokea ikiwa umepita mwaka mmoja tangu kutokea kwa tukio la majambazi kuua askari wanne na kupora silaha baada ya kuvamia kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga jijini hapa.


Alichokiongea Waziri Nchemba Baada yakufika Eneo Walipouwawa Askari Polisi Dar

0
0
Tukio la kuwawa kwa Askari Polisi wanne katika shambulio lililofanywa na watu wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi usiku wa August 23 2016 zimeendelea kuchukua headline ambapo safari hii Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alifika eneo la tukio ambapo pia Ayo TV ilipata nafasi ya kufanya naye mahojiano.

Waziri Nchemba amesema…
’Kumetokea shambulio la uvamizi lenye nia ya uovu ambalo limeua askari wanne, vijana wamefika na wataendelea na msako kuhakikisha waharifu wote wametiwa nguvuni‘
‘Tukio lilitokea majira ya saa moja na nusu usiku ambapo bado uchunguzi unaendelea na taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi, kifupi ni kwamba shambulio lilifanywa kwa kutumia usafiri wa pikipiki na niwakati vijana wakibadilishana lindo lakini niwahakikishie wananchi kuwa watuhumiwa wote watatiwa hatiani‘ –Waziri Mwigulu Nchemba

Ningelikuwa Magufuli Ningeruhusu Chadema Waandamane Kwa Amani Kuepuka Doa Kwa Serikali

0
0
Ningelikuwa Magufuli ningeliwaruhusu ‪#Chadema‬ wafanye maandamano na mikutano yao ambayo yako kisheria kwa mujibu wa katiba na sheria ya vyama vya siasa.

Kisiasa Chadema wameshinda, wana ajenda ambayo ina legitimacy ndani na nje ya nchi. Ajenda ni kuilinda na kuihifadhi Katiba. It is clear and simple to grasp kuwa MagufuliJP has somewhat thrown the law out of the window kwa kukataza mikutano na maandamano ambayo sheria ya vyama vya siasa imetaja kuwa ni halali. Kama Chadema watafanya walivyopania, any crackdown on them ni doa kubwa kwa Serikali ya Magufuli and a looser in the run ni ‪ CCM‬ kwa sababu Magufuli ni Mwenyekiti wa CCM

Ni wakati sasa CCM na Chadema warudi kwenye meza ya mazungumzo ‪Nchi‬ kwanza. Kwa nini CCM na Chadema ? @MagufuliJP ni Mwenyekiti wa CCM na makatazo haya yote yanainufaisha CCM si Serikali ambao kuilinda katiba ni jukumu lao.


Imeandikwa na Thomas David Maqway

UKUTA Waipeleka Serikali Kanisani na Misikitini

0
0
Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) uliotangazwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanyika kwa maandamano na mikutano ya hadhara Septemba Mosi mwaka huu umeipeleka serikali kanisani kuomba msaada.Anaandika Josephat Isango.

Tayari baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya nchini wamekutana na viongozi wa makanisa kuwaomba waambie waumini wao wasitoke kuandamana na kwenye mikutano ya hadhara ya Chadema.

MwanaHALISI online limefanikiwa kuona barua za kutoka wilaya kadhaa kwenda kwa viongozi wa dini ambazo zilielekeza kufanyika vikao katika ofisi za wilaya kati ya tarehe 22- 23 Agosti 2016 ajenda kuu ikiwa ni kuwashauri viongozi wa dini wawatangazie waumini wao kuwa UKUTA ni sawa na uvunjifu wa amani.

Wakuu wa wilaya hao wamewaonya viongozi wa dini kuwa kama wafuasi wao wataandamana itakuwa ni sawa na viongozi wa dini kushiriki maandamano na mikutano ya hadhara.

Waraka wenye kumb Na.ab.214/433/01 “B” 03 ya Agosti 18 mwaka huu, iliyosainiwa na Kaimu Rozalia J Njiani, Katibu Tawala wa Wilaya ya Karagwe ambayo MwanaHALISI online limeiona ni moja kati ya nyaraka nyingi zilizosambwazwa kwa viongozi wa dini nchini

Viongozi wa dini wameonekana kukasirishwa na uamuzi huo wa serikali lakini baadhi yao wamenukuliwa wakitoa msimamo dhidi ya wito huo wa serikali.

MwanaHALISI online limefanikiwa kuona kiongozi mmoja wa dini akimwandikia mwenzake kuwa “Muda wote tumekuwa kiunganishi kwa vyama vyote. sauti ya kinabii ilibaki pale pale inapotakiwa kuwa hata kama Kanisa lilionekana kuegamia upande mmoja, sheria za nchi ni lazima ziheshimiwe na katiba ya nchi iheshimiwe ndio msimamo wa sisi viongozi wa dini, hatutatetereka.”

Haya yanajiri ikiwa ni muda mchache tangu ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kutangaza kuvikutanisha vyama vyote vilivyojiandaa kufanya maandamano vikutane katika meza ya mazungumzo.

Ukuta ulitangazwa kama azimio la Kamati Kuu ya dharura ya Chadema iliyoketi tarehe 23-26 Julai, 2016 kujadili hali ya siasa na uchumi wa Taifa tangu serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani mwezi Novemba, 2015.

Maigizo Yanaendelea..Moshi Napo Jeshi la Polisi Laonyesha Mkwala wa Kudhibiti Maandamano

0
0
Moshi. Mazoezi ya Polisi mkoani Kilimajaro yaliyodumu kwa takriban saa nne yaliyofanywa na vikosi vya askari wa kutuliza ghasia na magari ya washawasha, yametikisa mji wa Moshi na kuzua hofu kwa  wananchi.

Baadhi ya wananchi walishangazwa na kitendo hicho cha polisi  kuzunguka wakiwa na mabomu ya machozi na gari la maji ya washawasha.

Mkazi mmoja, Peter Lyimo alisema ameshtushwa kuona magari ya polisi yakizunguka, huku milio ya milipuko ya mabomu ikisikika.

Naye Mary Kavishe alisema: “Tumezoea kuona polisi wakifanya mazoezi kambini kwao, siyo kuzunguka katikati ya mji.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa  alisema wanafanya mazoezi ya kawaida ya kujihami na wahalifu  na kulinda wananchi na mali zao.

“Ni mazoezi ya kawaida na yanafanyika mkoa mzima kwa ajili ya kuimarisha askari wetu,  ili kujihami na matukio mbalimbali ya kihalifu,” alisema.

Mahojiano na Aliyenusurika Katika Shambulio Lililoua Askari Wanne

0
0
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba anasema tukio limeondoa maisha ya askari wanne na kujeruhi raia wawili.

Majeruhi mmoja anaitwa Ally Chionda ambaye ni mfanyabiashara wa duka la vifaa vya ujenzi karibu na benki ya CRDB ambayo pilisi wamepoteza maisha.

Anadai walikuja majambazi kwenye muda kama wa saa 1:15 usiku wakiwa na pikipiki kama tano na kila pikipiki ilikuwa na watu wawili.

Kulikuwa na watu sita au saba ambao walikuwa wamebeba bunduki.

Walipofika walianza kupiga risasi upande wa eneo la benki na upande wa duka lake.

Bahati mbaya risasi moja ilimpata kwenye mguu wa kushoto ikatokeza na kwenda tena kwenye mguu wa kulia.

Majeruhi anaendelea vizuri na anategemea kufanyiwa x-ray kwa uchunguzi zaidi.
 VIDEO:

Belle 9 atinga kambi ya WCB, afanya mazoezi na Diamond

0
0
Baada ya vocalist, Rich Mavoko kusaini WCB ya Diamond, huwenda msanii wa muziki wa R&B kutoka Morogoro, Belle 9 na yeye akasaini ndani ya label hiyo.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Bugger Movie Selfie’ ameonekana akifanya mazoezi ya bendi ya Diamond katika ofisi za WCB.

Kwa mujibu wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Belle pamoja na Diamond wameonekana wakiimba wimbo ‘Mdogo Mdogo’ kwa pamoja huku wakicheza.

Hatua hiyo imefufua matumaini mapya kwa mashabiki wa kumuziki kuona huweza WCB ikamsaini msanii hiyo kama ilivyofanya kwa Rich Mavoko.

Kwa sasa label ya WCB ina wasanii wanne, Harmonize, Rich Mavoko, Raymond aka Rayvany pamoja Queen Darlin.

6 Job Opportunities at CVPeople Africa

Flaviana Matata Aushtaki Mfuko wa PSPF Mahakamani

0
0
Mwanamitindo wa Tanzania anayefanya kazi zake nchini Marekani, Flaviana Matata ameushitaki mfuko wa pensheni wa PSPF mahakamani akitaka alipwe shilingi milioni 165 kutokana na mfuko kwa kosa la kukiuka mkataba wao kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania.

Flaviana ambaye ni balozi wa mfuko huo wa PSPF kupitia kwa mwanasheria wake Edward Lisso wa Law Associates Advocates wameushitaki mfuko huo kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Aidha inadaiwa kuwa Mwanamitindo huyo ameiomba mahakama iuamuru mfuko huo kumlipa kiasi cha milioni 100 ikiwa ni kama fidia kutokana na kupoteza muda na fedha nyingi ikiwa ni pamoja na kukosa fursa nyingine za kibiashara na makampuni mengine wakati akifanya mawasiliano na mlalamikiwa na ugumu alioupata wakati akifuatilia suala hilo.

Mwanamitindo huyo ameongeza kuwa anakula hasara ya kiuchumi kwa vile picha zake zinaendelea kutumika kinyume na mkataba wake na mfuko huo. Shauri hilo lipo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Magreth Bankika na litatajwa Septemba 22, mwaka huu.

Diamond na Wizkid wakutana, je kuna collabo kati yao?

0
0
Kwa hili linalotokea kwa Diamond kwa sasa ni kama kero kwa baadhi ya watu lakini ni sherehe kwa upande wa mashabiki wake kutokana na kila siku anaibuka na stori mpya na kubwa ambazo zinateka vichwa vya habari.

Baada ya hapo jana stori ya kumpatia zawadi ya gari Raymond kukiki, leo yameibuka mapya na makubwa zaidi baada ya hitmaker huyo wa Kidogo kuonekana akiwa na staa wa Nigeria, Wizkid huku mashabiki wakijiuliza nini kinaendelea?

Vipande viwili vya video alivyopost Diamond kwenye mtandao wake wa Instagram akiwa na staa huyo wa Nigeria vimewashtua mashabiki kutokana na hitmaker huyo wa ‘Shaba’ kwa sasa siyo msanii wa kitoto kwa kuwa muziki wake tayari tayari umepenya nchini Marekani na tayari ameshafanikiwa kufanya collabo na mastaa wa nchi hiyo akiwemo Swizz Beat, Drake na Chris Brown.


Haikuwa ngumu kwa hitmaker wa ‘Kidogo’ kukutana na staa huyo kutokana tayari wameshakutana mara kadhaa ikiwa ni pamoja na kufanya show kwenye jukwaa moja ikiwemo ile ya ‘One Africa’ iliyofanyika nchini Marekani mwezi uliopita pamoja na ile iliyofanyika nchini mwaka jana kwenye viwanja vya Leaders Club.

Hata hivyo inadaiwa kuwa vipande hivyo vya video vinavyowaonyesha wasanii hao walikutana Afrika Kusini na siyo Bongo kama watu wanavyofikiria kwakuwa huenda Wizkid aliondoka Dar August 22.

Mke wa Billionea Msuya Apandishwa Kizimbani Kwa Mauaji ya Dada Yake Msuya

0
0
Mke wa aliyekuwa bilionea wa madini maarufu jijini Arusha, marehemu Erasto Msuya, Miriam Msuya amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. akikabiliwa na mashtaka ya kumuua dada wa bilionea huyo, Aneth Msuya.

Mshtakiwa huyo akikabiliwa na mashtaka ya kumuua dada wa bilionea huyo, alifikishwa mahakamani hapo jana asubuhi akiwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi huku baadhi ya ndugu waliokuwa katika eneo la Mahakama wakilia kwa uchungu mkubwa. Miriam Msuya ambaye alisomewa mashitaka yake na Wakili wa Serikali Diana Lukondo, mbele ya Hakimu Mkazi, Magreth Bankika.

Naye Wakili Diana alidai kuwa, Mei 25, mwaka huu katika eneo la Kibada, Kigamboni, Dar es Salaam, mshitakiwa alimuua Aneth Msuya ambaye ni wifi yake. Wakati huo mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu mashitaka na kurudishwa rumande kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu, na pia kisheria mashitaka yanayomkabili hayana dhamana. Upande wa Jamhuri ulidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Miriam alikamatwa wiki chache zilizopita nyumbani kwake Sakina mkoani Arusha na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kwa ajili ya kusomewa mashitaka yanayomkabili. Wakati bilionea Msuya aliuawa Agosti 7, 2013 kwa kupigwa risasi 22 wakati akiwa karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA), Aneth aliuawa kwa kuchinjwa shingo akiwa nyumbani kwake Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa matukio yaliyokuwa yakiripotiwa Polisi tangu Erasto auawe, ndugu hao wamekuwa wakipatwa na matukio mfululizo likiwemo la dada yake, Antuja Msuya kumwagiwa dawa inayodaiwa kuwa ni sumu akiwa amelala chumbani, na Esther Msuya na mumewe Samuel Charles walinusurika kuuawa kwa kupigwa risasi wakiwa katika baa jijini Dar es Salaam.

Hakimu Bankika aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 6, mwaka huu itakapotajwa tena.

Mr Blue: Barakah na Naj Walitaka Kunivunjia Ndoa Yangu

0
0
Mr Blue amekiri kuwa skendo yake kuwa amekuwa akiwasiliana na ex wake, Naj ambaye kwa sasa ana uhusiano na Barakah Da Prince ilitaka kuivunja ndoa yake.

Akiongea na Clouds FM, rapper huyo wa ‘Mboga Saba’ amedai kuwa mke wake, Wahyda sasa amekuwa na wivu wa kufa mtu tangu kuzuke skendo hiyo.

“Sasa hivi naona kama wivu umezidi baada ya hii skendo ya hawa jamaa kuitengenezea kiki kwasababu wanataka kutoa nyimbo yao, skendo kwamba mimi nilimpigia yule mwanamke mwingine nani anaitwa, Najma yule. Wametengeneza kweli kabisa, mimi nimezipata za kunyapianyapia kwamba wametengeneza ili kukikisha nyimbo zao,” amesema Blue.
“Lakini wamenikosea sana kwasababu wanataka kugombanisha ndoa yangu, mimi nina mke ujue, siwezi kumpigia mtu ambaye nimemwacha, ni kosa kubwa sana, halafu mke wangu yule ni mwanamke ambaye walikuwa watatu kupigania nani awe na mimi, yaani bora hata ningempigia mtu mwingine,” amesisitiza.

“Ilifika karibu kama siku mbili tuna ugomvi mimi na mke wangu, ni kitu kikubwa sana, nimekasirika sana, nimechukia sana na nawaambia mashabiki wangu, alichokifanya Barakah na watu wake, kama sio yeye simlaumu, kama watu wake nilikuwa naomba waoneshe proof kwenye mitandao waoneshe namba yangu niliyompigia, waioneshe kwamba ni hiyo kweli sio unaongeaongea tu.”

Godbless Lema Afunguka Kuhusu Askari Waliouwawa Dar na Majambazi, Adai ni Ishara Mbaya

0
0
Kwanza ninawapa pole familia za Polisi wote waliouwawa waliokuwa kwenye majukumu yao ya ulinzi wa raia na mali zao.

Ni huzuni kubwa Polisi kuuwawa na silaha kwenda kwenye mikono ya wahalifu, tukio kama hili ni muhimu likatukumbusha kwamba Taifa linaweza kujengwa vyema kama kila mmoja atawajibika katika haki na sheria , kumbe Polisi wanaweza kuuwawa na Watu wasio na huruma na wasiotii sheria , kama ambavyo Polisi wasio na huruma na utii kwa Katiba wanavyoweza kujiandaa kuvunja ukuta unaotaka uwajibikaji wa matumizi sahihi ya Katiba na sheria.

Ni ishara mbaya sana kuona walinzi wetu wanauwawa, lakini ni ishara mbaya zaidi kuona walinzi wetu wakiwa kwenye mazoezi hadharani ya kujipanga kudhibiti na pengine hata kuua Wananchi wanaodai haki yao Kikatiba ya mikutano ya vyama vya Siasa.

Uimara wa Jeshi letu utajengwa na uhusiano mzuri kati yake na raia na sio silaha za kisasa na mazoezi ya vitisho hadharani.

Poleni sana Watanzania kwa tukio hili baya, ni matumaini yangu kuwa watu hawa watatiwa nguvuni haraka iwezekanavyo.

Godbless Lema.

Mwanafunzi Afukuzwa Shule Kwa Ushirikina

0
0
UONGOZI wa Shule ya Sekondari Mwatisi Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, umemfukuza mwanafunzi mmoja (jina tunalo) kwa madai ya ushirikina.

Mwanafunzi huyo anadaiwa kuhusika na kitendo cha baadhi ya wanafunzi shuleni hapo kukumbwa  na matatizo ya kuanguka na mapepo kwa muda wa miezi miwili mfululizo.

Mwanafunzi huyo pia anahusishwa na mzuka wa ajabu uliotokea hivi karbuni, ambapo ulikuwa ukianua vyakula vya watu wakati wakianika nje, huku ukiwakumba wanafunzi wa kike waliokuwa wakikimbilia porini na kuzua taharuki kwa wakazi wa eneo hilo.

Hali hiyo ilisababisha uongozi wa shule hiyo kuitisha mkutano wa hadhara  ulioshirikisha viongozi  wa  dini,  machifu na watu  wengine, lengo likiwa ni kufikia mwafaka  wa sakata hilo.

Furaha Mwakalundwa, Mwinjilisti  wa  Kanisa  la  Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Konde Jimbo la Mwakaleli, alisema kufukuzwa kwa mwanafunzi huyo hakuwezi kuleta tija kutokana na kwamba masuala ya ushirikina hayana uthibisho.

“Siku zote masuala ya ushirikina hayana uthibitisho, hivyo ni vyema hii kazi wangetuachia watumishi wa Mungu, ili tuendelee kuitatua kwa  nguvu za Mungu. Kumwondoa  mwanafunzi  huyo hatuwezi kujua kama kweli ni mhusika au laa,” alisema Mwakalundwa.

Baadhi ya wanafunzi walisema kuondolewa kwa  mwanafunzi mwenzao kumeleta faraja kutokana na hali hiyo kupungua kwa asilimia  90 ukilinganisha na awali.

“Alikua akiingia tu darasani au kila anapokutana na mwanafunzi yeyote walikuwa wakianguka na kupata kama kichaa na kuanguka na kusababisha  wanafunzi na walimu kumchukia,” alisema mmoja wa wanafunzi katika shule hiyo.

Walimu na wanafunzi walikuwa wakimwogopa na kumkimbia  kila anapoonekana ikiwamo kuogopa kumpatia adhabu  wakihofia kukumbwa na sintofahamu hiyo.

Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo, Japhet Boniface, licha  ya  kukiri kuwepo kwa adha hiyo, alisema  kwa sasa hali iko shwari ukilinganisha na alipokuwepo mwanafunzi huyo.

“Vitendo kama hivyo vimekuwa vikijitokeza mara kwa mara kitu ambacho kinatupa wakati mgumu kujua ukweli wa jambo hilo,” alisema.

Mkuu wa  Shule hiyo, Eliza Halinga, alisema mwanafunzi huyo hajafukuzwa shule isipokua uongozi uliamua kumhamishia shule nyingine ili kunusuru hali yake kutokana na kila mwanafunzi kumchukia, hali iliyosababisha wanafunzi na walimu wengi kutofika  shuleni kwa hofu.

“Tuliamua kumwita mzazi wake ili kuongea nae ili tuweze  kumhamishia  shule  nyingine  kwani  kila  mwanafunzi  alikuwa  akimchukia  kutokana na kunguka kwao, pia licha  ya  kunguka  kwao  lakini kila akikutana na wanafunzi wenzake  walikuwa wakianza kuanguka na kujipigapiga,” alisema Halinga.

Kimenuka..Mbowe Awekwa Katika Orodha ya Wadaiwa Sugu wa NHC, Mwenyewe Adai ni Njama

0
0
Nimepata taarifa ya mkutano wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Waandishi wa habari kuhusu kilichoitwa “wadaiwa sugu” wa NHC ambapo katika orodha hiyo kampuni ambayo nina hisa ya Mbowe Hotels Co.Ltd imeorodheshwa kama mdaiwa anayedaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni moja.

Nakiri kuwepo kwa mgogoro wa kibiashara wa miaka mingi baina ya Kampuni hii na NHC. Aidha kampuni hii imekuwa ikilipa kodi stahiki kwa NHC kwa mujibu wa makubaliano yetu ya kibiashara.

Kumekuwepo na ukakasi wa muda mrefu kuhusiana na mkataba wetu wa umiliki, uendelezaji na uendeshaji wa jengo hili unaochagizwa na msimamo wangu wa kisiasa.

Haki na Uhuru wetu wa kufanya biashara kama raia wengine umekuwa ukiingiliwa mara kwa mara katika mazingira yanayoambatana na Vitisho kiasi ambacho Maamuzi kadhaa hayafanyiki kwa hofu ya kisiasa kwamba “Itakuwa kumwongezea nguvu Mpinzani”. Hivyo, ningependa umma wa Watanzania uelewe kuwa sidaiwi na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC). Kufuatia utata huu wanasheria wa Kampuni wanashughulikia jambo hili kwa taratibu za kibiashara na kisheria.

Naomba kuweka wazi kwa yeyote anayehusika. Sitafungwa fikra, sitafungwa mdomo na sitaacha kuutetea Ukweli, Haki na Demokrasia katika nchi hii kwa misingi ya “kulinda kinachodhaniwa ni maslahi yangu ya kibiashara”. Wafanyabiashara wengi wanafungwa fikra na midomo ndani ya nchi hii kwa kuogopa hila na ghiliba za watawala.

Ni heri kufa masikini nikiwa nimesimamia ukweli, kuliko kuishi tajiri niliyetawaliwa na ubinafsi, woga, hofu na ubatili.

Natambua kuna jitihada za kutumia kila silaha na kila hila dhidi yetu katika Kipindi hiki.

Mwisho, Natoa rai kwa wanachama na wapenzi wa Haki katika Taifa hili, wasiogope. Haki itaweza kucheleweshwa kwa muda tu, lakini kamwe haiwezi kuzuiwa. Binadamu akikufungia mlango Mungu wa Haki atakufungulia dirisha.

Ubatili ni wa mpito lakini Haki ni ya milele.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya Agosti 25

0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya Agosti 25

Wanaowabeza Polisi Mitandaoni ‘Kushughulikiwa’

0
0
JESHI la Polisi limefura. Ni kufuatia watu mbalimbali kulibeza mitandaoni kwa madai kuwa, limejikita katika matamko na mazoezi ya kukabili maandamano ya vyama vya siasa vya upinzani, kuliko kujipanga kukabiliana na uhalifu mkubwa ukiwemo ujambazi, anaandika Pendo Omary.

Askari wanne waliuawa katika tukio la ujambazi lililotokea usiku wa jana, eneo la Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam na kuibua maoni tofauti ya wananchi katika kipindi hiki ambacho polisi wamekuwa wakijitokeza mitaani na kufanya maonyesho kwa madai ya kujiweka tayari kuwakabili wahalifu.

Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi hapa nchini amewambia wanahabari hii leo kuwa, jeshi hilo halitavumilia ‘ushabikiaji’ wahalifu unaofanywa na baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii huku wakilibeza jeshi la polisi.

CP Marijani aliwaita wanahabari ili kuzungumzia mazingira ya tukio la kutokea kwa mauaji ya askari wa jeshi hilo siku ya jana, ambapo amesema, kitendo kilichotokea jana sit u ni uhalifu bali ni “tangazo la vita dhidi ya Polisi”.

“Wahalifu walifanikiwa kupora bunduki zetu mbili aina ya SMG na risasi 60 na hawakuchukua pesa wala kuharibu mali yoyote ya benki hiyo. Maana yake wahalifu hao walilenga kuwashambulia askari polisi wetu,” amesema na kusisitiza;

“Inashangaza kuona baadhi ya watu wanashabikia uhalifu kutokea kupitia mitandao ya kijamii na natoa onyo kali kwao, waache kuhamasisha uhalifu maana tunawasaka, tutawakamata na kuwahoji ili sheria ichukue mkondo wake.”

Jeshi hilo limesema, tayari limewakamata baadhi ya watu wakihusishwa na mauaji hayo.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images