Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Godbless Lema Afungukia Mauaji ya Askari Wanne Dar, Adai ni Ishara Mbaya

0
0
Kwanza ninawapa pole familia za Polisi wote waliouwawa waliokuwa kwenye majukumu yao ya ulinzi wa raia na mali zao.

Ni huzuni kubwa Polisi kuuwawa na silaha kwenda kwenye mikono ya wahalifu, tukio kama hili ni muhimu likatukumbusha kwamba Taifa linaweza kujengwa vyema kama kila mmoja atawajibika katika haki na sheria , kumbe Polisi wanaweza kuuwawa na Watu wasio na huruma na wasiotii sheria , kama ambavyo Polisi wasio na huruma na utii kwa Katiba wanavyoweza kujiandaa kuvunja ukuta unaotaka uwajibikaji wa matumizi sahihi ya Katiba na sheria.

Ni ishara mbaya sana kuona walinzi wetu wanauwawa, lakini ni ishara mbaya zaidi kuona walinzi wetu wakiwa kwenye mazoezi hadharani ya kujipanga kudhibiti na pengine hata kuua Wananchi wanaodai haki yao Kikatiba ya mikutano ya vyama vya Siasa.

Uimara wa Jeshi letu utajengwa na uhusiano mzuri kati yake na raia na sio silaha za kisasa na mazoezi ya vitisho hadharani.

Poleni sana Watanzania kwa tukio hili baya, ni matumaini yangu kuwa watu hawa watatiwa nguvuni haraka iwezekanavyo.

Godbless Lema.

Chama cha Mrema TLP Chataka Zanzibar Imtenge Maalim Seif

0
0
CHAMA cha Tanzania Labour(TLP) kimemuandikia barua Rais wa Mapinduzi wa Zanzibar, Dk Mohamed Ali Shein na kumtaka kuanzia sasa wamtenge Katibu Mkuu wa CUF , Maalim Seif Sharif Hamad (pichani), kwa kutomualika kwenye shughuli zozote za kitaifa mpaka atakapojirekebisha na kuitambua rasmi serikali iliyopo madarakani.

Aidha, kwa kuwa CUF inadai kwamba haiitambui serikali hiyo basi ruzuku kwa chama hicho isitishwe kuanzia sasa hadi hapo chama hicho kitakapoitambua rasmi serikali hiyo na kuacha kuhamasisha wananchi wasilipe kodi.

Katika barua ya chama hicho iliyosainiwa na Mwenyekiti wake, Augustine Mrema ilisema chama hicho kimesikitishwa na wanalaani kitendo kilichofanywa Hamad ambaye pia alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais kwenye serikali ya Umoja wa kitaifa wa Zanzibar (SUK) wakati wa maziko ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, marehemu Mzee Aboud Jumbe cha kukataa kumpa Rais Shein mkono wa kusalimiana.

Alisema kuleta tofauti za kisiasa msibani kwa makusudi, Maalim Seif ameendelea kuwagawa Wazanzibari kisiasa na kushindwa kumuenzi marehemu Aboud Jumbe, ambaye pamoja na kuiongoza Zanzibar kwa amani na utulivu pia ndiye aliyemlea Maalim Seif kisiasa.

Alisema tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa marudio uliosusiwa na CUF, Maalim Seif amekuwa akileta chokochoko na uchochezi dhidi ya serikali ya Zanzibar akidai kwamba haitambui na kuwataka wananchi wa Zanzibar kugoma na kuwataka wasilipe kodi kwa serikali

Wanaume ‘Wazaa’ Mapacha Watatu wa Kupandikizwa

0
0
WANAUME wawili wanaoishi kama mume na mke (mashoga) nchini Afrika Kusini wanasemekana kuwa watu wa kwanza katika ukanda huo na huenda duniani kwa kuwa wazazi wa mapacha watatu, wawili wakiwa wanafanana, kwa kupitia mtu mwingine aliyebeba mimba.

Wazazi hao ambao walikuwa majirani na mwanamichezo za zamani mlemavu, Oscar Pistorius, walikutana na mtu waliyempatia mbegu zao wakati wa mashitaka ya mauaji yaliyokuwa yanamkabili.
Christo na Theo Menelaou wamewachukua watoto wao nyumbani kwao mjini Pretoria baada ya kukaa hospitali kwa wiki tatu za matatizo.  Kutokana na kuzaliwa kabla ya wakati wao, Julai 2, mapacha hao walijikuta maisha yao yakining’inia kati ya uhai na kifo.

couple (1)Joshua alikuwa mtoto wa kwanza kuzaliwa kwa njia ya upasuaji na ndiye alikuwa mzito kuliko wote akiwa na uzito wa kilo 1.8; Zoe alifuatia akiwa na kilo 1.3 na Kate aliyekuwa na kilo 1.3 pia.

Watoto hao waliwekwa kwenye mashine za kuwasaidia kupumua hadi walipokuwa na nguvu za kutosha na kuweza kuondoka katika hospitali ya Sunninghill ya Johannesburg.

Waliondoka siku tofauti kwenda nyumbani, ambapo Joshua alikuwa wa kwanza kuruhusiwa siku ya Julai 22,  akafuata Zoe aliyeruhusiwa siku kumi baadaye na Kate ambaye aliruhusiwa Agosti 4.
Christo Menelaou aliliambia shirika la utangazaji la Sky News: “Ukiwa shoga, siku zote unafikiri kwamba haiwezekani ukawa mzazi hata kama una upendo kiasi gani.

“Ni vigumu kupewa mtoto wa kuasili na kila mara tuliambiwa kwamba ni wazazi wa kawaida tu ndiyo huruhusiwa.  Pia hatukuweza kufikiri kwamba tungempata mtu ambaye angekubali kubeba mbegu za mashoga.

Hata hivyo, mama mmoja mwenye watoto watatu, waliyekutana naye wakati wa mashitaka ya Pistorious, alikubali kutubebea mbegu zetu.”

Sheria za Afrika Kusini kuhusu upandikizaji wa mbegu kwa watu wengine, iliwataka wanaume wote wawili hao, mtu mwenye kubeba mbegu zao na mumewe wasaini mkataba mbele ya jaji kusisitiza kwamba walikubaliana kwa hiari katika jambo hilo na kwamba pasingekuwepo na kupeana fedha au kubeba gharama zozote.

Wawili hao walikwenda kwenye benki ya mayai na kuchagua mayai  ambapo yai moja lilirutubishika  na mbegu ya Christo na kuwekwa katika tumbo la mbeba mimba na baadaye aliwekewa yai lililokuwa na mbegu ya Theo.

Baada ya wiki kumi za mimba hiyo, uchunguzi ulionyesha kwamba moja ya mayai hayo yaliyorutubishika lilikuwa limejitenga na mbeba mimba alikuwa ana mapacha watatu, wawili wakiwa ni wenye kufanana.

Wakati ambapo madaktari wengi waliwashauri wanaume hao kwamba mbeba mimba huyo akatishe uhai wa mapacha wawili ili kutoa fursa ya mtoto wa tatu kuendelea bila matatizo, hatimaye walimpata mtaalam wa masuala ya watoto ambaye alisema angewasaidia jinsi ya kuhakikisha watoto hao wanazaliwa salama.

Dk Heidra Dahms, ambaye ni mtaalam wa masuala ya watoto katika Hospitali ya Sunninghill na aliyesimamia kuzaliwa kwa watoto hao, aliliambia shirika la Sky News : “Ni jambo adimu sana.  Sijawahi kusikia kitu kama hicho hata siku moja.”

Watoto walikuwa ni wadogo mno, mapafu yao yalihitaji msaada wa ziada ili kupumua na Theo alilazimikakulala kando ya kitanda hadi walipopata nguvu.

Hata hivyo, wazazi hao wanakabiliwa na changamoto ya kumfanyia upasuaji Zoe kutokana na kasorokwenye moyo, upasuaji ambao unahitajika kufanyika katika kipindi cha miezi sita.
Pamoja na yote hayo, wawili hao  wanasherehekea kuitwa ‘baba’, jambo ambalo hawakutegemea kamwe lingewezekana.

Hivi sasa wanaendelea kuwatunza watoto wao hao watatu nyumbani kwao kwa msaada wa mayaya wawili usiku na mchana ambapo kila mtoto amefungwa kidude kinachotoa sauti iwapo watashindwa kupumua.

Theo alisema: “Tunalazimika kuwasugua taratibu kwenye migongo yao au kutekenya vidole vyao ili kuwakumbusha kupumua.

“Tunajisikie tumebarikiwa sana,” alisema kwa furaha.

Witness: Nimejichora tattoo kiunoni ili nisisaliti ndoa yangu

0
0
Msanii hip hop hapa nchini, Witness aka Kibonge Mwepesi, ameitaja sababu ya kujichora tattoo ya jina la mpenzi wake Ochu Sheggy kwenye kiuno chake.

Akiongea katika kipindi cha E-News cha East Africa TV, Witness amesema ameamua kufanya hivyo ili kuepuka kumsaliti mpenzi wake.

“Ukiweka tattoo sehemu kama niliyoweka mimi(kiunoni) inazuia, hata unapotaka kumsaliti mwenza wako yule unayekuwa naye inamnyima hamu kabisa na anashindwa hata kukutamani tena,” alisema Witness.

Pia Witness alisema kuwa watu wanadhani kuwa kuolewa ndiyo kumaliza kila kitu lakini kwa sehemu ambayo mapenzi yao yamefikia hakuna kitu ambacho anakihitaji tena kwakuwa mapenzi ni kuungana mkono na Ochu anamsaidia katika kila kitu anachofanya.

Busu la Nelly Kamwelu shavuni kwa Diamond akiwa na Wizkid lawatoa povu mashabiki (Video)

0
0
Haipiti wiki bila Diamond kuwatoa povu mashabiki, hata kama alichokifanya si kwamba alidhamiria.

Jumanne hii hitmaker huyo wa ‘Kidogo’ alipost video akiwa na starboy, Wizkid. Haijulikani wamekutana Dar au Afrika Kusini. Lakini video hiyo ilitafsiriwa vibaya baada ya Miss Universe 2011, Nelly Kamwelu, kutokea kusikojulikana na kumbusu Diamond shavuni.


Haijulikani Nelly alikuwa mwenyeji wa nani, katika ya Diamond au Wizkid. Busu hilo limetafsiriwa vibaya na baadhi ya mashabiki wanaodai kuwa Diamond amemkosea heshima mpenzi wake Zari.. here we go again!


Hizi ni baadhi ya comments:

officialmafitah

Dat girl kissing you nigga…how about you zari going meet her soon me too

nkunzu39

Zari atachoma mtu

shelmie_muliro

Hebu kujeni uku muone. Mimi hii ujinga siwezani aty dem anadandia chali yangu anamkiss…heeeh fire brigade ingekua ilishaitwa…

b_ngina

Diamond has no respect for zari. .must u post that surely

fufulopez

That kiss? @diamondplatnumz

missremy1

@diamondplatnumz You are an Idiot to post this rubbish!!! ….Not a father material
vitu911: Mmmmmmmmm this vid tho …. @diamondplatnumz u r a star an artist we respect that fact but don’t do this to your fans n family… Respect your woman, have limits ., baba T I love n respect u so much don’t do this to me I begoooo … Leave such kind of life to idris not u … U r a daddy !!!!!! See how Kanye respects Kim , #psuare ‘Elikem ,2baba , to many but mention a few …. Man with beautiful n classy Women …. U r giving haters more reasons to throw stones @zarithebosslady don’t do that @diamondplatnumz … I love u your hard to die fan from Zambia ,,,but its important to respect other peeps feeling .. God has blessed u with a #phenomenon beautiful woman … Be content with wat u have u don’t know wat thaaaa future holds for uuuuuuh

grace_buns

I remember you said in the interview your sugar maama is jealous of your female fans and don’t you think she will get hurt seeing that lady in the background grabbing you

pizzaoriginal

But Diamond when will you ever grow up and start acting like a really grown up? Is it fame that is disturbing you that you can’t tell what to post and not to post or we can say your PR is lacking behind? Where is the damn respect for your wife then? Your so disrespectful boy and get to know that because there was no need of posting this clip. Wat were you trying to prove? That your with wizkid lets say so but he showed you that he respects himself by giving you space when the gal came to peck you. SO STUPID OF YOU!! SO DISRESPECTFUL!! GROW SOME BALLS!! ACT LIKE A FATHER NOT A BOY

Mama Diamond Hapendezwi na Hiki Mitandaoni Kuhusu Mwanae Diamond na Baba yake

0
0
Mama yake mzazi na Staa Diamond Platnumz amefunguka na kuzungumza kinachomkera kwenye mitandao kuhusiana na Diamond Platnumz.

Mama huyo aliipata heshima millardayo.com na & Ayo TV kuyaongea :
Sio kwenye magazeti tu hata kwenye instagram kuhusu Diamond amjali Baba yake hawa watu wanaoandika hivyo wananikera sana ninaumia kwani Diamond kila mwezi anapeleka hela ya matumizi kwa Baba yake sasa sijui hayo maneno yanatoka wapi’
‘Mimi na Baba Diamond tunaongea muda mrefu hata ukisema nimpige utamsikia akiongea lakini nashangaa kutwa watu wanasema Naseeb hatoi huduma kwa Baba yake ni habari si za kweli, sasa hivi anakaa Kagera Dar es Salaam na siku hizi mbili nitaenda tena kumpelekea Chakula na nitaipost ili waone’

Taarifa kuhusu uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Uliofanywa na Rais Magufuli Leo

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 25 Agosti, 2016 amemteua Bw. Andrew Wilson Massawe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Kabla ya uteuzi huo Bw. Andrew Wilson Massawe alikuwa Mkurugenzi wa Mifumo ya Kompyuta katika Benki Kuu Tanzania (BOT).

Bw. Andrew Wilson Massawe anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Modestus Francis Kipilimba ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Uteuzi wa Bw. Andrew Wilson Massawe unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
25 Agosti, 2016

Mwigulu Nchemba 'Watu Wanaofurahia Tukio la Kuuawa Polisi Watafikishwa Kwenye Vyombo vya Sheria'

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema watu wote wanaofurahia tukio la kuuawa Polisi wanne jana watafikishwa kwenye vyombo vya sheria kujieleza

Kufuatia kuuawa Askari Polisi wanne jana baadhi ya watu hasa mitandaoni walionyesha kufurahia jambo hilo

Jeshi la polisi: Tunafanya mazoezi kupambana na uhalifu

0
0
Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, limeendelea na mazoezi yake kwaajili ya ukakamavu ili kujiweka sawa na kupambana na tatizo la uhalifu.


Akiezungumza na waandishi wa habari Kamishna wa polisi kanda ya Dar es salaam, Simon Siro, aliwatoa hofu wananchi kuwa wasiwe na wasiwasi na zoezi hilo kwani halipo kwaajili ya kuwatisha bali lengo ni kupambana na wahalifu na majambazi.

“Eeh kimsingi ni mazoezi ambayo tunayafanya kupitia maeneo mbalimbali kwa maana kwamba lengo kubwa ni kuzuia uhalifu hilo ndo lengo la kwanza, la pili ni kupambana na uhalifu kwasababu tunapokuwa tunapita maeneo mbalimbali lolote linaweza kujitokeza, wahalifu wanaweza jitokeza”, alisema kamanda Siro.

Aliongeza kwa kutoa mfano wa matukio yaliowahi kutokea alisema, “matukio mengi unaweza kuona kama ya panya rodi yanatokea sana sana maeneo ya Mbagala, lakini tukaona kwanini tufanye mazoezi haya kimya kimya ni vizuri wananchi wa kaona jeshi lao wakaona ukakamavu wa askari wao.”

“Hata miaka ya nyuma tulikuwa tunafanya na wala hatuna nia mbaya kabisa kwamba tunatisha wananchi hapana hatuna lengo la kutisha tunafanya katika mazoezi yetu ya kawaida na lengo kubwa kuzuia uharifu kwenye maeneo kwasababu naamini mtu muharifu akiona polisi anapita anakimbia”, aliongeza .

Naye kamishna wa oparesheni wa mafunzo ya jeshi la polisi Nsato Nsazya, aliwataka wananchi wasikejeli mazoezi hayo na kusema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kufanya hivyo kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia mitandao ya kijamii.

Mkuu wa Mkoa Paul Makonda Aibiwa Simu

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-salamm, Paul Makonda ameibiwa simu jana baada ya kufanya kikao na waandishi wa habari alipokuwa na balozi wa Korea nchini na aliporudi ofisini na kutaka kumpigia mtu simu ndio alibaini simu haionekani.

Mugabe aagiza wanamichezo wa Zimbabwe walioshiriki Olimpiki wakamatwe?

0
0
Kuna habari imesambaa mtandaoni kuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi wa nchi hiyo Augustine Chihuri kuwakamata wachezaji wote wa timu iliyokwenda kushiriki michuano ya Olimpiki nchini Brazil.

Inasema Mugabe amechukua hatua hiyo baada ya kuumizwa na wachezaji hao kushindwa kupata hata medali moja kwenye mashindano hayo huku pesa iliyowekezwa kwenye timu ili kuiwakilisha nchi ingeweza kutumiwa kununulia dawa na kujenga shule.

“Jambo hili ni sawa na mwanaume asiyelijali kuoa wanawake watano, maana yake nini? Nitahakikisha tunagawana hasara, wote watailipa serikali bila kujali huku wakijua kuwa fedha zilizowapeleka huko zinatoka kwenye mifuko ya wananchi,” Mugabe anadaiwa kusema.

“Tumepoteza pesa za taifa kwa ajili ya hao panya tunaowaita wanamichezo. Kama hauko tayari kujitoa na kushinda japo medali ya shaba kama wenzetu wa Botswana walivyofanya, sasa kwanini ulienda kupoteza pesa zetu,” ameongeza.

Cha kuchekesha zaidi, Mugabe alidaiwa kusema, “kama tulihitaji watu kwenda Brazil kuimba wimbo wetu wa taifa na kupeperusha bendera, tungewaagiza warembo na vijana watanashati kutoka Chuo Kikuu cha Zimbabwe wakatuwakilishe.”

Zimbabwe ni miongoni mwa mataifa ambayo wanamichezo wake hawakufanikiwa kushinda medali ikiwa inawakilishwa na wanamichezo 31. Mchezaji ambaye alionekana kufanya vizuri ni yule aliyekamata nafasi ya nane.

Hata hivyo kuna uwezekano habari hii inaweza kuwa ni ya kutengenezwa (satire) kama nukuu mbalimbali za kuchekesha ambazo amekuwa akidaiwa kuzisema.

Je Unapenda Kuwa na Makalio na Miguu Mizuri ? Markson Beauty Products Zipo Hapa Kwa Ajili yako

0
0
HABARI NJEMA MARKSON BEAUTY PRODUCTS
Baada ya kupata cheti cha bidhaa bora kwa mwaka 2015-2016, Sasa kampuni hii inasambaza huduma zake ndani na nje ya nchi kwa vibali maalum. Bidhaa zetu zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa. Hazina kemikali wala madhara. DAWA ZETU NI YA:-

  1. kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @100,000/=
  2. Kuongeza shepu (hips na makalio) kwa/= (a)Dawa ya kunywa au kupaka @150,000/=(b)Vidonge @170,000/=
  3. Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:- (1)Mafuta @100,000/= (11)Vidonge @150,000/=
  4. Kupunguza unene na manyama uzembe @120,000/=
  5. Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-(a) Gely ya kupaka @100,000/= (b) Vidonge maalum @120,000/= (c) Handsome up original @170,000
  6. Kuondoa mvi milele zisiludi tena @100,000/=
  7. Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito @120,000/=
  8. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:- (a) Dawa ya kunywa au kupaka @120,000/= (b) Mkanda wa kawaida @100,000/= (c) micro-computer belt unaovaibret @200,000/=
  9. Kupunguza maziwa na kuyasimamisha @90,000/=
  10. Kushepu miguu na kuwa minene @100,000/=
  11. Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @90,000/=
  12. kubana uke na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke @100,000/=
  13. Taiti za hips na makalio @150,000/=           
NB: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii kwa bidhaa halisi. Wasiliana nasi :-(+255) 0767447444 na 0714335378 Google MARKSON BEAUTY.
Follow us
@Markson_beauty_pr
@Markson_beauty_pr

Rais Yoweri Museveni Kutawala Uganda Milele, Muswada wa Kubadili Katiba Kuwasilishwa leo

0
0
Leo Serikali ya Uganda itawasilisha muswada Bungeni unaotaka kubadilisha Katiba ili Rais Yoweri Museveni aweze kutawala milele.

Nini maoni yako juu ya hiki kinachotaka kufanyika?

Romy afunguka Diamond kutokufika kwenye birthday yake

0
0
BAADA ya hivi karibuni ndugu wa Mwanamuziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’, kufanya sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kuhudhuriwa na mastaa kibao isipokuwa msanii huyo na kudaiwa kuwa wana bifu, Romy Jones ‘DJ RJ’ ameibuka na kueleza kilichotokea.

Tetesi zilizagaa kwamba Diamond na Romy wana bifu ndiyo maana hakuonekana kwenye sherehe hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Next Door jijini Dar huku mastaa kama AY, Wema Sepetu na wengine wengi wakihudhuria ambapo Romy ameibuka na kueleza kuwa Diamond alikuwa na projekti muhimu studio ndiyo maana hakuonekana.

“Diamond ni ndugu yangu hatuwezi kugombana na mama zetu bado wako hai, wangekuwa hawapo labda hapo tungeweza kugombana. Sababu ya yeye kutohudhuria kwenye sherehe yangu ni kwamba alikuwa na projekti muhimu sana studio siku hiyo na ilipofika saa kumi usiku akataka aje nikamwambia asije ndiyo tunamalizia
.
Kifupi hatuna bifu kama watu wanavyosema, tuko vizuri kabisa,” alisema Romy.

Diamond Platnumz aikataa Mimba ya Lynn LIVE

0
0
Msikilize Diamond Platnumz Akikana kabisa kuwa na mahusiano na Mrembo Lynn, Adai hana mawasiliano naye na wala hawajawahi kumuona tena toka alivyofanya video ya Kwetu na Raymond..

Msikilize Hapa chini:

Shilole azungumzia bifu la Bill Nas na TID

0
0
Baada ya TID kudai kuwa Bill Nas hana shukrani, Shilole ameibuka na kumtetea rapper huyo wa label mpya,  ‘LFLG’.

Bado Bill Nas amekuwa akisema kuwa aliondoka Rada bila tatizo.

Akiongea na Perfecto TV, Shilole amesema Bill ni kijana mtulivu.

“Wanamuonea sana Bill Nas, kwasababu  ni kijana mtulivu ambaye anaelewa nini anafanya. Hapendi competition ila kuna watu wanataka kufanya competition naye na kutaka kutengeneza jambo ambalo halina maana,” amesema Shilole.

“Ni kweli hakuna mtu aliyemjua Bill Nas kabla hajawa kwa TID lakini mimi naamini anamheshimu sana TID.”

TLP: Mtengeni Maalim Seif hadi atakapoitambua serikali

0
0
Chama cha Tanzania Labour(TLP) kimemuandikia barua Rais wa Mapinduzi wa Zanzibar, Dk Mohamed Ali Shein na kumtaka kuanzia sasa wamtenge Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kutomualika kwenye shughuli zozote za kitaifa.

Katika barua ya chama hicho iliyosainiwa na Mwenyekiti wake, Augustine Mrema ilisema chama hicho kimesikitishwa na wanalaani kitendo kilichofanywa na Maalim Seif wakati wa maziko ya marehemu Mzee Aboud Jumbe cha kukataa kumpa Rais Shein mkono wa kusalimiana.

Alisema kuleta tofauti za kisiasa msibani kwa makusudi, Maalim Seif ameendelea kuwagawa Wazanzibar kisiasa na kushindwa kumuenzi marehemu Aboud Jumbe, ambaye pamoja na kuiongoza Zanzibar kwa amani na utulivu pia ndiye aliyemlea Maalim Seif kisiasa.

Alisema tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa marudio uliosusiwa na CUF, Maalim Seif amekuwa akileta chokochoko na uchochezi dhidi ya serikali ya Zanzibar akidai kwamba haitambui na kuwataka wananchi wa Zanzibar kugoma na kuwataka wasilipe kodi kwa serikali.

UKAWA Wakubali Kurudi Bungeni Baada ya Mkutano na Viongozi wa Dini

0
0
Vyama vya CHADEMA, NCCR MAGEUZI, CUF na ACT Wazalendo ambavyo vilisusia vikao vya bunge vimekubali kurejea bungeni baada ya mkutano wao na viongozi wa dini hapo jana.

RC Makonda: Polisi Mkiwakamata Wahalifu Wapigeni Bila Huruma, Watakaohoji Waje Kwangu

0
0
Leo Paul Makonda mkuu wa mkoa wa DSM akiwa anaongea na waandishi wa habari ofisini kwake akasema watakao vunja sheria wapigwe na Polisi yeye ndoo atajibu je?

Sheria inasemaje kwa mhalifu nini umhimu wa mahakama hizi kauli zinalipeleka taifa pabaya sana viongozi tujaribuni kuchunga ndimi zetu ili tuokoa taifa hili

Matukio Yote Tanzania Yamefunikwa na UKUTA

0
0
Inaelezwa watu 56 wameuawa kanda ya ziwa lakni hakuna ufuatilaji wala maelezo ya kina. Kuuawa kwa askari wanne nayo sio issue, ahadi za rais, vurugu mkutano wa CUF, bomba la mafuta, ufuatiaji wa mapato ya kila mwezi ya serikali, majipu, mafisadi na mahakama ya mafisadi, vyote ni kama vimepotezwa na UKUTA.

Mitaani ni UKUTA, media ni UKUTA, kanisani na misikitini ni UKUTA, serikali na vyombo vya dola UKUTA, sokoni, shuleni na hospitali UKUTA, bbc, cnn, cctv nk

UKUTA, UKUTA, UKUTA! Haijawahi kutokea. Je upo kweli? Nini athari yake?
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images