Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live

Kuahirisha Ukuta, Polisi Wapumua

0
0
JESHI la Polisi limepumua baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuahirisha mikutano na maandamano yao, anaandika Pendo Omary.

Hatua ya kuahirisha mikutano na maandamano iliyotangazwa kufanyika chini ya mwavuli wa operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta (Ukuta), imepongezwa na Simon Sirro, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Kulikuwepo na vuta nikuvute kati ya Chadema na serikali kuhusu Ukuta hivyo kuzua taharuki na hisia za kutokea machafuko iwapo juhudi za kutafuta suluhu zingeshindikana.

Maandamano hayo yalitarajiwa kuanza kufanyika kesho lakini leo Freeman Mbowe, mwenyekiti wa chama hicho ametangaza kusitisha kwa kile kilichoelezwa, uchaguri wa taasisi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuisha mazungumzo ya taasisi hizo na Rais John Magufuli.

“Nawashukuru sana viongozi hawa kwa uzalendo waliouonesha kwa kusimamisha mikutano na maandamano yao.

“Ila kuhusu kesho, wananchi wasishangae kuona magari yetu yakipita barabarani wakajiuliza kulikoni wakati Chadema wametangaza kutoandamana. Sisi kama Jeshi la Polisi bado tupo kwenye oparesheni zetu za kupambana na wahalifu,” amesema Siro.

Aidha, Sirro amesema oparesheni inayoendeshwa na jeshi hilo katika Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam inaendelea vizuri na mpaka sasa tayari linawashikilia watuhumiwa zaidi ya 20 baada ya kufanya msako mkali.

“Watu zaidi ya 20 wamekamatwa. Wengi wanaeleza namna wanavyolifahamu tukio (mauaji ya askari wanne), lakini wengine ni wahusika katika matukio mengine ya uharifu. Ukamataji bado unaendelea katika maeneo ya Vikindu na Dar es Salaam,” amesema Sirro.

Job Opportunities at CVPeople, Click Here to Apply

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya Septemba 2, Ikiwemo ya Magufuli Kuchapa Noti Mpya

0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya Septemba 2, Ikiwemo ya Magufuli Kuchapa Noti Mpya

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya Septemba 2, Ikiwemo ya Magufuli Kuchapa Noti Mpya

0
0
Baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kutangaza kuvifungia kwa muda usiojulikana vituo viwili vya redio, Radio 5 na Magic FM kwa tuhuma za uchochezi, Radio 5 wametoa kauli kwa mashabiki wake juu ya tukio hilo.

Radio 5 kupitia facebook, wametoa taarifa hii.

Good Morning Tanzania.

Habarini Wapendwa wetu kupitia Mitandao yetu ya Kijamii. Baada ya Kimya cha Siku kadhaa Tumerudi Rasmi kuendelea Kukuhabarisha Wewe Mpendwa Msikilizaji / Mfuatiliaji wa Radio 5.

Tunapenda Kuthibitisha kuwa Hatutakua Hewani kwa Kipindi ambacho Bado Hakijulikani, Baada ya Kujiridhisha Ya Kuwa Tumefungiwa “Kurusha Matangazo Hewani” ila bado tunaruhusiwa Kuendelea Kuwahabarisha kupitia Mitandao Yetu ya Kijamii, hivyo Tunapenda Kuchukua Nafasi hii Kuwashukuru Nyie kwa Kuendelea Kuwa Nasi katika Kipindi Hiki Kigumu na Kifupi.

Endelea Kupata Taarifa na Matukio yote (Habari, Burudani, Michezo n.k) Yanayojiri Hapa Nchini na Nje ya Nchi Kupitia Kurasa Zetu za Facebook, Twitter na Instagram ambapo Kote Tunapatikana kupitia @Radio5tz .

Kaa Mkao wa Kula Kuna Mengi Mazuri Yanakuja Kupitia Kurasa Hizi. Ahsanteni Sana kwa Suppoti Yenu na Endeleeni Kuwa Nasi.
Tunashukuru.
#Radio5tz

Producer Nahreel Aelekezea Jinsi Alivyokutana na Mpenzi Wake Aika

0
0
Add caption
Tunapohitaji kuzungumzia moja kati ya couples za mastaa wa kibongo  zenye muonekano wa kupendeza kwenye macho ya mashabiki na jamii kwa ujumla,lazima utapata list ndefu yenye majina makubwa kama   DAIMOND na ZARI au JUX na VANESSA na wengine kibao


Ila moja kati ya Bombastic couple in town ni ya AIKA na NAHREEL kwa pamoja wanaitwa NAVY KENZO mara kadhaa tumemskia AIKA akielezea namna walivyokutana sasa kwa mara ya kwanza NAHREEL aeleza namna walivyo kutana yeye na mpenzi wake huyo,Nahreel aliongea hayo walipokua katika moja ya show za fiesta mara alipopata nafasi ya kuongea na wanafunzi huko bukoba.


“Aliwaambia wanafunzi, nilikutana naye shule, na mimi nikawaambia, na sasa tunatumia akili yetu ya shule kufanya mziki

Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha tano Awamu ya pili

0
0
Ofisi ya Rais -TAMISEMI inatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya Pili (Second Selection) kwa mwaka 2016.

Jumla ya wanafunzi 3,918 wakiwemo wasichana 2,413 na wavulana 1,505 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili kwa ajili ya kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya kwanza.

Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 1,864 wakiwemo wasichana 1,099 na wavulana 765 sawa na asilimia 47.58 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; na wanafunzi 2,054 wakiwemo wasichana 1,314 na wavulana 740 sawa na asilimia 52.42 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara.

Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2015 wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili atakuwa amepoteza nafasi hii.

Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 inapatikana kwenye tovuti ya OR-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz

Imetolewa na Katibu Mkuu,
OR-TAMISEMI

Tumia link hii kupata matokeo : 

==> Waliochaguliwa kidato cha tano awamu ya pili 2016 

==>Waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi 2016

Baada ya Kuacha Muziki, Mzee Yusufu Kuanza na Hili

0
0
Mfalme wa muziki wa taarabu nchini, Mzee Yusufu, ameondoka nchini leo Agosti 31, 2016 kwenda kuhij Makkah ili kutimiza moja kati ya nguzo kuu za dini yake ya Kiislam.

Mzee kabla hajakwea pipa, eNewz ilifanikiwa kufanya mahojiano naye ambapo amesema hatua ya kwenda kuhiji aliipanga iwe mwaka 2018 lakini kwa vile ana nguvu na uwezo ameona aende mwaka huu.

“Nilipanga kwenda kuhiji mwaka 2018 lakini Allah kanifanya niamue tu kwenda mwaka huu kwa kuwa nimeona nina uwezo wa kwenda na kutimiza nguzo hii muhimu katika dini ya kiislamu na namuomba Mungu anijalie uzima nirudi salama ili niweze kwenda tena kwa mara nyingine” Mzee Yusuf aliiambia eNewz.

Akiwa amemsindikiza Mzee uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, baba mzazi wa mzee Yusuph amesema mwanaye kuacha muziki ni jambo zuri hasa kuamua kumtumikia Mungu na kusema anazidi kumuombea mema.

“Mzee kuacha muziki ni jambo la kheri pia kitendo cha kuamua kuacha kuimba na kuendelea kumtumikia Allah ni vizuri zaidi hivyo namuombea Mungu aendelee na moyo huo huo” Aliongea baba mzazi wa msanii huyo.

Hata hivyo eNewz iliendelea kupiga story na mke wake ambaye pia ni muimbaji wa Band ya Jahazi, Laila Rashid ambaye alisema “Mimi binafsi namuombea Mzee kila la kheri katika maamuzi aliyoyafanya na Mungu ampe nguvu katika kila jambo analopanga kulifanya kwa sasa.

Pia Laila alimalizia kwa kusema sababu iliyopelekea kuachiwa albam ambayo ilitungwa wakati mzee akiwepo na kusema wameiachia kwa kuwa ilirekodiwa kipindi mzee akiwa kwenye muziki hivyo ilikuwa lazima albam hiyo itoke na kusema wakati ukifika naye atafuata nyayo za mzee kuacha muziki.

Steve Nyerere Ajigamba 'Mimi Nina Majumba sio Nyumba'

0
0
Msanii mkongwe wa filamu Steve Nyerere amedai yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanamiliki nyumba nyingi lakini hataki kuzionyesha.

Akiongea katika kipindi cha Uhondo cha EFM Jumatano hii, Steve Nyerere amedai yeye haoni ufahari wa kuonyesha mali alizonazo kama wanavyofanya baadhi baadhi ya wasanii.

“Mimi nina majumba sio nyumba ila sitaki kuonyesha instagram,” alisema Steve Nyerere. “Pia kuna nyumba kubwa ambayo ndiyo nitaamia ikiisha, kwa sasa hivi nimepanga Mkwajuni Kinondoni na naishi na familia yangu,”

Katika hatua nyingine mwigizaji huyo amewataka watanzania kuhudhuria show yake ya ‘East African STANDUP COMEDY’ ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi katika hotel ya Protea jijini Dar es salaam.

China kujenga barabara ya kulipia kutoka Dar hadi Dodoma

0
0
China kujenga barabara ya kulipia kutoka Dar hadi Dodoma, Imekaaje Hiii
Toa Maoni yako hapa chini

Ujumbe Huu wa Vanessa Mdee Kwa Jux wa Wakuna Wengi

0
0
Staa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ametumia fursa ya siku ya kuzaliwa ya mpenzi wake, ambaye pia ni Staa wa muziki wa R&B hapa Bongo, Juma Jux kumwandikia ujumbe muhimu kudhihirisha ni kwa kiasi gani anampenda huku akiutaja wimbo wao wa pamoja, #Wivu kuwa ndiyo nguzo ya kukutana na kuanzisha uhusiano wao:


Kuoitia ukurasa wake Instagram, Vee Money ameandika;

When we first met I was an upcoming songstress with a fast tongue and one hit song on the radio. You … well you were pretty much the same. Your boy asked me if I would spit some bars on your song. I said no. Then walked into the studio and met you and instantly had a change of heart. Fast forward to 2yrs later, tumekuwa. You’ve got the biggest song in the country #Wivu and a multi million dollar brand #AfricanBoy and as for me well … kitu kimoja hakijabadilika though. Kwako sisikii. Lol! Lakini hayo yoteee ni mifano tu ya jinsi gani ukiwa na mahusiano na mtu anayekujenga kifikra na vinginevyo maisha yako yanaweza kukaa sawa. Siwezi kueleza ni jinsi gani uwepo wako katika maisha yangu yamenibadilisha na kunikuza na kuniboresha. All things are God’s design. Namuomba Mungu akuongoze and akupe maisha marefu sana sana sana. Maisha yenye mafanikio, afya bora na furaha tele. Una moyo wa kipekee sana tofauti na mtu yeyote ninayemfaham. Nasikitika kuwa mbali na wewe leo hii lakini unajua nikipata, umepata na tunazidi kwenda #Juu. Oh by the way kwa mashabiki wetu ngoma yetu ya kwanza ya pamoja inaitwa #Juu 😉 Basi nisaidieni kumtakia mpenzi wangu Heri ya siku ya kuzaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa Akwama Kuhamia Dodoma

0
0
SERIKALI Mkoa wa Dodoma imesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atahamia rasmi mkoani humo mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge vinavyoanza wiki ijayo, Septemba 6.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema baada ya kufika Dodoma, ataanza kuratibu utaratibu wa wizara mbalimbali kuhamia katika Makao Makuu hayo ya nchi.

Pamoja na hayo Jeshi la Polisi limejipanga kuongeza vituo vya Polisi ili kuimarisha ulinzi wakati serikali itakapohamia na hakuna mwananchi atakayenyang’anywa ardhi yake kwa sababu yoyote ile.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari jana, Rugimbana alisema kama mkoa walishauri ujio huo ufanyike mara baada ya kikao cha Bunge na Waziri Mkuu ameridhia suala hilo.

Alisema Waziri Mkuu atakuwa Mratibu wa wizara zote kuhamia Dodoma na kazi hiyo ataianza rasmi mara baada ya kuwasili mkoani humo.

Alisema maandalizi yanaendelea vizuri na ukarabati wa nyumba ya Waziri Mkuu umefikia asilimia 90.

Alisema Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christine Mndeme aliyekutana na makundi mbalimbali kwa ajili ya mapokezi ya Waziri Mkuu.

“Awali tulisema atakuja Septemba Mosi lakini baada ya kushauriana tumeona aje mara baada ya vikao vya Bunge kwani pilikapilika nyingi zitakuwa zimepungua, kama serikali ikiamua kuja leo tutaipokea kwani maandalizi ya serikali kuja Dodoma yamekamilika kwa asilimia 70,” alisema.

UVCCM Waichokonoa Chadema, Wadai Wana Siasa za Maigizo Baada ya Kushindwa Kufanya Operesheni UKUTA

0
0
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umewavaa viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kile walichodai kuendesha siasa za maigizo baada ya kushindwa kuzindua Operesheni UKUTA, Septemba 1.

Kupitia taaria yake kwa vyombo vya habari, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, amesema kuwa Chadema walijua kuwa hawana ubavu wa kufanya maandamano na mikutano nchi nzima Septemba 1 na kwamba walichofanya ni kuwatia hofu wananchi.

“UVCCM tulijua, tulielewa na kutambua bayana kwamba Chadema walikuwa wanafanya maigizo katika siasa, hawana ubavu wala jeuri ya kuandamana kwa madai ya kipuuzi na ambayo sio ya msingi kwa mustakabali wa nchi yetu,” alisema Shaka.

Aidha, Shaka alikanusha sababu zilizotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuahirisha maandamano hayo kuwa wameombwa na viongozi wa dini ili waweze kukaa na pande zote kujaribu kutafuta suluhu kwa amani.

“UVCCM inatamka bayana kuwa hakuna majadiliano, mazungumzo wala mijadala itakayojadiliwa kati ya Serikali ya CCM na Chadema. Tunaomba Serikali ya Rais John Magufuli iendelee na mikakati yake ya kisera,” Shaka ameongeza.

Kaimu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM alisisitiza kuwa Chadema hawana ubavu wa kufanya maandamano na mikuano nchi nzima Oktoba 1 kama walivyosema, baada ya kushindwa kufanya hivyo Septemba 1.

Shaka amesema wanachokifanya hivi sasa Chadema kinatokana na kushindwa kubuni mikakati ya kufanya siasa ili chama chao kiimarike na kukubarika.

Juzi, Chadema walitangaza kuahirisha uzinduzi wa oparesheni UKUTA nchi nzima, iliyokuwa imepangwa kufanyika jana (Septemba 1) kwa maandamano na mikutano nchi nzima.

UVCCM pia walitangaza kuahirisha maandamano yao ya nchi nzima waliyokuwa wamepanga kuyafanya Agosti 31 kwa lengo la kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi aliyoifanya ndani ya kipindi kifupi.

Maandamano ya pande zote mbili yalipigwa marufuku na Jeshi la Polisi nchini.

Video: Diamond na Ne-Yo washoot video ya wimbo wao ‘Marry You’

0
0
Hatimaye Diamond na Ne-Yo wameshoot video ya wimbo wao, Marry You.

Video imefanyika jijini Los Angeles, Marekani. Wimbo huo ulirekodiwa kitambo baada ya Diamond kumfuata Ne-Yo Nairobi alikoenda kwenye kipindi cha Coke Studio Afrika, msimu wa tatu.

Baada ya hapo wawili hao walikutana tena Marekani kumalizia baadhi ya vipande. Mwezi May, Ne-Yo na Diamond waliuimba wimbo huo pamoja kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kwenye tamasha la Jembeka.

Tazama Video Hapa:

Huenda Idris Elba Akawa James Bond Mpya

0
0
Idris Elba ni miongoni mwa majina yaliyoingia kwenye orodha ya mwisho ya waigizaji wanaotazamiwa kuchukua nafasi ya James Bond, mpya.

Muigizaji huyo, 43, ametangazwa kuwa mmoja wa waigizaji wanaoweza kuchukua nafasi ya Daniel Craig anayetaka kujiondoa.

Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Sun:

To get anyone to take over from Daniel will be a tough job. There will be a lot of trepidation about a new Bond, but Idris’ talent and proven appeal gives executives a lot of heart. Idris may be a little older than the other candidates but he looks like he is still in his 30s. MGM are confident that they are in a pretty strong place with a raft of talent available.

Wengine walioingia kwenye orodha hiyo ni pamoja na Aidan Turner, Luke Evans, na Tom Hiddleston.

List Biashara Yako Leo Bure na Mtandao wa Listzetu.com Uweze Kujulikana Mtandaoni

0
0
Listzetu.com ni mtandao unaoleta kwa ukaribu Biashara na Jamii,  website ya Listzetu.com inaorodhesha kurasa za biashara tofauti ili wateja waweze kufikia biashara hizi kwa kuonyesha picha, anuani pamoja na njia za mawasiliano kufikia biashara hizi, Pia wateja wanaweza toa maoni yao kuhusu biashara au sehemu walizotembelea

Kupitia website ya listzetu.com utaweza kutafuta migahawa, hostel,saluni, club, mashule, nan.k.

Listzetu.com itakuwezesha kuwasiliana nawahusika wa Bishara husika kwa urahisi .

Website ya listzetu.com Humsaidia mmiliki wa Biashara kutambua faida na hasara za Biashara yake.
Kwani kupitia website hiyo Wateja wanaweza kueleza kama wameridhik ana Hudumaa ula, hii humsadia miliki wa Biashara kuboresha biashara yake zaidi.
___________
Jinsi ya kujiunga na website hiyo tembelea kurasa ya listzetu.com, ilikutengeneza kurasayako, pia kwa wasiowafanyabiashara, katika website hiyo Nisehemu nzuri ya Kugundua unachokitaka bila gharama yeyote.Tafuta biashara zilizoko karibu na wewe
___________
Biashara yako inastahili kujulikana, Fanya maamuzi sasa kuwa karibu na Wateja wako, pata taarifa zako zote kuhusu biashara yako na Huduma zake kwa ujumla.

Mambo ya kuulizia yameshapitwa na wakati ingia Listzetu.com tafuta unachokitaka.

Kwa wafanyabiashara Listzetu.com inapackage Mbili moja ya Bure nanyingine ya kulipia. Jiandikishe na Moja yapo uweze Kutangaza biashara na kuweka biashara yako mtandaoni.


Vifaa Vyote vya Freeman Mbowe Vilivyokamatwa Jana na NHC Vitauzwa Baada ya Siku 14 Ili Kufidia Deni Analodaiwa

0
0
VIFAA vilivyokamatwa jana vya klabu ya usiku ya Bilicanas na ofisi ya gazeti la Tanzania Daima, vyote vinavyomilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, vitapigwa mnada na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) siku 14 kuanzia jana, endapo atashindwa kulipa Sh. bilioni 1.2 za deni la pango la miaka 20.

Mbowe alikuwa mpangaji katika jengo la NHC lililopo makutano ya mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi, katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Vyombo hivyo vilikamatwa jana na kampuni ya udalali ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyopewa kazi ya kuondoa vifaa hivyo baada ya Mbowe kushindwa kulipa deni hilo ndani ya miezi miwili ya notisi ambayo shirika hilo lilikuwa limempatia.

Meneja wa Kitengo cha Kukusanya Madeni kutoka NHC, Japhet Mwanasenga aliyekuwa akisimamia ukamataji wa vyombo hivyo, alisema Mbowe ana muda wa wiki mbili kuanzia jana kulipa deni la Sh. bilioni 1.172 vinginevyo vitapigwa mnada.

Vifaa vilivyokamatwa ni pamoja na kompyuta, meza na viti.

Alisema taratibu zote zilifuatwa kabla ya kumuondoa mteja wao, ikiwamo notisi na kwamba vifaa hivyo vitashikiliwa kwa muda huo wa wiki mbili.

“Tunashikilia vyombo kwa muda wa wiki mbili na iwapo atashindwa kulipa vitapigwa mnada na dalali, (mdaiwa) akishindwa kulipa anapangishwa mwingine,” alisema.

Alisema shirika hilo linahitaji fedha kwa ajili ya ujenzi na uendelezaji wa majengo yake hivyo mteja ambaye anadaiwa ajiandae kuondolewa wakati wowote na kwamba zoezi la jana ni mwanzo tu.

Baadhi ya watu wamelihusisha tukio la kuondolewa Mbowe katika ofisi hizo na masuala ya kisiasa.

Lakini Mwanasenga alisema uamuzi wa kumuondoa ofisi hizo hauna uhusiano na masuala ya kisiasa.

Alisema wapangaji wa jengo hilo wapo wengi pamoja na wadaiwa na kwamba baada ya mchakato huo kuanza mdaiwa yeyote atakayeshindwa kulipa kodi ataondolewa.

Akizungumza na waandishi wa habari katikati ya wiki iliyopita, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu alisema pamoja na Bilicanas, shirika linazidai taasisi za umma, binafsi na watu binafsi jumla ya Sh. bilioni 15.

Notisi ya siku 60 ya kuondoka Bilicanaa pamoja na majengo ya wadaiwa wengine ilishatolewa, Mchechu alisema. Notisi hiyo ilikuwa inaisha juzi.

Alisema baada ya muda huo kumalizika, utekelezaji wa kuondolewa katika majengo hayo utaanza ukiambatana na uchukuaji wa hatua za kisheria.

Mchechu alisema mbali ya Bilicanas, wadaiwa wengine ni Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi inayodaiwa Sh. bilioni mbili, Benki ya Azania (Sh. milioni 161) na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa (Sh. milioni 631).

Wadiawa wengine walitajwa kuwa ni Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Sh. bilioni 1.3), Wizara ya Ujenzi (Sh. bilioni mbili), Tume ya Utumishi (Sh. milioni 109) na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Sh. bilioni moja.

Mchechu alisema ukusanyaji wa madeni hayo kwa nguvu ni mkakati wa shirika hilo kukusanya fedha ili kusaidia ujenzi wa nyumba za watumishi wanaohamia Dodoma.

"Mwaka huu ujenzi unaanza Dodoma," alisema Mchechu, hivyo "fedha tunazodai zitatusaidia kukamilisha uwekezaji mjini humo."

Alisema kuwa fedha hizo zitatumika kwa ujenzi wa nyumba za watumishi 300 hadi 500 mkoani Dodoma.

Alisema ujenzi huo unatarajia kuanza mara moja na utachukua miezi 12.

Kwa mujibu wa Mchechu, Sh. bilioni 60 za ujenzi wa nyumba hizo zitatokana na fedha za ndani.

Alisema shirika hilo limenunua ekari 240 eneo la Iyumbu, ekari saba Chamwino, nne Bahi na Chemba ekari nne pia ikiwa ni kuunga mkono azma ya serikali ya awamu ya tano kuhamia Dodoma.

Alisema fedha nyingine zitapatikana baada ya nyumba 97 za shirika hilo zilizopo Medeli mjini Dodoma kuuzwa.

Wema Sepetu Atoa Tahadhari Kwa Wabaya Wake

0
0
Madam Wema Sepetu amewatumia ujumbe wa tahadhari wabaya wake wanaomfuatilia anga zake.

Ni ukweli usiopingika kuwa Wema amekuwa akihangaika mara nyingi huku na kule ili apate mtoto lakini mambo bado yamekuwa yakienda kombo kwa kuishia kuumia huku baadhi ya watu wakimkejeli kwa matusi wakisahau jambo la kupata mtoto ni neema ya Mungu pekee.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Wema Sepetu ameweka picha ya Blac Chyna mwenye ujauzito inayomuonyesha sehemu yake ya tumbo na kuandika, “Na ningeomba mfunge kweli account zenu ikifika hii hali…. Mxxxxxxiiiuee.”

Mapema mwaka huu ilidaiwa kuwa Wema ana ujauzito wa Idris Sultan lakini baada ya muda walitoa taarifa za kutoka kwa ujauzito huo japo haijajulikana kama ilikuwa ni kweli au ni kiki. Usikate tamaa madam Wema ipo siku machozi yako yatageuka furaha.

CHADEMA Wagoma Kuhamia Dodoma, Wadai Hawana Mpango Huo

0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema wazo la kuhamia Dodoma halimo kwenye ajenda zake.

Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji alisema chama hicho hakina mpango wa kuhamia Dodoma kwa sababu hayo ni masuala ya kisiasa yasiyo na msingi kiuhalisia.

“Sisi makao yetu makuu yapo Dar es Salaam, hata katiba yetu ndivyo inavyosema, tutaendelea kuwa hapahapa. Hayo ni mambo ya kisiasa yasiyo na misingi ya kiuhalisia, hata mazingira hayaruhusu, kwa hiyo sisi tutaendelea kuwa hapa (Dar es Salaam),” alisema Dk Mashinji.

Chama cha ACT Wazalendo kilisema kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi ni miongoni mwa ajenda zake.

Kauli ya CHADEMA Kuhusu Hatua za NHC na Rasilimali za Mwenyekiti Mbowe

0
0
Kutokana na habari zilizoandikwa leo na vyombo vya habari mbalimbali nchini kuhusu tukio la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia kwa madalali wake 'kuvamia' jengo lenye rasilimali za Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe;

Kwa kuwa habari hizo zimehusisha hatua hiyo ya NHC na itikadi au msimamo wa kisiasa wa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ambaye ni mmoja wa wanahisa wa Mbowe Hotels Ltd ambayo ni mmiliki wa rasilimali hizo zilizovamiwa (Ofisi za Free Media na Club Billicanas) na waandishi wa habari wametutafuta kutaka kauli ya chama juu ya suala hilo;

Katika hatua ya sasa, tunapenda kusema kuwa Chama kitalitolea msimamo suala hilo baada ya kuwasiliana na kushauriana na wanasheria wa Mwenyekiti Mbowe ambao wanalisimamia na kulifanyia kazi suala hilo mahakamani.

Imetolewa, Sept' 2, 2016 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

Je Kuwa MTU Maarufu Kunawezesha Kufanya Kila Kitu Kwenye Tasnia Mbali Mbali?

0
0
The industry is too big you cant own it all. The growth of all things depend on focus, persistence and passion and in math we only have 100% to build legacy and less than that to create life style.

Imekuwa jambo la kawaida sana kwenye tasnia yetu kumuona mtu maarufu kutaka kuwa kila kitu katika jamii yetu ukimuuliza kwanini utasikia niliambiwa naweza so nikathubutu. Swali ni je kuwa maarufu kunawezesha kuwa kila kitu katika tasnia? Kama kawaida yetu reference kwa wazungu mtu atatoa mfano mbona Arnold aliweza kuwa mtunishaji misuli bora, mwigizaji bora na Governor hahahaha ukweli ni kwamba kila kitu alikipa nafasi na muda wake hakufanya vyote wakati mmoja. Focus yake kubwa ilikuwa awe bingwa wa dunia katika kutunisha misuli akatwa taji hilo.

Akaingia kwenye sanaa ya maigizo akatusua ulimwengu mzima, kuwa mwanasiasa akafanikiwa pia kuwa Governor wa California jiji kubwa kabisa marekani. Then, katoka kwenye siasa karudi kwenye movies .Amefanikiwa kuacha legacy sababu alitoa muda kwa kila career. @Sammisago ni presenter na blog yake ni moja ya blog kubwa zinazotembelewa na watu wengi.

Lakini cha kushangaza leo anataka kuwa mwanamuziki wakati dunia ya habari ndo kwanza inaanza na wale wenye focus walioanza mapema watafaidika zaidi. @divathebawse #AlaZaRoho ingetikisa Afrika kwa uwezo wako mkubwa lakini umekosa focus, muziki tena? @Idrissultan ni moja ya watu ambao ukisikiliza interview zake unaweza amini upeo wake kuhusu focus aliyonayo damn!

Tunakuwa na mtu zaidi ya @Kevinhart4real duniani. Lakini leo anataka kuwa kila kitu. Unakipindi cha radio ambacho ni masaa saba, unataka uwe bora kwenye comedy na kesho unataka kuwa bora kwenye filamu how many percent do you have as an individual? Is true that one can produce tremendously result when he/she does things partially?

 Leo wewe unachukuliwa kama presenter wakati wengine wanakufahamu kama comedian. Je, itawezekana kuruhusu watu wengine kuwa comedians kupitia wewe and wakaifanya 100%? Huu ni ubinafsi na kwann tunaifinya hii tasnia yetu? @Bongo5 chief editor anataka kutoa mixtape, sasa hivi tutawezaje kupata bloggers wakubwa wa kushindana kimataifa kama wote watakuwa wanamuziki?
Viewing all 104429 articles
Browse latest View live




Latest Images