Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

Hatimaye Shamsa Ford Afunga Ndoa na Chidi Mapenzi

$
0
0
STAA wa Bongo filamu nchini, Shamsa Ford amefunga ndoa na Rashidi Said ‘Chidi Mapenzi’ ambaye ni mfanyabiashara wa maduka ya nguo.

Sherehe za ndoa hiyo zilifanyika nyumbani kwa wazazi wa Shamsa eneo la Sinza, Afrikasana jijini Dar es Salaam.

 Awali, Shamsa alidumu katika penzi na Dickson Matoke ‘Dick’ na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Terry na kisha  kufunga ndoa ya kimila nyumbani kwa mwanaume huyo, Tarime mkoani Mara ila baadaye waliachana na kuangukia kwa staa wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’  ambaye penzi lao halikudumu.


Rais Magufuli ataka Jecha apewe Tuzo ya heshima, Amtaka Dr Shein Apunguze Upole, Watakaomsumbua Awataje Washughulikiwe

$
0
0
RAIS John Magufuli, amemtaka Dk. Ali Mohamed Shein, kumpa tuzo Jecha Salim, mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, kutokana na kile alichokiita kazi nzuri aliyoifanya visiwani humo mwaka jana, kwa kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu.

Rais Magufuli aliyasema hayo jana  jioni, katika ziara yake ya kikazi visiwani Pemba. Wakati Rais Magufuli akichaguliwa katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, Dk. Shein alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar kufuatia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi mwaka huu.

“Nampongeza sana Jecha kwa kazi nzuri aliyofanya kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, na kwa kweli Dk. Shein kama kuna  tuzo zako utakazotoa, naomba usimsahau kumpa na Jecha,” alisema Rais Magufuli.

Rai Magufuli pia alimtaka Rais huyo wa Zanzibar kumtaarifu yeye ili awashughulikie watu wote wanaomsumbua visiwani humo au wanaoonekana kumzidi nguvu.

“Rais Shein kama kuna mtu unaona anakusumbua wewe au anakupa tabu nijulishe mimi tu, hata dakika tano hazitapita nitamshughulikia,” ameeleza.

Kauli hiyo inakuja, ikiwa ni zaidi ya miezi kumi sasa tangu hali ya mahusiano baina ya wananchi wa Zanzibar iwe tete, tangu pale Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC) alipotangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Mahusiano hayo mabaya yamesababisha, wafuasi wa vyama vya CUF na CCM vyenye nguvu zaidi visiwani humo, kufikia hatua ya kusitisha ushirikiano katika shuguli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kutohudhuria misiba na kutonunua bidhaa za mtu wasiyeendana naye kiitikadi.

“Niombe vyombo vya ulinzi na usalama wafuatilie hao wanaokatakata na kuchoma karafuu washughulikiwe bila huruma. Atakayejaribu kuichezea amani, atacheza yeye tena mchezo asiojua kuucheza,” aling’aka Rais Magufuli.

Tangu kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana visiwani Zanzibar, hali ya usalama imekuwa si ya kuridhisha.

Nyumba na mashamba ya karafuu yamekuwa yakichomwa moto, huku baadhi ya watu wakitiwa mbaroni  na vyombo vya dola kwa tuhuma hizo

Ndoa Yamfanya Mwana FA Kuacha Kufanya Mambo Haya

$
0
0
MAPEMA mwezi Juni, mkongwe kwenye gemu la Muziki Bongo, ambaye pia ni staa wa Wimbo wa Bado Nipo Nipo, Hamisi Mwinjuma aliuaga ukapera baada ya kufunga ndoa na mzazi mwenzake ambaye ni akauntanti, aliyezaa naye mtoto aitwaye Maleka.

Ni zaidi ya miezi miwili sasa mkali huyo akiwa kwenye maisha ya ndoa ambapo akichonga na gazeti hili MwanaFA amefunguka mambo matatu ambayo hayafanyi tangu ‘avute jiko.’ Msikie mwenyewe;

Kupiga Misele sana: “Kwa kweli tangu nioe, imenibidi kupunguza baadhi ya ratiba ambazo zilikuwa zinanichukulia ‘time’ huko nyuma na kunifanya wakati mwingine kuwa nje ya nyumbani. Kwa kuwa mimi siyo mtu wa kujirusha kiivo, suala hili limekuwa rahisi na inanipasa kuwa karibu zaidi na familia.

Kuondoa mtazamo hasi juu ya ndoa. “Kipindi cha nyuma nilikuwa ‘sometime’ nasikia kuwa mtu akioa hasa msanii kuna uwezekano mkubwa wa kupotea kwenye gemu, si kweli, mtazamo huo tangu nioe nimeuondoa kabisa kwa kuwa mke wangu ni mtu wa burudani na anafahamu ninachokifanya. Kikubwa ni kupanga ratiba juu ya mambo yangu na kujua nini natakiwa nifanye katika wakati husika.”

Kujisahau. “ Kuna wakati unafika ukiwa mwenyewe tena mwenye mafanikio unaweza kujisahau na kuona kuwa umefika, mafanikio uliyoyapata yanatosha. Lakini ukweli ni kwamba kutokana na kuwa na familia inanibidi kufanya kazi kwa bidii, kwa kuwekeza kwenye muziki wangu na mambo mengine ili kuhakikisha familia yangu inapata kila kitu inachokitaka. Zaidi ni kuwaandalia maisha bora ya leo na kesho!”

Mbali na hayo MwanaFA alimaliza kwa kuwashauri wanamuziki ambao wanayaogopa maisha ya ndoa na kuamini wakifanya hivyo watafeli kuondoa mtazamo huo na kuwahakikishia kuwa familia ni jambo la heri na humfanya mtu kukomaa zaidi ili kufika mbali

Afikishwa Mahakamani Kwa Kumuita Rais Magufuli ni Kilaza

$
0
0
ELIZABETH Asenga (40), mkazi wa jijini Dar es Salaam amepandishwa kortini jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kuandika maneno ya kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa What’s App.

Akisomewa mashtaka yake na Leonard Chalu, wakili wa serikali, mbele ya Hakimu Huruma Shahidi, mwanamama huyo, alidaiwa kufanya kitendo hicho kilicho kinyume na Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.

Wakili Chalu alidai kuwa, mnamo tarehe 06 Agosti mwaka huu, mtuhumiwa huyo aliandika kwenye mtandao wa what’s App ujumbe uliosomeka;

“….Rais kilaza kama huyu wetu, angalia anampa Lissu umashaghuli… f****l** lile, kwanza picha yake ukiweka ofisini ni nuksi tupu na ukiamka asubuhi ukakutana na picha yake, siku yako inakuwa ina mkosi mwanzo mwisho.”

Hata hivyo, mshitakiwa Elizabeth, alikana mashtaka hayo huku wakili wa serikali akidai kuwa, upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Mtuhumiwa alipewa dhamana yenye masharti yanayohitaji wadhamini wawili huku kila mmoja akitakiwa kusaini hati ya shilingi 3 millioni.

Kesi hiyo imeahirishwa na inatarajia kutajwa tena mnamo tarehe 22 Septemba, mwaka huu.

Staa wa Bongo Movie Irene uwoya Adaiwa Kuzaa Mtoto Ambaye Hajafanana na Baba yake

$
0
0
September 02  2016 kwenye U Heard ya Soudy Brown amezungumza na  staa wa Bongo Movie Iren Uwoya kuhusu taarifa zilizosambaa kwenye mitandao kuwa mtoto aliyemzaa si wa mume  wake Ndikumana kwa kuwa hajafanana naye, millardayo.com imekuwekea full stori.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza:

Msanii Mr Blue Acharuka..Kuwachukulia Sheria Naj na Baraka da Prince Wanaodaiwa Kuivuruga Ndoa yake

$
0
0
Msanii wa bongo flava Mr. Blue ambaye hivi karibuni alipatwa na msuko suko wa kuyumba kwa ndoa yake, kutokana na kusambaa kwa tetesi za kuwasiliana na ex wake Najma Dartan, amesema yuko tayari kumchukulia hatua za kisheria aliyesababisha ugomvi huo.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mr. Blue amesema yeye binafsi hakuwasiliana na Naj, isipokuwa habari hizo zilipoanza alidhani ni kiki inayotengenezwa na Naj na Baraka The Prince, ili kuachia wimbo wao wa pamoja.

Mr. Blue aliendelea kusema kuwa baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya na ndoa yake kuwa mashakani, aliamua kumfuata Baraka na kumuuliza kuhusu suala hilo, lakini Baraka alikanusha na kusema yeye hajui chochote kuhusu hilo.

"Ile habari ilikuwa ya uongo, mwanzoni mi nilihisi Baraka na mchumba wake Najma watakuwa wameitengeneza kwa ajili ya mambo yao ya kutafuta kiki, kwa sasabu ilisemekana kuna nyimbo yao wanataka kutoa Baraka na Najma, kwa hiyo wanatafuta kama kiki kutumia ubavu wangu, nikabahatika kukutana na Baraka na kumshika mkono, na kumwambia akubali mbele za watu, akasema hajui hiyo taarifa", alisema Mr. Blue.

Mr. Blue aliendelea kusema kitendo hicho amabcho kiliyumbisha ndoa yake hawezi kukifanya kwa sababu tayari ana mke, na hawezi kurudiana na mtu ambaye alishaachana naye, na iwapo ikithibitika ni wao kina Baraka na Najma ndio wametengeneza habari hiyo ili kupata kiki, hatosita kuwachukulia hatua za kisheria.

"Hatua za kisheria lazima zichukuliwe unajua hivi vitu sio vitu vya kuharibiana, mi sa hivi nishakuwa mtu mzima, siwezi kurudia matapishi ambayo nishawahi kuyatapika, eti nikampigie Najma sijui niwe nae, kwa sababu mimi najua mke wa kumuoa najua mwanamke wa kuwa naye ndio maana nikamchagua mke wangu, na nampenda na amenizalia watoto wazuri, kwa hiyo siwezi tena kufikiria eti kumpigia Najma, siwezi kufikiria kugombana na Baraka The Prince, kwanza hatulingani, mi wakati naanza mziki ye bado yuko shule anasoma, kama ni kweli ni wao japokuwa Baraka amenithibitishia sio wao, nikijua ni wao lazima nitafute njia ya kuwashikisha adabu", alisema Mr. Blue

Bodi ya Mikopo Kumwaga Fedha kwa Waombaji wote

$
0
0
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema wale wote walioomba mkopo mwaka huu na kukidhi vigezo watapewa.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema hayo juzi mjini hapa wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa watu watano waliorejesha mkopo wa elimu ya juu kwa mkupuo na kwa hiari.

Badru alisema idadi ya walioomba mkopo mwaka huu ni wanafunzi 88,000 ambao bodi itahakikisha wale wote waliokidhi vigezo, wanapatiwa fedha kwa ajili ya elimu ya juu.

Mkurugenzi huyo ambaye amehimiza walionufaika na mikopo kulipa madeni yao, alisema mwaka jana, wanafunzi waliokopeshwa ni 55,000.

Kuhusu waliopewa vyeti ikiwa ni hatua ya kuwatambua, ni pamoja na mfanyakazi wa VETA Shinyanga, Richard Jafu aliyerejesha kwa mkupuo Sh 14,749,950 na Francis Mwilafi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo aliyelipa Sh 15,115,200.

Wengine ni Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga aliyerejesha Sh 255,000; Profesa Peter Msoffe ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM) aliyerejesha Sh 1,430,749.

Mwingine ni Mbunge wa Biharamulo, Oscar Mukasa ambaye kiasi alichorejesha hakikutajwa ingawa mkurugenzi mtendaji wa HESLB, alisema amerejesha kiasi kikubwa kwa mkupuo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wadau hao walisisitiza umuhimu wa wanufaika wa mikopo kuirejesha kwa hiari ili kuiwezesha bodi hiyo kukopesha wanafunzi wengine.

Mbunge wa Biharamulo, Mukasa alishauri bodi hiyo kuangalia uwezekano wa kurekebisha vigezo kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi watokao maeneo ya pembezoni kunufaika na mikopo hiyo ya elimu. Kwa upande wake, Mbunge wa Vwawa, Hasunga alisisitiza wabunge wanaodaiwa warejeshe mkopo kwa mkupuo.

Kijana wa Miaka 19 Atolewa Macho Kisa Ushirikina

$
0
0
Kijana mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa jimbo la kaskazin magharibi mwa Nigeria la Bauchi anasema kuwa macho yake yalitolewa na watu waliotaka kuyatumia kwa ajili ya sababu za ushirikina.

Viungo vya mwili wa binadamu ambavyo hutumiwa katika imani za uchawi ama kwa ajili ya mazingaombwe hutolea kutoka kwa watoto nchini Nigeria, na mara nyingi watu wazima huwa hawaathiriwi.

Hussain Emmanuel, ambaye kwa sasa anatibiwa katika hospitali ya mji wa Bauchi, anasema shabulio lililomuacha bila uwezo wa kuona tena, lilitokea wiki mbili zilizopita katika kijiji kilichoko eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi la Tafawa Balewa.

Anasema alirubuniwa na watu wawili katika kijij cha Marti kilichopo karibu na mto waliomshawishi aende kuogelea .

Bw Emmanuel, ambaye hufanya kazi yake ya kibinafsi kama fundi wa magari, anasema alikuwa pamoja na watu hao wawili kwasababu mmoja wao alimuahidi kumpa kazi kusini mwa Nigeria.
Lakini walipokwenda mtoni walimshabulia, wakataka kumnyongana na mnyororona shingoni na baadae wakaamua kumgonga kiasi cha kupoteza fahamu.

Alipoamka, hakuweza kuona , ndipo alipopiga mayowe hadi alipookolewa na wapita njia ambao walibaini kuwa macho yake mawili yalikuwa yameondolea.

Polisi wanasema wanachunguza kisa hicho, na hawakutoa kauli yoyote kuhusiana na sababu ya washukiwa hao kutekeleza kitendo hicho.

Nafasi za Kazi CVPeole, Bonyeza Hapa Kusoma na Kuapply

Nay Wa Mitego amchimba mkwara mume wa Shamsa Ford

$
0
0
Nay Wa Mitego ameonekana kumchimba mkwara mwanaume aliyemuowa aliyekuwa mpenzi wake, Shamsa Ford.


Nay na Shamsa walikuwa na mahusiano mwaka 2015 japo mahusiano yao hayakufanikiwa kudumu kwa muda mrefu na kila mtu kufuata njia yake huku wakidai bado ni marafiki wa kawaida.

Kitendo cha kuolewa kwa Shamsa kinaweza kikawa kimemtoa povu rapper huyo kutokana na kipande cha video alichokiweka kwenye mtandao wake wa Instagram na kuandika ujumbe unaosomeka:

TANGAZO TANGAZO TANGAZOOOO😡😡😡
Naskia my #COUSIN Kaolewaaaa Sasa uyo aliyemuoa ipo siku nitampiga Tukio Kama hiiiiiiiiiii😂😂😂🏃🏿🏃🏿🏃🏿🏃🏿
Nina hasiraaaaaaaa🔫🔫😡👹

Shamsa Ford amefanikiwa kufunga ndoa Ijumaa hii na mpenzi wake mfanyabiashara wa maduka ya nguo Rashidi Said aka Chidi Mapenzi.

Picha: Mkubwa Fella aonyesha nyumba 4 za wasanii wa Yamoto Band ‘watu wanaongea sana’

$
0
0
Mkurugenzi wa Yamoto Band, Mkubwa Fella ameonyesha nyumba nne za wasanii wake wa Yamoto Band baada ya baadhi ya watu kuhoji kuhusu mafanikio ya wasanii hao.
Nyumba nne za wasanii wa Yamoto Band
Nyumba nne za wasanii hao

Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii akiwa Mbande Kisewe, Chamazi jijini Dar es salaam, Fella amesema ameamua kuonyesha nyumba hizo baada ya kuchoka maswali ya watu kuhusu mafanikio ya wasanii hao.


“Leo nimewaita hapa Mbande Kisewe siyo kuzindua ila kuwaonyesha kwa sababu kuna meseji nyingi nazipata, Mkubwa vipi mbona watoto wananenepa wanavaa vizuri, maendeleo vipi, mbona kuna wasanii wamekuja juzi tu, tunawaona wanafanya vitu vikubwa. Kwa hiyo nimewajengea hizi nyumba lakini bado hazijazinduliwa, nataka uzinduzi wake Mh rais mtaafu Kikwete aje azindue na kuwakabidhi hawa vijana nyumba zao,” alisema Fella.

Aliongeza, “Kwa hiyo nataka wale wanaosema Yamoto wananini waone nini kimefanyika, kwa sababu nilikuwa natengeneza kitu kikubwa, siyo vibanda majumba na mlivyoyaona. Kwa hiyo 80% nyumba zimekamika, kuna vitu ambavyo sijamalizia kwa sababu kila mtu najua atataka kuweka manjonjo yake kwenye nyumba yake, kwa hiyo ndani ya miaka mitatu tulichovuna tumekiwekeza kwenye hizi nyumba, ni kubwa naza kisasa kabisa,”

Meneja huyo siyo mara yake ya kwanza kuwajengea wasanii wake nyumba, alishafanya hivyo kwa Temba na Chege pamoja Juma Nature. Angalia picha.

Source:Bongo5

Install Application ya SIASA HURU Kwenye Simu yako Kupata Habari za Siasa Kwa Urahisi

$
0
0
Kama wewe ni mpenzi wa Habari za Siasa basi hii ni habari njema kwako...Download Siasa Huru Application Kutoka Google Play Store Kwenye Simu yako itakurahisishia upataji wa Habari na Breaking News za Siasa kwa urahisi....

Bonyeza HAPA Kuinstall Kwenye Simu yako fasta....

Au Nenda Google Play Store Kwenye Simu yako Alafu Search 'Siasa Huru' Kisha Install


Bulaya: Nimemsamehe Wassira

$
0
0
MSUGUANO uliodumu kwa muda mrefu kati ya Esther Amosi Bulaya na Stephen Wassira, umefika kikomo, anaandika Pendo Omary.

Kauli ya Bulaya ambaye ni Mbunge wa Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inaakisi kufungua ukurasa mpya dhidi ya hasimu wake wa kisiasa wa muda mrefu na mwanasiasa mkongwe Stephen Wassira.

“Nimemsamehe Mzee Wassiri,” ni kauli aliyoitoa Bulaya wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii leo kuhusu harakati za kisasa jimboni kwake pia hatma ya msuguano kati yake na Wassira uliokuwepo kwa muda mrefu.

Msuguano kati ya Wassira na Bulaya ulianza wakati Bulaya akiwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na muda mfupi baada ya (Bulaya) kuonesha dalili ya kulitaka jimbo hilo lililokuwa likiongozwa na Wassira.

Hata baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, msuguano huo uliendelea na hata Wassira kwenda mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi kutokana na Bulaya kutangazwa mshundi.

“Sikutegemea kama Wassira angenishitaki, nilitarajia angenipa ushirkiano na kunipa uzoefu ili tufanye kazi nzuri ya kuwapatia maendeleo wananchi wa Bunda Mjini,” amesema Bulaya ambapo maelezo zaidi yamo kwenye gazeti la MwanaHALISI la Jumatatu wiki ijayo.

Ushirikina Watikisa Watumishi Serikalini

$
0
0
WANACHAPWA bakora, wakiwa wamelala ndani wanajikuta wapo nje bila kujua wametokaje. Hawa ni watumishi wa umma katika Mkoa wa Simiyu, anaandika Dany Tibason.

Hatua hiyo imeonekana kumkera Jumanne Sagini, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu ambapo amesema, kitendo cha wakazi hao kuwachapa watumishi hao na na kuwalaza nje kwa njia za kishirikina, kimesababisha wengi wahame mkoa huo.

Sagini ametoa kauli hiyo mjini hapa jana katika Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), alipopewa nafasi ya kueleza hali halisi ya mkoa huo kabla ya kamati kufanya mahojiano na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima.
Amesema, wakazi wa mkoa huo wamekuwa na tabia ya kuwachapa watumishi wa umma wakiwemo walimu hadharani mara wanapokiuka mila na desturi za eneo jambo ambalo ni kinyeme cha kanuni na sheria za utumishi wa umma.

Sagini ambaye, aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, alifafanua kuwa mbali na watumishi kuchapwa pia wamekuwa wakijikuta wamelala nje wakati wao walikuwa wamelala ndani.
“Mimi nilipofika pale nimekuta mambo hayo ambayo ni ya ajabu sana, nimewambia kamwe watumishi hawawezi kukaa na kufanya kazi huku mtabaki nyuma wakati wote.

“…, kama walimu wanawafundishia watoto wenu wanakuwa madaktari na vyeo mbalimbali serikali leo mnawachapa fimbo hadharani, nikawambia lazima mbadilike,”amesema.
Amesema, hali hiyo imesababisha mkoa na halmasauri zake za wilaya kukosa watumishi ambao ni wataalam na hivyo kuwa katika hali mbaya kiutendaji.

Katibu tawala huyo amesema, wamefika pale lakini hakuna wataalam wa kutosha na wachache waliopo  ni wageni na kwamba, wakipelekwa watalam wanakaa mwezi, miezi mwaka mmoja na baadaye wanaondoka kutokana na tabia za wakazi wa eneo hilo.

Amesema, kukosekana kwa wataalam, kumesababisha washindwe kuandaa vitabu vya LAAC, kushindwa kujibu hoja za Mkaguzi na Mhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), hivyo vitabu vilivyokuja mbele ya kamati yako ni vya hovyo kabisa wala havifai.

Hata hivyo, kamati hiyo ilishindwa kufanya mahojiano na halmashauri hiyo, kwa madai kuwa imejaa madudu, ubadhirifu hivyo kamati haiko tayari kuwahoji na kuishia kutoa maagizo.

Sagini aliomba nafasi ili atumie uzoefu alionao kwa kufanya kazi muda mrefu TAMISEMI, kushirikiana na watendaji waliopo ili waweze kuandaa upya vitabu vya LAAC, kujibu hoja za CAG na kuziwasilisha kwa CAG kwa ukaguzi na ndipo warejee tena kwenye kamati hiyo kwa mahojiano.
“Mheshimiwa mwenyekiti, nimeona nizungumze hali halisi iliyopo kwa utangulizi ili kamati yako ijue ni wapi pa kuanzia na kuishia, binafsi nimepitia vitabu hivyo sijaridhika kabisa, licha ya kuwa watendaji wanaweza kuwa wanajiamini na kuwa tayari kuhojiwa ila mimi nasema hakuna kitu hapa,”amesisitiza.

Kwa upande wake Daudi Nyalamu, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo amekiri kuwepo kwa vitendo hivyo katika eneo hilo ambapo ameahidi kukaa na wenzake na kubadili tabia hiyo na kuikomesha kabisa.

“Ni kweli kabisa kama alivyosema, RAS hali halisi ndivyo ilivyo, watendaji hawakai wanahama mara kwa mara hivyo utendaji kuwa mgumu, haya ambayo kamati mmetuagiza, tutakwenda kushirikiana na kuyafanyaia kazi,” amesema.

Rais Magufuli Ataka Jecha Apewe Tuzo

$
0
0
RAIS John Magufuli, amemtaka Dk. Ali Mohamed Shein, kumpa tuzo Jecha Salim, mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar, kutokana na kile alichokiita kazi nzuri aliyoifanya visiwani humo mwaka jana, kwa kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu, anaandika Pendo Omary.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo jioni, katika ziara yake ya kikazi visiwani Pemba. Wakati Rais Magufuli akichaguliwa katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, Dk. Shein alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar kufuatia uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi mwaka huu.

“Nampongeza sana Jecha kwa kazi nzuri aliyofanya kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, na kwa kweli Dk. Shein kama tuzo zako utakazotoa, naomba usimsahau kumpa na Jecha,” amesema Rais Magufuli.
Rai Magufuli pia amemtaka Rais huyo wa Zanzibar kumta
arifu yeye ili awashughulikie watu wote wanaomsumbua visiwani humo au wanaoonekana kumzidi nguvu.

“Rais Shein kama kuna mtu unaona anakusumbua wewe au anakupa tabu nijulishe mimi tu, hata dakika tano hazitapita nitamshughulikia,” ameeleza.

Kauli hiyo inakuja, ikiwa ni zaidi ya miezi kumi sasa tangu hali ya mahusiano baina ya wananchi wa Zanzibar iwe tete, tangu pale Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi visiwani humo (ZEC) alipotangaza kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Mahusiano hayo mabaya yamesababisha, wafuasi wa vyama vya CUF na CCM vyenye nguvu zaidi visiwani humo, kufikia hatua ya kusitisha ushirikiano katika shuguli za kiuchumi na kijamii ikiwemo kutohudhuria misiba na kutonunua bidhaa za mtu wasiyeendana naye kiitikadi.

“Niombe vyombo vya ulinzi na usalama wafuatilie hao wanaokatakata na kuchoma karafuu washughulikiwe bila huruma. Atakayejaribu kuichezea amani, atacheza yeye tena mchezo asiojua kuucheza,” ameng’aka Rais Magufuli.

Tangu kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana visiwani Zanzibar, hali ya usalama imekuwa si ya kuridhisha.

Nyumba na mashamba ya karafuu yamekuwa yakichomwa moto, huku baadhi ya watu wakilalamikia kukamatwa na kuteswa na vikosi vya ulinzi na usalama visiwani humo.

Kauli ya leo Rais Magufuli huenda ikachochea zaidi uhasama miongoni mwa wazanzibar, kwani inaonekana kulenga zaidi kuwashughulikia wapinzani wa chama tawala pamoja na Rais Shein kuliko kutafuta suluhu na maridhiano baina ya pande hizo mbili zinazohitilafiana.

Ukiamua Kukisemea Kila Kinachosikika Katika Uongozi wa Magufuli Utajitia "Stress" tu

$
0
0
Inahitajika nidhamu ya hali ya juu sana kifikra na kimaamuzi, kutoyumbishwa na habari zinazovuma kila kukicha katika taifa letu kwa sasa. Juzi UKUTA, jana kupatwa kwa jua, leo noti mpya kuchapishwa, kesho mtu kakamatwa kwa kumtukana Rais, hujakaa sawa mara wanafunzi hewa!

 Ukiamua kukisemea kila kinachosikika utajitia "stress" zisizo na sababu na utapoteza uelekeo. Huu ndio wakati unaohitaji kujipambanua na kujidhibiti, kwa sababu kinyume na hapo unaweza kugeuka mbwa unaehangaishwa na mifupa inayorushwa kila siku.(tena mingine kwa makusudi kukupoteza na kutafuta huruma zako). Ndio maana kwa sasa nimeamua kutohangaika kabisa na taarifa za habari hasa za kwenye TV!

 Kila siku ninashangilia maisha (huwezi kunikuta nikilalamika hata kwa bahati mbaya), kwa sababu ninajua(kwa uhakika kabisa) kwamba mabadiliko yamelifikia taifa kwa ajili ya manufaa yangu! Full stop! Mengine wanajua wenyewe wanaohusika nayo, hayanihusu!
 #SmartMind

Masanja na Mpoki Kimenuka Vibaya

$
0
0

Siku chache tangu m c h e k e s h a j i mwenye jina kubwa Bongo, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ auage ukapera kufuatia ndoa yake iliyozua gumzo, nyepesi nyepesi za mjini zinasema kuwa kutoonekana katika shughuli hiyo kwa msanii mwingine, Silvery Mujuni ‘Mpoki’ kunatokana na bifu zito lililopo kati yao, Risasi Mchanganyiko limedokezwa.

Mpoki na Vengu walikuwa ndiyo wasanii pekee wa kundi mahiri la vichekesho la Orijino Komedi ambao hawakutokea katika shughuli hiyo ambayo awali ilianzia katika Kanisa la Miito ya Baraka Kariakoo na baadaye katika Ukumbi wa Prime Rose, Mbezi Beach jijini Dar. Inafahamika kuwa Vengu ana matatizo ya kiafya na hajaonekana hadharani kitambo sasa.


KISIKIE CHANZO
 Chanzo chetu ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake, kilisema ilikuwa ni jambo la lazima kwa Mpoki kuwepo katika shughuli hiyo, kwani alikuwa jijini, lakini kuwepo kwa tofauti kati yao, kulisababisha mtangazaji huyo wa redio kwa sasa, kutoonekana kwenye harusi na tafrija ya memba mwenzake huyo, anayetajwa kuwa ndiye mwenye mafanikio zaidi kuliko wote ndani ya kundi lao. “Mimi nawaambieni Masanja na Mpoki kuna kitu. Jiulizeni kwa nini waigizaji wengine wa kundi lao walijitokeza kumsapoti mwenzao kwa kukata mauno kasoro lakini Mpoki hakuhudhuria wakati alikuwa hapahapa mjini akiendelea na mishemishe zake? Fuatilieni, kuna kaukweli,” kilisema chanzo hicho.

RISASI MCHANGANYIKO LAINGIA MZIGONI
Kufuatia madai hayo, gazeti hili liliingia mzigoni kufuatilia ukweli wa jambo hilo na sehemu ya kwanza, ilikuwa ni kwenye mitandao ya kijamii ambako lilihoji kulikoni Orijino Komedi? Katika mtandao mmoja maarufu Bongo, wachangiaji mbalimbali nao walionesha kuhoji sababu za msanii huyo, ambaye pia hujiita Mwarabu wa Dubai, kutoonekana, wakidai kuwepo kwa matatizo kati yao, yanayosababishwa na masilahi. “Ishu siyo Masanja na Mpoki ni Mpoki na Kundi la Orijino Komedi. Kundi linaonekana kama limekufa, hawatoi kazi mpya, kila mtu anaonekana kufanya kazi kivyake na  hawashirikiani katika shughuli za kijamii kama zamani,” aliandika mchangiaji mmoja katika mtandao huo. Mchangiaji mwingine alisema kuwa tatizo linalotokea ni ukweli kuwa Masanja Mkandamizaji, ambaye ni kinda katika sanaa kuliko Mpoki na Joti, amefanikiwa sana kutoka kimaisha kuliko wenzake, jambo linalowafanya waingiwe na kinyongo. Baada ya mitandao hiyo na kuona maoni hayo ya wachangiaji, gazeti hili liliamua kukata mzizi wa fitina kwa kujaribu kuwafikia wasanii hao ili kupata ukweli wao.

HUYU HAPA MASANJA MKANDAMIZAJI
“Mimi na Mpoki ni kama ndugu kaka, hakuna kitu kama hicho, siku ya ndoa yangu alikuwa na mambo yake binafsi, ndiyo maana hakuweza kutokea, lakini wengine walimuwakilisha, kwa hiyo hizo tetesi hazina mashiko kabisa,” alifunguka Masanja na kuongeza; “Madai ya kundi kumomonyoka pia hayana ukweli wowote, Orijino Komedi inaendelea na kazi zake kama kawaida, napenda kuwaambia tu Watanzania kwenye kundi letu kulikuwa na mlango wa kuingilia tu na hakuna wa kutokea, kama mnabisha au mnataka kuamini zaidi basi zungumza na msemaji wa kundi, Seki,” alisema.

MPOKI ASAKWA, AKAUSHA
 Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Mpoki kupitia simu yake ya mkononi, lakini haikupokelewa na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, alikataa kusema lolote, badala yake akajibu; “Namba ya Masanja hiyo muulize,” alisema huku akitoa namba ya muigizaji mwenzake huyo. SEKI SASA Kiongozi na msemaji wa kundi hilo, Sekioni David maarufu kama Seki, alisema kundi lao lipo imara ingawa ni muda mrefu hawajatoa kazi. “Wasanii wapo mapumziko na tunatumia muda huu ili kuboresha mikataba yetu ili tutakaporudi, tutakuja na kitu kingine tofauti kabisa.” Kuhusu kutoonekana kwa Mpoki harusini na kwenye sherehe, msemaji huyo ambaye pia ni msanii wa kuigiza sauti za watu, alisema; “Kwa nini humuulizi Vengu, kulikuwa na wawakilishi wake pale mbona huwasemi? Si unafahamu kama Mpoki pia ni MC? Siku hiyo alikuwa na kazi nyingine ndiyo maana hakutokea.”

Majambazi ‘Yatangaza Himaya yao’

$
0
0
Handeni. Siku moja baada ya majambazi kumuua mlinzi katika Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (Sekomu), Tanga, majambazi ambao idadi yao haijafahamika, wamefunga Barabara ya Segera – Chalinze katika Kijiji cha Kwachuma wilayani Handeni kwa zaidi ya saa mbili na kupora fedha na simu za abiria waliokuwa kwenye magari usiku wa kuamkia jana.

Katika tukio hilo, watu watano walijeruhiwa kwa mapanga na kupelekwa Hospitali ya Magunga Korogwe.

Juzi, majambazi yalivamia Sekomu na kulipua moja ya mabweni ya chuo hicho, kisha  kumuua Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Tele Security, Yohana Shemzigwa na kumjeruhi mlinzi mwenzake, Abuu Rajab.

Akizungumzia tukio la usiku wa kuamkia jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alisema majambazi hao walifunga barabara saa tano usiku kwa kutumia magogo kisha kuanza kuwapora mali watu waliokuwa wakipita kwa magari eneo hilo.

VIDEO: Alichokizungumza JPM Kuhusu Maalim Seif Kukataa Mkono wa Rais Shein

$
0
0
Kituo cha TV cha Azam TV kimeripoti kwamba September 3 2016 Rais Magufuli akiwa kwenye ziara yake visiwani Zanzibar ametoa hotuba ambapo amemshauri Rais wa Zanzibar kuwa mkali zaidi huku akizungumia tukio la Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif kukataa mkono wa Rais Shein wakati akimsalimia.

’Kama mtu anaukataa mkono wako na wewe kataa mkono wako kufanya mambo yake, ajifunze ajue mkono wako una thamani, haiwezekani mbele ya watu unashike mkono anakataa halafu unatoka ofisini unasema unasaini hapa hela ya huyu kwenda kutibiwa’:-JPM

Unaweza kutazama hii video hapa chini kutazama ilivyokua.

Mrisho Ngasa Atua Bongo..Hatma Yake Hii Hapa Baada ya Kuvunja Mkataba na Free State

$
0
0
Baada ya Mrisho Ngasa kukanyaga ardhi ya Tanzania maswali kwa wadau wa soka yamekuwa ni kutaka kujua kama mchezaji huyo wa zamani wa Yanga ataruhusiwa kujiunga na klabu yoyote itakayomuhitaji.

Sports Extra ya Clouds ilimtafuta afisa habari wa TFF Alfred Lucas ili kujua taratibu na kanuni zikoje endapo kama kuna timu itataka kumsajili Ngasa kwa ajili ya michuano ya ligi kuu Tanzania bara lakini hata ikibidi mashindano ya kimataifa.

Lucas amesema Ngasa ananafasi ya kujiunga na timu yeyote itakayomuhitaji huku usajili huo ukitakiwa kufanywa kabla ya Septembre 6.

“Hata sisi tumeiona taarifa ya Ngasa kuwa hana mkataba tena na Free State Stars sasa kwa usajili wetu wa hapa nyumbani anaweza akapata nafasi kwasababu dirisha la usajili la FIFA linafungwa September 6 na hii lazima ieleweke vizuri sana, kilichofanya Yanga achelewe wakati ule ni usajili wa ndani kwa maana ya kwamba sisi TFF tulifungua usajili wa ndani kuanzia 15 June -16 August lakini kwa upande wa kimataifa dirisha linafungwa September 6”, Alfred Lucas alikaririwa na Clouds FM kupitia Sports Extra.

“Kwahiyo kama itatokea timu inamtaka kwasababu kama ameshapewa barua ya kuachwa kwaiyo inaweza ikamlinda kufdanyiwa  usajili.”

Ngasa amerejea Tanzania September 3 akitokea South Africa ambapo alivunja mkataba wake na klabu ya Free State Stars inayoshiriki ligi kuu nchini humo.

Baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa jijini Dar, Ngasa hakuwa tayari kuzungumza lolote juu ya kuvunja mkataba na kurejea nyumbai badala yake akasema: “Nimerudi nyumbani kwa sasa imi ni mchezaji huru nimekuja kupumzika kidogo kisha nitasema nitaenda kucheza wapi.”
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images