Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Wanawake Waongoza Utoroshaji Dhahabu, Tanzanite Viwanja vya Ndege

$
0
0
SERIKALI imebaini kuwa asilimia kubwa ya madini aina ya tanzanite na dhahabu yanatoroshwa nchini na wanawake ambao huyavaa kwenye maeneo tofauti mwilini na kusema ni mapambo hivyo wanapopita kwenye mashine za ukaguzi katika viwanja vya ndege huwa vigumu kubaini kama ni utoroshaji.

Kutokana na hali hiyo, serikali imejipanga kudhibiti sonara mbalimbali nchini zinazotengeneza mapambo ya madini hayo kwa kuwa imebainika wizi mkubwa unafanywa na wao kwa kivuli cha kutengeneza mapambo.

Hayo yalibainishwa juzi jioni na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati akizungumza kwenye kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC1).

“Unakuta mama, amevaa madhahabu, bangili nyingi na vito vingine unadhani amejipamba kumbe ndio anatorosha madini yetu nje hivyo, huwezi kumzuia, sasa tumejipanga kushughulika na sonara, tumegundua wizi mkubwa wa madini hayo unafanywa huko,” alisema Profesa Muhongo.

Alisema pamoja na serikali kupunguza kasi ya wizi wa madini hayo, bado tatizo linaendelea na kwamba hivi karibuni Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) ulikamata tani 10 za madini zilizokuwa zikitoroshwa nje.

Alisema juhudi za serikali tangu mwaka 2012 zimekuwa zikifanywa za kuanzisha madawati kwenye viwanja vya ndege nchini yanayofuatilia na kudhibiti utoroshwaji wa madini na tangu kuanza kwa kazi kwa madawati hayo wamefanikiwa kudhibiti kiasi kikubwa cha madini.

Wakati Profesa Muhongo akisema hayo, Kamishna wa Madini nchini, Paul Masanja alizungumzia utoroshwaji wa madini hayo nje katika maeneo tofauti na kusema kiwango kinachotoroshwa ni kikubwa.

Alisema takwimu za mwaka 2013 zinaonesha kuwa asilimia 80 ya madini ya tanzanite yalisafirishwa nje ya nchi kwa njia za panya na kuzinufaisha nchi za Kenya ambayo ilisafirisha na kuuza tanzanite yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 100.

India nayo iliuza tanzanite yenye thamani ya Dola milioni 300 wakati Tanzania inayozalisha madini hayo ikiambulia Dola milioni 38 kutokana na mauzo ya nje ya madini hayo.

Akizungumzia sekta ya madini kwa ujumla, Profesa Muhongo alisema inawezekana kwa siku za nyuma nchi ilifanya makosa, lakini ni vyema wakaangalia hali ya sasa na baadaye ili kusifanywe makosa tena.

“Tuwe wakweli, inawezekana hapo zamani tulifanya makosa kwenye madini, lakini tunachofanya sasa ni kuangalia tulipo na baadaye ili tusifanye tena makosa, tunataka sekta hii ichangie mapato ya taifa kwa asilimia 10 kutoka asilimia 3.5 ya sasa,” alisema.

Alisema serikali inachofanya hivi sasa ni kusaidia Watanzania ambao ni wachimbaji wadogo wadogo wa madini ili wawe wa kati, kwa kuwawezesha zana za kisasa za uchimbaji ili wakuze uchumi wao na taifa badala ya kutegemea wachimbaji wakubwa kutoka nje.

Katika kutekeleza hilo, alisema Septemba 15, mwaka huu wachimbaji wadogo wataanza kupewa ruzuku ya vifaa hadi vya Sh milioni 200 kwa ajili ya kuwawezesha kuchimba kisasa na kuongeza mapato.

Kuhusu usambazaji wa umeme, Waziri Muhongo alisema kwa mwaka huu wa fedha 2016/17 bajeti ya ndani pamoja na wahisani kutoka nje ya nchi ya kusambaza umeme vijijini imefika Sh trilioni moja na hiyo ni hatua kubwa itakayofanya mapinduzi kwenye maeneo mengi vijijini.

“Tumepitisha kwenye Bunge la Bajeti la mwaka huu, tumetenga shilingi bilioni 535.4 sawa na ongezeko la asilimia 50 haya ni mafanikio ya REA II, na wahisani nje wametupa fedha na jumla ya bajeti kwa mwaka huu ya umeme vijijini ni trilioni moja,” alisema na kuongeza kuwa katika kutekeleza mradi wa umeme vijijini wa REA III, idadi ya wananchi watakaopata umeme itaongezeka.

Kuhusu sekta ya gesi, alisema hivi sasa asilimia 45 hadi 50 ya umeme unaozalishwa nchini unatokana na gesi, jambo lililookoa fedha nyingi ambazo zingetumika kuzalisha umeme wa mafuta.

Alisema faida za gesi nchini ni nyingi na kwamba matumizi ya gesi katika kuzalisha umeme yamesaidia kuwapunguzia wananchi mzigo kwa kufuta tozo ya huduma kwenye manunuzi ya umeme na pia kwa wateja wapya wanaoomba kuunganishiwa umeme kwa mara ya kwanza, hawalipi fedha za fomu ya maombi.

Akizungumzia kwa mara nyingine mabadiliko ndani ya Shirika la Umeme (Tanesco), Profesa Muhongo alisema ni lazima lifanyiwe mabadiliko makubwa ili liende na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano.

“Sitaki kuzungumza mengi hapa kuhusu Tanesco, lakini kwa muundo wake na utendaji wake na huku tunakokwenda lazima lifanyiwe mabadiliko makubwa sana, itakuwa Tanesco inayochapa kazi kwa kasi yetu, isiyo na rushwa, wizi, uzembe iko njiani inakuja hiyo,” alisema.

Akizungumzia mafuta na gesi alisema ili nchi iwe ya uchumi wa kati, taifa linategemea uchumi wa gesi na viwanda na kwa kuanza kiwanda cha mbolea kitajengwa Kilwa mkoani Lindi kwa ushirikiano baina ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na majadiliano yako kwenye hatua nzuri na wadau wakiwemo Ujerumani, Denmark na Pakistan.

Baada ya ujenzi wake kukamilika, alisema kwa siku kitazalisha mbolea tani 3,850 na uzalishaji huo utasaidia kuboresha sekta ya kilimo na hivyo kuisaidia pia sekta ya viwanda.

Jipatie Dawa Asili za Kutengeneza Shepu, Kuondoa Michirizi Chunusi, Kurefusha Nywele Toka Markson Beauty Products

$
0
0
HABARI NJEMA MARKSON BEAUTY PRODUCTS
Baada ya kupata cheti cha bidhaa bora kwa mwaka 2015-2016, Sasa kampuni hii inasambaza huduma zake ndani na nje ya nchi kwa vibali maalum. Bidhaa zetu zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa. Hazina kemikali wala madhara. DAWA ZETU NI YA:-

  1. kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @100,000/=
  2. Kuongeza shepu (hips na makalio) kwa/= (a)Dawa ya kunywa au kupaka @150,000/=(b)Vidonge @170,000/=
  3. Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:- (1)Mafuta @100,000/= (11)Vidonge @150,000/=
  4. Kupunguza unene na manyama uzembe @120,000/=
  5. Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-(a) Gely ya kupaka @100,000/= (b) Vidonge maalum @120,000/= (c) Handsome up original @170,000
  6. Kuondoa mvi milele zisiludi tena @100,000/=
  7. Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito @120,000/=
  8. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:- (a) Dawa ya kunywa au kupaka @120,000/= (b) Mkanda wa kawaida @100,000/= (c) micro-computer belt unaovaibret @200,000/=
  9. Kupunguza maziwa na kuyasimamisha @90,000/=
  10. Kushepu miguu na kuwa minene @100,000/=
  11. Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @90,000/=
  12. kubana uke na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke @100,000/=
  13. Taiti za hips na makalio @150,000/=           
NB: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii kwa bidhaa halisi. Wasiliana nasi :-(+255) 0767447444 na 0714335378 Google MARKSON BEAUTY.
Follow us
@Markson_beauty_pr
@Markson_beauty_pr

KISA Cha Kusikitisha 'Baba Yangu Alisababisha Nilale na Mjomba Wangu, Kamwe Sitamsamehe'

$
0
0
Nimeona leo nitoe siri yangu hapa ya muda mrefu ambayo imekuwa ikiniumiza sana pale tu ninapokumbuka, nakosa raha na amani inapotea.

Kwa ufupi kabisa, nilizaliwa mkoani Mara wilaya ya Musoma mjini maeneo ya Nyakato, mama yangu alibeba mimba yangu akiwa darasa sita hivyo hakumaliza shule. Ilibidi akae nyumbani mpaka pale alipojifungua, kwa wakati kulikuwa hakuna sheria kali kwa wanaowapatia wanafunzi mimba wakiwa shule. Na aliyempatia hiyo mimba naye alikuwa mwanafunzi mwenzake lkn alikuwa la saba yeye alimaliza shule. Baba yake mama ambaye ni babu yangu alikuwa na uwezo mkubwa hivyo hakushindwa kutulea mimi na mama.

Nikiwa na miaka 6 ndipo nilipokuja kumjua baba yangu wakati huo nae alikuwa amekuwa mtu mzima, alikuja akanisalimia akaondoka, kwao pia walikuwa vizuri kimaisha.

Nikiwa na miaka 9 naanza darasa la kwanza wakati huo tulikuwa tunaingia shule tukiwa na umri mkubwa tofauti na sasa. Mama aliolewa na mume mwingine na alikuwa ni askari jeshi, alifanikiwa kuzaa nae watoto wanne jumla kwenye familia yetu tukawa 5 wasichana tukiwa wawili na wavulana wakiwa 3. Tuliishi vizuri sana, na familia ilikuwa na furaha sana na hatimaye tulijenga nyumba nzuri sana mtaa wa Majita road hapo hapo musoma. Nakumbuka nikiwa darasa la sita babu yangu kizaa mama alifariki duniani na ndiye aliyekuwa tegemeo la familia ya kina mama. Pia wakati huohuo baba yangu wa kufikia walikorofishana na mama kupelekea mpaka wakaachana na alihamishwa kuja Dar es salaam Lugalo. Sisi tulibaki Musoma tukiendelea na maisha.

Kumbuka wakati wote huo baba yangu mzazi ajaonekana kwa kipindi kirefu. Kwa upande wangu si kuwa na shida na nilifika mahali nikamsahu kabisa. Mama alikuwa anajituma sana alikuwa ana hotel yake hapo hapo Musoma hivyo alivyoachana na baba yangu wa kufikia akutetereka kiuchumi. Nilisoma na Mungu alinijalia kichwani nilikuwa vizuri toka darasa la kwanza nilikuwa nashika nafasi ya kwanza nikishuka sana nafasi ya pili mpaka la saba. Baada ya kuhitimu la saba Mungu alinijalia nikafahulu vizuri na kuingia kidato cha kwanza.

Wakati nikiwa kidato cha pili baba alikuja kutoka Arusha maana alikuwa anakaa huko, alipokuja alinikuta naendelea na masomo yangu vizuri. Alifika mpaka nyumbani nakumbuka mama alipomuona alimfukuza, wakaja watu kusuluisha na wazee kwamba ampe nafasi ya kumuona mwanae mama alikataa. Akamwambia wakati huo alikuwa wapi? Basi siku moja niko shule maana nilipangiwa hapo hapo Musoma sekondari, alifahamu ninapo soma kaja kaulizia walimu akanipata, niliitwa darasani nilipotoka nikamuona lakini sikumjua vizuri maana ni siku nyigi sana. Akanambia ni baba yako kwani umenisahau? Nilikataa kuongea lakini alinisihi sana mwisho nilikubali kuongea nae wakati anaondoka akanipa laki moja za matumizi akaondoka. Nilipofika nyumbani nilimpa mama hiyo pesa alishangaa nimetoa wapi, nikamwelezea yote basi mama akapokea. Kesho baba akaja akaomba msamaha hapo mama akamwambia kikubwa nataka umsaidie mwanao basi. Basi baba akaondoka.

Nilipofika kidato cha tatu mama alianza kuugua sana, tukaanza kuzunguka mahospitali kila akipimwa hakuna ugonjwa, tukaenda Bugando ugonjwa haukuonekana, tukaenda Muhimbili pia ugonjwa akuonekana kumbuka mama ndiye tegemeo la familia pesa za matibabu zilitoka kwake mpaka ikafikia hatua tukafilisika hotel ikafungwa hali ikawa mbaya sana. Tukaanza kuishi kwa shida sana. Tukashauriwa twende kwa waganga tukazunguka, alikuwa anapata nafuu kidogo kisha ugonjwa unarudi tena. Nikaanza kumtafuta baba ili atusaidie kila nikiongea nae kwa njia simu anatoa ahadi tu mwisho nikakata tamaa. Kwa baba wa kufikia aliyoko Dar nae alikuwa kimya sana alisahau hata familia yake kabisa. Hivyo tulikata tamaa kabisa na mababa hawa. Tukaamua kuishi maisha yetu bila kutegemea wao tena.

Nilisoma kidato cha nne kwa shida sana, tukitoka shule mimi na wandogo zangu tunaenda kutafuta vibarua vya kufanya ili tupate kula. Mpaka nikamaliza form 4, baada ya matokeo kutoka nikawa nimefahuru vizuri nikapagiwa shule ya advance huko Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro. Hapo ndipo ilikuja kesi ni wapi pa kupata pesa ya shule. Jamani umasikini mbaya sana, kama ujapitia mshukuru Mungu sana. Mama yangu wakati huo hali yake iliendelea kuimarika baada kwenda kwenye Maombi. Tuliangaika sana na mama lakini hatkufanikiwa kupata pesa ya kutosha.

Namshukuru Mungu kwa kipindi chote hicho sikuwahi kukutana na mume japo nilikuwa mzuri mtaani kwangu, walinisumbua mpaka waume za watu lakini hawakunipata. Lkn nilipata wazo nikasema baba yangu yuko Arusha na mm nimechaguliwa Mkoa wa Kilimanjaro ni mikoa iliyokaribu. Nilimpigia simu nikaongea nae nikamwambia nimefahalu lkn sina pesa akasema wakati unakuja shule pitia hapa Arusha nitakupa pesa za shule. Basi nikaona unafuu mkubwa, nikajianda maana muda ulikuwa ushafika. Arusha huko alikuwepo mjomba wangu tumbo moja na mama alikuwa askari wa FFU hapo Arusha lakini alikuwa na roho mbaya sana hawezi kumpa mtu msaada kirahisi. Nilimtaarifu pia kwamba nitakuja na nitafikia kwake alikubali.

Siku ya safari nilimtaarifu baba akasema sawa, nikamwambia nitafikia kwa Mjomba alafu ndio nakuja kwako kuchukua pesa za shule, tukakubaliana. Nilipofika Arusha majira ya saa 2 usiku mjomba alikuja akanipokea akanipeka kwake, mjomba alikuwa na mke na watoto wa 3, ila wakati nafika nilikuta mke wake ameenda kwao likizo, yupo mfanyakazi wa ndani na watoto, cha ajabu nilianza kutafuta baba kwenye simu akupatikana tena.

Nilikaa kwa mjomba siku 4 bila baba kupatikana kwenye simu sikuwa na pesa yoyote. Ikabidi nimwombe mjomba anisaidie angalau kidogo niende shule baba akipatikana akinipa nimrudishie mjomba alikataa katakata. Niliwaza sana sikujua ninzie wapi nilikata tamaa ya kusoma tena, ikabidi nimwombe mjomba nauli ya kurudia kwetu Musoma napo aligoma akasema subiri mpaka baba yako apatikane. Siku moja jioni katoka kazini akaniita chumbani kwake nilishutuka lakini akasema njoo nikupe pesa za shule, kweli nilipoingia ndani akanipa laki tatu, nikamshukuru sana sikuamini, nilipotaka kuondoka akanishika mkono akanitazama akanimbia naomba nilale na wewe usiku wa leo, niliogopa na kushituka sana, alifunga mlango akanitishia mwisho nilipoa akafanya anachotaka kufanya, aliniumiza sana maana sikuwahi kufanya kideto hicho. Baada ya kumaliza akanipa hizo pesa nikajianda kwenda shule kabla sijaenda akanifanya tena alinigeuza mke wake, sikumwambia mama yangu chochote maana angesikia yawezekana angekufa kabisa. Lakini yote hayo kwa sababu ya shida.

Nikafanikiwa kwenda shule, nilisoma vizuri na mjomba akawa anakuja hapo shuleni kuniletea pesa za matumizi siku za Jumapili nakunichukua kwenda gesti, maisha yangu yalikuwa hayo mpaka namaliza kidato cha sita, nikarudi nyumbani Musoma mama alifurahi sana aliposikia mjomba alinisomesha, lakini nilikuwa siri yangu. Mjomba alitaka nilirudi tena Arusha huku nikisubiri kwenda chuo kikuu. Nilikataa kabisa na mimi nilikuwa tayari nimetimiza malengo ya kishule sikuwa na hamu tena bali niliendelea kujutia dhambi niliyofanya.

Mungu alisadia nikapangiwa chuo cha Dar es salaam, nilipata mkopo hivyo ulinisaidia mpaka namaliza chuo, nikakutana na rafiki wa kiume mwanachuo mwenzangu, tulipohitimu tulifunga ndoa na sasa tuna watoto 2. Hii ni siri kubwa sijahawahi mwambia mume wangu. Baba aliposikia nimemaliza chuo akajitokeza, nilifukuza kwangu na kamwe sitaweza kumsamehe katika maisha yangu.

Chama cha Wananchi CUF chamtaka Rais Magufuli aache kutumia madaraka vibaya

$
0
0
Chama cha Wananchi CUF chamtaka Rais Magufuli aache kutumia madaraka vibaya na kumwambia stahiki anazopewa Maalim Seif zipo kisheria.

Wamesema Kitendo cha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar kushiriki mkutano wa CCM ni ushahidi tosha kuwa tume ya uchaguzi si chombo kilicho huru.

Inawezekana Hatumuelewi Rais Dkt. Magufuli..ila yeye Anazidi Kuchanja Mbuga

$
0
0
Amani iwe kwenu!

Nimejaribu kutafakari kidogo juu ya kauli kadhaa za rais wetu akiwa katika baadhi ya ziara na kubaini kitu..
1. Inawezekana kauli tata za mh. ni za makusudi na zinalengo la kubadili sura nzima ya siasa tulizozoea..Hii nikiwa na maana kwamba wakati tukiwa bize kujadili kauli tata hizo teyari yeye anapata mwanya wa kufanya mambo ya msingi ambayo anatarajia kuyafanya!Ni kama unaweka nyama na wakati huo huo unampigia mluzi mbwa..lazima aweweseke!

2.Kauli zake nyingi pia zina vichekesho na mikwara mingi..Hii mikwara inaweza kuwa na lengo la kuwaweka sawa watendaji au watu waovu!Kwa jinsi navyoona haya yote anayafanya makusudi kwa kuamini kwamba meseji zinafika na watu wanamsikiliza neno kwa neno!

3.Kwa kuzingatia kuwa watanzania na wanasiasa ni watu wa porojo na propaganda basi naona anacheza kama pele kwenye hili na wanasiasa wengi hawajamstukia!Vyama vya upinzania visipokuwa makini vitabaki kujadili hotuba zake badala ya kujikita kwenye main agenda za vyama vyao..

4.Pia muheshimiwa kuna wakati kwenye hotuba mambo ya sirini huyaweka wazi wazi..Nahisi anafanya makusudi kuwa hata wale wanaofanya maovu na kusitiriwa kisiasa basi kuna siku watawekwa hadharani..amefanya watu wa deal na wala rushwa kubwa kuwa waangalifu maana kuna siku wanaweza kusemwa hadharani..Miaka ya nyuma hatukuzoea hii na tunaona kama wanadhalilishwa..

5.Tukumbuke rais wetu ni msomi wa Phd na si bure lazima huwa anajitafakari baada ya hotuba zake lakini pamoja na hilo bado wimbi la kauli tata linaendelea na bila shaka ni makusudi kwa lengo maalum kwa kuzingatia aina za siasa tulizozoea..Yaani huwa anapiga pale pale tunapoona amekosea au atakosea na mbaya zaidi huwa haachi kurudia pale anapoona watu wamekwazika!

Kitu ninachokiona ni kuwa rais anataka kututoa kwenye aina za siasa tulizozoea,yaani analeta a new era of politics!Wito wangu kwa viongozi wa upinzani na wanaharakati kama kweli mnataka kuisaidia hii nchi mjikite kwenye ajenda zenu na si hotuba zake kwa vipande hasa vyenye utata!Atawapoteza na wakati huo huo yeye anaendelea kuchanja mbuga kisiasa na kwenye ajenda zake..In short I can call him as a game changer and a smart president..

By Sonaderm/JF

Polisi Wafyatua Risasi na Mabomu ya Machozi Kuwatawanya Wafuasi wa Prof. Lipumba

$
0
0
Jeshi la Polisi limelazimika kufyatua risasi angani na kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Prof. Lipumba waliokuwa wakimzuia mwenyekiti wa muda wa CUF, Julius Mtatiro, kuingia ofisini eneo la Buguruni.

Wafuasi hao wameeleza kuwa wameamua kumzuia kwani Msajili wa Vyama vya Siasa ametaka shughuli zozote ndani ya CUF zisiendelee hadi hapo mgogoro wa uongozi utakapotatuliwa.

Itakumbukwa hivi karibuni CUF kilimteua Julius Sunday Mtatiro kuwa mwenyekiti wa muda baada ya mwenyekiti aliyekuwepo, Prof. Lipumba kijiuzulu Agosti 2015.

Julius Mtatiro leo amefanya mkutano na waandishi wa habari  katika ofisi za Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam ili kuzungumzia kauli zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiwa visiwani Zanzibar.

CUF Wamjibu Rais Magufuli, Wadai Maalim Seif Hawezi Kubembeleza Haki yake ya Kikatiba

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​
Imetolewa leo Tarehe 4/9/2016​


MWENYEKITI WA CCM, RAIS JOHN MAGUFULI AACHE KUTUMIA MAMLAKA YAKE VIBAYA AHESHIMU MISINGI YA HAKI,DEMOKRASIA, KATIBA NA SHERIA ZA NCHI YETU​
Waheshimiwa wanahabari,
Awali napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru kwa kuitikia wito wetu, nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kutupasha habari mbalimbali zinazohusiana na hali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ndani ya nchi yetu na nje ya mipaka yake.
Lakini pia kuwapa pole kutokana na namna mnavyotekeleza majukumu yenu katika mazingira magumu ya hofu na vitisho vinavyofanywa na watendaji wa serikali ya awamu ya tano.
Nitumie fursa hii pia kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza rasmi kuzungumza na vyombo vya habari toka BARAZA KUU LA UONGOZI CUF TAIFA liniamini na kunipa dhamana kubwa ya utendaji na usimamizi wa chama chetu kwa kuniteua kuwa MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI WA CHAMA CHETU CHA WANANCHI CUF TAIFA, tukisimamia majukumu yaliyopaswa kufanywa na Mwenyekiti wa Chama Taifa na Makamu Mwenyekiti Taifa.
Naahidi nitatekeleza wajibu wangu kwa uaminifu mkubwa na weledi wa hali ya juu kwa madhumuni ya kuwaletea watanzania mabadiliko sahihi ya maendeleo ya kisiasa na kiuchumi wanayoyataka katika Taifa letu.

Waheshimiwa wanahabari,
Tumewaiteni na kuomba kuzungumza nanyi kwa lengo la kujibu kauli zilizotolewa na Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli alizozitoa juzi na jana (tarehe 2-3/9/2016) katika mikutano ya hadhara aliyoifanya katika kisiwa cha Pemba, uwanja wa Gombani na Unguja katika uwanja demokrasia (Kibandamaiti) na kupitia nyinyi tufikishe ujumbe wetu kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais JOHN MAGUFULI na watanzania kwa ujumla. Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amezungumza mambo mengi na pia amejikita katika kutoa kauli za dhihaka na mipasho dhidi ya Chama cha Wananchi CUF na katibu mkuu wetu Maalim Seif Sharif Hamad jambo ambalo tunaamini kwa hadhi na heshima ya nafasi yake na hadhi ya taasisi ya urais hakupaswa kufanya hivyo kama kiongozi wa nchi.
Pamoja na masuala mengine Mwenyekiti wa CCM, Rais JOHN MAGUFULI amesema amekwenda kuwashukuru wananchi wa Unguja na Pemba kwa kumchagua yeye pamoja na Dokta Ali Mohamed Shein, amewahahakishia Wazanzibari kuwa atailinda amani ya nchi kwa nguvu zake zote na yeyote atakayejaribu kuivuruga amani atamshughulikia kwa nguvu zake zote bila huruma, ataulinda Muungano kwa nguvu zake zote na lazima uendelee kudumu katika kipindi chote cha utawala wake.
Tatu, amezungumzia maendeleo – Maji, viwanda, miundombinu, uvuvi na kadhalika lakini pia amezungumzia kuitunza amani akitolea mifano ya nchi zisizokuwa na amani ikiwemo Libya, Iraq, Syria, Somalia na mauaji ya kimbali yaliyotokea Rwanda mwaka 1994.
Magufuli amepongeza aliyooiita “kazi nzuri ya majeshi” nadhani kwa kuisaidia kupata ushindi na kuwathibiti wanaotaka mabadiliko na amempongeza Jecha Salim Jecha, Mwenyekiti wa ZEC, kwa kufuta uchaguzi wa tarehe 25/10/2016 uliompa ushindi Maalim Seif Sharif Hamad, na kumuombea apewe tuzo kwa kazi nzuri aliyoifanya.
Anashangaa kwanini Dokta Shein ameunda serikali kwa kuvishirikisha vyama vingine wakati alishinda (Shein) kwa asilimia 99 huku akijigamba kuwa yeye kamwe hawezi kuingiza na hataingiza mtu hata mmoja kutoka upinzani katika serikali yake pamoja na kupata ushindi wa asilimia 58 anasahau kuwa hivi karibuni amemteua Mwenyekiti wa TLP Mhe. Agustino Lyatonga Mrema, kuwa Mwenyekiti wa bodi ya PAROLE.

MSIMAMO WA CUF JUU YA KAULI ALIZOZITOA RAIS MAGUFULI:

1. THE CIVIC UNITED FRONT (CUF CHAMA CHA WANANCHI) kimesikitishwa na kauli zisizofaa kwa heshima na hadhi ya taasisi ya urais na nafasi yake kama kiongozi wa nchi kutoka kauli za uchochezi, kupandikiza chuki na uhasama, kuwagawa wananchi na kutaka kujenga chama chake kwa njia ya vitisho na kutumia vyombo vya dola.
Tunamtaka Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli atambue kuwa hatoweza kujenga umoja wa watanzania kwa kutoa kauli za kuimarisha chuki, uhasama na kutosimamia haki, na kuunga mkono vitendo vya uvunjaji wa demokrasia na sheria za nchi.
Rais Magufuli hawezi kuwa mfano wa kuigwa kwa vizazi vijavyo katika mikakati ya mataifa masikini ya kulinda sheria, haki za kiraia, utawala bora na kuleta maendeleo shirikishi (Inclusive Develeopment).

2. Kauli nyingi za kuchochea chuki na uhasama alizozitoa Rais Magufuli si za kwanza wala si ngeni kwa Wazanzibari. Kisiasa wazanzibar na hasa wafuasi wa CUF (ambao ni wengi) wamekuwa waathirika wakubwa wa matumizi makubwa ya ukandamizaji na unyanyasaji iunaofanywa kikatili sana kupitia MAJESHI, MAZOMBI, JANJAWIDI nakadhalika.
Mauaji yaliyofanywa na Serikali ya CCM chini ya utawala wa serikali ya awamu ya Tatu iliyoongozwa na Benjamini William Mkapa Januari 26-27, 2001 yalisababisha watu 46 kuuliwa na vyombo vya Ulinzi, watu 38 wameuwawa kwa kificho mpaka leo hawajaonekana. Watanzania 658 waliojeruhiwa, na 135 waliopata vilema vya kudumu katika maisha yao.
Aidha zaidi ya wazanzibar 4000 waliishi kama wakimbizi Shimoni, Mombasa nchini Kenya, orodha yao tumeiambatanisha na taarifa hii. Kama kweli Rais Magufuli anataka kulinda amani ya Tanzania haiwezekani kuwa raia wamekuwa wakipigwa na kuteswa na kukatwa viungo vyao na kuporwa mali zao na vikosi vya majeshi, Mazombi na akiwa kimya na kutoa kauli za kubariki vitendo hivyo.
Kwa mtizamo wa Magufuli, ukatili na uhuni unaotendwa na MAZOMBI ukiungwa mkono na vikosi vya majeshi ya SMZ na vile vya Muungano eti ndiyo ulinzi wa amani. Lakini, Kauli mfano wa hizi zimewahi kutolewa na watangulizi wake na viongozi wa Zanzibar waliopita.
Hata hivyo mwisho wa yote hawakuweza kufanikiwa kuwahadaa wazanzibari kudai haki yao na mwaka hadi mwaka wazanzibar wanaotaka mabadiliko wawekuwa wakiongezeka na kuidhihirishia dunia kuwa hawawezi kuvunjwa moyo na vitisho, hujuma na ukandamizaji.

3. Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amemsifia Dokta Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa kuwa Rais wazanzibar kwa kura nyingi. Jambo hili linachekesha na kustaajabisha dunia, kwani Hata mtoto mdogo anayeishi Zanzibar au Tanganyika anatambua kuwa Dr. Shein si rais halali wa Zanzibar.
Ni rais aliyeingizwa madarakani kwa kile kinachoweza kuitwa “tyranny of the highest order of the African Power Mongers who are ready to shed blood for power” yaani “udhalimu wa kiwango cha juu kabisa kinachofanywa na viongozi waroho wa madaraka ambao wako tayari kumwaga damu ili watawale”.
Katika uchaguzi halali wa tarehe 25/10/2016. Wazanzibar walimchagua kwa kura nyingi kabisa, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa Rais wao. Wazanzibari wanajua hivyo, Watanzania wanajua hivyo, Waafrika wanajua hivyo na dunia inaimba wimbo huo. Kujidanganya kuwa Dokta Shein ni rais halali wa Zanzibar ni uotaji wa ndoto ya mchana kuwa Tanzania ina viwanda kila kata na kila kijiji, ndoto ambayo kwa aina ya uongozi wa John Magufuli haiwezi kutimia.

TAKWIMU ZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA TAREHE 25/10/2015:

Wapiga kura wote wa NEC Zanzibar ni 417,882. Kura alizopata LOWASSA 211,033 = 50.05% kura alizopata MAGUFULI ni 194,317= 46.50% Ushindi wa kura za lowassa dhidi ya Makufuli ni 16,721.

ZEC wapiga kura wote ni 402,354. Kura alipigiwa Maalim Seif ni 207,847 =53.32%. kura alizopata Dokta Ali Mohamed Sheni ni 182,011 =46.68%. Ushindi wa Maalim Seif Sharif Hamad dhidi ya Dk Sheni ni kura 25,836.

Kwa matokea haya ni wazi kuwa Wanzanzibar wameikataa CCM. Wazanzibar hawakuwachagua wagombea wa CCM John Magufuli na DK Shein wake.

4. THE CIVIC UNITED FRONT (CUF CHAMA CHA WANANCHI) kinaendelea na msimamo wake uliotolewa na kikao cha Baraza KUU la uongozi Taifa kilichofanyika tarehe 2-3 April, 2016 wa kutoyatambua matokeo ya uchaguzi huo haramu na batili, na kwa msingi huo halimtambui Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar, haliwatambui waliotangazwa kuwa Wawakilishi na wala haliwatambui waliotangazwa kuwa Madiwani. Baraza Kuu linaungana na wananchi wa Zanzibar waliokataa kuwapa uhalali watu hao na kwa hivyo halitoitambua Serikali, Manispaa na Halmashauri za Wilaya zitakazoundwa na watu hao.
CUF itaendeleza msimamo wake wa kutoshirikiana na Serikali haramu iliyoundwa na dokta Shein kutokana na uchaguzi batili uliofanyika kinyume na Katiba ya Zanzibar, kinyume na Sheria ya Uchaguzi.
Kwa vyovyote vile, Serikali ya dokta Shein haitakidhi matakwa ya Katiba ya Zanzibar na hivyo CUF haitoshiriki kwenye uvunjaji wa Katiba ya nchi.

5. Chama Cha Wananchi CUF, kinaendelea na msimamo wake wa kuutambua uchaguzi mkuu uliokuwa halali, huru, wa haki na uliofanyika katika hali ya amani na utulivu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na pia linayatambua matokeo yake ambayo yanaonyesha wazi kwamba chaguo la Wazanzibari ni CUF na Maalim Seif Sharif Hamad Kitendo cha zaidi ya asilimia 80 ya Wazanzibari kususia uchaguzi haramu na batili wa tarehe 20 Machi, 2016 kimezidi kuyapa nguvu maamuzi yao ya tarehe 25 Oktoba, 2015 mbele ya macho ya Watanzania na kwa Jumuiya ya Kimataifa.
Chama cha CUF na Viongozi wake hawawezi kuyumbishwa na watu wenye weledi mdogo sana na siasa za Zanzibar, kama alivyoonesha Rais John Pombe Magufuli. Vitisho vyote vilivyotolewa na Magufuli dhidi ya wanaosimamia HAKI SAWA KWA WOTE na misingi ya kidemokrasia, havitarudisha nyuma juhudi za kuijenga Zanzibari na Tanzania mpya.

6. Tunamtaka Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli afahamu kuwa stahiki zote anazopewa Maalim Seif zipo kisheria kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama wanavyopewa viongozi wastaafu wengine hapa nchini.
Stahiki hizo si hisani inayotoka mfukoni mwa kiongozi yeyote Yule. Wala si fedha za CCM, ni fedha za watanzania zinazotokana na makusanyo ya kodi zinazolipwa na wananchi.
Sheria ya Mafao ya Viongozi wastaafu wa Kisiasa ya Zanzibar (The Political Leaders Retirement Benefits Act) namba 6 ya mwaka 1999 iliyopitishwa na Dr. Salmin Amour tarehe 15 Mei 2000) imeeleza wazi kuwa viongozi wote wa kisiasa waliohudumu katika serikali ya Zanzibar kuanzia mwaka 1995 kwenda mbele watakuwa na haki isiyoondolewa kwa namna yoyote, ya kupokea stahiki zote muhimu kama viongozi wastaafu.
Rais Magufuli amekuwa rais wa kwanza Tanzania mwenye kutoa kauli zenye ukakasi kwa jamii, zenye kugongana na tabia ya kufanya maamuzi bila kuangalia katiba na sheria za nchi. kwake yeye urais siyo taasisi, ni mtu, kwa Magufuli urais ni ubabe, dhuluma, vitisho, kukandamiza na kutojali katiba na sheria za nchi.
Huenda Taifa letu limepata janga kubwa la kitaifa katika awamu hii ya uongozi wa nchi. Ni jambo la aibu sana kuona rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavunja sheria za nchi yake na anamhamasisha rais wa Zanzibar afanye kama anavyofanya yeye.

7. Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli anazungumzia kulinda amani bila kuzungumzia kulinda haki. Na wakati huo huo anachochea matumizi makubwa ya kijeshi yasiyozingatia sheria kwa wananchi. Mifano aliyoitoa ya nchi zilizoingia katika uvunjifu wa amani haina uhusiano kabisa na masuala yanayoendelea katika nchi yetu.
Rais Magufuli anasahau kuwa nchi hizo anazozitolea mifano, ziliharibiwa kwa sababu ya kuwa na viongozi walioamini katika nguvu za kijeshi (kama yeye) kuliko uongozi wa kidemokrasia na wa kufuata sheria. Raia wa nchi hizo anazozitaja Magufuli walinyimwa haki za msingi za muda mrefu na watawala ndipo wananchi walipoanzisha harakati za kujikomboa, majeshi yaliyoziunga mkono hayakuweza kuzima nguvu ya mabadiliko.
Ni jambo lisilokubalika hata kidogo kuwa na rais ambaye kila kukicha mahubiri yake ni namna gani “majeshi yake yatawashughulikia raia wa nchi yake”.
Hizi ni hotuba zinazowafanya wananchi wajiandae kisaikolojia kupambana na majeshi yao. Watanzania hawakumchagua Magufuli ili ayaandae majeshi kwa ajili hiyo, alikabidhiwa nchi hii ikiwa na amani na CUF haitakuwa tayari kumuona anaiingiza katika migawanyiko, vitisho na visasi ambavyo vinaweza kuzaa machafuko.

8. Kitendo cha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar –ZEC (Jecha SALIM Jecha) kuhudhuria na kushiriki katika mkutano wa CCM uliofanyika Unguja ni ushahidi tosha kuwa tume ya uchaguzi ya ZEC si chombo kilicho huru na kwamba tume hiyo ipo hapo kuhakikisha kuwa Serikali ya CCM haiondolewi madarakani na wananchi wanaotaka mabadiliko ya uongozi wa kisiasa nchini na kwamba ZEC ni tawi la CCM linalotekeleza matakwa yao.
Kwa msingi huo huo, CUF na vyama vingine ambavyo vinapigania mabadiliko hapa Tanzania vitaendeleza mipango imara ya kupigania kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi Zanzibar na Tanzania Bara (NEC na ZEC).
Ni jambo lisilokubalika hata kidogo kujisifia ushindi wa kupora katika uchaguzi kutokana na kupendelewa na Tume ya Uchaguzi ikishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

9. Tunamtaka Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli atambue kuwa; CUF ni taasisi kubwa ya kisiasa nchini iliyo na wawakilishi wa kuchaguliwa na wananchi kutoka kila kona ya nchi yetu, CUF ina wabunge 18 kutoka Pemba, inawabunge wanne (4) kutoka unguja, inawabunge 10 kutoka Tanzania bara.
CUF ni chama cha kitaifa kweli, na tangu mwaka 1995 mpaka sasa CCM haijawahi kupata kiti hata kimoja cha uwakilishi toka Pemba. Magufuli asaidiwe na chama chake, kwamba matamanio yake ya kuifanya Tanzania iwe nchi ya mapambano ya kijeshi na raia hayatafikiwa.
Akumbushwe kuwa kauli zake zimejaa uchochezi wa kila namna anajaribu kuwaghadhibisha wananchi (Provoke), ghilba za kisiasa za waziwazi na nia ovu iliyojaa visasi. Kauli za namna hii akiendelea kuzitoa katika kipindi cha miaka yake mitano, ataimaliza huku kila mtanzania akijiridhisha kuwa nchi ilipata rais ambaye hakujua nini maana ya urais, na kwa vyovyote vile hakuwatendea haki waliomchagua.

Mwisho:

Sote tunatambua kuwa Serikali ya CCM kwa kumtumia Mwenyekiti wake, Rais John Magufuli imeshindwa katika ulingo wa kisiasa kwa kushindana kwa hoja, imekosa uvumilivu wa kisiasa na badala yake inaendesha nchi kwa mfumo wa mabavu bila kuzingatia sheria, haki na wajibu, taratibu na kanuni. Hebu tujiulize, ni nchi gani duniani ambayo ilishinda NGUVU YA UMMA INAYOTAKA MABADILIKO?

Madhumuni ya harakati za kupigania uhuru wa nchi yetu miaka ya 1953-1961 yalikuwa na lengo la kutuondoa watanganyika kutoka katika utumwa, unyonyaji, unyanyasaji, ukandamizaji, ubepari na ubeberu wa rasilimali za Taifa letu na watu wake. Jeshi la mkoloni lilikuwa likitumika kuwadhalilisha wazee wetu.
Leo hii baada ya miaka 55 ya kujitawala, tukiwa ndani ya mfumo halali wa kisheria wa demokrasia ya vyama vingi nchini, serikali ya CCM kwa kumtumia Rais John Magufuli inaturudisha nyuma na kufanya vitendo vibaya zaidi kwa raia wake kuliko ilivyokuwa ikifanywa na wakoloni! Cha kusikitisha takwimu hazionyeshi jeshi la polisi lilipotumia nguvu kubwa kupambana na raia kisha raia wakafungua mashtaka mahakamani, Serikali (Jeshi la polisi) ni lini lilishinda kesi hizo. Mauaji ya mwandishi David Mwangosi ni ushahidi wa hili na kesi nyingine nyingi orodha ni ndefu ambazo zikifikishwa mahakamani haki inaangukia kwa walioshtakiwa?
Tunamtaka Rais Magufuli atambue kuwa kamwe hatoweza kuzuia nguvu kubwa ya watanzania iliyo tayari kuleta HAKI SAWA KWA WOTE na mabadiliko sahihi ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, na kuboresha hali za maisha na kipato cha mtanzania kwa kutumia vyema rasilimali za nchi yetu. Tuna kila sababu ya kuunganisha nguvu zetu kama watanzania kumzuia Rais kwa njia ya amani asiendelee kuikanyaga katiba ya nchi aliyoapa kuilinda.
Tunahitaji Taifa letu liwe salama na hatuhitaji kwa namna yeyote ile uvunjwaji wa sheria na matumizi ya nguvu kubwa za vyombo vya dola yanayoandaliwa na rais mwenyewe ili yafanywe dhidi ya wananchi wadai demokrasia.

THE CIVIC UNITED FRONT (CUF- Chama Cha Wananchi) Kinawataka watanzania wote bila ya kujali itikadi za vyama vyetu kusimama imara kutetea misingi ya uongozi wa Taifa letu kwa kuilinda na kuihifadhi katiba na sheria za nchi yetu na kuhakikisha zinaheshimiwa, zinafuatwa na kuhifadhiwa na kila mmoja wetu.

THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-Chama Cha Wananchi) tunawahakikishia watanzania wote kuwa daima tutaendelea kusimama imara na kuwaunganisha watanzania wote ili kuimarisha umoja na mashirikiano baina yetu ya KUDAI HAKI SAWA KWA WOTE NA DEMOKRASIA YA KWELI kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

HAKI SAWA KWA WOTE
___________________________

JULIUS MTATIRO
MWENYEKITI KAMATI YA UONGOZI CUF -TAIFA
juliusmtatiro@yahoo.com

Mawasiliano:

Salim Bimani - 0777414112
Mkurugenzi habari, uenezi na mahusiano na ummah

Mbarala Maharagande
Naibu Mkurugenzi

maharagande@gmail.com
0784 001 408

DKT International Tanzania Yazindua "Trust Community Maternity Homes"

$
0
0

Dar es salaam, Tanzania, Shirika lisilo la kiserikali DKT International Tanzania limezindua mfano wa Kliniki mpya ziitwazo “Trust community maternity homes kwa ajili ya wananchi wa kipato cha kawaida zinazoendeshwa na wakunga mbalimbali.
“Trust Community Maternity Homes” – Ni kliniki zinazojitosheleza zilizotengenezwa kwa ubunifu kwa kutumia kontena ya kusafirishia mizigo, kliniki hizi zimetengenezwa maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu.

Kiliniki za “Trust Community Maternity Homes”  zilizinduliwa kwa umma  wakati wa uzinduzi wa kliniki ya “Trust Health & Wellness Clinic “ ya Dar Es Salaam na ofisi  mpya za DKT International Tanzania  mnamo tarehe mbili September, 2016

“Kila mwaka, wanawake milioni moja hapa Tanzania ambao hawakukusudia kupata ujauzito hupata ujauzito” alisema mkurugenzi mkuu wa DKT international, Raphael da Silva.

“Hali hii si tu kuwa ina athiri wanawake hawa kifedha, afya zao binafsi na hali ya kiuchumi ya familia zao, lakini pia zinapelekea kuongeza uhitaji wa Serikali kutoa huduma za kiafya pamoja na elimu kwa watoto hawa .Kama tunaweza kufanikisha kutoa huduma zenye ubora wa hali ya juu za afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa jamii katika miji midogo na wanajamii ambao hawapati huduma hizi kiurahisi, tutafanikiwa kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya wanawake hawa” alisema.

“Trust Community Maternity Homes ni kliniki zinazojitosheleza ndani ya kontena la kusafirishia mizigo, zinazoendeshwa na wakunga wataalamu na wenye uzoefu wa muda mrefu kama washirika chini ya kliniki mama za “Trust health and wellness clinics” .  Alisema meneja mradi, Karoli Mango.

“Kliniki hizi zinatoa ubora ule ule wa huduma , usiri na msaada  sawa sawa na Kliniki zetu nyingine za Trust  zinazopatikana mikoani hapa nchini .Kliniki yetu ya kwanza ya “ Trust community maternity homes” ya mjini  Kahama iko katika hatua za mwisho za  maandalizi kabla ya ufunguzi” aliongeza.

Trust ina mpango wa kuingia mikataba yenye masharti mepesi na wakunga wazoefu ambayo itawawezesha kukodisha na baadae kuzi miliki kliniki hizi.  Wakunga wanaotoa huduma hizi watatumia kliniki hizi ambazo ziko ndani ya kontena ambazo zinatumia umeme wa sola , zenye uwezo wa kutoa huduma kamili za afya ya uzazi na uzazi wa mpango, pamoja na huduma nyingine za afya kwa jamii. Wakunga hawa watajipatia kipato kwa kutoza kiasi kidogo cha fedha kwa huduma na bidhaa zitakazo tolewa katika kliniki hizi.

Kwa sasa , kuna “ Trust health and wellness  clinic” nne  ambazo ziko Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya and Mwanza  na pia kuna kliniki  na hospitali washirika  30  ambazo zinatoa huduma kwa kutumia chapa ya Trust.

Kliniki ya Msasani peninsula ya Dar Es Salaam ilifunguliwa mapema mwezi Julai.

 Kuhusu DKT International Tanzania
Shirika Iilianzishwa mwaka 2014, DKT International Tanzania  ni shirika la kimataifa lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya afya ya uzazi,uzazi wa mpango na kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI . Hapa Tanzania  chapa zake mama ni Trust , Fiesta na Bull.




Meneja Masoko wa DKT International Tanzania Sialouise Shayo akionyesha baadhi ya bidhaa kwa waandishi wa habari zinazopatikana kwenye Kliniki mpya ya uzazi wa Mpango iliyozinduliwa jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam. Kliniki hiyo ni maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango.


Meneja Mradi wa programu ya Trust community maternity homes kutoka DKT International Tanzania Carol Mango akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa kliniki hizo mpya zilizotengenezwa maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu. Uzinduzi wa kliniki hizo ulifanyika jana katika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es salaam.


Mkunga kutoka DKT International Tanzania Adella Hugo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye Kliniki mpya ya uzazi wa Mpango iliyozinduliwa jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam. Kliniki hiyo ni maalumu kwaajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la DKT International Tanzania Raphael da Silva akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kliniki mpya za Shirika hilo zijulikanazo kama “Trust community maternity homes”. Kliniki hizo mpya ni maalumu kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwa wanawake wanaoishi kwenye miji midogo katika jamii yetu. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Makao makuu ya Shirika hilo Masaki, jijini Dar es salaam.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la DKT International Tanzania Raphael da Silva akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na vifaa vinavyopatikana ndani ya Kliniki mpya na ya kisasa iliyozinduliwa katika makao makuu ya Shirika hilo hivi karibuni jijini Dar es salaam kwa ajili ya Afya ya uzazi kwa kina mama.

LICHA ya Kufungwa Nigeria, Gavana wa Nigeria Awazawadia Taifa Stars Milion 21

$
0
0
Licha ya kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Nigeria, Taifa Stars wamevuna kitita cha dola 10,000 kutoka kwa Gavana wa jimbo la Akwa Ibom State, Udom ambapo ndipo unapopatikana Uwanja wa Uyo uliotumika kwenye mchezo wa jana.

Kitita hicho ni sawa na shilingi za Kitanzania ml 21.7 na Gavana huyo alitoa wakati waliokuwa wakipata chakula cha usiku kwa pamoja baada ya mchezo huo.

Ikumbukwe kuwa katika historia ya timu hizi mbili, Tanzania haijawahi kuifunga Nigeria katika michezo yote waliyowahi kukutana zaidi ya kuambulia vichapo na sare.

Gavana huyo ametoa kiasi hicho cha fedha kutokana na ari ya upiganaji iliyooneshwa na wachezaji wa Stars, ambao walikuwa wakiongozwa na nahodha wao Mbwana Samatta ambaye kabla ya mchezo huo alikuwa gumzo kwa Wanigeria.

Hata hivyo, jana kuna wachezaji ambao walionesha kiwango kikubwa sana kilichowapa mashaka Nigeria. Wachezaji hao ni pamoja na Aishi Manula, Simon Msuva na mabeki wa kati Vincent Andew na David Mwantika.

Vilevile Gavana huyo pia aliwapa Nigeria Naira mil 10 kama pongezi kwa ushindi wao waliopata na kuahidi kuwapa zaidi endapo watafanikiwa kupata nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Russia.

TRA yakusanya trilion 1.158 kwa mwezi Agosti na kuvuka lengo, Kariakoo kuwa mkoa maalum wa kodi

$
0
0
KATIKA harakati za kuhakikisha kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa Wakati, Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imejiwekea mikakati mbalimbali ya kuongeza wigo wa vyanzo vya Mapato pamoja na kukusanya Mapato kikamilifu.

Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo;
Kulifanya eneo la Kariakoo kuwa Mkoa Maalumu wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha biashara hapa nchini na kuhakikisha kila mfanyabiashara anakuwa na Mashine ya Kielektroniki ya kodi (EFDs) na kuitumia ipasavyo.
Katika kutekeleza hilo Mawakala wote wa EFDs wamefungua ofisi ya pamoja katika jengo la Al-Falah Towers lililopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo ili kurahisisha upatikanaji wa mashine hizo na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika matumizi ya mashine hizo.
Aidha Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA Bw. Richard Kayombo ametoa wito kwa wananachi na wafanyabiashara kujitokeza kuhakiki taarifa zao za usajili wa TIN kabla ya Tarehe 15 Oktoba 2016 katika vituo vifuatavyo kwaajili ya zoezi hilo kwani muda hautaongezwa baada ya tarehe hiyo maana baada ya tarehe hiyo zoezi hili litahamia mikoa mingine.

Vituo hivyo vya uhakiki ni pamoja na:
Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)
Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara.
Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala- Zakiemu
Wilaya ya Kigamboni: Ofisi za TRA Kigamboni
Pamoja na kuhakiki taarifa zao, wafanyabiashara wote ambao hawana TIN nchini wanaombwa kufika katika ofisi ya TRA iliyoko karibu nao ili kujisajili kuepuka kukumbwa na msako unaondelea hivi sasa nchi nzima pamoja na uhamasishaji.

Wakati huo huo Bw. Kayombo amewahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kutekeleza agizo la Serikali la kufunga mashine za EFDs kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2016 kwani kinyume na hapo ukaguzi utaanza kufanyika kuanzia tarehe 1 Oktoba na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kukiuka agizo hilo.

Katika kuhakikisha kwamba kodi ya ongezeko la thamani VAT inakusanyawa kwa Wakati Mamlaka inawakumbusha walipakodi wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani - VAT kuwasilisha ritani ya kila mwezi kabla au tarehe 20 ya kila mwezi badala ya tarehe 27 iliyokuwepo kabla ya mwaka hu wa fedha.

Kwa upande wa walipa kodi zaa makadirio na kodi za makampuni (Corporation Tax) wanakumbushwa kulipa kodi zao mapema mwezi hu wa tisa badala ya kusubiri msongamano mwisho wa mwezi ambao unaweza kuwasababishia usumbufu.

Hivyo hivyo walipakodi wote wanaodaiwa madeni ya kodi za nyuma au malimbikizo wanakumbushwa kutembelea Mameneja wa mikoa, Wilaya na ofisi mbali mabli za TRA zinazowahudumia ili kujadiliana namna ya kulipa madeni hayo.

Kutokana na mikakti mizuri iliyowekwa na uiongozi wa TRA na serikali Mpaka sasa baadhi ya mikakati hiyo imeanza kuonyesha mafanikio na mwelekeo mzuri wa makusanyo ambapo kwa kipindi cha mwezi Agosti 2016 TRA imekusanya Trillioni 1.158 ikilinganishwa na lengo la Trillion 1.152 ambayo ni asilimia 100.57. ambapo Mwezi Agosti mwaka 2015 TRA ilikusanya billioni 923.

Wito wetu kwa wanahabari na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kutuunga mkono kwa kuhimiza kutoa risiti pamoja na kudai risiti katika kila manunuzi pamoja na kutoa taarifa za dalili za ukwepaji wa kodi wa aina yoyote mahali popote nchini

Mwakyembe: Mafisadi, Wachochezi Kukiona

$
0
0
SERIKALI imesema itafanya mapinduzi makubwa katika sekta ya sheria, yatakayowezesha kufikiwa kwa mchakato wa Katiba Mpya, kukomesha rushwa, kuipa meno Sheria ya Ndoa na Mirathi na kuipa majukumu Mahakama ya Rushwa na Mafisadi.

Maeneo mengine yatakayofanyiwa kazi ili kuboreshwa ni Sheria ya Mitandao, Sheria ya Kupata Taarifa, lakini pia kupelekwa bungeni kwa Muswada wa Sheria ili kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wa kupata huduma za kisheria.

Hayo yalisemwa juzi usiku na Waziri wa Sheria na Katiba, Dk Harrison Mwakyembe wakati akizungumza katika kipindi cha ‘Tunatekeleza’ kinachorushwa hewani na Kituo cha Televisheni cha TBC1, kwa lengo la kuainisha shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Katiba Mpya Inayopendekezwa
Akizungumzia Katiba Mpya Inayopendekezwa, Mwakyembea alisema mchakato wa kupata Katiba mpya ya Tanzania, ambao uliachwa kiporo na Serikali ya Awamu ya Nne, upo pale pale ingawa utekelezaji wake utakwenda polepole.

Alisema uthibitisho kuwa mchakato huo, utaendelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano ni kauli iliyotolewa na Rais John Magufuli mara kadhaa kwamba serikali yake itaendelea na mchakato huo ili kupata Katiba mpya.

“Na mimi (Mwakyembe) niseme vivyo hivyo, nina uhakika kuwa litafanyika hivyo, alichokifanya Rais ni kuzipa nguvu mamlaka husika ili kuendelea na mchakato huo bila kuingiliwa,” alisema Dk Mwakyembe.

Aliwataka wananchi kuendelea kuiamini serikali wakati ikiendelea na mchakato huo na kuongeza; “Tunayo Katiba ambayo tunaendelea kuitumia ili kuongoza nchi, hivyo tutaenda polepole na kazi hiyo ili kuhakikisha kuwa tutakapoimaliza tunapata Katiba mpya itakayokidhi matakwa ya wananchi walio wengi,” alisema.

Rushwa kwa mahakimu na majaji
Dk Mwakyembe alisema yamekuwepo malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi kuhusu mfumo wa utoaji haki, huku wakiwanyooshea vidole Majaji na Mahakimu kuhusika na vitendo vya rushwa, hatua ambayo imeifanya serikali kuchukua hatua.

Alisema katika kupambana na tatizo la rushwa kwa Majaji na Mahakimu, serikali imeagiza kila wilaya na mkoa kuunda Kamati ya Maadili ya Mahakama ili ziweze kupokea masuala yanayohusu ukiukaji wa maadili kwa watendaji wa Mahakama.

“Mahakama ni chombo cha haki, ni lazima kiwe kitakatifu pasipo kutiliwa shaka, kuna sheria inayoagiza kila wilaya au mkoa kuwe na Kamati za Maadili ya Mahakama zenye kuangalia mwenendo wa Mahakimu kuanzia Mahakama za Mwanzo,” alisema Dk Mwakyembe.

Alisema kamati hizo zitawasaidia wananchi wenye malalamiko kutoa madukuduku yao ambapo kwa ngazi ya wilaya, kamati hiyo inasimamiwa na Mkuu wa Wilaya na kwa Mkoa inasimamiwa na Mkuu wa Mkoa.

Waziri huyo alisema chini ya mkakati uliowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano, malalamiko ya rushwa kwa Majaji na Mahakimu yatafika mwisho na kuongeza kuwa uundwaji wa kamati hizo ni hatua ya awali.

Divisheni ya Mahakama ya Rushwa
Kuhusu Divisheni ya Mahakama ya Rushwa, Waziri Mwakyembe alisema tayari Majaji 15 wamepelekwa Chuo cha Mahakama Lushoto kwa ajili ya kuongeza ujuzi na kuongeza uelewa wa namna ya kuendesha kesi za mahakama hiyo kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi tafsiri za sheria mbalimbali.

Alisema lengo la kuundwa kwa mahakama hiyo muhimu nchini ni kuongeza ufanisi katika kusikiliza kesi za rushwa na ufisadi wa aina mbalimbali.

“Kwa sasa tunamalizia maandalizi, vifaa na majengo tayari, pia majaji 15 wamepelekwa Lushoto ili waangalie maeneo yanayowashika wengi pamoja na kutafsiri sheria mbalimbali, yote hayo ni katika kujiandaa ili tusikwame,” alisema.

Alisema katika mahakama hiyo hakutakuwa na kesi za miaka iliyopita na kwamba kesi zitakazokuwa zikiwasilishwa huko zitakuwa zinasikilizwa na kuisha huku akisema sheria ya uanzishwaji wake ilianza kutumika rasmi Julai 8, mwaka huu, ikiwa imeainisha vigezo vya kesi zenye sifa za kutua katika mahakama hiyo.

Huduma ya kisheria kwa wasio na uwezo Kuhusu eneo hilo la huduma ya kisheria kwa wasio na uwezo, Waziri Mwakyembe alisema serikali itapeleka bungeni muswada wenye lengo la kuanzishwa kwa huduma hiyo lengo, likiwa ni kupanua wigo wa wasiokuwa na uwezo wa kugharamia waweze kufikiwa.

Alisema, wizara yake tayari imeanza mchakato wa kuunda muswada huo wa kutungwa kwa Sheria ya Msaada wa Kisheria, ambayo itapelekwa bungeni hivi karibuni. Alisema hadi sasa kuna vikundi na asasi 290 zinazotoa huduma za kisheria nchini zikiwa na watumishi 4,500 na kwamba lengo ni kupanua zaidi wigo wa wananchi kuweza kupata huduma za kisheria hata kama hawana uwezo.

“Wanawake sasa wapige vigelegele, kwani majadiliano yataanzishwa ili kufikia maridhiano kwa wote kwani hii ni sheria inayogusa maslahi ya watu mbalimbali katika eneo la kimila, kidini na kiutamaduni.”

Alisema wanawake wamekuwa wakiteseka na kuonewa katika suala la mirathi na kwamba mara nyingi huonewa kwa sababu ya kukosa elimu.

Alisema serikali pia itapeleka bungeni muswada wa kutaka maridhiano kuhusu Sheria ya Ndoa na Mirathi ili wanawake wengi waweze kunufaika katika masuala ya mirathi tofauti na ilivyo sasa.

Kuhusu Sheria ya Mtandao alisema pamoja na kuwa hivi sasa sheria hiyo inatumika, lakini kumekuwepo na msuguano wa kimantiki baina ya pande mbili za wananchi, wakiwemo wanaosema inabana na wengine wakisema inalegezwa, hivyo serikali kuona umuhimu wa kuwepo kwa mjadala wa kitaifa kuona suala hilo lipatiwe ufumbuzi bora zaidi.

Sheria ya Ndoa
Akizungumzia Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, Waziri Mwakyembe alisema rufani iliyokatwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu pingamizi la sheria hiyo, ina nia njema kwani inataka maridhiano yafikiwe kwanza na wananchi wenyewe kuhusiana na uboreshaji wa sheria hiyo badala ya kutumia njia ya mkato.

Alisema uamuzi wa Mahakama Kuu uliitaka Serikali kufuta vifungu viwili cha 13 na 17 vya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 vinavyoeleza mtoto wa miaka 14 na 15 anaweza kuolewa kwa idhini ya mzazi au Mahakama.

Alisema, serikali inaelewa, pia kilichosemwa na Mahakama si kigeni kwa serikali, na suala hilo pia lilifika katika Baraza la Mawaziri likajadiliwa kwa kina ikielezwa njia ya kutumia katika kupitisha sheria bila ya kutoka nje ya utamaduni wa maridhiano.

“Tanzania ina utamaduni wake wa maridhiano na kuongea, sasa muda umefika, kama serikali hakuna pingamizi lakini tutafikaje huko ni kwa nji ya ya mkato au kwa kuzungumza,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza kuwa ndio maana rufaa ilikatwa.

Kuhusu suala la umri wa mtoto wa kike kuolewa, Waziri huyo alisema serikali imeliona, lakini ingependa Watanzania kujadiliana kwanza, na kwamba isitafsiriwe kuwa serikali inapinga maoni ya wadau bali inachokifanya ni kuangalia njia bora zaidi ya kufikia azma hiyo.

Kijana Shoga Amtia Doa Mwanamuziki Raymond wa wasafi, Adai Wana Mahusiano

$
0
0
Leo katika kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii nimekutana na post za kijana wa kiume ambazo zinamuhusu msanii Raymond wa wasafi,post za kijana huyo ni tata kiasi kwamba nilishindwa kufahamu kijana huyo anauhusiano gani na msanii huyo wa wasafi? 
Post za huyo kijana ni hizi hapa kama zilivyopostiwa na Huyo kijana maana inaonyesha wanafahamiana! Haijajulikana kama ni kweli au huyu kijana shoga anatafuta kiki mjini 




Uhuru Kenyata Akanusha Kuwepo Mvutano Wa Kiuchumi Kati Ya Tanzania Na Kenya

$
0
0
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Jumamosi alikanusha ripoti za vyombo vya habari kwamba kuna mvutano baina ya Kenya na Tanzania.

Akizungumza mjini Mombasa wakati wa ufunguzi gati la makontena katika bandari ya Mombasa, Kenyatta alipuuzia maneno kwamba kuna mvutano wowote na badala yake akasema kuwa nchi hizo zinasaidiana.

Alisema anaona kwenye vyombo vya habari kwamba kuna “mgogoro baina yetu, lakini nataka kusema wazi wazi kwamba Kenya na Tanzania hazina mgogoro wowote baina yao,” alisema.

Kenyatta alisema uchumi wa nchi hizo mbili umefungana kwa miaka mingi na ni kwa ajili ya faida ya watu wa nchi hizo mbili.

Alitaja kufunguliwa kwa njia inayojulikana kama “northern frontier” ambayo itaunganisha bandari ya Mombasa kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania, hadi Bujumbura, Burundi – njia ambayo itafupisha urefu wa kutoka Bujumbura hadi Mombasa kwa kilomita 300 nzima.

“Afrika Mashariki haiko katika mashindano ya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kenyatta. “Afrika Mashariki inashindana na dunia. Tunataka kujaliana (pale penye mapungufu). Tunataka tutumie nguvu zetu ili kukua, kuendeleza na kuinua uchumi wetu,” alisema.

Kutokuwepo kwa Rais John Magufuli wa Tanzania katika mkutano wa hivi karibuni wa kimataifa na Tokyo mjini Nairobi kulizusha uvumi kuhusu uhusiano wa nchi za eneo hilo.

Kiongozi huyo wa Tanzania ametembelea Uganda na Rwanda tu tangu achukue madaraka Oktoba mwaka jana ukilinganisha na rais aliyemtangulia Jakaya Kikwete ambaye alikuwa akisafiri sana nchi za nje.

Rais Magufuli pia hakuhudhuria mikutano karibu mitano ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na mkutano wa shirika la biashara duniani na mikutano mikuu ya AU mjini Addis Ababa na ule wa Kigali Rwanda hivi karibuni.

Majibu ya Mkurugenzi NHC Kuhusu Kudaiwa Kuingiza Siasa Kwenye Shirika Hilo

$
0
0
Baada ya Shirika La Nyumba la Taifa kupitia kampuni ya udalali kutoa samani mbalimbali katika jengo la Club Bilicanas na jengo lenye Ofisi ya Free Media kufuatia mmiliki wa ofisi hizo Freeman Mbowe kudaiwa kutolipa deni ambalo ilielezwa kuwa anadaiwa na shirika hilo.

Aidha hivi karibuni ziliripotiwa habari kuwa Mbowe amesema kinachofanyika ni siasa kwani wanafanya kama kumkomoa kwa sababu mara zote amekuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali kuhusu hali ya siasa nchini.

Kupitia kipindi cha funguka kinachorushwa na kituo cha television cha Azam Tv, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu amejibu madai hayo kwa kusema……..

’National Housing ninayoiongoza mimi haijawahi kusukumwa kwa mkono wa siasa, na tungekuwa tumesukumwa na mkono wa siasa tusingefanya haya tuliyoyafanya kwa muda mfupi, taasisi za serikali zimeshagusa machungu yetu, hata chama tawala idara yake makao makuu‘

TCU Yatangaza Kuanza Udahili Awamu ya Pili Kwa Wanafunzi Wanaojiunga Vyuo Vikuu

$
0
0
Tunapenda kuutangazia Umma kuwa tulifunga mfumo wa pamoja wa udahili tarehe 31/08/2016 saa sita usiku ili kuchakata maombi ya waombaji waliofanikiwa kuomba udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017.

Hata hivyo kutokana na wengine kushindwa kufanikiwa kutokana na sababu mbali mbali, Tume inatangaza kuwa itafungua maombi kwa awamu ya pili kuanzia tarehe 12 hadi 23 Septemba 2016 ili kuruhusu makundi yafuatayo kuomba udahili.
Waombaji watakaokuwa wamekosa nafasi kwenye awamu ya kwanza
Waombaji wa kidato cha Sita walioshindwa kuomba katika awamu ya kwanza
Waombaji wenye vigezo vya Stashahada ambao walishindwa kuomba kutokana na matokeo yao kuchelewa kufika NACTE kwa wakati,
Waombaji ambao wamemaliza mitihani ya “Cambridge” mwaka 2016 na matokeo yao yameshatoka,
Waombaji waliofaulu mitihani ya RPL,
Waliokuwa wanafunzi wa vyuo vikuu watakao kuwa na uthibitisho toka vyuo vyao vya awali.

Baada ya hapo Tume haitaruhusu tena maombi ili kuruhusu taratibu zingine za kiudahili kuendelea kwa ngazi ya Bodi ya Mikopo na vyuoni.
Asanteni
Imetolewa na
Prof. Eleuther Mwageni
 Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
02 Septemba 2016

Kuchanganya Biashara, Uchumi na Siasa Kunatusababisha Tutoe Majibu Mepesi Katika Maswali Magumu

$
0
0
TRA wanapotoa statement kuhusu kupungua kwa mizigo kunakotokana na ongezeko la kodi na kusema kuna Propaganda dhidi yao, kuna tofauti gani na Mbowe kusema kuondolewa kwake na NHC pale Bilicanas ni kwa sababu za kisiasa na kwamba ni kwa kuwa yeye Mpinzani? ....
Tuna tatizo kama nchi.

Kuchanganya Biashara, uchumi na siasa kunatusababisha tutoe majibu mepesi ktk maswali magumu.
#KuanzaUpyaSiUjinga.

By Habib Mchange

Mtandao hatari wa Majambazi Wanaswa Dar es Salaam

$
0
0
Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wanadaiwa kukamatwa na polisi wakiwa na zana mbalimbali ambazo hutumiwa na vyombo vya ulinzi zikiwamo silaha za vita na sare za polisi.

Vitu hivyo vinadaiwa kutumiwa na watu hao kufanya   ujambazi.Inadaiwa kwamba watu hao ni wale waliovamia na kuiba fedha katika jengo la Sophia House lililopo Keko   Dar es Salam wakiwa wamevaa sare za polisi na kutumia gari   ya Noah.

Taarifa  kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kwamba watu hao ni pamoja na mwanamke mmoja aliyekamatiwa   Bunju  katika Manispaa ya Kinondoni ambako vilikutwa vitu vyote vilivyoporwa na wanaume wawili waliokamatiwa   Mbagala Manispaa ya Temeke,   Dar es Salaam.

Chanzo hicho kilieleza kwamba silaha zilizokamatwa  ni pamoja na bunduki tatu za SMG na risasi zake 260, bastola 16 na risasi zake 526, panga moja na michimbiko mitatu ya kung’olea mageti..

Vitu vingine ni   pingu za chuma 45 na tatu za plastiki, ‘radio call’  12 , kamera ya CCTV moja, gari moja   ya Noah, sare ya polisi jozi moja, ‘pump action tatu na mkasi mmoja.

Wabunge wa Upinzani Kuanza Vikao vya Kutafuta Suluhu na Naibu Spika

$
0
0
Kambi rasmi ya upinzani imepanga kufanya vikao vya kujadili suluhu ya kudumu ya mgogoro na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson uliosababisha wabunge wanaounda Ukawa kususia vikao vinavyoendeshwa na kiongozi huyo.

Vikao hivyo vinapangwa kufanyika wakati mkutano wa nne ukianza rasmi kesho, baada ya kuahirishwa mwishoni mwa Juni mwaka huu wakati wa mkutano wa Bajeti.

Mbunge wa Vunjo (NCCR- Mageuzi), James Mbatia alieleza jana kuwa uamuzi wa kufanya vikao hivyo umefikiwa baada ya upinzani kukaa kikao na viongozi wa dini Agosti 24 mwaka huu ili kutafuta suluhu ya kudumu.

“Kikao cha kwanza tutakaa kamati ya uongozi ya wabunge wa upinzani kujadili suala hilo na baadaye tutamaliza na kikao cha wabunge wote ili kubaini njia endelevu za kumaliza jambo hilo,” alisema Mbatia ambaye ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi.

Wabunge wa Ukawa wamekuwa wakisusia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika kwa madai ya kutoridhishwa na uongozi wake tangu Mei mwaka huu, baada ya Dk Tulia kukataa kujadili hoja ya kufukuzwa wanafunzi zaidi ya 8,000 stashahada ya ualimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

Hata wakati wakisubiri kufanyika vikao hivyo ambavyo Mbatia hakutaka kuelezea kwa undani, upinzani ulitangaza kurudi bungeni baada ya mkutano wao na viongozi wa dini.

Katika mkutano na wanahabari Agosti 25, Mbatia kwa niaba ya vyama vilivyoshiriki mkutano huo wakiwamo ACT-Wazalendo, alisema wangejadiliana namna ya kufanikisha jambo hilo kama sehemu ya kutii ushauri wa viongozi hao wa kiroho.

Hata hivyo, haijawekwa bayana iwapo kesho Ukawa wataendelea na vikao hata kama Dk Tulia ataendelea kuongoza kiti hicho ama la.

Mbatia alisema jana kuwa watatoa taarifa rasmi leo namna vikao hivyo vitakavyofanyika na siku husika.

Kuhusu kupata taarifa ya mwenendo wa mchakato wa kutafuta maridhiano ulioelezwa na Spika Job Ndugai hivi karibuni, Mbatia alisema hawajapata chochote na wao wanasikia kwenye vyombo vya habari kama wengine.

Alipoulizwa ni lini vikao vya maridhiano kati ya pande hizo yataanza, Ofisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bunge, Owen Mwandumbya alisema Spika anatarajiwa kufika ofisini leo na kwamba kama ataona kuna haja ya kufanya hivyo atapanga utaratibu wa namna anavyoona inafaa.

TETESI: Profesa Lipumba Adaiwa Kujiunga ACT Wazalendo

$
0
0
Kwa muda wa takribani saa kadhaa sasa kumekuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na mwenyekiti mwenza wa UKAWA, Prof. Ibrahim Lipumba amejiunga na chama cha ACT- Wazalendo.

Taarifa hizo zimeenda mbali na kueleza kuwa, muda huu kuna kikao kinafanyika juu ya uamuzi wa ACT kumchukua Prof. Lipumba na kuwa mwenyekiti wa sasa wa ACT, Mama Anna Mghwira ajiandae kupisha nafasi hiyo.

Chama cha ACT- Wazalendo hakijatoa taarifa yoyote kuhusu tetesi hizi na wala Prof. Lipumba hajazungumza juu ya hili.

Tunaendelea kufuatilia ukweli juu ya taarifa hizi, endelea kuwa nasi kwa taarifa kamili.

TAJIRI Steve Nyerere Atangaza Kuoa Januari

$
0
0
Msanii mkongwe wa filamu Steve Nyerere aliwasurprise baadhi ya wasanii wenzake wa filamu katika harusi ya Shamsa Ford baada ya kutangaza anaoa mwezi januari mwakani.

Akitoa neno kwa niaba ya wasanii wenzake katika harusi ya Shamsa Ford iliyofanyika Sinza Afrikasana Ijumaa iliyopita, Steve Nyerere aliwaabarisha wasanii wenzake kuwa ataoa Januari 2017.

“Mimi sina maneno mengi yakusema zaidi ya kuwapongeza na kuwaombea muishi salama, pia mungu akipenda na mimi nitafunga ndoa Januari,” alisema Steve.

Baada ya kusema kauli hiyo, kuliibuka shangwe kutoka kwa wasanii ambao walihudhuria ndoa.

Viewing all 104709 articles
Browse latest View live


Latest Images