Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104781 articles
Browse latest View live

Video: Raymond Akiri Kuzama ‘Penzini’ Kwa Avril wa Kenya, Amuambia Mbele ya Mashabiki Mombasa

$
0
0
Raymond ameamua kuusemea moyo wake mbele ya mashabiki maelfu kwenye show ya WCB, Mombasa, Kenya.

Muimbaji huyo wa ‘Kwetu’ alimpandisha jukwaani mrembo wa Kenya, Avril na kumuimbia wimbo maalum kuelezea hisia zake waziwazi kuwa ni msichana anayempenda na kuwaacha mashabiki wakiangusha shangwe za kutosha.

Hakuuishia hapo, Ray alipost picha akiwa na Avril na kuandika:
Trust me @theavieway I really love you … thanks for coming … God bless you.”

Avril naye alionesha kudata kwelikweli na dogo huyo kwakuwa hakuisha kupost picha na video za show yake.

“This song that @rayvanny serenaded me with should be my next collabo hmmmm #ThinkingOutLoud,” aliandika kwenye picha aliyoweka Instagram akiwa na mkali huyo wa freestyle.



Hadi sasa tunafahamu kuwa Avril yupo single baada ya kuachana na mpenzi wake Msouth na pia Ray hajawahi kuonesha kuwa na msichana yeyote na hivyo wawili hawa wanaweza kuwa ‘perfect combo.’

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Raymond, Harmonize na Rich Mavoko walikuwa na show kwenye mjini wa mwambao wa Mombasa nchini Kenya.

Harmonize aogopa kufanya kazi na Rayvan

$
0
0
Msanii wa kundi la WCB Harmonize amesema kwa sasa hayuko tayari kufanya colabo na kuwapa watu muda wa kuwatengenezea ushindani kati yao.

Akipiga story ndani ya eNews amesema “Colabo ni kubadilishana mashabiki kwa wakati nafanya colabo na Diamond nilikuwa nikilenga kuwa kuna mahali muziki wa Diamond umefika wa kwangu haujafika na pia Diamond ana'hit' nyingi kwa hiyo likuwa ni mpango wa kufikisha muziki wangu mbali”
“Ningekuwa naogopa colabo basi ningeogopa kufanya colabo na Diamond kwa kuwa ni muimbaji mzuri kuliko Diamond lakini niliamua kukaza tu ili kufika mbali, lakini pia inabidi tupate muda tutengeneze wimbo mzuri ili kitoke kitu kizuri”.aliendelea kusema Harmonize.

Pia hakusita kuelezea maswala ya mahusiano yao na Wolper akisema “siku zinavyozidi kwenda binadamu anapata mawazo mapya pamoja na kukua lakini pia nafikiri ilikuwa ni upya ndo maana kila siku tulikuwa tukifanya mambo mbalimbali kwa kuwa wote tulikuwa tukitamaniana".

Wazanzibar Waisifia Hotuba ya Rais Magufuli

$
0
0
Baadhi ya wakazi wa Zanzibar wamempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kutoa hotuba waliyoiita ‘safi’ inayosadifu hali ya maisha ya watanzania.

Kwa siku na nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa Zanzibar walisema kuwa hotuba ya Rais Magufuli aliyoitoa katika mkutano wa kutoa shukrani baada ya uchaguzi uliopita, imejenga imani kubwa kwa maendeleo na wananchi sambamba na kukemea suala la ubaguzi miongoni mwa wananchi na viongozi.

Moja kati ya wakati wa Zanzibar waliweza kutoa maoni tofauti tofauti kuhusiana na hotuba hiyo.

“Rais Magufuli alizungumzia vizuri suala la amani, halafu vilevile bila amani usingeweza kuja kunihoji hapa kwa hiyo amani ndio kila kitu,” alisema mkazi mmoja wa Zanzibar.

“Kwanza nampongeza mheshimiwa rais kwasababu hotuba yake imetufanya sisi vijana tuamke na tufanye kazi na sio kukaa maskani kama unavyotuona hapa,” alisema kijana mmoja.

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli alisisitiza zaidi suala la maendeleo.

“Tunataka maendeleo, na mimi niwaombe ndugu zangu watanzania wote, lengo letu kubwa liwe maendeleo kwa watanzania, maendeleo kwa wazanzibar, maendeleo kwa wapemba, tupeleke Tanzania yetu mbele,tupeleke Zanzibar yetu mbele, vyama tuweke pembeni,” alisema.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya Septemba 6, Ikiwemo ya Ukawa Kumaliza Mgomo Bungeni

$
0
0

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya Septemba 6, Ikiwemo ya Ukawa Kumaliza Mgomo Bungeni

Wema: Nitalipa Pesa Matibabu ya Baba diamond

$
0
0
Kwa kuonesha hana kinyongo na ex bf wake Wema sepetu amesema kuwa atapigana kufa na kupona mpaka pale hali ya baba yake diamond itakapo tengemaa

Ufafanuzi wa ACT- Wazalendo Kuhusu Taarifa ya Pro Lipumba Kujiunga na Chama Hicho

$
0
0
Baada ya kumalizika kikao cha kamati kuu ya Chama cha ACT Wazalendo kilichofanyika leo septemba 05/2016 jijini Dar esSalaam

Kesho Jumanne Septemba 06/2016,Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo watakutana na waandishi wa habari na kuelezea masuala mbali mbali muhimu yanayoendelea sasa ikiwemo:
• Hali ya Uchumi wa Taifa
• Hali ya Kisiasa ya Taifa
• Hatari ya Kuvunjika Kwa Umoja wa Kitaifa

Wapi:Makao Makuu ya ACT wazalendo yaliyopo Sayansi Kijitonyama jirani na Kanisa la KKKT

Muda:Saa tano kamili asubuhi (11:00am)

Kuhusu taaarifa zilizosambaa za Prof. Lipumba kujiunga na chama hicho, ACT- Wazalendo wamesema kuwa hawana taarifa yoyote ya Prof. Lipumba kujiunga na chama hicho na pia kikao cha leo hakihusiani na ajenda yoyote ya kupokea wanachama.

Muhimu kuzingatia muda

Abdallah Khamis
Afisa Habari
0655549154

Raymond Aeleza Sababu ya Kumuimbia Avril Jukwaani

$
0
0

Raymond alisababisha yowe kubwa mwishoni mwa wiki katika show ya WCB mjini Mombasa alipompandisha mrembo wa Kenya, Avril aliyekuwa mmoja wa watu waliohudhuria.

Akiongea na Bongo5, Raymond amefunguka;

Sikutegemea kabisa kwamba nitamuona Avril katika show , walikuja watu wengi lakini wakati nipo stejini nikaona VIP kama kuna mtu kakaa, kuangalia vizuri nikaona ni Avril so kwa heshima yake na thamani ya muziki wake nikaona kaja kwenye show ambayo naperform nikaona kabisa ni heshima kubwa kaonesha, nisingeweza kuonesha tu kwa kutaja jina lake kwa mbali, nikatamani aje stejini, nikatamani niwe naye stejini. Namshukuru kaja kwenye show na sikutegemea kumuona. Ndio nikamuita kwenye steji nikamuimbia watu wakafurahi, naye amefurahi naye mwenyewe alifurahi, na kuonesha kuwa alifurahi pia, kapost hadi picha tukiwa stejini naye amesema ameappreciate. Kikubwa nilichokigundua pale ni support kutoka moyoni kabisa, sababu ukiangalia Avril ni msanii wa nchi nyingine kabisa na mimi ni msanii wa nchi nyingine, lakini katoa dhana ya matabaka, kavuka boundaries, kaonesha kuwa sisi ni ndugu tunasapotiana. Kiukweli nimefurahi sana na naamini na yeye kafurahi.

Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi, Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu

$
0
0
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio mbalimbali ya kihalifu katika mkoa wa Dar es Salaam, wameuawa na majambazi wenzao katika eneo la Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Licha ya kuuawa kwa majambazi hao, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwakamatwa watu zaidi ya saba, wanaosadikiwa kuhusika na tukio la majibizano ya risasi na polisi, lililotokeo Vikindu lililosababisha kifo cha askari mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu, Simon Sirro alisema kabla ya kuuawa watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo tofauti ya Mbagala, Keko na Kawe jijini humo.

Alisema watu hao walikamatwa kufuatia tukio la ujambazi, lililotokea Agosti 29, mwaka huu katika Jengo la Sophia House maeneo ya Veta Changombe, ambapo majambazi hao walidaiwa kupora Sh milioni 35 na kutoweka kwa kutumia gari aina ya Toyota Noah lenye namba bandia T 549 BPK.

Aliongeza kuwa uchunguzi wa tukio hilo, uliendelea kufanyika na Septemba 3, timu ya upelelezi kutoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, iliweka mtego na kufanikiwa kuwakamata majambazi hao watatu na walipohojiwa walikiri kufanya matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha na kuweza kutaja silaha mbalimbali walizonazo.

Kamanda Sirro alisema majambazi hao, waliwapeleka askari eneo la Mbezi Chini katika nyumba waliyokuwa wamekodi na askari walifanya upekuzi na walifanikiwa kupata silaha mbalimbali, zikiwemo bunduki 23 na risasi zaidi ya 800 na vitu vinginevyo.

Alitaja silaha hizo kuwa ni bunduki za kijeshi tatu aina ya SMG zikiwa na magazini nane na risasi 120, bastola 16, magazini tatu za bastola na risasi moja, Shot gun pump action tatu na risasi 130, bastola 16 magazini na risasi 548 na bunduki tatu aina ya Shot gun na risasi zake 130.

Aidha alisema walikuta redio za mawasiliano 12 na chaja zake tatu, darubini za kuonea mbali tatu, pingu za plastiki 45, majaketi ya kuzuia risasi matatu, mkasi mmoja wa kukatia vyuma, mtarimbo mmoja, risasi baridi za kutishia 37, boksi moja la kusafishia silaha, nyundo kubwa moja, pingu za chuma tatu, mashine moja ya kuhifadhia kumbukumbu na magari mawili.

Alisema uchunguzi wao ulibaini kuwa majambazi hao Septemba 6, mwaka huu walipora bunduki aina ya Shot gun yenye namba 006091830, ikiwa na risasi moja katika barabara ya Mbozi Chang’ombe.

Sambamaba na hayo, majambazi hao walikiri kuhusika na wizi wa mamilioni ya fedha katika Benki ya Habib African ya Kariakoo mwaka 2014 na Benki ya Stanbic mwaka 2014, wakitumia gari aina ya Toyota Noah.

Kamanda Sirro alisema baada ya mahojiano zaidi, majambazi hao walisema wanazo silaha nyingine ambazo wamezificha Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani. Ndipo askari walifuatana na watuhumiwa hao hadi kwenye msitu wa Vikindu.

Alisema askari walipofika eneo hilo, walilodai ni karibu na zilipo silaha hizo, walishuka kwenye gari na kuingia porini wakiwa wamewatanguliza watuhumiwa mbele majira ya usiku.

Aliongeza kuwa wakiwa msituni humo na askari wakiwa wenye tahadhari kubwa, ghafla walisikia milio ya risasi ikitokea mbele, ambapo askari walilala chini na baadaye zikisikika sauti zikisema ‘mmetuua sisi’.

Alisema baada ya risasi za mfululizo kutulia, askari walishuhudia majambazi hao ambao walichelewa kulala chini wakati risasi zikipigwa wakiwa wamejeruhiwa sehemu za kifuani na tumboni huku wakivuja damu nyingi.

Alisema askari walipiga risasi kuelekeza eneo zilikotokea risasi na walipoendelea kusonga mbele, walikuta silaha aina ya SMG ikiwa imetelekezwa na haikuwa na risasi ndani ya magazine, hivyo kufanya idadi ya silaha za SMG kufikia nne.

Aidha alisema askari waliwabeba majambazi hao na kuwapeleka kwenye gari kuelekea hospitalini, lakini wote walifariki dunia wakiwa njiani kutokana na kutoka damu nyingi.

Akizungumzia tukio la Vikindu, Sirro alisema wamefanikiwa kuwakamata watu hao wanaosadikiwa kuhusika na tukio ambalo lilisababisha kifo cha askari mmoja.

“Majambazi hao walikuwa ni kundi la kama watu 14 na tayari tumewakamata zaidi ya saba ambao mpaka sasa tunawashikilia kwa mahojiano zaidi ili kufanikisha upelelezi,” alisema Kamanda Sirro.

Pia alisema kumekuwa na taarifa mbalimbali, zikisambazwa katika vyombo vya habari zikidai kuwa katika tukio la Vikindu, kuna askari anahusika na tukio hilo na kudai taarifa hizo si za kweli na hakuna askari aliyehusika katika tukio hilo.

Katika tukio lingine, jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa makosa ya wizi wa magari manane, likiwemo gari moja la kibalozi.

Kamanda Sirro alisema magari hayo yaliibwa jijini Dar es Salaam na kuuzwa kwa watu mbalimbali jijini hapo na mikoani na watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na mara upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Sirro alisema katika tukio lingine jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita wanaodaiwa kuhusika na kuvunja nyumba usiku na kuiba.

Alisema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na mara upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.


Lipumba: Rais Magufuli Amebeba Agenda ya UFISADI - Vyama vya Upinzani Vinapaswa Kujipanga Upya

$
0
0
Ni katika kipindi cha Morning Trumpet asubuhi ya leo Prof alipoulizwa ni kwa nini alikuwa mpinzani wa kwanza kumtembelea na kumpongeza Rais Magufuli baada ya kuchaguliwa?

Professa alijibu bila mashaka kuwa Rais Magufuli anamkubali kwa kubeba agenda ambayo ndiyo iliyokuwa ikiwapa kiki wapinzani. Kwa sasa vyama vya upinzani vinaweza kabisa kupotea visipojipanga vizuri.

Hili linathibitishwa kwa mfano na mabadiliko yaliyoletwa na Lowasa ndani ya CHADEMA. Tangu Lowasa alivyoitwaa CHADEMA sijawahi sikia CHADEMA ikikemea UFISADI, sanasana wamegeuka watetezi eti Magufuli anawaonea mafisadi.

Hongera Professa!! wewe na Dr Slaa ndio mmethibitisha kuwa ni wapinzani wa kweli ambao lengo lenu ni maslahi ya taifa na sio wengine ambao lengo lao kwa sasa hata halijulikani.

Taarifa ya Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Kuomba Kujiuzulu..Ukweli Huu Hapa

$
0
0
Ofisi ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote.

Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki.  Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu.

Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo na CVPeople Africa-Tanzania

Fella Agonga Mwamba Kumrudisha Kundini Juma Nature..Asema Haya

$
0
0
Mkurugenzi wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family, Mkubwa Fella ameonekana kugonga mwamba juhudi zake za kutaka kurudisha mahusiano yake ya kazi na msanii wake wa zamani wa Kundi la TMK Family, Juma Nature.

Hapo awali Juma Nature alikuwa msanii wa Kundi la TMK Wanaume Family la Mkubwa Fella lakini baadae aliondoka na kwenda kuanzisha Kundi lake la TMK Wanaume Halisi.

Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii, Fella amedai wasanii ambao wanamthamini ni wale ambao yupo nao.

“Mimi ndo hanitaki, anaona mimi sina maana, lakini walioona mimi na maana ndo hawa ambao nipo nao mpaka sasa,” alijibu Fella baada ya kuulizwa kama ana mpango wowote na Juma Nature kwa sasa.

Kauli hiyo inaonyesha meneja huyo ameonga mwamba juhudi zake za kutaka kumrudisha msanii huyo kundini baada ya kuhaidi mara kadhaa kufanya hivyo.

DIAMOND Platnumz Awashangaza Mashabiki Wake Tena Kwa Kuimba "Remix ya All The Way Up"

$
0
0
Diamond Platnumz amejiongezea aka zingine mpya, Jini na Vampire. Jumatatu hii aliachia kipande cha verse kwenye hit single ya Remy Ma na Fat Joe ‘All The Way Up’ kilichoyakuna masikio ya mashabiki wake.

 Sikiliza hapo chini

Janga Kubwa Linalowatafuna Wasomi Wengi Tanzania ni Kutegemea vyeti Kama Mkombozi wao Kiuchumi

$
0
0
Janga kubwa linalowatafuna wasomi wengi ni kutegemea vyeti kama mkombozi wao kiuchumi; badala ya kutegemea uwezo wao kiakili. Ndio maana wakikosa ajira wanachanganyikiwa na wakiwa ajirani wanachanganyikiwa zaidi kwa mishahara isiyotosha kutimiza ndoto zao. Ukienda shule nenda kwa mtazamo wa kupata maarifa ambayo hata kama vyeti vitakuwa kabatini; yatakufanikisha.

#SmartMind

RAIS Magufuli Atonesha Donda la Mbowe

$
0
0
RAIS John Magufuli amepongeza hatua ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kumwondoa Freeman Mbowe, katika jengo ambalo amekuwa akipanga kwa muda mrefu, anaandika Pendo Omary.

Siku tano zilizopita, Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) pia Mbunge wa Jimbo la Hai aliondolewa kwenye jengo hilo na mawakala wa NCH, Fosters Auctioneers kwa madai ya kushindwa kulipa deni la zaidi ya Sh. 1.3 Bilioni huku mvutano wa kuwepo kwa uhalali wa deni hilo ukiendelea.

Jengo hilo lipo katika makutano ya Mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es Salaam ambapo mawakala hao walichukua vifaa vya kampuni hiyo katika upande wa uzalishaji Gazeti Tanzania Daima chini ya Kampuni ya Free Media.

Rais Magufuli alilisifu shirika hilo leo asubuhi wakati akizungumza na baadhi ya waliokuwa wapangaji katika nyumba za NHC zilizokuwepo Magomeni Kota ambazo zilibomolewa mwaka 2012.

Kwenye mkutano huo Rais Magufuli amelitaka shirika hilo ndani ya siku saba kuwaondoa wapangaji wote wanaodaiwa na serikali kwenye nyumba zake.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amesema, ndani ya miezi miwili kuanzia leo serikali itaanza kujenga nyumba za waliokuwa wakazi wa eneo hilo.

Waliokuwa wapangaji katika nyumba za Magomeni Kota zilizomilikiwa na serikali waliondolewa kwa mkataba na Manispaa ya Kinondoni katika makazi hayo mwaka 2012 kupisha ujenzi wa makazi mapya kwa muda wa mwaka mmoja.

Katika mkataba huo makubaliano yalikuwa; manispaa hiyo kuwalipa wapangaji hao kodi ya nyumba ya muda wa mwaka mmojo na mara baaya ya ujenzi kupangishwa katika nyumba hizo na baadaye kuuziwa, hata hivyo mpaka sasa hakuna kilichotekelezwa.

Rais Magufuli amesema, “kwa sasa eneo hili la heka 33 lipo mikononi mwangu. Ndani ya miezi miwili, tutaanza kujenga nyumba na majengo ya mwanzo ni ya wakazi 644. Tutaanza kutoa fedha mwezi huu.

“Yatakapo malizika kujengwa, orodha ya majina yote ninayo wawe wapo hai au watoto wao ndio watakaoingia kwenye nyumba hizo. Nikishamaliza kujenga hizo nyumba hao wakazi 644 watauziwa nyumba.”

Rais Magufuli amesema, ujenzi wa nyumba hizo utakapokamilika ndani ya muda wa mwaka mmoja kuanzia sasa, kabala ya wakazi hao kuuziwa nyumba hizo, serikali itawaruhusu kuishi kwa muda wa miaka mitano bila kulipa kodi ambapo baada ya muda huo kupita ndipo watauziwa. Hatua hiyo inalenga kufidia ghalama walizotumia tangu waondolewe katika nyumba hizo.

Chanzo:Mwanahalisi

Matusi yavunja mkutano wa Obama na Rais wa Ufilipino

$
0
0
Rais wa Marekani Barack Obama amevunja mkutano wake na Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte,  baada ya  Rais huyo, kumwita Obama ‘Mwana wa Kahaba’

Obama awali alikuwa amesema kwamba angemuuliza kiongozi huyo maswali kuhusiana na mauaji ya kiholela ya watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ulanguzi wa dawa za kulevya Ufilipino.

Lakini Bw Duterte, ambaye ameunga mkono mauaji hayo, alisema iwapo hilo lingefanyika: "Putang ina (mwana wa kahaba) nitakutusi katika mkutano huo."

Maafisa wa Obama wamesema badala yake kiongozi huyo sasa atakutana na Rais wa Korea Kusini.

Msemaji wa baraza la Taifa la Usalama Marekani Ned Price amewaambia wanahabari kwamba Obama atakutana na Park Geun-hye katika mkutano wa Mataifa ya Kusini Mashariki mwa bara Asia (Asean) mjini Laos, ambapo viongozi wamekusanyika kwa mkutano mkuu.

Obama, aliyetua Laos baada ya kuhudhuria mkutano wa G20 mjini Hangzhou, China, alitarajiwa kuuliza maswali kuhusu ukiukwaji wa haki za kibinadamu Ufilipino.

Lakini akiongea mjini Manila Jumatatu kabla ya kuondoka kuelekea Laos, Duterte alishutumu hilo na kusema ni "kukosa adabu" na akamtusi rais huyo wa Marekani. Aliongeza kwamba: "Tutagaragazana matopeni kama nguruwe iwapo utafanya hilo."

Kisha, alizungumzia kampeni ya kukabiliana na walanguzi wa dawa za kulevya ambapo washukiwa 2,400, wakijumuisha walanguzi na watumizi, wameuawa nchini Ufilipino tangu achukue mamlaka mwezi Juni.

"Kampeni dhidi ya dawa za kulevya itaendelea. Wengi watafariki, wengi watauawa hadi tuangamize mlanguzi wa mwisho na kumuondoa kutoka barabarani ... hadi mtengenezaji wa mwisho wa dawa hizi auawe, tutaendelea."

 Obama awali alidunisha matusi hayo na kusema aliwaomba maafisa wake kuchunguza iwapo huu ni wakati mwafaka wa kuwa na mashauriano ya kufana.

Baadaye, maafisa wake walivunjilia mbali mkutano huo.

Ziara ya mwisho ya Obama bara Asia akiwa kama rais imejaa vioja. Alipowasili Uchina, alijip kwenye mzozo wa itifaki kati ya maafisa wa Marekani na Uchina ambapo alikosa kuwekewa zulia jekundu.

Matusi

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Duterte kutumia lugha chafu kuwarejelea viongozi mashuhuri.

Alimwita Papa Francis "mwana wa kahaba", waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Keryy "mwendawazimu" na majuzi alimweleza balozi wa Marekani nchini Ufilipino kama "mpenzi wa jinsia moja ambaye ni mwana wa kahaba".

Wanafunzi 3918 wachaguliwa kujiunga kidato cha tano kwa awamu ya pili

$
0
0
WANAFUNZI 3,918 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano awamu ya pili kujaza nafasi zilizokuwa wazi kutokana na ufinyu wa nafasi na baadhi ya wanafunzi kutoripoti kwa wakati.

Taarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe ilisema kati ya wanafunzi hao wasichana ni 2,413 na wavulana 1,505.

“Kuchaguliwa kwa wanafunzi hao kumefuatia kuwapo kwa nafasi zilizoachwa wazi na wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni tangu kuchaguliwa kujiunga na kidato cha Tano katika awamu ya kwanza” alisema Mhandisi Iyombe.

Aidha Mhandisi Iyombe alibainisha kuwa kati ya wanafunzi 1,864 sawa na asilimia 47.58 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati ambapo kati yao   wasichana 1,099 na wavulana 765.

Mhandisi Iyombe aliongeza kuwa katika masomo ya Sanaa na Biashara wanafunzi takribani 2,054 (52.42%) wamechaguliwa kujiunga na masomo hayo, ambapo kati yao wasichana ni 1,314 na wavulana 740.

“Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili atakuwa amepoteza nafasi hii” alisema Mhandisi Iyombe.
Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano awamu ya pili mwaka 2016 inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz.

Hawa ni mastaa wa US waliodai wataihama nchi hiyo Donald Trump akishinda Urais

$
0
0
Orodha kubwa ya mastaa wa Marekani imeapa kuihama nchi hiyo iwapo Donald Trump atashinda uchaguzi na kuwa rais.

Iwapo mgombea huyo wa chama cha Republican akishinda, mastaa kama Jon Stewart, Cher, Barbra Streisand, Samuel L. Jackson, Chelsea Handler na Lena Dunham wamesema watahamia Canada au nchi zingine duniani, lakini sio kuwa chini ya uongozi wa bilionea huyo mwenye mdomo mchafu.

“If he were elected, I’m moving to Jupiter,” aliandika muimbaji mkongwe, Cher.

Kwa upande wake muigizaji mkombwe, Jackson alisema, “If that motherf- -ker becomes president, I will move my black ass to South Africa.”

Hata hivyo wapo mastaa ambao awali waliwahi kutoa ahadi kaka hizo wakazivunja pindi George W. Bush alipoingia White House mwaka 2000.

Wasichana kunigombania siyo dhambi – Steve Nyerere

$
0
0
Msanii mkongwe wa filamu Steve Nyerere amedai wasichana kugombana kwa ajili ya staa ni jambo la kawaida hivyo yeye ashangai kusikia bado kuna wasichana wanagombana kwa ajili yake.

Akiongea katika kipindi cha Uhondo cha EFM wiki hii, Steve Nyerere amedai ameshazoea kusikia wasichana wakigombana kwa ajili yake.

“Unapozungumzia kuna watu waligombana kwa ajili yangu, kwangu mimi kama staa inawezekana labda wameonyeshana kwenye picha, huyu ndo mpenzi wangu,” alisema Steve. “ Lakini unapokuwa super stars kuna watu wanampenda Will Smith yupo Marekani, kuna wabongo wanapigana kwa ajili ya Kim Kardashian. Kwa hiyo mimi nataka kusema inapofikia sehemu fulani ya mafanikio na watu wakakujua siyo dhambi kuongelewa, hata kwangu siyo dhambi, mimi napenda waendelee kuniongelea hivyo na kunipigania hivyo kwa maana ni staa,”

Mwigizaji huyo amesema kwa sasa anaishi na mwanamke na pia ana watoto.

SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Septemba 7, Ikiwemo Magufuli Kuwapa Wadaiwa NHC Siku 7

$
0
0


SOMA Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Septemba 7, Ikiwemo Magufuli Kuwapa Wadaiwa NHC Siku 7
Viewing all 104781 articles
Browse latest View live




Latest Images