Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live

MMMHH...HIII NI KWELI AMA NDIO SIKU YA WAJINGA...ETI DIAMOND NA MAMA YAKE...MHHH

$
0
0
Du! Nimekutana na Hii Screen Shot ya Gazeti hilo hapo juuu mpaka it almost made me choke on my water....alafu Baadae nikakumbuka leo ni siku ya wajinga.....Mweeeee

SIMBA WAJUTA KUMFUKUZA KIBADENI...NI BORA MARA MIA KULIKO HUYU KOCHA MZUNGU

$
0
0
Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Simba,  Zdavko Logarusic ‘Loga’  ametimiza mechi 10 za Ligi Kuu Bara akiwa amekusanya pointi 12  lakini amezidiwa na Abdalah Kibadeni, ambaye aliinoa na timu  hiyo kwenye mzunguko wa kwanza kwani alikusanya pointi 20 katika idadi hiyo ya mechi.

Simba ikiwa chini ya Loga tayari imepoteza nafasi ya kuwania nafasi tatu za juu baada ya kufungwa Jumapili iliyopita na Azam 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hivyo kubaki nafasi ya nne na pointi zake 36.

Azam inaongoza ligi ikiwa na pointi 53, wakifuatiwa na Yanga (46) na Mbeya City imekamata nafasi ya tatu na pointi 45 wakiiacha Simba kwa tofauti ya pointi tisa wakati zimebakiza michezo mitatu.

Loga alikabidhiwa jukumu la kuinoa Simba, Desemba mwaka jana baada ya uongozi wa klabu hiyo kumfuta kazi Kibadeni na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo kwa madai ya kutoridhishwa na matokeo ya timu yao.

Wakati huo Simba ilikuwa ikishika nafasi ya nne ikiwa na pointi 24.

Kibadeni alidumu katika klabu hiyo kwa kipindi kisichozidi miezi sita na kuiongoza kushinda mechi tano, wakitoka sare tano katika michezo 10 kabla ya kufungwa na Azam.

Mcroatia huyo aliyeanza kibarua chake kwa kishindo kwa kuiongoza Simba kushinda mabao 3-1 dhidi ya Yanga katika mechi ya kirafiki ya `Nani Mtani Jembe’, alishindwa kuhamisha mafanikio hayo katika ligi.

Tangu Januari 26, mwaka hu, Loga ameiongoza Simba kushinda mechi tatu tu, akitoka sare tatu pamoja na kufungwa mechi nne dhidi ya Mgambo Shooting (1-0),  Coastal Union SC (1-0), JKT Ruvu (2 - 3) na Azam FC 2-1.

 Logarusic alisema: “Nashangaa tunacheza sisi lakini tunafungwa, nafikiri ni kutokuwa makini, tunacheza kwa kufikiria pasi na mashuti,” alilalamika kocha huyo wa zamani wa Gor Mahia ya Kenya.

Naye nahodha wa Simba, Nassor Masoud ‘Cholo’ alisema matokeo mabaya waliyoyapata kwenye kipindi hiki ni funzo kwao na sasa wajipange kwa ajili ya msimu ujao.

Cholo alisema: “Tulichokipata, kinatukumbusha kuwa, duniani kuna kupanda na kushuka, sisi tumeshateleza haina jinsi, tukubaliane tu na matokeo haya.”

MAKACHERO WA KAGAME WAKAMATWA DODOMA

$
0
0
Mashushushu wanawake wanne raia wa Rwanda wanaoaminika kutumwa na Rais Paul Kagame wamekamatwa mjini Dodoma. Wamekamatwa wakiwa wameshajenga uhusiano wa karibu na baadhi ya viongozi waandamizi pamoja na wajumbe wa Bunge la Katiba.

Pamoja nao Rwanda inadaiwa kuingiza makachero wengine wengi ili waungane na wakimbizi wa Kitutsi walioingia hapa nchini katika miaka ya 1958/1959 na mwaka 1994. Habari kutoka vyanzo vya uhakika zinasema wapelelezi wengi wamekuwa wakiingia nchini kupitia Karagwe mkoa wa Kagera, ambako kumeanza kuonekana kama sehemu ya Jamhuri ya Rwanda.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Tanzania imethibitisha kukamatwa kwa makachero wanawaeke wanne raia wa Rwanda, wakijifanya ni makahaba, lakini baada ya uchunguzi imebainika pasi na shaka kwamba ni makachero toka Rwanda. Ukahaba unatumika kama moja ya nyezo adhimu katiak shughuli za ukachero.

Duru za uchunguzi zimebaini kuwa wanawake hao ni sehemu ya makachero waliotumwa kuichunguza Tanzania, kwa lengo la kulinda maslahi ya Rwanda. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mathias Chikawe, amethibitisha kukamatwa kwa wanawake hao, lakini amekataa kuingia ktika undani wa suala hilo.

Habari ipo kwa kirefu gazeti la Jamhuri.

NAMPENDA KWASABABU ANANIGUSA PENYEWE KWENYE KIPELE

$
0
0
Nimepatikana mwenzenu, nimekutana na kijana hana adabu hata kidogo, amechukua moyo wangu mzima mzima. Kijana anasura mbaya yani hana hata mvuto ila uwanjani usipime, mambo anayo ni fanyia naogopa hata kusimulia ila kiufupi ni kwamba anaweza ndio mana niko nae. Mhhh Hatari....!

UMESHAWAHI JIULIZA BARACK OBAMA ANATUMIA SIMU GANI? CHECK HAPA

$
0
0
For the past eight years, the well-connected world leader would use nothing but a BlackBerry to get their email on the move – and it is still Barack Obama’s phone of choice, according to a report published by the UK’s premier newspaper, the Guardian.

The newspaper says Mr Obama uses a model specially enhanced by the US National Security Agency. But the news earlier this month that the White House Communications Agency is testing other phones, including models by Samsung and LG, sent shivers through fans of the struggling Canadian smartphone company, which has just announced an annual loss of $5.8 billion.

“For a world leader, security is much more than just having a passcode on your phone; it also means protecting it against attempted incursions from all the amateur and professional hackers, and more importantly spy agencies, who want to know to whom, when, what and where you have been speaking and reading

“For a country’s leader to have their phone eavesdropped is the ultimate failure of their national spy agency, and a huge loss of face. With enhancements, BlackBerry has been the spy agencies’ phone of choice to guard against that so far. Now, though, Apple and Samsung – the two largest makers of smartphones – are starting to knock on the security services’ doors,” says a report published by the Guardian on Sunday.

And what if BlackBerry goes away? Though it may have pulled out of a death spiral, BlackBerry’s position as the phone of choice for top executives is less clear – and Apple has been touting (pdf) ever-improving security on its iPhone, which has been edging out BlackBerrys even in financial institutions such as Goldman Sachs, once a redoubt for the keyboard-reliant phones. Yahoo, Pfizer and Halliburton have all said sayonara too.

As rival devices improve their security, it could only be a matter of time before Apple or Samsung becomes the US leader’s phone – perhaps not during Obama’s presidency, but in his successor’s.

Though the White House press secretary has insisted that “the executive office of the president is not participating in a pilot programme” to replace Obama’s BlackBerry, it might only be a matter of time – though if Hillary Clinton succeeds him, her well-known affinity for it could extend its survival just a little longer.


UTAJIRI WA MASANJA MKANDAMIZAJI NI HATARI TUPU...DIAMOND NA JIDE CHA MTOTO

$
0
0
UTAJIRI wa komediani maarufu nchini  Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ni kufuru! Tena unatisha na sasa anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wanaomiliki fedha na mali nyingi Bongo, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.

Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa mbele ya usafiri na mjengo wake.

HABARI MEZANI

Awali, habari kuhusu utajiri wa Masanja ilitua mezani mwa gazeti hili kama kidokezo, hapo mwandishi wetu akaingia mzigoni na kuanza kuchunguza kwa kina mali anazomiliki msanii huyo na kugundua kuwa ni kati ya mastaa mabilionea Bongo.

“Masanja sio yule tena. Ana mpunga (fedha) mrefu sana. Hakuna msanii wa maigizo Bongo anayeweza kumfikia kwa sasa. Hao wengine ni mbwembwe tu, lakini pesa imelala kwa Masanja,” kilipasha chanzo chetu.

Kikaongeza: “Kwanza ana ghorofa lipo Tabata, hapo ndipo anapoishi. Pia ana magari kibao ya kifahari, mashamba ya mpunga na Kampuni ya OK Security inayolinda sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi nyeti nchini.

Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ akiwa kwenye pozi na miongoni mwa magari yake.

“Ni msanii gani mwenye kampuni kubwa kama ya Masanja? Wengi wanaishia kudai wanatayarisha filamu ambazo hata matunda yake hayaonekani.”

Uchunguzi wetu ulibaini ukweli wa mali za msanii huyo na mambo mengine mengi yanayoingia kama vyanzo vya mapato yake.

MAGARI SITA

Ilibainika kuwa, Masanja anamiliki magari sita, yakiwemo ya kifahari. Baadhi ya magari hayo ni Toyota Land Cruiser V8, Nissan Hardboad na Toyota Verossa.



NYUMBA TATU BONGO

Pia, mkali huyo wa kuvunja mbavu, anamiliki nyumba tatu za maana jijini Dar es Salaam, moja ni ghorofa ipo Tabata, nyingine Kigamboni na nyingine haifahamiki eneo rasmi ilipo.

Hata hivyo, imebainika kuwa mbali na mijengo yake hiyo iliyopo jijini Dar, nyumbani kwao Mbarali, Mbeya ana mjengo wa maana.



MASHAMBA KIBAO

Msanii huyo hayupo nyuma kwenye kilimo, ana mashamba kadhaa Kigamboni jijini Dar es Salaam lakini linalotia fora ni lile lililopo Mbarali lenye ukubwa wa hekari 50 ambalo analima mpunga.



NI MSANII WAMAIGIZO TAJIRI ZAIDI?

Kwa utajiri huo, ipo minong’ono kuwa, nyota huyo anaweza kuwa kwenye namba za juu za wasanii wa maigizo wenye mkwanja mrefu.

Wengine wanaotajwa kwenye orodha ya waigizaji matajiri Bongo ni Husna Posh ‘Dotnata’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ na Amri Athumani ‘Mzee Majuto’.

MATAJIRI BONGO FLEVA

Katika muziki wa Bongo Fleva, wasanii wanaoaminika wana utajiri mkubwa zaidi ni Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Joseph Haule ‘Profesa Jay’.

Wasanii hao wanamiliki mijengo ya maana, achilia mbali magari ya kifahari na miradi kadhaa.



MASWALI KUHUSU MASANJA

Utajiri wa Masanja umeonekana kuibuka ghafla huku vyanzo vyake vya kumwingizia kipato vikijulikana ni sanaa ya uigizaji, muziki na huduma ya uchungaji.

Je, kwa uigizaji tu katika Kundi la Orijino Komedi ‘OK’ ndiko alikopata mkwanja huo na kuanzisha miradi hiyo mikubwa?

Kama ndiyo, kwa nini memba wenzake ndani ya kundi hilo hawana maendeleo makubwa kama yeye?

Kazi nyingine ya Masanja ni muziki wa Injili ambapo kwa sasa albamu yake ya Hakuna Jipya iko sokoni. Je, albamu hiyo na shoo anazofanya zinaweza kuwa chanzo cha utajiri huo?

Lakini pia Masanja ni mchungaji ambaye anahudumu katika Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) ‘Mito ya Baraka’ lilicho chini ya Askofu Bruno Mwakiborwa. Je, mshahara anaoupata kutokana na huduma hiyo unaweza kuwa chanzo cha mapato yake?

Risasi Mchanganyiko halikutaka kupasua kichwa, juzi lilimsaka Masanja kwa simu na kumhoji juu ya mali zake ambapo kwanza alithibitisha kweli anamiliki mali hizo na nyingine ambazo hakupenda kuzitaja.

“Ni kweli nina nyumba tatu hapa mjini, kampuni ya ulinzi na mashamba ya mpunga eka 50 nyumbani Mbarali, Mbeya. Kuhusu magari pia ni kweli kabisa. Mimi ni mtumishi sitakiwi kusema uongo,” alisema Masanja.

FAHAMU HISTORIA FUPI YA WASTARA SAJUKI TOKA ALIPO ANZA KUIGIZA MPAKA SASA

$
0
0
Wastara Sajuki si jina geni kwenye ulimwengu wa bongomovies. Ni mmoja wa wanadada wanofanya vizuri sana kwenye filamu nchini na wenye ushawishi mkubwa sana ndani ya tasnia hii. Ifuatayo ni historia fupi ya mwanadada huyu.

Early life
Wastara Juma Issa alizaliwa Septemba 27, mwaka 1983 huko mkoani Morogoro. Mwaka 1989 akajiunga na Shule ya Msingi Mvomelo ‘A’ na kufanikiwa kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 1995. .Mwaka 1996 alijiunga na Sekondari ya Agricalture mkoani humo.

Career
Mwaka 1999 Wastara aliingia rasmi kwenye sanaa ya maigizo na filamu yake ya kwanza kucheza iliitwa Utaishia kunawa akiwa na gwiji wa vichekesho nchini King Majuto.



Mwaka 2004 mpaka 2006 alianza kuonekana kwenye mchezo wa Miale uliokua unarushwa na kituo cha television cha ITV

Akutana na Jennifer Mgendi

Wastara hakudumu sana kwenye kundi hilo, alikutana na kina Jenifa Mgendi ambaye pia walifanikiwa kuigiza naye filamu iliyowashirikisha baadhi ya wasanii wa kitambo akiwamo Dino na wengineo.

Mwaka 2007, Wastara alifanya usahili kwenye filamu ya mdau Ande John iliyofahamika kama Pelemende, akafaulu na kuigiza kwenye filamu hiyo kisha zikafuata filamu nyingine kama Penina kabla ya kutimkia nchini Kongo kufanya biashara.



Akutana na Sajuki

Aliporejea kutoka Kongo, Julai, 2007, Wastara aliitwa na mwigizaji Shija ambaye alimuomba aigize naye filamu baada ya kumuona kupitia kazi mbalimbali alizowahi kufanya hapo nyuma.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Wastara kukutana na Sajuki ambaye sasa ni mumewe wa ndoa kwani Shija alikuwa akifanya kazi zake za uigizaji kwa kupata msaada mkubwa kutoka kwa Sajuki.

Wastara alicheza filamu kadhaa akiwa na Shija pamoja na Sajuki hadi baadaye walipokuja kugundua kuwa matatizo ya uhusiano yaliyowakuta (Sajuki na Wastara) yanafanana kwani kila mmoja wao alitendwa na mpenzi wake ndipo walianzisha uhusiano wa kimapenzi.

 “Eeeeh! Kazi na dawa, tuligundua kuwa matatizo yetu yanafanana. Taratibu tukaanza uhusiano ili kufarijiana,” anasema Wastara.

FILAMU WALIZOZALISHA

Wakiwa ndani ya umoja wao, Sajuki na Wastara, walifanikiwa kuporomosha filamu zaidi ya 20 ikiwemo Mboni yangu iliyopata umaharufu mkubwa

 APATA AJALI

Wakati harakati za ndoa zikiwa zimepamba moto, mwaka 2009 Wastara alipata ajali ya pikipiki iliyosababisha akatwe mguu.

Wakati huo tayari alikuwa ameshachumbiwa na Sajuki.

Juni mwaka huo huo,

wasanii hao waliopitia changamoto kadhaa za maisha, walifunga ndoa na kuanza rasmi maisha ya mume na mke.

Baada ya hapo, kupitia kampuni yao ya Wa-Jey waliendelea kuzalisha filamu kama Briefcase, The Killers, Seven Days na nyinginezo.

Tarehe 2 mwezi wa kwanza (1) mwaka 2013 Wastara alimpoteza mume wake kipenzi Juma Kilowoko (sajuki) jambo lillilosababisha kupumzika sanaa kwa muda na badae alilejea kwenye tasnia na kutoa filamu ya Shaymaa amabayo ilipata umaharufu mkubwa

Nampaka sasa anaendelea kufanya filamu nchini Tanzania

WATANZANIA WALIOLIPULIWA NA OSAMA KULIPWA Sh 672 BILION

$
0
0
Watanzania wanne waliojeruhiwa katika mlipuko wa bomu katika ubalozi wa Marekani mwaka 1998 na wengine watano waliofariki dunia katika mlipuko huo watalipwa fidia ya Sh672 bilioni, kiwango ambacho ni sawa na bajeti ya wizara nne za Tanzania.

Watanzania hao waliuawa na wengine kujeruhiwa katika moja ya mashambulizi pacha yaliyotokea kwa wakati mmoja jijini Dar es salaam na Nairobi, Kenya na ambayo yaliratibiwa na Osama Bin Laden akitumia mtandao wa kundi la Al Qaeda mwaka 1998 kwenye ofisi za balozi za Marekani.

Katika mashambulizi hayo yaliyotokea saa 4:00 asubuhi Agosti 7, 1998, Wakenya 200, Watanzania 10 na Wamarekani 12 walipoteza maisha na pia magaidi wawili nao walikufa.

Kati ya Watanzania 10, ni kesi za watu wanne tu waliouawa tu zilizofunguliwa kudai fidia ya watu hao kupoteza maisha.

BONDIA CHEKA AWA MTORO DARASA...KITI CHAKE CHAOTA KUTU

$
0
0
BONDIA Francis Cheka ametajwa kuwa mwanafunzi anayeongoza kwa kukacha vipindi vya darasani chuoni anakosoma huku mwalimu wake, James Mkisi akibainisha kuwa kutokana na utoro wa bondia huyo hata kiti na meza yake darasani vimeanza kuweka kutu.

Cheka alipewa ofa ya masomo na Chuo cha St Joseph cha mjini Morogoro mwezi mmoja baada ya kutwaa taji la Dunia la WBF Agosti mwaka jana kwa kumpiga Phil Williams wa Marekani jijini Dar es Salaam.

“Inavyoonekana Cheka hataki shule, tangu tumempa nafasi hii aliingia darasani siku moja na hakuonekana tena, mwezi uliopita alikuja akatuambia sasa anahitaji kusoma, tukamsha§uri aanze upya muhula ulioanza Machi kwa kuwa wenzake walimuacha.

“Baada ya hapo hakuonekana tena, huyu mwanafunzi anatuchanganya sana inaonekana hataki kusoma ukizingatia alishakuwa bingwa wa Dunia,” alisema mwalimu Mkisi.

Alisema hata uwaziri wa michezo aliokuwa amepewa hivi sasa cheo hicho kinakaimiwa na naibu wake baada ya Cheka kutoonekana kwa miezi kadhaa sasa na kubainisha kuwa bado nafasi waliyompa ipo palepale hadi mwishoni mwa mwaka huu kama hajatokea shauri yake.

Cheka alikiri kutokwenda shule na kusema kuwa alibanwa na shughuli za kifamilia kama baba ingawa anajipanga kuanza masomo yake ya kompyuta, biashara na lugha aliyopangiwa kusoma chuoni hapo.

JAMAA AKESHA AKIOMBA MUNGU KATI YA MCHEPUKO NA MKE WAKE WA NDOA NANI NI KUTOKA KWA MUNGU?

$
0
0
Habari wapendwa,kuna kitu kinanikera mpaka nimeamua kuongea na inabidi tumuogope Mungu,kuna jamaa mmoja alioa akafukuza mke wake,badae akamrudia mke wake Mungu akawajalia mtoto mmoja,wakati huyo mke ana mimba jamaa akachepuka bahati mbaya mchepuko ukapata ujauzito,jamaa akachanganyikiwa kwa sababu aliuambia mchepuko hana mke yani walishaachana,sasa jamaa akakimbilia nigeria kwa TB Joshua ili aambiwe nani mke kutoka kwa Mungu wakati mke wa kwanza alifunga nae ndoa,baada ya jamaa kurudi akatulia ndani ya miezi 6 huku akimuomba Mungu amuonyeshe,wiki 2 zilizopita kasema Mungu kamuonyesha mchepuko ndio mke wake,ila nigeria hakuambiwa kitu,sasa kwa mke halali hataki kupasikia wala habari za mtoto.

TAHADHARI..UWIZI WA KITOTO KATIKA MA-BANK

$
0
0

Kuna wizi unafanyika kwenye mabenk kwa kweli unatia aibu na kujidhalilisha tu.

Nilikua mlimani city natoa pesa kwa ajili ya kumtumia jamaa yangu yuko Exim bank mimi niko CRDB, Basi nkatoa pesa CRDB nkaenda pale EXIM mlimani city hapohapo, Nkahudumiwa na kijana wa dirisha la kwanza toka mlango wa kuingilia. 

Basi nkamkabidhi jamaa hela kama milioni tatu,akahesabu ziko sawa nkampa karatasi ya deposit akaangalia kwenye desktop yake then akanambia hiyo akaunt(ya jamaa ninaye mtumia) iko dormant jamaa hakuitumia muda mrefu, basi jamaa akanirudishia hela zangu, unfortunately muda wa kufunga bank ulikua umefika, nlikua katika watu wa mwisho kuhudumiwa. 

Basi nkatoka nkampigia jamaa na kumweleza hali halisi, jamaa akakataa na kusema jana tu alitoa pesa kwenye akaunt yake, nkamwambia nakutumia kwa tigo pesa akakubali. Nkaingia ofisi za tigo pesa hapohapo mlimani city, nkaweka folen. nlipompa cashier ahesabu zimepungua kama elfu 80. nlikasirika sana, kurudi kule washafunga, basi ikala kwangu.

Ila yule jamaa nimemkariri nkikutana nae lazima nimseme na njaa za kitoto.Hivyo wakuu kosa nililofanya ni kumuamini aliponipa sikuhesabu. kuwenu makani na hawa watu.

By dikembe

UGANGA WA MAPENZI..KUMBE NYAMA YA MJUSI NDIO HUCHANGANYWA NA CHAKULA NA KUPEWA MWANAUME

$
0
0
JE UNAYAFAHAMU MAMBO HAYA?


Haya madudu wanayofanyiwa baadhi ya wanaume na akina mama yapo kwa kila kabila, utafiti umebaini kuwa ni moja ya taaluma ya Kibantu katika kuongeza au kuthibiti chachu ya mapenzi na ambayo ikitumiwa vibaya inaweza kumfanya mwanaume kuwa chizi wa akili na pengine kupoteza maisha au kazi yake kabisa.

Ukiacha makabila yaliyozoeleka kwa mambo haya ya wanawake kutumia mbinu hizo za asili kuwavuta wanamume katika mapenzi(!) kama vile waTanga, Wahaya, Wanyakyusa, Wapemba, na makabila ya Pwani, inasemekana yapo makabila mengine, ambayo wanawake wanatumia teknolojia kali zaidi na yenye kutia kichefuchefu kama ukijua kuwavuruga wanaume.

Inadaiwa taaluma hiyo ya asili ambayo kwa sasa imeanza kupotea kutokana na wadada na akina mama wengi kuanza kumjua Mungu inaambatana na matumizi mabaya ya baadhi ya viumbe hai ambavyo huwezi kuvidhania vinaweza kulegeza ujanja na nguvu za mwanaume. Inasadikika kuwa wataalamu wa kutengeneza madudu haya ni wanaume wenyewe (waganga wengi wa kienyeji ni wanaume).

Viumbe hivyo ni pamoja na yule mjusi mweupe na laini anaypenda kuishi katika nyumba zetu (mjusi kafiri) wa jamii hii:

Ukichaganyiwa kwenye menyu (chakula maalumu), hapo utakuwa huchungulii hata barazani, wewe unakuwa ni mtu wa chumbani taulo tu, kila kitu huko huko. Hata kazini hutaki tena.


Pia kuna mijusi wale wanaokaa kwenye mawe au miamba ya mtoni au ziwani:

Ukifanyiwa na mjusi wa aina hizi, inadaiwa kuwa maisha yako ni mdura, ukitoka ndani waenda kazini au kanisani au msikitini, ukirejea tu ni ndani kwenye TV au chumbani na pengine kama ni mtu wa kinywaji wewe kinyawji chako ni cha kuagizia na kuwekewa kwenye jokofu, (friji) mtaani na viwanja unaona nuksi na mama una:

yako mengi tu hii mfano wake tu toa maoni yako.

RAHA YA KUTONGOZWA...

$
0
0
Hivi dada zangu huwa mnaenjoy mkiwa mnatongozwa?

Ni kweli kuwa usipotongozwa kama wiki tu hivi wajisikia vibaya?

Najua kuna suala la umri hapa kwenye sanaa hii ya utongozwaji,

Lakini napenda tu nipate jibu la jumla,

Jamani huwa mnajisikiaje?

DIAMOND AKIWA STUDIO AKIREKODI COLABO NA MNAIGERIA

$
0
0
Maneno yanaumba !!! kwa jitihada zake Diamond Platnumz kama alivyosema kwamba ni lazima Wanigeria watamtambua time hii na kweli ndio inatokea hivyo.
Baada ya kuthibitisha kwamba atafanya kolabo kadhaa Lagos Nigeria Zikiwemo mbili za D’Banj na msanii wake, kazi imeanza kuonekana siku mbili baada ya kutua.
Diamond ameanza na hii ya kurekodi na Mnigeria mwingine mrembo aitwae Waje

CHRISS BROWN AMTUMIA KARRUECHE MESEJI YA MAPENZI AKIWA JELA.."KUMBE HAWAJAACHANA"

$
0
0
So, we guess this means Chris Brown and Karrueche Tran are together again (surprised?).
Breezy left a voice message for his fans and his lady on Tran's phone while still in jail, which she played on speaker and recorded as an Instagram video to share with all of Chris' admirers last night—and also to let everyone know that they're an item.
"I'm callin' all my fans, you know I love y'all, thank you for all the support," you can hear Brown say in the video. "Thank you for everything. The ["Loyal"] video just came out so I hope you all enjoy that. And most importantly, K, Karrueche, I love you. So thank you."

PREZZO AONYESHA VIATU VYA THAMANI ALIVYONUNUA KWA DOLA 995..SAWA NA SH 1,622,844 TZS

$
0
0
Prezzo kama ilivyo kawaida yake kujishow off ..leo amepost picha akiwa amevaa viatu vipya aina ya Giuseppe Zanotti  ambayo gharama yake ni dola 995 za kimarekani , ukibadilisha kwa hela ya Tanzania ni kama Milion moja na Laki sina na ushee hivi.....
-Regina Iwole

MVUA BALAA...EMBU MSHAURI HUYU JAMAAA...MAANA NI KAMA HAJAAMINI

$
0
0
Balaaa la Mvua hilo Jamaa kaamka Asubuhi anakuta hali kama hiyo ahamini macho yake ameng'ang'ani kwenye gari siku nzima...Usiombe yakukute kama huyo jamaa alafu gari yenyewe una week moja ndio limefika kutoka japan na umelinunua kwa Mkopo wa Bank...Mweee Inaumajeeeeee!!

TAREHE YA KUTOLEWA KWA ALBUM MPYA YA MICHAEL JACKSON YATANGAZWA

$
0
0
Yes, Najua huwezi Amini lakini ukweli ni kwamba kuna album mpya ya Michael Jackson Baada ya Miaka Mitano ya kifo chake, Sony na Epic Records, wametangaza kutoa album mpya ya marehemu huyu itakayoitwa "Xscape"

Epic CEO L.A. Reid handpicked eight previously unreleased tracks by Michael Jackson, which have been 'contemporized for modern ears' and added new production by Timbaland and Rodney Jerkins.The album drops May 13th. 
-John K

KAJALA AWAVULIA UVIVU WATU WALIOMTUKANA MWANAYE HUKO INSTAGRAM

$
0
0
Instagram kumechafuka, yani watu wanatukana wanavyojisikia, hawaogopi kitu chochote kile. Matusi hayo yamemkuta kajala, katukaniwa mtoto wake hadi kashindwa kukaa kimya. Hiki ndo alichokiandika Instagram kuhusiana na ishu hiyo.
Nadhani kila binadamu anaufanya kitu anacho penda lkn kama nyinyi wote mnaona mm ninacho fanya nakosea siwezi kuwaraumu nawaomba mnitukane usiku kucha mkilala nitukaneni mkiamka nitukaneni nimeshazoea nilikuwa naumia mwanzo lkn sasa siumii tena ninacho waomba amjui nimepata tabu gani na mwanangu kwaiyo kama anae wakosea ni mm na sio mtoto wangu basi naomba mnitukane mm na umaya wangu msimuingize mwanangu please please nawaomba sana kiroho safi .....

JOKATE MWEGELO ADAI BADO YUPO SINGLE TOKA AMEACHANA NA DIAMOND

$
0
0
Jokate Mwegelo yupo single and ready to mingle.. atleast for now. Staa huyo mwenye vipaji lukuki alisema hayo Jumatatu hii kwenye kipindi kipya cha TV1, ‘The One Show’ anachokiendesha kwa kushirikiana na Ezden Jumanne aka The Rocker.

Katika kipindi hicho cha kwanza kuoneshwa, watangazaji hao walianza kwa kuhojiana wao kwa wao kwanza na moja ya maswali aliyoulizwa Jokate ni kama yupo kwenye uhusiano wowote wa mapenzi. Jokate ambaye pamoja na kuwa muigizaji wa filamu pia ni muimbaji wa muziki na mjasiriamali, alisema kuwa kwa sasa yupo single lakini haimaanishi kuwa wanaume hawamsumbui kumtaka kimapenzi.

Jokate amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mchezaji wa basketball wa timu ya Oklahoma City Thunder, Mtanzania Hasheem Thabeet pamoja na uhusiano uliodumu kwa kipindi kifupi na staa wa muziki, Diamond Platnumz.
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live




Latest Images