Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Baada ya Kudaiwa Anavaa Cheni Feki..Jack Wolper Aonyesha Cheni zake za Dhahabu

$
0
0
Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amewaziba mdomo wanaomsema anavaa cheni fake za dhahabu.

Mwigizaji huyo ambaye kwa sasa yupo kwenye mahaba mazito na Harmonize, amesema kwa sasa hataki kuonyesha vitu kama hivyo kwa kuwa wakati wake wakufanya hivyo ulishapita.

“Stylish flevaaaa zone msioneane wivu nikiwa tajiri nitaweka kila mmoja sehemu yake wanangu sawa madinizii. Sema mimi mswahili sana najipenda navyowashuhulikia waswahili wenzangu kwa maneno yao yakutunga, msinifanye niwe naonyesha paka nachokula kila siku maana naweza pia,” aliandika Wopler Instagram.

Aliongeza,

“Angalieni maisha yenu, kwahyo tusipofanya show off sio hatuna, vingine tunawaachia chipukizi jamani sahivi tunatakiwa tuonyeshe magorofa . Stay tune Mazafokoooziii delivere,”

Kwa sasa mwingizaji huyo amejikita zaidi kwenye biashara kuliko katika kuzalisha filamu.

WEMA Sepetu Achukizwa na Mtangazaji Soudy Brown Kumrekodi Mama yake Bifu la Man Fongo

$
0
0
Baada ya kusambaa audio katika mitandao ya kijamii ambazo mama Wema anasikika akimpandishia mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown, Wema Sepetu amemvutia wire mtangazaji huyo akimtaka kuacha kumzungumzia mama yake katika mambo ambayo hayaeleweki.

Chanzo mgogoro huo mkubwa kati ya Wema Sepetu dhidi ya Christian Bella na Man Fongo kwa pamoja, unahusiana na masuala ya show ambazo ‘design’ wamezungukana na mama ameingilia kati!.

Hivyo Soudy kama kawaida yake aliongea na Man Fongo kujua upande wake wa mkasa huo, lakini alijikuta katika wakati mgumu alivyoamua kumpigia mama Wema ili apate chochote kitu kuhusu ubuyu huyo.

Ijumaa hii Wema Sepetu kupitia kipindi cha U Head, aliamua kumtolea uvivu mtangazaji huyo akimtaka kutomwingiza mama yake katika mambo alioyaita yakijinga.

“Soudy hebu acha kumweka mama kwenye hayo mambo, nakuomba mama yangu sijamuweka kwenye hayo mambo, mama yangu ni mtu mzima namweshimu, nakuomba achana na mambo hayo sijui kumpigia simu, sijui maswala ya Man Fongo, nani anamjua Man Fongo?,” aliuliza Wema. “Man Fongo kweli yule wakukaa kubishana na mama yangu, kwa nini mnamrekodi mama yangu hivyo, mimi sipendi,”

Barua ya Wazi Kwa Mwanamuziki Alikiba

$
0
0
Wasalaam wakuu!
Sio siri uzalendo umenishinda haswaa! Yote ni juu ya Alikiba "Kingkiba" Maana mpaka sasa nashindwa kuelewa ni Nani aliyekuroga hadi unaendesha mziki wako kizaman sana.

Uliporudi na "Mwana" ilikuwa ni nyota njema na tumain jipya kwa sisi mashabiki wako dunian kote, Kweli hakuna anayebisha kwamba kuanzia "Mwana, Chekecha Cheketua, Nagharamia mpaka sasa "Aje" umefanikiwa kweli kweli kuzitingisha kuta za mabaazazi na mahafidhina wa Mziki wa Bongflava waliotaka kujimilikisha mziki kwa kujifanya miungu watu, Kwa hilo nakupa pongezi.

Ni ukweli uliowazi kuwa umerudi na Kasi ya "4G" ila ubaya ni 4G inayosoma "H", Alikiba sisi fans wako umeendelea kututesa kwa muda mrefu sana hasa kwa mambo yako unayofanya sisi hayatupendezi kabisa, Nilitaka waraka huu uwe wa siri ila mbinu zote hizo zimeshindikana. Na haya yafuatayo ni miongoni mwa mambo yanayotutesa sisi washabiki zako.

1. UKOSEFU WA COLLABO ZA KIMATAIFA, maana tangu ujinasibu kuwa una collabo na fally pupa na wasanii wengine wakubwa ni miaka imepita, Kweli Alikiba wewe ni wa kutupa collabo za wakina Nuh mziwanda, Abbyskilz, Dayna nyange, ommy dimpoz, Hapa najiuliza target yako hapo ni market ipi? Ali mbona unatutesa kiasi hiki?For How long we gonna wait?

2. PAGE ZAKO KWENYE SOCIAL MEDIA ZINABOA SANA, Mi nachofahamu social media ni sehemu adhimu na muhimu sana ya mafans kuwasiliana na msanii wao, kwa kupata updates mbalimbali, ila kwako hili suala limekuwa kinyume, Acc zako mfano Instagram 70% ya posts zako ni birthday za watu, kazi zako hatuon kabisa ukipost, Pia msanii gani muda mwingine unakaa week nzima bila kupost kitu kabisa, Unataka fans wako wafanyaje?

3.MSIMAMO WAKO KUHUSU TUZO, hapa napo tunashindwa kukuelewa je unataka tuzo au hautaki? Tangu mwaka umeanza tumeshuhudia ukipata nominations za tuzo mbalimbali Africa( Afrimma, UEA awards, Afrima Nigeria, AEUSA,AYCA Awards, African Oscar awards etc) lakin hata siku moja hatujawah kuona ukiripost au kuapreciate hicho kitu, mfano mwezi August ulishinda tuzo 2 za #AfricanOscarChoiceAwards lakini cha ajabu umekausha hadi leo kurepost hicho kitu, hapa sasa tunabaki njia panda, je unadharau waandaaji wa tuzo au sisi fans wako tuliokesha tukikupigia kura? Hapa tunaomba majibu au tupotezee kukusuport kwenye tuzo.

4: UCHELEWESHAJI WA PROJECT ZAKO, Hapa napo Alikiba umekuwa jipu sugu, tunashindwa kuelewa je tatizo ni wewe au management yako? Porojo na ahadi zimekuwa nyingi bila vitendo, Tunahitaji majibu ya kutosha zaidi tunataka tuone tofauti ya msanii wa Sony global music na wasanii wa mchangani

5. USIRI KATIKA MIKATABA NA MALI ZAKO, Hapa napo ndio kumekuwa na jipu sugu lenye ukungu kabisa, Sababu mara nyingi umekuwa ukiulizwa maswala adhimu kuhusu profit unazopata kutokana na mikataba yako ya Sony music na endorsement unazopata kama ubalozi wa Wild aid, ubalozi Jam food nutrition, Mali unazomiliki etc, Lakin umekuwa na kigugumizi kujibu, Mashabiki zako tuna kiu ya kusikia msanii wetu ananufaika vipi na mziki wake, na hili pia ni haki yetu ya msingi. Tuna mengi sana ila kwa leo tuishie hapa.

Imeandikwa na Shardcole

Chidi benzi Adaiwa Karudia Matumizi ya Madawa ya Kulevya

$
0
0
Ama kweli sikio la kufa halisikii dawa, hatimaye Chidi benzi licha ya kuripoti hapo awali ya kuwa ameachana na madawa ya kulevya na kurudi na ngoma iitwayo chuma na kufanikiwa kupenya na hiyo nyimbo, chidi kaamua kurudia katika matumizi ya dawa za kulevya

Mwana harakati wa kupambana na matumizi ya dawa za kulevya Kalama Masudi au ukipenda muite Kalapina amehaidi kumtafuta kwa udi na uvumba chidi benzi ili amrudishe tena sober house lakini akasema pia hii ndiyo itakuwa mara yake ya mwisho kumsaidia , akirudi tena atamuacha kwa kuwa ana muona chidi ana kitafuta kifo kwa nguvu kwa kuwa madawa ya kulllevya anayo tumia chidi benzi au chidi chuma kama anavyojiita mwenyewe ni makali sana

Shilole: Sitaacha Kutoka na Serengeti boys, Mniache na Maisha yangu

$
0
0
Mwanamuziki wa Bongo flava asieishiwa vimbwanga mitandao kwa skendo ya kutoka na vijana wadogo walio chini ya umri wake(Serengeti Boys) amefunguka na kusema asipangiwe ni nani wa kuwa naye na ataendelea kutoka na viboi vyake.

Akiongea mbele ya Camera za eNewz, Shilole amesema mashabiki wanahitaji yeye awe na mzee lakini yeye haoni haja ya kuwa na mzee kwa kuwa hawawezi ‘kumpetipeti’ na kuwataka wamuache achague anachotaka kwa vile nyumbani yeye ni Zuwena na jukwaani ni Shilole.

“This is my life, nikiwa nyumbani ni Zuwena na nikiwa kwenye TV ni Shihi, maisha yangu mimi ya nyumbani au maisha yangu binafsi wao yasiwahusu sana ninaangalia upendo wangu upo wapi.

Nikisema niangalia mashabiki nini wanacho taka wao wanataka niwe na mzee, sasa maisha yangu nianze kuwa na mzee nianze kumburuza! mimi ninahitaji kijana aanze kunipetipeti” Alifunguka Shilole kwa madaha.

Lakini Shilole alimalizia kwa kusema kuwa mpenzi wake mpya wa sasa ni msanii wa muziki na wala hajawahi kubahatika kuwa na mpenzi ambaye ni dakitari au mwalimu, bali ana nyota ya kukutana na wasanii tu.

Akifafanua zaidi kwenye muonekano wake katika video ya Rayvan, Shilole amesema hakuvaa chochote ndani(chupi) zaidi ya ‘night dress’, hivyo ilimbidi atupie kileo ili aweze kufanya scene hiyo.

Jinsi ya Kumpata Mpenzi Mwenye Mapenzi ya Kweli...

$
0
0
Habari za jumapili wapendwa, bila shaka sote tu wazima wa afya na wale ambao afya zao zina mushkeli Mungu awatie nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Kila mmoja wetu anatamani au kupenda kuwa katika mahusiano yenye furaha na amani. Kila mmoja anapenda kuwa na mpenzi mwenye mapenzi ya kweli na pasiwe na chembe za kusalitiana.

Tunaishi katika ulimwengu wenye changamoto nyingi na kiwango cha uaminifu kinazidi kushuka kila kukicha. Katika hali kama hiyo watu wengi wamejikuta wapo njia panda wasijue washike wapi au waachie wapi kwenye suala zima kuwa kwenye mahusiano. Leo ningependa kushirikiana nanyi katika namna nzuri ya kumpata yule mwenye kukidhi matakwa ya nafsi yako hata katika nyakati hizii ngumu na za tabu kama ifuatavyo:-

Badilisha mtazamo wako na mfumo wa maisha yako 

Kwa ukawaida watu tunaokutana na kushirikiana nao kwenye maisha yetu ni watu waliovutwa na namna sisi tulivyo ambapo kupitia watu hao ndio unapata taswira kuwa wewe ni mtu wa aina gani.

Tunapata wapenzi wa hovyo hovyo kwa kuwa sisi wenyewe ni wa hovyo hovyo
Tunapata wapenzi wasio waaminifu kwa kuwa tunajiweka katika mazingira ya kutoaminika
Tunapata wapenzi wa kututumia na kutuacha kwa kuwa tumejiweka katika mtazamo wa kutumiwa na kuachwa
Jinsi tunavyojiweka ndivyo tunavyowavutia watu wa kaliba yetu. Kabla ya kuweka masharti yako ya mpenzi umtakaye kwanza unatakiwa ujiangalie wewe mwenyewe kuwa unaendana na sifa hizo? Mfumo wako wa maisha unawavutia watu wa aina hiyo?

Utakuja kugundua kuwa hata wewe mwenyewe haufanani na hilo unalolitaka, sasa utapataje kitu usichofanana nacho? Ndege wafananao huruka pamoja. Unatakiwa kwanza ubadilike ili watu wazuri waje kwenye maisha yako!!!

Rahisisha mahitaji yako

Katika ulimwengu wa nyama na roho hakuna mkamilifu kati yetu kwa hiyo ni vigumu kumpata mtu mwenye sifa zote unazozitaka wewe kwa kuwa hukushiriki hata chembe kwenye uumbaji huo. Hata wewe mwenyewe una mapungufu yako tena pengine ni makubwa sana isipokuwa waungwana kwa kuwa wanajua kuwa hakuna mkamilifu wanaamua kukuvumilia.

Weka mahitaji yako machache na yale ya msingi. Watu wanadumu kwenye mahusiano si kwa kuwa ni wakamilifu bali kwa uvumilivu na kusameheana. Toka katika ulimwengu wa fikra pambana na hali halisi. Watu wengi wamejijengea taswira nzuri za mahusiano katika ulimwengu wa kufikirika. Taswira nzuri walizojijengea na kuishi nazo ni ngumu kuziweka katika hali ya kawaida kwa kuwa nafsi zao zina matarajio makubwa kupita ukweli ambao upo mezani.

Matokeo ya watu hao ni kubadilisha wenzi kila mara kwani wanapambana kuuridhisha ulimwengu wa nafsi. Ndio hao unakuja kuona anakwambia nataka mwanamume awe mrefu kidogo, mweusi kidogo, awe na vibonyeo kwenye mashavu na awe na kifua kilichojengwa kimazoezi wenyewe wanasemaga six pack.

Wanaume nao utawasikia nataka mwanamke mwenye urefu wa wastani, awe na umbo namba nane, maziwa yaliyojaa vyema kifuani na awe na neema za Allah. Kwa kawaida hayo ni maelezo yanayotoa taswira ya kupendeza lakini katika ulimwengu halisi ni ngumu kukidhi matakwa hisia hizo.

Kuwa na subira

Wahenga walinena kuwa subira huvuta kheri. Wakati mwingine mambo mazuri yanachelewa kutufikia kwani siku zote mambo hayawezi kuwa kwa jinsi tunavyotaka sisi. Kwahiyo unapaswa kuwa na subira. Wengi wamejikuta wameangukia kwenye maumivu makali ya moyo baada ya kukosa subira.

Wakati mwengine subira kidogo tu inaweza ikatuokoa na majanga makubwa sana. Siku hizi imekuwa sio jambo la ajabu kuona amekutana na mwanamke leo na leo wakaenda kufanya ngono na kesho yake wanatangaza ndoa. Sasa sijui itakuwa ndo ya aina gani kama sio kituko?

Nawasilisha.

Picha/Video: Diamond Akusanya Kijiji Mombasa

$
0
0
Mkali wa muziki kutoka Tanzania, Diamond Platnumz ameendelea kuonyesha umwamba wake nchini Kenya katika show iliyofanyika Mombasa Jumamosi hii na kuhudhuriwa na maelfu ya watu.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri Afrika pamoja na kimataifa, ameendelea kudhihirisha ukubwa wake baada ya show yake kuhudhuriwa maelfu wa mashabiki.

Kupitia instagram yake, Diamond aliandika “It’s 4:35 am now in East africa… am now going to sleep then right after waking up, will start posting my all Mombasa show Pictures…. thanks,”

Angalia video:

Wema Sepetu atumia show ya vigoma Tanga kuzindua bidhaa yake mpya ya viatu vya kike

$
0
0
Malkia wa filamu Wema Sepetu ametumia show yake ya vigoma iliyofanyika Jumamosi hii katika Viwanja vya Mkwakwani mkoani Tanga kuzindua bidhaa yake mpya ya viatu vya kike.


Mwigizaji huyo ambaye mwishoni mwa mwaka jana alizindua bidhaa yake ya kwanza ya lipstick, amesema bidhaa hiyo itaanza kupatika madukani hivi karibuni.

“Wakati naanza kutumia jina langu kwa ajili ya kuendeleza brand yangu ya Wema Sepetu, nilianza na lipstick na sasa nimekuja na viatu vya kike,” alisema Wema mbele ya umati wa watu waliojitokeza katika usiku wa vigoma. “Hivi viatu ni vya kitamaduni kabisa kwa sababu wanasema uzalendo kwanza,”

Aliongeza, “Kwa hiyo nilisema nifanye kitu gani ambacho kitawakilisha na uzinduzi wa hivi viatu, nikasema niandae show ya usiku wa kitu fulani, kwa hiyo nilivyokuwa nataka kuzindua hivi vitu nikasema nitumie akili, nifanye usiku wa Kiswahili, kwa sababu hata hivi viatu vinaenda Kiswahili, nikafikiria usiku wa vigoma, tumeanza Dar es salaam na kutaamua tuje Tanga na baadae mikoa mingine,”.

Mwigizaji huyo amesema anaamini akizunguka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ataweza kupata support kubwa kwenye bidhaa zake pamoja na kazi zake za filamu.

Kutana na Mtangazaji Mchafu Zaidi Duniani

$
0
0
Raphael Tenthani inasemekana kuwa ndiye mtangazaji mchafu zaidi kutokea duniani

Raphael mara zote utakazo kutana nae huwezi ukamkuta nadhifu , mara kwa mara utamkuta amevaa nguo zilizo chakaa na muda mwingine nguo zenye matobo au viraka

Raphael ingawa ni mwandishi wa habari katika shirika la habari la BBC nchini malawi lakini kwenye suala la usafi yeye limemkalia kushoto sana ,wakati mwingine unaweza ukakutana nae nywele hajachana, viatu vimeachama , mdomo unanuka na mara kwa mara anakuwa katika hali ya ulevi

Raphael amekuwa gumzo sana katika mitandao ya kijamii huku wengi wakimuhisi huenda anafanya hivyo ili asivunje masharti ya mganga

Ni kawaida kumuona Raphael akirusha habari akiwa mchafu bila kujali mahali husika alipo kuwepo.

Msanii wa Bongofleva Rayvanny Avurugwa na Shepu ya Snura Kitandani Wakati wa Ku-Shoot Video

$
0
0
Baada ya kutoka video ya “Natafuta Kiki” pamekuwa na zengwe, kwa kile kilichoonekana kuwa ni mahaba juu ya Snura na Rayvanny kwa lile denda zito lililopigwa kitandani.

Akipiga stori na eNewz Rayvanny amesema “Ni kweli ile scene ya kitandani ilinipa wakati mgumu sana, hasa ukizingatia ile shepu ya Snura, kuna wakati nilisahau kama tuko location”.

Lakini kwa upande wa Snura anasema yeye aliifanya ile scene kama kazi tu, kama ambavyo script ilimtaka afanye ndicho alichokifanya, na wala hakumtamani Ray.

Snura kwa ujasiri akaongeza kwa kusema “Kama script inataka nimkiss hata mwanangu ninaweza kufanya hivyo”.

Lakini pia kwa upande mwingine Ray alipoulizwa juu ya sababu za kutumia video aliyojishut na Wema katika birthday ya Romy Jones, alisema “Sina tatizo kabisa na Wema na tokea zamani nilitamani sana Wema aonekane kwenye hii video yangu, lakini ilishindikana kumpata sababu ya u-bize wake hivyo nikaona bora nitumie tu ile video tukiwa kwenye birthday ya Romy Jones”.

Walichofanyiana Shilole na Nuh Mziwanda walipokutana kwenye basi la Fiesta

$
0
0
Shilole na Nuh Mziwanda walikutana kwenye basi walipokuwa wanaenda Fiesta, wasanii hawa wamekuwa na bifu na walichuniana walipokutanishwa kwenye kipindi cha tv clouds na wamekuwa wakipigana majungu mitandaoni.

Lakini walipokutana kwenye basi Shilole alimuambia Nuh Mziwanda yaishe na kumwambia yupo kwa ajili yake na kumwagia mabusu mazito, pengine watarudiana. Angalia:

Selection Za Vyuo Vikuu Kwa Walioomba Kujiunga na Vyuo Mbalimbali Mwaka Huu Zimetoka

$
0
0
Selection za TCU kwa walioomba kujiunga na vyuo mbalimbali kwa mwaka wa masomo 2016/2017  zimetoka.

==> Bofya hapa  kuangalia   <<Selection Status >> 

NB:  Tumia index number yako na password

Kaka Yangu Julius Mtatiro, Usifuate Njia ya Waliopotea

$
0
0

Linaandika Gazeti la Mwananchi; ''BUNDI WA TIMUA TIMUA ATUA CUF NYAMAGANA'' katika habari kuna taarifa kuwa Viongozi waandamizi watano (5) wa CUF wilayani Nyamagana wamefukuzwa. Viongozi hao akiwemo Mwenyekiti wa Wilaya hiyo Ndg Salum Mkumbukwa, aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo Ndg Faida Potea, Mkurugenzi wa Mipango na Chaguzi Mohamed Makongoro, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Hamza Shido, Omary Abubakar Mkurugenzi wa Utawala na Nazar Nyampangula Mkurugenzi wa Siasa, taarifa hiyo ikaendelea kudai kuwa Viongozi wengine 2 wamewekwa chini ya uangalizi maalum ambao ni wakurugenzi wa Idara ya Fedha na Ulinzi.

Sababu kubwa iliyotolewa ni kuwa Viongozi hao hawakuwasilisha taarifa za mpango kazi wa ofisi yao. Ukiitazama sababu hii "KUTOWASILISHA TAARIFA ZA MPANGO KAZI WA OFISI" na kuilinganisha na adhabu ya kufukuzwa, utajiuliza maswali ambayo yanaweza kusababisha mtikisiko mkubwa wa ubongo, ni jambo haliingii akilini.

Haiitaji kuwa msomi wa chuo kikuu kujua kuwa sababu sio hiyo, ila kwa kuwa sababu yenyewe haiwezi kuwekwa hadharani, inatafutwa sababu nyingine "cover up" ya kujustify maamuzi ya kufukuzana.

Hili ni moja ya tatizo kubwa ndani ya vyama vya siasa vya upinzani, tatizo hili limeshakuwa donda ndugu ambalo limeshakuwa la kudumu kwa upinzani. Vyama hivi ambavyo vinadai na kupiga kelele ya udikteta na kuminywa kwa demokrasia nchini, ni kama vile vinatazama kibanzi kwa jicho la jirani ikiwa kwao kuna Boriti.

Kwa tafsiri ya shule na iliyo kikatiba, Chama cha Siasa** ni muungano wa watu (wanachama) wenye itikadi fulani waliopania kuishika na kuendesha serikali. Chama ni wanachama, sera na itikadi. kwa tafsiri hii vyama vingi vya upinzani Tanzania havina qualification ya kuwa vyama vya siasa, maana vyama hivyo vina wamiliki (ambao sio wanachama) ambao wakiamua iwe hivi inakuwa hivyo na wakiamua kufukuza yeyote kwa maslahi yao wanafanya hivyo. Vyama havina sera wala itikadi inayoeleweka.

Ni vigumu leo kutofautisha umiliki wa Mbowe kwa Tanzania Daima ama Protea hotel na Umiliki wake wa CHADEMA, namna anavyooperate, anavyotoa amri na kusimamia execution ya mikakati yake ni kama vile CHADEMA ni mali yake kamili ambayo anao mpango wa kuirithisha kwa wanawe.

Spika wa Bunge Tukufu la Jamhuri alijaribu kuwasihi na kuwashauri wapinzani juu ya tabia hii ya hovyo ya kufukuzana kila asubuhi. Lakini ni kama wana masikio na hawasikii na wana macho na hawaoni.

Kinachosikitisha ni pale ambapo hata Viongozi vijana ambao tulidhani wakati fulani kuwa tunaweza kushirikiana nao kuijenga TANZANIA NJEMA, nao wamekuwa wafuasi wakubwa wa hulka na mwendo huu wa upotevu. Mtatiro, kaka yangu utafukuza wangapi..? Maana watu si mawe kuwa utayageuza unavyotaka, kila asubuhi atatokea kwa kuhoji na kuuliza kwanini unigeuze, utafukuza wote..??? ili ubaki na nani..?

Imezaliwa ACT ikiwa ni alama ya kudumu ya udikteta wa MBOWE, Mtatiro unataka kuzalisha ACT nyingine..? Wakati mwingine tujifunze kupevuka kiakili, haya mambo yana mwisho. Waswahili wanasema hata mwisho una mwisho wake.....hautabaki MWENYEKITI wa MPITO milele...itendee haki nafasi yako, vijana wenzako tujivunie kuwa umeipitisha CUF katika wakati mgumu na ukaiacha salama. KUFUKUZANA hakutokuacha wewe salama wala CUF haitabaki salama.

Wolper Na Harmonize Wala Bata Serengeti

$
0
0
WASANII wawili ambao ni wapenzi wanaogonga vichwa vya habari Bongo, Jaqueline Wolper na Rajab ‘Harmonize’ wikiendi iliyopita wamekula bata kwenye mbuga ya wanyama ya Serengeti.

Wawili hao waliondoka Dar es salaam Jumamosi wiki iliyopita na kuelekea Arusha kwa ajili ya mapumziko ya wikiendi na baadae kuungana na Rich Mavoko pamoja na Raymond Jumatatu ya sikukuu ya Eid (jana)  kwa ajili ya show Mkoani Tanga.


Wolper kupitia instagram aliandika: Asante Raj wangu kwa kunipeleka vacation… nime enjoy saana Harmonize.

Kwa upande wa Abby ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Tour ambayo iliwapeleka ameandika:

The experience we had together was extremely amazing! I Was so impressed with the way you guys handle each other. This left me with memories of the entire trip to Serengeti .Thank you so much for trusting  Napanda Safaris to plan for your vacation .Can’t wait for our next plans as we discussed and the preparations has started now!

Utendaji Makini wa Mh Rais Magufuli Wapaisha Sekta ya Utalii

$
0
0

Utendaji wa JPM waipaisha sekta ya utalii Uchambuzi wa kina wa hali ya mambo katika sekta moja muhimu ya utalii, eneo linaloiingizia Serikali takribani asilimia 25 ya fedha za kigeni, unaonesha, pamoja na kelele za hivi karibuni, watalii wengi wameongezeka nchini hasa katika kipindi cha Julai mpaka Agosti mwaka huu ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.

Uchunguzi zaidi umeonesha kuwa watalii wengi waliokuja nchini au wanaofikiria kuja nchini hawajaguswa na ongezeko hilo la kodi zaidi ya kujali aina ya vivutio vilivyoko nchini, hali ya amani na wapo wanaovutiwa pia na utawala wa Rais John Pombe Magufuli ambaye anasikika duniani kote hivyo wanakuja kuona hali ya siasa nchini.

Katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, takwimu za watalii waliotembelea hifadhi hiyo, kwa kipindi cha Juni hadi Agosti, 2015 na Juni hadi Agosti, 2016 nako zinaonesha ongezeko.

“Kwa kulinganisha idadi ya watalii waliotembelea Hifadhi ya Ngorongoro kwa miezi mitatu (Juni-Agosti 2015) na mwaka Juni hadi Agosti,2016, inaonekana kuwa idadi ya wageni imeendelea kuongezeka hivyo mapato pia yameongeza.

“Kwa mantiki hiyo hadi sasa utekelezaji wa kodi mpya haujaathiri mapato na haijawa kikwazo bado kwa watalii kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro,” inasema taarifa ya hali ya utalii nchini ambayo gazeti hili limeiona sehemu yake.

Tayari watalii wenyewe na wataalamu wa sekta hiyo waliokuja nchini kwa wingi licha ya kodi kuongezeka, ripoti hiyo ya kina inaainisha, wengi hawakuonekana kubabainishwa na kodi hiyo:

“Watalii waliohojiwa kwenye malango na mahoteli walionyesha kutoelewa kuwa VAT imeanza kutozwa na baadhi walishangaa kwamba Serikali haikuwa inatoza kodi fedha zilizokuwa zinalipwa na watalii waingiapo Hifadhini,” inasema ripoti hiyo.

Akiandika katika makala yake iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza Why VAT will not kill hotels, tourism na kuchapishwa na gazeti moja la kila siku nchini, mmoja wa walimu wanaofanyakazi nchini Australia na mtalii wa mara kwa mara kuja Tanzania na sehemu nyinginezo Afrika, Sabine Barbara anasema:

“Hali ya kisiasa ya nchi inaweza kuwa na athari zaidi kwa watalii kuliko kuongezeka kwa ada za kuingia katika mbuga za wanyama….juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano zitapimwa unapofika mwisho wa mwaka kuliko kuanza kuwatisha watu hivi sasa kuwa kodi zitapunguza watalii.”

Takwimu hizi zinakuja wakati ambapo wiki iliyopita akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA, kinachorushwa na TBC1, Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akidokeza na kuthibitisha kuwa kodi mpya ya VAT haikuwa imeathiri idadi ya watalii wala mapato ya nchi.

Akizungumzia jana na gazeti hili kuhusu kuongezeka kwa watalii licha ya wasiwasi wa awali wa kodi hiyo ya VAT, Meneja Mawasiliano wa TANAPA, Bw. Paschal Shelutete, alisema ni kweli kuna ongezeko hilo na wao walilitarajia.

“Ni kweli kwamba watalii wameongezeka kuja kutembelea hifadhi zetu na vivutio vingine vya nchi. Hakuna mtalii anayeweza kushindwa kuja nchini kwa sababu ya kutakiwa kulipa kodi. Bahati nzuri wenzetu wanautamaduni wa kuheshimu sana kodi na ndio maana hawajastushwa na kodi hiyo,” alisema.

Takwimu hizi, hasa katika kuelekea mwaka mmoja wa uongozi wake, zinampa Rais Magufuli nguvu ya kuendeleza zaidi utawala wake unaojikita katika kuhakikisha kodi za Serikali zinalipwa ili kuiongezea Serikali mapato kwa lengo la kufikia azma ya kujitegemea.

Itakumbukwa kuwa Julai mwaka huu Serikali ilianza kutekeleza kodi mpya ya ongezeko la thamani (VAT) katika sekta ya utalii, hatua iliyopingwa na wadau wa sekta hiyo kuwa ingeathiri idadi ya watalii wanaokuja nchini.

Miezi miwili baadaye, takwimu zinathibitisha kuwa ongezeko hilo la kodi ambalo Rais Magufuli mwenyewe amepata kulitetea, tofauti na mawazo ya wengi, halijaathiri, na badala yake sababu nyingine kama vivutio vilivyopo nchini na hali ya amani na utulivu vimeendelea kuifanya Tanzania iwe na mvuto zaidi kwa watalii.

Takwimu ambazo kutoka kutoka vyanzo mbalimbali Serikalini, sekta binafsi na kwa wadau wa utalii wenyewe, zinathibitisha kuwa wakati kwa mwaka mzima wa 2015 idadi ya watalii waliongia nchini ilikuwa 1,1376,182 idadi hiyo imeongezeka mwaka huu.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa kwa kuangalia ulinganifu wa takwimu za mwaka jana kipindi kama hiki na mwaka huu, takwimu za Hifadhi za Taifa (TANAPA), zinaonesha idadi ya watalii wote katika kipindi cha Juni-Julai 2016 imeongezeka kwa sana.

Ongezeko hilo pia limeongeza mapato yatokananyo na viingilio hifadhini ambapo yameongezeka kwa wastani wa asilimia 19.7 huku mapato yatokanayo na vyanzo vingine yakiongezeka kwa wastani wa asilimia 13.

Julai mwaka huu, Serikali ilianzisha kodi ya VAT ambayo itakuwa ikikatwa kwenye huduma za uongozaji watalii, kuvinjari (safari) na ada za viingilio (park fees) hifadhini. Huduma za malazi zilishakuwa zikitozwa kodi hiyo tangu awali.

“Baada ya miaka ya 10 sekta ya utalii kufaidika na msamaha huo, Serikali iliona sekta imeimarika na ni vema sasa ichangie zaidi katika mapato ya nchi moja kwa moja kwa kuondoa msamaha huo,” anasema mtaalamu mmoja wa masuala ya kodi katika sekta binafsi na kuongeza:

“Hivyo, msamaha huo ulifutwa kupitia Finance Act ya mwaka 2016 (Juni). Takwimu am,bazo hata sisi tunazo zinaonesha katika kipindi hiki cha Julai na Agosti, 2016 ambapo huduma za utalii zimeanza kutozwa VAT hapakuwa na athari ya mapato kwa Serikali.”

Na Mwandishi Wetu, Gazeti la Majira, Sept., 13, 2016

WAKATI Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ikielekea kutimiza mwaka mmoja Novemba mwaka huu, mageuzi makubwa anayoyafanya, staili yake binafsi ya uongozi na mafanikio katika kulinda misingi ya amani vimeendelea kuwavutia wageni wengi duniani.

Katika kuelekea mwaka mmoja wa Serikali ya Magufuli, wachambuzi wanaweza kutazama utawala wake kwa namna tofauti kwa kuangalia na kuzingatia nyanja za uchumi, siasa, jamii na teknolojia.
Uchunguzi wa unaonesha kuwa sera na staili ya uongozi wa Rais Magufuli hasa katika nyanja za uchumi zimeanza si tu kuwavutia wageni kutoka nje lakini pia kuipatia nchi mapato yaliyokuwa yakipotea awali.

TAZAMA Video Mpya: Sauti Sol - Kuliko Jana!

$
0
0
Kundi la muziki la Sauti Sol kutoka nchini Kenya limezidi kufanya vizuri katika tasnia ya muziki barani Afrika na nje ya Afrika. Hapa chini ni video ya wimbo wa ‘Kuliko Jana’ iliyotoka Septemba 12, 2016.

Mbunge wa Tarime John Heche Ashawishi Bunge Kuridhia Posho za Kikao cha leo Zipelekwe Kwa Wahanga wa Tetemeko

$
0
0
Mbunge wa Tarime John Heche (UKAWA-Chadema) amefanikiwa kulishawishi bunge kuridhia posho za leo tarehe 13 za wabunge zipelekwe kagera kwa wahanga wa Tetemeko.
Katika hoja yake mbunge huyo machachari amewataka wabunge waondoe tofauti zao na kukubali posho zote za wabunge leo zikasaidie wahanga hao wa tetemeko.
Wabunge wote kwa pamoja bila kujali tofauti zao wameridhia hoja hiyo kwa asilimia mia moja

Siwezi Kuyarudia Matapishi Niliyoyatapika - Mr Blue

$
0
0
Msanii wa Bongo Fleva Mr. Blue ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake wa 'Mboga Saba' amefunguka na kusema kuwa saizi yeye ni mtu mzima anaangalia maisha yake na familia yake hivyo hawezi kurudia matapishi ambayo tayari alishakwisha yatapika.

Mr Blue alisema haya kupitia kipindi cha eNewz ya EATV alipokuwa akifafanua juu ya taarifa zilizokuwa zimezagaa mtaani kuwa alimpigia simu aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Naj ndipo hapo aliposema hawezi kurudia matapishi aliyokwisha yatapika.

"Niliongea na Baraka The Prince alisema kuwa wao hawakufanya hilo jambo, lakini kama wangekuwa ni wao lazima ningetafuta njia ya kuwashikisha adabu maana huko ni kuharibiana. Mimi saizi nimeshakuwa mtu mzima siwezi kurudia matapishi ambayo nilishakwisha yatapika mwanzo' alisema Mr Blue.

Hakuna mtu atakayenipangia muziki wa kufanya – Nay wa Mitego

$
0
0
Huenda sumu ya adhabu ya BASATA kwa Nay wa Mitego ikawa haikukolea vyema.

Ni sababu rapper huyo ameibuka na kudai kuwa, hakuna mtu anayeweza kumpangia aina ya muziki wa kufanya, na kwamba hivi karibuni ataachia wimbo uitwao ‘Utakula Jeuri Yako’ ambao ni makavu kwa kwenda mbele na huenda ukazua ‘sheshe’ jingine.

“Nobody can stop me,” alisema Nay katika mahojiano kipindi cha Extra Fleva, cha Uplands FM ya Njombe kinachoendeshwa na Ergon Elly. “Muziki wangu uko pale pale, kitu ninachowaahidi mashabiki wangu, soon, siku nikiamka tu kuna wimbo unaitwa ‘Utakula Jeuri Yako’ patawaka.”

Nay alisisitiza kuwa hata katiba hairuhusu mtu kumzuia mtu mwingine kitu cha kuongea.

Hivi karibuni Nay alifungiwa kwa ufupi kujihusisha na muziki na kupigwa faini ya shilingi milioni 1 kutokana na maudhui ya wimbo wake Pale Kati uliofungiwa.

Alisema kuwa adhabu hiyo ilikuwa na madhara kiasi kwa muziki na biashara yake.

Haya Hapa Majina ya Makampuni na Wafanyabiashara Waliochangia Maafa ya Tetemeko la Ardhi Kagera Pamoja na Kiasi Walichotoa

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongea na Mabalozi na Wawakilishi wa wafanyabishara Ikulu jijini Dar es Salaam kutoa taarifa ya tatemeko la ardhi na maafa yaliyotokana tarehe 10 September 2016.

Waziri Majaliwa amewaomba wawakilishi hao kutoa misaada mbalimbali ili kuungana na Serikali kuwasaidia walioathirika mkoani Kagera.

Baadhi ya Taasisi na Balozi zilizo ahidi kutoa michango ni:-

= TBL Wamechangia Milioni 100

= Azania Group Wanatanguliza Milioni 20

= Wafanyabiashara wa Mafuta wa rejareja watakusanya Milioni 250 na watakabidhi ijumaa ya week hii

= Kagera Sugar wanatoa Milioni 100 na tani 10 za sukari.

= Serengeti wanatoa saruji mifuko 800

= Pepsi Cola 50 Millioni

= Hatiamaye Regnald Mengi anatoa mchango wake wa Milioni 110.

= Protas Ishengoma anatoa msaada wa Milioni 5.

= GBP, MOIL na OILCOM wameahidi kujenga shule mbili (Ihungo na Nyakato) zilizoharibiwa vibaya.

= Puma wanachangia 50 Milioni

= Agusta Tanzania wanatoa Milioni 10

= Camel Oil wanachangia mifuko 1,000 ya Cement

= Tippa waachangia milioni 20

= Orexy wanachangia Milioni 50

= Waislamu wa madhehebu ya Al-Shafy, Ijumaa na Adhuhuri wanachangia Milioni 1.

= Sahara Tanzania wanachangia Milioni 20

Wizara ya Mambo ya Nje watafanya matembezi ili kuhamashisha uchangishaji wa fedha na wataanzia Polisi Oysterbay.

MAJUMUISHO:

Waziri Charles Mwijage nafanya majumuisho ya fedha zilizopatikana ni kama ifuatavyo:

1. Fedha taslimu ni Milioni 646,

2. Ahadi ni Milioni 705,

3. Dola za Kimarekani 10,000

4. Yuro 10,000.

5. Mfuko ya Sementi zaidi ya 2800,

6. Ahadi ya ujenzi wa Shule mbili ndani ya siku 30.

JUMLA KUU, Bilioni 1 na Na Zaidi ya Milioni 300
======

Ahsanteni kwa kuwa nami........
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images