Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104771 articles
Browse latest View live

Job Opportunities at CVPeople, Apply Before 31 Oct 2016

$
0
0
EARLY CHILDHOOD DEVELOPMENT ADVISOR POSITION

Effectively plan and deliver the ECD project activities and coordinate effective implementation
Provide technical expertise using the most up-to-date evidence base in ECD, care for child development (CCD), and low-cost material development to ECD technical leads in Zonal offices
Develop and deliver capacity development workshops on ECD to Zonal teams.
Responsible for financial oversight, management of ECD strategy, and ensuring compliance with donor and NGO's regulations and procedures
Work within and coordinate ECD interventions across a number of partners working within a consortium




APPLICATION INSTRUCTIONS:

Online application ONLY. You must be registered with CvPeople Africa to apply for this position.
Click HERE to Apply

=================


SALES EXECUTIVE-AUTOMOTIVE POSITION 


Maintains relationship with Clients by providing support,information,and guidance,researching and recommending new opportunities,recommending profit and service improvements
Assist manager in marketing campaigns and also in scheduled physical inventory counts.
Prepare reports by collecting, analyze and summarizing information.
Negotiating the terms of an agreement and closing sales.
Coordinate the ordering, receiving and delivery of products in a timely manner.
Recording sales and order information and sending copies to the sales office, or entering figures into a computer system.
Identifies business opportunities by identifying prospects and evaluating their position in the industry researching and analyzing sales options.
Update and prepare daily reports.





APPLICATION INSTRUCTIONS:

Online application ONLY. You must be registered with CvPeople Africa to apply for this position.
Click HERE to Apply

Wabunge wote wa CUF Wamkataa Profesa Ibrahim Lipumba

$
0
0

Wabunge wote wa Chama cha Wananchi (CUF) wametangaza rasmi kutomtambua aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

Wamemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kutomkumbatia mwanasiasa huyo aliyebobea katika uchumi, ikielezwa kwa sasa hana sifa za kuwa mwenyekiti wa chama hicho, labda aanze upya mchakato.

Wameeleza msimamo huo jana mjini Dodoma na Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Mngwali ambaye pia ni Kiongozi wa Wabunge wa CUF katika mkutano baina ya waandishi wa habari za Bunge na wabunge wa CUF isipokuwa Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya aliyesimamishwa uanachama, ingawa anaendelea kutimiza majukumu yake bungeni.

Mngwali alisema Profesa Lipumba amekuwa akijaribu kukiyumbisha chama na hivi karibuni kudai amekaririwa akisema anasubiri barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya kuthibitishiwa kuendelea na uenyekiti wake.

“Wakati anajiuzulu uenyekiti Agosti 5, mwaka jana aliutangazia umma na kudai anakwenda Rwanda kwa kazi aliyodai ya utafiti ili aje kuisaidia serikali, lakini inashangaza sasa anataka kujirejeshea uenyekiti. Hilo hatukubali kwa kuwa chama kina taratibu zake,” alisema.

Aliongeza kuwa, alikiacha chama katika wakati mgumu kuelekea Uchaguzi Mkuu, lakini kikaimarika zaidi kwa kupata wabunge 43, madiwani 287, kuongoza manispaa mbili na halmashauri za wilaya tatu, hivyo wanashangazwa kuona akitaka kurejea, tena kwa kutumia nguvu.

“Tunataka ifahamike kwa dhati kuwa, sisi wabunge, hatumtambui tena Profesa Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF,” alisema Mngwali na kumtaka Msajili kutomuidhinisha Lipumba, kitendo alichodai kitachochea mgogoro ndani ya chama.

Aliongeza kuwa badala ya kutumia mabavu kutaka kurejea madarakani, ni vyema akabaki na heshima yake, kwani amekitendea mambo mengi chama hicho na kwamba wanamheshimu, hivyo afuate taratibu za kichama kutaka kuwania tena uenyekiti.

Mngwali alisema wamekubaliana na uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF wa kuwasimamisha uanachama Lipumba na wenzake tangu Agosti 28, 2016 kutokana na kile kinachodaiwa kukiuka Katiba ya chama hicho. 

Miongoni mwa tuhuma zao ni kusababisha vurugu wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Uchaguzi Agosti 21, mwaka huu jijini Dar es Salaam uliokuwa unalenga kumthibitisha Juma Duni Haji kuwa Mwenyekiti mpya.

Hata hivyo, kutokana na vurugu zilizoibuka, mkutano huo ulivunjika. Mbali ya Lipumba na Sakaya, wengine waliositishiwa uanachama ni Abdul Kambaya ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Ashura Mustapha, Omar Mhina, Thomas Malima, Kapasha M. Kapasha, Mohamed Habib Mnyaa, Haroub Shamis na Mussa Haji Kombo.

Ashura ni mjumbe wa Baraza Kuu na aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma CUF wakati Mnyaa na Kombo, walikuwa wabunge kipindi cha 2010/2015, Mnyaa akiwakilisha Jimbo la Mkanyageni na Kombo Jimbo la Chake Chake, kisiwani Pemba.

Kutokana na kusimamishwa kwa viongozi hao, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alimtangaza Julius Mtatiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara kuwa kiongozi wa Kamati ya Uongozi wa muda inayowajumuisha pia wabunge Katani Ahmed Katani na Savelina Mwijage ambao ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

KUTOKA BUNGENI: Rais Magufuli Kuhamia Dodoma Rasmi Mwaka 2020

$
0
0

Leo Septemba 16, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha mkutano wa nne kwa Bunge la 11 uliodumu kwa muda wa wiki mbili, amesoma ratiba ya serikali kuhamia Dodoma.

“Ili kufanikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma, tayari imeandaliwa ratiba itakayowezesha Serikali kuhamia Dodoma kwa awamu, kuanzia mwezi Septemba, 2016 hadi mwaka 2020, bila ya kuathiri bajeti yetu ya mwaka 2016/2017 kama ifuatavyo”–


1. Septemba 2016 – Februari 2017.

Waziri Mkuu na Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wote, Manaibu Makatibu Wakuu wote watahamia Dodoma katika Awamu ya Kwanza. Aidha, kila Wizara itatakiwa kuhamisha Watumishi wa Idara moja au mbili, na wakati huo huo kuendelea kuweka utaratibu wa kupeleka Watumishi wa Idara nyingine kuhamia Dodoma;

2. Machi 2017 – Agosti 2017.

Kipindi hiki kitawapa fursa watendaji wa wizara mbalimbali kuweka katika Bajeti zao za mwaka 2017/2018 gharama za kuendelea kuhamisha watumishi wake kuja Dodoma.

3. Septemba 2017 – Februari 2018.

Katika awamu hii, Wizara zitaendelea na uhamishaji wa Watumishi wa Idara zilizo ndani ya Wizara.

4. Machi 2018 – Agosti 2018.

Katika kipindi hiki, Wizara zinatakiwa kuendelea kuhamisha watumishi wake.

5. Septemba 2018 – Februari 2020.

Katika kipindi hiki, Wizara zinatakiwa kuendelea kuhamisha watumishi wake.

6. Machi 2020 – Juni 2020.

Katika kipindi hiki, Ofisi ya Rais ikiongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watakuwa wanahamia Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitumia wasaa huu kuzishauri Wizara zote kuanzisha mifumo ya utunzaji kumbukumbu wa kielektroniki badala ya kuhama na mafaili kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma, tunataka Dodoma iwe ya kielektroniki, alisisitiza Waziri Mkuu.

ZITTO Kabwe Afunguka Kuhusu Utafiti wa Twaweza Kuhusu Imani Waliyonayo Wananchi Kwa Rais Magufuli

$
0
0
Kura za Maoni zilizotolewa na TWAWEZA zinaibua maneno ambayo unashangaa kuyasikia kwa wasomi, wengine maprofesa. Kwangu mimi naona masuala 2 muhimu


  • Matokeo yanaonyesha IMANI kubwa ambayo wananchi wanayo kwa Rais Magufuli. Hata hivyo IMANI hiyo inakuja na wajibu mkubwa sana na Rais asitumie vibaya imani hiyo. Kiongozi mwenye busara hawezi kutumia imani hii kwa kukandamiza demokrasia na kukanyaga Katiba. 
  • Matokeo pia yanaonyesha kuwa Wabunge na Madiwani kwa kiasi kikubwa wana IMANI ya wananchi wao wanaowawakilisha. Huu ni wajibu na fursa kwa Wabunge wa Upinzani kuonyesha uongozi mahiri wenye kutoa majawabu ya changamoto za wananchi kwenye maeneo yanayoongozwa na Vyama vya Upinzani.


Tujifunze kukubali tusiyopenda kuyasikia. Wakati tunapambana vita adhimu sana dhidi ya Udikteta Mamboleo unaonyemelea nchi yetu, pia kwa nguvu hizo hizo tuonyeshe tofauti ya kiuongozi katika Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji tunayoongoza

By Zitto Kabwe

MAJAMBAZI, Mali za Wizi na Silaha Vyakamatwa Dar

$
0
0

Kikosi maalum cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha cha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 5 wa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali.

Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Saimoni Sirro akionesha baadhi ya vifaa vilivyokamatwa.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Kamishna Saimoni Sirro wakati akitoa taarifa ya kukamatwa majambazi wa 5 na kukutwa na silaha aina ya shotgun, bastola 3 na risasi 49.

Katika tukio lingine Polisi mnamo tarehe 5.9.2016 majira ya saa 8 usiku maeneo ya Magomeni mtaa wa Makumbusho waliokota begi lililokuwa na bastola mbili, sambamba na hilo wamefanikiwa kukamata magari 4 ya wizi, hati za magari na watuhumiwa wawili wa uhalifu huo wamekamatwa.
Jeshi hilo limetoa wito kwa viongozi wa serikali za mitaa kupitia kamati za ulinzi wa mitaa kuimarisha ulinzi na kuwataka wamiliki wa nyumba za kupanga kuhakikisha wanaweka kipengele cha kuwepo na picha katika mikataba ya kupangisha nyumba zao kutokana na uwepo wa wimbi la uhalifu.

Wakati huo huo Kamanda Sirro amesema Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kipindi cha siku 11 wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 882,570,000 ikiwa ni tozo za makosa ya usalama barabarani na makosa mengineyo.

Mimi Sishindani na Mtu yeyote - Baraka The Prince

$
0
0
Msanii Baraka The Prince ambaye ameachia kazi yake mpya yenye jina la 'Nisamehe' amefunguka na kusema kuwa katika muziki hakuna mtu ambaye anashindana naye kwa kuwa yeye anasimama mwenyewe na aina ya muziki anaofanya haufanani kabisa wasanii wa WCB

Baraka The Prince alisema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo na kudai kuwa muziki anayofanya yeye ni wasanii wachache ambao wanafanya na kusema mara nyingi yeye anafanya jambo kutokana na mipango yake na matakwa ya mashabiki ila hafanyi kazi kwa kuangalia nani kafanya nini na nani.
"Siku zote mimi nasimama kama Baraka The Prince sijawahi kufanya kitu sababu fulani kafanya ila siku zote mimi huwa nafanya kazi kwa kuangalia mashabiki zangu wanataka nini na kuangalia mipango yangu. Kwanza sijawahi kufikiria kushindana na mtu yoyote yule kwenye muziki kwa sababu mimi najua nina muziki wa tofauti kabisa na miziki yao wanaofanya wao, watu wengi watafanya muziki wa mchaka mchaka watafanya nini lakini ukija upande wangu mimi watu tunaofanya muziki huu tunahesabika lakini kwenye miziki yao kuna watu karibia mia na kitu mpaka wengine hawajatoka wanafanya miziki yao" alisema Baraka The Prince

Mbali na hilo Baraka The Prince alisema kuwa yeye alikuwa na mipango ya kufanya kazi na Alikiba miaka mitano nyuma na anasema alijua kuwa wimbo wake wa sita lazima aimbe na Alikiba na imekuwa hivyo.

"Mimi nilikuwa na mipango ya kuja kufanya kazi na Alikiba miaka mitano nyuma na nilipanga kabisa wimbo wangu wa sita lazima niimbe na Alikina na imekuwa, mimi ni mtu ambaye huwa naishi kwa mipango saizi wimbo wangu wa kumi nishajua nitafanya na nani kama Mungu atazidi kutupa uhai, lakini pia ukiangalia muziki ninaofanya mimi na Alikiba ni sawa japo kuwa Alikiba yeye ni mtu wa kubadilika lakini nikisikiliza wimbo wowote wa Alikiba najifunza kitu hivyo yeye ni miongoni mwa wasanii walionivutia kwenye muziki huo wa Bongo Fleva" aliongeza Baraka The Prince

Meneja Wa Diamond Platinums Afunguka Kuhusu Ali Kiba Kufanya Show Kwa Kushtukiza Jukwaa Moja Na Diamond Platinums Kenya

$
0
0
Meneja wa Diamond azungumzia Ali Kiba kufanya show kwa kushtukiza kwenye jukwaa moja na Diamond Kenya..

International Meneja wa Diamond Platnumz ‘Sallam Sk’ ameongea na Sammisago Kupitia ENews leo kuhusu Ali Kiba kufanya show kama msanii wa kushtukiza kwenye jukwa moja na Diamond Platnumz.

Sallam anasema “Sisi hatukuambiwa kama Ali Kiba atakuwepo kwenye show kwa hio Ali Kiba alikuwa kwenye show kama Suprise, nashukuru muziki wetu wa Tanzania unazidi kukua,

tulichofanya ni kitu mkataba wetu umesema tufanye , na tuliperform kwa saa mbili, hawakuandika Diamond is a Tanzanian artist, ila waliandika International Artist, kama alitangazwa Diamond pekee yake, akaje msanii mwingine pia hio ni sawa tu”

Hii ni hatua nyingine inayothihirisha kuwa ladba hakuna beef kati yao na kwamba wote wanakubalika kama wasanii wa kimataifa….

Simba, Azam Hapatoshi.. Warushiana Tambo Mechi ya Leo Ligi Kuu Bara

$
0
0
Michuano ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inatarajia kuendelea tena leo ambapo Simba na Azam FC zinazotarajia kukutana kwenye Uwanja wa Uhuru zimeelezea kuhusu mchezo huo.

Afisa Habari wa Simba SC Haji Manara amesema, kikosi kimejiandaa vizuri kwa ajili ya kuweza kupambana na wanauchukulia huo kama michezo mingine hivyo wanaamini wataweza kuvuna pointi tatu mbele ya Azam FC.

Manara amesema, mpaka sasa wana majeruhi wawili pekee ambao ni mshambuliaji Ibrahim Ajibu na kiungo Mwinyi Kazimoto ambao daktari anaendelea kuangalia hali zao kama wataweza kucheza mchezo wa kesho au bado wataendelea kuwa katika uangalizi.

Kwa upande wake Afisa Habari wa Azam FC Jafary Iddy Maganga amesema, mchezo huo utakuwa na changamoto kubwa kutokana na wote kuwa na pointi sawa katika msimamo wa ligi lakini watapambana ili kuhakikisha wanashinda huku akiwataka waamuzi wa mchezo huo kusimamia sheria 17 za soka ili kuhakikisha timu inashinda kutokana na uwezo wake.

Maganga amesema, kwa upande wao majeruhi ni walewale ambao walikuwa nao katika mchezo dhidi ya Mbeya City ambao ni mshambuliaji Gonazo Bi Thomas, Beki Erasto Nyoni na Agrey Morris pamoja na Mlinzi wa kati Paschal Wawa.

Michezo mingine itakayopigwa hapo kesho ni Mtibwa Sugar wakiwakaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Manungu Mkoani Morogoro, Mbeya City akiwakaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine Mkoani Mbeya, Mwadui FC akiikaribisha Yanga Uwanja wa Mwadui Mjini Shinyanga na Ruvu Shooting akiikaribisha Mbao FC Uwanja wa Mabatini Mkoani Pwani

Mgogoro wa CUF Wachukua Sura Mpya..Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha Nusura Kutekwa na Wanachama

$
0
0
Filamu ya mgogoro wa CUF sasa imeingia hatua mpya baada ya wanachama watatu kuhojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutaka kumteka mkurugenzi wa uchumi na fedha wa chama hicho, Jorah Bashange.

Chama hicho kikuu cha upinzani visiwani Zanzibar kimekuwa na mgogoro wa kiungozi tangu Profesa Ibrahim Lipumba ambaye alijivua uenyekiti Julai mwaka jana, atangaze nia ya kurejea kwenye uongozi.

Katika tukio la jana linalodaiwa kutokea saa 2.30 asubuhi wakati Bashange akitoka nyumbani kwake, limeripotiwa kituo cha polisi cha Buguruni wilayani Ilala.

Kamanda wa Ilala ambayo kipolisi ni mkoa, Salum Hamduni aliiambia Mwananchi kuwa watuhumiwa hao wanahojiwa na polisi.

Master Jay Aweka Wazi Sababu za Wasanii wa Bongo Kumkimbia Producer Marco Chali

$
0
0
Mtayarishaji mkongwe wa muziki na mmiliki wa studio ya 'Mj Records' Master J amefunguka na kusema kuwa ukimya wa 'Producer' Marco Chali kwenye muziki unatokana na wasanii wengi kuogopa gharama zake.

Master Jay alisema haya kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kudai kuwa wasanii wamekuwa wakiwakimbia watayarishaji wa muziki ambao wameweka misimamo yao kwenye gharama za utengenezaji wa muziki.

"Mimi nilishakaa na Marco Chali nilimuuliza juu ya hatma ya maisha yake, maana anaweza kuwa anafanya kazi na kazi zinasikika sana lakini yeye hapati maslahi, hivyo toka alipobadili malipo ya utengenezaji wa kazi wasanii wakakimbia, hivyo saizi yeye ameweka kiwango chake ukitaka kufanya naye kazi, hivyo wasanii wanakimbia na kwenda kwa watayarishaji wengine ambao wanatengeneza muziki kwa bei ya chini. Siyo Marko Chali tu saizi hata Lucci toka ameweka kiwango chake anachohitaji kufanya kazi wasanii wamemkimbia anafanya matangazo tu" alisema Master Jay

Mbali na hilo Master Jay anasema kuwa watayarishaji wengi wa muziki hivi sasa bongo hawapo vizuri kiuchumi ukilinganisha na wasanii kutokana na ukweli kwamba maproducer hao hawana msimamo, hawana umoja hivyo wasanii wanakuwa wanawatumia.

"Unajua hili suala siwezi kuwalaumu wasanii kwani wao ni wafanya biashara wanataka faida lakini ukweli ni kwamba sisi maproducer hatuna msimamo, hatuna umoja ndiyo maana wasanii wanatutumia wanavyotaka, maana wewe ukiweka bei ya juu wanakwenda kwa mwingine ambaye atatengeneza ngoma zao kwa bei ya chini, hivyo unakuta msanii ana maisha mazuri lakini producers wana maisha ya chini sana" alisema Master Jay

UTAFITI:Faida za Kiafya Kwa Wanawake Wenye Makalio Makubwa Hizi Hapa

$
0
0
Licha ya mvuto yaliyonayo yakiwa kwenye jinzi, makalio makubwa ya wanawake ni kinga kwa kisukari na magonjwa ya moyo.

Wataalamu wa afya wanadokeza kwamba makalio ni muhimu kwa afya ya binadamu kwani huwezesha kusimama na kutembea vile anavyoonekana. Na cha pekee, hueleza afya ya mtu hasa mwanamke.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza unaeleza uhusiano uliopo baina ya mwonekano wa makalio ya mwanamke na hatari yake ya kupatwa na magonjwa hayo kwa kuzingatia mgawanyo wa mafuta mwilini.

Majibu ya utafiti huo yanaeleza kuna uhusiano wa karibu kati ya mgawanyo wa mafuta mwilini na afya ya mwanamke ingawa mafuta hayo hayasambazwi kwa usawa kwenda sehemu tofauti za mwili.

Kiasi kikubwa cha mafuta kikihifadhiwa kwenye matiti ni hatari kwa afya kwa sababu yapo karibu na moyo kwani huongeza uwezekano wa kuziba kwa mishipa ya damu, lakini makalio ya wastani yanaashiria siha njema.

Utafiti huo ulibaini uvungu wa makalio hasa sehemu za juu za mapaja na nyonga ndiko yanakohifadhiwa mafuta ya ziada au fatty acids ambayo ni kinga dhidi ya magonjwa hivyo mhusika kuwa na afya njema.

“Mafuta yasipohifadhiwa sehemu salama huenda kwenye ini au mishipa ya damu ambako huweza kusababisha kisukari au magonjwa ya moyo,” anasema Dk Konstantinos Manolopoulos, kiongozi wa utafiti huo.

Ipo tofauti kati ya mwanamke na mwanaume kuhusu usambazaji wa mafuta mwilini.

Inaelezwa kwamba wanawake wanahifadhi zaidi mafuta sehemu ya chini ya mwili; mapaja, nyonga na makalio kuliko wanaume.

Hii ni habari njema kwa wanawake na wasichana ambao bado wanapata siku zao kwani kwa mujibu wa Dk Manolopoulos, kuwa mwanamke mwenye homoni za kike ni kinga ya magonjwa ya moyo kwa kiasi fulani. Lakini baada ya kukoma kwa hedhi, homoni hubadilika.

“Mwonekano wa kike unapotea na badala yake kitambi huanza kujitokeza. Badala ya mafuta kwenda makalioni, sasa yanahifadhiwa tumboni hivyo kuongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya magonjwa hayo hivyo kuwa sawa na wanaume wa umri huo,” anasema huyo.

Utafiti wa awali uliofanywa mwaka 2008 na kuchapishwa kwenye International Journal of Obesity kwa kutumia panya ulionyesha kwamba licha ya mafuta yanayohifadhiwa tumboni kuyeyushwa kwa urahisi, ni hatari kwani huziba mishipa ya damu na kurahisisha mshtuko wa moyo.

Ingawa hakuna uhakika wa namna mwili unavyogawanya hifadhi ya mwilini, watafiti hao wanabainisha kwamba watu wenye makalio makubwa wana nafasi ndogo ya kupata maradhi hayo hata watakapozeeka.

Dk Benjamini Rulakuze wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), anasema unaunga mkono utafiti huo na kufafanua kuwa magonjwa ya moyo na kisukari husababishwa na wingi wa mafuta katika mwili.

Dk Rulakuze anasema sehemu za tumbo, matiti, mapaja na makalio ndiyo hutumika zaidi kuhifadhi mafuta kwa mwanamke na endapo mtu atakuwa na mafuta mengi yanaweza kuathiri mishipa ya damu kwani hurundikana na kuifanya mishipa ya damu kuwa miembamba na kuzuia damu kupita kwa urahisi hali inayorahisisha shinikizo la damu.

Anasema: “Mafuta huathiri ufanisi wa kongosho kuzalisha homoni ya insulini ambayo hutumika kusafirisha sukari ya mwili kwenda kwenye seli za mwili ili zitumike kuupa mwili nguvu.”

Anasema endapo sukari itashindwa kuingia katika seli za mwili na kuyeyushwa, mtu anaweza kupata kisukari aina ya kwanza na ya pili.

Na endapo mafuta yatakuwa mengi yanaweza kubadili oksijeni iliyokuwa itumike kusafirisha glucose na kufanya seli zishindwe kupokea sukari hiyo, hivyo kuibakiza sukari kwenye damu na kusababisha ongezeko la sukari katika damu.

Daktari huyo anaeleza kuwa mbali na wanawake, wanaume ambao hupata matatizo ya kisukari na magonjwa ya moyo ni kutokana na mafuta mengi katika tumbo na kusababisha kitambi ambavyo wengi wetu hudhani kuwa ni afya.

“Endapo mafuta hayo yataongezeka zaidi huathiri mfumo wa damu kwa kuziba mishipa hivyo kuinyima nafasi ya kutosha kupita na kusababisha shinikizo la damu,” anasema.

Anaeleza kuwa ili kuepukana na matatizo hayo ni vema mtu akafanya mazoezi kila wakati ili kujiweka sawa na kupunguza mafuta mwilini. Mazoezi hayo yanaweza kuwa ni kukimbia, kukata tumbo na mengine ambayo husaidia kupunguza mwili.

Mbali na mazoezi ameshauri kuwa makini na matumizi au ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi kama nyama na kupendekeza matumizi ya mafuta ya mimea.

Daktari mwingine, Eliza Wampembe wa Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili (Muhas) anasema mbali na sababu hizo, kisukari kinaweza kurithiwa kutoka kwa wazazi au wanafamilia wengine ambao walikuwa na ugonjwa huo ndani ya ukoo.

Dk Eliza anabainisha kuwa mgonjwa wa moyo na kisukari yupo hatarini kuathirika na maambukizi mengine kwani huathiri figo na kongosho, hivyo kupunguza kinga za mwili.

“Miongoni mwa athari za kisukari ni miguu kuwa na vidonda visivyopona kwa urahisi kiasi cha kukatwa kwa baadhi ya wagonjwana kusababisha ulemavu ambao hawakuzaliwa nao,” anasema.

Pia, shinikizo la damu husababisha matatizo ya figo, macho, kiharusi, misuli ya tumbo na kutosikia vizuri.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2015 ya Shirikisho la Kisukari (IDF) Afrika, zaidi ya watu milioni 14 barani humo wana ugonjwa huo na idadi inaweza kuongezeka hadi kufikia milioni 34 mwaka 2040 endapo jitihada za dhati za kukabiliana nao hazitachukuliwa.

Ripoti hiyo inasema asilimia 66.7 ya watu wote barani Afrika wana kisukari, kati yao asilimia 79 ni wenye umri zaidi ya miaka 60.

Ripoti imeeleza ugonjwa huo ulisababisha zaidi ya vifo vya watu 300,000 mwaka 2015.

Licha ya mikakati ya Serikali kukabiliana na magonjwa mbalimbali, wataalamu wa afya wanashauri kila mwananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari zinazotolew

Shilole Aeleza Kilichomsukuma Kupatana na Nuh Mziwanda

$
0
0
Baada ya hivi karibuni Sholole na Nuh Mziwanda kupatana, Shilole amefunguka na kuzungumzia nini kimemsukuma mpaka akapatana na mkali huyo wa wimbo ‘Jike Shupa’.
Wawili hao ambao walikuwa wapenzi waliachana kwa kutupiana maneno huku Nuh Mziwanda akionekana kumlaumu Shilole kwa kumpotezea muda.

Akiongea na Uhead ya Clouds FM Ijumaa hii, Shilole amedai ameamua kumaliza tofauti zake na Nuh Mziwanda kwa kuwa muimbaji huyo wa ‘Jike Shupa’ alikuwa anapoteza kujiamini pale anapokutana naye.

“Nikwambia kitu situation moja ambayo ipo, Nuh akiniona mimi huwa anapoteza kujiamini,” alisema Shilole. “Sasa ili kumueka sawa na aweze kuwa vizuri lazima na mimi nimwonesha am good. Kwa hiyo alivyoniona nipo good na yeye akawa fresh na furaha imerudi na nazani maisha yanaendelea,”

Hata hivyo mkali huyo wa wimbo ‘Say My Name’ alikanusha kurudiana na Nuh Mziwanda huku akidai kwa sasa wao ni washkaji.

Bifu la Diamond na Ali Kiba Halipo Tena..Picha ya Kwanza Wakiwa Pamoja Wakirekodi Yavuja

$
0
0
Diamond vs Ali Kiba Beef has end, Finally your Number one website of Tanzania  website has Captured a Photo of Two finest Bongo Flavor  from Tanzania Ali vs Diamond are on the same Studio Recording their Hit Song, is this Means that their Beef and Mis Understanding has become to an end so that they can finally remove their Difference? let us wait and See, i cant wait for this collaboration of Diamond Platinum vs Ali kiba!!!!!!

HATIMAYE Faiza Ally Atoa Stori ya Maisha Yake Inayomuumiza na Kumfanya Hivyo Alivyo Hivi Sasa...Sugu Atajwa

$
0
0

Faiza Ally Afunguka Historia ya Maisha yake Kama ifuatavyo:

Naomba niileze ujinga wangu kwenye mtandao nikiwa naamini kuna elimu kutoka kwa mjinga na muelevu.... Naomba mfatilie Maana Huwenda yakawa magazeti mengi sana.....okay Kila siku mwenzenu nalia sana nalilia mapenzi .... Naombeni niwape storia yangu ya mapenzi inayo husu umaskini....nazani Leo imefika siku Kwa wasio jua wajue Kwa nini naumia sana na sisahau Maana wkt mwingine nahisi nimejizulumu sana duniani lkn wkt mwingine najiona niko sawa Kabisa .... wkt mwingine nahisi nimemkosea sana baba Sasha (Sugu) Na wakati mwingine naona amenikosea sana any way naombeni msome halafu mnipe mawazo yenu lkn msinihukumu mpaka mwisho wa stori........ STORI OF MY LIFE..... mm ni mtoto wa mwisho katika familia yangu....nimekua Kwenye shida sana Japo baba yangu alikua na uwezo wkt huo.... Na nilichukia sana umaskini - nilitamani maisha mazuri juu yangu na familia yangu.... Nilipo kuwa kuwa niliondoka nyumbani ktk umri mdogo sana na nilikua msichana mwenye NDOTO sana .... Nimeanza kuhaso kitambo sana ikafika wkt nikajipa majukumu makubwa sana Kwenye familia.... Nilianza kumtunza mama ktk umri mdogo ... Nilianza kusomesha watoto katika umri ambao hata mimi nilikua mtoto sana - kiasi watoto nilio anza kusomesha mmoja sasa yuko form four na kuna wengine wawili na hii yote nilitaka kubadilisha familia yangu.... Kwa hivyo nimeishi Kwa kujinyima sana mpaka leo ili nitumize malengo na nibadilishe muonekano wa familia yangu.... Kuna wkt ilikua una niwia vigumu sana Kwenye mahusiano kutokana na majukumu niliyo nayo ..... Kwa hiyo Kwa miaka mingi nimefanya Kila niwezalo ili familia yangu isimame na nilifanikiwa Kwa Kweli ... Mama yangu na familia yangu wanakula vizuri ... Wanaenda shule Pamoja na mavazi mazuri.... Kiufupi nimetoka mbali sana na familia yangu.... Nimesimama Kama baba,mama,dada,anti na Kila kitu.... Nakumbuka kuna wkt marehemu bibi yangu aliwahi kumwambia mama huyu mtoto wako ni bora unge mzaa mwanaume .... Kutokana na hayo yote imenijengea ujasiri wa kuona Kila kitu naweza peke yangu bila kutegemea mwanaume na kuwa na maamuzi yoyote kuona kwamba ntaweza tu chochote kilichopo mbele yangu.... Lkn Kwa Kweli Hilo jambo Japo kuna wkt najisifu lkn huwa kina niumiza sana .....INAENDELEA

Nuh: Siwezi Kurudiana Na Shilole

$
0
0
MSANII wa Bongo Fleva anayetamba na Wimbo wa Jike Shupa, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amesema kuwa japo kuna tetesi zinaenea mtaani kwamba amerudiana na aliyewahi kuwa mpenzi wake, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ suala hilo halina ukweli wowote ndani yake na wala hafikirii kabisa kurudiana na mwanadada huyo.

Tetesi za Nuh kurudiana na Shilole zilianza kuvuma baada ya kusambaa kwa kipande cha video kilichowaonesha wakipatanishwa wakati wakiwa kwenye safari za Tamasha la Fiesta na watu kujiongeza kuwa wamerudiana.

Nuh Mziwanda akiwa na mpenzi wake wa zamani Zuwena Mohammed ‘Shilole’.

“Kilichotokea ni kwamba mimi na Shilole tumeondoa tofauti zetu za kibinadamu ambazo tulikuwa nazo baada ya kuachana.

Lakini kuhusu kurudiana hahitakuja kutokea hata siku moja na siwezi kurudi nyuma kwenye hili maana nina mpenzi wangu ninayempenda,” alisema Nuh.

Wananchi Waliopo Dar es Saalam Kupatiwa Matibabu Bure

$
0
0
Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Saalam iliyo chini ya mheshimiwa Paul Makonda imeratibu tukio maalum litakalofanyika siku ya tarehe 24-25/09/2015 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja. Ambapo wananchi watakaojitokeza kwenye tukio hilo maalum watapatiwa matibabu bure.

Taarifa iliyotolewa na mkuu wa mkoa kupitia akaunti yake ya Instagram imeeleza kwamba wananchi watapata fursa ya kupimwa magonjwa zaidi ya kumi (10) na kupatiwa matibabu bure.

Hivyo wananchi wote wanaombwa kujitokeza kwa wingi.

Rais Magufuli Apokea Taarifa Ya Tetemeko La Ardhi Mkoani Kagera, Akabidhiwa Msaada Wa Dola Laki Mbili Utoka Kwa Rais Museveni Wa Uganda

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amepokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Tetemeko hilo limetokea Kagera na mikoa jirani ya Mwanza, Geita na Kigoma.

Pamoja na kupokea taarifa hiyo Rais Magufuli amepokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki mbili (USD-200,000/-) sawa na shs 437 milioni kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

Pia amepokea taarifa ya mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

Katika taarifa yake  Majaliwa amesema tetemeko hilo limesababisha vifo vya watu 17, majeruhi 440, nyumba 2063 zimeanguka, nyumba 14,081 zipo katika hali hatarishi na nyumba 9,471 zimepata uharibifu mdogo, huku watu 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

Matembezi Dar yakusanya Sh1.5 bilioni za waathirika wa tetemeko Kagera

$
0
0
TAKRIBANI shilingi bilioni 1.5 zimechangwa kufuatia matembezi ya hisani yaliyopewa jina la “Walk for Kagera” yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 septemba mwaka huu mjini Bukoba Mkoani Kagera.

Akizungumza mara baada ya matembezi hayo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe Ally Hassan Mwinyi aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza na kushiriki matembezi hayo ya hisani.

“Nawapongeza sana wadau wote mlioshiriki katika matembezi haya, mmeonyesha mshikamano mkubwa kwa umoja wenu mmeweza kuchangisha jumla ya shilingi 1,502,680,000 hii inatia faraja sana muendelee na moyo huo” Alisema Mzee Mwinyi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wahanga wa tetemeko hilo wanapatiwa huduma stahiki na kwa wakati.

Balozi Kijazi aliongeza kuwa kutokana na kuguswa na tatizo hilo Serikali pamoja na Taasisi zake imetoa msaada wake ambao unakadiriwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni kuthamini utu wa wahanga.

“Najua kuna athari kubwa imetokea kutokana na tetemeko hili, sisi kama Serikali tunafanya kila jitihada kuhakikisha wahanga wote wanapata misaada na kurejesha huduma zote katika hali yake” Alisema Balozi Kijazi.

Awali akisoma maelezo ya tathmini ya athari za tetemeko hilo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi amesema kuwa hadi kufikia tarehe 16 idadi ya vifo ni 17, nyumba zilizoanguka zimefikia 840 huku zilizoharibika zikiwa ni 1264 na majengo 44 mali ya Taasisi za umma yameharibika.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mabalozi nchi, Balozi wa Zimbabwe ametoa pole kwa wahanga wa tukio hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania pale panapo hitaji msaada wao.

Matembezi hayo ya hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi yaliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu.

Mrembo Laura Kwai Atwaa Taji la Miss Higher Learning Institutions 2016

$
0
0
Mshindi wa Taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Laura Kwai akipunga mkono kwa mashabiki wa ulimbwende mara baada ya kutangazwa kutwaa taji hilo jana katika Ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni mshindi wa pili wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Evelyn Andrew pamoja na mshindi wa tatu wa taji la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016, Clara Nyaki (kulia). Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL).

 Sehemu ya wadau na wapenzi wa masuala ya urembo wakiwa katika mapozi ya picha kwenye Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 jana.

 Sehemu ya Jopo la Majaji wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakijadiliana jambo kabla ya kutoa matokeo kwenye shindano hilo jana..

 Sehemu ya Washiriki wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakichuana katika miondoko mbalimbali ya mavazi.

Baadhi ya maofisa na wafanyakazi wa TTCL ambao ni wadhamini wakuu wa Shindano la TTCL Miss Higher Learning Institutions 2016 wakipiga picha na Balozi wa TTCL, Glory Gidion mara baada ya kumaliziki kwa shindano hilo.

Ngoma Amfunga Mdomo Julio, Yanga Yailaza Mwadui

$
0
0
Mchezo umemalizika  kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, wageni Yanga wamepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwadui FC, yote yamefungwa na Donald Ngoma.
Viewing all 104771 articles
Browse latest View live




Latest Images