Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

ZARI Amuumbua Hamisa Mobetto, Aanika Live Uchafu Wake na Diamond

0
0
Zile tetesi za muda mrefu kuhusu mwanamuziki Diamond Platnums pamoja model maarufu nchini, Hamisa mobeto aka Salome kuvunja amri ya sita huenda zikazaa matunda soon baada ya hivi karibuni mzazi mwenzie ,ambaye pia ni mpenzi wake wa sasa, Zari Hassan ambapo kupitia page yake ya snapchat amepost picha za hereni huku zikiwa zimeambata na ujumbe mzito, ambapo alimtaka mwenye hereni hizo cheap alizozisahau chumbani kwake akazichukue mara moja.

Hata hivo kwa mujibu wa wapenda umbea mjini aka team chambua kama karanga waliweza kuzichambua hereni hizo vizuri na kubaini kuwa zilishawahi kuvaliwa na mwanamitindo maarufu nchini Hamisa Mobetto(pichani) aka SALOME.

Huenda hii ikawa habari Kali kwa wiki hii, hata hivyo bado Zari hajafunguka chochote kuhusu mmliki wa hereni hizo, wala Hamisa bado hajazungumzia chochote kama ni kweli uchafu huo (kama alivyoita Zari) ni wake au sio

Alikiba na Timing Mbaya, Kapoteza Tena Pambano Dhidi ya Diamond Platnumz

0
0
Mimi ni mpenzi mkubwa wa muziki na hasa muziki wa dansi ingawa nyimbo nyingi sizijui. Nikiwa mdogo nilikuwa napenda sana kuwasikiliza Washirika Tanzania stars na mpaka sasa nikisikia nyimbo yao yoyote natulia kwa makini kusikiliza. Hiyo ilikuwa bendi pendwa kwangu kabla hawajasambaratika na kujikuta nikitekwa na wakongo hasa hasa Wenge Musica BCBG na kidogo ikaingia Nouvelle Generation.

Waliposambaratika hao nilijikuta katika majonzi baadae nikapata faraja kwenye nyimbo za dini. Bado nafuatilia muziki ila si kwa nguvu ile tena, itokee tu (in sheikh Kipozeo tone).

Niingie kwenye mada. Muziki wa Tanzania umekuwa kwa kiasi kikubwa na unapozungumzia mastaa wanaotamba vilivyo utawakuta Ali Kiba na Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz. Watu hawa wamejijengea umaarufu mkubwa na kujitengenezea mashabiki ambao wamegeuka mahasimu wakubwa kwenye mitandao ya kijamii hasa instagram.

Mimi binafsi si shabiki wa mtu yoyote kati ya hao ila kuja mmoja akitoa wimbo wake (hit song) najikutaga nafuatilia mwenendo wake kwa mashabiki na vyombo vya habari. Kimsingi Alikiba alivuma sana kabla ya Diamond na alifanikiwa kufanya show nyingi nje ya nchi hususan Uingereza na Marekani ambapo nahisi ilikuwa mwanzo wake wa kuporomoka kimziki kabla hajaamshwa na watu wanaomchukia Diamond na kumtengeneza kama mtu atakayemshusha Diamond kimuziki.

Alikiba amesahau kazi yake kama mwanamziki amejikuta kwenye harakati za kupambana kumshusha mwenzake ili akae kileleni. Hii itaugharimu muziki wa Tizii kwani kushuka kwa Diamond hakutamuweka Ali Kiba juu kivile kwa kuwa hajui kukaa kileleni. Katika harakati zake za kumshusha Diamond kileleni amejikuta yeye na timu yake wakijaribu ku counter pale Diamond anapoachia hit song mpya.

Kitu kilichonisukuma kuandika huu uzi ni baada ya Diamond kuachia wimbo wake wa Salome ambao ni remix ya wimbo Maria Salome wa Saida Karoli. Siku moja baada ya kuachia wimbo huo Alikiba naye akaachia wimbo wake wa Nitulize. Nimezisikiliza nyimbo zote mbili kwa kiasi ila nimefuatilia ni kwa kiasi gani nyimbo hizo zimepokelewa na mashabiki na kugundua Alikiba amefanya Tuming mbaya sana.

Ni afadhali angeacha Salome akakaa hewani kwa wiki moja au mbili ili atoe yake. Sio uongo kuwa Diamond ana mashabiki wengi across the continent na hayo yanathibitishwa na kauli ya wanamuziki wenzake wa Afrika kama akina Mafikizolo na Davido. Labda niongee kidogo, Jumatatu nilikuwa niko bored nyumbani na wife hayupo kaenda msibani nikawa naangalia chanel hazinivutii baadae nikajikuta nimeweka chanel E.

Hapo nilikuta Mafikizolo wakiwa wanahojiwa walivyomtafuta Davido. Baada ya kumpata Davido ili wafanye collabo aliwaambia pia wamtafute Diamond kwani ni mtu mwenye mvuto kimuziki na ana mashabiki wengi ambapo kila msanii wa Afrika anatamani kuwa kama Diamond. Hiyo testimony inanipa fursa ya kusema Diamond yuko mbali sana kimuziki kuliko Alikiba.

Mwisho nakuomba msomaji uangalie youtube mapokezi ya Salome na Nitulize halafu uniambie nani anafanya vizuri. Alikiba alipofanya vizuri alirudi kulala na kushtuka underground wake kawa leader wake. Akitaka kufanikiwa ajiwekee malengo ya kutoka alipo kusogea mbele na si kumkimbiza mtu.

Na pili akumbuke yeye yuko chini ya lebo ya watu wengine ( sony) wakati mwenzake anafanya muziki chini ya lebo yake mwenyewe kwa hiyo sijui kama hiyo itamtengenezea wigo wa kuwa na lebo yake kama anavyojaribu kufanya kwa kuwachukua baadhi ya wanamuziki kama Baraka da Prince kuwa ndani yake.

Imeandikwa na Kingwipa1

TETESI za Bifu Kati ya Raymond na Harmonize Kutoka WCB, Meneja Wao Asema Haya

0
0
Meneja anayewasimamia wasanii wa WCB wakiwemo Harmonize na Raymond, Ricardo Momo, amekanusha tetesi kuwa mafahari hao wamekuwa wakivimbiana na kwamba kila mmoja anajiona bora.

Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Supa Mega cha Kings FM ya Njombe, Prince Ramalove, Ricardo amedai kuwa wawili hao wanaishi kwa upendo mkubwa.

“Hayo ni maneno tu, sisi tunaishi kama ni familia moja, natamani siku moja uje uone tunavyoishi, tunataniana , tupo kwenye shida tunasaidizana,” amesema.

“Hakuna hata mmoja mwenye ugomvi na mwenzake, hayo ni maneno tu ya watu wa nje, hakuna matatizo yoyote yaliyotokea kati ya Harmonize na Raymond.”

Ujenzi wa Daraja la Salender kuanza 2017 na Kukamilika Mwaka 2020

0
0
Rais John Magufuli amekutana na balozi wa Korea Kusini Ikulu Dar, Rais amesema kampuni ya Kikorea inayofanya Designing ipo hatua za mwisho na itatangaza tenda hivi karibuni na ujenzi wake unatarajia kuanza mwezi wa Juni 2017.

Daraja hilo litakuwa na urefu wa km 7 na km 1,4 zitajuwa ndani ya bahari kusaidia kupunguza foleni fedha hizo zimetolewa na Exim ya Korea Kusini
Magufuli pia ameema ana mpango wa kumteua balozi akaiwakilishe Tanzania Korea Kusini kwa kuwa ni marafiki.

Pia wamezungumzia ujenzi wa meli mpya ziwa Victoria ambapo wakorea hao watawatuma watalaamu wao kufanya ukaguzi, ujenzi wa meli upo kwenye bajeti ya serikali.

Crazy GK: Sifanyi Show Bongo Chini ya Shilingi Milion 30

0
0
Naheshimu muziki wa GK lakini kwa nlichomsikia anasema ni wazi kua atakwama...umepotea kwenye anga ya muziki then unarudi halafu unasema kua hufanyi show chini ya milioni 30. Dah aisee...Diamond, Rayvany, Harmonize, Navykenzo, Alikiba Wasemeje? na wakali wengine wanaotingisha katika anga ya muziki redioni kwa sasa?

Duh!  Mwana umechemka hapa. Swali ni kua are you worth 30 million kaka mkubwa ?? katika zama hizi ?

Orodha ya Wasanii Watakaowania Tuzo za MTV MAMA 2016, Navykenzo, Diamond na Alikiba Ndani

0
0
Orodha ya wasanii watakaowania tuzo za MTV MAMA 2016, Jumamosi ya Oktoba 22 kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome, Afrika Kusini imetoka – kuna vipengele tisa. Tanzania inawakilishwa na Alikiba, Diamond na Navy Kenzo.

Hii ni orodha kamili ya wasanii waliochaguliwa kuwania tuzo hizo

Best Live Act

Stonebwoy (Ghana)
Cassper Nyovest (South Africa)
Mafikizolo (South Africa)
Mr Flavour (Nigeria)
Eddy Kenzo (Uganda)

Best POP/ ALtenative

Tresor – Never let Me Go
Shekinah & Kyle Deutsch – Back to the Beach
Timo ODV – Find My Way
LCVL ft Sketchy Bongo – Cold Shoulder
Desmond & The Tutus – Pretoria Girls

Personality of the Year

Caster Semenya
Linda Ikeji
Pearl Thus
Wizkid
Pierre Emerick

Best Group

Toofan (Togo)
Micasa (South Africa)
Navy Kenzo (Tanzania)
R2Bees (Ghana)
Sauti Sol (Kenya)

Best Male

Black Coffee (South Africa)
Diamond Platnumz (Tanzania)
AKA (South Africa)
Patoranking (Nigeria)
Wizkid (Nigeria)

Best Lusophone

NGA
Nelson Freitas
C4 Pedro
Lizha James
Preto Show

Best International Act

Beyonce
Drake
Adele
Future
Rihanna

Best Collaboration

AKA ft Yanga, Burna Boy, Khuli Chana – Baddest
Dj Maphorisa, ft Wizkid, Dj Buckz – Soweto Baby
Nasty C ft Davido, Cassper Nyovest – Juice Back (Remix)
Sauti Sol ft Alikiba – Unconditionally Bae
Patoranking ft Sarkodie – No Kissing

Best Hip Hop

Emtee (South Africa)
Ricky Rick (South Africa)
YCEE (Nigeria)
Olamide (Nigeria)
Kiff No Beat (Ivory Coast)

MAMBO Yamwendea Kombo DAVIDO..Akosa Tuzo za MTV Mama Mwaka Huu, Mwenyewe Ajipa Moyo Kwa Kusema Haya

0
0
Baada ya kutotajwa jina lake kwenye tuzo za MTV MAMA 2016, Davido amejipa moyo kufanya vizuri mwakani kwenye tuzo hizo.

davido

Kupitia mtandao wake wa Twitter, muimbaji huyo ameandika, “I really shouldn’t be nominated this year For what?? I got three MAMAS in two years I’m good ! Still gonna be a great show! BUT NEXT YEAR 😈.”



Davido amefanikiwa kushinda tuzo tatu za MTV MAMA ndani ya miaka miwili mfululizo huku tuzo mbili kati ya hizo zikiwa ni ‘Best Male’ alizoshinda mwaka jana na mwaka juzi.

Tangu staa huyo aliposaini mkataba na kampuni ya Sony Music mapema mwaka huu mambo yameonekana kumwendea kombo huku akiwa hajaachia wimbo hata mmoja na kuvunja mara kadhaa ahadi yake ya kuachia albamu yake iliyotakiwa kutoka tangu mwaka jana.

HARD WORK Pays...AIKA na Nahreel Ndani ya MTV Mama Awards 2016

0
0
Kundi la Navy Kenzo ambalo linaundwa na Aika na Nahreel limefanikiwa kuingia katika Mchakato (Nomination) wa kutafuta washindi wa MTV Mama Awards 2016 Kwenye kipengele cha Group Bora la Muziki Afrika,

Nimeanza na kuandika Hard Work Pays Kwasababu ni dhahiri kuwa hawa jamaa wamefanya kazi hasa katika miaka ya karibuni katika kazi zao za muziki huu wa Bongo Flava Hapa Tanzania, Ukiangalia nyimbo zao za hivi karibuni kama Game na Kamatia chini ni nyimbo ambazo waliamua kuwekeza pesa hasa ili kufika kiwango cha kimataifa na kuweza kuwafanya wajulikane Afrika nzima

Hawa ni Mfano mzuri sana wakuigwa na wasanii wengine wa hapa Bongo , Katika tuzo hizo Kutoka Tanzania Wasanii walioweza kufanikiwa kuingia katika mchakato Navykenzo, Diamond na Ali Kiba...

Kazi imebaki kwetu mashabiki kuwapigia kura ili waweze kushinda Tuzo Hizo

MSWAHILI Aachi Asili..Diamond Amrushia Dongo Mume wa Zamani wa Zari..Huku Akijisifia Kwa Nyumba Aliyonunua Afrika Kusini

0
0
Mwanamuziki Diamond ametupa Jiwe Gizani ambalo ninaonekana kumlenga mume wa zamani wa Zari Hassan....Lisome mwenyewe Hapa chini:


Diamondplatnumz

They are busy bragging them selves that they are Rich while their Kids staying in the Renting House... and now a person wich they are daily abusing and saying that he's broke & Poor Bought a House, so that their Kids can have a better life, as they always wish on Social Media..... Happy Birthday Mama tee i hope you like our new South African House....Can't wait for your Big weekend in Zanzibar tomorrow....I love you So much mama tee, we ndio Salome wa Moyo wangu pekee @zarithebosslady 😙🌷🎉🎂🎂🎉🌷 (Wanakazana kujisifu Matajiri Ilhali watoto zao wanaishi kwenye Nyumba zakupanga... halaf leo yuleyule wanaemtukana kutwa kwenye Mitandao kuwa Masikini, kajawa na shida, Kanunua nyumba kulekule kwao ili watoto wao waishi Maisha bora kama wanayoyatamani... Heri ya siku ya Kuzaliwa Mama tee wangu.... Nakupenda sana na unalifahamu hilo...natumai umeipenda Nyumba yetu hii mpya South Africa... nasubiria kwa hamu kusheherekea nawe siku yako hii kubwa kesho zanzibar.....

WEMA Sepetu Akunwa na Wimbo wa Diamond 'Salome' Ajirekodi Akiimba, Diamond Asema Haya

0
0
Malkia wa filamu Wema Sepetu amekunwa na wimbo mpya wa Diamond Platnumz ‘Salome’ na kuamua kujirekodi video huku akiimba wimbo huo.

Diamond alipost video instagram inayomwonyesha mwigizaji huyo akiimba wimbo ‘Salome’ huku akiandika ujumbe wa kuonyesha kufurahishwa na kitendo hicho.

“Hivi huku patakuwa ni kupatwa kwa nini?. Tisha sana ‘Salome’ wake Idris Sultan full Video link in my BIO and @rayvanny Bio,” aliandika Diamond kupitia instagram.

Hatua hiyo huwenda ikafungua njia zaidi kwa wawili hao kuaidia katika mambo yao.

List Ya Vyuo Vilivyotoa Selection Ya Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Vyuo Vikuu Mbalimbali 2016/2017

Orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na UDOM mwaka wa masomo 2016/2017

0
0
Kupata majina ya wanafunzi walichaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma ngazi ya Shahada, katika mwaka wa masomo 2016/2017,<<Bonyeza hapa>>

Diamond Platnumz Awanunulia Watoto wa Zari Nyumba South Africa..Adai Walikuwa Wanaishi Nyumba ya Kupanga

0
0
Kupitia ukurusa wake wa instagram, mwanamuziki diamond platnums amepost mjengo wake mpya uliopo south Africa, huku akimpongeza mzazi mwenzie (mama tiffah) kwenye siku yake ya kuzaliwa

Dongo la Diamond Lamtoa Mapovu Aliyekuwa Mume wa Zari Ivan....Meseji zavuja Zari Akimuomba Msamaaa

0
0
Hali ni Tete Madale....Dongo la Diamond aliloandika kuhusu wale wanaojisifu kuwa wanahela lakini watoto wao wanaishi kwenye nyumba ya kupanga limemfikia mwenyewe ambae ni mume wa dhamani wa Zari aitwaje Ivan , Nimepitia kwenye mitandao nimekuta mazungumzo yaliyovuja ambayo yanasemekana ni kati ya Zari na Ex Wake huyo baada ya Ujumbe wa Diamond Kuwafikia mpaka watoto wao ambao walizaa pamoja.

Nimekuwekea Hapa hayo mazungumzo ambayo yasemekana yamevuja kutoka kwa mmoja wao:



Ruby Awapiga Vijembe Clouds FM na Ruge Kwenye Wimbo Wake Mpya Soma zaidi Hapa

Queen Tipha afunguka baada ya mpenzi wake, Ben Pol kuonekana kwenye picha akibusiana na Snura

0
0
Latifa Mohamed aka Queen Tipha amefunguka baada ya kusambaa mitandaoni picha za mzazi mwenzake, Ben Pol akionekana wakibusiana na Snura wakati walipokuwa mkoani Tabora kwa ajili ya tamasha la Fiesta.

Queen Tipha amekiambia kipindi cha Clouds E cha Clouds TV kuwa hakushtuka baada ya kuona picha hizo kwa kuwa mpenzi wake huyo alikuwa kazini.

“Nimeamka asubuhi nikaona watu wengi wamenitag, nilichukulia kawaida kwa sababu ni mtu ambaye ninamuamini na aliniaga kuwa anaenda kazini,” amesema Queen Tipha.

“Sikuona kama ni kitu cha ajabu kwa kuwa yule ni msanii mwenzake na rafiki yake pia. Nimechukulia kawaida tofauti na watu wanavyofikiria,” ameongeza. Queen Tipha aliwahi kuwa mshindi wa pili kwenye Miss Tanzania 2013 na wamefanikiwa kuzaa mtoto mmoja na mpenzi wake Ben Pol.

Wimbo Mpya wa Ruby Kijembe kwa Mawingu na Ruge? Usikilize Hapa

0
0
Nimeusikia kwa mara ya kwanza wimbo wa mwanadada Ruby baada ya kujitoa katika matamasha ya Fiesta. Wimbo unaitwa Wale Wale, mwadada kama kawa kaimba poa sana wimbo unamelody kali sana yaani zile zinaitwaga "Catch Melodies".

Lakini maudhui ya wimbo ukiyasikiliza vizuri naona kama katupa jiwe kwa Clouds na Bwana Mutahaba. Embu Fanya Kuusikiliza Hapa....Siku hizi Mwendo wakutupa mawe Gizani tuuuuu

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo na CVPeople Tanzania, Bonyeza Hapa

Uvutaji wa Bangi na Michepuko Wasababisha Ndoa na Brad Pitt na Angelina Jolie Kuvunjika

0
0
Moja ya couple maarufu na iliyokuwa inapendwa duniani yavunjika rasmi
Machungu ya talaka Angelina jolie na Brad pitt. Baada ya angelina jolie kusign karatasi za talaka siku ya jana.. Brad pitt afura na kusema Angelina Jolie ni mwendawazimu.

Hii itakuwa ni talaka ya pili ya Brad pitt. Ya kwanza ni ile ya kuachana na kimwana Jennifer Aniston. kwa jolie hii itakuwa talaka ya tatu. Ya kwanza
ni ya kuachana na Johnny Lee Miller na Billy Bob Thornton

Hii talaka inakuja baada ya Jolie na Brad Pitty kuishi pamoja kw miaka 12 na miaka 2 ya ndoa Angelina jolie asema Brad Pitt ni mlevi sana na ana matatizo ya hasira. Jolie hakuwahi kufurahishwa na malezi ya Brad kwa watoto. Angelina jolie ameiomba mahakama apewe watoto wote sita aishi nao

- taarifa za ndani zinasema jolie (41) amemtaliki brad pitt baada ya kugundua ana mahusiano na mwanamke mwingine marion cottilard. Jolie asema Brad Pitt alikuwa anakula sana bange.. ni risk yeye kuongoza familia.

Polisi Wataovaa Nusu Uchi au Mlegezo Kwa Askari wa Kiume Kuchuliwa Hatua Kali

0
0
Picha:Polis Kutoka Kenya Linda Okele Akiwa na vazi la Kubana Mwili lililozua Gumzo Nchini Huko
Naibu Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Abrahman Kaniki amewaagiza makamanda na maofisa waandamizi wa jeshi wa mikoa yote kuhakikisha wanasimamia nidhamu ya uvaaji kwa askari wa kike na kiume na watakaokutwa wamevaa sare zinazoonyesha sehemu za miili yao watachukuliwa hatua.


Akizungumza na askari hao wakati akifungua kongamano la siku 3 la mtandao wa polisi wanawake mjini Dodoma, Naibu IGP , Inspekta Jenerali huyo amepiga narufuku uvaaji wa sketi fupi kwa askari wa Jeshi hilo.

“Kwa wale wanaume, yeyote ambaye anavaa ‘kata k’ kamanda na kesi yakujibu, hivyo hivyo ma-WP ambao wanavaa kinyume na taratibu ambazo zipo jeshi la polisi kamanda ana kesi yakujibu, lakini itakwenda sambamba na yule in charge,” alisema Kaniki.

Pamoja na hilo amewaonya viongozi wa jeshi ambao wamekuwa wakivunja utaratibu , ikiwamo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na askari wa chini , kwa kuwa hiyo ni sawa na kumkabidhi mtu kondoo kuwachunga na badala yake akawala .

Atumia Asali Kufanya Sehemu Nyeti Kuwa Ndogo na Kubana, Nyeti Zaoza

0
0
Nawaletea Kama Nilivyotumiwa:

Miaka 3 iliopita nimekuwa katika matatizo makubwa sana nawashwa sana ukeni, hospitali wanasema ni fungus, natumia dawa baada ya wiki tatizo linarudi pale pale, nimekuwa mtu wa kujikuna muda wote, uchi unawaka moto kwa kujikuna, nimeendelea na tiba mpaka likaibuka tatizo lingine.

Kila ninapofanya tendo ndoa napata maumivu ambayo hayaelezeki wakati mwingine mpaka naanza kubleed, kurudi tena hospitali wakasema nipime vipimo vya kansa, ikabidi watoe kinyama ndani na kufanya vipimo, majibu yalipotoka wakasema hakuna kansa lakini tatizo linazidi kuongezeka siwezi tena kufanya tendo la ndoa lakini madaktari katika vipimo vyao wakagundua ndani ya uke kwenye mlango wa kizazi kuna wekundu mwingi sana, badala ya rangi ya pink kumbe ile rangi nyekundu ni sehemu ambayo inashambuliwa sana na bacterial wasiosikia dawa, wakajaribu kupeleka dawa hapo kwenye hilo eneo lililoathirika bado ilishindikana kuwaua walikuwa bado wanaonekana wanashambulia, ikabidi madatari muhimbili waniulize jinsi ninavyofanya usafi katika uke wangu, nikawaeleza ukweli nilichokuwa nafanya.

NASAFISHA KWA KUINGIZA VIDOLE NDANI, NAJIINGIZA ASALI NA PAMBA NDANI ILI UKE UWE UMEBANA NA VINGINE VINGI TU, TUNAVYOSHAURIANA WASICHANA.(VIUNGA ****) madaktari wakaniambia sababu ya matatizo yangu ni nimeua bakteria wote ambao ni walinzi ndani ya uke ndio maana uke wangu umeshambuliwa sana sana na bacteria ambao hawasikii dawa.

NDUGU ZANGU MAKUNGWI WENZANGU, LEO HII NALIA PEKE YANGU NILIKUWA NIKIUNGA SANA UKE WANGU KWA VIUNGIO NA NAINGIZA VIDOLE VYENYE KUCHA NDEFU NAINGIZA MPAKA SABUNI ILI KUOKOA MAISHA YANGU MADKTARI WAMESEMA NI LZM WANITOE KIZAZI CHANGU SABABU NIKIACHA ITAGEUKA NA KUWA KANSA HALI YANGU NI MBAYA BADO BINTI MDOGO NATOLEWA KIZAZI MIAKA 29 TUSIKU YA JUMATATU NDIO NAFANYIWA OPERATION YA KUTOLEWA KIZAZI...

NAOMBA MNIWEKE KTK SALA ZENU OPERATION IENDE SALAMA.

....NAWAPENDA WOTE....

TUMA UJUMBE HUU NA KWA WENGINE KAMA MIMI NILIVYOUPOKEA NA KUUTUMA KWAKO! Hata kama we ni mwanaume mfundishe mkeo au bintiyo
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images