Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104657 articles
Browse latest View live

Install Application ya Blog Hii ya Udaku Special Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

$
0
0

Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 




Baraza Kuu la Uongozi CUF lamfuta uanachama Profesa Lipumba

$
0
0
Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF) Taifa lililokutana Zanzibar leo limemfukuza uanachama Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba.

Taarifa kutoka katika mkutano chama hicho unaeleza kuwa, wajumbe wote waliohudhuria wamepiga kura ya kuridhia kufukuzwa uanachama kwa Prof. Lipumba.

Hatua hii imekuja ikiwa ni siku chache tangu Prof. Lipumba kurejea na kusema kuwa yeye ni mwenyekiti halali wa chama hicho kufuatia maamuzi yaliyotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi.

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF limefikia uamuzi huo kwa mujibu wa Katiba ya Chama, Ibara ya 10 (1)(c)

TUNDU Lissu ailaza chali Jamhuri, kesi ya Dennis Wilson aliyemkashifu Rais Magufuli

$
0
0
TUNDU Lissu, Mwanasheria Mkuu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameiangusha Jamhuri katika kesi ya kumkashifu JPM iliyokuwa ikimuhusu Dennis Wilson

Wilson, mwanachama wa Chadema alishtakiwa na Jamhuri ya Tanzania katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa kuandika maneno ya kuudhi na kutaja jina la JPM katika mtandao wa kijamii.

Katika taarifa zilizotufikia muda huu kutoka Kisutu zinaeleza kuwa, mahakama hiyo imetupilia mbali kesi hiyo kutokana na washitaki (Jamhuri) kushindwa kufafanua uhalisi wa kifupisho JPM.

“Sababu ni hati magumashi ya mashtaka ambayo haikuwa na maelezo ya kutosheleza kwasababu watesi wetu (Jamhuri) hawakufafanua maana ya kifupisho ‘JPM’ ambaye ndiye walidai ameudhika na maneno ya Wilson.

“Mahakama imekubaliana na hoja yetu kwamba, JPM inaweza kuwa kifupisho cha Juma Pumba Maharage au majina yoyote yanayoanzia na JPM.

“Mahakama imewaelekeza washtaki kama wanataka kuendeleza vita yao basi walete hati ya mashtaka inayoeleweka,” amesema Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki.

Hata hivyo, baada ya mahakama kutupilia mbali shauri la Jamhuri, mshtakiwa (Wilson) alikamatwa tena.

“Tunawasubiria warudi tena mahakamani. Wakirudi tutaomba huyo JPM aliyeudhika na maneno ya Wilson aje atoe ushahidi wa kipi kilichomuudhi,” amesema Lissu

Tokea Ametua Ubelgiji, Takwimu Zinaonyesha Samatta Ni Hatari Zaidi Dakika 20 Za Mwisho

$
0
0
Mshambuliaji Mbwana Samatta akiwa na timu yake ya KRC Genk amefikisha mabao sita ukijumlisha yale ya Ligi Kuu ya Ubeligiji pamoja na mechi za Europa.

Katika mabao hayo sita, mawili ni ya Europa na manne ni ya ligi lakini inaonekan Samatta ni hatari zaidi katika dakika za mwisho.

Kwani katika mabao hayo sita, ni bao moja tu dhidi ya Oostende katika mechi iliyochezwa Julai 31, ndiyo alifunga katika dakika ya 10.

Lakini mabao mengine yote, amefunga kuanzia dakika ya 73 hadi 80, hali inayoonyesha kuwa kila dakika 20 za mwisho, ni mtu wa kuchungwa kweli.

Mabao aliyofunga katika mechi za Europa ni dhidi ya NK Lokomotiva, alifunga katika dakika ya 83 na mechi ikaisha kwa sare ya mabao 2-2. Mechi ya pili dhidi ya timu hiyo, akafunga pia katika dakika ya 80.

Wanaume Siku Hizi Mbona Mnalia lia Sana Kuchunwa?

$
0
0
Hata maandiko matakatifu yameandikwa mwanaume utahangaika juani ili umlishe mkeo na mwanamke atazaa kwa uchungu, sasa imekua siku hizi wanaume kumhudumia mwanamke imekua ni kulia lia sana mwanaume wa ukweli anatakiwa ajue mpenzi wake au mke anamhudumia vipi.

Hivi mnadhani nyie wavulana unakua hujaoa una mpenzi tu unataka aishi vipi unakuta unatoa vielfu 50 unalalamkika mpaka povu linakutoka unataka kumiliki msichana mrembo mzuri huku unatoa kihamsini unalalamika sana starehe gharama ukiona vyapendeza ujue vimegharamiwa.

Ebu kueni wastaarabu basi kutwa kulia lia humu JF, mnawadhalilisha sana kina dada anakuja kwako kajigharamia mwenyewe mapouda nini unamgaragaza unamtindua wewe ukimpa kihamsini unalalamikaaaaaa sasa unatakaje?

Acheni hizo basi ukimtoa out akija na rafiki yake wakinywa savana tu mnalia sasa mnataka wanywe viroba? Au safari?

Jinsi ya Kumlinda Mumeo Asichepuke

$
0
0
Wanawake wengi hawajui nafasi ya mume, hivyo kufanya mambo kiholela na kujikuta NDOA inaanza kuleta matatzo.

Jinsi ya kumlinda mumeo:

1. MAPISHI
Unapokua upo jikoni unaandaa chakula, ni lazima ujue kuwa anaekula ni mumeo, hivyo ni vizuri ukatumia ujuzi wako wote kuhakikisha mumeo anakula chakula kizuri. Wanawake wanapika chakula kizuri siku za sikukuu ndo anajitahidi kutumia uelewa wake wote katika kupika ili tu aonekane na majirani.
Au siku ukisikia mumeo anakuja na mgeni rafki yake alafu yamkini ni mtu mwenye cheo fulani ndo unataka upike vizuri.
KWA IYO USITAKE KUPIKA VIZURI ETI KWA SABABU KUNA MGENI AMEKUTEMBELEA BALI IWE NDO TABIA YAKO KWA MUMEO

2. USAFI
Wanawake bado hawajajua kuwa usafi ni kivutio pia kikubwa kwa mwanamume. Na kama tunavyojua kuwa usafi maana yake ni "kila kitu mahali pake"
Sasa wanawake utakuta vijiko vya chakula vipo kwenye kitanda eti kwa sababu tu ana mtoto mdogo. Au nguo za mikojo ya mtoto unaweka chini ya kitanda mpaka zinaanza kutoa harufu. USAFI NI MUHIMU SANA, IWE KWAKO MKE, AU MAZINGIRA YA NYUMBA. NA HAPA SIMAANISHI KUWA MSAFI KWA MAANA YA KUJIPODOA.

3. MANENO MAZURI
Mke ni lazma ujue maneno ya kuongea na mumeo. Maneno mazuri yatamlinda mumeo pale atakapoyasikia kwa wengine. NA HATA KAMA MUMEO HATAONYESHA KUJALI, BADO WEWE MKE UNATAKIWA KUENDELEA KUKAA KWNYE HIYO NAFASI.

Mungu akusaidie ewe mke kuitumia nafasi yako.

Mama Diamond Amtumia Salama za Birthday Wema Sepetu...Zari Alinyimwa.....Kunani?

$
0
0
September 28, 2016 ni siku ambayo anazaliwa mrembo na mwigizaji wa Filamu, Wema Sepetu ambapo pamoja na watu wengi kumtakia kila la kheri  yupo pia Mama mzazi wa Diamond Platnumz ambaye kwenye akaunti yake ya Instagram amepost picha ya Mama yake Diamond akaisindikizia na maneno haya ..

Happy birthday.. Mamy akee @wemasepetu mungu akuongezee umri na akujali kheri akufungulie Mlango wa baraka kwa kila uliombalo.Amin😘😘 👑🎉

Kupatwa Kwa Mrembo Huddah: Azama Kimapenzi Kwa Mchagga!

$
0
0
Haya jamani yule Sosholaiti wa Kenya kazama kwa Mchaga wa Kishumundu (Sina uhakika). Kaka huyo ajulikanaye kama Danford Kessy amemteka mrembo huyo ambaye amekiri kuwa ni muda mrefu amekuwa akijilinda lakini sasa amefika bei kwa Mkaka huyo Handsome
Tazama Picha ya mwanaume huyo hapa:


Agness Masogange Aamua Kupima Ukimwi na Kutuonyesha Kukata Mzizi wa Fitina

$
0
0
Baada ya Mrembo Tunda kuanika Majibu yake ya Ngoma tukayaona...Agnes Masogange nayeye awafunga midomo walikuwa wakimsema ana Ugonjwa...Aanika wazi majibu yake. .imethibishwa kuwa Hana HIV...je ukipata nafasi utamshauri nini? ?? Tia neno kwako

Nafasi za Kazi CVPeople Tanzania...Bonyeza Hapa

Mahakama yakana kuitambua kampuni iliyotumiwa na NHC kumtimua Mbowe

$
0
0
Mahakama Kuu imekana kuitambua kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyohusika kuondoa vitu vya kampuni za Freeman Mbowe kwenye jengo la Shirika la Taifa la Nyumba (NHC).

Hayo yalibainishwa jana na kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema, Peter Kibatala wakati wa usikilizwaji wa maombi yaliyofunguliwa na mlalamikaji huyo kupitia kampuni ya Mbowe Hotels Ltd dhidi ya NHC na kampuni hiyo ya udalali.

Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo jana, pamoja na mambo mengine Mbowe aliiomba Mahakama iliamuru NHC na kampuni hiyo wamrejeshe katika jengo hilo pamoja na vifaa na mali zake zinazoshikiliwa na kampuni hiyo.

Wakili Kibatala aliieleza Mahakama kuwa mteja wake aliondolewa katika jengo hilo kinyume na sheria.

Alidai dalali aliyetumiwa na NHC kuziondoa kampuni za Mbowe katika jengo hilo hajasajiliwa na Mahakama kwa kuwa walimwandikia Msajili wa Mahakama barua kujua kama anatambulika, lakini alijibu kuwa haimtambui.

Kutokana na majibu ya msajilihuyo kupitia barua yake ambayo wameiwasilisha mahakamani kama kielelezo, Kibatala alidai sheria na mchakato mzima uliotumika vilikuwa ni batili.

Mawakili wa NHC, Ipilinga Panya na Aloyce Sekule walidai shirika hilo kabla ya kumtimua Mbowe lilimwandikia notisi ya siku 30 iliyokwisha kisha akaongezewa siku 30 zingine kama sheria inavyotaka ambazo ziliisha na kumpa tena siku 14, lakini hakulipa deni.

Wakili wa kampuni ya Foster Auctioneers and General Traders, Aliko Mwamanenge alidai madai ya kuwa mteja wake ni dalali wa Baraza la Usuluhishi na kwamba anayesajiliwa kama dalali ni mtu binafsi na siyo kampuni, hayana ukweli kwani upande wa mlalamikaji ulipoandika barua kuulizia uhalali wake ulipaswa kuuliza jina la mmiliki kampuni hiyo.

Hata hivyo, wakili wa mlalamikaji Kibatala alidai notisi zinazodaiwa kuandikwa na NHC zilipelekwa mahali pasipohusika kwa kampuni ya Free Media badala ya Mbowe Hotels ambayo ina mkataba na NHC. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Sivangilwa Mwangesi anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha hadi Oktoba 18, mwaka huu atakapotoa uamuzi wa maombi hayo ya mlalamikaji.

Septemba Mosi, wafanyakazi wa kampuni ya udalali ya Foster Auctioneers and General Traders walifika kwenye ofisi za kampuni ya Free Media na kuondoka vifaa mbalimbali vya kazi, zikiwamo kompyuta na viti kwa madai kwamba mmiliki wake, Mbowe anadaiwa na NHC fedha nyingi za kodi ya pango.

HALI ya afya ya Spika mstaafu, Samuel Sitta si nzuri..Apelekwa Nchini Ujerumani

$
0
0
HALI ya afya ya Spika mstaafu, Samuel Sitta si nzuri,baada ya Serikali kumpeleka nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi.

Habari za uhakika  zinasema Sitta alipelekwa Ujerumani juzi kwa matibabu baada ya afya yake kubadilika ghafla.

“Nilimtembelea siku moja kabla ya kupelekwa nje ya nchi, kwa kweli hali ya afya yake ilikuwa imedhoofu, namwombea Mungu amsaidia apone haraka ili arudi kuendelea na majukumu yake.

“Nimesikitishwa mno na taarifa za kuzushiwa kifo mzee wangu huyu, Mungu ni mwema najua bado anampigania uhai wake…hii tabia ya mitandao ya kijamii kumzushia mtu kifo sijui inafaidika nini.

“Mpaka anaondoka nchini kwenda matibabu natambua amekuwa asikumbuliwa mno na tatizo la miguu, sasa mimi si daktari wake siwezi kuongeza zaidi,”kilisema chanzo chetu.

Septemba 19, mwaka huu, Rais Dk. John Magufuli alimtembelea Sitta hospitalini alikolazwa kwa muda sasa kumjulia hali, kisha kumwombea dua Mungu amsaidie.

Siku iliyofuata Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa naye alimtembelea hospitalini kumjulia hali.

Sitta ameshika  nyadhifa mbalimbali, zikiwamo za Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, uwaziri na ubunge kwa kipindi kirefu.

Chidi alikuwa apelekwe Ulaya kwenye matibabu kama angemaliza muda wa matibabu Sober House – Kalapina

$
0
0
Rapper Kalapina mmoja kati ya wadau ambao walimsaidia Chidi Benz kumpeleka Sober House amefunguka kwa kusema kuwa kitendo cha Chidi Benz kukatisha muda wa matibabu akiwa Sober House kumemkosesha vitu vingi pamoja na kupelekwa Ulaya kwa ajili ya matibabu.

Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Jumanne hii, Kalapina amesema Chid Benz alikuwa hajapata matibabu sahihi alipotoka ‘sober house’.

“Chid Benz hakumaliza muda wa matibabu alivyotoka ‘sober house’ ndani ya siku 28, kwahiyo mi namuomba afikirie faida alizozipata sober na faida anazozipata sasa hivi akiwa mtaani, nafasi bado ipo kwake kwa sababu tumeplay part kubwa hadi Chid Benz akae sawa, kwa hiyo anatakiwa atusikilize, nafasi ipo kubwa kwa Chid Benz kuweza kujisahihisha”, alisema Kalapina.

Kalapina amesema Chidi Benz alipata wafadhili wa kumpeleka nchi za nje kwa matibabu zaidi, lakini ikashindikana kutokana na kitendo hicho.

“Kulikuwa kuna safari ya yeye na Ray C kupelekwa Ulaya, wafadhili walikuwa wanataka kuwapeleka Ulaya kwa matibabu zaidi, lakini ilitakiwa subira kidogo, ndani ya siku 28 yeye amechoka kukaa sober anataka kukaa mtaani, sasa wafadhili wakishaona uko mtaani tena ku’invest hela yao inakuwa ngumu wanaona bado hujapona”, alisema Kalapina

Prof. Lipumba: Sing'oki ng'o. Mimi ni Mwenyekiti halali CUF, Kikao kilichonivua uanachama ni batili

$
0
0
Katika mahojiano na sauti ya Amerika VOA Swahili jana jioni, Mwenyekiti aliyejiuzulu wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa yeye bado ni Mwenyekiti halali na kikao kilichomvua uanachama ni batili.

Akihojiwa na mwandishi wa habari mahiri Sunday Shomari, Mwenyekiti huyo aliyejiuzulu amesisitiza kuwa yeye bado ni mwenyekiti halali kwa mujibu wa katiba ya CUF na kikao kilichoongozwa na Mhe. Katani huko Unguja ni batili na yeye anaendelea na shughuli za kichama kama kawaida.


Wema Sepetu Awashukuru Waliomtumia Salamu za Birthday

$
0
0
Jumatano hii ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya staa wa filamu Wema Sepetu ambao ndugu, jamaa pamoja na marafiki walimtakia heri na mafanikio mrembo huyo.

Moja kati ya vitu ambavyo vilileta gumzo kwenye mitandao ya kijamii ni baada ya mama Diamond kum-wish malkia huyo wa filamu huku akimkaushia Zari ambaye ni mama watoto wa Diamond.

Pia dada zake na Diamond walim-wish maklia huyo.

Baada ya kupokea salamu za watu mbalimbali kutoka katika kila kona ya dunia malkia huyo wa filamu na yeye aliamua kuwashurudu huku akionyesha kile ambacho hakukitarajia.

Wema kupitia istagram aliandika:
Wow… wow… wow… daah.. sijui cha kuandika.. am just out of words… Wema mimi nitamlipa nini Mungu kwa Neema na Baraka zake anazonijalia kila siku…?? Napenda kutoa shukrani zangu za Dhati kwa mumumu wangu, My family, my management, teamkazi wale kwa kufungua dimba last Night with that amazing suprise… alafu sasa huku insta, snapchat, twitter and kila site ambazo mmepost about My birthday nashindwa cha kusema.. toka nimeamka najitahidi kujibu kila post ninazoziona.. ila zinanielemea… ila ninajitahidi, nitajitahidi na nitahakikisha najibu Kila ambayo nakutana nayo… ila Daaah You Guys mnajua kupenda.. mpaka najiogopa kwa mapenzi mnayonipa.. what should i say?? Wakwe vepe?? Mawifi je?? Wake wenza nao ndani? Boyfriends🙈🙈 nacheka peke yangu….. And sometyms hadi machozi ya furaha yananitoka… Nimekuwa Cry baby wa kujitegemea tokea saa sita usiku…. Na nadhani zoezi litaendelea mpaka siku hii iishe…. Nawapenda jamani… #AmaBeBack


Nini Kimemkuta Mwanamuziki Ommy Dimpoz?

$
0
0
Wanaukumbi kwema,

Leo naombeni mnijuze nini kimemkuta mwanamuziki Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz ambaye kuna kipindi tuliaminishwa kuwa atakuja kumzidi kama sio kumfunika na kumpoteza kabisa Diamond.

Ikumbukwe Ommy Dimpoz alianza vizuri kwa kutoa vibao matata kama Nainai, Baadae, Tupogo na Ndangushima. Baada ya hapo ametoa nyimbo zilizoshindwa kutamba kabisa...mfano mzuri ni Wanjera. Kwasasa dimpoz amepotea na kafunikwa na vijana wadogo akina Rayvan na Harmonize, Je ni nini kimemsibu staa huyu aliyekuwa anafananishwa na Diamond kwa uwezo wake Kimuziki?

Chris Brown jukwaa moja na Alikiba Mombasa Kenya

$
0
0
Baada ya kuwa msanii Pekee kutoka East Africa kuingia kwenye Nomination za MTVEMA International. Na Baada ya kumfunika Diamond Kule Mombasa. Alikiba ameitwa Tena, Safari hii akiwa na Msanii Mwenye Utukutu mkubwa lakini akiwa kipenzi cha wadada Duniani kote, Mmarekani Chriss Brown. Wakati Chris Brown akithibitisha kwenye clip ya video inayosambaa kwenye mitandao tangu jana kuwa Tamasha hilo litafanyika Katika Jiji la Mombasa Tarehe 8 OCtober 2016.

Mwanamuziki wa Bongo Fleva apandishwa kizimbani kwa kuimba wimbo wa kichochezi

$
0
0
Mwanamuziki wa Bongo Fleva Fulgency Mapunda maarufu Mwana Cotide amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kwa tuhuma za kuimba na kusambaza wimbo wenye maudhui ya kichochezi.

Mwana Cotide ameiamba wimbo wenye jina “Dikteta Uchwara” ambao aliusambaza kupitia mtandao wa YouTube kitu ambacho kinavunja sheria ya makosa ya mitandao

Diva:Mastaa wa Bongo Waelewe Thamani yao, Mimi Nachaji Milioni 3.5 Kwa Appearance tu

$
0
0
Mtangazaji wa Clouds FM, Diva The Bawse amewataka mastaa wa Tanzania kutambua thamani ya brand zao na kuacha kujichukulia poa.


Amedai kuwa mastaa wengi wamekuwa wakitumika bure kufaidisha watu wengine na anadhani ni muhimu wakaacha kujishusha kiasi hicho.

Anadai kwa upande wake yeye, hafanyi kitu bure na kudai kuwa hata kuonekana kwenye saa moja kwenye party ya mtu, ni lazima awe amemlipa.

“My standard rate is 3.5 million in one night that including 30 minutes hosting, na sikai less than hour naondoka,” Diva ameandika kwenye blog yake.

“Ifike stage celebs wajue value yao na sio kutumika tu kwa faida ya watu wengine. Chochote unaona pia napost kwenye account zangu za mitandao kinalipiwa., lazima ujue kama wewe ni maarufu lazima ulipwe hata kutweet brand ya mtu mwingine,” ameongeza.

Mtangazaji huyo ana zaidi ya followers milioni 1.1 kwenye Instagram na amekuwa akiingiza mkwanja mrefu kwa kupost matangazo mbalimbali.

Nuh Mziwanda Azinguana na Uongozi Wake, Adai Viongozi Wanataka Umaarufu Kuliko Kazi

$
0
0
Mkali wa wimbo ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda amezinguana na uongozi wake ambao alikuwa anafanya nao kazi kwa madai umeshindwa kufanya kazi aliyoitaka.

Mapema mwaka huu Petit Man alimchukua msanii huyo na kuamua kumsimamia ikiwa ni wiki chache toka aachane na wasanii wa Endless Fame ya Wema Sepetu.

Nuh amedai yeye ni msanii mkubwa na meneja huyo ameshindwa kumfikisha pale ambapo alikuwa anataka kwenda.

“Nimetoka kule kwa ajili tu ya sababu zangu binafsi inabidi ni’move on, mi sio msanii mdogo inabidi niwe na meneja ambaye anajielewa na anajua msanii ambaye ninaye ni msanii ambaye yupo katika level gani, kama meneja anashindwa kujua msanii ambaye anafanya naye kazi siwezi kudeal naye, kwa sababu nilishapotezaga time katika muziki three years kwenye mapenzi, sa siwezi kupoteza mwezi mmoja kwa mtu ambaye kanikuta tu nimeamua kufanya naye kazi, kwa hiyo ni bullshit mi naachana naye naendelea na mambo yangu mengine”, Nuh Mziwanda alikiambia kipindi cha Planet bongo cha EA Radio.

Aliongeza, “Siyo kwa ubaya kwa uzuri, niliamua kufanya naye kazi, lakini kashindwa kupresent kile kitu ambacho mi nilikihitaji, narudia tena mi ni msanii mkubwa, inabidi ajue msanii mkubwa inabidi awe na nini na nini, kuna vitu avijue kama meneja, sasa kufanya kazi na meneja ambaye na yeye anataka ustar, ni kitu ambacho hakiwezekani”, alisema Nuh Mziwanda.

Nuh Mziwanda pia alisema anaamini jitihada zake ndizo zimemfikisha hapo alipo, na kukanusha kauli ambayo watu wengi wamesema kuwa kwa kuwa sasa ana studio, amekuwa na dharau kwa uongozi wake.


Viewing all 104657 articles
Browse latest View live




Latest Images