Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Mbwana Samatta Kuitoa Kimasomaso Genk leo

$
0
0
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta leo ataiongoza timu yake ya KRC Genk kusaka ushindi dhidi ya US Sassuolo ya Italia katika  Kundi F la mashindano ya Ligi ya Europa.

Genk itakuwa nyumbani kuwakaribisha Waitaliano  hao, Sassuolo ambao katika mchezo wao wa kwanza walifungwa na Athletic Club Bilbao ya Hispania, hivyo kufanya mchezo huo kuwa na umuhimu wa pekee kwa timu zote leo saa 4:05 usiku.

Samatta katika mchezo uliopita alishindwa kufurukuta kabla ya kutolewa kutokana na kuumia walipopokea kipigo kutoka kwa SK Rapid vienna ya Austria  inayocheza dhidi ya mabingwa wa zamani wa mashindano hayo, Athletico Bilbao.

Samatta ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alianzia benchi na kuingia dakika 70, alitengeneza bao la kufutia machozi la Genk lililofungwa na Leandro Trossard. Walichapwa 4-1 na  KV Kortrijk ukiwa ni mchezo wa pili mfululizo wakipoteza kwenye Ligi Kuu ya Ubelgiji.

Manchester United yenye nyota wengi akiwamo Paul Pogba iliyoanza  vibaya kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Feyenoord ya Uholanzi itakuwa nyumbani, Old Trafford kuwakaribisha Zorya Luhansk, wakati Ajax ya Uholanzi ikiivaa Standard Liege ya Ubelgiji na Sparta Prague ya Czech itakuwa wenyeji wa Inter Milan ya Italia.























Habari

Makonda Awaponda Wanaobeza Jitihada za Rais Magufuli, ‘Hawajui Wanalolitaka’

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemmwagia sifa Rais John Magufuli kwa utendaji wake na kusema yeye ni mtu wa kutenda na sio maneno huku akiwapa vidonge vya wale wanaobeza jitihada zake.

Makonda ametoa kauli hiyo Jumatano hii kwenye uzinduzi wa ndege mpya za ATCL kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Mheshimiwa Rais naomba uendelee kutenda, sisi tumegawanyika kwenye upande wa fikra,kuna watu ambao hawajui wanachokitaka na hata ukiwafanyie yale ambayo ulifikiriA wao wanayataka kumbe sio,” alisema Makonda.

“Ikumbukwe wakati wa bunge tulikuwa tunafuatilia kusikiliza, Tanzania haina ndege tumezidiwa katika nchi za Rwanda tumezidiwa na wapi, umenunua ndege wanaanza kusema ndege zenyewe hazijang’aa, wamekuja kuzioshea airport, hawajui nini wanachokitaka. Hao hao walipiga kelele tunataka elimu bure,angalau na wananchi wa hali ya chini wapate elimu bure, wameanza kusema elimu yenyewe bure wakati majengo yanadondoka! Kwahiyo hawajui wanalolitaka. Hawa hawa wana lalamika foleni Dar es Salaam, umeamua kutujengea barabara hizo hela za barabara ingeenda kwenye chakula tunakufa na njaa, mheshimiwa rais hawajui wanalolitaka,” alieleza.

“Sisi tunaojua tunalolitaka tupo pamoja na wewe, tunakuunga mkono usiku na mchana na tutaendelea kukuunga mkono usiku na mchana na ninaamini kwamba wanasiasa wengi wanasubiri kutimiza ahadi zao katikati au mwishoni mwa kuelekea kampeni wewe hujasubiri, uliahidi ndege mwaka jana leo hata mwaka hujamaliza ndege zimeingia, wewe ni mtendaji ambaye tutaendelea kukuombea,” alisisitiza.

Future Kutumbuiza Kwenye MTV MAMA Pamoja na Diamond na Alikiba

$
0
0
Rapper wa Marekani, Future, ametangazwa kuwa msanii wa nje ya Afrika atakayetumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA, Oktoba 22.

Future ataungana na Alikiba na Diamond na wasanii wengine wa Afrika kwenye orodha ya wale watakaotumbuiza jioni hiyo jijini Johannesburg.

“We are proud to announce that @1future will be joining for the #MTVMAMA2016!!! #FutureMTVMAMA,” wameandika MTV Base kwenye Twitter.

Rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Nayvadius DeMun Wilburn ana album nne hadi sasa, Pluto (2012), Honest (2014), DS2 (2015) na EVOL (2016).

Hacker Achukua Account ya Instagram ya Mwanamuziki Chege..Ampiga Mkwala wa Nguvu na Kumpa Masharti Haya

$
0
0
Account ya Chege Chigunda imehakiwa na Hacker leo na Hacker huyo ametoa msimamo wake kama alivyoandika kupitia Instagram Account hiyo ya Chege :

#Regrann from #chegechigunda - Baada ya maisha kuwa magumu na Serikali kutogawa ajira kazi tu kunyakunyaku wafanyakazi serikalini bila kujua wanaenda kuwa watu wa aina gani mitaani, basi vijana wachawi weusi kama mm acha ile ya mzungu mchawi, tumeamua kujiajiri nakutumia elimu zetu kuhack account ili tu kujiingizia kipato. Maana nimesomea IT Serikali aitaki kunipa ajira ikidai bado inachomoa wafanyakazi fake! Sasa mnataka nibaki mtaani niibe live live? Hapana mm siibi live maana nikichosomea ni behind the scenes. Hahaha. Afu Serikali imeajiri mijitu ambayo haijui ata nn maana ya LOG OUT ipo tu pale TCRA. Mm naamini zile ajira tukipewa sisi vijana wachawi na wamiliki wa mitandao, hakuna mtu atalia kuwa amehackiwa account labda kama password atakuwa anashare na marafiki. Aya cut the Bullshit. Kaka Chege mm nishabiki yako mkubwa sana ila nimechukua I account sababu wewe unavimba sana siku izi mamae. Kitu kidogo tu unavimba wakati unajua kila mtu na cheo chake kwenye I dunia. Sasa ujifunze kwanzia leo sio kila mtu wakumchukulia poa kisa wewe ni Star. Eshimu kila mtu sio umuheshimu mkubwa fela tu. Sasa skia, mm nakupa account yako baada ya masaa ma3 yakufanya matangazo apa na wananchi wangu wasaka tonge kama mm na ww. Yakitimia masaa ma3 nitamtumia mkubwa fella PASSWORD ya I account kwenye DM yake. Afu wewe msanii mkubwa bwana unakosaje hata kuwa na IT master katika team yako? Sasa naanza kupata mwanga kwann DIAMOND PLATNUMZ CHIBU SIMBAAAAAAAA anawakimbiza sana. Jamaa team yake imekamilika sana afu pia avimbi. Angelikuwa anavimba ningeshachukua account yake mapema. Maana mm huwa sihack nachukua kama yangu. Kwaiyo tuliza Pumbu zako baba baada ya masaa ma 3 nakupa account yako iyo yote ni kwasababau napenda muziki wako. Ila acha kunivimbia. Pia uwe unaweka account security bana. OK ndugu zanguni followers wa chege LETENI MATANGAZO DM KWANZIA SASA nina masaa ma3 yakujidai umu Kiroho safi. Na baba chege mzee wa acha waoane. Skia, nikiona mtu anataka kama kuirudisha I account ndani ya masaa aya ma3, AKIYANANI NITAIFUTA I ACCOUNT, NA KUMBUKA NIKISHADELETE HAKUNA FALA ANAWEZA IRUDISHA I ACCOUNT TENA. so be a mother faking Good boy.

UTAFITI Twaweza: Nchi Haiongozwi Kidikteta Kama Inavyodaiwa

$
0
0
Ripoti ya utafiti mpya wa taasisi ya Twaweza uliozinduliwa leo jijini hapa unaeleza kuwa Watanzania wengi hawaoni kama nchi inaendeshwa kidikteta baada ya mtu mmoja kati ya 10 waliohojiwa kueleza nchi inaongozwa kwa mfumo huo.

Matokeo ya utafiti huo uliofanywa kwa njia ya simu kati ya Septemba 24-29 mwaka yanasema kuwa watu sita kati ya 10 sawa na asilimia 58 walipinga kuwa nchi inaongozwa kidikteta huku asilimia 31 wakieleza kutokuwa na uhakika.

Katika utafiti huo unaoitwa "Demokrasia, udikteta na maandamano: wananchi wanasemaje", mwananchi mmoja kati ya watatu alitafsiri udikteta kuwa ni kitendo cha Serikali kutumia nguvu  wakati wa kuitawala nchi.

Licha ya wananchi wengi kueleza hawaoni nchi ikiongozwa kidikteta, ripoti hiyo iliyohoji watu 1,602 wa Tanzania Bara inaeleza kuwa wananchi saba kati ya 10 wanaunga mkono demokrasia kama mfumo bora wa Serikali, mtazamo ambao unaoshabihiana na wafuasi wa vyama mbalimbali nchini.

Sanjari na kuhoji masuala mbalimbali namna ya uendeshwaji wa nchi, Twaweza walihoji watu pia ufuasi wao kwa vyama vya siasa ambapo asilimia 66 walieleza kuwa karibu na CCM huku asilimia 19 wakiwa karibu na upinzani hususan Chadema. Watu wawili kati ya 10 (asilimia 15) walisema hawana ukaribu na chama chochote.                      

PROF. Tibaijuka Akataa Kupokea Shilingi 200 Millioni

$
0
0
Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anne Tibaijuka amesema amepata tuzo nchini Marekani ikiwa ni kuthamini mchango wake akiwa Umoja wa Mataifa lakini akakataa kuchukua fedha dola 100,000( zaidi ya Sh 200 milioni) ambazo huambatana na tuzo hiyo.

Alisema alikataa kupokea fedha hizo kwa sababu maadili ya nchi yetu hayaruhusu kupokea zawadi kama hiyo.

Alisema lakini aliwaeleza kwamba katika mkoa anakotoka kumetokea tetemeko la ardhi na kuna maafa.

Alisema wao wataamua cha kufanya lakini yeye binafsi amekataa kupokea fedha hizo.

Chadema Kuahirisha Tena Operation Ukuta?

$
0
0
KESHO Ijumaa ya tarehe 30 Septemba, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), huenda kikatangaza kuahirisha tena uzinduzi wa operesheni iliyobatizwa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta)

Uzinduzi wa operesheni Ukuta, ulitangazwa tarehe 27 Julai mwaka huu na kwamba ungefanyika mnamo Septemba Mosi, mwaka huu hata hivyo uliahirishwa siku moja kabla ya kufanyika kwake kutokana na kile kilichoitwa, ‘ombi la viongozi wa dini’.
“Tunatangaza kuahirisha mikutano na maandamano ya Ukuta kwa kuwa viongozi wa dini, wametuomba tuwape angalau wiki tatu ili wafanye mazungumzo na Rais John Magufuli ili kutafuta suluhu ya suala hili na kama ikishindikana basi tutaifanya Oktoba mosi mwaka huu,” alisema Freeman Mbowe Agosti 31, mwaka huu.

Mbowe ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni.
Hata hivyo, wiki iliyopita Salum Mwalimu, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, alipoulizwa  kuhusu uzinduzi wa operesheni hiyo hasa ikizingatiwa kuwa zimebaki siku chache kabla ya Oktoba Mosi, alijibu kuwa, “Ukuta siyo tarehe.”

“Ukuta ni fikra zinazoishi ndani ya mioyo ya watu na zitaendelea kuishi. Suala siyo kubaki kwa siku tano au kumi. Tunasubiri tupate mrejesho kutoka kwa viongozi wa dini halafu tutafanya uamuzi juu ya suala hilo,” alisema.

Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, ametoa taarifa jioni ya leo akisema, chama hicho kitatoa tamko juu ya suala hilo siku ya kesho.

“Taarifa rasmi kuhusu Ukuta na hatima ya siku ya maandamano na mikutano nchi nzima iliyotangazwa na chama, itatolewa kesho Ijumaa, Septemba 30, 2016, saa 5:00 asubuhi, mzungumzaji mkuu atakuwa ni Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama Taifa,” amesema Makene.

Dalili za awali zinaonyesha kuwa, Chadema inaweza kuahirisha tena kufanyika kwa uzinduzi wa operesheni hiyo kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo kuchelewa kupata majibu ya viongozi wa dini juu ya jaribio lao la kuonana na Rais John Magufuli ili kutafuta suluhu.

Taarifa zaidi zinadai kuwa, mpaka sasa jaribio la viongozi wa dini kuonana na Rais Magufuli na kujadili suala la kuruhusu kufanyika kwa mikutano na maandamano nchi nzima limegonga mwamba.
Pia chama hicho kinaonekana kutofanya maandalizi yoyote ya msingi kulinganisha na joto la maandalizi lililokuwepo kuelekea uzinduzi wa operesheni hiyo Septemba Mosi mwaka huu kabla ya kuahirisha.

Itakumbukwa kuwa, wiki mbili zilizopita, gazeti moja la kila siku liliripoti kuwa Rais Magufuli amekataa kuonana na viongozi wa dini ili kuzungumzia suala la Ukuta.

Habari ya gazeti hilo ilikuwa na kichwa cha habari, “Rais Magufuli awatosa viongozi wa dini.”
Vuguvugu la uzinduzi wa operesheni Ukuta mwezi uliopita, lilisababisha jumla ya wanachama na viongozi wa Chadema 230 kukamatwa na Jeshi la Polisi katika maeneo mbalimbali hapa nchini na wengine 28 kushikiliwa mahabusu mpaka tarehe 1 Septemba ilipopita

ATOLEWA Macho na Mwizi Anayejiita Scorpion Maeneo ya Buguruni

$
0
0
Kuna jamaa anajulikana kwa jina la Scorpion anakaa maeneo ya Buguruni huyo jamaa inasemekana ameshafanya matukio mengi sana ya kuwaibia watu na kuwaua huku akiwatoa macho.

Jamaa hilo likatili lisilo na chembe ya huruma amefanya tukio lingine ambapo amempiga visu kaka wa watu na baada ya hapo akamtoa macho yote mawili.

Akielezea kwa uchungu tukio hilo mwanaume aliyefanyiwa tukio hilo mkazi wa tabata Makuburi anasema alikuwa akitokea kazini kwake mida ya saa nne usiku ndipo akashukia maeneo ya buguruni sheli na kwenda katika vibanda vya kuku akawa ananunua ndipo alipotokea jamaa huyo  na kumwambia kuwa anashida aalipomuuliza shida yake jamaa huyo hakujibu chochote na baada ya hapo alianza kumjeruhi kwa kumpiga visu mgongoni na tumboni.


Alijaribu kupiga kelele za kuomba msaada lakini hakuna mtu yoyote aliyesogea kumsaidia japo kulikuwa kumejaa watu wengi barabarani hapo.Hakuishia hapo baada ya kumchoma visu mgongoni na tumboni alimsogeza barabarani kisha akamchoma visu machoni na kumtoa macho huku watu wakishuhudia tukio lote.

Hakutetewa na mtu yoyote kwa sababu watu wanamuogopa ameshafanya matukio mengi kama hayo na mtu anabojaribu kuingilia kibao kinamgeukia.



Akiongea na Geha.. Kaka aliyetolewa Macho akielezea kwa uchungu

Mimi nina ofisi yangu iko tabata  nilifunga saa nne nikaona gari zinachelewa ikapita bajaji ikasimama nikapanda ikaenda kuniacha buguruni sheli,Wakati naenda kituoni nikaenda kununua kuku barabarani kwa ajili ya mboga ya nyumbani…

Nikasimama nachagua kuku nikatoa hela kabla hajanirudishia chechi akatokea jamaa huyo mwizi akaniambia “ninashida kaka” nikamwambia “ongea shida yako mana ninaharaka nikitoka hapa nawahi nyumbani” akawa hajasema chochote nikasema huyu mtu kama ni mwizi lakini hapa mbele za watu hatoniibia na mawazo yangu ataniomba hela nitamwambia ale anachotaka nimpe hela niondoke zangu yani hata sijapewa chenchi na muuza kuku nikaanza kupigwa visu vya mgongo wauza kuku wapo hapo hapo watu wako hapohapo hakuna hata mmoja aliyetoa kauli,tena napiga kelele jamani nisaidieni mwizi nikapigwa visu vya tumboni huku anakata nikajaribu nimshike akanin’gata nikapiga sana kelele jamani mwizi ananiua yani wala sisikii kauli zao zaidi ya yule mwizi akisema “yani hapa hakuna mtu atakaye kusaidia”

Baada ya hapo nikapoteza fahamu akanisogeza pembeni akanichoma visu kwenye macho  akaondoka watu wanashuhudia tena nasikia kuna wengine walichukua video,akanivuta barabarani ili nigongwe na gari sasa gari zikawa zinanipisha,kuna watu madereva wa pikipiki walikuwa wanaona,

Yani hapa mimi sioni kitu ambacho naumia sana sasahivi rafiki yangu anakuja naongea nae lakini simuoni mzazi wangu simuoni…

Kuna msamaria mwema alikuja akaniambia anataka kunisaidia nikamwambia anipeleke nyumbani akaniambia hapana wewe umeumia akanipeleka polisi buguruni nikachukua PF3  akanipeleka hospitali Amana ndipo ndugu zangu wakaja wakanipeleka Muhimbili,Nikafanyiwa operation

Anajulikana Buguruni ni mtu wa ajabu sana,

Nilivyotoka Muhimbili nikaenda CCBRT wakaniambia huyu amekutoa macho sikuridhika pia nikaenda KSMC wameniangalia vizuri macho wakanitoa nyuzi wakasafisha wakaniambia wanauwezo wakuniweka macho  bandia lakini uwezo wakuniwekea macho yakafanya kazi hakuna labda nikajaribu India…

Mimi ningekuwa najua buguruni kuna mauaji wala nisingeendaga lakini nilikuwa sijui,sasahivi ukienda kuulizia kuna mtu anaitwa scorpion buguruni utaambiwa huyo muuaji mbaya sana amenitoa macho..

Nimeumia sana dadadangu kwa sababu nina familia nna watoto  kwa mtu yoyote anayenijua mimi lazima aliesana tangu nimeumia walimkataza hata mama yaangu mzazi asije juzi ndio kaja, muda wote analia anakwambia “yani bira wangenitoa mimi lakini sio wewe mwanangu”

Nikikaa huwa nalia sio mara moja kwa siku ninaposikia sauti ya mtoto nalia rafiki yangu alikuwa ananifwata ofisini leo anakuja kuniona nyumbani,nafikiria huyu mtu kwanini kanifanyia hivi wakati kabla hajanitoa macho kila kitu alikuwa ameshachukua…

Mama Diamond ni Moja ya Walionifanya Niache Kumshabikia Diamond

$
0
0
Wakuu Salaam Sana
Mimi Nilikua shabiki mkubwa wa Diamond Platinums Baada ya uswahili na uanakijiji uliopitiliza wa Mama yake kujianika privacy zao kwenye mitandao ya kijamii na kuonekana familia yake hawajiheshimu nimeacha kumshabikia Mond na nimeshachoma kazi zake zote za kwake nilizonunua , Mliobaki kama mashabiki zake mwelezeni aige mfano hata kwa wasanii wengine wakubwa ambao mama zao hawatukani hovyo kwenye mitandao ya kijamii.

By Arovera

Je, Wivu ni Dalili ya Mapenzi ya Dhati au Roho Mbaya?

$
0
0
Leo nimekutana na huu mjadala mahali ulionifanya nilete hilo swali hapo juu.

Ni hivii, nimekutana na mtu siku za karibuni na kuanzisha urafiki wa kawaida tu. Sasa katika mazungumzo likaja swala la mapenzi na wivu. Mwenzangu anaamini kuwa na wivu sio mapenzi kwa kuwa, wivu ni dalili ya kumnyima mwenzio kupata kile roho inapenda. Kwamba, kwake yeye hata kama ikitokea akaoa, hatomnyima mke wake kutembea na mwanaume mwingine yeyote atayependa. Tena ikibidi atume na video kabisaa ili impe stimu wakati manzi ake analiwa.

Wakuu, je ni kweli wivu ni dalili ya uchoyo? Na kwamba kama unampenda mtu kwa dhati huwezi kuwa mchoyo kwake. Kule uzunguni mume/mke huwa wanapeana nafasi ikitokea mmoja wapo kamtamani mtu mwingine wanakubaliana kuonja. Tuwaeleweje hawa watu? Maana ni binadamu wenzetu.

Nawasilisha hoja kwa majadiliano.

Karibuni

Ukiona Mwanaume Ana Miaka 27 Bado Hajajitegemea Huyu ni Hasara

$
0
0
Sifa ya mwanaume kujituma, kutafuta pesa na kujipanga. Hivi unakuta kijana umri unaenda bado anategemea kwa wazazi msosi ni hotpot family huyu ni hasara.

Kuna mwanaume mpaka anaoa bado yupo kwa wazazi na mke anampeleka hapo hapo kwenye nyumba ya familia, ndiyo hapo ndoa inakua ngumu kwa mawifi na mashemeji na wazazi zinaanza chokochoko kibao. Wanaume wa hivi ni walaini sana, hadi kitandani ni walaini.

Wapo sana wanaume wa hivi ila kiukweli mwanamke anavutiwa na mwanaume mgumu yaani anayejua kuhangaika na kujitegemea. Hawa wanategemea hadi siku ya ndoa wapewe zawadi ya kiwanja, au nyumba na wazazi. Wanataka sofa, kitanda, vyombo vya ndani siku ya harusi.

Shosti ukiona mwanaume wa hivi shituka mapema ni mwanaume Hotpot Family....

Lulu Diva Amdhalilisha Tiffah Wa Diamond

$
0
0
Video queen matata Bongo, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ anadaiwa kumdhalilisha mtoto wa Mbongo Fleva anayefanya vizuri kwa sasa, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Latifa ‘Tiffah’ kwa kumuita mbwa wake jina Shikiki, ambalo pia ni jina jingine la utani la mtoto huyo.


Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, mrembo huyo amemuita mbwa wake huyo jina hilo, kitu ambacho kimetafsiriwa na wengi kama ni kumdhalilisha mtoto huyo wa staa mkubwa Bongo.

“Jamani Diva anatafuta matatizo makubwa na D i a m o n d , kwanini kampa mbwa wake jina kama hilo ambalo pia huwa linatumiwa na Tiffah? Ana hatari sana,” kilisema chanzo chetu.

Gazeti hili lilipomtafuta Lulu na kumuuliza kuhusu ishu hiyo, alisema ni kweli mbwa wake anaitwa Shikiki lakini hakuwa akijua kwamba mtoto wa Diamond, jina lake lingine ni hilo.

“Jamani mimi sikuwa najua kabisa kama Tiffah, jina lake lingine ni hilo, mimi nilimpa tu kama watu w e n g i n e wanavyowapa m a j i n a mbwa wao,” alisema Diva.

Mke wa Mtu Amponza Mwanamuziki Tunda Man

$
0
0
Msanii wa Tip Top Connection, Tunda Man ameshindwa kuachia video ya wimbo wake mpya ‘Mwanaume Suruali’ baada ya kumtumia mke wa mtu kama video queen.

Muimbaji huyo ambaye bado anafanya vizuri na wimbo ‘Mama Kijacho’, ameiambia Bongo5 kuwa ameshindwa kuachia kazi hiyo kutokana na mume wa mwanamke huyo kuzuia video hiyo sitoke.

“Kuna video ya wimbo wangu mpya ‘Mwanaume Suruali’ ambayo ilikuwa itoke hivi karibuni lakini kwa bahati mbaya mume wa video queen ambaye ametumika kwenye video amezuia video isitoke,” alisema Tunda. “Kwa hiyo bado tupo kwenye mazungumzo, kama akiruhusu itoke video itatoka hivi karibuni,”

Akifafanua zaidi kilichotokea Tunda alisema “Mimi nilikuwa nipo Dar nilimwachia mtu kazi Zanzibar ya kutafuta location na mambo mengine, kwa hiyo kwa bahati mbaya au nzuri akampata mwanamke ambaye na mimi nilipenda aonekane kwenye video. Kweli tukafanya naye video na pesa yake akalipwa, lakini mwanamke hakusema kama yeye ni mke wa mtu, kwa hiyo baada video kumalizika zile picha za behind the scene mume wake akaziona ndo akaamua kutushtaki ili video isitoke. Lakini tunashukuru mungu mambo yanaenda vizuri soon mambo yakienda kama yalivyopanga ngoma itatoka,”

UTAFITI Twaweza ‘Wambeba’ Tena Magufuli

$
0
0
RIPOTI ya utafiti mpya wa taasisi ya Twaweza imeeleza kuwa watanzania wengi wanaunga mkono, hatua ya Rais John Magufuli kupiga marufuku mikutano na maandamano ya kisiasa hapa nchini, anaandika Aisha Amran.

Matokeo hayo yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,602 kati ya tarehe 23 na 29 Agosti, mwaka huu kwa njia ya simu. Utafiti huo ulihusisha wananchi wa Tanzania Bara pekee na kwamba watu 6 kati ya 10 wamepinga kuwa nchi inaongozwa kidikteta.

Watu hao ni sawa na asilimia 58, walipinga kuwa nchi inaongozwa kidikteta huku asilimia 31 wakieleza kutokuwa na uhakika juu ya suala hilo.

Katika utafiti huo unaopewa jina la, “Demokrasia, udikteta na maandamano” unaripoti kwamba  asilimia 80 ya watanzania waliohojiwa, wanasema  baada ya uchaguzi, vyama vya upinzani vikubali kushindwa na visaidiane na serikali kuijenga nchi.

Huku asilimia 20 pekee ndiyo wananchi wakisema wapinzani waifuatilie na kuiwajibisha serikali iliyopo madarakani.

Katika hatua nyingine, ripoti hiyo imedaia kuwa asilimia 71 ya wafuasi wa vyama vya upinzani wanaunga mkono kufanyika kwa mikutano huku asilimia 37 ya wafuasi wa chama tawala nao wakiunga mkono kufanyika kwa mikutano ya hadhara.

Aidha ripoti hiyo ya Twaweza inadai kuwa, asilimia 48 ya waliohojiwa juu ya kuanzishwa harakati za Umoja wa Kupinga Udikteta (UKUTA), wanapinga umoja huo huku asilimia 22 pekee wakiunga mkono umoja huo.

Pia asilimia 55 ya wafuasi wa vyama vya upinzani waliohojiwa, wanaunga mkono harakati za umoja huo huku asilimia 44 wakiwa hawaungi mkono na asilimia 6 ya wafuasi wa CCM wanaunga mkono juhudi za Ukuta.

Aidan Eyakuze, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, amesema watanzania wengi wanaunga mkono mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni.

“Hili ni jambo la kuzingatiwa na serikali kwa sasa, wananchi ya hawakubaliani na kauli inayosema kuwa Rais Magufuli ni dikteta, wanasema ili kulinda amani  na kuchochea kasi kubwa ya maendeleo lazima hatua thabiti zichukuliwe,” amesema Eyakuze.

Picha Mpya za Mrembo Lulu Diva...

$
0
0
Upcoming actress, Lulu Diva has shared her amazing pics of herself on Instagram account, Diva lulu who is so beautiful and has nice figure, see her another pics of herself as she shared on her Instagram account;


Ndege Binafsi ya Cristiano Ronaldo Yaanguka, Hakuwemo Ndani

$
0
0
Ndege binafsi ya mchezaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ilianguka wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege wa El Prat jijini Barcelona, Jumatatu. Hakuna majeruhi walioripotiwa.

Kwa mujibu wa ESPN, Ronaldo, aliyekuwa Dortmund kipindi hicho wakati Real Madrid ilikuwa ikijiandaa kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa waliotoka sare ya 2-2 katika hatua ya makundi dhidi ya Borussia Dortmund, hakuwa ndani ya ndege hiyo wakati inaanguka.

Mshambuliaji huyo huikodisha ndege hiyo, Gulfstream G200, aliyoinunua kwa €19m kufanya kazi zingine wakati asipokuwa akiitumia.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Hispania, matairi ya magari hayo yalivunjika wakati ikitua na hivyo kutoka nje ya njia.

Tibaijuka Ahofia ESCROW.....Akataa Zawadi ya Milioni 200

$
0
0
MBUNGE wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM), amepata tuzo ya Umoja wa Mataifa (UN) ikiwa ni mchango wa kuthamini kazi aliyoifanya, huku akikataa kupokea zawadi ya Dola 100, 000 za Marekani, ambazo ni zaidi ya Sh milioni 200.

Profesa Tibaijuka alitoa taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisema tuzo hiyo ya Maendeleo Endelevu ilidhaminiwa na mwana Mfalme wa Bahrain, Khalifa bin Salman Al Khalifa.

Alisema, hatua ya kuzikataa fedha hizo, ni njia ya kukwepa mtego kama uliomkuta mwaka juzi baada ya kupokea fedha za Escrow Sh bilioni 1.6 kutoka kwa mfanyabiashara,  James Rugemalira.

Tuzo hiyo ambayo ni heshima kwa Tanzania, alikabidhiwa Septemba 24, mwaka huu na inajulikana kama ‘His Royal Highness Prince Khalifa bin Salman Al Khalifa Award  for Sustainable Development’.

Profesa Tibaijuka alisema, alikabidhiwa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha maendeleo duniani.

Alisema tuzo  hiyo ya heshima hutolewa kila baada ya miaka miwili na washiriki wakuu huwa ni wale waliowahi kufanya kazi na Shirika la Umoja wa Mataifa.

Mwaka huu, Waziri Mkuu wa Bahrain Khalifa bin Salman ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo, alisema.

“Tuzo hii nimepewa Marekani ikiwa kama sehemu ya kutambua mchangoa wangu katika kuhamasisha maendeleo  na nilikabidhiwa katika Makao Makuu ya UN na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali duniani.

“Na huambatana na zawadi ya Dola za Marekani 100,000 (Sh milioni 200).    Sikuzichukua fedha hizi, kama mnavyojua maadili ya nchi yetu unaweza ukapokea  yakaibuka mambo mengine.

“Ingawa kwenye ule mkutano niliwaambia kuwa sipokei fedha kutokana na hali halisi … niliwaambia kuwa kama mnavyojua katika mkoa ninaotoka (Kagera) kuna tetemeko limetokea,” alisema Profesa Tibaijuka.

Alisema kupokea tuzo hizo si kwa ajili ya mafanikio yake binafsi bali kwa Watanzania wakiwamo wapiga kura wake wa Muleba Kusini ambao muda wote wamekuwa wakimtia moyo wa kufanyakazi kwa bidii.

Profesa Tibaijuka ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema ameuachia Umoja wa Mataifa (UN)  na wadhamini wa tuzo hiyo waamue cha kufanya kuhusu fedha hizo.

Katika kupokea tuzo hiyo, mbunge huyo alisindikizwa na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Dk. Augustine Mahiga  na Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM).

Waziri Mkuu Kuhamia Dodoma Leo

$
0
0
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajia  kuhamia rasmi Dodoma leo.

Majaliwa anahamia mjini hapa ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhamia Dodoma ambako ndiko yaliko makao makuu ya nchi.

Julai 25 mwaka huu, katika kilele cha siku ya mashujaa kilichofanyika mkoani hapa, Waziri Mkuu Majaliwa alisema ifikapo Septemba mwaka huu, Serikali itakuwa imehamia mjini hapa.

Hatua hiyo ya  waziri mkuu   ilitangazwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alipozungumza  na waandishi wa habari.

Alisema   Waziri Mkuu anatarajiwa kuwasili leo mchana akitokea   Dar es Salaam alikokuwa akiishi.

“Baada ya kuwasili hapa  atafanya ziara ya siku mbili katika Manispaa ya Dodoma Oktoba mosi na Oktoba 2 mwaka huu   kukagua hatua mbalimbali za maandalizi ya kupokea   Serikali mkoani hapa.

“Wakati wa ziara hiyo, atakagua majengo ya Serikali, maeneo ya kutolea huduma za afya, kituo cha umeme cha Zuzu, masoko, chanzo cha maji Mzakwe na maeneo ya viwanda.

“Kwa hiyo  maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mapokezi ya waziri mkuu yamekamilika na uongozi wa mkoa unaendelea kuwajulisha wananchi na wadau wote katika maeneo yatakayohusika na ziara hiyo, washiriki kwa ukamilifu.

“Kwa niaba ya uongozi wa Mkoa wa Dodoma, tunampongeza Waziri Mkuu Majaliwa kwa kuitikia na kutekeleza uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kuhamia makao makuu mjini hapa,”

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa leo CVPeople Africa

Mwimbaji Ray Vanny Adai Ilifika Wakati Akawa Anaichukia Sauti yake...Afunguka Haya Kuhusu Diamond Platnumz

$
0
0
Mwimbaji Raymond Amefunguka ya moyoni kuhusu boss wake aliyemtoa Kimuziki Diamond Platnumz:

Rayvanny
Mengi yako Moyoni Mwangu.lakini kiukweli siamini hapa nilipo.nilikata tamaa,sikujiamini tena kama ntaweza kufika.kuna muda nilijiona sina bahati hadi nikaanza kuichukia sauti yangu.lakini wewe ulinishika mkono nakunionyesha njia mengi umenielekeza haukuishia hapo ukaona unipe nafasi tufanye kazi moja mimi na wewe #SALOME . Am so proud of you @diamondplatnumz
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images