Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Askari Polisi Ajidhalilisha, Apokea Rushwa Mbele ya Camera Zanzibar

$
0
0
#ZanzibarPolice #corruption#Zanzibar #Tanzania Although Zanzibar was a beautiful place to visit, officials were trying to take bribes from the moment we landed (like the Yellow Fever scammers in Arrivals, then the car hire scammers in the airport car-park). That may explain my frustration at the end of this video.

Although I had a valid ‘Foreigners Driving Permit’, OFFICER ALI here – of the Police Post in Mahonda – stopped us at his roadblock on the second day and demanded a $40 bribe to allow us to drive on. After a long debate, he pockets 60,000 Tanzanian Shillings (about $28) without a receipt – and still tries to shake my hand.

(For those commenting that we should not have paid, the other option was to wait there for TWO DAYS until after Eid, and then pay a court official!) The offence was not carrying my national driving license, even though I had already shown it to get the Zanzibar 'Driving Permit'.

But the money went straight into his pocket.

By Pete Taylor Tazama Video Hapa:

PICHA ya Gari Mpya Alilonunua Mchezaji Mbwana Samatta Huku Ubelgiji

$
0
0
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ametumia kiasi cha milioni 130 kununua gari yake ya kwanza nchini Ubelgiji.

Gari hilo alilonunua mchezaji huyo ni Benz Cla220 Cdi AMG Sport 2016 ambayo gharama yake inadaiwa kuwa ni €46,680.

Samatta amechukua uamuzi huo baada ya kufanikiwa kupata leseni inayomruhusu kuendesha gari nchini humo baada ya kunyimwa miezi kadhaa iliyopita.

Inadaiwa kuwa mchezaji huyo analipwa kiasi cha €35,600 kutokana na mkataba wake wa kuichezea timu ya Genk ambao utamalizika mwaka 2020.

Kwa sasa Samatta ameonekana kuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa kwenye timu ya KRC Genk ambayo inashiriki kwenye michuano ya Europa League japo amekuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili akiuguza majeraha.

RAIS Magufuli Atafuna Mfupa Uliomtoa Jasho Kikwete

$
0
0
RAIS John Magufuli ameweka rekodi mpya ya kulipa deni la taifa ambayo haikuwahi kufikiwa katika kipindi cha miaka 12 iliyopita.

Katika rekodi yake hiyo mpya, Rais Magufuli amefanikiwa kulipa deni la taifa la ndani na nje ya nchi katika kipindi kifupi cha miezi mitatu kwa kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa na mtangulizi wake, Rais Jakaya Kikwete, katika kipindi chote cha miaka 10 aliyokaa madarakani.

Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya uchumi wa taifa iliyotolewa jana mbele ya waandishi wa habari na Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu ofisini kwake Dar es Salaam, Rais Magufuli amelipa shilingi bilioni 99 za deni la ndani na amelipa pia Dola za Marekani milioni 90 za deni la nje kwa muda wa siku 90.

Taarifa hiyo ya Gavana Ndulu inaonyesha kuwa kasi hiyo ya ulipaji deni la taifa kwa fedha za ndani ambalo hivi sasa limefikia shilingi trilioni 51 haijawahi kufikiwa kipindi chote cha Serikali ya awamu ya nne.

“Serikali imelipa Dola za Marekani milioni 90 kwa deni la nje ambazo ni sehemu ya Dola za Marekani bilioni 600 zilizokopwa Benki ya Stanbic na imelipa pia shilingi bilioni 99 za deni la ndani.

“Ninaposema limelipwa si kwamba Serikali haikopi kabisa, hapana, kinachofanyika kwa sasa fedha zinazokopwa ni ndogo kuliko zile zinazolipwa tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

“Utaratibu huo wa ulipaji uliwahi kutokea kati ya mwaka 2003 na 2004 na unaweza kupunguza kasi ya kuongezeka deni la taifa,” alisema Gavana Ndulu.

Katika mkutano huo, Gavana Ndulu alizungumzia pia mwenendo wa ukuaji uchumi kwa nusu mwaka unaoanzia Januari mpaka Juni 2016 kwa kueleza kuwa ukuaji wa pato la taifa umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 5.7 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2015.

Povu Lamtoka Nuh Mziwanda Akimtetea Ali Kiba...Adai Ana Roho Nzuri

$
0
0
Nuh Mziwanda Ametetea uamuzi wake wakumpigia promo Ali Kiba Kwenye page yake ya Instagram ili watu wamvotie ashinde tuzo...

Ameandika Haya hapa kuwalengo wote wanaomponda:

Iam_mziwanda
"Eeeeh bana nasemaje nasaport anaenisaport msinipangie mana inaeezekana hamjui wema wa jamaa kwangu 'mchizi yupo na roho ya kusema SAWA haijalishi upo kwenye wadhifa gani katika muziki na ndio mana collabo zake nyingi anapiga na wasanii wachanga 'I salute u Ali n plz let us keep on voting to him Heshima irudi nyumbani"

Neno Moja Kwa Nuh Mziwanda

Maisha ya Wasanii Hawa Baada ya Kudiss na Kujitenga na Clouds Media...

$
0
0
Nimekaa nikiwaza yani msanii akigombana na clouds kwanini inakua ngumu sana kusimama tena kimuziki? angalia

Jay dee karudi na ndindindi katamba kidogo tu kaja na ngoma yake mpya jiiiiiii imebuma haskiki tena.na ameanza kusahaulika tena

Wagosi wa kaya wakina mkoloni chaaliiiii

Mapacha nao hamna kitu kaaabisaaaaa

Dudu baya nae kuleee

Dan Msimamo kapuni

Rama D kajaribu kufulukuta wapiii

Rubby hata wimbo wake mpya haujulikani tu

Hawa jamaa wana hila gani wanafanya? daah kazi kweli kweli kwa mtindo huu wasanii acha waendelee kua watumwa tu maana njaa haina adabu..

Happy Birthday Diamond Platinumz (Icon wa Tanzania)

$
0
0
Leo October 2 ndo siku aliozaliwa Naseeb Abdul Juma ukipenda muite Diamond Platinumz huyu ndo icon wa mziki wa Tanzania na ni moja ya watu aliofanya mziki wetu sasa ivi unapigwa kwny channel za kimataifa na baadhi ya wasanii wanapata nomination zao za kwanza katika izo tuzo licha ya kuwepo kwenye game kabla ya Diamond,

Ni Diamond huyu huyu ndie inspiration kwa vijana na watoto wa Tanzania waliokataliwa na baba zao kulelewa na mama tu ila wakaja kutusua kimaisha ivyo pia kutoa fundisho mtoto hakataliwi hasa kwa wanaume wanapenda kukana mimba na pia amethibitisha kuwa unaweza usiwe na elimu kubwa ila ukafanikiwa kimaisha kupitia kipaji chako na ikumbukwe hamna aliezaliwa hapa duniani bila kipaji.

Happy birthday Naseeb Abdul Juma, (Diamond Platinumz) uishi miaka mingi na heri duniani na uendelezee moyo wa kuwasaidia wasanii wenzako kufika level iyo na kutoa ajira kwa vijana wa kitanzania kupitia lebel yako na kampuni yako WCB

Abdu Kiba Ampa Mimba Mwanafunzi wa Miaka 19 na Kumtelekeza..Binti Aelezea Tukio Zima

$
0
0
Abdu Kiba anashtumiwa kumpa mimba mwanafunzi, mwanafunzi huyo anadai walikutana Instagram, kisha akampa namba yake ya simu wakawa wanachat WhatsApp ndipo walipoendelea kuwasiliana hadi kukutana na kuja kufanya mapenzi na sasa hivi amemruka

Angalia Video Hapa Binti Akielezea Tukio zima mpaka kupewa Mimba

STORI ya Kusikitisha ya Mwanamuziki Rah P Baada ya Kuwa Mapenzini na Mwanamume Muuza Madawa ya Kulevya

$
0
0
Ni stori ambayo aliitoa kipindi cha nyumba kidogo lakini leo nimeona niwaletee na ninyi mtazame akielezea kilichomkuta na mpaka kupotea kabisa katika anga za muziki wa Bongo Flava.....Its so touching yaai i cant watch this twice. she is a good woman, really strong african woman i like her style, naona rap style yake imebadilika. i like the song Ushaurinwa bure, I think she can do wonders akifanya talk show. there are so many women going through such paths, imagine hearing these stories from Tanzanian women....

Tazama Video Hapa

Dada wa Diamond Esma Platnumz Adai Baba yake ni Mwarabu

$
0
0
Imefichuka kuwa mama Diamond alitoka na Muarabu na kuzaa mtoto wa kike ambaye sasa ni mkubwa ambaye anajulikana kwa jina la Esma 
Mtoto huyo amesema kuwa huwa hapendi kufahamika ndio maana anajitahidi kuweka 'low profile'.

Mtazame Hapa mtoto huyo ambae ni Nusu Mwarabu nusu Mwafrika:

BREAKING News: Simba, Yanga Marufuku Uwanja wa Taifa

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezifungia rasmi timu za Simba na Yanga kutumia uwanja wa Taifa mpaka pale zitakaporuhusiwa tena na Serikali.

Nape ametoa amri hiyo leo Jumapili ikiwa ni siku moja baada ya mashabiki wa klabu ya Simba, kung'oa viti vilivyopo kwenye majukwaa ya uwanja huo kwa kile walichokidai kupinga uamuzi wa Refa, Martin Saanya aliyechezesha mechi hiyo.

"Simba na Yanga hawatoutumia tena uwanja huu mpaka pale Serikali itakapoona kuwa mazingira yanaruhusu," alisema Nape.

Wanakijiji Mvumi -Chamwino Wachoma Moto Gari na Kuuwa Maafisa wa Taasisi ya Kilimo

$
0
0
Wakuu kuna habari zinasambaa mitandaoni kuwa kuna Maafisa wa Taasisi ya Kilimo ya Seliani iliyopo Mkoani Arusha wameuawa na wanakijiji wa Mvumi.

Kukatokea kutokuelewana kati ya maafisa hao na wanakijiji,kiasi cha maafisa hao kuchomwa moto wao na gari lao. Picha zinatisha.

Wanakijiji wa Mvumi Wilaya ya Chamwino ndio wamechoma gari ya serikali na kuchoma maafisa wa serikali wakiwa ktk majukumu yao.

Watu 35 tayari mbaroni wakiwemo viongozi wa kijiji.

Waziri wa mambo ya ndani aliposema ugaidi haijaingia tanzania, hii maana yake nini? Ama magaidi wanatoka maeneo gani hasa?

Gaidi huzaliwa ndani ya nchi husika. Sasa tukio hili ni ugaidi tosha. Usisubiri alshabab ama bokoharamu, matukio kama haya ni ugaidi tosha.

Note picha za waliochomwa zinatisha sana

Diamond Aeleza kisa cha Kukataa Kusainishwa na Label ya Jay Z, Roc Nation

$
0
0
Diamond Platnumz alitosa kusainishwa na label inayomilikiwa na Jay Z, Roc Nation.

Akiongea kwenye kipindi cha The Playlist cha Times FM, staa huyo alisema hiyo ni moja tu ya label kubwa za Marekani alizozitolea nje. “Wakati nipo BET, Roc Nation walinifuata wakitaka wanisaini,” alisema Diamond.

“Acha Roc Nation kuna baadhi ya record label nyingi sana kubwa, nyingi sana, tena hawanifuati hivi hivi, wananifuata na ofa,” aliongeza.

“Lakini kila kitu ni target, mimi siku yoyote ukisikia nimefanya kazi na label kubwa duniani, sio kuwa under record label, ila pointi yangu itakuwa kwamba kuona namna gani wanaweza kukuza muziki wangu kidunia zaidi, nitafanya kila kitu mwenyewe. Kupata collabo na msanii yeyote mimi naweza kupata sababu Kimarekani collabo sio story, hela yako, ni biashara, mtu hawezi akakupa bure mfanye nyimbo ili upate hela, ukanye show yeye anafaidika na nini?”

Kingine Diamond alisema kama ni msanii mkubwa inakuwa rahisi kupata collabo za aina hiyo.

“Nataka mtu akinisaini, nataka muziki wangu uuzike kama wanavyouza akina Jay Z, Kanye West. Sitoingia eti Diamond kaingia na record label fulani, WCB itaingia na kampuni fulani na ikiingia ni katika makubaliano ya kuuza muziki katika digital kuona ni namna gani muziki wangu utauza sehemu fulani kwa bei nzuri.”

Source:Bongo5

Barua ya Baraza Kuu la CUF kwenda kwa Msajili wa Vyama vya Siasa

$
0
0
BARUA YA BARAZA KUU LA CUF KWENDA KWA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA.

CUF/HQ/KM/016/10 Date: 27/09/2016

Jaji Francis S.K. Mutungi,
Msajili wa Vyama vya Siasa,
DAR ES SALAAM

YAH: MSIMAMO NA USHAURI WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSU UONGOZI WA KITAIFA WA CHAMA CHA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF)

Tafadhali husika na somo hapo juu pamoja na barua yako ya tarehe 23 Septemba 2016 yenye Kumb Na. HA.322/362/14/85 kuhusu somo tajwa.

Baraza Kuu la Uongozi la The Civic United Front (CUF) – Chama Cha Wananchi, kupitia Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama, limepokea barua yako tajwa hapo juu pamoja na taarifa fupi inayoainisha msimamo na ushauri wa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa Chama cha The Civic United Front (CUF) na kuijadili kwa kina. Yafuatayo ni majibu na msimamo wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF ambayo tunapenda kuyawasilisha ili ofisi yako iyafanyie kazi.

Awali ya yote, tunakupongeza kwa namna ulivyofuatilia kwa kina, kupitia wadhifa wako kama Msajili wa Vyama Vya Siasa Tanzania, malalamiko yaliyowasilishwa kwako na watu uliowatambua kwenye taarifa yako fupi.
Aidha, tumebaini kuwa ofisi yako imejikita katika kutoa tafsiri ya Katiba ya Chama cha The Civic United Front (CUF) toleo la mwaka 2014 pamoja na tafsiri ya matukio na maamuzi ya vikao vya Chama kwa mujibu wa ufahamu wako.

Pili, tumebaini kuwa ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa haina mamlaka ya kisheria kutoa “Msimamo na Muongozo” kwa chama cha siasa kilichosajiliwa nchini Tanzania. Majukumu ya ofisi yako kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha ofisi yako, Sheria ya Vyama Vya Siasa Sura ya 258, haikupi mamlaka ya kutoa msimamo na Muongozo.

Badala yake, unapewa mamlaka ya kuhifadhi kumbukumbu na taarifa za vyama vya siasa. Majibu haya yanatokana na ukweli kuwa ofisi yako imewahi kuonywa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam katika shauri la Madai Na. 6 la mwaka 2003 baina ya Emmanuel Nyenyemela and Another Versus Registrar of Political Parties and Others mbele ya Mheshimiwa Jaji Mihayo. Mahakama ilieleza kama ifuatavyo kwenye ukurasa wa pili wa hukumu:

“In the same vein, I do not see anywhere in the Political Parties Act where the Registrar has power to bless or condemn meetings of political parties or decisions that they make”. (Katika Muktadha huo huo sioni mahali popote kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa ambapo Msajili wa Vyama ana mamlaka ya kubariki au kupinga vikao vya vyama vya suasa au maamuzi yanayofanywa na vikao hivyo).

Tunapenda utambue kuwa uamuzi na muongozo huo wa Mahakama Kuu ya Tanzania haukuwahi kutenguliwa na Mahakama yoyote ile na hivyo tunaamini wewe ukiwa na weledi katika taaluma ya sheria na Jaji wa Mahakama kuu, unafahamu uamuzi huo na namna ya kuutumia.

Tatu, pamoja na kubaini yaliyomo kwenye aya zilizotangulia hapo juu, tunapenda upokee majibu yetu kuhusiana na kila kipengele ulichoongelea kwenye Taarifa yako fupi kama ifuatavyo:

1. MAMLAKA NA WAJIBU WA MSAJILI KUSHUGHULIKIA MGOGORO HUU
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF linasikitika na upotoshaji wa makusudi uliofanywa na ofisi yako kuhusu tafsiri ya vifungu vya Sheria ya Vyama Vya siasa, Sura ya 258 ulivyovitaja katika ukurasa wa pili wa Taarifa yako fupi ili kujipa mamlaka ya kushughulikia kile ulichokiita mgogoro wa Uongozi katika Chama chetu.

Tunapenda urejee vifungu ulivyotumia ambavyo tunavichapisha tena hapa chini:
Kifungu cha “8A (1) There shall be a Registrar of Political Parties into which names, addresses, and other particulars of Registered Political Parties or national leaders of Political Parties shall be entered.” (Kutakuwa na Msajili wa Vyama vya Siasa ambako majina, anwani na taarifa zingine za Vyama vya Siasa vilivyosajiliwa au viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa zitawekwa).

Kifungu cha 10(f) “No Political Party shall be qualified to be fully registered unless …..(a)…….(e) (Hakuna Chama cha siasa kitakachofaulu kupewa usajili wa kudumu hadi……)
(f) it has submitted the names of the national leadership of the party and such leadership draws its members from both Tanzania Zanzibar and Mainland Tanzania, and” (kiwe kimewasilisha majina ya uongozi wa kitaifa na uongozi wa chama hicho uundwe na wanachama kutoka Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara, na)

Ukivisoma vifungu hivyo hapo juu, katika sheria tajwa, utabaini kuwa havina kabisa uhusiano na kukupa wewe mamlaka au wajibu wa kuchunguza na kujiridhisha kuhusu usahihi wa mabadiliko katika uongozi wa Kitaifa wa Chama na ama kutengua au kubariki maamuzi halali ya vikao halali vya chama chochote. Zingatia pia hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo tayari tumeitaja hapo juu. Tumejiridhisha kuwa mamlaka uliyojitwisha hayakuwa yako na pia hukuyatenda kwa kuzingatia misingi ya haki.

2. KUJIUZULU KWA PROFESA IBRAHIM LIPUMBA NA KUTENGUA BARUA YAKE YA KUJIUZULU
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF linatambua kuwa Chama cha The Civic United Front (CUF) kinaongozwa na Katiba yake halali, toleo la mwaka 2014. Tunapenda utambue kuwa kujiuzulu kwa kiongozi ni wakati wowote kwa mujibu wa Ibara ya 117(1). Kuhusu utaratibu uliowekwa na ibara ya 117(2) hauathiri haki ya kiongozi kujiuzulu wakati wowote.

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba aliandika barua ya kujiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa CUF Taifa kuanzia tarehe 5/08/2015 ambayo ni siku aliyoandika barua hiyo na aliutangaza uamuzi wake huo mbele ya vyombo vya habari tarehe 6/8/2015.

Katika Barua yake ya kung’atuka wadhifa wa Mwenyekiti wa Taifa wa CUF ilisema ;
”Leo tarehe 5 Agosti 2015 najiuzulu rasmi nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa CUF. Naendelea kuwa Mwanachama na kadi yangu nimeilipia mpaka 2020.”

Prof. Lipumba alitekeleza kujiuzulu kwake bila kusubiri kukubaliwa na Mkutano Mkuu wa Chama kwa mujibu wa Ibara 117(2) ya Katiba ya Chama. Prof. Lipumba alikua na mamlaka ya kuhakikisha kuwa Mkutano Mkuu unaitishwa ili kukubali kujiuzulu kwake lakini hakufanya hivyo.

Kama ulivyoeleza katika taarifa yako, Katiba ya CUF inatambua haki ya kujiuzulu uongozi lakini haizungumzii kutengua uamuzi wa kujiuzulu. Prof Lipumba asingeweza kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu kwa sababu alishautekeleza. Na aliacha ofisi na majukumu ya Mwenyekiti wa Taifa wa CUF kwa mujibu wa Ibara ya 91 ya Katiba ya Chama kwa zaidi ya miezi kumi. Kuna msemo “you can not eat a cake and have it.”

Kwa hiyo suala la Prof. Ibrahim Haruna Lipumba kurudi kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa CUF Taifa baada ya zaidi ya miezi kumi ni wazo chelewefu (afterthought) na ndiyo maana amekua akiitika wito wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kama Mwalikwa kutoa maoni juu ya mambo mbalimbali.

3) BAADHI YA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU MAALUM KUHITAJI PROFESA LIPUMBA AITWE KATIKA CHUMBA CHA MKUTANO KUJIELEZA.
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF limesikitishwa kwamba hujajielekeza kabisa juu ya namna Prof. Lipumba alivyovamia Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa tarehe 21/08/2016 akiwa na genge la wahuni ambao sio wajumbe wala waalikwa wa mkutano huo (kama yeye) na wahuni hao wakiwa na silaha mbalimbali na kwa hiyo tunachukulia kwamba unaunga mkono vitendo hivyo.

Ibara ya 117(2) ya Katiba ya CUF haitoi fursa kwa kiongozi aliyejiuzulu kujieleza juu ya kujiuzulu kwake mbele mkutano husika. Hata hivyo, umuhimu huo haukuwepo kwa sababu chama kiliridhika kwamba ni yeye ndiye aliyejiuzulu na aliondoka ofisini na akaacha kutekeleza majukumu yake ya Mwenyekeiti wa CUF Taifa.

Pia alikabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa mkono wake mwenyewe tarehe 05/08/2015 na siku iliyofuata ya tarehe 06/08/2015 aliufahamisha umma kupitia vyombo vya habari kwamba alijiuzulu na alithibitisha hiyo. Maelezo ya Profesa Ibrahim Lipumba yalikuwa tayari yanafahamika kwa wajumbe wengi wa Mkutano na hakukuwa na suala jipya kuhusiana na kujiuzulu kwake.
Hivyo haukuwa sahihi hata kidogo kusema kuwa Profesa Lipumba alipaswa kujieleza mbele ya Mkutano Mkuu.

Msimamo wako huo ni kinyume na Katiba ya CUF na hali halisi ilivyokuwa. Mashaka uliyojijengea kuwa huenda barua iliyosomwa haikuwa yake hayana msingi wowote maana tangu mwaka 2015 ofisi yako imekuwa ikifanya kazi na Chama cha CUF kupitia viongozi wengine na ukiwa Mtanzania tunaamini ulipata taarifa za kujiuzulu kwake kwa njia nyingi. Ofisi yako pia ilipokea taarifa rasmi kutoka CUF, kwa hiyo inashangaza sana kusikia kuwa hata ofisi yako haikuwa na taarifa za kujiuzulu kwa Profesa Lipumba.

4). UHALALI WA KURA ZILIZOPIGWA KUKUBALI AU KUKATAA PROFESA LIPUMBA KUJIUZULU.
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF linabaini tafsiri ya matumizi ya ibara ya 77(8) (d) ya Katiba ya CUF ambayo tunapenda kuidurusu hapa chini:
“77(8) Kwa madhumuni ya kijifungu cha (7) cha kifungu hiki, maamuzi muhimu ni pamoja na
(d) kuwasimamisha, kuwaachisha au kuwafukuza uongozi na/ au uanachama viongozi wakuu wa Kitaifa wa Chama pamoja na viongozi wengine wa Kitaifa kama ilivyoainishwa ndani ya Katiba hii.”

Kijifungu hicho hakihitaji tafsiri yoyote na kiko wazi, kwamba matumizi ya kifungu hiki ni pale ambapo yanajadiliwa masuala ya kuwasimamisha, kuwaachisha au kuwafukuza uongozi na au uanachama viongozi wakuu wa Kitaifa wa Chama. Katiba hii haitoi wajibu wala haifanyi suala la kujiuzulu Kiongozi wa Kitaifa wa Chama kuwa ni jambo muhimu linalohitaji kupigiwa Kura kwa mujibu wa tafsiri yako. Ikiwa Lipumba angelikuwa anasimamishwa, anaachishwa au kufukuzwa uongozi au uanachama ndipo matakwa ya uamuzi muhimu kikatiba yangelifanyika.

Lakini Profesa Lipumba alijiuzulu mwenyewe, hakusimamishwa, hakuachishwa na wala hakufukuzwa uanachama au uongozi kwa hiyo Mkutano Mkuu wa CUF kikatiba hauwezi kushughulikia suala la kujiuzulu kwa kiongozi kama uamuzi muhimu.

Tambua pia kuwa Katiba ya CUF ni yetu wenyewe na wewe ni Msajili, tunaifahamu vyema sisi wanachama na viongozi kuhusu maudhui yake kuliko wewe ambaye mara zote tunakupa taarifa baada ya maamuzi ya vikao na Katiba hiyo kuwasilishwa kwako kwa usajili tu. Kujiuzulu kwa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kulifanyiwa maamuzi kwa mujibu wa Ibara ya 115(1) ya Katiba ya CUF na siyo ibara ya 77(7).

Kura zilizotakiwa ni zaidi ya nusu tu na siyo 2/3 (theluthi mbili) na kura zilizopigwa kubariki kujiuzulu kwake ni 476 ambazo ni asilimia 70 ya idadi ya wajumbe wote wa Mkutano Mkuu na kwa hiyo maamuzi ya ibara ya 117 (2) yalifanywa kwa uhakika, kikatiba na bila shaka yoyote.
Taarifa za vurugu wakati wa maamuzi siyo ya kweli. Unatambua kuwa vurugu hizo zilitokea baada ya ajenda ya kukubali kujiuzulu kwa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kukubaliwa na ajenda hiyo kufungwa na mkutano kuahirishwa kwa mapumziko na kwamba baada ya mapumziko na wakati mkutano uko kwenye ajenda ya pili ndipo vurugu zilitokea.

Hata hivyo, unatambua kuwa vurugu hizo alizisababisha yeye mwenyewe Prof. Lipumba alipofahamu maamuzi ya Mkutano na wakati wa Kuchagua Mwenyekiti mpya wa kujaza nafasi yake iliyoachwa wazi kwa kujiuzulu.

5). UHALALI WA KIKAO CHA BARAZA KUU LA LA UONGOZI LA TAIFA CHA TAREHE 28 AGOSTI 2016.
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF limebaini kuwa ofisi yako imetambua Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa cha tarehe 28 Agosti 2016. Hatuna mashaka na mtazamo huu kwani ndiyo ukweli.

6). MAMLAKA YA BARAZA KUU LA UONGOZI KUCHUKUA HATUA ZA KINIDHAMU.
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF halina mashaka na utambuzi wako wa mamlaka ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya viongozi wa Kitaifa wa Chama.
Tunakushauri kifungu ulichotumia ukisome pamoja na vifungu vingine ambavyo ni Ibara ya 82(1) (m) na 83(1).

7). UTARATIBU WA KUCHUKUA HATUA ZA INIDHAMU.
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF linapenda kukufahamisha kuwa taarifa ya Kikao cha dharura ilikuwa sahihi na ajenda ilikuwa inafahamika kwa wajumbe wa Kikao kuwa ni kujadili hujuma. Hata hivyo, tunakanusha tuhuma kuwa Maamuzi muhimu kwa mujibu wa ibara ya 77(8) na 81(4) hayakufanyika kwa kuzingatia matakwa ya 2/3 ya wajumbe.

Utatambua kuwa maamuzi yote ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa yanaweza kufanyika kwa maafikiano au kwa wingi wa kura. Tunakushauri urejee Ibara ya 81 (3) ya Katiba ya chama ambapo hata maamuzi muhimu yanahusika.

Tafsiri ya neno “Unanimously” hayamaanishi “Consensus”. Tunajiridhisha kuwa neno Unanimously kwa muktadha wa Chama chetu ni kuwa wajumbe wote walipiga kura na hakukuwa na mjumbe aliyepinga. Hatukuwahi kupata taarifa za mtu yeyote aliyethibitika kuwa alinyimwa fursa ya kupiga kura. Kama maamuzi yalifanyika unanimously, basi yalifanyika kwa wingi wa wajumbe zaidi ya 2/3 kila upande. Katiba ilizingatiwa.

8. UTEUZI WA VIONGOZI WA KITAIFA ULIOFANYWA NA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA.
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF linapenda ufahamu kuwa ibara ya 101 inalipa Baraza Kuu la Uongozi Taifa uwezo wa kuunda Kamati yoyote na hivyo kujumuisha uwezo wa kuunda Kamati ya Uongozi ilipoona kuna haja hiyo. Kamati iliyoundwa ni halali kwa ajili ya utekelezaji mzuri wa sera na itikadi za chama. Majukumu ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa yana lengo la kusaidia utekelezaji mzuri wa sera na itikadi za Chama, kwa hiyo majukumu ni yale yale na siyo tofauti.

Kwa mantiki hiyo, Kamati zote mbili yaani ile ya awali iliyokuwa chini ya Mwenyekiti Mhe. Wakili msomi Twaha Issa Taslima na hii ya sasa iliyo chini ya Mhe. Julius Mtatiro zote ni halali kwa mujibu wa katiba ya Chama. Ofisi yako ilipokea taarifa ya Chama na inayo (ambalo ndilo jukumu lako) iliyokuwa ikikueleza kuundwa kwa Kamati ya Uongozi ya awali iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mhe. Twaha Taslima ambayo hukuhoji uhalali wake na uliitambua na hata kufanya kazi nayo ilipokuwa ikiwasiliana na wewe. Haiwezekani uone na utambue uhalali wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kuunda Kamati ya Uongozi kwa kipindi cha Agosti 2015 hadi Agosti 2016 lakini usione uhalali wa kuundwa Kamati ya aina hiyo hiyo iliyoundwa tarehe 28 Agosti, 2016.

9. UHALALI WA UTEUZI WA VIONGOZI WA KITAIFA ULIOFANYWA NA KIKAO CHA BARAZA KUU LA TAREHE 28 AGOSTI 2026.
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF linapenda kusisitiza kuwa uteuzi ulikuwa halali kama tulivyoeleza hapo juu. Kama ulivyoeleza wewe, utabaini kuwa mamlaka ya uteuzi wa viongozi wa Kitaifa ni Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na ndicho kilichofanyika na ambacho ni msimamo wa Chama. Na hiyo ina maana kuwa msimamo wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF ni kuwa Ndugu. Julius Mtatiro, Ndugu. Severina Mwijage na Ndugu. Katani Katani ndiyo wajumbe wa kamati hiyo ya uongozi na wanatambulika kikatiba katika chama chetu kama Wajumbe wa Kamati ya Uongozi hadi hapo chama kitakapochagua Mwenyekiti mwingine.

10). HITIMISHO
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF limejiridhisha kuwa katika taarifa yako fupi umeweka hitimisho ambalo linatoa hukumu (judgment) badala ya kushauri au kutoa taarifa kama ulivyoitaja.

Kama tulivyokwisha kueleza kwenye utangulizi wa barua yetu na kwa kuzingatia Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 toleo la mwaka 2015 na kwa kuzingatia hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam, mbele ya Mhe. Jaji Mihayo ambayo tunaiambatanisha na barua hii kwa taarifa, tafadhali tambua kwamba hukumu yako ni batili na haina mashiko kisheria.

Kwa yale ambayo umetoa ushauri kwa mujibu wa Katiba ya Chama chetu, Chama kina hiyari ya kuukubali au kuukataa ushauri huo kwa kuzingatia misingi ya Katiba yake, Kanuni zake na kuhakikisha haki sawa kwa wote inatendeka wakati wote.

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF linasisitiza kuwa maamuzi yaliyofanywa na vikao halali vya Chama vya Mkutano Mkuu Maalum wa tarehe 21/08/2016 na Baraza Kuu la Uongozi la Chama Taifa la tarehe 28/08/2016 ni halali na tunakusihi uyatambue hivyo.

Tunakukumbusha na kukukusihi usiruhusu Ofisi yako itumike vibaya kutuletea mitafaruku na migogoro isiyo ya lazima katika Chama chetu na hata kusababisha uvunjifu wa amani kama ilivyotokea Jumamosi, tarehe 24 Septemba, 2016 katika Ofisi Kuu ya chama chetu Buguruni Dar Es Salaam. Ushauri huu unazingatia ukweli kuwa Msajili wa Vyama Vya Siasa Tanzania ni mteule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa. Nguvu ya Chama cha CUF Tanzania inafahamika na hasa katika ushiriki wake na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2015.

Matukio yaliyojitokeza Zanzibar na siasa za nchi hii ni lazima yazingatiwe wakati ukitekeleza majukumu yako ili kuepuka kutumiwa vibaya na watu walioshiriki kuhujumu chama chetu na demokrasia wakati wa uchaguzi mkuu wa 2015 na marudio yake 2016 kwa Zanzibar. Taarifa tulizo nazo za malengo ya Profesa Lipumba kuhujumu siasa za Chama Cha Civic United Front (CUF) na mahusiano ya Chama na taasisi nyingine zinajidhihirisha katika matukio yaliyofanywa na Profesa Lipumba tarehe 21 Agosti 2016 (Ubungo Plaza, Dar Es Salaam – kwenye Mkutano Mkuu Maalum) na tarehe 24 Septemba 2016 (wakati akitekeleza kwa nguvu kile anachokiita “kurudishiwa uenyekiti wake na Msajili) baada ya barua yako tajwa.

Mwisho, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF haliukubali ushauri wako kwa sababu umevuka mipaka ya mamlaka yako uliyokabidhiwa na Sheria namba 5 ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992, imekiuka miongozo ya mhimili wa Mahakama ambayo imekwishatolewa juu ya mamlaka yako na unakiuka misingi ya katiba ambayo inamtaka kila mtu aliyepewa mamlaka katika nchi yetu azingatie sheria za nchi.

Kwa sababu hiyo Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front CUF linakujulisha rasmi kuwa, maamuzi ya vikao halali vya chama kwa maana ya Mkutano Mkuu wa Taifa tarehe 21 Agosti 2016 na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la tarehe 28 Agosti 2016 yanabakia pale pale na kwamba Profesa Lipumba siyo Mwenyekiti wa The Civic United Front CUF Chama Cha Wananchi na kuwa, wanachama na viongozi wote waliosimamishwa na ama kufukuzwa katika kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa cha tarehe 28 Agosti 2016 wanaendelea kuwa chini ya maamuzi hayo hadi pale mchakato wa kikatiba wa kuwasikiliza (kwa waliosimamishwa) utakapokamilika.
Hatua yoyote ile ya kutengua maamuzi yoyote ya vikao halali vya chama chetu itafanywa na vikao husika vya chama au vikao vya juu yake kama ambavyo katiba yetu imeelekeza na kwamba hatutakubali Ofisi yako kutuamulia nani anapaswa kuongoza chama chetu kwa wakati gani ama tujiongoze katika chama chetu kwa namna gani.

Tunawasilisha.
HAKI SAWA KWA WOTE

…………………………………..

MAALIM SEIF SHARIF HAMAD
KATIBU MKUU

NAKALA;
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba
Kilongawima, Kunduchi,
Dar es Salaam.

Bwana Ridhiwani H. Kilala na Wenzako wawili

Bwana Abdul Kambaya na Shashu Lugeye.

WATAFITI Wauawa Kinyama..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya Octoba 3

$
0
0


WATAFITI Wauawa Kinyama..Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya Octoba 3

DIAMOND Abaki na Nguo ya Ndani ‘Boxer’ Wakati Akisherekea Birthday yake

$
0
0
Jumamosi hii ilikuwa ni siku ya kuzaliwa ya staa wa muziki, Diamond Platnumz ikiwa ni wiki moja toka atoke visiwani Zanzibar kusherekea birthday ya mama watoto wake, Zari.


Muimbaji huyo alikata keki mbele ya wasanii wake wa WCB huku akiwaacha midomo wazi mashabiki wake wa kwenye mitandao jamii kwa kitendo cha kusherekea birthday hiyo huku akiwa na nguo ya ndani ‘boxer’ akidai alikuwa anaogopa kumwagiwa maji.

Pia mastaa mbalimbali walimtumia salamu za heri na baraka staa huyo anayefanya vizuri na wimbo ‘Salome’.

Rich Mavoko
Happy Birthday Big Nna Zawadi Yako Ya Gari Lakini La Udongo 😂😂 So Wambie Hao Wanaokumwagia Maji Nikilileta Waache Kwanza

Harmonize
Happy birthday my brother #simbaa nikisema niandike mengi sitomaliza ila unajuwa vyenye nakuzimia na na kukuheshimu….🙏🙏🙏 maisha marefu furahiya siku yako 🎂🔥🔥

Rayvanny
Jus me and birthday boy @diamondplatnumz Bigie Mungu Akupe Maisha Marefu ndugu yangu maana ukinasa hatunasuliki mwiiiiiiiiingiiiiiiiii wa materials enjoy your day

MAN United Yashindwa Kutamba Nyumbani, Yalazimishwa Sare na Stoke City

$
0
0
Klabu ya Manchester United imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Stoke City katika mechi ambayo Manchester United iliotawala mchezo kwa kipindi cha mda mrefu.

Baada ya kipa wa Stoke kuokoa mashambulio mengi katika kipindi cha kwanza cha mechi,United ilijiweka kifua mbele baada ya mchezaji wa ziada Anthony Martial kufunga bao la kwanza.

Ilikuwa pigo kubwa kwa Stoke ambayo ilikuwa haijafanya shambulio lolote katika ngome ya United.

Lakini baada ya Jon Walters kupiga krosi, Allen alifika na kusawazisha hivyo basi kufuinga midomo ya mashabiki wa United ambao walikuwa wakiimba katika kipindi chote cha mchuano huo.

Stoke City ambayo iko katika nafasi ya pili kutoka mwisho sasa imejiongezea matumaini ya kuondoka katika eneo la mkia la ligi hiyo ya Uingereza.

ACT-Wazalendo Waitisha Mkutano wa Kidemokrasia Kupigania Upatikanaji wa Katiba Mpya

$
0
0
Chama cha ACT- Wazalendo kimepanga kuwasha moto mjadala wa Katiba mpya katika mkutano wake kidemokrasia kilioitisha jijini Dar es Salaam Oktoba 8.

Mkutano huo unalenga kufufua mchakato wa Katiba Mpya kwa kuzingatia michakato ya katiba za nchi nyingine za Afrika, alisema Katibu wa itikadi na uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu alipozungumza na waandishi jijini Dar es Salaam  jana.

Alisema katika kupata uzoefu, ACT Wazalendo imemualika Adabu Namwamba, ambaye ni kiongozi wa Chama cha Labour cha Kenya kilichofanikiwa kubadilisha katiba yake baada ya mchakato mrefu.

 Aliwataja wageni wengine kuwa ni mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus Kibamba ambaye naye atatoa mada kuhusu suala hilo.

Mchakato wa kuandika Katiba mpya nchini umekwama katika hatua ya kupiga Kura ya Maoni baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushindwa kukamilisha uandikishaji wapigakura kwa muda uliotakiwa.

Mchakato huo uligubikwa na vikwazo kadhaa, ikiwa ni pamoja na vyama vinne vya upinzani na baadhi ya wajumbe kususia kwa maelezo kuwa Bunge liliacha Rasimu ya Katiba iliyokuwa na maoni ya wananchi na kuingiza sera za CCM.

Katika mkutano huo, kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe atawasilisha mada kuhusu hali ya nchi kwa mtazamo wa chama hicho.

“Kiongozi wetu atawasilisha uchambuzi mpana wa kina zaidi kuhusu hali ya nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani,” alisema. 

Pia, mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Anna Mghwira, ambaye aligombea urais mwaka jana, ataeleza uzoefu wake katika uchaguzi, wakati mshauri wa chama hicho, Profesa Kitila Mkumbo atachambua mwelekeo wa chama hadi mwaka 2020.

“Chama kinatoa wito kwa wananchi wanaotaka kushiriki katika mkutano huo kuwasiliana na ofisi ili kujiandikisha,” alisema. 

TIMU ya Vijana Serengeti Boys Yashindwa Kufuzu Fainali za Africa

$
0
0
Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys imeshindwa kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika nchini Madagascar mwaka 2017 baada ya kupoteza mchezo wake wa mwisho wa kufuzu dhidi ya Congo Brazzaville kwa kufungwa bao 1-0 ugenini.

Bao pekee katika mchezo huo limefungwa dakika za mwisho katika mchezo huo na kuzima ndoto za watanzania kuisuhudia timu yao ikienda kuliwakisha taifa kwenye michuano mikubwa barani Afrika.

Kocha wa Serengeti Boys Bakari Shime amesema matokeo hayo huenda ni mipango ya Mungu licha ya wao pia kuwa na mipango yao kuhakikisha timu inafuzu kwenye mashindano ya AFCON.

“Ni ngumu hata kuelezea, kimsingi tulifanya kilakitu kizuri na tulifanikiwa kwa kilakitu, game tuliikamata lakini kosa dogo ambalo tumelifdanya wenzetu wakalitumia na kutumaliza. Vijana walicheza vizuri sana hawajawahi kucheza kama walivyocheza leo”.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Dar es Salaam, Serengeti Boys ilishinda kwa magoli 3-2, hivyo kuruhusu goli 1-0 ugenini kunafanya matokeo ya jumla kuwa 3-3 lakini Tanzania inatupwa nje kwa sheria ya goli la ugenini.

RAIS Magufuli: Hakuna Fedha za Tetemeko Kwenda Magereza. Wafungwa "Watetemeke" Kujenga Magereza yao

$
0
0
“Katibu Mkuu Kiongozi, hakuna kuwapelekea wafungwa wa Karagwe fedha yoyote, hizi za maafa ya tetemeko. Watetemeke na kufanya kazi,” alisema Rais Magufuli na kuibua kicheko kwa watu waliohudhuria hafla hiyo.

Rais John Magufuli amesema Serikali haitajenga Gereza la Kitengule Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera lililobomoka kwa tetemeko la ardhi, badala yake ameliagiza Jeshi la Magereza liwatumie wafungwa kufanya kazi hiyo.

Alitoa agizo hilo juzi wakati akifunga mazoezi ya kijeshi ambayo kitaalamu yanaitwa ‘amphibious landing’ yaliyofanyika Kijiji cha Baatini, Bagamoyo mkoani Pwani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).

Katika mazoezi hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na kushuhudia wanajeshi wakilikomboa eneo lililotekwa na maadui ukanda wa majini, Rais Magufuli alimtaka Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kutopeleka fedha za maafa kujenga gereza hilo

Mwanamuziki Diamondplatnumz Asherehekea Siku yake ya Kuzaliwa Kwa Kula Chakula Cha Mchana na Watoto Yatima,

$
0
0
Mwanamuziki Diamondplatnumz asherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kula chakula cha mchana na watoto yatima, na kuwasaida vitu mbalimbali. 

Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images