Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Baraka The Prince na Alikiba Wametuletea Video yao Mpya..Itazame Hapa

$
0
0
Ni Single mpya iitwayo Nisamehe ambayo ilirekodiwa April 27, 2016 kwenye studio za producer Emma The Boy  na wakali kutoka kwenye label ya Rockstar 4000 Baraka The Prince na Alikiba
Itazame Hapa Chini:

MTV MAMA Awards 2016..Wameongezeka Watanzania Watatu Kwenye List ya Kuwania Tuzo Hizo

$
0
0
Sept 21, 2016 majina ya mwanzo ya wasanii watakaowania tuzo za MTV MAMA 2016 yalitajwa huku  Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz na kundi la Navy Kenzo pamoja  na Alikiba ndio wasanii wa Tanzania waliotajwa kuwania tuzo kubwa za Africa za MTV Africa Music Awards 2016.

Sasa basi habari njema leo October 2, 2016 MTV MAMA 2016 wametaja majina mengine ya wasanii watakaowania tuzo hizo ambapo kwa upande wa Tanzania wameongezeka  wasanii watatu akiwemo Raymond wa WCB, Vanessa Mdee na Yamoto Band.

Diamond Platnumz  ametajwa kwa mara ya pili kuwania tuzo hizo katika kipengele cha Artist of the Year ambacho anachuana na Black Coffee (South Africa), Sauti Sol (Kenya), Yemi Alade (Nigeria), Wizkid (Nigeria).

Mara ya kwanza Diamond Platnumz alitajwa kuwania kipengele cha Best Male ambacho anachuana na Black Coffee (South Africa), Wizkid (Nigeria), AKA (South Africa),  Patoranking (Nigeria).


Vanessa Mdee anawania kipengele kimoja cha Best Female ambacho anachuana na Josey (Ivory Coast), Mz Vee (Ghana), Tiwa Savage (Nigeria), Yemi Alade (Nigeria).

Alikiba ametajwa kwa mara ya pili kuwania kipengele cha Song of the Year kupitia wimbo aliyoshirikishwa na Sauti Sol uitwao Unconditionally Bae.

Kenya imewakilishwa na kundi la Sauti Sol katika  kipengele cha Song of the year na Artist of the year pamoja na Kansoul kwenye kipengele cha Listerners Choice Awards.

 Huku Uganda ikiwa imewakilishwa na wasanii wawili ambao ni Eddy Kenzo  anayewania kipengele cha Best Live Act pamoja na Sheeba anayewania kipengele cha Video of the Year pamoja na Bebe Cool katika kipengele cha Listener’s Choice Awards.

Raymond wa WCB ametajwa kuwania kipengele cha Best Breakthrough Act ambacho anachuana na  Babes Wodumo (South Africa), Emtee (South Africa), Falz (Nigeria), Franko (Cameroon), Nasty C (South Africa), Nathi (South Africa), Simi (Nigeria), Tekno (Nigeria), Ycee (Nigeria).

Yamoto Band wametajwa kuwania kipengele cha Listener’s Choice Awards ambacho wanachuana na Burna Boy (Nigeria), Adiouza (Senegal), Kansoul (Kenya), Meddy (Rwanda), Prince Kaybee (South Africa), Zaho (Algeria), Kiss Daniel (Nigeria), E.L (Ghana), Bebe Cool (Uganda), Latifa (Tunisia), Saad Lamjarred (Morocco), Tamer Hosny (Egypt), Jay Rox (Zambia), The Dogg (Namibia), Sidiki Diabate (Mali), Adiouza (Senegal), Den G (Liberia), Jah Prayzah (Zimbabwe), LIJ Michael (Ethiopia), Messias Maroca (Mozambique).

Hivi ndio vipengele 7  vipya vya wasanii watakaowania  tuzo za MTV MAMA 2016, Jumamosi ya 22 October 2016 kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome Afrika Kusini.


Mtoa Macho Buguruni Akamatwa na Polisi

$
0
0
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro amesema jeshi hilo limemkamata mtuhumiwa ‘Scopion’ aliyehusika katika matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha eneo la Buguruni jijini humo.

Sirro alitoa kauli hiyo jana Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kujadili usalama katika eneo hilo ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Alisema mtuhumiwa huyo anayejulikana kwa jina maarufu kama Scopion alikamatwa baada ya polisi kupewa taarifa za matukio ambayo ameyafanya ikiwemo la kumchoma kisu, kumtoa macho na kumsababishia upofu, Said Ally.

"Nimesikia wananchi wanalalamika hapa kuwa tumeshindwa kumkamata Scopion, ni nani kwa Jeshi la Polisi asikamatwe, tayari tumemkamata na sheria itachukua mkondo wake, hakuna mtu anayeweza kushindana na jeshi," alisema.

Aidha Sirro alisema baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo na kuhojiwa aliutaja mtandao wake wote na tayari wameukamata, hivyo amewataka wakazi wa eneo hilo kutokuwa na hofu kwani mtuhumiwa huyo hayupo tena katika eneo hilo.

"Najua suala hili bado lipo mahakamani hatuwezi kulizungumzia sana, bahati nzuri alipokamatwa alieleza aliyoeleza na tukafanikiwa kuukamata mtandao wote, hivyo hakuna haja ya kuwa na uwoga eneo hili lipo salama," alisema.

Kabla ya kauli hiyo ya Sirro, wananchi wamelalamikia askari wa eneo hilo ambao walishindwa kuchukua hatua kwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifahamika muda mrefu. Sadiki Mgaya ambaye alishuhudia tukio la kuchomwa kisu na kutolewa macho kwa Said Ally, alisema mtuhumiwa huyo alisema kuwa amekuja kwa ajili ya kulipa kisasi kwa wakabaji baada ya yeye kukabwa.

Alisema baada ya kufanya tukio hilo, askari walifika katika eneo hilo na mtuhumiwa huyo akiwa hapo na wananchi waliwaonesha askari lakini hawakuchukua hatua zozote badala yake waliwataka wananchi wamkamate.

Aidha wananchi hao pia wamemlalamikia Mkuu wa Kituo cha Polisi Mnyamani na kudai kuwa amekuwa akipelekewa taarifa za uhalifu ikiwemo za vibaka lakini mtu anapokamatwa akifika kituoni hapo anatoa rushwa na kuruhusiwa kuondoka.

Lakini akiondoka askari wengine wanatumwa tena kumkamata. Kauli hizo za wananchi zikamfanya Sirro kutoa kauli ambapo alisema askari na maofisa wote ambao wanashindwa kutimiza wajibu wao watachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa mahakamani pamoja na kufukuzwa kazi.

"Najua wapo askari na maofisa wa ovyo ambao hawajui kutimiza wajibu wao, lakini nikuahidi Mkuu wa Mkoa tutawachukulia hatua, nimesikia hapa wananchi wanalalamika askari wanachukua rushwa, tutachunguza tukijiridhisha basi ni lazima tuchukue hatua," aliongeza.

Aidha Sirro alisema watafanya doria kubwa katika eneo hilo ili kuwakamata wote wanaohusika na matukio ya kihalifu kwani wamebaini katika eneo hilo bado kuna uporaji mdogo mdogo.

"Tutarudi hapa tunaomba ushirikiano wenu bila ninyi kutuambia hatuwezi kujua, nawaomba wazazi muwakanye watoto wenu ambao wanahusika na matukio hayo kwani tutakapoanza msako huo wasije wakalalamika, uhalifu haulipi na mwisho wa siku utamkosa mtoto wako," alisisitiza.

Kwa upande wake Makonda aliwataka wananchi hao kujitolea kufanya ulinzi shirikishi na kuwataka wananchi kuchangia ulinzi huo ili vijana hao wahusike kufanya ulinzi na kulifanya eneo hilo libaki na amani.

"Tuna wajibu wa kufanya ulinzi shirikishi wananchi mtoe michango, hapa Sirro amesema mapungufu yaliyopo kwenye vituo yanafanyiwa kazi, niwaase tu mjiepushe na matukio ya kuhalifu kwani wale watakaokamatwa sheria itachukua mkondo wake," alisema Makonda.

Diamond Asherekea Birtday yake Akiwa Uchi

$
0
0
Diamond Platnumz alisherekea birthday yake kwa kuvua nguo zote na kubaki na ya boxer tu alipokuwa anasherekea siku yake ya kuzaliwa Tazama Video:

Diamond Awapiga Clouds Kijembe Cha Kiutu Uzima

$
0
0
Katika kipindi cha D'wikend chat show cha clouds TV, ameulizwa " Meneja wako Sallam analalamikiwa yupo too hasrh and over protective to you. Unalizungumziaje?". Amejibu " Sallam yupo kwa ajili ya kulinda brand...kuna watu ukishakuwa na jina wa nataka wakutumia wakitumie bure halafu ukishuka wanakuacha wanafuata MTU mwqingine na mifano IPO..."Amerudia sentensi hiyo mara mbili. Kwa maoni yangu .Hili ni dongo la kiutu uzima kwa Clouds na Ruge

Rapper Witness: Nimechora Tatoo Kiunoni ili Nisichepuke

$
0
0
Mwanamuziki wa muziki wa kufoka foka nchini Tanzania, Witness, a.k.a Witness kibonge Mwepesi, ameelezea sababu ya kuchora tattoo yenye jina la mpenzi wake wa sasa Ochu Sheggy katika kiuno chake.

Akizungumza ndani ya eNewz amesema “Ukiweka tattoo sehemu niliyoweka mimi inazuia hata unapotaka kumsaliti mwenza wako yule unayekuwa naye ina kunyima hamu kabisa na anashindwa hata kukutamani tena”.

Pia aliendelea kusema kuwa watu wanadhani kuwa kuolewa ndiyo kumaliza kila kitu lakini kwa sehemu ambayo mapenzi yao yamefikia hakuna kitu ambacho anakihitaji tena kwa kuwa mapenzi ni kuungana mkono na Ochu anamsaidia katika kila kitu ninachofanya.

Diamond Akiri Mimba Ya Mobeto Kuharibika

$
0
0

BAADA ya ukimya wa muda mrefu kutawala kuhusu ujauzito alionao mrembo anayesumbua Bongo, Hamisa Mobeto, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibuka na kukiri kuwa mimba ya mrembo huyo imeharibika.

Diamond aliyekuwa akitajwa kuwa mhusika wa kiumbe hicho, alifunguka hayo kupitia Kipindi cha D’ Wikend Chart kinachorushwa na Runinga ya Clouds mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo pamoja na mambo mengine aliyozungumza, alikanusha taarifa za yeye kuwa mhusika lakini akakiri kwamba mrembo huyo alikuwa mjauzito na sasa mimba imeharibika.

“Mimi mwenyewe nilikuwa sijui kama ana mimba lakini ndiyo hivyo tena imeharibika so yupo kwenye wakati mgumu. Tumpe pole na tumpe pole pia aliyekuwa mhusika wa kiumbe hicho.

Mimi si mhusika bwana, hata wakati tunashuti naye Salome nilikuwa sijui kama ni mjamzito lakini ndiyo hivyo kwa sasa hatuna budi kumuombea arudi katika hali yake ya kawaida,” alisikika Diamond. Ijumaa Wikienda lilimvutia waya Mobeto ili kuweza kumsikia kama ana lolote kuhusu ishu hiyo, simu yake iliita bila majibu.

Ujauzito wa Mobeto ulikuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi waliamini mhusika ni Diamond kitendo ambacho kilisababisha maneno kumfikia mpenzi wa staa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ na kutibua hali ya hewa lakini kwa sasa mambo yako shwari baada ya Zari kuelewa kwamba Mobeto hana madhara.

JE, ni Maadili Baba Kumnunulia Bintiye ' Pedi ' na Kujua Kuwa Yupo Mwezini?

$
0
0
Siku hizi nimekuwa nikiwaona baadhi ya akina Baba ambao binafsi nawaita wa ' hovyo hovyo ' wakija na Mabinti zao tena wakubwa tu Madukani na hasa katika Supermarkets mbalimbali na kuwanunulia ' Pedi ' tena kuna wakati unakuta ' Li Dingi ' hilo hilo bila hata chembe ya aibu linamchangulia ' Bintiye ' aina ya ' taulo ' za kutumia.

Kama hii haitoshi hivi punde tu wakati na Mimi nikipanda Mti wangu nilioubatiza ' Le Mathematicien GENTAMYCINE ' niliweza kumsikia ' mubashara ' kabisa Baba mmoja akiongea na Simu na Mtu mwingine kuwa akimaliza tu kupanda Mti anataka kupitia dukani kumnunulia ' Bintiye ' taulo za Kike ' Pedi ' kwani alipotoka tu nyumbani kwake asubuhi hii alivyomuona tu alihisi kuwa ameanza safari yake ya kwenda ' Moon '.

Najua humu kuna akina Mama zetu na Wazee wenye MAADILI kabisa hivi haya mambo ya ' hovyo hovyo ' wayafanyayo Wazazi wa siku hizi hasa wa Kiume kwa Mabinti zao hususan kuwanunulia ' Pedi ' na kujua kuwa wapo ' Moon ' wamerithi kwenu nikimaanisha kuwa na nyie huko nyuma mlikuwa mkifanyiwa hivi au ni ' Uzungu ' tu umetuharibu na tunakosa maadili na kujua mipaka ya Baba juu ya Binti yake ambaye ni mkubwa na ameshavunja Ungo?

Badilikeni Wanaume wenzangu na akina Baba na jifunzeni kujua mipaka yenu hasa kwa Mabinti zenu.

Asubuhi na Jumamosi njema nyote.

Tahadhari Kwa Wadada Mnaopenda Kuvaa Shanga Kiunoni...

$
0
0
Bwana Yesu asifiwe!!!

Wanawake wengi wanapenda kuvaa shanga kiunoni wakiamini zinawavutia wanaume wengi katika mapenzi.

Napenda kutoa tahadhali kwa wanaopenda kuzivaa hasa kiunoni kuwa asilimia 80% ya shanga zinazouzwa zikiwa zimeshasokotwa zinatengenezwa na waganga WA kienyeji au watu ambao ni mawakala WA shetani na kuzinuizia mapepo kwa malengo yafuatayo:


Kuharibu au kuiba nyota za watu
Kuwafunga wanawake uzazi
Kuwaunganisha na mtandao WA kuzimu
Kuvuruga mfumo WA hedhi WA wanawake
Kuwafanya wanawake kuwa makahaba, kwa sbb unatamani kukutana na wanaume wengi ili wakujue km unavaa shanga na unazitumia
Kuwafunga kimafanikio
Kuwafanya wasidumu kwny ndoa wanapoolewa.
Kuwafanya wafikirie ngono zaidi.


Sasa unaweza usinunue kwa mganga lakn aliyetengeneza ni mganga au agent WA shetani.

Ww unaweza kununua kwa MTU na ukamwona WA kawaida, au yeye anaeuza yamkini hajui lakn alyetengeneza alikuwa na kusudi.

Unahitaji kuwa makini sana Dada zangu na vitu vinavyovaliwa sirini.

Ni unaponunua ukazikomboa kwa damu ya Yesu ili kufuta Yale maagano na manuizo yalyoambatanishwa nayo.

Nami ninazikomboa kwa mamlaka ya Jina la Yesu kwa yeyote mwenye nazo nafuta manuizo yote kwa Damu ya Yesu, km unazo TYPE AMEN.

By Illovo

(VIDEO) INAUMA SANA: Msikie Anavyosimulia Jinsi Alivyotobolewa Macho Na “Scorpion”

$
0
0
Tazama jinsi kijana Saidi Ali akielezea namna alivyovamiwa na kutobolewa macho hadharani, aliyemtendea unyama huo wa kutisha ni Salum Mpepe maarufu kwa jina la Scorpion. Video:

Jamhuri Kiwelu Julio Ametangaza Rasmi Kuachana na Kazi ya Ukocha

$
0
0
Kocha wa klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga Jamhuri Kiwelu Julio, October 2 2016 ametangaza kujiuzulu kufundisha soka la nchini Tanzania kufuatia kutoridhishwa na maamuzi yanayofanywa na marefa uamuzi huo umeonekana kuwashtua walio wengi, hiyo ni baada ya kupata kichapo kutoka kwa Mbeya City akiwa katika uwanja Sokoine Mbeya kwa kupoteza kwa goli 1-0.

Jamhuri Kiwelu Julio baada ya mechi hiyo aliongea na waandishi wa habari na kusema kuwa saivi atakuwa anaenda kuangalia mpira uwanjani ila hawezi tena kuwa kocha wa mpira Tanzania.

“Kuanzia leo na kuendelea, sitaki tena mpira. Najiuzulu mpira moja kwa moja sitaki kwasababu mpira wa Tanzania unachezwa kwa siasa sana. Mpira unachezwa kwa ajili ya kufurahisha watu hata wasiokuwa na uwezo waonekane wanajua, hiki kitu kinaumiza sana”, amesema Julio baada ya mchezo kati ya Mbeya City vs Mwadui uliomalizika kwa vijana wa Julio kulala kwa bao 1-0 ugenini.

“Nimeshafundisha mpira Qatar, Yemen na Dubai lakini sijawahi kufeli lakini kuna kundi la watu wanajua huyu ukimfanyia hivi unamharibia ni kuharibu mpira wetu ndio maana vilabu vyetu vikienda kwenye mashindano ya kimataifa havifanyi vizuri.”

“Kwahiyo kuanzia sasahivi natangaza sitaki kuwa kocha wa mpira wa Tanzania tena labda nikipenda niwe naenda kuangalia mpira lakini kinyume cha hapo sitaki mpira kwasababu tunakoelekea siko. Kuna watu watasikitika kutoka kwangu kwenye mpira lakini kwa kipindi hiki bora nipumzike nifanye kazi nyingine kwanza, mawashuru watanzania wote waliokuwa karibu na Julio.”

Diamond Azungumzia Ugomvi wa Zari na Mama yake na Michepuko

$
0
0
Diamond platnumz amesema hakuna ugomvi ndani ya familia yao kati ya mama yake, dada yake na Zari ila mashabiki ndio wanaokuza kwa kuwa wana IQ ndogo ya kutafsiri kinachopostiwa mtandaoni na watu hao
Kuhusu kuwa na mahusiano na wasichana wengine amedi kuwa watu wanadi hivyo kwa kuwa kila wakimuona na msichana mzuri wanafikiri anapiga kwa kuwa wao wana mazoea ya kupiga kila msichana mzuri

Mgogoro wa Uongozi Unaofukuta ndani ya CUF Unaendelea Kuchukua sura Mpya

$
0
0
Mgogoro wa Uongozi unaofukuta ndani ya Chama cha wananchi CUF unaendelea kuchukua sura Mpya baada ya kamati ya Uongozi ya chama hicho kutotambua mabadiliko ya kurugenzi ya chama hicho yaliyofanywa na M/kiti wa Cuf Prof Ibrahim lipumba ambaye alivuliwa madaraka na Baraza la Uongozi la Cuf hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dsm M/kiti wa kamati hiyo Julius Mtatiro amesema mabadiliko hayo hawayatambui huku pia wakishutumu msajili wa vyama vya siasa kwa kumtambua Prof.Lipumba kama m/kiti halali wa CUF kwa madai tayari wameshamvua uanachama.

Wabunge wa chama hicho wameomba kukutana na msajili wa vyama vya siasa kwa ajili ya kuzungumzia mgogoro huo.

Polisi yamtia mbaroni askari aliyechukua rushwa kutoka kwa raia wa kigeni Zanzibar.

$
0
0
Jeshi la Polisi Zanzibar limemkamata askari wake anayetuhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa raia wa kigeni baada ya kumkamata kwa kosa la barabarani na kumuachia huku akimuahidi kumlinda.

Uamuzi huo wa jeshi la polisi Zanzibar umetolewa na kamishna mkuu wa jeshi hilo hapa Zanziabr CP Hamdan Omar Makame wakati akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya polisi ambapo amesema jeshi la polisi limesikitishwa sana na kulani kitendo hicho cha askari huyo akipokea rushwa kwa kosa la raia huyo kutovaa mkanda na kitendo hicho kusambazwa kwenye mitandao ambapo amemtaja askari huyo ni sajeti Talib Hamad na siyo jina la Ali huku pia akisema kitendo hicho kilifanyika Mkokotoni na sio Mahonda kama alivyokaririwa askari huyo kwenye mahojiano ya mtandao.

Kamishna mkuu huyo wa polisi Zanzibar amesema kwa sasa askari huyo atachukuliwa hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za kipolisi na ikithibitika kuwepo kosa la jinai atapelekwa kwenye vyombo vya sheria vya dola huku na akisisitiza wananchi waendelea kutoa ushirikiano.

Kwa mujibu wa tukio hilo lilivyoonekana kwenye mtandao huo raia huyo alikamtwa kwa kosa la kutovaa mkanda wa gari na askari huyo aliamua kuchukua leseni ya barabara na kumuhakikishia kuwa aendele na safari na atamlinda huku akionekana akipokea fedha taslimu.

Mlinzi wa zamani wa Michael Jackson aiponda timu ya ulinzi ya Kim Kardashian, adai wasipokuwa makini atauawa

$
0
0
Mlinzi wa zamani wa Michael Jackson, ameiponda timu ya ulinzi ya Kim Kardashian, kuwa inabidi wawe makini kwasababu staa huyo anaweza kupigwa risasi katika umati wa watu kwakuwa anajulikana pengine zaidi hata ya Rais wa Marekani.

Matt Fiddes, aliyefanya kazi kama bodyguard wa MJ kwa miaka 10, anasema alishangazwa mno na majambazi waliopita kwenye mlango wa hoteli ya kifahari ya de Pourtalès alipokuwa anakaa Kim– achilia mbali kufika hadi chumbani kwake.


Kardashian alikuwa akilindwa na mlinzi wake mkuu, Pascal Duvier alipovamiwa na kutishiwa bunduki. Awali alikuwa na dada zake wawili walipokuwa wakijirusha kwenye klabu ya usiku.
Nyota huyo, 35, aliibiwa pete na mikufu ya thamani na watu hao waliokuwa na silaha, wakiwa na vinyago usoni na wakiwa wamevalia kama polisi.

Akizungumza na MailOnline,  bodyguard huyo wa zamani na gwiji wa sanaa ya mapigano, alisema: Watu pekee wa kuwalaumu, ni timu yake ya ulinzi. Ni mwanamke maarufu zaidi duniani, huenda akawa anajulikana kumzidi hata rais wa Marekani.

“Ana mamilioni ya mashabiki na anatakiwa kuwa na walinzi waliojiandaa. Nilipokuwa na Michael hilo lisingetokea. Majambazi lazima wangepita  kwenye mlango wa mbele, achilia mbali kwenda chumbani kwake,” alifafanua.

Akielezea jinsi alivyokuwa akifanya, alisema: Tungevikagua vyumba kabla hajaingia na kila muda alipoenda popote. Tungekuwa na watu mlangoni na mtu mwingine kwenye njia ya kwenda chumbani na hata kumwamsha kila baada ya saa tatu au nne kuangalia kama yuko sawa.”
“Yupo kwenye level sawa. Ni nyota mkubwa.”

Amedai kuwa shambulio jingine la mtu aliyemvamia hadharani Kim akitaka kumbusu makalio yake, lingekuwapa angalizo kubwa la kuweka mambo sawa.

Anadai kuwa Michael Jackson alikuwa na walinzi 50 hadi 60.

Walioua Watafiti Wakimbia Kijiji, Profesa Lipumba Apata Pigo...Magazeti ya leo

$
0
0


Walioua Watafiti Wakimbia Kijiji, Profesa Lipumba Apata Pigo...Magazeti ya leo

Profesa Lipumba Apata Pigo, Baraza la Wadhamini CUF Lagoma Kumtambua, Lapanga Kufunga Jengo la Chama

$
0
0
TAMKO LA BODI YA WADHAMINI YA THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – CHAMA CHA WANANCHI) KUFUATIA KIKAO CHAKE KILICHOFANYIKA JANA, TAREHE 2 OKTOBA, 2016

Kwa kuzingatia hali iliojitokeza katika chama chetu cha THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi) kufuatia hatua ya makusudi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kutupandikizia vurugu na fujo kwa kujipa mamlaka asiyokuwa nayo ya kutuamulia nani awe Mwenyekiti wa Chama, hatua ambayo imesababisha mtu anayeitwa Ibrahim Haruna Lipumba na genge lake tarehe 24 Septemba, 2016 kuvamia na kuhodhi jengo la Ofisi Kuu ya Chama iliyopo Buguruni, Dar es Salaam, Bodi ya Wadhamini ya Chama iliona kuna haja ya kukutana na kuchukua hatua za kukabiliana na matukio hayo.

Bodi ya Wadhamini ya The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) imefanya kikao chake, tarehe 2 Oktoba, 2016 katika Makao Makuu ya Chama, mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Abdallah Said Khatau.

Tumefanya hivyo kwa kutambua wajibu wetu kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Sura 258 ya Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Political Parties Act, Cap 258) na Katiba ya CUF ya 1992 (Toleo la 2014).

Ni vyema ieleweke kwamba kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kinapaswa kuunda Bodi ya Wadhamini ambayo ndiyo inayokuwa mmiliki na msimamizi wa mali zote za chama cha siasa husika. Kifungu cha 21 cha Sheria ya Vyama vya Siasa kinalieleza hilo kama ifuatavyo:

“21. —(1) Every political party which has obtained a certificate of full registration shall appoint a board of trustees to manage the properties and any business or investment of the party.

(2) Every board of trustees shall be duly incorporated under the Trustees Incorporation Act and every party shall, not later than sixty days from the date of full registration, submit to the Registrar—
a) the names and addresses of the members of ther board of trustees; and
b) a copy of the certificate of incorporation.”

CUF kilitimiza masharti hayo ya kisheria kwa kuunda Bodi ya Wadhamini, na Katiba ya Chama ya 1992 (Toleo la 2014), Ibara ya 98 ikafafanua zaidi namna inavyopatikana, pamoja na nguvu na uwezo wake kichama, kama ifuatavyo:

“98._ (1) Kutakuwa na Bodi ya Wadhamini ya Chama itakayoteuliwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kwa mujibu wa sheria za nchi kwa kipindi cha miaka mitano (5) na mjumbe anaweza kuteuliwa tena baada ya muda wake kumalizika.

(2) Bodi itakuwa na wajumbe wasiozidi tisa (9), watano (5) kutoka Bara angalau wawili (2) wakiwa ni wanawake na wanne (4) kutoka Zanzibar angalau mmoja (1) akiwa ni mwanamke ambao watateuliwa kwa masharti yanayohitajika ya Sheria ya Bodi ya Wadhamini na utaratibu uliowekwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

(3) Bodi ya Wadhamini itakuwa ndiyo mdhamini pekee wa fedha na mali za Chama pamoja na madeni na itafanya shughuli zake kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa na sheria ya nchi inayohusu Wadhamini.

(4) Bodi inaweza kushitaki au kushitakiwa kwa niaba ya Chama.

(5) Bodi itawajibika kwa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama ambalo linaweza kuweka utaratibu unaofaa wa kuendesha shughuli za Bodi hiyo, na itafanya vikao vyake angalau mara mbili kwa mwaka.

(6) Mwenyekiti na Naibu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini watachaguliwa na Wajumbe wa Bodi kutoka miongoni mwao, kwa sharti kwamba Mwenyekiti akitoka upande mmoja wa Jamhuri ya Muungano, Naibu Mwenyekiti atatoka upande mwengine wa Jamhuri ya Muungano.”

MAAMUZI YA BODI YA WADHAMINI:
Kufuatana na uwezo wake uliotajwa hapo juu na kwa kuzingatia nafasi yake kama mdhamini pekee wa fedha na mali za Chama (rejea Ibara ya 98(3) iliyotajwa hapo juu, Bodi ya Wadhamini imefikia maamuzi yafuatayo:

1. Imepuuza wito wa mtu anayeitwa Ibrahim Haruna Lipumba alioutangaza jana kwamba eti amemtaka mtu mwengine anayeitwa Thomas Malima kuitisha kikao cha Bodi ya Wadhamini. Lipumba kwa sasa si Mwenyekiti tena wa CUF na pia si mwanachama wa CUF baada ya kufukuzwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

2. Itaendelea kuwajibika kwa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama kama inavyotakiwa na Ibara ya 98(5) ambalo ndilo linaloiteua Bodi na litaheshimu maamuzi yote ya Baraza Kuu la Uongozi la Taifa likiwa ndiyo chombo chenye dhamana ya kusimamia uongozi na uendeshaji wa Chama.

3. Itachukua hatua za kisheria chini ya uwezo wake iliopewa na Ibara ya 98(3) na 98(4) kurejesha chini ya dhamana yake mali zote za Chama zilizovamiwa, kuporwa na kuhodhiwa na Ibrahim Lipumba na genge lake ikiwemo jengo la Ofisi Kuu ya Chama iliopo Buguruni, Dar es Salaam.

4. Itachukua hatua za kisheria chini ya uwezo wake iliopewa na Ibara ya 98(4) dhidi ya Ibrahim Lipumba kumtaka alipe gharama na hasara zote alizozisababisha kwa kuvamia Mkutano Mkuu Maalum wa Taifa wa Chama, tarehe 21 Agosti, 2016 katika Ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza na genge lake kufanya vurugu, ghasia na uharibifu wa mali za hoteli na hatimaye kuvuruga Mkutano Mkuu jambo lililosababisha hasara ya takriban Sh. 600 milioni; na kisha kuvamia Ofisi Kuu ya Chama, Buguruni, Dar es Salaam, tarehe 24 Septemba, 2016 ambapo alisababisha hasara ya takriban Sh. 50 milioni.

5. Itachukua hatua za kisheria chini ya uwezo wake iliopewa na Ibara ya 98(4) kwa kumshtaki Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kuingilia maamuzi halali ya vikao halali vya Chama na kulazimisha kukichagulia Chama chetu Mwenyekiti kinyume na onyo lililowahi kutolewa na Mahakama Kuu dhidi ya Ofisi yake kutokuwa na mamlaka ya aina hiyo.

6. Inawahakikishia wanachama wote wa CUF wa Tanzania Bara na Zanzibar kwamba Bodi yao ya Wadhamini iko makini na itasimama pamoja nao kulinda mali zote za Chama.

7. Inaionya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa iwache kuingilia mambo ya ndani ya uongozi na uendeshaji wa Chama cha CUF.

HAKI SAWA KWA WOTE

Abdallah Said Khatau
MWENYEKITI WA BODI

Joran Lwehabura Bashange
KATIBU WA BODI

Mastaa 10 Wadaiwa Kuanika Miili Yao Kunasa Wanaume!

$
0
0
Hali ngumu na raha ya ubuyu usimung’unye mwenyewe! Ishu inayotrendi kwa sasa kwenye ulimwengu wa ubuyu wa mjini ni aibu ya baadhi ya mastaa wa kike Bongo kudaiwa kuwanasa wanaume mtandaoni kwa njia ya picha zinazoonesha sehemu kubwa ya miili yao.


Kufuatia ishu hiyo, kumeibuka malalamiko kwamba, picha hizo haziishii tu mitandaoni bali zinawafikia hata watoto wao na kumomonyoa maadili ya Kitanzania kwani baadhi ya watu, wakishavutiwa nazo, huzichukua na kutumiana kwenye simu hivyo kusambaa kwa watu wengi zaidi.

Chanzo makini ambacho ni mfuatiliaji wa karibu wa ishu za mastaa kimeeleza kwamba, baadhi ya mastaa hao wamekuwa wakisingizia kuwa wanatangaza nguo hasa za ndani ndiyo maana huvaa kihasara.



UGUMU WA MAISHA?
Lakini nyuma ya pazia, inadaiwa kuwa kutokana na ugumu wa maisha kwa sasa, ndiyo mbinu mpya ya kujipiga promo kwa ajili ya kujiuza kwa wanaume ambao huwatafuta baada ya kuona picha hizo. “Ninyi hamjui tu! Kama hamuamini, chunguzeni, wasichana kibao wa mjini pamoja na baadhi ya mastaa wamebuni njia rahisi ya kujiuza mitandaoni. “Wanachokifanya ni kwenda studio na kupiga picha kali zinazoonesha maungo yao kisha wanatupia mitandaoni.

WAWILI WATANGAZA MAFANIKIO
“Kuna wawili (mastaa) ambao ni marafiki zangu, wanasema wamefanikiwa kupata dau kubwa kwa siku kutoka kwa wanaume kwa sababu tu ya kujipigia promo wenyewe,” kilimwaga ubuyu chanzo hicho.


WALIOTAJWA HAWA HAPA
Baadhi ya mastaa wanaotajwa kujipigia promo kwa wanaume ni pamoja na Isabela Mpanda ‘Bella’, Hamisa Mobeto, Gift Stanford ‘Gigy Money’, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Husna Maulid, Faiza Ally Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’, Mwanaisha Said ‘Dyna’ na Tunda Sebastian.
.

UBUYU YABAINI KITU
Kufuatia sakata hilo, Kona ya Ubuyu Ulionyooka ilizungumza na baadhi ya mastaa waliotajwa ambapo wapo waliokiri kuwa, biashara hiyo inalipa zaidi kwani haina gharama lakini pia walidai kuwa kila mtu ana maisha yake na anajua anapopatia mkate wake wa siku bila kujali kujiondolea utu.



MSIKIE GIGY:

“Kama inalipa, haimhusu mtu, ninachojua ni kweli wapo wanawake wengi wanaojiuza, cha muhimu ni kujua dau lako na siyo kufuatilia maisha ya wengine, mimi naishi maisha yangu.

” HUYU HAPA BELLA
Kwa upande wake Bella alifunguka kuwa, yeye si wale waliopo kwenye kundi hilo ila anapenda tu kupiga picha hizo kwa sababu ya mwili alionao na pia ikumbukwe kuwa aliwahi kuwa miss na kazi yake ya muziki na uigizaji vinamruhusu.


TUNDA ANAFUNGUKA:
“Mimi napenda kufanya nitakacho, siangalii watu wanataka nini ILIMRADI ni ukurasa wangu, siwezi kuzuiwa kufanya lolote. Kuhusu wanaume, hata wakija wengi huwa nawapotezea tu na wala hawajakosea kwa sababu wapo wanaodhani tunapiga picha kwa ajili hiyo na kutuma komenti kibao.” Hao ni baadhi ya mastaa waliopatikana na kupewa nafasi ya kujitetea lakini katika uchunguzi wa Wikienda, ilibainika kuwa wengi wanaoweka picha hizo, lengo lao huwa ni kutangaza nguo kama walivyowahi kujitetea Hamisa Mobeto, Lulu na wengineo.

NENO LA MHARIRI
Siyo hukumu ya Wikienda wala msomaji wake kuwa mastaa wanaotajwa ni kweli kwamba wanajiuza kwa njia hiyo lakini kama kweli wanafanya hivyo, wanapaswa kujiheshimu kabla ya kuumbuliwa kwani kila mmoja anajua kwamba tukimvalia njuga tutamuumbua.

Kama ni suala la matangazo ya nguo, basi wafanye matangazo kwa wakati kisha kujiweka kiheshima na siyo kila nukta kutupia picha za nusu utupu. Pia kama ishu ni kukosa wachumba, wakumbuke kuwa ndani ya mitandao hiyohiyo kuna uwezekano wa kuwepo kwa wachumba na wakwe hivyo ni rahisi kupoteza sifa za mke bora.

Vodacom Tanzania Kuendelea na Gulio la Simu-Janja Kwa Bei Nafuu Kupitia Kampeni Mpya ya Banduka Kijanja

$
0
0
Kampuni ya simu za mkononi chini, Vodacom Tanzania baada ya kufanya gulio mwisho wa wiki iliyopita ambapo simu imara ziliuzwa kwa bei nafuu kuwahi kutokea. Kampuni hiyo inaendelea kuwawezesha Watanzania kumiliki simu imara kwa bei nafuu kwa kuendelea na gulio katika maduka yao “Hatutoacha hadi kila Mtanzania awe ameunganishwa” kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao.

Kwa taarifa tulizonazo ni kwamba simu zinazopatikana ni pamoja na Smart 7, SmartKicka, Tecno, Itel na Huawei. Mteja akifika dukani kwa ajili ya kununua simu mojawapo ya simu hizi anatakiwa kununua kifurushi tu atapatiwa simu ya kijanja na orijino kulingana na kifurushi alichonunua. Mfano, mteja akinunua kifurushi chenye dakika 1,400, SMS 10,000 na 5GB za intaneti atapewa Smart 7 BURE kabisa.

Simu zote zitakuwa zimeunganishwa na intaneti ambapo mitandao kama Facebook, Twitter, WhatsApp, Snapchat na Instagram tayari zimeingizwa kwenye simu. Unaweza kutembelea kurasa za Vodacom Tanzania za mitandao ya kijamii kufahamu zaidi au duka la Vodacom lililo karibu yako

Baada ya Kuachana na Mbunge wa Donge,Wastara Arudiana na Mpenzi Wake wa Zamani

$
0
0
Mwigizaji Wastara aliwahi kuingia kwenye vichwa vya habari Tanzania kutokana na ndoa yake kuvunjika ndani ya siku 80 akiwa kaolewa na Mbunge wa Zanzibar.

Kabla ya ndoa hiyo Wastara alikuwa kwenye uhusiano na mshikaji ambaye ni staa wa Bongo Movie pia ambaye anaitwa Bondi, sasa basi baada ya taarifa kuenea katika mitandao mbalimbali kwamba amerudiana na Bondi leo ameyazungumza haya juu ya taarifa hizo.

‘Unajua watu hawajui tulipotoka yule ni mtu wangu wa muda mrefu ni makosa yake tu alinikosea ndio sababu ya mimi kuachana naye na ndipo nikaamua kwenda Zanzibar kuolewa yakatokea yaliyotokea na sasa niko na Bondi yaani nimerudiana naye nimesamehe yaliyopita kwasasa tuna kama miezi miwili tangu turudiana katika uhusiano wetu’
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images