Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Kidoa Adai 'Anayenitaka Anifuate na Mabunda Yakutosha'

$
0
0
Staa anayepamba video za wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva a.k.a Video Queen, Asha Salum ‘Kidoa’ amefunguka kuwa malipo kidogo anayopata kutokana na kazi hiyo yamemfanya aamue kukaa pembeni na kugeukia uigizaji.

Akizungumza na Gumzo la Town la Mtanzania
Jumamosi, Kidoa amesema kwa sasa yupo bize zaidi katika uigizaji wa tamthilia na filamu mbalimbali.

Anasema: “Hakuna kitu kwenye u-Video Vixen, tunalipwa kidogo sana. Kwa sasa sitaki tena. Naweza kusema hakuna cha maana zaidi ya kuonekana… lakini kama mtu akija na pesa ya maana, naweza kushiriki kwenye video yake.”

Alipoulizwa pesa ya maana ni kiwango gani, haraka alisema: “Pesa ya kueleweka. Nimechoka kufanya kazi isiyokuwa na malengo, mtu akija na milioni yake, naingia mzigoni. Chini ya milioni moja, sishiriki video ya msanii kabisa.”

“Niseme ukweli, kwa sasa najivunia nimekuwa hot cake kwenye tamthilia… natafutwa sana na ninafanya kazi hata tano ilimradi tukubaliane.

“Ujue tamthilia na filamu wananilipa vizuri sana, pesa ambayo sijawahi kulipwa na ninahisi huko kwenye video za wasanii sikuwahi kufikiria kupata fedha kama hizi, ndiyo maana nimefumbuka macho na kuitambua thamani yangu,” anasema.

Anasema pamoja na kwamba kwa sasa amepata
mapokezi mazuri na makubwa kwenye tamthilia na filamu, awali walimgomea wakidhani hana kipaji.

“Mimi kipaji changu hasa ni uigizaji, sikuwa na ndoto za kuwa Video Vixen kabisa. Niliwafuata baadhi ya wasanii na watayarishaji wakubwa lakini walinitosha wakiamini labda sina kipaji, lakini leo hii wameona uwezo wangu wamenikubali.

“Siwezi kukataa kuwa video za wasanii wa
Bongo Fleva zimenisaidia, kwakweli zimenitoa lakini hazilipi. Maisha siyo kuonekana tu, lazima uwe na kitu unaingiza ndiyo utaona raha ya kazi,” anasema Kidoa ambaye video ya Akadumba ya msanii Ney wa Mitego ndiyo iliyomtambulisha.

-Mtanzania

Dogo Janja Ataka Kuoa..Madee Adai ni Dharau Kwake

$
0
0
Dogo Janja ambaye sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Kidebe’ amefunguka na kutangaza rasmi kuwa ana mpango wa kutaka kuoa na kusema kwamba muda si mrefu anaweza kuvuta jiko na kuweka ndani.

Dogo Janja alisema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo ambacho kilikuwa kinarushwa moja kwa moja kutokea Manzese na kusema kuwa suala hilo lipo kwenye mchakato ila ni kweli ana mpango wa kuoa muda si mrefu.

‘Yah ni kweli nataka kuoa muda si mrefu nitavuta jiko hivyo siwezi kusema ni lini ila suala hilo lipo kwenye mchakato” alisema Dogo Janja Kwa upande wa Madee ambaye ni mlezi wa Dogo Janja kimuziki na katika maisha ya kila siku alisema kuwa kitendo cha Dogo Janja kutaka kuoa kabla yake itakuwa kama dharau hivyo anapaswa kusikilizia kwanza mpaka yeye afanye mambo kwanza ndipo na yeye atangaze.

“Ha ha ha ha Dogo Janja kuoa kabla yangu itakuwa kama dharau aiseee anapaswa kusubiri kwanza mimi nifanikishe jambo hilo ndiyo yeye afuate” alisema Madee

DOWNLOAD Application ya SIASA HURU Kwenye Simu yako Kupata Habari za Siasa Kwa Urahisi

$
0
0
Kama wewe ni mpenzi wa Habari za Siasa basi hii ni habari njema kwako...Download Siasa Huru Application Kutoka Google Play Store Kwenye Simu yako itakurahisishia upataji wa Habari na Breaking News za Siasa kwa urahisi....

Bonyeza HAPA Kuinstall Kwenye Simu yako fasta....

Au Nenda Google Play Store Kwenye Simu yako Alafu Search 'Siasa Huru' Kisha Install

Saida Karoli " Nilitumiwa, Ukiona Ninapoishi Utasikitika

$
0
0
Saida Karoli anaogopa kugusa hata jani, akidhani
ni nyoka anayetaka kumng’ata

Ni kwasababu licha ya kufanya vizuri kimuziki
miaka kadhaa iliyopita, hakupata chochote na
bado anaishi katika mazingira magumu.
“Niliumizwa kuanzia mwanzo, ni vitu vichache
nilivyovipata, kama mkibahatika waandishi wa
habari wenye makamera na wakija kwangu
watashuti kulingana na nilivyo, wataona
mazingira ninayoishi ndipo watanzania watazidi
kufunguka zaidi,” Saida alimwambia mtangazaji
wa Jembe FM, Natty E.
Kwa sasa Saida Karoli anaishi jijini Mwanza. Hivi
karibuni amerejea tena kwenye midomo ya watu
baada ya Diamond kurudia wimbo wake Salome.

Bunge Uganda Laimwagia Sifa Tanzania

$
0
0
BUNGE la Uganda limeipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na Baraza la Maadili lenye nguvu kuliko nchi nyingine Afrika ambalo linashughulikia watumishi wa umma ikiwemo kupambana na vitendo vya rushwa.

Akizungumza katika mkutano kati ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ya Uganda na Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma jana Dar es Salaam, Kiongozi wa kamati hiyo, Jacob Oboth-Oboth alisema kuwa katika nchi za Afrika, Tanzania pekee ndio lenye baraza imara na kwamba huenda Nigeria ndio inafuata.

Oboth ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Budama Kusini Wilaya ya Tororo, Uganda, alisema sababu ya kuja nchini ni kujifunza namna sekretarieti hiyo inavyofanya kazi kutokana na kupewa meno na sheria iliyopo kwenye Katiba.

"Uganda tuna mpango wa kufanya marekebisho ya sheria iliyotungwa mwaka 2002 kwa lengo la kuwa na watumishi wawajibikaji na utawala bora na kwamba bila ya kujifunza hawawezi kujua uzoefu uliopo na namna ya kuondokana na changamoto hizo," alisema.

Kamishna wa Maadili ya Utumishi wa Umma nchini, Jaji Salome Kaganda alisema wabunge hao wa Uganda waliomba kuja kubadilishana uzoefu na Sekretarieti ya Maadili ya Tanzania ili kuona inavyofanya kazi.

"Tumewashauri kwamba baraza letu ni chanzo cha Katiba ya mwaka 1977 na makatazo yake yamebainishwa katika katiba. Mfano, mbunge akionekana na hatia kinyume na katiba, anapoteza sifa kwamba haruhusiwi kugombea kwa miaka mitano kupigwa faini au kupewa onyo," alisema Jaji Kaganda.

Alifafanua kuwa walichokuja kujifunza wabunge wa Uganda ni kutokana na sheria yao ya maadili kuwepo kwenye vitabu vya sheria pekee wakati kinachotakiwa, sheria itakayotungwa iendane na katiba yenyewe ili kuipa meno.

Wimbo wa Chura Kutoka Kwa Snura Sasa Ruksa Kupigwa Maredioni na Kwenye TV

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemruhusu msanii wa muziki, Snura Anthony Mushi ‘Snura’ kuachia video yake mpya ya wimbo ‘Chura’ baada ya msanii huyo kufanya marekebisho ya video ya wimbo huo na kukubaliwa na wizara.

Aidha, katika barua ya wizara imemtaka Snura kuomba radhi mbele ya waandishi wa habari ili video hiyo ianze kuchezwa. Mapema mwaka huu video ya wimbo huo ulitangazwa kufungiwa na serikali baada ya video hiyo kukosa maadili ya kitanzania.

Akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Maisha Basement jijini Dar es salaam, Snura amesema anamshukuru Mh waziri Nape Moses Nnauye kwa kumkubalia ombi lake la kuiruhusu kazi hiyo kutoka.

“Mh Nape ameuruhusu wimbo wangu mpya wa Chura na video Chura kupigwa na kuonyeshwa katika vituo mbali mbali vya radio na runinga baada ya kuona video yangu mpya ya wimbo ina maadili na ujumbe ndani yake ikiwa ni kukidhi makubaliano ya awali kwamba wimbo wangu ‘Chura’ utafunguliwa pale nitakapofanya video mpya ya muziki yenye maadili ya kitanzania,” alisema Snura.

Aliongeza, “Video yangu mpya Chura inaeleza maana halisi ya neno Chura. Chura ninayemzungumzia ni mwanamke anayeruka ruka katika mahusiano kwa kubadilisha wanaume mbalimbali matokeo yake kupata magonjwa sugu,”.

Pia katika barua hiyo ya Mh Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amempa onyo kali msanii huyo kutokurudia kufanya tena video zisiyokuwa na maadili ya kitanzania.

Paul James ‘PJ’ arejea Clouds FM

$
0
0
Paul James ‘PJ’ amerejea tena Clouds FM akitokea EFM. Anakuwa mtangazaji wa pili wa EFM kuchukuliwa na Clouds katika kipindi cha mwezi mmoja, baada ya Kicheko.

PJ aliyeondoka Clouds mwanzoni mwa mwaka huu akiwa na Gerald Hando, ametambulishwa rasmi Jumatano hii. Anamfuata mtangazaji mwingine aliyehama Clouds akaenda EFM na kisha kurejea tena kwenye kituo hicho, Gardiner G Habash.

Mtangazaji huyo anayesifika kwa uhodari wa kuchambua magazeti, alikuwa na mchango mkubwa wa kukifanya kipindi cha Joto la Asubuhi cha EFM kujipatia umaarufu ndani ya muda mfupi. Kupokonywa kwa PJ EFM kunachocheza zaidi uhasama kati yake na Clouds FM.

VIDEO: Utani wa Mchekeshaji Eric Omondi Kwa Wanaotaka Kuwa Kama Rais Magufuli

$
0
0
Eric Omondi raia wa Kenya ambaye ni moja kati ya watu waliobarikiwa vipaji vingi ikiwemo uwezo binafsi wa kuchekesha kupitia maneno na mwili wake pia.

Baada ya kufanya ile ya mambo ya kuzingatia kwa wale wanaotaka kuwa kama Diamond Platnumz, Akothee, leo katusogezea nyingine ambayo inamhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli. Eric Omondi katuletea mambo muhimu unapaswa kuyazingatia kama unatamani kuwa kama Rais Magufuli

Unaweza kumtazama Omondi kwenye hii video hapa chini…

Wimbo ya Salome Waongoza Kwa Kununuliwa Huko Kenya Kati ya Nyimbo 100

$
0
0
Wimbo wa salome ulioimbwa kwa kukutanisha mafundi wawili kutokea lebo ya WCB Diamond Platnumz AKA Simba Jini na Rayvanny umekimbiza ile mbaya huku nchini Kenya kwa kushika namba moja kati ya nyimbo 100 bora zinazoongoza kwa kununuliwa huko Kenya

Daaaah kubaaabeki WCB sio watu wa mchezo mchezo bhana aisee kila wimbo wanaoutoa ni hit song tofauti na kina naniliu

BSS Kuna Uchawi Gani? Mbona Wengi Hawafanikiwi?

$
0
0
Waungwana leo kwenye pita pita yangu nilikutana na miongoni mwa washiriki wa BSS aliyekuwa miongoni mwa waliofanya vizuri (jina kapuni) akiwa kachoka sana mpaka nikamuonea huruma, sasa nikawa najiuliza hivi hili shindano lina manufaa gani? Kwa nini washiriki wengi hawafanikiwi na majina yao hufifia baada ya muda mfupi?

Tuchukulie mfano mtu kama Jumanne Idd mpaka leo hajulikani halipo alkadharika Walter Chilambo, Kayumba , AngelMarry Kato , Steven Lupenza, Nasibu Fonabo nk ni miongoni mwa vijana ambao wana uwezo mkubwa sana wa kuimba lakini cha ajabu hawafanikiwi kulinganisha na washiriki wengine kama vile Harmonize ingawa alitoka mapema na kuonekana si chochote leo hii katudhihirishia kwamba yeye ana uwezo gani....

By Hance mtanashati


Jibu la Mdau

Kwanza ni jambo la kujiridhisha kuwa si BSS tuu bali hata huko nje shows kama za the voice, SA idols, xfactors, na Got talents za nchi nyingi, ni watu wachache sana walio shinda mashindano ya aina hii wame make ki muzik.
Kwanini!!?
1. Lengo la mashindano, waandaji huwa wanaandaa kwa ajili ya faida yao na kupata wadhamini, na mara nyingi wakisha maliza shindano hawawekezi kwa nguvu kubwa kwani kuna shindano la mwakani inabidi waandae tena, hawana time na wewe
Pia washindanaji lengo lao kubwa zaidi ni kupata yale mamilioni tuu, wakisha pewa kuna msemo unasema easy come easy go
2. Mashabiki wa mashindano, askudanganye mtu, watanzania wanao fuatilia BSS ni chini ya milioni 10, wanao piga kura ni chini ya laki moja, kwa hiyo kama msanii ukishinda unakuwa hujapata fan base kubwa bado isipo kuwa ki portion kidooogoo cha wale walio angalia na wakajisumbua hata kupiga kura,,na wengi wanai piga kura huwa wanaanza kwanza kukuonea huruma ya kimaisha mfano unakumbuka Jumaanne Idd kwa hiyo Raymond akitoa wimbo mmoja uka hit anapata fan base kubwa kuliko wewe mshindi
3. Mziki ni zaidi ya kukopi nyimbo za watu, angalia yule mshindi wa mwaka jana kayumba alishnda kwa kuimba imba taarab za kina isha mashauz sasa je akitoka BSS ana uweza huo mziki!!? Mpaka yeye mwenyewe hajui afanyeje yaani

*Sababu ni nyingi lakini kikubwa ni wasanii wajiamini wahue uwezo wao ni zaid ya kuimba BSS, ndio maana mara nyingi unakuta wanao fanikiwa ndio wale walio shika u tano, au ukumi, kwa kuwa it takes more than to win BSS ili kuwa msanii

By Ice Man 3D

Diamond Afunguka Haya Kuhusu Issue ya Mama yake Kutopost Picha ya Zari Siku ya Kuzaliwa Kwake

$
0
0
Habari za kuwepo kwa bifu kati ya Mama mzazi wa Nassib Abduli aka Diamond Platnumz na Zari ambayeni mpenzi wa msanii huyo na Mama wa mtoto wake wa kwanza zilichukua sura mpya.

Mwezi uliopita baada ya Mama mzazi huyo kutopost picha ya Zari kwenye BirthDay yake na kuja kupost picha ya Wema Sepetu akimtakia Birth Day njema.

Kwenye The Playlist ya Times FM, Diamond aliulizwa swali hilo ambapo alifunguka kwa kusema kuwa inabidi ifike mahala kuwa wawape watu kitu cha kuzungumza kwakuwa kibongo bongo familia yao inatizamwa kama ya kina Kardashian.

“Sisi ndio pambo la mitandao, Mtu akiamka lazima aingie kwenye familia ya kina Diamond ajue inafanya nini, ni familia ambayo ina mshikamano na ipo kibiashara zaidi”.
“Inabidi tuwape watu vitu vya kuzungumza zaidi, Kila kinachofanyika kinafanyika kwa makusudi na Mama yangu na Zari wanaelewana sana, ndio maana Zari yupo Tanzania kwa sasa”

Jinsi ya Kumtuliza Mumeo Asitoke Weekend

$
0
0
Siku hizi wa naume licha ya kukimbia nyumba zao kwa kisingizio cha kazi maajabu weekend hasa Jumamosi utasikia wanaaga nafika hapo njiani naja naenda kununua gazeti.

Kumbe wanaenda kunywa supu na mambo mengine unasubiri wee mpaka alasiri au jioni

Hivyo wanandoa wengi hili limekuwa tatizo mwanaume kiguu na njia asb mchana na njia kumuacha mama na watoto.

Nini kifanyike hasa weekenda Mwanaume ashinde NYUMBANI akikupumzikia??

Zipo njia nyingi mojawapo SUPU YA WEEKEND NA MAZUNGUMZO NA MKAO

Ni kweli wanawake wengi hamjuagi kuwakalisha waume home.

Anza hivi
Siku uko home wewe amka mapema kabla yake anza makeke jikoni…

Mara blenda priiiii… juice… ama milk shake…. hahahaha..Utaona anasogea jikoni..

Wakati anakunywa juice ama milk shake…Anza kukuna nazi…

Chambua mnafu…

Hapo jikoni kuna kanyama kanachemka… katia kitunguu tupia viazi 2 na ndizi.Hahaha..

ile harufu ikianza kutoka utasikia anafuata maji jikoni… hahahaha kwenye friji… wala hatumi..

Hahaahha… utasikia nini kiko jikoni?Hahahaa.

Mmiminie supu…

Na ndizi mbili na kiazi kimoja kapilipili mbuzi pembeni..

Muulize kuna chapati…Mpe.. hahahahaha..Akimaliza supu nakuapia atasinzia..

.Akishtuka ugali na mnafu na nyama umeiva…Mpe ale..Mshushie na glass ya mtindi…Hahahaha..

analewa full Hata kama kuna mama junior anaambiwa usipige…

Hahahahahaha….Baada ya hapo acha apumzike… aoge…

Kisha funga ka khanga kako kepesi jilaze pembeni.. woiiiiiiiii..



Mkimaliza muombe pesa ya sokoni…

NAKUAPIA HATA KAMA JANA YAKE ALIKUPA ATAKUPA TENA.

Hahahahaha.. jamani…

Hahahahaha… yani kwa raha ya supu… nakuapia utaambiwa hata mama alipiga simu jana… hahahaha.. ama utasikia mamii.. njoo uone njoo… unaitiwa kitu cha kwenye tv.. hahaha.

Hata hujaona mwanzo ila kwa raha yakasupu utaitwa…

Hata kama huna kalio nakuambia utapigwa kibao hata cha mgongo…. hahahahahahahahahaha.

Sasa wewe unaamka chai na mkate kama chuo cha uhazili…
Wali maharage kama jeshi...

Hii ndo Sababu Inayomfanya Mwanamuziki Diamond Asishiriki Fiesta 2016

$
0
0
Hatimaye Diamond ametoa sababu ya kutopanda jukwaa la fiesta 2016,Akihojiwa na kipindi cha jahazi cha clouds fm Diamond amesema kuwa ndoa (mkataba) yake na Kampuni ya Simu ya Vodacom ndio sababu inayomfanya asishiriki Fiesta mwaka huu...
Wadhamini wakuu wa Fiesta ni Tigo hivyo kufanya hivyo kungeleta mgongano wa maslahii....

Huyu Hapa Jambazi Scorpion Amtoboa Macho wa Buguruni Akiwa Chini ya Ulinzi wa Polisi

$
0
0
Pichani : Scorpion, mwenye fulana nyekundu, akiwa mahakamani leo chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Leo katika mahakama ya wilaya ya Ilala, mkazi wa buguruni kwa mnyamani anayetuhumiwa kuwachoma watu visu na kisha kuwatoboa macho, Salum Henjewele maarufu kama Scorpion amepandishwa kizimbani na kusomewa tena shtaka la unyang’anyi  wa kutumia silaha .

Kesi ya Scorpion, ambaye alikamatwa baada ya kumchoma visu na kisha kumtoboa macho, Said Ally mkazi wa mabibo Hostel, inasikilizwa na hakimu Adolf Sachore.
Leo kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upande wa mashtaka umeieleza mahakama kuwa upepelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na hivyo mtuhumiwa amerudishwa rumande

Maalim Seif na Lipumba Kukutanishwa Kumaliza Mgogoro wao

$
0
0
Wajumbe wa bodi chama cha wananchi CUF, wanaandaa utaratibu wa kuwakutanisha katibu mkuu wa chama hicho Maalim Seif na mwenyekiti wake, Prof.Ibrahim Lipumba ili kuwapatanisha kutokana na mgogoro ulioibuka na ambao unaendelea kukigawa chama hicho.


Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wajumbe hao wa CUF wanne kati ya watano kutoka Tanzania bara wamesema wanahuzunishwa na mgogoro ndani ya chama hicho.

Mjumbe wa bodi CUF,Peter Malebo ameeleza kuwa watawaita viongozi hao makao makuu ili waweze kupata suluhu na kumaliza mgogoo huo unao endelea.

“Ndio maana wenzetu wamekaaa Zanzibar kwa kurubuniwa wale wajumbe wa bodi,na sisi tumekaa hapa ilA sasa viongozi wetu wakuu tumuombe Maalif Seif pamoja na Profesa Lipumba,tutawaita waje hapa makao makuu na wajumbe wote wabodi tukae nao tumalize mgogoro wetu,” aliomba Malebo.

Hivi karibuni, baraza la uongozi la chama cha Wananchi (CUF), lilitangaza kumfukuza uanachama Lipumba. Alifukuzwa kwa kile kilichoelezwa kuwa amekwenda kinyume na katiba ya chama na kufanya uasi kwa wanachama.

Mrembo Amber Lulu Adaiwa Kukamatwa na Madawa ya Kulevya..Marafiki zake Wamkana Live

$
0
0
Mwanadada mrembo ambae amejipatia umaarufu mkubwa siku za karibuni kwa kutokea katika videos kadhaa za Bongo Fleva Amber Lulu inasemekana kwamba yuko chini ya usimamizi wa polisi kwa siku ya pili sasa.

Sababu ya kuwa chini ya Ulinzi inasemekana kuwa amekamatwa na Sembe (Madawa ya kulevya) huko Airport mkoani Arusha akijiandaa kuyasafirisha hadi nchini China.Gossip Cop Soudy brown alizinyaka taarifa hizo na akaona haitakuwa mbaya kama atapiga story na watu wa karibu wa mwanadada Amber Lulu ili kupata ukweli juu ya suala hilo.Ndipo alipomvutia waya Gigy Money. Mapovu yaliyomtoka mwanadada Gigy sio ya polepole, na kudai kuwa kimbelembele cha mwanadada Amber Lulu ndio kimemfanya kupata matatizo.

Soudy Brown hakuishia kwa Gigy tu, alimvutia waya na rapper Young Deeambaye kwa mujibu wa Gigy Money inasemekana kuwa ndiye boyfriend wa mwanadada Amber Lulu. Na Young Dee alikana kabisa kumjua mrembo huyo na akadai kuwa hajui chochote kinachoendelea kuhusiana na msichana huyo.

Ubuyu wote nimeukusanya hapa chini kwenye hii video unaweza kuitazama.

Ali Kiba Ataja Sababu iliyomfanya Asioe

$
0
0
Alikiba ameitaja sababu iliyomfanya ashindwe kumuoa mwanamke yeyote kati ya watatu aliozaa nao.

Hitmaker huyo wa Lupela alisema kuwa hakupenda kulazimisha iwe hivyo.“Unajua hauwezi kumuoa mtu kama hamuelewani.

"Nia yangu ilikuwa ni kustick na kila mama wa mtoto wangu toka nilipoanza. Lakini mambo yanaenda tofauti, huenda tunapogombana anatafuta mtu mwingine,” anasema Kiba.“Kwahiyo hautakiwi kuforce mapenzi, mimi nataka nikae na mtu ambaye tutaelewana,” ameongeza.

Alikiba ana watoto wawili wa kike, Amiya Kiba, Chamy Kiba na mmoja wa kiume, Sameer Kiba. Wote ni watoto wa mama tofauti.

VIDEO ya Kusikitisha, Walimu Wakichangia Kumpiga Mwanafunzi Ofisini

$
0
0
Video hii ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia leo alfajiri inawaonyesha walimu wakichangia kumpiga mwanafunzi mmoja ndani ya ofisi.

Walimu hawa wanaonekana si tu wanampiga mwanafunzi huyo kwa viboko, bali wengine wanampiga makofi ya uso, huku walimu wengine wakiwasihi wamuache mwanafunzi huyo kwani wanaweza kumuumiza.

Haijaweza kufahamika mara moja jina la shule hii, lakini ni ya nchini Tanzania kwani ukutani inaonekana nembo ya serikali. Kwa yeyote anayefahamu anaweza kutuandikia hapa chini ili kuweza kuuhabarisha umma.

Tazama Hapa Video:

Waziri Ndalichako awatimua Chuo walimu wa mafunzo waliompiga mwanafunzi shule ya Kutwa Mbeya

$
0
0
Hatimaye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Ndalichako amewafukuza chuo walimu waliohusika na kumpiga mwanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya kutwa Mbeya.

Mpaka sasa Mkuu wa Shule na baadhi ya walimu wamefikishwa katika kituo cha polisi kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo.

Zitto Kabwe Awamwagia Sifa UKAWA ......Atia Neno Kuhusu Mgogoro wa CUF

$
0
0
Kiongozi Mkuu wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameisifia nguvu ya vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa kile walichokifanya hasa katika uchaguzi wa mwaka jana.

Akizungumza jana katika mahojiano maalum na kituo cha runinga cha Clouds TV, Zitto alisema kuwa chama chake hakiwezi kubeza nguvu kubwa iliyooneshwa na umoja huo na kwamba uliweka historia katika chaguzi zote zilizowahi kufanyika nchini.

“Ukawa umeweka historia Kubwa zaidi katika chaguzi za nchi yetu japo kuwa kuna madhaifu ila hatuwezi kupuuza nguvu ile,” alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini.

Hata hivyo, pamoja na kusifu nguvu ya muungano huo wa hivyo vya siasa ambavyo ni Chadema, Chama Cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD, Zitto alisisitiza kuwa chama chake hakitajiunga na umoja huo kutokana na maazimio na miiko waliyoiweka katika Azimio la Tabora la chama chake.

“Hatukuweza kujiunga na Ukawa kwasababu tuliweka kanuni zetu wazi  tulizozitangaza katika azimio la Tabora,” Zitto anakaririwa.

Katika hatua nyingine, Zitto alizungumzia mgogoro wa uenyekiti wa CUF unaoendelea ndani ya chama hicho na kutoa rai kwa vyama vingine vya siasa kutowafarakanisha.

Alisema kuwa CUF inapaswa kuachiwa suala hilo walimalize wenyewe katika vikao vyao vya ndani ya chama na sio vinginevyo.

Aliongeza kuwa kutokana na mgogoro unaoendelea ndani ya CUF, hivi sasa ajenda yao kubwa [kupinga kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Oktoba]imewekwa kando bali sasa wanatafuta uhalali wa kiongozi wa chama hicho.

“Rai yangu tusichochee kabisa mgogoro huu bali ni tuwe kama madaraja ya kufanikisha mgogoro huu kumalizimika kwa amani,” alisema.

Hata hivyo, mapema wiki hii Baraza Kuu la Uongozi wa CUF lilifungua shauri mahakamani kuhusu mgogoro wa uongozi ndani ya chama hicho, wakimshataki Msajili vya Vyama vya Siasa nchini pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

 Katika shauri hilo, wanapinga uamuzi wa Msajili kuandika barua ya kumtambua Profesa Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa chama hicho huku wakidai kuwa alijiuzulu na taarifa za kujiuzulu kwake waliziwasilisha kwa Msajili.

Baraza hilo limedai katika shauri hilo kuwa katiba na sheria ya vyama vya siasa haimpi mamlaka Msajili kuingilia maamuzi ya ndani ya vyama vya siasa. Shauri hilo bado halijaanza kusikilizwa.
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images