Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Maafa Tena Kagera: Ugali wa Sumu Waua Mama na Watoto Wanne

$
0
0
MAMA na watoto wake wanne wamefariki dunia katika Kijiji cha Kyebitembe wilayani Muleba mkoani Kagera, baada ya kula ugali unaosadikiwa kuwa na sumu.
Waliofariki dunia ni Julitha Julius (35), Haujeni (14), Superius (12), Julius (4) na Paschazia mwenye umri wa miezi sita.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamilanda, Trasias Baltromeo, alidai kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa tisa mchana.
Baltromeo alidai familia hiyo baada ya kumaliza kula walianza kutapika na walifariki dunia wakati wakipelekwa katika Kituo cha Afya cha Kimaya kilichoko jirani na kijiji hicho.

Alisema baada ya kula walianza kutapika na kuhangaika, hata hivyo wananchi walifika ili kutoa msaada wa kuokoa maisha yao lakini haukuzaa matunda ambapo walifariki.

ìNilipofika nilikuta hali si nzuri, nilikuta wakiwa wanatapika, hivyo nilitoa taarifa Kituo cha Polisi Kyebitembe ambapo walifika wakati wakiwa wanakimbizwa hospitali ndogo ya Kimeya ambapo mama yao na watoto wawili walifariki,îalisema.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Augustino Ollomi, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo na hakuna mtu aliyeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.
Ollomi alisema miili ya marehemu inafanyiwa uchunguzi na wataalamu wa afya ili kujiridhisha na kutambua aina ya sumu iliyowaua.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Richard Ruyango, alisema jopo la wataalamu wa afya na Jeshi la Polisi walikwenda katika Kituo cha Afya cha Kaigara na Hospitali ya Rubya kufanya uchunguzi.

Alisema baada ya kufanya uchunguzi watalaamu hao hawakuweza kubaini aina ya sumu iliyokuwepo katika chakula hicho, hivyo wamechukua sampuli kwa ajili ya kupelekwa Ofisi ya Mkemia Mkuu mkoani Dar es Salaam, kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Mkuu huyo alikemea vitendo vya mauaji vinavyofanyika katika tarafa ya Kimwani kwani hilo ni tukio la tatu kwa mujibu wa vyombo vya dola la familia kuwekewa sumu kwenye vyakula na watu kupoteza maisha.

ìKitendo hiki kinasikitisha cha kuondoa uhai wa mwezio na si mafundisho ya Mungu licha ya waliofanya hivyo kuwa miongoni mwa waumini wa kiroho kwani wangetumia sheria kushitakiana kama hakuna usalama,îalisema.

Ruyango alisema Jeshi la Polisi na kamati za ulinzi na usalama za kijiji na kata, zimepewa jukumu la kufanya uchunguzi na kubaini waliohusika ili wachukuliwe hatua za kisheria.

DOWNLOAD APP ya SIASA HURU Kwenye Smart Phone Yako Kupata Habari na Matukio ya Siasa Kirahisi

$
0
0

Install Android Application ya Siasa Huru Sasa Ipo Google Play Store , Fanya Kuinstall Kwenye Smart Phone yako kupata habari na Matukio ya Siasa kwa wakati...

Bonyeza HAPA Kuinstall 

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya SIASA HURU Kwenye Simu yako ili Kupata Habari zetu Haraka

Navy Kenzo waeleza jinsi ratiba ya AliKiba ilivyovuruga mipango yao

$
0
0
Wasanii wa Kundi la Navy Kenzo ameshindwa kuachia kwa wakati kolabo yao na AliKiba kutokana na mkali huyo wa wimbo ‘Aje’ kuwa busy hali ambayo imewafanya washindwe kumpata kwa ajili ya kushoot video.

Wakizungumza katika kipindi cha The Playlist cha Times FM Jumamosi hii, wasanii hao wamesema zaidi ya mara mbili walipanga kushoot video hiyo lakini wameshindwa kumpata msanii huyo.

“Kolabo na AliKiba ipo tayari kabisa lakini time table yake imekuwa ngumu,” alisema Aika “Mara ya pili tumepanga kushoot video lakini tumeshindwana kwa ajili ya yeye time table yake. So tukiona inazidii kuchelewa itabidi tuitoe kwa namna yoyote,”

Nahreel aliongeza, “Mara ya pili hii tumepanga kutaka kushoot video lakini yeye alikuwa yupo busy, labda safari hii tukienda MTV MAMA kama tukipata muda tunaweza kufanya kwa sababu kila kitu kipo tayari,”

Waimbaji hao wamesema plan yao ilikuwa nikuachia kolabo hiyo ikiwa na video.

Muna Afunguka Kumuingiza Wema Kwenye Madawa Ya Kulevya!

$
0
0
Mrembo aliyewahi kufanya vyema kwenye tasnia ya maigizo Bongo, Rose Alphonce ‘Muna’, amefungukia madai ya watu kumtuhumu kuwa amemwingiza shosti wake Wema Sepetu ‘Madam’ kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kwa kusema madai hayo hayana ukweli.

Akizungumza na paparazi wetu, Oktoba 5, mwaka huu, Muna alisema mbali na kumhusisha kumwingiza Wema kwenye madawa hayo, amekuwa pia akituhumiwa kuwa yupo kwenye orodha ya wabeba unga jambo ambalo halina ukweli wowote na kwamba watu wanajaribu kumharibia sifa yake kwa kuwa tu yupo karibu na Madam.


“Sijamuingiza Wema kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kama watu wanavyosema, mimi mwenyewe sijawahi kujihusisha na biashara hiyo wala kuwa kwenye matumizi ya dawa hizo.

“Wasifikirie ukaribu wangu na Wema ndiyo eti naweza kumfundisha vitu vya ajabu, kwanza Wema hajawahi kutumia wala kujihusisha na matumizi ya aina yoyote ile ya madawa ya kulevya na kama angekuwa anatumia dawa hizo, angekuwa ameshaharibikiwa.


“Mimi nina kampuni yangu (hakuitaja jina) najitahidi kuikuza kila siku ili tuweze kusonga mbele. Hata ninaposafiri mara nyingi ni kwa ajili ya kampuni yangu.

“Halafu kwanza Wema nimefahamiana naye akiwa mtu mzima na wala hakuwa mtoto hivyo suala la mimi kumuingiza kwenye mambo maovu siwezi zaidi najitahidi kumfanya awe mfanyabiashara mzuri ndiyo maana utaona siku hizi kila kukicha tunajitahidi kubuni shoo mbalimbali za kutuingizia kipato,” alisema Muna.

Kwa muda mrefu Muna amekuwa akitajwa kwenye biashara ya madawa ya kulevya huku madai hayo yakichagizwa na safari zake za mara kwa mara nje ya nchi zisizofahamika kwa haraka na kama haitoshi, mrembo huyo amekuwa akidaiwa kumfundisha Wema kuvuta ‘unga’ jambo ambalo Muna amesema halina ukweli wowote.

Aina Kumi Za Waume Ambao Wake Zao Wanakereka Kuwa Nao

$
0
0
Kila ndoa inachangamoto zake na maana halisi ya ndoa ni ule uwezo wa wanandoa kuvumiliana katika changamoto hizo. Kuna changamoto za kimungu ambazo wanandoa hawawezi kuziepuka lakini kuna zile za kiuanadamua mbazo nyingi ni za kimakusudi na mtu huamua tu kuwa hivyo. Katika kuangalia ndoa leo nimeona nichambue aina kumi za waume ambao wake zao wanakereka kuwa nao;

(1) Wanaojione Kama Wafalume (King Husband); HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea.

(2) Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband); Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake.

(3) Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband); Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke.

(4) Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband); Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida.

(5) Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband); Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao.

(6) Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband); Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wanawake, hawajali tena.

(7) Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband); Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwa na mke akifanya kosaa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwakifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa.

(8) Mume Mtalii (Visiting Husband); Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto.

(9) Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband); Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke.

(10) Mwanaume Mbahili (Miserly Husband); Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake.

Hiyo nji baadhi tu ya aina ya wanaume ambao wanawake wengi wasingependa kuwa nao. Kama mwanaume upo hivyo jua mke wako hafurahii na anavumilia tu. Ndoa ni furaha amua kubadilika na usimfanye mke wako kuishi na wewe kwa kujilazimisha. Kama ni mume jiulize uko namba ngapi hapo na kama ni mke mezea namba ya mumeo na jua hauko peke yako.

Mwanamke Aliyemnyofoa Ulimi Mwanaume Wakati Wakila Denda Afikishwa Mahakamani

$
0
0
Mwanamke anayedaiwa kumng’ata ulimi kijana Saidi Mnyambi (26) siku 28 zilizopita, kwa kile kilichodaiwa kutaka kufanya naye mapenzi kwa nguvu, hatimaye amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Singida.


Mwanamke huyo, Mwajabu Jumanne (36) mkazi wa eneo la Mandewa nje kidogo ya mji huu amefikishwa mbele ya Hakimu Flora Ndale akishitakiwa kwa kosa la kujeruhi kwa kunyofoa theluthi moja ya ulimi wa kijana Mnyambi wakati wakipeana denda.

Wakili wa Serikali, Michael Ng’hoboko alidai mbele ya hakimu Ndale kuwa Septemba 12 mwaka huu majira ya saa 2.45 usiku katika eneo la Mandewa Manispaa ya Singida, kwa makusudi, mama huyo alimng’ata ulimi Mnyambi na kumsababishia jeraha na maumivu makali.

Mwendesha mashitaka huyo alidai kuwa mshitakiwa Mwajabu alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 225 cha Kanuni ya adhabu Sura ya 16 Sheria za nchi kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mshitakiwa alikana kosa na kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 24 itakapotajwa tena.

Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana ya watu wawili waliotoa ahadi ya Sh milioni moja kila mmoja.

Source: Habari Leo

Zitto: CCM imechanganyikiwa

$
0
0
KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimechanganyikiwa na sasa kimepoteza mwelekeo wa kutatua matatizo makubwa yanayoikumba Tanzania hivi sasa.

Akizungumza katika Mkutano wa Kidemokrasia uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, Zitto alisema kuchanganyikiwa huko kwa CCM ndiko kunakosababisha serikali ya Rais John Magufuli iseme mengine na katika utekelezaji wake yafanyike mambo mengine.

“Tunatambua kuwa serikali ya Rais Magufuli imeweka mkazo katika kujenga viwanda. Hili ni jambo jema kwa kuwa likitekelezwa vizuri litachochea ukuaji wa ajira kwa vijana nchini. Hata hivyo, pamoja na nia njema, haielekei kwamba serikali ya CCM inaelewa namna ya kutelekeleza lengo hili zuri.

“Kutokana na mkanganyiko wa kifalsafa, serikali haijui ni nani hasa anapaswa kujenga viwanda kati ya serikali yenyewe na sekta binafsi. Matokeo yake imekuwa ikivizia miradi ya sekta binafsi na kukimbilia kuizindua wakati huo huo serikali ikitoa kauli ambazo zinarudisha nyuma ari ya wafanyabiashara wazalendo kuwekeza katika viwanda,” alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini.

Mkutano wa kidemokrasia ni kikao pekee rasmi cha kikatiba katika chama cha ACT- Wazalendo ambapo viongozi na wanachama wanakutana ana kwa ana na kubadilisha mawazo kuhusu chama na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Mkutano huo wa kwanza na wa aina yake hapa nchini umehudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka nchi na vyama marafiki kwa ajili ya kubadilisha uzoefu katika nyanja mbalimbali.

Zitto ambaye amekuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 15, alisema nchi sasa inahitaji mwelekeo, falsafa na namna mpya ya kutatua matatizo ya Tanzania; akisema CCM kwa sasa haina mwelekeo wowote – miaka takribani 25 baada ya kuachana na siasa ya Ujamaa na Kujitegemea.

Katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho, Posta, jijini Dar es Salaam, Zitto alitoa mifano ya masuala mbalimbali yahusuyo uchumi, ajira, jinsia na elimu kupitia hotuba yake iliyokuwa na maneno takribani 5000.

Kuhusu vita dhidi ya rushwa inayoendeshwa na serikali ya Rais Magufuli, Zitto alisema ACT kinaunga mkono juhudi hizo ingawa hadi sasa wanaoshughulikiwa ni mawakala wa rushwa walioko serikalini na si wala rushwa wenyewe.

Mwanasiasa huyo pia aliponda mwenendo wa serikali wa kuzuia shughuli mbalimbali za kisiasa na kusema hakuna namna ambayo nchi inaweza kupambana na ufisadi pasipo kujali misingi mingine ya haki za watu.

“Mtu yeyote anayedai kwamba anaweza kupambana na ufisadi na kuleta maedeleo kwa kukanyanga demokrasia na utawala wa sheria ni mwongo na anastahili kukataliwa na kukemewa mapema kabla hajaota pembe.

“Tunasisitiza kuwa mtu yeyote wa kawaida au kiongozi anayesema kwamba anaweza akapambana na ufisadi kwa kukanyaga misingi ya demokrasia na utawala wa sheria mtu huyo ni fisadi na anataka kujenga himaya mpya ya ufisadi. Mtu huyo, pamoja na mambo yake yote, yafaa akataliwe na kudharauliwa haraka,” alisema.

Katika hatua nyingine, Zitto alisema kwamba juhudi za kuboresha elimu hapa nchini zitakuwa na maana tu endapo walimu ndiyo watakuwa kipaumbele na si madawati wala madarasa. Alisema upatikanaji wa madawati na maabara utakuwa na maana tu endapo walimu watakuwa na motisha ya kufanya kazi.


“Tafiti zinaonyesha kwamba ili kuboresha ubora wa elimu kitu kikubwa na cha msingi kabisa kuliko vyote ni kuwekeza kwa walimu na taaluma ya ualimu. Maeneo muhimu ni mafunzo ya walimu na kuhakikisha kwamba wanakuwa na motisha wa kutosha katika kufanya kazi zao. Bahati mbaya hapa Tanzania serikali na jamii kwa ujumla hatuthamini kazi ya ualimu.

“Taaluma ya ualimu imekuwa ni daraja la kujiokoa baada ya kukosa sehemu zingine. Walimu wetu wanaofundisha katika mazingira magumu sana hatuwathamini na wakati mwingine hata tunawabeza.

Pia alitoa wito kwa asasi za kijinsia kupigia kelele suala la ajira kwa wanawake kwa vile alisema hivi sasa wanaume wanapata ajira zaidi kuliko wanawake, jambo alilosema linapaswa kurekebishwa.

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alitumia fursa hiyo kueleza kuhusu changamoto za ajira kwa vijana hapa nchini; akisema zaidi ya theluthi mbili ya nguvukazi iiyopo nchini haijaajiriwa katika sekta rasmi.
Mbele ya waliohudhuria mkutano huo kutoka ndani na nje ya nchi, Zitto alieleza kusikitishwa kwake na mwenendo wa nchi za Kiafrika katika siku za karibuni, aliosema unafanana na hali ilivyokuwa kwenye miaka ya 1960.

“Tunashuhudia uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu katika mataifa ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudani ya Kusini na Ethiopia. Machafuko yote haya yanasababishwa na kupuuzwa kwa haki za kiraia na kidemokrasia.


“Tunatoa wito maalumu kwa taasisi za kiraia, taasisi za dini na vyuo vikuu katika bara la Afrika kusimama imara katika kulinda utawala wa sheria na demokrasia ya vyama vingi. Tunazitaja taasisi hizi kwa sababu kazi zao na uwepo wao unategemea sana uwepo wa demokrasia katika nchi yoyote duniani. Demokrasia ya vingi ikichezewa na hatimaye kufififshwa taasisi za kiraia, taasisi za dini na vyuo vikuu haviwezi pia kuwa na uwezo wa kufanya kazi zao kwa uhuru.

“Chama chetu kinamtaka Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila aheshimu Katiba ya nchi hiyo na kuruhusu uchaguzi kufanyika kama ilivyopangwa ili kuwezesha mpito wa kidemokrasia kwa amani kabisa. Tanzania haiwezi kuendelea kupokea wakimbizi wa kongo kwa makosa ya wanasiasa wanaong’ang’ania madaraka kinyume na Katiba,” alisema Zitto.

Mwisho

Chanzo: Ukurasa wa FB wa ZZK

Waisusia hospitali mwili wa marehemu

$
0
0
Mwili wa Chihula Mboyelwa (89), aliyefariki dunia katika Hospitali ya Mkoa wa Geita umesuswa na familia yake.

Watoto wa Mboyelwa wameamua kugoma kuuchukua mwili wa baba yako kwa madai kuwa kifo chake kimesababishwa na uzembe wa wauguzi.

Mtoto wake, Bahati Chihula amesema Oktoba 6, mwaka huu alimfikisha baba yake katika hospitali hiyo kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na kulazwa wodini.

Amesema juzi asubuhi wakiwa na baba yao wodini aliingia muuguzi na walinzi wanaolinda hospitali na kuwataka wanaowauguza watoke nje kwa kuwa muda wa kuona wagonjwa haujafika.

“Nilimuomba nesi (muuguzi) aniruhusu nimpeleke baba yangu chooni kwa kuwa alitaka kujisaidia, lakini nesi alikataa na kuniambia hiyo ni kazi yake, “amesema na kuongeza:

“Nilikubali kutoka na kumwacha baba yangu baada ya dakika chache nikiwa getini nilipigiwa simu kuwa baba yangu ameanguka chooni”.

Natamani Kuzaa Mtoto wa Kiume - Kajala

$
0
0
Diva katika kiwanda cha filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameweka peupe hisia za moyo wake kuhusu kiu yake ya kupata mtoto wa kiume.

Huyu hapa anafunguka: “Najua mtoto ni mtoto lakini kwa sasa natamani kuwa na mtoto wa kiume ili Paula naye ajivunie kuwa na kaka. Siku zote nilitamani nipate watoto wenye jinsia tofauti na sasa tayari ninaye wa kike ni zamu ya kumpata mwingine wa kiume,” alisema Kajala na kuongeza:
“Natamani kuzaa na mwanaume yeyote aliye tayari na anayejitambua na kuwa tayari kuitwa baba na kugharamia matumizi ya watoto wangu na kuipa familia matunzo bora.”

Kwa upande mwingine, Kajala ameweka wazi kuwa anatamani kuvuka nje ya nchi kimafanikio, jambo ambalo tayari kwa sasa limeanza kuonyesha dalili kwa kiasi kikubwa.

“Nataka kufanya sanaa ya kuvuka mipaka, nimejitahidi kadiri nilivyoweza ndiyo maana baadhi ya kazi zangu zimeanza kuvuka mipaka hasa kwa nchi za jirani zaidi zikiwa ni zile zinazozungumza lugha ya Kiswahili,” alisema Kajala.

Divaloness Ajibu Tuhuma za Kujiuza Hyatt Hotel Baada ya Chat Kuvuja Akichati na Danga....

$
0
0
Divaloness ajibu tuhuma za kujiuza Hyatt hotel baada ya Chat Kuvuja akichati na Danga...

Kupitia Kwenye Ukurasa wake wa Instagram ameandika haya hapa :
...
#Regrann from #divathebawse - LOL jaman wanawake wana mambo hahaha anyways . unaambiwa alietengeneza chat zangu za so called kudanga kwenye system ya cyber crime anaitwa Mirry au Maarufu kama Tzshade sijui nini anaishi Dubai , alichat na mwenzie akaenda whatsapp yangu ya biashara na ku crop kisha kuunganisha chat zake aka edit ila pia akasahau crop vizuri 😂😂 , adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake like yoh that number is Public sweetheart, na iko all over yangu binafsi ya smart nahisi aliikosa 😂😂😂 na alipokosea ni kusema rafiki yangu tammy sijui yaan umebugi man sinaga rafiki wa Kike na siendag mahotelini mie afu unapenda kiki na jina langu eeh? damn it babe erm acha obsession zako lol, una hate sana like si ndo kwanza yaan Maisha murua na vodacom yaan Mungu anashusha tu baraka zake.

akaanza post au sambaza akijifanya katumiwa lol Dada kaz unayooooo... loneliness lmaoo kumbe she planned all that, nimwambie tu keep doin the hating ila watu wamekuchoka na uzushi wako. kila siku nasikia mana ata sifatilii unapost pic zangu mbaya na nzuri like bitch i don give a fuck sikujui sitak shobo sitak mazoea .. ushamu whatsapp mara kibao msichana wangu wa matangazo like anakulia Buyu like

nahisi una matatizo ya utindio wa Ubongo and You need a HUG hahaha. mi sio sizoeleki ovyo .. nina sura mbili na siambiliki and i don't give a fuck, like told u once hating ikibuma.. eeh start telling n spreading lies uko hyatt hata kuniona wenzio hawajawah niona mi sio mtu wa cheap ass kwenda kila kona erm get a grip get a life huko lol

fyi hyatt siujui ata mlango wake ulivyo Lamada nako napapita tu , double tree yeah das ma chillin session n nalipia mwenyewe nikienda for bidness meeting mi silipiwi ovyo v2 ww yaan umepuyanga kwa zile chat, asa dola 1000 to 1500 nisingekuwa nafanya kazi till late basi mana huo mtelemko ata vat sikatwi like Yoh .. umepuyangaa. Kudanga ain't ma shit. Get well soon hahahahahaha +971 56 233 3028 namba hio ndo yake unaambiwa

afu mekujibu for my fans n my profesheno reason ukno huwag sina time na haters like u , yan daily u Post celebs watukanwe ..like unapata nini

Hili la Chriss Brown Kuvunja Simu ya Shabiki Kenya ni Kweli au Kawaida ya Majirani Kutafuta Kiki?

$
0
0
Muimbaji mashuhuri wa Marekani mtindo wa Hip Hop Chris Brown, yupo Kenya kwa tamasha la muziki mjini Mombasa eneo la pwani.

Lakini tukio ambalo halikunukuliwa kwenye kamera limegubika vyombo vya habari nchini.

Shabiki mmoja mwanamke anatuhumu kuwa Chris Brown ameivunja simu yake alipojaribu kupiga picha 'selfie' alipowasili katika uwanja wa ndege Mombasa.

Kwa mujibu wa gazeti mmoja nchini "Daily Nation,'' mwanamke huyo anasema CB alimpokonya simu kutoka nyuma alipojitayarisha kuipiga picha hiyo na kuirusha chini.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa simu ya msichana huyo aina ya iPhone 6 iliyomgharimu takriban dola 900, haikuvunjika lakini kizuia kioo na kifunikio cha simu viliharibiwa.

Shabiki huyo aliyesema amenunua tiketi kuhudhuria tamasha hilo, ameghadhabishwa na ameamua kutohudhuria tamasha hilo.

Tuhuma zake zimesababisha gumzo kuu katika mtandao wa Twitter kupitia #DeportChrisBrown ambapo Wakenya wanajadili iwapo muimbaji huyo nyota arudishwe Marekani.

Hisia zimegawanyika ambapo baadhi wanamtetea Chris Brown na wengine wakitaka atimuliwe Kenya.

Kanda ya video iliyowekwa na @KinyanBoy katika twitter inaonekana kumuonyesha Chris Brown akipuuza ombi la mwanamke huyo kupiga selfie na anampita bila kumgusa.

Lakini mwanamke huyo aliyejitambulisha kama Brenda Chepkoech, amezungumza na televisheni ya NTV nchini, anasisitiza kuwa tukio hilo limetokea baada ya kanda hiyo kuwekwa kwenye mtandao na ni muda mfupi kabla ya CB kuingia garini na kuondoka.

Mnamo Julai mwanamuziki mashuhuri wa Congo, Koffi Olomide alirudishwa Congo kutoka Kenya baada ya kuzuka video katika mitandao ya kijamii akionekana kumpiga teke mojawapo ya wachezaji wake densi katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Nairobi.

Wakenya walighadhabishwa katika Twitter na kutaka atimuliwe.

Koffi aliomba radhi lakini tamasha lake lilifutiliwa mbali na alirudishwa Kinshasa kwa ndege.

Siku chache baadaye waandalizi wa tamasha lake jingine Zambia pia walilazimika kufutilia mbali tamasha hilo kutokana na shinikizo kufuatia tukio la Kenya.


NB: mpaka sasa sijaona video inayomuonyesha brown akifanya hicho kituko,

Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Siku ya Leo Katika Magazeti...Bonyeza Hapa

$
0
0

EXCLUSIVE: Babu Seya, Papii Watuma Ujumbe Mzito Kwa JPM!

$
0
0
Kwa Wabongo walio wengi, majina ya Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ siyo mageni. Wao ni wafungwa wanaotumikia kifungo cha maisha ndani ya Gereza la Ukonga, Dar baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kulawiti na kunajisi watoto 10.

Tangu kufungwa kwao, mwaka 2004, miaka 12 iliyopita, mengi yamesemwa, mengi yameandikwa, lakini wenyewe hawajawahi kufungua vinywa kusema lolote, hivyo kwa mara ya kwanza, Septemba 3, mwaka huu, Risasi Mchanganyiko, limekutana nao ndani ya gereza hilo na kufanya nao mahojiano yaliyochukua dakika 55.

ILIKUWAJE?
Septemba 2, mwaka huu, Risasi Mchanganyiko lilipata taarifa kwamba, wafungwa hao waliandika barua kwa Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ wakiomba msamaha kutoka kwake ili waachiwe huru.
Ili kuweka sawa mzani wa habari, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu Mkuu wa Gereza la Ukonga, ACP Stephen Mwaisabila na kumuuliza kuhusu uwepo wa madai hayo ambapo alisema:
“Hakuna kitu kama hicho. Hivi ni kwa nini baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika habari za hawa watu wawili bila ukweli wowote?”


Risasi Mchanganyiko: “Sasa ukweli ni upi kamanda?”
ACP Mwaisabila: “Ukweli ni kwamba si kweli, hawajaandika barua. Mimi nadhani nyie mngekuja hapa ili muongee nao mbele yangu, muwasikie wenyewe. Maana muda mrefu nasoma kwenye magazeti habari za hawa watu ambazo si za kweli. Wengine wanaandika wameachiwa, wengine wanasema Babu Seya amelazwa yu hoi. Njooni muone kama kweli yupo hoi.”
Risasi Mchanganyiko: “Itakuwa vizuri sana kamanda. Ili tuzungumze nao mambo mengine ambapo Watanzania wakisoma, ukweli na uongo utajulikana.”
ACP Mwasabila: “Sawasawa.”seyaaaa-7…Wakiwa katika sura ya majonzi.

NDANI YA GEREZA LA UKONGA
Ndani ya gereza hilo, maisha yalikuwa yakiendelea. Wafungwa walionekana kufanya shughuli zao za kila siku. Hakukuwa na dalili zozote za vurugu wala uvunjifu wa amani. Wafungwa walionekana wanaishi maisha ya maelewano na askari wao.

BABU SEYA, PAPII WAITWA

Baada ya salamu na mkuu wa gereza, askari mmoja alitumwa kwenda kuwaita wafungwa hao. Ndani ya dakika kumi, wakafika na kupeana salamu na Risasi Mchanganyiko.

BAADA YA SALAMU SASA

Baada ya salamu, Risasi Mchanganyiko lilianza maswali papohapo.
Risasi: “Tulipata taarifa kwamba, mmeandika barua kwa Rais Magufuli kuomba msamaha kutoka kwake. Hii habari imeenea mtandaoni. Hebu tuambieni, ipoje?
Babu Seya: “Iko hivi, sisi…”


Papii: (akadakia yeye, baba yake akanyamaza) “ngoja niseme mimi. Ukweli ni kwamba, barua niliandika mimi mwaka 2010. Ilikwenda kwa Rais Kikwete (Jakaya, wakati huo). Lakini tangu pale sijawahi kuandika tena barua. Hiyo inayosambaa mtandaoni ni ileile inajirudia. Kwa Magufuli hatujawahi kuandika barua.”

KUHUSU RUFAA YAO
Risasi: “Sawa. Kwa nafasi hii tungependa kuzungumza na nyie mambo mbalimbali ambayo hamjawahi kuyasema tangu mmeingia gerezani. Hebu tuanze na kesi yenu. Kuna wakati ilisemekana mmekata rufaa Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika yenye makao yake Arusha, mkipinga kifungo. Je, nini kinaendelea?”
Papii: “Ni kweli. Ila ilichotakiwa ni wao baada ya sisi kupeleka hati yetu, walitakiwa kuja kutuhoji ili wajue tulichoandika ni sawa au kuna ya kuongezea. Lakini hawajatokea.”


WANAAMINI WATATOKA?
Risasi: Kwako Babu Seya. Je, mnaamini kuwa iko siku moja mtatoka gerezani?”
Babu Seya: “Mimi naamini kwa haki ya Mungu iko siku lazima. Nasema hivi kwa sababu, Mungu ndiye anayejua ukweli wa kesi tuliyofungiwa. Anajua nini kilitendeka.”
Papi Kocha: (anaunga mkono maneno ya baba yake kwa kutingisha kichwa).

BABU SEYA AUTAJA WIMBO WA SEYA
Risasi: “Kwani kwako Babu Seya, unataka kusema kuna namna katika ile kesi yenu? Hiyo namna iko wapi?”
Babu Seya: “Chanzo cha yote yale ni Wimbo wa Seya niliouimba mimi na mtoto wangu (Papii). Ule Seya wa Mivano. Pale ndipo pana chanzo, lakini siwezi kusema nini kilitokea, siko tayari kusema.”

SIKU YA KWANZA GEREZANI ILIKUAJE?
Risasi: “Hivi siku yenu ya kwanza kuingia hapa gerezani ilikuaje? Mlilia kwa kiasi gani?”
Babu Seya: “Wala! Tulimwamini Mungu. Tulijua Mungu ana makusudi yake na iko siku itajulikana ukweli umesimamia wapi.”

MAISHA YA GEREZANI
Risasi: “Maisha yenu hapa jela yakoje? Maana tukiwaangalia tunawaona mpo fiti sana.”
Babu Seya: “Kama hivi, tunaendelea vizuri sana. Tumezoea na hakuna unyanyasaji wowote.”

KUNA UGONJWA UMEWAPATA GEREZANI?
Risasi: “Kumekuwa na madai kwamba, wewe Babu Seya unaumwa. Wakati mwingine ikadaiwa upo hoi. Je, kuna ugonjwa umekupata ukiwa hapa au mwanao?
Papii: (anatingisha kichwa kukataa).
Babu Seya: “Mimi niliumwa, nikaenda kupimwa na kugundulika nina diabetes (kisukari). Ni kama miaka minne iliyopita (2012).
“Ninapoonekana Muhimbili (hospitali), huwa nakwenda kliniki. Kwa hiyo siyo kweli kwamba nakuwa hoi. Kisukari ni ugonjwa kama magonjwa mengine na nimeupata kama wanavyoweza kuupata watu wengine ambao hawapo gerezani.”

WAMESHIKA IMANI GANI GEREZANI?
Risasi: “Wengi wakiingia gerezani hubadili imani. Wapo ambao huamua kuokoka. Nyie je, tangu mmefika mmebadili madhehebu?”
Papii: “Hapana, sisi tuko na imani yetu ileile ya Romani Katoliki. Tulipokuwa nje, kanisa letu lilikuwa pale Sinza, Shule ya Msingi Mashujaa kwa mbele (Barabara ya Hoteli ya Lion).”
Risasi: “Tangu mmekutwa na hatia na kutupwa huku jela, viongozi wenu wa dini wameshakuja kuwajulia hali?”
Papii: “Hapana.”



BEBU SEYA BENDI ALIMUACHIA NANI?
Risasi: “Tunajua Babu Seya ulikuwa na bendi yako ya muziki, Achigo Band na ulikuwa ukipiga pale Lion Hotel. Je, ulimwachia nani?”
Babu Seya: “Ile nilimwachia mwanangu mkubwa.”
Risasi: “Mbangu?”
Babu Seya: “Hapana, kaka yake.”

BABU SEYA ANA MKE?
Risasi: “Babu Seya umeacha mke uraiani?”
Babu Seya: (anasikitika) “Hapana, mke wangu alifariki dunia kabla mimi sijakumbwa na ile kesi.”

LAKINI UKWELI NI UPI, WALIBAKA?
Risasi: “Msamaha wa binadamu ni jambo muhimu sana. Hata Mungu anauona na unaposema ukweli na kukiri kile ulichokifanya, anaweza kukusamahe. Maana kama ni kufungwa tayari mpo kifungoni, hakuna sababu ya kudanganya tena. Je, ukweli wenu ni upi? Ni kweli mlibaka???”
Kutokana na ufinyu wa nafasi, mahojiano na Babu Seya na Papii Kocha yataendelea kwenye Gazeti la Risasi Jumamosi, usikose.

LAKINI UKWELI NI UPI, WALIBAKA?
Risasi: “Msamaha wa binadamu ni jambo muhimu sana. Hata Mungu anauona na unaposema ukweli na kukiri kile ulichokifanya, anaweza kukusamahe. Maana kama ni kufungwa tayari mpo kifungoni, hakuna sababu ya kudanganya tena. Je, ukweli wenu ni upi? Ni kweli mlibaka?”

Kutokana na ufinyu wa nafasi, mahojiano hayo yalikatwa hapo bila wao kujibu. Sasa sikia majibu yao…
Babu Seya: “Kusema ukweli kwa haki ya Mungu nakuapia, mimi wala dogo huyu (Papii) hakuna anayehusika na yale madai. Hata siku ya kukamatwa, mimi nilikuwa nyumbani wakati ule pale Sinza, nikashangaa navamiwa, naambiwa nimebaka wale watoto. Huyu dogo (Papii) yeye alikuwa ametoka Arusha, akaunganishwa kwamba naye alikuwemo.
“Ndiyo maana nikasema kwamba ule Wimbo wa Seya wa Mivano pana kitu. Lakini sikisemi. Wale watoto mimi hata kuwajua siwajui maskini ya Mungu.”
Risasi: “Kwa hiyo hamkubaka?”
Babu Seya: “Kwa vile hukumu imeshapita, mahakama ikatuona tuna hatia, hakuna namna ambayo tunaweza kusema zaidi ya kukiri kwamba tulifanya kwa sababu tulikutwa na hatia…
Papii: (akadakia) “Maana hata tukisema hatukubaka, watu watatuuliza kwa nini sasa tuko gerezani? Mtu ukishahukumiwa tafsiri yake ulitenda kosa na ndiyo maana ulikutwa na hatia hata kama hukufanya lile kosa.”

WAWAOMBA WATANZANIA WAWASAMEHE
Risasi: “Kwa maana hiyo mnapoyazungumza hayo, mnawaambia nini Watanzania?”
Babu Seya: “Tunawaomba watusamehe kwa yote yaliyotokea na watuombee kwa Mungu siku moja tutoke gerezani ili kuungana katika ujenzi wa taifa.”

WAKITOKA GAREZANI WAMEPANGA KUFANYA NINI?
Risasi: “Ni kawaida kwa watu waliofungwa wakitoka gerezani kubadili mstari wa maisha. Wengine huamua kumtumikia Mungu, wengine hufanya shughuli yoyote tofauti na ile ya awali. Je, nyie ikitokea mmetoka jela, mmepanga kufanya shughuli gani?”
Babu Seya: “Kwanza ikitokea tukaachiwa huru tutachanganyikiwa. Hivyo hatujawahi kupanga cha kufanya. Maana tukisema tukitoka tutamtangaza Mungu, watu watasema tumechanganyikiwa (kicheko, Papii naye kicheko).
“Lakini tukisema tuendelee na muziki, pia watu watasema tunarudia mambo yetu. Kwa hiyo tutaangalia cha kufanya wakati ukifika.”
Risasi: “Babu Seya umesikika ukisema uliishi Sinza. Kwani kwa sasa maskani ya familia yako ni wapi?”
Babu Seya: “Yapo Kimara. Pale Sinza niliuza nyumba baada ya ndugu kunishauri ili nibadilishe mazingira.”
Risasi: “Familia yako ikoje sasa?”
Babu Seya: “Familia haiko sawa kwani roho ni mimi na ndiyo niko gerezani. Kwa hiyo familia haiko sawasawa maana roho haipo (kicheko).”

UJUMBE WAO MZITO KWA MAGUFULI NI HUU
Risasi: “Mlisema kuwa, mliwahi kuandika barua kwa Jakaya Kikwete kabla ya Rais Magufuli. Je, kwa Magufuli mnampa ujumbe gani?”
Babu Seya: “Sisi kwa nafasi hii ya leo, tunamuomba sanasana Rais Magufuli aitishe faili la kesi yetu (huku Papii akitingisha kichwa kukubaliana na maneno ya baba yake). Asome mwenyewe mwanzo hadi mwisho, aone ukweli uko wapi! Lazima atabaini ukweli kwamba kufungwa kwetu kulitokana na nini!
“Lakini naamini kwamba, Mungu hawezi kuacha jambo ambalo si la kweli liendelee kujulikana si la kweli kwa muda wote, lazima kuna siku atainua nguvu zake na ukweli utajulikana. ”

IKITOKEA HAKUNA NAMNA YA KUTOKA
Risasi: “Je, endapo itatokea njia zote za kutoka jela zimeshindikana, mtafanya nini?”
Babu Seya: “Tutamshukuru Mungu na kumwachia yeye kila kitu. Kwani lazima atakuwa na makusudi yake.”

KUTOKA MOYONI KWA BABU SEYA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Babu Seya alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, anamwomba Mungu ikiwezekana hata kama yeye hatatoka, basi mwanaye, Papii atoke ili akafanye maisha yake.
“Unajua mimi umri umekwenda. Sasa huyu dogo (Papii) bado kijana. Alikuwa ana malengo yake, yote yamepotea. Mimi hata nikibaki basi Mungu asaidie yeye atoke,” alisema Babu Seya.

KUNA MWENYE CHEO?
Risasi liliwashuhudia wote wakiwa na mikanda kiunoni ambayo kwa mfungwa, inaashiria ni nyapara (msimamizi wa wafungwa).

BABU SEYA ALITABIRI TETEMEKO LA BUKOBA
Katika kusimulia zaidi maisha ya gerezani, Babu Seya alisema amekuwa akisali sana kiasi kwamba, wakati mwingine Mungu humwonesha mambo yajayo.
“Siku tatu kabla ya tetemeko la ardhi kule Bukoba, mimi nililala nikasikia sauti ikiniambia; ‘fungua macho uangalie’. Kufungua hivi nikaona ardhi inatetemeka. Nikalala tena, nikaambiwa tena.
“Nikamfuata dogo (Papii) na wenzake, nikawaambia kutatokea tetemeko la ardhi. Kweli, baada ya siku tatu tukasikia Bukoba kumetokea tetemeko na limesababisha maafa.”

AOMBA KUANDALIWA TAMASHA
“Kwa hiyo kutokana na tukio la tetemeko, mimi naomba kama inawezekana serikali ituandalie tamasha mimi na dogo tupige ili kuwachangia waathirika wa tetemeko,” alisema Babu Seya.

WANAMUZIKI WANAKWENDA KUWATEMBELEA?
Risasi: “Tangu mmefungwa jela, kuna wanamuziki wanakuja kuwatembelea?”
Babu Seya: “Ilikuwa zamani, siku hizi wameacha. Ila mwanamuziki anayekuja sana mpaka sasa ni King Kiki (Kikumbi Mwanza Mpango).

PAPII KOCHA ANAMMISI NANI?
Risasi: “Kwako Papii. Unaweza kusema unawamisi akina nani kuwepo kwako jela?”
Papii: “Nawamisi mashabiki wangu wote. Pia, nawamisi Bongo Fleva na Bongo Muvi. Nammisi mwanamke niliyezaa naye mtoto mmoja, anaitwa Mariam.
“Lakini namuomba Rais Magufuli aendelee kufanya mambo yake vizuri kama tunavyosikia maana yakiharibika na sisi huku gerezani mambo yatakuwa mabaya.”
Risasi: “Basi tunashukuru sana, tunawaombea kwa Mungu.”
Babu Seya: “Na sisi tunashukuru sana, muende salama na mzidi kutuombea.”
Waandishi: Oscar Ndauka na Elvan Stambuli/GPL.

SBL Yazindua Shindano la Wapiga Mziki (DJ) Mix Master Itakayoshirikisha Mikoa Mitano

$
0
0

Dar es Salaam,  Oktoba 9, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza kuzindua shindano la DJ bora ambalo linalenga  kuibua na kukuza vipaji katika sekta ya muziki na burudani nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa  uzinduzi wa shindano hilo jijini Dar es Salaam, Mkrugenzi wa Mawasiliano wa Serengeti John Wanyancha alisema kuwa  shindano hilo limedhaminiwa na  bia inayozalishwa na kampuni hiyo Smirnof Black Ice, na wakati huo huo  ikimaanisha kuwapatia mashabiki wa muziki  fursa ya kufurahia  vibao vya muziki vya hivi karibuni vitakavyochezeshwa na ma-DJ walio na vipaji vikubwa.

 Kwa mujibu wa Wanyancha, Smirnof Black Ice ni chapa inayoongoza  katika vighezo vya bia iliyotayari kunyweka ikiwa ni maarufu mioongoni mwa wanywaji wa tabaka la kati katika maeneo yote ya mjini na vijijini.

 “Tunaamini kwamba kupitia shindano hili SBL itawapa wakati mzuri  wapenzi wa muziki watakaokuwa wanatembelera baa  wakati tukitoa fursa maridhawa ya kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji katika ulimwengu wa muziki na ma-DJ.

Mkurugenzi huyo aliyataja majiji ambayo yatakuwa wenyeji wa matukio na idadi ya ma-DJ watakaotoa burudani  katika mabaa kwenye mabano kuwa ni Dar es Salaam (20), Dodoma (4), Arusha (5), Morogoro (4), na Mwanza (5). Shindani hilo linaanza mwezi huu wa Oktoba na  litadumu hadi Desemba.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa hadhira inayolengwa katika  mashindano hayo ni  vijana walio na umri kati ya miaka 18 hadi 30 na kufafanua kuwa burudani hiyo inawafaa sana  wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vingine vya elimu ya juu pamoja na vija walio na weledi.

“Itakuwepo zawadi nono kwa ma-DJ watakaoshinda,” alisema na kubainisha kwamba zawadi hizo zitajumuisha seti ya vifaa vya kuchanganya muziki, kompyuta mpakato na mashine kuchanganya muziki kwa washindi watatu watakaoingia fainali.

 “Tunatoa wito kwa ma-DJ wote, wasimamizi wa baa na wapenzi wa muziki katika majiji haya  kushiriki kwa wingi katika shindano hili la kuvutia  ili kufurahia na  burudani inayotolewa na sekta ya muziki nchini Tanzania,” alisema Wanyancha.

MWISHO

Simba, Yanga, Ruksa Uwanja wa Uhuru

$
0
0
Bodi ya ligi Tanzania imethibitisha timu za Simba na Yanga zitautumia uwanja wa Uhuru kwa mechi zao za nyumbani baada ya serikali kuzizuia kuutumia uwanja wa taifa kama uwanja wao wa nyumbani kwenye mechi zao za ligi kuu.

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Boniface Wambura amesema, mechi ijayo ya Yanga wataanza kucheza kwenye uwanja huo dhidi ya Mtibwa mchezo unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi October 13.

“Mechi zao watacheza kwenye uwanja wa Uhuru, kwahiyo mechi zao zote za nyumbani watakuwa wakitumia uwanja huo. Serikali ilizifungia kutumia uwanja wa taifa, uwanja wa Uhuru uko wazi wanaweza kuutumia wakati wowote,” anathibitisha Boniface Wambura.

Awali vilabu hivyo vilikuwa vinautumia uwanja huo kwa mechi zao za ligi kabla ya Simba kuulamimikia kuwa unawasababishia majeraha wachezaji wao na kuomba kurudishwa kwenye uwanja wa taifa.

Serikali ilichukua uamuzi wa kuufungia uwanja wa taifa kufatia vurugu za mashabiki zilizozuka kabla na wakati wa mchezo wa Yanga vs Simba uliochezwa October Mosi. Kabla ya mechi hiyo, mashabiki waling’oa mageti manne kabla ya mashabiki wa Simba kung’oa viti wakati mechi ikiendelea kwa madai klabu yao ilikuwa ikionewa katika mchezo huo.

Mama Diamond Akimtambua Vizuri Mwanaye Atampenda Sana Zari

$
0
0
MWAKA 2009 Diamond Plutnumz akiwa ndiyo kwanza ameingia katika ulimwengu wa umaarufu, alihojiwa na jarida fulani maarufu ambalo kwa sasa halitoki tena juu ya matarajio yake katika muziki na maisha.

Japo kwa nyakati zile wengi huenda hawakumuelewa, ila Diamond alisema kuwa, dhamira yake ya kwanza anataka kuwa mwanamuziki maarufu sana Afrika halafu awe mwanamuziki tajiri.

Kutoka mwaka 2009 mpaka sasa siyo miaka michache. Katika yale aliyoongea Diamond kuna picha kubwa ya kweli inakuja katika akili ya kila mdau wa kweli wa Bongo Flava.

Kuna kila dalili ya Diamond kuishi ndoto yake kama Mungu akizidi kumpa uhai na ukumbusho wa dhamira yake. Ila wakati mwingine ndoto katika maisha siyo kitu cha kushangaza sana.

Kila mmoja ana ndoto yake. Kuna wanamuziki walikuwa na ndoto kama za Diamond na wengine zaidi yake ila wengi wamekata tamaa na wengine wakaona kama ni ujinga kuwaza hivyo.

Msingi wa ndoto katika maisha ni mikakati ya namna ya kuifikia. Katika hili kuna somo hapa kwa Diamond. Mbali na jitihada zake za usiku na mchana na kuwa na timu kubwa ya uongozi yenye watu makini na  uelewa wa kutosha kuhusiana na muziki wa nyumbani na wa kimataifa.

Hapa nawazungumzia watu kama Said Fella, Babu Tale, Salami, Ruge Mutahaba nk. Katika akili ya kawaida ukiwa na watu hawa na kuwasikiliza kwa makini na kutumia akili yako vyema, una nafasi kubwa sana ya kuwa msanii mzuri.

Ila kando na hivyo, Diamond anaonekana kuwaza nje ya sanduku (to think outside the box) kitu ambacho wanamuziki wengi wanashindwa.

Diamond katika kufikia ndoto yake anaangalia anakaa na nani, marafiki zake ni akina nani na mwisho ni nani anayelala naye kitanda kimoja na kumuita mpenzi au mke wake.

Hapa ndiyo kuna kitu ambacho mama Diamond, dada yake Diamond na wengine wanapaswa kuelewa. Toka zamani imetajwa, nyuma ya mafanikio ya kila mwanaume kuna mwanamke makini.

Hapa Diamond ndipo karata yake ya ushindi huenda inapopatikana. Mwenyewe aliwahi kuandika katika mitandao ya kijamii kuhusiana na mahusiano yake na Wema Sepetu.

Mbali na kuandika mengi ila pointi zake zilieleza kuwa Wema wa kipindi kile (sijui wa sasa) alikuwa anawaza sana starehe na sifa. Kwa maelezo yake ni kuwa wakati watu wakimlaumu kuwa eti anatumia nyota ya Wema kufanya vizuri katika biashara yake ya muziki, Wema mwenyewe alikuwa hana muda na filamu zake zaidi ya starehe na kutafuta sifa za kuitwa tajiri hali hana kitu.

Alipoachana na Wema na kuingia katika mahusiano na mwanadada mrembo, makini na mfanyabiashara, Zarina Hassan ‘Zari the boss Lady’, Diamond aliwahi tena kukiri kuwa toka awe na mrembo huyo kutoka Uganda hata mtazamo wake kimaisha na kibiashara umebadilika na kukua zaidi.

Hapa ndipo kuna somo halisi. Zari ni zaidi ya mwanamke kwa Diamond. Zari ni mshauri, mama wa watoto na dira yake ya kimafanikio ya jabali huyo wa Tandale.

Mtu mwingine kwa sababu zake za Kiswahili anapotamani Zari na Diamond waachane, kwa sababu yoyote ile, hajui kuwa maumivu na madhila ya wawili hawa kuachana siyo ya Zari pekee ila yatamgusa kwa kiwango kikubwa na Diamond mwenyewe.

Watu wajifunze kutoka kwa akina Tiger Wood na wengineo. Baada ya mwanamichezo huyo kuachana na mke wake hata ufanisi wake katika michezo ukashuka na akayumba sana kiuchumi.

Rai yangu ni kuwa, kama mama Diamond ana uhasama au chuki yoyote binafsi na Zari, inabidi afahamu mwanaye amependa na anafaidika kiakili na kimwili kwa binti huyo.

Hiyo misuguano inayosemwa naona haina maana kabisa

Huyu Ndo Mwalimu Aliyerekodi Tukio la Kikatili la Kupigwa Mwanafunzi na Walimu Mbeya Day

$
0
0
Pichani ni mwalimu aliyechukizwa na kitendo cha walimu wanne waliomshambulia Mwanafunzi kama wamekutana na Scorpion, pia alisikika akisema "mwalimu muacheni mtamuumiza" naamini ameokoa wanafunzi wengi wanaopigwa kama nyoka mashuleni bila sisi

HUYU NDO MWALIMU NDIYE MWALIMU ALIYE REKODI TUKIO LA KIKATILI LA KUPIGWA MWANAFUNZI NA WALIMU MBEYA DAY

Matani ya Stan Bakora Yamtoa Povu Barakah The Prince

$
0
0
Mchekeshaji Stan Bokora baada ya kufanya cover ya wimbo ‘Nisamehe’ wa Barakah Da Prince kumezuka mtafaruku baina ya wawili hao.

Barakah The Prince amedai hajapenda jinsi Stan Bakora alivyomwigiza katika video hiyo.

Muda mchache baada ya video hiyo kutoka, Baraka The Prince aliandika: Matani ni mazuri ila yakizidi yanaweza kuleta matatizo… heshima ichukue nafasi yake tafadhali mzee utani huu sijaupenda iwe mwanzo na mwisho tafadhali.

Kwa upande wa Stan Bakora alisema kila video ambayo anafanya cover ni lazima azungumze kwanza na mwenye kazi na kukubaliana naye.

Nahitaji kumuua Young D wa zamani- Young D

$
0
0
Rapa Young Dar es Salaam alimaarufu kama Young D amesema kwamba huu ni wakati wake kumuua yule Young D wa zamani na kurudi kivingine akiwa na mtazamo mpya vichwani mwa watu na mashabiki zake.


Young D alisema hayo kupitia kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz kinachorushwa na EATV Ting'a namba moja kwa vijana, Young D anasema baada ya kutangaza rasmi kuacha ngada mfumo wake wote wa maisha ameubadili ili kuweza kumfuta yule Young D ambaye watu walimfahamu na kumjenga Young D mpya.

"Mfumo wangu wote wa maisha ulikuwa haupo sawa hivyo Chochote nachofanya saizi kama hakinipeleki kwenye siku yangu ya mafanikio basi hakina nafasi kwenye maisha yangu, ni vitu ambavyo naamua mimi mwenyewe kama mtoto wa kiume kuna muda naamua kuwa hiki ni kwa ajili ya maisha yangu, mimi hapa nina Mama yangu na familia inaniangalia hivyo maamuzi niliyoamua ni kuikana nafasi yangu, yaani nataka nimuuwe yule Young D wa zamani pia nimlete huyu Young D mpya ambaye huyu mpya atawafanay watu wamsahau yule wa zamani kama aliwahi kuwepo" alisema Young D

Baraza la Mitihani Nchini Limetoa Ratiba ya Kufanya Uhakiki wa Vyeti Kwa Watumishi Wote wa Serikali

$
0
0
Hatua ya Baraza la Mitihani nchini (Necta) kutoa ratiba ya kufanya uhakiki wa vyeti vya kidato cha nne, sita na ualimu kwa watumishi wote wa umma sasa ni wazi imezidi kupandisha joto kwa vigogo na watumishi mbalimbali ambao hawana sifa za kielimu kushika nafasi walizo nazo.

Katika taarifa yake ya sasa Baraza la Mitihani nchini, limetangaza kuwafuata katika maeneo yao ya kazi watumishi wote walioko katika mamlaka za mikoa, halmashauri na manispaa kwa ajili ya kufanya uhakiki wa vyeti vyao hivyo vya kitaaluma.

Kwa mujibu wa barua iliyosainiwa na  Edga Kasuga kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo kwenda kwa Makatibu tawala wa Mikoa, uhakiki utafanyika katika ofisi za Makatibu Tawala wa mikoa kuanzia Oktoba 10 hadi 14 mwaka huu, ingawa ratiba nyingine ya uhakiki imeonyesha zoezi hilo litafikia tamati Novemba 7 mwaka huu.

“Ili kufanikisha zoezi hilo Baraza limetaka kupata orodha (nakala- laini ya soft copy) ya watumishi wote wa umma waliopo katika Mkoa, Halmashauri na Manispaa.

“Nakala za vyeti vya kidato cha nne, cha sita na ualimu vya watumishi wote walioandikishwa na chumba cha kufanyia uhakiki,” inaeleza taarifa hiyo ya Baraza la Mitihani.

RATIBA YA UHAKIKI

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Baraza la Mitihani, uhakiki huo utafanywa katika makundi matano katika mikoa tofauti tofauti.

Oktoba 10, mwaka huu kundi la kwanza litafanya uhakiki katika Mkoa wa Mtwara, kundi la pili Singida, kundi la tatu Rukwa, kundi la nne Katavi na kundi la tano litakuwa Geita.

Oktoba 17 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Lindi, la pili Manyara la tatu Songwe, la nne Kigoma na la tano litakuwa Mwanza.

Oktoba 24 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Morogoro, la pili Arusha, la tatu Mbeya, la nne Tabora na la tano Mara.

Oktoba 31 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Pwani, la pili Kilimanjaro, tatu Ruvuma, la nne Shinyanga na la tano Simiyu.

Novemba 7 mwaka huu, kundi la kwanza litakuwa Dar es Salaam, la pili Tanga, la tatu Njombe, la nne Dodoma na la tano Iringa.

 – MTANZANIA
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images