Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

Nauli za ATCL zitakazotumika kuanzia Oktoba 14 hadi 28

$
0
0
Ndege mbili mpya za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q400 zinatarajia kuanza kazi wakazi  wa mikoa ya Mwanza, Arusha na Zanzibar watakuwa wa kwanza kupata ofa.

Ofisa Habari wa shirika hilo, Lilian Fungamtama amesema  safari  mpya za ndege hizo  ikiwamo ya Dar es Salaam - Mwanza, nauli iliyopangwa ni Sh160,000.

Amesema safari za  Dar es Salaam - Arusha nauli yake itakuwa Sh180,00 na Zanzibar - Dar es Salaam ni Sh85,000.

“Ofa hii imetolewa na ATCL kwa safari mpya za ndege hizo,” alisema Fungamtama.

Amesema hakutakuwa na safari ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar, lakini itakuwapo ya kutoka Dar es Salaam -Arusha hadi Zanzibar.

 “Ndege ya kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha ndiyo itakayokwenda kuchukua abiria Zanzibar haitatokea Dar es Salaam moja kwa moja,” alisema.

 Akifafanua kuhusu nauli hizo, Fungamtama alisema nauli  ya kutoka Dar kwenda Kigoma itakuwa katika madaraja mawili ambayo ilikuwapo tangu awali.

Amesema bado ndege hizo hazijaanza safari katika mikoa yote hadi hapo watakapotangaza.

Akizungumzia safari za nje ya nchi, alisema itakuwapo ya kutoka Dar es Salaam - Hahaya hadi Comorro ambayo nauli yake ni Sh543,950 kwenda na Sh926,650 kwa kwenda na kurudi.

 “Lengo letu ni kutoa huduma nzuri itakayomridhisha kila mteja,” alisema Fungamtama.


Muziki Wampa Baraka The Prince Mjengo wa Maana

$
0
0
Msanii wa bongo fleva nchini Tanzania ambaye aliwahi kupata tuzo ya msanii bora anayechipukia mwaka 2014 /2015 kupitia wimbo wake ya 'Jichunge' Barakah The Prince ameonesha matunda aliyoyapata kutokana na muziki tangu aanze kuimba mwaka 2014.


Miongoni mwa mafanikio aliyopata ni pamoja na kujenga nyumba kubwa yenye vyumba 5 huku nje akiwa ameweka sehemu ya kuogelea (Swimming Pool)

eNewz ilipiga naye story katika site yake hiyo aliyoijenga maeneo ya Tegeta jijini Dar es Salaam akiwa na mpenzi wake wa sasa, Naj ambaye pia ni msanii wa bongo flevana kusema kuwa wametumia fedha nyingi sana kwenye hiyo nyumba na bado haijakamilika na kwamba hayo ni matunda ambayo ameyapata kutokana na kazi ya muziki na ushirikiano na mpenzi wake huyo.
“Namshukuru sana mke wangu Naj kwa sababu ana mchango mkubwa sana hadi hapa nilipofika pia kwa sasa siwezi kutaja fedha ambayo nimeitumia hapa kwa sababu ni hela nyingi sana hadi sasa na kama unavyoona nyumba bado haijaisha kwa hiyo nikimaliza kila kitu nitasema ni shilingi ngapi nimetumia” Amesema Baraka The Price.

Hata hivyo msanii huyo aliongeza kwa kusema hivi karibuni anatarajia kufunga ndoa na penzi wake Naj baada tu ya kumaliza mjengo wake huo

Wanawake wa Dar na Kope Bandia Hatarini

$
0
0
Wanawake wanaotumia kope bandia wanahofiwa kuwa na
hali ya hatari ya kupata upofu wa macho kutokana na gundi
wanazotumiwa kutumia kope hizo kuripotiwa kuripotiwa
kuwa na athari kwenye macho yao.
Tahadhari hiyo imetolewa na mratibu wa huduma ya macho
ya mkoa wa Iringa, Dk George Kabona,alipokuwa akitoa
tathmini ya huduma ya macho ikiwa ni sehemu ya kuelekea
maadhimisho ya siku ya afya ya macho duniani.
“Ningependelea wasipende kuzivaa kama fasheni ya
kawaida,kwasababu zina madhara sana. Kwasababu hizo
kope unabandika kwa kile kitu ambacho ile chemical ya
kubandikia ndio huwa inaogopwa zaidi kuliko hata kope
zenyewe. Ingekuwa labda unazibana na stapler hivi labda
lakini kuna kitu unabandikia ile kitu ndio jicho halikitaki
kama kinaendelea kukaa pale muda mrefu,”alisema Kabona.

'Performance' ya Chris Brown Mombasa Yamchefua Rama Dee

$
0
0
Katika show hiyo, alisindikizwa na wasanii kama Wizkid kutoka Nigeria, Alikiba kutoka Tanzania, Vanessa Mdee kutoka Tanzania na baadhi ya wasanii kutoka nchini Kenya na Uganda.

Katika show hiyo msanii huyo maarufu kutoka Marekani Chris Brown alionekana akiimba kwa kufuatiliza CD yaani 'Playback' na si kufanya muziki 'live' jambo ambalo limemfanya mwanamuziki Rama Dee kutoka Tanzania kuonesha kuwa hakupenda kile alichofanya msanii huyo mkubwa.

Rama Dee kupitia ukurasa wake wa Instagram alindika na kuwataka watu wa Afrika kushtuka kwani yeye hajapendezwa kabisa na kile alichofanya Chris Brown kwenda kuimba kwa kuifuatiliza CD nyuma ili hali inafahamika kuwa yule ni msanii wa kimataifa, hivyo alipaswa kuonesha utofauti mkubwa katika kufanya show.

"Huyu naye kaenda Mombasa kaweka 'CD' kaanza kuimbia juu. Ndiyo msanii wa kimataifa huyu? Tuamke waafrika jamani" aliandika Rama Dee

Nilimpenda Msichana Kumbe ni Jini, Amenitesa Sana

$
0
0
Naitwa Patrick Bundala niko mailimoja Kibaha ni mwajiriwa wa serikali ni Askari ila nyumbani ni Tabora na huku niko kikazi tu, nina mke na watoto 4.

Kuna kitu kibaya kilinitokea nikiwa kozi ya uongozi huko Zanzibar mwaka 2009, tukiwa kozi tulikua tunapata mapumziko siku za weekend hivyo kutumia nafasi hiyo kwenda kutembea beach na siku hiyo ya tukio baya.

Ilikua jumamosi ambapo tuliondoka tukiwa wengi tu kama 50 na kwenda maeneo ya kilimani karibu na migombani ambako kuna beach nzuri sana na siku ya jumamosi jioni beach huwa inajaa watu wa kila aina na siku hiyo haikua mara ya kwanza mimi kwenda huko beach kwani kila weekend lazima niende huko beach ili kuburudisha macho na kuangalia mazingira na watu maana mimi kwa Zanzibar ilikua mara ya kwanza kwenda hivyo kwa umaarufu wa Zanzibar nilitaka hadi natoka huko niwe na cha kuwasimulia huku nyumbani kumbe ilikua bahati mbaya sana kwangu siku hiyo,

Wakati siku hiyo tumefika beach tulitawanyika kila mtu eneo analotaka na wengine walienda kuogelea na mimi licha ya kufahamu kuogelea lakini siku hiyo sikutaka kuogelea lakini nilitaka kutafuta binti mzuri ili nimtongoze na tuwe wapenzi na nilienda pembeni kidogo eneo ambalo watu walikua wachache na kukaa mkao wa kuangalia watu na baada kama ya dakika 40 alipita dada mmoja aliyevaa ninja akiwa ni nusu mwaarabu na nusu mwafrika na nikajikuta namtamani sana alinipita kidogo na kugeuka na kuniangalia na mimi nikaona hiyo ndio nafasi ya kumwogelesha na kikamwita akaja na ajabu sikumwambia chochote lakini sijui aligundua kuwa natafuta mwanamke maana alisogea na kunisalimia na akakaa pembeni yangu na kunichangamkia sana,

na kwa sababu nilitaka mpenzi nilidhani kuwa huyo ni changudoa ambaye huwa anaenda kutafuta wanaume beach,

Baada ya kukaa tuliendelea na story na ajabu yule dada akaniambia mwenyewe kuwa amenipenda sana maana nimemjali na mimi nikaona kuwa hiyo nafasi ya kumpata mrembo yule siwezi kuipoteza na muda huo huo nikaanza kumwambia mambo ya mapenzi maana nilidhani ni kahaba na nilipomwambia hivyo alicheka na kusema amekubali ila anataka ajue kwanza jina langu,

kwa sababu ya kuepusha maswali ya kuulizwa zaidi na ili asije akakataa kwa sababu ya majina yangu ya kikristo japokua hata kanisani sijawahi kwenda nilimwambia kuwa mimi naitwa Saleh Juma na yeye akasema anaitwa Munira, akafurahi sana na kusema kuwa nafaa sana na amefurahi sana kukutana na mimi.

Sikutaka kuopoteza nafasi hiyo nilimwambia kuwa tunaweza kuwa wote usiku ule? akasema mbona mapema sana nikasema kwa sababu amenivutia sana, akaongea kwa madaha na kusema amekubali na kwa sababu ya binti yule nilisahau yote na kumwambia tuondoke twende tukaongelee guest house akakubali na tukaondoka saa ile ilie na kupanda gari za airport na tukashukia mkunazini na kutafuta gest tulipata na nikaalipia na tukaingia chumbani na lengo langu japokua nililipia chumba hadi asubuhi lakini nilitaka tu tufanye mapenzi na niondoke kuwahi foleni ya usiku kule kozi,

Tukiwa chumbani tulianza michezo ya kimapenzi na akanivulisha nguo zote na mimi nikamvulisha nguo zote isipokua nguo ya ndani na baadae kidogo akashuka kitandani na kusimama huku akinitazama kwa macho makali sana nikaanza kushtuka na ghafla kibanio chake cha nywele kikaachia ghafla na tukio la ajabu sana likatokea nywele zake zikalefuka na kuongezeka zikajaa chumba chote,

Nikiwa nimejilaza kitandani nilikaa ghafla na baada ya muda kidogo zile nywele zilisinyaa na kuwa za kawaida na kile kibanio kijiweka mahali pake na kubana nywele,

Munira akasema kuwa yeye ni jini na anataka tu damu yangu kwani ana njaa sana nilikimbilia mlangoni ghafla huku nikiwa uchi na kujaribu kufungua mlango lakini haukufunguka japokua hatukufunga, akasema siwezi kumtoroka hata siku moja na kwa sababu mimi nimempenda na yeye amependa nyama yangu na damu yangu,

Nilijikaza lakini nilikua hoi karibu na kuzimia na nikaona njia iliyobaki ni kupiga kele ili watu waje kunisaidia na nilipopiga kele sauti haikwenda kokote maana nilipanua mdogo kwa nguvu zangu zote lakini sauti iliyotoka ni kama namng'ong'eza mtu kiukweli nilikua kama nimechanganyikiwa na niliposhidwa zoezi hilo niliwaza kuwa njia iliyobaki ni kulibembeleza tu lile jini na nilipoliangalia nilikuta linakwato miguuni na miguu ina manyoya kama mbuzi na meno limetoa na kuwa marefu zaidi ya rula ya kupigia mistari,

Hakuwa tena yule msichana mrembo munira ambaye nilimpenda sana kwa muda mfupi, Nilimwambia yule jini anibadilishie adhabu akakataa na nilijikuta naomba maombi kwa MUNGU anihurumie na ajabu kama dakika 5 zilizofuata mlango uligogwa na ghafla lile jini likawa Munira yule wa beach na kwa sababu ya mlango kuendelea kugongwa yule jini alienda kufungua na mimi muda huo nikaanza kuvaa nguo kiaskari yaani nusu dakika nimeshavaa zote,

Alikua ni dada wa mapokezi akileta chakula chipsi mayai na na soda na munira kwa ujanja akasimama katikati ya mlango na kuanza kusema sisi hatukuagiza chochote na muda huo huo nikamwambia yule dada aingie ndani maana kuna kitu nataka kumtuma akaja na alipokaribia tu nikatoka ghafla na kumwaga kile chakula chote huku nikisema kuwa yule dada sio mtu ni jini yule dada mhudumu naye akaakimbia na sikujua kilichoendelea ila nadhani yule jini alipotea muda huohuo maana nilipofika tu nje nilimkuta akinisubiri na kuniambia sina ujanja wa kumtoroka na kwasababu ilikua ni barabarani na watu wengi wanapita nilipiga kelele na kusema jamani niokoeni na vijana fulani waliokua wanapita mmoja wao akasema wewe umekua chizi yaani unaongea peke yako niliondoka kwa kukimbia kama mita 100 na kupanda gari ambayo ilinipekeka hado kambini.

Nilipofika tu kambini nilimwona tena yule jini na akaniambia kuwa kuniua lazima anaiue tu tena usiku uleule nilipiga tena kele na askari wenzangu wakaanza kucheka sana wakisema nimepandisha mashetani na nikawaelezea kuwa sijapandisha chochote ila ni hali halisi na nikawasimulia mwanzo wa tukio hadi mwisho na usiku huo sikulala maana usiku wa saa 7 nilimwona tena yule munira jini na nikapiga kelele na wenzangu kwa hasira wakasema nisiwasumbue lakini mmoja wao ambaye ameokoka akaniambia namhitaji YESU ili niwe huru.

Kwa sababu ya shida nilimwambia niko tayari kuokoka kuanzia sekunde ile, akasema kuwa wao wana kundi lao la maombi hapo kozi ambalo ni kundi la waliookoka kutoka makanisa mbalimbali na huwa wana ratiba ya maombi hivyo muda ukifika atanijurisha ili twende wote na muda huo akaniombea ulinzi wa MUNGU.

Muda wa maombi ulipofika tulikwenda na niliombewa na wakati wa maombezi ikasikika sauti kuwa ipo siku watanipata tu, lakini namshukuru MUNGU sana maana nilipona tangu saa ile na nimeendelea na wokovu hadi leo na hakuna chochote walichofanya. Nampenda YESU na namshukuru sana kwa kuniponya na kuniokoka pia kuniepusha na mabaya yale. MUNGU akubariki sana ndugu mtumishi wa MUNGU

Majambazi 4 walioua polisi wanne Mbagala, wauawa

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewaua majambazi 4 na kukamata silaha ya jeshi hilo iliyoporwa atika tukio la ujambazi kwenye uvamizi wa Benki maeneo ya Mbande Mbagala ambapo polisi wanne waliuawa.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema majambazi hayo ndiyo waliohusika na mauaji ya polisi na kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba waliuawa baada ya majibizano ya risasi na polisi katika pori la Dondwe mpakani mwa Chanika na Mkoa wa Pwani.

Kamanda Sirro amesema jumla ya silaha 2 na risasi 24 na bomu moja lililotengenezwa kienyeji, vimekamatwa katika matukio tofauti jijini humo sambamba na kuwakamata 'Panya Road' 10 wenye umri wa miaka chini ya 18 wanojihusisha na matukio ya uporaji katika maeneo ya Mbagala Jijini Dar es Salaam.

Vijana hao wenye umri chini ya miaka 18 wanaojihusisha na matukio ya uhalifu maeneo ya Mbagala walifikishwa mbele ya wanahabari ambapo Kamanda Sirro ameitaka jamii kuwalea watoto wao vizuri na kuendeleza ulinzi wa polisi jamii kwenye maeneo yao.
Aidha Jeshi hilo pia limekamata shehena ya mafuta ya kula yenye madumu 453 kwa kukwepa kodi yenye thamani ya shilingi 14,296, 680 na mtambo bandia wa kutengeneza pombe aina ya Konyagi, rola 57 za viroba pamoja madumu sita yenye ladha ya kutengenezea kinywaji hicho.

U HEARD: Ya Video queen wa Jike Shupa kuzaa na Juma Nature

$
0
0
October 13, 2016 kupitia U Heard ya Clouds FM, mtangazaji Soudy Brown amepiga story na mrembo aliyeonekana kwenye Video ya star wa hit single ya Jike Shupa, Nuhu Mziwanda aitwaye Zena Abdallah ambaye ameeleza kuhusu mtoto wake ambaye inadaiwa alizaa na msanii Juma Nature.

Mtoto wangu ni mkubwa ana miaka nane, Juma asingeweza kukataa mtoto wake jamani hawezi kukataa damu nzito kuliko maji anafanana naye sema tu ni mweupe sababu mimi ni mweupe. Na anampa matunzo sababu anaishi naye kwake tangu akiwa na miaka miwili:- Jike Shupa

Kuipata stori kamili Play hapa chini.

Aliyepigwa na Walimu Mbeya aeleza kwanini hakwenda Hospitali

$
0
0
Jina lake ni Sebastian Chinguku mwanafunzi wa shule ya sekondari Mbeya Day kidato cha tatu ambae video yake ya kupigwa fimbo mateke na makofi na Walimu ilisambaa sana kwenye mitandao na imekua gumzo mpaka viongozi wa Serikali ikiwemo Mawaziri kuingilia kati.

Anachokisema leo Sebastian kwenye AyoTV ni kwamba hakwenda Hospitali baada ya kuumizwa na kipigo cha Walimu sababu aliogopa angeulizwa PF3 lakini pia baada ya kipigo alishindwa kuendelea kwenda shule sababu ya maumivu na nguo za shule zilichanika akipigwa.


‘Baada ya tukio walimu waliniuliza mimi kama mimi nafanyaje, nikawaambia mimi nasamehe hili swala baada ya kuona Walimu wameshachukulia mimi ndio mwenye matatizo, nilihofia kufukuzwa shule moja kwa moja maana kosa langu niliambiwa ni kosa la kupiga Walimu‘ anasema Sebastian

‘Baada ya hapo sikuona haja ya kwenda Polisi au kulifikisha hilo swala popote kwengine kwasababu nilishawasamehe tarehe 28 September, nikabaki nyumbani tu baada ya tukio nikawa nauguzwa na pacha wangu ambaye ni mdogo wangu, Baba yuko kikazi Mbozi na mama yuko Dar anauguza… shule sikwenda toka September 28‘ – Sebastian


Sebastian anasema chanzo cha kupigwa na Mwalimu ni kutokufanya kazi iliyotolewa na Mwalimu darasani siku ya Jumatatu
 ‘Sikuweza kuifanya sababu sikwenda shule Jumatatu nilikua naumwa, nilipokwenda Jumatano nikakuta adhabu inatolewa, nikamuelezea Mwalimu kuwa nilikua naumwa lakini hakunisikiliza hivyo nikakubali kuadhibiwa

JE Ni Sahihi Kumlazimisha Mwanaume Akuoe?

$
0
0
Habari zenu,

Hivi ni sahihi pale uko na mpenzi wako yapita mwaka, miaka ajawahi kukuambia kuhusu ndoa au labda alikuhaidi kuja nyumbani lakini siku zayoyoma hakuna matokea yoyote je, ni sahihi kumlazimisha akuoe au huyu yupo kwa ajili ya kupotezeana muda tu?

Polisi Dar Yaua Majambazi Wanne Wanaodaiwa Kuwaua Askari Wanne Waliokuwa Lindo Mbagala DSM Mwezi Agosti, Yakamata 'Panya Road' 10.

$
0
0
Kikosi Maalumu cha Kupambana na Ujambazi wa Kutumia Silaha cha Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kilifanikiwa kukamata watuhumiwa wanne wa ujambazi waliohusika katika mauaji ya askari polisi 4 katika benki ya CRDB iliyopo maeneo ya Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, amesema watuhumiwa hao walikamatwa wakati wa majibizano ya risasi yaliyotokea Oktoba 11, 2016 katika pori la Dondwe lililopo Chanika.

“Kikosi kilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja, baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa ni jambazi na ndiye aliyehusika katika mauaji ya askari polisi huko Mbande,” amesema.

Kamanda Sirro ameongeza kuwa “Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na tukio hilo akiwa na wenzie saba, alitupeleka mahala walipo wenzake, ila alikimbia, wenzie walipojua polisi wapo maeneo hayo, walianza kurusha risasi ndipo polisi nao wakaanza kurusha risasi.”

Kamanda Sirro amesema kuwa, watuhumiwa hao walizidiwa na mashambulizi ya risasi ambapo walijeruhiwa vibaya na kwamba walifariki dunia wakiwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Amesema askari polisi walifanikiwa kuipata bunduki ya kijeshi aina ya SMG iliyofutwa usajili ambayo watuhumiwa hao waliipora kutoka mikononi mwa polisi waliowaua mbande ikiwa na risasi 22 ndani ya magazine.

Katika tukio lingine, Kamanda Sirro amesema mnamo Oktoba 11, 2016 maeneo ya magomeni polisi wakiwa doria walifanikiwa kukamata bastola moja aina ya bereta baada ya kutelekezwa na kundi la vijana.

Pia amesema Jeshi la Polisi limekamata watuhumiwa watatu wakiwa na bomu moja la kienyeji, mapanga manne, visu viwili, na bisibisi moja.

Vilevile Jeshi la Polisi Dar es Salaam Oktoba 12, 2016 walikamata panya road zaidi ya 10 maeneo ya Mbagala.

Meneja wa Alikiba Ajibu Tuhuma za Show ya Mombasa na za Kutunishiana na Wizkid

$
0
0

Aidan Charlie ambaye ni meneja msaidizi kutoka kwenye Menejimenti ya mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba ameongea kuhusu tuhuma mbalimbali zilizotolewa dhidi ya Alikiba kutokana na show ya Mombasa iliyofanyika weekend iliyopita na zifuatazo ni kauli zake.


  • Sio kweli kwamba Alikiba alisema yeye ni msanii mkubwa Afrika Mashariki hivyo Wizkid ndio alitakiwa kupanda stejini kabla yake, alietoa hizo habari kadanganya.



  • Kilichotokea ni kwamba kiujumla Waandaaji hawakuwa wamejipanga vyema, show ilitakiwa kuanza saa nane mchana lakini wakaipeleka mbele mpaka saa tatu usiku.



  • Ishu ilikua wakati Chris Brown alipofika kuliangalia jukwaa na kuzoea mazingira ilibidi seti yote ya Alikiba iliyopangwa jukwaani iondolewe pamoja na watu wa Ali, hiyo ikafanya Alikiba achelewe kufanya rehearsal ambapo alimaliza saa mbili usiku na kurudi hotelini kwenda kujiandaa na show.



  • Tumerudi tu hotelini tunapigiwa simu kuambiwa mnatakiwa kupanda kwenye stage ikabidi Alikiba arudi uwanjani lakini muda ulikua umeyoyoma na Chris Brown alitakiwa kutumbuiza mapema ili awahi Airport.



  • Hakuna kutunishiana misuli kokote kati ya Wizkid na Alikiba, wawili hawa wako vizuri na walikua wanaongea backstage na Wizkid alimwambia Ali haondoki uwanjani mpaka aone show yake

Imeripotiwa Kupotea Kwa Rais wa Malawi, Peter Mutharika

$
0
0
Habari kubwa zinazotrend sasa hivi mtu wangu moja nii hii iliyoripotiwa na kituo kikubwa cha habari Kenya cha Citizen kupotea kwa Rais wa Malawi, Peter Mutharika ambae hajarudi nchini kwake tangu alivyoondoka kuelekea New York Marekani kwenye mkutani mkubwa wa Umoja wa Mataifa kwa mujibu wa rekodi imetajwa kuwa aliondoka nchini New york, September 15 2016 na mpaka sasahivi hajawasili nchini kwake Malawi.

Rais Mutharika amepotea kwa muda wa wiki 3 tangu sasa aondoke nchini kwake na imepelekea raia wa nchi hiyo kuweka hashtags kwenye mitandao ya kijamii zikisema #bringbackMutharika haswa kwenye twitter kama unavyoona hapo chini.

TCRA Yapiga Marufuku Uuzwaji wa Samsung Galaxy note 7 Hapa Nchini

$
0
0
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepiga marufuku uingizaji na usambazaji wa simu za mkononi za Smartphone Samsung Galaxy note 7 kwa kuwa zina matatizo ya betri.

TCRA pia imewataka wananchi ambao tayari wanatumia simu hizo kuzizima na kuzirudisha haraka katika maduka walikozinunua.

Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy, amewataka watanzania wajihadhari kuitumia simu hiyo kwa kuwa Kampuni ya Samsung yenyewe imeiondoa sokoni.

“Simu hiyo tayari Samsung wenyewe wamesema ina matatizo ya betri na mara mbili sasa imelipuka,” amesema Mungy.

Amewaomba watu wenye simu za aina hiyo kuzirudisha madukani haraka wabadilishiwe ama kurudishiwa fedha zao.

“Hata kama uliletewa zawadi kutoka nje ya nchi nawaomba warudishe huko   kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza,” amesema Mungy.

Hivi karibuni simu aina hiyo iliyothibitishwa na kampuni hiyo kuwa ilikuwa salama, ilishika moto kwenye ndege nchini Marekani.

Simu hiyo inadaiwa kushika moto ikiwa mikononi mwa abiria aliyekuwa kwenye shirika la ndege la Southwest Airlines.

Shirika hilo liliwaondoa kwa dharura abiria waliokuwa kwenye ndege  iliyokuwa imepangiwa kusafiri kutoka Louisville, Kentucky, hadi Baltimore, Maryland muda mfupi kabla ya kupaa.

Picha: Tunda Man afanya ‘Send-off’ na mrembo huyu

$
0
0
Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Tunda Man pamoja na mpenzi wake wa muda mrefu wamefanya ‘send-off’ wakijiandaa kuingia katika maisha ya ndoa.
tunda3

Alhamisi hii usiku zilisambaa picha katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha Tunda Man pamoja na mpenzi wake wakiwa kwenye ‘send-off’.

Mmoja kati ya wasanii ambao walihudhuria shughuli hiyo ni Dojo Janja ambapo alimpongeza msanii huyo kwa hatua hiyo.

“From❤️ congrats my big brother captain @tundamantz. Kesho tunabeba jiko letu mapema mapema tu, hatucheleweshi mambo. Mimi ninao wengi sijui nioe yupi,” aliandika Dogo Janja Instagram.

Wiki chache zilizopita, muimbaji huyo wa wimbo ‘Mama Kijacho’, aliiambia Bongo5 kuwa atafunga ndoa hivi karibuni.

“Kusema kweli suala la kuoa naoa hivi karibuni. Kwa hiyo mtu yeyote anakaribishwa na nipo tayari kuingia kwenye maisha ya ndoa,” alisema Tunda Man

Gigy, Amber Lulu Waingia Kwenye Vita Baridi

$
0
0
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kuwa baada ya habari kuzagaa kuwa Amber Lulu amekamatwa na polisi Arusha akiwa na unga, Gigy amekuwa akimsema mwenzake huyo vibaya, mazingira yaliyosababisha wawili hao waanze kuraruana kwa maneno.

Akizungumza hivi karibuni, Amber Lulu alisema: “Nawashangaa hao wanaonisema vibaya kufuatia hizo tetesi, hasa Gigy ila siwezi kujibishana naye kwani siyo levo yangu.”
Gigy naye akafunguka: “Ni kweli nilimsema kuwa kama kweli kakamatwa na unga atakuwa katuaibisha sana. Huo ndiyo ukweli sasa akitokwa na povu atokwe tu.”

Ubunge wampita Kushoto baada ya Mahakama ya Rufaa Kutupilia Mbali Maombi Yake

$
0
0
Hatimaye mbio za David Kafulila kupinga mahakamani matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa Kigoma Kusini ya Oktoba mwaka jana uliompa ushindi Husna Mwilima (CCM) zimefika ukingongoni baada ya mahakama ya rufaa kutupilia mbali maombi yake.

Jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa waliokaa mjini Tabora, jana lilitoa maamuzi yake kuhusu rufaa ya Kafulila na kueleza kuwa wameyatupilia mbali maombi hayo kwakuwa yamekosa nguvu yenye uhalali wa Kisheria.

Aidha, Mahakama hiyo ya Rufaa imemtaka Kafulila ambaye hakuhudhuria mahakamani hapo, kulipa gharama zote za shauri hilo la madai namba 212 la mwaka 2016.

Akizungumza baada ya maamuzi hayo ya Mahakama ya Rufaa, Mbunge wa Kigoma Kusini, Mwilima alisema Kafulila alijua kuwa hakuwa na madai yoyote mahakamani na kwamba alicholenga ni kumsumbua ili akose muda wa kuwatumikia wananchi wake.

“Kafulila alijua fika kuwa hakuna kesi ya yeye kukata rufaa. Lakini alikata rufaa kunisumbua ili nikose muda wa kuwatumikia wananchi waliniingiza bungeni,” alisema Mwilima.

Kafulila alifungua shauri la madai namba 2 la mwaka 2015 katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora, akipinga ushindi wa Mwilima. Katika shauri hilo, Kafulila aliwalalamikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Msimamizi wa uchaguzi na Husna Mwilima.

Mahakama Kuu iliyatupilia mbali maombi ya Kafulila ya kutaka kutengua ubunge wa Mwilima ndipo Mbunge huyo wa zamani wa Kigoma Kusini alipoamua kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa ambayo ni Mahakama ya juu zaidi nchini.

Kesi hiyo iliyovuta umakini wa wananchi wengi jimboni humo na huenda ndio kesi ya uchaguzi iliyovuta watu wengi zaidi tangu kumalizika kwa uchaguzi wa mwaka jana, imefikia ukingoni kwa kuhalalisha ubunge wa Mwilima.

Diwani Chadema Anaswa na Dawa za Kulevya, Bunduki Diwani Chadema Anaswa na Dawa za

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Diwani wa kata ya Izira, Paschael Silimba (Chadema) baada ya kumkamata akiwa na dawa za kulevya aina ya bangi na bunduki moja aina ya gobole.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, George Kyando amesema kuwa jeshi hilo lilimkamata Kyando katika eneo la soko kuu ambalo hufanyia biashara yake ya kuuza mifuko ya salfeti, baada ya kupata taarifa na kuamua kumfuatilia.

Alisema kuwa baada ya kumpekua katika vifurushi vya bidhaa hiyo anayoiuza kwa kushirikiana na mkewe, walibaini uwepo wa bangi kiasi cha robo kilo.

“Baada ya kufanya upekuzi kwenye duka la diwani huyo, tumefanikiwa kukamata bangi kiasi cha robo kilo. Ni bangi kavu ambayo imeshaandaliwa tayari kwa ajili ya kufanya packing na kuuzwa,” alisema Kamanda Kyando.

Akizungumzia silaha aina ya gobole waliyoikuta nyumbani kwa diwani huyo anayodaiwa kuimiliki kinyume cha sheria, alisema ingawa ni silaha ya kizamani ina nguvu ya kuua tembo.

“Silaha hii ina nguvu sana, ina uwezo wa kuua tembo na ni hatari sana akipigwa binadamu kwa silaha hii. Kwahiyo msiione hapa mkaidharau, ina nguvu sana,” aliongeza.

Kamanda Kyando aliwataka viongozi wote waliopewa dhamana na wananchi kutotumia nyadhifa zao kufanya uhalifu. Alitoa wito wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kufichua uhalifu bila kujali waliofanya uhalifu huo.

Ester Bulaya Kuwekwa Kikaangoni Jumatatu

$
0
0
ESTER Bulaya, Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, mkoani Mara anatarajia kupanda kizimbani Jumatatu ya tarehe 17 Oktoba, mwaka huu ili kutoa ushahidi wake katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge inayomkabili, anaandika Charles William.

Bulaya atalazimika kuhojiwa na kujibu maswali ya mawakili wa upande wa walalamikaji kwa upana zaidi baada ya kiapo chake kuingizwa katika kumbukumbu za Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza.
Hatua hiyo inakuja baada ya Jaji Noel Chacha wa mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi lililowekwa na Costantine Mutalemwa, wakili wa waleta maombi ambaye alikuwa akiomba baadhi ya aya zilizopo katika hati ya kiapo cha Bulaya zifutwe.

Tundu Antiphas Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ndiye wakili wa Bulaya katika kesi hiyo ambapo amepiga kambi mkoani Mara kwa takribani wiki mbili sasa wakati shauri hilo likiendelea.

Katika kesi hiyo namba moja ya mwaka 2015, walalamikaji ni watu wanne wakiongozwa na Magambo Masato, watu hao wamejitambulisha kama wapiga kura katika jimbo la Bunda Mjini huku Steven Wassira, aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa ni miongoni mwa mashahidi wa upande wa walalamikaji.

Mkurugenzi Amgomea Waziri Mkuu

$
0
0
AGIZO la Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, kuwataka watendaji wa Serikali kutoa taarifa katika vyombo vya habari juu ya mipango ya maendeleo inayofanywa na serikali, limepuuzwa na Godwin Kunambi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, anaandika Dany Tibason.

Leo baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi uliofanyika ili kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere, muasisi wa Taifa la Tanzania, Kunambi amekataa kuzungumzia lolote juu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu la kuondoa nyumba za tope katikati ya Mji wa Dodoma.
“Siwezi kuongea jambo lolote kwa sasa ninawaachia Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa waongee. Bora ningekuwa nazungumza na radio au TV lakini katika gazeti siwezi kuzungumza chochote, niache tu,” amesema Kunambi alipozungumza na mwandishi wa MwanaHALISI online.

Pamoja na mwandishi kumkumbusha kuwa Mkurugenzi ndiye mtendaji mkuu wa manispaa hivyo ni vyema akatoa ufafanuzi juu ya hatua gani ambazo manispaa yake imezichukua mpaka sasa ili kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kuondoa nyumba za tope na kuboresha miundombinu lakini Kunambi aligoma.

Hivi karibuni baada ya kuanza utekelezaji wa kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi, Waziri Mkuu Majaliwa alijitambulisha kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Dodoma na kuwaagiza wakuu wa Idara mbalimbali pamoja na watendaji wa serikali kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa vyombo vya habari.

“Toeni taarifa za utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya serikali katika vyombo vya habari bila kukibagua chombo chochote,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Kitendo cha Kunambi kukataa kuzungumzia mipango ya maendeleo hususani utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu la kuondoa nyumba za tope katikati ya mji ni kupuuza agizo lake la awali la kutaka taarifa muhimu za mipango ya maendeleo zitolewa katika vyombo vya habari bila kuvibagua vyombo hivyo.

Faiza Ally Awaponda Wasanii wa Bongo, Asema Wanawake Watalalwa Wakizeeka Wataachia Wenzao

$
0
0
Msanii wa filamu Tanzania, Faiza Ally amefunguka kuhusiana na mwenendo wa tasnia ya Bongo Movie inayoendelea kwa sasa. Kupitia mtandao wa Instagram, muigizaji huyo amedai kuwa kwa sasa uigizaji si kazi ya kuichagua kuifanya labda uwe na njia mbadala tofauti na iliyopo sasa.

“Katika wasanii ambao wengi watakufa maskini Tanzania ni wasanii wa filamu… Na hii itakua Kama laana itakayo dumu kwa muda mrefu sana……! Wanaume wataishia kujenga labda na maisha ya kula Na kulala Na kulala na wanawake wengi huo ndio utakua utajiri wao ! Wanawake watalalwa wakizeeka wataachia wenzao itakua ndio mtindo …

Na ujana haudumu muda mrefu ! Mpaka pale ambao wanaume wataamua kufanya kazi Na kutenda haki Kwa wasanii hasa wa kike…. Na wanawake watakapo ona wana uwezo binafasi bila kutumia mastaa wa kiume kazini…. Na zaidi kutumia hela zao ktk kuwekeza ktk kazi …. kiukweli huwa nachoka sana pale ninapo ona haki hupati pamoja Na kufanya kazi … Kuna wkt najuta kuipenda sanaa… Na Ndio Maana Nilipo produce movie yangu ya kwanza niliacha Kwa muda mrefu sana …

Na nahisi baada ya hii mpya ntakaa Tena kuangalia soko Tena Kwa mara nyingine…. Kwa sasa filamu sio kazi ya kuchagua Na Kama unachagua Basi uwe Na namna ya kipato tofauti Na FILAMU…. Vinginevyo Kama mwanamke utaishia kugawa uroda mpaka yesu ashuke ! Kama mwanaume utabaki kuomba mpaka Basi…. Walio shika soko ni watu wenye roho mbaya ambao wanahisi wakiachia karakta zingine zitawashinda Na Kwa akili zao fupi wana hisi Ndio ujanja kumbe wana zidi kushusha soko la filamu….

Mm huwa namuona Diamond ni bonge la mjanja ambavyo Ana ibua wasanii wapya kupitia wasafi…. sio mjinga Kabisa amegundua hata kuwa Diamond milele….. yaani Kama ningekua nimejikita sana huko ningejambia hewani lkn MUNGU NI MWEMA kuna maisha zaidi ya filamu….. Any way lkn sitaacha kamwe kufanya filamu Kwa sababu napenda Lkn Kwa wkt Na sio kutumika kijanga….. Kinadada wanatumika sana lkn maendeleo hakuna Kabisa …. Wanaume wa bongo movie sio watu wazuri Kabisa …. Machoni Kama watu……
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images