Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Lionel Messi Anatuhumiwa Kuzuia Mchezaji Mwenzake Asiitwe Timu ya Taifa

$
0
0
Timu ya taifa ya Argentina inatajwa kuwa katika nafasi mbaya ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi, hiyo inatokana na Argentina kuwa nafasi ya tano katika msimamo wenye timu 10 huku timu nne za juu ndio zitafuzu.

Kufuatia Argentina kuvuna point mbili katika mechi zao tatu zilizopita, mjadala kutoka katika moja ya vituo vya TV Argentina umetoa madai tofauti kutokana na urafiki wa Lionel Messi na kocha wa timu yao ya taifa ambao umetajwa kuwa Messi amemshawishi kocha asimuite Mauro Icardi kikosini licha ya kuonesha uwezo mkubwa akiwa na Inter Milan.

Urafiki wa karibu wa Messi na mchezaji mwenzake wa zamani wa FC Barcelona  Maxi Lopez ambaye ana ugomvi na Mauro Icardi kutokana na kuwa alimpokonywa mke, hivyo Messi anatajwa kutovutiwa na kitendo hicho na kumshawishi kocha asimuite Icardi, Mauro Icardi ameichezea Argentina kwa dakika 8 tu, hivyo wengi walitamani kumuona akiongeza nguvu.

UTAFITI: Nairobi Imetajwa Kwenye Top 10 ya Majiji Yenye Foleni Zinazokera Duniani

$
0
0
Watu wangu wa Kenya hii inaweza kuwa taarifa mbaya kwao hasa wakazi wa jiji la Nairobi. Ni baada ya kutoka list ya majiji 10 yaliyotajwa kuwa na kiwango kikubwa na foleni za Magari ambazo hupelekea kuwa kera watumiani wa barabara za jiji hilo.

Jiji la Nairobi limetajwa kushika nafasi ya 9 ya majiji yenye foleni zinazoongeza kiwango kikubwa cha hewa chafu ya Carbon dioxide na zinazokera duniani.

Utafiti uliofanywa na mtandao wa Numbeo umezingatia kiwango cha muda unaotumiwa na magari ya kusafirisha abiria kila katikati ya miji na kuonesha kwamba wastani wa chini wa muda unaotumiwa na abiria kwenye foleni ni dakika 65.20 kwa kila safari moja.

Kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Kenya zilizotolewa mwka huu mwezi wa Tano zilionesha kuwa Serikali inapoteza kiasi cha shilingi milioni 58.4 za Kenya kwa siku ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni moja za Tanzania kutokana na foleni za magari nchini humo.

Kwa Africa, Nairobi imeshika nafasi ya tatu ikiwa nyuma ya jiji la Pretoria kutoka Afrika Kusini na jiji la Cairo nchini Misri

Hii ndio Top 10 ya majiji yenye foleni zaidi duniani.

1. Manila, Philippines – Dakika za kusubiri foleni: 54.33

2. Pretoria, South Africa – Dakika za kusubiri foleni: 52.25

3. Recife, Brazil – Dakika za kusubiri foleni: 57.85

4. Tehran, Iran – Dakika za kusubiri foleni: 59.84

5. Miami, Florida – Dakika za kusubiri foleni: 59.20

6. Kolkata, India – Dakika za kusubiri foleni: 58

7. Cairo, Egypt – Dakika za kusubiri foleni: 58.61

8. Pune, India – Dakika za kusubiri foleni: 60.86

9. Nairobi, Kenya – Dakika za kusubiri foleni: 65.20

10. Mumbai, India – Dakika za kusubiri foleni: 66.18

Majibu ya Chris Brown Kuhusu Kumvunjia Simu Shabiki Airport Mombasa

$
0
0
Mwimbaji staa kutoka Marekani Chris Brown October 8 2016 aliungana na wasanii wengine akiwemo Wizkid wa Nigeria, Vanessa Mdee, Alikiba na wengineo kutumbuiza kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music Festival lililofanyika  Golf Club Mombasa.

Iliripotiwa kuwa staa huyo kuwa na tuhuma za kumvunjia shabiki Brenda Chepkoech simu alipowasili Airport Mombasa ambae alikuwa katika harakati za kutaka kupiga nae selfie, leo Oct 14 2016 kituo kikubwa cha habari cha Kenya, eDaily kimeripoti majibu aliyatoa Chris brown kuhusu tuhuma hizo na hiki ndicho alichokiongea staa huyo…

”Brenda Chepkoech aliyenipa tuhuma za kumvunjia simu yake oct 8 2016 alikuwa anataka free tickets ili aweze kufika kwenye show hiyo’ – Chris Brown

Imeripotiwa kuwa dada huyo alikua anawafata Chris Brown na kundi zima kuomba ticket na kutaka kupiga selfie na staa huyo lakini ombi lake halikusikilizwa, chris aliwambia marafiki zake…
’ Hata picha inaonyesha sikumsogelea dada huyo wala simu yake, Hapana sio uongo mwingine kuhusu mimi tafadhali’– Chris Brown

Mmoja waandaji wa show hiyo Thandie Ojeer alihojiwa na edaily na haya ndio aliyoyazungumza…

’ Chris hakuwa na hasira kabisa, ilikuwa mara yake ya kwanza kufika Kenya na ame enjoy kuwepo Kenya, pia ameahidi kurudi siku moja na kukaa zaidi na kufanya tour next time– Thandie Ojeer

VIDEO: Navy Kenzo Wamevitaja Vigezo Wananvyoangalia Kusign Msanii Kwenye Label yao

$
0
0
Nikitaja list ya wasanii kutoka bongoflevani pia miongoni ma group ynayofanya vizuri kwenye game huwezi kuwaacha Navy Kenzo ambapo kwasasahivi ni miongoni mwa wasanii wa Tanzania waliokuwa nominated kuwania tuzo za MTV MAMA 2016 kwenye kipengele cha Best Group zitakazo tolewa nchini South Africa Oct 2016.

Kama mnavyofahamu Navy Kenzo, Nahreel ni producer pia wana label yao binafsi ya mziki ambayo wameielezea kuingiza wasanii wao sokoni hivi karibuni Millardayo.com na AyoTV ilipokutana nao walieleza licha ya kusign tu wanamuziki kwenye label yao lakini pia wamevitaja vigezo vyao wanavtoangalia ili kusign msanii chini ya label hiyo na haya ndio waliosema.
‘Tunaplan ya kusainisha wasanii wenye vipaji awe mkubwa ama mdogo, lakini tunaangalia msanii ambae tunawezakufika nae mbali, tunangalia pia ubunifu wake, perssonality, uchapakazi na juhudi ambayo msanii anao so kujua hivi tunaka na msanii kidogo kujua hivi kabla hatujamsainisha‘ – Navy Kenzo

Tazama Video DC Richard Kasesela Akionyesha Jinsi ya Kushika Bunduki na Kupambana na Adui Katika Vita

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akionyesha jinsi ya kushika bunduki na kupambana na adui uwapo katika uwanja wa mapambano.

Ushikaji wa bunduki wakati wa pambano huwa ni changamoto kwa sababu usipokuwa umejiweka sawa ukifyatua risasi kutokana na msukumo unaweza kuanguka.

Katika video hii, baada ya DC Kasesela kumaliza anapongezwa na Wanajeshi waliokuwa katika mazoezi hayo kwa namna alivyofanya vizuri. Itazame video hapa chini.

VIDEO: Maneno ya Snura kuhusu mahusiano yake na Benpol

$
0
0
Ni kutoka kwenye basi lililobeba Wasanii wa bongofleva wakiwa safarini kwenye show za FIESTA 2016, tamasha ambalo linafanyika kwenye mikoa mbalimbali Tanzania sasa hivi.

Kwenye basi la Wasanii utajionea maongezi yao mbalimbali wakizungumzia ishu za kimaisha, kuuliza maswali, wakicheka pamoja na kuongelea mengine mengi, nimekusogezea hapa chini video ya alichozungumza Snura kuhusu mahusiano yake na Ben Pol

’Ben Pol Dodoma ni nyumbani kwao na mimi ni ukweni ndomaana alichukuwa nafasi hiyo ya kuntambulisha kwa ndugu zake na familia, Ben Pol alinipadisha kwenye stage kunitambulisha ndo ikatokea kitu kama kile sio kwamba tulifanya show pamoja mimi na yeye hapana …’ – Snura

Mwanamuziki Diamond Asema Haya Kuhusu Kufanya Collabo na Wasanii wa Kike Bongo

$
0
0
Mtu wangu leo October 15 2016 nakukutanisha na hii stori kutoka kwa mkali kutoka Bongoflevani Diamond Platnumz kuhusu mipango yake ya kufanaya collabo na watoto wa kike kutoka Bongoflevani na haya ndio yalikuwa majibu ya Diamond Platnumz.

‘Nimeshafanya wimbo na Linnah pia dada yangu Queen Darleen unajua pia uchache wa wasanii wa kike kwenye soko letu la muziki ndio linafanya tuwe na collabo chache na wasichana  unajua kuna wengine wanaogopa labda kuja kuniomba collabo lakini wasiogope sisi hapa tuna uongozi wakija tunafanya‘ Diamond Platnumz

Amini Amrushia Dongo Linah Sanga...Adai Nyimbo zake za Sasa Sio Nzuri Zinakosa Uyeye....

$
0
0
Amini aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Linah uliodumu kwa miaka mingi kabla ya kuachana na kila mmoja akawa na maisha yake.

Pia Amini aliwahi kumwandikia msanii huyo nyimbo kadhaa zilizofanya vizuri. Lakini sasa hitmaker huyo wa ‘Bado Robo Saa’ amesema kuwa Linah wa sasa si yule wa zamani katika uimbaji.

“Linah wa sasa anakosa uyeye aliokuwa nao mwanzo wakati mimi namuandikia nyimbo,” Amini alimwambia mtangazaji wa Kings FM, Prince Ramalove.

“So nyimbo anazozipata sasa hivi sio nyimbo za kuimba yeye. Nafikiri pia mwandishi anayemuandikia bado hajamjulia jinsi ya kumwandikia nyimbo za aina gani au idea ya aina gani, vile vile studio anazorekodia au producer anayerekodi naye anakuwa hajamjulia,” aliongeza.

Amini anasema bado ana uwezo wa kumwandikia Linah kwakuwa ni kwake ni sehemu ya biashara

Diamond Kufanya Collabo na Mwanamuziki Usher Raymond....

$
0
0
Spidi ya Diamond kulitafuta tobo la Marekani inatisha. Akiwa na collabo kibindoni na French Montana, Yo Gotti na Ne-Yo ambaye watakuwa na ziara ya pamoja Uingereza Disemba mwaka huu, muimbaji huyo wa ‘Salome’ ametoa hint ya mradi mwingine ujao na role model wake mwingine – Usher.

Ametoa hint hiyo Ijumaa hii wakati akimpongeza muimbaji huyo wa ‘No Limit’ katika siku yake ya kuzaliwa.
“Happy Birthday Bro… Can’t wait for our Big day! @usher,” ameandika kwenye Instagram.
Kwa muda mrefu Diamond amekuwa akiwataja Ne-Yo na Usher kuwa ni watu anaowaangalia sana.

Bilionea Mohammed Dewji Akoshwa na Mafanikio ya Mwanamuziki Diamond...Asema Haya

$
0
0
Miongoni mwa bilionea wa Afrika aliyekuwa Mbunge wa Singida na CEO wa MeTLGroup, Mohammed Dewji, afunguka kuhusu Diamond platnumz.

 Dewji amemwaga sifa kwa mwanamuziki Diamond Platnumz kuwa ni miongoni mwa wanamuziki wa wakubwa barani Afrika lakini mwenye uwelewa mzuri.
Kupitia account yake ya Instagram, Mohammed Dewji, aliweka picha yake akiwa na Diamond na kuandika maneno hayo kwa Kingereza yaliyo someka hivi..

Today afternoon with @DiamondPlatnumz

 One of Africa’s biggest and smartest artists in the music industry #TanzaniansUnite

Tetesi za Rapper Chemical Kuwa Mapenzini na Producer Wake Maximizer

$
0
0
Rapper wa kike Bongo, Chemical amefunguka kwa kuelezea
sababu inayomfanya afanye kazi nyingi na mtayarishaji wa
muziki  Maximizer.

Akiongea na mtangazaji wa Radio Maisha ya Dodoma,
rapper huyo amesema Max amekuwa akimpatia kwenye
beat zake.

“Nina nyimbo nimefanya na maproducer wengine lakini
nafanya nyimbo nyingi na Maximizer kwa kuwa tumetoka
pamoja kwahiyo nikienda naye mimi nakuwa nasimama na
Max naye anasimama na pia ni mtu ambaye ananipatia sana.
Ninaweza nikaenda kufanya kazi sehemu nyingine lakini
nikiwa na Max nakuwa poa,” amesema Chemical

Rapper huyo ameongeza kuwa hana mahusiano yoyote ya
kimapenzi na Max kama baadhi ya watu wanavyofikiria.

Chris Brown Anyemelea Penzi la Rihanna Upya...Adaiwa Kujipendekeza Kwa Ndugu wa Rihanna

$
0
0
Chris Brown anaanza kuonekana kama anataka
kurudisha namba ambayo imepotea kwa Rihanna.

Kupitia mtandao wa Hollywoodlife umeripoti kwamba Chris
brown ameanza kuonyesha dalili zote za kurudisha penzi lake
kwa Rihanna baada ya kuonekana kuwa karibu na familia ya
mwanadada huyo kwa kuwatumia zawadi mbalimbali ili
kuonyesha kuwa jina lake lisisaulike katika familia ya
Rihanna.

Kupitia taarifa zilizotolewa chini ya kapeti zimesema
kwamba Chris Brown amerudi tena kwa Rihanna, amemtuma
msaidizi wake Barbados akiwa na vifurushi vyake Rihanna
na familia yake. Ametuma pombe kali, maua na rundo la
midoli kwa ajili ya watoto wote Pia aliweka michoro ambayo
ilikuwa imefunikwa na inaonekana alitengeneza mwenyewe.

Belle 9 Aupiga Vijembe Mziki wa Singeli..Adai ni wa Kupita Hawezi Jiingiza Huko

$
0
0
Belle 9 amesema hafikirii kabisa kufanya muziki wa
Singeli.

Muimbaji huyo wa R&B amesema huo ni muziki wa
kupita na katu hauwezi kudumu.

Alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa swali na mtangazaji
iwapo atafanya muziki huo mashabiki wakimtaka.

“Sitegemei,” alisema Belle9

“Hata kama nitafanya, sitofanya kama release song sababu
Singeli ni muziki fulani hivi ambao unapita, ni bubble gum
music. Sasa hivi watu wanaushabikia lakini itafika time
utapita, sio muziki wa kustick.”

JE UNAKUBALIANA NAYE?

Dc Makete Atoa Maagizo Mazito Kwa Walimu Wanaotembea Na Wanafunzi

$
0
0
Katika kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, wanafunzi wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kusoma kwa bidii kwa kuwa taifa linawategemea ikiwemo kuja kushika nyadhifa mbalimbali baada ya kuhitimu masomo yao

Kauli hiyo imetolewa jana na Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessi yaliyoadhimishwa kiwilaya katika shule ya Sekondari Lupalilo

Aidha Mkuu huyo ametoa Onyo kali kwa walimu wote wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi na kusema sheria zipo wazi kwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua, huku akiwataka wanaofanya hivyo kama wapo kuacha vitendo hivyo mara moja

Naye diwani wa kata ya Tandala Mh Egnatio Mtawa ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete akishukuru kwa hotuba ya mgeni rasmi amesisitiza maagizo hayo wahusika wayafanyie kazi ili kuepusha madahara yatakayoweza kujitokeza endapo maagizo hayo yatapuuzwa

Awali katika maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine wanafunzi wa shule ya sekondari Lupalilo wamepatiwa elimu ya Virusi vya Ukimwi na UKIMWI kazi iliyofanywa na Mratibu wa Ukimwi sekta zote Wilaya ya Makete Bi Ester Lamosai ambapo pamoja na mambo mengine amemueleza mgeni rasmi jinsi ambavyo shule nyingi hazipo salama kwa sasa

Barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka Kisutu Yachimbika

$
0
0
Barabara ya mradi wa mabasi yaendayo haraka katika kituo cha Kisutu,kilichopo katika Makutano ya barabara ya Libya na Morogoro,Mtaa wa Mtendeni,Kata ya Kisutu,Manispaa ya Kinondoni,Dar Es Salaam,inaendelea kuchimbika kufuatia sababu mbalimbali ikiwemo kinachoonekana kama mamlaka husika kuzembea ama kutochukua hatua stahiki kunusuru hali ilivyo mahala pale.

Chanel Ten,imeshuhudia Madereva wa magari ya mwendo wa haraka wanaopita mahala hapo namna wanavyopita kwa taabu wakijitahidi kudhibiti mwendo mahala hapo,  huku wengine wakichepuka kidogo hivyo kusababisha kingo za barabara katika eneo hilo nazo kuendelea kuathirika.

Kituo hiki kimezungumza na baadhi ya madereva taksi wa kituo cha Kisutu,wanaoegesha pembeni mwa makutano ya barabara hiyo ya  Libya na Morogoro,wakiwemo waenda kwa miguu wanaotumia barabara hiyo kutoka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar Es Salaam,kuhusiana na kuchimbika kwa barabara katika eneo hilo.

Mwana Samatta Atajwa Tuzo ya Mchezaji Bora ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

$
0
0
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya GENK ya nchini Ubelgiji ametajwa miongoni mwa wachezaji 30 wanaowani Tuzo ya Mchezaji Bora ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Wachezaji wengine ni pamoja na Mkenya Victor Wanyama anayecheza ligi kuu ya Uingereza katika klabu ya Tottenham Hotspur, Denis Onyango kutoka Uganda anayekipiga katika klabu ya Mamelodi Sundowns.

Hapa chini ni orodha kamili.

1. Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)

2. El Arabi Hillel Soudani (Algeria & Dinamo Zagreb)

3. Islam Slimani (Algeria & Leicester City)

4. Samuel Eto’o (Cameroon & Antalyaspor)

5. Benjamin Mounkandjo (Cameroon & Lorient)

6. Serge Aurier (Cote d’Ivoire & PSG)

7. Eric Bailly (Cote d’Ivoire & Manchester City)

8. Yao Kouasi Gervais ‘Gervinho’ (Cote d’Ivoire & Hebei Fortune)

9. Mohamed Salah (Egypt & Roma)

10. Mohamed El Neny (Egypt & Arsenal)

11. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Dortmund)

12. Andre Ayew (Ghana & West Ham)

13. Victor Wanyama (Kenya & Tottenham)

14. William Jebor (Liberia & Wydad Athletic Club)

15. Mehdi Benatia (Morocco & Juventus)

16. Hakim Ziyech (Morocco & Ajax)

17. John Mikel Obi (Nigeria & Chelsea)

18. Kelechi Iheanacho (Nigeria & Manchester City)

19. Ahmed Musa (Nigeria & Leicester City)

20. Cedric Bakambu (DR Congo & Villareal)

21. Yannick Bolasie (DR Congo & Everton)

22. Sadio Mane (Senegal & Liverpool)

23. Kalidou Koulibaly (Senegal & Napoli)

24. Keegan Dolly (South Africa & Mamelodi Sundowns)

25. Itumeleng Khune (South Africa & Kaizer Chiefs)

26. Mbwana Samatta (Tanzania & Genk)

27. Aymen Abdennour Tunisia & Valencia)

28. Wahbi Khazri (Tunisia & Sunderland)

29. Dennis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)

30. Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns)

Atembea Siku 21 Kwenda Dodoma Kumfuata Waziri Mkuu ili ufikisha malalamiko yake ya Kuporwa Ardhi

$
0
0
Mkazi wa Kilindi, Tanga Angela Basso , aliyetembea kwa miguu kwa muda wa siku 21 pamoja na Watoto wake Janeth Peter (9) na Happy Peter (7) kuja Mkoani Dodoma kuonana na Waziri mkuu ili kupeleka malalamiko yake ya kudhulumiwa mashamba yake ya hekari 30 na kuchomewa nyumba .

MKAZI wa Kilindi mkoani Tanga, Angela Basso, akiwa na watoto wake wawili Happy(7) na Janeth Peter(9), amelazimika kutembea kwa mikuu kwa siku 21 hadi mkoani Dodoma kwa lengo la kumuona Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili amsaidie kurudishiwa hekari 30 za mashamba yake aliyozoporwa.

Basso alifika mjini Dodoma akiwa na watoto wake hao, ambapo alisema aliona ni vyema kwenda Dodoma kuonana na Waziri Mkuu kutokana na kuporwa mashamba na kuchomewa nyumba yake katika kijiji cha Kwendigole wilayani Kilindi na wanaume wawili ambao waliojitokeza kwa nyakati tofauti wakidai ni maeneo yao.

Alisema alipita hatua zote zinazotakiwa kuomba mashamba, ambapo awali alipatiwa hekari 10 na kijiji na akazifanyia shughuli za kilimo na kujenga nyumba yake ya kuishi, lakini baada ya kwenda kujifungua alikuta mazao yamefyekwa na yeye kutakiwa kuondoka kwenye eneo hilo.

Mwanamke huyo alisema baada ya kunyang’anywa alifikisha malalamiko yake kuanzia uongozi wa kijiji hadi wilayani na baadaye akapatiwa eneo jingine la hekari 20, lakini alijitokeza mtu mwingine na kudai eneo hilo ni mali ya kanisa, licha ya kumiliki kihalali eneo la Hembekali.

“Nilikwenda kushtaki kwa serikali ya kijiji, kata na baadaye kwenda kwa mkuu wa wilaya ambako iliamuliwa nirudishiwe mashamba yangu, lakini hawakufanya hivyo mwisho wa siku nikafukuzwa kabisa kuishi kwenye eneo hilo,” alisema Basso

Mwanamke huyo alisema baada ya kutimuliwa alianza kuishi maisha yake kituo cha mabasi Muheza na baadaye alifukuzwa kituoni hapo kwa madai watu hawaruhusu kulala ama kuishi hapo na ndipo akaamua kuanza safari ya Dodoma baada ya kusikia Waziri Mkuu amehamia Dodoma.

Akisimulia machungu ya safari yake, Basso alisema akiwa njiani walikuwa wakila mahindi ya kukaanga na maji ya kunywa na kulala porini muda mwingine giza linapowakuta katikati ya pori.“Naomba kusaidiwa jamani nimeanza kufuatilia tangu mwaka 2012 lakini bila mafanikio jambo ambalo limechangia familia yake kusambaratika kutokana na kukosa pa kuishi huku watoto wangu hawa wakikosa elimu kwa kutangatanga,”alisema Mwanamke huyo

Basso aliomba Serikali itende haki ili yeye aweze kupata haki yake ya kurejeshewa mashamba yake na kurudi katika eneo hilo ili watoto wake wawili wapate nafasi ya kusoma. Mwanamke huyo alisema kwa sasa amekuwa kama mkimbizi kutokana na kukosa hana mahali pa kuishi huku mumewe naye akiikimbia familia yake baada ya kuporwa ardhi hiyo ambayo ilikuwa kama kitega uchumi chao.

Simba Yaipa Kichapo Kagera Suger 2 - 0 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar leo

$
0
0
Simba imezidi kujichimbia kileleni baada ya kuichapa Kagera Sugar kwa mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba iemfikisha pointi 23 kileleni baada ya ushindi huo wa mabao yake yaliyofungwa na Muzamiru Yasini na Shiza Kichuya.

MECHI NYINGINE LEO:
JKT Ruvu 1-1 Mwadui
Stand United 1-1 African Lyon

Baraka Da Prince Atokwa Povu na Kumtukana Msami Baada ya Kudai Anamtamani Najma

$
0
0
Baada ya baraka da prince kutupitia picha mpenzi wake kwenye instagram msanii mwenzake Msami alicomment kwa kumtania lakini baraka alipandwa na harisa na kumtukana mwenzake

Abdu Kiba Aeleza ni Kwanini Ali Kiba Hafanyi Nae Kolabo

$
0
0
Abdu Kiba ameelezea kuwa Ali Kiba hafanyi nae kolabo kwa kuwa Ali Kiba yupo bize na wasanii wengine
Pia amesema hana mpango wa kwenda wasafi ila anaweza kufanya nao kolabo
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images