Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Orodha ya Marais 10 Kutoka Nchi za Afrika Wanaoongoza Kwa Kuwa na Kiwango Kikubwa cha Elimu

$
0
0
Orodha ya Marais 10 kutoka nchi za Afrika wanaoongoza kwa kuwa na kiwango kikubwa cha elimu.

10) Ellen Johnson Sirleaf (Liberia)

Elimu: Master of Public Administration (M.P.Adm.), Bachelor of Economics (BEc), Associate Degree in Accounting (A.A.)

Ellen Johnson Sirleaf ni Rais wa 24 wa Liberia ambaye bado yupo madarakani hadi sasa. Amesomea katika vyuo mbalimbali kikiwemo Chuo wa West Africa, Madison Business College. Alijiunga na Taasisi ya Uchumi Boulder, Colorado, mwaka 1970.


9) Faure Gnassingbe (Togo)

Elimu: Master of Business Administration (M.B.A), Bachelor of Business (B.B.A).

Faure Gnassingbe alipata elimu yake ya msingi na sekondari Lome, Shahada ya uchumi kutoka Paris nchini Ufaransa na MBA katika Chuo Kikuu cha George Washington nchini Marekani.



8) Robert Mugabe (Zimbabwe)

Elimu: Master of Laws (LL.M.), Master of Science (M.Sc), Bachelor of Laws (LL.B), Bachelor of Science (B.Sc), Bachelor of Education (B.Ed), Bachelor of Administration (B.A.A), Bachelor of Arts (B.A.)

Robert Mugabe amepata Shahada yake moja kutoka katika chuo cha Fort Hare nchini Zimbabwe. Shahada nyingine alizipata kwa kusoma chuo huria.


7) Ibrahim Boubacar Keïta (Mali)

Elimu: Master of Political Science (M.S.), Master’s degree in History (M.A.)

Ibrahim Boubacar Keita amekuwa Rais wa Mali kuanzia mwaka 2013. Amesoma vyuo mbalimbali Paris nchini Ufaransa, Bamako, Dakar nchini Senegal.



6) Dr. Ameenah Gurib (Mauritius)

Elimu: PhD in Organic Chemistry, Bachelor of Science in Chemistry (B.Sc.)

Dr. Ameenah Gurib-Fakim ni Rais wa Mauritius, amepata Shahada yake ya kwanza ya Chemistry kutoka Chuo Kikuu cha Surrey mwaka 1983 na Shahada ya Uzamivu (PhD) kutoka katika Chuo Kikuu cha Exeter nchini Uingereza.



5) Dr. Mulatu Teshome (Ethiopia)

Elimu: Ph.D. in International Law, Bachelor’s Degree in Philosophy (B.Phil.)

Dr. Malatu Teshome amekuwa Rais wa Ethiopia tangu mwaka 2007. Elimu yake ameipata kutoka nchini China.


4) Alassane Ouattara (Côte d’Ivoire)

Elimu: Ph.D. in Economics, Master of Economics (M.Econ.), Bachelor of Science (B.S.),



3) Dr. Peter Mutharika (Malawi)

Elimu: Doctor of Juridical Science (J.S.D.), Master of Laws (LL.M), Bachelor of Laws (LL.B.),


2) King Mohammed VI (Morocco)

Elimu: Doctor of Law (J.D.),  Master of Advanced Studies (M.A.S.), Bachelor of Laws (LL.B.)



1) Dr. Thomas Boni Yayi (Benin)

Elimu: PhD in Economics and Political, Master of Economics (M.Econ.)

NORA: Niliingia Vitani na Johari, Kisa Mapenzi!

$
0
0
KUTOKA moyoni! Bila kumtaja mwanaume husika, mwigizaji wa kitambo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’amekiri kuwahi kuingia vitani na staa mwenzake, Blandina Chagula ‘Johari’ kisa kikiwa ni kugombeapenzi la mwanaume mmoja maarufu jijini Dar (jina ni siri yake).


Katika mahojiano maalum na gazeti hili, Nora alifunguka kuwa hali hiyo ilitokana na maisha ya usichana yaliyochangiwa na umaarufu na umri.

“Huyo mwanaume alikuja kwa lengo la kunitaka lakini nikawa nahisi kama Johari na baadhi ya rafiki zake walitaka kuninyang’anya, nikaamua kumvaa Johari,” alisema Nora ambaye kwa muda mrefu alikuwa haivi na Johari.

Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Afya Afariki Dunia Kwa Ajali ya Gari leo

$
0
0
Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya Afya kwa Umma wa Wizara ya Afya, Maendekleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Hellen Semi amefariki dunia katika ajali ya barabarani iliyotokea leo Chalinze mkoani Pwani.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, msemaji wa Wizara ya Afya, Maendekleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Nsachris Mwamwaja amesema amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi ambapo maofisa hao walikuwa wakielekea Dodoma kuhudhuria mkutano wa Waganga wa Mikoa unaotarajiwa kuanza kesho.


Mbali na Mkurugenzi huyo aliyefariki, Dk Neema Rusibamayila ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya alijeruhiwa katika ajali hiyo.

Jackline Wolper Kuhusu Wanaosema Ana Mimba ya Miezi Mitatu…

$
0
0
Ni October 16 2016 ambapo msanii kutoka kwenye tasnia ya Filamu Jackline Wolper  aliingia kwenye kikaango cha mashabiki wake baada ya kupost picha ikionesha ana ujauzito huku wengi wakiwa na maswali tofauti.


Sasa basi staa huyo aliamua kuyaandika haya kupitia ukurasa wake wa instagram na kusema
Hatimaye nikakavua kale kamkanda nakukatua kaa mkanda kametengeneza mimba yamiezi mitatu wakati ndo kwanza mwezi...Mkanda leo ndo mwisho wako tena nakuacha huku huku china ndege aupandi bhana’

Afande Aitolea Ufafanuzi Picha Aliyopiga na Makamu wa Rais Samia Baada ya Watu Kudhani Ameondoka ACT

$
0
0
Kitendo cha Afande Sele kupiga picha weekend hii akizungumza mbele ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan mkoani Morogoro, kiliibua tetesi katika mitandao ya kijamii zikidai huwenda mwanachama huyo wa ACT amekitosa chama hicho.
afande
Afande Sele akiwa mbele ya msafara wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan

Mwanahiphop huyo ambaye aligombea ubunge katika uchaguzi uliyopita kupitia ACT Wazalendo, wiki moja iliyopita alionyesha kutoridhishwa na mwenendo wa chama chake.

Jumamosi hii baada ya watu kuona picha hiyo na kudhani amekitosa chama cha ACT, aliandika

Aisee Watanzania sisi wengi wetu hata sijui nani katuloga kiasi cha kufunga kabisa uwezo wetu wa kufikiri nakushindwa kutofautisha hata vitu vidogo na vya kawaida sana vinavyotokea ktk maisha yetu ya kila siku…hebu tazama hiyo picha utaona mimi nipo na makamu wa rais,mkuu wa mkoa wetu na viongozi wengine wa serekali,hiyo inamaanisha kwamba hapo niliitikia wito wa serekali sio wito wa chama chochote cha siasa kitu ambacho hata viongozi au wabunge wa upinzani hufanya hivyo kwasababu serikali na viongozi wake ni mali yetu sote kama raia wa Tz sio mali ya chama fulani hata kama viongoz hao wametokana na chama hicho lkn wakishachaguliwa na wananchi wakapewa dhamana ya kuongoza tayari wanakua ni viongoz wa watu wote ktk taifa sio viongozi wa watu wa chama chao tu,sasa nashangaa pale mtu mmoja kwa sababu ya uvivu tu wakufikiri au labda kwa makusudi tu anaamua kuambukiza uvivu wake huo wa kufikiri na kutofautisha mambo kwa watu wengine…mimi nimeitikia wito wa serekali’mamlaka’ninayoamrishwa kuyatii hata ndani ya vitabu vitakatifu sio chama…lkn pia ktk hali ya kawaida tu ninani mwenye utimamu wa akili ktk taifa lolote awezae kukaidi wito wa makammu wa rais ambae ni sawa na rais wa taifa lake?lkn hata kama ingekua kweli mimi nimehama chama ingawa sifikirii kufanya hivyo bado yangebakia kuwa ni maamuzi yangu na yangepaswa kuheshimiwa…nyongeza ni kwamba hata yule mgombea urais wa marekani kupitia chama cha Republican mr donald trump siku za nyuma alikua ni mwanachama mtiifu wa chama cha mpinzani wake bibi clinton cha democratic na maisha yanaendelea..watz tujifunze maana ya maisha halisi tusijenge taifa la uzushi,fununu na kupakaziana…muwe na j’pili kareem akina ndugu nyote!

Nitajuaje ama Mke au Mume Wangu Anatoka Nje ya Ndoa? Mambo Gani Yanaweza Yakaonyesha?

$
0
0
Dalili za Mke anayetoka nje ya ndoa:

1) Anatembea na vidonge vya majira kwenye mkoba wake, wakati mume amefanyiwa Vasectomy (Kufunga kizazi kwa mwanaume)
2) Anakuwa na namba ya siri ya simu ambayo mume haijui
3) Anatumia muda mwingi anapokwenda sokoni au kufanya manunuzi ya wiki
4) Anajinunulia nguo za gharama zikiwemo nguo za ndani bila kumshirikisha mume
5) Anakuwa akitegemea zaidi ushauri kutoka nje kwa watu wengine zaidi ya mumewe
6) Anaacha kuvaa pete ya ndoa bila sababu
7) Anapopigiwa simu akiwa karibu na mumewe anaizima au kwenda kupokelea nje
8) Anakuwa hajali tena mambo ya familia na hujiamulia mambo yake mwenyewe
9) Ni rahisi sana kusema ‘nipe talaka yangu’ inapotokea kutofautiana hata kwa jambo dogo.
10) Dharau na kejeli kwa mume hujionyesha waziwazi

Dalili za mume anayetoka nje ya ndoa:

1) Unakuta Condom kwenye mkoba wake au kwenye gari lake wakati umefunga kizazi au unatumia vidonge vya majira.
2) Anapunguza au anaacha kabisa kuwa outing na familia yake
3) Unakuta lipstick kwenye kiti cha gari lake ambayo huifahamu
4) Ghafla anataka mjaribu aina mpya ya kufanya mapenzi
5) Anafanya kazi masaa mengi ya ziada lakini malipo hayaonekani kwenye salary slip
6) Hali au anakula kidogo sana nyumbani kwa kuwa ameshakula kwa nyumba ndogo
7) Nguo zake zinanukia manukato (Perfume)ambayo hata huyafahamu
8) Unakuta alama ya lipstick kwenye shati lake
9) Anakuwa na namba ya siri ya simu na wakati mwingine zaidi ya tatu ambazo mke hazijui
10) Anapopigiwa simu akiwa karibu na mkewe anaizima au kwenda kupokelea nje

Mtatiro amwambia Gavana Benki Kuu Tanzania "Mungu anakuona"

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ameandika haya kupitia ukurasa wake wa facebook

Gavana Benno Ndulu, Mungu anakuona! Ukweli utakuweka huru, hali ya uchumi wa nchi yetu ni mbaya mno. Unapaswa kuwaeleza Watanzania ukweli huo na kushauri njia za kufuata na hatua ambazo serikali inapaswa kufanya. Kuendelea kusisitiza kuwa Uchumi wa nchi unaimarika wakati mambo kibao sana yamesimama serikalini kwa visingizio lukuki ni kujidanganya wewe mwenyewe. Ukweli na Uwazi ni moja ya siri muhimu za Uongozi imara duniani. Niwakumbushe watanzania ule msemo wa Kiganda "...President Museveni has more than 30 Economic advisers, when they convene to advise him it is him (Museveni) who advises the advisers". (Rais Museveni anao washauri wa Uchumi zaidi ya 30, na wanapokaa kumshauri ni yeye "Museveni" ndiye anawashauri hao washauri".

JSM.

Video: Mrembo Atinga Global Afichua Siri Za ‘Scorpion’

$
0
0
Mrembo aitwaye Talta Msofe (21) akiwa katika pozi baada ya kutinga katika ofisi za Global Publishers kufichua siri za mtuhumiwa huyo, Salum Njwete ‘Scorpion’, mkazi wa Yombo Machimbo jijini Dar es Salaam.

Tazama hapa video Akifunguka

Mungai:Kikwete Alinitosa ili Kuwafurahisha Walimu..Magazeti ya Leo

$
0
0


Mungai:Kikwete Alinitosa ili Kuwafurahisha Walimu..Magazeti ya Leo

Beyonce Aongoza List ya Mastaa Anaolipwa Pesa Nyingi Kufanya Show

$
0
0
Mastaa wa muziki nchini Marekani kila siku wanazidi kutengeneza pesa kutokana na kazi zao ikiwemo mikataba ya showz mbalimbali wanazozifanya. Ili kuhakikisha haupitwi na chochote mtu wangu nakusogezea hii kuhusu kiasi cha pesa wanacholipwa mastaa wakubwa kama Drake, Rihanna, Beyonce, Nicki Minaj, Jay Z na wengine wengi ili kufanya show moja tu.



Inawezekana ulikuwa na maswali juu ya gharama wanazotoza mastaa hawa ili kufanya show moja tu, Mrembo Beyonce ametajwa kuongoza kwa kuhitaji pesa nyingi zaidi ili aweze kufanya show moja tu popote duniani.

Hii ni list ya wasanii na kiasi cha pesa wanazotoza kwa show moja

Beyonce – Dola milioni 2 na zaidi

Drake – Dola Laki 5 mpaka Milioni 1.

Rihanna – Dola Milioni 2 na zaidi.

Kanye West – Dola Laki 5 na zaidi.

Lil Wayne – Dola Laki 4.

A$AP Rocky – Dola laki 3.

Fetty Wap – Dola Laki 6

Martin Garrix – Dola Laki moja na nusu.

Kendrick Lamar -Dola Laki 5 mpaka Milioni 1.

Nicki Minaj – Dola Laki 5.

J. Cole – Dola Laki 2.

The Weeknd – Dola Laki saba na nusu mpaka Milioni 1.

Avicii – Dola Laki 5.

Jay Z – Dola Milioni 1 na zaidi.

Pharrell Williams -Dola Laki 5 mpaka Milioni1.

Walimu Waipa Serikali Siku 15 Ilipe Madeni Yao

$
0
0
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimetoa siku 15 kwa Serikali kumaliza madai yao ya muda mrefu vinginevyo watachukua maamuzi magumu.

Rais wa CWT, Gratian Mukoba amesema kuwa uvumilivu wao umeelekea kufikia ukingoni kwani wamekuwa wakikaa mezani na Serikali mara kwa mara na kupewa ahadi za kutatua matatizo yao lakini hadi sasa hazijatekelezwa.

Alisema kuwa Agosti  22 na 23 mwaka huu, Baraza la chama hicho cha walimu lilipitisha maazimio kupitia kikao chake, maazimio ambayo yalisainiwa pia na upande wa Serikali kwa ahadi kuwa wangeyafanyia kazi lakini imeendelea kuwa kimya.

“Siku chache baadae tuliambiwa tusubiri mchakato wa kuhakiki watumishi ukamilike. Lakini licha ya mchakato huo kukamilika Serikali imeendelea kukaa Kimya,” Mukoba anakaririwa na Tanzania Daima.

Aliyataja madai hayo kuwa ni pamoja na posho ya madaraka kwa wakuu wa shule, muundo wa madaraka, walimu kutopandishwa madaraja na kulipa madeni ya walimu.

“Ninachoweza kukwambia ni kwamba mwishoni mwa Oktoba ambao umebakiza siku 15 tutachukua uamuzi mzito ambao haujawahi kutokea na hatutaki lawakama kutoka sehemu yoyote ile,” alisema Mukoba.

Rais huyo wa CWT alidai kuwa ingawa Serikali imepiga hatua katika sera ya elimu bure na madawati, lakini mazingira ya walimu na ufundishaji yameendelea kuwa magumu hivyo ni vigumu kupandisha ubora wa elimu.

Nyumba Aliyosema Barakah The Prince Anajenga ni ya Mama yake Naj, Kwa Mujibu wa Msanii Aliyeoa Kwa Akina Naj

$
0
0
Kwa wengi haikuwa rahisi kuamini maneno ya Barakah The Prince kuwa anamalizia kujenga mjengo wake aliouonesha kwenye Instagram.

Ni kwa sababu ujenzi si suala la lelemama na linaloweza kutokea kwa usiku mmoja. Pia wengi walitia shaka uwezo wa msanii huyo katika kipindi hiki kuweza kujenga nyumba kama hiyo. Na sasa huenda mashaka hayo yakawa yamepata uthibitisho wa uhakika.


Alawi Junior (katikati) akiwa na shemeji yake, Naj (kushoto) mwenye uhusiano na Barakah

Ni kutoka kwa Alawi Junior – msanii wa Bongo Flava aliyemuoa na kuzaa na dada yake Naj, Lady Naa. Alawi amepost Instagram video ya nyumba ambayo Barakah alidai ni ya kwake na kuandika: Done🏠👍Hongera sana Mama mkwe #zaharaDattan nyumba yako kali sana.”


Cha kufurahisha ni kuwa Barakah na mpenzi wake Naj Dattan walihojiwa na EATV na wote kuthibitisha kuwa ni nyumba ya Barakah!

“Namshukuru sana mke wangu Naj kwa sababu ana mchango mkubwa sana hadi hapa nilipofika pia kwa sasa siwezi kutaja fedha ambayo nimeitumia hapa kwa sababu ni hela nyingi sana hadi sasa na kama unavyoona nyumba bado haijaisha kwa hiyo nikimaliza kila kitu nitasema ni shilingi ngapi nimetumia,” Barakah The Prince alikiambia kipindi cha E-Newz cha EATV.

Swali ni kama maneno ya Alawi ni ya kweli, kwanini Barakah anadanganya?

Bongo5

Mwimbaji Koffi Olomide Achukua Dakika Moja Kuwaomba Msamaha Wakenya Kwa Kumpiga Mwanamke

$
0
0
Mwanamuziki wa Congo Koffi Olomide ambaye mwezi July aliwasili  Nairobi Kenya  akiwa na wanamuziki wake pamoja na dancers wake kwa ajili ya show na baadae kuripotiwa kukamatwa kwa tuhuma za kumshambulia dancer wake wa kike ni baada ya kusambaa kwa video iliyomuonyesha akifanya kitendo hicho.

Koffi Olomide aliachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha siku mbili kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali,  na hiyo ilielezwa kuwa kuachiwa kwa koffi Olomide kulikuja baada ya Mahakama ya Kinshasa kusema kuwa hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya JKIA.

Baada ya kupita miezi kadhaa tangu kutokea kwa tukio hilo na Koffi Olomide kutowahi kujitokeza hadharani kulizungumzia, amejitokeza kupitia kipindi cha Television cha Churchill Show amewaomba msamaha wakenya na mashabiki wake kwa ujumla na kusema …….

’Kupitia Churchill show, nataka kusema na nyinyi na kutuma ujumbe wa upendo, heshima na urafiki, mimi nasikitika kwa kile kilichotokea na maombi yangu nisamehewe kwa kile kilichotokea, mimi ni mwanadamu tu licha kwa kuwa ni maarufu’:- Koffi Olomide

Stan Bakora Ajibu Mapigo Kwa Barakah The Prince

$
0
0
Mchekeshaji maarufu Stan Bakora amefunguka juu ya povu lililomtoka Barakah The Prince siku kadhaa baada ya kuachia parody ya wimbo ‘Nisamehe’.

Kupitia kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Stan amesema kuwa kama asingefanya vile video ingekuwa ya kawaida tu na isingeleta maana.

Barakah ameshindwa kuelewa. Kama nisingefanya vile ile video isingeleta maana, lazima uonyeshe uhalisia. Kwani Baraka si mweusi kweli?,” amesema Stan. Stan aliendelea kwa kumtania Barakah kwa kumwambia kuwa hapa mjini [Dar es Salaam] ndio kwanza ana Christmas mbili.

Awali baada ya Stan kuachia parody hiyo, Barakah aliandika kwenye Instagram: Matani ni mazuri ila yakizidi yanaweza kuleta matatizo… heshima ichukue nafasi yake tafadhali mzee utani huu sijaupenda iwe mwanzo na mwisho tafadhali.”

Wakuu wa Wilya 'Washindana' Kuwaweka Ndani Wanasiasa

$
0
0
Wakuu wa wilaya mbalimbali nchini wameanza kuwasweka mahabusu baadhi ya watendaji na wanasiana ambao wanakwenda kinyume na maagizo yao ili kurejesha uwajibikaji katika maeneo yao.

Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997, kifungu cha 15 (1) inawapa mamlaka wakuu wa mikoa na wilaya kutoa amri ya mtu kukamatwa na kuwekwa ndani kwa saa 48 pale anapobaini kwamba mhusika ametenda kosa fulani.

Wakuu wa wilaya sasa wanatumia mamlaka hayo pale watendaji wao wanaposhindwa kutimiza maagizo yao. Suala la watendaji kuwekwa ndani limeshuhudiwa katika wilaya za Sengerema, Arumeru, Rorya na Newala.

Oktoba 13 mwaka huu, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole alimsweka ndani kwa saa 12 kaimu mkurugenzi wa wilaya hiyo, Oscar Kapinga na kaimu mhasibu wa halmashauri hiyo, Paul Sweya kwa kushindwa kutekeleza agizo la mkuu huyo la kutafuta fedha kwa ajili ya kuwalipa wanaofanya usafi katika mji wa Sengerema.

Inaelezwa kuwa watu hao wanaofanya usafi hawajalipwa fedha zao kwa zaidi ya miezi sita, jambo lililomsukuma Kipole kuagiza walipwe.

Tukio jingine ni lile la Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti kuwaweka ndani madiwani wanne wa Chadema kwa madai kwamba wamekuwa wakimkwamisha kutekeleza kazi zake.

Miongoni mwa waliowekwa ndani ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Noah Lembrise ambaye alilala katika Kituo cha Polisi cha Usa River. Wengine ni Happy Gadiel, Nuru Ndosi na Winfrida Lukumay.

“Hawa (madiwani) wamekuwa wakivuruga ziara zangu kwa kupita kwa wananchi na kupotosha dhima ya Serikali kuhusu maendeleo.”

Huko Newala, Mkuu wa Wilaya, Aziza Mangosongo alimlaza katika Polisi kaimu meneja wa Mamlaka ya Maji Mradi wa Makondeko, Athumani Semkondo na fundi Mohamed Salum kwa saa 48 kwa kuvikosesha maji vijiji 14 vyenye wakazi 60,000.

Mangosongo alisema kulifanyika hujuma ya kuziba bomba ili maji yasipatikane katika vijiji hivyo lakini kaimu mkurugenzi huyo alishindwa kufuatilia taarifa aliyopewa kwamba vijiji hivyo havipati maji ili achukue hatua.

“Kama mkurugenzi alikuwa na taarifa na hakuchukua hatua, kuna nini kimejificha hapo? Lazima nitahisi kuna jambo ndiyo maana nikaamua akalale rumande kwa saa 48 kwa sababu nina mamlaka kisheria. Akae humo ndani kwanza ajitafakari,” alisema Mangosongo.

Hali kama hiyo ilitokea pia katika Wilaya ya Rorya baada ya mkuu wa wilaya hiyo, Simon Chacha kuwaweka ndani watu 10 akiwamo Diwani wa Kigunga (Chadema), Vitalis Joseph baada ya kutokea mgogoro kati ya vijiji viwili na kusababisha mazao kufyekwa.

Diwani huyo alifika eneo la tukio na kukuta mazao yamefyekwa, hata hivyo, Chacha aliagiza akamatwe na kuwekwa ndani pamoja na watu wengine kwa kuhusishwa na uharibifu huo.

“Tumewachukua baadhi ya watu ili kuisaidia Serikali kupata uhalisia wa tukio hili, na ninawaambia wananchi wa Rorya kuwa Serikali hii ya awamu ya tano haitaki mzaha na yeyote anayejitokeza kufanya vitendo viovu tutamshughulikia,” alisema Chacha.

 Maoni ya wadau

Wadau mbalimbali wamepinga hatua ya wakuu wa wilaya kuwaweka ndani watendaji wa halmashauri wakisema wanafanya hivyo kwa lengo la kuwakomoa.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Gaudence Mpangala amesema amri hizo zimekuwa zikitolewa katika maeneo ambayo upinzani unaongoza, jambo analolitafsiri kama ni kuwakomoa wapinzani.

Alisema sheria hiyo inatumika kukandamiza demokrasia kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake. Alisema wakuu wa wilaya wanatakiwa kutumia sheria inayowapa mamlaka hayo kwa wahalifu wa makosa ya jinai na wahujumu uchumi.

“Madiwani na wakurugenzi ni watendaji tu, kuwaweka ndani kwa kushindwa kutekeleza maagizo ya mkuu wa wilaya ni kuwaonea. Sheria hiyo ya saa 48 itumike kwa wahalifu na wanaohujumu uchumi,” alisema.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alisema sheria inayotumika bado ina sura ya kikoloni kwa sababu haiendani na taratibu za menejimenti ya watumishi.

Alisema kumweka mtumishi ndani siyo njia nzuri ya kumwajibisha kwa sababu uongozi wa sasa unafuata mfumo wa kufanya kazi kwa pamoja.

“Unapomweka mtu ndani tayari umemhukumu na mara nyingi amri hiyo inatolewa na wakuu wa wilaya ili kuonyesha kwamba wana uwezo wa kufanya jambo,” alisema.

Katibu Mkuu wa CCK, Renatus Muabhi alisema wakuu hao wanataka kujijengea sifa kwa Rais wakidhani kwamba kuwaweka watu ndani ndiyo uwajibikaji.



Ruby Ampoza Vanessa Mdee Kwa Maneno Haya Baada ya Kukosa Tuzo

$
0
0
Ruby amemwandikia ujumbe wa kumsifia na kumtia moyo Vanessa Mdee baada ya kukosa tuzo ya Afrimma 2016 zilizofanyika wikiendi hii huko Dallas, Marekani.

Muimbaji huyo mwenye sauti ya dhahabu kupitia mtandao wake wa Instagram ameandika:

Tuzo aliyokupa Mungu love inatosha don’t worry about what happened yesterday ur still the best vee let them take that award this year but doesn’t mean that ur not the best 😫😫minnachojua tuzo yetu Tanzania tuendelee tu kufanya kazi kwaajili ya nchi yetu thats enough I know they know thats ur the one from TANZANIA....all in all love you @vanessamdee

Hata hivyo Vanessa hajaonesha donge lolote kwa msanii wa Kenya, Akothee aliyeshinda tuzo hiyo baada ya kupost picha yake na kumpongeza. Pia Jumapili hii alimpeleka lunch. Akothee alipost video akiwa na Vanessa na kuandika: Goofing around @vanessamdee yooo that lunch was hilarious thanks mamaaa 💪❤😍 but what lipstick has put together let not hand wipe.”

Pia alirepost picha aliyoweka Vanessa na kuandika: Kazi iendelee
Thanks mummy spending time with you at lunch was a great time spent.”

Diamond Platnumz, Harmonize na DJ D-Ommy ndio washiriki kutoka Tanzania waliofanikiwa kushinda tuzo hizo huku Linah, Alikiba, Yamoto Band na Mose Iyobo wakiwa ni washiriki wengine kutoka Tanzania waliokuwa wametajwa kwenye tuzo hizo.

Nataka Kuwa Mcha Mungu, Maisha ya Kuendekeza Dunia Nimeyachoka – Shamsa Ford

$
0
0
Malkia wa filamu na mama wa mtoto mmoja, Shamsa Ford amefunguka kwa kusema kuwa kwa sasa anataka kujikita zaidi kwenye ibada ya kufanya mambo ambayo yanampendeza mwenyezi Mungu.
Shamsa akizungumza baada ya kufunga ndoa

Mwigizaji huyo ametangaza uwamuzi huyo ikiwa ni miezi michache toka afunge ndoa na mfanyabishara wa maduka ya nguo, Chidi Mapenzi.

Maisha ya kuendekeza dunia nimeyachoka. Natamani ifike siku kwa kudra za Mwenyezi Mungu nibadilike. Natamani niwe mmoja ya wale watakaopata nafasi ya kwenda peponi pamoja na familia yangu . natamani nifanye IBADA kama ulivyoamua Mwenyezi Mungu. NATAMANI matendo yangu yawe ya kukufurahisha wewe Mwenyezi Mungu ili umauti utaponikuta niwe msafi..G9T MY PEOPLE. ..INSHAAALLAH MWENYEZI MUNGU ATUPE MWISHO MWEMA. .
Mashabiki wake katika mitandao ya kijamii wameonyesha kupendezwa na uwamuzi huo huku wachache wakimuuliza maswali kama ataendelea kufanya tena filamu.

Stori Mpya Kuhusu Sababu ya Scorpion Kumtoboa Mtu Macho

$
0
0
Makala hii imeanza kuzunguka katika mitandao mbalimbali ya kijamii leo asubuhi ikielezwa kutoka kwa mkazi wa Buguruni anayesema anakifahamu vyema kisa cha Scorpion kumtoaboa macho mkazi wa Dar es Salaam aliyefahamika kwa jina la Said Ally.

Katika habari zilizotolewa na mhanga, alisema kuwa alikuwa akitokea kazini kuelekea nyumbani na alipokuwa akinunua mahitaji yake ya nyumbani eneo la Buguruni, ndipo alivamiwa na mtu huyu anayefahamika kama Scorpion na kumfanyia ukatili huo.

Hii hapa chini ndiyo stori mpya inayoeleza kwa upande mwingine sababu za tukio hilo.

Inaelekea wanaume wa mkoani hawamjui scorpion. Halafu sisi watu wa Buguruni tunamjua huyo Saidi na shughuli zake, na pia tunajua shighuli za Scorpion ndio maana watu hata hawakuhangaika nao.

Watu waliwaacha wamalize mambo yao.

Tunaangalia tu watu wanavyo shadadia mambo wasiyoyajua kwa undani wakipiga kelele dunia nzima ikiwa ni pamoja na mkuu wa kaya ya Jiji.

Scorpion ni mtu aliyeamua kujichukulia sheria mkononi kwa kuwa uwezo huo anao.
Kwa maana ya uwezo wa kupambana na mtu yoyote ambae ni mtukutu. Anapiga kareti kama za kwenye kideo na physic yake sio ya wanaume hata 2 wa kawaida. He is a man na nyongeza.

Kwa kifupi ni kwamba Buguruni kuna watu watanashati na wanashughuli zao za maana lakini wanamiliki mitandao ya vibaka ambao hupora na kuwaletea mizigo wanayopora.

Na hiyo ndio wanapopatia hela zao nyingi.

Hujawahi kujiuliza Tv, radio, vipochi, simu na vitu vingine kama hivyo vikiibiwa huwa vinaenda wapi?

Wale waibaji huenda na kumkabidhi mtu halafu wanapewa hela flani ndogo(ya kula).
Yeye huvitakatisha vile vitu kwa kuviuza kupitia legitimate channels kwa yeye hubaki kuwa mtu legit.

Scorpion alikua ametangaza kiama kwa vibaka pale Buguruni. Na alikua anawashughulikia kweli. Hivyo he was posing a danger kwenye biashara za watu.
Wakati vibaka wakindelea kushughulikiwa na hali ikionekana imeanza kuwa swari, yani vibaki waliosalia wanahamia kambi nyingine kama vingunguti, gomz etc.
Ndugu wa kike wa mpiga kareti (rafiki wa scorpion) akaporwa pochi iliyokua na simu maeneo ya Buguruni sheli.

Scorpion akaamua kumsaka muhusika na hakufanikiwa kumtambua. Akaamua kutuma ujumbe kwa mkuu wao ambae ndie mhanga wa macho, kuwa anataka arejeshewe mali iliyoporwa.

Kama kawaida ya wapanga misheni mkuu akapiga kimya.

So Scorpion akaamua kudeal nae, the boss himself ndio akamfuata alipomkuta and the rest of the story baada ya kumfuata face to face mtakua mmeipata kwenye media.

Sasa nyie mpeni mamilioni na assets bosi wa wahalifu kisa mnamhurumia wakati hamumjui.

Ndio maana watu hawakutaka kuingilia kesi wakati jamaa anasurubiwa. Sie wa buguruni tunaelewa.

Mtu hakurupuki tu kumtoboa toboa mtu asiyemjua.

PICHA: Wasichana 21 Waliokuwa Wametekwa na Boko Haram Walivyokutana na Familia zao

$
0
0
Aprili 2014 zaidi ya wasichana 270 walitekwa wakiwa shuleni katika mji wa Chibok na wapiganaji wa Boko Haram, mpaka leo ikiwa ni baada ya zaidi ya miaka miwili tangu kutekwa kwa wasichana hao, Alhamisi ya October 13, 2016  ziliripotiwa taarifa za kuachiwa kwa baadhi ya wasichana hao na kurejeshwa baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa serikali ya Nigeria na viongozi wa Boko Haram.

Leo October 17 2016 Wasichana 21 wa Chibok hatimaye wamekutana na familia zao

VIDEO: ‘Alitajwa Mke wa Marehemu Mmoja Mimi Nafahamu Wako Wanne au Watano’-Magufuli

$
0
0
Leo October 17 2016 Rais John Magufuli ameongoza wananchi wa jiji la Dar es salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa meya wa jiji hilo Dk. Didas Masaburi aliyefariki October 12 2016.

Baada ya msomaji wa wasifu wa Dk. Masaburi kutaja kuwa  marehemu ameacha mke mmoja, Rais Magufuli alipata nafasi ya kuzungumza na kusema anafahamu Dk. Masaburi alikuwa na wake wanne au watano na hata watoto anafahamu kuwa anao zaidi ya 20, aidha Rais Magufuli amewaomba watoto wa marehemu kushikamana na kuwa wamoja, unaweza kuangalia video hii hapa chini....
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images