Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Jambazi Awajeruhi Kwa Bomu Askari na Raia Wanne Kigoma

$
0
0
Polisi na raia wanne wamejeruhiwa kwa bomu la kutupwa kwa mkono walipokuwa wakimkamata mtuhumiwa wa ujambazi kwenye Kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 14.

Alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Yahya Kamuhanda (49) mkazi wa kijiji hicho. Mtui aliwataja majeruhi hao kuwa ni askari polisi F.3187 Koplo Isaya na raia Saidi Mohamed, Seleman Kashali, Joseph Daudi na Hassan Nasibu, wote wakazi wa Kijiji cha Uvinza.

Alisema askari walipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba Kamuhanda anajiandaa kufanya uhalifu hivyo waliweka mtego eneo la Uvinza Madukani alikokwenda kununua mahitaji.

Alidai kuwa alipotambua anafuatiliwa alitupa bomu ndipo polisi walimpiga risasi mguuni na wananchi walimvamia na kumshambulia kabla ya askari kutumia nguvu kumwokoa asiuawe kwa kipigo.

Mtui alisema mtuhumiwa alipohojiwa alisema alificha bunduki kijijini kwao Lukole wilayani Ngara mkoani Kagera, ambako askari walikamata SMG yenye namba 78GA5062 ikiwa imefukiwa ardhini.

 Pia, walikamata magazini saba, moja ilikuwa na risasi 40, nne (risasi 30 kila moja) na mbili (risasi 20 kila moja) na risasi 75 zilikuwa kwenye mfuko wa sandarusi. Pingu moja na funguo zake, maski tisa na laini 20 za mtandao wa Halotel ambazo hazijasajiliwa.

Mtui alisema mtuhumiwa huyo alifariki dunia juzi akipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma (Maweni). Alisema majeruhi wote watano walipata matibabu hospitalini hapo na waliruhusiwa kurudi nyumbani.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Afikishwa Mahakamani Kwa Kosa La Kumtishia Bastola Askari wa Usalama Barabarani (Trafiki)

$
0
0
Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro baada ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, Emmanuel Mkumbo kufikishwa ili apandishwe kizimbani kujibu mashtaka sita, likiwamo la kutishia kuua.

Tukio zima la kumpeleka mahakamani, kumpandisha kizimbani na kumsomea mashtaka kwa muda wa dakika 30 hivi lilitawaliwa na vituko. Kwanza, ni jaribio la kuwaficha wanahabari.

Kabla ya kufikishwa mahakamani, Polisi mkoani Morogoro iliwaarifu wanahabari kuwa ingetoa taarifa kuhusu mkurugenzi huyo lakini saa 4:30 asubuhi wakati Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Ulrich Matei akijiandaa kuzungumza nao, alipigiwa simu akatoka nje ya ukumbi na aliporejea alisema hawezi kutoa taarifa tena na akaondoka.

Waandishi walipofika mahakamani saa 5:00 asubuhi walikuta Kamanda Matei akishuka kwenye gari na alipanda tena akasogea kando kuzungumza na baadhi ya askari wake.

Pili, baada ya hakimu kumaliza kusikiliza kesi hiyo, Mkumbo hakurudishwa mahabusu mahakamani hapo kama ilivyo ada ili kusubiri utaratibu mwingine badala yake mshtakiwa huyo alihamishiwa chumba cha hakimu ambacho hakikuwa na kesi inayoendelea.

Humo ndugu zake walimpelekea koti kubwa jeusi na kofia aina ya pama, hivyo alitoka akiwa tofauti na alivyoingia akiwa na fulana yenye rangi nyeupe, bluu na nyeusi. Baada ya kuvaa alitoka akiwa amezingirwa na polisi, huku ndugu wakiwazuia wanahabari kumpiga picha.

Mashtaka dhidi yake
Mkumbo ambaye ni mkazi wa Tegeta jijini Dar es Salaam alipandishwa kizimbani kujibu mashtaka sita, la kwanza likiwa la kutishia kuua kwa bastola na la pili ni la usalama barabarani lenye makosa matano.

Alisomewa mashtaka hayo na mawakili wa Serikali Sunday Hyera na Edgar Bantulaki. Katika shtaka la kwanza, mbele ya hakimu Agripina Kimaze anadaiwa Oktoba 15, saa 10:30 jioni alitenda kosa la kutishia kuua eneo la Mkambarani, Manispaa ya Morogoro.

Anadaiwa katika shtaka hilo la jinai namba 226 la mwaka 2016, alitishia kumuua kwa bastola askari namba 5057, Koplo Tuti Ndaga wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, kinyume na kifungu namba 89 (1),(2),(a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu namba 16.

Katika shtaka la pili la ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani lenye makosa matano, ilidaiwa kuwa; kwanza, siku na muda huo eneo la Mbuyuni Mkambalani, mshtakiwa alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Prado lenye rangi ya kijivu bila kuwa na leseni.

Pili, ilidaiwa alikuwa akiendesha gari hilo ambalo halikuwa na bima; tatu, alikutwa akiendesha kwa mwendo kasi; na nne, alikataa kupeleka gari Kituo cha Polisi cha Kingoluwira kama alivyoamriwa na askari, WP namba 5392 Sajenti Anna.

Ilidaiwa katika shtaka la tano kwamba, wakati akiendesha alisimamisha gari katikati ya barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam kwa uzembe, bila uangalifu wala kuzingatia watumiaji wengine wa barabara. Mkurugenzi huyo alikana mashtaka yote yanayomkabili.

Hakimu Kimaze alitoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kwamba awe na mdhamini mmoja kwa kila shtaka, yaani shtaka la jinai na la usalama barabarani lenye makosa matano, wote wawe wakazi wa Morogoro na mmoja akitakiwa kuweka dhamana ya Sh500,000 kwa kosa la kwanza na Sh1 milioni kwa kosa la pili.

Mshtakiwa alikidhi masharti ya dhamana na kuachiwa huru, huku gari likiendelea kushikiliwa kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Morogoro.

Hakimu Kimaze aliahirisha shauri hilo hadi Oktoba 31, usikilizwaji wa awali utakapoanza baada ya upande wa mashtaka kudai upelelezi umekamilika.

Watu 13 Kizimbani Kwa Mauaji ya Watafiti Dodoma

$
0
0
Wanawake wanne na wanaume tisa wamefikishwa mahakamani mjini Dodoma na kusomewa mashtaka ya mauaji ya watafiti wa Chuo cha Utafiti wa Udongo na Maendeleo ya Ardhi kilichopo Selian mkoani Arusha.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Joseph Fovo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu.

Wanadaiwa kuwaua Nicas Mag- azine, Theresia Nguma na Faraji Mafuru, Oktoba Mosi kwenye Kijiji cha Iringa Mvumi wilayani Chamwino.

Wakili wa Serikali, Beatrice Nsana aliwasomea mashtaka hayo jana akidai walitenda kosa hilo la jinai kinyume na kifungu cha 196 na 197 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu na marekebisho yake ya mwaka 2002.

Washtakiwa hao ni Cecilia Mwalu, Dorca Mbehu, Edna Nuno, Grace Masaulwa, Juma Madeha, Albert Chimanga, Sosteness Mseche, Julius Chimanga, David Chimanga, Lazaro Kwanga, Yoramu Samamba, Edward Lungwa na Simon Samamba, wote wakazi wa Kijiji cha Iringa Mvumi.

Kesi hiyo namba 36/2016 iliahirishwa hadi Oktoba 31. Nsana alidai upelelezi haujakamilika.

Serikali imeyasainisha mikataba ya kujiendesha kwa faida Mashirika 12 ya Umma.......Yatakayojiendesha kihasara kuchukuliwa hatua.

$
0
0
Taasisi na Mashirika ya Umma nchini yametakiwa kujiendesha kwa faida huku yakiwa na mtazamo wa kiushindani na makampuni yaliyo chini ya sekta binafsi na kwamba hakuna sababu yoyote kwa mashirika hayo kuendeshwa kwa hasara na kugeuka mzigo kwa serikal

Msajili wa Hazina nchini Bw. Lawrence Mafuru ametoa agizo hilo jana jijini Dar es Salaam wakati akisaini makubaliano ya kiutendaji na taasisi 12 za umma, mkataba unaohusisha malengo ya uendeshaji, namna ya kuhudumia wananchi sambamba na usimamizi bora wa rasilimali za umma zilizopo ndani ya mashirika hayo.

Zoezi hilo la linafanya idadi ya taasisi ambazo msajili wa hazina amesaini nazo makubaliano kufikia thelathini tangu aanze utaratibu huo unaoendana na falsafa ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji katika taasisi na mashirika ya umma.

Katika maelezo yake Bw. Mafuru amesema haikubaliki kuona makampuni na taasisi za umma zikiendelea kupata hasara kwa kutekeleza majukumu yale yale ambayo taasisi na makampuni binafsi yanapata ufanisi na faida pasipo visingizio vyovyote.

Mamilioni ya Simba na Yanga yashikiliwa Selcom

$
0
0
KAMPUNI ya Selcom Tanzania Limited inashikilia zaidi ya Sh. Milioni 130 za mapato ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Oktoba 1, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hiyo ni baada ya kuondolewa kwa makato mengine yote muhimu kwenye mapato ya jumla ya mchezo huo ulioingiza Sh. Milioni 320 Simba na Yanga zikitoa sare ya 1-1.

Habari za ndani ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE imezipata zinasema kwamba, fedha hizo zimezuiwa kwa maelekezo ya Serikali kufuatia uharibifu uliojitokeza katika mchezo huo wa Oktoba 1, mwaka huu mashabiki wa Simba wakivunja viti.


Tokeo la picha la SIMBA WAVUNJA VITI

Na taarifa zinasema kwamba Serikali imezuia fedha hizo hadi hapo uchunguzi utakapokamilika juu ya hasara iliyojitokeza, ambayo kimsingi Simba wamekubali kulipa.

Habari zinasema mchezo huo uliingiza Sh. Milioni 320 wakati uharibifu uliofanywa na Simba unakaribia kuwa wa Sh Milioni 400.

Makato ambayo yamekwishaondolewa kwenye mapato hayo ni pamoja na asilimia18 ya VAT, asilimia 15 ya gharama za Uwanja, asilima 9 ya Bodi ya Ligi, asilimia 5 ya TFF, asilimia 3 ya DRFA na asilimia 8 ya gharama za mchezo.
Wenyeji Yanga SC wanastahili kupewa asilimia 40 ya mapato hayo wakati asilimia 20 ni za waliokuwa wageni, Simba SC.

Tayari Simba SC wameandika barua TFF kuomba wapatiwe mgawo wao wa mchezo huo kwa kuwa wanahitaki fedha za kujiendesha kwa wakati huu na deni hilo watalipa taratibu.

Hatua hiyo inakuja kufuatia mashabiki wa Simba kufanya vurugu Uwanja wa Taifa Oktoba 1, baada ya Yanga kupata bao la kuongoza dakika ya 26 lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Bao hilo lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga. Na katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba SC, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele.

Kwa hali hiyo, mchezo ukasimama kwa takriban dakika tano baada ya mashabiki wa Simba kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na kutupa uwanjani. Polisi walitumia milipuko ya gesi za kutoa machozi kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea hadi Simba SC wakasawazisha dakika ya 87 kwa bao la Shizza Kichuya. Lakini tayari TFF imeipiga Simba SC faini ya Sh. Milioni 5 kwa kosa hilo.

DC Kinondoni 'Awatia Ndani' Watendaji Kwa Uzembe

$
0
0
Mkuu  Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amewaweka ndani kwa saa 24 mkandarasi wa wilaya ya Kinondoni Abdul Digaga na Maafisa watendaji wa 4 wa kata ya Mikocheni kwa kushindwa kutekeleza maagizo yake na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
wa

Mhe Hapi amesema, hatua ya kuwaweka ndani watendaji hao na mkandarasi itawakumbusha juu ya utekeleza wa miradi wanayotakiwa kusimamia na nini majukumu yao kwa wananchi kwa madai kuwa uzembe umekithiri.

“Ofisi inapesa kwa miaka miwili sasa ya kujenga Zahanati lakini wamekalia tu pesa hizo tangu 2014, pia miradi ya barabara na kushindwa kuweka polisi jamii ndani ya kata hiyo licha ya kupewa maagizo kwa miezi 3 sasa hii ni dharau kwangu na Rais aliye nituma” amesema
Aidha Hapi amewataka watendani wote wa kata na maafisa ugani waliopo katika wilaya hiyo kujiengua kwenye nyadhifa zao endapo wanaona hawawezi kuendana na kasi inayotakiwa na serikali ya awamu ya tano.

Lakini pia amemtaka mkuu wa kituo cha polisi wa manispaa ya kinondoni kuwakamata watendaji kata wote ambao hawajaunda vikundi shirikishi na kuwaweka ndani kwa muda wa masaa 24 ili waweze kujieleza.

Roma Asababisha Kushushwa Kwa Stamina Jukwaani Fiesta ...Stamina Afunguka Haya

$
0
0
September 18 ndio siku ambayo mvua ya burudani ya Fiesta 2016 ilikuwa inashuka katika uwanja wa Jamhuri Stadium mjini Morogoro.

Usiku huo jambo ambalo lilimake headlines kinomanoma ni kitendo cha wasanii wawili Roma Mkatoliki na Stamina kushushwa jukwaani baada ya msanii @Roma2030 kutumia lugha isiyo ya kimaadili katika show hiyo.

Roma alisikika katika interview kwenye U-herad ya September 10 lakini Stamina alikuwa hahitaji kuzungumzia kabisa suala hili kutokana na alivyo kasirishwa na kitendo hicho ukizingatia show ile ilikuwa ni yakwake na #Roma alimpa mashavu tu kama surprise.

Stamina kwa mara ya kwanza ameamua kuzungumzia kilichotokea usiku ule, ikiwa ni baada ya usiku wa jana kupiga bonge moja la show kwenye Fiesta pande za Mbeya akiwa na msanii Roma Mkatoliki.
.
“Always shows zangu za Morogoro huwa napenda kufanya vitu vya kitofauti, kama unakumbuka Fiesta ya mwaka juzi kwenye show yangu ya Moro nilimdondosha #FidQ kama surprise, na hicho ndicho nilitaka kukifanya mwaka huu kwasababu me na Roma kuna goma tumepiga nikaamua nimuweke kama surprise. Show tulipanga fresh lakini kama unavyoujua muziki wa Roma unavitu flani hivi ambavyo sio vizuri kimaadili kiasi kwamba vimewahi kumsababishia kufungiwa. Alichokosea Roma ni kutaja yale maneno pale uwanjani ukizingatia ni show ambayo ilikuwa inaruka LIVE, na kama inavyo julikana kwenye show ya LIVE huwezi kutukana, na hicho ndio kitu killichosababisha muziki kuzimwa.” Alisema Stamina

Z Anto Aeleza Kwanini Amekataa ofa ya Kujiunga na WCB ya Diamond

$
0
0
Msanii wa muziki ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo ‘Binti kiziwi’, Z Anto amefunguka na kusema kuwa mpaka sasa kuna label zaidi ya nne ambazo zinamuhitaji kufanya naye kazi lakini amekataa kufanya nao kazi.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo kimya, amesema alipata ofa ya kujiunga na WCB lakini alikataa kwa kuwa yeye mwenyewe anadai anatamani kufanya kazi nje ya WCB.

“Unajua mimi tatizo langu huwezi kufanya kazi kwa kubahatisha, mpaka saizi kuna ‘label’ nyingi zaidi ya tano zinanihitaji kufanya kazi, hivyo sipendi kukurupuka lazima nitulie nione nawezaje kujiunga na moja kati ya hizo. Maana nikibugi kuchagua ‘label’ ambayo inaweza kunisimamisha kufikia pale napotaka mimi nitakuwa nimejimaliza mwenyewe. Nilikuwa na maongezi na Babu Tale, nikapewa ofa kurekodi na kujinga WCB, lakini mimi natamani kufanya kazi nje ya Wasafi, nipo tayari kufanya kazi na Tip Top Connection” Z Anto alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV.

Akieleza sababu ya kukataa ofa ya kujiunga WCB, Z Anto alisema “Sisi ni washairi ujue na siku zote mafahari wawili hatuwezi kufanya kazi sehemu moja, nachoweza kuwaambia ni kwamba ukimya wangu una mambo mengi mazuri na saizi kuna label moja kubwa ambayo mimi natamani kwenda kufanya nao kazi na mambo yanakwenda sawa nitakaribia kuanza nao kazi muda si mrefu,’ alisema Z Anto

Mahakama Yaitupilia Mbali Kesi Ya Mbowe Hotels Dhidi Ya Shirika La Nyumba La Taifa (NHC ) Maha

$
0
0
Mahakama kuu kitengo cha Ardhi imetupilia mbali kesi ya maombi ya kurejea katika jengo iliyokuwa ofisi ya Tanzania Daima pamoja na ukumbi wa bilcanas.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, Sivangilwa Mwangezi ambaye amesema kuwa taratibu zote zilifuatwa kuondoa vitu katika jengo hilo.

Amesema katika hukumu hiyo hakuna mtu aliyevunjiwa haki yake ya msingi kutokana na kufuatwa kwa Sheria dhidi ya madai ya Shirika la Nyumba NHC, kwa Mbowe HotelS.

Wakili wa upande wa NHC, Aliko Mwamnenge amesema kutokana na hukumu hiyo Mbowe hotelS wanadaiwa sh. Bilioni 1.7 na NHC.Amesema vitu haviwezi kurudishwa mpaka pale mlalamikiwa atakapolipa deni lake kwa NHC.

Nae Wakili upande Mbowe Hotel, John Malya amesema wamepokea hukumu na kuomba nakala ili kuweza kuifanyia kazi.Amesema kuwa nakala wakiipata wanaweza kuamua katika kukata rufaa.

Rais Magufuli Amtumbua Mkurugenzi wa Mkinga Baada ya Kumtishia Askari Bastola

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Emmanuel Mkumbo. Uteuzi wa Mkurugenzi mpya atakayejaza nafasi hiyo utatangazwa hapo baadaye.

Mkurugenzi huyo aliyetumbuliwa kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumtishia bastola askari wa kike wa usalama wa barabarani (Traffic). Soma taarifa hii kutoka Ikul

Wanafunzi UDSM Waitupia Lawama Bodi ya Mikopo

$
0
0
Mwisho mwa wiki iliyopita wizara ya elimu ilitangaza majina ya wanafunzi watakaopata mikopo na vigezo vilivyotumika ikiwemo wanafunzi waliosoma masomo ya sayansi, walemavu, yatima, pamoja na ufaulu wa waombaji huku vigezo hivyo vikiwaacha nje wanafunzi wanaochukua masomo ya sanaa.

Wakizungumzia mabadiliko hayo, wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, wamesema hakuna aliyetarajia kutokea kwa hali hiyo kwani hawakutangaziwa mapema kwamba utaratibu wa utoaji mikopo umebadilika. Wengine wamedai kuwa wazazi walikuwa wamekwisha wasafirisha watoto kutoka mikoani wakitegemea udhamini kutoka bodi hiyo.

Naibu waziri wa mikopo UDSM, Abdul Nondo amesema, “Ukiangalia taarifa ambayo imetoka bodi ya mikopo kwamba itatoa fedha kwa wanafunzi ambao watasoma Sayansi,itatoa fedha kwa yatima,itatoa fedha kwa walemavu wale ambao ni maskini. Wamesema shule za kata kwa kulipa ada shilingi elfu 20/70 mpaka kufika chuo sasa hivi na kufanya vizuri. Wanapewa vigezo vya kutopewa mikopo na kubaguliwa kwamba as if they are not students.”

Kwa upande wake waziri wa mikopo wa UDSM, Kasunzi Eliud alisema, “Unaweza ukafika kuna mwanafunzi wa sayansi ni daktari lakini ametokea katika familia tajiri, tunasema familia inayojiweza. Lakini mimi mtoto wa mkulima ambaye nimeweza kusoma kwa shida kwa kuungaunga pesa mpaka nikafika chuo kikuu, leo hii vigezo vinakuja kutoka kwamba mwanafunzi anayesomea masomo ya arts hawezi kupata mkopo.”

Q Chief Ajutia Kujiingiza Kwenye Madawa ya Kulevya..

$
0
0
Ikiwa ni mwaka mmoja toka msanii wa muziki, Q Chief akiri kutumia Madawa ya kulevya na kuamua kuacha mwenyewe, muimbaji huyo bado anaumia akikumbuka jinsi Madawa ya kulevya yalivyomwaribia maisha yake.

Muimbaji huyo ambaye mpaka sasa bado ana mashabiki wengi katika muziki wake, aliacha matumizi ya Madawa ya kulevya baada ya bintie kumuelezea adha anayopata shuleni.

“Nilijiuliza kwa nini namtesa mwanangu kwa kitu kisicho na faida, nikala kiapo kuachana na ‘unga’ na ninashukuru kwa sasa nimezaliwa upya, japo kila nikikumbuka namna nilivyotaka kupoteza nakosa amani,” Q Chief aliliambia gazeti la Mwanaspoti.

Kwa sasa muimbaji huyo ambaye yupo chini QS Mhonda Entertainment anajipanga kuachia wimbo wake mpya ambao video yake ameshoot Afrika Kusini.

Harufu Soko la Samaki Feri Imekuwa Kero..Wateja Wakimbia

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema amesema harufu mbaya inayotoka kwenye soko la samaki la feri inasababisha baadhi ya wateja wasifike sokoni hapo kununua samaki.

Akikabidhi bodi mpya ya soko hilo, Mjema amesema wateja wasipofika kununua samaki mapato ya soko yanapungua na kusababisha soko liendelee kuchakaa.

Ameipa bodi mpya ya soko hilo miezi mitano kumaliza tatizo la harufu hiyo na kuongeza mapato vinginevyo ataivunja.Mkuu wa wilaya alielezwa na Meneja wa Soko, Nico Eliakimu kuwa wanakusanya ushuru wa Sh 105 milioni kwa mwezi

Wanasayansi Kuanzisha Nchi Mpya Angani...Watu 50,000 Watuma Maombi Kuhamia Huko

$
0
0
Wanasayansi hao wanataka kuunda taifa anga za juu ambalo litaitwa Asgardia

Kundi la wanasayansi mjini Vienna, Austria wameanzisha mpango wa kuunda taifa la amani la aina yake ambalo litakuwa na jina Asgardia.

Taifa hilo litaundwa katika anga za juu, eneo.

Maelezo kwenye tovuti ya wanasayansi hao yanasema taifa hilo litakuwa nje ya udhibiti wa mataifa yoyote ya sasa na litakuwa katika mzingo wa dunia, eneo ambalo vyombo vya anga za juu huzunguka dunia.

Wanasayansi hao wanapanga kurusha satelaiti ya kwanza, ya kuanzisha taifa hilo, mwishoni mwa mwaka ujao.

Matumaini ya wataalamu hao ni kwamba siku moja hivi karibuni watatambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Lakini baadhi ya wataalamu wanatilia shaka uwezekano wa mpango huo kufanikiwa ikizingatiwa kwamba sheria za kimataifa huzuia mataifa kudai umiliki wa maeneo anga za juu.

"Raia" wa Asgardia, ambao watachunguzwa kwa makini kabla ya kukubaliwa, mwishowe watapewa hata pasipoti, anasema Lena de Winne, mmoja wa maafisa wakuu wa mradi huo ambaye alifanya kazi kwa miaka 15 katika Shirika la Anga za Juu la Ulaya (EPA).

Maelfu ya watu tayari wameonyesha nia ya kutaka kujiunga na taifa hilo

Mradi huo unaongozwa na shirika la Aerospace International Research Center, ambalo lilianzishwa na mwanasayansi Mrusi, ambaye pia ni mfanyabiashara, Dkt Igor Ashurbeiyli.

Mashindano yanaandaliwa kuamua bendera na wimbo wa taifa wa nchi hiyo mpya.

Profesa Sa'id Mosteshar, mkurugenzi wa Taasisi ya Sera na Sheria za Anga za Juu ya London, amesema itakuwa vigumu kwa Asgardia kutambuliwa kama taifa ikizingatiwa kwamba haitahusiana na taifa lolote linalojitawala duniani, na pia 'raia wake' wengi watakuwa ardhini.

Tayari zaidi ya watu 50,000 wamewasilisha maombi mtandaoni kutaka kuwa raia wa taifa hilo

Taarifa Muhimu: Serikali Yatangaza UHAKIKI wa Wanafunzi Wote Walioko Vyuo Vikuu Ambao Wanasoma Shahada

$
0
0
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inawatangazia Viongozi wa vyuo vyote vinavyotoa shahada nchini vya umma na vya binafsi kuwa kutakuwa na uhakiki wa ubora wa vyuo hivyo.  

Uhakiki huo utaanza siku ya Jumatano Oktoba 19, 2016, hivyo, vyuo vyote vinatakiwa kutoa ushirikiano kwa timu za wataalamu zitakazofika kwa ajili ya kufanya uhakiki huo.

Aidha, katika ukaguzi wa sifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuo vyote, Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), itatoa majina ya wanafunzi wanaotambuliwa na kwamba walidahiliwa kupitia TCU katika Programu zao za Shahada katika vyuo mbalimbali vinavyotoa shahada nchini siku ya Jumanne Oktoba 18, 2016.

Hivyo, wanafunzi wote wanatakiwa kuangalia majina yao katika Tovuti ya TCU na kwa yeyote ambaye hataona jina lake awasiliane na Uongozi wa TCU haraka iwezekanavyo ili kupata maelezo Zaidi. Mwanafunzi ambaye hatazingatia haya ndani ya wiki mbili atapoteza sifa za kuendelea na masomo.

Imetolewa na:

Katibu Mkuu
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Mwanafunzi Apigwa Dar, ‘Afa, Afufuka’ Mochwari

$
0
0
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Lumo wilayani Temeke, Isack Ernest alionja mauti baada ya kupigwa na wananchi kiasi cha kufikiriwa kwamba amekufa, akapelekwa chumba cha maiti ambako alizinduka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto alisema jana kwamba kijana huyo alipigwa hadi kupoteza fahamu na alipofikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke aliwekwa kwenye chumba cha maiti pamoja na kijana mwingine aliyeuawa katika tukio hilo.

“Mwanafunzi huyo hali akiwa amelazwa pamoja na maiti nyingine zinazosubiri kuwekwa katika majokofu, alitikisika kutokana na baridi ya chumba cha maiti, wahudumu wakamwona na kumtoa, wakamvalisha nguo za maiti nyingine, akarudishwa hospitalini kwa ajili ya huduma,” alifafanua Kamanda Muroto.


Mbunge Afafanua Sakata la Mishahara Mitano Hewa

$
0
0
Mbunge wa Makete (CCM), Profesa Norman Sigalla ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, amekanusha kiasi cha fedha kilichoingia kwenye akaunti yake kwamba si Sh23 milioni bali ni Sh5,091,734.96 ambazo zilikuwa hazieleweki.

Profesa Sigalla alitoa maelezo hayo jana alipofika ofisi za gazeti hili, baada ya kudaiwa kupokea mshahara wa ukuu wa wilaya kwa miezi mitano wakati alikwisha acha kazi hiyo alipoteuliwa kugombea ubunge wa Makete na kushinda.

Hali hiyo, iliyoelezwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh23 milioni, ilitokana na madai kwamba hata baada ya kuacha kazi aliendelea kupokea mshahara wake wa ukuu wa wilaya wa Sh4.6 milioni kutokana na ofisa utumishi wa ofisi ya katibu tawala wa Mkoa wa Ruvuma kumrudisha kwenye orodha ya malipo ya mshahara.

Video: Godbless Lema Avuruga Hotuba ya RC Gambo

$
0
0
Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema amepinga vikali hotuba iliyokuwa ikisomwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo la Burka nje kidogo ya jiji la Arusha.

Hayo yametokea leo Oktoba 18, 2016 ambapo shughuli hiyo ilisimama baada Lema kuvuruga hotuba hiyo na kuipinga vikali akidai imejaa upotoshwaji na siasa ndani yake.

Lema alikuwa akipaza sauti kubwa akisema yeye ndiye aliyetafuta eneo hilo la ujenzi kutoka kampuni ya Mawala Advocate. Bofya hapa kutazama video

Wateule wa Magufuli Jifunzeni Kwake Katika Kuheshimu Michango ya Watu

$
0
0
Nampongeza Sana Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa uwezo wake mkubwa wa Kuheshimu Michango ya watu katika jambo fulani la kimaendeleo au tu la kijamii, nitatoa Mifano michache.

1. Wakati akiwa Waziri wa ujenzi Kule Hai eneo la Kwa Sadara palikuwa na Uzinduzi wa Barabara. Mgeni Rasmi katika shughuli ile alikuwa ni Rais wa Kipindi hicho Jakaya Mrisho Kikwete.

Wakati Magufuli anatoa neno la shukrani kama Waziri Muhusika, aliona Faida ya kumpa nafasi Mbunge wa Jimbo hilo Freeman Mbowe. Nina hakika waandaaji wa hafla Ile hawakumweka Mbowe kwenye ratiba lakini Magufuli aliheshimu uwepo wake na kuuthamini na kumkaribisha aseme kidogo.

2. Mwezi April mwaka huu 2016, tayari Akiwa Rais wa Nchi. Wakati wa Uzinduzi wa Daraja la Kigamboni, Rais alikuwa mtu wa mwisho kuzungumza, aliwasikiliza wote waliozungumza kabla yake, lakini hakuna hata mmoja aliyejaribu hata kutaja Jina la Mkurugenzi aliyestaafu wa NSSF Dkt. Ramadhani Kitwana Dau. Japokuwa ni Wakati wa Uongozi wa Dau ndio shirika hilo lilifanikiwa kugharamia sehemu kubwa ya ujenzi wa Daraja hilo.

Kabla hajazungumza. Rais alimuinua Dau, akamsifia na Kuheshimu mchango wake na Taasisi aliyoiongoza. Hakuna aliyeamini macho yake pale, kila mtu aliamini kuwa Rais akikutengua katika wadhifa na kukupangia wadhifa mwengine basi wewe ni mbadhilifu au Jipu, Dau akaogopwa, hakuwekwa kwenye Ratiba akihisiwa kuwa ni Jipu, Rais akauthibitishia Umma kuwa Dau hawezi kutenganishwa na ufanikishwaji wa Daraja lile.

3. Siku ya Uzinduzi wa Mradi mpya wa kupokea simu wa Jeshi la Polisi.
Rais aliwasikiliza wazungumzaji, wote walisahau kuwa Tukio lile lilifanyikia Kinondoni na Halimashauri ya Kinondoni ipo chini ya Upinzani ikiongozwa na meya Boniface Jacob.
Rais alimuita Meya aje kusalimia, Japo meya hakuwepo lakini aliheshimiwa.

4. Jana kwenye Kuaga Mwili wa Marehemu Masaburi, Rais aliona namna ambavyo sehemu kubwa ya wake wa Marehemu walivyotengwa na kutambulishwa mke mmoja tu . Rais akaweka Sawa kumbukumbu na kusisitiza Marehemu alikuwa na wake zaidi ya waliotajwa.
Mifano ni Mingi Mingi Mingi mno.

Leo inasambaa Video na taarifa inayoonyesha mgogoro wa kujitakia kabisa.
Mgogoro ambao Rais kila Mara amefanikiwa kuukwepa, Mgogoro wa Kuheshimu mchango wa mtu mwengine hata kama ni Mdogo.

Nimemuona Mbunge wa Arusha Mjini God bless Lema analalamika, analalamika Mkuu wa Mkoa wa Arusha kushindwa Kuheshimu mchango wake katika kufanikisha upatikanaji wa Mradi wa ujenzi wa Wodi ya wazazi mkoani humo.

Ukiiangalia vizuri ile video, unaweza kuwadharau wote wawili,
Unaweza kumdharau Lema analalamika kutokuwa recognized,
Lakini unaweza pia kumdharau Mkuu wa Mkoa kwa kushindwa kuona mchango wa kiongozi kijana mwenzake hata kama wanatofautiana itikadi.

Haingii akilini katika shughuli za kiserikali kuona viongozi wa mikoa na wilaya wa CCM na au vyama vingine wakiheshimiwa akadharauliwa Mbunge hata kama wa Upinzani.

Kulikuwa na shida gani kwa Gambo kumtaja Mbunge Lema hata kwa kuwepo kwake tu pale?,
Kulikuwa na ugumu gani kwa Lema kumsubiri Gambo Amalize ili athibitishe kuwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho kuwa hakumtaja na amepotosha kama alivyodai? .

Nawaona pia vijana wakijadili swala hili katika msingi wa KI-UKAWA UKAWA na KI-CCM CCM,
hapana vijana wenzangu, hili ni zaidi ya vyama vyenu, hili ni jambo linalitutaka tutumie Busara zaidi kuliko Ushabiki.

Hakukuwa na haja ya kurumbana kwenye hili,
Hakukuwa na sababu ya kuonyeshana misuli, kwamba mimi ni Mbunge na Mimi ni Mkuu wa Mkoa.
Hakukuwa na haja ya viongozi wetu kuonyeshana tofauti zao hadharani, tena mbele ya wanaowaongoza na wafadhili wa Mradi huo.

Hakukuwa na sababu yoyote ya viongozi hawa kugombea Fito katika nyumba wanayoijenga wao wenyewe.
Ni Wakati Sasa wa wateule wa MAGUFULI kubadilika.
Too much is harmful.
Nawasilisha
Ndimi
Habib Mchange

Majibu ya Waziri Mwigulu Nchemba Kuhusu Tuhuma za Kughushi Vyeti vya Taaluma, Kuiba Jina

$
0
0
Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.

Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.

Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.

Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.

Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.

Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.

Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira

Mwigulu,
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>