Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live

Hawa Ndio Wasanii 3 Ambao Lulu Anawakubali Kwenye Bongo Fleva

$
0
0
Msanii mahiri wa filamu Bongo, Elizabeth Michael aka Lulu amewataja wasanii watatu anaowakubali kwenye muziki wa Bongo Fleva.

Muigizaji huyo alikuwa akijibu swali la mmoja wa mashabiki wake kwenye mtandao wa Twitter, lililokuwa linauliza “wasanii gani watatu anaowakubali kwenye Bongo Fleva?”

Lulu alijibu swali hilo kwa kuandika, “Beka, Maua Sama na Alikiba.”

Rammy Galis:Nilikaribishwa Freemason Nikakataa

$
0
0
Star wa Bongo Movie Rammy Galis amefunguka na kukiri kuwa kuna watu hususani wasanii wanaojihusisha na kundi la Freemason na kwamba yeye mwenyewe aliwahi kualikwa kwa njia ya simu yake ya mkononi ajiunge na kundi hilo lakini alikataa.


Akizungumza katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa LIVE kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV, Galis amesema yeye hajajiunga na Freemason na wala hatafanya hivyo lakini alishawahi kutumiwa ujumbe wa kujiunga.

Galis alikuwa akijibu swali kutoka kwa mmoja ya mashabiki wake aliyetaka kujua iwapo Diamond pia yupo katika kundi la Freemason au illuminati kama ilivyokuwa ikidaiwa kwa marehemu Steven Kanumba, ambapo alisema kuwa yeye hawezi kufahamu, na kukiri kuwa suala hilo kwa wasanii lipo na ni la kawaida.

“Kwa kuwa nimeulizwa, ngoja nijibu, ukweli kuna siku nilipata meseji kama ilivyo kwa ujumbe wa tigo pesa au M-Pesa, iliyokuwa na kichwa kilichosomeka Freemason, ujumbe huo ulinitaka nijiunge na Freemason, kama niko tayari kujiunga na biashara hiyo nijibu ujumbe huo na kama sitaki nifute ujumbe huo, nilipojaribu kufuatilia zile namba zikaonesha kwamba hazitambuliki (Unknown number), basi nikaufuta na wala sijafuatilia tena, kwahiyo kuhusu Diamond, mimi sijui” Amesema Galls

Aidha msanii huyo amesema anatarajia kuachia filamu kali mwezi Desemba mwaka huu na kuwataka wananchi kumuunga mkono kwani itakuwa na ubora wa hali ya juu na kwamba ameitengenezea nje ya nchi na wasanii wakubwa wa Nigeria.

Pamoja na hayo Rammy Galis amewataka wasanii wa Bongo Movie kukaza katika soko la sasa na kuto kata tamaa kwani mafanikio hayaji bure bila kuweka juhudi za makusudi .

Singeli Imenipa Nyumba na Gari – Man Fongo

$
0
0
Msanii wa muziki wa Singeli nchini Man Fongo amefunguka na kusema anashangaa mafanikio makubwa ambayo ameyapata ndani ya muda mfupi kupitia muziki wa Singeli hususani kupitia kazi yake ya ‘Hainaga ushemeji’ ambayo imemtambulisha vyema kwa jamii.

Man Fongo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya EATV alisema kuwa muziki huo umebadilisha maisha yake ndani ya muda mfupi na sasa anaona maisha kwake ni kama mepesi akilinganisha na kipindi cha nyuma.

“Kupitia Singeli saizi nimepanga nyumba nzima Tabata, nina miliki gari yangu Toyota Altezza , unajua haya kwangu ni mafanikio yaliyokuja kwa muda mfupi sana kutoka kuishi gheto chumba kimoja mpaka sasa naishi nyumba nzima, familia saizi inaniangalia mimi hivyo naweza kusema Singeli ina neema sana kwangu na mafanikio kwangu yamekuja haraka mpaka nashangaa” alisema Man Fongo


Live Stream: MTV Africa Music Awards 2016, leo (Bonyeza Hapa)

Bebe Mpya wa Wema Sepetu Anyoosha Maelezo

$
0
0
Model' anayedaiwa kuchukua nafasi ya Idriss kwa kutoka kimapenzi na mrembo Wema Sepetu, amejikuta akiweka hadharani mahaba yake kwa mrembo huyo kwa kutoa maelezo yanayothibitisha kuwa hivi sasa yeye na Wema ni wapenzi.

Kijana huyo anayefahamika kwa jina la Calisah, alikumbana na kibano kizito kupitia kipindi cha FNL kinachuruka kila Ijumaa kupitia EATV, pale alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa mahusiano yake na mrembo huyo ambaye alikuwa Miss Tanzania mwaka 2006.

Calisah alisema Wema ni msichana mrembo na mwenye mvuto kwa kila mwanaume, hivyo hata yeye anavutiwa naye na anapenda kuwa naye katika mahusiano, lakini akagoma kusema iwapo tayari wameanza mahusiano au la.

Calisah pia alijifagilia kuwa uzuri wake ndiyo uliomfanya Wema kumzimikia na kuwatosa wote aliokuwa kuwa nao.

"Wema is a beautiful girl, sexy and every man's dream, na mimi pia ni mvulana mzuri ambaye mwanamke yeyote angependa kuwa na mimi, akiwemo Wema mwenyewe, siwezi kusema moja kwa moja kwamba sisi ni wapenzi, lakini lakizima ujue kuwa Wema ni mzuri na mimi mzuri"
Alipotakiwa kutamka sababu za kumpora Wema kutoka kwa Idriss, Carissa amesema hamjui vizuri Idriss, na kwamba hakumbuki kama Tanzania imewahi kuwakilishwa na mtu anayeitwa Idriss katika mashindano ya Big Brother Afrika akisema "Who? Idriss, kwani amewahi kuwa Big Brother? Which year?"

DIAMOND: Nitaudhihirishia Ulimwengu Afrika Mashariki Kuna zaidi ya Wasanii

$
0
0
Diamond Platnumz yupo kwenye mission – ya kuuonesha ulimwengu kuwa Afrika Mashariki si ya mchezo mchezo kwenye muziki.

Akipost picha akifanya rehearsal na dancers wake kwenye ukumbi wa Ticket Pro jijini Johannesburg patakapofanyika tuzo hizo, Diamond ameandika, “Tafadhali sana ndugu zangu naomba kesho msikose kutazama tunzo za MTVMAMA…. kijana wenu nimepanga kuwadhihilishia Ulimwengu Kuwa Africa Mashariki kuna zaidi ya Wasanii

Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Apagawe Kwako

$
0
0
Kuna vitu vingi ambavyo unaweza kutumia kwa manufaa yako ili kufanya wanawake wakuone unavutia. Amini usiamini, hivi vitu si lazima uwe tajiri wala uwe na urembo wowote. Mwanzo kati ya vitu hivyo vingi ni rahisi kuvitumia kwa urahisi. Hii hapa ni orodha ya mambo ambayo ukiyazingatia yatakufanya wewe uwe na mnato kwa mwanamke yeyote yule.

1. Uwezo wako wa nishati
Nishati inaweza kuwa na mkusanyiko wa vitu kadhaa, kama vile kuhisi kwa vipepeo ndani ya tumbo, kusuka, wasiwasi ama vitu tofauti kabisa. Kwa mtizamo wa moja kwa moja, nishati inahusiana na yote yale ambayo yanamfanya mwanamke kujiskia raha wakati anapokuona ama kutaka kuutumia muda wake mwingi akiwa na wewe. Nishati inacheza nafasi kubwa katika mapenzi kama wataka kumtongoza mwanamke na ufaulu kwa urahisi. Ili kupeana nishati zaidi kila wakati unapokuwa na mwanamke, hakikisha kile kikuu unachohitaji kufanya ni kumchekesha, kumsapraiz, umguse kwa bahati mbaya mara kwa mara, kuwa mwenye michezo nk. Zote hizo zitamfanya kukufikiria wewe mara 24/7.

2. Mbinu utakayoitumia kumsifu
Kulingana na utafiti kutoka NBC unadai ya kwamba wanawake wengi hawajiskii huru kupewa ama kupokea sifa kutoka kwa wanaume. Lakini usikatwe na tamaa! Vile ambavyo utampongeza mwanamke inaweza kucheza pakubwa kufaulu kumpata mwanamke unayempendae baada ya muda. Afterall ukimsifu kitofauti tofauti anaweza kukubali ama kukuona kama wewe ni mzaha kwake. So kuhepa aibu kama hizi ndogo ndogo, unafaa umsifu mwanamke kwa jambo ambalo ni la kwake pekee, yaani kitu ambacho utamsifu nacho hakipatikani kwa mwingine. Mfano waweza kumakinika kwa kitu ambacho anafanya wakati flani na utumie ujuzi wako wa kiume kumsifia na jambo hilo. Mfano unaweza kumsifu kwa uwezo wake wa kuimba, kuchora, mtindo wake wa kutembea nk. [Soma: Mbinu ya kutongoza kwa wale wanaojifunza]

3. Upambo wako
Si lazima uwe mwanamume wa kuvutia ili umvutie mwanamke. Utafiti umebainisha kuwa wanawake hawavutiwi na urembo wa mwanamume, nywele zake wala ngozi yake. Mwanzo kuwa mrembo kama mwanamume kuna ubaya wake mwingi ikizingatiwa kuwa unaweza kuonekana kama pleya ambaye unapendwa na wanawake wengi.

Kile ambacho unachohitajika hapa ni uhakikishe kuwa uwe nadhifu kimwili na mavazi yako. Kufanya hivi kutakusaidia wewe kuonekana mtu timamu halikadhalika inakufanya wewe kuwa na confidence ya kapproach demu yeyote yule.

4. Ujuzi wako wa kutangamana
Lazima atleast uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kuweza kutangamana na wengine. Kama mwanamume lazima uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kutangamana na wengine kwa urahisi. Hii inamaanisha kuwa lazima uwe na ujuzi flani wa kuongea na wanawake ndipo utakapojua jinsi ya kumfanya apagawe na wewe.

5. Kiwango chako cha kujiamini
Kitu cha mwisho ambacho ni muhimu kwako kuwa nacho ni kujiamini. Kujiamini ni njia moja wapo ya lazima uwe nayo ili uweze kuiteka hisia ya mwanamke yeyote yule.[Soma: Njia za kuwa na confidence kama mwanaume]

KUMBUKA: Vitu vyote tulivyoeleza hapo juu havitakuwa na manufaa yeyote yale iwapo kama hutaweza kujiamini kama mwanamume. Hivyo ni lazima kwako kuhakikisha kuwa mwanzo unajijenga kwa kuwa na confidence. Hii ni kuanzia kujitambua wewe mwenyewe bila kujishuku, kuongea bila woga wowote wala kutoingiwa na wasiwasi wakati wowote ukiwa karibu na mwanamke.

MTV Mama Awards 2016: Watanzania Waambulia Patupu, Nigeria na South Africa Wang'ara

$
0
0
Usiku wa Jumamosi ya October 22 2016 Johannesburg Afrika Kusini ndio siku ambayo zilitolewa rasmi tuzo za MTV Mama 2016 kwa wasanii waliofanya vizuri kwa mwaka 2016, mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee mkusanyiko wa matukio yote kwenye videos.

Ni kawaida kwa watu maarufu kupewa heshima ya kutoa tuzo kwa kumtangaza mshindi, mshindi wa Big Brother Africa 2014 Idriss Sultan kutokea Tanzania na msanii na mtangazaji wa TV kutoka Angola Weza Solange walipewa heshima ya kutoa tuzo ya kundi bora.

Msanii wa Bongofleva Alikiba kutoka Tanzania, Sauti Sol kutokea Kenya na mrembo Yemi Alade kutokea Nigeria ambaye pia alishinda tuzo ya msanii bora wa kike walikuwa ni miongoni wasanii waliopewa nafasi ya kuperform.

Wasanii kutoka Tanzania wanaounda kundi la Navy Kenzo Aika & Nahreel walikuwa ni baadhi ya watu maarufu waliopewa heshima ya kutoa tuzo za MTV Mama 2016.

Msanii wa Nigeria Wizkid alipopanda kwenye state kuchukua tuzo yake ya msanii bora wa kiume MTV Mama Awards 2016, tuzo ambayo ilikuwa inawaniwa pia na mtanzania Diamond Platnumz.

Jina la mtanzania Diamond Platnumz lilikuwa katika list ya wasanii watakaoperform katika tuzo za MTV Mama 2016, Diamond aliperform wimbo wa Kidogodogo aliowashirikisha P Squre wa Nigeria.

Baada ya baadhi ya wasanii kuperform Partorankig wa Nigeria, Sarkodie wa Ghana, Kored Bello, YCEE na Falz wa Nigeria walikuwa katika list ya wasanii watakaoperform katika tuzo hizo.

Zamu ya utolewaji wa tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana ilikuwa ya msanii wa South Africa DJ Maphorisa akiwa kawashirikisha Wizkid wa Nigeria na DJ Buckz ndio waliofanikiwa kushinda tuzo hiyo ya MTV Mama 2016.

Wizkid hakuishia kushinda tuzo mbili pekee katika usiku huo, lakini waandaaji walikuwa wamemuweka katika list ya wasanii walioperform pamoja na DJ Maphorisa na Emcee.

Msanii Yemi Alade kutoka Nigeria ambaye anafanya vizuri na hit songs zake kadhaa ndio alitangazwa mshindi wa tuzo ya msanii bora wa kike ya MTV Mama 2016.

Baada ya kushinda tuzo ya msanii bora wa kiume kwa mwaka 2016, Wizkid wa Nigeria allitangazwa pia kuwa mshindi wa tuzo ya msanii bora wa mwaka wa tuzo za MTV Mama 2016.




Tanzania safari hii hakuna msanii aliyefanikiwa kushinda tuzo hata moja ya MTV Mama 2016, kwa upande wa tuzo ya Best Breakthrough Act aliyokuwa anawania Rayvanny wa WCB ilichukuliwa na Tekno wa Nigeria wakati tuzo ya chaguo la wasikilizaji iliyokuwa inawaniwa na Yamoto Band ilichukuliwa na Jah Prayzah wa Zimbabwe.




Msanii kutoka United State of America USA Future ndio alikuwa msanii wa mwisho kutoa burudani na kuhitimisha sherehe za utoaji wa tuzo hizo za MTV Mama 2016 kutoka Johannesburg Afrika Kusini.


Nimekuwekea Video Jinsi ALI KIBA Alivyoimba na Sauti Soul MTV Mama Hapa

$
0
0
Nimekuwekea Video Jinsi ALI KIBA Alivyoimba na Sauti Soul MTV Mama Hapa
Tazama Video Hapa Chini Kisha toa Maoni yako

Mwigizaji JB Anusurika Kifo Katika Ajili ya Gari

$
0
0
Mwigizaji wa filamu na mtayarishaji, Jacob Stephen ‘JB’ Ijumaa hii amenusurika kifo katika ajali ya gari.
bongo

Mwigizaji huyo ambaye hivi karibuni alikuwa mkoani Arusha katika shindano la Mama Shujaa, amewataka mashabiki wake kutambua kwamba anaendelea vizuri pamoja na wanzake ambao walikuwa kwenye gari hilo.

Asanteni wote mlionipa pole kwa ajali ya jana,” aliandika JB instagram. “Hakika Mungu ni Mwema, nipo poa mimi na wenzangu wote. Namshukuru sana Mungu.Thank you JESUS,”

Kwa sasa mwigizaji huyo anafanya vizuri na filamu yake, ‘Kalambati Lobo’.

Ajali za barabarani nchini Tanzania zinatajwa kuwa ni moja kati ya matukio ambayo yanasababisha vifo vingi nchini.

Mastaa wa Kike Kutoka Familia za Mboga Saba Bongo

$
0
0
NAIJUA familia ya mboga saba? Wengine wanapenda kuwaita watoto wa kishua ama familia bora. Hii ikiwawakilisha watoto wanaozaliwa kwenye familia yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi, kiasi cha kutumia mlo mmoja ukiwa na mboga tofauti na zinazobadilishwa kila uchao. Ndio, kuna familia nyingine bhana mlo unakuwa na mboga moja na huwa ni hiyo hiyo deile mpaka inachosha.

wee
Ingawa kuna dhana kuwa watoto wa kishua huwa wavivu kujitafutia kwa sababu kila anachokotaka hukipata tu nyumbani, lakini ukweli sio wote. Kuna wengine wanaamua kuchakarika kutafuta maisha yao wenyewe, hata hawalingani na wale waliotokea familia za watu duni ambao walikatisha masomo ili kusaka noti wakiwa kwenye umri mdogo kabisa.

Mwanaspoti inakuletea baadhi ya mastaa wa kike waliozaliwa kwenye familia ya mboga saba, lakini wanakomaa kivyao vyao ile mbaya wakijichanganya na wenzao kusaka noto kwa jasho na damu.

VANESSA MDEE

Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988. Vanessa anatokea familia bora ya Sammy Mdee ambaye kwa sasa ni marehemu. Enzi za uhai wake, baba ya Mzee alikuwa mtu mzito kwenye nchi hii akiwa mume wa Sophia.

Akiwa na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. Vanessa Mdee alikulia miji ya New York , Paris, Nairobi na Arusha, lakini kwa sasa jamaa anatisha mbaya kwenye fani ya muziki akitamba ndani na nje ya Afrika.

JOKATE MWENGELO

Huyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku baba yake akifanya kazi serikalini.

Kumbuka Jokate alizaliwa Washington DC, Marekani ambapo wazazi wake walikua wakifanya kazi huko. Alipomaliza masomo ya juu ya Sekondari pale Loyola ndipo alipoanza kujichanganya kwa kuwania taji la Miss Tanzania mwaka 2006 na kushika nafasi ya 2 nyuma ya Wema Sepetu, kisha kuhamia kwenye fani ya muziki, utangazaji, mitindo na ubunifu na sasa akipiga fedha.

WEMA SEPETU

Wema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye familia ya kibalozi akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa marehemu Balozi Isaac Sepetu.

Wema alizaliwa mwaka 1988 katika hospitali ya St. Andrew ya Dar es Salaam na amesoma elimu yake ya awali mpaka sekondari kwenye Shule ya Academic International iliyopo Dar es Salaam kabla ya kwenda Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka Chuo Kikuu cha Limkokwing.

Alianzia shindano la urembo akitwaa mataji kadhaa ikiwamo la Miss Tanzania 2006 kisha kuhamia kwenye filamu na sasa anaendelea kukimbiza akimiliki kampuni yake na akizalisha bidhaa zenye jina lake. Achana kabisa, ila ukiamua kubisha we bisha tu.

Amber Lulu Afunguka Kukamatwa na Madawa ya Kulevya, Bifu na Gigy Money na Uhusiano wake na Young Dee

$
0
0
Msikilize hapa akihojiwa na mtangazaji wa Kings FM, Prince Ramalove ambapo amezungumzia kwa mkato tetesi za kukamatwa na madawa ya kulevya, bifu na Gigy Money, uhusiano wake na Young Dee na fedha anazolipwa kufanya video.

Huyu ni Msanii Mwingine Kutoka Afrika Aliyesaini na Lebo ya Sony Music

$
0
0
Ijumaa ya tarehe 21 October 2016, Afrika kusini ikiwa ni tawi la Sony Music Entertainment, kampuni ya masuala ya Entertainment kwa upande wa Afrika, ilitangaza kumsaini msanii mwingine ndani ya lebo hiyo, Ycee ambaye anafanya kazi na lebo ya Tinny Entertainment.

Mkataba aliosaini YCEE unaonesha kuwa Sony Music watasimamia albam yake ya kwanza na ngoma zake zote zitakazoanza kutoka pamoja na usambazaji wake kuanzia sasa zitakua chini ya mwavuli wa Sony Music. Kwa shavu hilo inamaana kuwa Ycee anaungana na Nigerian superstar Davido, pamoja na Alikiba kwenye familia ya mastar kutoka Afrika walikula deal la Sony Music.

Kwa mujibu wa Michael Ugwu, General Manager wa Sony Music West Africa amesema “Nina furaha kubwa sana kuwakaribisha Tinny Entertainment pamoja na msanii wao Ycee ndani ya familia ya Sony Music Entertainment West Africa. Nimekuwa nikishuhudia team hii ikikua kwa haraka kwenye miaka ya karibuni na nimeshangazwa na jinsi walivyoweza kufikka hapa, Ycee ni msanii mkali sana wa Hip Hop barani Afrika na muda sio mrefu atakua kwenye level za mbali sana.”

Kwa upande wa Arokodare ‘Tinny’ Timilehin, ambaye ni CEO wa Tinny Entertainment, amesema

“Tuko na furaha sana kwa upande wetu na msanii wetu Ycee. Huu ni uthibitisho kuwa tumefanya kazi kubwa sana mpaka kufikia hapa. Na katika kuonesha furaha yake juu ya deal hiyo,

Eddy Kenzo Awatolea Uvivu MTV Base, Adai Ameshinda ila Tuzo Akapewa Mwingine

$
0
0
Msanii wa Uganda Eddy Kenzo asema kuna namna inafanyika kuamua washindi wa MTV Mama na si upigaji wa kura maana kwenye kipengele change yeye ndo alikuwa na kura nyingi akifuatiwa na Mr. Flavour huku alieshinda Casper nyovest alikuwa na tatu kwa wingi wa kura...

Eddy KenZo Ameandika namnukuu
"Mimi Balozi wa mtandao wa Simu wa Airtel, Bahati Mbaya Mtandao wa Simu wa MTN ndo Wadhamini wa TuZo Za #mtvmama2016 na Mshindi ktk kipengele nilichotajwa Ni Balozi wa MTN (umeona eeeh) Eddy Kenzo akaendelea kutoboa "kumbuka nimetumbuiza ktk nchi 35 Na nchi 10 Kati ya Hizo nimetumbuiza nikiwa na nyomi la Kwenye Viwanja vya Mpira kuna nn mafanikio gani Zaidi ya hayo?
.
Walituambia tupige Kura Na Mashabk zangu walifanya hivyo Kwa kwenda kwenye mitandao ya MTV, Eddy Kenzo akasisitiza "Nenda Kwenye mtandao wao Na bonueza kipengele Cha #BestLiveAct Na ukajionee Mshindi nani, sina wivu mm (Kama Jux 🙈) Ila na lalamika kwasababu walituambia tupge Kura na mashabiki wakafanya maamuzi, nenda Kwenye page MTV ukaangalie walichosema Hata Kwenye emails, mm Eddy Kenzo ndo niliyepigiwa Kura Zaidi ya wote ktk kipengele Cha Best Live Act Na Msanii Ston Boy alikua wa Pili, Mr Flavour alikua wa TATU, Na Caspa Nyovest alikua wa Nne ktk Platforms zote MTV Base Africa, lakini mwisho wa cku mtu wa 4 ndo amepewa TuZo, jamani jamani Hata ingekua Wewe Povu lingekutoka tu, au mm ckuwaelewa waliposema tupige Kura Kwa Msanii unayempenda? Eddy Kenzo akamalizia Kwa kuwashukuru mashabiki zake Na Mwenyezi Mungu, imetafsiriwa Na MAKOROKOCHO @soudybrown .
Eheeeeeee nimejitahd kutafsiri Na ka dictionary Kangu ka kunyapia nyapia 🙈
.
Kwa anachokimaanisha Eddy Kenzo Ni kuwa wasanii Kama Navy Kenzo Hata wangefanya nn wasingepata TuZo kwasababu Ni mabalozi wa AIRTEL Tanzania, pia Bwana Diamond Platnumz asingeweza kupata TuZo kwasababu yeye Ni Balozi wa Vodacom, Ya Moto Band Na Ali KIBA nao wasiweza kupata TuZo kwasababu Ni mabalozi wa mtandao wa Simu wa @shilawadu Kazi kweli kweli #mtvmama2016 sio watu wa Spoti Spoti -

Crazy GK Adai Kweli Alikiba ni Mfalme wa Mziki....

$
0
0
Mkongwe huyo wa mziki ameyasema maneno hayo katika kipindi cha MY PLAYLIST knachotushwa na clouds tv, aidha amesema kuwa Alikiba ni mwanamziki anaejielewa, mwenye sauti nzuri na anejua kuitumia vilivo, ametumia muda huo kuongelea wimbo wa AJE kwa kusema kua ni wimbo ambao hauchuji haraka kama wengine, pia amesema kua wimbo wa AJE kila siku ukiutizama na kuusikiliza unagundua kitu kipya tofauti na ulichoona au kusikiliza jana.

Hongera mfalme Kiba kwa kutoa nyimbo zisizochuja haraka kama wale pia kupongezwa na wanamziki wakongwe wanaojua historia ya mziki wa bongo na walio kwenye mziki muda mrefu kama GK.



Joketi Kujenga Viwanja Vya Michezo

$
0
0
Mrembo, Jokate Mwegelo ameahidi kujenga viwanja vya michezo kwa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mahafali ya nane ya shule hiyo, Jokate alisema atajenga viwanja hivyo kupitia kampeni yake yake ya kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified.”

Amesema ameguswa na changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo na kuamua kusaidia kwa kupitia kampeni yake hiyo.

Tayari Jokate amekabidhi viwanja katika shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani.

Nimekuta Chupi ya Mke Wangu Chumbani Kwa Mdogo Wangu wa Kiume

$
0
0
Jamani Leo ni Siku ya saba tangia nikute chupi ya mke wangu chumbani kwa mdogo wangu wa kiume,nimekaa nalo moyoni naona niwashikirikishe wenzangu nione mnishauri nini

Ni hivi Ninaishi na mke wangu,mwaka wa NNE sasa,tuna mtoto mmoja,nina Mdogo wangu,anaishi hapa tangia January niliponunua bajaj ili awe anaendesha ili kusaidia wazazi wetu nyumbani kijijini,sasa jumapili iliyopita Wife aliwahi sana asubuhi kwenda kanisani pamoja na mtoto, Mimi nilibaki nimejilaza mpaka kama SAA moja na nusu Hivi, nilivyokumbuka kuwa nilikuwa na Ahadi Fulani, katika kufanya maandalizi sikiweza kuiona pass, so nikaenda straight chumbani kwa dogo katika kuitafuta ndo nilipo kutana na chupi ya mke wangu, ambayo Mimi mwenyewe nilimununulia so imechoka choka kiasi chake,nilishikwa na butwaa kwani namwani sana wife, dogo mwenyewe heshima kwa sana, nilichukua simu na kupiga picha kadha na kuzificha kwenye private vault, ile chupi nikaaicha palepale, wife hajasema chochote mpaka sasa, nawaza namna ya kuanza kumuulizia japo ameshahisi kuwa siko normal,coz nikimuona usoni nakuata hasira imepnada sana,kwa kifupi naogopa ukweli kuwa mke wangu amenisaliti kwa mdogo wangu,mpaka sasa simuoni kama mke wangu tena, namuona kama bundi kajificha chumbani kwangu, naomba mnishauri kwani Mimi kwa haraka haraka naona nimwite kaka yake aje amchukue kabla sijamfanya kitu mbaya, tatizo hasira zangu hupanda pole pole sana, kuzishusha ni kazi sana

By Shonkoso


Je ni Kweli Mwanaume Ukiwa na Gari Utawanasa Wadada Wengi Mjini?

$
0
0
Mwanaume hata uwe mzuri wa sura kivipi lakini huna gari na vijisenti kidogo mfukoni, hakika utasumbuka sana kutongoza na kukubaliwa kirahisi na mwanamke. Bila kumumunya maneno wala nini, ni ukweli usiofichika kuwa wanawake wengi wamekuwa dhaifu sana punde wakitongozwa ama kufuatwa na mwanaume mwenye gari hata kama sio lake.

Yaani wanawehuka kiasi kuwa warahisi kuwapata kwenda nao kuwabungunyua papuchi. Wengine huwa wanajilengesha wenyewe kwa mbinu zozote wajuazo. Msichana/mdada/sistadu whatever ukimpatia lifti mara kwa mara utakuta kiulaini unaachiwa papuchi mwaa.

Kisa Cha Mama Mkwe wa Mwendokasi Alivyookoa Ndoa Isivunjike

$
0
0
Tafadhali WANAUME wenzangu naomba usome kisa hiki kwa makini sana. Usipuuze.

“Mpaka sasa hivi bado anaendelea kukupiga?” Mama John alimuuliza mkwe wake.” Ndiyo mama tena amezidi, yaani kila siku nimekuwa kama ngoma, nimechoka Mama nibora nirudi kwetu, kwetu sijaua Mama..” Anna aliongea huku akitokwa na machaozi. Mama mkwe wake alimuangalia kwa huruma, kisha akamuambia.

“Usiondoke mwanangu, nitaongea naye…”

“Haitasaidia chochote Mama, mara ngapi tumekaa vikao kuongea naye lakini habadiliki. Wanangu wameshakuwa wakubwa naondoka, sitaki kuendelea kuteseka…”

“Hapana usiondoke mwanangu, sasa hivi nilazima akusikilize…”. Anna alikuwa amekata tama, miaka nane ya ndoa yake ilikuwa ya mateso sana na mara kadhaa alishamlalamikia mama mkwe wake kuhusu tabia ya mumewe kumpiga lakini haikusaidia.

Kila mara mumewe alisema atajirekebisha anapokuwa mbele ya wazazi wake lakini akifika nyumbani huanza upya akimpiga hata kwa kushitaki. Anna alishafanya maamuzi ya kuachana na mumewe, tayari alishapata chumba chake na alienda kumpa tu taarifa Mama mkwe wake ambaye walikuwa wakipatana sana.

“Wewe nenda nyumbani nitakuja huko huko kuongea naya, safari hii atanisikiliza, si bado mnafuga Kuku?” Mama mkwe wake alimuuliza swali ambalo hakuelewa kuwa lilikuwa linahusiana na nini na kupigwa kwake, lakini alijibu. “Ndiyo Mama bado tunafuga…”

Alijibu na Mama mkwe wake alimuambia kwenda nyumbani kwake na kesho yake angeenda kuwatembelea. Anna aliondoka akiwa na wasiwasi, wazo la kumuacha mumewe lilikuwa palepale, hakuwaza ni kitu gani ambacho angefanya ambacho kingemfanya kubadilisha mawazo yake.

***

Jioni ya siku iliyofuata Mama John alifika nyumbani kwa mwanae, John alikua bado hajatoka kazini na Anna alikuwa akijiandaa kupika chakula cha usiku, Mama John alimuambia mkwe wake siku hiyo anataka kupika yeye. Ingawa Anna hakutaka lakini alilazimishia mpaka akawa hana namna, aliingia jikoni na kuanza kupika akiwaambia watu wote kukaa sebuleni kuangalia TV.

John aliporejea alimkuta mkewe na watoto wakiangalia TV aliambiwa Mama yake yupo na yuko jikoni anapika, alitaka kufoka kwanini mkewe anamufanyisha kazi Mama yake ambaye alikuwa mzee lakini Mama yake alitokea na kumuambia yeye ndiyo kaamua kupika.

John alikuwa ampole kwani pamoja na ukali wake kwa mkewe lakini bado alimpenda na kumuogopa Mama yake kama mtoto. Alikaa kistaarabu sebuleni kama mkewe, Mama yake alimaliza kupika na kutenga chakula mezani, Anna na Mfanyakazi wa ndani walipotaka kumsaidia alikataa na kusema atafanya kila kitu mwenyewe.

Alitenga chakula mezani na kumpakulia kila mtu kwenye sahani kisha akawakaribisha. Ingawa haukua utaratibu kwa maana kila alikuwa akipakua chakula chake mwenyewe lakini hakuna aliyeongea, wote walifurahia chakula cha Mama.

Wakiwa wamekaa mezani baada ya sala, John alichukua kijiko na kuchota chakula, alipandisha mkono wake kukiweka mdomoni lakini kabla hajafika mdomoni Mama yake ambaye alikaa pembeni yake akimuangalia alikipiga kile kijiko chakula kikamwagika.

“Acha kula hicho chakula, chukua hiki?” Mama John aliongea huku akichukua sahani iliyokuwa na chakula cha John na kumsogezea ile ya kwake. Watu wote walishangaa kwa kile kitendo lakini Mama John hakujali, aliichukua ile sahani na kijiko alichotumia John akarudi jikoni kisha baada ya muda akarudi na sahani nyingine ambayo alikula yeye.

John aliuliza nini kinaendelea lakini Mama yake alifoka “Kula, hakuna kuongea wakati unakula! Unakuwa kama sikukufundisha nidhamu?” Mama yake alimjibu kwa sauti ya juu. Waliendelea kula kimya kimya, hakuna aliyetaka kuongea.

***

Baada ya kumaliza kula, Mama John hakutaka mtu aguse vyombo, aliondoa vyombo mwenyewe na kuvipeleka jikoni. Kila kitu kilikuwa chakushangaza hawakujua kwanini kaamua kufanya hivyo. Baada ya kuondoa vyombo na watoto wenda kulala, ulikuwa ni wakati wa wakubwa nao kulala.

Kabla ya kwenda kulala Mama John alirudi jikoni na kuchukua sahani ya chakula, ilikuwa ni ile ambayo alimkataza mwanae kula. “Naomba mnisindikize nnje..” Aliwaambia na wao bila kujua kuwa alikua anataka kufanya nini walinyanyuka na kuongozana naye, “Uje na funguo za banda la Kuku”. Aliamrisha na Anna alienda kuchukua funguo la banda la Kuku.

Walifika katika banda la Kuku, kulikuwa na mabanda matatu, Mama John aliwaambia kufungua moja ambapo alimwaga kile chakula kwenye lile banda la Kuku ambao walianza kukimbizana, alifunga banda na kuwaambia waende wakalale. Bila kujua sababu zake za kufanya hivyo waliingia ndani kulala kila mmoja akiwa na mawazo yake.

***

Siku iliyofuata ilikua ni Alhamisi hivyo Anna na Mumewe walitakiwa kwenda kazini. Waliamka mapema na kukuta Mama mkwe kashaamka zamani na kashaandaa chai, ulikua ni mshangao kwani mara kadhaa alikuja kukaa pale na hakuwa akifanya hivyo. Aliwaandalia chai mezani na kwa mara nyingine John alipotaka kunywa alimzuia na kubadilisha kikombe.

Walimuuliza kwnaini anafanya hivyo lakini alikataa kuwajibu akiwaambia wanywe chai kwanza. Walikunywa chai na baada ya kumaliza wakati wakitaka kuondoka, aliwaambia waende kwanza kwenye banda la Kuku. Walifika na baada ya kuangalia, katika mabanda mawili hakukuwa na kitu, Kuku walikuwa salama.

Lakini katika banda lile ambalo alikua wamemwagia chakula ambalo lilikua na kuku zaidi ya kumi, wote walikuwa wamelala chini wamekufa. John na mkewe walistuka na kushangaa nini kimetokea, Mama yake aliwaangalia akiwa maetulia kwa muda kisha akasema.

“Unaona mwanangu, hicho ndiyo chakula nilichokutengea mezani jana. Nilikuwa nimeweka sumu kama ambavyo nimeweka katika chai asubuhi, kijiko kimoja tu au funda moja la chai vilitosha kukufanya kuwa kama hao Kuku hapo!” Aliongea huku akiwaangalia namna walivyokuwa wanashangaa midomo mizito hata kufunguka.

“Jana niliokoa maisha yako, lakini ningeweza kukuacha ule na subuhi ukaamka kama hao Kuku nikawaambia majirani umekufa kwa presha kama ambavyo naweza sema hawa Kuku wamekufa na kideri…

Mkeo kila siku analalamika unampiga, kila siku nakusihi acha kumpiga mkeo lakini husikii. Jana alikuja kwangu na kuniambia kuwa kachoka na anataka kuondoka, huyu ni mke mwema, wengine wanapochoka hawaondoki bali wanakuondoa wewe.

Nikuulize kitu kimoja wakati una miaka mingapi?” John alilisikia swali lakini hakuweza hata kujibu bado alikuwa ameshikwa na butwaa. “Huwezi kujibueee… mimi nakumbuka miaka 35, hembu niambie wakati unakua kuna Babu yako hata mmoja ambaye ulimuona…?

“Hapana, hata siwakumbuki…” John alijibu kinyonge kabisa.

“Na Bibi zako…”

“Wote wapo mpaka sasa…”

“Nadhani sasa umepata jibu… chezea kila kitu lakini si mwanamke anayekupikia chakula! Usifikiri kila mwanaume anayekufa ni Mungu kapanga, wengine ni wake zao wamechoka tu kupigwa na kunyanyasika. Mke wako anaondoka kwakuwa ana kazi anajua anaweza kujihudumia, hembu jiulize kama angechoka halafu hana kazi anajua ukimuacha anaenda kuwa ombaomba…

Mimi ni Mama yako nimeona mengi, acha kujifanya mwanaume kuliko wanaume wengine, mwanaume kamili hampigi mke wake anenda kupigana na wanaume wenzake. Mimi naondoka, sitegemei kusikia umempiga mkeo tena…

Kama unataka kuendelea kumpiga basi anza kupika mwenye…” Mama John alimaliza kuongea kisha akarudi ndani akiwaacha wote wameduwaa, alichukua mfuko wake aliokuja nao na kutoka nnje kuondoka. Alirudi na kumuona mwanaea amepiga magoti akimuomba mkewe msamaha…”

Anna alikubalia kumsamehe mume wake ambaye aliahidi kutokurudia tena. John aliahidi kubadilika na kweli alibadilika, alianza kuwahi kurejea nyumbani na kurudisha mapenzi yote kama kipindi cha uchumba, hakumpiga tena mkewe na sasa ndoa yao ina miaka kumi na tano bila ugomvi wowote.

Ndalichako, Mahiga Wawavuruga Chadema..... CCM wajichagulia Meya bila mpinzani

$
0
0
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo kimeususia uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, hali iliyopelekea wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya uchaguzi peke yao na kuwapigia kura wagombea wao bila upinzani.

CCM wamemchagua Benjamin Sitta kuwa Meya wa Manispaa hiyo kwa kura zote 18 za wajumbe wa chama hicho. George Manyama amepata Baraka za wajumbe hao wa chama tawala kuwa Naibu Meya wa Manispaa hiyo.

Chadema waliususia uchaguzi huo kwa madai kuwa CCM wamechakachua kwa kuwaleta Profesa Joyce Ndalichako (Waziri wa Elimu) na Balozi Agustine Mahiga (Waziri wa Mambo ya Nje) kupiga kura katika Manispaa hiyo ili hali waliapa na kusajiliwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala. Hivyo, sio wajumbe halali wa Kinondoni na hawakupaswa kupiga kura.

Wajumbe wa Chadema wanadai kuwa uchaguzi uliofanywa na CCM peke yao sio halali kwani pamoja na mambo mengine akidi ambayo ni 2/3 ya wajumbe waliopaswa kufanya uchaguzi huo kuwa halali haikutimia.

Chadema imepanga kupinga uchaguzi huo mahakamani
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live


Latest Images