Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

JOKATE NA GODZILLAH KITUGANI KINAENDELEA...?

0
0
Mlimbwende Jokate Mwengelo na King Zillah Msanii wa Bongo fleva wakifanya yao maeneo ya kujidai, sasa hii ni Clip ya Moja ya kazi zao hapo bado ni kizungu mkuti….Endelea Kuwa nasi tutakujuza..!!!

SITTA:SAINI ZA NYERERE NA MSEKWA ZIMECHEZEWA KWENYE HATI YA MUUNGANO

0
0
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amekiri “kuchezewa” kwa saini ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na sehemu ya saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa zilizopo kwenye hati ya sheria ya kuridhia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema ni kweli kuna maneno katika hati hiyo ya sheria namba 22 ya 1964, iliyosainiwa na Nyerere na Msekwa, Aprili 25, 1964, yameongezwa.

Alisema katika saini ya Nyerere kumeongezwa herufi “us” kwa kompyuta na katika sehemu ya saini ya Msekwa kumeandikwa neno “Msekwa” kwa kompyuta, jambo ambalo ni makosa. Sitta alisema walioongeza maneno hayo ni wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuona sehemu ya maandishi kwenye saini hizo hayasomeki, lakini walifanya makosa.

“Wale vijana walipoona document (nyaraka) haisomeki waliongeza “us” mwisho kwa kompyuta kwenye saini ya Nyerere, ila walifanya makosa maana bora kitu kionekane kufifia hivyo hivyo lakini kibaki na maana yake,” alisema.

Hata hivyo, Sitta alisema kwa waliofanya kazi na hayati Baba wa Taifa wanatambua saini iliyopo kwenye hati ya sheria hiyo ipo sawa ukiondoa makosa ya kuwekwa herufi hizo.

Kuhusu saini ya Msekwa, alisema pia kulifanyika makosa katika sehemu ya saini hiyo, kuandikwa kwa kompyuta “Msekwa”.

“Ni saini ya Msekwa, lakini vijana wa chamber kwa AG waliongeza neno “Msekwa” kwa kompyuta. Ni mtu asiyejua thamani na uhalisia wa saini ni kubaki ilivyo hata kama kwa miaka 100 hata mtu aje kuisoma kwa darubini,” alisema.

Hata hivyo, alisema maudhui ya hati ya sheria hiyo, iliyosainiwa rasmi Aprili 25, 1964 ni sahihi kama ambavyo walikubaliana waasisi wa Muungano, Nyerere na Karume.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema alisema kwamba hafahamu kama ofisi yake inahusika na kuchezewa kwa saini hizo, tofauti na madai ya Sitta.

Sheria iliyopitishwa Z’bar

Sitta alisema ili kuondoa utata, ameagiza kupatiwa hati ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume (Presidential Decree) aliyotoa kusaini makubaliano kwani wakati huo, hakukuwa na Bunge.

“Karume alitumia Baraza la Mapinduzi akatumia amri ya Rais akasaini. Tunatarajia kuipata hiyo, sasa tutakuwa tumepata nyaraka za Bara na Zanzibar,” alisema Sitta.

PICHA ZIKIONESHA TUKIO LA WATU WATATU WALIO KUFA KWA KUFANIKWA NA KIFUSI BUNJU

0
0





Watu Watatu wamekutwa na tukio la kufukiwa na kifusi maeneo ya machimbo ya kifusi huko Bunju , watu hao walikuwa wakichimba kwa bahati mabaya udongo ukamong'onyoka na kuwafukia, wananchi mbali mbali walijitokeza na kusaidia zoezi la uokoaji kwa bahati mbaya wote walipatwa wakiwa wameshafariki ....Walio fariki imefahamika ni bwana Msagala, Jacob na Mwando wote ni wakazi wa Bunju....RIP

JUA VITU 5 AMBAVYO HUTAKIWI KUMSHIRIKISHA BOYFRIEND WAKO NI HIVI HAPA

0
0
Where to draw the line in a relationship is very important. Certain info should only be limited to you.

Personal affairs call for careful attention. And when it comes to a relationship, it makes all the more sense to keep certain personal information and details to self. The same applies to your boyfriend too. You too might be having very true and genuine feelings for each other, but being careful always helps one as an individuals. Here’s a list of things never to share with your boyfriend:

Don’t share the password
Never ever share password of any sort. Be it your email or facebook or twitter id password, keep the sensitive information to yourself. No matter how close you guys are, there is no point in sharing passwords. Let you two have your different worlds.

Don’t share your diary
It may seem romantic to share your thoughts by sharing your diary, but that too is highly avoidable. Never ever should you let your boyfriend know how you think and what you think.

Don’t share personal pics and videos taken on your smartphone
If the pics of you two are clicked or videos are taken on your smartphone, do not transfer those to him. Transfer those to your computer or tablet. And delete from your database. If they are of too intimate in nature and you do not like the whole set of relatives of either side take notice of those, delete them from your smartphone silently without informing him.

Don’t reveal best friend’s secrets
Your best friend has been there and done that for you all the time. But don’t make the mistake of revealing your best friend’s secret to him. This will be absolute betrayal to your best friend. So keep some secrets to yourself.

Don’t share your secrets too
You never know when a relationship can go sour. So avoid sharing all the crucial and sensitive information that is related to you till you are sure of his conduct and intentions. If he is too inquisitive, just give a rough sketch of you as a person, but do not give too many details of your life.

VITU NANE VYA KIPUMBAVU AMBAVYO WADADA HUFANYA KWENYE MAPENZI

0
0
1. Kuishi na mwanaume ambaye ajakutolea mahari au kukuoa. Hii inachoma lakini ndio ukweli wenyewe. Usiwe mjinga 

2. Kukubali kuwa mke wa pili. Samahani sana nitakao gusa imani zao

3. Kuvaa pete ya uchumba ya mwanaume ambaye even hata kwenu apajui. Na pengine hata wazazi wako hawajui

4. Kutumia picha ya boyfriend wako kama profile picture wakati yeye hana hata wazo la kufanya hivyo.

5. Kumpa thamani yako PRIDE (Bikira), mwanaume ambaye ajatoa pesa ya mahari

6. Kupika chakula mara kwa mara na kufua nguo kuonyesha upendo kwa boyfriend wako ambaye sii mume wako.

7. Kutokumuheshimu mzazi wako kwa sababu tu ya mwanaume ambaye wazazi wako hawamjui

8. Kumpa mwanaume sex kirahisi tu kwa sababu amekuambia atakuoa

JITAMBUWE!!!

NASH MC AWEKA WAZI HISIA ZAKE KWA MREMBO MENINAH

0
0
Unaweza kuichukulia kivyovyote lakini maandishi ya member wa Tamaduni Music, Nash MC yameeleza wazi kuwa anamzimia mrembo  na mwimbaji wa kundi la Shosteez, Meninah la Diva. 

Comment ya Nash MC aliyoiweka kwenye post ya Jabir Saleh a.k.a Kuvichaka aliyokuwa ameweka kwenye ukurasa wa  Facebook akiwa na Dayna Nyange ambaye atakuwa mkali wa The Jump Off kuanzia wiki ijayo, ilikuwa na ujumbe wa wazi kwa mtangazaji huyo. 

 “Siku ukimhoji menina nistue maana mamzimia kweli.” Aliandika Nash MC. 

Hata hivyo, ujumbe huo haukuishia kwa Kuvichaka na akaupeleka kwa watu wengine ambao wanaweza kukutana na Meninah au wale ambao walidhani ametereza tu kuandika kwa uwazi. 

“Hilo lipo wazi na mkimuona mwambieni.” Alisisitiza Nash MC. 

Rapper huyo wa Naandika alijitoa kwenye lawama binafsi na kuchombeza kiutani kuwa kilichomsukuma na upendo. “Sio mm ni sababu ya mapendooooooo!” 

KANISA KATOLIKI JIMBO KUU TABORA LADAIWA KUTAKA KULIPULIWA

0
0
Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Tabora ambalo limedaiwa kutaka kulipuliwa majira ya saa nne asubuhi ya leo baada ya kubainika kuwa mtu mmoja ambaye alifika Kanisani hapo na kutaka kumrubuni mlinzi kwa kumpatia kiasi cha shilingi elfu ishirini ili aweze kutekeleza dhamira yake ambayo haikufanikiwa baada mlinzi kutoa taarifa kwa uongozi wa Kanisa hilo ambao walitoa taarifa kwa makachero wa Jeshi la Polisi Tabora na kufanikiwa kukamatwa kwa mtu huyo.

MGOMBEA UBUNGE CHALINZE KUPITIA CHAMA CHA AFP AJERUHIWA KWA MAPANGA

0
0
Mgombea Ubunge katika Jimbo la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ramadhani Mgaya kupitia chama cha AFP amejeruhiwa kwa mapanga na watu wasio julikana.

Mgaya amesema amevamiwa na kujeruhiwa na mtu ambaye hamfahamu majira ya saa sita za usku akiwa katika nyumba ya kufikia wageni ya Goodtime Chalinze.

"Nimevamiwa na kujeruhiwa na mtu ambaye simfahamu ahsante uongozi wa chadema kwa kunisaidia,"alisema Mgaya.

Mgaya amesema ameumia mikononi wakati nikipangua nakujitetea mvamizi alikuwa na panga. Mbali na yeye pia amesema pia kiongozi wa Chadema, Mwita Waitara naealijeruhiwa kwakuwa alikuwa moja ya watu waliokuwa wakimsaidia.

UKAWA WAUMBUANA BUNGENI

0
0
TABIA ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, hasa kutoka vyama vya upinzani waliounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutafuta kasoro ndogo ndogo za kutaka Bunge liahirishwe mara kwa mara, imewatokea puani. Jana baadhi ya wajumbe hao akiwepo Ismail Jussa Ladhu, Tundu Lisu, John Mnyika na Moses Machali, walisimama kupinga marekebisho ya kanuni za Bunge Maalumu kwa madai kuwa yameletwa haraka haraka na yana nia ovu.

Mtindo wao Alianza Jussa, akasema wajumbe hawana jedwali la marekebisho ya Kanuni hivyo ni bora hoja ya marekebisho hayo iahirishwe ili kuwapa nafasi ya kuyapitia na kuleta jedwali lao la marekebisho.

Wakati Jussa akidai wengi wao hawana jedwali hilo la marekebisho, alishangaa kuona wajumbe wenzake wengi, akiwemo aliyekaa naye wakipepea juu jedwali hilo, kuonesha ni yeye peke yake na baadhi ya wachache hawakuwa na jedwali husika kwa kuwa wengi walikuwa nayo.

Lissu Jussa alilazimika kukaa baada ya kuona hali hiyo, lakini akasimama Lissu na kutoa hoja ya kutaka mjadala wa marekebisho hayo, uahirishwe kwa madai kuwa hawajayasoma.

“Je, ni busara kwa wajumbe kujadili mapendekezo ya marekebisho haya sasa hivi wakati hatujafanya mashauriano, hatujasoma wala hatujayatafakari?” Alihoji Lissu na kuendelea; “Naomba uahirishe kikao hiki…haiwezekani kujadili mabadiliko haya bila kuyapitia Makamu Mwenyekiti.”

Mnyika Mnyika alisimama na kuunga mkono hoja ya Lissu na Jussa kwa madai mapendekezo hayo yameletwa ghafla ghafla, wakati sehemu kubwa walikuwa nayo tangu mwishoni mwa wiki iliyopita na waliyatumia kukataa marekebisho hayo huku Lissu akiyaita ni takataka.

Huku akisema kuwa mapendekezo hayo yameletwa ghafla ghafla, Mnyika alisahau na kusema kuwa mapendekezo hayo yaliwahi kuletwa kwa maana alishayaona na ndiyo yalikataliwa, sasa yameletwa tena yakiwa yameongezwa kipengele kipya cha C.

Akijadili mapendekezo ya marekebisho hayo, alitaka Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu, isipewe mamlaka zaidi ikiwemo ya kuongeza muda na kupanga sura za rasimu ya Katiba za kujadili kwa madai kuwa haina usawa wa mgawanyo wa makundi ndani ya Bunge hilo.

Pia alipinga mapendekezo hayo kumuongezea Mwenyekiti wa Kamati mamlaka ya kusimamia nidhamu ndani ya Kamati ambapo akiona kuna mjumbe analeta fujo, anaruhusiwa kuagiza mpambe wa Bunge, kumtoa mjumbe husika nje ya ukumbi na asihudhurie kikao kwa siku nzima.

Machali Machali alipopewa nafasi, aliendelea kuunga mkono kuwa mapendekezo hayo yameletwa ghafla ghafla na wamepewa dakika 15 kuyajadili, kama wanataka kuleta mabadiliko hawatapata haki hiyo. Pia alipinga mapendekezo hayo kuongeza madaraka kwa Mwenyekiti wa Kamati kumtoa nje mjumbe anayehatarisha utulivu wakati wa majadiliano, akidai kuwa baadhi ya wenyeviti wanatukana wajumbe.

“Sitarajii Mwenyekiti wa Kamati atumie lugha isiyo ya staha, halafu mjumbe akitumia atolewe nje kwa kutumia mpambe wa Bunge,” alisema Machali.

Waumbuliwa Wakati wajumbe hao wa Ukawa wakipendekeza Bunge liahirishwe jana wapate nafasi ya kujadili mapendekezo hayo ya mabadiliko ya Kanuni, ikiwezekana walete majedwali yao ya mabadiliko, mjumbe mwenzao Felix Mkosamali, alisimama na kuhoji wajumbe hao ni wapinzani wa aina gani.

Mkosamali aliyeunga mkono mapendekezo hayo kwa asilimia 100, aliwataka wapinzani wenzake waachane na tabia ya kupinga vitu vidogovidogo visivyo na msingi wowote.

“Wapinzani lazima tupinge mambo ya msingi na sio kupinga vitu vidogovidogo, huo ni upinzani wa aina gani? Mpinzani akipinga suala la kura ya wazi na kutaka kura ya siri, hilo ni suala la msingi.

“Lakini ni mpinzani gani anayepinga wajumbe kupewa muda wa kupumzika na kufanya utafiti siku ya Jumamosi kama inavyopendekezwa katika kifungu cha 14?”

Alihoji huku akipigiwa makofi. Alisema hata Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu si kamati ya vichaa kuleta hoja ya kubadili Kanuni na kuongeza muda wa kujadili sura za rasimu ya Katiba.

“Tumeona wote hapa siku mbili hazitoshi, eti mpinzani anaamka na kupinga…mnapinga vitu vidogovidogo wakati mambo ya msingi mnabadilika badilika, tusipoteze muda hapa,” alisisitiza Mkosamali.

Kauli ya Mkosamali iliungwa mkono na wajumbe wengi, akiwemo Job Ndugai, Fahmy Dovutwa na Jafo, lakini mjumbe Ezekiel Oluoch, alizidi kuwashambulia wapinzani hao huku akikubaliana na Mkosamali.

KIKWETE AWAPA WANANCHI SHAMBA LA EFATHA

0
0
RAIS Jakaya Kikwete ameagiza kurejeshwa kwa shamba la ekari takribani 12,000 kwa wananchi ambalo liliuzwa kwa taasisi ya Efatha Ministry inayoongozwa na Nabii Josephat Mwingira. Agizo hilo la Rais Kikwete limetolewa jana kupitia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana wakati akiwahutubia wakazi wa Kata ya Moro katika Kijiji cha Mawenzusi.

Wakati akiwasili kijijini hapo Kinana alipokewa na mabango yenye ujumbe unaozungumzia kilio cha wananchi kudhulumiwa shamba hilo.

Wananchi hao wakiongozwa na Mbunge wao wa Sumbawanga Mjini, Hillary Aeshi pamoja na Diwani wa Kata hiyo ya Moro, Festo Mwananjela, waliwasilisha kilio chao kuhusu unyang’anyi wa shamba hilo na taasisi hiyo ya Efatha, hali ambayo imewaacha wakazi wa eneo hilo bila kuwa na eneo lolote la kufanyia shughuli za kilimo.

Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara, Mwananjela alisema shamba hilo kabla ya kutaifishwa na Serikali lilikuwa ni maeneo ya kilimo ya wakazi wa eneo hilo, lakini baadae lilichukuliwa na Serikali kwa ajili ya kuendelezwa, hata hivyo Serikali ilishindwa kuliendeleza na kuliuza kwa taasisi hiyo.

“Cha kushangaza ni muda mrefu tangu shamba hilo kuuzwa kwa taasisi hiyo, lakini hakuna shughuli zozote zinazoendelea kwenye mashamba hayo huku wananchi wa maeneo hayo wakinyanyaswa na kupigwa pindi wanapotumia njia zilizomo ndani ya shamba hilo ambazo walikuwa wakitumia tangu awali,” alisema.

Naye Mbunge Aeshi alimuonesha Kinana, kijana Nuru Togwa aliyekatwa masikio yote mawili na walinzi waliowekwa kwenye shamba hilo wakati akipita akitoka kijijini kwake kuelekea Sumbawanga Mjini.

Kinana akizungumzia sakata hilo alisema, wananchi hao kutokurejeshewa shamba hilo na Serikali ni dhuluma na haikupaswa kuliuza shamba hilo bila kushirikisha wananchi hao.

“Serikali ilitakiwa iombe radhi wananchi baada ya kuona imeshindwa kuliendesha shamba hili, ingelirejesha kwao na si kuliuza kwa mwekezaji mmoja na kuacha watu 16,000 wakiwa hawana sehemu yoyote ya kufanyia shughuli zao kilimo, hii si haki,” alisema.

Aidha, alionya juu ya watu wanaojiita wawekezaji ambao wanakuja nchini na kuchukua maeneo makubwa ya ardhi ya wananchi kwa madai ya kuwekeza na badala yake wamekuwa wakitumia mashamba hayo kukopea na kujinufaisha wenyewe na si kufanya shughuli iliyokusudiwa.

Alisema kuna watu wengi wanaojiita wawekezaji wako maeneo mengi na si mkoani Rukwa peke yake, ambao wamejichukulia maeneo hayo kwa kigezo cha jina la uwekezaji na matokeo yake nchi imekuwa na maeneo makubwa yasiyoendelezwa huku wananchi wa maeneo husika wakitaabika kwa kukosa ardhi.

“Serikali inayaona haya lakini imekaa kimya, hii ni dhambi inayohitaji kusahihishwa haiwezekani sehemu kubwa ya mashamba asilimia 70 nchini yaliyokabidhiwa kwa wawekezaji iwe haifanyiwi lolote, kwani kama wangefanya inavyokusudiwa kwa kuendeleza shughuli za kilimo Tanzania isingekuwa na njaa,”alisema

Kinana aliwahakikishia wakazi hao kwamba Tume ya Mkoa iliyoundwa kwa ajili ya kufuatilia suala hilo mapendekezo yake ambayo ni kutaka kurejeshwa kwa shamba hilo mikononi mwa wananchi na mwekezaji huyo kupatiwa sehemu kidogo yanafanyiwa kazi.

Kabla ya kuondoka mkutanoni hapo Kinana aliwatangazia wakazi hao kwamba tayari amezungumza na Rais Kikwete ambaye ameridhia shamba hilo lirejeshwa mikononi mwa wananchi ili waendelee na shughuli zao za kilimo.

STAR WA 12 YEARS A SLAVE CHIEWETEL EJIOFOR KUWA KUBWA LA MAADUI KWENYE MOVIE YA JAMES BOND

0
0
Nyota wa filamu ya 12 Years A Slave, Chiewetel Ejiofor huenda akapata mchongo mkubwa zaidi kwa kushiriki katika filamu maarufu duniani ya James Bond.

Watu wa karibu na watayarishaji wa filamu mpya ya James Bond iliyopewa jina la ‘Bond 24’, wameuambia mtandao wa TheWrap kuwa hivi sasa watayarishaji hao wameelekeza macho yao kwa Chiwetel Ejiofor kuchukua nafasi ya mhusika anaepambana/anaempinga mhusika mkuu Daniel Craig. Kwa lugha ya uswahilini tunamuita ‘kubwa la maadui’.

Vyanzo hivyo vimeeleza kuwa mbali na kumtafuta muigizaji wa kiume, waandaaji wa Bond 24 pia wanamtafuta muigizaji wa kike mpya atakayekuwa na kazi kubwa katika filamu hiyo.

Hata hivyo, imesemekana kuwa tayari waigizaji waigizaji wawili wa kike wa Sweden Ida Engvoll na Disa Ostrand wamefanyiwa majaribio kwa ajili ya kushiriki katika filamu hiyo.

Bond 24 itakayoongozwa na Sam Mendes inatarajiwa kuanza kushutiwa August mwaka huu, na imepangwa kutoka November 6, 2015.

VIDEO MPYA:RICH MAVOKO-ROHO YANGU

0
0

Angalia Video Mpya ya wimbo wa Rich Mavoko ‘Roho Yangu’, moja kati ya hits za mwaka 2013/2014. VIDEO HII HAPA CHINI:

HALIMA KIMWANA APEWA ZA USO BAADA YA KUKOSEA KINGEREZA INSTAGRAM

0
0
Watu hata hawana huruma ..Hawachelewishi kitu ..baada ya Mwanadada halima Kimwana Ndugu yake na Diamond Kupost Picha Akiwa na Penny Mpenzi wa Diamond wa zamani na kuandika Caption ya Kingereza Kibovo (Bcz we Happy) Watu waliidaka hiyo Picha na Kuanza Kuichambua kama Karanga:


MWACHENI KAJALA APUMUE-KWANI AKITAKA KUFANYA KITU LAZIMA AOMBE RUHUSA KWA WEMA?

0
0
Mambo ya Insta...Team Ukweli na Uwazi yaaamua kuwachamba live wale wote walioponda Kajala kupiga picha na Penny pamoja na Wolper:


WADADA MIKOROGO NI NOMA...ONENI MWENZENU ALIVYO SASA

0
0
Mwee Hata siamini ...Nimekutana na hii Picha Mahali eti Wameandika ndio Maimatha Alivyo kwa sasa ...Weupe wote Ule wa Mkorogo umepotea...Kama ni Hivyo Basi Wadada Mjifunze mkorogo sio Deal ..utapendeza miaka michache tu ...Mkorogo ukisha kuchoka unarudi kuwa mweusi....

MWANAUME ATAKAYE MNUNULIA MAMA YANGU NDEGE NDIO NITAMPA ATOE BIKIRA YANGU

0
0
Muimbaji wa kike wa Nigeria, Adokiye Kyrian amesema bado ni bikira na ataendelea kuwa hivyo hadi pale atakapopata mwanaume sahihi.

Kwenye mahojiano na jarida la Vanguard, muimbaji huyo mrembo alisema: Hujawahi kuona msichana mrembo ambaye ni bikira? Mtu yeyote atakayemnunulia mama yangu ndege binafsi nimemuahidi (mama yangu) ataushika moyo wangu.”

Aliongeza kuwa haamini katika mapenzi na ana uhusiano na career yake tu. Amesema usanifu wa majengo (Architecture) ndiye mumewe muziki ndio boyfriend wake. Adokiye anaamini kuwa mapenzi ni hatari na kwamba hakuna mapenzi ya kweli. Akiwa na miaka 23 muimbaji huyo sasa ni balozi wa amani wa Umoja wa Mataifa.

MAFIKIZOLO WAUPA WIMBO WAO JINA LA KISWAHILI..VIDEO KUFANYIKA HAPA TANZANIA

0
0
Kundi la muziki la Mafikizolo kutoka Afrika Kusini ambalo lipo nchini kwajili ya show moja itakayofanyika leo Mlimani City, lina mpango wa kufanya video ya wimbo wao mpya ‘Nakupenda’ hapa Tanzania kabla ya kuondoka.

“Tungependa kufanya video ya Nakupenda hapa Dar kwani jina la wimbo ni la kiswahili na itapendeza hivyo, bado hatujapata director wa kufanya video hii ila ndio mpango wetu”waliiambia Sammisago.com

Pia Mafikizolo wamesema wamefanya mabadiliko makubwa katika muziki wao ili kukidhi haja za bara zima la Afrika.

“mabadiliko ya muziki wetu yalifanyika ili kuteka soko la bara lote la Africa na zaidi ikiwezekana ndio maana Khona na Happiness zina miondoka tofauti”. Alisema Nhlanhla Nciza

Katika hatua nyingine Mafikizolo wamethibitisha kuwa wanampango wa kufanya kazi na msanii mkubwa kutoka Tanzania atakaye tajwa hivi karibuni na collabo hii ndio chanzo cha kuboresha mahusiano mazuri na wasanii wa Tanzania.

Source:Sammisago.com

SINA BUDI KUSEMA NAWAHESHIMU SANA WANAWAKE WOTE

0
0
Rai yangu kwenu wanaume wenzangu...

Waheshimuni sana WANAWAKE. 

Nimegundua kwamba kumdharau mwanamke yoyote yule ni sawa na kumdharau mama yako mzazi kwasababu mama yako nae alikua binti wa kawaida tu kabla hajakuzaa wewe.

Vivyo hivyo huyo mwanamke unayemdharau leo will probably be mama wa FULANI in the near future.

Huyo FULANI anaweza akawa Rais wako, mchungaji wako n.k, bila kujali kwamba amezaliwa(ametoka) kwenye tumbo la mwanamke wa aina gani (malaya au anayejiheshimu). Kitanda hakizai haramu.

Nina ushuhuda...

Dada yangu amejifungua, nilikua nasikiaga tu eti "hakuna kama mama", sasa nimethibitisha.

Hakubahatika kujifungua kwa njia salama, hivyo baada ya kujifungua ameteseka sana na mshono, wakati huohuo halali usiku, mtoto akihitaji kunyonya hata kama ni usiku wa manane anaamka kwa tabu kwasababu ya maumivu makali ya mshono anayoyapata, ila anahakikisha anamnyonyesha au kumbembeleza.

Wakati mwingine mtoto akicharuka halali usiku kucha, namuonea huruma sana ila yeye kwake ni faraja kumuona mwanae kapumzika!

Imefikia kipindi namtazama mama yangu usoni bila kummaliza, kumbe alipata shida zote hizi! 

NAWAHESHIMU SANA WANAWAKE WOTE! Maneno haya yanatoka moyoni mwangu.

MSEKWA "SITTA ANA LAKE JAMBO"

0
0
Siku moja baada ya Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samwel Sitta kukiri kuchezewa kwa saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Msekwa amesema, ‘mzungumzaji huyo ana lake jambo’.

Sitta akizungumza na gazeti hili juzi mjini Dodoma alisema ni kweli kuna maneno katika hati hiyo ya sheria namba 22 ya 1964, iliyosainiwa na Nyerere na Msekwa, Aprili 25, 1964, yameongezwa.

Alifafanua kuwa saini ya Nyerere imeongezwa herufi ‘us’ kwa kompyuta na katika sehemu ya saini ya Msekwa kumeandikwa neno ‘Msekwa’ kwa kompyuta, jambo ambalo ni makosa. Sitta alisema walioongeza maneno hayo ni wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuona sehemu ya maandishi kwenye saini hizo hayasomeki, lakini walifanya makosa.

Msekwa akizungumza na gazeti hili jana alisema: “Saini iliyo katika hati original (halisi) ni ya kwangu mimi, lakini huyo anayesema zimechezewa muulizeni atakuwa na lake jambo. Kama kompyuta imekosea ni leo kwa kuwa kipindi hicho kompyuta hazikuwapo.”

Aliongeza: “Ana lengo gani la kutilia shaka, ana lengo gani la kusema imechakachuliwa, kinachotakiwa ni hati original ambayo iko ofisi ya Katibu wa Bunge itolewe, kwanini tuendelee kuandikia mate wakati wino upo?”

Maoni mengine

Mjumbe wa Bodi ya Kituo cha Taarifa kwa Wananchi Umma (TCIB), Hebron Mwakagenda alisema yote hayo yanatokea ni kuvuruga hoja iliyopo mezani.

Alisema kitendo cha kupoteza muda kuzungumzia suala la kuchezewa kwa saini halitakiwi kwani kama maudhui yake hayakuchezewa basi hoja ya muundo wa Muungano uamuliwe na wananchi wenyewe.

“Tusianze kupoteza muda kwa mambo ambayo hayapo cha msingi wananchi wenyewe waulizwe wanaupenda Muungano au la lakini tusianze kumtafuta mchawi kuwa saini zimechezewa wananchi waamue wenyewe kuhusu Muungano,” alisema Mwakagenda.

Sakata lilivyoanza

Utata huo ulianza wiki hii baada ya kamati za Bunge Maalumu la Katiba kuanza vikao vyake vya kujadili sura ya kwanza na ya sita ya Rasimu ya Katiba, zinazohusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wake.

Hali hiyo ilitokana na kutopatikana kwa hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na ile ya Sheria ya Baraza la Mapinduzi ya kuridhia Mkataba wa Muungano.
Aprili 2 mwaka huu, Kamati namba 2 ilimwalika, Spika Mstaafu wa Bunge la Muungano, Pius Msekwa kutoa ufafanuzi kuhusu hati hizo, lakini uhalali wa saini zake uliibua malumbano makali. Msekwa aliitwa kutokana na kwamba ndiye aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika wakati huo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Shamsi Vuai Nahodha, alithibitisha kutokea utata huo na kwamba walilazimika kumuita Msekwa ili kupata ufafanuzi wa masuala kadhaa na Msekwa alisema saini zilizopo katika hati hiyo ni ya kwake.

Nahodha alisema kwa maelezo ya Msekwa, inaonekana hati ya Muungano ipo Umoja wa Mataifa (UN), kwani kabla ya Muungano, Tanganyika ilikuwa na kiti chake UN na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar hali kadhalika.

Aliongeza kuwa baada ya UN kuomba uthibitisho wa Muungano, ndipo walipelekewa hati hiyo na kwamba haijawahi kurejeshwa.

Kwa upande wake Katibu wa Bunge la Katiba, Yahya Hamis Hamad alisema hati hiyo ipo Dar es Salaam na ni moja tu, hivyo siyo rahisi kuipeleka bungeni Dodoma.

SKENDO YA USAGAJI MASTAA WA KIBONGO...LINAH AFUNGUKA

0
0
MWANADADA anayekimbiza ndani ya Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ amesema anakiri kuwa usagaji upo kwa mastaa lakini yeye hajawahi kushiriki.

Linah alifunguka hilo alipokuwa akifanya mahojiani na paparazi wetu hivi karibuni akasema:
“Usagaji upo tena kwa mastaa wengi lakini kwa upande wangu mimi sijawahi kufanya hicho kitu na wala sitegemei kujihusisha nayo.”
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images