Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live

Lukuvi Afafanua Jinsi Utapeli wa Ardhi Unavyofanyika

$
0
0
Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi, ameeleza jinsi matapeli wa ardhi wanavyoshirikiana na baadhi ya maafisa ardhi hasa wa halmashauri za manispaa na jiji kutekeleza utapeli wa ardhi kwa kutumia barua bandia.

Lukuvi ameeleza hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha ‘KUMEKUCHA’ kinachorushwa na kituo cha runinga cha ITV.

“Mtu akinunua ardhi hupewa karatasi za ofa ambazo hivi sasa zilizojaa ni feki, lakini wapo wajanja na matapeli wanatumia ofa hizo kudhulumu viwanja vilivyo wazi. Mfano wakiona kiwanja kipo wazi wanakwenda katika halmashauri wanashirikiana na baadhi ya maafisa ardhi wasio waaminifu, wanauliza namba ya ploti ya kiwanja husika na anayemiliki,” alisema.

“Wakishajua namba na mmiliki wa kiwanja huiondoa ofa halali katika faili kisha afisa ardhi anaiweka feki, siku mmiliki halali akienda kuulizia kiwanja chake katika halmashauri anakuta ofa yake haipo ipo ya mtu mwingine ambaye ameghushi tarehe ya barua ya ofa,”aliongeza.

Aidha Lukuvi alisema matapeli wa ardhi huyafahamu maeneo yaliyo wazi na kwamba asilimia kubwa hushughulika na yale ambayo wamiliki wake wamefariki dunia.

“Hawa matapeli huyajua maeneo vizuri, na wanachokifanya ni kutengeneza ofa feki kisha kuziweka katika faili za halmashauri, ukienda mmiliki halali unaambiwa ni tapeli kwa kuwa barua yako haiko katika faili,” amesema na kuongeza,”Matapeli wanaishi mjini kwa kutengeneza ofa bandia, wastaafu,yatima na wajane wanalizwa kila siku,” amesema.

Ametoa agizo kwa maafisa ardhi wa kanda kutotoa huduma wala kushugulika na barua za ofa kwa sababu baadhi yao ndio wanaobadilisha ofa halali za watu.

Rais Magufuli Awasili Nchini Kenya, Ahimiza Ushirikiano zaidi kati ya Kenya na Tanzania

$
0
0
Rais wa Tanzania John Magufuli ameanza ziara yake ya kikazi katika nchi jirani ya Kenya leo ambapo kando na kufanya mazungumzo na Rais Kenyatta atazindua pia barabara.

Kwenye ziara hiyo ya siku mbili, Rais Magufuli anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake ikiwa ni pamoja na kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.

Barabara hiyo, ambayo inaunganisha maeneo mbalimbali ya jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini, ni moja kati ya miradi mbalimbali ya ujenzi wa barabara ambayo imekuwa ikitekelezwa na serikali ya Kenya kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo kuu.

Rais Magufuli akiwa nchini Kenya amewakaribisha Wakenya wote wanaotaka kufanya biashara na kuwekeza Tanzania, waje hata leo.

Waziri Kigwangalla Amesema Wanawake Wanaofanya Ngono Bila Kinga Kupata Saratani ya Mlango wa Kizazi

$
0
0
Naibu waziri wa Afya Hamisi Kigwangala amesema kuwa wanawake wanaoshiriki tendo la ndoa bila kinga wapo hatarini kupata virusi vinavyoitwa HPV vinavyosababisha Saratani ya mlango wa kizazi

Kigwangala amesema wanawake wanaofanya ngono bila kinga wanaweza kupata saratani ya mlango wa kizazi, ambapo husababishwa kwa kufanya ngono bila kinga,huambukizwa kwa kujaamiana.

Kigwangala amesema kuwa kati ya wanawake 100,000 wanawake 50.9% wanaweza kupata saratani ya Shingo ya kizazi,na kati ya hao asilimia 37.5% wanapoteza maisha hivyo serikali imeanza kutekeleza utafiti wa mradi ambao utahusisha wasichana wenye umri kati ya miaka 9-14 katika wilaya ya Moshi na utakapokamilika wataanza utoaji wa chanjo hiyo kwa nchi nzima, amewataka kutokufanya ngono mapema.

Amesema kuwa Saratani ya mlango wa kizazi haionyeshi dalili wala maumivu yeyote amesema mgonjwa anaweza akawa nao kuanzia miaka 10-15 bila kujitambua huku dalili zikiwa zinakwenda taratibu sana.

Kwa upande wake Dkt. Mathew Kasumuni kutoka hospital ya mount Meru amesema kuwa dalili za Sratani ya Mlango kizazi ni kutokwa na damu bila mpangilio, kutokwa na majimaji yenye harufu kali, amewataka wanawake watakapoziona dalili hizo wawahi hospitali mapema kabla tatizo halijawa kubwa.

Aidha Masumuni amesema kuwa unaweza kujikinga ili usipate saratani ya mlango wa kizazi kwa kupima saratani ya mlango wa kizazi mapema, kupunguza idadi ya kuzaa watoto wengi,kupunguza idadi ya wpenzi wengi, ukifanya ngono watumie kinga.

Sambamba na hayo Dkt.Mwanahamisi Lyinga amesema kuwa zipo njia kuu tatu za kupima saratani ya mlango wa kizazi mabazo ni pamoja na kutumia Darubini,Upimaji wa( DNA)wa kirusi,pamoja na Via utambuzi wa kuona kwa kutumia Siki.

Kwa upande wake Sr. Noela Lyinga ambaye ni muuguzi katika hospitali ya Mountmeru ametoa elimu kwa wanawake wawe wanajikagua matiti yao kila wanapomaliza mzunguko wao wa hedhi kila mara ili kuona kama yapo mabadiliko katika matiti yao ambayo yanaweza kuleta saratani ya matiti.

Lyinga amewataka wanawake mara wanapoona dalili yeyote ambayo siyo ya kawaida katika matiti yao wasisite wawahi hospitali mapema wakafanyiwe uchunguzi na vipimo ili kama utagundulika ugonjwa waweze kupatiwa matibabu kwa haraka zaidi.

Chanzo: Michuzi

Hamisa Mobetto Afunguka Kuhusu Tetesi za Bifu Lake na Zari Hassan

$
0
0
Hamisa Mobetto amefunguka juu ya mahusiano yake na first lady wa Madale, Zari The Bosslady baada ya tetesi za kutoka na Diamond.

Mrembo huyo amemuambia mtangazaji wa kipindi cha The Playlist cha Times FM, Omary Tambwe aka Lil Ommy kuwa hajawahi kuwa na urafiki na Zari na wala hawana uadui wowote.

“Unajua huwezi kusema kuwa mimi na Zari tuko sawa au hatupo sawa kwa sababu hatujawahi kuwa marafiki, na mimi nimemjua kwa sababu ‘Kazaa’ na bosi wangu [Diamond Platnumz],” amesema Hamisa.

Malkia huyo wa video ya Salome ameongeza kuwa amewahi kuonana na Zari mara moja pekee ambapo ilikuwa ni kwenye 40 ya Tiffah mwaka jana.

Wema Sepetu Amuandikia Ujumbe Miss Tanzania Mpya

$
0
0
Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amedai mshindi wa shindano la Miss Tanzania 2016, Diana Edward alistahili kuchukua taji hilo.

Kupitia Instagram, Wema ameandika:

When You Nailed that question Properly, I knew that The Crown was Yours…. Congratulations mdogo wangu… You deserve it… And I have a very good feeling about Your performance in the Miss World Beauty Pageant…. You will do Tanzania Proud… @dianaflave @dianaflave @dianaflave @dianaflave … #GoodMorningWorld

Faraja Nyalandu aliyewahi kushika taji hilo naye amekuwa miongoni mwa watu waliompongeza mshindi huyo

‘Makonda’ Feki Awatapeli Wachina Mil 22.8

$
0
0
Dar es Salaam. Raia wa China wametapeliwa fedha taslimu Sh 22.8 milioni wakidai kuwa sauti waliyoisikia kwenye simu ya kiganjani iliyotumiwa na tapeli ilifanana na ya  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro alisema jana ofisini kwake kuwa Oktoba Mosi, mwaka huu mfanyakazi wa Kampuni ya Group Six ambaye  ni raia wa China, Marco Li (24) alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni Makonda.

Sirro alisema tapeli huyo alimtaka raia huyo atoe Dola 3,500 za Marekani kwa ajili ya msaada wa kumsomesha mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Manilla kilichopo nchini Ufilipino.

“Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Jensen Hung (39) alikubali ombi la mkuu wa mkoa huyo feki na kumtuma msaidizi wake, Marco Li aende ofisini kwake kwa ajili ya kujiridhisha,” alisema Sirro.

Mwaka Mmoja wa Magufuli Kama Rais "Kamwe Huwezi Kuleta Mabadiliko ya Kimsingi Bila ya Kuwa na Kiwango Fulani cha Uwendawazimu"

$
0
0
Ndugu zangu,
Juzi hapa kwenye siku yake ya kuzaliwa, Rais wa Awamu ya Tano, Dr John Pombe Magufuli yumkini aliacha kula keki yake ya kusheherekea siku yake hiyo na kuamua kuwa kazini.
Zikatujia taarifa kubwa mbili; utenguzi wa uteuzi wa DCI na ziara ya kushtukiza wizara ya Maliasili na Utalii.

Nataka niwe mkweli kwa nafsi yangu, kuwa hata kama tungekuwa, kama nchi, na utaratibu wa kuwa na Rais wa kipindi cha mwaka mmoja, basi, huyu tuliye naye sasa, John Pombe Magufuli, angekuwa amemaliza muda wake wa mwaka mmoja akiwa ameacha alama nyuma yake, alama za kudumu muda mrefu.

Ukweli nchi yetu imeanza kubadilika na fikra za watu wake pia zimeanza kubadilika. Maana, ilifika mahali, kuna walioacha kazi kwenye NGO- Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kwenda kufanya kazi Serikalini ikiwamo kwenye Halmashauri zetu wakitamka wazi kuwa kwenye NGO kazi nyingi, wanarudi Serikalini na kwenye Halmashauri kupumzika na kula posho za safari na nyinginezo.
Nchi haiwezi kusonga mbele ikiwa na watu wenye mitazamo kama hiyo. Ni lazima kuwe na nidhamu ya utendaji kazi na kuheshimu sheria, kanuni na taratibu. Na wenye kukiuka hayo, ni lazima wajue kuna adhabu yenye kuendana na matendo yao maovu. Ndiyo siri kubwa ya nchi za wenzetu zilizoendelea.


Nilipata kuandika hapa, kuwa inavyoonekana; Magufuli Ana Uwezo Wa Kumwona Bata Na Sungura Kwa Wakati Mmoja..! ( Novemba 30, 2015)
Hii ni dhana kongwe ya kimtazamo iliyojengeka kifalsafa. Ni uwezo wa mwanadamu katika taswira moja kuwaona viumbe wawili wenye kufanana. Hivyo, inahusu uwezo kuliona jambo hilo hilo katika sura tofauti.

Ndio, kuna kuona kikiwa na kuona kama. Kuliangalia jambo kwa mtazamo tofauti.
Mwanafalsafa Thomas Kuhn yeye anazungumzia dhana ya ' Paradigm Shift'. Ni ile hali ya uwepo wa mapinduzi ya kifikra na ya kisayansi yenye kupelekea mabadiliko ya kimsingi katika jambo lile lile tulilokuwa na mazoea nalo.

Captain Thomas Sankara, kiongozi mwanapinduzi aliyeuawa wa Burkina Faso, katika wakati wake, alizungumzia umuhimu wa kuwa na ujasiri wa kuyapa mgongo mazoea ya kale.
Sankara aliacha hiba njema ya kuenziwa ndani ya nchi yake, Afrika na duniani. Mwanamapinduzi huyu alikuja kuawa kwa kupigwa risasi na wapinga mapinduzi na maendeleo ya Burkina Faso.
Sankara alipata kukaririwa akisema: “Ningependa kuacha nyuma yangu, imani ya kuwa, kama tunaimarisha kiwango fulani cha uangalifu na oganaizesheni, basi, tunastahili ushindi.

Kamwe huwezi kuleta mabadiliko ya kimsingi bila ya kuwa na kiwango fulani cha uwendawazimu. Hali hii inatokana na kutoshinikizwa na taratibu zilizozoeleka, kuwa na ujasiri wa kuzipa mgongo kanuni za kizamani, ujasiri wa kuanzisha mustakabali. Ni wendawazimu wa jana waliotuwezesha kuyafanya tuyafanyao leo. Ninataka kuwa mmoja wa wendawazimu hao.” (Hayati, Kapteni Thomas Sankara)

Yumkini tunachokishuhudia kwenye nchi yetu ni Magufuli's paradigm shift'. Hali ya kuwa na mabadiliko ya msingi.
Na hii ya Magufuli paradigm shift inaweza kuibadili nchi kwa haraka, maana kila mmoja atalazimika kubadilika.
Maggid,
Iringa

Mr Blue Asema Hahitaji Meneja Kwenye Muziki Wake

$
0
0
Msanii wa muziki wa kurap, Mr Blue amesema hahitaji kuwa na meneja wa kumsaidia katika kazi zake za muziki kwa kuwa tayari alishawahi kuwa na mameneja zaidi ya watatu ambao hawakumpatia mafanikio.
f1cbmr-Blue-ft-alikiba-mboga-saba

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mboga Sana’ amesema alikuwa hawezi kuishi kwenye tasnia ya muziki bila kuwa na meneja lakini kutokana na kuona mchango wao kwake haukuzaa matunda.

“Mimi nilikuwa siwezi kuendesha maisha yangu ya muziki bila kuwa na meneja na nilifanya kazi chini ya mameneja watatu lakini kwa sasa nimesema basi sihitaji meneja tena nahitaji ushauri wa wadau namna ya kuboresha kazi zangu,” Mr Blue alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.

Rapa huyo pamoja na AliKiba wameshiriki kusapoti ngoma ya Abby Skills inayokwenda kwa jina la Averina , ambapo Abby amewataka mashabiki kumuunga mkono ili arejee vyema kwenye game kama zamani.

Magufuli: Huwa Nawasiliana na Rais Kenyatta, Hatuna Bifu Kama Watu Wanavyozani

$
0
0
Baada ya mwaka mzima tangu kuchaguliwa, rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kwanza ya kiserikali nchini Kenya.

Kulikuwepo uvumi kuwa huenda kuna tofauti kali ya rais huyo na mwenzake wa Kenya hasa baada ya rais Magufuli kukosa kuhudhuria mkutano mkuu wa kibiashara ulioandaliwa jijini Nairobi.
Ziara hiyo ya siku mbili inanuiwa kudhihirisha nia safi kati ya Kenya na Tanzania pamoja na kuimarisha biashara.

Mkenya Aibuka Mshindi wa Maisha Plus

$
0
0
Olivie Kiarie wa Kenya ameibuka mshindi wa shindano la Maisha Plus. Fainali za shindano hilo zilifanyika mwishoni mwa wiki.

Ushindi huo umempa Olive kitita cha shilingi milioni 30 za Kitanzania.

Shindano la Maisha Plus lilishirikisha nchi za Afrika Mashariki.

Taarifa Kutoka Ikulu: Rais Magufuli na Rais Kenyatta Wazindua Barabara ya Southern By-pass

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta leo tarehe 01 Novemba, 2016 wamezindua barabara ya Southern By-pass iliyojengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi nchini Kenya.

Sherehe ya uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 28 na inayounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi imefanyika katika eneo la Karen nje kidogo ya Jiji la Nairobi.

Akizungumza katika sherehe hiyo Rais Magufuli amempongeza Rais Kenyatta na Serikali yake kwa kujenga barabara hiyo ambayo sio tu itawasaidia wananchi wa Kenya bali pia itawasaidia wananchi wa Afrika Mashariki wanaotumia barabara zinazopitia Nairobi.

Rais Magufuli pia ameishukuru Serikali ya China kupitia benki yake ya Exim ambayo imetoa mkopo wa kujenga barabara hiyo, kwa kuendelea kuziamini nchi za Afrika Mashariki na kuzikopesha mikopo inayosaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara.

“Wananchi wanahitaji maendeleo na haya ndio maendeleo, barabara hii itasaidia kuinua uchumi na itasaidia masuala ya kijamii” amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amesema viongozi wa Afrika Mashariki wameamua kufanya kazi ya kuharakisha maendeleo na kuinua maisha ya wananchi, na kwamba ili kufanikisha hilo wamedhamiria kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara zinazounganisha nchi wanachama na kujenga vituo vya pamoja vya utoaji wa huduma za mpakani (One Stop Border Post).

Kwa upande wake Rais Kenyatta amesema kujengwa kwa barabara hiyo kumesaidia kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi na pia kutaboresha shughuli za maendeleo ya wananchi.

Mhe. Kenyatta amemshukuru Rais Magufuli kwa kuungana nae kuzindua barabara hiyo na amesema Kenya itaongeza juhudi katika utekelezaji mradi wa ujenzi wa barabara zinazounganisha Kenya na Tanzania zikiwemo barabara ya Malindi kupitia Saadani hadi Bagamoyo nchini Tanzania na barabara ya Voi – Taveta- Horiri-Arusha.

Sherehe za uzinduzi wa barabara ya Southern By-pass zimehudhuriwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe. William Ruto.

Kabla ya kuzindua barabara hiyo Rais Magufuli ametembelea kiwanda kidogo cha kusindika maziwa cha Eldoville kilichopo katika eneo la Karen ambacho kinamilikiwa na familia ya mkulima Bw. James Karuga.

Familia hiyo ilianzisha kiwanda cha kusindika maziwa mwaka 1985 kwa uzalishaji wa chini ya lita 1,000 kwa siku na hivi sasa imefikia uzalishaji wa lita 5,000 kwa siku na inatarajia kuongeza uzalishaji hadi lita 70,000 katika mwaka mmoja ujao baada ya kuongeza kiwanda cha pili.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Nairobi
01 Novemba, 2016

Serikali Yahakiki Vyeti vya Ndoa, Walimu Wajiandaa Kugoma

$
0
0
Gazeti la Tanzania Daima limeripoti kuwa Serikali imeanza uhakiki wa vyeti vya ndoa kwa watumishi wa umma. Hatua hiyo ambayo imewashtua watumishi wengi wa umma, imeelezwa kuwa ni mwendelezo wa harakati za Serikali ya Rais John Magufuli kuhakiki watumishi wa umma ili kuondokana na watumishi hewa.

Wakati Serikali ikianza na uhakiki wa vyeti vya ndoa, kazi ya uhakiki wa watumishi hewa na vyeti vyao vya elimu inaendelea sehemu mbalimbali nchini.

Kwa muhibu wa Gazeti hilo, habari ambazo limezipata zinasema kuwa serikali imeanzisha uhakiki huo nchi nzima kwa madai kuwa baadhi ya watumishi wa umma wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kwamba wana ndoa ili kupata nauli na stahiki zingine za likizo wakati hawana ndoa.

Habari zaidi zinasema kuwa walimu wakuu wa shule zote za Wilaya ya Ilala wamepewa siku mbili kutekeleza agizo hilo kwa walimu wao.

Mmoja wa walimu hao ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe, alilithibitishia Tanzania  daima kuwa ametoa siku mbili kwa walimu wa shule yake wenye vyeti vya ndoa waviwasilishe kwake.

"Kweli tumepewa agizo hilo leo manispaa ya Ilala na tumetakiwa kuwasilisha vyeti hivyo kesho na tayari baadhi ya walimu wangu wamefanya hivyo leo na kesho zoezi hilo linakamilika"

Alipoulizwa sababu ya kuwepo kwa zoezi hilo, mwalimu huyo alisema hajui lakini anahisi lina lengo la kudhibiti taarifa za uongo za watumishi wakati wa kuomba likizo.

Wakati walimu wa shule za Ilala wakitakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ndoa, wilaya nyingine za Temeke, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni hawana taarifa hizo.

Mmoja wa walimu kutoka Manispaa ya Ilala alisema kuwa uhakiki huo una lengo la kutaka kuchelewesha zaidi malipo na stahiki za walimu za likizo ambazo hazijalipwa kwa miaka mingi.

Barua ya Tupac Kuuzwa Shilingi Milioni 378

$
0
0
Ni miaka 20 tangu afariki rapper mkongwe, Tupac. Na sasa barua ambayo aliiandika, mwenyewe inatarajiwa kuuzwa kwa kiasi cha $172,750 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 378 za kibongo.

Kampuni ya Goldin Auctions, imesema barua hiyo iliyondikwa na Tupac Shakur ni moja ya vitu kumi vilivyokuwa vikimilikiwa na rapper huyo ambavyo vyote vitauzwa kwa mtonyo wa $206,625.

Linah Adai Amejaribu Kumweka Sawa Recho Lakini Ameshindwa

$
0
0
Msanii wa muziki Linah Sanga amedai kuwa amejaribu kuzungumza na msanii mwenzake Recho ili kumrudisha kwenye nafasi yake lakini ameshindwa.
Linah na Recho

Akiongea katika kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV wiki hii, Linah amesema tayari ameshamfuata Recho mara kadhaa ili amweleze kinachomsibu lakini amekuwa msiri.

“Sisi wasanii tulilelewa kwa kushirikiana kwa kila hali na tulipenda kwa sababu kuna wakati tunaishi pamoja, tunatungiana nyimbo,” alisema Linah “Kwahiyo kwa upande wangu mimi na niseme ukweli namfutilia sana Recho, shoga yangu vipi? Mbona kimya, fanya hivi lakini huwezi kujua kwanini yupo vile na kwanini anashindwa kubadilika,”

Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo ‘Upepo’ amekuwa kimya kwa muda mrefu bila kuweka wazi kitu kinachomsibu.

Wema Sepetu Atangaza Kupumzika Instagram Kwa Muda...Maneno Maneno Yamkimbiza

$
0
0
Maskini Watu wanaingilia life ya Wema Sepetu mpaka ametangaza kujitoa Insta kwa muda....Chaaa!!!! Waliokuwa Marafiki zake na Timu Wema hali si shwari, Munalove na Hope wanashutumiana kumsengenya Wema na kumuendea kwa mganga....
Toa maoni yako kwake kuhusu wanaomuingilia life yake

Majibu ya Jux Alipoulizwa Kama ana Mpango wa Kumuoa Vanessa au Kuzaa Nae

$
0
0
Msanii Jux amejibu kuwa hajui kama atakuwa na mtoto na Vanessa wala hajui kama atamuoa, ila amesema Vanessa amemsaidia kwenye maisha yake kwa kuwa kuna vitu anavijua na yeye havijui Msikie Hapa:

Unamshauri Nini Diamond Katika Ngoma yake na Rich Mavoko Inayokuja?

$
0
0
Aisee kwanza huyu jamaa anastahili Hongera nyingi sana, Huyu ni identity ya taifa kwa sasa within and outside of Africa.

Huyu jamaa pia ana busara na moyo wa kiume sio wa kulialia, juzi alipokosa award ktk MTV awards aliwapa moyo wasanii wenzake wa kitanzania katika ujumbe aliouandika instagram kutokata tamaa kwani watazichukua tu.

Ingawa atakuwa busy sana mpaka mwakani ila Salam amesema kuwa Diamond bado anatoa nafasi kwa watanzania kumshauri afanye nini ili kuboresha mara dufu nyimbo zake hususan videos.

Katika kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), Diamond Platnumz ameishaimba na

Harmonize wimbo wa BADO

Rayvanny wimbo wa SALOME

wimbo utakaofuata ataimba na Rich Mavoko (pacha wake kisauti)

Unamshauri nini SIMBA?

Mimi namshauri kwanza katika video yake asimtumie Mwanamke wa kizungu as his Video Queen.

Kuna mabinti wa kiafrika hasa wa kitanzania wazuri sana tu na inapendeza akiwatumia hao na sio wazungu.

Toa ushauri wako wa kuboresha kazi ya Platnumz.

Tausi Mdegela: Watoto wakiniona wanatafuta vitenesi tucheze

$
0
0
Mwigizaji wa bongo muvi kwa upande wa komedi Tausi Mdegela amesema, mara nyingi akiwa sehem za matembezi, watoto wengi wanamkimbilia na wengine kutafuta vitenesi ili wacheze wakidhani supastaa huyo ni mtoto mwenzao.

Watoto wengine wanakuwa wanawasumbua wazazi wao(mama zao) wawanunulie nguo kama alizovaa Tausi. Tausi amesema anapenda sana watoto na muda si mrefu anategemea kufunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu japokuwa hakusema ni lini. Ameongezea pia mchumba ambae anatarajia kufunga nae ndoa ana kimo kirefu mwenye kuweza kuzima taa wanapokuwa chumbani. Muigizaji Tausi ameongea haya wakati anahojiwa na Dina Marios katika kipindi cha uhondo E fm radio.

Wema Sepetu Amehairisha Kuondoka Instagram Adai 'Toka Lini Mwenye Nyumba Akaacha Nyumba Yake'

$
0
0
Wema Sepetu Haendi Mahali soma hapa akimwaga povuuuu!!!! Ameandika Haya Kwenye Ukurasa wake wa Instagram baada ya mwanzo kudai ameamua kupumzika Instagram:

Wemasepetu
Life has got to Go on.... Nimepitia makubwa zaidi and this is Not something to Bring Me Down kabisa... Siwezi Kalfisha nafsi yangu kwa watu wasio na worth kwangu... Yes U got me for a Minute But Hey I know how to Bounce Back... I aint goin no where... The Love I recieve from people around me is too strong.... Never will I shed another tear for stupidity... Kama maneno ni sumu basi nadhani ningekuwa nishakufa zamani... So talk the talk... And I'll walk the walk... #TokaLiniMwenyeNyumbaAkaachaNyumbaYake... 

Kujitibu Vipele vya Chunusi Kwenye Uso Kwa Njia za Asili Tiba Mbadala

$
0
0
Kuna  idadi  kubwa  ya  watu   wanao  kabiliwa na  tatizo  la   vipele vya  usoni

(  Chunusi  ). Kuwa  na  chunusi  ni  jambo lenye  karaha  sana,  kwani  linakufanya upoteze  mvuto  wako  wa  asili  na  hivyo kukukosesha  raha.

Zipo  njia mbalimbali   za  asili  zinazo  weza kutumika  kutibu  tatizo  la  chunusi  na  vipele vya  usoni.

 Ifuatayo  ni  miongoni  mwa  njia   bora kabisa  na  ya  uhakika  itakayo  kusaidia kuondokana  na  tatizo  la   Chunusi  au  vipele kwenye  uso.


Komamanga: Maganda  Ya   Mkomamanga  yaliyosagwa, yakichanganywa  na  habbat  sodah  ya unga, hutengeneza  dawa  nzuri  ya  asili  ya  kuondoa  tatizo  la  vipele  vya  usoni  (  chunusi  )


Habbat Soda : Hii  ni Habbat Sodah Ya Mbegumbegu. Habbat  Sodah  iliyosagwa  ndio  inayo hitajika katika kutengeneza   dawa  ya asili  ya  kuondoa  tatizo  la  vipele  vya  usoni  ama chunusi.

MAHITAJI :
Habbat  Sawdah  ya  Unga  iliyo sagwa.
Nusu  kikombe  ya  maganda  ya komamanga  yaliyo  sagwa.
Nusu  kikombe  ya  siki  ya tofaha(apple )

MATAYARISHO   NA MATUMIZI 
Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu)
kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple).

Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila  siku  usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubarid.

NJIA HII IMETUMIWA NA WATU WENGI NA IMEWASAIDIA SANA. JARIBU NA WEWE KUTUMIA NJIA HII UONE MAFANIKIO YAKE.
Kwa  habari  na  taarifa  mbalimbali  kuhusu masuala  ya  tiba zitokanazo  na  dawa  za mimea  na  vyakula lishe
Viewing all 104712 articles
Browse latest View live




Latest Images