Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Mke wangu Ananiambia Anatongozwa Sana, Nifanyeje?

$
0
0
Mke wangu amenishangaza sana baada ya kuniambia kuwa akiwa kazini au mizunguko huko mtaani kuwa anatongozwa sana na wanaume mbali mbali lakini eti anawakataa wote....

Maswali yangu
Wataalam wa mambo hivi Inapofikia hatua mke wako wandoa anakwambia hivyo ina maana gani?
Hivi Kweli Mwanamke anaweza kwa siku atongozwe na wanaume watano na kuwakataa wote?


Mapenzi Sio Kujifungia Chumbani tu na Kufanya Ngono

$
0
0
Mapenzi ni ubunifu, unaweza ukaona kitu kidogo lakini kitu hiko ukikifanya kwa mlango wa mapenzi kinakuwa kikubwa na hakiwezi kusahaulika kirahisi kwa mwenza wako. ukizungumzia mapenzi watu weusi wengi tunajua mapenzi ni kujifungia chumbani na kutiana tu, hapa ndo wazungu wanapotupiga bonge la gepu pale wakiwakamata dada zetu.

Basi ili kufanya mapenzi yako yaonekane mapya kila siku si lazima kila siku mjifungie chumbani kufanya staili mpya au sio lazima kila siku mtoke kwenda kula dina sehemu nzuri.

Unaweza ukamchukua mpenzi wako ukaenda nae sehemu ilio tulivu kisha mkaanza kusoma vitabu(hii inategemea na nyie wawili mnapendelea vitabu vya aina gani ila sio vya kemia au physics

Inapendeza sana mkiwa mmekaa pamoja mkisoma vitabu, mkabadilishana mawazo kwa kile kilichoandikwa kwenye kitabu. inaweza mkaenda beach(tulivu) au sehem ambayo unahisi mtakaa mtatulia bila usumbufu, mkasoma vitabu vyenu taratiiibu.

Wema Sepetu Atoboa Siri...Adai Maadui zake Wana Skendo Ambayo Magufuli Apendi

$
0
0
Wema na Muna ndani ya Bifu zito..soma Hapa Alichoandika Wema Sepetu

BY@wemasepetu - Yes I got Guts to post my Dogs... And I love them to the Core... ila panic zisije kuwapeleka jela... Maana sijui mtawatishia amani wangapi... Tunapoelekea Polisi watawahusu na hivi mna kaskendo ambacho Magufuli hakapendi...😷😷😷... Oooops nisimwage mchele.... Sema Gucci (Bucci) wangu anapenda sana kukunwa... But Vanilla gets sooo jealous...


Rose Ndauka Atetea Kuvunjika Kwa Ndoa Yake...Adai ni Tatizo la Jamiii

$
0
0
Malkia wa filamu Rose Ndauka amewataka watanzania kujua kuvunjika kwa ndoa sio tatizo la wasanii wa filamu pekee bali ni tatizo la jamii nzima.

Mwigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae, Naveen amesema kwa sasa yeye bado yupo yupo kuingia kwenye maisha ya ndoa.

“Ndoa ni makubaliano ya watu wawili, mimi bado nipo nipo kidogo,” Rose alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM “Tusiwatazame tu bongo movie hata kwenye jamii ya watu wa kawaida ndoa hazidumu zinavunjika,”

Mwigizaji huyo mwaka uliopita aliachana na mpenzi wake aliyezaa naye mtoto mmoja mwenzi mmoja kabla ya tarehe waliotangaza kufunga ndoa.

Faiza Ally Akerwa na Wanaomtukana Wema Sepetu Kuhusu Kutopata Mtoto

$
0
0

Faiza akerwa na wanaomtukana Wema Sepetu...

Jisomee.......

Faizaally_
" Hakuna kitu huwa kinanikera Kama watu wanao mtukana Wema kuhusu mtoto ...nachukia sipendi .... Hivi nyinyi mlio zaa mnajua mme zaa kinani ? Kwa nn msikae mka wao mbea watoto wenu mema badala ya kumkashifu mtu ambae hajazaa? Unajua bora kutokuzaa kuliko wewe usie jua umemzaa nani? Vipi Kama umezaa jambazi,shoga Au toto lolote tu lisilo kuwa Na faida yoyote ? Hebu kaeni muombee vizazi vyenu Maana hamjui mlivyo zaa vitakua kinanani huenda bora haya huyo Wema ambae hajazaa,by the way Wema Bado mdogo sana ...ktk umri Kama w Wema hata mm nilikua sijazaa sijui hata kinacho wafanya mumkatie tamaa Wema .... INSHAALLAH KWA UWEZO WA ALLAH IKO SIKU WEMA ATAZAA TENA SIO KUZAA TU NA ATAZAA MTOTO MWENYE FAIDA.... wapumbavu wote mnao weka picha za watoto Na kumuweka Wema Na mbwa ... Sio bure lzm mna laana Maana hamuogopi hata Mungu...lol kutwa kumsakama mtoto wa watu ....? Haya nyinyi mlio zaa mnakataba Na Mungu hao watoto wenu wataishi ? MUOGOPENI MUNGU WATU WAMEZAA NA WATOTO WAMEKUFA WAMEBAKI WAGUMBA .... 😞 Mungu anawaona ! Kila binaadamu Ana mapungufu usitumie mapungufu ya mwenzio kumkera kutwa"

Kwa Upuuzi Huu Nitaendelea Kuwasifu Mahausigeli Wanaovunja Ndoa za Watu!

$
0
0
Kila siku na kila mahala ukipita au ukibahatika tu kukutana na akina Dada na akina Mama waliopo katika Ndoa au hata Mahusiano tu ' lawama ' zao kubwa ni kwa hawa Dada zetu wa Kazi nyumbani maarufu kama ' mabeki tatu ' kuwa wanashiriki kwa kiasi kikubwa sana katika kuwaharibia ' mahusiano ' yao kwa ' kubanduana ' na Wapendwa wao hasa Wachumba au Waume zao.

Kinachonisikitisha na hata kunishangaza pia ni Kitendo cha hawa hawa Dada / Mama zetu wao kuelekeza tu ' lawama ' zao kwa ' mahausigeli ' pasipo hata wao wenyewe ' kujitathmini ' ni wapi huwa wanakosea kwani ' kimantiki ' haiwezekani Mahusiano yao au Ndoa zao ziharibiwe bila sababu ' maalum '.

Katika chunguza chunguza yangu ya ' kutukuka ' kabisa ya kutaka kujua labda ' tatizo ' ni nini niliamua kulifuatilia ' kiumakini ' mno hili jambo na nikagundua mambo kadhaa ya ' kipuuzi ' ambayo Dada zetu walio katika Mahusiano au Mama zetu walio katika Ndoa zao huyafanya ambayo kwa kiasi kikubwa Mimi binafsi nawasapoti 100% ' mahausigeli ' kwani wanatumia ' upopoma wa kutukuka ' unaofanywa na hawa wenye Wachumba / Waume zao.

Mambo yenyewe ya ' kipuuzi ' ni kama yafuatayo:
Mama  anaenda kuajiri ' hausigeli ' mzuri kuliko hata yeye tena kwa kila kitu.
Mama  anaruhusu ' ukaribu ' wa ' kupitiliza ' wa Baba / Mchumba na ' Hausigeli '.
Mama  anamruhusu ' Hausigeli ' kuvaa ' vimini ' mbele ya Baba / Mchumba.
Mama  anaruhusu ' Hausigeli ' amfulie ' Nguo ' Baba / Mchumba.
Mama  anaruhusu ' Hausigeli ' awe na mazoea ya kuingia ' Master Bedroom '.
Mama  anaruhusu ' Hausigeli ' aandae ' Chakula ' cha Baba / Mchumba huku yeye akiwa ' busy ' anatizama ' Isidingo ' na ' akitiririka ' na WhatsApp.

Mama anajifanya kuiga mambo ya ' kizungu ' kwa kuonyesha ' manjonjo ' yake ya ' Kimahaba ' tena mbele ya ' Hausigeli ' kitu ambacho huwafanya ' Mahausigeli ' wengi kuweza kuangalia ' udhaifu ' wao na pale Wao wakija ' kutongozwa ' tu akina Baba / Wachumba huwa hawakatai na ikifika wakati wa ' kubanduana ' huyu ' Hausigeli ' atamfanyia Baba / Mchumba ' manjonjo ' yake yote hivyo kumfanya kuonekana bora zaidi na hapo ndipo mwisho wa ' mahaba niue ' kwa akina Dada / Mama na kubaki kulaumu tu na kulia lia.

Wadada wa Kazi wote nchini Tanzania ' ninawasifu ' sana na nawaombeni endeleeni hivyo hivyo kuzitumia ' fursa ' hadi hawa akina Dada na Mama ' wakome ' na ' wanyooke ' kwa ' kuziharibu ' Ndoa zao / Mahusiano yao.

GENTAMYCINE

Wanaojichubua Wana Matatizo ya Kisaikolojia

$
0
0
WATU wanaopenda kujibadilisha miili na ngozi zao kwa kutumia vipodozi vyenye kemikali za kujichubua na kubadilisha mwonekano wa sehemu za maumbile yao wametajwa kuwa miongoni mwa watu wanaosumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia.

Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Profesa Penina Mlama alisema wanawake na wanaume ambao wanatumia vipodozi hivyo wana matatizo ya kujiamini, hivyo huchukua uamuzi wa kujibadilisha.

Aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa kati ya Shirika la Codersia na Majumuhi (Pan African) ya Kigoda cha Mwalimu Nyerere wa kujadili mabadiliko ya mwili ambayo yamekuwa yakifanywa na watu mbalimbali.

Alisema watu wamekuwa wakifanya mabadiliko kwa kujichubua, kujichora mwilini (tattoos), kuongeza maumbile bila kujua kuwa kuna madhara makubwa ya kufanya hivyo.

“Mabadiliko haya yana madhara makubwa kiafya na kijamii…wengi wanaojibadilisha hawajiamini na wana matatizo ya kisaikolojia, mabadiliko haya yana gharama kubwa sana, lakini hata baada ya kupata madhara pia ni gharama,” alisema Profesa Mlama na kuongeza kuwa, katika mkutano huo wataangalia kiini cha kujibadilisha, huku akiainisha kuwa baadhi ya watu wanaojibadilisha wanafanya hivyo kutokana na msukumo katika jamii na kutaka wafanane na watu wengine.

Msomi huyo alisema kwa hapa nchini, tatizo kubwa la kujichubua lipo kwa wanaume na wanawake na baada ya mkutano huo wataangalia zaidi eneo lingine lililoathirika zaidi.

“Tutafanya utafiti kwa nini watu wanaongezeka kwenye madhara ambayo ni gharama, kwa nini wanafanya hivyo na kama wana elimu ya kutosha juu ya wanachokifanya,” alisema.

Naye Katibu Mtendaji wa Codesria, Ebrima Sall alisema, pamoja na kwamba watu wanaofanya hivyo wana matatizo ya kisaikolojia, lakini pia wataangalia namna ya kuzishauri serikali namna ya kudhibiti matumizi ya vipodozi hivyo.

Alisema watajaribu kuangalia namna ya kushauri watunga sera, serikali na vyombo vinavyohusika na biashara namna ya kuzuia vipodozi hivyo, kwa kuwa vimekuwa vikihusika katika kutoa vibali vya kuingizwa kwake.

Sall alisema suala la watu kujibadilisha miili yao limekuwa tatizo kubwa duniani, huku akieleza kuwa kwa Afrika hilo linakuwa ni jambo la kushangaza kwa sababu wanawake na wanaume wamekuwa wakiacha utamaduni wa Kiafrika.

Diamond Afunguka Kuhusu Ukimya wa Rich Mavoko

$
0
0
Msanii Diamond Platnumz amefunguka na kusema kuwa ukimya wa Rich Mavoko unatokana na msanii huyo kujipanga na kazi zake mwenyewe na kudai mpaka sasa amefanya kazi nyingi na kali sana.


Diamond Platnumz alisema hayo hivi karibuni kupitia kipindi cha Friday Night Live na kusema kuwa Rich Mavoko amefanya kazi nyingi lakini yeye mwenyewe anaziweka pembeni na kutaka kufanya kazi kali zaidi.

"Mimi mwenyewe nimefanya nyimbo nafikiri mbili na Richard na muda wowote zinaweza kutoka, sema Richard ni mtu fulani ambaye anajipanga hivyo kipindi hiki anajipanga akianza kufumuka na mabomu yake ni hatari, maana anajipanga kila wimbo akirekodi anakwambia hii bado, akirekodi nyingine tena anakwambia hii bado yaani naweza kusema Richard ni msanii ambaye ana nyimbo nyingi sana kali. Kuna wimbo pale unaitwa 'Sijaona' WCB nzima  wanaikubali lakini yeye anakwambia hii bado, ila akisema hivyo akileta ngoma nyingine inakuwa kali zaidi. Kwa hiyo ni mtu ambaye Mwenyezi Mungu kamjalia kipaji na mwenyewe anakuaga hana papara" alisema Diamond Platnumz

Bifu la Wema Sepetu na Muna Lafika Pabaya...Wema Amshutumu Muna Kumfanya Mama yake Ndondocho

$
0
0
Wema na Munalove Bifu zito ameandika haya:

From @wemasepetu
Rose Alphonce Nungu... Nakuita tena kwa mara ya pili Rose Alphonce Nungu.... Unanitafutia nini wewe mwanamke...!? Nini nimekukosea wewe dada...? Niliapa na Miungu yote siwezi kupost kitu chochote kwa account yangu kinachokuhusu wewe ila wallahy wewe dada You are pushing my buttons... Tena una push buttons zangu kikweli kweli cuz nimekaa kimya na yako mengi.... Usijisahaulishe leo nimekuja kwako na ukalia mno kutaka vitu visitoke kwenye mitandao... Sasa nakwambiaje Rose, mimi sitovitoa mitandaoni cuz im nat dat illiterate kama wewe... But nataka kukuuliza kitu, kwanini unamfanya mama angu kama ndondocha wako...? Let me tell u one thing, Rose, I have been in the industry kwa miaka 10, Never have I taken my mum kwenye sehemu za starehe tena usiku wa manane... Ntamuita mama angu pale ninapojua kuwa uwepo wa mam unahitajika kwenye hafla hii... Umekuja ukaamua kujiweka karibu na mama angu kiasi cha kwamba mimi tena nikawa sio shoga ako bali mama angu ndo ukamtawala.... Ulikuwa una yako... Leo hii umeweza kumteka mama angu kiasi cha kwamba unamfanya ajione yuko age sawa na wewe... Mama angu ni wa kwenda mango garden jamani? sijawahi... Mama angu ni wa kukaa mpaka usiku wa manane kwenye wanja za starehe? Sijawahi.. Mama angu leo hii ni wa kumlisha maneno ya uongo na kweli akaonekana mbele ya binaadam ananikana mtoto wake wa kumzaa...? Muna ulichomfanya mama angu Mungu ndo anajua na ipo siku isio na jina basi atakuadhirisha ila kaa ukitambua watoto wake wote hatupendi... So back to topic ya leo, umeona uendeleze ushenzi wako kwa kuanza kutunga uongo kwa watu wangu wa karibu... kama ulivyotangaza kwenye magroup yako kuwa unanipa mabwana... Hivi Rose, mimi leo hii wewe unitaftie bwana kwakuwa wewe hutaki mabwana wa maana... Honey mimi sitafutiwagwi bwana... Mabwana wananitongoza wenyewe na mara nyingi nakuwa na mtu ninaempenda sio niliotafutiwa... Mimi sio mtoto mdogo... Sasa naona umeanza na @junaithar kesho na kesho kutwa usiwasahau @directorjoan na @sweetlorah ... Afadhali hawa dada zangu naweza kuwapostia hata biashara zao na wakanilipa ... Niambie nini umefanya kwangu wewe.. Umenidhulumu vingapi nimekaa kimya..niseme?

Kampuni ya Black Fox iliyokuwa ikifanya Kazi na Juliana Isawafo Aliyekutwa Ameuwawa Arusha Yafunguka

$
0
0
Wiki hii katika mitandao ya kijamii kuna picha ambazo zimesambaa zikiuonesha mwili wa msichana anaesadikika kuwa amekufa baada ya kubakwa na watu ambao hawajajulikana na kutupwa nje ya eneo la Chuo Kikuu cha Tumaini (Makumira Arusha).


Mwili wa msichana huyo ambaye jina lake halisi linadaiwa kuwa ni Juliana Isawafo, ulikutwa katika bonde la mpunga jirani na chuo hicho majira ya saa 5 asubuhi siku ya Jumatano.

Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho, (jina lake halikufahamika mara moja) ameuthibitishia mtandao wa Radio5 Arusha kutokea kwa tukio hilo.

Bongo5 ilimtafuta Mkurugenzi wa kampuni ya Black Fox, kampuni ambayo ilikuwa inafanya kazi na model huyo hapa jijini Dar es salaam.

“Juliana sisi tunamjua kama model wa Black Fox na mimi ni managing director,” alisema Mkurugenzi huyo. “Alikuwa ni model lakini pia alikuwa ni dansa Arusha, sisi kuna mtu alitupigia simu akatuambia kuna mtu wenu amefariki, tukawapigia simu ndugu zake kuthibisha tukaambiwa ni kweli. Kwahiyo sisi kama sisi tufanya mkutano ili tupeleke rambirambi kwa ndugu,”

Pia mkurungenzi huyo alisema issue za model huyo kubakwa azitakuja kufafanuliwa na jeshi la polisi likikamilisha upelelezi wake.

“Kwa sasa hivi jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi lakini tunachojua mwili wake umeokotwa jana asubuhi na watu wanadai amekutwa katika hali ambayo anaweza akawa amebakwa. Lakini mimi nadhani vitu kama vivyo tuliachie jeshi la polisi litakuwa na taarifa rasmi kwa sababu wao watajua nini kilitokea.

Pia mkurugenzi huyo alisema watatoa taarifa zaidi ya nini kinaendelea pamoja na kutangaza nini wameandaa kwa ajili ya kuwapa pole wafiwa.

Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo amesema Juliana hakuwahi kufanya kazi na Diamond kama baadhi ya watu wanavyozungumza katika mitandao.

Katika mitandao ya kijamii Alhamisi hii kulizuka uvumi usio wa kweli kuwa model huyo aliyefariki ni yule aliyeonekana katika video ya wimbo Salome wa Diamond Platnumz.

Kwa upande Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema tukio hilo lilitokea jana saa 11:30 asubuhi eneo la Makumira.

Alisema taarifa za awali zinaeleza kuwa Novemba 1 mwaka huu muda wa saa 18:30 jioni marehemu aliondoka nyumbani kwake kwenda kwenye sherehe ya kuzaliwa “Birthday Party” ya rafiki yake ambayo ilipangwa kufanyika kwenye baa iitwayo V. I. C iliyopo eneo la Kilala lakini hakuonekana katika sherehe hiyo.

Siku ya pili Novemba 2, polisi walipata taarifa juu ya kuwepo kwa mwili ambao umekutwa kando ya barabara ya kuelekea Ndolo Lodge, baada ya askari kufika eneo hilo walikuta mwili huo ukiwa mtupu na pembeni yake kulikuwa na nguo zake.

Alisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa mwili huo ulikutwa na alama za kucha shingoni na uvimbe sehemu za siri kitendo kinachoashiria alikuwa amebakwa.

Alisema hadi sasa chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana na hakuna mtuhumiwa yeyote aliyekamatwa huku msako ukiwa unaendelea ili kuwabaini wahusika wa tukio hilo huku mwili wake ukiwa umehifadhiwa hospitali ya Mount Meru kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari.

Ali Kiba Afunguka..Adai Hakiwezi Kunikuta Kilichomkuta Davido Sony Music

$
0
0
Yapata miezi miwili sasa tangu tuzisikie taarifa za msanii mkali kutoka Nigeria Davido kutoa malalamiko kwa uongozi wa lebo ambayo inasimamia kazi zake kwasasa #Sony Music.

Malalamiko hayo yalitokana na kilichosemekana kuwa uongozi huo unamzuia msanii Davido kuachia kazi mpya bila kujali kuwa ni kipindi kirefu kimepita kwa msanii huyo bila kutoa kazi mpya.

Kutoka Bongo Flevani msanii @officialalikiba naye pia yupo chini ya uongozi huo wa Sony Music. Ila yeye ameiambia Perfect255 kuwa jambo kama lile lililomtokea Davido yeye haliwezi kumkuta kutokana na mkataba wake ambao amesaini na kampuni hiyo.

Ni baada ya kuulizwa kuwa yeye amejipanga vipi kama endapo litatokea kama lililomtokea msanii mwenzake Davido katika lebo hiyo. “Nimejiandaa vizuri, na pindi unapokuwa unasaini kitu ina maana kuwa umekubaliana na kila kitu, kwahiyo mimi pia nina matakwa yangu na hata wao pia wana matakwa yao, kwahiyo kitu ambacho kipo hapo ni kwenda na agreement. Me siwezi kukaa muda zaidi ya miezi 3 bila kutoa ngoma, na huo ndio mkataba wangu jinsi unavyosema.” Hayo ndio yalikuwa majibu ya Aikiba.

Mama Wema Sepetu Afunguka Kuhusu Ugomvi wa Wema na Munalove....Adai Marafiki Wanamtumia Kumuuza Kwa Wanaume

$
0
0
Bifu ya Wema Sepetu na Muna Love imeingia ukurasa mpya baada ya Mama Wema Sepetu kujitokeza na kuongea Mengi huku akimpelekea Wema Lawama na kumtetea Muna..Nimekuwekea Sauti hapa chini mama Wema Akiongea kuhusu sakata hilo na kuhusu Wema Kutumiwa na Kuuzwa kwa Wanaume....

Sikiliza Hapa:

Rais Magufuli Atamani Kuhudhuria Tamasha la Fiesta Dar

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema alitamani kuhudhuria tamasha la muziki la Fiesta ambalo litafanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club.
Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii Ikulu jijini Dar es salaam, Magufuli alisema alitamani kuhudhuria tamasha hilo ili apige tumba lakini majukumu ya kazi yamembana.

“Natamani kwenda Fiesta siku ya kesho sema hii kazi inanibana kwa kuwa itakuwa live nitaifuatilia kupitia kwenye runinga,” alisema Magufuli.

Pia Rais huyo ambaye kesho November 5 anatimiza mwaka mmoja toka aingie madakani, alimmwagia sifa msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto kwa kufanya muziki wenye maadili na kuelimisha.

Naumia Sana Moyo Kwa Nayosikia Kuhusu Mchezo wa Kuruka Ukuta mpenzi Wangu Anaofanya

$
0
0
Kupenda kunaumiza kama hujawahi kupenda na usitamani kupenda kwa kweli ..na mpenzi wangu kwa kweli mtoto mashalaaa kaumbika na kajaliwa kiukweli yeye ananipenda sana kuna siku alinitamkia chochote nachotaka atanipa ili mradi nisimpoteze ..

Sana naumia maana nilipata habari na mtu wa karibu kua mpenzi wangu anaruka ukuta nilipuuzia nikaona hayo ya uongo sasa nimekuja kusikia tena juzi kwa baadhi ya watu kua huyu ni tabia yake kurishwa ukuta toka yupo chuo sasa nikipima na maneno yake kua chochote nachotaka atanipa picha inanijia maana kila tuwapo faragha ananiwekea mitego ya ajabu ajabu tuu ..

Sasa uyu nilikua na malengo nae aje awe mke sasa naingiwa na hofu unaeza oa mke anaefanya huo uchafu? sasa heshima si itashuka jamani? nifanyeje?

Polisi wa Kike wa Kiislamu Waruhusiwa Kuvaa Hijabu

$
0
0
Serikali ya Scotland imeidhinisha vazi la hijabu na kulijumuisha kwenye sare za maafisa wa polisi wa kike wa Kiislamu ili kuongeza idadi yao katika idara hiyo.

Mkuu wa idara ya polisi nchini humo Phil Gormley, ametoa maelezo na kubainisha furaha kubwa kwa kutangaza uamuzi huo, na kufahamisha nia yao kutaka kusaidiana na maafisa wa Kiislamu katika suala la usalama wa taifa.

Muungano wa maafisa wa polisi wa Kiislamu SPMA nchini humo pia ulitoa maelezo na kufahamisha kwamba uamuzi huo utaweza kuimarisha mahusiano bora kati ya jamii za Scotland na jumuiya ya Kiislamu.

Mkuu wa SPMA Fahad Bashir alisema, ''Uamuzi huo uliochukuliwa na serikali ni sahihi. Tunapata faraja kuona nchi yetu ikichukuwa hatua muhimu kama hizi zenye mwelekeo mzuri.''

Hapo awali, maafisa waliokuwa wakiruhusiwa kuvaa hijabu walikuwa ni wale waliohudumu kwa miaka zaidi ya 15 na wanaoshikilia nyadhifa za juu.

Katika mwaka 2001, sare rasmi za polisi zilitambulishwa ambapo hijabu pia ilijumuishwa.

Mr Nice Azungumzia Tetesi Kuwa Ana Ugonjwa wa Ukimwi

$
0
0
Gazeti la Taifa Leo la nchini lilifanya mahojiano na msanii mkongwe wa muziki wa Tanzania Mr Nice. Katika moja swali ambalo aliulizwa ni kuhusu tetesi ambazo zimesambaa nchini humo kuwa ana HIV.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya muziki wake nchini Kenya, alikanusha uvumi huo huku akieleza nini kilimkuta mwaka jana mpaka akalazwa hospitali kwa miezi kadhaa.

“Kaka wewe mwenyewe ukinicheki nilivyo fresh nina ngoma kweli?,” Mr Nice alimuuliza mwandishi huyo huku akicheka. “Siugui Ukimwi lakini ni kweli mwaka jana nililazwa hospitali kwa miezi mitatu kuanza October. Nililishwa sumu kali wakati wa kampeni za uchaguzi lakini hatukuweza kubaini ni nani alifanya hivyo lakini tulijua ni mambo ya siasa na nikamwachia Mungu.

Katika hatua nyingine Mr Nice alisema Tanzania kuwa na wasanii wengi kwenye tuzo za MTV MAMA 2016 kuliko jirani zake Kenya na Uganda kulitokana juhudi za msanii moja moja.

“Kusema kweli wasanii wa Tanzania wamekuwa wakishindana wenyewe kwa wenyewe, kila mmoja anataka kufanya kazi nzuri kuliko mwenzake. Kwahiyo binafsi naona hii hali imesaidia kuwajenga wasanii wa Tanzania pamoja na muziki kiujumla,”

Dr. Cheni Aeleza Sababu za Kutojihusisha Tena na Filamu Nchini

$
0
0

Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini, Dr Cheni amesema hatatoa tena filamu nyingine kutokana na hali ya kibiashara ilivyo katika tasnia ya filamu hapa nchini

Dr. Cheni alisema hayo alipokuwa akizungumza na E News ya EATV ambapo alisema kuwa kazi zao hazina ulinzi na haiwafaidishi wasanii ndio maana huoni umuhimu wa kuendelea kutoa kazi hizo

Dr. Cheni alisema ukitoa leo filamu mpya baada ya siku moja utaikuta imesambaa nchi mzima ikiwa inauzwa tena kwa bei chee, alipoulizwa hadi lini ndo atatoa filamu, alisema kuwa hadi hapo Serikali itakapoingilia kutatua suala la kazi zao

"Siwezi kutoa tena filamu hadi Serikali itakapo hakikisha kuwa kazi zetu zipo salama, ukitoa filamu leo siku moja ya pili ya tatu unazikuta chini zinauzwa ambazo ni bandia, kilio chetu sisi bongo movie ni kazi zetu zinaibwa, namuomba Rais Magufuli aingilie kati suala hili kwani vijana wengi wamejiajiri kwenye bongo movie "alisema Dr Cheni

Tundu Lissu Akataa Kujisalimisha Mahakamani Bila Barua ya Wito

$
0
0
Siku moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuagiza Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akamatwe kwa kushindwa kuhudhuria kortini, mbunge huyo amedai hana taarifa hizo hivyo hawezi kujisalimisha popote.

Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, alidai atajisalimisha tu kwenye vyombo vya dola au kwenda mahakamni ikiwa atapelekewa barua aliyoandikiwa na mahakama na kutiwa saini na kugongwa muhuri na hakimu.

“Kaka, mimi siwezi kufanyia kazi za magazeti katika masuala ya kisheria, nipo hapa ninaendelea na shughuli zangu kama kawaida na kama mnavyoniona niko katika kuwawakilisha wananchi wa jimbo langu,” alieleza Lissu.

Mwanasheria huyo mkuu wa Chadema alitoa maelezo hayo jana alipohojiwa kuhusiana na habari zilizoandikwa na vyombo vya habari, kwamba Mahakama ya Kisutu juzi iliagiza mbunge huyo akamatwe baada ya kushindwa kuhudhuria katika kesi inayomkabili.

Mbali ya mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa kwa Lissu, pia iliagiza iandaliwe hati ya kuitwa mahakamani kwa wadhamini wake ili wajieleze kwa nini wasilipe fungu la dhamana walilotia saini ambalo ni Sh10 milioni.

Kwa mujibu wa Hakimu Mkazi wa Kisutu, Thomas Simba, Lissu amekuwa hahudhuri kortini kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili pamoja na wahariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa na mchapaji wa magazeti, Ismail Mehboob.

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14 mwaka huu, Dar es Salaam, Lissu na wenzake walikula njama za kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti la Mawio lenye kichwa cha habari: “Machafuko yaja Zanzibar”.

Juzi, siku ambayo kesi hiyo ilipangwa kutajwa tena, Lissu hakuwapo mahakamani kutokana na kile mdhamini wake Robert Katula alichodai kuwa mshtakiwa huyo anaendesha kesi ya uchaguzi Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Mwanza hivyo asingeweza kuhudhuria.

Kutokana na maelezo hayo wakili wa upande wa Jamhuri, Patrick Mwita aliomba mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa mshtakiwa jambo ambalo Hakimu Simba alikubali pamoja na wito kwa wadhamini kufika mahakamani Novemba 21, mwaka huu.

Alipoulizwa kuhusu hatua hiyo, Lissu alisema kuwa wito wa kwenda mahakamani ni lazima barua iwe imeandikwa na kugongwa muhuri na kutiwa saini ya hakimu wa mahakama na siyo kusikia na kwenda bila ya kuwepo kwa wito kamili.

Bodi ya Mikopo Elimu Ya Elimu ya Juu Yaagizwa Kuwapa Wanafunzi Fedha Zao ifikapo Leo

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB), imeagizwa kuhakikisha kuwa fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo zinapelekwa vyuoni ifikapo leo.

Agizo hilo lilitolewa bungeni jana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako baada ya wabunge mbalimbali kuomba miongozo kwa Spika kuhusu kuwapo kwa wanafunzi wengi waliokosa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/17.

Mwongozo kwa Spika ulitiliwa mkazo na Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete aliyeeleza kuwapo taarifa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuwa wanafunzi wanataka kugoma kwa kukosa fedha za mikopo.

Kutokana na miongozo hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga aliitaka Serikali kutoa maelezo.

Akitoa kauli ya Serikali, Profesa Ndalichako alisema fedha za mikopo kwa ajili ya wanafunzi zilikwenda vyuoni wiki moja iliyopita.

“Tatizo lililotokea kwa UDSM sijui kama walidanganyana au la lakini hawakujaza fomu. Serikali haitatoa mkopo kwa mwanafunzi ambaye hajajaza fomu. Na waliosaini leo wataingiziwa fedha zao kwenye akaunti na vyuo,”alisema.

Kuhusu wanaoendelea na masomo, Profesa Ndalichako alisema wanafunzi wote wanufaika na wanaoendelea na masomo wataendelea kupatiwa mikopo kama ilivyokuwa mwaka uliopita.

Alisema wanafunzi ambao vyuo vyao vimewasilisha HELSB taarifa za matokeo, Bodi imekwishawatumia fedha vyuoni kwa ajili ya kuwapa mikopo wanafunzi hao.

Hata hivyo, alisema taratibu za kuwabaini wanafunzi wenye sifa zinaendelea na wasio na sifa wataendelea kuondolewa kupata mikopo.

Pia, alikiri kuwa ucheleweshaji wa matokeo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo umeathiri kasi ya kutuma fedha vyuoni.

“Wizara yangu imekwishaagiza vyuo vyote ambavyo havijawasilisha matokeo ya mitihani ya wanafunzi wao kwa mwaka wa masomo uliopita, kufanya hivyo mara moja,”alisema.

Ndalichako alisema hadi kufikia Novemba 3 mwaka huu, Sh71.042 bilioni zilikwishatumwa vyuoni kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo.

Akizungumzia utoaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/17, Ndalichako alisema katika mwaka huo, Sh483 bilioni zimetengwa na zimelenga kutoa mikopo kwa wanafunzi 119,012, wanafunzi 93,295 wanaoendelea na masomo na wa mwaka wa kwanza 25,717.

Ndalichako alisema katika mwaka wa fedha 2016/17 wanafunzi 58,010 walidahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na orodha yao iliwasilishwa HELSB na hadi Novemba 2, mwaka huu, wanafunzi 21,190 wa mwaka wa kwanza wamepewa fedha. Kati yao 4,321 ni yatima, 118 wenye ulemavu na 87 ni waliosoma sekondari kwa ufadhili wa taasisi mbalimbali.

Master J: Mimi na Hermy B ni kati ya watayarishaji wa muziki tunaoishi maisha mazuri

$
0
0
Ni ukweli usiopingika kuwa hakuna muziki pasipo kuwa na watayarishaji wa muziki – lakini wao ndio wamekuwa wakiongoza kuishi maisha ya chini zaidi.



Akiongea na kipindi cha Ladha 3600 ya EFM, mtayarishaji mkongwe wa muziki hapa nchini Master Jay amesema kuwa kwa Bongo ni maproducer wachache wenye maisha ya kwendana na hadhi yao.

“Kati ya maproducer wanaoishi maisha mazuri hapa mjini ni mimi na Hermy B,” amesema Jay.

Master ameongeza kuwa yeye alishtuka mapema ndio maana akaamua kuachana na kazi hiyo kutokana na kutoona faida na kazi hiyo wakati huo huo akiwa na familia inayomtegemea.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images