Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Wema Sepetu Ashindwa Kujizuia Kwa Ushindi wa Tuzo Tatu Kwa Diamond...Asema Haya

$
0
0


Maneno ya Wemasepetu leo baada ya Diamond Kushinda tuzo tatu

"Makofi matatu kwa Tuzo tatu... "Tanzania's Pride..." Sema picha hii Kali saaaaaaanaaaaa... Utasema sio wa Tandale...(Sorry Bro)... Congrats once again...!!"

Diana Alia Kutelekezwa na Kamati ya Miss Tanzania

$
0
0
Miss Tanzania 2016 Diana Edward ambaye ndiye mrembo anayetarajiwa kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunia 'Miss World', ameilalamikia kamati ya mashindano hayo kwa kumtelekeza.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Diana ambaye kwa sasa anatakiwa awe kwenye maandalizi ya mashindano ya Miss World, amesem abado hajapata msaada wowote kutoka katika Kamati ya Miss Tanzania na serikali, ikiwa zimebaki siku chache  kuweza kufikia kwenye mashindano hayo ya dunia.

Amesema kuwa kwa sasa yeye anachohitaji kwa sasa ni suport pamoja na msaada mkubwa kutoka kwa serikali, kwani yeye binafsi anajitahidi kufanya pale anapoweza.

"Tanzania, viongozi, serikai, Miss Tanzania cometee, i need suport, i need what i deserve, unajua mimi ni mtu ambaye najiongeza, kwa hiyo nikipewa suport kidogo i push it up, kuna watu ambao nimewaomba suport wamenipa vya kutosha, kwa hiyo i need what i deserve", alisema Diana.
Kwa upande wa msemaji wa Kamati ya Miss Tanzania ameruka kuhusika na suala hilo.

Diva Loveness Amtaka Kiba Abadili Gilfriend...Adai Jokate Anamtia Gundu

$
0
0
Mtangazaji wa Ala za Roho kipindi kinachorushwa na Clouds FM, Diva the bawse ametoa kauli kupitia mtandao wa twitter ambayo imezua gumzo kutokana na alicho kiandika.

Mwanadada Diva aliweza ku tweet kuhusiana na uwezo wa alikiba katika kuimba na kumalizia kuwa “Girlfriend anakutia gundu” kitu ambacho wengi walijiuliza inamaana Jokate (Kama inavyo julikana kuwa ndiye wa Kiba) kuwa anamtia gundu!

Mwanamuziki Alikiba ni miongoni mwa wanamuziki wenye nguvu nchini Tanzania huku akichuana kwa mashabiki na Diamond Platnumz.

Je unadhani mtazamo wa Diva kuhusu mpenzi wa Kiba ni waukweli au Alikiba anafanya muziki mzuri usio na gundu?

Kauli ya Mwisho ya Samwel Sitta Baada ya Daktari Kumueleza Kuwa Asingeweza Kupona

$
0
0
Kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanza nia (2005-2010), Samuel Sitta, mwanae wa kiume ameweka wazi maneno matatu ya mwisho aliyoyatamka, yenye maana nzito katika maisha.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta ambaye ni mtoto wa kiume wa marehemu, alisema kuwa baba yake alitoa maneno matatu ya kuukubali ukweli wa maisha baada ya Daktari kumueleza kuwa asingeweza kupona.

“That’s life (hayo ndiyo maisha),” Benjamin alikariri maneno ya baba yake. Alisema hayo yalikuwa maneno yake ya mwisho baada ya kuelezwa ukweli na daktari wa hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu.

Maneo ya Sitta ni funzo kubwa kwa watu wote kuwa maisha huanza na huisha, hiyo ndiyo maana ya maisha na hakuna aishie milele hivyo tuishi kwa kuzingatia maana hiyo ya maisha na kuikubali.

Sitta ambaye anakumbukwa kwa kauli mbiu yake na matendo ya kusimamia ‘kasi na viwango’, alifariki kutokana na ugonjwa wa tezi dume uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

Alitangaza kustaafu siasa muda mfupi baada ya kukamilika kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, ambapo yeye alikuwa mmoja kati ya waliokuwa msitari wa mbele kumnadi mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt. John Magufuli aliyeshinda uchaguzi huo.

Benjamini alieleza kuwa marehemu atazikwa Urambo Mkoani Tabora na kwamba ratiba ya mazishi itatolewa na Ofisi ya Bunge ambayo ndiyo inayoratibu mazishi

“Tumempoteza baba na kiongozi ambaye tulikuwa tunamtegemea kwa ushauri na masuala mbalimbali, tutafuata yale aliyokuwa akituelekeza,” alisema Benjamini.

Hakika Taifa limempoteza mtu muhimu, pengo lake halitazibika kamwe. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!

Angalia Thamani yako, Yanini Kumng’ang’ania Asiyekupenda?

$
0
0
Ili mapenzi yaweze kuwa bora kwa kila aliye katika mahusiano, huwa ni vyema kila mmoja kuiona thamani ya mwenzake. Ukipenda kujiangalia mwenyewe  si ajabu mwenzako kupata hisia za kuwa humthamini wala humjali.

Muunganiko wenu katika mapenzi maana yake tayari mmekuwa kitu kimoja. Katika mimi unaweka sisi.

Ila pia ni vyema ikakumbukwa ladha na maana halisi ya mapenzi ipo kwa anayekupenda na kukuthamini. Unapokuwa na uhakika kama anakupenda na kukuthamini hapo ndipo nafsi yako itatulia na kuwa na amani. Ndani ya mapenzi na mtu wa aina hii ni amani na utulivu kwa kwenda mbele. Hakuna majuto wala majonzi ya kila siku.

Unapoamua kuwa katika mahusiano na mtu ambaye hakupendi, bali unakuwa naye kwa kuwa tu unampenda jua umejiingiza katika utumwa. Mapenzi ni suala la kihisia zaidi. Mwenzako anapokosa hisia na wewe maana yake hata uwepo wako hauthamini inavyopaswa. Na hapo ndiyo tunaona yale mahusiano ya kingono yanapozaliwa na si ya kimapenzi kwa maana halisi.

Yaani mwenzako anapokuwa na mihemko ya kingono ndipo anapokutafuta na si vinginevyo. Niliwahi kuongea na msichana mmoja aliyewahi kuniambia anampenda kijana mmoja ambaye anauhakika kabisa yeye hampendi. Alinambia uhakika huo kaupata kutokana na kijana huyo kumtakia  kuna msichana yupo anampenda na kumjali ila si yeye.

Kuonesha zaidi kumpenda msichana yule mwingine, jamaa aliwahi kumwambia kama ikitokea hata huyu msichana akagombana na yule mpenzi mwingine wa yule jamaa, kijana yule alikuwa radhi kumdhuru huyu msichana.

Hata kwa matazamo wa haraka hapo unaweza kugundua ni kwa namna gani huyu msichana alikuwa haitajiki. Ila cha kushangaza msichana huyu(aliyeongea na mimi) alimwambia mvulana husika yuko radhi kuwa naye hivyo hivyo.

Aliamua kuwa hivyo akiamini ipo siku jamaa atamuelewa. Kweli walikuwa pamoja. Ila  unajua kinachomkuta sasa?

Kila jamaa anapogombana na yule msichana mwingine anamtumia huyu kingono na mambo mengine yasiyo ya kimapenzi, na bila kutafakari mara mbili huyu msichana anafanya kwa kile anachoamini hali hiyo itamfanya huyu jamaa amfikirie zaidi. Kuna kitu cha kuangalia hapa.

Suala la mapenzi si suala la kuoneana huruma wala aibu. Mapenzi ni hisia. Unapojitoa kwa mwenzako kwa kila jambo na unamuona haelekei ujue hana hisia na wewe. Kwanini unakubali kuteseka na kuumia kila siku kwa kumuangalia yeye tu?

Ndiyo, unampenda sana, unamjali sana na unamuhitaji sana, ila kama yeye hakutaki wa kazi gani? Ni muda wa kujiangalia na wewe sasa.

Ona thamani yako kama binaadamu, jionee huruma jinsi unavyoteseka kila siku kwa mtu asiyeona thamani yako.

Wewe ni binaadamu mwenye hadhi na thamani, bila kujali muonekano wala rangi yako. Unahitaji mwenye kukuthamini na kukujali na si anayekufanya kama mdoli wake ngono au kadi yake ya pesa. Kataa utumwa wa mapenzi kwa kuiona thamani yako.

Ni vyema ukalia kwa kumkosa kuliko kuonekana unaye wakati moyoni siyo wako. Hakuna sifa ya kuwa na mtu mwenye fedha au muonekano mzuri ikiwa hakujali wala haupo moyoni mwake. Mapenzi ni amani na raha.

Mapenzi hufanya watu wafurahi na kusahau shida zao. Ila jiulize kwanini kwako hayako hivi? Unaenda kwa mwenzako badala afurahie uwepo wako, yeye anaona unajipendekeza. Unampigia simu na kumpa maneno mazuri ya faraja, yeye anaona unamsumbua. Sasa wa kazi gani? Siku njema wapendwa.

Sakata la Diva Kudai Jokate ni Gundu Kwa Ali Kiba..Gigy Money Afunguka Haya

$
0
0

Mwanadada Diva aliweza ku tweet kuhusiana na uwezo wa alikiba katika kuimba na kumalizia kuwa “Girlfriend anakutia gundu” kitu ambacho wengi walijiuliza inamaana Jokate (Kama inavyo julikana kuwa ndiye wa Kiba) kuwa anamtia gundu?

Leo Mrembo Gigy_Money amejitokeaza na kupost picha hii hapa chini na kuandika maneno ya kumtetea Jokate:

"Honestly jojo wangu mtoto classic uyu 😍wache waseme unagundu ila mwisho wa siku watakuelewa tu kwa mafanikio yako hadi unafikia umri wao yani we utakua Michael Jackson wa kike unajituma mwaya #USIFORCETUFANANE #HATUFANANI" Gigy Money

Mwanamuziki AT Nae Achukizwa na Kauli ya Diva Loveness...Amwangushia Diva Kichambo cha Nguvu

$
0
0

Kauli ya Diva kuwa Jokate ana Gundu Hivyo Ali Kiba Amuache Bado inaendelea kuwatoa mapovu baadhi ya wasanii wa Bongo....
Msanii wa Mduara AT nae amechukizwa na kauli hiyo na kuamua kuchukua jukumu la kumchamba Diva kisawa sawa....Embu jisomee Mwenyewe hapa chini......

AT_original Ameandika haya kupitia ukurasa wake wa Insta:

"Du hili penzi lenu lina sabuni mbona linatoa watu Mapovu? Kuna Bibi mmoja umepiganae pic Wigi lake kaam Jumba la Kunguru limemsimama km Linashangiria #Goli au ni Mama yetu wa kambo?Au ndio mambo ya Kushoboka Uzeeni? Hana wazo ata moja sijui alikosa bwana ujanani kwa muda huu asubiri mvi tu lisura Pana km #Sinia,Km kweli mshauri Angeliteuliwa na #Rais! Na km anataka wanaume wadogo wadogo aende #leba wamejaa Kushindana na #Jojo ni sawa na kushindana na popo kwa kuona Usiku. Mwambieni kupendwa sio #kujamba km kwa kila mtu inawezekana,Au ana vidudu vyake vipya nini? anavitafutia hifadhi hehehe.!! Amuwaache #Jojo aende kwa #kiba kwani Ufalme wa kupendana ni wao wenyewe,ABaki na Shepu lake la kitunguu #Swaumu!! Yaani bwana wako anakazi ameacha kufuga #Punda anakufuga wewe. #tena wewe ni Kopo tu huna bahati ata uwe jipya vipi hukai kwenye kabati!! #Ewe #Mola huyu Shetani Toleo jipya Duniani ss ni wakazi gani?Tunakuomba kwa dua zote #Mlaani maana hatujui ni #Kuwadi #somo, #kungwi au ni #Mshenga! Maana kavamia shughuli si yake katoa na #Sare ataadhirika mwenyewe mchana kweupeee.!!! Damu imeshakata hata hubleed tena bado unajiona kijana km unajua kupangia watu mtu wa kua nae eka na wako tumuone. hujui kuchagua Nguo za kuvaa utaweza kumchagulia mtu mpenzi?mwaka huu utakunya Mavi makubwa kilo 2 na hufanikiwi Ngo'oo...!! #USILOLIJUA #USILIBEBEE #KIFUA #LITAKUTOA #DAMU #ZA #PUA." Ameandika AT

Ufahamu Ugonjwa Uliosababisha Kifo cha Spika Mstaafu wa Bunge Samweli Sitta

$
0
0
Ugonjwa wa Saratani ya Tezi Dume umetajwa kuwa ndio chanzo kilichopelekea kifo cha Spika Mstafuu wa Bunge la Tanzania, Samwel John Sitta.

Mtoto wa marehemu Samwel Sitta, Benjamin Sitta ambaye ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni alisema kuwa baba yake alifariki kutokana na saratani ya tezi dume ambayo ilikuwa imesambaa mwilini kiasi cha kumfanya ashindwe kutembea.

Samwel Sitta alifarika alfajiri ya jana nchini ujerumani alipokwenda kwa ajili ya kupatiwa matibabu ikiwa ni kwa mara ya pili kwenda nchini humo baada pia ya kwenda India kwa ajili ya matibabu.

Wataalamu wa afya wameeleza kuwa ugonjwa huu huwaathiri zaidi wanaume wengi wenye umri kuanzia miaka 60. Aidha, wameeleza kuwa tezi dume hupatikana chini ya kibofu cha mkojo na imezungukwa na mirija ya mkojo.

Mbali na watu wenye umri kuanzia miaka 60, watu wengine walioko kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu ni pamoja na wanaume kutoka Afrika (Weusi), wanaume ambao kwenye familia zao kuna historia ya ugonjwa huu.

Saratani hii hupelekea maumivu makali ya mifupa kwenye nyonga, mapajani na kiunoni, uume kushindwa kufanya kazi, kupungua uzito, uchovu, kichefuchefu, baadhi ya sehemu za mwili kushindwa kufanya kazi.

Kuna vipimo vya aina tatu vya saratani ya tezi dume ambapo, vipimo vya kwanza ni vile ambavyo hufanyika kuangalia kama mtu ana ugonjwa huo, vipimo vya pili hufanyika kuthibitisha kama ni saratani ya tezi dume au ni uvimbe tu, na vipimo vya tatu hufanyika kuangalia madhara yaliyosababishwa na ugonjwa huo.

Matibabu yake hufanyika ambapo mgonjwa akiwahi hospitali, tezi hizo huondolewa ili kuizuia saratani kusambaa zaidi mwilini, huweza pia kupatiwa tiba ya miozi, dawa.

Inashauriwa na wataalamu wa afya kuwa, kwa wanaume wote wenye umri kuanzia miaka 50 wafanye vipimo ili kuweza kufahamu kama wana saratani ya tezi dume au la.

Wema Sepetu 'Me I dont Deal With Washamba, Nilijua Muna Alikuwa Mshamba Alivyokuja ila Nikaweka Ustaa Pembeni na Kumkubali'

$
0
0
Wema Sepetu Akihojiwa na Kipindi cha E News cha Clouds FM ameulizwa kuhusu beef lake na Muna na Kudai kuwa yeye huwa hadeal na Washamba akaongeza kusema kuwa urafiki na Muna ulikuja na kuuruhusu akijua Muna ni Mshamba lakini alikubali kuweka Ustaa Wake pembeni na kukubali awe Rafiki yake lakini mwisho wake ndio yaliyotokea....

'Me I dont deal with washamba, i knew she was mshamba alivyokuja lakini nilisema nisiweke ustaa nimchukulie kama vile jinsi alivyo'


Alikiba Azungumzia Madai ya Kunyimwa tuzo ya MTV EMA na Kupewa Wizkid

$
0
0
Alikiba amefunguka kuzungumzia tetesi za kwenye mitandao ya kijamii kuwa amenyimwa tuzo ya MTV Europe Music Awards (EMA) katika kipengele cha Best African Act na badala yake tuzo hiyo kwenda kwa Wizkid.

Hatua hiyo imekuja baada ya muimbaji huyo wa Aje kuonekana kuongoza kwa kura nyingi zilizopigwa na mashabiki kupitia mtandao wa tuzo hizo.

“Kiukweli mpaka sasa hivi mimi mwenyewe sijui ni kwa sababu gani, watanzania na mashabiki wote hawajui ni kwa sababu gani. Kama ulivyozungumzia na juhudi zilivyokuwa zikifanyika pale na watu walipiga kura kweli, kwa sababu watu wanavyokuwa wakipiga kura pale mabadiliko yanakuwa yanaonekana,” amekiambia kipindi cha Jahazi cha Clouds FM.

“Kwa hiyo mashabiki walikuwa wanataka kujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea at least tuweze kupata hata voice ya explanation kiundani ili kila mtu afahamishwe ni kitu gani au ni vigezo gani wametumia kufanya mimi nisishinde ile tuzo. Hiko ndio kitu tunachosubiria na menejimenti yangu.”

Muimbaji huyo alikuwa akiwania tuzo hiyo pamoja na wasanii wengine, akiwemo Olamide na Wizkid kutoka Nigeria na Black Coffee na Cassper Nyovest wa Afrika Kusin

Mwanamuziki RUBY Awachana Waimbaji wa Kike Bongo.....

$
0
0
Ruby amefunguka kwa kudai kuwa wasanii wengi wa kike kwenye muziki wamekuwa ni wabinafsi.

Muimbaji huyo mwenye sauti ya dhahabu, amemuambia mtandazaji wa kipindi cha Playlist cha Times FM, Lil Ommy kuwa huenda kungekuwa na wasanii wengi wa kike kwenye Bongo Fleva kama wangekuwa wanashirikiana kwa kufanya kazi kwa pamoja.

“Mimi hainiumi ila inanishangaza sana kwanini wanawake kwa wanawake hatusapotiani, mbona wanaume kwa wanaume wanafanya muziki wanafanya vitu vingi pamoja. Ni kitu cha ukweli kabisa kwenye industry wanawake hatufanyi kolabo wanawake kwa wanawake, ni kitu ambacho si kizuri kwa sababu huenda tungekuwa na wasanii wengi wa kike kwenye muziki,” amesema Ruby.

Ruby ameongeza kuwa msanii unatakiwa uwe mnyeyekevu kwa kila mtu lakini uangalie ni wakati gani unatakiwa kufanya hivyo.

Majina ya Wasanii Watakaowania Tuzo za EATV Awards yatajwa, Nao ni…

$
0
0
Awamu ya kwanza ya kutaja majina ya wasanii watakaowania tuzo za EATV kwa mwaka huu wa kwanza yametajwa Jumanne hii.

Kwa kuanzia yametajwa majina ya wasanii kutoka katika vipengele viwili kati ya kumi vilivyopo kwenye tuzo hizo huku zoezi hilo likitarajiwa kufanyika kwa siku nne ambapo litakamilika Ijumaa hii ya Novemba 11.

Hii ni orodha ya wasanii waliotajwa kwenye vipengele hivyo.

Mwanamuziki bora chipukizi

Man Fongo
Feza Kessy
Ruky Baby
Mayunga
Bright

Muigizaji bora wa kiume

Saidi Ali – Ndugu wa mume
Meya Shabani – Profile
Daudi Tairo (Duma) –
Salim Ahmed (Gabo) – Safari ya Gwalu
Dotto Matotora – Likwacha Lala

Alikiba Ameshinda MTV Ema Kwa Kura Lakini ni Ukweli Hakustahili zaidi ya Wizkid!

$
0
0
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu Alikiba kupokonywa ushindi huko MTV EMA.Naomba hapa nitumie nafasi hii kufafanua kilichotokea ili kuweza kuondoa huu utata.

Kwa mujibu wa Mtv Ema Alikiba ameshinda kwa kura nyingi sana alizopigiwa na mashabiki na wamemtangaza kuwa katika kipengele cha kura nyingi Ali ndio mshindi.

Naomba tufahamu kwamba Tuzo kubwa kama MTV EMA na BET kuna vipengele ambavyo maamuzi yake hayategemei kura za mashabiki bali huamuliwa na wadhamini, majaji pamoja na waandaaji wa Tuzo. Kipengele hiki huangaliwa ni kiasi gani msanii anafanya vizuri katika category aliyowekwa cz inawezekana msanii akakosa kura nyingi lakini anastaili kupata tuzo kutokana na mchango wake katika mziki.

Kipengele hicho ndicho kilichomfanya Wizzy ashinde Tuzo hiyo ya MTV EMA.
Kiukweli MTV EMA hawajakosea katika hilo cz watanzania wengi walimpigia kura Kiba bila kujali team zao lakini kwa viwango vya kimataifa kiba hawezi kumfikia hata Robo Wizkid.

Alikiba alitakiwa kuwaambia ukweli mashabiki zake na sio kulalamika kwenye media kuwa haelewi kilichotokea wakati anafahamu ukweli wote. Kulalamika kwa Ali kutamsababishia picha mbaya na sidhani kama MTV EMA watakuja tena kumchagua kuwania Tuzo hizo katika Category yoyote ile.

Natumaini nimeeleweka japo kwa uchache.

By Sele Mkonje

Uchaguzi Marekani:Donald Trump Anaelekea Kushinda Uchaguzi wa Marekani

$
0
0
Waswahili wanasema usiemtaka kaja, Mgombea Donald Trump anaelekea Kushinda uchaguzi wa Marekani baada ya kuongoza katika majimbo mengi huko Marekani ambapo kura zimeanza kuhesabiwa asubuhi hii....

Kwa sasa Trump ana kura 244 za wajumbe na Clinton 209. Mshindi anahitaji kura 270 za wajumbe.
Mshindi anahitaji kupata kura 270 kati ya jumla ya kura 538 za wajumbe ndipo atangazwe mshindi.

DIAMOND Afunguka Kuhusu Familia Ilivyombadilisha, Kumsaliti Zari, Nyumba ya South Afrika na Ziara na Neyo UK

$
0
0
Nilipokuwa Lagos, Nigeria, siku mbili kabla ya kufanyika kwa tuzo za Afrima, nilikaa kitako na Diamond Platnumz kuzungumza mambo mbalimbali kuhusu muziki na maisha yake binafsi. Haya ni sehemu ya tuliyozungumza kwenye interview hiyo.



Kuhusu jinsi familia ilivyombadilisha

Nafikiri familia imenifanya niwe nazingatia kile ninachokifanya, nikimaanisha kwamba kuwa makini kwasababu nikifeli sio tu timu yangu bali nafelisha na familia yangu. Kwahiyo nakuwa najitahidi kufanya sababu ya nchi yangu, timu yangu lakini pia mwanangu, kesho na kesho kutwa aweze kuwa proud kusema kwamba ‘baba alifanya hiki na hiki.’ Na kunipa akili ya kuinvest sana sababu usipoinvest usifikiri kwamba unaweza kufika mbali sababu kila mtu anafanya kitu ili kutengeneza msingi bora wa familia yake, vijana wanaokuja isije kubaki story kwamba mtu fulani alivuma sana halafu mwisho wa siku tee.

Kuhusu lugha anayotumia Tiffah kuwasiliana

Ni Kiingereza. Sababu bado hajakuwa katika hatua ya kuongea kabisa lakini maneno yake yote anayozungumza ni ya Kiingereza, hata akisema sitaki, atasema ‘I don’t want it.’ Kwahiyo ndio maana tumempeleka academy ili iwe rahisi sana kwa yeye kuelewa lugha kirahisi kwasababu pale nyumbani kwao wanazungumza mpaka Kiganda, kuna Kiswahili kidogo, kuna Kiingereza kwahiyo inaweza ikamchukua hata miaka mitano hadi ashike vitu vyote, lakini kwenye academy wanafundisha Kiingereza tu, inakuwa rahisi kwake kuzungumza Kiingereza.

Kuhusu lugha anayotumia anapokuwa anazungumza na Zari

Kiingereza. Kadri siku zinavyokwenda anakuwa anakielewa Kiswahili, nafikiri kwasababu ndio maana hata mkiongea Kiingereza kiasi gani lakini lugha ya kwenu itabaki kuwa ya kwenu. So tunaongeza, sometimes ananiskia mimi na familia tunaongeza Kiswahili, sometimes namfundisha maneno ya Kiswahili lakini pia mwenyewe ni mwepesi na hata mkikutana naye anakielewa Kiswahili hapo si sana.

Kuhusu tetesi za kumsaliti Zari

Kitu ambacho niko proud sana ni mpenzi wangu mimi ni mwelewa sana, na tangia tunaanzana anaelewa kwamba mimi ni maarufu, yeye ni maarufu. Mimi nitasikia vitu kwake, yeye atasikia vitu kwangu, ni staa nakaa Tanzania, of course ni mtu ambaye nikiwinda siwezi kukosa au kuna mtu anaweza kuniwinda kinamna yoyote.

Lakini mwisho wa siku ni ufahamu wangu mimi kuwa mwanaume na ni namna gani naweza kumheshimu mwenzangu, kuweza kumpenda mwenzangu, naweza kumlindia heshima yake, anajikinga vipi na hivyo vitu vibaki kuwa story na sio vitu vya kweli kwasababu kusema vitasemwa tu. There is no way simba akapita katika zizi la swala akaondoka watu wakasema hakula swala hata mmoja, watasema tu alikula hata kama hakula.

Bongo5

Ruby Afunguka Juu ya Tetesi za Kusaini WCB...

$
0
0
Muimbaji wa kike mwenye sauti ya dhahabu kwenye Bongo Fleva, Ruby amefunguka juu ya tetesi zilizosambaa kuwa amesaini kujiunga na lebo ya WCB.

Ruby amepinga kujiunga na lebo hiyo lakini amedai kuwa anapenda kuwa karibu na Diamond kwa ajili ya kujifunza vitu vingi kutoka kwake.

“WCB hawana roho mbaya unaenda tu muda wowote kama unajua ni nini kimekupeleka pale, kwani mimi kuonekana WCB ndio nipo WCB? Diamond ni msanii mwenzangu, nikiwa naye najifunza vitu vingi, it doesn’t mean nikiwa naye nimejiunga WCB. Kumbuka pale kuna studio na kuna producer Lizer pale watu tunataka kufanya naye kazi,” amemuambia mtangazaji wa kipindi cha The Playlist cha Times FM, Lil Ommy.

Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Wale Wale’ aliouachia mwezi Septemba mwaka huu.

Donald Trump Aishangaza Dunia Nzima Kwa Kushinda Urais wa Marekani

$
0
0
Mgombea wa Chama cha Republican, Donald Trump ameshinda uchaguzi mkuu wa Marekani baada ya kufikisha kura 276 huku Hillary Clinton akiwa na kura 218.

Hillary Clinton amempigia simu Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump na kumpongeza kufuatia ushindia huo alioupata.

Akizungumza na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi, Trump amewataka raia wote wa Marekani, waliomchagua na ambao hawakumchagua kuungana na kuanza kuijenga nchi yao kwani muda wa kampeni na siasa za kugawanyika umekwisha.

Rais Magufuli Ampongeza Donald Trump Kwa Kushinda Kiti cha Urais Wa Marekani

$
0
0
Leo November 9, 2016 Marekani imeweka historia nyingine baada Donald Trump wa chama cha Republican kutangazwa mshindi wa kiti cha Urais, na tayari ameanza kupokea pongezi kutoka kwa viongozi wa nchi mbalimbali ikiwemo Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ametoa pongezi zake kwa Rais Donald Trump kupitia ukurasa wake Twitter

Congratulation President-Elect and people of America for a democratic election,I assure and people of Tanzania for a continued friendship.
— Dr John Magufuli (@MagufuliJP) November 9, 2016

Maskini: Yule Mtoto Aliyepandikizwa Betri Moyoni Afariki Dunia

$
0
0
Mtoto Happiness Josephat (6) aliyefanyiwa upasuaji wa kupandikiza betri moyoni katika Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), amefariki dunia.

Mama mzazi wa Happiness, Elitruda Malley amesema Happiness alifariki dunia ghafla juzi mchana.

Alisema   Jumapili, mtoto huyo alikuwa mzima na walikwenda kanisani kutoa sadaka ya shukrani kama ishara ya kumshukuru Mungu kwa mambo aliyowatendea na wakarudi nyumbani salama.

“Jana tumeamka vizuri lakini ghafla hali yake ilibadilika akaanza kulalamika kuwa anajisikia vibaya, tukamkimbizia Hospitali ya Selian hapa Arusha lakini tukiwa njiani alifariki dunia,” alisema.

Elitruda alisema kifo cha mwanawe kimemhuzunisha mno na  daima atamkumbuka.

“Alikuwa tayari amesharudi shuleni, alikuwa akiniambia kuwa atasoma kwa bidii ili ndoto yake ya kuwa daktari bingwa itimie aweze kusaidia watu wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali,” alisema.

Hata hivyo, alisema maziko ya Happiness yanatarajiwa kufanyika leo huko Mbulu mkoani Manyara.

Mkurugenzi wa JKCI, ambako Happiness alifanyiwa upasuaji, Profesa Mohamed Janabi amesema taarifa hiyo imemshtua ikizingatiwa mtoto huyo alikuwa anaendelea vizuri.

“Sikuwa na taarifa, nitawasiliana na mama yake   tujue hasa shida gani ilitokea, maana zipo sababu nyingi labda alipita jirani na mitambo ya umeme au simu, hizo ni sehemu hatarishi kwa mtu aliyewekewa betri kwenye moyo,” alisema.

Happiness alifanyiwa upasuaji huo wa historia nchini Julai 15, mwaka huu katika Taasisi ya JKCI wa kuwekewa betri maalumu kwenye moyo ambayo kitaalamu inaitwa ‘pacemaker’.

Kwa mujibu wa madaktari waliokuwa wakimtibia mtoto huyo, wakati alipopekekwa hospitalini hapo, mapigo yake ya moyo yalikuwa 20.

Walisema  hali hiyo kwa mtoto si ya kawaida kwa vile  anapaswa kuwa na wastani wa mapigo 60 hadi 100 kwa umri wake.

Mtoto Happiness alizaliwa na tatizo hilo ambalo mara nyingi hali hiyo huwakumba watu wazima.

Moja ya ndoto za mtoto huyo ambayo alinukuliwa akiisema ni kuwa daktari bingwa wa kutibu magonjwa mbalimbali.

Martin Kadinda Amkana Wema Sepetu..Adai Yeye Sio Meneja Wake Toka 2014

$
0
0
Mbunifu huyo wa mavazi ameiambia Bongo5 kuwa kwa sasa yeye na Wema Sepetu ni kama kaka na dada na sio meneja wake tena.

“Mimi kum-meneji Wema nimemaliza kama miaka miwili iliyopita, mkataba uliishia hapo, lakini tukasimama kama mtu na kaka yake,” alisema Martin. “Kwa hiyo umeneja ule wa ukaka na udada upo mpaka tunaingia kaburini lakini kama umeneja wa mkataba uliisha na ukabaki ule umeneja wa imani baada ya kuaminiana,”

“Tuliona hakuna umuhimu wa kuwa na mikataba kwa sababu tayari tumeshaaminiana, kwa sababu sasa hivi mimi Wema nimeshamchukulia kama ndugu yangu na yeye kama kaka yake. Kwahiyo kugombana kupo lakini baadaye mnawekana sawa na maisha yanaendelea,”

Aliongeza,
“Ukaribu wa mimi na Wema umepungua kwa sababu mimi kwa sasa nafanya mambo yangu na yeye anafanya mambo yake kwa sababu zamani Wema alikuwa anafanikiwa sana nakuniacha mimi nikiwa pale pale, kwa hiyo sasa hivi kila mtu anafanya mambo yake hatuwezi kuwa tunajenga kwake halafu kwangu kunaungua,”

Katika hatua nyingine mbunifu huyo wa mavazi amewataka mashabiki wake wa fashion kusubiria mambo mazuri kutoka kwake.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images