Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

Vanessa Mdee Kuja na Reality Show yake Kupitia Youtube

0
0
Katika kutengeneza muitikio mzuri zaidi wa album yake ya kwanza na inayosubiriwa kwa hamu, Money Mondays, Vanessa Mdee amepanga kuja na reality show.

Show hiyo itakuwa ya dakika moja tu na itatoka kila wiki kupitia channel yake ya Youtube. Ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa tuzo za Youtube kwa nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara.

Kwa muda sasa Vee amekuwa akizungumzia ujio wa album hiyo itakayoshirikisha mastaa wa ndani na nje ya Afrika.


Tazama Video Mpya ya Msanii Wildad Kutoka Lebo ya The Industry iliyo Chini ya Navy Kenzo

0
0
Lebo ya The Industry iliyo chini ya umiliki wa kundi la Navy Kenzo imeachia ngoma nyingine ya msanii wao Wildad iitwayo Get It On.

Wimbo unapatikana Mkito na unaupata hapo chini.
Bonyeza HAPA


Msanii huyo wa RnB amekuja kuteka mioyo ya kina dada kwa muonekano na sauti yake ambayo ni kivutio kikubwa katika kuimba kwake.

Akizungumza mara baada ya kuachia wimbo huo kwenye ofisi za Mkito, Masaki jijini Dar Wildad amesema, “Nimekuja kuleta ladha mpya ya RnB na kipaji changu ni cha kipekee na lengo kubwa la ni kuvuka mipaka”.

Wildad alijiunga na “The Industry” May mwaka huu wa 2016 na ngoma yake pamoja na video vinaashiria kuwa ana matarajio makubwa ya kuifikisha RnB ya Tanzania kwenye matawi ya juu.

Itazame hapa video yake.

Shilole Ampongeza Nuh Mziwanda baada ya Kufunga ndoa Kimya Kimya

0
0
Shilole amempongeza Nuh Mziwanda kwa kuongeza idadi ya wasanii walioukimbia ukapera baada ya kufunga ndoa kimya kimya na mpenzi wake Nawal.

Kupitia mtandao wa Instagram, Shilole ameandika ujumbe unaosomeka, “Hongera Nuh Mwenyezi Mungu awatie baraka tele kwenye ndoa yenu.”

Hitmaker huyo ameungana na mastaa wengine waliofunga ndoa mwaka huu akiwemo Mwana FA, Shamsa Ford, Nyandu Tozzy, Tunda Man, Mabeste na wengine.

Nuh na Shilole waliwahi kuwa wapenzi kwa muda mrefu lakini mwishoni mwa mwaka jana waliachana huku kila mmoja akianzisha mahusiano mapya.M

Hakeem 5: Ali Kiba Ana Roho Mbaya, Siwezi Kumuomba Msamaha

0
0
Msanii wa kitambo wa bongo flava, Hakeem5 akiulizwa kuhusu ushauri aliopewa na Abby Skills kuhusu kumuomba msamaha Ali kiba amedai katu hawezi kufanya jambo hilo
Amesema yeye aliongea ukweli kuhusu Ali Kiba na ukweli sio lazima umfurahishe kila mtu.
Pia ameongezea Ali Kiba ana roho mbaya na hata kolabo alilofanya na Abby Skills ilitokea tu baada ya yeye Hakeem5 kuongea

Tazama Video Mpya ya Wimbo wa Rosa Ree Kutoka The Industry iliyoko Chini ya Nahreel

0
0
Rapper Mkali wa Kike kutoka Tanzania Rosa Ree Aliyoko chini ya lebo ya Mziki ya The Industry siku ya leo ameachia Rasmi wimbo wake wa Kwanza unaoitwa One Time, Nimekuwekea Link ya Kudownload Wimbo Huo Hapa chini na Video:

DOWNLOAD AUDIO HERE

Alikiba Atoa Tamko, Awataka Mashabiki Waache Kumtukana Wizkid Aseme yeye ni Shabiki wa Wizkid

0
0
Hatamae Alikiba ametoa tamko rasmi kuwataka mashabiki wake kuacha kumtukana Wizkid kwenye mitandao , hii imetokana na alikiba kupewa tuzo ya MTV Ema aliyokuwa amepewa mwanzo Wizkid
Mashabiki hao walivamia ukurasa wa Wizkid na kuporumosha matusi mazito.

Ameandika Haya:

I am not happy with what has been going on, on social media . I have a great appreciation for @wizkidayo as a fellow artist and as a fan . I am very disappointed and saddened by the insults and attacks directed at him, and I want to be very clear that I condemn this behaviour and I believe none of my true fans are part of this irrational silliness and stupidity as they know I have always had love for @wizkidayo
Drown out the noise from the haters bro, congratulations on your very successful year. Much love from my real fans and from Tanzania 🇹🇿 Pamoja #KingKiba

Amber Lulu: Sijiachii Utupu Ili Nitamaniwe

0
0
MWANAMITINDO ambaye pia ni muuza nyago kwenye video za Kibongo, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ ameweka wazi juu ya picha anazoposti kwenye mitandao ya kijamii zinazomuonesha akiwa nusu utupu kuwa haweki hivyo kutamanisha wanaume.

Akizungumza na Global TV Online kupitia kipindi cha Exclusive Interview mchana wa leo, Amber ambaye ametokea kwenye video kibao za Kibongo ikiwemo Too Much ya Darassa na Inde ya Dully alisema, wapo watu wengi wamekuwa wakimtumia meseji kwa kumtamani kisa wameona picha zake.

“Mi naposti kwa ajili ya biashara za nguo, navalishwa na kampuni then ninapoposti nguo ile inakuwa sokoni sasa kuna watu wengine wanakuja juu kwa kunitamani sa nawashangaa huko kunitamani vipi?,” alisema Amber.

Amber pia alizungumza juu ya mastaa aliotoka nao kimapenzi hadi sasa na kusema kuwa wanazidi 100

Q-CHIEF Adai Patoranking Kasababisha Mpango Wake wa Kuoa Hivi Karibuni Usogee Mbele

0
0
Msanii mkongwe katika tasnia ya bongo fleva Q Chief amefunguka na kusema kuwa haikuwa jambo dogo na jepesi kufanya collabo na msanii Patoranking kutoka nchini Nigeria.

#Chillah amedai kuwa pesa nyingi zimetumika kufanikisha collabo hiyo kiasi cha kufanya hata mpango wake wa kuoa usogee mbele.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo cha East Africa Radio Q Chief anadai kuwa pesa za kutosha zilitumika jambo ambalo limefanya ashindwe kutimiza ahadi yake aliyowahi kuitoa kuwa ataoa siku za karibuni.
.
“Kiukweli namshukuru sana Qs Mhonda kwani alisimamia hili, kiukweli pesa ya kutosha imetumika kukamilisha kazi hii, hivyo haikuwa rahisi mimi kufanya na #Patoranking maana wenzetu wanaangalia wapi wametoka na wapi wanataka kwenda, wanafanya kazi na nani kwa maslahi gani, hivyo kabla ya kufanya kazi na wewe wanafanya utafiti wa kutosha, hata yeye alijaribu kunitafuta kwenye mitandao, na kuona kazi zangu akaona nafanya nini, aliangalia kama niko marketable baada ya hapo aliporidhika tukafanya kazi” alisema QChief

Zitto Kabwe: Marehemu Samweli Sitta Amenilea kwa Kunisomesha

0
0
Alfajiri ya tarehe 7 Novemba 2016, tunaamka na kukutana na habari za kusikitisha kuwa Mzee Samwel John Sitta, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangulia mbele ya haki. Babu alikuwa mgonjwa kwa kitambo kidogo akisumbuliwa na saratani ya tezi dume.
Majonzi ni makubwa kwa Taifa kutokana na sababu kubwa kwamba Samwel John Sitta alitumikia nchi yetu kwa muda mrefu na kwa uadilifu mkubwa.

Sisi wengine pia kwa kiasi fulani kukua kwetu kisiasa kumetokana na utumishi wake uliotukuka kwa nchi yetu alipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika tanzia hii ninamkumbuka Mzee Sitta Kwa namna nilivyofahamiana naye binafsi na namna nilivyomshuhudia katika kazi zake.

Sitta ananigusa mimi binafsi moja kwa moja. Alikuwa babu yangu. Tukiwa bungeni akiniandikia kitu alikuwa akitumia neno hilo “babu” kwa mwandiko wake mzuri usiotoka kwenye kumbukumbu zangu kabisa.

Aliniapisha kiapo cha ubunge Desemba 29, 2005. Maneno ambayo aliniambia baada ya kunikabidhi Kanuni za Bunge na Katiba ya Nchi niliyaandika kwenye daftari langu la kumbukumbu siku hiyo hiyo jioni.

Baada ya kula kiapo cha utii na cha uaminifu kawaida wabunge hupewa mkono na mwapishaji na kupewa nyaraka za kazi. Kwa upande wangu Mzee Sitta alinikumbatia na kuniambia, “utakuwa kiongozi muhimu sana kwa nchi yetu. You have a bright future.”

Maneno haya hayajawahi kutoka katika kumbukumbu zangu na kila nikipata misukosuko yangu kisiasa huyakumbuka na wakati mwingine yeye mwenyewe alikuwa akinipigia na kunikumbusha na kunitia moyo. Babu alikuwa mlezi wa wanasiasa vijana.

Sitta pia amenilea kwa kunisomesha. Mwaka 1996 nilikuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Galanos jijini Tanga nikisomea mchepuo wa Historia, Jiografia na Uchumi (HGE).

Hali ya hewa ya Tanga haikunipenda, hivyo nikawa naumwaumwa sana. Pia nilitaka kusoma Hesabu badala ya Historia. Wakati wa likizo ya Desemba mwaka 1996, nilitoka Tanga nikaenda Dar es Salaam, Wizara ya Elimu kuomba uhamisho kwenda shule yenye Somo la Hesabu, kidato cha Tano na Sita. Nikakataliwa. Lakini nikaambiwa kuwa Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari wakati huo Bwana Ndeki alisoma na Samwel Sitta.

Kipindi hicho Mzee Sitta akiwa Mkurugenzi wa Investments Promotion Centre (IPC) kabla haijabadilishwa jina kuwa Tanzania Investments Centre (TIC). Nikaenda Ofisi za IPC mahali ambapo leo ni CRDB Tawi la Azikiwe.

Nilipofika Katibu Muhtasi wake akaniuliza kama nina miadi na bosi wake, nikasema hapana. Akaniambia hawezi kukuona. Nikasisitiza sana na kumlilia dada yule aniruhusu dakika chache tu. Akaniruhusu.

Nilipofika Mzee Sitta aliniuliza shida zangu kwa heshima kubwa. Nikamwambia kwamba ninataka kuhama shule. Akaniomba matokeo yangu ya Kidato cha Nne, nikampa maana nilikuwa natembea nayo. Alipoyasoma akaniambia, “wewe hupaswi kuhangaika kutafuta shule maana kwa matokeo yako unaweza kusoma shule yoyote nchini ya chaguo lako”. Akainua simu akampigia Bwana Ndeki. Kisha akaniandikia kikaratasi niende wizarani muda uleule. Nilipofika wizarani nikapewa uhamisho kwenda Shule ya Sekondari Mazengo.

Nilipotoka nje ya wizara nikakutana na kijana mwingine anaomba uhamisho, yeye anatoka Mazengo anataka kwenda Tosamaganga, Iringa. Akaniambia, achana na Mazengo hakuna mwalimu wa Uchumi na hali ya vyoo ni mbaya sana. Nikarudi kwa Mkurugenzi. Mzee aliyenipa uhamisho aliponiona narudi na kumwambia sitaki Mazengo akachukua fomu zangu za uhamisho na akachukua ‘whiteout’ akafuta Mazengo na kuweka Tosamaganga huku akisema kwa hasira “ nyie watoto wa wakubwa bwana”. Sikujali nikaenda zangu Tosamaganga kusoma Economics, Geography na Mathematics (EGM).

Sitta akaendelea kufuatilia maendeleo yangu shuleni na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi ya InWent nchini Ujerumani.

Nilipotoka Ujerumani kusoma masomo ya Juu ya Biashara ya Kimataifa mwaka 2004 ilipaswa niwe na mradi wa kitaaluma. Nikachagua kuunganisha kampuni za Kijerumani na Tanzania kwa kuandika mradi wa kuchukua wafanyabiashiara 20 kutoka Tanzania na kuwaunganisha na wengine 20 kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya.

Ilibidi kupata Taasisi ya Tanzania kwa ajili mradi huo na Mzee Sitta akawa mstari wa mbele kuhakikisha mradi unafanikiwa na tukautekeleza kwa umakini kwa msaada wa ofisa wa TIC aitwaye Phina Lyimo.

Mwaka mmoja baadaye tukakutana na Mzee Sitta bungeni, yeye akiwa Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki na mimi nikiwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini. Ulezi wake ukaendelea mpaka mauti yalipomkuta leo mapema asubuhi (jana). Nimempoteza babu mlezi.

Sitta alikuwa mwana mageuzi (reformer) na kupitia uanamageuzi wake alifanya mabadiliko makubwa sana katika uendeshaji wa shughuli za Bunge. Sisi tuliohudumu kwenye Bunge la Tisa, tukimwita Spika wa Viwango na Kasi, tuliona wenyewe juhudi zake za kuliweka Bunge katika nafasi yake ya Kikatiba. Licha ya kuhakikisha kuwa maslahi ya Wabunge yanalingana na hadhi ya Bunge, alihakikisha pia kuwa Bunge linaisimamia Serikali sawa sawa. Haikuwa kazi rahisi sana kwani kulikuwa na mvutano mkubwa sana kati ya Spika Sitta na Waziri Mkuu Edward Lowasa katika kuleta mabadiliko hayo.

Tulikuwa tunaambiwa kuwa mvutano huo ulitokana na tetesi kwamba Sitta ndiye alipaswa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na hivyo kuwa na msuguano na aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo. Si Sitta wala Lowasa ambaye alithibitisha ama kukanusha tetesi hizo. Sitta ametangulia mbele ya haki, labda Edward Lowasa ataweza kusemea hili siku za usoni.

Sitta alitumia fursa ya msuguano huo kufanya mabadiliko makubwa ya kanuni za Bunge na kutoa uhuru mpana wa mawazo ndani ya Bunge na kuhakikisha kuwa taarifa za Kamati za Bunge na hususani Kamati za Usimamizi wa Serikali zinasomwa na kujadiliwa ndani ya Bunge kwa mujibu wa Kanuni.

Wakati wa Bunge la Nane, Taarifa za CAG hazikuwahi kusomwa hata mara moja. Ni kutokana na mabadiliko haya ya kanuni ndipo Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (Poac ) ilianzishwa Machi, mwaka 2008.

Nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa kamati hiyo na kuingia kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge ambayo kipindi hicho tuliiona kama kamati ya wabunge wazee. Namna nilivyoingia kuwa Mwenyekiti wa Poac nayo ni hadithi nyingine ya namna ya malezi ya kiuongozi yaliyofanywa na Spika Sitta.

Sikuwa nimejaza fomu kuomba Kamati ya Poac. Wakati huo ulikuwa ni wakati wa vuguvugu la Buzwagi (Mkataba wa Madini uliosainiwa na Waziri wa Nishati hotelini nchini Uingereza kwa siri ). Nilikuwa mjini Bagamoyo kwenye kazi za Kamati ya Bomani nikiwa na Harrison Mwakyembe na Ezekiel Maige.

Spika wa Bunge akanipigia simu, akaniambia “Babu, kesho kuna uchaguzi wa Kamati za Bunge. Nimekuteua Kamati ya Poac ambayo ni kamati mpya itakayokuwa chini ya Kambi ya Upinzani. Najua hukuomba kuwa mjumbe wa kamati hii, lakini nahitaji damu changa kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge. Naomba unikubalie na kesho uwepo Dar es Salaam kwa ajili ya uchaguzi na ugombee. Utashinda maana nimeshafanya kazi yangu”. Sikuwa na namna ya kukataa japo nilitaka sana kuendelea kuwa Kamati ya Fedha na Uchumi chini ya Abdallah Kigoda, ama Kamati ya Nishati na Madini chini ya Mzee William Shelukindo.

Ombi la Mzee ni amri. Nikawa Mwenyektii wa Poac na kuwa mmoja wa washauri wakuu wa Spika wa Bunge. Kamati ya PAC ikawa chini ya Mzee John Cheyo na Kamati ya Laac ikawa chini ya Dk Wilibrod Slaa. Ilikuwa ni Bunge lenye meno kweli kweli.

Spika Sitta alikuwa mbabe. Ubabe wake ulimsababisha kufanya maamuzi ambayo wakati mwingine yalimweka kwenye matatizo na wananchi. Mfano mzuri ni suala la Hoja Binafsi ya Buzwagi na Hoja ya Wizi wa Fedha Benki Kuu ( Epa). Mwanzoni, Spika alikuwa upande wa wabunge wenye hoja hiyo yaani mimi na Dk Slaa kiasi cha kuziboresha hoja zile kwa kalamu yake mwenyewe. Wabunge wa chama chake hawakuwa wanapenda hoja hizi na hivyo Waziri Mkuu Lowasa akamweka kwenye wakati mgumu sana wa kuegemea upande wa Serikali. Hoja ya Dk Slaa akaitupa kuwa ‘ ni makaratasi ya kuokoteza’. Hoja yangu akaiingiza bungeni na akasimamia kusimamishwa kwangu bungeni. Wananchi walimkasirikia sana.

Siku moja usiku, nikiwa nyumbani kwa Freeman Mbowe Mikocheni, Sitta akanipigia simu kulalamika kuwa wafuasi wangu wanamtukana kwa meseji. Akaniambia niwakataze. Nilimkubalia tu, lakini sikuwa na uwezo huo. Nchi ilikuwa imevimba. Ilikuwa Oktoba 2007, Sitta alijua namna ya kusoma nchi na kuwapa watakacho, wakati mwingine. Mwezi Novemba, katika kujibu kiu ya wananchi kuhusu uwajibikaji na kufuta makosa ya Buzwagi na Epa, Spika alisimamia kuundwa kwa Kamati Teule kuchunguza suala la Mkataba wa Richmond. Yaliyofuata yalikuwa historia. Taarifa ya Kamati Teule ilisababisha ‘kuanguka’ kwa Serikali kwa mara ya kwanza katika hsitoria ya Tanzania, Waziri Mkuu Lowasa alilazimika kujiuzulu ndani ya Bunge, Baraza la Mawaziri likavunjika na Serikali mpya kuundwa chini ya Mizengo Kayanza Pinda.

Spika Samwel Sitta akawa ni Spika pekee wa nchi yetu aliyeshuhudia uundwaji wa Serikali mbili ndani ya miaka mitano ya uspika wake. Mzee Msekwa yeye alikaa miaka 10 na Waziri Mkuu mmoja, ingawa mwaka 1993-1995 naye aliona mabadiliko ya mawaziri wakuu, kutoka John Malecela kwenda kwa Cleopa Msuya. Baada ya kujiuzulu kwa Lowasa, Samwel Sitta hakurudi nyuma tena. Aliendelea kuwa Spika wa Viwango mpaka alipomaliza muda wake katika Bunge la Tisa.

Spika Sitta alikuwa mwepesi kuomba msamaha alipokosea. Nakumbuka siku moja mwaka 2009 alimfukuza bungeni mzee mwenzake John Cheyo kwa makosa ambayo Cheyo hakufanya. Baadhi yetu tukakasirishwa sana na kitendo kile. Nikaenda kumwona Mzee Sitta ofisini kumwuliza kulikoni amdhalilishe mwenzake namna ile. Akanieleza kuwa hakuwa sawa na atamwomba radhi John Cheyo. Tukiwa kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge kwa ajenda za kawaida tu, Mzee Sitta akamwomba radhi Mzee Cheyo.

Nikikumbuka kisa hiki nacheka sana maana Jaji Werema aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alicheka mpaka kuanguka chini. Sababu? Mzee Sitta aliketi kwenye kiti chake, wenyeviti wote wa kamati tukiwa tumetulia tuanze kikao. Mzee Sitta akasema, “John, naomba radhi kwa tukio lililotokea bungeni wiki iliyopita. Sijui nilikuwa nina nini siku hiyo, nadhani nilisumbuliwa na watu wanaopitapita jimboni kutaka kunitoa, nisamehe mzee mwenzangu”. Kicheko ukumbi mzima na Cheyo akamkubalia radhi yake huku naye akicheka na yakaishia hapo. Wazee hawa wawili wameandika pamoja kitabu, ‘Bunge lenye Meno.’

Nimwelezeje zaidi Babu? Nimwelezeje zaidi Spika wa Kasi na Viwango Samwel Sitta? Mwanasiasa shupavu, jasiri, mwenye ngozi ngumu, mbabe, mnyeyekevu inapobidi na mwenye uthubutu. Tangulia Babu. Tangulia Mtemi wa Unyanyembe Samwel John Sitta. Umeondoka duniani lakini bado unaishi kupitia kazi zako kwa nchi yetu.

Mwandishi wa makala haya ni Kiongozi wa ACT- Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini.

Wizkid Amtolea Uvivu Shabiki wa Tanzania Aliemtukana Instagram

0
0
Baada ya Mtv ema kumpatia Alikiba tuzo ya african act kutoka kwa Wizkid ,mashabiki wa Tanzania hasa wa Alikiba wamevamia ukurasa wa Instagram wa star huyo wa Nigeria na kumtukana.
Leo Wizkid ameshindwa kuvumilia baada ya shabiki mmoja kumtukania mama yake.

Mange Kimambi na Ndoto yake ya Kugombea Ubunge 2020..Afunguka Haya Pamoja na Kutochukua Uraia wa Marekani

0
0

Akijibu hoja ya kwa nini hachukui uraia wa USA,Mange kupitia ukurasa wake wa Instagram alijibu anaogopa kuukana uraia wa Tanzania kwani atapoteza ndoto yake ya kugombea ubunge 2020
Soma Alichoandika Hapa Chini:

Mwanamuziki TID Awashukia Clouds FM...Adai Kuwashitaki Wamlipe Milioni Mia Tano

0
0
 Mwanamuziki TID inaonekana amejiunga na Vita iliyoanzishwa na Lady Jay Dee dhidi ya Radio Clouds FM Baada ya makala moja kutoka huku ikisema kuwa Album ya TID iliyomtoa Sauti ya Dhahabu kuwa alifanywa na Clouds FM


HII NI DHULUMA YA WAZI WAZI HUU WIMBO UMEFANYIKA KWELI CLOUDS MALIPO YOTE YAMELIPWA CLOUDS....BRAZA RUGE NAOMBA HELA ZANGU hivi Clouds FM mshawahi Kutenengeneza Zeze Song. .!? I WANT MY MONEY SHOW ME CONTRACT naomba Haki Yangu Sikuogopi I want Clouds FM kwa Kudanganya hivi wanilipe Milioni Mia Tano ....Ushapata Pesa Nyingi Sana Hauna Haja ya kuendelea,My Legal Team is Ready to Bring this Fake Institution Down

Akaongeza Kwa Kuandika

"MY Mentor @majani187 in any other way did you Produced this Song in clouds Fm Studio?....? Mimi nataka kulipwa Haki Yangu siwezi kukubali"

Maandamano ya Kumpinga Trump Yaingia Usiku wa Tatu

0
0
Maandamano yameendelea nchini Marekani dhidi ya Donald Trump katika miji kadhaa ya Marekani kwa usiku wa tatu mfululizo.

Mjini portland katika jimbo la Oregon polisi walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya mamia ya waandamanaji waliyokuwa wakiandamano kutoka kila upande wa barabara za mji huo.

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Vanderbilt mjini Tennessee, wamekuwa wakiimba nyimbo za uwanaharakati wa kutetea mageuzi na kufunga barabara ya Nashville kwa mda.

Maandamano hayo hata hivyo yalikuwa ya amani huku mengine zaidi yakitarajiwa kuendelea katika jimbo la chicago baadaye leo.

Kibonge Sexy: Mi na Chid Benz Tumebaki Marafiki Tu...Naposti Picha Nusu Utupu Kwa Ajili ya Biashara

0
0
ALIYEKUWA demu wa staa wa Hip Hop, Rashid Makwiro ‘Chid Benz’, Bhoke ‘Kibonge Sexy’ kwa mara ya kwanza amefungukia uhusiano wao kuwa kwa sasa hawako kimapenzi kama zamani.

Akichonga na Global TV Online leo, Bhoke ambaye pia ni mwanamitindo na video queen mnene kuliko wote Bongo alisema, ni muda mrefu tangu awe na Chid kimapenzi na kilichobaki kwa sasa ni urafiki tu.

“Umebaki urafiki wa karibu, wa kumjulia hali na kuzungumza naye tu lakini si wapenzi tena,” alisema Kibonge Sexy.

Kibonge Sexy aliongeza tena, katika maisha yake hamuogopi mtu hivyo anavyoposti picha za nusu utupu anafanya biashara za nguo na hata kaka zake wawili wanajivunia na kutambua kitu gani anakifanya.

Michirizi Inayoonekana Kwenye Miili ya Akina Dada Inaashiria Nini?

0
0
Hivi Ile michirizi inayoonekana kwa baadhi ya kinadada nyuma ya goti wakiwa wamevaa sketi fupi huwa ni ishara ya utamu wao kama Mwana FA alivyoimba  "Michirizi ya utamu nyuma ya goti mimi hoi na moyo hai sio toi " au ugonjwa wa ngozi?



Mange Kimambi Atoa Ushauri Kwa Wasanii Kuhusu Unyonyaji Unaosemekana Unaofanywa na Clouds FM Kwa Wasanii...

0
0

Mange Kimambi Amefunguka na kuwashauri wasanii wa Bongo Flava kuhusu Radio Clouds FM ambayo wasanii wengi wamekuwa wakilalamika chini chini kuwa inawanyonya, ameandika haya hapa chini:


Mange Kimambi
"I love how Ruby @iamrubyafrica anajitahidi kuwa shujaa na ku-survive bila clouds but ukweli ni kwamba mwisho wa siku atashindwa tu na atashuka tu kimziki Kama inavyokuwa kwa Jide..... Tena Huyu anaweza kupotea kabisaaaaa kwenye anga ya muziki.....
.
.
Ruby hawezi kushindana na giant Kama Clouds. Jide mwenyewe na umaarufu wake na u-legend wake Clouds wanam-maliza kidogo kidogo..Yani Jide isingekuwa kwamba she is a legend tungekuwa tumeshamsahu. Ni vile she is too big to easily take down....
.
.
Nawarudi Tena clouds itaendelea kuwaonea wasaniiii wa Tanzania for as long as mkiendelea kutengana hivi.hakuna msaniii mmoja atakaewaweza clouds.Na tatizo linakuja kwamba wale ambao sasa hivi wako poa na clouds hawataki kusaidiana na wenzao ambao sasa hivi wanaisoma namba. Hawajui kwamba kuna siku na wao yatawafikaaaaaa..... Mfano mzuri Dina Marios, wafanyakazi kibao pale clouds walifanyiwa alichofanyiwa yeye Ila yeye akawa busy anacheka na mabosi hakujua kuna siku itafika zamu yake. Na ilipofika kalia lia insta na hakuna aliemsaidia.
.
.
Wanamuzidi wa TZ inabidi muamke now.Tatizo hamjaijua nguvu yenu, mnadhani clouds Ina nguvu Hapana nyinyi ndo mnaeipa clouds nguvu. Ukisikiliza clouds asubuhi mpaka usiku, 90% ya mziki unaopigwa ni bongo flava, mahojiano ni 100% bongo flava artists, Fiesta Yao ni 100% bongo flava artists. Sasa hamuoni kuwa nyinyi ndio kiini cha clouds??Without you clouds is nothing. But lazma muwe kitu kimoja. Clouds inatakiwa iwaheshimu Kama mnavyoheshimiwa na Efm au east Africa radio.
.
.
Nawahakikishia wasanii wa Tanzania Asilimia 90 tu mkigoma ngoma zenu kupigwa clouds au ku-perform fiesta au kuhojiwa na Kina soudybrown basi clouds is dead. Watabaki na wanamuziki wao wa THT na Diamond.. redio haitoendeshwa na wasaniii hao tu.Diamond mwenyewe kashikwa na Ruge, pesa yake kubwa inaliwa na Ruge.hao kina Babu Tale sijui Salaam ni wauza sura tu, real manager wa Diamond is Ruge.So Diamond msimtegeee kwenye huo mgomo..Mi nawaambia hivi hamjaijua nguvu yenu, wagomeeeni wiki 2 tu ngoma zenu zichezwe Efm na radio zingine tu, wao clouds wapige ngoma za Dai na THT, na fiesta mgome wote kuperform muone kama Ruge hatokuwa muungwana....

Wasaniii wa Tanzania inabidi muutilie manani ule msemo unaosema , the enermy of my enermy is my friend. Kwa Kiswahili ni kwamba ' Adui wa adui yangu ni rafiki yangu.... Adui makubwa mkubwa wa clouds kwasasa hivi ni Efm so nyinyi lazma m-join forces na Efm in order kuwanyooosha clouds....
.
.
Ndio sio wasaniiii wooote watakaokubali kuwagomea clouds. Lazma kutakuwa na masnitchi wachache. hao wachache waacheni lakini wengi wenu angalau 80% yenu mkiwapa nguvu Efm, clouds wataomba pooo..... inabidi wasaniiiii mpunguze nguvu ya clouds... ngoma zenu zikipigwa Efm na ma interview yoooote ya umbea yakifanyika Efm wananchi wenyewe woooote wataanza kusikiliza Efm watahama clouds. Na clouds hawawezi kukubali kupunguza listeners wataomba poooo then mtafanya kazi kwa kuheshimiana.
.
.
You guys have to come together na muondoe kabisa huuu udikteta wa clouds....sijawahi kuona wala kusikia duniani eti radio station inaweza Kugoma kupiga nyimbo ya msaniii kisa hawampendi... hapa marekani ukiona radio imeacha kupiga nyimbo ya mwanamuziki flani ujue ni sababu ya wananchi Kama vile ilivyotokea kwa Chris brown radio na TV zilivyocha kupiga ngoma zake baada ya kumpiga Rihanna... Yani inabidi Mwanamuziki awe kakosea jamiiii nzima kwa kitu kikubwa na sio eti sababu bosi wa radio hampendi..... Its very stupid..... .
.
Inabidi muungane na mtuambie ni wasaniiii gani waliokataaa kujiunga na huo mgomo ili wananchi wawanyoooshe kwa kugomea show zao.....😂...... seriously hata wale ambao sasa hivi mnapendwa na mabosi wa clouds lazma muwasaidie wenzenu sababu na nyie kuna siku tu yatawakuta..
.
. . .
Yamoto band wenyewe wametendwa na Ruge. Wanamdai mamilioni. Ile kumdai Ruge kawapoteza kwenye ramani.... Yamoto band pia manager wao alikuwa Ruge , babu Tale anauza sura tu. Hana msaaniii yoyote anaem-manage... Yani ukiona msaniii eti manager wake ni Babu Tale au Salaam we jua ni msaniiii wa clouds....
.
.
Clouds FM is the CCM of the music industry.... The dictatorship has to end. Ni nyinyi wasaniiii wenyewe mtaoweza kuwanyooosha clouds" Mange

Boss Ananitaka Kingono, Nipo Njia Panda Naomba Ushauri

0
0
Katika harakati za kutafuta kazi nilibahatika kufika ofisi moja maeneo ya Mwenge (Dar es salaam) kwangu ilikua faraja kubwa sababu kiukweli nilikua nahangaika sana na hali ya ugumu wa maisha na sikutaka kabisa kuwa tegemezi kwa mtu yoyote (wakiwemo wazazi) niliamini kunipa elimu ni mtaji muhimu na tosha na lilikua jukumu langu kuandaa maisha yangu mwenyewe na kujitegema

Nilipofika pale niliomba kuonana na boss ila nikaambiwa haiwezekani labda ningekua na appointment, kutokana na uzoefu hii kauli nilikua nimekutana nayo mara kadhaa hivyo ilikua hainisumbui sana, nikamwambia yule receiptionist kuwa nilikua na appointment (kiukweli sikua nayo na nakiri nilidanganya na nilikosea ila sikuwa na namna mbadala) akaniuliza nimwambie we ni nani nikasema mwambie (tax consultant)

Waliongea mawili matatu then nikaruhusiwa kuingia nadiriki kusema shida ni mwalimu mkubwa sana kwani sikuwa na woga wowote kuonana na yeyote na kujinadi, baada ya mazungumzo na mahojiano ya kama dakika sita yule manager (mwanamke) akaniambia alhamisi niende nikafanye interview na kutokana na intro niliyoitoa hiyo siku (Jumanne).

Haikua kazi kwangu kupata hiyo kazi hata baada ya interview ya alhamisi, tulikubaliana terms za kazi na mshahara then nikapewa mkataba. Nilifurahi sana nikijua sasa mipango yangu itaenda vema (kwakweli mshahara ulikua mzuri tu) hadi nikaanza kupangilia biashara ndogondogo ili kuinua uchumi wangu.

Nilianza kazi wiki iliyofuata na wafanyakazi wenzangu walikua watu wema sana kwangu hivyo nilifanya kazi kwa furaha na ufanisi sana mpaka hali ilipokuja kubadilika.

MABADILIKO

Baada ya wiki moja mambo yalianza kubadilika pale ofisini, mara kwa mara boss alikua na vikao visivyokua na mbele wala nyuma na mimi na akawa mkali kwa wafanyakazi wenzangu especially wa kike na taratibu wakaanza kuniogopa.

Siku moja aliniita ofisini (ilikua Ijumaa) na akaniambia nifunge mlango nilishtuka sababu normally ukiingia ofisini lazima ufunge mlango cha kushangaza akaniambia ni-u lock nikafanya alivyotaka,

Hakuna cha maana alichoniambia zaidi ya story za kifamilia tu oooh mara mumewe (aliekuwa meneja kabla hajaumwa) anasumbuliwa na kisukari na presha na anapata taabu sana mi nikawa msikilizaji tu na aliongea muda mrefu hadi jua likazama na watu waliondoka ofisini alibaki mlinzi tu.

Aliongea mengi na mwisho akaniambia anataka nimsaidie (ngono) kitu ambacho kilinishtua kidogo ukizingatia ni mtu mzima rika la mamaangu, nilimbembeleza kuwa hapo si pahali salama ili tu aniache siku hiyo ili nikajipange jinsi ya kuepukana nae na kuikabili ile hali.

Alinikomalia sana hadi kunivamia physically na alionekana wazi alikua desperate for sex ila nilifanikiwa kumpanga na akanielewa baada ya hiyo siku ofisi nzima wakahisi nilizini na yule boss hivyo kukawa na minong'ono mingi na sikuwa na namna ya kuwaaminisha vinginevyo.

Tangu hapo ni wiki ya pili sasa huyu mama ananisumbua sana, ananiahidi mambo mengi kama nitakubali kusex nae na ni dhahiri nikimtamkia kuwa SITAKI nitapoteza kibarua kwani ye ndo meneja hapa na ndo anaajiri na kusitisha ajira,

Leo hii (Jmosi) kanipigia simu na kuniambia kesho saa saba ana kikao na mimi cha kikazi ila location naona hata aibu kuisema. Wakuu najua kuna watu humu wakike na kiume ambao wamekutana na hali kama yangu,

Naipenda kazi na sina pa kushikilia kwa sasa lakini pia sitaki kuisaliti imani yangu na msimamo kwa kupenda vitu vya dezo na kufanya uzinzi na mtu wa rika la mama yangu, ni dhambi kubwa na pia ni kinyume cha maadili ya jamii yetu lakini pia nikifikiria matokeo ya kuachishwa kazi (na mipango niliyokwisha iweka kichwani kwangu) roho inaniuma sana nabaki nikiwaza na kuwazua bila kujua haswaa nishike wapi.

Msimamo wangu ni kutokulala na huyu mama no matter the consequences ila naomba mnipe chakula cha akili ili akinifukuza kazi basi niwe nimeimarika kisaikolojia kwa ushauri wenu na nisitetereke sana kisaikolojia.

Asanteni

Rapper wa Kike Chemical Adai yeye Bado ni Bikra Hajawahi Guswa na Mwanaume

0
0
Msanii wa kizazi kipya anaepeperusha bendera ya Tanzania kwa kupitia songi lake jipya linalokwenda kwa jina la "I'M SORRY MAMA" mwanadada Chemical, amesema yeye ni bikira(hakuwahi kujigi jigi tangu azaliwe).

Chemical ameongea hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha D'WIKEND CHATSHOW kinachorushwa kupitia clouds tv. Chemical ameongeza, licha ya kuwa bikira hajawahi kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja(ulesbian).

Vilevile ameongezea, yeye hana gharama kabisa, kwasababu hatumii mavitu ya gharama kama wadada wa mjini(hapaki miwanja, haweki manywele ya bandia, na makororo mingine ya thamani) ambayo wadada wa mjini wamekuwa wakitumia.

Pichani msanii chemical akiwa na msanii mwezake wa bongo muvi bibie wema sepetu

Nilifanya Collabo na AliKiba Nipate Ugali-Ommy Dimpoz Afunguka

0
0
Msanii Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa amerudi kwenye game na kolabo ya wimbo wa 'Kajiandae' aliyofanya na Alikiba tena, ametoa sababu ya kuamua kufanya tena kollabo na msanii huyo.

Akizungumza kwenye FNL ya East Africa Television na East Africa Radio, Ommy Dimpoz amesema mara ya kwanza alivyofanya kollabo ya Nai Nai na Alikiba ilikuwa ili atoke kimuziki, lakini kollabo ya sasa ni kama tu collabo zingine, na sio kumtumia kurudi kwenye game.

"Nai nai ilikuwa mimi nimemshirikisha Ali nilikuwa natafuta njia ya kuuona ugali, lakini sasa hivi tumekuja kama Ali na Ommy kazi ya pamoja, mimi nilikuwa zangu break, nimerudi kwa hiyo haijalishi nimeimba na nani", alisema Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz alishawahi kumshirikisha Alikiba kwenye wimbo wa 'Nai nai' ambao ndio ulimtambulisha kwenye ulimwengu wa bongo fleva, na sasa kaamua kurudi na kazi nyingine akiwa na alikiba pia, inayoitwa 'Kajiandae'.

Hii Ndio Kauli ya Basata Kuhusu Tetesi za Kuwepo Kwa Bifu Kati ya Alikiba na Diamond

0
0
Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) ambalo ni walezi wa wasanii pamoja shughuli za sanaa nchini, limekiri kusikia tetesi ya bifu inayoendelea kati ya mastaa wawili wa muziki nchini, Ali Kiba na Diamond.

Akizungumza na Bongo5 wiki hii, Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza amesema amesikia kuna bifu kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba lakini hawajapokea taarifa rasmi ambayo inaonyesha mmoja kati yao akilalamika kuhusu mwenzie.

“Kwa upande wa serikali au BASATA tunafanya kazi kwa kuzingatia maandishi au taarifa rasmi, kwahiyo suala kuwepo kwa kutokuelewana kati ya Ali Kiba na Diamond halijatufikia rasmi,” alisema Mngereza. “Huu ni ushabiki au mashabiki ndio wanaleta haya, kwa hiyo ni ushabiki wa team hii na hii na tunaliona. Lakini kwa kuwa halijaja rasmi likija rasmi tutalishughulikia,” aliendelea kuongeza Katibu huyo.

Aidha alisema, “Lakini tukikutana na wao wenyewe wapo safi, kwa hiyo wanaosababisha hivyo ni mashabiki kwa sababu hata wachezaji wa Simba na Yanga wale ni wachezaji wapo kwenye tasnia moja, ni marafiki wanakaa pamoja, wanakula pamoja ni kama wanamichezo wa ngumi, wewe ukiwa nje unaangalia wao wanapigana kweli lakini ule ni mchezo. Kwahiyo mimi hii naona ni ushabiki wa mashabiki ambapo kimsingi huwezi kuwazua. Pia ni kwa sababu hakuna aliyelalamika, kimsingi sisi ni walezi wa wasanii mmoja angelalamika sisi tungeuwita upande mwingine,”
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images