Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

Mbunge Godbless Lema Akipona Katika Hili Abadili Mbinu zake Katika Siasa

$
0
0
Siasa za kutengeneza matukio ya kujiongezea umaarufu zinaanza kumwendea vibaya Lema.

Idadi ya watu waliojitokeza mahakamani katika kesi ya Lema leo imekuwa ndogo sana ukilinganisha na uhamasishaji uliofanyika.

Picha zinazorushwa kutoka maeneo ya mahakama hazioneshi zile "nyomi" tulizozizoea pindi Lema anapopelekwa mahakamani.

Hata wanachama kindakindaki wanaofuatilia kesi hii kwenye mitandao kama Facebook wamekuwa wakimtaja Bananga pekee kama chanzo cha taarifa kutoka mahakamani.

Hata tukio linalopewa umaarufu la mwanamke anayedaiwa kuzimia linaripotiwa kwa picha inayoonesha watu wachache sana wakiwa na mama huyo.

Muda umefika Lema atathmini siasa zake zisije zikampa maumivu makali kuliko matokeo yaliyotarajiwa.

By THINKINGBEING

TID Aituhumu Clouds FM Kuuza wimbo ‘Zeze’ Marekani Bila Makubaliano (Video)

$
0
0
Msanii mkongwe wa muziki Khalid Mohamed aka TID ameingia kwenye mgogoro na kituo cha redio cha Clouds FM baada ya kukituhumu kituo hicho kimejiingizia fedha kwa kuhadaa wao ndio waliotayarisha wimbo wa Zeze.

Muimbaji huyo ametoa tuhuma hizo kupitia mtandao wa kijamii wa istagram pamoja na kuweka kielelezo cha kava ya CD ambacho amedai amekipata nchi za nje.

Kupitia instagram, TID alipost picha (hapo juu) na kuandika:
HII NI DHULUMA YA WAZI WAZI HUU WIMBO UMEFANYIKA KWELI CLOUDS MALIPO YOTE YAMELIPWA CLOUDS….BRAZA RUGE NAOMBA HELA ZANGU hivi Clouds FM mshawahi Kutenengeneza Zeze Song. .!? I WANT MY MONEY SHOW ME CONTRACT naomba Hakuna Yangu Sikuogopi I want Clouds FM kwa Kudanganya hivi wanilipe Milioni Mia Tano ….Ushapata Pesa Nyingi Sana Hauna Haja ya kuendelea,My Legal Team is Ready to Bring this Fake Institution Down


Bongo5 ilimtafuta TID na kuzungumza naye ili kujua ukweli kuhusu taarifa hizo na atachukua hatua gani ili kuisaka haki yake.

“Ile ni CD ambayo imeuzwa Marekani na duniani kote na yale ndio maelezo yake,” alisema TID. “Hiyo kazi ipo Mahakamani, naenda Mahakamani, kwahiyo nahitaji wanasheria ambao watapigana kupata haki yangu,”

Nilipumzika Muziki Kula Bata – Ommy Dimpoz

$
0
0
Msani Ommy Dimpoz amesahihisha mashabiki walipokuwa wakisema msanii huyo kafulia baada ya kukaa kimya muda mrefu kwenye game, na kusema aliamu tu kupumizka kwa muda na si kama alifulia.

Ommy Dimpoz akiwa na Rooney Visiwani humo
Akizungumza kwenye FNL ya East Africa Television, Ommy Dimpoz amesema watanzania wamekuwa na mtazamo tofauti sana hasa pale msanii anapokuwa kimya kwenye kazi zake, na kukimbilia kumlaumu.

“Mimi nilikuwa kimya nilikuwa nafanya mambo yangu mengine, lakini sio kama kukaa kwangu kimya nilikuwa nimepotea nimepotea kwenye muziki, unajua watanzania wamekuwa na tafsiri tofauti, kuna watu wanatake break kija Justin Timberlake wanakaa miaka 7 7, na mimi nilikuwa zangu vacation, ma Ibiza huko (Ibiza ni sehemu ambayo watu wenye mkwanja mrefu duniani ndio huenda kula bata), sasa nimerudi nataka kufanya kazi”, alisema Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz ambaye amerudi na ngoma mpya ya Kajiandae ambayo amefanya na Alikiba na tayari ameshaachia video yake, imepata ushabiki mkubwa mitandaoni kutokana na video yake.

Diamond Aonyesha Uwezo Mkubwa wa Kuimba Live Coke Studio, Tazama Hapa Wimbo Wake na Cassper Nyovest Ambao Umekuwa Gumzo

$
0
0
Diamond Aonyesha Uwezo Mkubwa wa Kuimba Live Coke Studio, Tazama Hapa Wimbo Wake na Cassper Nyovest  Ambao Umekuwa Gumzo

Tazama Hapa Video:

Video ya Wema Sepetu Akipeana Mate na Calisah Kitandani Yavuja..Itazame Hapa

$
0
0
Video imevuja ya mwadada Sepenga akifanya yake ,juzi kati alihojiwa juu ya mahusiano yake na Calisah alimkana akasema ni rafiki na hawajawahi fanya lolote, sasa leo Video imevuja huko instagram kila page inatembea anakiss na huyu dogo,huyu ndio Wema sepetu sasa sijui lini atatulia na kuacha mambo ya Skendo..


BONYEZA HAPA KUTAZAMA VIDEO

Alikiba Afunguka Kuhusu Ugomvi wake na Hakeem 5

$
0
0
Stori hii ilianza baada ya Abby Skills kusema Hakeem 5 lazima amuombe msamaha Ali Kiba ili wafanye kazi tena na mambo yake yaende sawa.

Ali Kiba alisema “Kuhusu Hakeem 5, naweza kusema kwanza ni ndugu yangu kama Abby Skills na wengine. Tunaheshimiana nae sana. Sina ugomvi nae, tumefanya kazi nae kwa mapenzi yote tulipokuwa lebo moja G-records

Kuhusu colabo na kutofanya video ya wimbo wa Hakeem 5 Kiba anasema “Ishu ipo hivi, nakumbukuka kabla sijapumzika kimuziki kipindi kile tulifanya kazi na Hakeem 5, nakumbuka ilikuwa inaitwa MADEBE. Baada ya kuitoa ilifanya vizuri, then nikaamua kupumzika miaka mitatu.

Niliporudi rasmi akanifata tufanye video! Nikamwambia kweli?? Upo serious! Yani nyimbo ina miaka, then tuifanye video kweli. Ni Unprofessional kwa kweli.”
Kuhusu kufanya nae colabo tena, Kiba aliniambia “Sitaki kufanya nae tena nyimbo, sijamkosea Hakeem lakini sitakuja kufanya nae kazi.”.

Install APP ya Blog Hii ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

$
0
0

Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 



Kundi la Kigaidi la ISIS Lapiga Marufuku Uvaaji was Chupi na Boxers Kwa Wanaume

$
0
0
Kile kikundi cha kigaidi kijulikanacho na kuogopwa kwa ukatili wa kutisha hili kuleta hofu kimeenda hatua zaidi mbele kwa kuweka sheria kali.

Wahuni hao Wamepiga marufuku uvaaji wa boxer na Chupi kwa wanaume kwasabab ni kimagharibi badala yake unatakiwa uvae bukta ndefu inayovuka magotini ama kitambaa unachojifunga kiunoni kama taulo. Na ukibainika kuvaa hivyo hatua kali itachukuliwa dhidi yako.

Wanajeshi wa Iraq na Kurd walishangaa kukuta mabandiko hayo yanayokataza uvaaji wa Chupi na Boxers walipoukomboa mji wa Hammam Al Allil kusini mwa Mosul dhidi yao.

Pia ISIS imepiga marufuku kunyoa ndevu, kusikiliza mziki na kuvaa jeans zilizobana.

Baraka Da Prince Anahitaji Msaada wa Haraka

$
0
0
MTOTO wa miaka miwili badala ya kusema kikombe akatoa tusi, hufai kumpiga wala kumgombeza. Unachotakiwa kufanya ni kumtia nguvu katika juhudi zake za kujifunza na kumwambia kwa usahihi neno kikombe linavyotamkwa. Hivyo ndivyo hata kwa mtu mgeni katika miji mikubwa.

Mshamba akitoa huko mashambani na kukutana na lifti  katika majengo makubwa na kutaka kuvua viatu kisha ndio aingie, ukimcheka utakuwa juha.

Sasa unamcheka nini na hayo mambo kwao hakuna? Unashanga kitu gani yeye kuvua viatu na kutaka kuingia katika lifti wakati huko kwao kafundishwa ni ustaarabu ukikuta maeneo nadhifu uvue viatu?

Nimetoa mifano hiyo nikikumbuka tabia ya msanii Baraka Da Prince. Kwa siku za hivi karibuni bwana mdogo amekuwa na matukio na kauli za ajabu na cha kushangaza watu wanamshangaa na wengine kumtolea maneno makali.

Ni kweli Baraka anafanya mambo ya kijinga, yasiyofaa kufanywa na mtu anayejitambua. Ila mimi sishangai hayo mambo kufanywa na mtu aina ya Baraka.

Yangefanywa na Diamond, Ali Kiba na akina Chegge  ningeshangaa mno. Nishangae vipi Baraka kuposti nyumba ya mama yake Naj na kusema ni yake wakati najua kijana wetu huyu bado hajatokwa matongotongo machoni?

Katu siwezi kushangaa na yeyote atakayemshangaa, nitamshangaa yeye. Ni jambo linalotarajiwa kabisa kwa kijana ambaye miaka mitatu nyuma alikuwa akishindia kababu na mihogo huku akiwa ndani ya kaptura chafu isiyojulikana rangi yake, viatu vilivyotoboka na akiwa anadhihakiwa na kila msichana anayejaribu kumchombeza, kuwafanyia unyama ndugu zake kisa kuwa na msanii Naj katika mapenzi.

Baraka ni kwanini asitokwe na akili kwa Naj wakati miaka mitatu iliyopita alikuwa akimuona bibie katika magazeti na majarida akiwa kakumbatiwa na Mr Blue, msanii ambaye Baraka huyu amekuwa akimuona toka kipindi anaomba Shilingi ishirini akanunue ice cream kwa mama John?

Siwezi kumlaumu Baraka. Kumlaumu Baraka kwa ujinga anaoufanya ni sawa na kulaumu mtoto mdogo anapotukana kipindi akijifunza kuongea.

Siku moja katika mitandao ya kijamii Baraka baada ya kuposti picha ya mpenzi wake, Najma Dustan, msanii mwenzake, mtoto wa mjini Msami akamtania kwa kujifanya anamtamani Naj.

Kilichotokea kiliniacha hoi kwa kicheko. Baraka akatokwa na matusi kwa Msami na kumwambia akamtamani dada yake.

Baraka anatupa maneno haya kwa mtu ambaye amekuwa akionekana katika video na magazeti kwa zaidi ya miaka sita sasa.

Anatokwa povu la kijinga kwa Msami kwa kudhani kuwa eti ni kweli anamtamani mpenzi wake huku akiwa amesahau ni Msami huyu ambaye aliwahi kudaiwa kutoka na mastaa wengine wakubwa wa Bongo.

Msami ni mtoto wa  mjini sana kuliko Baraka. Msami kaona mengi ya kimjini kuliko yeye. Kutoka  dansa hadi kuwa msanii mwenye kueleweka, Baraka anatakiwa ajue uzito wa Msami.

Yeye bado ni mgeni katika jumba la mastaa, anayofanya ni sehemu ya ulimbukeni wa kawaida kwa mgeni. Kumlaumu au kumkosoa sana ni kumkosea.

Anayofanya Baraka ni sawa na mtu ambaye hajawahi kumiliki au kuendesha gari zuri la thamani. Atatembea kila eneo kutaka kuonesha kuwa anaendesha gari zuri. Huu ni  ulimbukeni.

Muda ukipita atakomaa.

Nick wa Pili: Hatumminyi Lord Eyez, Bado Amesimamishwa

$
0
0
Nick wa Pili amekanusha madai yaliyowahi kutolewa na rapper Lord Eyez dhidi ya member wengine wa Weusi kuwa wamekuwa wakimminya.

Akizungumza na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, Nick ambaye ni msemaji wa kundi/kampuni hiyo, amesema Lord Eyez bado amepigwa benchi. “Kama umesimamishwa unawezaje kusema unaminywa? Yaani mwanafunzi kama umepewa suspension utasemaje tena shule inakuminya wakati wewe uko suspended?” amehoji Nick.

“Kila kitu kinaendeshwa kisheria, kwahiyo unaposema unaminywa kuna watu wanavunja sheria na yeye anaelewa kabisa kanuni na taratibu za kampuni, hakuna hata mtu mmoja aliyepo kwenye nafasi ya kuvunja sharia kumkandamiza mtu mwingine, kitu kama hicho hakiwezekani,” ameongeza rapper huyo.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, mwanzoni mwa October, 2016, Lord Eyez alisema akiwa mmoja wa waasisi wa kampuni hiyo, atakuja kueleza zaidi ya ndani yanayoendelea. Alidai kuwa makubaliano ya kampuni hiyo ni kuwa member asiyepanda kutumbuiza hapati mkate wake, na yeye kwakuwa hahusiki sana na show zao amekuwa akiambulia patupu.

“Kimuziki uhusiano wetu na Weusi mimi Joh Makini Gnako na Nick wa Pili tupo vizuri ila kwenye maslahi kuna kuminywa sana,” alisema. Rapper huyo aliyewahi kung’ara enzi za Nako 2 Nako, alipanda kwenye show ya Fiesta jijini Arusha baada ya kualikwa na Barakah Da Prince. 4

“Nilipanda na Barakah Da Prince kwasababu Barakah ndiye aliyeona umuhimu wangu mimi kuwepo Arusha. Alinifata nikiwa bado sijapokea simu ya mtu yeyote,” alisema.

“Kuna watu waliingilia kati kuweka zengwe nisitumbuize na Barakah lakini nilifanikisha kwa kishindo.”

December mwaka jana hata hivyo alipohojiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Lord Eyez alikuwa na hadithi tofauti. Alisema bado yupo fresh na kundi hilo na anatarajia kuachia ngoma mbili, ‘Hardcore’ na ‘Shida Mpya’ alizomshirikisha member wa kundi hilo G -Nako.

“Lord Eyez bado nipo na nilikuwa na napikapika vitu,” alisema. “Juzi kati nilikuwa na G-Nako tukiwakilisha Weusi kampuni na sasa hivi tayari tumeandaa kazi mbili, moja inaitwa Hardcore na nyingine Shida Mpya,” aliongeza.

“Kwahiyo nawaambia mashabiki wangu wakae mkao wa kula, nataka nifunge mwaka halafu nifungue kwa kasi kwa sababu nataka mwaka 2016 uwe mwaka wangu.”

Donald Trump Kuwarejesha Wahamiaji Marekani Kwao

$
0
0
Donald Trump asema kati ya wahamiaji haramu milioni mbili ama tatu watasafirishwa kutoka Marekani baada ya kuapishwa kuwa rais wa chi hiyo.

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Marekani,CBS, Trump amesema wahamiaji wote wenye rikodi za uhalifu, ikiwemo makundi ya wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya ndio watakuwa kipaumbele chake .

Hatma ya wahamiai haramu milioni nane na ushee waliosalia itafahamika mara tu mpaka utakapokuwa salama.

Donald Trump ameongeza kuwa semhemu ya ukuta ambao aliahidi kujenga kwenye mpaka baina ya nchi yake na Mexico, unaweza kuwa ni uzio.

Facebook Yakana Kumsaidia Ushindi Donald Trump

$
0
0
Mwanzilishi wa mtandao wa facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa atatumia kila njia kukabiliana na habari za uongo,huku akikana madai kwamba mtandao huo ulimsaidia rais mteule wa Marekani Donald Trump.Mark Zuckerberg akana facebook ilimsaidia Donald Trump kushinda uchaguzi

Katika chapisho lake katika mtandao wa facebook ,Zuckerberg amesema kuwa atatangaza mikakati ya kukabiliana na habari zisizo na ukweli hivi karibuni.

Amesema hatua hiyo itachukua muda mrefu ili kuhakikisha kuwa marekebisho yanayofanywa hayatakuwa na athari zozote ama upendeleo.

Ameongezea kuwa zaidi ya asilimia 99 ya habari zilizopo ndani ya mtandao huo ni za kweli.

''Ni habari chache sana zilizo na uwongo na utapeli.Utapeli unaoendelea haupendelei mtu mmoja wala hata siasa'', aliongezea.

Amesema kuwa haiwezekani kwamba utapeli uliopo ulibadilisha mwelekeo wa uchaguzi nchini Marekani.

Kwanini Seline Ameondoka The Industry? Haya ni Majibu Toka kwa Navy Kenzo na yeye Mwenyewe

$
0
0
May 6 mwaka huu, label ya The Industry inayomilikiwa na Nahreel na Aika (Navy Kenzo) iliwatambulisha wasanii wake watatu, Rosa Ree, Seline na Wildad.

Baada tu ya kuwatambulisha, walianza kwa kuachia kazi ya Seline iliyoitwa Njoo. Na wiki hii, kazi za wasanii wawili, Rosa Ree na Wildad zimetambulishwa lakini uongozi wa The Industry ukatangaza kuwa Seline hayupo nao tena.

“Tahadhari kutoka uongozi wa The Industry Studios Tanzania, msanii Seline (Roseline Muhagachi) hayupo tena chini ya uongozi wa Lebo ya The Industry inayomilikiwa na Navykenzo (Aika na Nahreel),” ilisema taarifa hiyo.

“Hii ni kutokana na matukio mbali mbali ya utovu wa nidhamu ambayo yalitokea akiwa chini ya uongozi wa Lebo hiyo. The Industry Studios haihusiki na shughuli,matangazo wala matukio yoyote yanayomuhusu mwanadada Roseline Muhagachi anayejulikana kwa jina la kisanii Seline,” yaliongeza.

Bongo5 imezungumza na Seline kutaka kujua upande wake ukoje na kama tuhuma za nidhamu ni za kweli. Seline ana hadithi tofauti huku akikanusha kuonesha utovu wa nidhamu na kwamba ni yeye ndiye aliyejiondoa.

“There is a very sad story behind all of that,” anasema.

“Halafu mimi nimejitoa The Industry mwenyewe hakuna aliyeniondoa pale. Nilienda kuinvest hela yangu pale, a lot of money, and hawakufanya kazi wanayopaswa kufanya,” ameongeza.

“I am a professional, nimefanya kazi hadi na government za nchi nyingine, kweli leo nitolewe kwenye studio kisa misconduct?”

“Kifupi I invested my money kwao and they didn’t work on our terms and many more factors behind it,” amesisitiza.

Tayari Seline ameachia wimbo wake, Dollar kama msanii anayejitegemea.

ACT-Wazalendo walaani kauli ya Serikali kutowajengea wananchi......Wadai kauli hiyo ni fedheha kwa waathirika na Wadau.

$
0
0
Watanzania wanakumbuka kuwa mnamo tarehe 10 Septemba, 2016 lilitokea tetemeko la ardhi katika eneo la Kanda ya Ziwa na hususan Mkoa wa Kagera.

Tetemeko hilo lilisababisha athari mbalimbali zikiwemo vifo, majeruhi, uharibifu wa makazi na miundombinu ya umma na watu binafsi. Jumla ya Watu 117,721 wameathirika kwa kupoteza makazi yao, mali na athari za kisaikolojia katika Wilaya za Bukoba, Missenyi, Muleba, Karagwe na Kyerwa.

Aidha, jumla ya watu 17 walipoteza maisha na 560 walijeruhiwa. Vilevile, nyumba 2,072 za makazi zilianguka kabisa na nyumba 14,595 za makazi zilibomoka, baadhi zina kuta au kupata nyufa kubwa na hivyo kuzifanya kuwa hatarishi kwa makazi ya binadamu. Vilevile, maafa haya yalisababisha uharibifu mbalimbali wa miundombinu ya barabara na majengo ya watu na taasisi mbalimbali, ikiwemo shule na Hospitali.

Kufuatia maafa hayo, wananchi na taasisi mbalimbali, pamoja na nchi marafiki, waliitikia wito wa kuwasaidia wahanga wa maafa na kukarabati miundo mbinu iliyoharibika. Hadi kufikia mwezi Oktoba, Fedha, Vyakula na Vifaa mbalimbali vya Ujenzi vilikuwa vimepatikana kwa njia ya michango mbalimbali.

Chama chetu kimeshtushwa na kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kwamba Wananchi walioathirika wajitegemee wenyewe na kwamba misaada yote iliyotolewa Ni ya Serikali na Taasisi zake tu. Kauli hii ya Mkuu wa Mkoa haikubaliki kwani inadhalilisha waathirika na watu wote waliojitoa kuwasaidia waathirika hao.

Tunachukulia kauli hii kama tangazo la wizi wa uaminifu wa wananchi waliochanga. Ni busara ya kawaida kuwa hatua ya kwanza katika kushughulikia maafa ni kurudisha hali ya maisha ya watu katika hali ya kawaida sambamba na ukarabati wa miundombinu. Aidha, suala la ujenzi wa miundo mbinu ya taasisi za umma ni jukumu la msingi la serikali. Kwa sababu hii:

• ACT Wazalendo tunaitaka serikali kuu kujitenga na kufuta kauli ya mkuu wa mkoa wa Kagera kwa sababu inaigombanisha serikali na wananchi inaowaongoza.

• ACT Wazalendo tunaitaka serikali kuelekeza ni misaada iliyopatikana kwa michango ya wananchi, taasisi na nchi rafiki katika kusaidia wananchi walioathirika kurudi katika maisha ya kawaida, ikiwemo ukarabati na ujenzi wa nyumba za kuishi.

• ACT Wazalendo tunatoa wito kwa taasisi za kiraia nchini kuchukua nafasi yake katika kuendelea kuikumbusha serikali wajibu wake wa msingi wa kuboresha maisha ya watu.

Janeth Rithe
Katibu wa Taifa ACT Wazalendo, Kamati ya Maendeleo ya Jamii
13/11/2016, Dar Es salaam.

Kulikoni Ikulu, Serikali na CCM Wanachelewa Kutoa Majibu ya Tuhuma za Msingi Kama Hizi?

$
0
0
Ndugu wapendwa, kumezuka tuhuma nyingi wiki iliyopita...kwanza ilikuwa ya mhe. Mbowe bungeni, ya wabubge hupewa ten M, akanyamazishwa.

Tukasubiri tamko la chama tawala kimya, serikalini kimya, ikulu kwa rais kimya hadi leo.

Pili ishu ya kagera hakuna ufafanuzi wa maana hadi sasa tunaumizana na maswali wenyewe but serikali ipo kwa nini isije na majibu na kuondoa huu kma ni upotoshwaji wa habari kama watu wanavyodai.

Serikali hii haijawah kuwa na kigugumizi kwa swala lolote, kuna tatizo gani la mawasiliano kujibu hizi hoja, kwenye Chama Ole sendeka kimya, serikalini (waziri mkuu) kimya, ikulu (rais) wetu kimya nani wa kutupa majibu sahihi?

Martin Kadinda Afunguka Asema Wema Sepetu Anaangushwa na Marafiki zake

$
0
0
Mbunifu wa mavazi kutoka Bongo, Martini Kadinda amesema hawezi kumchagulia Wema Sepetu marafiki wa kuwa nao karibu na hawezi kujiingiza kwa lolote katika ugomvi wao.

Akipiga story ndani ya eNewz, Kadinda amesema ugomvi ambao unatokana na marafiki zake Wema unamshusha Wema kwa kuwa Wema ni mtu maarufu na ana jina kubwa hivyo alichokifanya ni kumzuia Wema kuweka ugomvi wake katika mitandao ya kijamii.

Pia Martin ameendelea kuwasihi mashabiki zake kuendelea kumpenda Wema na kazi zake ambazo anazifanya na siyo vinginevyo na pia wasimuhukumu Wema kwa mambo yanayoandikwa mitandaoni kwa kuwa hawajui chanzo chake.

TB Joshua Afunguka 'issue' ya kumtabiria Clinton Ushindi Marekani Ambao Uligonga Mwamba

$
0
0
Mhubiri mashuhuri raia wa Nigeria TB Joshua amevunja kimya baada ya utabiri wake kuwa mgombea urais nchini Marekani Hillary Clinton angeshinda, kugonga mwamba.

Mhubiri huyo alikejeliwa kwenye mitandao ya kijamii wakati ujumbe wa utabiri wake, kufutwa na baadaye kurejeshwa katika akaunti yake ya Facebook kufuatia ushindi wa Donald Trump.

Hata hivyo, wafuasia wake wamekuwa wakimtetea wakisema kuwa utabiri wake ulitimia kwa sababu Bi Clinton alishinda wingi wa kura licha ya yeye kushindwa kutokana mfumo unaotumiwa kwenye uchaguzi nchini Marekani unaofahamika kama "electoral College".

Ujumbe mpya katika akaunti ya Joshua ya Facebook unaunga mkono maoni hayo,ukisema:

"Tumeona matokeo ya uchaguzi nchini Marekani. Baada ya kusoma, utaelewa kuwa hii inahusu kura nyingi, kura ya waamerika wengi"

"Kwa hali hii tunahitaji roho ya nabii kutambua au kumuelewa nabii." TB Joshua anaendelea kusema.

Model Calisah Afunguka Baada ya Kusambaa Kwa Video yake Akimla ‘Denda’ Wema Sepetu

$
0
0
Weekend hii katika mitandao ya kijamii kumesambaa video inayomuonyesha malkia wa filamu nchini Wema Sepetu akiliwa denda na model Calisah.

Wawili hao ambao walitumia nguvu nyingi kufanya siri mahusiano yao, wameumbuka kupitia video hiyo iliyosambaa katika mitandao ya kijamii.

Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Calisah amesema hajui ni nani ambaye amesambaza video hiyo mtandaoni kwani walikuwa nayo yeye pamoja na Wema.

“Nilikuwa nachati na Wema kawaida ghafla nikaona notification, kufungua ndio nikakuta hiyo video na mimi ndio nilikuwa mtu wa kwanza kumuuliza Wema kwa sababu video nilikuwa nayo mimi na Wema,” alisema Calisah.

Pia model huyo amedai video hiyo imemsababishia matatizo katika familia yake pamoja na kumpoteza bibi yake kwa presha

Haya ndio madhara 6 ya kutoa Mimba

$
0
0
Kutoa mimba ni nini?
Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.

Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba.

Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano. Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?

Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu isipokuepo ndio basi tena.

Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…

1. Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa mara nne zaidi kuliko ambao hawatoi mimba. Vifo hivyo vimekua vikisababishwa na kujiua wenyewe kutokana na kujuta kwa maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya kimwili yatokanayo na kutoa mimba. Vifo ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%, mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.

2. Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka hii ya karibuni wanawake wengi ambao wanalia kutopata watoto wana historia za kutoa mimba miaka iliyopita, na wengi wao nilionana nao wanajuta sana kwa maamuzi yao. Hii inatokana na madhara makubwa waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba kutoka.

3. Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko wa uzazi una utando maalumu amaboa hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi. Lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia huko.matibabu ya tatizo hili ni kukata mrija husika tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..

4. Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya mda husika akibeba mimba nyingine. Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu  na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili maisha yao yote.

5. Kansa ya mlango wa uzazi:
Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.

6. Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…

Mwisho
kumbuka kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimba...maumivu ya kukosa mtoto ni makali sana kuliko aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Hawa wanaozaa sasa hivi unawaona malaya ipo siku utawakumbuka utakapo ambiwa na daktari kwamba labda itokee miujiza ndo utazaa.Kama hutaki mimba tumia njia za uzazi wa mpango kwani kuendelea kutoa mimba kutakupa adhabu ya kukosa mtoto ambayo adhabu hiyo utaitumikia maisha yako yote..kwa maelezo zaidi

Channel Mpya DSTV TRACE MUZIKI Kwa Ajili ya Afrika Mashariki Inaboa

$
0
0
Nimekuwa mfuatiliaji mkubwa wa Channel mpya ya DSTV kwa ajili ya East Africa inayoitwa Trace Muziki Kwa ajili ya kupiga ngoma za wanamuziki wa kutoka afrika mashariki, lakini nimekuwa disappointed kwani wanarudia nyimbo mpaka zinaboa, ni kama wana play list ya wasanii wachecha ambao wamewalipa kurudia nyimbo zao kila wakati..najua Afrika mashariki kuna wanamuzki wengi tu lakini walioko kwenye rotation yao hawazidi kumi hasa wakenya...
Badilikeni....KIFUPI MNABOA tunawanamuziki wengi sana East africa najua mnatumiwa kazi nyingi sana mnazitia kampuni....
DSTV tunahitaji burudani Badilikeni basi tuendelee kuwatazama

By Mdau
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images