Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Wagonjwa 4 Kati ya 7 wa Tezi Dume, Hufariki Dunia

$
0
0
Makamu wa Rais aliyasema hayo jana mkoani Mwanza wakati wa uzinduzi wa upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi na saratani ya shingo ya kizazi na saratani matiti.

Alisema kuwa kati ya watu saba, wanne wanafariki dunia kutokana na tezi dume ambayo huwapata wanaume.

Akizungumzia saratani ya kizazi na ya matiti Makamu Rais alishauri jamii hasa akina mama kupima afya zao ili kuepuka matatizo hayo ambayo yamekuwa yakiongoza kwa vifo vya watu wengi.
Amebainisha kuwa serikali kwa kutambua hilo imetoa shilingi bilion tano ili kujenga vituo vitatu vya afya katika kila halmashauri nchini.

Babu wa Miaka 89 Ajichimbia Kaburi Canada

$
0
0
"Wajukuu watajua kwamba babu yao alishinda kaburi lake," anasema Bw Kickham

Mzee wa umri wa miaka 89 nchini Canada amegongwa vichwa vya habari nchini humo baada yake kujichimbia kaburi.

Mzee huyo bado yuko buheri wa afya.

"Huwa napenda kuchimba," Jimmy Kickham, kutoka kisiwa cha Prince Edward Island, aliambia CBC News.

Ameongeza kwamba anajivunia kukamilisha mradi huo wake wa kibinafsi.

Bw Kickham, ambaye anamiliki kazi ya ujenzi, amekuwa akichimba makaburi ya wengine pamoja na mitaro kwa zaidi ya miaka 60.

"Siku moja, niliamua kwamba nikifanikiwa kutimiza miaka 90 ningejichimbia kaburi langu."

Bado ana afya nzuri na atatimiza umri wa miaka 90 siku ya Alhamisi.

"Huwa napenda kuchimba. Ni moja ya mambo ambayo yamo kwenye mwili wake. Ni kazi tu. Pesa.

Nilikuwa nachimba kila walichotaka nichimbe, ninaweza," aliambia shirika la utangazaji la Canada.

 Afisa wa makaburi asijiliza Bw Kickham akifafanua ni kwa nini ameamua kuchimba kaburi lake
Bw Kichkam bado huwa anfanya kazi, akitumia trekta alilonunua miaka 45 iliyopita.

"Si jambo la ajabu kwangu kuchimba kaburi, ni kawaida. Nimeyachimba makaburi mengi, Mungu ndiye ajuaye," anasema.

Hata hivyo anaeleza kwamba ilichukua muda kwa familia yake kukubali mpango huo wake.

"Nilienda kwa padri kwanza na kisha kwa msimamizi wa mazishi na kupata vipimo, ingawa tayari nilijua vipimo kutokana na makaburi niliyoyachimba awali," anasema.

Anataka kuzikwa kitamaduni, ambapo sanduku la msonobari huwekwa kaburini mapema kabla ya maziko yenyewe.

Eric Gallant, mfanyakazi katika kanisa la St Alexis, Rollo Bay, anasema hajawahi kushuhuria kisa kama hicho awali.

"Kitu pekee ambacho sasa hakipo ni jeneza tu," anasema.

"Na mimi!" Bw Kickham aliongeza upesi.

Lady Jay Dee Afunga Ndoa Tena..Apost Picha Akiwa Honey Moon

$
0
0
Msanii nguli na namba moja nchini kwa upande wa kina dada binti machozi, komamdo, anaconda, lady jay dee amefunga ndoa weekend hii kupitia mtandao wa I.G amepost baadhi ya picha akila honey moon uko Zanzibar

Kibosile Amtema Mrembo Tunda Baada ya Kugundua Anachepuka na Diamond

$
0
0
Kibosile aliyekuwa anam sponsor mrembo Tunda, ikiwa ni apamoja na kumjengea nyumba ya milioni 100 , gari pamaoja na kumpa fedha nyingi za matumizi amemtema
Sikiliza Hii Hapa chini ni baada ya kugundua mrembo huyo anatoka na mwanamuziki Diamond

Nisha Bebe Alia Tena...Apewa Ujauzito na Kuachwa Solemba, Atuma Ujumbe Huu Kwa Muhusika

$
0
0
Msanii Nisha kwa mara nyingine tena amepata title ya u 'single parent'...

Ni baada ya kupewa mimba na kisha kuachana na baby dady wa kijacho hiko bila hata kusubiri mrembo huyo ajifungue.....

Ila Nisha kasema haina noma kama yule wa kwanza alimlea bila msaada wa baby dady, huyu ataanzaje kushindwa?

Huu Hapa Ujumbe wa Nisha Kwa Aliyempa Mimba na Kusepa:

Donald Trump Azikataa Dola 400,000 za Mshahara wa Rais..Adai Atajilipa Dola 1 Kwa Mwaka

$
0
0
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema hataki kulipwa mshahara wa rais wa $400,000 atakapochukua hatamu Januari mwakani. Badala yake atakuwa akilipwa dola moja ya Marekani ($1) pekee kila mwaka  sawa na shilingi 2000 ya kitanzania.

Alifichua mpango wake huo wakati wa mahojiano na Lesley Stahl kipindi cha 60 Minutes cha CBS News.

Ingawa hakujua rais huwa analipwa pesa ngapi, Bw Trump alisema alidhani anahitaji kuchukua tu $1.

Baada ya Bi Stahl kumjulisha kwamba mshahara wa rais ni $400,000, alisema: "Hapana, sitaupokea mshahara huo. Sizichukui kamwe."

Rais huyo mteule anatimiza ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni.

Aliambia waliohudhura mkutano wake Septemba kwamba mshahara wa rais si jambo kubwa kwake.

Kinana: Lowassa ni Rafiki Yangu Sitaki Kuamini Kama Ana Nongwa na Mimi

$
0
0
''Ni rafiki yangu, lakini kuna urafiki na kuna nchi. Binafsi nadhani sisi bado ni marafiki. Tangu uchaguzi umekwisha tumeshakutana mara nyingi, tumeshapigiana simu mara kadhaa. Tunazungumza, sitaki kuamini kwamba ana nongwa, na hata kama ana nongwa nitamuelewa. Unajua, kama nilivyosema hapo mwanzo, kuna urafiki wangu na Lowassa na kuna nchi'' - Abdulrahmaan Kinana.

Orodha ya Wadaiwa Sugu HESLB Yaibua Mapya

$
0
0
Orodha ya wadaiwa sugu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), imedaiwa kuwataja wanufaika ambao baadhi walishamaliza kulipa madeni yao.

Pia, yapo majina ya watu ambao hawajawahi kuomba mkopo na wengine walisoma nje ya nchi.

Mapema wiki hii Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru, alitaja kiasi cha fedha wanazodaiwa wanufaika hao 142,470 kuwa ni Sh2.39 bilioni. Hata hivyo, baadhi ya majina yaliyotolewa katika tovuti ya HESLB ikidai kuwa ni wadaiwa sugu, wametajwa kimakosa.



Kila Kona ni Maumivu

$
0
0
Uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano kubana matumizi, kudhibiti ukusanyaji kodi, kuondoa upendeleo wa zabuni na kuzuia shughuli za Serikali kufanyika katika hoteli umeibua kilio kwa makundi tisa ambayo masilahi yake yameguswa moja kwa moja.

Baadhi ya makundi hayo ni ya wafanyabiashara, wanafunzi wa vyuo, wanasiasa, wabunge, watumishi wa umma, vyombo vya habari, wanawake na waathirika wa bomoabomoa eneo la Bonde la Msimbazi.

Katika makundi hayo, yapo yaliyojikuta katika maumivu kutokana na nia njema ya Serikali kuboresha mfumo wa ukusanyaji kodi, kudhibiti mianya ya rushwa na matumizi yasiyokuwa ya lazima lakini yapo yanayolia maumivu kutokana na makosa katika uamuzi usiozingatia sheria na kusababisha athari kubwa katika mfumo mzima wa maisha.

Waziri Mkuu Kumtumbua Makonda Iwapo Atashindwa Kukomesha Matumizi ya Shisha

$
0
0
Warizi Mkuu, Kassim Majaliwa amesema atamwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda iwapo hatasimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya dawa za kulevya, aina ya shisha.
waziri-mkuu-kassim-majaliwa

Hatua hiyo inatokana na kauli ya Makonda kuwatuhumu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi Suzan Kaganda, kulegalega kusimamia suala hilo huku akihofia wanaweza kuwa wamehongwa na watu waliotaka kumhonga lakini akakataa.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Umeme katika Jiji la Dar es Salaam.

Alisema katika udhibiti wa suala la shisha, mkuu huyo wa mkoa amefanya kazi nzuri, na kwamba kwa kuwa ameshatoa maelekezo, akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Makonda hana budi kuyatekeleza.

Alisema alivyosikia anawaagiza wakuu wake wa wilaya wote kusimamia maagizo yake na kama hawakusimamia atachukua hatua, basi naye atachukua hatua kwake (Makonda) asipotekeleza suala hilo ambalo kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni tatizo kubwa.

“Sasa mimi nasema nakuagiza wewe usimamie na kama hutasimamia suala hilo nitakuchukulia hatua, hivyo hangaika na shisha kwa wanaopuliza wakiwa wamelala hakikisha unawadhibiti,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa wakati akijibu sehemu ya salamu za Makonda alipopewa fursa ya kusalimia wananchi katika hafla hiyo.

Katika salamu zake, Makonda alisema Waziri Mkuu alipiga marufuku matumizi ya shisha, hivyo alimwagiza Kamanda Sirro kuhakikisha suala hilo linatekelezwa kwa kiwango kikubwa.

“Lakini Waziri Mkuu nimeshangaa kupita katika baadhi ya maeneo na kuona watu wameanza tena kuvuta shisha na nilipouliza wakasema wewe ndiyo umetoa kibali cha shisha,” alieleza Makonda na kuongeza alishangaa Waziri Mkuu alipiga marufuku shisha, ni lini ametoa kibali kuanza kutumika.

Lakini mkuu huyo wa mkoa alienda mbali zaidi na kudai kuna kikundi cha watu 10 waliokwenda kwake ambao anawatambua kama “maajenti wa shetani” ambao wanapata faida kati ya Sh milioni 35 mpaka Sh milioni 45 kwa mwezi kutokana na dawa hizo za kulevya.

Alidai watu hao walipanga mikakati ya kumshawishi kupokea Sh milioni tano kwa kila mmoja kwa mwezi yaani Sh milioni 50 ili asipige kelele kuhusu shisha na wao waendelee kupata faida. “Shisha imerudi katika Mkoa wa Dar es Salaam na nimeshamuagiza Kamishna Sirro, lakini nimeona kama ana kigugumizi… lakini sijajua kama hizi tano tano zimepita kwake na pia RPC wa Kinondoni nimemuona hapa, lakini hawa wana kigugumizi sijui kama hizi tano tano zimepita kwao,” alisema Makonda.

Alisema aliamua kufanya ziara mwenyewe na kushuhudia watoto wadogo wanavuta shisha, hivyo uwezekano miaka 10 ijayo vijana wengi kuwa matatizo ya afya, hivyo kumwomba Waziri Mkuu kutochoka kusimamia suala hilo na taasisi zote ili likome katika mikoa yote.

Kuhusu wafanyabiashara wadogo, alisema suala hilo linamnyima usingizi na kutoa rai kwa wakuu wa wilaya kuwa, kama kuna mkuu wa wilaya atachelewa kutekeleza yale aliyoagiza kuwapeleka machinga katika maeneo yaliyoruhusiwa atachukua hatua kabla ya Waziri Mkuu kufanya hivyo.

Source: Habari Leo

Picha:Vera Sidika Aonyesha Nyumba yake na Gari Analomiliki ni ‘Kufuru’

$
0
0
Mrembo maarufu wa Kenya, Vera Sidika ameonyesha kuwa na yeye ni miongoni mwa mastaa wanaomiliki vitu vya thamani.

Kupitia mtandao wa Instagram, Vera ameuonyesha mjengo wa kifahari anaoumiliki pamoja na gari aina ya Range Rover na kuwaacha mashabiki mdomo wazi.



“I still remember the days I prayed for the things I have now. Just believe in the person you want to be and then work hard for it. Because the Limit to your abilities is where you set them. Have a productive week ahead. 👑QVB👑,” aliandika Vera kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao huo.

Hatua hiyo ya mrembo huyo kuonyesha mali zake hizo imeonekana ni kama amemkejeli hasimu wake Huddah Monroe.

“I wonder why Huddah sees Vera as a. Challenge??? The beef is real.. Am happy my queen is more matured than her =, ignoring her to the fullest,” amecomment mmoja wa mashabiki kwenye picha hiyo.

Taarifa Kuhusu Kinachoendelea Kwenye Kesi ya Scorpion Mtoa Macho Mahakamani

$
0
0
Upelelezi wa kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu kama Scorpion anayetuhumiwa kumsababishia upofu wa kudumu Saidi Mrisho umekamilika na hatimaye shauri hilo litasomwa Novemba 30 mwaka huu katika mahakama ya manispaa ya Ilala.

Njwete anatarajiwa kusomewa mashtaka yake baada ya yale ya kwanza kufutwa ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kusikilizwa baada ya kufunguliwa mashtaka mapya.

Huyu ndiye Scropion, kijana aliyejizolea umaarufu ambapo watu wengi hupenda kumshuhudia kila aingiapo na kutoka mahakamani huku kila mmoja akizungumza lake kwa kesi inayomkabili.

Alipoingia mahakamani leo, aliomba ufafanuzi wa wazi juu ya mashtaka yanayomkabili ambapo upande wa jamhuri kupitia kwa wakili wake Chesensi Gavyole walisema ushahidi umekamilika.

Kutokana na kuombwa ufafanuzi, Hakimu anayesimamia kesi hiyo Flora Haule amesema baada ya upelelezi huo kukamilika kesi hiyo itasomwa Novemba 30 mwaka huu, hivyo mshtakiwa atapata ufafanuzi wa mashtaka yake .

Ikumbukwe kwamba Oktoba 19 mwaka huu, Salum Njwete maarufu kama Scropion alifutiwa kesi na kisha kusomewa upya mashtaka yake kutokana na uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliyeomba kufanya hivyo baada ya hati ya awali kuwa na mapungufu ya kisheria

Tuzo Aliyonyang'anywa Wizkid yampa Alikiba umaarufu Nigeria

$
0
0
Mara tu baada ya EMA kueleza kinagaubaga jinsi walivyokosea kumpa Tuzo Wizkid badala ya Alikiba ,vyombo vya habari vya burudani nchini Nigeria vimemwelezea Alikiba kama msanii aliyepaswa kubeba tuzo ambayo Wizkid amechukua.

Kitu kilichoibua hoja zaidi ni baadhi ya mashabiki wa East Africa kuja juu na kudai kuwa msanii wao yuko vizuri kuliko Wizkid kitu ambacho kiliandikwa pia na vyombo vya habari huko ikiwemo magazeti, blog na redio...
Baadhi ya watu walionekana kushangaa lakini huku wengine walidai ni msanii aliyeko chini ya Sony.
Post ya Alikiba iliyoeleza uungwana wake kuhusu wanao mtukana Wizkid imeandikwa pia katika vyombo vya habari pia TV mbalimbali zimetoa habari hii.
Hapo karibuni kuna mitandao iliyoeleza uwepo wa msuguano baina ya Wizkid na Alikiba juu ya nani atangulie stejini na chombo hicho kimeeza kuwa hiyo ilipelekea kuchelewesha show lakini haikuwa proved kama ndivyo...

Dalili Muhimu za Mwanamke Aliefika Kileleni Mkiwa Faragha..

$
0
0
Wanaume wengi sana hua tunadanganywa na wenza wetu kua tumewaridhisha vya kutosha lakini ukweli hua hakuna kitu

Hua wanafanya kwa nia njema tu kwani wanaume hua tunajiskia amani sana kuambiwa umemfikisha mtoto wa kike kwani ni jambo la kishujaa kama trumph uchaguzi us

kwa uzoefu wangu,mwanamke aliefika kileleni hua anakua hivi bila hata kuuliza au kusubili kuambiwa

1.MWILI KUISHIWA NGUVU

mwanamke aliefika orgasm hua anaishiwa nguvu mwili baada ya safari ndefu ya mikito,ukiona baada ya sex msichana anauwezo wa kufanya kazi nzito nzito jua umefanya kazi butu sio mpaka uambiwe

2.KUPITIWA NA USINGIZI BAADA YA MECHI

ukiona ka beby kako kamepitiwa na usingiz gafla baada ya sex jua kaz imeenda sawia,ikumbukwe kufika orgasm ni mechanism inzito,

3.MUSCULAR CONTRACTION

mwanamke anaekalibia/ aliefika kileleni misuli hubana na kuachia ,hii ni kwa mwili mzima hadi kwenye vagina,hilitendo pia hufuatiwa na mwili kutoa jasho.
ukiona ivo ujue kazi zimeenda sawia

Wakuu huu ni uzoefu wangu niliopata nikiwa field,

Ukiona mpenz wako hajaonyesha izo dalili muhimu basi jua hakuna kitu

Kama unajua dalili zingine zile kuu na muhimu tiririka

Wazee Pigeni kazi tutokomeze fake orgasm tunazodanganywa na kupewa kiburi ili tutoe chapaa

Calisah Afunguka Kuhusu Mtu Aliyevujisha Video Akilana Mate na Wema Sepetu

$
0
0
Sinema ya model Calisah imezidi kushika kasi – amefunguka kwa kudai kuwa ni yeye au Wema Sepetu ndio waliovujisha video inaowaonesha wakilana denda.

Siku chache zilizopita mwanamitindo huyo wa kiume alikamatwa na polisi kwa kosa la kudaiwa kusambaza kipande hicho cha video lakini baadae aliachiwa.

Akiongea na kipindi cha Campus Vibes cha Times FM, Calisah amesema, “Nilienda kwa Wema tukawa tunaongea vizuri tu najaribu kumuelezea, lakini hata yeye alishangaa kuona polisi wameingia. Si yeye ni wapambe wake ndio walienda kituoni, wabeba pochi tu, tena afadhali wangekuwa wanawake ni wanaume.”

“Picha zile tunazo mimi na yeye, kwa hiyo kama sio mimi niliyesambaza ni yeye na kama sio yeye ni mimi. Mimi sijasambaza siwezi kumdhalilisha mwanamke kiasi kile. Sasa hivi nampenda kama mshikaji kwa sababu tayari nina mwanamke mwingine ninayempenda,” ameongeza.

Rais Magufuli Asaini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016

$
0
0
Rais John Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 iliyopitishwa na Bunge katika mkutano wake wa tano mjini Dodoma.
4-5

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa Rais Magufuli amesaini sheria hiyo jana tarehe 16 Novemba 2016 na kuwapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwake.


Udhaifu Huu wa Ali Kiba Unamfanya Diamond Ang'are

$
0
0
Ni ukweli usiopingika wasanii Diamond na Alikiba ni lulu ya taifa kwa sasa hasa unapozungumzia suala la usambazaji wa muziki wa Bongo Fleva kwenda zaidi kimataifa na kuufanya uwe na thamani hata kwa wasanii wengine watakapofikia level zao.

Leo nazungumzia utofauti mkubwa wa wasanii hawa wawili ambao mimi kama #KİJANAMZALENDO nimeuona, Alikiba anaimba vizuri kuliko Diamond lakini kupitia kigezo cha kuimba pekee hakiwezi kumfanya kuwa Msanii mzuri kuliko wengine but kuna mambo mbalimbali ambayo msanii yeyote anapaswa kuyafanya ili awe bora zaidi kuliko wenzake.

1 Alikiba amekuwa akiamini yeye binafsi anaweza kufika international bila kufanya kazi na wasanii wa nje ya nchi Jambo ambalo Si la kweli ili Msanii yeyote uweze kufanikiwa kimataifa lazima ufanye Collabo na wasanii wa level hiyo mfano Wizkid sasa Dunia inamjua kupitia Drake, Davido dunia inamfahamu kupitia Meek Mill,

2 kufanya media tour na Show za kimataifa; Miongoni mwa mambo ambayo Alikiba yanamfanya awe tofauti na Diamond, Alikiba hafanyi media tour za nje anafanya za ndani tu Ndani kila mtu anaufahamu uwezo wake so tunataka aupeleke nje ya Tz pia aanze kufanya matamasha ya kimataifa haiwezekani msanii unataka kwenda kimataifa halafu kwa mwaka Unaperfom Majukwaa matatu tu.

3 Kupunguza Collabo na wasanii wa kawaida; kitu kingine ambacho Kiba anapaswa kukizingatia ni kupunguza Collabo haşa wa wasanii wa kawaida ambao wanataka kupata jina kupitia yeye simaanishi kwamba asikuze vipajj lakini anaweza kuwasaidia kwa kuwasaini kwenye Lebo yake ili bado awe na nguvu ya kuwasapoti.

4 Kuongeza Timu ya washauri: Kingine Kiba anapaswa kuongeza idadi ya watu anaofanya nao kazi ambao ni official lakini hata kuwafanya nao wawe mastaa ili popote wanapofanya interview nado yeye atajwe mfano Alichofanya DİAMOND amembrand DESİGNER, DANCERS ,MAMA, MTOTO, DADA kote huko bado jina lake linatrend

#kijanamzalendo #ilovetz #maoniyangu

Mwanaume Fanya Hivi ili Mkeo Akuone Mtenda Miujiza Kila Siku..Hakika Hatasikia la Mtu...

$
0
0
Hili ni fundisho kwa vijana wengi ambao wanataabika, suala la fedha limekuwa mwiba mkubwa na chanzo kikubwa cha mahusiano na ndoa kuyumba. Nimelazimika nije na ushauri huu ambao utawasaidia vijana wa kileo ambao wanataabika na ndoa hususani suala la fedha.

Kinachowaumiza vijana wengi katika fedha na wenza wao ni tabia ya wanaume kuwa wazi kwa kutoa taarifa za pato lake kamili. Jambo la uwazi ni jema lakini muwe na kiasi kwani usipokuwa na akiba ya 'taarifa za kipato chako' utakosa fusra ya kufanya miujiza pale mambo yanapokwama.

Fanya hivi. Mfano kipato chako ni shilingi milioni moja kwa mwezi, mweleze kwamba unapokea shilingi laki 7 na hizo tatu hakikisha unaweka katika sehemu salama ambayo hata ikitokea umekufa familia yako itafaidika, mfano benki kila unapochukua mshahara hakikisha unaacha laki tatu kama akiba asiyoijua. Sasa katika hii laki saba panga matumizi pamoja na akiba ya pamoja.

Wanawake wanapenda 'mshtuko/suprise'..so siku ya siku ukiona kanuna unamtoa shoping lazima ataona umetenda muujiza kwa nia njema. Hapa ndipo pale utasikia mwanamke anasema 'mme wangu ana akili kweli'. Ikitokea una marupurupu fulani kama safari nk hakikisha unatoa kiasi na ziada unaweka chimbo. Hii itakupa upenyo wa kuwasaidia hata wazazi wako na ndugu zako bila kumhusisha mara kwa mara kwani wanawake wengine hawapendi usaidie ndugu na jamaa. Fanya mbinu hii hata kama kipato chako ni laki tano weka hata elfu hamsini chimbo ili uweze kutenda baadhi ya miujiza.

Wanawake wote duniani wamejaliwa karama ya kutumia hela yote ya mmewe, yaani ukimwambia kuna hela hii yeye ataandika orodha ya mahitaji ya familia ni kwani njema ila pesa zikiisha yeye hujitoa na kukulaumu kwanini ulitumia pesa zote. Yaani dharura ikitokea yeye hayupo ni lako hilo na ukishindwa kutatua hapo ndipo dharau inaanza...utasikia 'mme wangu hana msaada kabisa' yaani hajali kabisa matatizo anatumia pesa zote bila uangalifu.

Haya yote yanahitaji ustadi mkubwa na utimamu, kumbuka siku zote mwanaume anatakiwa kuwa mtu wa mshitukizo/surprise kwa kutumia kipato kile kile alichonacho. Yaani tunasema uwe na uwezo wa kutengeneza hela (money creator). Ikitokea dharura unamuangalia usoni huku ukitabasamu, unamwambia 'mke wangu usihuzunike ngoja nifanye mpango nitatue hii shida'.

Hii ndio mbinu tuliitumia sisi na kuweza kuishi na mama/bibi zenu bila bugdha.

Nawakilisha.

Install APP ya Blog Hii ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

$
0
0

Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 



Umoja wa Ulaya (EU) Wasema Tanzania ina haki kutosaini Mkataba EPA kama Haijaridhika Nao

$
0
0
BALOZI wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Roeland Van de Geer amesema Tanzania ina haki ya kuamua kutosaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara na Jumuiya ya Ulaya (EPA) hadi itakapojiridhisha manufaa yake.

Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu masuala mbalimbali pamoja na kujibu maswali ya wanahabari hao.

Akizungumzia suala la Tanzania kutosaini mkataba huo wa EPA, ambao nchi wanachama waliosaini hufanya biashara bila kutoza kodi, Balozi Van de Geer alisema ingawa wasiwasi wa Tanzania kuwa mkataba huo utadhoofisha juhudi za nchi za kufufua viwanda vyake, haoni kama kuna ushindani kwenye hilo.

“Ingawa sioni ushindani unaohofiwa na Tanzania kwenye soko la EPA, lakini uamuzi wake wa kutosaini ni haki yao na nisisitize kuwa ni vyema Tanzania isisaini mkataba wowote ambao wana mashaka nao hadi pale watakapojiridhisha umuhimu wake,” alisema Balozi Van de Geer.

Aliongeza ni vyema nchi ikachukua muda kujiridhisha badala ya kukimbilia kusaini, kwa sababu endapo baadaye wataona mkataba huo hauna manufaa na huku wameusaini, watasononeka hivyo ni vyema wakaupitia na kuona kama una maslahi kwao.

Awali, Septemba mwaka huu, Mwenyekiti wa EAC, Rais John Magufuli alisema viongozi wote kwa pamoja walikubaliana kupewa muda wa miezi mitatu ili Sekretarieti ya EAC iangalie na kupitia masharti ya EPA kabla ya kusaini ili kila mmoja afaidike.

Hata hivyo, katika jumuiya hiyo ya EAC, nchi ambazo tayari zimesaini mkataba huo ni Kenya, Rwanda na Uganda na nchi zilizobaki ni Tanzania na Burundi.

 Rais Magufuli alisema katika kikao hicho, walibaini mambo 10 ambayo yanapaswa kuangaliwa kabla ya kufikia uamuzi kwa maslahi ya nchi na wananchi.

Mwenyekiti alitaja mambo ya kuangaliwa kuwa ni kwa namna gani nchi za EAC zitafaidika, njia gani itatumika kuzuia bidhaa za kilimo na kulinda wakulima, usawa, makusanyo yatokanayo na bidhaa zitakazoingizwa, Burundi itasainije huku ikiwa imewekewa vikwazo na EU, kujitoa kwa Uingereza EU na athari zake, kukosekana kipengele cha kuruhusu nchi nyingine kujihusisha na nchi za EAC kibiashara, kukosekana ushuru wa forodha na kipengele cha nchi kujitoa pale inapoona haijaridhika na mkataba.

Rais Magufuli alisema mkataba huo ukisainiwa kwa wakati huu, nchi wanachama zinaweza kuingia kwenye mtego mbaya.

Akizungumzia kujiondoa kwa Uingereza kwenye EU, Balozi Van de Geer alisema EU bado iko imara na umoja huo utaendelea kuwa miongoni mwa mataifa yenye uchumi imara duniani.

Kuhusu kiwango cha biashara baina ya Umoja wa Ulaya na Tanzania kwa mwaka, Balozi Van de Geer alisema hivi sasa mauzo yamefikia dola za Marekani bilioni mbili kwa mwaka huku akimsifu Rais Magufuli kwa sera yake ya viwanda na kusema umoja huo unamuunga mkono.

Aidha, aliisifu Serikali ya Awamu ya Tano kwa kujitahidi kuendesha nchi kwa kutumia vyanzo vya mapato vya ndani kwa wingi, badala ya bajeti kutegemea wahisani wa nje.

“Tumeona juhudi za serikali kwenye suala la bajeti ya sasa utegemezi wa wahisani kutoka nje ni chini ya asilimia 15 ya bajeti, ukilinganisha na awali ambapo bajeti kwa asilimia 40 ilikuwa tegemezi kwa wahisani, tunaona mabadiliko, na hii inaifanya Tanzania kuondoka kwenye nchi za kundi masikini zaidi duniani,” alieleza.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images