Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Mwanamke Afa Akiombewa Kwa ‘Nabii’, Akutwa Hana Nywele Kichwani Pamoja na Nyusi za Macho

$
0
0
Mwanamke mkazi wa Unga-Limited jijini hapa, Lightness Kivuyo ameripotiwa kufa wakati akifanyiwa maombi nyumbani kwa mchungaji aliyejulikana kama ‘Nabii Rajabu’ eneo la Kwa-Mrombo pia jijini hapa.

Kwa mujibu wa dada wa marehemu, Juliana Kivuyo, Lightness alikuwa amesindikizwa nyumbani kwa nabii huyo nyakati za usiku na mumewe aliyemtambulisha kama Shafii Mohammed na kwamba wakati akifanyiwa ibada ya maombi, alianguka na kufariki miguuni mwa ‘Mtume,’ huyo.

“Baadaye shemeji alikuja nyumbani akihema, huku anadai kuwa dada alikuwa kwenye hali mbaya kule kwenye maombi,” alisema Juliana na kuongeza kuwa alitoka mbio kwenda Kwa-Mrombo nyumbani kwa Nabii Rajab na kumkuta dada yake amelazwa kwenye kochi, akiwa bila nguo isipokuwa tu khanga alizofunikwa nazo.

Nabii huyo pia anadaiwa kumnyoa nywele zote pamoja na nyusi za macho wakati akimfanyia ‘huduma,’ hiyo.

Polisi jijini hapa wamethibitisha tukio hilo wakiongeza kuwa tayari watu wawili wamekamatwa kutokana na kifo hicho cha ‘maombi tatanishi.’

Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Charles Mkumbo ameongeza kuwa atatoa taarifa kamili mara baada ya kikao chake na Mkuu wa Mkoa.

Mganga Mkuu katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Jacqueline Uriwo amekiri kupokea mwili wa marehemu, lakini akasema, “Kwanza walijaribu kutudanganya kuwa huyo mama alikuwa hai na kwamba aliletwa kwa ajili ya matibabu, lakini tukagundua kuwa walichokileta ni mwili mfu, hivyo tukampeleka kwenye chumba cha kuhifadhi maiti!.”

Mkurugenzi wa Huduma ya Mazishi katika hospitali hiyo ya mkoa, Dk Francis Coster alisema mwili ulipelekwa hapo na mume wa marehemu ambaye alisisitiza kuwa mkewe hajafa, bali kazimia tu na kwamba mara nyingi huzimia kwa saa nyingi.

Dk Coster aliongeza kuwa ilibidi na wao wasiweke mwili kwenye jokofu na kuulaza kwenye machela kwa saa sita na ndipo wakaamua kuuweka kwenye droo za maiti, kwani ilikuwa wazi sasa kwamba asingeamka tena asilani.

Waganga hospitalini hapo wamekiri kuwa mwili wa marehemu uliletwa hospitalini hapo ukiwa umenyolewa upara, lakini ukiwa na mikwaruzo pamoja na uvimbe hususan maeneo ya mikono na kifua.

Baba mkubwa wa marehemu, Ally Kivuyo ambaye ndiye mlezi wa Lightness, alisema mume wa marehemu alimtaarifu juu ya kifo hicho na kuongeza; “Lakini baadaye nikaletewa taarifa nyingine kuwa Lightness kumbe alikufa wakati akifanyiwa maombi au vitu vingine, nyumbani kwa mtu anayeitwa ‘Nabii Rajabu,’ hapo basi ikabidi niwataarifu polisi ambao walikuja kumkamata mumewe pamoja na huyo anayejiita nabii au mtabiri.

Source: Habari Leo

Je, Paul Makonda Anajua Mantiki ya Alichosema Kuhusu Waliotaka Kumuhonga Mil 50 Kisheria?

$
0
0
Kwanza nianze kwa kusema kuna mambo mengi ninakubaliana na utendaji wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lakini kuna mambo machache ambayo yananipa ukakasi unaonifanya nitimize wajibu wangu kama raia katika kumkosoa, kumuelimisha na kumjenga zaidi katika utendaji wake kama Mkuu wa Mkoa.

Jambo moja ambalo linapelekea msingi wa mada yangu ni kuhusu hii kauli yake aliyonukuliwa akisema,
"Kuna kikundi cha watu kumi ambao hao walikuja kwangu na mimi niliamua kuwatambua kama maajenti wa shetani, walikuja kwangu wanapata faida kati ya milioni 35 mpaka 45 kwa mwezi, wao walio kumi wakakubali kupanga mkakati eti wa kunishawishi nikubali niwe napokea milioni tano tano kwa mwezi kwa watu kumi maana yake milioni 50. Nikae kimya nisipige kelele juu ya shisha ili wao waendelee kupata faida".

Hii kauli ukiichambua katika msingi wa lateral thinking huwezi kugundua impact iliyobeba hasa ikichukuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Mkuu wa Mkoa kama mwakilishi wa Rais wa Tanzania ambaye pia Rais ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama lazima aelewe kuwa sheria ya kupambana na rushwa katika kifungu cha 39(1-2) inamtaka aijulishe TAKUKURU kama anadhani kuna matendo ya rushwa.

Kifungu cha 39(1) kinasema;
39.-(1) Every person who is or becomes aware of the commission of or the intention by another person to commit an offence under this Act shall be required to give information to the Bureau.

Kama hiyo haitoshi, Makonda lazima aelewe kuwa soliciting bribes ni kosa la jinai ambalo limefafanuliwa katika kifungu cha 15(1a-b) ya sheria ya The Prevention and Combating of Corruption Act 2007.

Moja ya vifungu vya Sheria inasema;
15.-(1) Any person who corruptly by himself or in conjunction with any other person-
(a) solicits, accepts or obtains, or attempts to obtain, from any person for himself or any other person, any advantage as an inducement to, or reward for, or otherwise on account of, any agent, whether or not such agent is the same person as such first mentioned person and whether the agent has or has no authority to do, or forbearing to do, or having done or forborne to do, anything in relation to his principal’s affairs or business; or

(b) gives, promises or offers any advantage to any person, whether for the benefit of that person or of another person, as an inducement to, or reward for, or otherwise on account of, any agent whether or not such agent is the person to whom such advantage is given, promised or offered and whether the agent has or has no authority to do, doing, or forbearing to do, or having done or forborne to do, anything in relation to his principal’s affairs or business, commits an offence of corruption.

(2) A person who is convicted of an offence under this section, shall be liable to a fine of not less than five hundred thousand shillings but not more than one million shillings or to imprisonment for a term of not less than three years but not more than five years or to both.

Hoja ya msingi hapa ni kutaka kufahamu kama Mkuu wa Mkoa, Makonda ametoa taarifa hii TAKUKURU? Kama alitoa taarifa, kwa nini hakuweka mtego wa kuwakamatisha kwa TAKUKURU.

Kama hajatoa taarifa rasmi, kwa nini hajatoa wakati sheria inamtaka afanye hivyo achilia mbali yuko ndani ya serikali ambayo imelifanya tatizo la rushwa kama ni kipaumbele cha kwanza katika kuwatumikia Watanzania?

Makonda hafahamu kuwa kukaa kimya bila kutoa taarifa kwenye vyombo husika kunamfanya avunje sheria kama ilivyoainishwa kwenye Penal Code CAP 16 Chapter V na pia sheria ya kupambana na rushwa ambayo imeaninishwa katika kifungu cha 30 kinachosema;
30. Any person who aids or abets another person in commission of an offence under this Act commits an offence and shall be liable on conviction to a fine not exceeding two million shillings or to imprisonment for a term not exceeding two years or to both.

Makonda hafamu kuwa sheria hazina siasa pamoja na kwamba siasa wakati mwingine hazina sheria?

Makonda kama Mkuu wa Mkoa anatakiwa awe mfano kwa wananchi wake katika kuwafichua wavunja sheria lakini anachokifanya kwa sasa ni kuwaficha wavunja sheria huku akicheza mchezo wa kisiasa.

Makonda timiza wajibu wako wa kuwafichua wahalifu kama Raia na Mkuu wa Mkoa lakini pia unatakiwa ufahamu ukubwa na umuhimu wa madaraka uliyopewa katika kuwatumikia wananchi.

Makonda naomba uwataje waliotaka kukupa rushwa ya milioni 50 ili watanzania wawafahamu kwa sababu wana haki kikatiba kuwafahamu.

Video ya matamshi ya Makonda kuhusu kushawishiwa rushwa ya milioni 50
By MsemajiUkweli/Jamii Forums

Mama Diamond Afunguka Kuhusu Nyumba ya Madale..Adai ni yake Kama ni Kuhama Ahame Diamond na Zari

$
0
0
Nasemaje bim'danga Mama Chibu Ndo kishasema Mjengo wa Madale anaumiliki yeye, na wale waliokua wakimsimanga kuwa awapishe Kina chibu Na Zari kwenye Mjengo washindweeee, bi Maza anasema wataondoka wao Na wajukuu ila yeye wa hapahapa haondoki ng'ooooooo, Hiyo imekuja baada ya kukumbusha kauli ya Diamond kabla hajatoka ya kuwa nyumba ya kwanza kujenga itakuwa zawadi kwa mama..... 

 Msikilize Mama Diamond Hapa Chini:

Haya Hapa Matokeo ya Forbes Person of the Year Aliyokuwa Anawania Rais Magufuli

$
0
0
Aliyekuwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali na Wakili nchini Afrika Kusini Thuli Madonsela leo ametangazwa kuwa ndiye mshindi  wa Tuzo ya Mtu Mashuhuri Afrika ya Forbes (Person of the Year #POY2016).

Tuzo huyo hupewa mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuiinua jamii kwenye njanja mbalimbali za maisha kama vile uchumi, siasa, utamaduni.

Katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo, Thuli Madonsela alikuwa akichuana na Michiel Le Roux kutoka Afrika Kusini, Rais wa Mauritania, Ameenah Gurib, Jamii ya watu wa Rwanda na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Mwaka 2015 tuzo hii ilikwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya MeTL, Mohammed Dewji.

Mimba ya Nisha Bebee Yazua Balaa..Adai Baba Kijacho Wake Hawezi Hata Kujinunulia Sabuni ya Kufulia Boxer

$
0
0

Ujauzito wa Mwigizaji Nisha Bebee umezidi kuzua sinto fahamu kutokana na vichambo anavyopost mtandaoni kwenda kwa Muhusika wa Ujauzito huo..leo tena amepost akimtolea uvivu kama ifuatavyo:

"Watu wanasema nimepewa mimba na kutelekezwa, guyz kuna tofauti kati ya kutelekezwa na kutotaka mtoto wako amjue baba ake.
Since nimeamua kuwa wazi wananipigia kama machizi.. NASEMA HIVI SUBIRINI DNA ZA MACHO naanzaje kumtambulisha mwanangu kwa baba namnunulia hadi sabuni ya kufulia boxer mwanaume mzima unaolewa na demu.. star ushuzi star jina pesa hana mfukoni tena koma kutuma marafiki zangu.. tena moods zangu za sasa hivi sizo nichokonoe nikupost unazopiga vizinga hela za maandalizi ya show xiiew.. I'M DONE"Nisha

Kinara wa Matusi Instagram Akamatwa na Polisi Baada ya Kutoa Matusi Makubwa Kuhusu Perfume Mpya ya Diamond

$
0
0
Kijana mmoja ambaye anatumia jina la Shilolekiuno_official Huko Instagram  hatimae amekamatwa na jeshi la polisi kwa kutukana na kukashifu watu mbali mbali mtandaoni, kijana huyo amekuwa akiandika matusi mazito na kukashifu watu mbalimbali akiwemo Mwanamuziki Diamond,

 Jana Baada ya Diamond Kutangaza Kuleta Perfume mpya zenye jina lake sokoni, mtu huyo anayetumua jina la @shilolekiuno_officail aliingia mtandaoni na kuandika matusi makubwa ambayo siwezi kuyaweka hapa kuhusu Perfume hiyo ya Diamond

Meneja wa Diamond Ameandika Haya:


Lemutuz Naye Ameandika Haya:

Godbless Lema Akwama Tena Kupata Dhamana, Arudishwa Gereza la Kisongo

$
0
0
Hatma ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), ilishindwa kujulikana jana baada ya mawakili wa Serikali kuweka pingamizi, wakipinga Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kusikiliza maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na mawakili wa mshtakiwa.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Jaji Sekela Moshi, alisema   kutokana na pingamizi hiyo, atasikiliza hoja za sheria zilizowasilishwa mahakamani hapo kabla hajatoa uamuzi wowote juu ya dhamana ya mshtakiwa.

Aliwaelekeza mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja za sheria kabla mahakama haijaendelea na hatua yoyote.

Jaji Moshi alisema atatoa uamuzi kuhusu mvutano huo wa sheria,  Novemba 22, mwaka huu

Katika maombi hayo namba sita ya mwaka 2016, Jamhuri iliwakilishwa na mawakili, Matenus Marandu na Paul Kadushi wakati Lema anatetewa na jopo la mawakili sita ambao ni Peter Kibatala, John Mallya, Adam Jabir, Sheck Mfinanga, Faraji Mangula na Charles Adiel.

Katika shauri hilo jana, hoja za sheria za pingamizi zilianza kusikilizwa saa 4:54 asubuhi hadi saa 7:25 mchana ambako mawakili wa Serikali na wale wa upande wa utetezi, walichuana vikali kujenga hoja.

Akiwasilisha pingamizi hilo, wakili Kadushi, aliiomba mahakama iwaruhusu kuwasilisha pingamizi moja na kama mahakama ikishindwa kuridhia pingamizi hilo, wawasilishe pingamizi la pili.

Alidai   maombi hayo yaliyosainiwa na wakili Kibatala yanalenga katika kifungu cha 372 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinachoipa Mahakama Kuu kufanya mapitio ya mashauri ya kesi za mahakama za chini.

Alidai   hoja ya sheria inasema   mabadiliko ya sheria yaliyofanyika mwaka 2002 yaliondosha haki za pande zote katika kesi za jinai kuomba rufaa au mapitio ya uamuzi mdogo uliofanywa katika mahakama zinazoongozwa na mahakimu nchini.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 43 (2) cha sheria ya mahakama za mahakimu, maombi hayo yanakinzana na kifungu hicho kwani uamuzi huo mdogo unaopingwa na mawakili wa mshtakiwa, haujamaliza shauri la jinai.

“Lakini pia, uamuzi huo unaobishaniwa na mawakili wa mshtakiwa, uko katika ukurasa wa 17 hadi 19, hivyo mahakama inafungwa na sheria kusikiliza rufaa au mapitio katika uamuzi mdogo.

“Kwa kuwa uamuzi ni mdogo mahakama inakuwa na uamuzi wa kutupilia mbali maombi haya na kusubiri tuendelee na mwenendo wa kesi. Lakini, kama mahakama haitavutiwa au kushawishiwa  na hoja hii, tunaomba kutoa hoja ya pili,”alidai wakili Kadushi

Baada ya hatua hiyo, hoja ya pili iliwasilishwa ikisema maombi ya Lema hayajakidhi matakwa ya sheria, kifungu cha 359 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2,002.

Kwa mujibu wa wakili Kadushi, kifungu hicho kinaelekeza namna mtu asiporidhika na uamuzi uliotolewa na mahakama ya chini, anavyotakiwa kukata rufaa mahakama kuu.

“Msingi wa sheria umeshawekwa na mahakama kuwa maombi ya kufanya mapitio kamwe siyo mbadala wa rufaa na uamuzi mwingi umetamka hivyo,” alidai wakili Kadushi.

Katika maelezo yake, wakili huyo alirejea mashauri mbalimbali ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa yenye kesi za namna hiyo na kudai kuwa kulikuwa na haki ya waleta maombi kukata rufaa na haki hiyo ipo mpaka sasa.

Wakili Kibatala
Kibatala ambaye alikuwa akiwawakilisha mawakili wenzake watano, alidai   hoja za sheria zilizowasilishwa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri hazina msingi katika sheria na akaiomba mahakama izitupilie mbali.

Aliiambia mahakama   kwamba hakimu aliyeruhusu wakili wa Serikali kusimama kabla hajafikia mwisho wa uamuzi aliokuwa akiusoma ni ishara kuwa mahakama hiyo haikuongozwa vizuri jambo ambalo linaifanya Mahakama Kuu iingilie kati na kutoa maelekezo.

“Hoja walizoleta Serikali hazijakidhi matakwa ya sheria. Kwanza kabisa, pingamizi lao halijasema linakuja kwetu au linakwenda kwa mahakama kwa sababu sisi na Serikali tumeitwa hapa mahakamani na hii ni kama mwananchi wa kawaida kwenda kwa msajili kulalamika kisha jaji akaziiita pande zote mahakamani,” alisema Kibatala.

Alisema  wanaishangaa Serikali kuzungumzia kifungu cha 43 ambacho barua ya maombi yao haijakizungumza na pia mahakama kuitisha majalada na kupitia yaliyotokea mahakama za chini, inajenga mamlaka na kuruhusu mahakama kuu kuitisha majalada hayo kupitia mwenendo au uamuzi.

“Kifungu cha 373 cha sheria hiyo ya makosa ya jinai, kinaelezea jinsi Mahakama Kuu inavyoweza kupata taarifa ya upungufu wa mwenendo katika mashauri yanayoendelea mahakama za chini.

“Mfano mahakama za chini zinaruhusiwa zenyewe kupeleka majalada mahakama kuu ili kupitia mwenendo au kupata taarifa yoyote au kuomba namna ya kurekebisha  wanapokosea na hata mwanasheria mkuu wa Serikali amewahi kutumia mfumo huu katika kesi mbalimbali,” alisema Kibatala.

Alisema mahakama kuu ina mamlaka ya kupokea malalamiko na kuyafanyia kazi na ina uhuru wa kuitisha majalada na kusikiliza maombi ya upande wowote kati ya Serikali au utetezi.

Katika maelezo yake, Kibatala alisema kifungu cha 148 (3) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kinasema rufaa inaweza kukatwa kama mtu amenyimwa dhamana ila uamuzi wa mtu kunyimwa dhamana haukatazi mshitakiwa kuomba mapitio ya uamuzi huo.

“Mahakama ilijivua mamlaka ambayo inayo ikiwa ni pamoja na kazi yake ya sheria. Katika hili, hakimu alikosea kumruhusu wakili wa Serikali kusimama katikati ya uamuzi.

“Nasema hivyo kwa sababu kifungu cha 148 (6) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinasema mahakama ikitoa dhamana kwa mshitakiwa ni lazima ifikie mwisho wa hatua ya uamuzi wake kwa kuweka  masharti ya dhamana.

“Lakini katika suala hili, mahakama iliishia njiani baada ya wakili wa Serikali kuingilia kati na kueleza kusudio la kukata rufaa.

“Jukumu letu ni kuiongoza mahakama na siyo kuviziana ili tushinde. Hapa Kadushi amedai haturuhusiwi kuomba mapitio au rufaa ila akasema tulipaswa kukata rufaa na siyo kuomba mapitio ya mwenendo wa uamuzi ule.

“Kwa misingi hiyo, ndiyo maana tunasisitiza kwamba pingamizi la Jamhuri halina mashiko yoyote ya sheria, tunaomba litupiliwe mbali na mahakama isikilize maombi yetu,” alisema Wakili Kibatala.

Katika maombi hayo, Lema kupitia mawakili wake, anaiomba mahakama hiyo ifanye mapitio ya majalada ya kesi za jinai namba 440 na 441 ya mwaka huu ambako anakabiliwa na makosa ya uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli

Mawakili hao wa Lema wanaomba ombi hilo kwa sababu wakati Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Desderi Kamugisha akisoma mwenendo wa uamuzi huo uliokuwa na kurasa 22 hivi karibuni, alisema mahakama hiyo inamwachia Lema kwa dhamana kwa masharti atakayopewa na mahakama hiyo.

Hata hivyo, kabla hajakamilisha uamuzi huo akiwa katika ukurasa wa 21 kati ya kurasa 22, mawakili wa Serikali walisema Serikali inakusudia kukata rufaa juu ya uamuzi huo.

Wakati hayo yakiendelea, jana nje ya mahakama kuu, kulikuwa na ulinzi mkali wa   polisi na askari magereza waliokuwa na silaha za moto.

PAUL Makonda "Mnasubiria Nitumbuliwe, Mimi Najua Nipo Kwa Kusudi la Mungu"

$
0
0
Baada ya kauli ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kusema atamwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda iwapo hatasimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya dawa za kulevya, aina ya shisha, Makonda afunguka.

Akiongea Ijumaa hii katika kipindi cha Power BreakFast kinachorushwa na Clouds FM, Mkuu huyo amesema anajua kuwa kazi za serikali ni zakupita huku akidai yeye anamtegemea Mungu katika kazi zake.

“Mimi bahati mbaya ninajua kuwa hizi kazi ni zakupita watu wengine unakuta wanasema huyu jamaa atanyooshwa tu, atatumbuliwa, tutaona mimi sikomolewi kwasababu mimi najua nipo kwa kusudi la Mungu. Wakati wa Mungu ukipita mambo mengine yatajitokeza, lakini ninachokijua ni kitu kimoja asilimia 80 ya watu hawafanyi kazi ipasavyo katika ofisi zao,”

Aidha Makonda alisema ripoti nyingi anazoletewa zinaonyesha mtaani hali ni shwari lakini akienda kuzungumza na wananchi unakuta mambo tofauti na yale yalioandikwa kwenye ripoti.

Pia mkuu huyo amezindua kampeni iitwayo ‘Dar es salaam Mpya’ ambayo itamfanya kuzunguka katika sehemu mbalimbali za jiji hilo kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuzipatia majibu.

Kamanda Sirro Afunguka Kuhusu Wasiwasi wa Makonda kwa Jeshi la Polisi

$
0
0
Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuonekana kuwa na shaka juu ya jeshi la polisi kwenye harakati za kutokomeza matumizi ya Shisha – Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es salaam Simon Sirro amefunguka juu ya tuhuma hizo.

Kamanda huyo amekiambia kipindi cha Sun Rise cha Times FM leo kuwa jeshi la polisi wanafanya kazi kwa mujibu wa Sheria na Operesheni ya kutokomeza Shisha jijini inaendelea kama kawaida kilicho baki ni mwanasheria mkuu wa serikali kuandaa mashtaka kwa watuhumiwa.

“Watu wamekamatwa ni wengi, kimsingi kazi inafanyika, sasa huo ni wasiwasi kama wasiwasi basi unabaki kuwa wasiwasi, kikubwa niseme tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni. Yeye ni Mwenyekiti wangu wa kamati ya ulinzi na usalama kwa hiyo ninaamini kama ana wasiwasi na chombo chake najua atakuja kutuita na kutuambia nini cha kufanya,” amesema Sirro.

“Lakini kama ana wasiwasi zaidi yeye ni kiongozi wetu atajua atachukua hatua gani dhidi yetu, kwa hiyo namuachia mkuu wangu wa kazi yeye ndio atajua nini cha kufanya.”

Msanii wa Bongo Flava Mo Music Anyang'anywa Gari Hadharani

$
0
0
Mwanamuziki Mo Music, amefuatiliwa Kisha ameshushwa kwenye gari na madalali wa benki, Inasemekana ni Mambo ya Kushindwa kulipa mkopo... Sikiliza Hapa Stori Nzima:

Mitindo ya Kulala Huelezea Kipimo Cha Mapenzi Baina ya Wanandoa au Wapenzi

$
0
0
Wakati wa kulala si lazima wapenzi wafuate utaratibu ule ule kila mara.Hii inawezekana msimamo wa akili ulivyo kwa wakati huo.Fuatilia mitindo ya ulalaji na maana yake

KUKUMBATIANA
Mtindo huu hutumika sana kwa miaka 5 ya mwanzo wa ndoa.Mume huweka miguu juu ya mkewe na mikono kumkumbatia eneo la kifuani.Aina hii hupendwa sana na wanawake kwani hujiona yuko salama
Ni alama ya mahusiano bora ya kimapenzi.

KUTAZAMANA
Hukumbatiana lakini baada ya saa 2 au 3 hujibagua na kila mmoja kulala upande wake.Ni alama ya kusaidia kuondoa mkinzano unaoweza kujitokeza.

MALIWAZO YA MUME
Hushikana mikono na mke kuweka kichwa chake kwenye mabega au juu ya kifua cha mumewe.
Ni alama ya tafsiri ya mapenzi ya dhati ya mume kwa mke.

BARAFU WA MOYO
Mke hupanda juu ya mume na wanaweza kujadiliana mambo mbalimbali.Ni alama nzuri nyakati za maelewano.

KILA MMOJA UPANDE WAKE
Ikiwa mmoja kaweka mguu mmoja au mkono kwa mwenzake,mtindo huu hujulikana kama daraja la mahusiano.Si alama ya kutiliwa mashaka

USINGIZI BARIDI
Pale wanandoa wanapolala kama wasiotambuana bila kugusana pasipo kujielewa ni alama kuwa wako mbali kifikra.Hutokea pale mvuto usipokuwepo
Hali hii isiruhusiwe ikue.

VISIWA TOFAUTI
Wanalala bila ushirikiano kwa visingizio vya kuchoka,ni kama visiwa viwili tofauti.
Chanzo chaweza kuwa matatizo ya kimwili,kiakili au kiuchumi.Hali hii ikitokea mara kwa mara huweza hata kuachanisha wapenzi

MGONGO KWA MGONGO
Mtindo huu hujitokeza sana kwa wapenzi.Ingawa wanaweza kupeana migongo lakini wanaweza kuwasiliana.Ni alama ya kawaida na wanasaikolojia wanauita mtindo huu "muda wa kupumzika"

MZIGO USIOHITAJIKA
Kila mmoja hulala kivyake na mara nyingi ni kama vile wanandoa wanataka kuonyeshana umwamba.Kila mmoja hamjali mwenzake,,hali hii si ya kawaida ni mbaya sana kwani hutengana kuanzia wanapopanda kitandani hadi kunapokucha.Si ajabu hata kununua vitanda viwili au kulala vyumba tofauti.Wanasaikolojia wanaita hali hii kiburi na jeuri.

Majibu ya Jeshi la Polisi Makao Makuu kuhusu tuhuma za Rushwa dhidi ya Kamanda Sirro

$
0
0
Jeshi la polisi nchini limesema litafanya uchunguzi wa tuhuma za rushwa dhidi ya Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro na baadhi ya makamanda wa mikoa akiwemo kamanda wa mkoa wa Kinondoni Susan Kaganda.

Kauli hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, CP Robert Boaz katika makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.

Kauli hiyo ya CP Boaz kwa niaba ya jeshi la polisi imetolewa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hivi karibuni kuwatuhumu makamanda hao kuwa wanasita kuwachukulia hatua watumiaji na wauzaji wa kilevi cha shisha kwa madai kuwa huenda wakawa wamepokea rushwa kutoka kwa wanaojishughulisha na biashara hiyo.

Makonda alitoa tuhuma hizo licha ya yeye ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama katika kanda hiyo kutoa maagizo wahusika kuchukuliwa hatua.

CP Boaz alisema, kuhusu tuhuma ya rushwa suala hilo lina taasisi zake zinazohusika, na kwamba jeshi hilo limepokea tuhuma hizo dhidi ya askari wao kwa hiyo watazichunguza kubaini ukweli.

Godbless Lema ni Shujaa wa Siasa Tanzania Asiyepigia Goti Watawala

$
0
0
Kwako Comrade G.Lema; Najua mapito unayopitia kwasasa, ni mapito makubwa sana yenye historia kubwa inayochochea hasira na kuamsha hisia Kali.

Nataka ujue na dunia ijue upo Mahabusu siyo kwasababu ya kubaka ama kuzini, upo kwasababu umekataa uonevu,umekataa kuishi ukiwa umepiga goti umekataa kuwatukuza wasiyositahili kutukuzwa, umekataa kuwapa utukufu usiyokuwa wao wala ukuu usiyositahili kwao.

Furaha yangu nipale ninapowaona wanajaribu kutisha mtu asiyeogopa mtu ambaye wakati wote amekuwa akiyaishi Yale anayonena...

Comrade Lema... najua jambo lililopo mbele yako ni jambo dogo kwako kwa aina ya siasa zako naona wanazidi kuiambia dunia na ulimwengu aina ya kamanda wanaopambana naye...

Comrade Lema... Wewe ni shujaa wetu na itabaki kuwa hivyo, unatupa somo sisi Wanasiasa wengine namna ya kuitafuta haki bila kuipigia goti, unatupa somo kubwa sana, kama tulifikiri tumefika tusahau na tuone ndiyo kwanza tumeanza Safari ya mabadiliko, Umetuamsha ya kwamba tulikuwa tumejisahau kuna wajibu tumeupuuza kipindi Fulani...

Comrade Lema.... Jina lako lipo juu ya Mlima mrefu hakuna wakufikia kileleni pale isipokuwa Jah pekee ndiyo mwenye Mkono huwo, Maono yako ni makubwa si Rahisi Mwanadamu asiye kuwa na Imani kufikiri kuwa ni imani na imani hukaa na mwenye imani...

Comrade Lema... Mara nyingi sana umekuwa ukituambia USIOGOPE nasi twasema USIOGOPE imani yetu IPO kwako...

Comrade Lema... Umekuwa ukisema ni heri ya vita inayitafuta haki na usawa kuliko amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu, ni maneno ya kijasiri yanayoweza kutamkwa na mtu mwenye hofu ya mungu kwakuwa anajua alitendalo...

Comrade Lema... Huna mfano wa kufananishwa kwasasa kwa aina ya siasa zako za level ya juu sana, pengine ni kwasababu unaongoza jimbo lenye Wananchi wenye uelewa mkubwa sana, ndiyo maana umekuwa ukifikiri makubwa wakati wote.

Comrade Lema... Wananchi wako wa Arusha mjini wanakupenda sana kuliko mtu mwingine yoyote yule mpaka imefikia mahali wanazuia wasije mahakamani siku ya kesi zako, Ila hakimu ameliona hilo na kukemea, huu ni upendo wa wazi kutoka kwa Wananchi wako Mpaka walikuweka ndani Wanaona wivu wanaamua kutumia nguvu kuwazuia...wanatamani wangependwa wao Ila haitawezekana kwakuwa Wanawaarusha wanakuamini wewe...

Comrade Lema: kwasasa kila Mwanasiasa kijana anatamani kufanya siasa kama zako, huu ni utukufu usiyolazimishwa bali umekuja wenyewe kwa upendo...

Comrade Lema... Uimara wako,ujasiri wako unazidi kutuimarisha na kutupa nguvu na sababu za msingi za kutokukata tamaa, Watu wanasema, kama Mbunge anaswekwa ndani kwanini Mimi Mwananchi wa kawaida niogope kwenda ndani kama sababu ya msingi ni kukataa uonevu au dhuluma...

Comrade Lema... Kukaa kwako ndani kumewatoa watu wengi hofu ya kutokukata tamaa ya kupigania mageuzi kwakuwa huko nako wanaishi binadamu wala siyo wanyama...

Comrade Lema.... Nakutakia ijumaa njema tutakutana jumanne Mahakamani nikiwa na makamanda wengi kutoka kila pembezoni ..... Ur Comrade Henry Kilewo
NEVER SAY NEVER

Nisha Bebee Afunguka Tena Kuhusu Mimba yake, Aongelea Mazingira ya Kubakwa Yaliyomtokea Mpaka Kupata Mimba

$
0
0

Mwigizaji Nishabebee Anaendelea kufunguka kuhusu ujauzito wake kupitia ukurasa wake wa Instagram, Hapa chini ameongelea mazingira aliyopata hiyo mimba:


"Mtu pekee anayejua ukweli ni mimi.. pengine kweli nimekosea kwa kuweka hapa na kusema nanunua hadi sabuni ya boxer.

Ila kama ungevaa kiatu changu ungejua nnayopitia wkt huu.
coz ni kipindi ambacho siwezi vumilia kero wacha niwe mkweli wa hili,ni bora uwe na mtu ambaye mko kwenye mahusiano ndo akakupa mimba,kuliko hamko kwenye mahusiano akatumia rafiki zako anataka kukuona then kwa suprise akaja ukashindwa mfukuza coz hamkuachana kwa ugomvi na was like hamna kinachoendelea then rafiki yako alipoondoka akakubaka kisa tu ana nguvu za kukumiliki na anajua udhaifu wako.

Kinachoniuma zaidi zaidi ni kuwa kwenye mahusiano mengine na kupata mimba ya mwengine wakati uhusiano ulikwisha kwisha na akamove on na mwingine na mm niko ok kwa hilo ilhali yalisemwa mengi ya uongo na mm nikajitajidi kutofichua siri za niliyewahi kumpenda.
i've been through a lot... FUC.K U AND I HATE U FOR THIS" Nisha


Hasheem Thabeet Aazimia Kurejea Katika Ligi ya NBA....

$
0
0
Muda mfupi baada ya Timu yake ya mpira wa kikapu ya Gloden State Warriors kuifunga timu yake ya zamani kwa pointi 26, Novemba 3, Kevin Durant alikuta na Hasheem Thabeet ambaye aliwahi kuwa nae katika timu moja ya Oklahoma City Thunder ambaye alikuwa natafuta kazi. Wote waliwahi kuwa Na. 2 kuchaguliwa kwenye orodha ya NBA draft za mwaka 2007 na mwaka 2009.

Wakati Durant alikuja juu na kuwa superstar, Thabeet hakuwahi kuweza kufikia hatua hiyo, akiwa ametokea chuo cha Connecticut, na kucheza katika timu nne za NBA na tatu za D-League kabla ya kuwa mchezaji ambaye yuko huru kucheza timu yeyote nab ado hajachukuliwa na timu yeyote mpaka mwaka 2015.

Durant bado anamatumaini makubwa na Hasheem na kwamba ipo siku atapewa nafasi.

Kwa maneno yake alisema: ‘Hasheem anajua hamna mtu anayemuonea huruma, na wala yeye mwenyewe hajionei huruma, yeye ni ni mmoja wa wachezaji wenye juhudi na pia ni mtu mzuri sana, na ni mmoja kati ya mchezaji mwenza mzuri sana kuwahi kuwa nao karibu. Ipo siku atapata nafasi, kwa sasa anajaribu kuwa mvumilivu’.

Baada ya kuumia kwa hisia zake aliposhindwa kuendelea NBA, Thabeet mwenye umri wa miaka 29 sasa, anaamini kwamba, mwili wake, akili yake na uwezo wake kimchezo umeshapikwa na kuiva sasa baada ya kuenda San Francisco kufanya mazoezi na Frank Matrisciano na Meneja wa zamani wa NBA, Milt Newton mwishoni  mwa mwezi Aprili.

Thabeet aliongelea kujifunza kwake mpira wa kikapu tangu akiwa na miaka 15 hapa nchini Tanzania mpaka kufikia kuchaguliwa kuwa  Na. 2 kwenye draft ya NBA na mpaka baadae kufeli kabisa.

Kwa sasa Hasheem anaamini bado umri wake unaruhusu, alipokua kiakili mwkaa jana ni tofauti na alipole hii, mazoezi anayofanya mniji San Francisco yamemsaidia sana kutengeneza mwili na kuchonga kiakili, ana imani sana na mwalimu wake wa mazoezi.

Ameamua kubakia nchini Marekani kuendelea na mpira huo wa kikapu. Anajua wazi Watanzia tunamuangalia na tunamuamini sana.

Alipoulizwa ni kitu gani ambacho angeweza kufanya tofauti katika kipindi chote alichochezea Ligi ya NBA, alisema angeendelea kuwa mtulivu kama livyokuwa na kufanya kile tu alichopswa kufanya. Na cha zaidi angeliomba kuuliza au kuambiwa sababu kwanini hawakuendelea naye tena. Kwani kitendo cha kumuengua mtu bila kusema wapi amekosea, hakumjengi mchezaji.


Wasichana 'Mnao ombaomba' Hela, Imefanya Wanaume Wasiamini Wasichana

$
0
0
Tabia ya wasichana kuwaombaomba wanaume hela bila sababu imeondoa imani na heshima kwa wasichana.

Utakuta wasichana hao wana kazi, wana biashara ila kutwaa kuombaomba.

Hii tabia imefanya wanaume waone kuwa wasichana wote wanatabia hiyo hiyo.

Pia imesababisha hata kushindwa kuwapa hela wale wasioomba eti kwakuwa wanakuwa wanawapima tabia hiyo.

Enyi wasichana 'ombaomba' acheni tabia hiyo, mnashusha heshima za wasichana wote

Alichokizungumza Ester Bulaya Baada ya Mahakama Kuu Kumpa Ushindi dhidi ya Wasira

$
0
0
November 19, 2016 Kesi ya kupinga matokeo ya Ubunge wa Ester Bulaya iliyofunguliwa na wapiga kura wa jimbo la Bunda dhidi ya aliyekua mgombea wa CCM Stephen Wasira ilitolewa hukumu yake ambapo Mahakamu Kuu ilimpa ushindi na kumthibitisha Ester Bulaya kuwa Mbunge halali.

Mshindi wa Ubunge wa jimbo hilo Ester Bulaya amezungumza kuelezea jinsi alivyoyapokea maamuzi ya Mahakama Kuu chini ya Jaji Noel Chocha juu ya kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na wapiga kura wanne wa mgombea Stephen Wasira.

“Kiukweli namshukuru sana Mungu, na wananchi wa jimbo la Bunda Mjini kwasababu walishaamua na mahakama imeamua lakini kwa uvumilivu wao na hivi ninavyozungumza kuna watu wametoka Musoma kwa miguu mpaka Bunda wakishangilia ushindi wa Mbunge wao” – Ester Bullaya

Polisi Wamchunguza Kamanda Sirro Tuhuma za Paul Makonda

$
0
0
MAKAO Makuu ya Jeshi la Polisi nchini imesema inachunguza tuhuma zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda dhidi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi Suzan Kaganda kuhongwa ili wasidhibiti matumizi ya dawa za kulevya aina ya shisha.

Makonda alitoa tuhuma hizo baada ya kudai kuwa viongozi hao wa polisi wamekuwa wakilegalega kusimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya dawa za kulevya, aina ya shisha.

Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai katika makao makuu ya jeshi hilo, Kamishna wa Polisi, Robert Boaz alisema hayo jana wakati akijibu swali kuhusu hatua za jeshi hilo zilizochukuliwa kutokana na tuhuma zilizotolewa na Makonda. “..kama ilivyo taratibu zetu tunapopokea tuhuma dhidi ya kiongozi wa jeshi hili au askari yeyote tunafanya uchunguzi, kwa hiyo hata tuhuma hizi tunazifanyia uchunguzi kubaini kama ni kweli,” alisema alisema Boaz.

Wiki hii wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Umeme katika Jiji la Dar es Salaam uliofanywa na Waziri Mkuu, Makonda aliwatuhumu viongozi hao wa polisi kwa kulegalega kusimamia suala hilo huku akihofia wanaweza kuwa wamehongwa na watu waliotaka kumhonga yeye lakini akakataa.

Lakini mkuu huyo wa mkoa alienda mbali zaidi na kudai kuna kikundi cha watu 10 waliokwenda kwake ambao anawatambua kama “maajenti wa shetani” ambao wanapata faida kati ya Sh milioni 35 mpaka Sh milioni 45 kwa mwezi kutokana na dawa hizo za kulevya.

Alidai watu hao walipanga mikakati ya kumshawishi kupokea Sh milioni tano kwa kila mmoja kwa mwezi yaani Sh milioni 50 ili asipige kelele kuhusu shisha na wao waendelee kupata faida.

“Shisha imerudi katika Mkoa wa Dar es Salaam na nimeshamuagiza Kamishna Sirro, lakini nimeona kama ana kigugumizi… lakini sijajua kama hizi tano tano zimepita kwake na pia RPC wa Kinondoni nimemuona hapa, lakini hawa wana kigugumizi sijui kama hizi tano tano zimepita kwao,” alisema Makonda.

Alisema aliamua kufanya ziara mwenyewe na kushuhudia watoto wadogo wanavuta shisha. Katika suala hilo, Waziri Mkuu Majaliwa alisema atamwajibisha Makonda ikiwa hatatekeleza agizo hilo la kuondoa matumizi ya shisha katika Mkoa wa Dar es Salaam.

“Sasa mimi nasema nakuagiza wewe usimamie na kama hutasimamia suala hilo nitakuchukulia hatua, hivyo hangaika na shisha kwa wanaopuliza wakiwa wamelala hakikisha unawadhibiti,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa wakati akijibu sehemu ya salamu za Makonda alipopewa fursa ya kusalimia wananchi katika hafla hiyo.

Akijibu tuhuma hizo katika moja ya luninga nchini, Kamanda Sirro alisema mapambano dhidi ya watumiaji wa dawa hizo za kulevya za shisha yanaendelea na wameshakamata watuhumiwa wengi na kuongeza kuwa sasa kesi za wahusika wa biashara hizo ziko kwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) mwenye mamlaka ya kuwafikisha mahakamani.

Sikiliza Wimbo Mpya wa Diamond Aliyomshirikisha Neyo Kutoka Marekani

$
0
0
Sikiliza Wimbo Mpya wa Diamond Aliyomshirikisha Neyo Kutoka Marekani, Bonyeza Hapa Chini Kuusikiliza:

Ruge wa Clouds FM Amsifia Ruby, Adai Ana Kipaji cha Hali ya Juu

$
0
0
Mwanzilishi wa THT na Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, amesema licha ya Ruby kuwa na tofauti naye na kujiondoa kutoka kwenye usimamizi wake, hawezi kushuka kimuziki sababu ana kipaji cha hali ya juu.

Miezi miwili iliyopita, Ruby alijiondoa kwenye usimamizi wa THT na kukataa kutumbuiza kwenye tamasha la Fiesta hali iliyotafsiriwa kuwa hilo linaweza kuwa anguko lake. Hata hivyo bado muimbaji huyo anaendelea kuwika ikiwa ni pamoja na kushiriki kwenye kipindi cha Coke Studio Africa ambako amejinyakulia sifa za kutosha.

Akiongea na mtangazaji wa Mashujaa FM ya Lindi, Baby Dinny, Ruge amesema kipaji cha Ruby ni ‘unstoppable’ na kwamba kama akipata waandishi wengine wazuri atafika matawi ya mbali.

“Mimi naamini Ruby ana kipaji sana. Binafsi ana kipaji cha ukweli kabisa wala sio uongo,” alisema Ruge. “Kama atashuka labda itakuwa ni mambo yake tu mwenyewe lakini sidhani kama kuna namna kipaji chake kitashuka,” aliongeza na kumshauri kuwa apate watunzi wengine wazuri wa kumsaidia. Anadai kuwa nyimbo zake tatu, Na Yule, Forever na Sijutii, ziliandikwa na yeye akishirikiana na Amini na Barnaba.

Kwa upande mwingine, Ruge amesema haoni kama kuna tatizo Ruby kuondoka THT kwakuwa tofauti na wengine wanavyodhani, THT si label bali ni kama chuo ambacho wasanii mbalimbali hunolewa.

“Yeye ameona yuko tayari kivyake kwenda kwenye sehemu anayoweza kupata maslahi zaidi, ndio hivyo tu, kwahiyo sioni kama kuna shinda,” amesisitiza Ruge.

Pia amedai kuwa muda wowote ambao muimbaji huyo atahitaji ushauri kutoka kwake, milango iko wazi kwakuwa bado ataendelea kumchukulia kama mdogo wake. Msikilize Hapa:
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images