Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104771 articles
Browse latest View live

SAKATA la Oparesheni UKUTA: Viongozi wa Dini Waendelea Kusubiri Maombi Yao Kujibiwa na Rais Magufuli

$
0
0
Viongozi wa dini nchini waliopanga kumwona Rais John Magufuli kwa mazungumzo kuhusu hali ya siasa nchini wanaendelea kusubiri maombi yao kujibiwa licha ya kupita zaidi ya siku 90 sasa.

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo  jana alisema: “Siwezi kusema Rais amekataa kuonana nasi, hapana. Labda ni kwa lile tulilokuwa tuende kumuona nalo (Ukuta) lakini kwa mazungumzo mengine milango ya Rais iko wazi,” alisema.

Wazo la viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu kutaka kuonana na Rais lilibuniwa Agosti ili kuzuia maafa ambayo yangejitokeza baada ya Chadema kutangaza kufanya maandamano waliyoyapa jina la Ukuta, Septemba Mosi.

Hata hivyo, Dk Shoo alielekeza atafutwe Katibu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji Dk Leonard Mtaita kwa maelezo zaidi akisema ni mmoja wa wanaoratibu suala hilo.

Dk Mtaita alipotafutwa kwa mara ya kwanza Septemba azungumzie kama barua waliyopeleka kwa Rais imejibiwa alisema tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera na kusababisha maafa makubwa litachelewesha mpango wao wa kukutana na Rais.

Hata hivyo alipotafutwa tena jana, Dk Mtaita aliomba atafutwe mwenyekiti mwenza wa kikao kilichoibuka na wazo hilo ambaye ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim.

“Tumewaachia wenzetu walioko Dar es Salaam, Sheikh Salim ndiye mwenyekiti mwenza na yeye yuko Dar na ndiye alijitolea kufanya mawasiliano na Mheshimiwa Rais,” alisema Dk Mtaita.

Sheikh Salim alipotafutwa ili aeleze alipofikia kufanikisha kuonana na Rais alijibu kwa kifupi tu: “Sisi tuko katika kusubiri. Barua tulishatuma kwa Mheshimiwa Rais. Tunasubiri tu”.

Msemaji wa Serikali, Hassan Abass alipoulizwa alitaka atafutwe Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Gerson Msigwa kwa kuwa ndiye msemaji wa Rais.

“Mtafute Msigwa maana yeye yupo karibu na Mheshimiwa (Rais Magufuli) na anajua ratiba zote,” alieleza.

Alipotafutwa, Msigwa aliwataka viongozi hao kuendelea kusubiri kwa kuwa kila kitu kina utaratibu wake na pia inategemea ratiba ya Rais.

“Kama wameandika, wasubiri watajibiwa,” alisema Msigwa.

Viongozi wa Chadema wanaposoma Katiba na Sheria ya Vyama vya Siasa wanaona wana haki ya kufanya mikutano ya ndani na hadhara na maandamano mradi tu Jeshi la Polisi litaarifiwe siku na mahali pa shughuli hiyo.

Rais Magufuli alipiga marufuku siasa za ushindani hadi mwaka 2020 jambo ambalo Chadema waliamua kujitokeza kupinga kwa maandamano.

Mbali ya Rais Magufuli, Jeshi la Polisi lilitangaza kuwa ni marufuku kufanya mikutano na maandamano.

Hali hiyo iliyotishia kuwepo makabiliano yenye maafa ndiyo iliyowaibua viongozi wa dini ambao walichukua hatua kwanza kuwasihi viongozi wa Chadema na pili kuwataka wasubiri mrejesho.

MBUNGE Godbless Lema Aingia Siku ya 22 Mahabusu

$
0
0
MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameendelea kusota katika mahabusu ya Gereza la Kisongo mjini hapa akiingiza siku ya 22 leo baada ya jana kukwama katika azma yake ya kutaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kufanya marejeo ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha uliomnyima dhamana.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Moshi ndiye aliyetupilia ombi la Lema, hivyo kumfanya arejee mahabusu huku mawakili wake wakihaha kuhakikisha wanakata rufaa ili kuomba dhamana hiyo katika ngazi nyingine ya kisheria.

Aidha, Jaji Moshi ameridhia ombi la Lema kupitia kwa mawakili wake Sheck Mfinanga na Peter Kibatala la kukata rufaa mahakamani hapo ili kesi hiyo isikilizwe na hatimaye Lema kupata dhamana baada ya kupitiwa na jaji atakayepangiwa.

Akitoa uamuzi huo mahakamani hapo, Jaji Moshi alisema kimsingi hoja ya mawakili wa Lema ya kutaka mahakama hiyo kuitisha faili na kulipitia haina msingi wowote kisheria hivyo anaitupilia mbali hoja hiyo na kutoa rai kwa mawakili hao kukata rufaa Mahakama ya Rufaa ili dhamana ya Lema isikilizwe.

“Mahakama hii haiwezi kupitia faili la kesi hii ya Lema ya kupata dhamana hivyo siwezi kupitia faili hili, bali nashauri mkate rufaa ili iweze kusikilizwa,” alisema Jaji Moshi.

Awali Wakili wa Serikali, Paul Kadushi aliwasilisha pingamizi Mahakama Kuu la kuitaka wasisikilize maombi ya Lema ya kutaka mahakama hiyo iitishe faili la kesi namba 440/441 kwa madai yapo makosa ya kisheria yaliyofanywa awali na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa lengo la kumnyima dhamana mbunge huyo.

Akiwasilisha hoja zake mbele ya Jaji Moshi katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Kadushi akisaidiana na Materu Marandu alisema anawasilisha hoja mbili za pingamizi za mahakama hiyo kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Alisema kimsingi maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo kutaka mahakama hiyo iitishe faili la kesi namba 440/441 yanakinzana na kifungu cha 43 (2) cha sheria ya Mahakama ya Mahakimu. Katika kesi hiyo, Lema anashitakiwa kwa kutoa maneno ya kumtusi Rais katika maeneo tofauti.

Kadushi alisema uamuzi unaopinga kufanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ya kukubali kutompa dhamana Lema ni uamuzi mdogo na haukuwa na sababu za kukataa dhamana.

“Mahakama yako inafungwa mikono na kifungu hiki kufanya mapitio au uamuzi mdogo, hivyo tunaomba mahakama itupilie mbali maombi hayo,”alisema Kadushi ambaye wakati akiwasilisha hoja zake alikuwa akinukuu mashauri mbalimbali ya kesi zinazofanana na hiyo.

Aidha, Kadushi alisisitiza kuwa wao wanatambua haki ya kukata rufaa ipo wazi kwa mleta maombi ila itakuwa jambo geni kama mahakama itawapa nafasi kusikiliza maombi yao. Alisema hoja ya pili ya pingamizi lake, linatokana na mleta maombi kutokidhi matakwa ya kisheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Katika sheria ya makosa ya jinai, kifungu cha 359(1) ya mwaka 2002 kuwa mtu asiporidhika na maamuzi ya mahakama ya chini kama ilivyo katika kesi hiyo, kamwe hawezi kuwa na mbadala wa mapitio ya rufaa.

Akijibu hoja hizo Wakili anayemtetea Lema, Peter Kibatala akiwa na jopo la mawakili wenzake, Adam Jabir, Sheck Mfinanga, John Mallya, Faraji Mangula na Charles Adiel, alipinga kuwekewa pingamizi hilo na kuomba mahakama isikilize maombi yao.

Alisema wao wamefungua maombi hayo kuiomba Mahakama Kuu kuitisha jalada la kesi ya mahakama ya chini ili kuona uhalali wa kutotekelezwa kwa uamuzi wa kutoa dhamana, kwani kilichokuwa kinasubiriwa ni masharti ya dhamana.

“Huyu mshitakiwa alipewa dhamana , ila kabla ya mahakama haijatoa masharti ya dhamana, upande wa serikali ukasimama kabla mahakama haijaweka masharti ya dhamana ambayo lazima ifanye hivyo, wakasema wameonesha nia ya kukata rufaa na mahakama ikakubaliana nao bila kutekeleza amri yao,” alisema Kibatala.

Aliomba mahakama hiyo itupilie mbali pingamizi la serikali na kuiomba kuendelea na kazi iliyokusudia kuifanya ya kupitia maombi yao ili kutoa dhamana kwa mshtakiwa au iamuru mahakama ya chini kuendelea na uamuzi wake.

Wakili wa mbunge huyo baada ya maombi yao kugonga mwamba, walikuwa kwenye hekaheka ya kukamilisha kuandika rufaa ili kumnasua Lema atoke mahabusu.

Baada ya kutoka nje ya Mahakama Kuu, Wakili Mfinanga alisema wanamalizia kukamilisha taratibu za wao kukata rufaa Mahakama Kuu na wataomba rufaa hiyo isikilizwe kwa hati ya dharura ili kumnasua Lema mahabusu.

HONGERA Rais Magufuli kwa Kutupunguzia Mabishoo Mtaani

$
0
0
Usawa huu wa mh magu nmeupenda sana, mabishoo wamepungua kwa kasi sana waliobaki ni vichwa ngumu kweli kwao somo la nyakati walishafeli totally.

Ama kweli mia tano tutaacha kuiita jero, book tutairudishia utukufu wake wa kufahamika kama sh.elf moja.

HAPA MSOTO TU.

BAADA ya WCB Kutoa Wimbo , Ommy Dimpoz Atao Mapovu, Diamond Amjibu na Kuvujisha Siri ya Ugomvi Wao

$
0
0
Hii baada ya domo na mavoko kuachia ngoma povu likamtoka ommy akimshushia domo kuwa aache mziki wa ujanja ujanja akimanisha kuwa domo aache tabia zake za kununua view, tunzo kuwa awekeze kwenye mziki mzuri usio na ujanja ujanja naye domo hakuwa mbali akamjibu kuwa nae apunguze tabia za kipunga


Hata hivyo kama mnavyojua Diamond na uswahili wake hakutaka kuacha lipite kimya kimya akaamua kumjibu ommy dimpoz kwa kutupia dongo


VIDEO Mpya: Mabibi na Mabwana.. Tumealikwa Kuitazama Mpya ya Rich Mavoko ft. Diamond

$
0
0
WCB wanayofuraha kutualika kuitazama video mpya ya kijana wao Rich Mavoko ambayo kamshirikisha Boss wake Diamond Platnumz, ukishamaliza kuitazama video hii ni ruhusa kuacha na comment yako umeionaje na wimbo wenyewe ili wakipita baadae wajue watu wao wameipokeaje.

HALI Ngumu...Kampuni ya TSN Yatangaza Kupunguza Idadi ya Wafanyakazi wake..Sababu Hizi Hapa

$
0
0
HALI Ngumu...Kampuni ya TSN Yatangaza Kupunguza Idadi ya Wafanyakazi wake kutokana na Sababu Kadhaa ambazo wameziainisha kwenye barua hii hapa chini:

Nimekuta Mafuta ya KY na Babcare Kwenye Mkoba wa Mchumba Wangu

$
0
0
Ni jambo limenishangaza kifupi sina tabia ya kumfuatilia mpenzi wangu iwe kwenye simu au kwenye mambo mengi but hii ilinibidi tuu.

Wakati mchumba wangu alipokuja kwangu weekend hii na kushinda siku tatu nikajitoa ufahamu ili nisiishi kama fala nikajikuta nikiwa room nikachukua mkoba wake nikawa naangalia nilihamaki baada ya kukuta mafuta ya KY na babycare, mawazo yalinipeleka mbali sana kwa kweli hadi kupelekea kuvuta picha tuwapo faragha mbona my wangu sehemu zake za siri siyo kavu labda huwa anakauka (lubricant)?

Sasa nikakosa jibu ila nikaogopa kumuuliza maana ningeweza kuzua mengine. Sasa nijikaze nimuulize au nitumie njia gani kumuuliza au haya mafuta ya ulainishaji anatembea nayo kwa ajili gani na hajawahi kutumia na mimi...

Mwanaume Aliyefanya Ngono na Wanawake 104 Huku Akijua ana Ukimwi Haikumiwa

$
0
0

MALAWI: Mwanaume Eric Aniva, aliyeshiriki ngono na wanawake tofauti 104 akitekeleza mila huku akijua ameathirika na UKIMWI, amehukumiwa kifungo cha miaka 2 jela.

Amepatikana na hatia ya kutekeleza mila zenye madhara chini ya sheria za jinai za taifa hilo

Wanawake wawili wajane waliotoa ushahidi mahakamani walisema walilazimishwa kufanya mapenzi na mtu huyo ili kutakasa roho za waume zao ambao walishafariki.

Mbwana Samatta Atemwa Tano Bora ya Mchezaji Bora Afrika...

$
0
0

Shirikisho la soka barani Africa (Caf) limetoa orodha ya majina ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2016, jina la mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta halipo katika orodha ya wachezaji hao waliofanikiwa kuingia tano bora.


Samatta alikuwepo kwenye orodha ya awali safari hii alikuwa akiwania tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa ujumla baada ya msimu uliopita kushinda tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wa ndani wakati akiitumikia klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


Nahodha huyo wa Stars anaecheza klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji amewaacha wachezaji wanaocheza kwenye vilabu vya Bundesliga, Premier League, na Serie A.


Orodha ya wachezaji watano wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika


Pierre-Emerick Aubameyang of Gabon and Borrusia Dortmund

Riyad Mahrez of Algeria and Leicester

Sadio Mane of Senegal and Liverpool

Mohamed Salah of Egypt and Roma

Islam Slimani of Algeria and Leicester

Wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.


Khama Billiat of Mamelodi Sundowns and Zimbabwe

Keegan Dolly of Mamelodi Sundowns and South Africa

Rainford Kalaba of TP Mazembe and Zambia

Hlompho Kekana of Mamelodi Sundowns and South Africa

Denis Onyango of Mamelodi Sundowns and Uganda

Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) Yataadharisha Kuhusu Uwezekano wa Kuja Kwa Mvua Kubwa

$
0
0

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) yataadharisha kuhusu uwezekano wa kuja kwa mvua kubwa yenye upepo, yawataka wananchi wachukue tahadhari.

Yasema mabadiliko ya hali ya hewa kwa sasa yanatokana na kuwepo kwa msimu unaotawaliwa na uwepo wa LANINA ambayo ni ongezeko la hali ya baridi katika eneo la Ikweta ya Bahari ya Pasifiki.

Bado matarajio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa na upepo vitaendelea kuwepo katika msimu huu mpaka mwezi Disemba na mabadiliko kidogo yatajitokeza kwa baadhi ya mikoa ambapo mvua zitanyesha kwa wastani.

KAULI ya Basata Kuhusu Video Mpya ya Wimbo wa Rich Mavoko na Diamond Platnumz

$
0
0
Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) ambalo husimamia wasanii pamoja na kazi zao ikiwa ni wasanii wa filamu pamoja na wale wa muziki limesema kuwa linapitia video mpya ya mwanamuziki Rich Movoko aliyomshirikisha Diamond Platnumz kuona kama kuna vitendo vya udhalilishaji  wa kijinsia.

BASATA kupitia ukurasa wao wa Twitter wameandika kuwa wapo thabiti kusimamia maadili katika sanaa na udhalilishaji wa wanawake. Aidha wameeleza kuwa video hiyo iliyotoka jana usiku inayokwenda kwa jina la Kokoro ipo katika uhakiki kujionea kama picha za wanawake waliomo kwenye video hiyo zinakiuka maadili ya kitanzania na muda si mrefu watatoa taarifa.

BASATA wamekuwa wakiwafungia wasanii wengi wanaokiuka maadili ya sanaa ambapo miongoni mwa wasanii wengi waliofungiwa ni pamoja na Nay wa Mitego, Snura huku wengine wakipewa onyo na video nyingine kuzuiwa kuchezwa mchana kwa mfano Zigo Remix ya AY Ft. Diamond Platnumz na Asanteni Kwa Kuja ya Mwana FA.

Lebo ya WCB ya DIAMOND Platnumz Yaingia Partnership na Lebo Kubwa ya Music ya Universal Music

$
0
0
Mwanamuziki Diamond Platnumz ametangaza kwa mara ya kwanza kuwa lebo yake imeingia partnership na lebo kubwa ya Muziki Duniani inayojulikana Kama Universal Music, Lebo hiyo itakuwa inasambaza kazi za Wasanii wote wa WCB na Mkataba wake adai amelipwa Dola Milion Moja...
Diamond Ameongea hayo katika Kipindi cha XXL cha Clouds FM,,,

YAMETIMIA...Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Limetangaza Kupunguza Idadi ya Wafanyakazi Wake

$
0
0
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limetangaza kupunguza idadi ya wafanyakazi wake ikiwa ni njia ya shirika hilo kuweza kujiendesha kwa faida na kufikia malengo yake.

Mkurugenzi Mkuu wa shirikia hilo, Mhandisi Ladislaus Matindi alisema kuwa mchakato wa kupunguza asilimia 90 ya wafanyakazi wa shirika umekamilika na utaratibu wa kuanza kulisuka upya shirika utaanza hivi karibuni.

Mkurugenzi huyo alisema asilimia 10 ya wafanyakazi watakaobaki ndio waliokidhi vigezo vinne walivyovitoa ambavyo ni uaminifu, elimu, uzoefu na kujali wateja.

Kwa upande mwingine alisema kuwa wafanyakazi wengine wameenguliwa kwa sababu hawawezi kwendana na kasi inayotakiwa kwa sasa na shirika hilo.

Kwa sasa shirika hilo lina wafanyakazi 221 ambao wanaelezwa kuwa ni wengi kuliko mahitaji halisi. Katika mpango huu wa kupunguza wafanyakazi, wanatarajia kupunguza takribani wafanyakazi 200.

Kuna taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na shirika hilo kuwa tayari limewasimamisha kazi takribani wafanyakazi wote katika kituo cha nchini Comoro na kile cha jijini Mwanza.

DIAMOND Kaamua Kufunguka Yote Leo...Nimekuwekea Kauli Zote Alizosema Leo Ikiwemo ya Ommy Dimpoz Kutuma Watu Wamuombe Msamaha

$
0
0

Nimekuwekea hapa Maneno Aliyosema Diamond Leo Kwenye Kipindi cha XXL:


Ommy Dimpoz ameshatuma watu wengi sana kuomba msamaha, amenipigia hadi simu lakini sikupokea. Ila nimemsamehe- @diamondplatnumz #XXL


Wanajisifu wana sauti nzuri lakini makoo yanawakauka na 'show' hawapati, wakifanya nyimbo haziendi mbali- @diamondplatnumz #XXL

Kama mimi ni msanii wa ujanja ujanja mbona nafanya nyimbo zinakwenda kimataifa na matamasha kimataifa yanajaa?- @diamondplatnumz #XXL

Mimi ni mtu mstaarabu sana lakini watu wananiona kama nina kejeli, na kila wakitaka kushindana na mimi wanashindwa- @diamondplatnumz #XXL

Wimbo wa I Will Mary You niliyomshirikisha Ne-Yo haujavuja lakini ulitoka ukaanza kusambazwa Marekani na Ulaya- @diamondplatnumz #XXL

Mimi ni mtu mstaarabu sana lakini watu wananiona kama nina kejeli, na kila wakitaka kushindana na mimi wanashindwa- @diamondplatnumz #XXL

VIDEO ya Kokoro yazichezea Sharubu za ‘Simba’ Aliyekuwa Usingizini (BASATA), Ladai Litatoa Tamko

$
0
0

Rich Mavoko na Diamond Platnumz wamezichezea sharubu za simba mkali aliyekuwa usingizini.

Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA limehisi kuna udhalilishwaji wa wanawake kwenye video hiyo na limesema litatoa tamko lake iwapo litaifungia video hiyo au lah!

“Ktk kusimamia maadili ktk Sanaa & udhalilishaji wanawake tuko thabiti.Video ya #kokoro ya #Mavoko inapitia uhakiki.Taarifa itatoka,” limeandika baraza hilo kwenye akaunti yake ya Twitter.

Video ya wimbo huo iliyofanyika nchini Afrika Kusini inaonesha wanawake waliopo kwenye Jacuzzi huku maziwa yao yakiwa wazi licha ya kupakwa rangi ya dhahabu.

Mitandao ya Whatsap, Facebook Yamtesa Waziri wa JPM

$
0
0

Matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii yameendelea kulalamikiwa kuathiri mafanikio ya wanafunzi, licha ya kuwapo zuio wasiitumie wakati wa masomo.

Kilio cha hivi karibuni kuhusu mitandao hiyo ni cha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako aliyesema miongoni mwa changamoto zinazosababisha ongezeko la mmomonyoko wa maadili kwenye jamii ni pamoja na wanafunzi kutumia muda mwingi katika mitandao hiyo.


Profesa Ndalichako alisema wanafunzi wamekuwa wakitumia mitandao hiyo kwa kusoma, kuwasiliana na kusambaza picha zisizokuwa na maadili. Kwa hapa nchini mitandao inayopendwa na watu wengi ni Whatsap na Facebook.


Alisema kutokana na hali hiyo baadhi yao hafanyi vizuri katika masomo yao, hivyo kila mzazi, taasisi za kidini zinatakiwa kushiriki katika kusaidia kuondoa athari hizo.


Profesa Ndalichako alisema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa wanafunzi wa sekondari za Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya ‘Kampeni ya Kitaifa ya Kujenga na Kukuza Maadili, Haki za Binadamu, Uwajibikaji, Utawala Bora na Mapambano dhidi ya Rushwa kabla ya kufikia kilele cha Siku ya Maadili nchini Desemba 10, mwaka huu.


“Lakini kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya wazazi na walezi unakuta wanatetea watoto wao wanapofanya makosa na hawatoi ushirikiano, sasa kwa mazingira hayo tutakuwa tunajenga kizazi cha namna gani?” alihoji.


Alisema adhabu kwa wanafunzi zinatakiwa kutolewa kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya shule badala ya msukumo kutoka nje. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Binto Musa alisema mmomonyoko wa maadili unasababishwa na uwezo mdogo wa kuchambua athari mbaya na nzuri zinazotokana na utandawazi.


Mwalimu wa Sekondari ya Azania, Hamida Mgalu alisema mzazi na mwalimu wakishirikiana, wanafunzi watakuwa na maadili.

Wakenya Wamtamani Rais Magufuli, Wadai Wanatamani Aende Kugombea Urais Kwao

$
0
0

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Kenya (COTU), Bw. Francis Atwoli amesema anaikubalia kasi ya Rais Magufuli katika kupambana na rushwa.

Pia amewataka Watanzania wamuunge mkono badala ya kulalamikia kasi kwani wao wanatamani mwakani aende kugombea kwao katika uchaguzi mkuu ujao.
Ametoa kauli hiyo katika Mkutano Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere ulioko Chuo cha Mipango, nje kidogo ya mji wa Dodoma, uliofunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

“Ninawasihi wanaTUCTA suala la rushwa msilipe nafasi. Mpambane nayo kwa sababu kule kwetu imeota mizizi. Muungeni mkono Rais Magufuli, badala ya kulalamika kuwa kasi yake ni kubwa mno. Mnasema eti ana spidi sana, mkiona taabu mtuazime japo kwa mwaka mmoja ili aje atunyooshee mambo kule kwetu,” alisema huku akishangiliwa.

Amewataka wahimize uhusiano uliopo baina ya vyama vya wafanyakazi, waajiri na Serikali iliyopo madarakani na kuwataka wadumishe umoja miongoni mwa viongozi na wanachama mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi.

Mwanafunzi Apigwa Risasi na Polisi Dar, Askari Wawili Watiwa Mbaroni

$
0
0

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari Gerezani, Shakil Sures amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kujeruhiwa kwa risasi na polisi kwenye mazingira ya kutatanisha. 


Tukio hilo lililotokea Jumatatu eneo la Fire, Upanga licha ya watu kusikia milio ya risasi, kushuhudia polisi wakipita na kumuona kijana huyo akiwa tayari kajeruhiwa, lakini hakuna mwenye maelezo sahihi kuhusu nini kilitokea hadi askari hao wakachukua hatua hiyo. 


Baadhi ya waliokuwapo eneo la tukio siku hiyo walidai kuwaona askari waliokuwa eneo hilo wakirusha risasi, bila kujua walikuwa wakipambana na nani. 

Mmoja wa mashuhuda, Athumani Simba alidai walidhani ni majibizano ya risasi kati ya askari na majambazi, baada ya kuona gari la polisi likipita eneo hilo. 


“Niliwaona askari wawili wakielekea eneo la Fire huku wakipiga risasi, ghafla nilimuona mwanafunzi akilia huku akiwa ameshika mguu wake akiomba msaada,”alisema Simba. 

Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema mwanafunzi huyo alifikishwa hospitalini hapo jioni ya Jumatatu na kwamba jeraha lake linaendelea vizuri. 


“Tumempokea mwanafunzi Shakil juzi jioni na kidonda chake kimesafishwa na kinaendelea vizuri,” alisema Aligaesha. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Hamduni Salum alisema upelelezi kuhusu tukio hilo unaendelea. Hata hivyo, hakueleza mazingira ya tukio lenyewe yalivyokuwa. 


“Tunawashikilia askari polisi wawili waliokuwa zamu siku hiyo ya tukio, upelelezi unaendelea ili kuangalia kwa nini walitumia nguvu kubwa kiasi hicho,”alisema Kamanda Salum.

Hawa ndio mastaa waliotajwa kwenye Most Stylish East African Females 2016

$
0
0

Kituo cha runinga cha MTV Base kimeyataja majina ya mastaa wa kike kutoka Afrika Mashariki wanaojulikana kama Most Stylish East African Females.

Mastaa waliotajwa na kituo hicho ni pamoja na Vanessa Mdee (Tanzania), Lupita Nyong’o (Kenya), Zari (Uganda), Juliana Kanyomozi (Uganda),Victoria Kimani (Kenya) na Avril (Kenya).

Wengine waliotajwa ni pamoja na Rosa Ree kutoka lebo ya The Industry inayomilikiwa na Navy Kenzo, Sheebah Karungi (Uganda) na DjEynie (Kenya).

Makonda Aagiza Kukamatwa Kwa Mwenyekiti wa Mtaa Gongolambotona Kumweka Ndani

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameliagiza jeshi la polisi kumkamata mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Gongolamboto, Bakari Shingo baada ya kutuhumiwa kukusanya mapato kwa kutumia risiti anazozichapisha mwenyewe kinyume na Halmashauri inavyoagiza pamoja na kutoitisha mikutano ya hadhara kwa muda mrefu na kushirikina na wahalifu

Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi kulalamika kwa kumtuhumu mwenyekiti huyo kukaa muda mrefu bila kusoma mapato ya mtaa huo pamoja na kughushi stakabadhii za mapato.

Lawama hizo zimempelekea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambaye yupo kwenye ziara yake katika wilaya ya Ilala Pugu Kajiungeni, kumuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni kumsweka rumande Mweyekiti huyo mpaka upelelezi utakapo kamilika.

Akitoa ushahidi kuhusu sakata hilo Mkazi wa Gongo la Mboto na Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Pili Seif ameeleza kuwa hiyo imekuwa ni tabia ya mwenyekiti huyo kwa muda mrefu na taarifa zimefikishwa kwenye mamlaka husika ikiwemo kwa Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema, Mkurugenzi Msongela Nitu na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Viewing all 104771 articles
Browse latest View live




Latest Images