Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104768 articles
Browse latest View live

FULL INTERVIEW: Kitu Diamond Amesema Kuhusu Ommy Dimpoz, Nani Mkali, Universal, Rihanna na Rick Ross

$
0
0
Mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz alifanya mahojiano na XXL ya CloudsFM November 23 2016 chini ya Watangazaji B Dozen, Mami Baby na Kennedy na kuongea ishu nyingi kwa uzito ikiwemo kusaini mkataba na Universal, maneno kati yake na Ommy Dimpoz, bonyeza play hapa chini kusikiliza kila kitu:

ALI KIBA Ashinda Tuzo za NAFCA na The Nol

$
0
0
Alikiba ashinda tuzo mbili za The Nollywood & African Film Critics (NAFCA)

Alikiba ameshinda vipengele viwili kwenye tuzo za heshima kubwa za The Nollywood & African Film Critics (NAFCA) ambazo hutolewa nchini Marekani.

Tuzo za mwaka huu zilitolewa wikiendi hii kwenye ukumbi wa Alex Theatre of Glendale, huko California. Zilikuwa ni tuzo za 6 na zilionekana katika nchi mbalimbali duniani.

Alikiba ameshinda kipengele cha Favorite Artist of The Year na Favorite Song of The Year

NDOA Yangu Imekuwa Chungu..Ndugu wa Mume Wamezidi, Nishauri Nifanyeje?

$
0
0
Mimi nipo kwenye ndoa miaka saba sasa na tuna mtoto mmoja, tunaishi Nyanda za juu kusini. Tuliishi kwa amani miaka mitatu tu, tukiwa mimi na mume wangu na mtoto. Baada ya hapo imekua tabu, mimi kwetu kuna ahueni ya kiuchumi, yaani sitegemewi na wazazi wangu labda mimi ndio niombe msaada kwako. Lakini kwa upande wa mume wangu imekua tatizo yeye ndio anaetegemewa, yaani ndio star kwao.

Sasa kadiri siku zinavyozidi kwenda ndio wategemezi wanazidi, watoto wa ndugu zake wa kuwasomesha ndio wanazidi, applicants wa misaada kutoka kwao ndio wanazidi wanaomba hata ambavyo wangeweza kujisaidia wenyewe kwa jinsi anavyowaendekeza.

Anafanya bidii kuwatafuta watoto wa ndugu zake hata waliotelekezwa na wazazi wao tena wakingali hai anawajaza home. Yote hayo ninayavumilia na ninapambana nayo. Mimi sijabahatika kupata ajira tangu nimehitimu masomo yangu, yeye ndio ana ajira. Lakini mimi sijabweteka najishughulisha na kilimo na hata chakula tunachokula (mpunga na mahindi) nalima mwenyewe.

Sasa kila nikijaribu kumuelimisha kwamba sichukii kuwasaidia ndugu zake na hata kuwasomesha watoto wa ndugu zake bali kuwepo na namna ya kuwasaidia wakiwa makwao na si kuwajaza hapa home inaleta stress maisha yanazidi kuwa magumu mwenzangu hataki tena ananichefua kwa kunijibu ati kwani kuna shida gani mbona chakula kipo ndani, yaani hakuna shida ya chakula kabisa.

Hakika majibu haya yananivunja moyo kuendelea na kilimo, nawaza labda niache kabisa kulima ili nione kama ataweza kununua chakula cha kulisha familia kubwa namna hii. Kubwa zaidi sasa na linalonichanganya hasa na ninaomba ushauri wenu ndugu ; Ni kwamba kama vile hawa waliopo hapa home na tunaowasomesha huko makwao hawatoshi, sasa amemtafuta binti wa marehemu kaka yake ambae ana umri wa miaka 24 na ana watoto wawili, anataka amtoe huko anakoishi (anaishi mikoa ya Mashariki, anajishughulisha na kuuza bar, kwa mujibu wa maelezo ya baba mtu) aje tuishi nae hapa home.

Nimemuuliza sababu ya kumchukua binti mkubwa kama huyo tena aliyezoea maisha ya bar; kanijibu anatanga tanga kwa sababu baba yake alikufa, ngoja aje tukae nae tuwasomeshe na hao watoto wake (binti kasema watoto wote hawana baba); hivi ninapoleta uzi huu baba mtu kishaanza mchakato wa kutafuta shule kwa ajili ya mtoto (mjukuu) mkubwa ambae ana miaka sita. Anamtafutia private school aanza chekechea mwakani.

Kazi anayofanya ni ya kipato cha kawaida kiasi kwamba misaada imezidi uwezo (wanadrain) mara nyingi tunabaki hatuna hata senti tano! Hata ninapofurukuta kwa kufanya biashara ndogondogo mbali na kilimo najikuta mtaji unakata, nabaki kuzubaa tu.

Sasa jamani mwenzenu kama binadamu, tena kijana mwenye ndoto za maisha ya mbeleni nashindwa la kufanya, naishiwa hamu ya hii ndoa yangu, natamani nitoke nikapange na mwanangu nipambane kivyangu lakini tena roho inanisuta! NIPO NJIA PANDA, nifanyeje jamani na tabia ya mwanaume huyu! Na hasa huyu binti na watoto wake, natamani nipate namna nyingine ya kumsaidia lakini asije hapa home coz tayari tupo kumi hadi sasa, na hiki ni kipindi cha likizo huwa tunafika mpaka kumi na tano na haya ni maisha ya mjini (u can imagine)!

Msaada jamani!

Nawaomba wale wanaolete mizaha wapite kimya coz nahisi wataniongezea stress

By Sisame

Godbless Lema na Siasa Ngumu Zisizo Wapendeza Watawala...

$
0
0
Kuna Godbless Lema mmoja tu hapa Tanzania kwa Africa Mashariki unaweza kumfananisha na Kizza Besigye ambaye police hawakatiki nyumbani kwake.

Hawa ni wanasiasa ambao wameamua kufanya siasa ngumu zisizo wapendeza watawala.
Ni watu ambao kusikia kukamatwa na police kwao siyo story tena Bali inaweza kuwa story siku watakapo amua kukaa kimya, Ila kusikia wapo Central police, Wanapandishwa kizimbani,Wapo Magereza hilo siyo jambo geni wala halitakuwa geni Bali tutastuka na kushangaa pindi watakapo kaa kimya tutakuwa na maswali mengi ya kujiuliza.

Ujasiri wao wa kufanya siasa ngumu za level hiyo unawabakisha kuwa Wanasiasa bora wa upinzani wakati wote wenye ushawishi Mkubwa wakati wote.

Ushawishi wao hupelekea Mara kwa Mara kwa wafuasi wao kupata shida Mara nyingi kila waenda mahakamani hukutana na vigingi vingi vingi Mara kukamatwa Mara kufukuzwa ili mradi wasionekane wapo wengi mahakamani kwenda kuwatia moyo.

Wataendelea kubaki kuwa Wanasiasa wa saisa ngumu za kiafrika ambao wameamua kupambana na changamoto hizo wazi wazi bila kuwa na chembe ya uoga....

By Henry Kilewo

PICHA: Waziri Nape Alipomtembelea Diamond Platinumz Ofisini Kwake

$
0
0
Waziri wa Habari Nape Nnauye alipomtembelea Diamond Platinumz ofisini kwake jana. Bila shaka amenogewa na midundo ya Kokoro.

Barakah The Prince aumizwa na mengi kwenye muziki

$
0
0
Hitmaker wa Nisamehe, Barakah The Prince ametoa yake ya moyoni kuhusu kinachomuumiza kwenye Bongo Fleva.

Muimbaji huyo amedai uteam ndio sababu iliyochangia kukosa tuzo kubwa za kimataifa za muziki. Kauli hiyo ya muimbaji huyo imekuja wakati ambapo kumekuwa na vita ya maneno ya kejeli na matusi kati ya Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz.

Kupitia mtandao wa Instagram, Barakah ameandika:

Mungu saidia game ya #Tanzania tupendane na tuheshimiane(….)inasikitisha sana team team zinarudisha sana music industry yetu nyuma..tumekosa tunzo nyingi kubwa na zamaana,sababu ya kukosa umoja na mshikamano wa mashabiki..tunatengeza matabaka baina ya mashabiki na mashabiki…Heee Mwenyezi MUNGU ingilia kati swala hili.. #NISAMEHE link kwa bio yangu

Kadinda Ataja Sababu Za Zutoonekana Na Mademu

$
0
0

Habari na Imelda mtema
Unapowazungumzia wanamitindo wakubwa Bongo, huwezi kuacha kumtaja Martin Kadinda. Licha ya kupata umaarufu kupitia kazi yake, Kadinda aling’ara zaidi alipoanza kumsimamia supastaa mkubwa Bongo, Wema Sepetu akiwa meneja wake.

Kazi yake ya uanamitindo imempatia tuzo kibao zikiwemo Mwanamitindo Bora Afrika Mashariki 2015, Mbunifu Bora wa Mavazi ya Kiume Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo na nyingine nyingi.

Juzikati alipiga stori na gazeti hili na kufunguka mambo kibao kuhusu maisha yake na kueleza sababu inayomfanya asipende kuonekana na mademu. Shuka nayo:

Amani: Mambo vipi Kadinda! Unaweza kumwambia msomaji umaarufu wako umetokana na nini?

Amani: Umaarufu wako ulitokana na nini?

 Kadinda: Ulitokana na  na kazi yangu ya ubunifu wa mavazi ndio chanzo cha umaarufu wangu.

Amani: Kuna ukweli wowote kuwa jina lako lisingekuwa kubwa kama usingekuwa meneja wa Wema?

Kadinda: Ukubwa wa jina langu umetokana na kazi zangu ila kwa kiasi kikubwa ni kwa watu maarufu niliowavalisha wamenisaidai sana mimi kufahamika  na pia moja malengo yangu ya kummeneji wema ni kuongeza wigo katika biashara zangu na kiukweli amenisaidia sana ninamshukuru siku zote kwa hilo kila wakati.

Amani: Changamoto gani unakutana nazo kama meneja wa staa mkubwa Bongo?

Kadinda:  Unapokuwa una hela unaishia kufanya kazi kutokana na  kile anachotaka  mhusika pia ni ngumu sana kumsimamia mtu ambaye ana malezi tofauti  na uliyolelewa wewe hivyo inakuchukua  muda sana kuelewana na kuendana njia moja  na pia binadamu tunaishi kutokana na kile tunachokiamini hivyo changamoto za watu wanaotuzunguka  na utofauti wa ndoto ndio changamoto zenyewe.


Amani: Kipindi cha Wema yupo na aliyekuwa kigogo wa Ikula  Ck, vilizuka vitu vingi sana kuwa uliweza kujenga nyumba kwa kutumia hela zake wakati yeye hana nyumba unazungumziaje hilo?

Kadinda: Naomba nirekebishe kauli za watu mimi  sina  nyumba nina kibanda ambacho nimejenga kwa nyuma ya nyumba yetu  familia hivyo huwa napaita banda la uani na hata hivyo nimejenga kipindi cha  ‘ Single Buttons’ na n ilikuwa sijaanza kufanya kazi na Wema kama meneja wake.

Amani: Sasa kama wewe meneja  wake kwanini kwa kipindi chote hujaweza kusimamia kuwa na nyumba yake mwenyewe?

Kadinda:  Unajua suala la nyumba kwa Wema kutokuwa nayo mpaka sasa ni aina ya nyumba anayotaka kujenga  inahitaji hela nyingi sana  lakini kwa vile tayari ana miliki kiwanja  hivi karibuni watu wataiona  hiyo nyumba ninayoongelea.

Amani: Ni mafanikio gani umeyapata mpaka sasa hivi kupitia unamitindo?

Kadinda: Kwa kweli sijafika sehemu ambayo naweza kusema nina mafanikio ila kikubwa nimeweza kuitangaza nchi yangu kupitia sanaa yangu hiyo na pia kuwa na mahusiano mazuri na wabunifu wakubwa  toka  nchi mbalimbali duniani na nimeweza kutembea sehemu tofauti.

Amani: Unazungumziaje watu kusema kuwa husimamii kazi za Wema ipasavyo  kwa maana anafanya vitu vingine ambavyo sivyo?

Kadinda: Wema sio mtoto mdogo mimi napaswa kumshauri tu na kumuonesha njia  suala  la yeye kutofuata  ninachomueleza  ni maamuzi yake binafsi  na pia ikumbukwe pia nafasi ya kummeneji Wema sio kwamba natembea nayo kama kuna mtu anahisi anaweza kufanya hivyo anakaribishwa.

Amani: Vipi kuhusu harusi yako maana ilivuma baadae ikapotea   na vipi kuhusu mchumba wako huyo?

Kadinda: ( kicheko) Hilo watu walizusha tu ,muda w akuoa mimi ukifiuka tu wataona picha tu kwetu suala la ndoa ni la kifamilia tu zaidi hao wengine wataishia tu kulike picha kwenye mitandao ya kijamii.

Amani: Kuna video ilivuma hivi karibuni ikimuonyesha Wema na mwanamitindo Calisah wakiwa kwenye picha tata unalizungumziaje hilo kama meneja?

Kadinda: Mimi sijaiona  nimesikia tu na hata kama ningekuwa nimeona nadhani Wema, Wema peke yake ndio anapaswa kutoa majibu ya kuhusu video hiyo maana ni maisha yake halisi.

Amani: Baada ya kutoa nguo yako aina ya Kwachukwachu unejipanga na kitu gani kingine?

Kadinda: Inachukua miaka miwili kuja na vazi jipya  kwahiyo tukutane 2017.

Amani: Nakumbuka kama kipindi cha nyuma ulishawahi kuwa meneja wa Lulu ni sahihi?

Kadinda: Hapana Lulu ni mtu wangu wa karibu tangu tupo shule ni kama mdogo wangu  na tunashauriana vitu mbalimbali.

Amani : Hivi karibuni  ilidaiwa mlikuwa kwenye mgogoro mzito na Wema mpaka hamkuwa mnazungumza vipi kuhusu hilo,na pia hujafikiria kuwakalisha pamoja Muna na Wema wakamaliz atofauti zao?

Kadinda: Migogoro yangu na Wema inatokea mara nyingi tu kwa hiyo ni kawaida kwetu kuhusu Muna na Wema sio mimi niliwakutanisha mwanzo kwenye urafiki wao  hivyo watapatana wenyewe tu kwasababu migogoro kwa marafiki ipo tu.

Amani: Kama meneja Wema alishakuwa na marafiki kama Kajala, Wema, Snura na Aunt ungependa kati ya hawa ni yupi angekuwa lakini wa kudumu kwake.

Kadinda: Mimi ningemshauri dada zake au mama yake lakini pia  unajua urafiki ni swala la mtu binafsi siwezi kusema yupi anamfaa, pia ili Wema aweze kufanikiwa zaidi anapaswa kufanya kazi zake mwenyewe.

Amani: Wanawake wengi wanakusema kuwa unaringa kwasababu hata ukiwaona wazuri huwatongozi japokuwa hujawahi kuonekana na mwanamke?

Kadinda: Naheshimu mwanamke hasa kwa kuwa  naamini sio kila mwanamke nitakayekuwa  nae kwa mahusiano  ndo nitakayemuoa na hiyo kwasababu nina binti yangu mdogo sitaki akue akiona habari zangu za mahusiano sio malezi ninayomlea ndio maana  familia yangu na mahusiano yangu nayaweka mbali na media.

Amani: Kama meneja ungetamani Wema  awe na nafasi gani katika jamii?

Kadinda: Kila anayempenda Wema,anataka kuona akiwa na nyota inayong’aa Tanzania na Afrika nzima kwa ujumla hilo ndio ombi langu kwake tu.

Amani: Kuna ugomvi ulitokea kati ya wewe na mama Wema kwa madai kuwa ulipewa hela ya kumnunulia Wema kiwanja ukanunua kisichokuwa na hadi ya pesa uliyopewa vipi hilo?

Kadinda: Sijawahi kuigombana na mama Wema hayo ni maneno  tu nagombanaje na mama sasa? Siwezi ni maneno tu.

Amani: Kumbe una mtoto nilikuwa sijui

Kadinda: ndio nina binti wa miaka nane sasa nilimpata nikiwa shule.

Amani: Nakushukuru sana Kadida kwa ushirikiano wako?

Kadinda: Asante sana.

GPL

Namchukia Mwanaume Aliyenipa Mimba - Nisha Bebe

$
0
0

Msanii wa bongo movie Nisha Bebe amesema ujauzito wake unampa hisia tofauti na mawazo mpaka anafikia hatua ya kupost mambo tofauti tofauti kwenye mitandao yake kwa kuwa hampendi mwanaume aliyempa ujauzito huo.

Akiongea ndani ya eNewz Nisha amesema amevumilia miezi mitano bila mtu kujua kitu chochote juu ya mimba yake lakini kwa sasa ameshindwa kuvumilia na hiyo ni kutokana na maumivu anayoyapata na kwamba mimba aliyoibeba ni ya mtu ambaye hampendi tena.


Pia Nisha amesema mwanaume aliyempa mimba ni mtu ambaye anapenda kujionesha sababu ambayo ilipelekea wakaachana pia Nisha amesema anamuomba Mungu mtoto wake asifanane na baba yake na kama ikitokea akifanana naye hatakuwa budi ya kumficha bali atampa mtoto wake kila anachokitaka kwa kuwa mtoto hana kosa lolote.

Tanzania Yaporomoka Kwa Nafasi 16 Viwango vya FIFA

$
0
0

Tanzania imeporomoka kwa nafasi 16 katika viwango vya soka vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa mwezi Novemba

Kwa mujibu wa orodha mpya iliyotolewa leo (Novemba 24) na FIFA, Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya 144 mwezi Oktoba hadi 160 mwezi huu kati ya mataifa 205 ambayo ni wanachama hai wa FIFA.

Kushuka huku kwa viwango kunatokana na kujikusanyia pointi 146 ikilinganishwa na pointi 212 ilizokuwa nazo mwezi Oktoba, ikiwa imecheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe na kupoteza kwa kipigo cha mabao 3-0.

Kwa upande wake Zimbabwe, imepanda kwa nafasi 8 kutoka nafasi ya 110 hadi ya nafasi ya 102.

Kwa mataifa ya Afrika Mashariki Rwanda imepanda kwa nafasi sita hadi nafasi ya 101 wakati Kenya ikishuka kwa nafasi 4 hadi ya 89 na Uganda imeshuka kwa nafasi moja kutoka 72 hadi 73 ikiwa ndiye kinara wakati Burundi imepanda kwa nafasi 5 kutoka nafasi ya 138 hadi 133

Mataifa mengine katika ukanda wa CECAFA, Ethiopia imepanda kwa nafasi 11 hadi nafasi ya 115, huku Sudani ikipanda kwa nafasi 8, kutoka nafasi ya 148 hadi ya 140.

Afrika inaongozwa na Senegal nafasi ya 33 ikifuatiwa na Ivory Coast nafasi ya 34, Tunisia nafasi ya 35, Misri 36 na Algeria ni ya 38.

Katika 10 bora, Argentina imeendelea kushika nafasi ya Kwanza ikifuatiwa na Brazil, Ujerumani, Chile, Ubelgiji, Colombia, Ufaransa, Ureno, Uruguay na Hispania.

Baraka Asema Watu Hawajui Yeye na Ali Kiba Walipitoka..Achukia Kuitwa Chawa wa Alikiba

$
0
0

Mkali wa Bongo fleva Baraka Da Prince amewapa makavu mashabiki ambao wanamsakama kwa kumwambia yeye ni mfuasi wa Alikiba.

Akiongea na Perfect255 @barakahtheprince_ amedai kuwa watu hawajui yeye na @officialalikiba wametoka wapi na ni jinsi gani wanaishi kiasi kwamba wanakuwa karibu kiasi hicho.
.
“Alikiba ni miongoni mwa wasanii ambao ni Role Model wangu, Alikiba ni msanii ambaye ameni inspire mimi katika muziki wangu kwahiyo mimi hata kuimba nyimbo yake sioni kama ni kitu cha ajabu. Na ukizingatia ni mtu ambaye nafanya nae kazi katika record label moja kwahiyo ni brother ambaye muda mwingi nipo naye. Ninapo mpresent pale ambapo yeye hayupo sioni kama ni ajabu kwasababu sometimes mimi naenda kwenye show nakutana na fans wa Kiba, kwahiyo nikipiga ngoma yake hata moja inakuwa ni poa.” alisema #Barakah
#letitshine

Audio: Ommy Dimpoz Afunguka Kisa Cha Kukosana na Diamond Platnumz

$
0
0
Katika interview ndefu aliyofanyiwa Alhamis hii kwenye kipindi cha XXL kupitia Clouds FM, Ommy Dimpoz amefunguka kwa kina visa na mkasa vilivyopelekea akosane na swahiba wake wa zamani, Diamond Platnumz.


Ommy amelazimika kusimulia hayo baada ya Jumatano kupitia kipindi hicho hicho, Diamond kuelezea uhusiano wao na jitihada ambazo Ommy amewahi kuzifanya ili kuomba wayamalize.

Hitmaker huyo wa Wanjera amesema katika urafiki wao wote na Diamond, ni yeye ndiye alikuwa mwaminifu (loyal) zaidi katika kuuenzi lakini kuna wakati mwenzake alianza kuonesha kumficha baadhi ya vitu hasa vinavyohusiana na kazi.

Amesema mara zote alikuwa akimshirikisha kwenye mipango yake ikiwa ni pamoja na kumsikilizisha nyimbo zake kabla ya kutoka ili kumuomba ushauri na kutolea mfano alivyomsikilizisha wimbo wake Tupogo na kumweleza kuwa amepanga kuongeza vionjo vya saxaphone kwa kumtumia King Malou. Hata hivyo anadai kuwa siku chache baadaye alishangaa kumkuta Diamond akiwa na mpiga saxaphone huyo akiingia kionjo kwenye wimbo wake ‘Number 1’ katika studio za MJ Records.

“Nikajiuliza kuwa pengine labda alikuwa na wazo kama hilo, sikutaka kujiuliza mengi, unajua sometimes ukijiuliza mengi utaenda far zaidi, nikauchuna tu,” alisema Ommy.

Anasema baadaye alisikia akimuambia Marco Chali kuwa amchomee CD kwakuwa anasafiri na walipomaliza Ommy alimuuliza kuhusu safari hiyo lakini Diamond alimuambia kuwa alikuwa akimdanganya tu producer huyo wa MJ Records na kwamba hakuna safari yoyote.

“Kesho yake naona anapost picha yupo kwenye ndege, nikajiuliza ‘huyu si nilimuuliza jana kama anasafiri, si ni mwanangu’, nikasema anyway labda ni safari imejitokeza ghafla you never know,” ameeleza Ommy.

Baadaye mshkaji wao Halima Kimwana alikuja kumwambia kuwa Diamond alienda Afrika Kusini kufanya video yake kitendo kilichomwacha na maswali mengi lakini anadai alipuuzia. Amesema baada ya muda ndipo Diamond alipofanya uzinduzi wa video ya Number 1 na yeye mwenyewe kualikwa.

Amesimulia tukio jingine ambalo lilimuumiza ni baada ya kumuomba Diamond waende pamoja Marekani kwenye tuzo za Afrimma kwa gharama zake mwenyewe ili amsaidie kumtafutia connection.

“Sasa kila siku nikiuliza safari lini naona mtu anaingilia huku anatokea huku.”

Anadai swahiba wake huyo aliendelea kumchenga hadi alipokuja kugundua amesafiri bila kumwambia na siku hiyo akawa hapokei simu zake. “Baada ya kupita masaa mengi, jioni anakuja kunicheck yuko transit South Africa ‘mwanangu ilitokea ghafla nikasafiri.’ Kwahiyo nikajiuliza nikasema hapa kuna style za kupunguzwa. Kibinadamu unajua lazima uchekeche.”

Ommy pia alielezea jinsi ambavyo alikuwa mtu wa kwanza afanye collabo na Davido na alikuwa tayari kutoa $3,000 lakini baadaye Sallam, meneja wa Diamond, alikuja kumweleza kuwa Dangote yupo tayari kutoa $5,000 ili wafanye naye. Anasema aliachana na collabo hiyo na kutafuta nyingine na Iyanya ambayo nayo pia alikuja kugundua baadaye rafiki yake huyo ameshaiwahi.

Hata hivyo Ommy amedai kuwa kitendo cha yeye kumtumia Wema Sepetu kwenye video ya Wanjera ilikuwa kama sababu tu ya Diamond kuvunja ushkaji wake. Amesema ni kwasababu amekuwa na urafiki na Wema hata kabla ya kukutana na Chibu na kwamba hadi ‘first kiss’ yao aliishuhudia kwa macho yake.

Ommy ambaye jina lake ni Omari Nyembo, amesema kukosana kwao hakukuwa sababu ya yeye kumchukia pia Wema kwakuwa urafiki wao haukusika na kwamba kipindi Ommy anaenda SA kufanya video hiyo, Wema alikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine na kukanusha kuwahi kutoka naye kimapenzi.

“Kwahiyo nikaona kuna suala lilikuwa kwamba mtu ametafuta sababu. Hebu niambie Wema amekuwa na mahusiano na watu wangapi wengine ambao leo hii bado unaona D yuko nao close? Kwanini nilipokuwa naye mimi tu ndio imekuwa tatizo?” amehoji staa huyo.

Kuhusu tuhuma za kutaka ‘kupumuliwa’ zilizotolewa na Diamond kwenye post yake ya Instagram dhidi yake, Ommy amesema pale ‘mtu anapotaka kukutana hakuchagulii tusi.’

“Sometime unapoitoa kauli, huwezi kujua itamwathiri mtu kwa kiasi gani, pengine itamwathiri kwa kiasi kikubwa kwasababu kuna mtu ataichukua ile kauli kiushabiki. Hata kwenye comments, mimi ninaweza kuzima comments zangu kwenye Instagram lakini nimeziacha na ukisoma comments utaona kabisa mwingine anakutukana ‘we shoga.’ Lakini as long as mimi ninajua mzima hainiathiri, kwanza hakuna tusi jipya, imeanza kutukanwa mimba!”

SIKILIZA HAPA:

Diamond Atoa Jibu la Utata Kufuatia interview ya Ommy Dimpoz

$
0
0
Inaitwa Tit for Tat! Baada ya Ommy Dimpoz kueleza kwa kina kuhusiana na sababu iliyopelekea wakakosana na Diamond, muimbaji huyo wa Salome, amejibu kupitia Instagram.

Majibu ya Diamond ni ya mafumbo kiasi na tayari yamepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki huku wengi wakichukizwa na kauli yake.

Ameandika:

Basi nlivyokuwa Mshamba Nikajua Mtu Mwenye Roho Mbaya na Mbinafsi Mungu ndio Humuadhibu na Kumfelisha kwa Roho Mbaya lake ili asifanikiwe… halaf Mwenye Roho nzuri Mungu Humlipa kwa Kumfanya afanikiwe zaidi na zaidi…. Asa nashangaa Mwenye Roho Mbaya eti Mungu ndio Kamfanikisha, halaf Maskini ya Mungu Mwenye roho nzuri eti Miguu juu…..au pengine labda Mwenyez Mungu kakosea kidogo kwenye Mahesabu yake..???😟 hii nayo ni #KOKORO ujue

PICHA 3: Mwanaume Aliyekuwa Akijifanya Mwanamke na Kutapeli Wanaume Akamatwa

$
0
0
Mwanaume mmoja nchini Uganda aliyefahamika kwa jina la Ivan Bebeto amekamatwa na Polisi akidaiwa kuwa amekuwa akijifanya yeye ni mwanamke na kuwatapeli wanaume.

Mwanaume huyo anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Katwe jijini Kampala akidaiwa kuwa hujifanya mwanamke ambapo huvalia mavazi ya kike na kujiweka kama mwanamke kisha kuwatapeli wanaume. Taarifa kutoka nchini humo zimeeleza kuwa mtuhuiwa huyo amekuwa akifanya ujanja huo kwa muda mrefu sasa hasa katika miji ya Nairobi, Kampala na Bujumbura.

Akiwa katika muonekano wa kike, mtuhumiwa huyo hujiita Queen.

Aidha, siku ya tukio hilo alikamatwa baada ya mwanamume mmoja aliyekuwa tayari amekubaliana nae kuanza kumtilia mashaka baada ya Bebeto kukataa kwenda nyumba ya kulala wageni kama walivyokuwa wamekubaliana kabla ya kupewa malipo.

Baada ya hali hiyo, mwanaume huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja alipiga simu Polisi na ndio Bebeto akakamatwa.

Rais Magufuli: Niliivunja Bodi ya TRA Baada ya Kuidhinisha Mabilioni ya Pesa Kwenda Benki Binafsi Kama Fixed Deposit

$
0
0
Novemba 20 mwaka huu Rais Magufuli alitengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo, Bernard Mchomvu na kuivunja hiyo bila kueleza sababu zozote.

Rais John Magufuli ameeleza sababu za kuivunja Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuwa ilitokana na bodi hiyo kuidhinisha mamlaka hiyo kuweka mabilioni ya fedha kwenye benki binafsi

Novemba 20 mwaka huu Rais Magufuli alitengua uteuzi wa mwenyekiti wa bodi hiyo, Bernard Mchomvu na kuivunja hiyo bila kueleza sababu zozote.

Akizungumza leo wakati wa sherehe za mahafali ya Chuo Kikuu Huria yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani, Rais Magufuli amesema kuwa TRA walichukuwa fedha mabilioni na kuweka fixed account benki 8 binafsi na bodi ikaidhinisha.

 TAZAMA HAPA VIDEO:

Walichoandika Diamond na Wema Sepetu kuhusu Ommy Dimpoz

$
0
0
Upo usemi kwamba fahari wawili hawakai zizi moja, ndicho kinaonekana kutokea kati ya mastaa wakubwa wa Bongo Flava nchini, Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz ambao waliwahi kuwa marafiki zamani, lakini sasa wamethibitisha wazi kuwa hawako poa kama mwanzo.

Kupitia Interview iliyofanywa ndani ya show ya XXL kupitia Clouds FM jana November 23, 2016, Diamond Platnumz alifungua kifua na kueleza mambo mengi sana juu ya tofauti yake yeye na Ommy Dimpoz ikiwemo lakini hakikuwekwa wazi sana chanzo cha kutofautiana kwao.

“Hivi jamani kweli mimi nigombane na Ommy Dimpoz kwasababu ya Wema Sepetu kweli? Siwezi kufanya hivyo. Mimi nafikiri tusilizungumzie nadhani wenye macho wameshanielewa kama hawajaelewa tangu jana waje kuelewa leo? watakuwa washaelewa. Dozen mimi naamua kumsitiri mwenzangu.” – Diamond

 Leo November 24, 2016 Ommy Dimpoz amepiga story na XXL ya Clouds FM pia, ambapo ameeleza kwa upande wake amepokeaje maelezo ya Diamond pamoja na ufafanuzi kuhusu ukaribu wake na watu ambao Diamond ameshatofautiana nao pamoja na kufanya kazi na Wema Sepetu.

“Mimi kwenda kushoot video ya Wanjera ndio ilikuwa sababu ya kutofautiana na Diamond, unajua mimi na Wema ni washkaji tangu hajaanza kuwa mpenzi wa Diamond, mimi nilimuweka Wema kwababu ana mashabiki wengi na nilitaka impact ya kazi yangu, mimi pia sijawahi kudate na Wema” – Ommy Dimpoz



Ushindi wa KRC Genk ya Mbwana Samatta Unaowafanya Watinge hatua Inayofuata Europa League

$
0
0
Usiku wa leo November 24 2016 timu ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ilicheza mchezo wake wa tano wa hatua ya Makundi ya UEFA Europa League dhidi ya timu ya Rapid Wien ya Austria.

KRC Genk katika mchezo huo wa tano walikuwa nyumbani katika uwanja wao wa Luminus, Genk wakiwa nyumbani walifanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 55 dhidi ya wageni wao Rapid Wien, kitu ambacho kimewasaidia kuibuka na ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Nikolaos Karelis dakika ya 11.

Kwa matokeo hayo Genk na Atletico Bilbao wanafuzu hatua inayofuata kutokana na wote kuwa na point 9 wakati Rapid Wien na Sassuolo ya Italia watakuwa wanasubiri mchezo wa mwisho wa kukamilisa ratiba, maana hata wakishinda watakuwa na point nane kila mmoja, point ambazo hazitoshi kuipiku Genk wala Atletico Bilbao.

FULL VIDEO: Paul Makonda Alivyoamuru Mwenyekiti Mwingine Akamatwe Katikati ya Mkutano

$
0
0
November 24 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salam, Paul Makonda ameendelea na ziara yake ya siku 10 ambayo lengo ni kukutana na wanannchi kwa ajili ya kusikiliza kero zao. Ilikuwa ni zamu ya Ilala na hapa ulikuwa ni mkutano wa hadhara Chanika, katika mkutano huo ulitawaliwa na kero kubwa moja ambayo ni suala la ardhi.

Moja ya kero iliyowasilishwa ni kuhusu mwenyekiti wa mtaa wa Zavala ambaye anatuhumiwa kuuza ardhi kinyume cha sherialikiwemo eneo lililotengwa kwa ajili ya kuhamishia wananchi wa kata ya Kipawa ili kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege.

RC Makonda baada ya kuwasikiliza baadhi ya wajumbe wa serikali ya mtaa waliotoa ushuhuda kuhusu tuhuma hizo aliamuru mwenyekiti kukamamtwa katikati ya mkutano. Unaweza kuangalia ilivyokuwa kwenye hii video hapa chini.


Ommy Dimpoz: Nilivurugana na Diamond Kisa Wema Sepetu, Aanika Bifu la Kiba na Diamond

$
0
0
STAA wa Bongo fleva hapa nchini, Ommy Dimpoz anayetamba na ngoma yake ya ‘Kajiandae’, amefungukia bifu lake na msanii mwenzake, Diamond Platinumz kuwa chanzo cha ugomvi wao ni Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu ‘Madam’.

Akizungumza leo Novemba 24, 206 wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, Dimpoz amesema mwanzoni walikuwa na urafiki mzuri na Diamond na walikuwa wakishirikiana mambo mengi kuhusu muziki wao, lakini baadaye hali ilikuwa tofauti baada, Diamond akaanza kumpoteza na kukwepa kufanya naye baadhi ya mambo kwa pamoja.

Dimpoz amesema hayo baada ya Diamond kusema mambo kadhaa kuhusu yeye wakati akifanya mahojiano jana kwenye kipindi hicho cha XXL.

Haya ndiyo maneno ya Ommy Dimpoz:

“Mimi nimefahamiana na Diamond miaka mingi kabla hajatoa hata wimbo wake wa Kamwambie.

“Diamond aliwahi kuniambia kuwa inabidi tuwe makini kwa sababu kuna watu wanasema mimi nakupeleka kwa waganga wangu.

“Lakini ilifika mahali nikaona kama anaanza kunikwepa.

“Kuna wakati hata nilipokuwa nikumuuliza kama anasafiri alisema hapana lakini unashangaa anapost picha yuko sehemu fulani.

“Nilimuomba twende wote AFRIMA Marekani akakubali, nilimwambia nitagharamia, lakini kila nikimuuliza safari lini hasemi.

“Siku nyingine nampigia simu hapatikani, alipopatikana yupo Afrika Kusini anaenda kwenye tuzo Marekani anasema ni ghafla.

“Mimi nilikuwa naonekana kama mzigo kwa Diamond, lakini sikujali maneno ya watu sababu nilijua nilipotoka naye.

“Mimi nilipanga kufanya ngoma na Iyanya (wa Nigeria) alipokuja Dar es Salaam, lakini nakuja kushtuka nakuta Diamond tayari amesharekodi naye.

“Mimi sikuwahi kugombana na Diamond, ni vitu vimetokea unaona tu mwenyewe kuwa hapa sitakiwi, unaamua kurudi nyuma.

“Baada ya choko choko zote, nilipo ‘shoot’ video ya Wanjera na kumuweka Wema (Wema Sepetu) ndio balaa lilipoanzia hapo.

“Mimi sikumweka Wema Sepetu kwenye wimbo wangu kwa makusudi, lakini ana amashabiki wengi na niliona hii itanisaidia.

“Wema ni rafiki yangu kitambo kabla hajaanza uhusiano na Diamond. Na walivyo-‘kiss’ mara ya kwanza kwenye gari nilikuwepo

“Mimi kuna wakati nilikuwa namuomba ata anitambulishe kama msanii wake kwa wasanii wakubwa ili tu nipate ‘connection’.

“Nashangaa kwanini Diamond achukie mimi kuwa karibu na Wema, mbona anaongea na wengine waliokuwa karibu naye, kwanini mimi?

“Mimi sina timu kwenye mitandao, labda mashabiki zangu tu, lakini sina timu yenye kazi ya kutukana au kubishana mitandaoni.

“Mimi sijali Diamond alivyonitukana, au wanaosema mimi shoga. Kikubwa nachoshukuru najijua kuwa mimi mzima, so sijali.

“Kuna wakati simu ilipigwa kutoka Sweden nikatumbuize, lakini Diamond alisema mimi nina nyimbo mbili na kutumbuiza sijui.

“Kuna wakati nilikuwa sina hela ya kutoa wimbo, nikamwambia Diamond anisimamie nitoe wimbo lakini hakufanya hivyo

Hata hivyo Dimpoz hakusita kumtuhumu Meneja wa Diamond, Sallam.

“Baada ya kuzungumzia ishu ya ‘viewers’, Sallam aliniambia kua kati ya vitu nilivyomuuzi ni kuzungumzia hilo.

“Nilipopost ‘insta’ kuhusu watu kununua ‘views’ YouTube, sikumtaja mtu, nilisema tu sasa hivi watu wanaweza.

““Baada ya kupost ‘insta’ kuwa kuna wasanii wananunua ‘views’ YouTube, nilikutana na meneja wa @diamondplatnumz, Sallam

“Meneja @Sallam_SK amekuwa akitaka mimi nimpigie Diamond simu tumalize, hata juzi ameniambia nikiwa na Shetta.

“Nikawa najiuliza kwanini @Sallam_SK kila mara ananitaka mimi ndio nipige simu, kwamba huyo mwingine ni ‘special’ sana?

“Mimi nilishamwambia Sallam kama anataka kutupatanisha, basi tukutane kwa AY kila mmoja aseme lake tuyamalize haya.

Kuhusu bifu la Ali Kiba na Diamond

“Kwenye wimbo wa Lala Salama wa Diamond, alitoa sauti ya Ali Kiba aliyokuwa ameingiza bila ya kumwambia Ali Kiba.

“Diamond na Ali Kiba walikuwa marafiki wakubwa, ila kitendo cha Diamond kutoa sauti ya Kiba bila kumwambia kilimkera sana.

Dimpoz akubali yaishe.

“Sisi tunahangaika kuwa kama Wanaijeria lakini wao tayari wamehama. Ukimsikiliza Wizkid anafanya vitu tofauti kabisa.

“Tunataka kuwapita Wanaijeria, lazima tushirikiane kwa sababu wao wapo pamoja na wanazidi kwenda mbali.

“Haya mabishano/bifu kwenye mziki ziwepo, ila ziwe na lengo la kujenga, tubishane kuhusu muziki na tutengeneze pesa wote.

“Mimi nimechangia kwa kiasi kikubwa kuandika wimbo wa Nasema Nawe wa Diamond, lakini sikuwahi kusema wala kutaka ‘credit’.

“Mimi nilimsadia kuandika sio kwamba yeye hajui, lakini ni kawaida ya wasanii kusaidiana hasa wanapokutana studio.

“Naheshimu mawazo ya Diamond na kuutambua mchango wake kwangu, na wala sishindani naye.

“Mimi naongea ukweli, sina tatizo na mtu. Naamini Diamond anavyofanikiwa ndio njia ya kufanikiwa kwa wasanii wengine.

“Kuna vitu ambavyo mashabiki hawafahamu ukiendeshwa kwa jazba utakuwa haufiki popote mziki ni kushi.
“Mimi nilimsadia kuandika sio kwamba yeye hajui, lakini ni kawaida ya wasanii kusaidiana hasa wanapokutana studio.

“Uandishi wa nyimbo ya #NasemaNawe ya @diamondplatnumz verse ya pili mimi nimeiandika!

“Kama kuna ubaya Mwenyezi Mungu aniepushe na haya, Sina ubaya wowote na jamaa..!

Kuhusu aliyekuwa meneja wa Ommy Dimpoz, Mubenga

“Kuhusu mimi na Mubenga, alisema kuwa haoni faida ya kufanya kazi na mimi hivyo anataka kufanya kazi zake mwenyewe.

“Nilimsihi Mubenga abako, lakini akaamua kuondoka akidai kuwa mimi ni tajiri lakini yeye hapati faida.

“Meneja Mubenga alishawahi kuniambia mbele ya @Nedyboy2 ifike mwisho wa kufanya kazi pamoja wala sina ubaya naye.” Amesema Ommy Dimpoz.

Kampeni ya Kumng’oa Trump Yashika Kasi

$
0
0

Ndoto za Donald Trump aliyechaguliwa hivi karibuni kuwa Rais wa 45 wa Marekani huenda zikayeyuka baada ya wajumbe sita wa Democratic watakaopiga kura za majimbo kuanzisha kampeni maalumu ya kuwashawishi wajumbe wengine kutomwidhinisha Rais huyo mteule.

Wajumbe hao ambao majina yao yalitangazwa jana wanaamini kuwa iwapo watafanikiwa kuwashawishi wenzao wengine 37 kutoka Chama cha Republican basi watakuwa wamefanikiwa kumzuia bilionea huyo kuingia ikulu.

Desemba 19 wajumbe 538 kutoka majimboni watakutana kupiga kura ya kisheria kumthibitisha Rais mteule anayetarajiwa kuapishwa Januari 20. Kura hizo zitahesabiwa mbele ya Bunge la Congress Januari 6.

Hatua ya wajumbe hao wa Democratic kuanzisha kampeni hiyo imekuja siku chache baada ya makundi ya kiharakati kuanza kukusanya saini nchi nzima ili kuwashinikiza wajumbe hao kutompitisha rais huyo ambaye tayari ameanza kutangaza vipaumbe vyake.

Mmoja wa wajumbe hao aliyetambulika kwa jina la Michael Baca anayewakilisha Colorado amekuwa akizunguka huku na kule kuwashawishi wajumbe wenzake kuepuka kumuunga mkono Trump wakati wa upigaji wa kura.

Mjumbe mwingine ambaye hakupenda jina lake kutajwa alisema kutokana na mvutano unaoendelea kujitokeza sasa kunaweza kuzusha hoja zitakazolazimisha kuangaliwa upya kwa mfumo unaotumika sasa kupitia kura za majimbo kumchagua rais.

Ingawa bado haijajulikana ni wajumbe wangapi wanaendelea kuwa waaminifu kwa kambi ya Trump lakini mchambuzi wa masuala ya siasa, Profesa George Edwards III amesema kama kutatokea wajumbe nane au 10 wakaamua kutomuunga mkono rais huyo mtarajiwa basi kunaweza kubadilisha ndoto za kiongozi huyo kuingia ikulu Januari 20 mwakani.

Tayari wafuasi hao wameitisha kampeni ya kuomba Wamarekani kuwaunga mkono mtandaoni kupitia tovuti ya www.change.org wa kuwashawishi wachaguaji hao kumchagua Clinton badala ya kumthibitisha Trump kwa kuwa hafai kuwa rais wa taifa hilo.

Ujumbe huo unaeleza kuwa iwapo watachagua kama ambavyo majimbo yamepiga kura katika uchaguzi huu, Trump atashinda.

“Hata hivyo, wanaweza kumpigia Hillary Clinton wakiamua,” inasomeka sehemu ya kampeni hiyo yenye kichwa cha habari; “Kura ya uamuzi: Mfanye Hillary Clinton kuwa rais Desemba 19”.

“Hata katika majimbo ambayo wajumbe hawatakiwi kufanya hivyo, wakiamua kura zao zitahesabika, wanaweza wakafanya uamuzi kidogo ambao tutaamini wafuasi wa Clinton watavutiwa nao.”

Mtandao huo unaeleza kuwa Clinton alishinda kura ya wengi hivyo anafaa kuwa rais kwa kuwa Trump alishinda majimbo yenye kura nyingi za majimbo basi mwenendo ukaonyesha bayana kuwa atashinda kura za uamuzi.

Katika uchaguzi uliofanyika Novemba 8 mwaka huu, Wamarekani waliwachagua wagombea wa urais kwa kura ya wengi na kuchagua wapigakura watakaomchagua rais mteule mwezi mmoja ujao.

Clinton aliongoza kura za wengi kwa zaidi ya kura 200,000 lakini Trump aliibuka mshindi kutokana na kushinda majimbo yenye kura nyingi za majimbo.

Ili Rais ashinde kinyang’anyiro hicho, anatakiwa kushinda kura 270 kati ya kura 538 zilizopo kutoka majimboni.

Kwa kutumia mfumo wa mshindi wa jimbo anashinda pia kura za uamuzi. Hadi sasa Trump ana kura 306 wakati mpinzani wake, Clinton akiondoka na kura 232. Ni mara chache kwa Marekani mshindi wa urais kuzidiwa katika kura za wengi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Fordham, Christina Greer alisema kati ya wajumbe 538 watakaopiga kura mwaka huu, 100 ni maseneta ambao ni wawili kila jimbo, wajumbe watatu kutoka makao makuu ya nchi, Washington D.C, na wabunge 435.

“Majimbo yote kasoro mawili ya Maine na Nebraska mgombea mwenye kura nyingi kwenye jimbo basi ndiye mshindi pia wa kura za wajumbe.

“Hii ina maana matokeo yakitoka tu mwenye kura nyingi huwa ni mshindi licha ya kura kusubiri kura za uamuzi Desemba 19,” Dk Dreer.

Hata hivyo, matumaini ya wafuasi hao wa Clinton huenda yasizae matunda kwa kuwa sheria za majimbo mengi likiwamo la Minnesota Marekani zinakataza uwepo wa “wajumbe wasiowaaminifu” na baadhi yanatoza faini kati ya Dola 500 (Sh1 milioni) za Marekani hadi 1,000 (zaidi ya Sh2 milioni).

Faini hiyo ni matokeo ya uamuzi wa Mahakama juu ya nchi hiyo iliamua mwaka 1952 wapigakura hao wawe wanakula viapo mapema wakati wa mkutano mkuu wa chama juu ya nani watamchagua, mtandao wa Factcheck.org unaochapisha habari za siasa, umeeleza.

Timu Lipumba, Maalim Seif zatwangana Mahakamani

$
0
0

KATIKA hali isiyo ya kawaida, wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), jana waligeuza Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, kuwa ukumbi wa masumbwi baada ya kutwangana baadhi yao walipojaribu kumzuia Profesa Ibrahim Lipumba kuingia kusikiliza kesi inayomhusu.


Watu hao ambao walikuwa wamevaa sare za chama hicho, walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili, moja likiwa kwa Profesa Lipumba, ambaye ni Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Upande mwingine ulikuwa wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama hicho, Abdallah Khatau, wanaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, ambao wamefungua kesi ya kupinga uenyekiti wa kutambuliwa na Msajili.

Jana saa 2:45 asubuhi, wafuasi wa pande zote mbili katika kesi hiyo iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini ya CUF dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, zilikuwa zimetanda kwenye korido za mahakama hiyo wakisubiri kuingia chumba cha korti kusikiliza shauri hilo.

Hata hivyo, baada ya mawakili kuingia katika ofisi ya Jaji Sekiet Kihio kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo, baadhi ya wafuasi hao walisimama mlangoni kumzuia Profesa Lipumba na watu wake wasiingie kwenye chumba hicho.

“Huwezi kuingia ndani hadi mawakili waingie", "kaja kufanya nini wakati kesi haimuhusu,""ondoka Lipumba…,” walisikika wakisema baadhi ya wafuasi hao.

Hatua hiyo ilisababisha wafuasi wa Prof. Lipumba kuanza kupiga kelele huku wakitaka wenzao wanaomzuia kutoka mlangoni ili aweze kuingia kusikiliza kesi hiyo.

Tukio hilo lilikuwa kama sinema baada ya timu ya Prof. Lipumba kumnyanyua juu juu mtu aliyesimama mlangoni kumzuia mlalamikiwa huyo kuingia mahakamani na baadaye walimshushia kipigo huku moja wao akisikika akisema “mnataka kuharibu kesi, toka hapa mlangoni na usirudi tena."

Wakati 'sinema' hiyo ikiendelea hakukuwa na askari eneo hilo hivyo kufanya fujo hizo zidumu kwa zaidi ya nusu saa mpaka askari polisi na magereza walipofika na kufanikiwa kuwatuliza wafuasi hao na Prof. Lipumba kuingia kusikiliza kesi yake.

Ndani ya chumba cha mahakama, Jaji Kihio aliwalaumu mawakili wa pande zote mbili kwa kuonyesha utovu wa nidhamu mahakamani hapo na kwamba hawakustahili kufanya hivyo.

“Nasikitika sana kwamba ninyi wote ni watu wazima inakuwaje mnaanzisha vurugu wakati kesi yenu imepangwa kwa ajili ya kutajwa?

“Kesi yenu inatajwa kwa dakika tano, nashangaa mnaamua kupigana, mawakili siku nyingine mnatakiwa kutoa taarifa kuwa mmekuja na wafuasi wengi ili twende mahakama ya wazi,” alisema Jaji Kihio.

Wakili wa Mlalamikaji, Juma Nassoro, aliomba Jaji Kihio ajitoe kusikiliza kesi hiyo.

Alidai kwamba wamewasilisha pingamizi dhidi ya majibu ya walalamikiwa kwa madai kwamba yana upungufu wa kisheria.

Alidai kuwa viapo vya walalamikiwa vina upungufu wa kisheria na kwamba vilitoa maelezo ya uongo pamoja na muapaji kuweka maelezo ya kuambiwa.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Gabriel Malata, aliwasilisha pingamizi la awali kwamba mahakama hiyo haijatoa kibali cha kufungua kesi dhidi ya walalamikiwa.

Jaji alisema kuhusu suala la kuombwa ajitoe bado hajapokea barua kutoka upande wa mlalamikaji na kwamba akipokea barua hiyo atatoa uamuzi siku ya kusikiliza pingamizi Desemba 6.

Mbali na Msajili, walalamikiwa wengine katika kesi hiyo ya madai namba 23/2016 ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Prof. Lipumba na wanachama wengine 11 wa CUF
Viewing all 104768 articles
Browse latest View live




Latest Images