Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104428 articles
Browse latest View live

Nafasi Mpya za kazi na scholarships Tanzania, Kenya na Uganda ( East Africa )


RUGE Awachana Basata...Adai Wamekuwa Kama Polisi Badala ya Kuendeleza Sanaa Tanzania

0
0

Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba amesema Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA linapaswa kubadili mfumo wa ufanyaji kazi kwakuwa kwa sasa linafanya kazi kama polisi kuliko kuuendeleza muziki wa Tanzania.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL Ijumaa hii, Ruge alisema baraza hilo limekuwa likionekana zaidi katika kuwaadhibu au kuwafungia wasanii kuliko kusaidia kukua kwa muziki ikiwemo kutoa milango zaidi kwa watu wanaotaka kuanzisha tuzo.

“Mlolongo wa tuzo unakuwa ni mgumu wakati ni jambo ambalo linatakiwa kupewa msukumo mkubwa sana. Baraza la sanaa, na vyombo vingine vimekuwa vikifanya zaidi ya upolisi kuliko kusukuma,” alisema.

Amedai kuwa kutokana na BASATA kupenda kufungia video au nyimbo, wasanii wamekuwa wakifanya makusudi kwakuwa kazi zao hupata kiki na video zao Youtube kupata views zaidi zinazowapa fedha kuliko kazi kuchezwa kwenye TV.

Anaamini kuwa baraza hilo linapaswa kuwa mbele kiteknolojia na kimawazo kuliko hata wasanii wenyewe na kuweza kwenda na mabadiliko ya muziki duniani.

Ruge amedai kuwa hata muziki wa dansi umeporomoka kwasababu hakuna chombo cha muziki ambacho kinawasaidia.

Nape Afunguka Kuhusu Kupotea Kwa Pesa Mtaani...Adai Serikali Inajua na Haikutokea Bahati Mbaya....

0
0
Nape Nhauye
Waziri Nape Amefunguka Kuhusu malalamiko ya Watu kuwa pesa zimekuwa ngumu kupatikana mtaani .....Amesema Haya :

“Serikali kuu tunatambua kwamba yapo maneno kwamba pesa mtaani haipatikani kweli si kweli?” alihoji. “Kuna watu wanasema hali ngumu sana mtaani tumekuwa hatujui limekuwa tatizo, lakini kwasababu hii tunajua na haijatokea bahati mbaya. Tunataka turudishe nidhamu ya pesa na matumizi ya pesa katika jamii yetu ili kazi halali ziheshimike.”
“Tulianza kufikia mahali kila mtu alikuwa anatamani afanye kazi za dili na hizo ndizo zilizokuwa zinaongeza mzunguko wa pesa ambao huzitolei jasho,”
 Alisema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa kuanisha fursa za biashara uliondaliwa na ubalozi wa India ukishirikiana na TCIAA mkoani Tanga

KIMENUKA..Kura za Urais Kuhesabiwa Upya Marekani

0
0
Tume ya uchaguzi katika jimbo la Wisconsin nchini Marekani limepokea ombi la kurudiwa kuhesabu kura za uchaguzi uliopita ambapo mshindi alikuwa Donald Trump aliyeshinda kwa kura chache wiki mbili zilizopita.

Ombi la kurudiwa kuhesabu kura liliwasilishwa na mgombea wa urais kupitia chama cha  Green Party Jill Stein ambaye pia ametaka kura zirudiwe kuhesabiwa katika majimbo ya  Michigan na Pennsylvania.
Hata hivyo ikiwa Hillary Clinton atashinda jimbo hilo hakutabadilisha matokeo ya ushindi wa Trump kwani lina kura 10 pekee za wajumbe wa uchaguzi.
 Kamisheni hiyo imethibitisha kupokea maombi hayo na kuainisha kutoa maelekezo muda si mrefu.

Kajala Naye Amjibu Wema, Kamuweka Wazi Mpenzi Wake (Video)

0
0
Na Hamida Hassan, Ijumaa
DAR ES SALAAM: Gumzo kubwa ndani ya wiki iliyopita ilikuwa ni kuhusu msanii wa filamu Bongo, Wema Sepetu kujiweka kwa modo aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Mgimbu ‘Calisah’ lakini siku chache baadaye Kajala Masanja akamjibu baada ya kudaiwa kujiweka kwa msanii wa filamu anayefahamika kwa jina la Mutra.
Habari za Kajala kujiweka kwa Mutra zilivujishwa na mtu wa karibu wa mastaa hao aliyeomba hifadhi ya jina lake huku ikidaiwa kuwa wamekuwa wakiongozana sehemu mbalimbali.


“Penzi la Kajala na Mutra ndiyo habari ya mjini, wanatoka kwa siri lakini ukikaa nao karibu utajua tu kuwa wana uhusiano, fuatilieni mtaujua ukweli,” alidai mtoa habari huyo.
Baada ya habari hizi kulifikia Ijumaa, Mutra alitafutwa kupitia namba yake ya simu ambapo alipopatikana alisema: “Mh! Ni kweli ila hatupendi kuweka wazi, lakini angeulizwa yeye kwanza, hata hivyo nipigie baadae nitakujibu vizuri kwa sababu nipo lokesheni.”

Alipopigiwa baadaye alisema kuwa Kajala ni mtu wake wa karibu wanafanya kazi zao za filamu. Alipobanwa kuhusiana na awali kukiri, alisema:“Dah! Naomba nisamehe kwa kukujibu hivyo, nilikuwa lokesheni ndiyo maana nikateleza kukujibu vile.”
Baada ya Mutra, Ijumaa lilimsaka Kajala kwa kumtumia ujumbe wa WhatsApp ambapo mahojiano kwa ufupi yalikuwa hivi:

Ijumaa: Kajala mambo, unadaiwa kutoka kimapenzi na msanii mwenzako Mutra, mnadaiwa kuwa karibu muda wote na mara ya mwisho mlionekana pamoja kwenye sherehe ya Steve Nyerere.
Kajala: Ndio hivyo.
Ijumaa: Ndio hivyo ni shemeji kwa sasa au? Funguka basi?
Kajala: Kimyaa.



GPL

CHADEMA Waibuka Mafichoni na Kulionya Jeshi la Polisi

0
0
NAIBU Katibu Mkuu (Bara) wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika amelitaka Jeshi la Polisi kuacha kufuatilia mikutano yao ya ndani, inayoendelea sehemu mbalimbali nchini.

Mnyika alisema hayo mkoani Singida juzi akiwa kwenye moja ya mikutano ya ndani, iliyoandaliwa na Chadema kwa lengo la kuimarisha viongozi wake ngazi ya kata na wanachama ili waweze kuwafikia wananchi wa vijijini.

Naibu Katibu huyo alisema siyo jambo zuri polisi inapotumika vibaya kufuatilia mikutano ya Chadema, wakati ipo kikatiba na kuruhusiwa na serikali.

Kwa mujibu wa Mnyika, mkutano huo uliokutanisha wajumbe wa wilaya ya Ikungi, jimbo la Singida Mjini na Singida Kaskazini, ulikuwa na lengo la kuwapika viongozi wa kata ili wakaijenge Chadema imara maeneo ya vijijini.

Akizungumzia mikutano hiyo, Waziri Mkuu mstaafu wa serikali awamu ya tatu ambaye hivi sasa ni mjumbe kamati kuu ya Chadema, Fredrick Sumaye aliwataka viongozi hao wa kata kuhakikisha chama kinapata mafanikio ili hatimaye kiweze kushika dola.

Mbali ya Mnyika na Sumaye, viongozi wengine wa Chadema waliohudhuria walikuwa Mbunge Ester Matiko (Tarime Mjini), Susan Masele (Mwanza), Rose Kamili (Manyara), Jesca Kishoa (Singida) na wajumbe wengine watatu wa sekretarieti ya Chadema makao makuu.

KAMPUNI ya MURO Investment Yatangaza Kuuza Mabasi na Vituo vyake vya Mafuta...Kunani?

0
0
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko kubwa la nyumba kipigwa mnada, viwanja, magari, hoteli na mali mbalimbali kutokana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni baadhi wa wakopaji kushindwa kurejesha fedha za mikopo walizochukua kutoka katika taasisi za kifedha.

Mbali na kupigwa mnada, baadhi ya hoteli na kumbi nyingine zimebadilishwa  matumizi ambapo nyingi zimefanywa hosteli kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo huku nyingine zikibadilishwa na kuwa shule na vyuo wakati wamiliki wengine wakiamua kuzifunga au kupunguza idadi ya wafanyakazi.

Kampuni ya Muro Investiment Co. Ltd inayomiliki mabasi ya safari za mikoani na vituo vya kuwekea mafuta imetangaza kuuza mali hizo. Kampuni hiyo haikueleza sababu za kuuza mali hizo.

Hili hapa chini ndilo tangazo la kampuni hiyo likielezea mali zinazouzwa.

MZEE wa Upako Aachiwa na Polisi...Agoma Kusema Kulichotokea Mpaka Kuwekwa Ndani

0
0
Anthony Lusekelo 
Siku chache zilizopita Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako wa Kanisa la Maombezi lililopo Ubungo, jijini Dar es Salaam alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanyia fujo jirani yake huku akimtolea maneno yasiyo sahihi.

Inadaiwa kuwa,Mchungaji Lusekelo alifikia atua hiyo baaada ya kukerwa na tabia ya jirani yake huyo kutangaza kuwa yeye ni mlevi na hivyo hapaswi kuwa mchungaji.

Tangu aachiwe na Polisi, jana alifika kanisani kwake katika ibada ya Ijumaa kama ilivyo kawaida ambapo wengi walitegemea kuwa angewaeleza waumini wake kuwa ni kitu gani hasa kilitokea hadi akakamatwa na Polisi.

Tofauti na matarajio ya wengi, Mchungaji Lusekelo alisema hatozungumzia suala hilo na akasema kuwa ambao tayari wameanza kulizungumziawao wanendelee sababu inaonekana kama wao ndio wanajua ukweli sana.

“Kuna kitu nilikuwa nataka nikiseme, lakini sitakisema ili waendelee kusema hao hao waliokuwa wanasema. Sisemi chochote, hao waliosema wakawaulize wenyewe” alinukuliwa Mzee wa Upako akitoa maneno hayo wakati wa ibada.

Wakati akinendele na mahubiri yake kanisani hapo, alisema kuwa kuna watu walitamani asiwepo tena. Najua wapo na watashindana lakini hawatashinda na nina amini Mungu atawalipa sawa sawa na matendo yao.

MAMA Profesa Tibaijuka Apewa Tuzo Nyingine ya Kimataifa

0
0
Profesa Anna Tibaijuka
ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ametunukiwa tuzo baada ya kutangazwa mshindi wa mwaka 2016 wa Taasisi ya Mafanikio ya Govan Mbeki (Govan Mbeki Lifetime Achievement Award), katika sherehe iliyofanyika usiku wa kuakia jana, kwenye Ukumbi wa International Convention Center (ICC) mjini Durban, nchini Afrika Kusini.

Profesa Tibaijuka, ambaye pia alipata kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN- Habitat), ametunukiwa tuzo hiyo kutokana na ufanisi aliouonyesha, ikiwa ni  pamoja na kuendesha mikakati na kampeni kubwa bila kuchoka ya kupambana na makazi duni na mazingira barani Afrika na duniani,  wakati akiliongoza shirika hilo.

Waziri wa Maendeleo ya Makazi wa Afrika Kusini, Lindiwe Sisulu, ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo na cheti Profesa Tibaijuka, baada ya kutangazwa mshindi.

Profesa Tibaijuka, ambaye ni Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), ametunukiwa tuzo hiyo baada ya kuonyesha kuthamini mchango wake wakati akiwa UN Habitat, kati ya mwaka  2000-2010.

Kiongozi huyo, licha ya kujipatia sifa lukuki wakati akiliongoza shirika hilo la Umoja wa Mataifa na hivyo kumuandalia njia nyepesi ya kushinda ubunge Jimbo la Muleba mwaka 2010 na hata kuteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, hata hivyo, sifa hizo zilitiwa doa baada ya kuhusishwa kwenye mgawo wa fedha tata zilizochotwa kutoka katika akaunti ya Escrow.

Profesa Tibaijuka, licha ya mara kadhaa kujitetea kwamba fedha hizo alipewa kwa ajili ya shule yake, baadhi wamekuwa wakidai kuwa kitendo hicho kimemuonyesha kuwa si mtu safi na anayestahili kuaminiwa.

Kwa maneno yake mwenyewe, Profesa Tibaijuka amekuwa akidai kuwa hayo anaonewa na kwamba hata kupokea kwake fedha hizo kumegeuzwa kuwa ni dhambi na wapinzani wake wa kisiasa.

Kutokana na hayo, wakati fulani alisikika akiunga mkono mpango wa Rais John Magufuli kuanzisha mahakama ya mafisadi.

Profesa Tibaijuka alisema chombo hicho kitachangia kutoa haki na kuweka ukweli bayana, kwakuwa watuhumiwa wengi wa ufisadi wanatolewa kafara.

Alisema  akiwa kama mmoja wa wahanga wa tuhuma za ufisadi,  kuanzishwa kwa mahakama hiyo kutasaidia, kwakuwa kuna kundi la watu ambalo linatolewa kafara na mafisadi ili kuficha madhambi yao.

“Ukishaanzisha mahakama ya mafisadi unatafuta haki na ukweli, Watanzania ni wepesi wepesi wa kuamini, Watanzania tuhuma tu wanaona tayari umeshakuwa convict (hatiani), mimi ni mmoja wa wahanga wa tuhuma za ufisadi na nilituhumiwa bila kuwa na uhakika, kuna mitandao ya mafisadi wenyewe wanahakikisha hawakamatwi na badala yake wanawapeleka wengine mbele ili wawatoe kafara,” alikaririwa Profesa Tibaijuka.

VIDEO: Diamond Akiri Kuandika Nyimbo Baada ya Kuumizwa na WEMA Sepetu na JACK Wolper

0
0
Watu walizungumza mambo mengi sana baada ya kusikia kuwa Harmonize na Jackline Wolper na uhusiano wa kimapenzi huku walio wengi wakiamini kuwa alikuwa akitafuta kiki tu.  Walioamini hivyo ni kutokana na uhusiano wa kimapenzi ambao uliwahi kuwapo kati ya Diamond Platnumz ambaye sasa ni bosi wa Harmonize na Wolper.

Katika mahojiano haya yaliyofanyika kipindi cha nyuma kati ya Zamaradi Mketema wa Clouds Tv na mwanamuziki Diamond Platnumz, Diamond alikiri kuwa aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wolper na pia aliandika wimbo wa Mawazo baada ya kuumizwa na msichana huyo.

Mbali na Wolper, Diamond amekiri kuwa aliwahi kuandika nyimbo nyingi kuhusu Wema Sepetu ambaye alikuwa ni mmoja wa watu aliowahi kuwapenda sana lakini wakamuumiza.

Swali ambalo limekuwa likiwatatiza wengi hadi leo, ni kwanini Diamond alimuacha Harmonize kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Wolper kama yeye alishawahi kutoka naye, tena akaishia kumuumiza?

Hapa chini ni video ya Diamond Platnumz na Zamradi Mketema walipofanya mahojiano kipindi cha nyuma.

Trey Songz Amenipa 'Kiki' Hadi Marekani - Vanessa

0
0

Msanii wa muziki wa bongo fleva, mwanadada Vanesa Mdee a.k.a Vee Money, amefunguka na kueleza faida alizopata kwa kuwa karibu na nyota wa muziki nchini Marekani Trey Songz.

Akiwa katika kipindi cha FNL cha EATV, Vanessa alitakiwa kueleza faida alizopata kutokana na skendo zilizovuma siku za hivi karibuni kuwa alitoka kimapenzi na Trey Songz kipindi walipokuwa nchini Kenya katika Coke Studio.

Katika majibu yake, Vanessa alisema kuwa hakuna jambo linalovuma kwake bila ya kuwa na faida, na kwamba skendo hizo zilivuma hadi Marekani, kwani aliandikwa katika baadhi ya blogs za Marekani kuhusu ukaribu wake na Trey Songz, kitu kilichomfanya kujulikana hadi katika taifa hilo lenye nguvu katika karibu kila nyanja, ikiwemo muziki duniani.

Katika FNL ya Sam Misago ilikuwa hivi.......
Swali: "Vipi ishu ya wewe na Trey Songz imekupa faida gani, je kuna Wamarekani wamekujua au imeishia hapa hapa?"

Jibu: "Yea, hakuna jambo naweza fanya bila manufaa, hiyo imenifanya niandikwe kwenye blogs kadhaa nchini Marekani, kwahiyo wamarekani wamenijua"

Trey Songz amekuwa akifananishwa kimuonekano na mpenzi wa Vanessa, Jux licha ya Jux mwenye kuweka wazi kuwa Trey Songz ndiye role model wake.

Wolper Avuta Ndinga Ya Milioni 20

0
0

Staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper amenunua gari lenye thamani ya shilingi milioni 20 ambalo kwa sasa anamalizia usajili wake

Ijumaa lilimbabatiza Wolper mitaa ya Kinondoni jijini Dar akiwa na gari hilo aina ya Toyota Alphard ambapo alipobanwa kama amelikodi kama wanavyofanya mastaa wengine au amenunua alifunguka kuwa ni lake kutoka kwenye hela yake halali.


 “Hii gari ni yangu kama mnavyoiona mpya kabisa, nimeinunua na ndo’ kwanza nashughulikia usajili,” alisema Wolper.

Wolper alisema kuwa anakwepa mambo yaliyompata kwenye ile gari yake iliyomletea matatizo aina ya BMW X-6 ambapo alipata funzo na sasa hawezi kufanya makosa


“Nimeamua nifanye usajili kabisa TRA, sitaki matatizo kabisa kuhusu magari, lile lilinifanya nipate funzo kubwa,” alisema Wolper.


Wolper mbali na kununua gari amefungua duka la nguo Kinondoni. Kufuatia mambo hayo makubwa aliyofanya msanii huyo, wadau walihoji kama mkwanja wa kufanyia yote hayo umetokana na safari ya China au kuna pedeshee kaamua kumpa maisha? Jibu analo mwenyewe.

Christian Longomba Asimulia Jinsi Alivyopona Kutoka Kwenye Upasuaji Uliohusisha Kupasuliwa Nusu ya Fuvu lake

0
0

Katika watu wanaoweza kuelezea kwa mfano halisi kuwa Mungu yupo, ni Christian Longomba ambaye kupona kutoka kwenye upasuaji uliohusisha kupasuliwa nusu ya fuvu lake (kama mtu unavyoweza kupasua boga kutoa mbege za ndani), ni kitu ambacho hadi sasa haelewi iliwezekana vipi.

Muimbaji huyo aligundulika kuwa na uvimbe mkubwa kichwani ambao kama usingetolewa ungeweza kuyakatisha maisha yake tena kwa maumivu makali au kumpa upofu.

Kwenye mahojiano na Mzazi Willy M Tuva jijini Los Angeles wanakoishi kwa sasa, mdogo wake, Lovy Longomba amesema hilo lilikuwa jaribu kubwa katika maisha yao na lilifanya kusimama kwa mipango yote waliyokuwa nayo. Anasema ili kufanyika kwa upasuaji huo, iliwalazimu kusaini makaratasi mengi kuridhia matokeo yote ambayo yangejitokeza baada yake.

Upasuaji huo ulidumu kwa saa 14. Hata hivyo Lovy anasema ilikuwa na kama bahati tu kwasababu kutokana na umri wake aliweza kupona haraka. Chris anasema asilimia 90 ya uvimbe ilitolewa kwa upasuaji na zingine 10 kutolewa na mionzi na hivyo kumfanya apoteze sehemu ya nywele zake za mbele. “Kabla ya kufanyika upasuaji niliambiwa nusu ya mwili wangu unaweza kupooza au utapoteza kumbukumbu zako. Itabidi ufundishwe tena jina lako, jinsi ya kutembea, jinsi ya kula, jinsi ya kutumia bafu kama mtoto tena,” alisema Chris. “Sasa hivi niko fit, kila kitu kiko sawa,” ameongeza.

Hata hivyo Lovy amesema katika wiki ya kwanza, Christian hakuweza kukumbuka mambo mengi japo kitu pekee alichokumbuka ni muziki na kwamba ndio uliomsaidia kurejesha kumbukumbu zaidi.

USHAURI Kutoka Kwa Nikk wa Pili Kwa Mnao Ogopa Kuingia Kwenye Ndoa.....

0
0

FROM nikkwapili - He he me sio mshauri..wanao ni Dm...kuuliza abt ndoa (marriage)....this is what i think...kuhusu ndoa....ndoa baada ya muda wengi huona kama kifungo, kikwazo cha kumkosa msichana yule, au jamaa yule, au bata lile na kadhalika......hapa wana miss the point.....kumbuka ukiwa shule ukaambiwa soma....na uachane na mambo kama starehe, movies nakadhalika...na leo kitabu kina kunakufaisha na wengi walio babaishwa na mambo mengine wanajuta......sasa ni sawa na ndoa....ndoa sio jela..ndoa ni taasisi muhimu itakayo kulinda thidi ya tamaa za ngono, starehe,.....na kukufanya uwekeze kwenye vitu vya maana future, kazi, biashara nakadhalika.......so kama shule ilivyokuwaga na changamoto za mitihani, fimbo, usingizi, ugumu wa bording ukavumilia na leo unakula matunda....sawa na ndoa nayo inachangamoto lakini ukivumilia matunda utayala mema sana sana........so wengi wanao zingua katika ndoa nikwakuwa wameshinda kuelewa hii dhana....na mwishowe huaribu maisha yao, wenzao wao na watoto....yani huwa kama wale waliokataa shule

Maoni: Rais Magufuli Ameleta Heshima Kazini na Adabu ya Fedha

0
0
Hakuna binadamu aliyekamilika, zaidi ya Mwenyezi Mungu pekee. Huku wahenga wanasema kila binadamu na mapungufu yake na upekee wake katika dunia hii, ingali kila mtu ana kitu chake cha tofauti ambacho Mwenyezi Mungu kampa ambacho hakifanani na mtu.

Kwanza nichukue fursa ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kwa jitihada zake zote alizofanya tangu aingie madarakani na anazoendelea kufanya kwaajili ya Watanzania kwa ujumla ikiwa lengo na madhumuni yake ni kukamilisha ahadi zake alizoziahidi pindi anapoingia madarakani.

Rais Magufuli ameifanya nchi ya Tanzania kuwa ni nchi ambayo hata viongozi wengine wa nchi jirani wamekuwa wakimsifia kwa utendaji kazi yake hasa katika kukemea mafisadi makazini, kuheshimu kazi, kufanya ziara zake za hapa na pale lengo ni kutaka kuifikisha nchi ya Tanzania mbali na iwe ni nchi ambayo siku moja kila mtu atamani kuishi.

Katika serikali hii ya awamu ya tano nimejaribu kuangalia kuwa kiongozi huyu ni kiongozi ambaye mara nyingi amekuwa akilia na wanyonge ilhali wapo waliokuwa wakijitokeza katika vituo vya runinga mbalimbali wengine wakiwa na ulemavu wa miguu hawawezi kutembea lakini wanatamani kufanya kazi lakini kiongozi huyo amekuwa akiwasaidia kwa kuwapa bajaji ili waweze kuendesha maisha au kusukuma hili gurudumu la maisha, lengo ni kuibadilisha Tanzania.

Hata hivyo tangu ingie madarakani, amekuwa akiwafukuza kazi viongozi ambao hawajitumi katika kazi zao, huku akipiga vita wale ‘wapiga dili’ wanaotaka kupata fedha huku akitumia msemo wa ‘kutumbua jipu’ ambao kila Mtanzania anautambua kwa sasa.

Rais Magufuli amekuwa akiwapunguza wanaoletea mzaha katika kazi za serikali huku akiwasihi kutochezea jasho la wananchi huku akiwaambia hivi wanatakiwa viongozi hao wajue kuwa wao wameajieiwa na wananchi hivyo kuwataka wasibweteke, wafanye kazi zinazowahusu wananchi kama walivyochaguliwa.

Kwasasa hivi viongozi wa nchi wamekuwa wakiiheshimu kazi kutokana na rais Magufuli kuingia ofisi mbalimbali za serikali kwa kushtukiza na muda mwingine hukutana na madudu yanayofanywa na watumishi wa umma ambapo yeye hupinga utendaji kazi huo.

Ziara zake tunaona zimeweza kuzaa matunda katika ofisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na bandari ya Dar es Salaam alipofika alikuta kuna upungufu wa mashine hivyo kutaka mashine zingine kuongezwa ili kazi zao waZIfanye kwa weledi na kujua mizigo inayoingia na kutoka katika bandari hiyo.

Pia alipo ingia katika ofisi za gazeti la Uhuru ambapo alipofika pale alikuta wafanyakazi hawalipwi mishahara lakini kazi zikiendelea kutendeka. Pia alifanya ziara ya kushtukiza wakati akimsindikiza uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akimsindikiza Rais wa Congo, Joseph Kabila na kufanya mahojiano na baadhi ya wafanyakazi wa eneo lile yaliyomfanya agundue madudu yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya wafanyakazi.

Kwa upande mwingine Rais Magufuli amepigana na kupambana na rushwa si kwamba marais wengine hawakupambana na rushwa, bali yeye kwa kiasi kikubwa amejitahidi na tunaamini ataendelea kupambana na janga hili. Ndio maana hivi karibuni wakati wa mkutano wake na wahariri na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari katika nukuu zake nilinukuu akisema ‘RUSHWA NI KANSA YA MAENDELEO YA NCHI‘ huku akisema tuipinge na kuikataa.

Hivi karibuni Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi alisema kila mtu kwa nafasi yake ameipinga rushwa lakini Rais Magufuli ameleta Tsunami katika rushwa na kusema kuwa kwa mwaka mmoja wa rais huyo amewazidi wao kipindi cha nyuma.

Walio chini yake wanajitahidi kwa nafasi zao kufanya ziara zao pia za hapa na pale kwa kufuata kauli mbiu ya uongozi huu ya ‘Hapa Kazi Tu. Hata maneno matakatifu husema asiyefanya kazi na asile kwa hiyo ni vyema kila mtu akapambana kwa nafasi yake kuepuka kuwapa watu lawama.

Kutokana na uongozi wake unaipiga vita rushwam ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za serikali, wananchi hususan wafanyakazi wanaiheshimu zaidi fedha wanayoipata kwa jasho kuliko ilivyokuwa awali ambapo fedha za dili ziliwafanya baadhi ya watu waishi kama miungu watu.

BY: EMMY MWAIPOPO

SALAMU za Rambirambi za Rais Magufuli Kufuatia Kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Raul Castro kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba Mhe. Fidel Castro kilichotokea tarehe 25 Novemba, 2016. Katika Salamu hizo Rais Magufuli amesema;

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Fidel Castro. Kwa niaba ya Serikali, Wananchi wa Tanzania na kwa niaba yangu mwenyewe natoa pole nyingi kwako, familia, Serikali ya Cuba na wananchi wa Cuba kwa kumpoteza mtu muhimu.

Fidel Castro alikuwa kiongozi shupavu wa karne, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na pia kwa misaada mikubwa aliyoitoa katika kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.

Alikuwa rafiki wa Tanzania na Afrika nzima, historia ya Tanzania na Afrika haziwezi kukamilika bila kumtaja Fidel Castro, hakika kifo chake sio tu ni pigo kwa Cuba bali pia kwa Tanzania na Afrika.

Naungana nawe na wananchi wa Cuba katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, na pia nakuombea kwa Mwenyezi Mungu wewe, familia na wananchi wote wa Cuba muwe na nguvu, subira na ustahimilivu kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu."

Pia Rais Magufuli amemuombea marehemu Fidel Castro apumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Jengo la Makao Makuu ya TANESCO Ubungo Kubomolewa Wakati Wowote Kupisha Ujenzi wa 'Interchange'

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli amesema kuwa Jengo la Makao Makuu ya TANESCO lililopo Ubungo litabomolewa wakati wowote kuanzia sasa ili kupisha ujenzi wa Ubungo Interchange yenye ghorofa 2 mpaka 3 hali itakayopunguza msongamano wa magari kwenye eneo hilo.

Rais Magufuli amesema kuwa Serikali imepata shilingi Bilioni 67 kwa ajili ya ujenzi huo hivyo wakati wowote jengo hilo litabomolewa kwa vile lipo kwenye hifadhi ya barabara.

Hongera sana Rais Magufuli kwa kukumbusha tena suala hilo ambalo uliahidi miaka kadhaa iliyopita japo liliwekewa kizuizi na Rais Kikwete. Kwa sasa wewe ndiwe mwenye Rungu hivyo naamini kuwa hilo litatekelezwa ili kuondoa Double Standard.

PICHA ya Aunty Ezekiel na Moses Iyobo Ikionyesha Ujauzito Yawa Gumzo Mtandaoni

0
0

Moja kati ya picha ambazo zimekuwa zikisambaa kwa kasi katika mtandao wa Instagram leo Jumamosi ya November 26 ni picha ya muigizaji Aunty Ezekiel pamoja na mpenzi wake Mose Iyobo.

Picha hiyo ambayo imepostiwa na baadhi ya watu ikiwemo Mose Iyobo mwenyewe inamuonesha Aunty Ezikiel akiwa mjamzito, kitu ambacho kimefanya baadhi ya mashabiki wao kutoa comment za pongezi.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mose Iyobo na Aunty Ezekiel wana mtoto wa kike anayejulikana kwa jina la Cookie hivyo kwa mujibu wa post ya Mose Iyobo inawezekana wakawa wanatarajia mtoto wa pili.

KUFUATIA Agizo la Waziri wa Elimu Wanafanzi wa IFM Wavuliwa Majoho Katikati ya Mahafali

0
0
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeanza utekelezaji wa agizo la Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kwa kuwazuia wahitimu wa ngazi ya cheti na stashahada kuvaa majoho na kofia wakati wa mahafali yao.

Kitendo hicho kilitokea katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam juzi baada ya mratibu wa mahafali ya 42 ya IFM, Dk. Godwin Kaganda, kutangaza utaratibu huo licha ya wahitimu wao kuvaa majoho yao.

Dk. Kaganda alisema utaratibu huo ni kwa mujibu ya miongozo iliyotolewa na Serikali kuhusu uvaaji wa majoho, ambao unataka yavaliwe na wahitimu wa kuanzia ngazi ya shahada na kuendelea.

“Wahitimu wote wa ngazi ya cheti na stashahada hamtovaa majoho wala kofia pamoja na kwamba mlishapewa awali, tunaomba radhi kwa sababu ndiyo miongozo tuliyopewa,” alisema Dk. Kaganda.

Wiki iliyopita, Profesa Ndalichako  alipokuwa akiwatunuku vyeti wahitimu wa mafunzo ya uongozi na usimamizi wa elimu kwa njia ya masafa, iliyotolewa na Wakala wa Usimamizi na Uongozi wa Elimu (ADEM) mkoani Mbeya, alisema kumekuwa na matumizi holela ya majoho suala linaloshusha hadhi yake na kuagiza yavaliwe kuanzia ngazi ya shahada.

“Siku hizi hata mwanafunzi akimaliza chekechea anavalishwa joho. Nafikiri haya majoho yangebaki kwa wanaohitimu digrii peke yake, ili hawa wengine nao watamani kufika ngazi hiyo na si kila mtu anavaa,” alisema Profesa Ndalichako.

Katika mahafali hayo, jumla ya wanafunzi 2,857 wa ngazi za cheti, stashahada, shahada, stashahada ya uzamili na shahada ya uzamili walihitimu masomo yao.

Akizungumza katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Baraza la IFM, Profesa Letisi Rutashoga, alielezea changamoto katika utekelezaji wa mpango wa muda mrefu wa chuo hicho, ikiwamo kupanua miundombinu na utoaji wa taaluma.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni uhaba wa fedha za kuanza mradi wa ujenzi wa kampasi mpya ya Msata iliyopo Bagamoyo na kuiomba Serikali kuupangia Sh bilioni 2.5 katika mwaka ujao wa fedha.

Pia aliomba kuyafanyia kazi mapendekezo ya kubadilisha sheria namba 3 ya mwaka 1972 iliyoanzisha chuo hicho, ili iweze kuendana na malengo ya sasa ya uendelezaji wa chuo.

SABABU Zilizofanya Waziri Mkuu wa Zamani Fredrick Sumaye Kunyang'anywa Shamba lake

0
0
Hatimaye shamba lililokuwa linamilikiwa na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, lililopo Mabwepande limefutiwa hati zake na umiliki umerudishwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ambayo itafanya utaratibu wa kupima viwanja na kuwagawia wananchi waliohusika kwenye mgogoro huo.

Hatua hiyo imekuja baada ya wananchi zaidi ya 250 kulalamikia unyanyasaji wanaofanyiwa kupitia shamba hilo, na Mkuu wa Wilaya hiyo, Ally Hapi kupeleka malalamiko hayo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambapo Rais John Magufuli aliidhinisha kufutiwa hati kwa shamba hilo.

Akizungumza na wananchi wa kata hiyo ya Mabwepande jana, Hapi alisema shamba hilo lenye ekari 33 limefutiwa hati zake tangu Oktoba 28, mwaka huu na kwamba tayari Sumaye ameandikiwa barua ya kutojihusisha na shamba hilo baada ya kushindwa kukidhi masharti ya kisheria.

“Vyombo vya ulinzi na usalama watakuwepo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba shamba hili halitafanyiwa shughuli zozote isipokuwa baada ya taratibu za Manispaa zitakapofanyika,” alisema Hapi na kuongeza;

“Mgogoro wa shamba hili ni wa muda mrefu uliowahusisha wananchi. Lakini tunayo idadi ya wananchi ambao walikuwepo kwenye huu mgogoro na sasa wataalamu wataandaa mpango bora wa matumizi ya shamba hili,” alisema.

Aliongeza kuwa, wananchi hao waliokuwamo kwenye mgogoro ambao wataonekana wana vigezo vya kupatiwa viwanja, watafikiriwa kwa masharti ambapo baada ya kupimwa viwanja hivyo watawekewa gharama nafuu kwa ajili ya wao kununua.

Pia alisema, wananchi hao wenye makazi ya kudumu kwenye eneo hilo, watahakikiwa ili kuepusha watu wasiokuwamo kujiingiza kwa lengo la kuonekana nao walikuwa sehemu ya tukio.

Hata hivyo, alisema wataendelea kutoa taarifa kwa Rais kuhusu maeneo ambayo wananchi wanayahodhi bila ya kuyafanyia kitu chochote ili nayo yafutiwe hati.

“Natoa rai kwa wananchi wengine wenye maeneo ambayo hawayaendelezi tutayafutia hati na tutayamiliki wenyewe Manispaa ya Kinondoni. Pia tuendee kumuombea kwa kazi zake nzuri ili Mungu ampe ujasiri wa kupambana na ukabaila unaofanywa na wanaohodhi rasilimali za umma,” aliongeza.

Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Aaron Kagurumjuli kwa upande wake alisema, watahakikisha hadi Alhamisi wiki ijayo, timu ya ardhi wanaanza kupima viwanja hivyo na kuwagawia wananchi kwa masharti watakayoweka.

Kagurumjuli alisema watakaopewa kipaumbele katika ugawaji wa viwanja hivyo ni wale wenye makazi ya kudumu na watu ambao hawana makazi ya aina hiyo, watafikiriwa.

Wakazi wa kata hiyo walimpongeza Rais kwa hatua hiyo na kueleza kuwa matatizo kama hayo yapo sehemu nyingi nchini na yanatakiwa kutafutiwa ufumbuzi.

Abdallah Mohammed alisema kuwa walikuwa wanapata mateso kutoka kwa baadhi ya maaskari ambao walikuwa wanawanyanyasa kwa kuwatoa majumbani mwao usiku wa manane na kuwafungulia kesi.

Happy Makole alisema walikuwa wanaishi kwa wasiwasi kwa kuwa askari walikuwa wanawakamata waume zao na kuwaacha peke yao.

“Tumenyanyasika sana kuhusu eneo hili, mimi niliachwa usiku wa manane nikiwa na mtoto wakati mume wangu alipokuja kukamatwa. Lakini pia yapo maeneo mengine tunaendelea kunyanyasika tunaomba wayafanyie kazi malalamiko yetu,” alisisitiza Makole.

 – HABARILEO
Viewing all 104428 articles
Browse latest View live




Latest Images