Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104771 articles
Browse latest View live

SERIKALI Yapiga Marufuku Kusoma Degree Bila Kupita Form Six

$
0
0

Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi kujiunga na masomo ya Shahada (degree) bila kupita kidato cha sita. Marufuku hiyo itaanza rasmi katikals mwaka ujao wa masomo. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.

Ndalichako amesema wanafunzi wanaofeli kidato cha nne na kwenda kusoma certificate na baadae diploma ili wajiunge vyuo vikuu hawataruhusiwa kujiunga na masomo ya shahada (degree) kama hawajarudia (reseat) masomo yao na kupata alama za kwenda kidato cha tano, na wafanye mitihani ya kidato cha sita na kufaulu ndipo wajiunge vyuo vikuu.

Katika utaratibu huo, wanafunzi wa kidato cha nne watakaoruhusiwa kusoma shahada (degree) bila kupita kidato cha 5 na 6 ni wale waliofaulu kidato cha 4 na wakachaguliwa kwenda kusoma katika vyuo vya ufundi daraja la kati (Technicians). Lakini wale wanaokosa "credit" za kuendelea form five na kuamua kwenda certificate mwisho wao utakuwa diploma.

Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa.

"Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha "points" za kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom course. Anapaswa kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la mitihani linatoa fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation course haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma" Amesisitiza Ndalichako.

Picha: Makonda Atinga 'Uwanja wa Fisi' Wanapojiuza Madada poa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akiteta na Mlemavu ambaye amemkuta katika eneo la uwanja wa fisi akinywa pombe za kienyeji na kumsihi aache kunywa pombe hizo, leo jijini Dar es Salaam. 

Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akiwa ameongozana na Kamanda   wa kanda maalum ,Simon Sirro kugonga nyumba za baadhi ya akina dada  ambao hufanya biashara ya kujiuza katika eneo la uwanja wa fisi, leo jijini Dar es Salaam. 


 Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akiwa na Kamanda wa kanda maalum ,Simon Sirro wakiangalia bia ambazo zinauzwa uwanja wa fisi zikiwa zimekwisha muda wake,ambazo inaelezwa zimekuwa zikitumika kwa ajili ya matumizi ya Binadamu, leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emanuel Masaka-Globu ya Jamii

Angalia Thamani yako, Yanini Kumng’ang’ania Asiyekupenda?

$
0
0

Ili mapenzi yaweze kuwa bora kwa kila aliye katika mahusiano, huwa ni vyema kila mmoja kuiona thamani ya mwenzake. Ukipenda kujiangalia mwenyewe  si ajabu mwenzako kupata hisia za kuwa humthamini wala humjali.

Muunganiko wenu katika mapenzi maana yake tayari mmekuwa kitu kimoja. Katika mimi unaweka sisi.

Ila pia ni vyema ikakumbukwa ladha na maana halisi ya mapenzi ipo kwa anayekupenda na kukuthamini. Unapokuwa na uhakika kama anakupenda na kukuthamini hapo ndipo nafsi yako itatulia na kuwa na amani. Ndani ya mapenzi na mtu wa aina hii ni amani na utulivu kwa kwenda mbele. Hakuna majuto wala majonzi ya kila siku.

Unapoamua kuwa katika mahusiano na mtu ambaye hakupendi, bali unakuwa naye kwa kuwa tu unampenda jua umejiingiza katika utumwa. Mapenzi ni suala la kihisia zaidi. Mwenzako anapokosa hisia na wewe maana yake hata uwepo wako hauthamini inavyopaswa. Na hapo ndiyo tunaona yale mahusiano ya kingono yanapozaliwa na si ya kimapenzi kwa maana halisi.

Yaani mwenzako anapokuwa na mihemko ya kingono ndipo anapokutafuta na si vinginevyo. Niliwahi kuongea na msichana mmoja aliyewahi kuniambia anampenda kijana mmoja ambaye anauhakika kabisa yeye hampendi. Alinambia uhakika huo kaupata kutokana na kijana huyo kumtakia  kuna msichana yupo anampenda na kumjali ila si yeye.

Kuonesha zaidi kumpenda msichana yule mwingine, jamaa aliwahi kumwambia kama ikitokea hata huyu msichana akagombana na yule mpenzi mwingine wa yule jamaa, kijana yule alikuwa radhi kumdhuru huyu msichana.

Hata kwa matazamo wa haraka hapo unaweza kugundua ni kwa namna gani huyu msichana alikuwa haitajiki. Ila cha kushangaza msichana huyu(aliyeongea na mimi) alimwambia mvulana husika yuko radhi kuwa naye hivyo hivyo.

Aliamua kuwa hivyo akiamini ipo siku jamaa atamuelewa. Kweli walikuwa pamoja. Ila  unajua kinachomkuta sasa?

Kila jamaa anapogombana na yule msichana mwingine anamtumia huyu kingono na mambo mengine yasiyo ya kimapenzi, na bila kutafakari mara mbili huyu msichana anafanya kwa kile anachoamini hali hiyo itamfanya huyu jamaa amfikirie zaidi. Kuna kitu cha kuangalia hapa.

Suala la mapenzi si suala la kuoneana huruma wala aibu. Mapenzi ni hisia. Unapojitoa kwa mwenzako kwa kila jambo na unamuona haelekei ujue hana hisia na wewe. Kwanini unakubali kuteseka na kuumia kila siku kwa kumuangalia yeye tu?

Ndiyo, unampenda sana, unamjali sana na unamuhitaji sana, ila kama yeye hakutaki wa kazi gani? Ni muda wa kujiangalia na wewe sasa.

Ona thamani yako kama binaadamu, jionee huruma jinsi unavyoteseka kila siku kwa mtu asiyeona thamani yako.

Wewe ni binaadamu mwenye hadhi na thamani, bila kujali muonekano wala rangi yako. Unahitaji mwenye kukuthamini na kukujali na si anayekufanya kama mdoli wake ngono au kadi yake ya pesa. Kataa utumwa wa mapenzi kwa kuiona thamani yako.

Ni vyema ukalia kwa kumkosa kuliko kuonekana unaye wakati moyoni siyo wako. Hakuna sifa ya kuwa na mtu mwenye fedha au muonekano mzuri ikiwa hakujali wala haupo moyoni mwake. Mapenzi ni amani na raha.

Mapenzi hufanya watu wafurahi na kusahau shida zao. Ila jiulize kwanini kwako hayako hivi? Unaenda kwa mwenzako badala afurahie uwepo wako, yeye anaona unajipendekeza. Unampigia simu na kumpa maneno mazuri ya faraja, yeye anaona unamsumbua. Sasa wa kazi gani? Siku njema wapendwa.

LADY Jay Dee Arusha Jiwe Kigazani Baada ya Kauli ya Ruge Kuwa Walishamalizana

$
0
0

Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, alidai kuwa vituo vyake vinaweza kuanza kucheza kazi za Lady Jaydee iwapo akiwaruhusu wafanye hivyo.

Kupitia Instagram, Lady Jaydee ameijibu ofa hiyo kwa dongo lililowaendea wasanii waliowahi kumshirikisha kwenye nyimbo zao lakini kwa kuogopa kuingia matatani na kituo hicho chenye nguvu nchini, walifuta sauti yake.

“Kwahiyo wale mlio omba collabo sijui feat baadae mkaenda kufuta chorus zangu mtafanyaje ? Habariiiiiiiiiii zenu buaaaaaana  #SawaNaWao #TofautiNaHesabuZao,” aliandika Jide.

Ruge alitoa kauli hiyo Ijumaa iliyopita kwenye mahojiano na kipindi cha XXL.

“Tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza, tulimaliza, tunasubiri order. Unajua kimsingi ulipopewa order ya kwamba ‘nyimbo zangu usipige, jina langu usiseme kwenye chombo chako, vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu’ hiyo ndio order. Kwahiyo labda tukikutana, nimuombe tena [Lady Jaydee] kama tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu,” alisema.

Ruge pia alisema ana muda mrefu hajawahi kukutana na Lady Jaydee, japo amedai ‘hata leo nikipata nafasi ya kahawa nitashukuru sana kwa huo mwaliko.’

Wiki kadhaa zilizopita Ruge na Joseph Kusaga walishinda kesi ya kuchafuliwa (defamation) iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Lady Jaydee na muimbaji huyo kuamriwa kuwaomba radhi.

“Tunashukuru walau tulishinda ile kesi lakini at least ilitengeneza mfano wa watu kuelewa kwamba tusipende kutuhumu vitu kama watu huna uhakika. Bahati nzuri pia hata katika hiyo kesi alisema mwenyewe hajawahi kusikia tunasema, aliambiwa na watu. Lakini ni mambo yashapita hayo.”

Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu 'Mzee wa Upako' Afunguka Kuhusu Sakata la Kuwatukana Majirani Zake

$
0
0

Siku tatu baada ya kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako, amejibu tuhuma hizo akisema anaishi kana kwamba hana jirani.“...Tunaishi kama majambazi tu, hujui jirani yako ni nani,” amesema.


Lusekelo amesema Yesu ambaye ni  mwana wa Mungu alikubali kudhalilishwa na baadaye kufa bila hatia hivyo na yeye alikubali kula kiapo katika nafasi ya utumishi wake.


Amesema magazeti wa  mitandao ya kijamii hayawezi kumshusha kwa kuwa hayakumpasha ila Mungu pekee.


Katika mahubiri yake yaliyohudhuriwa na waumini wengi kama ilivyo kwa Jumapili nyingine za karibuni kanisani kwake, Ubungo Kibangu, mchungaji huyo aliingia kwa mapokezi ya wimbo wa kuabudu uitwao ‘Angalia Bwana’ kabla ya waumini kuanza kumtunza kwa sadaka kama ilivyo kawaida ya ibada zake.


Katika mahubiri hayo alisema haiogopi jela, bali anaogopa kuvunja sheria za nchi na wala alipokamatwa na Polisi haikumtisha wala kumvunja moyo, kwani viongozi wa dini wamekula kiapo hadi kufa. 


Aidha, alisema wapo waliosema kuwa Mzee wa Upako alikuwa anatukana, alidai kuwa matusi yake yote ni maandiko na anayetaka ufafanuzi wowote akipata nafasi amuulize yameandikwa katika vitabu gani li apate kuelewa.

Alisema mpumbavu sio tusi hayo ni maelezo na Yesu alitukanwa sana, na hata ushenzi si tusi lina maana pana ya kwamba huna hofu ya Mungu, mjinga ana dhambi ya mauti, inayomsubiri kwenda peponi.

Hata hivyo, aliwausia waumini wa kanisa hilo kuwa kamwe wasimtukane mtu kwa umbo ama rangi yake kwa kuwa hakupenda kuzaliwa hivyo na waishi hivyo kwa kutenda mema kwa kuwa ufalme wa Mungu watauona.

Alisema tangu kutokea kwa tukio amekuwa akipigiwa simu na watu ambao hakuwategemea huku waandishi wakimtaka kuzungumzia chochote wakiwamo waandishi wa habari ambao alisema walikuwamo ndani ya kanisa hilo jana.

Akifafanua kilichotokea siku hiyo, alieleza kuwa alitoka saa 11 alifajiri bila kufafanua alikuwa akitokea wapi, ndipo alipokutana na watu wawili akiwemo Mmasai na dada mmoja alipowauliza wanatokea wapi katika eneo hilo ambalo wakazi wengi wa huko hutoka na magari yao, ndipo ugomvi ulipoanzia.

“Hawa watu wa magazeti wanataka kuuza magazeti, barabara hiyo nimeijenga mimi hivyo nilikuwa na haki ya kuwauliza maana ni kibarabara... washenzi wakubwa wanaandika tu, halafu wanasema nimewatukana majirani kule hakuna jirani hajui wanaingia saa ngapi na wanatoka saa ngapi na hakuna hata habari za asubuhi. Kila mmoja anatumia gari lake,”alieleza Mzee wa Upako.


“Kwanza waliandika habari kwamba waumini hawatakuja kanisani badala yake wamejitokeza bila kukatishwa tamaa. Wakati mnajitokeza hapa mbele (kutoa sadaka), alipita mama mmoja amebeba mtoto, nilimwombea mwaka jana hapa kwamba atapata mtoto na leo amepata mtoto, sasa mbona magazeti yasiandike habari hizo?”


“Kwa nini wasiandike hayo mazuri ‘front page’ (ukurasa wa mbele)?, halafu mnaandika Mzee wa Upako matatani,matatani babu yako.”


“Najua na leo mmekuja mpo humu mnasubiri niseme, nasubiri mmalize kwanza nyinyi halafu na mimi ndiyo nitasema, baada ya mwezi mmoja najua mtakuwa mmemaliza,”alisema.

Lowassa Awajibu wanasiasa waliodai ni mgonjwa na atakufa

$
0
0

Aliyekuwa  mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewashukuru wananchi kwa kumpigia kura kwa wingi licha ya baadhi kumsema vibaya kwa kumwita mgonjwa na kwamba angekufa.


Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alitoa kauli hiyo mjini Mbinga mkoani Ruvuma ambako chama hicho kipo katika ziara ya kufanya mikutano ya ndani.


Akizungumza ndani ya vikao hivyo, Lowassa pasipo kutaja jina la mtu yeyote alisema: “Mwacheni Mungu aitwe Mungu, kwa sababu wote hata walionisema mabaya baadhi yao wameshatangulia mbele ya haki.”


Alisema kitendo cha wananchi kumpigia kura kwa wingi pamoja na kwamba alikuwa akizungumziwa vibaya juu ya afya yake, ni wazi kuwa walikubali kubeba lawama juu yake.


“Bila ujasiri na umoja wa dhati, hawa jamaa wataendelea kutupiku… lakini niwashukuru vile vile kwa kukubali kubeba lawama juu yangu, wapo waliosema huyu ni mgonjwa atakufa, bado mlinipigia kura nyingi ila Mungu ndiye hupanga yote,” alisema.


Pamoja na hayo, Lowassa aliwataka wanachama wa Chadema kuendelea kuwa na ujasiri na kudumisha umoja kwa kuendelea kujipanga kwa uchaguzi wa mwaka 2020.


Hii ni mara ya kwanza kwa Lowassa kuzungumza juu ya watu ambao walihoji kuhusu mwenendo wa afya yake wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.


Baadhi ya wanasiasa, hususani wale waliokuwa wakimpinga, walijaribu kuionyesha na hata kuiaminisha jamii kwamba mwanasiasa huyo ni mgonjwa na hafai kuongoza nchi.


Wapo ambao walidiriki kusema kwamba Ikulu si hospitali na wala hakuna gari la kubebea wagonjwa.


Miongoni mwa wapinzani wake ni baadhi ya wanasiasa wakubwa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwamo viongozi waliosikika katika majukwaa ya kampeni  mwaka jana wakiwashawishi wananchi kutomchagua Lowassa kwakuwa hata akipata urais hatotawala muda mrefu atakufa.


Wapo waliokwenda mbali na kusikika wakimwambia Lowassa Ikulu si wodi ya wagonjwa, hivyo hafai kupatiwa nafasi ya urais kulingana na afya aliyonayo.


Mikutano ambayo Lowassa ameitumia kuzungumzia suala hilo, inafanyika nchi nzima pamoja na kuwahusisha wajumbe wa ngazi mbalimbali za chama.


Uwepo wa Lowassa katika mikutano hiyo imesababisha watu wengi kukusanyika wakitaka kumuona.


Hata Lowassa anapokuwa anaondoka katika eneo hilo kuelekea mahali kupumzika, wananchi wamekuwa wakiunga msafara kwa kumfuata nyuma.


Mikutano hiyo inatajwa kuwa sehemu ya operesheni ya siku 40 inayofanyika nchi nzima iliyopewa jina la ‘Amsha Amsha

WATUMISHI Waliosoma Vyuo Vikuu Bila Sifa Kufukuzwa Kazi

$
0
0

Baada ya matamko kadhaa kadhaa ya serikali kuhusu Sekta ya Elimu nchini hatimaye leo limeibuka jingine la kutimua watumishi wote wa umma waliojiunga na vyuo vikuu na kutunukiwa "degree" bila kuwa na sifa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako wakati akifungua maonesho ya vyuo vya elimu ya juu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo vikuu nchini (TCU) yanayofanyika viwanja vya Karimjee, jijini Dar.

Maonesho hayo yanashirikisha vyuo 61 ambapo 12 kati ya hivyo ni kutoka nje ya nchi.
Katika taarifa yake Ndalichako amesema Wizara yake inawasiliana na idara ya Utumishi ili kuwabaini watumishi wote waliojiunga vyuo vikuu bila sifa na wafukuzwe kazi. "Kama wewe ni mfanyakazi uliyesoma moja ya vyuo vikuu ukafaulu lakini hukuwa na sifa ya kujiunga na chuo kikuu, tutakunyofoa hukohuko kwenye ajira yako" Alisema Ndalichako.

Kufuatia agizo hilo la Ndalichako, watumishi wote waliosoma vyuo vikuu kwa kupitia foundation courses kama Pre Entry/Remidial/Certificates, etc,wataondolewa kazini. Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa ya kusoma degree. Amesema kuwa kama mtu hakupata points za kumuwezesha kujiunga chuo kikuu hata asome foundation course bado hatapata sifa, namna pekee ya kupata sifa ni kurudia mtihani wa kidato cha sita.

Agizo hilo pia litawagusa watumishi waliojiunga na elimu ya juu kwa ufaulu linganishi (equivalent pass) ambapo kwa wale waliotoka diploma na wakasoma degree bila kufikisha GPA iliyowekwa na NACTE watatimuliwa. Pia waliotoka kidato cha sita na kupata nafasi vyuo vikuu moja kwa moja lakini hawakufikisha "cut off points" zilizowekwa na TCU wataondolewa katika ajira zao.

Prof.Ndalichako amesema zoezi hilo litaanza baada ya kumaliza zoezi la uhakiki wa sifa kwa wanafunzi wanaopata mikopo. "Tukimaliza hawa wanaopata mikopo, tutahamia wasiopata mikopo kuona kama wana sifa za kusoma vyuo vikuu, baadae kwa wafanyakazi. Hata kama hukupata mkopo, lakini ulisoma chuo kikuu bila sifa hauko salama" Alisisitiza Ndalichako.

PAUL Makonda Atoa Siri " Wapo Wanaoshinda Kwa Waganga na Wanaovaa Hirizi Wasitumbuliwe"

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amendelea na ziara zake za kutatua kero za Wananchi ambapo leo ameianza wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza na Watumishi wa Umma wa Wilaya hiyo, Makonda alisema kuwa wapo wanaoshinda kwa waganga na wanaotumia hirizi ili kujikinga wasitumbuliwe.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya hiyo DC Ally Hapi amesema kuwa atahakikisha anawashughulikia watendaji ambao hawawajibiki ipasavyo katika nafasi zao.

VIDEO: Sababu za Wanawake Wengi Kutofika Kileleni Wakati wa Kufanya Tendo la Ndoa

$
0
0
Nimekuwekea Video Hapa Mtaalam Akielezea tatizo la Wanawake wengi kutofika kileleni wakati wa Tendo la ndoa....

HIZI Hapa Sababu Tatu za Jiji la Mbeya Kuwa la Pili Kwa Wingi wa Makanisa Afrika

$
0
0
Jiji la Mbeya ni la pili kwa wingi wa madhehebu barani Afrika likiongozwa na Lagos lililopo Nigeria.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika, jiji hilo lina makanisa 450 na Mtaa wa Sae pekee una madhehebu tisa huku Mtaa wa Simike ukitajwa kuongoza kwa vituo vya maombezi.

Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi ambaye ni kiongozi wa Kanisa la International Evangerism Assemblies of God, amesema migogoro ndani ya madhehebu, uroho wa madaraka na utapeli ni miongoni mwa sababu ya watu kuamua kuanzisha madhehebu kila kukicha.

Meya huyo ambaye pia ni msimamizi wa kanisa hilo katika mikoa ya Ruvuma, Iringa, Njombe na Rukwa, amesema hakuna ubaya wa kuwa na madhebu mengi kama yanaanzishwa kwa kufuata utaratibu, sheria na misingi ya Mungu.

Amesema madhehebu mengi ya kilokole jijini humo yaliibuka baada waamini kuamua kujitenga madhehebu yao ya awali kutokana na migogoro.

“Kuna madhehebu yanamiliki vyuo vya wachungaji wanaosomea kwa mujibu wa maadili ya Mungu, kama Lutherani, Wakatoliki, Moravian, Wasabato na la kwangu, lakini tatizo wapo wachungaji wa kujipachika ambao mara nyingi wanatiliwa shaka kwa vitendo vyao,” amesema meya huyo.

Mwananchi.

VIDEO: “Mimi Sina Ugomvi na Profesa Lipumba” – Katibu Mkuu CUF

$
0
0
Kiongozi wa C.U.F Maalim Seif amekaa mbele ya Wanahabari November 27 2016 Dar es salaam na kuongelea mambo mbalimbali, miongoni mwa maswali aliyoulizwa ni kama yeye na aliyekua Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Lipumba wana ugomvi?

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Shariff Hamad amesema kuwa yeye hana ugomvi wowote na anayetajwa kwasa kuwa ndiye mwenyekiti wa CUF Taifa Profesa Ibahim Haruna Lipumba kama inavyodaiwa au kusemwa na wanachama walioko upande wake, isipokuwa tofauti ipo kati ya Lipumba, kundi lake na Chama.

“Mimi sina ugomvi na Lipumba hata kidogo, Lipumba ana ugomvi na chama na kundi lake maamuzi yamechukuliwa na mkutano mkuu wa taifa hata ukinikutanisha mimi na Lipumba siwezi kubatilisha maamuzi ya mkutano mkuu wa chama ambayo yaliwafukuza uanachama chini ya baraza kuu la uongozi” – Maalim Seif Hamad

VIDEO:

Kiwanda cha Saruji cha Dangote Kimesitisha Uzalishaji wa Simenti...Sababu Hizi Hapa

$
0
0

Kiwanda cha Saruji cha Dangote kimesitisha uzalishaji kutokana kuelemewa na gharama za uendeshaji hatua inayowaacha watumiaji wake njia panda.

Mwezi uliopita Kiwanda hicho kilililamikia Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini(TPDC) kwa kushindwa kuwauzia gesi kwa bei rahisi wakati inazalishwa mkoani Mtwara

Pia kiwanda hicho kinapinga uamuzi wa serikali kupiga marufuku kiwanda chake kuingiza makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini na kutakiwa kutumia ya Liganga ambayo yapo chini ya kiwango na bei ghali.

NAFASI za Kazi Barclays Bank na Nyingine Nyingi Zilizotangwa Katika Magazeti Leo

Shigongo: Hivi Ndivyo Nilivyomalizana na CCM

$
0
0
INAHITAJI mtu jasiri sana kuzungumza ukweli, kwani ukweli umewagharimu watu wengi, ukweli unaweza kugharimu maisha, unaweza kukupeleka gerezani, unaweza kukufukuzisha kazi, unaweza kugharimu biashara yako! Mambo haya na mengine mengi huwafanya watu kuchagua kubaki kimya, hata kama walitakiwa kufungua midomo yao na kuzungumza ukweli dhidi ya uovu au ubaya fulani.

Mimi si mtu wa kukaa kimya ninapoona jambo fulani haliendi sawa, ndivyo nilivyoumbwa, huyo ndiye mimi, kukaa na maneno kifuani au kumwambia mtu maneno ya kumpamba wakati hakustahili siyo desturi yangu, nikifanya hivyo hujisikia kama nataka kufa wakati wowote, ndivyo nilivyoumbwa.

Nilipokuwa mdogo baba yangu (Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi) alizoea kuniambia “Mwanangu Shigongo unaongea sana, maneno mengine uwe unaweka akiba, utaongea kesho” kwa maneno mengine alichokuwa akinieleza baba yangu ni sawa na msemo wa Kiingereza usemao “SILENCE IS WISDOM” yaani kubaki kimya ni busara.

Tangu siku hiyo na kwa muda mrefu nilijitahidi kuwa ninakaa kimya ili nionekane mwenye busara, yalikuwa ni maisha ya mateso yasiyo na uhalisia, siku moja nikamsikia mtu aitwaye Martin Luther King akisema: “SOMETIMES SILENCE IS BETRAYAL” maneno ya Kingereza yanayomaanisha wakati mwingine kukaa kimya ni usaliti.

Nikaja kumsikia tena wakati mwingine mtu huyohuyo Martin Luther akisema: “THE HOTTEST PLACES IN HELL ARE RESERVED FOR PEOPLE WHOM DURING THE TIMES OF MORAL CRISIS MAINTAINED THEIR NEUTRALITY!” Maneno yaliyomaanisha maeneo yenye joto kabisa huko ahera, yameandaliwa kwa ajili ya watu ambao katika kipindi ambacho maadili yaliporomoka, wao waliamua kutokusema chochote.

Tangu siku hiyo nikatamka: “NITASEMA UKWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO” na hayo ndiyo yamekuwa maisha yangu, kuzungumza ukweli wakati wote,  badala ya kubaki kimya nikiumia kwa sababu tu nataka kuonekana nina busara, mwema, mzuri au nina hofu kwamba nikizungumza ukweli nitapata matatizo.

Hicho ndicho nilichokifanya wiki iliyopita kwenye ukurasa huu, niliamua kufunguka na kuzungumza ukweli tena kwa unyenyekevu, bila kumtukana mtu wala kumkebehi yeyote, ili kuondoa mambo mengi yaliyokuwa yamejaa kifuani kwangu, kufuatia deni kubwa ambalo ninakidai chama changu cha Mapinduzi (CCM) ambalo linatokana na kazi niliyopewa ya kuchapisha vifaa vya Uchaguzi Mkuu 2015.

Yawezekana kwa mujibu wa kanuni na taratibu za chama nilikosea kueleza hisia zangu hapa, lakini kama nilivyosema wiki iliyopita, kwa mazingira niliyokuwemo ndani yake, sikuwa na jinsi, kama kuna mtu yeyote nimemkwaza kwa uamuzi wangu wa kuzungumza ukweli, basi atanisamehe, halikuwa lengo langu kabisa kumuumiza yeyote bali kumwaga mambo yaliyokuwa yamejaa kifuani mwangu, ili nipate kuwa huru, kweli niko huru.

Niliandika waraka ule kwa hisia nyingi, nikielezea maumivu niliyokuwa nayo na namna ambavyo nilikuwa naelekea kufilisika kama chama changu cha Mapinduzi kisingenilipa deni ninalodai, hapa naomba nieleweke vizuri, sikusema “CCM IMENIFILISI” nilichosema ni kwamba wanaonidai wanatishia kuuza dhamana nilizoweka kama nisingelipa deni lao, maneno mengine tofauti na  hayo ni uchonganishi wenye lengo la kufitinisha na chama changu.

Nimelazimika kuandika tena leo kama nilivyoahidi wiki iliyopita, ili kuwaziba midomo wale wanaojiandaa kusema “AMEPIGWA MKWARA,UNACHEZA NA CCM WEWE?” CCM haiko hivyo, hayo mambo yanaweza kuwa kwenye vyama vingine vya siasa lakini si chama kilichokomaa kama CCM.

Wakati ninaandika kumbukumbu ile sikutegemea kabisa habari ile ingebadilika kuwa kubwa kiasi  ilivyofikia na kusababisha mjadala mrefu mitandaoni na kwenye vyombo mbalimbali vya habari, hicho ndicho kilichotokea. Baada tu ya kutoka siku ya Jumatatu, nilianza kupokea simu kutoka sehemu mbalimbali watu wakiulizia juu ya tukio hilo, wengine wakitaka kufahamu kiasi cha fedha nilichokuwa ninadai na nilifanya biashara gani na chama.

Wapo waliokwenda mbali zaidi na kuniuliza maswali kama “Shigongo huogopi?” “CCM wanaweza kukufanya chochote.” Hakika ilikuwa vurugu, watu wakijaribu kunipandikizia hofu na kunifanya niamini kwamba nilichokifanya, cha kufungua mdomo wangu na kuzungumza ukweli, pengine lilikuwa ni kosa kubwa lililostahili adhabu kutoka kwa Chama Cha Mapinduzi, niliwaeleza wazi kwamba “Niko tayari.”

Mtandaoni watu waligawanyika makundi mawili, wapo walioniunga mkono lakini pia wapo walioniponda hasa vikundi vya propaganda ambavyo vilijaribu kunipaka matope ili kuonesha kwamba nilikuwa sifai, fisadi ambaye nilitumiwa na baadhi ya watu ndani ya CCM kupitishia ‘dili’ zao.

Eti tisheti moja niliiuzia CCM kwa bei ya shilingi elfu 95 na kofia kwa bei ya shilingi elfu 50, nikisema maneno haya hayakuniumiza nitakuwa muongo, hakika nilivunjika moyo sana pale mtu ninayemheshimu ambaye ni mwandishi mkongwe (sitamtaja jina), lakini  anayeheshimika katika jamii, ambaye siku zote nimemchukulia kama rafiki, ndugu, anaposema mimi nilifanya udanganyifu katika tisheti nilizoiuzia CCM.

Kitu ambacho wengi hawafahamu ni kwamba, kazi hii niliyoifanya kwa chama changu ilikuwa ni kazi halali kimaandishi, tena chama chenyewe ndicho kilichopanga bei ya shilingi 5,650 kwa tisheti moja na shilingi 4,400 kwa kofia moja, siyo shilingi 95, 000 kwa tisheti na 50,000 kwa kofia.

Wote mnaufahamu uchaguzi wa mwaka jana ulivyokuwa mgumu, wa kupata au kukosa! Hakuna aliyekuwa na uhakika wa ushindi, iwe CCM au Ukawa na kuna wakati dalili zilianza kuonesha kama mgombea wa Ukawa alikuwa  na nafasi, wakati mwingine wa CCM ana nafasi, katika mazingira kama hayo mtu unaelezwa tu “Nenda katengeneze, ulete halafu tutakulipa” bila hata fedha za utangulizi!

Mfanyabiashara yeyote angejiuliza “Mh! Wakishindwa je? Nitalipwaje?” Mara moja angeachana  kabisa na biashara hiyo, lakini mimi niliamua kuchukua ‘risk’ na kuifanya kazi hiyo, nikiwa nimemtanguliza Mungu mbele, hebu jiulize leo hii Chama Cha Mapinduzi kiko madarakani, sijalipwa, je, kingeshindwa ingekuwaje?

Najua mtu au kundi lililoanzisha propaganda kuwa niliuza tisheti moja kwa bei ya shilingi 95,000 na kofia kwa shilingi 50,000 lilikuwa na lengo tu la kutaka nichafuke, bila kufahamu kuwa wakati ninapewa kazi hiyo na chama mwaka 2015, mwezi Mei, bei ya dola ilikuwa shilingi 1,700, leo hii nikiwa bado sijalipwa dola moja ni shilingi 2,200!

Thamani ya shilingi imeshuka, kwa kubadilisha shilingi nitakazolipwa kama ningelipwa leo kuwa dola, ninapoteza shilingi mia tano kwa kila dola moja, wafanyabiashara watakuwa wamenielewa kwamba kazi hii, ukiongeza na riba za benki tayari ina hasara kubwa! Labda nitoe mfano kidogo ili nieleweke;

Wakati huo kama nilihitaji dola 10,000 kwenda kufanya kazi hii ya kutengeneza kofia na tisheti ilikuwa ni lazima nitumie shilingi 17, 000,000 kuzinunua, leo hii CCM wakinilipa fedha zangu nikahitaji kununua tena kiasi kilekile cha  dola 10,000 wakati bei ya dola moja ni shilingi 2,200, sitahitaji tena 17,000,000 bali nitahitaji 22,000,000! Kwa hesabu hii rahisi tu, kwa sababu ya thamani ya shilingi kushuka, nitakuwa nimepoteza 5,000,000!

Pamoja na yote hayo mtu anakwenda mtandaoni na kusema eti niliiuzia CCM tisheti moja kwa bei ya shilingi 95,000, huu ni uongo wenye lengo moja tu la kunichafua ili nionekane sifai, lakini uongo huo haondoi ukweli kwamba ninakidai chama na ingekuwa vyema nikalipwa, hata wao wanafahamu mimi si msumbufu, kama hali imefikia hapa tulipo basi kuna tatizo ambalo ni vyema kulishughulikia badala ya kuendelea kunitengenezea timu za propaganda kunishambulia.

Nimetukanwa sana, nimeshambuliwa sana, lakini nataka tu kuutangazia umma kwamba haijalishi nitatukanwa kiasi gani, ilimradi nafsi yangu ni safi, kwamba nilichokisema ni kweli na tena ni haki yangu, sitanyoosha mikono, nitakipigania mpaka dakika ya mwisho ya uhai wangu.

Ukiwa na dawa ya meno mkono wa kushoto, mswaki mkono wa kulia na unataka kusafisha meno yako, hata ungefunga na kuomba siku arobaini ili dawa itoke kwenye chupa yake na kwenda kwenye mswaki, utasali mpaka Yesu anarudi hutashuhudia huo muujiza, atakuja mtu ambaye hata kanisani huwa haendi, atachukua chupa ya dawa na kuikamua, dawa itatoka na kuiweka kwenye mswaki kisha kusafisha meno yake.

Nilichokifanya wiki iliyopita ndicho hichohicho, kukamua ili nipate haki yangu, kuna mambo hapa duniani hayahitaji kufunga na kuomba ni kuchukua hatua tu, ukifunga na kuomba peke yake kwenye suala linalohitaji kuchukua hatua, mbele za Mungu unaonekana huna akili timamu.

Jioni ya siku hiyo ya Novemba 21, 2016, saa 3:30 usiku baada ya gazeti kutoka, nikiwa nyumbani mtu mmoja ambaye nisingependa kumtaja hapa, alinipigia simu na kuniambia “Eric, mzee Kinana anakutafuta, tafadhali mpigie muongee” baada ya kuzungumza naye nilianza juhudi za kumtafuta Katibu Mkuu bila mafanikio, mpaka nikaamua kulala matumaini yangu ni kwamba ningempigia siku iliyofuata.

Saa moja asubuhi niliondoka nyumbani kuwapeleka watoto shule ambako niliwashusha na kuelekea ofisini kichwa kikiwa kimejawa na mawazo mengi, karibu kila mfanyakazi niliyemwangalia usoni alionekana kuwa na sura ya ‘SIJUI ITAKUWAJE?” Hakuna mtu aliyekuwa akiniambia chochote.

 Saleh Ally, Mhariri Kiongozi Magazeti ya Michezo ni rafiki yangu, huwa yuko wazi sana kuongea na mimi chochote, lakini siku hiyo alikuwa akiniangalia kwa jicho la kwenye kona, hataki kukutanisha macho na mimi, moyoni nikatambua kwamba karibu watu wote ofisini walikuwa na hofu kubwa  sana na hatima yangu na yao.

Saa nne hivi asubuhi, nikiwa nimesimama nje ya ofisi, simu yangu iliita, nilipoangalia kwenye kioo niliona maandishi “SG”, moyo wangu ukadunda, maana nilifahamu kabisa mtu aliyekuwa akipiga simu ile kwa namna moja au nyingine alikuwa amechukia kwa uamuzi wangu wa kuzungumza ukweli, pengine alikuwa na hasira na angeweza kunitamkia maneno ya kuniumiza zaidi, nikasita kuipokea simu lakini baadaye nikajipa moyo.

“Shikamoo baba!”

“Marahaba hujambo Eric?”

“Sijambo.”

“Sasa wewe mwanangu umefanya nini tena?” aliniuliza.

Akaendelea kunisema kwamba kitendo ninachokifanya kilikuwa kibaya, nakumbuka nilichokisema peke yake kwake ni kwamba “Sikuwa na jinsi baba, hali yangu ni mbaya sana na hakuna mtu anayeonekana kujali.”

“Uko wapi?”

“Niko ofisini!”

“Hebu njoo haraka hapa Lumumba.” Ilikuwa ni sauti ya Katibu Mkuu wa CCM, mzee Kinana ambaye kwenye simu yangu nimeitunza namba yake kwa jina la “SG”

Moyo wangu ukinidunda, nikijua huko CCM Lumumba nilikokuwa naitwa kulikuwa na matatizo makubwa kwa sababu nimewaudhi viongozi wakubwa wa chama, nilimwita dereva wangu, Nyange na kumwambia: “Kimbia haraka sana kuelekea ofisi za CCM Lumumba!”

Dakika arobaini na tano baadaye tuliegesha mbele ya Jengo la CCM Lumumba, nikashuka na kuingia ndani, nikasaini kitabu cha wageni na kupandisha hadi ofisini kwa mzee Kinana, Katibu wake aliniambia: “Ingia mzee anakusubiri” mara moja nikaingia ndani na kumkuta mzee Kinana ameketi akiwa na Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Rajab Luhwavi.

Tofauti kabisa na matarajio yangu nilipokelewa kwa tabasamu, shinikizo langu la damu ambalo nahisi lilikuwa limekaribia mia mbili, kidogo likaanza kutulia! “Keti kwenye kiti Eric” alisema Luhwavi akiniangalia kwa jicho la huruma, nilipoketi mzee Kinana akaanza kunieleza kwamba hisia zangu zilikuwa zimeniondolea uvumilivu na kunituma kufanya maamuzi mabaya, muda wote huo nilikuwa kimya, nimemwacha mzee ambaye kwangu mimi ni mzazi aongee, ndivyo nilivyolelewa, kwetu sisi huwa hatufungui midomo kuongea wazazi wakiwa wanasema.

“Eric, mimi sikuwepo hapa nchini, nilikuwa nimempeleka nduguyo kutibiwa huko India, ndiyo maana ulikuwa hunipati kwenye simu, si kwamba nilifanya dharau!” aliongea mzee Kinana kwa upole tofauti kabisa na nilivyotarajia  na kuugusa moyo wangu.

“Kwa hilo naomba unisamehe baba, ningejua umepeleka mgonjwa nje ya nchi wala nisingezungumza maneno hayo, machungu niliyonayo moyoni ni makubwa, niko hatarini kupoteza mali za watoto wangu, nihurumieni!”

Muda mfupi baadaye mlango ulifunguliwa, akaingia mama Zakia Meghji akiongozana na Mohamed Seif Khatibu, niliwaamkia wote, timu nzima ikaanza kunisihi nitulie, nisifanye maamuzi yasiyo sahihi! Kifua changu kilikuwa kimejaa, sikuweza hata kuongea vizuri.

Baadaye mama Meghji na Khatibu waliondoka ofisini kwenda kwenye chumba cha kusubiria wakituacha sisi watatu; Mzee Kinana, Luhwavi na mimi tukiongea juu ya namna ya kulimaliza tatizo, wakakiri chama hakikuwa na fedha wakati huo lakini wangejitahidi kadiri ya uwezo wao kupunguza deni kidogokidogo mpaka limalizike, tukakubaliana kuwa na mawasiliano ya karibu badala ya kukaa kimya.

Niliondoka ofisini kwa mzee Kinana moyo wangu ukiwa umetulia kabisa, matumaini yakiwa yamerejea moyoni mwangu kwamba nisingepoteza haki yangu na watoto wangu! Tangu siku hiyo mpaka ninavyoandika kumbukumbu hizi, nina amani mno moyoni mwangu, ingawa sijalipwa, najua ipo siku ambayo haipo mbali nitalipwa nami nimalizane na wanaonidai.

Kuhusu suala la CCM na deni ninalodai hapo ndipo lilipofikia, sina maelezo zaidi ya hapo, nabaki kuwa mwanachama muaminifu wa Chama Cha Mapinduzi, kada aliye tayari kupigana usiku na mchana kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kustawi, nilichofanya ni kutumia uhuru wa kujieleza ambao upo ndani ya Chama Cha Mapinduzi na katiba ya nchi yetu.

Kitu kimoja nataka kuwaeleza Watanzania wenzangu  ni kwamba, wakati umefika wa watu kuachana na hofu nyingi iliyoligubika taifa na kuanza kuzungumza ukweli, badala ya unafiki na kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa hali ambayo inaendelea sana katika nchi yetu.

Hatuwezi kulisaidia taifa hili kama hatutazungumza ukweli, hatuwezi kutengeneza taifa la vijana waoga tu, ambao hawawezi kusimama na kuzungumzia yanayowaumiza, eti kwa sababu watapoteza kazi, watapoteza biashara, watawaudhi watu, la hasha! Kuzungumza ukweli ndiko kuliwafanya wazee wetu wa mwanzo wafanikiwe kuwaondoa Wakoloni katika nchi yetu, leo hii tuko huru kwa sababu walihatarisha maisha yao kwa ajili yetu.

Lazima tuzungumze pale tunapoona mambo hayaendi sawa, lazima tupaze sauti pale tunapohisi tunaonewa! Katika taifa hili watu wamechagua kukaa kimya, hata viongozi wa dini waliotarajiwa kuwa watu wa kwanza kukemea mambo maovu, sasa wanaogopa kusema kwa sababu tu hawataki kuwaudhi watu! Wakati umefika wa kila  mtu kusimama katika sehemu yake na kuzungumza ukweli, kama kweli tunayo nia ya dhati ya kulisaidia taifa letu, vinginevyo tutazama pamoja, hakuna atakayebaki salama.

Silaha ya mnyonge ni kelele, pazeni sauti zetu, Wakristo wanajua, Biblia inamtaja mtu mmoja aitwaye Batimayo, huyu alikuwa kipofu aliketi kando ya njia, akasikia kundi kubwa la watu linapita, alikuwa ni Yesu mponyaji ambaye Batimayo alishasikia habari zake.

“Nani anapita?” Batimayo alimuuliza rafiki yake.

“Yesu Mnazareti!”

Bila kupoteza wakati Batimayo alinyanyuka na kuanza kupaza sauti: “Yesu! Yesu! Nihurumie!” Yesu aliyekuwa amekwishapita eneo hilo alisikia sauti ya Batimayo, akageuka na kutembea mpaka mahali alipokuwa na kumuuliza: “Nikufanyie nini?”

“Ninataka kuona.”

Yesu akamponya Batimayo upofu wake! Sisi pia tukipaza sauti zetu, pamoja na unyonge tulionao tutapata uponyaji kiuchumi, kiafya, kielimu, nk.  Badala ya kuendelea kubaki kimya kama vile hatuumii, huo ni unafiki ambao hakika hautatusaidia chochote, STAND UP AND SPEAK.

Mwisho wa mjadala…

Ma Rapper 6 wa Kike Bongo Kuonyeshana nani zaidi Kwenye Wimbo Mmoja Uliyotayarishwa na Producer Nahreel....

$
0
0
Marapa 6 wa Kike Bongo Wameamua kuungana na kutoa wimbo mmoja kwapamoja, Marapa hao ni Stosh, Cindy Rulz, Rosa Ree, Chemical, Pink na Tammy wataonyeshana nani zaidi ya mwenzake  kwenye ngoma ya pamoja iitwayo ‘Hola Hola’ iliyotayarishwa na Nahreel

Wimbo huo uliopo kwenye mradi uliopewa jina Dada Hood utatoka Jumatano hii. Mtangazaji wa Clouds FM, Mamy Baby anahusika kusimamia Mradi Huo



Wafuasi wa Lema Watinga Mahakamani na Fulana Zenye Ujumbe Huu

$
0
0

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema tayari amefikishwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kusikilizwa rufaa yake.

Mawakili wa pande zote walikutana kwa jaji kupeana taarifa  kabla ya kesi kuanza.

Ulinzi umeimarishwa mahakamani huku wafuasi wa Lema leo wametinga mahakamani na fulana nyeupe zimeandikwa Jutice 4 Lema mbele zikiwa na picha yake.

Rufaa ya Godbless Lema Yagonga Mwamba Leo Tena...Arudishwa Selo

$
0
0

Rufaa ya mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema iliyopangwa kutolewa leo imeshindikana baada upande wa Jamhuri kuweka pingamizi ya kuwasilisha notisi badala ya rufaa, ambapo Mbunge huyo amerudishwa rumande kwa mara nne.


Upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiwakilishwa na mwanasheria Matenus J Marandu ambaye amesema wamefanya hivyo ili kuharakisha na wamekubaliana na pande zote mbili.


Wakili wa Chadema Peter Kibatala amesema wameshakamilisha taratibu za kisheria kuhusiana na pingamizi hilo na wanasubiri pingamizi hilo lililowekwa na upande wa serikali.


Jaji aliyekuwa akisikiliza pingamizi hilo Fatma Masengi ameelekeza upande wa serikali wawasilishe hoja zao kwa njia ya maandishi kabla ya November 30 ili aweze kutolea uamuzi December 2 mwaka huu.

YOUNG Dee Akiri Kurudiana na Mrembo Tunda..Adai yeye Ndio Alikuwa Tatizo Mpaka Wakaachana

$
0
0
November 28, 2016 U Heard ya Soudy Brown ndani ya XXL ya Clouds FM iko na story kuhusu uhusiano wa kimapenzi uliokuwepo kati ya rapa Young Dee ambaye aliwahi kuwa na uhusiano na Video Queen Tunda waliyeacha baada ya kutoelewana kupelekana polisi.

Baada ya kuwepo taarifa kwamba Tunda ameachwa na mwanaume anayetajwa kuwa alikuwa akimgharamia kwa kila kitu ikiwemo kulipia nyumba, kununua magari na starehe zote alizokuwa akizifanya kila siku, ikaja kuonekana ameanza kuwa karibu tena na Young Dee.

Leo Soudy Brown amepiga stroy na Young Dee ambaye ameeleza kuwa yeye na Tunda wako vilevile kama mwanzo hawakuwahi kugombana na ameamua kumsamehe Tunda kwasababu itakuwa kosa kubwa endapo hatamsaheme wakati yeye pia ana makosa makubwa zaidi ya hayo ya Tunda.

“Mimi nilikuwa na matatizo yangu mengi sana hata kufika hapa tu nimesamehewa sana vitu vingi katika watu ambao hawakutakiwa kusamehewa ni mimi ndio mana nimeamua kumsamehe, kwa yote ambayo Mungu amenisamehe nisiposamehe nitakua nakosea sana” – Young Dee

ALIKIBA Aicheka Kauli ya Diamond Kuhusu Pete ya Kijani!

$
0
0
Je unaikumbuka kauli ya Diamond aliyoitoa wiki iliyopita kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM kuhusu pete ya kijani?

Ngoja nikukumbushe japo kidogo kile alichokisema, “Mimi sina matatizo na watu ndio maana wakijaribu kushindana na mimi huwa wanashindwa. Hata ukiniangalia sina hata pete ya kijani kwenye vidole vyangu.”

Kumbe alikuwa amerusha jiwe gizani kwa upande wa pili. Inawezekana Alikiba ameshtuka hilo kutokana na picha aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram na kuandika, “Pete Ya Kijani 😂😂#BirthdayLoading29thNoV #KingKiba.”

Mwanzo ilionekana ilikuwa ni vita baridi ya maneno ya chini kwa chini kati ya mafahari hao lakini kwa sasa hakuna kilichojificha tena na kila kitu kipo wazi.

Wiki iliyopita hitmaker huyo wa Salome na Ommy Dimpoz walichafua hali ya hewa kwenye mtandao huo kwa kutupiana vita ya maneno ya kejeli na kukashifiana.

Chanjo Dhidi ya Ukimwi Kufanyiwa Majaribio Afrika Kusini

$
0
0
Chanjo mpya dhidi ya virusi vinavyosababisha Ukimwi itaanza kufanyiwa majaribio nchini Afrika Kusini Jumatano wiki hii.

Wanasayansi wanasema huenda ikawezesha binadamu kukabiliana na virusi hivyo iwapo itafanikiwa, shirika la habari la AP linasema.

Wakati wa majaribio hayo, ambayo yamepewa jina HVTN 702, wanasayansi wanatarajiwa kuwatumia wanaume na wanawake 5,400 ambao wanashiriki ngono kutoka maeneo 15 nchini Afrika Kusini.

Washiriki hao watakuwa wa umri wa kati ya miaka 18 na 35.

Majaribio hayo yatakuwa makubwa zaidi na ya kina zaidi ya chanjo ya Ukimwi kuwahi kufanyika nchini Afrika Kusini ambapo zaidi ya watu

"Ikitumiwa pamoja na silaha tulizo nazo sasa za kuzuia maambukizi, chanjo hiyo inaweza kuwa msumari wa mwisho katika jeneza la Ukimwi,"

Anthony Fauci, mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Maradhi ya Kuambukizana na Mzio ya Marekani (NIAID) amesema kupitia taarifa.

"Hata kama mafanikio yake yatakuwa ya kadiri, hilo linaweza kupunguza pakubwa mzigo unaotokana na maradhi hayo katika nchi zenye viwango vya juu vya maambukizi, mfano Afrika Kusini."

Chanjo ambayo itafanyiwa majaribio chini ya HVTN 702 ina uhusiano na majaribio ya chanjo yaliyofanywa mwaka 2009 nchini Thailand.

Chanjo iliyofanyiwa majaribio mwaka huo iligunduliwa kuwa na mafanikio asilimia 31.2 katika kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika kipindi cha ufuatilizi cha miaka 3.5 baada ya mtu kupewa chanjo.

Wanasayansi wametayarisha chanjo hiyo mpya mahsusi kutoa kinga pana na kwa muda mrefu na kwa kuangazia zaidi aina ya virusi vinavyopatikana kusini mwa Afrika.

Watakaoshiriki katika majaribio hayo ni watu wa kujitolea.

Wanachaguliwa bila kufuata mpangilio wowote, ambapo kundi moja litapokea dozi ya chanjo kwa kipindi fulani na jingine kipimo kisicho cha chanjo. Washiriki wote watadungwa sindano tano katika kipindi cha mwaka mmoja.

Washiriki watakaoambukizwa virusi vya Ukimwi katika kundi hilo watatumwa kwa wahudumu wa afya ili kupokea matibabu ya kupunguza makali ya virusi hivyo na pia kushauria jinsi ya kupunguza hatari ya kueneza virusi hivyo.


Afrika Kusini ina zaidi ya watu 6.8 milioni ambao wanaishi na virusi vya Ukimwi.

Taifa hilo hata hivyo limezindua mpango mkubwa wa kutoa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo na kuudhibiti, mpango ambao inasema ndio mkubwa zaidi wa aina yake duniani.

Kiwango cha wastani cha umri wa kuishi kilikuwa kimeshuka sana nchini humo na kufikia miaka 57.1 mwaka 2009 lakini kutokanana na juhudi hizo, kimepanda hadi miaka 62.9 kufikia 2014.

Matokeo ya majaribio hayo ya chanjo yanatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwaka 2020.
Viewing all 104771 articles
Browse latest View live




Latest Images