Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live

Masharti Ya Kumtext Mwanamke - Makosa 5 Wanaume Wanayofanya

$
0
0
Kila siku mara moja au nyingine huwa tunawatext wanawake. Aidha wawe ni wapenzi wetu, tunaowatongoza ama marafiki zetu. Na kila siku huwa tunapatwa na changamoto mbalimbali kutokana na matangamano yetu. So huwa kunakosekana nini? Ifuatayo ni orodha ya mambo 5 makuu ambayo wanaume wengi hukosea wakati wanapomtext mwanamke, na jinsi ya kutatua.


#1 kukata tamaa mapema kwa mwanamke
Kosa kuu ambalo wanaume wengi hufanya ni kukata tamaa mapema wakati wanapomtext mwanamke. Watamtext mwanamke, na kama hatajibu jumbe zake (ama kujibu kiuchache) watachukulia kuwa mwanamke huyu amepoteza interest na wanakata tamaa. Hili ni kosa kuu sana.

Kama inavyojulikana kikawaida ni kuwa mwanamke anaweza kutojibu meseji zako, na sababu hizo hazina uhusiano moja kwa moja na kutokuwa na interest kwako. Kwa mfano, anawezakuwa labda yuko busy, katika mood mbaya, ama labda hayuko sure ni kitu gani cha kukujibu kwa meseji. Kiufupi ni kuwa haujui kile ambacho kinazunguka kwa akili ya mwanamke, so haina haja ya kufikiria jambo baya.

So, iwapo kama mwanamke hakukujibu ama hayuko interested na wewe, lakini bado unataka kuongea na yeye, hivi ndivyo unavyopaswa kufanya; Mpe muda wa kutosha (siku chache ama hata wiki) halafu anza kumhusisha kwa meseji. Kama vile texts zozote za kawaida, hapa utakuwa unataka kuhakikisha kuwa unamvutia, unamfurahisha na unamchesha. Na zaidi ni kuwa unapaswa kutafuta swali ambalo litamlazimu yeye kureply meseji yako. Yote hayo, huu hapa ni mfano mzuri wa meseji ambayo itamhusisha mwanamke yeyote:

Hello mrembo...hivi kweli uko hai? Nitume kikosi cha maninja kije kikunusuru ama?

Yaweke maneno yako kuwa ya ucheshi, yawe na kamchezo flani na bila shaka utamfanya huyu mwanamke kutabasamu na kuwa katika hali ya kuchangamka. Kama utaweza kumfanya atabasamu basi muda mchache tu atakujibu.

2. Kutext mara nyingi.
Hakuna kitu ambacho kinaweza kuua nafasi yako kwa mwanamke kama kumtumia jumbe mara nyingi. Humfanya mwanaume aonekane mwenye tamaa hivyo kumfukuza mwanamke.

Kwa kuepuka haya yote hizi hapa ni njia unazoweza kuzitumia ambazo zinaweza kukusaidia kumtext mwanamke wakati sawa.

♥Unapomtext mwanamke, hakikisha kuwa jumbe zinakuwa 1:1, Unahakikisha kuwa kila meseji anayotuma unaijibu na moja (pia hakikisha urefu unakuwa sambamba)

♥Acha kumtext na jumbe zisizo na mwelekeo. Usimjibu mwanamke jumbe wakati ambapo haihitaji jibu. Kwa mfano, si lazima uijibu text ya mwanamke ya 'usiku mwema' kama utamwambia 'nawe pia'. Ikifikia hatua hii mazungumzo yenu yatakuwa yameisha. Inachotakiwa kutoka kwako ni kuhakikisha kuwa jumbe ya mwisho inaisha kutoka kwake.

♥Weka fikra ya wengi. Wakati ambapo unamtext mwanamke mmoja, huwa kawaida unakuwa na mtazamo finyu wa kumfiria sana mwanamke huyu ukiogopa asikuache. Well, kutatua swala hili, lile unalotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa katika akili yako weka ya kuwa una wanawake kadhaa ambao wanakufukuzia. Hii itakusaidia kuondoa uhitaji mwingi wowote.

3. Kuchukulia jumbe unazomtumia serious.
Kuna hali tofauti tofauti ya kuwa serious na mwanamke wakati wa mazungumzo lakini kutumia jumbe si moja wapo. Kujifanya kuwa serious wakati wa kumtext mwanamke kunachosha na hakuna mtu anapenda. Hivyo weka seriousness zako mbali kabisa na ulete hali ya ''nataka-tujuane-nawe''. Wakati unapomtext mwanamke, unapaswa kumakinika kuleta furaha.

Sasa, njia nzuri ya kuhakikisha kuwa unamfanya mwanamke anakuwa na shangwe wakati wote ni kwa kutumia 'emoticons'. Wanaume wengi wanajitenga kutumia emoticon wakidhania kuwa ni mambo ya wanawake, ukweli ni kuwa ni mambo ya wanawake na wanawake wanapenda kutumia emoticon. Pia zinasaidia kwa kuwa kile utakachokisema kwa kutumia emoticon mwanamke hatakipuuza. Hatobahatisha hisia zako kamwe kwa kuwa emoticon zinasaidia kupitisha ujumbe unaodhaminia. Na matokeo yake ni kuwa unaepukana na drama zozote zitakazojitokeza.

4. Kutotext wanawake wengi.
Wakati mwanaume anatext mwanamke mmoja, ni rahisi kwake kumaliza maongezi yake mapema kwa kuwa hana fikra pevu kama vile tulivyotangulia kusema awali. Kama unataka kuwa na fikra pevu na uwezo rahisi wa kutangamana na wanawake basi ni lazima uwe unatext wanawake wengi. [Soma: Njia 5 rahisi za kumwomba mwanamke namba ya simu]

Kufanya mazungumzo mengi na wanawake wengi kunakupa ufahamu na mbinu pana za kuweza kuzungumza na wanawake. Ustadi huu utakuja wenyewe iwapo utajikita kuongea na wanawake wengi na tofauti tofauti katika meseji zako. So kinachohitajika kwako ni kutafuta namba za wanawake tofauti tofauti na uanze kuongea nao kupitia jumbe.

5. Tunasahau lengo kuu la kumtext mwanamke.
Wakati mwingine wanaume wanasahau kwa nini wanawatumia jumbe wanawake. Wanakita kuongea mambo ya mbele, nyuma na ovyo bila msingi wowote ule. Wanasahau ile taswira kuu ya kumtext mwanamke. Taswira kuu kama tujuavyo ni kuhakikisha unatoka deti na mwanamke huyu.

Lakini usichukulie kuwa kuchat na mwanamke kupitia texts imepangwa, la. Unapaswa kutumia mfumo ule wa kawaida wa kuleta ucheshi, mzaha nk, kama tulivyoelezea awali. Hivyo basi, mbinu zako za kumtext mwanamke lazima ziwe za kuvutia, za nakshi na ambazo zitaleta msisimko ndani yake. Kama utamtext mwanamke bila mpangilia ama lengo flani, basi bila shaka atapoteza hamu na kuenda zake.

By Nesi Mapenzi

Diamond ft Neyo "marry You" Yashika Namba 2 UK, Aweka Record

$
0
0
Nyimbo mpya ya diamond ft Neyo iitwayo marry you ambayo official release imeshaachiwa United Kingdom (UK) shiku chache zilizopita imeendelea kufanya vizuri kwenye vituo mbali mbali.
Katika nyimbo mpya zilizotoka hivi karibuni diamond amekuwa akichuana na Bruno mars na wimbo wake wa Chunky.

Katika nyimbo bora za wiki zilizotoka hivi karibuni marry you imeshika nafasi ya 2 nyuma ya Chunky iliyokamata namba 1 kwenye kituo cha beat london, na kuweka record ya kuwa mtanzania wa kwanza kufikia level hiyo.

Ikumbukwe diamond na Neyo watakuwa na tour ya pamoja mwezi ujao huko UK

Hii ni hatua nyingine muhumu kwa diamond na mziki wake
Ikumbukwe wimbo wa marry you bado haujaachiwa kwa upande wa africa na video bado haijatoka
Japo kuna demo ilivuja

BARAKA The Prince Aikana Timu Kiba..

$
0
0

Kama ulijua Barakah The Prince ni team Kiba, utakuwa umekosea kwa mujibu wa muimbaji huyo.

Hitmaker huyo wa Nisamehe adai kuwa hayupo team yoyote kati ya Kiba na Diamond ila anachotaka yeye ni mashabiki kutoka pande zote hizo mbili.


“Mimi sina team kiukweli. Mimi ni shabiki wa Diamond lakini pia ni shabiki wa Ali. Diamond ameleta heshima kubwa kwenye muziki wa Bongo Fleva. Ali ni msanii mkongwe ambaye ameniispire sana kuingia kwenye huu muziki, lakini pia Diamond anafaa kuwa role model. Mimi nataka mashabiki wa team zote,” amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.


Muimbaji huyo yupo chini ya kampuni ya Rockastar4000 inayo msimamia Alikiba na Lady Jaydee.

Vanessa Mdee Apata Shavu Afrika Kusini

$
0
0
Vanessa Mdee amepata shavu la kuigiza kwenye tamthilia ya MTV Shuga Afrika Kusini kwenye msimu wa tano.

Kupitia mtandao wa Instagram, hitmaker huyo wa Niroge ameandika, “Ninafuraha sana kuwatangazia kuwa nitakuwa kwenye msimu mpya wa#MTVShuga itakuwa kazi yangu ya kwanza kabisa ya kuigiza na haitokuwa ya mwisho Inshallah.”

Vanessa ataungana na wasanii wengine kwenye tamthilia hiyo akiwemo Thuso Mbedu, Mohau Mokoatle Cele, Jezriel Skei, Emmanuel Ifeanyi, Nicki Mutuma na Adesua Etomi.

Hivi ndivyo MTV wameandika:

Shugafam! In the run-up to World AIDS Day, we are proud to reveal the cast for MTV Shuga in South Africa…

We are SO excited to announce that Vanessa Mdee, Thuso Mbedu, Mohau Mokoatle Cele, Jezriel Skei, Emmanuel Ifeanyi, Nick Mutuma and Adesua Etomi are heading up our amazing crew for the fifth series of MTV Shuga.

Following on from four seasons in Kenya and Nigeria, we are coming to Mzansi in a BIG way! Drama, Music, Love, Sex; MTV Shuga has it all. Underneath all of that though, MTV Shuga’s stories focus on real issues that affect real people.

At the core of our brand, sexual health, reproductive health, and social issues take centre stage. Young girls in South Africa have a lot on their plate, with research showing that they are particularly vulnerable to HIV infection and unplanned pregnancies. For a girl, the years between 15 and 24 are considered the most dangerous time for them to contract HIV. These are issues that need to be explored and tackled head on, which is exactly what we’ll be doing with the help of our dope cast!

Tanzanian superstar Vanessa Mdee will be flexing her skills as “Storm” – a dissatisfied trophy wife with a wandering eye. Also joining our fam is “Scandal!” actor Thuso Mbedo, who will play the role of Ipeleng, an ambitious schoolgirl who’s raising her little brother after the death of their mum. 17-year old Jezriel Skei, best known for his award-winning performance in “Four Corners” (2013), will rock the super-macho soccer look as “Q”.

Setting sail in the cool clubs, chilled spots and local schools of Braamfontein and the made-up township of ‘Zenzele’, MTV Shuga will welcome back our crew since day dot. Lovebirds Ikubese Emmanuel Ifeanyi, known for his role as ‘Femi’: a Nigerian music promoter who’s been living with HIV for 4 years, and Adesua Etomi, playing the role of ‘Sheila’, are touching down in South Africa for the new season.

Also returning to her hometown is Mzansi’s own Mohau Mokoatle Cele. Cele will be playing the role of a frustrated teenage singer called ‘Bongi’, whilst MTV Shuga veteran, Nick Mutuma, will be heading down south as ‘Leo’ tries to escape his troubled past.

Catch the premiere of MTV Shuga on MTV Base (DStv Channel 322) and BET (DStv channel 129), as well as other broadcasters, MTV networks and third party broadcasters around the world from 8 March 2017.

As always, the MTV Shuga Campaign is coming at you with a radio drama series, peer educator programme, comic book, mobile information service, social media and a range of digital platforms.

To stay in the loop, hit us up on Facebook, Twitter and Instagram, or visit our website for the latest news about the upcoming season.

South Africa, we’re coming for you!

Chadema Waja na Operation Mpya Baada ile ya UKUTA Kufeli

$
0
0
Baada ya kuanzisha na hatimaye kukwama kuitekeleza operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), Chadema imekuja na nyingine itakayokwenda kwa jina la ‘Kata Funua’.

 Operesheni hiyo mpya imetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikilenga kukipa chama hicho mafanikio katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule mkuu ujao.

 Mbowe amesema hayo katika kikao cha uchaguzi wa mwenyekiti wa kanda wilayani Masasi mkoani Mtwara.


“Kiongozi yeyote atakayeonyesha nia ya kutukwamisha hatutamvumilia, tutamuondoa ili tuweze kuendelea na safari yetu na kumaliza kutembelea kanda zote,” amesema.

 Amesema ziara hizo ndizo zitakazoipa nafasi chama hicho kuchukua maeneo mengi zaidi hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema umoja na mshikamano ndiyo msingi imara utakaowasaidia kuweza kufikia malengo.


“Ili kufanikiwa lazima kuwe na umoja imara baina ya viongozi wa chama. Mtu yeyote atakayekuwa na nia mbaya na umoja huu achukuliwe hatua mara moja ili kuepuka kutokea kwa migogoro,” amesema.


Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu amemshukuru Rais John Magufuli kwa kukipa fursa adhimu chama hicho kutokana na kuzuia mikutano ya kisiasa majukwaani jambo ambalo limewasaidia kujipanga vizuri katika uchaguzi ujao.


“Safari hii ni fursa kwetu, tumejipanga kiuhakika na si kwa kubahatisha tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji, mitaa mwaka 2019 na baadaye uchaguzi wa wabunge na Rais ifikapo 2020,” amesema.


Wizara ya Elimu Yakanusha Taarifa ya Wanafunzi wa Diploma Kuzuiwa Kujiunga Vyuo Vikuu

$
0
0
WIZARA ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imetoa ufafanuzi kwamba haijapiga marufuku watu wenye Stashahada wenye sifa kujiunga na vyuo vikuu badala yake walichokataza ni wanafunzi waliofeli kidato cha nne na cha sita kujiunga na vyuo vikuu bila kuwa na vyeti vyenye sifa.

Aidha, imesema kwa waliomaliza kupitia mfumo huo na wapo kazini ni wajibu wa waajiri wao kuhakikisha wana sifa za kazi wanazofanya na kutumia fursa hiyo kufanya mitihani ili kuwa na sifa zinazohitajika.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Stella Manyanya alitoa ufafanuzi huo jana Dar es Salaam kutokana na taarifa za upotoshaji zilizoenea mitandaoni kwamba serikali imepiga marufuku watu wenye Stashahada kujiunga na vyuo vikuu badala yake watakaoingia ni wenye sifa za kidato cha sita.

Manyanya alisema kwa waliopo vyuoni kwa sasa wanatakiwa kuhakikisha wanakuwa na sifa za shahada kwa kusafisha vyeti vyao na wapewe fursa ya kufanya mitihani hiyo waliyofeli na kama wamefaulu kozi hiyo, pia wataweza kufaulu mitihani hiyo itakayowapa sifa ya kusoma vyuo vikuu.

“Ni vitu tunavyovifanya wenyewe ila vina madhara makubwa, unakuta mtu anakaa nafasi kwa sababu ana vyeti, lakini uwezo hana… uhakiki utafanyika kwa vyeti na wanaofanya hivyo ni Utumishi,” alisema Naibu Waziri.

Alisema kwa watakaobainika pia kuingia vyuoni kwa sifa ambazo zilikuwa hazitakiwi kwa wakati huo ni batili zitafutwa na kwa watakaoingia kwa sasa vyuoni kwa kutumia njia zisizo rasmi na kubainika hata ikifika mwaka 2020 watafutwa kwa kuwa taarifa tayari wanayo.

“Kilichoongelewa siku ile ni kuruhusu kidato cha nne na kidato cha sita waliofeli kuingia kwenye ‘foundation course’ na diploma haikutajwa pale kwa kuwa haikuulizwa na hakuna kauli iliyotajwa pale kukataza watu wa diploma kwenda chuo kikuu,” alieleza Manyanya akirejea kauli ya Waziri wake, Profesa Joyce Ndalichako hivi karibuni katika mahafali ya Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) yaliyofanyika mkoani Pwani.

Profesa Ndalichako alikaririwa akisema vigezo vya udahili vinatakiwa kuzingatiwa.

“Nami ningependa nizungumzie kwamba foundation course hazimuongezei mtu sifa. Kama sifa ya kujiunga na chuo kikuu ni kufaulu kidato cha sita, kama amefeli Baraza la Mitihani linaruhusu kurudia mtihani, kwa nini anakwepa kule? Kwa nini? Kwa nini tunataka tuendeleze uchochoro,” alieleza Waziri Ndalichako.

Naibu Waziri alisema kuna njia mbili za kwenda chuo kikuu ikiwemo njia ya moja kwa moja na njia ya mbadala ya kuwa na vyeti vinavyotambulika na kinasimamiwa na mamlaka husika ambayo ni Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na wawe na ufaulu mzuri.

“Tanzania imejiwekea mifumo yake ya elimu ambayo inaendana na ngazi za kimataifa katika utoaji wa elimu na hapo awali tulikusudia kuhakikisha elimu inatolewa kwa watu wengi zaidi na hizo fursa zinawafikia wadau wote katika ngazi mbalimbali kwa kupanua elimu ya msingi hadi vyuo vikuu,” alieleza Naibu Waziri.

Alisema walitambua kuna wadau mbalimbali walitamani kusoma vyuo vikuu, lakini hawapati hiyo fursa na ndiyo wakaanzisha mfumo huo wa Chuo Kikuu Huria na mtu anaweza kusoma alipo na mfumo umekuwa ukiboreshwa siku hadi siku.

Alisema iliwekwa mifumo ya vyeti na ngazi zake kulingana na vigezo na hivyo siyo kila cheti kinachotolewa kinaruhusu mtu kwenda ngazi nyingine na kila mamlaka imepewa jukumu ili kulinda ubora wa elimu unaotolewa nchini.

Naibu Waziri alisema kutokana na uanzishwaji wa vyuo mbalimbali kumejitokeza changamoto na watu kutoka katika mfumo rasmi uliopangwa na kujiwekea mifumo binafsi ambayo imeingiza hata wanafunzi wa kidato cha nne ambao hawana sifa kuingia vyuo vikuu.

“Jambo hilo limesababisha kuwepo kwa msuguano, haiwezekani mtu afeli kidato cha nne bila kuwa na cheti kingine chochote anaingizwa katika kozi hiyo halafu anaingizwa chuo kikuu, sisi hatujarasimisha mfumo huo wa ‘foundation course’ na hatuna vipimo vyake,” alieleza.

Alisema kwa kawaida mwanafunzi mwenye diploma inayotambulika wamewekewa usawa wa alama fulani na kidato cha sita hivyo wanakuwa na sifa ya kuingia vyuo, lakini siyo waliofeli hivyo wanatakiwa kufanya utafiti zaidi katika kozi hiyo.

“Haiwezekani kila mtu akajianzishia mfumo wake tu, tulifikia eneo ambalo si zuri kama nchi na sasa tutaimarisha ubora…ukifeli kidato cha nne unatakiwa kwenda kusoma na kupata cheti kwenye mtaala unaotambulika na ukaenda diploma na unapofaulu unaweza kwenda chuo kikuu,” aliongeza.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Simon Msanjila alisema suala la ‘Foundation course’ limelenga kumuandaa mtu mwenye sifa ambaye amekuwa nje ya mfumo kwa muda mrefu ili kuingia chuo kikuu, lakini walichokuwa wakikifanya wengi ni kuwachukua waliofeli kidato cha nne na sita na kuwaingiza katika kozi hiyo na hatimaye kuwaingiza chuo kikuu.

Dadapoa 25 Mbaroni Kwa Kujiuza Moshi

$
0
0
Watu 66 wakiwamo wanawake 25 wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya kuuza miili maarufu kama dadapoa katika maeneo mbalimbali ya mjini Moshi, wanashikiliwa na polisi.

Licha ya kuwashikilia wanawake hao, polisi wamewakamata wafanyabiashara saba wanaojihusisha na biashara za dawa za kulevya na watumiaji.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita amesema watu hao walikamatwa Novemba 26 saa mbili usiku kwenye maeneo ya katikati ya mji katika operesheni ya kutokomeza biashara hizo haramu.

“Tukiwa na Diwani wa Mawenzi, Hawa Mushi tulishirikiana kuwakamata wahalifu mbalimbali katika mji wetu maana nyakati za usiku kuna mambo yanafanyika ambayo tusipoweza kuyakabili  mapema yanaweza kuleta madhara baadaye,” amesema Moita.

 Moita amesema baadhi ya wafanyabiashara wadogo ndiyo chanzo cha kuuza dawa za kulevya na huwaficha wanawake wanaofanya biashara ya miili yao usiku.

“Tumewakamata wanawake wanauza miili yao 25, wafanyabiashara wanaowalinda wanawake hao na kuuza dawa za kulevya saba na walikutwa wakitumia dawa hizo nao wako saba,” amesema Moita.

Pata Kifaa Chenye Uwezo 99% ya Kuongeza Ukubwa wa Uume wako Bila Madhara

$
0
0

Handsome up ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa uhakika na bila madhara. Inapatikana kwa @170,000/=tu. PIA kuna Gely ya kupaka @ 120,000/= na Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa @120,000/=.
Wasiliana nasi kwa no (+ 255 ) 0767447444 au 0714335378.

Follow us on Instagram:
@Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr 

MAUNO ya Mwendokasi Ndio Yanayoniweka Mjini – Gigy Money

$
0
0
Video queen ambaye haishiwi vituko, Gigy Money amefunguka kwa kusema kuwa mauno yake ya mwendokasi ndio kitu ambacho kinawafanya wasanii wengi wamtafute kwa ajili ya kufanya naye kazi.

Mrembo huyo ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM, amesema kuwa video queen ni kazi ambayo inalipa tofauti na watu wanavyofikia.

“Unajua kazi yoyote ukiiheshimu ni rahisi nayo ikakuheshimu,” alisema Gigy Money. “Mimi hii kazi naiheshimu ndio maana imeniweka mpaka hapa nilipo. Sasa hivi mimi ni mtangazaji wa kituo kikubwa cha redio, kwa hiyo mimi naweza kuwaambia watu wanatakiwa kuiheshimu hii kazi kama kazi nyingine,”

Aliongeza,”Kusema kweli sasa hivi mimi ni moja kati ya video queen ambao tunafanya kazi nyingi lakini haya yote yanatokana na nikipata kazi naifanya isavyo, napiga mauno ya mwendokasi mpaka mtu labda alipanga kunipa scene moja anajikuta nanipa mbili au tatu,”

VIDEO: RC Makonda Alivyoamuru Wenyeviti Watano Kuchukuliwa na Polisi Katikati ya Mkutano

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda November 28 2016 alimaliza ziara ya Dar Mpya ambayo alizunguka maeneo tofauti ya jiji la Dar es salaam kwa siku 10 kusikiliza na kutoa majibu ya kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Akiwa kwenye mkutano wa  mwisho Mwabepande suala kubwa lililojitokeza ni kuhusu utapeli wa viwanja, wananchi walilalamikia kutapeliwa viwanja wakati walivyouziwa kulikuwa na baraka zote kutoka kwa wenyeviti wa mtaa. Baada ya tuhuma hizo kutolewa wananchi waliwataja wenyeviti walioshiriki kuuza viwanja kitapeli na RC Makonda akaamuru wachukuliwe na polisi  kwa hatua zaidi. Unaweza kuangalia video hii hapa chini.

UGONJWA Unaoambukiza Kama UKIMWI, Kati ya Watu 100, Nane Wanao

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili inatarajia kuanza kufanya uchunguzi wa Virusi vya homa ya Ini (Hepatitis B) na kutoa tiba bure kwa wagonjwa watakaobainaika kuwa nao kwa kutumia dawa ya Tenefovir katika kipindi cha miaka mitano ijayo kuanzia tarehe 1 December 2016.

Tanzania itakua nchi ya pili ukanda wa Afrika Mashariki kuanza kutoka huduma ya uchunguzi na matatibu ya ugonjwa wa Ini baada ya Rwanda ambayo imeshaanza udhibiti wa tiba ya ugonjw ahuo.

Kwa mujibu wa Dr. John Lwegasha ambaye ni Daktari bingwa wa magonjwa ya Ini na Matumbo kutoka Hospitali ya Muhimbili amesema nchini Tanzania kati ya watu 100 watu nane wameambukizwa Virusi vya homa ya Ini.

Taarifa kamili ipo hapa. Bonyeza play kutazama

TAARIFA Kutoka Ikulu: Rais Magufuli na Rais Lungu Wakubaliana Kufufua Miradi ya TAZARA na TAZAMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu  tarehe 28 Novemba, 2016 wamekubaliana kuchukua hatua za haraka na madhubuti kuboresha utendaji kazi wa reli ya TAZARA na bomba la mafuta la TAZAMA ili miradi hiyo miwili ilete manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi Tanzania na Zambia.

Marais hao wametangaza kuchukua hatua hizo Ikulu Jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika muda mfupi baada viongozi hao kufanya mazungumzo rasmi ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku 3 ya Rais Lungu iliyoanza jana hapa nchini kwa mwaliko wa Rais Magufuli.

Katika mkutano huo uliorushwa moja kwa moja na vyombo vya habari vya redio, tevisheni na mitandao ya kijamii Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na kuzorota kwa utendaji kazi wa reli ya TAZARA ambao umeshuka kutoka usafirishaji wa tani 5,000,000 za mizigo mwaka 1976 hadi kufikia usafirishaji wa tani 128,000 kwa mwaka hivi sasa, huku utendaji kazi wa bomba la mafuta la TAZAMA nao ukiporomoka kutoka uwezo wake wa kusafirisha tani 1,100,000 za mafuta hadi kufikia tani 600,000 kwa mwaka hivi sasa.

Marais hao wamekubaliana kuwakutanisha wanasheria wakuu wa Serikali za nchi zote mbili haraka iwezekanavyo kwa lengo la kufanya marekebisho ya kisheria kwa maeneo yote yaliyoonesha kuwa kikwazo na pia kupanga upya menejimenti za TAZARA na TAZAMA ili ziweze kuendesha vyombo hivyo kibiashara na kwa manufaa yaliyokusudiwa wakati vilipoanzishwa na Waasisi wa mataifa haya mawili yaani Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Mhe. Dkt. Kenneth Kaunda wa Zambia.

“Tumekubaliana ni lazima tubadilike na tubadilike kwa haraka, vikwazo vinavyotokana na sheria viondolewe na manejimenti ya TAZARA ipangwe upya, na mimi nataka kusema kwa uwazi, ukiwauliza TAZARA watakwambia tatizo ni mtaji lakini ukweli ni kwamba tatizo ni menejimenti, ingekuwa tatizo ni mtaji, ule uliokuwepo mwaka 1976 umekwenda wapi? maana sasa hivi TAZARA ina vichwa 14 tu vya kuendeshea treni na ina upungufu mkubwa wa mabehewa” amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Rais Lungu amesisitiza kuwa katika kuimarisha TAZARA wamekubaliana kuweka pembeni siasa na kuirejesha TAZARA katika hali yake ya kibiashara kwa kuhakikisha inafanya kazi ya kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo iendayo kusini mwa Tanzania na nchini Zambia.

Mhe. Lungu ameongeza kuwa pamoja na kuimarisha bomba la mafuta la TAZAMA, Zambia inatarajia kunufaika na gesi iliyogunduliwa kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania na pia inajipanga kutumia vizuri fursa ya kufunguka kwa ukanda wa maendeleo wa Mtwara (Mtwara Corridor) na mpango wa ujenzi wa reli ya kati ambapo ukanda wa Kaskazini mwa Zambia una mawasiliano ya karibu na bonde la ziwa Tanganyika.

“Mhe. Rais Magufuli una muda wa kutosha katika uongozi wako na mimi nina muda wa kutosha pia, kwa hiyo kwa pamoja tunaweza kuimarisha maeneo yote ya kuinua biashara na uwekezaji kati ya nchi zetu mbili ikiwemo kuimarisha TAZARA na TAZAMA kwa manufaa ya wananchi wetu” amesisitiza Rais Lungu.

Kuhusu hali ya biashara kati ya Tanzania na Zambia, Rais Magufuli amesema Zambia ni nchi inayoongoza kwa kupitisha mizigo mingi katika bandari ya Dar es Salaam ambapo katika mwaka 2015 mizigo yenye uzito wa tani Milioni 1.9 ilipitishwa na kwamba kumekuwa na ongezeko la biashara kati ya Zambia na Tanzania kutoka Shilingi Bilioni 89.2 mwaka 2010 hadi kufikia Shilingi Bilioni 152.2 mwaka 2015.

Dkt. Magufuli amemhakikishia Rais Lungu kuwa Tanzania inaendelea kuboresha mazingira ya kufanyia biashara ikiwa ni pamoja na kuboresha zaidi bandari ya Dar es Salaam, kupunguza vizuizi vya barabarani kutoka 8 hadi 4, kushughulikia tatizo la vizuizi vya polisi na kujenga Kituo cha Pamoja cha Utoaji wa Huduma za Mpakani (One Stop Border Post)

“Tunataka mambo haya yote yaende haraka, wataalamu wetu ni lazima waharakishe kurekebisha vikwazo vyote vilivyokuwa vinatuchelewa, tufanye kazi pamoja kwa manufaa ya wananchi” amesisitiza Rais Magufuli.

Jioni ya leo Rais Edgar Chagwa Lungu anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam na kesho Rais Lungu anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku 3 hapa nchini.

VODACOM Tanzania Yapeleka Maombi ya Kujiunga na Soko la Hisa (DSE)

$
0
0
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza dhamira yake ya kuuza hisa kwa umma itakayofuatiwa na   kujiunga kwenye   Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya Elektroniki na Mawasiliano ya Posta (EPOCA) na sheria ya Fedha ya mwaka 2016 ambayo inaelekeza makampuni ya simu kumilikisha asilimia 25 ya hisa zake kwa wananchi kwa kujiunga na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Akizungumzia hatua hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Bwana Ian Ferrao alisema “Tunayo furaha kutangaza kuwa tumeanza rasmi mchakato wa kuuza hisa kwa umma kwa mujibu wa matakwa ya sheria na tumewasilisha maombi na utaratibu mzima utakaotumika kuuza hisa zetu na ratiba yetu nzima kuhusiana mchakato huu kwenye Mamlaka ya Usimamiaji wa Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Hisa (DSE).   Hatua hii ni kubwa na inadhihirisha kuwa Vodacom ipo mstari wa mbele katika kutekeleza agizo la kuuza hisa zake kwa umma  na inadhihirisha jinsi ilivyojipanga  kuendelea kuboresha na kukuza sekta ya mawasiliano nchini Tanzania katika siku za usoni”.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,(kulia) akimkabidhi hati ya maombi ya kujiunga na soko la hisa la Dar es Salaam,(DSE)  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama(wapili kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyike mwishoni mwa wiki katika ofisi za CMSA jijini Dar es Saalaam,Kushoto ni Meneja Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima.

Uuzaji wa hisa kwa umma  na kujiunga na Soko la Hisa kunapitia  hatua mbalimbali za  kupata vibali kutoka taasisi za serikali zenye mamlaka ya kupitia maombi na kutoa  vibali vya utekelezaji wake.Ferrao aliendelea kueleza “Tunaamini uuzaji wa hisa zetu kwa umma utazidi kukuza shughuli za Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE),kunufaisha watanzania kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla. Kampuni yetu haitajulikana kwa jina la mwanzo la Vodacom Tanzania Limited bali imekuwa na jina la Vodacom Tanzania Public Limited Company (Plc) ikiwa ni hatua ya awali ya kujiandaa kuingia sokoni. Tunawahakikishia kuwa mchakato wa kuingia kwenye hatua hii umeanza vizuri kwa mafanikio na tunaendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini kuhakikisha tunatimiza dhamira ya kuanza  kuuza hisa kwa wananchi yenye dira ya kuleta manufaa kwa wote.”

Ferrao alitoa msisitizo kuwa Vodacom inalo jukumu kubwa kuhakikisha hatua hii inaleta manufaa kwa pande zote zinatazohusika kuanzia  wanunuaji wa hisa, kuendelea kuwekeza , kuendelea kuleta mapinduzi ya ubunifu wa kiteknolojia na kuimarisha ubora wa huduma za kampuni kwa wateja wake “Tutaendelea kutoa mchango mkubwa wa ufanikishaji wa sera ya nchi ya miaka 5 ya kukuza sekta ya mawasiliano.Tutaendelea pia kuwaletea taarifa mbalimbali kuhusiana na mchakato wa kuuza hisa kwa umma unavyoendelea”Alisema Ferrao.

Mkurugenzi wa  Ushauri wa kutoka huduma za Orbit Securities Company Ltd. Gerase Kamugisha(kushoto)Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa DSE,Moremi Marwa, Mkuu wa masuala ya kifedha  wa Orbit Securities Company Ltd, Godfrey Gabriel, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia,wakionyesha hati za maombi ya kuijiunga na soko la hisa la Dar es Salaam,(DSE) mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,(watatu kushoto) akimkabidhi hati ya maombi ya kuijiunga na soko la hisa la Dar es Salaam,(DSE)  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana(CMSA) Nicodemus Mkama wapili (kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyike mwishoni mwa wiki  katika ofisi za CMSA jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima , wanaoshuhudia kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa  Ushauri wa kutoka huduma za Orbit Securities Company Ltd. Gerase Kamugisha, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (wapili kulia) na Mkuu wa fedha  wa kampuni ya Orbit Securities Company Ltd, Godfrey Gabriel (watatu kutoka kulia)

Maprofesa Wampinga Ndalichako

$
0
0

WASOMI, wadau wa elimu na wananchi wa kawaida wamekosoa tamko la Waziri  wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, wakisema kwamba halijafanyiwa utafiti na halitekelezeki kisheria.

Mwishoni mwa wiki, akiwa kwenye mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Ndalichako alisema kuanzia mwakani mwanafunzi yeyote hatajiunga na masomo ya Shahada bila kupitia kidato cha sita.

Alisema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.

Wakizungumzia tamko hilo kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali nchini, baadhi ya wasomi  walisema kabla ya waziri kuanza kutoa amri na matamko, alitakiwa kufanya utafiti kujiridhisha juu ya agizo lake hilo.

“Profesa Ndalichako hajasema ametoa wapi ujasiri wa tamko lake, ni kwa utafiti upi aliofanya yeye au hata kukasimu taasisi kwa niaba yake ili ifanye utafiti na kuja na majibu kuwa kidato cha sita ndicho kiwango bora cha kumpitisha mtu kusoma shahada ya kwanza?

“Binafsi naona haya ni matamko ya kisiasa yasiyoweza kutekelezwa kisheria, arekebishe sheria kwanza ndio aje kutoa tamko la kurekebisha mfumo wa elimu, vinginevyo anaweza kuharibu kuliko waliomtangulia,” alisema mkuu wa chuo kikuu maarufu mkoani Arusha ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.

Naye Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Tawi la Makumira, Mchungaji Profesa Josef Parsalao, alisema pamoja na lengo zuri la kurekebisha mfumo wa elimu, badala ya kuanza na amri na matamko, Serikali ilitakiwa kurekebisha kasoro zilizopo hatua kwa hatua.

“Sijui yeye Ndalichako alipitia hatua zipi za elimu, lakini upo ushahidi wa kuwapo kwa wasomi wengi wakiwamo wale wanaofundisha vyuo mbalimbali nchini, kupitia ngazi ya chini kabisa ya cheti na sasa ni maprofesa na walifundisha hawa wanaobeza ngazi hizo.

“Wapo majaji ambao walianza kazi ya ukarani mahakamani, wakajiendeleza kwa kusoma Chuo cha Mahakama Lushoto ngazi ya cheti, sasa ni madaktari na maprofesa wa sheria tunawategemea,” alisema Profesa Parsalao.

BANA

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, yeye alisema haamini kama alichosema Waziri Ndalichako ni tamko na uamuzi wa Serikali, kwani suala hilo haliko kwenye sera ya elimu na kuonya kuwa alifute haraka kwani hiyo si njia sahihi ya kuboresha elimu nchini.

Dk. Bana alikwenda mbali zaidi kwa kutoa mfano wa jinsi yeye alivyosoma kupitia mfumo huo unaopingwa na Ndalichako hadi hapo alipofikia.

“Kama kachukua uamuzi huo, nafikiri amekurupuka, kama anafikiria kidato cha sita ndiyo njia pekee, ameshauriwa vibaya na huo uamuzi aufute haraka sana na ni kinyume na utaratibu wa elimu kote duniani… utakuwa ni uamuzi wa dhambi ya asili na dhambi ya ubaguzi. Kama anataka njia ya kuboresha elimu aje tumfundishe.

“Mimi binafsi sikupitia kidato cha sita na kuna maprofesa zaidi ya 20 au 40 ninaowafahamu, yupo Profesa Baregu (Mwesiga Baregu) hakusoma kidato cha sita, kuna Profesa Mathew Luhanga ambaye alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa miaka 14, yupo pia Profesa Cuthbert Kimambo ambaye alikuwa Mkuu wa Taaluma UDSM na wengine wengi, ni watu wanaoheshimika kote duniani,” alisema.

PROFESA BAREGU

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Profesa Mwesiga Baregu, hakutofautiana na Dk. Bana. Yeye alisema mfumo uliopo unakubalika duniani kote na ndio ulioleta msemo wa ‘elimu haina mwisho’.

“Kauli ya waziri imeonyesha umuhimu wa kuwa na tume ya kitaifa ya kushughulikia suala la elimu, kwa sababu kweli kuna tatizo la ubora wa elimu yetu na halipaswi kunyamaziwa, lakini hii si njia sahihi ya kulitatua.

“Sijamwelewa waziri kwanini ameona diploma kwenda chuo kikuu ndiyo tatizo na kusema kuwa watu wote wana haki ya kujengewa mazingira ya kujiendeleza kielimu,” alisema Profesa Baregu.

PROFESA MPANGALA

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha mkoani Iringa (RUCO), Profesa Gaudence Mpangala, alisema anapinga uamuzi huo wa Profesa Ndachako kwani utawanyima watu uhuru wa kujiendeleza.

Profesa Mpangala naye aliwataja baadhi ya maprofesa anaowafahamu ambao hawakupitia kidato cha sita na akasema wamekuwa msaada mkubwa kwa taifa.

“Profesa Kimambo alikuwa mwalimu wangu wa Kiswahili, yeye alikuwa na elimu ya ualimu ‘Grade’ C wa shule ya msingi lakini amejiendeleza hadi amekuwa Profesa yupo pia Profesa Ndunguru na wengine wengi na waliopitia mfumo wa Cheti-Stashahada wanakuwa na uzoefu mkubwa kuliko wa kidato cha sita na wanafanya vizuri wakifika chuo kikuu,” alisema Profesa Mpangala.

TAMONGSCO

Akizungumzia kauli hiyo ya Profesa Ndalichako, Katibu Mkuu wa Vyuo na Shule Binafsi Tanzania, Benjamini Nkonya, alisema hawaelewi waziri huyo kutoa tangazo kama hilo ni kwa sababu watu wengi wamekuwa watumishi bora sana na wengi hawajasoma kidato cha sita au vinginevyo.

“Wito wetu kwa Serikali ikamilishe mchakato kwa kupeleka rasimu ya sheria mpya ya elimu bungeni, ili pawepo na Baraza la Taifa la Elimu ambalo litakuwa na wawakilishi kutoka sekta ya umma, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na sekta binafsi kama TAMONGSCO, ambayo itaandaa nyaraka (regulations) zote kabla hazijawekewa sahihi na kamishna wa elimu,” alisema Nkonya.

PROFESA MLAMA

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Penina Mlama, yeye alikubaliana na mawazo ya Waziri Ndalichako, akisema mfumo huo ni wa zamani na uliruhusiwa ili kutoa fursa kwa watu kusoma kwa kuwa nchi ilikuwa na wasomi wachache.

“Sasa hivi kuna wanafunzi wengi wa kidato cha sita na fursa nyingi za kusoma kidato cha tano na sita zipo, tofauti na kipindi cha miaka ya nyuma, hakuna ulazima sana wa watu kutegemea njia yingine wakati wanaweza kusoma kidato cha sita na kuwa sawa na wengine darasani,” alisema.

LALTAIKA

Kaimu Mkuu wa Idara ya Ubunifu, Usimamizi wa Teknolojia na Ujasiriamali katika Taasisi ya Sayansi ya Nelson Mandela, Dk. Amani Laltaika, alipongeza hatua ya Profesa Ndalichako, huku akisema amegundua tatizo katika elimu na amethubutu kuchukua hatua ya kurekebisha kuliko waliomtangulia ambao hawakuchukua hatua yoyote.

“Sifa ya kwanza ya kiongozi ni ubunifu na kutatua matatizo yaliyopo, nampongeza waziri kwa kugundua upungufu katika elimu yetu, kwa sababu walikuwapo mawaziri wengi katika nafasi aliyopo sasa, lakini hawakugundua,” alisema Dk. Laltaika.

SIFA ZA TCU KUJIUNGA NA VYUO

Mwezi Juni mwaka huu, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), ilitangaza utaratibu mpya kwa watahiniwa wa mwaka mpya wa masomo wa 2016 na 2017 wanaochukua shahada.

Utaratibu huo mpya ulikuja baada ya miezi miwili tangu kutumbuliwa kwa watendaji wa tume hiyo kutokana na kudahili wanafunzi wasio na sifa na kusababisha kupewa mikopo na Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Pamoja na sifa hizo ambazo ziliwahusu waliomaliza kidato cha sita, pia sifa hizo zilieleza kuwa wale watakaodahiliwa kujiunga na vyuo ni pamoja na watakaokuwa na utambulisho wa sifa za kielimu za kidato cha nne kuanzia alama nne ambazo ni D na kupanda juu katika mchanganuo wa alama za ufaulu wa B+, ikiwa A=75-100, B+=65-74, B=50-64, C=40-49, D=35-39 na F=0-38.

Sifa nyingine zinazotajwa ni wenye vyeti vya NVA daraja la tatu, wenye ufaulu si chini ya alama nne au sifa nyingine zinazokaribiana na hizo, ikiwa ni pamoja na zinazotambuliwa na Baraza ka Taifa la Mitihani (NECTA) na Elimu ya Mafunzo ya Ufundi (VETA).

Watahiniwa hao watatakiwa kuwa na angalau GPA ya 3.5 kwa stashahada ‘NTA’ daraja la sita au wastani wa B kwa cheti cha ufundi ‘FTC’ katika mchanganuo wa alama A=5, B=4, C=3 na D=2 au wastani wa daraja la B+ kwa wenye stashahada za ualimu au wastani wa daraja B+ kwa kitengo cha afya kama tabibu wa magonjwa ya binadamu na nyingine au cheti na stashahada nyinginezo.

Sifa nyingine zinazoangaliwa katika udahili huo ni pamoja na kuwa na ufaulu wa daraja la pili kwa wenye Stashahada zisizokuwa za NTA.

Imeandaliwa na Abraham Gwandu (Arusha), Jonas Mushi na Mauli Muyenjwa (Dar)

Source: Mtanzania

HASHIM Rungwe: Kinachooneshwa na Rais Magufuli ni Tabia zake na si Utendaji Wake

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Umma (Chaumma), Hashim Rungwe amesema kinachoonyeshwa na Rais John Magufuli katika kazi zake ni tabia zake binafsi, badala ya utendaji.

Rungwe, ambaye aligombea urais mwaka jana na kushika nafasi ya tano akiwa amepata asilimia 0.32 ya kura, alisema hayo alipofanya mahojiano na gazeti hili ofisini kwake jijini.

Rungwe alikuwa akizungumzia mwaka mmoja wa Magufuli, akisema kinachofanywa na Rais pamoja na wateule wake ni kutaka kuonyesha wanafanya vizuri kuliko watangulizi wao.

“Nasikia kelele na ukosoaji wa kila kilichofanywa kabla ya utawala huu. Ni hulka ya binadamu kudhani kuwa kila wazo lake ni bora kuliko wengine na atapenda kulitekeleza, hata ikimaanisha kwenda kinyume na taratibu zilizopo,” alisema Rungwe.

Pamoja na mtazamo huo, Rungwe alikiri kuwapo kwa maendeleo yaliyotokana na juhudi binafsi kwa kila mwananchi, huku akikosoa mambo mengi yanayofanywa na ama Rais mwenyewe au wasaidizi wake.

Alikumbusha kauli aliyoitoa Rais wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kisiwani Unguja kushukuru wananchi kwa kumchagua kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita kuhusu kitendo cha katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kukataa kumpa mkono Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein kwenye mazishi ya aliyekua Rais wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, Abood Jumbe.

Siku hiyo, Rais Magufuli alisema: “Mtu mmekutana kwenye msiba, mahali kwenye majonzi, mnamsindikiza marehemu. Kwa unyenyekevu wako Dk Shein ukatoa mkono wako kumsalimia mtu fulani. Huyu mtu akakatalia mikono yake na bado asubuhi yake ukasaini fomu zake za kwenda kutibiwa nje ya nchi.

“Haya ni mapenzi makubwa sana. Amekataa mkono wako. Huyohuyo akiugua unampeleka hospitali. Akitaka kusafiri nje, unasaini na unampa na fedha na posho za kwenda nje. Mimi nisingeweza.”

Pia Rungwe alikumbusha pia tukio lililojiri wakati wa uzinduzi wa Daraja la Nyerere ambako Rais aliwauliza wananchi kama amtumbue au asimtumbue aliyekuwa mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, marehemu Wilson Kabwe.

“Hizi ni tabia binafsi. Hatuhitaji kuzifahamu. Tunataka uongozi kwa kutumia sheria tulizonazo. Rais hafahamu tofauti hiyo. Urais ni tofauti na tabia zake ambazo anaweza akazifanya akiwa na familia yake au watu wake wa karibu,” alisema wakili huyo wa Mahakama Kuu.

Alisema kauli ya Rais kwamba angekuwa yeye asingesaini kuidhinisha malipo ya safari ya matibabu ya Maalim Seif baada ya kukataliwa kutoa mkono wa salamu, haina maana kwa kuwa hasira humpata mtu yeyote na si vyema kuzionyesha mbele ya watu.

“Rais kuonyesha hasira kiasi hicho si vizuri. Maalim alikuwa kiongozi wa nchi hii na anayo haki kwa kila analostahili, si mpaka amfurahishe mtu fulani,” alisema Rungwe na kufafanua kuwa hali hiyo ya kutaka kufurahisha ndiyo inayosababisha kila mtu ajaribu kumfurahisha Rais hata kwa kuvunja haki za wengine.

Alisema ipo mifano hai ya viongozi waliokuwa na nia njema ya kuwasaidia wananchi wao, lakini wakashindwa kufanikisha malengo yao.

“Rais Magufuli anaelekea huko hivyo washauri wake wachukue hatua mapema kabla mambo hayajaharibika,” alisema Rungwe.

Mwenyekiti huyo wa chama ambacho hakijapata uwakilishi bungeni, alisema hata Rais wa Awamu ya Kwanza, Mwalimu Julius Nyerere alikuwa na nia njema ya kuijenga Tanzania ya ujamaa na kujitegemea hadi akaasisi Azimio la Arusha, lakini hakufanikisha ndoto yake.

Alitaja mfano mwingine kuwa ni Zimbabwe ambako uchumi unayumba kutokana na sera zinazotekelezwa na Rais Robert Mugabe. Alisema alipoikuta nchi hiyo ni tofauti na alipoifikisha.

“Nilienda Zimbabwe, hali ni tofauti sana. Uchumi umeharibika kutokana na msimamo wa Rais,” alisema.

Miongoni mwa masuala ya kiuchumi yaliyobadilisha uchumi wa taifa hilo, kwa mujibu wa Rungwe, ni kutaifisha mashamba makubwa ya walowezi na kuyagawa kwa wakulima wazawa jambo, lililolalamikiwa na wengi.

Kutokana na mifano hiyo, Rungwe alimtaka Rais Magufuli kukumbuka mahitaji ya wananchi wote badala ya kuelekeza nguvu nyingi kupambana na kundi dogo la wezi kwenye jamii.

Alisema licha ya uzuri wa kupambana na wizi, rushwa na matumizi mabaya ya viongozi, wananchi wengi wana njaa ambayo haiwezi kumalizika kama hakutakuwa na chakula mezani kwao.

“Wezi na wala rushwa wameandikwa hata kwenye vitabu vitakatifu. Lazima wawepo kwenye jamii yoyote, lakini huwezi kuwatafuta wezi 100 na kuathiri maisha ya zaidi ya Watanzania milioni 50,” alisema.

“Mishahara haijaongezeka, pensheni hazilipwi kwa wakati lakini wateule wote wa Rais wanaishi maisha mazuri. Wamebadilika tangu walipoteuliwa. Wengine walikuwa wanafunzi, lakini sasa wanaongea lugha tofauti. Wananchi wanahitaji chakula mezani si vita visivyokuwa na mwisho,” alisema.

Utumbuaji
Kuhusu utumbuaji, Rungwe alisema umekuwa ukifanywa kinyume na taratibu, jambo alilosema linaongeza chuki miongoni mwa watumishi na Serikali yao.

“Utumbuaji unatengeneza chuki baina ya watumishi wa umma na mwisho wa siku Rais awe tayari kuwaomba radhi watumishi anaowatumbua,” alisema.

Alielekeza lawama kwa washauri wa Rais kwamba hawatekelezi wajibu wao kama inavyotakiwa ndiyo maana anaweza kuongea vitu ambavyo haviendani na hadhi ya ofisi anayoihudumu.

“Rais ni kama baba wa familia. Hawezi kumdhalilisha mbele ya kadamnasi mwanaye aliyekosea. Wanachofanyiwa watumishi na wafanyabiashara si sahihi. Ndiyo maana hawajafikishwa mahakamani. Wapo watumishi wanaoendelea kulipwa mishahara na hawafanyi kazi,” alisema.

Katiba Mpya
Alisema Rais Magufuli hajaonyesha nia ya kukamilisha mchakato wa kuipata Katiba Mpya ambao ulianza wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne na ukasitishwa kupisha Uchaguzi Mkuu.

“Rais hatakiwi kusitisha mchakato huo ambao ulianzishwa kwa baraka za chama chake na Watanzania wote wamekubali fedha zao zitumike kufanikisha hilo. Katiba na sheria ndizo zilizompa nafasi ya kuongoza nchi na si kitu kingine,” alisema.

Ila, alikosoa utaratibu uliotumiwa na Bunge Maaalum la Katiba (BMK) kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa kupiga kura, akisema haikuwa sahihi.

“Tulijaa wanasiasa. Maamuzi yetu yalitokana na itikadi zetu. Katiba si suala la chama. Marekebisho yafanywe kuanzia pale,” alishauri.

Chanzo: Mwananchi

NAFASI za Kazi Mohammed Enterprises na Nyingine Nyingi Zilizotangwa Katika Magazeti Leo

$
0
0

MBUNGE wa Ukonga Mh. Mwita Waitara Akamatwa na Kushikiliwa na Polisi kituo cha Polisi Chang'ombe

$
0
0
Mbunge wa Ukonga Mh. Mwita Waitara akamatwa na kushikiliwa na Polisi kituo cha Polisi Chang'ombe, Temeke.

Mh. Waitara amekamatwa muda mfupi uliopita katika eneo la UVIKIUTA alipokuwa amefuatilia mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya wananchi wa eneo hilo na kigogo mmoja wa serikali anayetaka kupora ardhi hiyo na kuwahamisha wananchi kwa nguvu.

Leo asubuhi wananchi wa UVIKIUTA wamekumbwa na bomoa bomoa iliyokuwa inasimamiwa na askari wa jeshi la Polisi kutoka Temeke.

Mh Waitara ambaye pia ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Kivule linakopatikana eneo hilo la UVIKIUTA ambalo lipo mpakani mwa wilaya za Ilala na Temeke (Kivule-Ilala na Mbande-Temeke), alifika eneo hilo kufuatilia bomoa bomoa hiyo ndipo Polisi wakamkamata na kumpeleka Chang'ombe.

Picha: Alikiba Asherehekea Siku ya Kuzaliwa Kwa Kutembelea Mbugani

$
0
0
 Leo ni siku ya kuzaliwa ya Alikiba. Na kusherehekea siku hiyo muhimu kwake, muimbaji huyo mahiri alitumia private jet kwenda na timu yake ya Rockstar4000 akiwemo Barakah Da Prince kwenda mbugani. Chini ni picha alizoweka kwenye Instagram.

KHADIJA Yusuph Amtaka Leila Rashid Aachane na Mambo ya Kidunia na Kumfuata Mumewe Mzee Yusuph

$
0
0
Msanii wa taarabu nchini Khadija Yusuph amemsihi wifi yake Leila Rashid kuachana na maswala ya muziki na kumfuata mume wake Mzee Yusuph kwa kuwa tayari mume wake kashaenda hija na ni dhambi kuacha kumsikiliza mume wake.

Akiongea ndani ya eNewz Khadija amesema ni vizuri Leila kumfuata mume wake kwa kuwa haoni sababu ya yeye kuendelea kuwa na kundi la Jahazi wakati mume wake Mzee Yusuph ameamua kumrudia Mungu na kuachana na maswala ya muziki.

Hata hivyo Khadija Yusuph amewaambia mashabiki waendelee kusubiria maamuzi ya Mzee Yusuph mwenyewe juu ya maamuzi ya mke wake kuendelea na muziki wakati yeye kaamua kumrudia Mungu na kuachana kabisa na mambo ya dunia.

TAZAMA Video ya Wimbo Mpya wa Navykenzo Hapa Waliomshirikisha Wildad-Feel Good

$
0
0
Wakijiandaa kuachia album yao ya kwanza ya kimataifa, Above In A Minute, Navy Kenzo wameachia videp ya ngoma yao mpya ‘Feel Good’ wakimshirikisha msanii wa The Industry, Wildad. Video imeongozwa na Justin Campos.
Viewing all 104706 articles
Browse latest View live


Latest Images