Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

DULLY Sykes Awa Mkali Baada ya Kuulizwa Kuhusu Bifu la Ommy Dimpoz na Diamond

$
0
0
Msanii Dully sykes alimind watangazaji waliokuwa wanamhoji baada ya kumuuliza kuhusu bifu la diamond na ommy dimpoz
Dully amesema hawezi kujibu hilo sababu huo ni u-shilawadu na yeye hapendi na ukizingatia wale ni 'wadogo zake' VIDEO:

YOUNG Dee: Tunda ni Mpenzi Wangu na Hatujawahi Kuachana

$
0
0
Msanii Young Dee amedai Tunda ni mpenzi wake na hawajawahi kuachana, pia amesema anampga ushauri wa kumbadilisha kwenye maisha ndio maana anapagawa naye sana
MTAZAME HAPA:

KUMNYIMA Lema Dhamana Hakutufanyi Tuvunjike Moyo... Bali Ndio Tumepata Ujasiri wa Kujiandaa zaidi

$
0
0
Kumnyima Lema Dhamana hakutufanyi tuvunjike Moyo... Bali ndiyo tumepata ujasiri wa kujiandaa zaidi na kutuambia Mabadiliko ya kisiasa tunayotaka lazima tuyalipie... Lema yupo Strong kuliko Jana,Lema siyo Mwepesi kama mnavyodhana inawezakuwa..
Mawakili wetu tunawapongeza kazi kubwa na ngumu ya kupambana kwenye vyombo sitahiki, Ninauhakika Mbele ya Mawakili wetu Mapambano kamwe hayatakoma.. Hii inaitwa Struggle of power... Comrade Wakili Msomi Peter Kibatala na Mawakili wengine Mnapigania haki Imani yetu bado ipo kwenu.. Neema Tarimo Lema Najua upo Strong hujawahi kutetereka Shemeji wangu wa nguvu...We shall overcome..NEVER SAY NEVER

By Henry Kilewo

VIDEO: Mtoto wa mh. Lema aongea baada ya baba yake kukosa dhamana

$
0
0
Godbless Lema Mtoto wa kwanza wa kiume wa Godbles Lema akiongea na wanahabari nje ya Mahakani ya Hakim Mkazi Jijini Arusha baada ya Baba yake kufikishwa Mahakamani hapo kwenye muendelezo ya kesi huku akikosa dhaman na kurudishwa Gereza Kisongo, kesi imehairihswa mpaka 2/2/2017

VIDEO: Magoli ya Samatta aliyoifungia KRC Genk vs Waasland-Beveren, Nov 30 2016

$
0
0
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayeichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta usiku wa November 30 2016 ameingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kuiongoza timu yake ya Genk kupata ushindi dhidi ya Waasland-Beveren.

Samatta aliifungia KRC Genk magoli mawili katika ushindi wa goli 3-1, Samatta akifunga magoli hayo dakika ya 15 na 42 na baadae mnigeria Wilfred Ndindi akapachika goli la tatu dakika ya 80.

SAKATA la Taasisi ya Mama Salma Kikwete Kukwepa Kodi

$
0
0

Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) imekanusha taarifa zilizochapishwa na gazeti moja linalochapishwa kila wiki kwa lugha ya Kiswahili kuwa Mwenyekiti wake, Salma Kikwete ana mzigo mkubwa bandarini ambao haujalipiwa ushuru na kodi.

Taarifa ya Wama iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na kusainiwa na Katibu Mtendaji wake Daudi Nassib, ilisema taarifa hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo gazeti hilo lilichapisha habari hiyo iliyokuwa na kichwa cha habari “Mali za Salma Kikwete kuuzwa kwa mnada?” katika toleo lake namba 486 la Novemba 30, mwaka huu “Kumetolewa madai eti kwamba taasisi ya Wama inayoongozwa na Salma Kikwete inao mzigo mkubwa bandarini ambao haujalipiwa ushuru na kodi.

Na kwa sababu hiyo, Mamlaka ya Mapato Tanzania imepanga kuuza mali hizo. “Kwa niaba ya Taasisi ya Wama napenda kutoa masikitiko yetu kwamba habari hizo ni za uongo na hazina ukweli wowote. “Kwa maoni yetu gazeti hilo lina dhamira mbaya dhidi ya Taasisi ya Wama na Mwenyekiti wake Salma Kikwete. Nia yao ni kupaka matope na kuchafua majina na sifa ya taasisi yetu na kiongozi wake.”

Katibu mtendaji huyo alisema ukweli kuhusu jambo hilo ni kwamba, Wama ilitumiwa maboksi 11 ya vitabu vikiwa ni zawadi kutoka Taasisi ya Nakayama ya Japan ambayo ndiyo iliyofadhili ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wama-Nakayama iliyopo Nyamisati, Kibiti na yalishatolewa bandarini yangu Agosti 10 mwaka na tayari vitabu viko shuleni na vinatumika.

“Hakuna mzigo wowote wa Taasisi ya Wama uliopo bandarini unaosubiri kutolewa wala kuuzwa na TRA,” imesema sehemu ya taarifa hiyo na kulitaka gazeti hilo kuomba radhi kwa Salma Kikwete na kwa Wama kutokana na taarifa hizo.

MTANGAZAJI Salama Jabir Ala Shavu Tuzo za EATV Awards 2016

$
0
0

Mtangazaji mahiri wa vipindi vya burudani nchini, Salama Jabir ametangazwa na EATV kuwa host wa tuzo za EATV Award 2016 ambazo zitafanyika Disemba 10 katika ukumbi wa Mlimani City.

Jumla ya tuzo 10 zinatarajiwa kukabidhiwa kwa wasanii wa muziki na filamu siku hiyo.

Kupitia twitter ya EATV, imeandika;

Tunamtambulisha kwako HOST EATV AWARDS 2016, mkali wa hizi kazi.
Salama Jabir

Moja kati kipengele ambacho kitakuwa na msisimko siku hiyo ni kipengele cha msanii bora wakiume ambacho Alikiba, FA, G-Nako, Shetta na Ben Pol wanapigana vikumbo kuondoka na tuzo hiyo.

TUME ya Utumishi wa Umma Yazungumzia Kuhusu Kuwatumbua na Kuwadhalilisha Watumishi wa Umma

$
0
0
Tume ya Utumishi wa Umma imetaja mamlaka sita zenye dhamana na madaraka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa umma kisheria ikiwa pamoja na kufuta nafasi za madaraka.

Vilevile, Tume hiyo imezitaka mamlaka za nidhamu zote kuzingatia sheria, kanuni pamoja na taratibu wakati wa kutekeleza majukumu yao kwani kwa kufanya hivyo, watumishi wanaotuhumiwa kufanya kosa watatendewa haki.

Tume ya Utumishi wa Umma imetoa maelekezo hayo siku chache baada ya viongozi wengi katika Serikali ya Awamu ya Tano wakiwamo wakuu wa mikoa na wilaya kuwachukulia kiholela hatua za nidhamu watumishi wa umma wakati baadhi hawana mamlaka hayo kisheria.

Baadhi ya wakuu wa mikoa wamekuwa waki- wasimamisha watumishi hadharani tena kwa kusikiliza malalamiko ya upande mmoja bila kuwapa walalamikiwa nafasi ya kujitetea, na wakati mwingine kudhalilishwa katika mikutano.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Msaidizi Tume hiyo, Enos Mtuso alisema kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003 madaraka ya kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wa umma yako chini ya watu wachache.

“Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 ilitungwa ili kuweka misingi ya kisheria katika kutekeleza malengo ya Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma iliyopitishwa na Serikali mwaka 1998.

Sheria hii ndiyo inayotoa uwezo kwa mamlaka za kinidhamu mbalimbali katika utumishi wa umma na kuweka misingi ya namna masuala hayo yanavyopaswa kushughuliwa,” alisema.

Mtuso alizitaja mamlaka hizo kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Katibu Mkuu Kiongozi, watendaji wakuu, wakuu wa idara na divisheni, na mamlaka za Serikali za Mitaa (Baraza la Madiwani).

Lakini alipoulizwa mkuu wa mkoa anapata wapi mamlaka ya kuwafukuza kazi watumishi wa umma na kuwadhalilisha mbele ya hadhara, Mtuso alisema wao kama Tume hawana mamlaka ya kuzungumzia jambo hilo kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanakiuka maadili na kwamba suala hilo liko chini ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Kauli ya Tume iliwekewa uzito na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman Jaffo ambaye amewataka wakuu wa idara kuacha kuwanyanyasa wafanyakazi kwani hali hiyo inasababisha wafanye kazi kwa hofu ya kutumbuliwa.

Akizungumza baada ya kuwatembelea watumishi wa umma wa Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam jana, Jaffo alisema wizara yake itatoa ushirikiano kwa watumishi wote wanaofanya kazi kwa bidii.

Katika hatua nyingine, Mtuso alitoa takwimu za mashauri ya nidhamu yaliyochukuliwa hatua katika kipindi cha 2014/2015 na 2015/2016 akisema jumla ya watumishi wa umma 249 sawa na asilimia 75 ya mashauri yote yaliyowafikia wakiwamo walimu 209 walifukuzwa kazi kwa makosa yaliyothibitika.

 Alisema Watumishi hao wamefukuzwa kazi kwa makosa mbalimbali ikiwamo, kukiuka maadili ya kazi, kutotekeleza majukumu, ubadhilifu, rushwa, wizi wa fedha na mali, udanganyifu, matumizi mabaya ya madaraka, uzembe, utovu wa nidhamu huku utoro kazini ukiwa na idadi kubwa ya waliofukuzwa kazi.

“Utoro kazini ni changamoto kubwa inayotukabili na ndiyo mashauri yake mengi yanathibitika, unakuta mtumishi haendi kazini siku tano na kuendelea bila sababu maalumu wala hatoi taarifa yoyote kwa waajiri wake kuwa anashida gani,” alieleza.

MSHIRIKI wa Bongo Star Search Aeleza Sababu ya Washindi Kushindwa Kufanya Vizuri Sokoni

$
0
0
Hadi sasa watu wanajiuliza nini kimetokea kwa Kayumba – mshindi wa Bongo Star Search mwaka jana. Mbona kijana huyo alionesha uwezo mkubwa wakati wa shindano hilo kiasi ambacho walimtabiria angekuja kuwa kuwa Diamond wa pili?

Alitoa wimbo ambao video yake ilifanyika nchini Afrika Kusini lakini haukuweza kufanya vizuri. Na sasa jina lake limesahaulika kabisa. Tatizo liko wapi? Mshiriki wa shindano hilo ameeleza maoni yake kwenye comment za post niliyoweka wiki kadhaa zilizopita kuhusiana na wimbo wa gospel wa Walter Chilambo ambaye aliwahi kushinda taji la BSS.

“Katika harakati za kutafuta majibu ya kwa nini washindi wa BSS hawafanyi vizuri kwanza nitakujibu kama mdau wa muziki, pili kama mshiriki wa EBSS 2012 pekee kutoka Mwanza aliyetolewa katika Top 09,” anasema.

“Kwanza tatizo kubwa la BSS ni kutopromote ubunifu. Haiwajengi washiriki wake katika kujitegemea kwenye utunzi na uimbaji. Shindano limebase kwenye kuimba covers, na hapa naenda mbali zaidi cover zinatakiwa ziimbwe kama original songs, no improvision sababu ukifanya hivyo utaonekana haujautendea haki wimbo.”

Ameendelea, “Pili, washiriki na hata ma judge wanawaza sana kuhusu ile million 50 itaenda kwa nani kuliko kuwaza katika ni mshiriki gani atakuwa brand mpya ya music na anaweza kusimama na kuuteka umma kwa performance, hili hupelekea kutumia kigezo kimoja tu kumpa mtu ushindi.

Tatu, ni management. Washindi wengi wanakosa management za uhakika sababu mara baada ya shindano kuisha tu, biashara inafungwa na msanii anaachwa akajitegemee. Na hapa hata kama utaona ana management ujue ni kwa muda tu kipindi ambacho hali yake kiuchumi inapokuwa nzuri. Baada ya hapo msanii huyo atarudi kuwa hovyo pengine hata zaidi ya alivyokuwa kabla hajaingia Lamborghini.”

“Nne ni elimu,” anaendelea. “Ni ukweli mchungu ila tuumeze tu ili tujifunze. Washiriki wengi wa BSS ni vijana wadogo sana kiumri na kielimu pia. Na wengi wao hutoka katika familia zenye kipato kidogo. Kwa hiyo wanapoingia mle kwenye shindano kwanza wanaona kama bahati. Pili nafasi pekee ya kijikwamua, tatu wanakuwa hawatambui haki zao na kubwa zaidi wanakuwa hawajajiandaa kuupokea u star. Ndio maana wengi wao kama sio wote hawawezi kusimama peke yao mara baada ya mashindano. Na wengine wakishaupata u star, kutokana na kukosa elimu ya kutosha kunawafanya wanakuwa malimbukeni hivyo kuishia kuharibu vipaji vyao.”

“La mwisho, Judges wajenge a fair platform kwa washiriki wote ili kupata washindi wa kweli, mihemko ipungue, wasitake sides, na wasiwe na personal interest kwa washiriki ili kupata mshindi wa kweli. Amini nakwambia katika most of the time, the best singers never win competition. Kwa kusema hilo pengine waimbaji bora hutolewa kwa vigezo(vya kijinga) vingine tu ili majaji waonekane wana power lakini matokeo yake ndio haya tunayoyaona. Their winners never move even a baby step ahead. Ni matumaini yangu umejifunza kitu.”

Bongo5

SOKO la Gigy Money lahamia kwa wasanii wachanga

$
0
0
Video Queen Gigy Money amesema kwa sasa wasanii wachanga wanamgombania kutaka atokelezee kwenye video zao.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Gigy Money amedai wasanii hao wanaamini akitokelezea kwenye video zao na wao watakuwa wametoboa.

“Kusema kweli sasa hivi underground wananisumbua sana,” alisema Gigy Money. “Wengi wanaamini nikishiriki kwenye video zao ‘nitawakikisha’ na watatoboa. Lakini nashukuru yote ya yote ni biashara wakija ni milioni moja nashiriki kwenye kwenye video kwa sababu ni wengi na bado kwa bei hiyo kuna baadhi wao nawachinjia baharini kwa sababu siwezi kutokea kwenye kila video,”

Pia Gigy alidai kwa sasa yeye ndiye video queen ambaye anafanya kazi nyingi za kulipwa nchini.

ALI KIBA na Producer Abydad Waingia Katika Mgogoro Mzito

$
0
0
Pengine aje inaweza ikawa nyimbo ya mwisho ya alikiba chini ya producer abydad ambaye ametengena nyimbo kadhaa za alikiba.

Abydad ambaye ametengeza hit kama #nagharamia #chekecha na #aje ambazo zilifanya vizuri Sana.

Hivi karibuni ilikuwa inatarajiwa kuachiwa #aje remix ambayo ilipangwa kuachiwa November 29 siku ya birth day ya alikiba,

Lakini habari zinazoendelea kusambaa ambazo zilianza Kama masihara ila kwa sasa zinaanza kuaminika kutokana na taarifa za watu wa karibu,

Ni kwamba abydad ndo anayechelewesha kutoka kwa aje remix na mpaka sasa amekataa kutia sahihi yake kwenye mkataba ili ngoma iwe released.

Abydad anataka 50%/50% katika nyimbo ya aje ikiwemo katika show iTunes na mapato yatakayo patikana abydad anataka nusu kwa nusu.

Kuna taarifa kwamba wcb wanamrubuni abydad ili aachane na kiba japo taarifa hizo sio confirmed

VIDEO ya Eric Omondi yamtoa povu Barakah The Prince

$
0
0
Baada ya Eric Omondi kuachia video ya parody ya wimbo wa ‘Kuliko Jana’ wa Sauti Sol, msanii wa Bongo Fleva Barakah The Prince amemjia juu mchekeshaji huyo.

Hitmaker huyo wa Nisamehe ameonyeshwa kuchukizwa na baadhi ya vipande vya kwenye video hiyo na kuamua kuweka wazi kupitia mtandao wa Instagram.

Kupitia mtandao huo, Barakah ameandika:

Ukiona unakosa cha kuchekesha watu bora utafute kazi nyingine ya kufanya kuliko alichofanya huyu sijui ndio anaitwa nan…kawakosea sana watu wote wenye imani ya kikristo…tafuta kazi nyingine… maana vichekesho nahisi umefikia mwisho…huyu jamaaa kafanya asubuhi yangu kuwa mbaya sana..shukuru wakristo ni wapole..ukifanya kitu ichi kwa Muslim..ungefanywa mfano..
VIDEO:

BONGO Movie Yazidi Kufa, JB Nae Aacha Kuigiza

$
0
0
Msanii wa siku nyingi wa bongo movie JB amestaafu kuigiza bongo movie, hii imesikitisha sana wadau wa sanaa, kuanzia mashabiki hadi wasanii wenzake..
VIDEO:


TANESCO yatimiza Agizo la Rais Magufuli la Kumpatia Umeme Bakhressa

$
0
0
SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limetimiza agizo la Rais John Magufuli la kukipatia umeme kiwanda cha kusindika matunda cha Azam Fruits Processing Plant, mali ya mfanyabishara, Said Salim Bakhresa kabla ya muda wa miezi miwili waliyopewa kukamilisha kazi hiyo.

Rais Magufuli alitoa agizo hilo Oktoba 6, mwaka huu alipokuwa anazindua kiwanda hicho kilichopo Mwandege, Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani kufuatia kilio kilichotolewa na uongozi wa kiwanda hicho kuiomba serikali iingilie kati ili kupata umeme wa uhakika kwa ajili ya uzalishaji bidhaa kiwandani hapo.

“Tayari tumetimiza agizo la Rais la kukipatia umeme kiwanda cha Bakhresa, Mkuranga Novemba 30, mwaka huu kwa kufikisha umeme kiwandani hapo,” Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Felchesmi Mramba alitoa maelezo hayo jana jijini Dar es Salaam.

Mramba alikuwa anatoa majumuisho kwa wahariri wa vyombo vya habari baada ya ziara ya kutembelea miradi ya ukarabati wa miundombinu ya usambazaji umeme jijini Dar es Salaam.

Alifafanua umeme umefikishwa kiwandani hapo na kilichobaki ni upande wa kiwanda chenyewe ambao unasubiri baadhi ya vifaa kutoka nje ili waweze kuingiza umeme ndani ya kiwanda.

Alisema Tanesco inajenga njia tatu za umeme kuelekea Mkuranga na mbili kati hizo ni kwa ajili ya viwanda vipya wilayani humo na moja kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

Katika juhudi za kuboresha miundombinu ya Tanesco ili kukidhi adhma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa viwanda, shirika lake linatekeleza miradi ya ukarabati wa miundo mbinu ya umeme kwa nchi nzima itakayogharimu Sh zaidi ya trilioni 5.4.

Alifafanua miradi hiyo ni pamoja na uzalishaji, usafirishaji na vituo vya kusambazia umeme ambavyo mifumo ya zamani ya analogia inabadilishwa na kuwekwa mifumo mipya ya ya kisasa ya dijitali yenye ufanisi mzuri zaidi.

Vituo vya usambazaji umeme vya Dar es Salaam vilivyotembelewa vikiwa bado vinaendelea na ukarabati wa mifumo ya zamani na kuweka ya kisasa ni pamoja na Muhimbili, City Center, Sokoine na Kituo cha Ilala.

SERIKALI Yakanusha Katibu Mkuu, Ofisi Ya Rais-utumishi Kujiuzulu

$
0
0
SERIKALI Yakanusha Katibu Mkuu, Ofisi Ya Rais-utumishi Kujiuzulu

TAZAMA VIDEO Jinsi Diamond na Jah Prayzah Walivyoimba Wimbo Wao Live Jijini Harare Zimbabwe

$
0
0
Tazama sehemu ya performance ya Diamond na Jah Prayzah ya wimbo wao Watora Mari kwenye ukumbi wa HICC jijini Harare, Zimbabwe.

YUSUPH Manji Atimuliwa Jengo la Quality Plaza. Apewa Saa 24

$
0
0
MAKAMPUNI yaliyo chini ya mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Mehbub Manji, yamepewa saa 24 yawe yameondoka katika jengo la PSPF PLAZA, zamani likijulikana kama Quality Plaza, vinginevyo yatang’olewa kwa nguvu na kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart.

Notisi iliyotolewa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma – PSPF ambao ndio wamiliki inataja kampuni zilizoko kwenye jengo hilo katika Kitalu Namba. 189/2 kwenye Barabara ya Nyerere kuwa ni Quality Group Company Limited, Gaming Management Limited, Q Consult Limited, Quality Logistics Company Limited na International Transit Investment Limited, ambazo ziko chini ya Manji.

Uamuzi wa kuyatimua makampuni ya Manji, Diwani wa Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, unafuatia uamuzi wa shauri lililokuwa katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi ambao ulitolewa na Jaji Mgetta Novemba 24, 2016, ambapo pamoja na mambo mengine, iliamuliwa kampuni hizo ziondoke mara moja.

"Katika shauri husika, Mahakama iliamuru miongoni mwa mambo mengine, kuondoka mara moja kwenye eneo husika linalojulikana kama PSPF Plaza, zamani Quality Plaza, lililoko kwenye Kitalu Namba. 189/2 kwenye Barabara ya Nyerere. Unatakiwa uwe umeondoka kwa amani katika muda wa saa 24 kuanzia tarehe ya notisi hii. Zingatia kwamba, kama hutaondoka katika muda wa saa 24, Mfuko umemwagiza dalali Yono Auction Mart and Co. Ltd kukuhamisha kwa nguvu," imeeleza notisi hiyo ya Desemba 2, 2016 kwenda kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Quality Group of Companies.

Manji kwa sasa ni mshauri wa makampuni ya Quality Group baada ya kujiuzulu rasmi uenyekiti mnamo Julai 15, 2016.

JOHN Heche: Kesi yenye dhamana inawezekana vipi kunyimwa dhamana?

$
0
0
 
Anaandika Comred Mbunge wa Jimbo la Tarime vijini John Heche.

Mahakama za Tanzania ni aibu kwa taifa, mahakama inapokua sehemu ya kunyima haki inafundisha watu tabia ya kutoheshimu mahakama.

Hili sakata la Lema kuna mtu aliniambia mapama litapigwa danadana mpaka feb kwa visingizio mbalimbali mwanzo sikuamin!

Sasa imethibitika hivyo inatia hasira sana. Kesi yenye dhamana inawezekana vipi kunyimwa dhamana!
Kama kesi ya kuota mtukufu amekufa haina dhamana ni bora ikaunganishwa na zile tatu za mauaji,uhaini na armed robbery ambazo sheria zetu zinatambua kwamba hazina dhamana, vinginevyo ni mahakama kutumika vibaya kunyima watu haki zao, na watu wataendelea kuona maona hata kama mtukufu hayapendi.
#Justice for Lema.

HAYA Ndio ya Majina Matatu yaliobaki Kuwania Tuzo ya Kocha Bora wa Dunia Mwaka 2016

$
0
0
Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA, wametangaza majina ya makocha watatu waliobaki katika kinyang’anyiro cha kuwania. Tuzo ya Kocha Bora wa Dunia mwaka 2016 ambapo mshindi atatangazwa Januari,9,2017 huko Zurich.

fifa

Haya ndio Majina ya makocha hao

1.Claudio Ranieri – Leicester

2.Fernando Santos – Portugal

3.Zinedine Zidane -Real Madrid

Kocha gani unaona anastahili kubeba tuzo hii andika komenti yako hapo chini

Ni Kweli Nafasi ya Diamond Imechukuliwa na Darassa?

$
0
0
Kutokana na ngoma aliyotoa Darassa kuifunika ngoma ya Rich Mavoko aliyomshirikisha Diamond, inasemekana kuna dalili tosha kuwa Diamond kijiti anaanza kumpatia Darassa taratibu bila yeye kujua.

Je kuna ukweli wowote hapo???
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images