Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

Hatimaye Diamond na Zari Wamepata Mtoto wa Kiume Leo Tarehe 6 Dec 2016

$
0
0


Ni good news nyingine kwa msanii wa Bongofleva Diamond Platnumz ambaye leo December 6 2016 mpenzi wake Zarina Hassan amefanikiwa kujifungua mtoto wake wa pili, Zari na Diamond wamepata mtoto wao wa pili baada ya kupata mtoto wao wa kwanza Tiffah August 2015.


HONGERENI SANA ZARI NA DIAMOND!

Ripoti ya Hospitali Kuhusu kilichosababisha mchezaji wa Mbao FC kufia uwanjani

$
0
0


Baada ya kufariki uwanjani kwa mshambuliaji wa timu ya Mbao FC Ismail Khalfan siku ya Jumapili ya December 4, leo December 6 2016 imetoka ripoti ya kilichosababisha kifo cha mchezaji huyo wakati wa mchezo kati ya Mbao FC dhidi ya Mwadui FC.

Ripoti iliyotolewa na hospitali ya mkoa wa Kagera kuhusiana na kifo cha mchezaji huyo, kupitia kwa jeshi la Polisi, Ismail alifariki uwanjani kutokana na kumpata tatizo la kusimama ghafla kwa moyo (sudden Cardiac Arrest-SCA).

Kamishina Msaidizi wa Kagera, Augustin Ollomi ametoa taarifa baada ya uchunguzi wa madaktari kuhusu kifo cha mchezaji huyo ambaye hakuwa na jeraha lolote walibaini kusimama ghafla kwa moyo (sudden cardiac arrest) kulisababisha kifo

SUDDEN CARDIAC ARREST-SCA
Kwa faida yako msomaji:
Kawaida moyo una mfumo wa umeme (heart electrical system), ambao unadhibiti mapigo ya moyo, mfumo huu ukisimama basi moyo unashindwa kusukuma damu sehemu muhimu kama ubongo na ogani kuu.

Moyo ukisimama bila kurudi katika hali yake unasababisha kifo ndani ya sekunde chache na njia pekee ya msaada ni kupita electrical shock ili kushtua mfumo wa umeme wa moyo, na hii inapaswa kufanyika ndani ya sekunde chache mno.
CHANZO: salehjembe

CUF Wakanusha Taarifa za Maalim Seif Kutaka Kukihama Chama Hicho

$
0
0

Chama cha Wananchi (CUF), kimesema taarifa zinazosambazwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kwamba Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad anataka kuhama chama hicho ni za kupuuzwa kwa kuwa hazina ukweli.


Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema hayo jana  baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa Maalim anataka kuondoka ndani ya chama hicho cha upinzani.


Alisema tangu kuibuka kwa mgogoro ndani ya CUF na Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba imekuwapo mikakati ya kuwakatisha tamaa jambo ambalo halitafanikiwa.


Mazrui alisema wanaopanga mikakati wamehangaika kila njia na wameonekana kukwama, hivyo kuibuka na mkakati wa kumzushia Katibu Mkuu kuhama chama.


“Hivi unafikiria Katibu Mkuu anaweza kuhama chama katika mazingira rahisi kiasi hicho? Hiki chama amekipigania vya kutosha wataondoka wao,” alisema.


Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka wana CUF kuendelea kutoa ushirikiano kwa Katibu Mkuu wao na kupuuza kauli za watu ambao wamepoteza mwelekeo kisiasa.


Alisema CUF si chama kinachotegemea mtu mmoja, na pia hakiko tayari kumpoteza Maalim kwa vibwagizo vya vibaraka wa chama tawala, ambao hawataki kupigania mabadiliko nchini.


Aidha, kuhusu chama kuwa kimya kuhusu madai yao ya ushindi katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana, alisema bado wanaendelea na mchakato huo na watatoa taarifa hivi karibuni kuhusu hatua waliyofikia.


Mazrui alisema kila kitu kinakwenda vizuri na kutaka wana CUF kuwa na subira katika kipindi hiki, kwani mambo mazuri hayahitaji haraka.


Alisema ushirikiano wanaopata kutoka jumuiya ya kimataifa ni mzuri hali ambayo inawapa matumaini ya kuhakikisha kuwa haki inapatikana.


“Suala la madai ya ushindi wa uchaguzi linakwenda vizuri, na naamini hatima yake itapatikana kwa busara, ni vema wana CUF kuwa na subira,” alisema.


Jana katika baadhi ya magazeti ziliandikwa habari zikimhusisha Maalim na kuhama CUF na kutajwa kutarajia kuhamia vyama vya ADA-TADEA, AFP au ACT-Wazalendo, ambapo viongozi wa vyama hivyo walikanusha taarifa hizo.


Hali kadhalika Katibu Mkuu huyo alihusishwa na kutaka kujiunga na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

ALICHOANDIKA Zari Baada ya Kurudi Nyumbani Akiwa na Mtoto wa Kiume

$
0
0

Hatimaye Zari na Diamond wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume aliyezaliwa saa 10:35 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki, Jumanne, December 6.

Mtoto huyo amezaliwa kwenye hospitali ya NETCARE ya Pretoria nchini Afrika Kusini.

Diamond na Zari wameonesha furaha kwa ku-share picha za mtoto kwenye mitandao yao ya kijamii...


zarithebosslady: thanking everyone for your prayers, we are all doing fabulously ok

ALICHOANDIKA Darassa Baada ya Dereva Kukamatwa Akicheza Wimbo Wake Huku Akiendesha Gari

$
0
0
Msanii wa Bongofleva Darassa ambaye kwa sasa anafanya vizuri na hit single ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Muziki’ ameamua kuweka wazi mtazamo wake kuhusu ile video iliyosambaa ikionesha vijana wakicheza wimbo wake  huku dereva akiacha  gari likienda.

Vijana hao wamekamatwa na polisi na Darassa ameamua kutoa mawazo yake kuhusiana na kitendo hicho ambacho kimewafanya vijana hao kukamatwa na polisi Itigi Singida, Darassa ametuamia account yake ya instagram kuandika ujumbe kuoneshwa kuguswa na

“Hawa ndugu zetu nimepata taarifa wamekamatwa kwa kosa la kutaka kusababisha ajali na unaweza kuona Kama mchezo ulielekea kubaya, ingeweza kua Tatizo kwao Au kumu sababishia mwingine, Naskia watakua mahakamani Leo I’m not so sure naendelea kufatilia”

“Nawaombea Tatizo hili Mungu awafanyie wepesi I’m sure wamejifunza Hawawezi kufanya tena mistake Kama Hii itokee, mizuka feelings mtu anaweza kufanya kitu njee ya mipango yake sometimes, Mungu awasaidie 🙏🏽 LENGO NI KUJENGA DUNIA KUA SEHEMU NZURI NA SALAMA KUISHI #Muziki“

Install APP ya Blog Hii ya UDAKU SPECIAL Kwenye Simu yako Kutoka Google Play Kusoma Habari Kirahisi

$
0
0

Download  Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu yako Kutoka Play Store Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi

Bonyeza Hapa CLICK HERE 



MAMBO 10 Ambayo ni Sumu Katika Mapenzi

$
0
0
KATIKA harakati zako za kutafuta mpenzi, unaweza kukutana na mwanamke ambaye kwa sababu moja au nyingine anakwondolea uwezo wako wa kufikiri, kutumia mantiki na pia kutumia akili yako ya kuzaliwa. Si lazima awe amekufanyia kitu, lakini inaweza kuwa ni ulevi wako tu unaosababisha ufanye mambo yasiyo ya kawaida. Pengine ndiyo maana baadhi ya wasanii huzungumzia suala la “kudata” kutokana na mapenzi.

Ni jambo jema kudhani kuwa wewe na mpenzi wako mnapendana kwa dhati na kwamba kila mmoja amefika kwa mwenzake, lakini kama mojawapo ya mambo haya kumi yaliyoelezwa hapa chini litajitokeza, basi fahamu kuwa yamkini umependa kuliko kawaida, yaani ni kama umenyweshwa sumu ya penzi. Kumbuka kupenda ni kuzuri, lakini kupenda kupindukia kunaweza kukutumbukia nyongo, kwani katika kila jambo kinahitajika kiasi.

1. WIVU WA KUPINDUKIA
Ni jambo jema kwa mwanamume kumtakia heri mpenzi wake na kufanya kila awezalo kuhakikisha kuwa hapati madhara, lakini iwapo utakuwa mtu wa wasiwasi na mashaka pale unapomwona mpenzi wako akizungumza na mwanamume mwingine, au anapotoka na marafiki zake wa kike, au anapovaa nguo inayomfanya atamanishe, basi fahamu kuwa tayari umekunywa sumu ya mapenzi.

Katika uhusiano wa kimapenzi, kuaminiana ni jambo muhimu sana. Kama kweli unataka mpenzi wako akupende kwa dhati, mwoneshe kuwa unamwamini na unaheshimu maamuzi yake, ikiwa ni pamoja na maamuzi ya kutoka na marafiki zake wa kike na kuwa na marafiki wa kawaida wa kiume. Ondoa hofu na acha kabisa kumpeleleza, maana wapo wanaume ambao hutumia muda wao mwingi kuwapeleleza wapenzi wao ikiwa ni pamoja na kuwategeshea kamera na rekoda za simu.

2. KUTOMWACHIA NAFASI MPENZI
Kama huishi na mpenzi wako ni jambo la kawaida kuwa na hamu ya kumwona mara kwa mara, lakini kumbuka kuwa mpenzi wako naye ana maisha yake na anahitaji nafasi ya kuwa peke yake kwa ajili ya mambo yake binafsi.

Hisia za kutaka kuwa na mpenzi wako muda wote zinaweza kudhaniwa kuwa ni za mapenzi ya dhati, lakini kwa hakika hiyo si ishara njema ya mapenzi ya kudumu. Hebu jiulize kama unaweza kuendeleza hali hiyo maisha yako yote. Ni wazi kuwa utachoka. Kwa hiyo, mpe mpenzi wako fursa ya kupumua. Namna hii mpenzi wako atajenga hamu ya kutaka kukutana nawe lakini ukiwa naye muda wote hamu hiyo itaisha.

3. KUMWAMULIA MPENZI MAMBO YAKE
Unaweza kujikuta ukisukumwa kumwambia mpenzi wako awe anavaa nini wakati gani, akutane na nani na kwa wakati gani au ale nini. Ukiona hivyo, fahamu kuwa hayo si mapenzi, bali umepitiliza na pengine mwisho wa uhusiano wenu unanukia.

Hata ukiachilia mbali suala zima la usawa wa jinsia, hakuna mwanamke ambaye angependa apangiwe kila kitu kuhusiana na maisha yake. Kama ilivyodokezwa hapo juu, kila mtu ana maisha yake na kilichowaunganisha ni mapenzi tu. Kama utataka kumpangia kila kitu ni wazi kuwa utaishia kuishi peke yako.

4. KUMUULIZA MPENZI MASWALI
Iwapo utajikuta ukimuuliza mpenzi wako maswali mengi yanayoonesha wasiwasi wako kuhusiana na mwenendo wake, fahamu kuwa kuna tatizo na tatizo hilo lisipopatiwa ufumbuzi utakuwa mwanzo wa mwisho wa uhusiano wenu.

Mwanamke angependa umuulize maswali ya kawaida kuhusiana na jinsi siku yake ilivyokuwa na kama marafiki zake hawajambo au la, lakini kila jambo lina mpaka wake. Mwanamke hatarajii kuwa kila mnapokutana atakuwa kama ameingia kwenye chumba cha mtihani au usaili wa kazi.

5. KUTOAMINI ANACHOKWELEZA MPENZI
Wakati mwingine watu hushindwa kuwaamini wenzao, lakini kwa sababu ambazo ni za msingi, lakini kuna wakati ambapo mtu hushindwa kumwamini mwenzake bila sababu yoyote ya msingi, au kwa sababu zisizo sahihi, kisingizio kikiwa ni mapenzi.

Kuna tatizo la kisaikolojia la kujishuku au kuwashuku wenzako. Hili ni jambo ambalo linaweza kukuharibia mustakabali wako katika mapenzi, maana husababisha kujengeka kwa mazingira ya kutokuaminiana. Ili uweze kwenda sanjari na mpenzi wako, amini kila anachokweleza hadi pale utakapokuwa na sababu za msingi za kutokumwamini. Na hata unapokuwa umelithibitisha jambo, endelea kuwa katika uhalisia wako.

6. KUACHA HOBI, MARAFIKI
Mahusiano ya kimapenzi mara nyingi huhusisha kila mmoja kuacha baadhi ya mambo yake kwa ajili ya mwenzake. Hata hivyo, lengo ni kuweka tu uwiano wa mahitaji, si kuacha kila kitu ulichokuwa nacho kwa ajili ya mwenzako, ama kwa shinikizo, au kwa kulewa penzi.

Iwapo utabaini kuwa marafiki zako sasa wamekuwa ni marafiki zako wa zamani na hobi zako zimebaki tu katika kumbukumbu japo kwa hakika bado unahisi mapenzi katika hobi hizo, basi tambua kuwa huyo mrembo wako amekunywesha sumu ya penzi na sasa huwezi hata kuitumia vema mantiki yako.

Mbaya zaidi, iwapo utabaini kuwa marafiki zako wapya ni marafiki wa siku zote wa mpenzi wako na hobi zako ni zile za mpenzi wako, basi tambua kuwa huna tena nafsi yako, bali umejisalimisha mzima mzima kwa mpenzi wako. Lakini msemo mmoja wa hekima unatwambia usiweke mayai yako yote kwenye kikapu kimoja. Yamkini unaelewa.

7. KUKUBALI KUPELEKESHWA
Pengine unakumbuka kuwa kuna nyakati ambapo ulikuwa na uwezo wa kujikita katika jambo moja na kulifanya kwa umakini, huku ukiwa pia mwerevu, mjanja na unayejisimamia, lakini leo unayeyuka kirahisi tu kama barafu iliyowekwa juani! Hii ni hatari kwa mustakabali wa maisha yako.

Mbaya zaidi ni pale utakapoiacha kazi yako inayokulipa vizuri na kufanya kazi nyingine kwa ajili ya kumfurahisha mpenzi wako. Ukifika hali hii ujue wewe mwenyewe kuwa hapo hakuna mwanamume.

8. UTAYARI WA KUFA KWA AJILI YAKE
Umewahi kujisikia kuwa na utayari wa kufa kwa ajili ya mpenzi wako? Kama jibu ni “ndiyo”, basi fahamu kwa hakika kuwa hayo uliyo nayo si mapenzi bali ni upumbavu. Pengine huku ndiko kunywesha sumu ya mapenzi. Kwa hakika, hakuna mwanamke ambaye anastahili kumfanya mwanamume yeyote kufa kwa ajili yake.

Yamkini wanaume wanaolengwa katika makala haya si wavulana wanaosoma sekondari, waliobalehe majuzi, ambao wakipenda au kupendwa hujiona kama wako katika sayari yao. Mwanamume aliyepevuka hujiamini na hayaweki maisha yake yote mikononi mwa mwanamke, hata kama mwanamke huyo angekuwa ndiye mrembo wa dunia.

Iwapo, ama kwa ujinga au kwa kufahamu umewahi kumwambia mpenzi wako: “Ukiniacha nitajiua,” na ukawa unaamini hivyo kabisa, basi yamkini unahitaji kutafuta msaada wa ushauri nasaha, maana kwa hakika umepotoka.

9. MUDA WOTE UNAWASILIANA NAYE
Vijana wa siku hizi ni watumiaji wazuri sana wa simu, lakini iwapo utabaini kuwa asilimia kubwa ya muda wako unautumia ama kwa kuongea au kuwasiliana kwa ujumbe mfupi na mpenzi wako, basi fahamu kuwa kuna tatizo ambalo linahitaji ufumbuzi wa haraka.

Kumbuka kuwa mapenzi hayachukui nafasi ya kila kitu. Yamkini huyo mpenzi wako amekukuta unaishi na kuna mambo ya muhimu ya kufanya. Hebu achana na simu kwanza ufanye mambo ya muhimu kuhusiana na maisha yako. Kama mpenzi wako hakwelewi katika hili basi hakufai.

10. NDUGU ZAKE WANAKUFUATILIA
Iwapo utabaini kuwa marafiki, ndugu na jamaa za mpenzi wako wanamtonya mpenzi wako kuhusiana na kile wanachokiita mwenendo wako mbaya, usipuuze hali hii. Kuna uwezekano mkubwa kuwa watu hawa wanayo sababu ya kuwa na wasiwasi na mwenendo wako, kwa hiyo jichunguze na kuangalia jinsi unavyoenenda.

Hata hivyo, jambo hili si ishara njema ya mustakabali mwema wa uhusiano wenu. Iwapo mpenzi wako ataweka watu wake wakufuatilie, maana yake halisi ni kwamba hakuamini. Katika hali kama hii, haitarajiwi kuwa mustakabali wa uhusiano wenu utakuwa mzuri, kwani kutakuwa na uingilizi mwingi wa ndugu, jamaa na marafiki zake. Unaweza kukubali kuendelea kuishi katika hali hii kwa kisingizio cha mapenzi, lakini ukweli ni kwamba hayatakuwa mapenzi bali karaha.

KUWA MAKINI
Kama unavyoona, hizi ni baadhi tu ya dalili kuwa mapenzi yako kwa mwanamke sasa yanaelekea katika ulevi, mithili ya ule wa dawa za kulevya. Jambo moja la kukumbuka ni kwamba kweli mapenzi ni kitu kizuri, lakini pia mapenzi yanahitaji kuwa jambo linaloashiria mustakabali mwema kwa wahusika wawili. Yakiwapo mambo haya kumi hauwezi kuwapo mustakabali mwema katika mapenzi.

ISIKILIZE Video ya Rais Magufuli Akiwapiga Marufuku Wakuu wa Mikoa Kuwasumbua Machinga

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga katika Jiji la Mwanza pamoja na mikoa mingine mpaka hapo mamlaka husika zitakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa na kwa kuwashirikisha wamachinga wenyewe.

Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo  tarehe 06 Desemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akionya kuwa kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kutekeleza agizo hilo aachie ngazi.
 VIDEO:

YALIYOJIRI Mwanza Mjini: RC, DC na CD Wataweza Kukalia Ofisi zao na Kutoa Maamuzi na Kueleweka?

$
0
0
FM Radio zote za jijini Mwanza sasa hivi ni mjadala wa maamuzi ya Rais na zinawekwa Clip za matamko ya Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya Nyamagana na Mkurugenzi (CD) wa jiji kuhusu suala la wamachinga waliyotoa siku zilizopita kuhusu suala hilo na kuonekana kuwa walikuwa tofauti kabisa na hiki alichosema Rais.

Hata mbunge wa Nyamagana alipohojiwa amepata nafasi ya kuwaruka kabisa viongozi hao kiasi cha kuonyesha maamuzi yao yalikuwa yao pekee kwa nia ya kukomoa Wamachinga na mama ntilie.

Hii ni fedheha kubwa sana kwa wateule hao wa kisiasa na kiutendaji na wanakosa kabisa sifa ya kuendelea kuwaongoza watu wa Mwanza kwa siku zijazo kwani hawawezi tena kuwa na maamuzi ambayo yatakuwa yamesimama bila kudharauliwa.

Je, wataamua wenyewe kujiuzulu ili kulinda heshima zao au watataka waendelee kufanya kazi kama picha tuu? Maana kila anayehojiwa mtaani anawaponda na kuwadharau kuwa kazi imewashinda ndio maana aliyewateua kaamua kuifanya mwenyewe.

UKWELI Mchungu: Wimbo wa Darasa 'Muziki' Wafunika wa Diamond 'Salome'

$
0
0
Kulingana na jinsi watu walivyopokea wimbo mpya wa darasa 'muziki' katika maeneo mbali mbali nchini, wimbo wa Diamond wa 'Salome' umekufa kifo cha mende..yani hausikiki tena...

Yani kila mahali ni wimbo wa darasa tuuu, ila wa Diamond hausikiki tena...

Hakika darasa 'hupendagi ujinga', naona umeamua kumsomesha namba anayejiita Simba, na hii yote ni sababu ya kuanza kuimba 'matusi tu'...sifa za kijinga..ndio zinamponza..

Nakupa pongezi sana kaka kwa kuimba nyimbo nzuri..endelea kufunika..

Ukweli mchunguu...!

DONALD Trump Ashtukia Mchezo Mchafu Unaotaka Kufanywa na Boeing Ununuzi wa Ndege ya Rais

$
0
0

MAREKANI: Donald Trump ametangaza nia ya kusitisha uagizaji wa ndege 2 mpya za Rais(Air Force One). Adai bei iko juu na huenda imezidishwa.

Ndege hizo ambazo gharama zake ni takribani dola za Marekani bilioni 4 zinatengenezwa na Shirika la Uundaji wa ndege la Boeing.

Trump amesema anahisi bei imezidishwa na shirika hilo linataka kuzidisha faida isivyo halali

WAFANYABIASHARA wa Viungo vya Binadamu Wakamatwa

$
0
0

Utawala nchini Misri umewakamata madaktari, wauguzi na maprofesa wanaoshukiwa kuwa kwenye mtandao wa kimataifa wa biashara ya viungo vya binadamu.

Kukamatwa kwa takriban watu 25 siku ya Jumananne pia kuliwahusisha wale wanaonunua viungo hivyo.

Utawala pia ulipata mamilioni ya dola na dhahabu.

Ni kinyume cha sheria kununua viungo vya binadamu nchini Misri lakini umaskini husababisha watu wengi kuuza viungo vyao.

Shirika la kupambana na ufisadi lenye nguvu, linadai kuwa mtandao uliolengwa uliwajumuisha wamasri na waarabu na ulitumia fursa hali ngumu ya kuichumi ya watu kununua viungo vya watu na kisha kuviuza kwa faida kubwa.

MWIMBAJI Rich Mavoko Achekelea Wimbo Wake Kuchezwa Radio za Uingereza

$
0
0

Kokoro umekuwa wimbo wa kwanza katika career ya Rich Mavoko kuchezwa na vituo vya redio vya nchini Uingereza vikiwemo #BBCRadio #1Xtra na #CapitalXtra.

@Richmavoko ameiambia amesema kuwa hayo ni mafanikio makubwa kwake.
.
“Katika ndoto zangu nilikuwa nafikiria nije kufanya kitu ambacho kitatoka nje ya mipaka, kufika west, kufika south, kufika sehemu ambazo nawaona wasanii ambao nawatamani wanafanya kazi kubwa wanafika,” amesema.

Mavoko amesema Kokoro ambao amemshirikisha @diamondplatnumz, ni wimbo wenye ladha ambazo hajawahi kufanya lakini risk aliyoifanya imezaa matunda.
.
“Namshukuru Mungu nimeona matunda yake, BBC sijawahi kuchezwa haki ya Mungu. Nimetumiwa nikiwa huku Marekani nikasema noma noma,” ameongeza Mavoko kwa furaha kubwa.

Muimbaji huyo amesisitiza kuwa kwa sasa ana hasira kubwa zaidi ya kuhakikisha anafika katika masoko ambayo hakuwahi kufika kwa kuachia kazi kali zaidi.
.
“Nataka niingie kwa nguvu,” anasema. “Nataka niingie nikiwa nachop muziki wa aina tofauti tofauti. Bado nitastick kwenye Bongo Flava kwasababu ndio muziki wa nyumbani, ndio maana #Kokoro home itafanya vizuri, nje itafanya vizuri kwasababu naweza nikafanya vitu vingi kwenye wimbo mmoja.”

UGOMVI wa CUF Wachukua Sura Mpya, Upande wa Lipumba na Maalim Seif Watangaza Kusimamisha Wagombea Kivyao

$
0
0

Mgogoro wa uongozi unaoendelea ndani ya chama cha CUF huenda ukaathiri ushiriki wake kwenye uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Januari 27 baada ya pande zote mbili zinazosigana kujiandaa kuteua wagombea.


Mbali ya mgogoro huo kuhofiwa kukiathiri chama pengine hadi kusababisha wagombea wake kuzuiwa, pia unaweza kuudhoofisha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).


Habari kutoka ndani ya chama hicho zinasema upande wa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Msajili wa vyama vya siasa uko kwenye maandalizi ilhali ule wa Katibu Mkuu, Seif Sharrif Hamad unatarajiwa kukutana na watendaji wa chama kujadili ushiriki wao.


Profesa Lipumba aliyeiongoza CUF tangu mwaka 1995, alijiuzulu kwa hiari uenyekiti wake Agosti 2015 lakini siku chache kabla ya CUF kuitisha mkutano Agosti mwaka huu wa kujadili barua yake, aliandika barua ya kutengua kujiuzulu na akarejea kazini.


Siku ya mkutano mkuu uliofanyika Ubungo Plaza, wajumbe waliridhia kujiuzulu kwake lakini walipoingia kuchagua mrithi wake, wafuasi wa Profesa Lipumba walivamia mkutano na kuuvuruga hali iliyosababisha baadaye kusimamishwa kwake.


Alipoulizwa jana namna CUF yenye mgogoro itakavyoshiriki uchaguzi wa madiwani katika kata 22 Bara na ubunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF, Julius Mtatiro alisema wapo katika mikakati kuhakikisha wanashiriki kikamilifu.


Mtatiro alisema muda wowote kuanzia sasa Katibu Mkuu, Maalim Seif atakutana na watendaji wa chama kujadili kwa kina suala hilo na kutoa maelekezo.


“Tutashiriki vizuri na niwaweke wazi Watanzania kuwa shughuli za chama zinaendelea kama kawaida hivyo kamati za utendaji zitatimiza wajibu wake wa kuwapitisha wagombea watakaojitosa kwenye kinyang’anyiro,” alisema.


Kuhusu Profesa Lipumba, Mtatiro alisema, “Hatuwezi kufanya kazi na mtu wa CCM kumsogeza karibu yetu ni kumleta atuharibie chama jambo ambalo hatuwezi kuliruhusu. Ingekuwa lile suala la kujiuzulu aliteleza tungemwelewa na kumsamehe lakini inavyoonekana yupo kwenye mipango yake katu hatuwezi kumuweka karibu.”


Lakini Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF anayemuunga mkono Lipumba, Abdul Kambaya alisema, “Tuna kikao leo (jana) upande wa Bara chini ya Mwenyekiti Profesa Lipumba kujadili suala hilo la uchaguzi, kuhusu upande wa Zanzibar sifahamu chochote.”


Akizungumzia uchaguzi huo mdogo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema upande wa Zanzibar, Salum Mwalimu alisema Ukawa utakuwa bega kwa bega na CUF katika uchaguzi huo kwani wanaitambua kuwa iko moja si mbili kama inavyotengenezwa na watu wasiopenda maendeleo ya chama hicho.


“Tunatambua na kuheshimu uamuzi wa wanachama na viongozi halali wa chama, CUF iko moja, kama kuna mtu anatengeneza propaganda alifanya hivyo akiamini anakwenda kukiua chama ajue bado kinaendelea kusimama,” alisema.


“Pale atakaposimamishwa mgombea kutoka chama hicho Ukawa tutamuunga mkono na kumpigania kuhakikisha anashinda. Tunaamini pia nao watafanya hivyo akisimamishwa mgombea wa Chadema, ”alisema Mwalimu


Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Juju Danda alisema mgogoro wa CUF hautaleta changamoto yoyote kwenye Ukawa kwa kuwa wanamtambua katibu mkuu. Alisema Ukawa unamtambua Maalim Seif na ndiye mtendaji mkuu wa chama hivyo watakuwa tayari kushirikiana naye katika kila jambo.


Kuhusu mpasuko unaoendelea ndani ya chama hicho, Danda alisema suala hilo waachiwe CUF wenyewe ndiyo watakaoamua. “Mtendaji Mkuu wa chama ni katibu si Mwenyekiti, na kwa kuwa tupo pamoja na Maalim hatuoni changamoto yoyote yeye ndiye anayesimamia uteuzi na tunategemea mambo yatakwenda sawa,” alisema.


Katika hatua nyingine hatima ya Jaji Sekieti Kihiyo anayesikilkiza kesi ya CUF kujitoa sasa itajulikana Desemba 14 atakapotoa uamuzi wa maombi ya wadai kumtaka ajiondoe.


Jaji Kihiyo alipanga kutoa uamuzi wa maombi hayo dhidi yake jana baada ya kumaliza kusikiliza hoja za pande zote katika kesi hiyo, ambazo zilizua mvutano mkali baina ya mawakili wa wadai kwa upande mmoja na mawakili wa wadaiwa pamoja na Jaji Kihiyo kwa upande mwingine.


Kesi hiyo imefunguliwa na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamnini wa CUF, dhidi ya Profesa Lipumba, Naibu Katibu Mkuu wa chana hicho Bara, Magdalena Sakaya pamoja na wanachama wengine tisa waliosimamishwa uanachama wa chama hicho.


Wengine ni Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, ambaye ndiye mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), ambaye ni mdaiwa wa pili.


Kesi hiyo ilitarajiwa kusikilizwa jana lakini kabla ya kuendelea, kiongozi wa jopo la mawakili wa wadai, Juma Nassoro aliieleza mahakama kuwa wadai wameandika barua wakimtaka jaji ajiondoe kuendelea na kesi hiyo kwa maelezo hawana imani naye.

SHILOLE na Mpenzi Wake Mpya Wavujisha Video Wakidendeka..Mashabiki Wauzika

$
0
0
Katika mitandao ya kijamii wiki hii imesambaa video inayomuonyesha msanii wa muziki, Shilole akiliwa denda ya kijana ambaye jina lake halikutambulika mara moja kitu ambacho kimewakera mashabiki wake.

Hii imekuwa ni tabia ya mastaa wengi kuvujisha video zao za siri hali ambayo inasababisha taharuki katika mitandao ya kijamii.

Baada ya kusambaa kwa video hiyo mashabiki wake wameonyesha kuchukizwa na kitendo hicho. Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki hao.

elizabethsommy
Shilole huna stress lkn my Dada duu cjawahi yaona haya kwako veeeepeeeeeee my sister wanaumeee haoo

zam_nasso
Hili lidada ni hayawani sana nawaonea huruma watt wake wanaona uchafu wa mama yao.

Da_dija
Afu aftr deiz utasikia wanajitia kupanick y hzo video zimerushwa without their willin’ wkt they keep a poz wanapojirecord, then hawachelewi kusema wamebakwa. anyways nilikuwa nauliza hizi sheria za mitandaoni zipo au zimetumbuliwa!!!!????.

ishaa_mashauzy
Eeeeee mungu huku tunakoendea mtatuonyesha hadi mkiwa mnakwichkwich alafu @shilolekiuno_badgirlshishi siuna watt wakike wakubwa unafikiri hawaoni haya looooooooooh

saratz
Anapenda vitoto uyu Dada tena bora kiwe kitoto cha umri wake sasa iki ni kidogo kuliko yeye VIDEO:

PAUL Makonda Kuwashindanisha Christian Bella na Banana Zoro Kuimba Live....Bella Ajigamba Kuchukua Mil 50 za Zawadi

$
0
0
Mkali wa masauti Christian Bella amejinadi kuwa atamshinda muimbaji mkongwe Banana Zorro katika pambano la kuimba live lililoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.


RC Makonda wiki moja iliyopita aliwataka wasanii hao wawili kuandaa show ya pamoja ili washindane kuimba live na mshindi atampatia tsh milioni 50.

Akiongea na Bongo5 wiki hii Christian Bella, amedai hana shaka na pesa hizo kwani anajua atamshinda Banana na kuondoka na kitita kicho kikubwa cha pesa.

“Tunamshukuru Mh Paul Makonda ni wazo zuri sana kwa kutujali vijana, kwa kujali vipaji na kuvithamini,” alisema Bella. “Kwahiyo sisi tunaiandalia mazingira ili kuangalia itakuwaje kwa sababu tunatakiwa kuwa serious sana lakini tumeshapanga itakuwa mwezi wa pili au wiki ya mwisho ya mwezi Januari,”

Aliongeza, “Kwa upande wangu mimi sasa najiandaa, mimi sitaruka sarakasi bali nitaperform vizuri ngoma zangu zote kali, niimbe zaidi, nitafanya performance ya hasira ili nipate hiyo hela. Lakini mimi naamini hiyo hela niyakwangu hata kama Banana Zorro ni mkali na anaimba vizuri, mkongwe, kipaji lakini naamini mimi nitachukua hiyo hela,”

YOUNG Dee Aeleza Sababu ya Kufanya Video na Mpenzi wake Tunda

$
0
0
Rapa Young Dee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya 'Furaha' amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa iliyompelekea yeye kufanya kazi na mwanamitindo Tunda

Young Dee akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio alisema kuwa aliamua kufanya video hiyo na Tunda kwa sababu kwanza ni mtu ambaye yupo naye karibu hivyo kwake haikuwa kazi ngumu kumuitaji lakini pia adai alikutana na wanamitindo wengine ambao kwake walikuwa wakubwa sana akamua ngoja afanye na mtu wake wa karibu.

"Kwanza unajua sijafanya muda mrefu video ya mapenzi, hivyo nilifikiria nikaona Tunda ni mtu sahihi kwanza ni mtu wangu wa karibu hivyo nikaona akisimama yeye kwenye video hii ataleta maana zaidi kwa kile nilichokuwa nimelenga kukifikisha kwa jamii, maana nilikutana na wanamitindo wengine kwangu walikuwa wakubwa sana. Lakini pia nikiwa na Tunda muda wote kwangu ni furaha tu" alisema Young Dee.

Mbali na hilo anadai kuwa kipindi ambacho aliachia wimbo wake wa 'Hands up' ni kama alikuwa amewahi sana kwani alikuwa anajiona anahitaji kupumzika kwanza, kujijenga upya ili kuingia kwenye ushindani kweli na kufanya kazi rasmi.

"Kipindi kile kiukweli niliwahi sana maana tulikuwa na mizuka sana lakini kuna siku nilipost picha Instagram mimi mwenyewe nilijiona nimekonda kweli, nikaona nahitaji kupumzika, kulala vizuri na kufanya mazoezi ili nikirudi nirudi kweli ndiyo kama sasa nipo fiti kwa ushindani ndiyo maana nimekuja na hii kazi ya 'Furaha'" alisema Young Dee

MAREHEMU Wanaodaiwa Mikopo HESLB, Kusamehewa

$
0
0
Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) pamoja na na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imejikuta ikitoa taarifa zinazokinzana kuhusu wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu ambao tayari wamekwisha poteza maisha.

Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya amesema wanafunzi ambao wamefariki huku wakiwa na deni la Bodi ya Mikopo wanasamehewa madeni yao kwa kuwa hawawezi kupatikana tena.
Manyanya alitoa ufafanuzi huo hivi karibuni wakati akiwa katika kipindi cha Kikaangoni kinachoruka kupitia ukurasa wa facebook wa EATV, ambapo alisema suala la kufariki ni mipango ya Mungu, na hakuna mtu anayeweza kujiua makusudi ili kukwepa kulipa deni lake.

Akifafanua zaidi wakati akijibu swali la mmoja kati ya wananchi waliouliza maswali, Manyanya alisema serikali ina uwezo wa kujiridhisha kuwa mdaiwa fulani amefariki kwa kufuatilia nyaraka muhimu, na kuwataka wadaiwa wasitumie msamaha huo kujisingizia vifo

"Mimi ndiyo serikali, unapaswa kuchukua taarifa yangu kwamba waliofariki wakati wanadaiwa, watasamehewa madeni yao, naamini hakuna mtu atajiua makusudi ili kukwepa, tukibaini kama kuna kughushi vifo, basi hatua za kisheria zitachukuliwa" Alisema Manyanya.

Hivi karibuni mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo akizungumza na East Africa Radio alisema kuwa madeni ya wadaiwa waliofariki yatalipwa na wanafamilia, wadhamini pamoja na ndugu walio hai.

MWIMBAJI Darasa Afichua Siri ya Nyimbo zake Kupendwa...

$
0
0

Muimbaji huyo ameliambia gazeti la Mtanzania kuwa baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye nyimbo za ujumbe ndio akaangalia ni kitu gani mashabiki wanataka akaamua kubadilika.

“Mwanzo nilikuwa nikitoa nyimbo zenye vionjo vyenye ujumbe wa kutosha lakini hazikuwa zikipokelewa sana ila nilipokaa na kufikiria zaidi, nikatambua nini mashabiki wanataka na ndiyo maana muziki wangu upo juu sana tofauti na zamani,” amesema.

Rapper huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wa ‘Muziki’ uliogeuka kama wimbo wa taifa kwa sasa.

ZARI Athibitisha Yeye na Mama Mkwe Wake Bado Zinaiva

$
0
0
Kuliwahi kuwepo uvumi kuwa Zari na mama yake Diamond Platnumz hawaelewani.

Tetesi hizo zilikuwa kubwa zaidi hivi karibuni baada ya Bi. Sandra kumchunia Zari kumpongeza kwenye siku yake ya kuzaliwa lakini akamtumia salamu ex wa mwanae, Wema Sepetu.

Lakini tangu Diamond na mama yake waende Pretoria, Afrika Kusini kwaajili ya kumwangalia Zari aliyejifungua Jumanne hii mtoto wa kiume, mambo yameonekana kuwa shwari.

Kwanza Diamond aliweka picha kwenye Instagram akiwa na wanawake hao wawili muhimu maisha mwake na mama yake kuirepost. Kwenye picha hiyo Diamond aliandika:
 Earlier today with my Favorite ladies, the ladies behind my success….. @kendrah_michael 💞 @zarithebosslady.”

Jumatano hii Zari ameweka picha na hiyo juu na kuandika: Snacking with mama in law @kendrah_michael what a laid back & chilled day.”

Ni furaha na amani tu kwenye familia ya Chibu kwa sasa.
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images