Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

BEKI Aliyenusurika Ajali Ya Ndege Iliyowaua Wabrazil Aanza Kutembea

$
0
0

Alan Ruschel, aliyesalimika kwenye ajali ya ndege iliyoua watu zaidi ya 70 wakiwemo wachezaji wa timu ya Chapecoense ya Brazil ameanza kutembea.

Ruschel ameanza kutembea kwa msaada wa mmoja wa madaktari na amewatumia salami mashabiki wa Chape na familia yake kwamba anaendelea vizuri.


 Beki huyo wa Chape amekuwa akiendelea kupata matibabu baada ya kuvunjika mifupa kadhaa mwilini mwake.

Wakati Ruschel anaendelea matibabu katika Kliniki ya Somer Clinic katika mii wa Rionegra, Colombia, miili ya wachezaji wa Chape ilirejeshwa Brazil kwa ajili ya mazishi.


Walipata ajali wakiwa njiani kwenda Medellin nchini Colombia kucheza mechi ambayo mwisho, imeamuliwa timu hiyo ipewe ubingwa.

MAMLAKA ya Hifadhi Ngorongoro yaanza Kujitetea Kuhusu Kupotea Kwa Faru John

$
0
0
Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha umesema umeanza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu la kutaka kuwasilisha nyaraka zote za kumhamisha Faru ajulikanae kama John na maelezo ya kupotea kwake.

Akizungumza na TBC, Mhifahi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt Fedrick Manonge amesema japo amepewa muda mfupi sana wa kuwasilisha taarifa hizo lakini wanajitahidi kuzikamilisha.

“Kwahiyo yeye alimuagiza waziri wa maliasili ni anataka nyaraka husika na anataka maelezo ya kilichotokea. Kwahiyo kwasababu inakuwa ngumu sana kusema details zingine kwasababu ilisemwa na nyie mlisikia hakukuwa na information za kumridhisha mheshimiwa waziri mkuu ndiyo maana akatoa hayo maelekezo. Kwahiyo mi nadhani kimsingi nikusubiri matokeo ya huo uchunguzi ambao kwa kweli ametoa siku chache sana, serikali ya awamu ya tano haina vificho eeh itaonekana wazi kilichotokea,” alisema Manonge.

Hivi karibuni waziri mkuu akiwa katika ziara ya kiserikali mjini Arusha alitaka kupata nyaraka za kumhamisha Faru John katika hifadhi hiyo.

MAOFISA wa Man United Waanza Kukerwa na Tabia za Kocha Mourinho

$
0
0
Maofisa wa klabu ya soka ya Manchester United inasemekana kwamba wameanza kuchoshwa na mwenendo na tabia za kocha wao Jose Mourinho.

Mourinho alisimamishwa kuwepo katika benchi la ufundi ikiwa ni baada ya kutolewa dimbani na muamuzi Jon Moss walipomenyana na West Ham kwenye Ligi Kuu, Mourinho alitolewa baada ya kufanya kitendo cha kuipiga teke chupa akipinga mchezaji wake Paul Pogba kuoneshwa kadi ya njano kwenye mechi hiyo.

Sasa hivi kuna habari zikatanabaisha kwamba maofisa wa Manchester wanatoa malalamiko ya kichinichini kwa kitendo cha kocha huyo kutuhumiwa kwa makosa ya Chama cha Kandanda cha England kwa mara ya 3 kwenye kipindi cha mwezi mmoja tu.

WASANII Watano Matajiri Kupita Wote Afrika Watajwa..Mtanzania Mmoja Yupo Kwenye List

$
0
0
Mara nyingi tumezoea kuona list za wasanii wakubwa wakitajwa kuingiza pesa nyingi zaidi Afrika, wiki hii imetoka list iliyoandikwa na eDaily kupitia ripota Brian Okoth ambayo imewataja wasanii watano kutoka Afrika wanaotajwa kuingiza pesa nyingi zaidi mwaka 2016.

5. Diamond Platnumz (Tsh. Bilioni 9,665,923,190.55)

Related imageMtanzania Diamond Platnumz huenda akawa msanii anayezungumzwa au kutajwa sana kwasasa barani Afrika kutokana na headlines anazotengeneza kila siku, mikataba yake na makampuni makubwa kwenye kazi zake pia inazidi kumuweka sehemu nzuri kifedha.

Hakuna shaka kwamba Diamond ni mmoja kati ya wasanii wanaoingiza pesa nyingi kupitia muziki wao kwasasa, na hili litaondoa utata kuhusu kiasi cha pesa alichotajwa kuwanacho staa huyu wa single ya Make Me Sing ambaye aliwahi kuzungumza na E!TV Jumapili ya, June 26 mwaka huu na ikaelezwa kuwa anamiliki pesa zinazozidi kiasi cha dola Milioni Mia Nne za Marekani (Zaidi ya Bilioni 9 za Tanzania).

Kiasi hicho cha pesa hakijaja tu kama suprise kwa Diamond, ambaye anatajwa kuwa ndiye msanii anayelipwa pesa nyingi zaidi kwenye show au event yoyote anayotakiwa kuhudhuria nchini Tanzania na pengine Afrika Mashariki kwasasa.

Pesa nyingi zinaelezwa kuingia kupitia shows alizofanya ndani ya Tanzania, East Africa na nje ya Afrika. Diamond Platnumz pia amekuwa balozi wa makampuni mengi makubwa ya biashara ikiwemo Vodacom, Cocacola, DSTV, Uber Taxi na Red Gold.

Ziko taarifa kuwa Diamond Platnumz huchaji si chini ya shilingi milioni 25 kwa show moja ya kawaida akiwa Tanzania, pia gharama hizo hufikia shilingi milioni 50 na kuendelea akiitwa na kampuni ya biashara na kama akiitwa nje ya Tanzania basi gharama zake huanzia shilingi milioni 200 na kuendelea.

Vyanzo vingine vya mapato ni pamoja na mauzo ya miito ya simu ambayo inaelezwa hakuna msanii yeyote Afrika Mashariki anayefikia mauzo yake kwenye ukanda wa maziwa makuu, pia anamiliki akaunti ya Youtube ambayo ipo kwenye list ya chaneli 10 zinazoangaliwa zaidi barani Afrika.

Hivi karibuni Diamond Platnumz ameingia kwenye biashara za kununua nyumba za zamani na kuzifanyia ukarabati ambapo huzipangisha, kitu kinachotajwa kumuingiza mkwanja mrefu zaidi jijini Dar es salaam, mbali na kumiliki record lebel yake ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo kwa mujibu wake Diamond aliwahi kusema wamesaini deal ya zaidi shilingi Bilioni 2 na lebel ya Universal Music Group ya Marekani ili kusambaza kazi za wasanii walioko chini yake ambao ni Rich Mavoko, Harmonize na Rayvany.

4. Wizkid (Tsh. Bilioni 25,676,809,453.47)

Kwa mujibu wa Infoguide Nigeria, mpaka kufikia December 2015 mwimbaji star Wizkid alikuwa anakadiriwa kumiliki kiasi cha dola Milioni  11.5 ambazo mpaka mwisho wa mwaka 2016 inaelezwa kuwa amefikisha dola Milioni 12.

Wizkid amekuwa na mikataba inayomuingizia pesa nyingi na makampuni kutoka Nigeria ikiwemo label yake ya Star boy Records aliyoianzisha mwaka 2010. Pia mwaka 2014 Wizzy alisaini deal ya kuwa balozi wa kampuni ya simu ya MTN ambao walimlipa zaidi ya shilingi milioni 300 na kampuni ya MTN rival Globacom ikapanda mara mbili ili kumtumia Wizkid kama balozi wao.

Deal hiyo ya miaka miwili inatajwa kumuingiza Wizkid zaidi ya shilingi milioni 900 kutoka kampuni ya Globacom na mwaka 2015 wakati akifanya sherehe ya kutimiza miaka 25 Wizkid alisaini upya mkataba wake na kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi.

Ukijumlisha kiwango cha pesa anachoingiza kutoa kwenye shows anazofanya, mauzo ya nyimbo zake, tuzo, zawadi pamoja na mikataba yake, inamuweka star huyo kwenye list wasanii wanaoingiza pesa nyingi zaidi nchini Nigeria. Zipo taarifa kuwa ili kuweza kumualika Wizkid aje kufanya show ya kampuni itakubidi umlipe si chini ya shilingi milioni 60.

Kumbuka pia mwezi August, 2015, WizKid alitajwa kwenye jarida la Forbes kama miongoni mwa mastaa 14 wanaoitangaza Afrika.

3. Davido (Tsh. Bilioni 30,502,418,406.03)

Kwa mujibu wa Nigerian Finder wameeleza kuwa Davido anamiliki utajiri unaofikia dola milioni 14 ambazo ni zaidi ya shilingi Bilioni 30 za Kitanzania.

Pamoja na kuzaliwa kwenye familia yenye uwezo mkubwa kifedha, hiyo haikumfanya Davido kurelax badala yake alitumia nafasi yake kama msanii kujenga jina lake na kufanya biashara inayomfanya kuingiza pesa nyingi kwenye akaunti zake.

Mwaka 2012, Davido alisaini deal na kampuni ya MTN TV kama balozi na akasaini deal nyingine na MTN Pulse kuwa muwakilishi wa kampuni hizo kwa kitita cha zaidi ya shilingi milioni 207 za Kitanzania, wakati huo huo mwaka 2014, Davido alilipwa zaidi ya shilingi milioni 341 kuwa balozi wa kampuni ya dawa za meno ya Close UP.

Pia Davido na kaka yake Adewale Adeleke wanamikili lebel ya muziki iitwayo HKN Music ambayo imekuwa ikiwaingiza pesa nyingi kupitia mauzo ya nyimbo za wasanii waliosaini lebel, mauzo ya albam pamoja mikataba ya matangazo.

2. Akothee (Tsh. Bilioni 132,683,540,000.00)


Huenda ikakushtua sana kutokana na jina la msanii huyu kutokua kubwa sana au kutofahamika sana kwa watu wengi, Mwimbaji Akothee kutoka Kenya anatajwa kuwa na utajiri unaofikia dola za Marekani milioni 61 ambazo ni zaidi ya shilingi za Tanzania Bilioni 132.

Mapema mwaka huu, mitandao ya habari za mastaa nchini Kenya iliripoti kuwa star huyo wa single ya Give It To Me alikuwa anamiliki zaidi ya shilingi za Tanzania Bilioni 8.

Akothee amekuwa akijishughulisha na biashara pamoja na kilimo huku chanzo kingine cha mapato kikitajwa kuwa ni fidia aliyolipwa kama talaka na mwanaume wa kizungu aliyeachana naye miaka kadhaa iliyopita.

1. P-Square (Tsh. Bilioni 277,752,822,639.34)




Wakiwa ni mastaa pekee kutoka Afrika kutajwa na jarida la Forbes mara mbili kwenye list ya wasanii wanaolipwa pesa nyingi zaidi Afrika, kundi la PSquare limeendelea kuweka rekodi ya kufanya shows za gharama kubwa kupita wasanii wote Afrika, huku wakipata mialiko kutoka kwa Marais wa nchi zaidi ya 5 na usisahau, mastaa hawa wanamiliki ndege binafsi.

Kwa mujibu wa jarida la watu maarufu la Forbes, mapacha hao Peter na Paul Okoye wanaounda kundia la P-Square wanamiliki utajiri wa zaidi ya dola za Marekani milioni 130 zinazotokana na mikataba ya kibiashara na makampuni mbalimbali, biashara za mafuta, mauzo ya muziki na shows wanazofanya.

HOFU Yatanda Binti Aliyechunwa Ngozi Karatu

$
0
0

HOFU imetanda wilayani Karatu katika Mkoa wa Arusha baada ya tukio la kwanza la uchunaji ngozi kuripotiwa katika mji mdogo wa Karatu.

Binti mdogo mwenye umri wa miaka tisa, ameuawa mjini Karatu baada ya kutekwa nyara na watu wasiojulikana wakati akielekea machungani na mifugo.

Mtoto huyo, Witness Andrew ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Darasa la Kwanza kwenye Shule ya Msingi ya Sumawe, alipatikana Jumatano usiku, akiwa tayari amekufa, baada ya kuripotiwa kupotea kwa zaidi ya saa 24 tangu alipoondoka nyumbani kwao akiwa anaswaga ng’ombe na mbuzi, Jumanne iliyopita.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kiwandani ambako mwili wa mtoto huyo ulipatikana, Alexander Lulu amesema maiti ta mtoto huyo ilikutwa ikiwa imetupwa shambani na baadhi ya viungo vikiwa vimenyofolewa pamoja na ngozi iliyochunwa na kuondelewa kabisa.

Witness pia alikutwa bila mguu, mkono na sehemu zake za siri na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Tloma wanadai ni masuala ya ushirikina. Mtoto huyo ndiye wa kwanza kuchunwa ngozi katika eneo la Karatu na tayari hofu imeanza kutanda hapa, watu wakihofia kuwa wachuna ngozi watakuwa wamevamia wilaya hiyo.

Baba ya marehemu, Andrea Paulo na Mama Paulina Petro wanasema mtoto wao alipotea tangu Jumatatu wiki hii alipotoka na mifugo kwenda kuchunga kwenye uwanda wa Tloma, lakini hakurudi nyumbani, na kwamba mifugo aliyokuwa nayo ilirejea yenyewe.

“Tulimtafuta mtoto kila mahali, lakini bila mafanikio, hata tulipoikuta maiti yake eneo la Kiwandani, tulishangaa maana tulishapita kwenye mashamba hayo mapema, lakini hatukumuona,” walisema wazazi.

Wanakijiji wa Tloma wanaamini kuwa mtoto huyo alitekwa na kupelekwa eneo jingine ambako ndiko alichinjwa kabla ya wauaji wake kumrudisha na kumtupa Kiwandani

SAKATA la Kuuawa kwa Faru John Lachukua Sura Mpya.......Watumishi Watano Watiwa Mbaroni

$
0
0

Maofisa watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wanaotuhumiwa kushiriki kumwondoa faru John kutoka katika Creta hiyo walikamatwa juzi kwa mahojiano ili kujua ukweli kuhusu mazingira ya kupotea kwake.

Hatua ya maofisa hao kukamatwa imekuja siku tatu baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuituhumu menejimenti, wafanyakazi wa NCAA na Baraza la Wafugaji (NPC) kuwa imejaa vitendo vya rushwa na wizi na asingeweza kuvumilia sakata la faru John ambaye alisema kuwa aliuzwa kwa Sh200 milioni kwenye Hoteli ya Grumet iliyo Hifadhi ya Serengeti na kuwa walipokea fedha za awali Sh100 milioni.

Waziri Mkuu alisema anataka kumwona faru huyo, nyaraka za kumhamisha na kama amekufa basi apelekewe hata pembe ofisini kwa kuwa anajua pa kuzipeleka.

Alisisitiza kuwa ikibainika kuna ambao wamekiuka taratibu watawajibika.

Habari za uhakika kutoka Ngorongoro, ambazo zimethibitishwa na Jeshi la Polisi zinasema kuwa maofisa hao watano wanashikiliwa katika kituo chao cha Ngorongoro kutokana na ushiriki wao kwa njia moja au nyingine.

Wanaoshikiliwa ni pamoja na Israel Naman ambaye alikuwa Kaimu mkuu wa idara ya uhifadhi wakati faru huyo akiondolewa.

Wengine ni Cuthbert Lemanya, ambaye alikuwa Mkuu wa Kanda ya Creta, Dk Athanas Nyaki ambaye anadaiwa kumdunga sindano ya usingizi ili aweze kubebwa.

Maofisa wengine waliokamatwa ni aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka ya Ngorongoro, Kuya Sayaleli na aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Ikolojia, Patrice Mattey.

Ofisa mmoja wa NCAA, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake jana alisema maofisa hao walikamatwa juzi jioni na jana walikuwa wanaendelea kuhojiwa.

“Tuiache serikali ifanye kazi kwani ni muhimu sana kujulikana ukweli wa tukio hili,” alisema ofisa huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo hakupatikana jana kuelezea tukio la kukamatwa maofisa hao, baada ya simu yake kupokelewa na msaidizi wake ambaye alieleza yupo kwenye kikao.

Lakini, ofisa wa mmoja wa polisi, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina kwa kuwa si msemaji alikiri kukamatwa maofisa hao kwa mahojiano.

Chanzo cha sakata
Akiwa katika ziara ya kikazi Ngorongoro, Waziri Majaliwa aliibua sakata la kuhamishwa kinyemela faru huyo na kudaiwa kupelekwa Grumet.

Waziri mkuu alitaka ukweli kuhusu upotevu wa John aliyeondolewa Creta na kupelekwa Grumet na kudaiwa kufa huku taarifa za kifo hicho zikifanywa siri.

Waziri Mkuu alitaka kupewa nyaraka zote zilizotumika kujadili kumuondoa faru na kuamua kumpeleka Grumet.

Waziri Mkuu alitoa hadi Desemba 8 (jana) awe amepata taarifa zote, ikiwamo ya daktari inayothibitisha kifo hicho na kwamba pembe za faru huyo zifikishwe ofisini kwake. Pia, Majaliwa alisema ikibainika wapo waliokiuka taratibu watawajibika.

RAIS Magufuli Ataja Mambo Yanayoikwamisha Tanzania

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameitaja rushwa kama changamoto sugu ambayo bado inaendelea kulitafuna taifa la Tanzania katika miaka yake 55 ya Uhuru.

Rais Magufuli ameitaja changamoto hiyo leo akati akiwaongoza watanzania katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanzania Bara ikiwa ni mara ya kwanza tangu aingie madarakani na kutaja changamoto nyingine kuwa ni tatizo la ajira pamoja na umasikini.

Akizungumza katika hotuba yake ya shukrani katika maadhimisho hayo ambayo yamefanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli, amesema kuwa serikali yake itaendelea kupambana na vitendo na rushwa na ufisadi, kwa ajili ya kuliletea taifa maendeleo.

Aidha Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa serikali itahikisha kuwa inaondoa uonevu hasa kwa wananchi wanyonge ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili ili kila mtanzania aweze kufaidika na matunda ya nchi yake.

Maadhimisho hayo ambayo kwa mujibu wa Rais Magufuli ndio ya mwisho kufanyika Jijini Dar es Salaam na kuanzia mwakani yataadhimishwa Dodoma, yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wastaafu na serikali pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali zenye uwakilishi hapa nchini.

VIDEO: Makomando wa JWTZ walivyoonyesha uwezo wao mbele ya Rais Magufuli

$
0
0
Leo  zimefanyika sherehe za maadhimisho ya 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru Dar es salaam, ambapo Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alikuwa mgeni Rasmi.

Mbele ya Rais Magufuli Makomando wa JWTZ walipata nafasi ya kuonyesha uwezo wao ikiwamo namna ya kukabiliana na adui.

Tazama hapo chini:

PICHA: Wema Sepetu ‘Alivyohost’ Party Kwenye Club Yenye Strippers, Nairobi

$
0
0
Kuna njia nyingi mtu maarufu anaweza kuingiza mkwanja, moja wapo ni appearances. Watu wenye majina makubwa hulipwa fedha nyingi kwa kutokea kwa muda mfupi tu kwenye club – na si lazima awe mwanamuziki.

Alhamis hii, Wema Sepetu ameingiza mkwanja wa kutosha kwa kuhost shughuli ya ulaji bata iliyopewa jina la Powerball Thursdays, kwenye kiota cha raha kilichopo Nairobi, Kenya, XS Millionaires Club.

Kiota hicho kina kila aina ya anasa, hadi strippers au kwa lugha ya heshima kiasi waweza kuwaita pole dancers. Na kwakuwa Wema si wa mchezo mchezo, XS Millionaires palitapika jana.



VIDEO ya Diamond Yaweka Rekodi Mpya Kenya...Yaongoza Kutazamwa zaidi na Wakenya Youtube

$
0
0
Video ya wimbo wa Diamond Platnumz aliomshirikisha Raymond, Salome, ndiyo video ya muziki iliyotazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube nchini Kenya, kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, kupitia takwimu ilizozipata.

BBC Swahili wamedai kuwa kwenye orodha ya nyimbo 10 kutoka duniani kote, nyimbo za Tanzania zimetazamwa zaidi. Takwimu hizo zinadhihirisha jinsi ambavyo Wakenya wanapenda muziki wa Bongo Flava kuliko nchi nyingine yoyote ukitoa Tanzania yenyewe.

Hadi sasa, Salome ina views zaidi milioni 9.8 kwenye mtandao wa Youtube.

Hii ni orodha kamili:

Salome – Diamond Platnumz na Raymond
Work – Rihanna na Drake
Bado – Diamond Platnumz na Harmonize
Sauti Sol – Unconditionally Bae, na Alikiba.
Work from Home – Ty Dolla Sign na Fifth Harmony
This is What You Came For – Calvin Harris
Kwetu – Raymond
Cheap Thrills – Sia na Sean Paul
Pillow Talk – Zayn
Ain’t Your Mama – Jennifer Lopez

TAARIFA Kuhusu Usalama Wa Dawa Aina Ya “Diclofenac” Na “Diclopar

$
0
0

TAARIFA KWA UMMA    28  Oktoba, 2016
USALAMA WA DAWA AINA YA “DICLOFENAC” NA “DICLOPAR”

1. TFDA inajukumu la kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

2. Hivi karibuni, TFDA imepokea taarifa ya kuwepo kwa hofu juu ya usalama wa dawa aina ya “Diclofenac” kupitia mitandao ya kijamii kama ilivyojitokeza mwaka  2013.

3. Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inapenda tena kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

a. Diclofenac ni dawa iliyoko kwenye kundi la dawa zinazojulikana kitaalam kama “Non – Steroidal Anti-inflammatory Drugs” (NSAIDs) ambazo hutumika kutuliza maumivu na kuondoa uvimbe unaosababishwa na magonjwa mbalimbali kama magonjwa ya viungo, mifupa, uvimbe wa fizi namaumivu ya kichwa.

b. Mamlaka imesajili dawa yaDiclofenac kutoka makampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi baada ya kutathmini ubora, usalama na ufanisi wake na hivyo dawa ya Diclofenacinayotumika nchini ni salama kwa matumizi ya binadamu. Aidha, tunapenda kusisitiza kuwa dawa yenye jina la kibiashara la Dicloparina mchanganyiko wa viambato hai vya Diclofenac na Paracetamolimesajiliwa na TFDA na ni salama kwa matumizi ya binadamu.

c. Hata hivyo Diclofenac, kama ilivyo kwa dawa nyingine, ina madhara yanayofahamika ikiwa ni pamoja na kusababisha vidonda vya tumbo, kuharisha, kutapika na kuwashwa mwili.

d. Pamoja na madhara yaliyoainishwa hapo juu, Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa ya nchi za Umoja wa Ulaya(European Medicines Agency yenye makao yake jijini London, Uingereza)ilitoa tahadhari kwamba watu wenye matatizo  ya moyo na shinikizo la damu, kisukari, waliowahi kupata kiharusi, wenye lehemu (cholesterol) nyingi kwenye damu, mshituko wa moyo na wanaovuta sigara wanaweza kupata matatizo kwenye moyo na mfumo wa damu ikiwa watatumia Diclofenac kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu.

4. Kufuatia taarifa hiyo, sanjari  na mifumo ya ufuatiliaji wa madhara yatokanayo na dawa nchini, TFDA inaendelea kufuatilia madhara yatokanayo na dawa hii kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kitaalam ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Aidha, tunawakumbusha watoa huduma za afya kutoa taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa kwa kujaza fomu maalum zinazopatikana katika vituo vyote vya afya nchinipamoja na kutumia mfumo mpya wa Kielektroniki unaopatikana katika simu za mkononi aina ya “Android” kupitia anuani ya mtandao: www. tfda.go.tz/adr

5. Mamlaka inashauri watoa huduma za afya nchini na wagonjwa kuchukua tahadharizamadhara haya hasa kwa watu wenye magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kisukari, wenye lehemu nyingi kwenye damu na wanaovuta sigara ikiwa ni pamoja na kutumia dawa mbadala.

6. Vile vile wananchi wanashauriwa kuepuka matumizi holela ya dawa bila kupata ushauri wa kitaalam ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)

ALICHOSEMA Mbwana Samatta Baada Jina lake Kutajwa Kwenye Wimbo wa Darasa na Mavoco

$
0
0

Baa ya jina lake kutajwa kwenye nyimbo za wasanii wa Bongo Flavor, mshambuliaji wa kibongo anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji amesema kwake ni heshima kubwa kuwepo kwenye nyimbo za wasanii na inaonesha ni namna gani wanavyothamini kitu anachofanya.

Star huyo wa soka la Tanzania ametajwa kwenye nyimbo mpya za Darasa (Muziki) na Rich Mavoko (Kokoro) ambazo kwa sasa zinafanya vizuri kwenye soko la muziki.

“Wasanii wakubwa kama hao wanapokuzungumzia na kukutaja kwenye nyimbo zao ni jambo la kujivunia, ni suala zuri na nimejisikia poa. Nimejisikia faraja yani moyo wangu umekuwa baridi, kumbe kuna kitu nafanya wanakipenda kwa hiyo fresh kabisa,” amesema Samatta amabye ame-assist goli moja lililofungwa na Heynen katika mchezo wa Europa League dhidi ya Sassuolo uliomalizika kwa Genk kupata ushindi wa magoli 2-0 ugenini.

“Yani hizo ndio ngoma zangu kwa sasahivi zilizonishika kwa kiasi kikubwa, nasikiliza muda mwingi hata nikiwa naenda kwenye game nasikiliza nazisikiliza hizo ngoma.”

RAIS Magufuli Atoa Msamaha Kwa Wafungwa 5,678 Katika Maadhimisho Ya Miaka 55 Ya Uhuru Wa Tanzania Bara

$
0
0

Katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe  9 Disemba, 2016 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:-

(i) Wafungwa wote wamepunguziwa moja ya sita (1/6) ya vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2 (i-xx).


(ii)Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, KIFUA KIKUU (TB) na SARATANI (CANCER) ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa ambao wamethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.


(iii)Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi ambao umri huo umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.


(iv)Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.


(v)Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili (Physical disability and mental disability) ambao ulemavu huo umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.


2.Aidha, Msamaha huu wa Mheshimiwa Rais hautawahusu wafungwa wafuatao:-


(i)Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa.

(ii)Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na adhabu hiyo kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha au kifungo gerezani.

(iii)Wafungwa waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani.


(iv)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na usafirishaji na matumizi ya madawa ya kulevya kama vile cocaine, heroin, bhangi n.k.


(v)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na uombaji, upokeaji au utoaji rushwa.


(vi)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya unyang’anyi na unyang’anyi wa kutumia silaha au kujaribu kutenda makosa hayo (robbery with violence, armed robbery and attempt robbery).


(vii)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kupatikana na silaha, risasi au milipuko isivyo halali (firearms, ammunitions and explosives).


(viii)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya shambulio la aibu, kunajisi, kubaka na kulawiti, au kujaribu kutenda makosa hayo.


(ix)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa kosa la kuwapa mimba wanafunzi wa Shule za Msingi na Shule za Sekondari na ambao walitenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.


(x)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya wizi wa magari na pikipiki au kujaribu kutenda makosa hayo.


(xi)Wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya Sheria ya Bodi ya Parole (Act. No. 25/1994) na Sheria ya Huduma kwa Jamii (Act. No. 6/2002).


(xii)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao.


(xiii)Wafungwa waliowahi kupunguziwa kifungo na Msamaha wa Mheshimiwa Rais na bado wangali wanaendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.


(xiv)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kupata masomo.


(xv)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la utekaji wa watoto, kupoka na kufanya biashara ya binadamu (Human Trafficking).


(xvi)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kukutwa na viungo vya binadamu.


(xvii)Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kujihusisha na  usafirishaji wa nyara za Serikali na ujangili (Poachers).


(xviii)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya       wizi/ubadhirifu wa fedha za Serikali.


(xix)Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kutoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi halali.


(xx)Wafungwa walioingia gerezani baada ya tarehe 9/10/2016.


3.Wafungwa wapatao 5,678 watafaidika na msamaha huu baada ya kupunguziwa1/6 ya vifungo vyao ambapo 1,340 wataachiliwa huru na wafungwa 4,338 watanufaika na kubaki gerezani wakitumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.



 Ni mategemeo ya Serikali kwamba watakaoachiliwa huru watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.


Imesainiwa na;

Meja Jenerali  Projest  Rwegasira

KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

9/12/2016

TIMU ya Mbwana Samatta KRC GENK Yaibuka na Ushindi wa Kishindo na Kushika Nafasi ya Kwanza

$
0
0
Baada ya kuahirishwa kwa mchezo wa Europa League kati ya Sassuolo ya Italia iliyokuwaicheze na KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta kwa sababu ya hali ya hewa ya uwanja kuwa na ukungu kiasi wachezaji kutoweza kuonana vizuri jana December 8.

Mchana wa December 9 2016 ulichezwa mchezo huo wa mwisho wa Kundi F katika uwanja wa Mapei Italia, KRC Genk imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli yakifungwa na Bryan Heynen dakika ya 58 baada ya kupewa pasi na Samatta na goli la pili lilifungwa na  Leandro Trossard dakika ya 81.

Matokeo hayo yamewafanya KRC Genk kuongoza Kundi F kwa kufikisha jumla ya point 12 wakifuatiwa na Athletic Bilbao ya Hispania wenye point 10, KRC Genk na Athletic Bilbao wamefanikiwa kutinga hatua ya 32 bora ya michuano hiyo, bado haijajulikana na atacheza na nani hadi droo itakapochezeshwa.

UFAFANUZI wa Ben Pol Kuhusu Kudaiwa Kuwa Mapenzini na Snura

$
0
0
Kama unakumbuka moja ya tukio kwenye tour ya Fiesta 2016 ambalo lilimake headlines ni pamoja na ishu ya Benpol na Snura kudaiwa kuwa mapenzini na Snura aliwahi kukiri kuwa kweli yuko mapenzini na Ben Pol ambapo alizungumza maneno haya……..

’Ben Pol Dodoma ni nyumbani kwao na mimi ni ukweni ndio maana alichukuwa nafasi hiyo ya kunitambulisha kwa ndugu zake na familia, Ben Pol alinipandisha kwenye stage kunitambulisha ndio ikatokea kitu kama kile sio kwamba tulifanya show pamoja mimi na yeye hapana …’ – Snura
Ben Pol ambaye ametoa ufafanuzi kuhusu ishu nzima ilivyokuwa ….
‘Unajua ile ilikuwa arts tulitengeneza tu sanaa fulani ya stage na haikuwa skendo wala haikuwa kiki, kuhusu kumtambulisha Dodoma, hapana wazazi wangu wenyewe hawapo Dodoma wako Dar es salaam’ – Ben Pol

MASTAA wa Tanzania Wema Sepetu, Alikiba na Wengine Walivyoshinda Tuzo za ASFAS 2016 Uganda

$
0
0
Usiku wa December 9 2016 Kampala Uganda ndio siku ambayo zilifanyika zile tuzo za fashion zinazojulikana kama Abryanz Style & Fashion Awards (ASFA 2016), kumbuka hizo ni tuzo ambazo zilikuwa zinahusisha mastaa mbalimbali Afrika wakiwemo mastaa wa Tanzania.

Tuzo zilitolewa na mastaa wa Tanzania kama Vanessa Mdee alifanikiwa kushinda tuzo ya (The Most Stylish Artist East African Female), Alikiba akichukua tuzo ya (The Most Stylish Artist East Africa) huku mrembo Wema Sepetu akishinda tuzo ya Best Dressed Celebrity East Africa Female.


List ya washindi wa tuzo za ASFA 2016

Humanitarian award – Millen Magese (Tanzania)
Best Dressed Celebrity West Africa – Deborah Vanessa(Ghana)
Continental Style & Fashion Influencer Female – Bonang Matheba (South Africa)
Continental Style & Fashion Influencer Male – David Tlale (South Africa)
Fashion Designer Of The Year UG – Anita Beryl (Uganda)
Fashion Designer Of The Year East Africa – Martin Kadinda (Tanzania)
The Most Stylish Artiste in Uganda – Eddy Kenzo (Uganda)
The Most Stylist Artiste East Africa Female – Vanessa Mdee (Tanzania)
The Most Stylish Artiste East Africa – Alikiba (Tanzania)
The Most Stylish Couple – Annabel Onyango na Marek Fuchs (Kenya)
Fashionista Of The Year Male – Abduz (Uganda)
Fashionista Of The Year East Africa  – Hamisa Mobetto (Tanzania)
Most Fashionable Music Video – Bebe Cool (Uganda)
Best Dressed Celebrity East Africa Female – Wema Sepetu (Tanzania)
Best Dressed Celebrity East Africa Male – Jamal Gaddafi (Kenya)
Most Fashionable Music Video Africa – AJE – Alikiba (Tanzania)
Best Dressed Media Personality/Entertainer – Idris Sultan (Tanzania)

TAARIFA ya Kifo Cha faru John yakabidhiwa Kwa Waziri Mkuu

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea taarifa inayoelezea utaratibu uliotumika kumhamisha faru John kutoka Hifadhi ya Ngorongoro kwenda Sasakwa Black Rhino Sanctuary iliyoko kwenye Hifadhi ya Grumeti.

Akizungumza katika kikao kilichofanyika nyumbani kwake Oysterbay leo mchana na kuhudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe na baadhi ya watendaji wa wizara yake, Waziri Mkuu amesema taarifa hiyo itafanyiwa kazi na wataalamu wa ofisi yake.

“Nilipokea taarifa yenu jana saa 7 usiku lakini nikaahidi kuwa leo tukimaliza sherehe za maadhimisho ya Uhuru tukutane na kujadiliana kuhusu taarifa yenu,” amesema.

Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Prof. Maghembe alisema hadi kufikia Desemba 2015 wakati faru John anahamishwa alikuwa na watoto 26 (sawa na asilimia 70.2) ya faru wote waliokuwepo ndani ya kreta.

“Kati ya faru 37 waliokuwepo ndani ya kreta, watoto wake walikuwa 26 sawa na asilimia 70.2. Uamuzi wa kumuondoa John ulikuwa ni muhimu ili kuwezesha kuongezeka kwa faru weusi na kupunguza tatizo la ‘inbreeding’ ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro,” alisema Waziri Maghembe.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili Robert Mande (Kushoto) na Mkuu wa Pori la Akiba la Ikorongo/Grumeti, Bw. Nollasco Ngowe.

Baada ya kuhamishiwa Sasakwa, Waziri Maghembe alisema Julai 10, 2016 afya ya faru John ilianza kudorora na alikufa tarehe 18 Agosti, mwaka huu. Taarifa hiyo iliandaliwa na Kamati ya Taifa ya Kuwalinda Tembo na Faru. Kamati hiyo inaundwa na Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Mkurugenzi Mkuu wa NCAA na Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro.

Akikabidhi pembe za faru huyo mbele ya Waziri Mkuu, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Bw. Robert Mande alimweleza kwamba pembe kubwa ya faru John ilikuwa na uzito wa kilo 3.6 na pembe ndogo ilikuwa na uzito wa kilo 2.3.

Desemba 6, mwaka huu, akiwa ziarani mkoani Arusha, Waziri Mkuu aliuagiza uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), umletee nyaraka zote zilizotumika kumhamisha faru maarufu kwa jina la ‘John’ kutoka kwenye hifadhi hiyo ifikapo Alhamisi, Desemba 8.

NAVY Kenzo Wapongezwa Kwa SHOW Nzuri Walioifanya Kenya Tuzo za Pulse Music Video Awards...

$
0
0

Baada ya kudondosha show ya kimataifa usiku wa kuamkia leo Wasanii pekee ambao waimeiwakilisha TANZANIA kwenye tuzo kubwa nchini KENYA za PULSE MUSIC VIDEOS AWARD Navy kenzo

Wamepongezwa na zaidi mashabiki 50 kupitia mtandao wa tweeter kwa performance iliyo washangaza watazamaji waliohudhulia tuzo hizo

Wasanii hawa ambao pia ndio walikuwa wasanii pekee wa kimataifa kutoka Tanzania waliozipamba tuzo hizo na kupewa heshima kubwa ya kuperform kwenye show ya Pulse Music Video Awards ambazo ndio awards kubwa Nairobi.na kenya kwa ujumla
Ambazo zimefanyika usiku wa Alhamisi 8 kuamkia leo. Katk ukumbi wa serena NAIROBI

WAIMBAJI Watano wa Bongo Flava Ambao Walichezea Shilingi Kwenye Shimo la Choo na Kupotea

$
0
0
Hapana shaka hata kidogo mziki wa Bongefleva umepanda chati kwa kasi sana kimataifa hasa barani afrika na wanamuziki wake wamekuwa na ushawishi mkubwa katika kiwanda cha muziki ndani na nje ya nchi..
Mpaka mziki huu umefanikiwa kufika hapo imekuwa ni safari iliyojaa milima na mabonde! Kuna ambao mziki umewapatia ajira na wametoka kimaisha na wapo ambao walichezea shilingi kwenye shimo la choo..


BIGGEST LOSERS

5. RAY C

Rehema chalamila (maarufu Ray C) alitikisa vya kutosha mwanzoni mwa miaka ya 2000 (2003 - 2007). Alijijengea mpaka image na heshima ya kuonekana ni moja ya malkia wa kiwanda cha mziki Tanzania akiwa sambamba na kina lady jaydee.! Dalili mbaya zilianza baada ya kuwa na ukaribu na Nako 2 Nako na hasa kiongozi wa kundi la N2N, lord eyez! Baadae wakanzisha mahusiano na muda si muda akajitumbukiza kutumia madawa ya kulevya and the rest is history.. Amepotea kwenye game na hakuna tumaini kama atarudi!!


4. 20 PERCENT

Mpaka sasa ndiye msanii namba mbili kwa kuzoa tuzo nyingi kwa usiku mmoja baada ya kuzoa tuzo 5 za KTMA mwaka 2013! Kuna kipindi ilikuwa kila nyimbo atakayoitoa muda mchache tu inageuka 'nyimbo ya taifa' inaimbwa mpaka na mtoto Mdogo anayejifunza kuongea.. Kizuri zaidi nyimbo zake zilikuwa na ujumbe kiasi hata leo hii ukisikiliza bado unaburudika.. Kilichotokea kwake mpaka kushuka na hatimaye kupotea kabisa kwenye game anakijua yeye pamoja na producer wake Man water.. Sijui ni mibangi au walikorofishana tu lakini kiwanda cha mziki tumepoteza kichwa hapa..


3. MARLAW

Moja kati ya mazingaombwe ya Bongofleva ambayo bado siyaelewi mpaka leo moja wapo ni hii!! Inawezekana vipi mtu mwenye kipaji, mashabiki, na influence kama Marlawa anapotea moja kwa moja??? Tatizo ni nini? Familia? Mbona kuna wasanii wengi tu wanafamilia na wanafanya vizuri?? Au kampeni za siasa 2010 ndio zilimponza? Lakini mbona ni wengi walishiriki zile kampeni lakini mpaka leo bado wanafanya vizuri?? Alafu kinachoshangaza mpaka leo jamaa ukimsikiliza anaimba unaona kabisa bado anajua?? Sijui ni nini kimemkuta.. Lakini kuna kipindi alipokuwa kwenye ubora wake aliiteka Bongofleva yote!


2. CHID BENZI

Hakuna cha Joh Makini, hakuna cha stamina, hakuna Niki mbishi wala young dee au sijui young nani.. Huyu ndio alikuwa mfalme wa Bongo Hip Hop na alipokuwa katika ubora wake aliiweka Bongofleva nzima kwenye kiganja cha mkono wake.. Walaaniwe wauza unga wote!


1. MR. NICE

Alikuwa ndiye diamond wetu, Alikiba wetu, Navy kenzo wetu.. Mpaka leo bado sijaelewa kinagaubaga hasa nini kilitokea, alibahatisha? Alifanyiwa figusu? Watu walichoka nyimbo za watoto? Alijisahau au pace ya ukuaji wa mziki ilimshinda akajikuta anakaa benchi bila kupenda??

MWANAUME Ongeza Ukumbwa wa Umbile (Cassava) lako Kwa Kutumia Kifaa cha Handsome Up....

$
0
0

Handsome up ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa uhakika na bila madhara. Inapatikana kwa @170,000/=tu. PIA kuna Gely ya kupaka @ 120,000/= na Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa @120,000/=.
Wasiliana nasi kwa no (+ 255 ) 0767447444 au
0714335378.
Follow us
@Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr @Markson_beauty_pr
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images