Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

Sifa 10 za Mtu Mwenye Penzi la Kweli Kwako....

$
0
0
Vijana wengi ambao wanapendana leo mapenzi yao hayadumu kiasi cha kubatizwa jina la utamu wa bazoka. Lakini yote hii inatokana na ukweli kwamba elimu ya mapenzi ambayo ni muhimu kwa binadamu haitolewi ipasavyo.

Ipo zana potofu kwamba kumfundisha mtoto mapenzi ni kumharibu, jambo ambalo si kweli bali inategemea mtoto huyo anafundishwa nini na kwa wakati gani. Lakini cha kushangaza zaidi hata watu wazima ambao ni wadau wa mapenzi hawayajui, matokeo yake wanajiingiza kwenye uhusiano wakiwa bumbumbu na hivyo kuteshwa na changamoto zinazowakabili.
Leo tutajifunza kwa undani sifa kumi za mpenzi bora ili tuweze kuwatambua wapenzi wetu kabla ya kuwapa mioyo na utu wetu. Sifa hizo ni hizi zifuatazo.

1.Mpenzi wa kweli ni yule ambaye hatangoja kujua nini unahitaji yaani hana sababu ya kusubiri kuombwa ndiyo atoe msaada.

2. Ni yule atakayejua wakati gani huna furaha au una furaha na atakuwa na wewe kwa hali zote mbili .

3. Ni yule atayekuwa tayari kukusikiliza kwa kile utakachosema, hatojali umeongea baya au zuri

4.Atakuwa na wewe wakati wa shida na raha. Hatakuwa mtu wa kuvizia vizia na kujisogeza wakati ukiwa na raha.

5. Mpenzi wa kweli atakuheshimu na hatopenda kuwa kikwazo cha maisha yako, atakulinda daima.

6. Atakupenda kwa moyo wake wote na wala si kwa ajili ya shinikizo fulani (pesa au mali)

7. Mpenzi wa kweli ni yule atakayeonyesha kuthamini nafasi yako kama rafiki au mpenzi mbele ya wengine, hafichi hisia zake mbele za watu, atakutetea na kukufanya wa kwanza.

8. Kwenye ukweli mpenzi mzuri atasema bila kukuficha na atapenda kukuonyesha mifano ya namna ya kuwa mkweli na mwaminifu.

9.Mpenzi wa kweli ni yule anayejiamini, asiyeyumba katika maamuzi hata kama atalazimika kufanya maamuzi magumu .

10.Atakuwa tayari kuvumilia, hatakuwa mwepesi wa hasira wala kutumia lugha chafu na ubabe.

NAFASI za Kazi East Africa Community na Makampuni Mengine Zilizotangazwa leo Magazetini

$
0
0

WANASIASA wa Upinzani Burundi Wamkataa Mkapa

$
0
0

Mkapa amesema kuwa makubaliano yataafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.

Wanasiasa wa upinzani nchini Burundi walio uhamishoni wamepinga jitihada za aliyekuwa rais wa Tanzania za kutatua mzozo ulio nchini humo.

Hii inajiri baada ya William Mkapa kuwaambia waandishi wa habari kuwa si jambo zuri kuendelea kutilia shaka uhalali wa Raia Pierre Nkurunzia.

Nchi ya Buurndi ilitumbukia kwenye mzoo baada ya bwana Nkurunziza kutangaza kuwa angewania muhula wa tatu.

Mamia ya watu wameuawa na maelfu kukimbia nchi kulipozuka ghasia.

Bwana Mkapa alipewa jukumu la kusaidia kutatua mzozo huo, na amesema kuwa makubaliano yataafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.

Baadhi ya wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni wanatafutwa na serikali kwa kupanga maandamano ya kupinga hatua ya Rais Nkurunziza hatua ambazo serikali inazitaja kuwa za kihalifu.

Wengine waliilaumiwa wa kushiriki kwenye mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli mwezi Mei.

Source: BBC

VIDEO: Rais Magufuli Akutana na Dangote Ikulu, Amhakikishia Mazingira Bora ya Uwekezaji

$
0
0
Rais Magufuli amemhakikisha mfanyabiashara wa Nigeria, Aliko Dangote kuwa itamwekea mazingira mazuri ya uwekezaji ili kuhakikisha kiwanda chake cha saruji kinaendelea kufanya kazi kwa ufanisi.

Rais amesema kuna ‘wapiga deal’ walikuwa wameingilia mradi wake huku Dangote akisema mwezi huu analeta malori 600 kwaajili ya shughuli zake na kubebea saruji na kwamba atanunua kila rasilimali kwaajili ya kiwanda hicho hapa hapa Tanzania. Pia amedai kuwa atatengeneza ajira zingine mpya zaidi ya 1,500.

VIDEO:

MSAIDIZI wa Mbowe, Ben Saanane Adaiwa Kupotea Tangu Nov 18, Hata Simu Zake Hazipatikani

$
0
0
Moja kati ya wasaidizi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa siku 22 hadi leo.

Taarifa zilizothibitishwa na ndugu zake pamoja na Chadema zimeeleza kuwa Ben Saanane ambaye ni Mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti wa chama hicho alitoweka tangu Novemba 18 mwaka huu na kwamba hata simu zake zote hazipatikani tangu wakati huo.

Kufuatia hali hiyo, familia yake imesema iliripoti katika kituo cha polisi kilichoko Tabata jijini Dar es Salaam anakoishi Saanane na kupewa jalada lenye kumbukumbu namba TBT/RB/8150/2016.

“Kaka anafanya kazi Chadema akiwa miongoni mwa wasaidizi wa Mwenyekiti Freeman Mbowe. Ametoweka katika mazingira ya kutatanisha maana kazini wanamtafuta na nyumbani wanamtafuta bila mafanikio,” mdogo wake Ben aliyejitambulisha kwa jina la Erasto Saanane anakaririwa na Tanzania Daima.

Aliongeza kuwa wamefanya jitahada zote wakisaidiana na Jeshi la Polisi, kuangalia katika hospitali zote pamoja na vyumba vya kuhifadhia maiti jijini Dar es Salaam lakini hawakupata jibu.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vicent Mashinji alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanaendelea na jitihada za kumtafuta ikiwa ni pamoja na kuandaa utaratibu wa kichama kufahamu undani wa tukio hilo.

Hata hivyo, Kamadna wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdun alipotafutwa na gazeti hilo alieleza kuwa ofisi yake haijapokea taarifa za tukio hilo.

Chanzo: Tanzania Daima

SIAD Karoli Adai Kxuachana na meneja wake kulimfanya apoteze mwelekeo kwenye muziki

$
0
0
Msanii mkongwe wa muziki wa asili, Saida Karoli amefunguka kwa kusema kuwa moja ya sababu ambayo ilimfanya apotee kwenye muziki ni kitendo cha kuachana na meneja wake.
saida-karoli

Muimbaji huyo ambaye aliachana na meneja wake toka 2007, amedai kitendo hicho kilimfanya ashindwe kujisimamia na kumfanya ashuke kwenye muziki.

“Baada ya kuachana na meneja wangu sikuweza kujisimamia mimi mwenyewe na pia kwa wakati ule ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu muziki una mambo mengi na mimi nimekulia kijijini kwahiyo kujua baadhi ya vitu ilikuwa ngumu sana,” Saida aliiambia BBC.

“Sina nilipo kosea lakini najua kila kitu chenye mwanzo hakikosi kuwa na mwisho, simaanishi huo ndo mwisho wangu ila kwa kuwa nilianza na mtu, sasa unapomalizana naye ni kama unaanza maisha mapya ndio kitu kilicho nitokea mimi,” aliongeza.

Pia muimbaji huyo amesema kwa sasa anajipanga kuja kwa kishindo na kufanya mapinduzi katika muziki wa asili nchini.

JE DADA Unahitaji Kuwa na Makalio Mazuri na Rangi Nzuri na Mkaka Kuwa Handsome? African Beauty Inakuletea Dawa Hizi

$
0
0

AFRICAN BEAUTY EXPRESS PRODUCTS ,DAWA ZETU ZIMETHIBITISHWA KIAFYA.
je Dada unahitaji Kuwa Mrembo? na kaka unahitaji Kuwa mtanashati?African beauty imewaletea products nyingi sana zenye ubora WA hali ya juu,hazina madhara wala kemikali,zinamatokeo ya haraka ndani ya wiki mbili tu,products hizi niuhakika sana% tunazo za
(1)kuongeza hipsi,MAKALIO,na mapaja @100000
(2)kunenepesha MIGUU na Kuwa soft(chupa ya Bia)@100000/=
(3)Kupunguza Kitambi(slimming)@100000/=
(4)Kupungua MWILI MZIMA(weight loose)@130000/=
(5)Kuwa Mweupe MWILI MZIMA (njano)@100000/=
(6)kunenepa MWILI mzima@90000/=
(7)Kupunguza MATITI na kuyasimamisha@80000/=
(8)kuongeza matiti@80000
(9)kurefusha NYWELE na kuzuia kukatika@80000/=
(10)kuondoa CHUNUSI,MADOA na makovu@80000/=
(11)kuondoa Michirizi ya uzazi na cream@80000/=
(12)kurefusha na kunenepesha uume kwa size uipendayo@100000/=
(13)kuongeza NGUVU za kiume@100000/=
Ndugu MTEJA bidhaa za African beauty in uhakika sana,ukitumia dose moja hauwezi kurudi tena,MTEJA atakapo nunua bidhaa kwetu ni lazima afuate dose ili aweze kuona matokeo mazuri,MTEJA nilazima afuate maelekezo ya wahusika WA kampuni,MTEJA kama Yupo bize na kazi zake anaweza kupelekewa Huduma Mpaka alipo,kwa Wateja WA mikoani Huduma utatumiwa kwa mabasi kiofisi zaidi,kama MTEJA hayupo bize na kazi anaweza kufika ofisini kwetu zilizopo kariakoo,mnazi mmoja,na Mlimani city kwa maelezo zaidi piga sim(+255)-0756697906,0716805391,0783300397 Whatsapp namba 0756697906 Facebook page AFRICAN BEAUTY unaweza kunifollow instagran
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
@AFRIC_IS_BEAUTY
@AFRIC_IS_BEAUTY


KIONGOZI wa ACT Wazalendo Atangaza Kujivua Uanachama na Kuachana na Siasa

$
0
0
Mimi Mchange Habibu Mchange, Leo Jumaamosi tarehe 10.12.2016, ninaujuza umma wa Watanzania, Rafiki zangu, ndugu na jamaa. Kwamba kwa kipindi kirefu sasa nimekuwa nikijihusisha na harakati za kisiasa, awali nikiwa mwanachama wa Chadema na baadae ACT WAZALENDO.

Kwamba katika Chama cha ACT WAZALENDO nimepata heshima ya kuwa kiongozi mwandamizi kama katibu wa Mipango na Mikakati na baadae Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa katika secretarieti ya Chama hicho.

Na Kwamba tangu kujiunga kwangu na Chama hicho nimekuwa mjumbe wa kamati kuu, mjumbe wa Halimashauri kuu na Mjumbe wa Mkutano mkuu wa Chama.

Kwa moyo mkunjufu kabisa, na kwa mapenzi mema na taifa langu.

Ninathibitisha Kwamba nimejitoa rasmi katika ushiriki wa aina yote ya siasa ili nipate muda mwingi zaidi kufanya na kusimamia shughuli zangu za kijasiriamali zinazonitaka nitoe fursa na huduma Sawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa.

Kwa mantiki hiyo basi, kuanzia Leo hii, nitaiomba jamii katika yote nitakayofanya inione nimefanya kama Mchange huru asiye mwanachama wa Chama chochote cha siasa.

Ninaomba uamuzi wangu huu uheshimiwe na kamwe nisihusishwe na aina yoyote ya siasa bali utanzania wangu.

Ningeweza kufanya uamuzi wangu huu kimya kimya, lakini kwa hatua niliyoifikia na ili kuweka kumbukumbu sawia ni budi niutoe kwa umma.

Ninafahamu kuwa kuwa mwanachama wa Chama cha siasa ni haki yangu ya kikatiba, lakini nimeamua kuihifadhi haki yangu hiyo kwa sasa Mpaka hapo nitakapoona inafaa kufanywa vinginevyo.

Ninawatakia kila la heri waliokuwa wanachama wenzangu wa ACT WAZALENDO katika kuyafikia malengo ya msingi ya uanzishwaji wa Chama hicho.

Kujiondoa kwangu kushiriki katika siasa kusihesabiwe kama sehemu ya kukwamisha au kurudisha nyuma matarajio na au malengo ya Chama hicho.

Tafadhali ichukueni hii kama chachu ya kuwafanya mfikie malengo mahsusi kwa wakati muafaka bila kurudi nyuma.

Msivunjike moyo, msirumbane, pendaneni,heshimianeni na shikamaneni ili mfikie lengo

Sasa nitabaki na kuendelea kuwa ndugu yenu, rafiki na swahiba. zaidi mtanzania mwenzenu. Tutaendelea kushirikiana katika mambo yote ya kijamii na kimaisha yasiyohusiana na mlengo wa kiitikadi wa kisiasa.

Kwa wanachama wa vyama vinginevyo kama CHADEMA, CUF, CCM, ADA TADEA na kadharika, nitaendelea kuwa rafiki mwema kwenu, jirani na ndugu wa kweli kama au pengine zaidi ya ilivyokuwa hapo awali.

Ninawatakia heri wanasiasa wote wa vyama vyote hapa nchini.

Ninawaomba radhi wote niliowahi kuwakosea, kuwa kwaza ama kuwafanya wajisikie vibaya kutokana na matendo yangu, maandishi yangu Misimamo yangu, matamshi yangu ama na mwenendo wangu wa kisiasa kwa kipindi chote nilichokuwa mwanachama wa vyama vya siasa hapa nchini.

Ninaahidi kuendelea kuwa mtanzania Mtiifu mwenye mapenzi mema kwa taifa langu huku nikiwatakia heri wanachama wapenzi na viongozi wa vyama vyote vya siasa.

Itoshe tu kufahamika Kwamba Mimi *Habibu Mchange,* kwa sasa si mwanachama, mpenzi wala mshabiki wa Chama chochote cha siasa.

Zaidi, Ninawaomba radhi watu wote ambao kwa namna moja ama nyingine nitakuwa nimewakwaza kutokana na uamuzi wangu huu.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

Wasalaam
Habibu Mchange,
0762178678.
Morogoro Tanzania

ORADHA ya Washindi wa Tuzo za EATV zilizotolewa Usiku Desemba 10

$
0
0
Jana Desemba 10, 2016 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam zimetolewa tuzo kwa wasanii mbalimbali wa muziki na wa filamu kutoka nje na ndani ya Tanzania.

Jumla ya tuzi 9 zilizotelewa kwa wasanii mbalimbali waliofanya vizuri kwa mwaka 2016 ambapo tuzo moja ya heshima ilitolewa kwa mtu aliyekuwa na mchango mkubwa katika saanaa ya Tanzania na hivyo kufanya jumla ya tuzo 10. Tuzo hii ilitolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Hapa chini ni orodha ya washindi wa tuzo mbalimbali zilizotolewa usiku wa Desemba 10.

Tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka- Safari ya Gwalu
Wimbo Bora wa Mwaka- Aje wa Ali Kiba
Video Bora ya Mwaka- Aje ya Ali Kiba
Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kiume- Salim Ahmed maarufu Gabo
Tuzo ya Mwigizaji Bora wa Kike-  Chuchu Hans
Kundi Bora la Muziki- Navy Kenzo
Mwanamuziki Bora Chipukizi- Amani Khamis maarufu Man Fongo
Tuzo ya Heshima- Dj Bonny Love
Mwanamuziki Bora wa Kike- Judith Wambura maarufu Lady JayDee
Mwanamuziki Bora wa Kiume- Ali Kiba
Mwanamuziki Ali Kiba ameweka rekodi katika tuzo hizi zilizotolewa kwa mara ya kwanza baada ya kutwaa tuzo tatu ikiwa ni Video Bora ya Mwaka, Wimbo Bora wa Mwaka, na Msanii Bora wa Kiume.

PICHA : Meli Yenye Malori 600 ya Kiwanda cha Dangote Yawasili Mtwara

$
0
0
Mfanyabiashara Alhaji Aliko Dangote leo alipokuwatana na kufanya mazungumzo na Rais Dk Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam alimthibitishia kuwa hana lengo la kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa badala yake anatafuta fursa nyingine za kuwekeza hapa nchini.

Katika kuthibitisha hilo, Mfanyabiashara huyo alisema leo meli yenye malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake itawasili nchini. Ameongeza kuwa lengo la kufanyabiashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.

Baada ya kufanya mazungumzo hayo, meli yenye magari hayo 600 imetia nanga katika bandari ya Mtwara ambapo ndipo kiwanda cha Saruji cha Dangote kilipo.

Aidha, imeelezwa kuwa wiki ijayo meli nyingine kutoka Korea Kusini yenye malori 451 inatrajiwa kuwasili katika bandari ya mkoani Mtwara.


MZEE Aliyeweka Tangazo la Kutafuta Mke Afunguka Sababu ya Kufanya Hivyo

$
0
0
Mzee Athumani Bakari Mchambwa (76) aliyeweka tangazo la kutafuta mke maeneo ya Mtoni Mtongani, Dar es Salaam amefunguka sababi ya kufanya hivyo.


Mzee Mchambwa ameiambia Global TV kuwa ameamua kufanya hivyo ili mwanamke yeyote atakayekuwa tayari kuolewa naye atambue mapema vigezo na masharti anayotakiwa kufanya na atakuwa anayatambua majukumu yake mapema kwani hata siku akibadilika hataweza kumsumbua sana.

Akitaja sababu ya kutafuta mke mwingine wakati tayari ameshaoa, Mzee huyo amesema, “Mimi nina kawaida ya kuwa na wake wawili, hayo ndio maisha yangu kutoka miaka yote lazima niwe na wake wawili. Sasa huyu mke mkubwa ndio alikuwa hapa Dae rs Salaam, kuangalia watoto wajukuu, nyumba na mambo mengine kadhalika.”

“Mara nyingine anapokuwa na wasaa anakuja shamba pia kucheki taratibu za shamba lakini la zaidi mimi na yule wa shamba tunakuwa shamba. Sasa nilichokuwa nakikusudia baada ya huyu kufariki lazima nipate mtu mwingine ambaye anisaidia mawazo ya kufikia pale ninapopataka mimi.”

Mzee huyo ameongeza kuwa mke wake huyo alifariki Agosti 6 ya mwaka huu.

MCHUNGAJI Awanywesha Waumini Dawa ya Kuua Bakteria “Dettol” ili Wapone Matatizo Yao

$
0
0
Mchungaji  maarufu kwa jina la Rufus Phala kutoka kanisa la AK Spiritual Christian lililopo Makgodu, Limpopo, Afrika Kusini amewashangaza watu kwa kitendo cha kuwanywesha  Dettol waumini wake ilihali ina madhara kwa binadamu.

Kwa mujibu wa Daily Sun SA, mchungaji huyo alifanya kitendo hicho kwenye ibada za kawaida kanisani kwake akiwataka waumini wenye matatizo na wanaohitaji maombi wanywe Dettol aliyokuwa ameishika mkononi mwake huku akiwambia watapona shida zao ikiwemo magonjwa.

“Nafahamu kuwa Dettol ni sumu, lakini Mungu ameniagiza niwape na muitumie. Mimi nilikuwa wa kwanza kuinywa,”  – Mchungaji.

Pia alisema kuwa amepokea meseji za WhatsApp kutoka kwa watu waliokunywa na wamethibitisha kupona. Baada ya kuwepo kwa taarifa hizo, amehojiwa Daktari kutoka Afrika Kusini, Dr Mabowa Makhomisane, ambaye amekiri kuwa Dettol ina madhara inapotumika tofauti na maelekezo ikiwemo kuinywa

“Mtu akinywa Dettol na ikafika tumboni, kimsingi hupunguza mzunguko wa hewa ya Oxygen mwilini. Hali hiyo ikitokea mtu anaweza kupoteza fahamu na kufariki.

 “Na kama mtu atatapika na bahati mbaya maji maji yakaingia kwenye mapafu yake, Detto itamsababishia ugonjwa wa Nimonia. Mapafu yatajikunja na mtu atashindwa kupumua”

Dr Makhomisane amewashauri watu waliokunywa dawa hizo waende Hospitali kupata vipimo ili kujua madhara waliyopata..

ALIKIBA Afunika Tuzo za EATV Awards

$
0
0
Mkali wa ‘Aje’, Ali Kiba jana aling’ara zaidi katika tuzo za EATV 2016 zinazoandaliwa na kituo cha runinga cha East Africa zilizotolewa katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika tukio hilo alikuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye huku msema chochote akiwa mtangazaji wa zamani wa kituo hicho, Salama Jabir.

Kiba aliongoza orodha kwa kunyakua tuzo tatu katika vipengele vyote vitatu alivyokuwa akiwania. Tuzo ya kwanza ni Msanii Bora wa Kiume, Wimbo Bora wa Mwaka (Aje), na Video Bora ya Mwaka (Aje).

Akitoa neno la shukurani mara tatu, Mfalme Kiba alisitiza kuwa tuzo hizo ni za mashabiki wake waliomuwezesha na kwamba yeye anachukua tu kwa niaba yao.

Tuzo nyingine nzito ya heshima ilienda kwa DJ Bony Love, aliyekuwa mmiliki wa studio za Mawingu na mmoja kati ya waasisi wa muziki wa Bongo Flava.

KUPOTEA Kwa Msaidizi wa Mbowe, Chadema na Polisi Watofautiana

$
0
0
Moja kati ya wasaidizi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha kwa siku 22 hadi leo.

Taarifa zilizothibitishwa na ndugu zake pamoja na Chadema zimeeleza kuwa Ben Saanane ambaye ni Mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti wa chama hicho alitoweka tangu Novemba 18 mwaka huu na kwamba hata simu zake zote hazipatikani tangu wakati huo.

Kufuatia hali hiyo, familia yake imesema iliripoti katika kituo cha polisi kilichoko Tabata jijini Dar es Salaam anakoishi Saanane na kupewa jalada lenye kumbukumbu namba TBT/RB/8150/2016.

“Kaka anafanya kazi Chadema akiwa miongoni mwa wasaidizi wa Mwenyekiti Freeman Mbowe. Ametoweka katika mazingira ya kutatanisha maana kazini wanamtafuta na nyumbani wanamtafuta bila mafanikio,” mdogo wake Ben aliyejitambulisha kwa jina la Erasto Saanane anakaririwa na Tanzania Daima.

Aliongeza kuwa wamefanya jitahada zote wakisaidiana na Jeshi la Polisi, kuangalia katika hospitali zote pamoja na vyumba vya kuhifadhia maiti jijini Dar es Salaam lakini hawakupata jibu.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vicent Mashinji alikiri kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanaendelea na jitihada za kumtafuta ikiwa ni pamoja na kuandaa utaratibu wa kichama kufahamu undani wa tukio hilo.

Hata hivyo, Kamadna wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Salum Hamdun alipotafutwa na gazeti hilo alieleza kuwa ofisi yake haijapokea taarifa za tukio hilo.

VIGOGO Kutoonekana Sherehe za Uhuru Kwazua Mjadala

$
0
0
Dar es Salaam. Kumekuwa na mjadala wa mahudhurio katika maadhimisho ya sherehe za Uhuru ya mwaka huu ambayo huenda yamevunja rekodi kwa viongozi wengi wa kitaifa na kimataifa kutoshiriki.

Licha ya hali hiyo kusababishwa na mambo kadhaa yakiwamo kuingiliana kwa ratiba za shughuli nyingine za kimataifa, ugonjwa na kufiwa kwa baadhi ya viongozi, wachambuzi wa masuala ya kisiasa wamedokeza kuwa huenda imetokana na hatua ya Rais John Magufuli kuahirisha sherehe za mwaka jana.

Lakini juzi, Rais Magufuli alitumia Sherehe za Miaka 55 ya Uhuru kueleza sababu, “Kwanza sherehe za mwaka jana ilibidi tusiadhimishe kama zilivyopangwa kwa sababu mbili; sababu ya kwanza zilikuwa zifanyike mwezi mmoja tu baada ya kuapishwa, kwa hiyo hata baraza langu na watendaji wangu wengine nilikuwa bado sijawateua.

“Lakini sababu ya pili, nilipoambiwa gharama za sherehe hizo mwaka jana zilikuwa (shilingi) bilioni nne, nikawa ninajiuliza bilioni nne kuna mambo yapi yatafanyika? Itakuwa ni kualika wageni, kutakuwa na chakula, kutakuwa na posho na kadhalika.”

Alisema alipouliza hizo posho na chakula wangekula Watanzania wote, akajibiwa kuwa ni kwa ajili ya wale tu walioalikwa, akaamua fedha hizo ziende kupanua Barabara ya Ali Hassan Mwinyi ambayo inapitiwa na Watanzania wengi.

Alisema ameamua sherehe za mwaka huu zifanyike kwa sababu gharama zake zimepungua kwa kuwa ziliishia palepale uwanjani, tofauti na siku nyingine ambazo Rais huandaa dhifa ya Taifa ambayo hufanyika Ikulu jioni.

Katika sherehe hizo, marais wawili wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kati ya watatu waliopo hawakuhudhuria kadhalika na Mama Maria Nyerere ambaye ni mjane wa Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Tanzania na mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli.

Pia, mawaziri wakuu wastaafu wote waliopo; Jaji Joseph Warioba, Dk Salim Ahmed Salim, John Malecela, Cleopa Msuya, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na Mizengo Pinda hawakuonekana.

Mbali ya hao, viongozi wote wa mhimili mwingine wa Dola, Spika wa Bunge, Job Ndugai na naibu wake, Dk Tulia Ackson pia hawakuwapo. Aidha, tofauti na sherehe kama hizo miaka ya nyuma, juzi hakuna mkuu wa nchi yoyote ya nje aliyehudhuria wakiwamo wa Afrika Mashariki.

Matukio hayo pamoja na lile la Rais Magufuli kutambua uwepo wa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa bila ya kumtaja Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita aliyekuwapo, yameibua mjadala mkubwa katika viunga mbalimbali na mitandao ya kijamii baada ya kumalizika kwa sherehe hizo.


Sababu za kutohudhuria
Akizungumzia kutohudhuria kwa viongozi hao, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Hassan Abbas alisema kwa kawaida viongozi wote wa kitaifa hualikwa na hata katika sherehe za juzi, walialikwa bila kujali wanatoka chama gani.

Licha ya Abbas kutofafanua, Lowassa na Sumaye huenda hawakufika katika sherehe hizo baada ya kukihama chama tawala, CCM na kujiunga na Chadema mwaka jana ambako Lowassa aligombea urais huku Sumaye akiwa mpiga debe wake mkubwa. Alishika nafasi ya pili nyuma ya Rais Magufuli.

“Kama mtu hajafika, muwaulize kwanini hawajafika mimi siyo wa kujibu hilo, ila viongozi wote walialikwa,” aliongeza.

Kuhusu kutokuwapo kwa viongozi wa mataifa ya nje, Abbas alisema, “Sidhani kama walialikwa lakini hilo linasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, na ‘statement’ (taarifa) ilitoka, muulizeni Waziri Jenista Mhagama.”

Hata hivyo, Waziri Mhagama hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo lakini katika taarifa yake kuhusu maandalizi ya sherehe hizo hakuzungumzia lolote juu ya wakuu wa mataifa mengine kuhudhuria.

Hata hivyo, licha ya kutokuwapo kwa taarifa yoyote rasmi ya kutohudhuriwa kwa baadhi ya viongozi wa kitafa imeelezwa kwamba Mkapa alikuwa Burundi katika utatuzi wa mgogoro wa kisiasa nchini humo na Kikwete alikuwa Msumbiji akihudhuria mkutano wa kimataifa uliokuwa ukijadili uwekezaji katika fursa za kielimu.

Pia Rais huyo wa Awamu ya Nne alituma salamu za Uhuru kwa Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Twitter akiwa Maputo, Msumbiji akisema: “Salamu za heri ya kumbukumbu ya miaka 55 ya uhuru wetu, kwetu sote na kwa Amiri Jeshi Mkuu, mheshimiwa Rais.”

Aidha, Pinda hakuhudhuria pengine kutokana na msiba wa baba yake mzazi, Xavery Mizengo Pinda (90) aliyefariki mwishoni mwa mwezi uliopita katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.

Kadhalika, Mzee Malecela hakuhudhuria pengine kutokana maradhi na Agosti Rais Magufuli alimtembelea kumjulia hali yeye na Spika Ndugai.


Maoni ya wachambuzi
Akizungumzia kutokuwapo kwa viongozi wa nje hasa mataifa ya jirani, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Iringa (UoI), Jimson Sanga alisema hilo linaleta maswali mengi katika jamii. Pia alisema ilikuwa ni jambo muhimu kwa viongozi wote wa kitaifa kuwapo uwanjani ili umoja na mshikamano unaohubiriwa majukwaani, uanze kuonyeshwa kwa vitendo na viongozi wenyewe katika tukio hilo muhimu kwa historia ya Taifa.

“Tunaposema Tanzania ina umoja na mshikamano lazima tuanze kuuona kwa viongozi wenyewe, wastaafu walipaswa kuwapo au la tuambiwe sababu za msingi za kutokuwapo kwao,” alisema.

Alisema alitarajia kuona sherehe hizo zikipambwa na marais kutoka nchi za jirani ikiwamo za Afrika Mashariki jambo ambalo halikutokea.

Sanga alionyesha wasiwasi wake kwamba huenda uamuzi wa Rais Magufuli wa kuadhimisha sherehe hizo kwa kufanya kazi mwaka jana, umewafanya viongozi wengine wa nchi za jirani kusita kuhudhuria.

“Urais ni taasisi hivyo, kama mwaka jana tuliadhimisha kwa kufanya kazi basi msimamo huo ungeendelea kwa sababu naamini kulikuwa na sababu za msingi za kufanya hivyo. Kwa mtazamo wangu, naona huenda jambo hilo limechangia sherehe hizi kukosa uwakilishi wa nchi za jirani hata zile ambazo Tanzania ilizisaidia kutafuta uhuru wake,” alisema.

Alisema ipo haja kwa Serikali kulijulisha Taifa ikiwa ilitoa mialiko kwa viongozi hao au haikutoa na sababu zake kuondoa sintofahamu iliyopo.

Profesa wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alizungumzia kutokuwepo kwa viongozi wa kitaifa ya nje na kusema hakuna mushkeli wowote.

“Hicho siyo kiashiria kwamba kuna mushkeli, Tanzania bado imeshikamana, hao viongozi wengine kama Rais mstaafu Kikwete najua yuko nje ya nchi lakini mkewe alikuwepo. Labda swali la kujiuliza kwa nini Lowassa na Maalim Seif Sharif Hamad hawakuwepo? Tanzania hii ni yetu sote, uhuru ni wetu, walipaswa kuwepo. Lakini bado sioni mushkeli, Tanzania bado ni moja,” alisema.

Kauli ya Profesa Bana iliungwa mkono na Profesa Gaudence Mpangala wa Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (Rucu) Iringa ambaye alisema hakuna tatizo kwa viongozi hao kutohudhuria kwani huenda walikuwa na dharura.

Alisema katika hotuba yake, Rais Magufuli aliwataja kwa majina viongozi wastaafu akiwashukuru kutokana na mchango wao katika kulifikisha Taifa mahali lilipo tangu Tanzania ilipopata Uhuru.

“Inawezekana tu walikuwa na shughuli nyingine, si muhimu wote kuwepo tulichukulie suala hili hivyo lilivyo,” alisema.

Hata hivyo, Profesa Mpangala aligusia suala la mgogoro wa CUF, hasa Rais Magufuli alipomtaja Profesa Lipumba aliyekuwapo uwanjani wakati wa sherehe hizo, kwamba inaonyesha anautambua uenyekiti wake wa chama hicho.

“Mimi nilitafsiri kwamba, Rais Magufuli anamtambua kama mwenyekiti wa CUF japo ni ukweli ni kwamba, uenyekiti wake una utata. Mtu alijiuzulu na kurudi tena, hii si sawa,” alisema.

Alisema kutambuliwa kwa Profesa Lipumba kama kiongozi wa chama cha siasa kunadhoofisha upinzani Zanzibar na Bara.

“Kunamdhoofisha Lowassa huku Bara na Maalim Seif kule Zanzibar kwa sababu inaonekana nyuma yake kuna sapoti ya wazito,” alisema.

ZAIDI ya watu 30 Wafariki Kwenye Mlipuko wa Lori Kenya

$
0
0
Idadi ya watu waliofariki katika ajali mbaya ya kuteketea kwa lori nchini Kenya, imepanda na kupita watu 30.

Kwa mjibu wa naibu kamanda mkuu wa jimbo la Nakuru Isaaca Masinde, ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia Jumapili katika eneo la Karai kwenye barabara ya kutoka Nairobi kuelekea Naivasha.

Lori moja la kubeba mafuta, lilianguka na kulipuka katika eneo la barabara hiyo yenye shughuli nyingi nchini Kenya na kusababisha mauwaji ya watu 30 papo hapo.

Watu wengine zaidi wamefariki wakitibiwa mjini Naivasha.

Shirika la msalaba mwekundu nchini humo, limesema lori hilo la mafuta, lililokuwa njiani kuelekea nchi jirani la Uganda, lilipoteza usukani na kisha kugonga magari kadhaa kwenye barabara kati ya Nairobi na Naivasha yapata kimomita 100 kutoka mji mkuu Nairobi.

Mtu mmoja kwa jina Moses Nandalwe aliyeshuhudia ajali hiyo, ameiambia BBC kuwa, magari kadhaa yalishika moto na kuanza kuchomeka, huku watu wengi waliofika katika eneo la ajali hiyo ili kushuhudia kilichotokea, wakikumbwa na moto huo na kisha wakachomeka.

Magazeti nchini Kenya yanaripoti kuwa zaidi ya watu 40 wanahofiwa kufa, huku magari 12 yakiteketea. Kuna taarifa pia kuwa maafisa kadhaa wa polisi pia wameangamia.

Miongoni mwa magari yaliyoteketea ni Basi moja la matatu lililokuwa na abiria 14, ambao wanahofiwa wote wamefariki.

Bw. Mwachi Pius Mwachi, naibu mkurugenzi wa shirika la kukabiliana na majanga nchini Kenya, amesema kuwa lori hilo la mafuta lilikuwa likiteremka kwa kasi, kabla ya kuanza kuungua.

Ajali hiyo mbaya imetokea nchini Kenya, wakati ambapo madaktari na wauguzi wakiendelea na mgomo wao, hatua ambayo imelemaza kabisa shughuli za matibabu katika hospitali za umma.Idadi ya watu waliofariki katika ajali mbaya ya kuteketea kwa lori nchini Kenya, imepanda na kufikia 40.

MWANA FA Adai Bifu ya Diamond na Ommy Dimpoz Inachangamsha Mziki ila Atoa Onyo

$
0
0
Msanii wa muziki wa hip hop, Khamisi Mwinjuma, maarufu mwana FA amedai bifu kati ya Diamond na Ommy Dimpoz ni vitu ambavyo vinahitaji kwenye muziki kwa kuwa vinachangamsha game.

Diamond na Ommy Dimpoz hivi karibuni waliingia kwenye bifu zito hali ambayo ilipelekea wawili hao kumtupiana maneno ya kashfa katika mitandao ya kijamii.

Akiongea na gazeti la Habari Leo wiki hii, Mwana FA alisema bifu la wasanii hao linachangamsha tasnia ya muziki na kusisitiza muhimu ni kudhibiti wasizuriane.

“Unajua hakuna kitu kisichokuwa na ushindani, mfano wewe upo Daily News lazima mtakuwa na washindani wenu, mnachotakiwa kufanya ninyi waandishi ni kujizuia msizuriane,” alisema FA.

“Inachangamsha muziki unapata wa kuwazungumzia, kukiwa na ushindani wa hapa na pale sifikiri kama ni kitu unachoweza kukizuia, game ikiwa rafiki sana nayo inakuwa haiwezi kuburudisha, haiwezekani mashabiki wawe wote wa wanamuziki wote hakuna kitu kama hicho,” aliongeza.

Pia rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Dume Suruali’ amedai kwa sasa bado ana mambo mengi ya kufanya katika kuendeleza muziki wake lakini pia kuendeleza familia yake pamoja na masuala ya biashara.

YOUNG Dee Afunguka Tuhuma za Kumtelekeza Mtoto ‘Mtoto ni Wangu Nimempokea’

$
0
0
Msanii wa muziki wa hop hop, Young Dee amefunguka na kuweka mambo sawa kuhusu tuhuma ambazo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amemtelekeza mtoto.

Uvumi huo ulikuwa zaidi baada ya rapa huyo kuhojiwa katika kipindi cha U-Heard cha Clouds FM juu ya tuhuma hizo na yeye kudai kuwa hamtambui mwanamke huyo ambaye anadai amezaa naye.

Baada ya kuona mambo yanaenda mbali zaidi, Young Dee alikaa na uongozi wake na kuamua kutoa taarifa hii..

Nawashukuru sana watu wote ambao wamekuwa waki-support kazi yangu mpya #Furaha Either Naomba radhi kwa mashabiki zangu ambao wamekwazika kwa njia moja au nyingine kutokana na taarifa za uongo zilizosambaa mtandaoni. Ikumbukwe tarehe 22 June mwaka huu niliitisha press nikaomba radhi kwa waTanzania na mashabiki zangu wote kwa ujumla, nikaeleza kuwa nimepitia kipindi kigumu sana na kuwa kuna mengi nimefanya ambayo sijivunii na najutia.

Niliahidi kubadilika na kuwa mfano mzuri kwa jamii. Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikipigana na nafsi yangu kuhakikisha sirudii makosa. Madhara yanayotokana na matendo niliyofanya kipindi kile hadi leo bado yananitafuna ila nimekuwa nikijitahidi kukabiliana nayo.

Nilipewa taarifa na mamisa kuwa ana mimba yangu ya (miezi 6), kama kijana nilishtuka na kupata ugumu kuikubali hali hiyo kutokana na kwamba nilikua nimetoka kwenye kipindi kigumu. Baada ya kutafakari nilimuomba aitunze hiyo mimba asiitoe!!! Kama ni mwanangu ntamlea. Kama ningekuwa na nia ya kumkana mtoto au kumtelekeza, kwanini nimwambie asitoe?

Si kutaka kumshirikisha mtu kwanza bila kuwa na uhakika kwamba kweli mtoto ni wangu. Management yangu sikuishirikisha kwa lolote kwa sababu inanisaidia sana katika kuhakikisha career yangu ya music ina imarika. Hivyo nilihisi ni taarifa ambayo inaweza kui-disappoint na kukatisha malengo. Hata familia yangu Mama, dada na ndugu sikuwaeleza kitu. Nilitaka nijipange vizuri, nijihakikishie kweli mtoto ni wangu, nitafute njia sahihi ya kueleza hili jambo.

Nimesikitika sana kuona kuwa sio kila mtu anafurahia unapofanikiwa, unapoamua kufanya kazi ili upate maendeleo. Wapo watu ambao bado watatafuta fursa ya kukuharibia maisha. Yote kheri Namuachia mungu baba. Mtoto wangu nimempokea kwa moyo mmoja. Ni mtoto wa kike, na anaitwa Tamar. Nimewataarifu ndugu na wazazi wangu kuhusu hili, nashukuru wamenielewa. Nimeuelewesha pia uongozi wangu, wamenielewa.

Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa Kumjaalia uhai mwanangu, amezaliwa akiwa salama kiafya. Shukrani za dhati ziende kwa uongozi wangu, kwani wamekua wakihakikisha nasimama katika njia sahihi bila kuyumba. Shukrani kwenu SHILAWADU kwa kujaribu kuzirudisha nyuma jitihada zangu za kimaendeleo.#YoungDaddy

VIDEO: Mzee wa Upako Aja na Mpya Adai Mke wa Mtu ni Sumu na Mume wa Mtu ni Maziwa

$
0
0
Mzee wa Upako aja na Mpya adai Mke wa mtu ni sumu na Mume wa mtu ni Maziwa.

ANGALIA VIDEO HII..

TRA Yamwadhibu Mtumishi Aliyemtolea Mteja Lugha Chafu

Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images