Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104423 articles
Browse latest View live

MAONI: Kwa Mujibu wa Vigezo vya EATV Awards, Alikiba Anastahili Tuzo 3 Alizopata

0
0
Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa muziki wa Tanzania na kwa jicho ziada, nimezifuatilia kwa kina tuzo za EATV zilizofikia kilele jana. Nimeona, kuna kuna watu wanalalamika pasipo kujua utaratibu wa tuzo hizi ukoje. Ili kuwa nominated kwenye EATV Awards, ilikuwa ni lazima kwanza msanii achukue fomu ya ushiriki ndipo aweze kuingizwa katika orodha ya wasanii watakaoshiriki.


Jopo la EATV likafanya mchujo kupata orodha ya watu 5 ambao watapigiwa kura.

Sifahamu vigezo vyao katika kuchagua nyimbo zilizostahili kuingia katika 5 bora kwa kila kipengele, lakini ninachojua ni kuwa nyimbo zote au wasanii waliopita kwenye 5 bora wamestahili kabisa. Ukipitia habari hii, Hawa ni washindi wa tuzo za EATV 2016, Alikiba akomba tuzo 3, utagundua kuwa kuna baadhi ya watu wanalalamika kuhusu Video bora ya mwaka.

Naweza kusema labda ni kwa sababu ya hizi Team fulani na Team fulani.

Ebu tafakari kidogo kwanza. Nini maana ya kupiga kura? Ukitazama orodha ya video 5 zilizoingia, nadhani hakuna ubishi kuwa AJE ya Alikiba imefanya vizuri kushinda video zote zilizoshindanishwa naye katika kipengele cha video bora.

Achilia mbali kura alizopata Alikiba na kumfanya kuwa mshindi wa video bora, bali msanii huyu ana hazina kubwa sana ya mashabiki na wanakesha wakimpigia kura.

Tazama kidogo washiriki wa kipengele hiki:

1. Alikiba – Aje
2. Shetta – Namjua
3. Navio – Njogereza
4. Joh Makini – Dont Bother
5. Lady Jaydee – Ndi ndi ndi

Hata kwa upeo mdogo tu, kinyang’anyiro cha kipengele hiki kilikuwa ni cha watu watatu Alikiba, Joh Makini, na Lady Jaydee, ” maana kwa haraka haraka tu ndio wenye nguvu zaidi kwa Tanzania.

Hivyo kwa mtazamo wangu, Alikiba amestahili kabisa kuchukua tuzo tatu alizo pata hapo jana. Hongera sana kwa EATV kwa kuweka alama katika tasnia ya burudani Tanzania. Bila shaka tutarajie mengi zaidi mwakani maana ninaamini huu ni mwanzo tu na ni mwanzo mzuri kabisa.

Napenda niaache kwa maneno haya tu, “Tuache maneno, tuwasapoti wasanii wetu wanaofanya muziki mzuri.”

Imeandikwa na Ally Msangi

HARMONIZE Anunua Kiwanja, Ajipanga Kushusha Ghorofa Hili Hapa...

0
0

Mwanamuziki Harmonize aliyoko chini ya lebo ya Muziki ya WCB Ameweka picha katika mtandao wake wa Instagram akionyesha kiwanja alichonunua na ramani ya mjengo wa Gorofa anaopanga kuujenga hivi karibuni....
Pichani akiwa na mama yake na madalali wa kiwanja hicho..

VIDEO: Rich Mavoko(KokoroMaster) alivyotikisa kwenye After Skul Bash

0
0

VIDEO: Rich Mavoko(KokoroMaster) alivyotikisa kwenye After Skul Bash

VIDEO: Kutana na Mtanzania anaefanana na Jay Z kimuonekano mpaka sauti

0
0
After School Bash ni tamasha ambalo huwa linafanyika kila mwisho wa mwaka na kukutanisha Wanafunzi mbalimbali na mastaa wa muziki bongoflevani, pamoja na hayo huwa kunafanyika mashindano mbalimbali ikiwemo ya hawa wanaofanana na mastaa…. Tazama hii video hapa chini kujionea


CCM Yakanusha Uvumi Ulioenea Mitandaoni

0
0

Taarifa ilikuwa hivi:
Kutoka hapa Lumumba ni kwamba Steven Wassira anachukua nafasi ya Ole Sendeka.

Peter Maduki anakuwa mweka hazina kuchukua nafasi ya Zakhia Meghji, na Kinana kabaki katika nafasi yake.

Naibu katibu Mkuu Makongoro Nyerere. Naibu Zanzibar ni Zahoro Ally.

PICHA ya Wapenzi wa Zamani ya Kajala na Petitman Yazua Gumzo..Petit Afunguka na Kuuliza Swali

0
0
Picha waliopiga Kajala na Petit Man Huko Snap Chat inavyoonekana imeleta sinto fahamu upande wa Petit na mpenzi wake na kumfanya aulize swali kwa mashabiki zake kama kupiga picha na mpenzi wake wa zamani ni kosa......

Petit man na Kajala walikuwa wapenzi kwa muda mrefu kabla ya kuachana nae na kuamua kumuoa mdogo wa Diamond Esma Platnumz

VANESSA Mdee Alistahili Tuzo ya Mwanamziki Bora Wa kike na si Lady Jay Dee

0
0
Japo ni tuzo za Tz.... ilikuwa haina baja ya kusemea hili maana tulilitegemea lakini ukweli lazima uwekwe wazi! Lady Jay De hakustahili kuchukua Tuzo aliyo chukua Juzi! Labda jana ilikuwa ni kwa Ajiri ya Wakongwe Tuuu lakini nafikiri hata tukifuatilia upigaji kuraa utaona Vanessa Mdee alikuwa anakura nyingi Tuuu!!!!

Tukiachana na kura Kwa sasa na kwa miaka 2 nyuma wakati lady Jay De alikuwa Nje ya nchi vanessa Mdee ndo amekuwa mtu anae iwakilisha vyema Tanzania Nje ya nchi kwa upande wa Kike hadi kuwa nominated Mara mbili Tuzo za Mtv! Ameshajijengea Mashabaki ndani na Nje ya nchi lakini mwisho wa siku anakosa Tuzo kisa Figisu Figisu!!

Tunaweza kugues why Vanessa Mdee kakosa tuzo lakini sio mahara pake hapa Japo waliotoa Tuzo wanajua ukwelii!! walio ona mchakato wa hizi tuzo waliamua kukaa Mbali!

Lakini kiukweliii Vanessa Mdee Alistahili hii tuzo bila ubishiiiiii.......Hata iwe kwa mchakato wa kuraaa Bado vanessa Ana Fan Base kubwaaa kuliko huyo!!!!

Haya ndo yanayo fanya watu kususia hizo Tuzo! ila Kwangu mimi kwa mwaka Huu Vanessa Mdee ndo the best

Imeandikwa na Danya/Jamii Forums

MZEE wa Upako Awaombea Kifo Waandishi wa Habari

0
0
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu Mzee wa Upako amesema waandishi wote wanaoandika habari za kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.

Kauli hiyo aliitoa jana ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yaliyoandikwa kwenye vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa.

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mpo humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema.



Mambo 6 Yakuzingatia Katika Mahusiano Ya Kimapenzi

0
0
Mara nyingi wengi wetu tumekuwa katika mahusiano na wapenzi wetu lakini hali sio kama ile ya awali wakati mnaanza mapenzi yenu.  Wanawake wengi wanalalamika kuwa  hawaoni upendo ule waliouzoea zamani wakati mapenzi yanaanza. Hata wanaume wengine wanalalamika pia kuwa penzi limeteremka kiwango baina yao.

Mara zote hushuka huku kwa ukaribu (intimacy) hakupangiliwi au kutazamiwa bali huja taratibu pasipo wapenzi kutambua, mara lugha hubadilika,  muda wakuwa pamoja hupungua, mambo huanza kufanywa kwa mazoea, vilivyo zoeleka kufanyika havionekani tena na taratibu hali hii ikikomaa huathiri hata tendo la ndoa. Katika hatua hii, wapenzi huanza kuchokana na kutotamaniana, hapa ndio kwenye upenyo wa mmoja au wote kuwaza njia mbadala.

Wengi walioachana au kutalikiana nao walipitia njia hii pia.
Ili kuepuka yote haya, haunabudi kujifunza njia za kuwasha moto wa upendo kila wakati na kuongeza ukaribu (intimacy) kati yenu.

Njia za kukusaidia

1. kucheka pamoja
Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kucheka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitafuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote.  Usiwe mgumu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu.  Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea.  Kama utaanza kujizoeza  hivi ukiwa nyumbani, taratibu  utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote.

2. Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake.  Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo.  Onyesha heshima katika vitu hivyo pia.  Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu.  Mjenge mwenzako mbele yawengine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye.  Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo.  Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyanyua  na sisi pia.

3. Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote.  Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala.  Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea, kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu kimwili.   Wengi wetu huweza kufanya haya kidogo tunapokuwa peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je, ni aibu? au nidhamu mbaya? au dhambi?

Kugusana ndio mwanzo wakuamsha hisia za kuhitajiana, (hembu jiulize kisirisiri, lini umegusana na mwenzako nje ya chumbani). Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza au kutovutiwa kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi waliopweke wanaotamani kuguswa.

Mguso huu wa upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa pia ni vema kujifunza kuijenga lugha ya mguso wa  tendo la ndoa katika  mahusiano yenu.

4. Zungumzeni hisia zenu
Kati ya vikwazo vikubwa katika ustawi wa mahusiano mengi hususani ya wanandoa ni kutokuwepo kwa majadiliano.  Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao.  Kama vile maisha yasivyo na ukamilifu, mahusiano na hata ndoa pia hazina ukamilifu.  Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia sio mkamilifu.  Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini kinachokusumbua. Kuendela tu na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo kuwa baridi juu ya mwenzako, jiwekeeni muda kila wiki ninyi wawili kutoka ili kuzungumza mambo yenu.  Mwambie umpendae yapi yanayojiri kila siku na zipi changamoto zako, mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa pamoja taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.

5. Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe tusiache maumivu na machungu yatawale mahusiano yetu.  Lazima tujifunze kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia.  Kutofautiana katika mahusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile vinavyowaudhi dhidi yetu.  Kila hisia za mmoja wetu zinaumuhimu.  Huwezi kuona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akuambie yanayo muumiza na msameheane.

6. Linda muonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi hatari hii hutokea tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko.  Ukaribu na mpenzi wako hauendelezwi tu bali pia unalindwa, pia muonekano  wetu lazima ume halisi na sio feki.  Vile tunavyoviona katika tamthilia na filamu sio ukaribu ulio halisi.  Kama tunataka tuonekane sawa na vile tunavyowaona wengine wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo bora katika mahusiano yetu.  Ukianza kupata  ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.
Lengo liwe kuvitafuta vile vyote  mpenzi wako alivyonavyo ambavyo  hukuza ukaribu wenu.  Mwenzako awe ndio mtu wa muhimu kuliko wote katika maisha yako.

TUZO Tatu Alizoshinda ALIKIBA Zamfanya Mwanamuziki AT Ajikojolee Kitandani....

0
0
Kabla ya tukio kubwa la #EATVAwards jana usiku, msanii AT aliahidi kuwa kama Kiba angeshinda tuzo basi kwa furaha angekojoa kitandani. Baada ya tuzo hizo na Kiba kulamba tuzo 3. AT ametimiza ahadi hiyo na kutupia picha insta.

Una neno gani kwa AT?

MZEE wa Upako 'Kila mwandishi Aliyeniandika Vibaya ikifika Mwezi wa Tatu Akiwa Hai, Mimi Naacha Kuhubiri Naenda Kuuza Gongo'

0
0
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu Mzee wa Upako amesema waandishi wote wanaoandika habari za kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.
mzee-wa-upako3

Kauli hiyo aliitoa jana ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yaliyoandikwa kwenye vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa.

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mpo humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema.

Source: Mwananchi

DIANA Edward Miss Tanzania Aingia Fainali za Beauty With A Purpose Miss World, Awapa Vidonge Wanaomsema Vibaya

0
0
Miss Tanzania 2016, Diana Edward, ameingia kwenye fainali za shindano la Beauty With A Purpose ambalo ni sehemu ya mashindano mbalimbali kwenye Miss World.

Beauty With A Purpose huhusisha miradi mbalimbali ya kijamii ambayo hufanywa na washiriki wa Miss World. Diana amewasilisha documentary ya masuala ya ukeketaji kwenye jamii ya watu wa Masai.

Fainali za Miss World mwaka zitafanyika December 18, nchini Marekani.

Pamoja na Diana kuonesha kufanya vizuri, tangu atawazwe kuwa Miss Tanzania mwaka huu, amekuwa akipokea maneno hasi.

“I’m not beautiful Yes,I’m not focused Yes,I’m in a vacation Yes,I’m dumb Yes,I’m not up todate Yes. Who knows tomorrow ONLY God can determine your future.Thanks for those who have been and still voting for me and supporting me no matter how much Haters are pushing me back you guys are still holding my hand and lift me up,” ameandika kwenye Instagram.

“Good News My Beauty with a Purpose Documentary for Masai Dondosha Wembe has shined again to TOP 20 waiting for the TOP position and has been said ever since there has never been such a wonderful message to the beauty pageant history of Miss World.Please Keep on voting for your Tanzania’s Best Kept Secret Princess Diana,I love myself though. One rule I was born to shade tears to fight and to become a champion,” ameongeza.

BAADA ya Kuzoa Tuzo Tatu EATV Awards, ALIKIBA Atumbuiza South Afrika Kwenye Tamash

0
0
Fresh kutoka kuchukua tuzo tatu za EATV Awards, Jumamosi hii, Alikiba alikwea pipa hadi jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwenda kutumbuiza kwenye, Mkhaya Migrants Awards. Zimetolewa Jumapili hii.

Tuzo hizo huandaliwa na wizara ya mambo ya ndani ya Afrika Kusini kuwatuza wahamiaji wanaofanya vizuri kwenye nyanja mbalimbali nchini humo.

DIamond Platnumz Amsifu Nahreel Kwa Kuvumbua Kipaji cha Rosa Ree...Adai Ndio Rapper Anaempenda Kwa Sasa Bongo

0
0
Diamond Platnumz ampongeza mtayarishaji na muimbaji wa kundi la Navy Kenzo, Nahreel.

Hitmaker huyo wa Salome ameonyeshwa kufurahishwa na Nahreel kwa kukitambulisha kipaji cha rapper wa kike kutoka lebo ya The Industry, Rosa Ree.

Kupitia mtandao huo, Diamond ameandika:

A big birthday wishes to the Most talented Bway @nahreel … Unapambana sana Mwanangu, Mungu aendelee kukufungulia wewe pamoja na team yako nzima ya the Industry… But all n all Shukran kwa kututambulisha kwa huyu dada…. one of My Favorite Female Rapper and Song at the moment! #OneTime @rosa_ree 💥🔫 Tazama Video ya Rapper huyo hapa:

YOUNG Dee Aonyesha Uanaume...Akutana live na Mama na Mtoto Wake

0
0

Baba, Mama na Mtoto !!!kwa pamoja tumpe Hongera Young D kwa kuikubali Damu yake...mama mtoto kafurahi mpka rahaa!!!
kweli instagram ni mtandao mzuri matatizo mengi yanapata ufumbuzi. 👌👌..
TUPIA NENO MOJA KWAO.

MTATIRO: Ni Kweli Kwamba Sijazungumza Lolote Kuhusu Ben, Nasubiri FINDINGS za Taasisi yake

0
0
Anaandika Comred Julias Mtatiro
BEN!
Ni kweli kwamba sijazungumza lolote kuhusu comrade #Ben_Saanane, nasubiri FINDINGS za taasisi yake, CHADEMA, ili kupata mwelekeo. Tuendelee kuomba kokote aliko awe salama! Lakini kwa sasa yapo matarajio matano;
1. Ben kupatikana akiwa salama na akatueleza nini kilimkuta.
2. Ben kupatikana akiwa ameteswa, hajitambui na asiyejiweza tena siku za mbele.
3. Ben kupatikana akiwa mfu, marehemu au asiye na pumzi tena.
4. Ben kutopatikana kabisa, kupotea moja kwa moja, milele.
5. Ben kupotea kwa muda mrefu kisha kuonekana mbele ya safari (atatueleza nini kilimsibu).
Ni Mungu peke yake ndiye anajua nini kimempata na nini hatma yake, mimi na wewe hatuwezi kujua, tuendelee tu kumtafuta kwa kadri tuwezavyo.
Let us continue to close the fingers for Ben.
#TunamtakaBenakiwahai
#BringBackBenAlive

HATIMAYE Ommy Dimpoz Aweka Picha Akiwa na Mpenziwe Instagram!

0
0
Baada ya maneno mengi kutoka kwa mashabiki wa upande wa pili kuwa ommy hapigi mechi na pia hawamjui shemeji

Ommy dimpoz ameamua kuweka picha ya shem wetu wakiwa pamoja
Hata hivyo picha hiyo ilikuwa na emoji zenye ishara ya malovee lakini kitu kilichoshangaza wengi ni Ommy kublock comment katika picha hiyo,,yani picha hiyo huwezi ku°° comment

MAJARIBU ya Wanawake Kwa Wanaume Kama Wanafaa Kuwa Nao Kimapenzi Mengi Hutoa Majibu Yasiyo Sahihi

0
0
Wanawake huaga wanawajaribu wanaume kwa majaribu fulani ili waweze kujua kama wanaune hao wanafaa kuishinao, bila ya kupima au kufanyia tafiti kama hayo majaribu yao wanayo yatumia kama yapo ndani ya uwezo wa wanaume hao, madhara ya udhaifu ya majari yao ni kwamba, hawawezi kujua kama wanadanganywa, kwasababu huaga hawajui uhalisia wa maisha ya mjaribiwa,

Pili huaga wanawapoteza watu muhimu, kwasababu huaga wanawafanyia majaribu wanaume bila kujua kama majaribu hayo yapo ndani ya uwezo wao, wanaume huonekana kama wameshindwa kumbe huaga hawajashindwa kiuhalisia, yaani huaga wanashindwa kwasababu majaribu huaga makubwa kwao kuliko uwezo wao kwa wakati huo...

Unakuta mwanamke anamjaribu mchumba wake labda amnunulie kitu fulani cha gharama lakini mwanaume kwa wakati huo anakuta anamajukumu mengine kama kujenga ama mengine basi mvulana akishindwa kutimiza anaonekana hafai na kukimbilia kwa mwingine ambae anaweza kumpa hivyo vitu vya starehe ya muda na kumuacha mwanaume potential ambae labda angevumilia wangefanya maisha pamoja....

Mwanaume Hajaribiwa Bwana....

JE DADA Unahitaji Kuwa na Makalio Mazuri na Rangi Nzuri na Mkaka Kuwa Handsome? African Beauty Inakuletea Dawa Hizi

0
0

AFRICAN BEAUTY EXPRESS PRODUCTS ,DAWA ZETU ZIMETHIBITISHWA KIAFYA.
je Dada unahitaji Kuwa Mrembo? na kaka unahitaji Kuwa mtanashati?African beauty imewaletea products nyingi sana zenye ubora WA hali ya juu,hazina madhara wala kemikali,zinamatokeo ya haraka ndani ya wiki mbili tu,products hizi niuhakika sana% tunazo za
(1)kuongeza hipsi,MAKALIO,na mapaja @100000
(2)kunenepesha MIGUU na Kuwa soft(chupa ya Bia)@100000/=
(3)Kupunguza Kitambi(slimming)@100000/=
(4)Kupungua MWILI MZIMA(weight loose)@130000/=
(5)Kuwa Mweupe MWILI MZIMA (njano)@100000/=
(6)kunenepa MWILI mzima@90000/=
(7)Kupunguza MATITI na kuyasimamisha@80000/=
(8)kuongeza matiti@80000
(9)kurefusha NYWELE na kuzuia kukatika@80000/=
(10)kuondoa CHUNUSI,MADOA na makovu@80000/=
(11)kuondoa Michirizi ya uzazi na cream@80000/=
(12)kurefusha na kunenepesha uume kwa size uipendayo@100000/=
(13)kuongeza NGUVU za kiume@100000/=
Ndugu MTEJA bidhaa za African beauty in uhakika sana,ukitumia dose moja hauwezi kurudi tena,MTEJA atakapo nunua bidhaa kwetu ni lazima afuate dose ili aweze kuona matokeo mazuri,MTEJA nilazima afuate maelekezo ya wahusika WA kampuni,MTEJA kama Yupo bize na kazi zake anaweza kupelekewa Huduma Mpaka alipo,kwa Wateja WA mikoani Huduma utatumiwa kwa mabasi kiofisi zaidi,kama MTEJA hayupo bize na kazi anaweza kufika ofisini kwetu zilizopo kariakoo,mnazi mmoja,na Mlimani city kwa maelezo zaidi piga sim(+255)-0756697906,0716805391,0783300397 Whatsapp namba 0756697906 Facebook page AFRICAN BEAUTY unaweza kunifollow instagran
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇
@AFRIC_IS_BEAUTY
@AFRIC_IS_BEAUTY


VIDEO: Ronaldo Mshindi wa Ballon d’Or 2016, Takwimu zake Kwa Mwaka 2016

0
0
Staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo amefanikiwa kushinda tuzo yake ya nne ya Ballon d’Or 2016, Ronaldo alikuwa akiwania tuzo hiyo huku mshindani wake mkuu akiwa ni Lionel Messi.

Ronaldo ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya nne akiwa kazidiwa mara moja na Lionel Messi aliyewahi kushinda mara 5, kwa mwaka 2016 Ronaldo ameisaidia Ureno kushinda Euro 2016, lakini katika mwaka 2016 pia Ronaldo amefunga jumla ya magoli 38 katika mechi 42 na assist 14.

Staaa huyo pia amehusika katika upatikanaji wa magoli 39 ya Ligi Kuu Hispania LaLiga katika mechi 30 huku yeye akiwa kafunga magoli 31 na assist 9, tuzo hiyo imepatikana kwa mfumo wa waandishi wa habari 173 dunia nzima kupiga kura.

Viewing all 104423 articles
Browse latest View live




Latest Images