Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

MSHINDI wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika 2016 wa BBC

$
0
0
December 12 2016 shirika la utangazaji la Uingereza BBC ndio lilitangaza rasmi mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa BBC kwa mwaka 2016.

Tuzo hiyo ambayo ilikuwa inashindaniwa na Sadio Mane wa Senegal/ Liverpool, Yaya Toure wa Ivory Coast/ Man City, Pierre Aubameyang wa Gabon/Dortmund amefanikiwa kushinda staa wa Algeria anayeichezea Leicester City ya England Riyad Mahrez.

SERIKALI Yacharuka Suala la Maiti 7 Kuokotwa Mto Ruvu, Waziri Mkuu Atoa Maagizi Mazito kwa Jeshi la Polisi

$
0
0
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi kufanya upelelezi kuwabaini waliohusika na mauaji ya watu saba ambao miili yao iliokotwa pembezoni mwa mto Ruvu wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani, ikiwa kwenye mifuko ya sandarusi, ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali imepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kuokotwa kwa miili hiyo Desemba 8, mwaka huu na kueleza kuwa matukio kama hayo, likiwemo la mjasiriamali kuuawa baada ya kutekwa mkoani Tabora, hayavumiliki wala kukubalika.

Alitoa maagizo hayo jana katika Baraza la Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) lililofanyika kitaifa kijijini Shelui wilayani Iramba mkoani Singida. Waziri Mkuu Majaliwa alikuwa mgeni rasmi.

Alisema, “Serikali kwa kushirikiana na Polisi, tena Waziri wa Mambo ya Ndani uko hapa (akimzungumzia Mwigulu Nchemba aliyekuwepo katika baraza hilo), tutaendelea na upelelezi ili wahusika wachukuliwe hatua kali.”

Jana akihojiwa katika kituo cha televisheni cha Star TV, Mwigulu alisema uchunguzi umebaini kuwa miili saba iliyookotwa Bagamoyo ni ya wahamiaji haramu.

Miili ya watu sita ilikutwa Desemba 7, mwaka huu kando ya mto Ruvu wilayani Bagamoyo ndani ya mifuko ya sandarusi na ikiwa imewekwa mawe ili isielee kisha mifuko hiyo kushonwa kama mzigo wa mazao na kutupwa mtoni.

Mwili mwingine uliokotwa Desemba 9, eneo hilo hilo na pamoja na kutokuwa katika mfuko wa sarandusi, ulikuwa umevuliwa shati na kuonekana na majeraha mgongoni na kwenye ubavu umekatwa na kitu chenye ncha kali.

Mwishoni mwa wiki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventure Mushongi alisema miili yote ilizikwa kwa kuwa ilikuwa vigumu kuwatambua kutokana na kuharibika vibaya huku kukiwa hakuna kitambulisho chochote kinachoashiria watu hao ni nani na wametoka wapi na kwamba Polisi inaendelea na upelelezi kubaini waliohusika na mauaji hayo na atakayebainika sheria itachukua mkondo wake.

Aidha, Waziri Mkuu alisema serikali ipo macho kukabiliana na tishio lolote la usalama na vyombo vya usalama vipo tayari muda na wakati wote.

Aliwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama kutoa taarifa wanapoona kuna hatari kwani viongozi wa dini na waumini wa dini hizo ndio walinzi wa Taifa.

Alisema uwepo wa vikundi vya uhalifu kama ‘panya road’ cha jijini Dar es Salaam ni hatari kwa jamii, kwani vinadhuru na kuvuruga amani na kueleza kuwa ni vijana na watoto wanaoishi katika jamii, walioko misikitini na makanisani na kutaka waripotiwe katika vyombo vya usalama ili washughulikiwe.

Alizungumzia ugaidi na kubambikizwa kesi, na kusema serikali itaendelea kusimamia mtu kupata haki zake na anayestahili adhabu, kuipata vile vile.

“Ni heri kuwa na watu 10 waliotoroka mahabusu kuliko mtu mmoja kukaa mahabusu kwa kesi ya kuonewa,” alisema Majaliwa.

Mwigulu anena kuhusu miili 7, Saanane
Akizungumza jana kwa simu kuhusu vifo hivyo vya Bagamoyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema serikali baada ya tukio hilo ilichukua hatua kupitia vyombo vya usalama na tayari Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu amemhakikishia wanalifanyia kazi.

“Kama nilivyosema awali, hatujajua asilimia mia kwa mia kama watu hao waliouawa wana connection (uhusiano) na wahamiaji haramu waliookotwa wamechoka sana hivi karibuni (juzi).

“Kuna wahamiaji 81 waliokotwa hawajitambui, wameishiwa nguvu kabisa, ni eneo hilo hilo kulikookotwa miili hiyo, tumehisi watu waliowabeba wahamiaji hao inawezekana wengine walikufa na kwa vile hawana utu, wakawafunga katika viroba (sarandusi) na kuwatupa, Polisi wanachunguza hili kwa kina,” alieleza Mwigulu.

Aidha, alisema pia Polisi inachunguza ikiwa miili hiyo ilitupwa kikatili na wasafirishaji wa binadamu ambao nao hawana utu.

Alipoulizwa kwa nini wazikwe haraka bila vipimo vya vinasaba, Mwigulu alisema kuwa alizungumza na IGP na kuelezwa kuwa miili hiyo ilikuwa katika hali mbaya sana, lakini pia kuzikwa hakuzuii uchunguzi kufanyika kujua chanzo cha vifo hivyo.

Kuhusu kupotea katika mazingira ya kutatanisha Ofisa wa Ofisi ya Chadema, Makao Makuu Dar es Salaam, Bernard Saanane Novemba 18, mwaka huu, Mwigulu alisema aliona taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na kwa kuwa alikuwa akimfahamu, alimpigia simu na kubaini simu haipatikani.

“Nilishtuka kuona hizi habari, binafsi ni rafiki yangu wa karibu, nilipoona hizi habari nilimpigia na sikumpata, baada ya kuona simpati nilimpigia Mbowe (Freeman- Mwenyekiti wa Chadema Taifa), lakini simu yake iliita kama vile mtu yupo nje ya nchi,” alifafanua Mwigulu.

Hata hivyo, alisema amemuagiza IGP awaagize polisi kumtafuta Saanane na kuhakikisha ufumbuzi wa kupotea kwake unapatikana na kujulikana alipo.

Juzi, Mwenyekiti wa Umoja wa Kizazi cha Kuhoji Tanzania (UTG), Malisa Godlisten akizungumza na waandishi wa habari, aliipa Chadema na taasisi za umma zenye dhamana ya usalama wa raia saa 72 kuanzia jana kuhakikisha Saanane anapatikana na kueleza umma chanzo cha vifo vya watu hao saba ambao miili yao ilikutwa kando ya mto Ruvu, Bagamoyo.

AUDIO: Mahali Harmonize Aliponunua Kiwanja Kwa Ajili ya Kujenga Nyumba

$
0
0
Ni Mwimbaji mwingine staa wa Bongofleva, makofi mengi amepigiwa kwenye utunzi pamoja na ukali wa melody, anaitwa Harmonize kutoka WCB. Staa huyo anaingia kwenye headlines baada ya kununua kiwanja kwa ajili kujenga nyumba yake, kiwanja hicho kipo Mivumoni mbele ya Madale nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

‘Kikubwa zaidi nimefanyakazi na wasanii wengi sana wakina Diamond, Raymond, AY unakuta wengine wanataka kununua nyumba na wengine wanataka kupanga na kwa upande wa Diamond mpaka sasa hivi nimeshamuuzia nyumba 15’;- Dalali

‘Na sasa hivi nipo na Harmonize huku Mivumoni amekuja kutafuta nae kiwanja kwa ajili ya kukamilisha mjengo wake kwa hiyo ni vizuri ukiona vijana kama hawa wanakuja na mawazo mazuri ya kutafuta viwanja, Mivumoni ipo mbele ya madale huku’;-Dalali

JAMBO Hili Limemfanya Mwigizaji Chuchu Hans Kukumbuka Siku Aliyovunja Ungo.....

$
0
0
Ushindi wa tuzo ya Muigizaji bora wa kike wa Tuzo za EATV 2016 kumemtoa machozi Chuchu Hansy na kumkumbusha mambo mengi aliyopitia kwenye maisha yake.

Muigizaji huyo ambaye hakuwepo kwenye usiku huo wa tuzo na kuwakilishwa na meneja wake, ametoa ya moyoni kupitia Instagram kwa kusema ushindi huo umemfanya akumbuke maneno aliyokuwa akipewa na mama yake katika kipindi cha ukuaji wake.

“Naamini kuna uwepo wangu kwa kila hatua tupigayo, ama hakika usitamalaki ya moyoni kwa kuyadhihaki ya machoni. Hii imenipa funzo zaidi ya lile alilonipa mama nikiwa na vunja ungo,” alisema Chuchu. “Mama aliniambia heshimu watu bila kuwa dhihaki kwa makundi,ama kuwa bagua kwa rika,”

“Niwashukuru wote mlio nipigia kura amahakika mme tenda vema,likini mimi sio bora kuliko wenzangu ila nadhani kwa wino wakura zenu ulistahili niwe BEST ACTRESS, niwashukuru zaidi na zaidi, nikiandika maneno haya machozi yananitoka lakini hii yote ni heshima mlio nivika NENO LA KALE NI ASANTE,” aliongeza.

Katika kipengele hicho cha muigizaji bora Chuchu alikuwa anachuana na Khadija Ally, Kajala Masanja, Rachael Bitulo, pamoja na Frida.

ZARI Awashangaza Wengi Baada ya Tumbo lake la Uzazi Kupungua Ndani ya Wiki Moja...Atoa Ushauri Huu

$
0
0

USHAURI WA ZARI KWA WAZAZI from #zarithebosslady - Good morning.... ladies no need to worry coz our bodies are different. But I did exercise during pregnancy which has helped my body get bk within 7days.... and for those stretch marks keep using olive oil during and after pregnancy. #

MANENO Tata ya Mzee wa Upako kwa Wandishi wa Habari, Jeshi la Polisi Kutoa Tamko Leo

$
0
0
DAR ES SALAAM: Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi 2017, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo.

Kauli hiyo ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na kumfanyia fujo jirani.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro jana  alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa sikukuu na atatolea ufafanuzi leo.

Mzee wa Upako: Wote Walionichafua Watakufa Mwakani, Wasipokufa Nitaanza Kuuza Gongo
“Anasema hao waandishi watakufa kabla ya Machi 2017 kwani yeye Mungu? Hilo ni suala zito, tumeandaa mkutano na waandishi wa habari tutalizungumzia suala hilo kesho (leo),” alisema Kamanda Sirro.

Katika kauli hiyo, Mzee wa Upako alisema kila mwandishi aliyemuandika vibaya ikifika Machi mwakani hatakuwa hai na kama wataendelea kuishi, ataacha kazi ya kuhubiri injili na kwenda kuuza gongo.

MREMBO Sanchoka: ‘Nilimuokota’ Idris Sultan Kwenye Apartment Sauzi, Amfungukia Gigy Money

$
0
0
MODO mwenye figa la kuvutia anayekuja kwa kasi kwenye tasnia ya urembo, Sanchoka yeye hupenda kujiita Sanchi ameanika namna ambavyo alikutana na anayedaiwa kuwa mpenzi wake kwa sasa, Mshindi wa Big Brother Africa 2014 na mtangazaji wa Choice FM, Idris Sultan.

sanchoka-7Akifanya mahojiano (Exclusive Interview) na Channel maarufu hapa mjini ya Global TV Online, Sanchoka amefunguka kuwa uhusiano wake na Idris ulianzia kwenye Apartment wakati walipokuwa wamekwenda Afrika Kusini (Sauzi) kushuhudia utoaji wa Tuzo za MTV Africa (Mama) hivi karibuni.

“Mimi na rafiki zangu tulipanga kwenda kushuhudia MTV Awards huko Sauzi, bahati mbaya apartment tuliyofikia ndipo alipokuwa amefikia Idris pia.”

“Tulikuwa watu wengi kwenye hiyo apartment, walikuwepo wakina Shilole, na wengine wengi,”

Akanusha kuhusu kuwa wapenzi

Licha ya kuelezea kinagaubaga alivyokutana na Idris, Sanchoka amekanusha kuhusu taarifa zinazosambaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mshindi huyo wa BBA 2014.

“Idris alikuwa ana-anounce (anatangaza) awards, kwa kuwa alikuwa VIP kule mbele, alinifuata na kuniomba niwe partner wake ili twende nikakae naye kule mbele, haikuwa urafiki wa mapenzi bali ulikuwa urafiki wa kawaida tu.” Ameeleza Sanchoka ndani ya Studio za Global TV.

Amfungukia Gigy Money

Mbali na kufunguka alivyokutana na Idris, Sauz amefunguka pia kuhusu uhusiano wake na modo mwenzake ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM, Gigy Money ambaye alidaiwa kutoka kimapenzi na Idris huyo huyo.

sanchoka-8“Uhusiano wao (Idris na Gigy) mimi haujani-affect chochote kwa kuwa mimi na Idris tulikuwa marafiki wa kawaida tu, na hatujawahi kuzungumzia kuwa na uhusiano wa kimapenzi”. Alisema Sanchoka.

Pia Sanchoka ameeleza kuwa yeye kwa sasa ana mchumba wake mbali na huyo wanayemsema mitandaoni (Idris), licha ya kutobainisha iwapo atafanya taratibu za kufunga naye ndoa siku za hivi karibuni.

SIMBA SC Yachezea Vitasa vya Mtibwa Sugar

$
0
0
KLABU ya Simba ikiwa na kipa wake mpya Daniel Agyei, jana imekubali kichapo cha mabao 2-1 katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Simba ilikuwa na nafasi ya kusawazisha katika mechi hiyo lakini beki, Janvier Bokungu akakosa penalti. Kipigo cha Simba, kinapunguza makali ya watani wake Yanga ambao walichapwa kwa mabao 2-0 na JKU ya Zanzibar wikiendi iliyopita.

Kipigo cha Yanga kiliwaamsha Simba ambao walitumia muda mwingi kuwananga watani wao, lakini leo mambo yamegeuka. Unaweza kusema hakuna kuchekana kwa kuwa Yanga ndiyo wanaotamba sasa.

SHEHE Mkuu Dar: Nipo Tayari Kuwafungisha Ndoa Diamond & Zari Bure! (Video)

$
0
0
SHEHE Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum ameweka wazi kutopendezwa na kitendo cha Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuendelea kuzaa nje ya ndoa na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’ akisema kuwa ni kinyume na maadili na sheria za dini ya Kiislam.

Shehe Salum aliyasema hayo juzi Alhamisi (Novemba 1, 2016) alipotembelea Ofisi za Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa Magazeti ya Championi, Uwazi, Ijumaa Wikienda, Ijumaa, Amani na Risasi zilizopo Bamaga, Mwenge jijini Dar na kuzungumza na waandishi pamoja na wafanyakazi wa idara nyingine.

Akijibu swali la Mwandishi Aziz Hashim aliyetaka kujua dini inasemaje kuhusiana na watu kama Diamond kuendelea kuzaa nje ya ndoa, shehe huyo alisema:

“Niseme tu kwamba hili si kwa Diamond na Zari tu bali kwa wote wanaofanya zinaa. Dini ya Kiislam inaeleza kuwa, kuzini ni dhambi. Hivyo kitendo cha Diamond kuendelea kuzaa nje ya ndoa hatakuwa na tofauti na wanyama wengine ambao nao wanazaliana bila kufunga ndoa.

“Tofauti ya binadamu na wanyama kama mbuzi, ng’ombe au nguruwe ni kwamba, sisi tunatakiwa kuzaliana baada ya kufunga ndoa, kinyume chake tutakuwa tunapata dhambi.

“Halafu sasa tukio la kufunga ndoa wala halichukui muda mwingi na halina gharama kubwa. Ni suala la wahusika kumtafuta tu shehe, anakuja anatia ubani kisha mnaendelea na maisha yenu. Kama ni kutumia pesa itakuwa ni elfu hamsini tu au laki moja.

“Labda niseme tu kwamba, hata mimi kama kweli wamedhamiria kufunga ndoa, niko tayari kuwaozesha bure kabisa, nitaweka gari yangu mafuta kuwafuata popote, wao wajipange tu wakiwa tayari wanitafute.”

Shehe huyo aliongeza kuwa, anaona litakuwa jambo jema kwa wawili hao kuoana kwani kuendelea kuzaa nje ya ndoa ni kuwakosesha haki watoto wao hasa ile ya kurithi mali. VIDEO:

MWAKANI Sitakuwa na Roho Nzuri - Fid Q Afunguka

$
0
0
Msanii nguli wa hip hop bongo Fid Q baada ya kushuhudia EATV AWARDS mwaka huu, ameanza kujipanga kwa ajili ya mwakani na kusema kuwa hatokuwa na roho nzuri kwenye kuachia kazi.


Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Fid Q amesema mwakani amejipanga zaidi kwa kazi zake na kuachia zenye ubora zaidi, na hatokuwa na huruma.

"Nitaendelea kufanya vitu vyangu, lakini nikuweke tu wazi, mwakani sina roho nzuri, yanatoka mawe juu ya mawe, machupa juu ya machupa, kazi juu ya kazi, sina roho nzuri kwa mwakani, kwa hiyo kama kuna msanii anataka kujipanga kushindana na mimi, ajue tu kwamba mi sina roho nzuri mwakani", alisema Fid Q.

Pia Fid Q alipongeza uaandaaji wa tuzo hizo zilizofanyika tarehe 10 Desemba katika ukumbi wa Mlimani City, na kusema ameupenda mwanzo walioanza nao EATV.

MMILIKI wa Mtandao wa Jamii Forums Maxence Melo Akamatwa na Polisi...Anyimwa Dhamana

$
0
0

DAR: Mwanzilishi wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo akamatwa na Polisi kwa kukataa kutoa taarifa za siri za watumiaji wa mtandao huo.

Anyimwa dhamana atakaa rumande mpaka kesho atakapofikishwa mahakamani.

Maxence ameendelea kushikilia msimamo kuwa ni uvunjwaji wa Sheria na Haki za wananchi kufanya hivyo.

YOUNG D 'Kwa Mara ya Kwanza Nimejisikia Tofauti Sana Baada ya Kumbeba tu Mwanangu'

$
0
0
Rapper Young Dee amesema kupata mtoto kumempa furaha ambayo hawajawahi kuwa nayo katika maisha yake.

Young amesema:

Kwa mara ya kwanza nimejisikia tofauti sana baada ya kumbeba tu mwanangu. Yaani nimejisikia tofauti hali ambayo sijawahi kuisikia wala kutegemea nitaisikia. Kwahiyo ni feeling mpya kabisa, yaani amenifanya nimepata kitu ambacho sijawahi kuwa nacho, nimepata kama nguvu hivi. Amenipa kila sababu ya kuamka asubuhi kwa kumfikiria yeye, chochote ambacho nakipata kinaenda kwa yeye. Yaani mpaka sasa hivi ameanza kubadilisha ratiba zangu, yaani kuna lifestyle ambayo naweza kuona ameshaweza kunibadilisha kwasababu kuna vitu ambavyo sivioni tena kuwa na umuhimu. Kuhusu uhusiano na mama yake ni uhusiano ambao uko vizuri sana sababu ni wa muda mrefu sijawahi kuacha kuwasiliana naye. Kwahiyo na hivi mtoto amezaliwa, nina uhakika utaimarika zaidi.

Mtoto wa Young Dee ni wa kike na anaitwa Tamar.

BIFU la Alikiba na Dully Sykes...Alikiba Afunguka Haya

$
0
0
Mkali wa wimbo Aje Alikiba baada ya kuondoka na tuzo tatu za EATV, amefunguka na kuzungumzia mahusiano yake na msanii mkongwe wa muziki na producer, Dully Sykes.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kuenea kwa taarifa za muda mrefu katika mitandao ya kijamii kwamba wawili hao hawaelewani.

Katika usiku wa tuzo za EATV, Dully ndiye aliyemtangaza mshindi wa video bora ya mwaka Alikiba kupitia video yake ya wimbo ‘Aje’ kabla ya kukabidhiwa tuzo na Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza.

Akiongea muda mfupi baada ya kuchukua tuzo hiyo akiwa pamoja na Dully Sykes, Alikiba alizishukuru tuzo hizo kwa kumkutanishwa na Dully Sykes huku akidai yeye anamchukulia kama baba katika muziki.

“Mwenyezi Mungu leo ametukutanisha, huyu mimi ndiye aliyenianzisha, huyu ndiye aliyenifanya niamini mimi najua kuimba, nilichokuwa nikiimba brother Dully Sykes muda mwingine nilikuwa namtoa mpaka machozi,” Ali alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV akiwa mbele ya Dully Sykes. “Nisipotokea siku mbili hata siku moja kwao lazima ataniulizia Ali yupo wapi. Sina simu sina nini, Dully Sykes alikuwa ananipenda sana sijajua sasa hivi lakini mimi kwangu Dully ni brother wangu na ninaweza nikamuita baba yangu wa kimuziki wa bongofleva. Mimi sina mengi ya kusema ila nataka ajue kwama mimi nampenda siku zote na nitampenda mpaka nakufa,”

Naye Dully Sykes baada ya kusikia kauli hiyo ya Alikiba na yeye alisema hana tatizo na muimbaji huyo wa Aje na kusema anampenda pia.

HUMPHREY Polepole Ateuliwa Kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey PolePole ameteuliwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi kuchukua  nafasi ya  Nape Nnauye

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na chama hicho kupitia ukurasa wake wa Twitter zinaeleza kuwa kikao chaHalmashauri Kuu ya Taifa kimemteua Polepole kushika wadhifa huo.

Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kimefanyika leo ambapo miongoni mwa mambo mengi yatakayojadiliwa ni pamoja na tathmini ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kimemteua Ndg @hpolepole kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi.
— Chama Cha Mapinduzi (@ccm_tanzania) December 13, 2016

HAYA Ndiyo Maamuzi Ya Halmashauri Kuu Ya Taifa Ya CCM Baada Ya Kikao Chake Cha Siku Moja

$
0
0
Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana leo tarehe 13/12/2016 jijini Dar es salaam kwa kikao cha siku moja cha kawaida. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imepokea taarifa ya Tathimini ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, baada ya kuitafakari taarifa hiyo, Halmashauri Kuu imeamua yafuatayo;-

1. Kupunguza idadi ya wajumbe wa vikao na idadi ya vikao vya Chama katika ngazi mbalimbali ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa Chama na kuongeza muda wa viongozi wa Chama kufanya kazi za Chama kwa Umma badala ya kutumia muda mwingi vikaoni.

Ili kuwa  na vikao vya Chama vyenye tija imeamuliwa kama ifuatavyo:-

a). Halmashauri Kuu ya Taifa kwa sasa ina jumla ya wajumbe 388 idadi ambayo ni kubwa sana, hivyo imeamuliwa idadi hii ipunguzwe na kuwa wajumbe 158 kama  ifuatavyo:-

Wenyeviti wa Mikoa
Mikoa ya Bara           26x1    =      26
Mikoa ya Zanzibar      6x1   =          6

Wajumbe wa NEC wa Mikoa
 Mikoa ya Bara    26x1         =        26
 Mikoa ya Zanzibar   6x4         =        24
Wajumbe wa NEC wa Taifa
 Kutoka  Bara    =               15
 Kutoka  Zanzibar     =               15

Nafasi za Mwenyekiti   =                7

Wajumbe wa NEC wa Jumuiya
        UVCCM     =        5
        UWT   =        5
        WAZAZI    =        5
Wajumbe wa NEC kutoka Bungeni     =        5

Katibu wa Kamati ya Wabunge wa CCM      =       1

Wajumbe wa  NEC kutoka BLW   =       3

Katibu wa Kamati ya Wawakilishi =       1

Wajumbe wa NEC – wanaotokana na Nyadhifa zao
- Mwenyekiti wa CCM                  =       1
- Makamu Mwenyekiti (B)         =       1
-Makamu Mwenyekiti (Z)           =       1
- Makamu wa Rais                        =       1
-  Waziri Mkuu                               =       1
- Makamu wa Pili wa Rais (Z)   =       1
- Spika wa Bunge                          =       1
- Spika  wa  BLW                           =       1
- Mwenyekiti wa UWT                =       1
- Mwenyekiti wa WAZAZI          =       1
-Mwenyekiti wa UVCCM             =       1
- Katibu Mkuu – WAZAZI            =       1
- Katibu Mkuu – UWT                   =       1
- Katibu Mkuu – UVCCM              =       1
                                              Jumla:      158
#. Vikao vya kawaida vya Halmashauri Kuu ya Taifa vifanyike kila baada ya miezi sita badala ya miezi minne kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

b). Kwa upande wa sasa imeamuliwa wajumbe wa Kamati Kuu wawe 24 badala ya 34 kama ifuatavyo:-

Mwenyekiti wa CCM.
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)
Makamu Mwenyekiti wa CCM        (Zanzibar)
Makamu wa  Rais
Katibu Mkuu wa CCM
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM  (Zanzibar)
Waziri Mkuu
Makamu wa Pili wa Rais (Z)
Spika wa Bunge la Tanzania
Spika  wa BWL
Mwenyekiti  wa WAZAZI
Mwenyekiti  wa UWT
Mwenyekiti  wa UVCCM
Katibu wa   wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa  Organaizesheni
Katibu wa   wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa  Itikadi na Uenezi
Katibu wa   wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa  Uchumi na Fedha
Katibu wa   wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa  Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Wajumbe  watatu (3)  wa kuchaguliwa  na Halmashauri Kuu kutoka Tanzania

Wajumbe watatu  (3) wa kuchaguliwa  na Halmashauri Kuu kutoka Zanzibar.

#. Vikao vya kawaida vya Kamati Kuu vipunguzwe ili vifanyike kila baada  ya miezi minne badala ya miezi miwili isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

c). Kwa ngazi ya mkoa, Wajumbe wa Kamati za Siasa za Mikoa wapunguzwe kwa kuondoa wajumbe  watatu ambao ni:-
Katibu wa Uchumi na Fedha wa Mkoa         -       1
Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Mkoa        -       2

#. Vikao  vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya Mkoa vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila  mwezi kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

d). Kwa upande wa Wilaya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya wapunguzwe kwa kuwoandoa:-
 Katibu wa Uchumi na Fedha wa Wilaya    -       1
 Katibu wa Kamati ya Madiwani                   -       1
 Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Kuu ya (W)-  2
  Jumla:  4

#.Vikao  vya kawaida  vya Kamati ya Siasa ya Wilaya  vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila  mwezi isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

#. Muundo wa Wilaya za Chama uendane na muundo wa sasa wa Serikali.

Kata,Tawi na Shina
Idadi ya kuanzisha Shina iwe wanachama 50  hadi 300.

Idadi ya kuanzisha Tawi iwe wanachama kuanzia 301 hadi 1,000.
Hata hivyo idadi hii izingatie eneo la kijiografia na wingi wa wanachama katika eneo hilo.

Vikao vya kawaida vya  Kamati za Siasa  za  ngazi hizi viwe vinafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.

#. Nafasi za Uongozi
Mwanachama anatakiwa kuwa na nafasi  moja tu ya uongozi wa kazi za muda wote kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za uchaguzi wa Chama Toleo la 2012 kifungu cha 22 na 23 ambazo zimetajwa kuwa ni:-
Mwenyekiti wa Tawi,Kijiji au Mitaa.
Mwenyekiti wa Kata/Wadi.
Mwenyekiti wa Jimbo, Wilaya na Mkoa.
Makatibu wa Halmashauri Kuu wa ngazi zote zinazohusika.
Mbunge, Mwakilishi na Diwani.

#. Viongozi wa kuchaguliwa waepuke kuwa watendaji badala yake waongoze na kusimamia shughuli za Chama kwa kuzingatia Katiba na Kanuni.

#.Vyeo ambavyo haviko kwenye Katiba
Vyeo  ambavyo havijatamkwa kwenye Katiba ya CCM haviruhusiwi katika Chama au Jumuiya zake mfano Umoja wa makundi mbalimbali kama Wenyeviti wa ngazi mbalimbali (mfano: Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM n.k), Makamanda (UVCCM), Washauri (UWT) na Walezi (WAZAZI) katika ngazi zote.

#. Uhakiki wa Wanachama wa CCM
Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kufanya uhakiki wa wanachama wa CCM  na Jumuiya zake ili kujua idadi sahihi ya wanachama wetu kwa wakati huu.   Uhakiki huu uendane na kutoa kadi mpya za uanachama za kielektroniki ili kuwa na udhibiti wa usahihi wa wanachama na kuondoa wanachama HEWA. Aidha, Kadi za UWT, WAZAZI na UVCCM zifutwe ili tubaki na kadi za CCM tu.

#. Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi
Jumuiya za CCM  zimetakiwa kufanya kazi zake kwa kuzingatia matakwa ya Katiba ya CCM na Kanuni za Jumuiya husika, kanuni za Jumuiya ziendane na  matakwa ya Katiba ya CCM.

#.Uaendeshaji  wa shughuli zote za Jumuiya za Chama na mali zake uwe chini ya usimamizi wa Chama Cha Mapinduzi. (Baraza la Wadhamini la Chama Cha Mapinduzi).
Makatibu Wakuu wa Jumuiya watakuwa wanateuliwa na Kamati Kuu  na  Manaibu Katibu Wakuu watateuliwa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

#. Wakati tukiendelea kubaki  na Bendera yenye rangi ya kijani na njano  na  alama ya jembe na nyundo, Halmashauri Kuu imeona ipo haja ya kuzifanya rangi hizo kuwa na muenekano wa kuvutia zaidi.

#. Utumishi  katika  Chama na Jumuiya zake. Katibu Mkuu wa CCM na Sekretarieti ipewe majukumu ya kusimamia ajira za Watumishi wa Chama na Jumuiya zake.

Nafasi za Makatibu Wasaidizi wa Mikoa na Wilaya zitaondolewa na badala yake kazi zao zitatekelezwa na Makatibu wa Jumuiya  za Chama wa Mikoa na Wilaya kwa utaratibu utakaopangwa.  Utaratibu huu utakipunguzia Chama Cha Mapinduzi gharama na kujenga umoja wa utendaji kazi wa Chama na Jumuiya zake katika Mikoa na Wilaya.

#. Tathimini ya hali ya Kisiasa na  Uchaguzi wa    Zanzibar .
Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza kuundwa kwa Kamati maalum ya kufanya tathimini ya kina kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar kwa ujumla na masuala yanayohusu uchaguzi wa Zanzibar 2015.

# Mwenyekiti wa Kamati ya udhibiti na nidhamu ametakiwa akamilishe kazi ya taarifa ya udhibiti kwa wanachama waliokiuka mienendo ya kiuanachama kabla ya kuanza uchaguzi Mkuu wa Chama mwezi Februari 2017, Mikoa na Wilaya ambazo hazijaleta taarifa zao za kiudhibiti ziwe zimefikisha taarifa zao kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Udhibiti na Nidhamu kabla ya tarehe 30/01/2017.

#. Uhakiki wa Mali za Chama uendelee kufanyika kwa kina na uchambuzi zaidi ukikamilika Taarifa yake iwasilishwe kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa mapema iwezekanavyo.

#. Maamuzi na mapendekezo haya yatapelekea kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba ya Chama na Kanuni za Jumuiya  za Chama.

#. Kwa mambo yale ambayo yatahitaji mabadiliko ya Katiba, Mkutano Mkuu utaandaliwa mapema mwakani na kutafakari na kupitisha mabadiliko hayo ya Katiba.

Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameteua wafuatao kujaza nafasi mbalimbali ndani ya sekretarieti ambazo zimekuwa wazi kutokana na waliokuwa wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya kiserikali.

#.Ndg. Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi.
#. Col. Ngemela Eslom Lubinga- Kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Asha-Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi
#. Humphrey Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndg. Nape Nnauye aliyeteuliwa kuwa Waziri.
#. Wajumbe wengine watabaki kama walivyo sasa.

Imetolewa na:-

NAPE NNAUYE
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
13/12/2016

HATIMAYE Anayedaiwa Kutumia Akaunti ya @shilolekiuno_official Kutukana Watu Atupwa Segerea

$
0
0

Hatimaye anayedaiwa kutumia akaunti ya @shilolekiuno_official atupwa Segerea baada ya kukosa dhamana katika Mahakama ya Kinondoni Mapema jana👌👌👌👌👌sasa mjihadhali na MAPOVU yasiyo kuwa na lugha za kistaarabu huko Instagram vinginevyo mtaishia Ukonga au Segerea👌👌👌

MCHEZAJI Yaya Toure Ashtakiwa Kwa Kuendesha Gari Akiwa Amelewa...Mwenyewe Adai Yeye ni Mwislam

$
0
0
Mchezaji wa klabu ya Manchester City ambaye ni raia wa Ivory Coast Yaya Toure amesema hajapinga shtaka la kuendesha gari akiwa amelewa wiki mbili zilizopita.

Hata hivyo, amesema kwamba hakunywa pombe makusudi alipokamatwa akiendesha gari akiwa mlevi.

Ameandika kwenye Facebook kwamba “inafahamika wazi kwamba mimi ni Mwislamu na huwa sinywi pombe.”

Hata hivyo, hajaelewa ni vipi alijipata akinywa pombe ama akajipata akiwa amelewa bila yeye kufahamu.

Gazeti la The Mirror la Uingereza linasema kwamba alidai alikunywa Diet Coke na hakujua kwamba kwenye jagi aliyokuwa akitumia kunywa palikuwa pameongezwa kilevi aina ya brandi.

Gazeti hilo linasema amepigwa marufuku kutoendesha gari kwa miezi 18 na kupigwa faini ya $68,000 (£54,000).

Mchezaji huyo amesema: “Daima nimekuwa nikikataa pombe. Yeyote anayenifahamu na anayefuatilia uchezaji wangu atakuwa bila shaka ameniona nikikataa shampeni ya Mchezaji Bora wa Mechi kwa sababu ya kujitolea kwangu kuheshimu dini yangu.”

“Ni muhimu kwangu kwamba niliiambia mahakama kwamba sikunywa pombe makusudi. Jaji akinihukumu mwenye alikubali kwamba sikuwa nimekunywa pombe makusudi.”

Amesema kesi yake ilihitimishwa Jumatatu na kwamba alikubali shtaka.

“Kuendesha gari ukiwa mlevi ni kosa kubwa na ingawa sikunywa pombe makusudi, nakubali marufuku na faini na naomba radhi kwa yaliyotokea,” aliongeza.

Source: BBC

LOWASSA Aja na Mpya...Adai T.B Joshua Ameitabiria Ushindi Chadema

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema ataingia Ikulu baada ya miaka minne ijayo na rafiki yake T.B Joshua amemtabiria kuwa Serikali ijayo itaongozwa na Chadema.

Lowassa, ambaye alishika nafasi ya pili katika kinyang’anyiro cha urais mwaka jana, ameshaonyesha nia ya kuingia tena kwenye mpambano huo wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Akizungumza na viongozi na wanachama wa Chadema mkoani hapa, waziri huyo mkuu wa zamani alisema ana uhakika wa kuingia Ikulu bila ya umwagaji wa damu.

DONALD Trump Amteua Tajiri Kuwa Waziri wa Mambo ya nje Marekani

$
0
0
Rais mteule nchini Marekani Donald Trump amemteua Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Exxon Mobil, Rex Tillerson kuwa  waziri wa mambo ya nje wa  Marekani.

Tillerson(64) ni Mkurugenzi wa Kampuni ya kimataifa ya mafuta na gesi ya Texas, Marekani .   Pia,   miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa duniani.

Tillerson anatajwa kuwa na uhusiano mwema na rais wa Urusi Vladimir Putin jambo ambalo limewatia wasiwasi wa wana Democrat na baadhi ya wa Republican

Uteuzi huo unahitaji kuthibitishwa na bunge la Senate.

Siku chache zilizopita ilibainika kuwa majasusi nchini Marekani wanaamini kuwa Urusi ilihusika na kushawishi ushindi wa Trump.

BINTI Mtanzania Aliyelipwa BILIONI 1 Ufaransa Kwa Kazi ya Siku 1

$
0
0
Herieth Paul ni Binti Mtanzania mwenye umri wa miaka 20 tu lakini jina lake limekua kubwa kila kukicha nchini Marekani akiwa ni Mwanamitindo mwenye umri mdogo lakini amepiga hatua kubwa kwenye kazi ya Uwanamitindo, bonyeza play kufahamu zaidi. 
 VIDEO:
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images