Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

ALIYEKIMBIA Mgomo wa Madaktari Kenya Ajifungua Watoto 5 Tanzania,

$
0
0
Moshi. Raia wa Kenya, Bahati Tabu (37) amejifungua watoto watano mjini hapa Mkoa wa Kilimanjaro alikokimbilia kupata msaada kutokana na mgomo wa madaktari na wauguzi unaoendelea nchini humo.

Mgomo huo unaohusisha madaktari na wauguzi zaidi ya 5,000 wa hospitali za Serikali, ulianza Desemba 6, mwaka huu na kudaiwa kusababisha zaidi ya wagonjwa 40 kupoteza maisha.

Hata hivyo, watoto wanne kati ya hao walifariki dunia kwa kufuatana kila walipozaliwa katika Kituo cha Afya cha Faraja Himo.

Akizungumza na gazeti hili kituoni hapo jana, mzazi huyo alisema huo ulikuwa ni uzao wake wa 11 na tayari ana watoto 10, miongoni mwa hao kuna mapacha.



Aeleza alivyokimbilia Tanzania

Bahati alisema alishindwa kwenda hospitalini nchini kwao kutokana na mgomo wa madaktari na wauguzi unaoendelea kushinikiza nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi.

“Baada ya kuanza kuumwa uchungu, majirani walinichukua na kunileta Tanzania kujifungua na nilipofika hapa (Himo) nilikuwa tayari nakaribia kujifungua,” alisema Bahati.

Alisema alijifungua kwa njia ya kawaida watoto hao, wanne wakiwa wa kiume, lakini bahati mbaya walifariki dunia na kubakia na wa kike mwenye uzito wa gramu 600.

“Imeniuma sana, sina jinsi namuachia Mungu kwani ndiye anajua kwa nini ameamua kunipa na baadaye kuwachukua tena,” alisema huku akibubujikwa machozi.

Alisema alipokuwa mjamzito, alikwenda kliniki na kuambiwa ana watoto wanne na siyo watano, majibu ambayo yalimpa woga na hofu ya namna ambavyo angewalea. “Nilijawa na hofu baada ya majibu hayo kwa sababu nimekuwa nikilea watoto wangu mwenyewe na huu uzao wa jana (juzi) wa mapacha ni wa 11, awali nilishazaa tena mapacha,” alisema Bahati.

Alisema anaishi kwenye nyumba ya kupanga na kujishughulisha na kazi ya kufua nguo za majirani ili aweze kuwatunza watoto wake 10 na baada ya uzao wa juzi watakuwa 11.

“Hapa nilipo sijui nitatokaje hospitali kwa sababu hata mwanamume aliyenipa mimba hatuna mawasiliano mazuri. Majirani ndiyo wameenda kuchangisha fedha ili nilipe bili,” alisema.



Daktari aeleza watoto walivyokufa

Daktari kiongozi wa kituo hicho, Dk Samwel Minja aliliambia gazeti hili kuwa walimpokea Bahati juzi akitokea Taveta Kenya baada ya kukosa huduma.

“Wakati anakuja chupa ya uzazi ilikuwa imepasuka na alituambia kuwa mimba yake ilikuwa na miezi sita, lakini anajisikia uchungu. Tulivyompima tuligundua kweli ni mimba ya miezi sita, lakini tumbo lilikuwa kubwa kuliko umri wa mimba. Kabla hatujamfanyia uchunguzi zaidi, akaanza kujifungua mtoto wa kwanza ambaye ni wa kike akiwa na gramu 600 baada ya muda mfupi alijifungua mtoto mwingine akakaa kama dakika tano akafariki.

“Baada ya dakika 15 tena akajifungua mtoto wa tatu ambaye naye alikaa dakika tano akafariki. Baada ya robo saa akajifungua mtoto wa nne ambaye naye alikaa dakika tano akafariki. Baadaye tumbo la mama likawa linaonyesha bado lina watoto. Akaa baada ya nusu saa hivi alijifungua mtoto wa tano ambaye naye alifariki baada muda mfupi,” alisema daktari huyo.

Kwa mujibu wa Dk Minja, Bahati alijifungua salama watoto wake wote na hali yake inaendelea vizuri.



MR Nice Afunguka Haya Baada ya Kuzushiwa Amefariki Dunia.....

$
0
0
Msanii mkongwe wa muziki, Mr Nice amesikitishwa na watu ambao wamemzushia kifo katika mtandao wa kijamii.


Mtandao mmoja wa kijamii uliandika taarifa za uongo kwamba muimbaji huyo amefariki akiwa nchini Tanzania.

Mr Nice ambaye yupo nchini Kenya amesema alishangaa kuona watu wakimpigiwa simu kwa nyingi na kuulizwa kuhusu afya yake na alivyofuatilia akagundua kuna mtandao umeandika taarifa za uongo kwamba amefariki.

Kupitia facebook, Mr Nice aliamua kuandika taarifa hii:

East africa vibes nawashukuruni sana kwa kunizushia kifo sina la kuwajibu ,,ila mungu awalipe kadri ya vile mnavyostaili kwa hiki mlichonizushia leo ….mungu ni wetu sote na hasikilizi amri za binadamu so atakaponihitaji ataniita kwa mapenzi yake but si nyie east african vibes mnaoweza kuniua wala yeyote yule chini ya hili jua …kama nyie hamuioni thamani yangu hilo ni juu yenu kwani huku niliko mimi ni kama lulu na maisha yanaendelea tena kwa kiwango cha juu kabisa ..hii si mara ya kwanza kunizushia kifo na mambo mengine ya ajabu ajabu ila all in all mi nipo na bado mtaniona sana nikiendelea kuwepo ….im total dissapointed kwakweli …mungu awape stahiki yenu ..THANKS SANA EATV 13/12/2016

UPORAJI Magari Sio Dili Tena Mjini...Wezi 22 Wakamatwa Kwa Uporaji wa Magari

$
0
0
Kikosi  maalumu cha kupambana na wizi wa kutumia silaha na wizi wa kutumia nguvu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, kimewakamata watuhumiwa 22 kwa makosa ya kuwapora wenye magari na wapitanjia kwenye mataa ya kuongozea magari.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Simon Sirro alisema watuhumiwa hao, wamekuwa wakijiunda kwenye vikundi na kuwanyang’anya watu wenye magari na watembea kwa miguu mali zao kama simu za mikononi, kompyuta, saa na fedha.

Alisema ufuatiliaji ulifanyika na kuwakamata watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti, ambapo Desemba 11 mwaka huu huko Temeke maeneo ya Keko Magurumbasi na mataa ya Veta na Chang’ombe walikamatwa watuhumiwa 10 kwa makosa ya wizi kutoka maungoni na wizi kutoka kwenye magari.

Aliwataja baadhi ya watuhumiwa hao kuwa ni Ayubu Amiri (19), mkazi wa Mtoni Mtongani, Shabani Fadhili(18) mkazi wa Keko, Herman Francis (26), mkazi wa Keko Magurumbasi na wenzao saba.

“Katika mahojiano watuhumiwa wamekiri kujihusisha na makosa mbalimbali yakiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha na kutumia nguvu,” alisema.

Aidha alisema uchunguzi wa awali umebaini mtuhumiwa Herman Francis anakabiliwa na tuhuma za mauaji, ambapo Machi 20 mwaka huu alimchoma mtu kisu na kutoroka kusikojulikana.

Wakati huo huo, Desemba 12 mwaka huu askari waliwakamata watuhumiwa wengine 12 kwa makosa ya wizi kutoka kwenye magari.

Watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Sande Kassim (18), mkazi wa Keko, Emmanuel Abeli (21), Paulo Abeli(18), Jafari Nyerere (22), Hamis Salum (22), Hemed Idrisa(22) wote wakazi wa Keko na wenzao sita.

Katika tukio lingine, polisi wamewakamata watuhumiwa wanne wanaojihusisha na wizi kwa kuwarubuni watu kwa kukodi magari yao na baadaye hutumia nguvu  kuwapora.

Watuhumiwa hao wametajwa kuwa ni Juma Kajeni (35), mkazi wa Tabata, Hamadi Kaganda (38), mkazi wa Mbagala, Mashaka Ally(62), mkazi wa Yombo na Mshamu Ally (32), mkazi wa Mtongani.

Alisema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.

Pia aliwatahadharisha wananchi na wamiliki wa magari kuwa makini kwa watu hao ambao huja kwa nia ya kuwalipa fedha nyingi au kukodi gari kwa kiwango kikubwa na kisha wanatokomea na gari.

Wakati huo huo, polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kupitia kikosi kazi chake cha kupambana na wizi wa magari kimekamata magari matatu ya wizi katika mikoa mbalimbali.

Sirro alilitaja gari lenye namba T 386 CGY aina ya Verosa rangi nyeusi, mali ya Abraham Robert wa jijini Dar es Salaam na gari hilo lilikamatwa mkoani Mbeya likiwa limetelekezwa.

Gari jingine ni lenye namba T 946 DGH aina ya IST rangi ya fedha ikiwa inaendeshwa na mtuhumiwa aitwaye Hamadi Saidi (27) mkazi wa Kimara Dar es Salaam ambalo lilikamatwa huko mkoani Morogoro, gari hilo liliibiwa maeneo ya Kawe Beach jijini Dar es Salaam.

Alilitaja gari lingine kuwa ni Mitsubishi Canter lenye namba T 753 CVZ ambazo ni namba bandia huku namba zake halisi zikiwa ni T.815 DJF mali ya Magreth iliibiwa maeneo ya Kimara Suka jijini Dar es Salaam.

Alisema mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa anaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika atapelekwa mahakamani.

Pia alisema  watuhumiwa wengine waliohusika na wizi wa magari hayo wanaendelea kutafutwa ili kubaini mtandao mzima wa wizi wa magari na watuhumiwa wengine wanaotafutwa kwa wizi wa magari hapo nyuma ambao walikimbia.

PROFESA Jay Akunwa Kisawa Sawa na Mwanamuziki Darasa Atoa ya Moyoni na Kumwambia Hivi

$
0
0
Mafanikio ya Mwanamuziki Darasa kwenye muziki yamemfanya Prof Jay Kusema haya Kupitia mtandao wa Instagram, Jay ameandika:

Mdogo wangu @darassacmg Imani yako, Kutokukata tamaa na Struggle yako ya Usiku na Mchana ndio imekufanya ufikie hapo ulipofikia, Nakumbuka wakati unashoot Wimbo wako wa USIKATE TAMAA uliniambia unatamani ufikie level za juu kama zetu, Nami nilikwambia hakuna kinachoshindikana chini ya JUA Ukiset GOALS, kufanya kazi kwa bidii na SALA yote Yanawezekana, Naamini kwa style hii ya JIWE juu Ya JIWE, NDOTO yako inakwenda kuwa kweli, Cha MSINGI usiridhike na mafanikio haya..HUU ni mwanzo tuu na mafanikio makubwa zaidi yako at your DOOR, Keep your eyes open and Keep ya HEAD UP,
SKY IS THE LIMIT, GO GET DEM… BLESS
#ACHA MANENO WEKA MUZIKI
@darassacmg @darassacmg

KASHFA Nzito Jeshi la Polisi na GSM

$
0
0
NSATO Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi pamoja na vigogo wengine wa serikalini wanatuhumiwa kushindwa kumsaidia Mtanzania Abdulswamadu Zacharia Omary (36) anayedai kutendewa vitendo vya kikatili, anaandika Josephat Isango.

Ukatili huo ni pamoja na kudhulumiwa mali na wafanyabiashara Said Sadi na Ghalib Said Mohamed.
Akisimulia mkasa huo huku akilia, kijana huyo anadai kufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo kutaka kunyongwa ndani ya chumba cha mahabusu kilichopo Kituo cha Polisi Oystebay, kitendo anachosema kiliratibiwa na jeshi hilo kuwasaidia wafanyabiashara hao kupoteza ushahidi lakini amekuwa akilalamika bila kusaidiwa.

“Nimekuwa nikitumiwa na baadhi ya vigogo wa polisi wanajidai kutaka kunisaidia lakini wakifika kwa huyu jamaa wanakaa kimya, polisi wanashirikiana na huyu aliyekuwa mmiliki wa Home Shoping Centre (HSC), kutesa watu, na mimi wanakataa kunilipa milioni zaidi ya 250, nilizofanyia kazi nikiwa kwao Yemen,” anasema Omary.

Akisimulia mkasa wa tukio, Omary anasema alipewa zabuni ya kujenga jengo la ghorofa 3 nchini Yemen bila kupewa mkataba, akakataa lakini alinyang’anywa hati zake za kusafiria na kuteswa kikatili hali iliyopelekea akubali.

“Nilisaidiwa na watu wa shirika la kimataifa la wahamaji (International Organisation for Migration) kurudi Tanzania, lakini tangu nimerejea nchini, hawa jamaa wa iliyokuwa Home Shoping Centre na GSM wana nguvu serikalini hadi ndani ya vituo vya polisi,” anasimulia.

Katika barua yake ambayo amewaandikia viongozi kadhaa wa taasisi za serikali ambayo MwanaHALISI online imeiona Omary amesema, viongozi hao wamewekwa kwenye mfuko na wafanyabiashara hao, kiasi cha kuifanya serikali idharaulike.

“Unasikia, hili suala linajulikana pote polisi, afande Marijani analipotezea kwa muda mrefu, nilielekezwa kwa afande wa Interpol anaitwa Ngonyani.
“Pia Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, (Takukuru) wanalifahamu lakini ndugu yangu kila aliyetaka kunisaidia huishia kukaa kimya, natamani sasa kumwona rais anisaidie,” anasisitiza.
Omary katika andishi lake ametaja hata viongozi wa dini ambao wamekuwa wakijipatia fedha kutokana na tatizo lake ambalo polisi wameshindwa kulifanyia kazi.

Ninatishwa, ninaambiwa hawawezi kufanywa lolote ndani ya nchi hii, wakisikia nimelalamika kwenye ofisi yeyote ya serikali hata polisi hunijibu “wewe unapolalamika unaenda kwao, sisi tunawaita wanakuja tulipo, unajihangaisha.”

Anadai tarehe 23 Julai 2015 alitekwa na Gharib Said Mohamed pamoja na Faisal kisha kupelekwa Masaki na kwamba, alipigwa na akawa hajitambua.

“Nilipojitambua nilijikuta Kituo cha Oysterbay nimefunguliwa mashtaka likiwemo la kumtukana rais, kutaka kulipua Ikulu, kukutwa na silala na niliwekwa rumande siku 46 bila kufikishwa mahakamani na namba ya jalada ilikuwa OB/IR/6365/2015, na OB/IR/11770/2015.
Nilipofikishwa mahakamani nilikuta mashtaka tofauti ambayo yalifutiliwa mbali na hakimu sababu hayakuwa ya kweli.

MwanaHALISI Online, limewasiliana na afande Lucy Ngonyani, aliyeshughulikia suala hilo na kukiri kuwa, analifahamu, yupo likizo na yeye sio msemaji wa jeshi hilo.

Alipoulizwa Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo alisema, “huyo kijana anapaswa afike ofisini kuniona, kama suala lake halijatekelezwa sio kuja huko kwa vyombo vya habari.”
Mtandao huu uliwatafuta watuhumiwa hao (Said Sadi na Gharib Sadi Mohamedi) kupitia simu zao za mkononi, pamoja na simu zao kuita kwa muda mrefu, hazikupokelewa.

Na hata walipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno kwenye simu zao, hawakujibu.

Chanzo:Mwanahalisionline

MWENYEKITI wa UVCCM Aliyeshitakiwa Kwa Kughushi Kitambulisho Cha Usalama wa Taifa Aachiwa Huru

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi(UVCCM), Arusha ameachiwa huru baada ya Jamhuri kusema hawana nia kuendelea na kesi hiyo, Mwenyekiti huyo wa UVCC alidaiwa kughushi kitambulisho cha Usalama wa Taifa.

Jeshi la Polisi Mkoani humo lilimkamata mnamo Septemba 2017 Mwenyekiti huyo wa UVCCM Mkoa ndugu Lengai Ole Sabaya kwa tuhuma za kughushi nyaraka mbali mbali za serikali (vikiwepo vitambulisho vya Idara ya Usalama wa Taifa ). VIDEO:

ALIKIBA Kaamua Kabisa Kuingia Studio na Mwanamuziki Vyonne Chaka Chaka Baada ya Kukutana

$
0
0

Alikiba ndani ya Studio nchini South Africa. ...Akipika Ngoma na Mama wa Muziki Africa...Yvonne ChakaChaka..!!
Unahis Ngoma itakuwaje? ?? Hapa kingkiba pale Mama ChakaChaka. ..toa utabiri wako hapa👇

SIKILIZA Wimbo Mpya wa Lady Jay Dee Akiwa na Mpenzi Wake Mpya Spicy......

$
0
0
Hivi karibuni kulikuwepo na tetesi nyingi sana katika mitandao ya kijamii zikisema kwamba mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Lady Jaydee amefunga ndoa na mwanamuziki wa Nigeria, Spicy, na sasa wawili hao wameachia wimbo wa pamoja, Together Remix



ALICHOANDIKA Kajala Baada ya Tetesi Kuwa Amerudiana na Petit Man

$
0
0
Katika mapenzi kuna kuwa pamoja na kuacha na cha msingi watu wanachokizingatia ni ku-move on na maisha, Kajala Masanja na Petit Man walikuwa wapenzi. Tena ilifikia kipindi  Kajala yupo jela, Petit alikuwa akimhudumia kwa kiasi kikubwa.

Lakini baadaye kila mmoja aliendelea na maisha yake ikiwemo Petit kumuoa dada yake Diamond, anayejulikana kama Esma. Lakini siku za hivi karibuni, wawili hao wameonekana kuwa karibu tena kiasi cha kuwafanya watu wahisi wamerudiana. Kajala amelazimika kuzizungumzia tetesi hizo na kukanusha kurudiana na ex wake huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo Kajala ameandika:

"Jamani i think this is too much sasa na mnavuka mipaka. ifike muda watu muwe mnatumia akili kufikiria mnavyotaka kusema. Hivi kama ulishakuaga na mahusiano na mtu na hayo mahusiano yakaisha So huruhusiwi kuongea nae?? Are you guys Owkay?? Hivi mnajua mchango wa Petit katika maisha yangu? Mnajua jinsi alivyonisaidia wakati niko katika kipindi kigumu cha jela? Au mnakua mnaongea tu ili mfurahishe watu... Petit sasahivi ni part ya familia yangu na sio mambo ya mapenzi. Kwani mimi sijui kama ana mke na ana familia? Why watu mnakua na akili fupi sana za kufikiri....mimi siwezi kuwa na ugomvi na esma kwasababu ya petit...esma ni mke wake na wana mtoto na kila mtu anajua...na mimi nitaendelea kumchukulia petit kama ndugu na rafiki wa karibu kwasababu ya mchango na msaada wake katika maisha yangu. Sitoacha kuongea na petit kwa ajili ya ujinga wenu mnaosema...haitawahi kuja kutokea...sasa basi, i think am clear na tumeelewana kabisa...nyie ndo mnakuaga chanzo cha watu kugombana bila sababu..tafuteni kazi za kufanya... have a lovely evening"

WAZIRI wa Afya wa Afrika Kusini Atoa Kali..Adai Wanaume Ambao Ucheza Dansi Sana Kumbi za Starehe Wana Maumbile ya Siri Madogo

$
0
0
Waziri wa Afya wa Afrika Kusini, Aaron Motsoaledi amezua mshangao mkubwa nchini humo baada ya kuwaonya wasichana akisema kuwa wanaume ambao hucheza sana kwenye sherehe na kumbi za starehe huwa na maumbile madogo ya uume.

Wanaume hawa huwa na fedha nyingi sana  na wanapokuwa katika kumbi za starehe hununua vinywaji vya ghali sana kiasi kwamba ni rahisi kuwavutia wasichana. Mara nyingi hupenda kucheza katikati ya ukumbi au hata juu ya meza sababu hupenda kuonekana na watu. Kaa mbali nao watakuambukia UKIMWI na maumbile yao ya siri madogo, alisema waziri huyo.

Lakini pia Waziri aliwaasa watu kuchukua tahadhari na kutumia kinga ili kujizuia na magonjwa ya ngono na mimba ambazo hazitarajiwi.

Audha, Waziri Aaron aliwataka wanaume haoa wenye maumbile madogo sehemu za siri kukaa mbali na watoto wa kike. Tunawatazama kaeni mbali na watoto hawa, alisema waziri.

Aliyetobolewa Macho Uso Kwa Uso na Scorpion Mahakamani

$
0
0

Kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’ imeendelea katika mahakama ya wilaya ya Ilala wakati shauri hilo lilipoletwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Wakati mshitakiwa akipandishwa kizimbani alidai ana wakili wake hivyo mahakama ilisubiri kwa muda wakili wa mshitakiwa Juma Nassoro na baada ya kufika mahakamani ndio kesi ilianza kusikilizwa.


Kesi hiyo ina mashahidi sita na mpaka sasa ameshasikilizwa mmoja ambaye ni shahidi namba moja Said Mrisho ‘aliyetobolewa macho’ ambaye leo December 14 2016 ametoa ushahidi wake mahakamani hapo akielezea tukio alilofanyiwa.


Baada ya kusikiliza kesi, mahakama hiyo imeahirisha shauri hilo hadi December 28 mwaka huu ambapo itaendelea na shahidi wa pili. 

MBUNGE Lema Anyimwa Dhamana Tena Leo....Wafuasi Watawanywa Kwa Mabomu ya Machozi

$
0
0

ARUSHA: Mbunge Lema amenyimwa dhamana amerudishwa Magereza ya Kisongo, kesi kusikilizwa tena siku ya Ijumaa, tarehe 16 Desemba 2016.

Inadaiwa kuwa baadhi ya wafuasi waliokusanyika mahakamani kusikiliza kesi hiyo walitawanyishwa kwa mabomu ya machozi.

KITUO cha Sheria za Haki za Binadamu(LHRC) Kimelaani Kukamatwa Kwa Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo

$
0
0

Kituo cha Sheria za Haki za Binadamu(LHRC) na Kituo cha Utetezi wa Haki za Binadamu(THRDC) kimelaani na kukemea kukamatwa na kuwekwa kizuizini Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo.

Vituo hivyo vimesema Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 1985 inayolitaka Jeshi la Polisi kutomshikilia mtu kwa zaidi ya masaa 24 bila kufikishwa Mahakamani.

Vimelitaka Jeshi la Polisi kuheshimu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara ya 15 inayotoa haki kwa kila mtu kuwa huru na kuishi kama mtu huru.

SIKILIZA Hapa Wimbo Mpya wa Nay wa Mitego Unaoitwa Siwezi

$
0
0
Baada ya nyimbo zake kadhaa zilizopita kuwa controversial, Nay wa Mitego ametuliza mpira kidogo na kuandika wimbo wa mapenzi, Sijiwezi. Umetayarishwa kwenye studio zake za Free Nation. Usikilize hapo chini.

Bonyeza Play Kusikiliza

WAFUASI wa CUF Watwangana Tena Mahakamani

$
0
0
Wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) kwa mara nyingine wametwangana tena makonde mahakamani.

Leo ni mara ya pili kwa wafuasi na wanachama wa chama hicho kutwangana makonde mahakamani wanapofika kusikiliza kesi inayozihusisha pande mbili za chama hicho.

Pande hizo ni  kati ya Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

Ugomvi huo ambao umewahusisha walinzi wa viongozi wa chama hicho maarufu kama mabaunsa wa pande hizo mbili umezimwa na askari polisi sasa hivi.

Kwa sasa wafuasi wa pande zote wameingia mahakamani wanasubiri jaji aingie kwa ajili ya kusoma ya kusoma uamuzi wa maombi ya upande wa Maalim Seif kumtaka Jaji Sekieti Kihiyo anayesikiliza kesi hiyo ajiondoe kwa madai kuwa hawana imani naye.




MATARAJIO Makubwa ya Kupata Kazi Baada ya Masomo, Yanatuponza - stuffzoom

$
0
0
Ni kweli kwamba tunapokuwa vyuoni au tunapopata nafasi za kujiunga na vyuo wengi wetu matarajio ni kumaliza na kuja kupata kazi nzuri zenye mishahara minono minono.

Ila matarajio huwa sio pale tunapomaliza vyuo na kukuta tunamaliza siku, miezi, miaka bila kupata kazi. Huwa inakatisha tamaa sana kwani hapo mwanzo matarajio yalikuwa makubwa sana na wengine huamua tu hata kuendelea na masomo ya juu kama uwezo upo huku wakiwa wanaendelea kutafuta kazi taratibu, au hata kuta tamaa kabisa na keundelea na mambo mengine.

Kuna namna ambavyo elimu yetu ya Tanzania inashindwa kuwatengeneza watu wakiwa bado vyuoni au masomoni, wanashindwa kutengeneza watu kukabiliana na wakati uliopo, na changamoto zake. Wanashindwa kutengeza watu kutotegemea ajira tu na kufikiria vitu vingine kama kujiajiri na kuwa wabunifu. Elimu yetu ni bado ile ya kukremishwa na misingi yake haina mashiko na maisha halisi ambayo mlengwa atakuja kupitia baada ya masomo yake, Hivyo hili ni tatizo kubwa sana na linahitaji ufumbuzi wa haraka.

Ushauri kwa serikali, Mfumo wa elimu yetu ya Tanzania unabidi kuangaliwa tena upya, kuna haja ya kubadilisha namna ya ufundishaji, uwe wa maisha halisi zaidi na kwenda na wakati, zama zina badilika kila siku lakini mitaala ni ile ile ya miaka hamsini iliyopita. Hakuna ubunifu kwenye baadhi ya mafunzo. Watu wanabidi wapewe elimu za kujitegeme na sio Kutegemea ili kuepusha "Disappointment" Baadae

Hapo chini ni njia chache unazoweza kutumia kupata ajira mpya, au kupata ajira bora zaidi

1. Sasa hivi sio muda wa kusoma tu course kwasababu unaipenda, soma kitu adimu, chenye soko kwenye ajira, Ajira ni ushindani kwasasa, hivyo ilikushinda lazima uwe na kitu ambacho wengi hawana.

2. Usichoke hata mara moja kutafuta kazi, na wala usivunjike moyo kama umeshaitwa kwenye interviews kadhaa na haziku zaa matunda, jua kwamba unavyofanya interviews nyingi zaidi zinakujenga na kukupa ujasiri zaidi na pia kujua makosa yako na kujirekebisha.

3. Omba kazi ambayo unaona unafiti, kulingana na elimu yako na ujuzi. Usiombe tu kazi kwasababu umeona Tangazo, na hiki ndio chanzo wakati mwengine chakutuma maombi mengi yasiyo na mafanikio.

4. Tengeneza Connections Zenye Faida, chati pia wasiliana na walio kutangulia kupata kazi, Maana Kazi nyingi siku hizi zinatangazwa ndani kwani ndani (internally) na ndio mana kuna makampuni huwezi kuona popote wametangaza kazi, Lakini wanaajiri .

5. Usidharau mitandao kazi nyingi hutangazwa Mitandaoni siku hizi, achana na zama za zamani za magazeti, Tembelea mitandao tofauti kama >> http://stuffzoom.com/

Nakutakia kila la Heri kwenye Pilika za Maisha - Stuffzoom

MADHARA ya Kutofanya Tendo la Ndoa Muda Mrefu

$
0
0
Habari zenu, nimeona niwaletee hili nina imani mtajifunza hasa kwa wale wasiofahamu,Ukikaa Muda Mrefu bila Kufanya tendo la Ndoa madhara yake ni kama haya:

Hasira za mara kwa mara katika mambo madogo,
kupendelea sana kuangalia picha za uchi,
Kusahausahau,
Kupendelea story za mapenzi,
Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mke),
Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu),
Kuumwa na kichwa,
Kukakamaa mgongo (wanaume),
Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba,
Kupoteza umakini ktk kazi (efficiency),

Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno,
Waweza ku-develop tabia mpya ambayo hukuwahi kuwa nayo ili iwe mbadala kama ulevi n.k.

UJUMBE wa Alikiba Baada ya Kukutana na Yvonne Chaka Chaka SA

$
0
0
Hitmaker wa wimbo wa Aje, Alikiba amepata bahati ya kukutana na nguli wa muziki nchini Afrika Kusini, Mama Yvonne Chaka Chaka wiki hii wakati alipokuwa mjini Johannesburg kwa ajili ya kutumbuiza kwenye utoaji wa tuzo za Mkhaya Migrants Awards.

Haikuwa kazi ngumu kwa Kiba kuonyesha hisia zake kupitia mtandao wa Instagram za kufurahishwa kukutana na muimbaji huyo wa nyimbo kibao zilizowahi kufanya vizuri duniani ikiwemo ‘Mamaland’ ambaye ilikuwa ndoto yake ya siku nyingi.

Kupitia mtandao huo, Ali ameandika:

It was a great honor and pleasure to meet Mama Yvonne Chaka Chaka who I have loved and admired all my life . Thank you for hosting us and sharing your memories, advices and guidance. I am truly grateful and looking forward to our project #KingKiba

WASOMI, Wachambuzi na Maaskofu Wafurahishwa na Magufuli Kwa Muundo Mpya wa CCM

$
0
0
WASOMI, wanasiasa wakongwe, wachambuzi wa kisiasa na viongozi wa dini nchini, wamepongeza muundo mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofikiwa juzi katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) chini ya Mwenyekiti wake wa Taifa, Rais John Magufuli.

Wameeleza kuwa muundo huo, utakiwezesha chama kushindana vizuri kisiasa.

Aidha wamesema Magufuli anavaa viatu vya Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika muundo huo wa idadi ndogo ya watendaji makini, lakini pia utasaidia kulinda siri za chama, kubana matumizi na kuwajibika ipasavyo kuisimamia Serikali.

Wamepongeza hatua ya Mwenyekiti wa chama hicho, Magufuli, ambaye pia ni Rais wa Tanzania, kumbakiza Katibu Mkuu wa chama, Abdulrahman Kinana kwani imeonesha kuthamini kazi kubwa aliyofanya katibu mkuu huyo ya kufufua chama kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, walisema kuwa maamuzi hayo yamefanyika kwa wakati muafaka na yalikuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu.

Mwanasiasa mkongwe nchini, Dk Chrisant Mzindakaya alisema uamuzi uliofanywa na Magufuli walikuwa wakiyasubiri kwa muda mrefu, kwani ndiyo muundo uliokuwepo siku za nyuma chini ya uenyekiti wa Mwalimu Nyerere.

Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Mzindakaya ambaye ni mwanachama wa chama hicho, alisema chama kikubwa kama hicho mabadiliko ni muhimu, kwa lengo la kujenga hali mpya kwa wanachama wake kwa ajili ya maslahi ya chama na wanachama wake.

Alisema kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu, walikuwa wengi zaidi ya wabunge, lakini awali kila mkoa ulikuwa na mjumbe mmoja, lakini kwa sasa kila wilaya kulikuwa na mjumbe, jambo lililofanya kudhoofisha nguvu ya chama na kutoka kwa siri za chama nje mara baada ya kikao.

“Kawaida maamuzi makubwa ya chama yanayofanyika ni siri, lakini hali ilikuwa tofauti kwani kila siri ilikuwa ikitoka nje; huku kuwa na utitiri wa viongozi kulisababisha chama kupata gharama kwa kuwalipa pale inapoitishwa mikutano ya Halmashauri Kuu,”alisema.

Dk Mzindakaya ambaye alikuwa waziri katika serikali zilizopita, alisema katika uteuzi wa wataalamu kwenye sekretarieti ni muundo muhimu, kwani sekretarieti ipo kwa ajili ya kumsaidia katibu mkuu.

Alisema kazi za kiutendaji hazitakiwi kufanywa kwa siasa, bali kwa kutumia utaalamu hivyo Mwenyekiti amefanya jambo sahihi.

Alisema pia ndani ya chama hicho, kulikuwa na tabia ya baadhi ya watu kujilimbikizia vyeo, kwani ilikuwa si jambo la ajabu kumuona mbunge akiwa pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na wakati mwingine ni mwenyekiti wa chama hicho mkoa.

Alisema jambo hilo lilisababisha wanachama wengine kukosa fursa kutokana na wajumbe hao, kulinda maslahi yao binafsi ya kisiasa na kiuchumi.

“Uamuzi huu kwa kweli wa kubadili muundo ni muhimu sana na unapaswa kupongezwa kwani kuna watu walikuwa na vyeo vingi katika chama kwa maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi huku wakiwakosesha wanachama wengine wenye uwezo fursa ya kukiendesha chama,“ alisisitiza Dk Mzindakaya.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kijamii, Dk Benson Bana alimpongeza Mwenyekiti wa Chama hicho kwa hatua aliyoifanya, kwani ameonesha kuwa anataka kuwa na CCM mpya.

Alisema mabadiliko anayoyapendekeza, yanayohusu marekebisho ya katiba, ni marekebisho chanya kwa uhai wa chama na kukipa chama nguvu mpya ya kukabiliana na mazingira ya kisiasa ya leo na chama kukirudisha kwa wananchama.

“Hiki ni chama cha wanachama kwaajili ya wanachama na alichokifanya Magufuli ni kuonesha nia ya kufanya,” alisema Bana.

Pia, alisema jambo alilolifanya Magufuli, la kupunguza mlolongo wa matumizi na vikao na wajumbe ndani ya vikao, ni jema na litasaidia mno chama.

“Hatuna ushahidi kama wingi wa wajumbe wengi, ndio ubora wa vikao, unaweza ukawa na wajumbe wachache na ukafanya jambo zuri; na siku zote mambo mazuri hayafanywi na watu wengi, yanafanywa na watu wachache na Magufuli ameliona hilo,” alisema Bana.

Aidha, alisema suala la kufuta vyeo mbalimbali katika chama, ni jambo zuri kwakuwa limeondoa wale watu ambao walitaka kukishikilia chama na kuona wa ndio wenye chama.

“Wapo waliokuwa ni makamanda wa chama, mara kamanda wa vijana, au mlezi wa wazazi. Haya yote yalikuwa yanazidisha chuki, fitina na ushindani usio na tija ndani ya chama, kwahiyo ni vizuri ameyafuta haya,”alisema.

Pia, alimpongeza Rais kwa kuwateuwa vijana ambayo ni damu mpya na kuwaacha wazee.

“Tunaamini vijana walioteuliwa, wanaweza kuhimili mikikimikiki kujibizana na vijana wa vyama vigine. Kwenye sekretarieti tungependa kati ya watatu aliowachagua mmoja angekuwa mwanamke, lakini nadhani kwa sasa hivi nguvu zake zipo kwenye kuleta ufanisi zaidi kuliko mambo mengine,”aliongeza.

Mwanasiasa maarufu Profesa Mwesiga Baregu alisema mabadiliko aliyofanya Magufuli lazima yatakuwa na sababu zake; na kwamba labda mwenyekiti huyo wa chama, ameona hawezi kufanya kazi na watu wengi.

Alisema kwa upande mwingine, mabadiliko hayo yanaweza kubinya demokrasia, lakini pia ameangalia watu wa kufanya kazi naye.

Baregu alisema kiini cha mabadiliko hayo, hakijajulikana, lakini amefumua muundo wa chama hicho kwa kuwatoa wale waliokuwemo katika uongozi wa awamu ya nne.

Wakati huo huo, Askofu wa Kanisa la Good News for All Ministry, Dk. Charles Gadi amekipongeza chama hicho cha CCM kwa mabadiliko waliyoyafanya na kuingiza vijana katika safu ya uongozi.

Askofu Gadi alisema chama hicho kimeonesha ukomavu wa kisiasa, hasa kwa kukiamini kizazi cha vijana ambao wanatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa ya kiuutendaji ndani ya chama hicho.

“Tunaamini kwamba CCM kwa kuwaweka vijana wengi watafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa sababu vijana hawa tayari walishaonesha utendaji wao katika maeneo tofauti,” alisema.

Aidha alisema hatua ya CCM kupunguza idadi ya wajumbe, itapunguza gharama za uendeshaji, hivyo kuongeza ujenzi wa miradi mbalimbali kupitia fedha hizo.

“Tunaamini kwamba kwa kupunguza gharama ya wajumbe, fedha hizo zinaweza kutumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya kijamii ikiwemo kujenga shule, maabara, madawati, hospitali na kuongeza upatikanaji wa dawa hospitalini,” alisema.

Katika kikao hicho cha NEC kilichofuatia kikao cha Kamati Kuu (CC) ya chama hicho kilichokaa Jumapili, idadi ya wajumbe wa NEC ilipunguzwa kutoa wajumbe 388 hadi wajumbe 158, ikiwa na maana kuwa wajumbe 200 wataondolewa kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM.

Wajumbe wa Kamati Kuu (CC) kutoka 34 hadi 24, wajumbe wa Kamati za Siasa za Mikoa wamepunguzwa watatu, wakati wilayani wameondolewa wanne; pamoja na kufutwa kwa vyeo vya Makatibu Wasaidizi wa Wilaya na Mikoa na wa Mchumi wa Wilaya na Mkoa.

Pia nafasi za uteuzi za wajumbe wa NEC za Mwenyekiti, zimepunguzwa kutoka 10 hadi saba.

Magufuli alisema hatua hiyo ni ili kutoa nafasi kwa viongozi na wanachama, kufanya kazi za chama kwa ufanisi Aidha, Magufuli alimbakiza katika nafasi yake ya Ukatibu Mkuu, Kinana huku sura mpya katika jamii zikichukua nafasi kubwa za uongozi katika chama hicho.

Miongoni mwa walioteuliwa ni Rodrick Mpogolo aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu upande wa Tanzania Bara na Humphrey Polepole anayekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, akichukua nafasi ya Nape Nnauye ambaye ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Yumo pia Kanali Ngemela Lubinga aliyeteuliwa kuwa Katibu wa NEC wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

Mbali na uteuzi, pia Magufuli alisema kwa kuwa kumekuwa na vitu na watu hewa katika kila eneo nchini, pia katika CCM kunahitajika uhakiki wa wanachama hewa.

Katika uhakiki huo utakaofanyika nchi nzima, pia alisema chama kitaanzisha mfumo wa kadi za kieletroniki na kuachana na kadi za sasa, zikiwamo za jumuiya yake ambazo zinafutwa rasmi.

Mabadiliko hayo makubwa ambayo baadhi yanahusisha Kanuni na Miongozo, yataanza mara moja na yale yanayohusisha Katiba ya CCM, yatapata idhini ya Mkutano Mkuu utakaoitishwa Februari mwakani na yamehusisha pia kufutwa kwa baadhi ya nyadhifa.

Aliposhika hatamu za CCM mjini Dodoma, katika hotuba yake, Dk Magufuli alieleza azma yake ya kuijenga CCM mpya, ikiwamo kuondokana na vyeo visivyokuwa na tija na pia kupunguza idadi ya wajumbe wakiwamo wa NEC.

Habari hii imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko, Lucy Lyatuu, Sophia Mwambe na Hellen Mlacky.

DAVIDO Aupigia Promo Wimbo Alioshirikishwa na Diamond Nchini Ufaransa

$
0
0
Davido ameonyesha kuwa bado anaukubali wimbo wa Diamond aliowahi kumshirikisha ‘Number One Remix’.

Wakati akifanya onesho nchini Ufaransa kwenye mji wa Paris wikiendi iliyopita Davido aliucheza wimbo huo huku mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo wakionekana kuimba pamoja na msanii huyo.

Hitmaker huyo wa ‘How Long’ ambaye atabaki kukumbukwa na Diamond kwenye maisha yake yote ya muziki ameendelea kuonyesha support kubwa kwenye wimbo huo ambao mpaka sasa umefanikiwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 18 tangu ulipotoka miaka miwili iliyopita.

VIDEO:

Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images