Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

KANALI wa Jeshi Aliyeteuliwa Kuwa Kiongozi CCM Afunguka Baada ya Wengi Kuhoji....

$
0
0

Wakati watu mbalimbali wakiwa na maoni tofauti kuhusu Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Halmashauri Kuu yake kumteua Kanali wa Jeshi la Wananchi wa Tanzaia (JWTZ) kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, mwenyewe ameibuka na kutolea ufafanuzi uteuzi huo.


Kanali Ngemela Eslom Lubinga amesema kuwa alishastaafu utumishi wake jeshini na kuwa angeweza kutumikia chama cha siasa kwani si mtumishi wa jeshi hilo tena. Kanali Lubinga aliyekuwa Msemaji wa JWTZ alisema kuwa alistaafu utumishi katika jeshi kuanzia Disemba 2 mwaka huu. Aidha, alisisitiza kuwa alijiunga na Chama cha Mapinduzi mwaka 1979.


Kikubwa kilichozua maswali kuhusu uteuzi huu ni kwa sababu wanajeshi na watumishi wengine wa umma hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waraka wa Utumishi wa mwaka 2015 unakataza watumishi wa umma kuwa wanachama wa vyama vya siasa lakini unatambua haki yao ya msingi ya kupiga kura.


Badhi ya maswali yaliyoulizwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii ni lini Kanali Lubinga alijiunga na CCM kiasi cha kuweza kuteuliwa katika nafasi ya juu kiasi hicho? Kama alijiunga na chama mwaka 1979 inaonyesha wazi kuwa alikiuka katiba ya nchi inayowataka wanajeshi kutojiunga na vyama vya siasa.


Akijibu swali hilo Kanali Lubinga alisema kuwa wakati wa mfumo wa chama kimoja wanajeshi waliruhusiwa kujiunga na chama cha siasa na kuwa baada ya kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ndipo walizuiwa na kadi walizokuwa nazo zilichukuliwa. 


Kanali Lubinga aliendelea kusema kuwa kadi zile hazikutupwa bali zilihifadhiwa na hivyo baada ya kustaafu Disemba 2 mwaka huu akachukua kadi yake na kuendelea na uanachama wake.


Wengi waliokosoa uteuzi huo walitaka kuhakikisha kuwa siasa za nchi haziathiri utendaji  wa majeshi yetu na utumishi wa watumishi wengine wa umma.

TCRA Wafanya Ukaguzi Wa Mwisho Na Kuiruhusu Radio 5 Kurudi Hewani Dec. 16

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA) , jana December 14 imefanya Ukaguzi wa mwisho, kujiridhisha na kuruhusu Kituo cha Utangazaji cha Radio5 Arusha kurudisha Matangazo yake hewani ifikapo December 16 mwaka huu 2016.

Akiongea na Viongozi na baadhi ya Wafanyakazi wa Radio 5 baada ya kukamilisha ukaguzi wao, Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA Bw. Fredrick Ntobi alisema wao kama Mamlaka Waliamua kuja kufanya ukaguzi wao kwa ajili ya kujiridhisha kurudisha Matangazo ya Kituo hicho hewani December 16 ambapo ndiyo tarehe rasmi ya kuisha kwa adhabu waliyokuwa wametoa kwa  kituo hicho.

Kituo cha Radio 5 kilisimamishwa na TCRA kurusha matangazo yaketoka  tarehe 16 September 2016 kwa kukiuka baadhi ya kanuni.

Mamlaka hiyo ilifanya ukaguzi wa Studio ya Kurusha Matangazo (On air Studio), Studio ya kuzalisha Vipindi (Production Studio), Chumba cha Habari (News room), Control Room, ofisi zote za Kituo pamoja na Mnara wa Kurushia Matangazo ambapo kote wamekuta kila kitu kiko sawa kwa kazi kama Mamlaka inavyotaka.

Hata hivyo Bw. Fredrick Ntobi akiwa ameongozana na Viongozi wa  TCRA kanda ya Kaskazini, aliwakumbusha Watangazaji na Waandishi kufuata Maadili ya uandishi wa habari ili kulinda Vituo vyao na Kulinda taaluma zao kwa ajili ya kuendelea kuhabarisha na kuelimisha Jamii nzima ya Watanzania.

“Mimi niwasisitize tu kuendelea kufuata maadili ya taaluma yenu ya uandishi wa habari, kufuata sheria na kanuni za uandishi wa habari ambao mmesomea, tumieni lugha Sanifu ambayo inakubalika kwa jamii na tasnia yenu na niwatakie maandalizi mema ya kurudi hewani pamoja na Sikukuu zinazokuja”. Alimaliza kwa Msisitizo Bw. Fredrick Ntobi.

Hata hivyo kwa upande wa Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio5, Bw. Robert Francis, aliwataka Wasikilizaji wa Radio5 kukaa mkao wa Kuhabarika, Kupata Burudani na kuelimika zaidi kupitia Radio5 kwani Wamejipanga vyakutosha kurudi hewani kwa Kishindo.

“Mimi niwaombe tu wasikilizaji wetu ambao najua wametumiss sana, wakae tayari Kuhabarika, kuelimika na kuburudika zaidi sababu mimi na Wafanyakazi wangu tumejipanga vya kutosha haswa ukizingatia kwamba mwaka mpya ndo huu unakuja.

"Kingine niwape pole tu wasikilizaji wetu wote kwa kutotusikia hewani kwa kipindi cha miezi mitatu, pamoja na Wadau ambao tumekuwa tukishirikiana kwa pamoja katika mambo mbali mbali niwaambie tu tunarudi rasmi Ijumaa ya tarehe 16 December 2016”. Alisema Mkurugenzi wa Radio5 Robert Francis.

VODACOM Yawatengea Wateja Wake Bilioni 5/- Kupitia Promosheni ya NOGESHA UPENDO Msimu Huu wa Sikukuu.

$
0
0
Wateja wa Vodacom Tanzania wameletewa promosheni mpya inayojulikana kama “Nogesha Upendo” ambayo itawawezesha wateja wake kujishindia zawadi za fedha taslimu, muda wa bure wa maongezi na vifurushi vya intaneti kila siku  katika msimu huu wa sikukuu. Zawadi zenye thamani ya shilingi Bilioni 5 zitatolewa kwa wateja ambapo  wateja wapatao  500 wataweza kujishindia shilingi milioni 1( Tshs 1,000,000) kila mmoja katika kipindi chote cha msimu wa promosheni.

Akiongea wakati wa uzinduzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia alisema “Vodacom Tanzania tunayo furaha kuzindua promosheni ya msimu wa sikukuu ya Nogesha Upendo inayolenga kuleta shamrashamra za furaha ya sikukuu kwa wateja wetu. Tunajua sikukuu hizi zinaleta familia za kitanzania na marafiki pamoja kufurahi na kutumiana salamu za upendo, tumeleta promosheni hii kwa ajili ya kuwazadia wateja wetu wote kila wanaponunua vifurushi vya muda wa maongezi na Data kila siku.” Promosheni hii itawezesha wateja wetu 500 kujishindia kila mmoja shilingi milioni 1/- katika droo za wiki na wengine watajishindia shilingi 100,000/- katika droo za kila siku katika msimu huu wa sikukuu kupitia promosheni hii”.Aliongeza kusema “Mbali na wateja kujishindia dakika tano za muda wa bure wa maongezi na kuperuzi internet,wateja wa Vodacom  pia kila watakaponunua vifurushi wataingizwa kwenye droo za kila siku na kila wiki za kujishindia vitita vya fedha.Kiasi cha shilingi milioni 700 zimetengwa kwa ajili ya kuwazawadia wateja wetu katika msimu huu wote wa sikuu”.


Kwa ujumla, Vodacom imetenga zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 5/- kwa ajili ya kuzawadia wateja wake kwa njia ya fedha taslimu, muda wa maongezi na bando za intaneti (MB) .Promosheni hii itakayodumu kipindi cha miezi 2 kuanzia leo ni kwa ajili ya wateja wote wa Vodacom ambao laini zao ziko hewani na watakanunua vifurushi vya kupata huduma mbalimbali za kampuni.

“Promosheni ya Nogesha Upendo imebuniwa kwa ajili ya kuwashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono muda wote,Tunawatakia heri katika msimu wa sikukuu na tunawakumbusha  wakati wote kufuatilia zawadi watakazokuwa wanazishindia kutoka mtandao wa Vodacom kuanzia muda wa maongezi na fedha taslimu zitakazowawezesha kufurahia sikukuu pamoja na familia zao na marafiki. Hivi ndivyo Vodacom tumejizatiti kufanya Maisha ya wateja wetu kuwa murua na kusambaza upendo.” Alisisitiza Mworia

VIDEO:

AFANDE Sele " Kuanzia Leo Natangaza Rasmi Kujivua Rasmi Uanachama ACT Wazalendo"

$
0
0

Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop kutoka mkoani Morogoro, Afande Sele ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya ubunge katika uchaguzi uliopita kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Alhamisi hii ametangaza rasmi kujivua uanachama wa ACT-Wazalendo.

October 3 mwaka huu rapa huyo alifunguka kuonyesha kutoridhishwa na mwenendo wa viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Rapa huyo kupitia Instagram, ameandika:

Habari za wkt huu akina ndugu nyote,naamini tupo pamoja ktk kujitafutia maisha na kulijenga taifa letu pendwa Tz ambalo ndani ya katiba yake kuna kipengele muhimu kinachotupa UHURU kwa kila mtu kufanya mambo yake apendavyo ilimradi tu havunji sheria za nchi….sasa kwa kuzingatia UHURU huo tuliopewa na KATIBA yetu mimi Leo natangaza rasmi kujivua uanachama wa chama cha ACT-Wazalendo na kutokua mfuwasi wa chama chochote cha Siasa bali nitabaki kuwa raia wa kawaida ndani ya nchi yetu huku nikiendelea na majukumu yangu mengine ya kimaisha mpaka hapo nitakavyoamua vingine kama nitakua na sababu ya kufanya hivyo…Nawatakia kila la kheri wote waliobaki ndani ya chama pia nawatia moyo mkuu wa kuendeleza harakati za ujenzi wa chama ili kuleta upinzani sahihi na imara utakaosaidia kujenga taifa kwa faida yetu na vizazi vijavyo…naomba ieleweke kuwa uamuzi huu’tarajiwa’sijauchukua kwa bahati mbaya hivyo naomba kila mmoja awe wa ndani au wa nje ya chama chetu aheshimu uamuzi wangu kama mimi ninavyoheshimu maamuzi ya watu wengine kwa mujibu wa KATIBA ya nchi inavyosema…Ahsanteni sana wadau tukutane MAISHANI

MAHOJIANO na Mchumba wa Lady Jaydee, Asema Wana Mipango Mizito

$
0
0
Mchumba wa Lady Jaydee kutoka Nigeria amesema anaitwa Spice kutoka Nigeria amesema yeye ni mwanamuziki na wanampango wa kufanya mambo makubwa na ady Jaydee ambayo hakuyataja ila akasema watu watarajie
Amesema anampendea lady JD kwa kuwa yupo simpla na mnyenyekevu na japokuwa anatabia ya kununanuna ana dawa yake

VIDEO:

WABONGO Noma...Comments Zafuruka Kwenye Page ya Instagram ya Miss World Kwenye Picha ya Diana Luqumay

$
0
0
WABONGO Noma...Comments Zafuruka Kwenye Page ya Instagram ya Miss World Kwenye Picha ya Diana Luqumay, Mpaka tunaenda mitamboni comments zilikuwa zimefika 25,128

MISS Tanzania wa Mwaka Huu Sio Mtu wa Mchezo Mchezo..Ona Alichowafanyia Wazungu na Huu Wimbo wa Darasa

$
0
0
Miss Tanzania 2016, Diana Edward ameendelea kuonyesha mapenzi yake ya kuendelea kuutangaza muziki wa Tanzania kwenye shindalo la Miss Wolrd linalofanyika nchini Marekani.

Mrembo huyo amepost kipande cha video kwenye mtandao wa Instagram akiwa na mamiss wengine wawili huku wakicheza wimbo wa ‘Muziki’ wa Darassa.

Siku chache zilizopita kupitia mtandao huo, Diana alipost kipande cha video kinamuonesha akiwa na Miss Hondurus, Kerelyne Campigoti Webster na Miss Mexico, Ana Girault wakiucheza wimbo wa Man Fongo, Hainaga Ushemeji.

Kwa sasa mrembo huyo amefanikiwa kuingia fainali ya shindano la Beauty With A Purpose ambalo ni sehemu ya mashindano mbalimbali kwenye Miss World ambalo fainali zake zitafanyika Disemba 18.

VIDEO:

TV E Inakuja Kubamba..Clouds FM na EATV Kazi Kwenu Kuboresha Vipindi na Quality za Graphics

$
0
0
Kwa wiki sasa nimekuwa nikiitazama hii Tv stesheni ya TV E.Kiukweli niseme nawapa sifa zifutazo:-
1. Logo yao ni nzuri sana na waliodesign hii logo nawapa credit za kutosha.Ukiangalia logo ya Clouds fm haina mvuto na hata waliodesign hawakuwatendea haki clouds.

2. Graphics zo ni nzuri sana hata muonekano wake ikiwemo mpangilio wa rangi ni mzuri sana, kwa hili nawapongeza sana na nahisi wana timu ya watu makini sana.Clouds graphics zao ni mbovu sana na hata mpangilio wa rangi ni mbovu pia sijawahi kupenda muonekano wa Clouds

Mwisho niseme CLOUDS TV mjipange sana kwasababu soon mtakwenda kupoteza watazamaji kutokana na mpangili mbovu wa vipindi vyenu,muonekano mbaya wa Tv.TV E nawapa pongezi kwa mwanzo huu mzuri na nawatakia muendelezo mzuri ili mtoe changamoto kwa EATV kwani Clouds TV si mshindani kabisa.

BABA Achinja Wanawe Wawili na Kisha Kujinyonga

$
0
0
Watoto  wawili wenye umri wa miaka mitatu na sita wa Kijiji cha Patane Kata ya Mambamiamba wilayani Same,  wameuawa kwa kuchinjwa na panga na baba yao mzazi Yohana Greson (26) na yeye mwenyewe kujining’iniza kwenye paa la nyumba.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, alisema tukio hilo lilitokea Desemba 13, mwaka huu  majira ya saa tano asubuhi katika Kijiji cha Patane.

Kamanda alisema baba huyo alifanya tukio hilo la kutisha baada ya mkewe Eva Tumaini (29) mkazi Kijiji cha Ghona kwenda shambani na kumwacha mumewe nyumbani akiwa na watoto wawili, Esta Yohana na Tumaini Yohana, ambapo alichukua panga na kuwachinja na yeye kujinyonga kwa kamba.

Alisema Polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na kwamba uchunguzi wa awali umebaini marehemu huyo alikuwa na tatizo la kifafa.

Alisema miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same kwa ajili ya uchunguzi zaidi na kwamba marehemu hakuacha ujumbe wowote na uchunguzi ukikamilika ndugu za marehemu watakabidhiwa miili hiyo kwa ajili mazishi.

SHINDA Gari la Bure Kama Zawadi ya X-Mass Kutoka Kampuni ya Cars From Japan..Magari Mawili Yanashindaniwa

$
0
0
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote...Basi Hawa Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ...Fuata Maelekezo hapa chini Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi

Bonyeza Hapa : SHINDA GARI

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako

Mwisho wa Kujisajili ni 22 Dec 2016 


LOWASSA Ahoji Uamuzi wa Rais Magufuli Kununua Ndege Badala ya Kutoa Huduma Kwa Jamii, Awataka Vijana Kuwa Imara 2020

$
0
0
Mjumbe  wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, ametaka vijana wa chama hicho kukabiliana na ukandamizaji wa demokrasia aliodai unafanywa na watawala.

Alisema hayo juzi alipokutana na vijana wa chama hicho ambao ni wanavyuo (CHASO) wa vyuo vikuu mkoani hapa.

Lowassa ambaye yuko Tabora  kwa ziara ya kuimarisha chama, aliwataka vijana hao kuwa na ujasiri wa kukabiliana na ukandamizaji wa demokrasia kwani vijana duniani ndio chachu ya mabadiliko.

“Nimekuja Tabora kuwashukuru kwa kura nyingi mlizonipigia na hamasa kubwa mliyoionesha kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana. Katika uchaguzi ule tulishinda, lakini ushindi mkubwa zaidi ni tulipofanikiwa kuvumilia na kuweka maslahi ya watoto, wazee na mama zetu mbele," alisema na kuongeza:

"Amani ni tunu muhimu sana kwa mustakabali wa Taifa kuliko kitu kingine chochote. Msikate tamaa, tumejipanga vema kwa uchaguzi ujao wa mwaka  2020 na hatutadhulumiwa tena haki yetu, kama ilivyokuwa mwaka jana,” alisema Lowassa.

Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani, alisema Jambo Kuu na la msingi ambalo wana Chadema wanatakiwa kuwa nalo sasa katika chama  ni umoja na mshikamano kati yao.

"Umuhimu wa umoja na mshikamano ndani ya chama chetu ni mkubwa sana, hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inajaribu kwa kila namna kukandamiza Upinzani na demokrasia na jambo hili si geni, ukirudi nyuma katika historia ya vyama vya siasa nchini, hata kabla ya Uhuru, unaweza kuona umoja ulivyoisadia TANU dhidi ya chokochoko za chama alichoanzisha mkoloni wakati ule - United Tanganyika Party (UTP) kukabiliana na kuidhoofisha TANU na kumzuia Mwafrika kupata Uhuru na kujitawala," alisema.

Aliwaambia vijana kwamba changamoto kama hizo ni za kawaida kwa vyama vingi vya upinzani hasa Afrika, ambavyo vinaungwa mkono na wananchi wengi wakiamini ni vya ukombozi.

Lakini pia alisema katika kujenga umoja na mshikamano huo ndani ya chama, ni lazima  nguvu kubwa ipelekwe kwenye matawi waliko wananchi.

"Katika chama chochote cha siasa watu wengi hawako ngazi za juu, bali mashinani. Ni lazima nguvu yetu kubwa ielekezwe huko kwa sasa, ili kuhakikisha chama kinakuwa na misingi madhubuti ambayo inaweza kutumika kukisaidia nyakati za uchaguzi," alisema.

Aidha, Lowassa ambaye katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana alipata asilimia 38 ya kura, alihoji umuhimu wa Serikali kununua ndege zaidi, kuliko kupeleka huduma muhimu vijijini.

"Tumesikia nia njema yao ya kuagiza ndege nyingine zaidi miaka miwili ijayo, lakini tunajiuliza, je isingekuwa busara kutumia fedha hizo kupeleka maji safi na salama mijini na vijijini?" Alihoji.

CHATU Afa Baada ya Kumeza Mbwa

$
0
0
CHATU aliyemeza mbwa mkubwa katika Jimbo la Warri nchini Nigeria, majuzi alikufa baada ya tumbo lake kuvimba kupita kiasi na kupasuka wakati anataka kupita katika senge’nge kwenye fensi.

iSenge’nge hizo zilimnasa tumboni na kusabisha lipasuke na akafa hapohapo.

Mashuhuda aliyepiga picha tukio hilo aliziweka picha zake katika mitandao ya kijamii kama onyo kwa watu wenye tamaa za kupata fedha kuliko mahitaji yako ya kawaida.

HUMPHREY Pole Pole Afunguka Haya Baada ya Kupewa Kijiti na Nape

$
0
0

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema atahakikisha chama hicho kinakuwa ni cha wanyonge na kuendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti.


Polepole ametoa kauli hiyo leo wakati akikabidhiwa rasmi ofisi na  Katibu anayemaliza muda wake Nape Nnauye katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.


Polepole alisema kwa misingi ya chama hicho imejengwa kuwasaidia na kuwa tete wanyongo hivyo katika muda wake wa uongozi atahakikisha chama kinasimama katima misingi hiyo ya kuanzishwa kwake.


“Msingi wa chama chetu ni utetezi wa wanyonge, tutahakikisha kinaendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti,” alisema Polepole.


Aidha, katibu huyo alisema kuwa katika kutekeleza majukumu yake aliyokabidhiwa leo na mtangulizi wake, atahakikisha anajikita zaidi katika kazi za itikadi zaidi kuliko uenezi kwa kuwa itikadi ndiyo inayokibeba chama.


Polepole alitumia muda huo kumshukuru Nape Nnauye anayemaliza muda wake na kusema kuwa ni kiongozi imara na kuwa katika muda wake aliweza kuitumikia vyema nafasi yake. Lakini pia alisema japo anamaliza muda wake, lakini atakuwa akimuhitaji mara kwa mara kwa ajili ya ushauri na mambo mengine.


Wakati huo huo, Polepole amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Dkt John Pombe Magufuli na Halmashauri Kuu ku kumwamini na kumpa majukumu hayo makuwa.

DARASA Afunguka Tuhuma za Kuiba Beat ya Saida Karoli Kwenye Wimbo Wake wa Muziki

$
0
0
Darassa Afunguka Tuhuma za Kuiba Beat ya Saida Karoli Kwenye Wimbo Wake wa Muziki
Video:

CHUCHU Hans Adaiwa Kuficha Mimba ya Ray Kigosi...Mwenyewe Afunguka Haya

$
0
0
Chuchu Hans Ajibu kuhusu tetesi za kuwa ni mjamzito na anaficha watu wasijue.....

Amesema Hivi:

“Unajua vitu kama hivyo ni too personal na nisingependa kuviongelea especially kwenye media. Lakini muda muafaka ukifika kila mmoja atajua nini ni nini, ila kwa sasa acha ikae hivyo watu waendelee kuhisi,” amesema muigizaji huyo.

Chuchu alifanikiwa kushinda tuzo ya muigizaji bora wa kike kwenye tuzo za Eatv Awards 2016 zilizotolewa Jumamosi iliyopita.

SIKILIZA Wimbo Mpya wa Diamond Platnumz na Neyo Unaitwa Marry You

$
0
0
SIKILIZA Wimbo Mpya wa Diamond Platnumz na Neyo Unaitwa Marry You

NAY wa Mitego " Nimefurahishwa na Young Dee Kumkubali Mtoto Wake"

$
0
0

Rapper Nay wa Mitego amedai kuwa amefurahishwa na kitendo cha Young Dee kumkubali mtoto wake Tamar.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM Alhamisi hii, Nay amesema, “Ukiwa na mtoto akili ya kutafuta inaongezeka, nilifurahi sana kumuona mdogo wangu Young Dee akimkubali mwanae.”

Nay ameongeza kwa kusema, “Mwaka huu nilikuwa kimya tu lakini mipango haikufeli, Pia mimi na Mr T-Touch yalipita nimefanya naye kazi muda mrefu kama ndugu. Siwezi kuongelea mabaya yake hewani, utakuwa ni utoto.”

Rapper huyo kwa sasa ameachia wimbo wake mpya ‘Sijiwezi’ ambao umetayarishwa kwenye studio zake za Free Nation.

WAHARIRI Walitaka Jeshi la Polisi Kumuachia Mara Moja Mwanzilishi wa JamiiForums, Maxence Melo

$
0
0

Wahariri Nchini (TEF) limelitaka Jeshi la Polisi kumuachia mara moja Mwanzilishi wa JamiiForums, Maxence Melo bila masharti yoyote.

TEF imesema inatetea haki ya uhuru wa kutoa mawazo na kukataa ukandamizaji wa polisi wanaodai wana maelekezo kutoka juu.

Jukwaa hilo limesema taarifa walizonazo zinaonyesha kuwa polisi wanaomshikilia Melo wanajiapiza kuwa hata kama mawakili wake watakwenda mahakamani hawatamwachia hadi atekeleze wakitakacho.

MWANDISHI wa Dar24 Akamatwa Kwa Habari ya ‘DC wa Ludewa Kukanusha Uzushi’

$
0
0
Askari wa Makao Makuu ya Jeshi Polisi jijini Dar es Salaam jana walimkamata na kumshikilia mwandishi wa Dar24, Chis Kika kwa kuandika habari kuhusu Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrea Tsere KUKANUSHA taarifa zilizoandikwa mitandaoni kuwa alilazwa chooni katika mazingira ya kutatanisha.

Kika amesafirishwa chini ya ulinzi wa polisi mapema leo kwenda Wilayani Ludewa kujibu tuhuma zinazomkabili.

Mwandishi huyo wa Dar24 aliandika habari yenye kichwa cha habari ‘DC akanusha kulala chooni na familia yake, asema hatishiki’. Katika habari hiyo mwandishi alimmnukuu Mkuu huyo wa wilaya ya Ludewa kuwa ‘ALIKANUSHA’ taarifa za zilizokuwa zimesambazwa mtandaoni na watu wasiomtakia mema.

Wakielezea mazingira ya kukamatwa na kushikiliwa kwa mwandishi huyo kutokana na kuandika habari hiyo ya kukanusha uzushi, uongozi wa Dar24 umesema kuwa askari ambao awali walitumia utambulisho bandia kuwa wanatokea Benki ya CRDB, walimchukua Kika na wenzake wawili na kuwapeleka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi ili kuhojiwa na wataalamu wa makosa ya kimtandao kwa madai kuwa habari hiyo inahusika na uvunjifu wa sheria ya Makosa ya kimtadao.

Baada ya mahojiano ya awali, Polisi waliwaachia wenzake na kuendelea kumhoji Kika kwa zaidi ya saa tano ambapo alitoa ushirikiano wa kutosha. Kika alikiri kuwa ndiye aliyeandika habari hiyo ya kumkunukuu Mkuu wa Wilaya akikanusha taarifa zilizotolewa awali na vyombo vingine vya habari, siyo Dar24. Na kwamba alifanya hivyo kwa nia njema ya kusaidia kufikisha ujumbe wa Mkuu huyo wa wilaya dhidi ya wanaomzushia.

Kika alionesha kushangazwa na madai kuwa taarifa hiyo inamkashfu mkuu huyo wa wilaya na badala yake alieleza kuwa ilikuwa ikisaidia kufuta habari ya uzushi na kusisitiza kuwa alinukuu alichokisema Mkuu huyo wa Wilaya ya Ludewa kwa nia njema, hivyo alipaswa kupongezwa na sio kukamatwa.

“Nilitegemea kuwa Mheshimiwa DC angetushukuru Dar24 kuwa tumemsaidia kufikisha kwa umma taarifa inayomsafisha dhidi ya kile alichokiita njama ya kumkwamisha badala ya kuagiza nikamatwe na nisafirishwe chini ya ulinzi kwenda Ludewa kujibu mashtaka ya kuwa nimemkashifu. Yeye alikanusha na vyanzo vingi vilimnukuu alitegemea tuandike nini?” Kika alihoji.

“Mimi sielewi, mnasema DC wa Ludewa anadai nimemkashfu kwa kuwa nimeandika kuwa alikanusha kuwa yeye na familia yake walilazwa chooni? Kwahiyo anamaanisha hakukanusha?” Kika aliongeza.

Baada ya kusikiliza na kuandika maelezo ya Kika, askari Polisi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi walisema wao wanatekeleza maagizo ya Mkuu wa Wilaya ya Ludewa na hivyo hawakuwa na uwezo wa kushughulikia jambo lolote ikiwemo kumpatia dhamana mtuhumiwa. Hivyo, waliendelea kumshikilia wakisubiri kumsafirisha chini ya ulinzi kwenda Ludewa mapema leo kwa hatua zaidi.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, askari polisi aliyejieleza kuwa ametumwa kutoka Ludewa kutekeleza ukamataji wa Kika, alikataa kuzungumza na Mwanasheria wa Dar24 kuhusu hatua zinazochukuliwa kumsafirisha mteja wake ambaye alikuwa anaumwa, ikiwa ni pamoja na kufahamu namna atavyoweza kutumia dawa alizokuwa akiendelea kutumia.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, Kika akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi huyo kutoka Ludewa tayari yuko safarini kwenda Ludewa kujibu tuhuma zinazomkabili, kwa kile kinachoelezwa kuwa ni utekelezaji wa sheria za makosa ya mtandao.

NAPE Nnauye Awaomba Msamaha Wapinzani na Waandishi wa Habari

$
0
0
Alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amewaomba radhi viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini kwa lolote ambalo aliwakwaza wakati akitekeleza majukumu yake katika nafasi hiyo.

Nape amewaangukia wapinzani pamoja na makundi mengine ya watanzania ikiwemo viongozi wenzake ndani ya chama leo wakati akikabidhi rasmi ofisi kwa kiongozi mpya anayechukua nafasi hiyo, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam, Humphrey Polepole katika ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho, Lumumba Jijini Dar es Salaam.

"Nawaomba msamaha viongozi wenzangu, wanachama, waandishi na hata wapinzani pale ambapo nimewaumiza katika kufanya kazi yangu, samahani sana. Nategemea ushirikiano niliopatiwa mimi na wanahabari utaendelea kwa ndugu yangu Humphrey Polepole, ni mtu mwenye weledi mpana" amesema Nape

Nape pia amekiri kuwa chama hicho kimemsaidia zaidi kwenye maisha yake kuliko yeye alivyokisaidia wakati akiitumikia nafasi hiyo.

"Nakiri mbele yenu kuwa chama kimenisaidia zaidi kuliko mimi nilivyokisaidia Chama, nashukuru Mungu kuwa nimemaliza kazi hii salama, nilipata wosia wa Mzee Kinana kuwa nishukuru nikimaliza salama"
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images