Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

NAY wa Mitego Awashukia Wanamuziki Wanao Fanya Hip Hop Ngumu...Adai Wajikusanye Waje Washindane Naye

$
0
0
“Hao wanaosema mimi sio mwana hip hop nipeleke nao kwenye show moja, hao walionitoa kwenye list ya hip hop. Tena ninachokuomba waandalie show yao Leaders waweke 16, niandalie show yangu Escape 1 peke yangu. Nakuambia wakipata watu kweli hip hop yao ina nguvu. Wote unaowasikiaga waandika, wanakesha, wanatweet ‘Nay si mwanahiphop’ wajikusanye kwenye show yao moja halafu mimi nipige pale upande wa pili halafu tuone nani atapata watu,” Nay aliiambia 255 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Wewe unakesha unanitukana kwenye mtandao wakati mimi nikiamua asubuhi naenda kununua gari mpya, nikiamua naenda kununua kibanda chenu kile cha familia mimi ninakinunua halafu wewe unaenda kukaa unanitukana kwenye mitandao, siwezi kukasirika,” amesisitiza Nay wa Mitego

MAWAKILI Sita Kumtetea Mmiliki wa JamiiForums...Tundu Lissu Akiwemo

$
0
0
Mawakili sita akiwamo mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Lissu wamejitokeza kumtetea mmiliki wa JamiiForums iwapo atapelekwa mahakamani.

#Justice For Lema

#Bring Back Ben Saanane

#Free Maxence Melo

HUMPHREY Polepole "Bado Naamini Muundo wa Serikali Tatu"

$
0
0
Katibu mwenezi mpya wa CCM aliyevaa viatu vya Nape, Humphrey Polepole amesema bado anasimamia msimamo wake alioutoa wakati wa bunge la katiba, kuwa Tanzania inahitaji muundo wa serikali tatu.

Msimamo huu unaonekana kwenda kinyume na msimamo wa chama chake.

Source: Mtanzania, Jambo Leo.

BAADA ya Kusemekana Anaficha Ujauzito wa Ray, Picha ya CHUCHU Hans Akiwa Mjamzito Yanaswa....

$
0
0

Baada ya Kusemekana kuwa Mwigizaji Chuchu Hans ni Mjamzito na kuwa anaficha watu wasijue  Wambea wa mjini tayari wamefuma picha yake akiwa ni Mama Kijacho...

Chuchu Hans Alikaririwa Akisema Haya:

“Unajua vitu kama hivyo ni too personal na nisingependa kuviongelea especially kwenye media. Lakini muda muafaka ukifika kila mmoja atajua nini ni nini, ila kwa sasa acha ikae hivyo watu waendelee kuhisi,” amesema muigizaji huyo.

SHINDA ZAWADI YA GARI BONYEZA HAPA

HATIMAYE Tunda Man Akiri Kuwa na Tofauti na Babutale...Adai Hali Hiyo Inamuumiza Sana

$
0
0
Tunda Man amefunguka sababu ilinayomfanya asielewane na bosi wake wa Tip Top Connection, Babutale.

Akiongea na EATV, muimbaji huyo wa ‘Mama Kijacho’ amesema, “Najutia kuwa na misunderstanding na bosi wangu. Kiukweli mimi na bosi wangu Babutale hatuko sawa, kosa silijui. Kuna kitu mimi nimemkosea may be au ameamua tu kukasirika na kiukweli hii kuwa mbali na bosi wangu kwenye kazi zangu ninazozifanya nakuwa mwenyewe tu kiukweli it’s pain, naumia.”

“Lakini sometimes mtu anaweza akawa na mwanae akamwambia nenda katafute maisha kivyake japo baba yake anakila kitu, kwahiyo unakuta mtoto anaondoka kutafuta maisha mengine, anabeba zege anafanyaje lakini anajutia kuwa mbali na baba yake. Lakini mimi najutia kwa sababu kazi zangu nakuwa na wakati mgumu wa kuzipush na kusupport kazi zangu lakini Alhamdulillah Mungu anasaidia.”

Tunda ameongeza kuwa kuna kipindi alipata dili la kufanya tangazo lakini kuna mtu alimpandia na nafasi hiyo akapewa msanii mwingine anayesimamiwa na Tale.

VIDEO: AIBU Msikilize Shilole na Engilish yake ya Igunga

$
0
0
AIBU Msikilize Shilole na Engilish yake ya Igunga..

ANGALIA VIDEO HII NA PIA USISAHAU KUBOFYA NENO SUBSCRIBE..

MMILIKI wa Jamii Forums Apandishwa Kizimbani Kisutu, Ashindwa Kutimiza Masharti ya Dhamana

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Jamii Media Limited, inayomiliki mtandao wa kijamii wa Jamii Forum (JF), Maxence Melo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi tatu tofauti lakini akasomewa mashtaka matatu.

Katika kesi hizo amesomewa mashtaka matatu, shitaka moja katika kila kesi.

Mashtaka hayo ni pamoja na kuendesha shughuli za mtandao wa kijamii bila kusajiliwa nchini na mawili ni kuzuia upelelezi.

Melo amefanikiwa kupata dhamana katika kesi mbili lakini akakwama katika kesi moja baada ya kushindwa kutimiza sharti la kupata wadhamini wawili na badala yake akampata mdhamini mmoja tu.

MWENYE Nyumba wa Msaidizi wa Mbowe Saanane Aliyepotea Aeleza ilivyokuwa

$
0
0
Mmiliki wa nyumba anayoishi kada wa Chadema, Ben Saanane aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha mwezi mmoja uliopita, Evance Mrosso amesema waligundua kuwa amepotea baada ya siku nne kupita bila kuonekana.

Mrosso aliyekuwa akiishi na Saanane maeneo ya Tabata Dampo, jana alilimbia gazeti hili kuwa haikuwa kawaida yake kukaa kimya kwa muda mrefu kwani ni mtu wa mawasiliano kwa ndugu zake, marafiki na majirani.

“Saanane ni mtu wa kutoka asubuhi na kurudi usiku na inaweza ikapita siku mbili tusionane kutokana na mwingiliano wa shughuli zangu na zake, lakini tunawasiliana kwa simu, ” alisema Mrosso.

Hata hivyo, Mrosso alisema hali ilikuwa tofauti baada ya kupita siku hizo nne ndipo aliamua kuwauliza jirani zake kama wamemuona na walimjibu kuwa hawajamwona.

“Nimeishi na Saanane kwa muda wa miaka mitano.Mara ya mwisho tulionana na kuwasiliana Novemba 12, wakati wenzangu tunaoishi nao walimuona kuanzia tarehe hiyo hadi 14, hata wao walishangaa kutomuona kwa sababu siyo kawaida yake,” alidai Mrosso.

Alisema baada ya kujibiwa hivyo, alichukua uamuzi wa kumtafuta kumpigia simu katika namba zake mbili alizokuwa akitumia lakini hazikupatikana.

Alisema baadaye aliamua kumpigia simu mmoja wa dada zake anayeishi Mbeya ili kumweleza suala hilo na kama aliwasiliana naye hivi karibuni.

“Dada yake akaniambia hawajawasiliana na Saanane kwa muda sasa. Hivyo alinishauri nitoea taarifa polisi. Lakini kabla ya kwenda polisi, nilienda ofisini kwake Chadema (Kinondoni) kumuulizia, nilimkuta mlinzi akanieleza kuwa hajaonekana kwa siku kadhaa ofisini hapo,” alidai Mrosso.

Juzi, Mwanasheria wa Chadema, Tundu lissu aliitaka Serikali kueleza kama inamshikilia kada huyo ambaye alikuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe.

Sanjari na hilo, Lissu aliitaka Serikali kufuatilia ujumbe wa vitisho aliowahi kutumiwa Saanane kupitia simu yake ya mkononi na mtu ambaye bado hajafahamika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni alisema polisi bado inaendelea na upelelezi.

“Taarifa zilizopo ni za kipelelezi hatuwezi tukaziweka hadharan, wakati uchunguzi wa tukio hili ukiendelea,” alisema Kamanda Hamduni.



Nafasi za Kazi Kiwanda Cha Dangote (NAFASI 594) Apply Hapa

$
0
0
NAFASI ZA KAZI DANGOTE CEMENT KUMBU NO;DIL/A00/2016/01

Kiwanada cha kuzalisha saruji cha DANGOTE Tanzania kilichopo mkoani Mtwara kilomita 23 bara bara ya Lindi, Kata ya Mayanga, Kijiji cha HIARI, kinaalika maombi ya nafasi za kazi za madereva wenye uzoefu wa magari makubwa ya mizigo yasio pungua uzito wa  tani 33 na urefu usiopungua mita 18


DEREVA GARI ZA MIZIGO NAFASI 594

SIFA ZA MWOMBAJI

                               I.            Awe na umri wa miaka 26 hadi 55

                            II.            Awe na lesini halali ya daraja E  na mwenye uzoefu usiopungua miaka mi 5 ya kuendesha magari makubwa ya mizigo uzoefu wa kuendesha maroli wenye urefu usiopungua mita 18

                         III.            Uzoufu usiopungua miaka mi 5 kwenye magari ya kuvuta tela

                         IV.            Ajue kuandika taarifa na uzoefu wa kuweka kumbu kumbu zake kwa ufasaha

                            V.            Awe na afya njema, akili timamu,  ari ya kufanya kazi kwa tija, mwadilifu, mbunifu awezaye kujisimamia mwenyewe,  katika kutimiza majukumu atakayo pewa

                         VI.            Awe na wadhamini wanaoaminika na awe tayari kuchukuliwa alama za vidole

                      VII.            Awe na uelewa wa kusoma na kuandika na kusikia  Kiswahili na kingereza kwa uufasaha muhitimu wa kidato cha IV/VI

                   VIII.            awe mtuami mzuri wa muda katika safari atakazo pangiwa  ndani na nje ya nchi

                         IX.            awe na uwezo mzuri wa kupaki garikwene nafasi zinazo bana

                            X.            awe na uwezo wa kusoma kiongoza ramani


VIAMBATANISHO

-          Barua ya maombi ichapishwe au iandikwe kwa mkono

-          Picha 2 za rangi zilizobanwa na vizuri katka barua ya maombi

-          Vyeti vya mafunzo VETA/NIT pamoja na taaluma

-          Cheti au barua kutoka muajiri wa sasa au aliyepita

-          Barua toka kwa wadamini wa 2 wanaoaminika zikiambatana na picha zao

-          Cheti cha afya kutoka hospitali inayotambulika na serikali

-          Cheti za kuzliwa

MSHAHARA KWA MWEZI

DILSS Faraja lla 2 ngazi ya 3


NAMNA YA KUWASILISHA MAOMBI

-          Andika nfasi unayoomba upande wa juu kulia  mwa bahasha  sambamba na kumbu kumbu namba ya tangazo

-          Pamoja na maelezo ya uombaji onyoesha chanzo cha taarifa ya uombaji

-          Maombi yatumwe kwa njia ya posta kupitia anuani  zilizopo hapo chini

-          Barua za mkononi hazitapokelewa

-          Barua zote zitumwe kwA

MKUU WA IDARA YA RASILIMALI WATU NA UTAWALA,

DANGOTE INDUSTRIES LIMITED TANZANIA,

S.L.P 1241,

MTWARA


  Kwa maulizo wasiliana nasi kwa barua pepe recruitment.tanzanis@dangote.co

Ngassa: Najua Kuna Maneno na Minong’ono Mingi Kuhusu Uwezo Wangu Muda si Mrefu yataisha

$
0
0
Hatimaye mchezaji Mrisho Ngassa aliyekuwa anacheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Fanja Fc ya Oman, amemwaga wino kuitumikia klabu ya Mbeya City fc akiungana na nyota wengine 9 waliojumishwa kikosini kwenye usajili wa dirisha dogo lililofikia tamati desemba 15.

Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja utaomuweka kwenye kikosi cha Kinnah Phiri mpaka Novemba 30, 2018,na kukabidhiwa jezi namba 10 iliyokuwa inavaliwa na Joseph Mahundi aliyetimkia Azam fc ya Dar es Salaam kufuatia kumalizika kwa mkataba wake.

Baada ya kusaini mkataba huo wa mwaka mmoja Ngassa amesema anatakakufanya kazi kwa kiwango ambacho kitaipa mafanikio timu yake mpya na kuwaziba ‘midomo’ wale wanaamini kwamba soka lake limefikia tamati.

“Najua kuna maneno na minong’ono mingi kuhusu uwezo wangu, muda si mrefu yataisha kwa sababu najua nini nataka kufanya, soka ndiyo maisha yangu, naomba watu wote walio nyuma ya timu hii waniunge mkono nina uhakika tutakuwa na majibu mazuri mwisho wa msimu” alisema Ngasa

SIKILIZA Stori ya Kusisimua ya Kijana Mwenye Jinsia Mbili 2 ya Kike na ya Kiume

$
0
0
Leo nimekuwekea Stori ya Kijana Ambae amezaliwa na jinsi mbili ya kike na ya kiume, kijana huyu anatamani akatwe moja abaki na moja...

Bonyeza Hapa Chini Kusikiliza Stori Nzima Mwanzo mwisho:


LADY Jaydee na Spicy Wathibitisha Kuwa Wapenzi, waeleza Walivyokutana

$
0
0
Lady Jaydee na Spicy wamethibisha rasmi kuwa ni wapenzi. Kwenye mahojiano na Bongo5, wawili hao wamedai kuwa wamekuwa pamoja kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

“Tulikutana miezi kadhaa iliyopita na tukaanza kuzungumza, tukaanza kufahamiana zaidi na leo tuko hapa,” amesema Spicy.

“Tulikutana katika mazingira kama haya, sababu wote ni wanamuziki, kwahiyo tulikutana katika mazingira ya muziki,” amesema Lady Jaydee.

Anasema walikutana nje ya nchi.

Hata hivyo Spicy amekanusha kile kilichokuwa kikielezwa mwanzo kuwa wamefunga ndoa.

Kwa upande wa namna uhusiano wao ulivyo, Spicy amesema, “Hadi sasa mambo ni mazuri, kila mtu binafsi siku zote tuna utofauti lakini mkiziongelea mnaweza kuwa na sehemu ambayo mtakutana ambapo mnaweza kuzimaliza.”

Jaydee anafahamika kwa kuwa msiri katika masuala yake binafsi, kwanini kwenye uhusiano huu amekuwa na uwazi zaidi?

“Ni kutokana na aina ya mtu ambaye niko naye,” amejibu Jide.

“Kwasababu naye ni mtu ambaye anafanya kazi kama ya kwangu kwahiyo mwisho wa siku sio rahisi sana kusema kila kitu kinaweza kisijulikane. Lakini mambo mengine ambayo yatakuwa ni ya kwetu, si lazima kila mtu awe anafahamu. Kama watu washafahamu kwamba tuko pamoja nafikiri hiyo inatosha, zaidi ya hapo waendelee kuenjoy muziki wangu na muziki wa Spicy pia,” amesisitiza Jaydee.

Kwa upande wa mapokezi wa shemeji zake, Spicy amesema watanzania wamekuwa wakimuonesha upendo wa hali ya juu.

Together ni wimbo ambao Spicy ameuandika na kuutayarisha mwenyewe japo kwenye verse ya Jaydee alilazimika kuzitafsiri na kuziboresha kuwa za Kiswahili.

VIDEO: Tazama Ukahaba Unavyofanyika Dar es Salaam Wazi Wazi Mchana Kweupe

$
0
0
Hapa ndo tulipofikia, Inasikitisha imefikia mpaka sasa makahaba wanajiuza mchana kweupe, embu angalia huyu mteja akifanya makubaliano na changodoa mchana kweupe 

BONYEZA PLAY HAPA CHINI UJIONEE:

WASICHANA Wanaoota Nywele Mwili Mzima Wakata Tamaa Kuolewa

$
0
0
Kutana na akina dada watatu wanaotoka katika familia ya watoto sita ambao wamestaajabisha wengi huko nchini India wakiwa na sifa yakuota nywele mithili ya manyoya ya mnyama Mbweha.

Wakina dada hao ni Savita (23), Monisha (18) na Savitri Sangli (16) ambao wanaishi katika kijiji cha Pune, India na wamerithi kwa baba yao uotaji nywele huo mwili mzima.

Wataalamu wanasema kuota nywele mwili mzima yaani hata kwenye sehemu ambazo hazipaswi kuota nywele ni ugonjwa ambao kitaalamu unafahamika kama ‘Werewolf Syndrome’ ambapo seli hubadilisha mfumo na kuzifanya nywele kuota sehemu zote mwili na ni ugonjwa wakurithi.

Na kwa wasichana hao wamekuwa wakiota nywele kwa haraka sana na nyingi mwili mzima, wana ndevu lakini pia puani kwenya paji la uso na sehemu nyingine nyingi, jambo ambalo linawafanya waonekane tofauti na wasichana wengine na wengi huwashangaa na wakati mwingi huwabeza.

Hali hii imezima kabisa ndoto zao kwani wanajiona tofauti na hivyo wanaamini hawataweza kupata mambo muhimu kama wanawake wengine kama vile kuolewa, kuajiriwa, kujiremba na hata kuvaa nguo kawaida kama ilivyo kwa wanawake wengine.

Na hii inawaumiza sana kwani kwa tamaduni za kijiji chao ikiwa umefikia umri wakuolewa na ukasalia nyumbani inahesabika kama mkosi kwa mtu binafsi, familia na kijiji kwa ujumla wake.

“Wanangu hawa watatu wananisononesha sana kwani hali yao inawanyima raha na wanatafuta njia yoyote yakuwasaidia kuziondoa nywele hizo ili wawe kama wasichana wengine. Gharama yakufanya ‘surgery’ kwa kila msichana zinahitajika dola za kimarekani 7000 ambazo ni sawa na shilingi 15,250,200 za kitanzania, hivyoi jumla zinahitajika shilingi milioni 45,750,600. Na kwa bahati mbaya sina hizo pesa,” alisema mama wa watoto hao

RAIA 13 wa Kigeni Wanaswa Wakifanya Ukahaba Wilaya ya Kinondoni

$
0
0
Wilaya ya Kinondoni imetajwa kuwa kinara wa madanguro ya raia wa kigeni wanaojihusisha na biashara ya ngono.

Hilo limethibitika baada ya kikosi cha Idara ya Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam kuwakamata wasichana 13, raia wa Nepal na India wanaodaiwa kufanya ukahaba kwenye madanguro wilayani humo.

Mkuu wa Idara ya Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam, John Msumule alisema wasichana hao ambao umri wao ni kati ya miaka 18 na 20 waliletwa nchini kwa ajili ya biashara ya ukahaba.

Alisema katika operesheni ya kuwatafuta wahamiaji haramu iliyofanywa na kikosi chake, waligundua kuwapo kwa madanguro manne Kinondoni ambayo yanawatumia raia wa kigeni.

“Kinondoni ndiyo imekithiri kwa madanguro yanayowahusisha raia wa kigeni. Hili suala halivumiliki tumejipanga kuyaondoa madanguro yote.

Kazi hiyo itafanyika ndani ya siku 10, kama wahusika wanajipenda wayafunge wenyewe. Ukipita muda huo na bado madanguro yapo mje mniulize imekuwaje,” alisema Msumule.

Kikosi hicho pia kinamshikilia Mtanzania, Mohamed Magamba kwa kosa la kukutwa na hati za kusafiria za raia wa mataifa manne tofauti.

Kwa mujibu wa Msumule, Magamba hujihusisha na utengenezaji wa hati za kughushi na kugonga mihuri kwenye hati za kusafiria.

“Tumemkamata na hati za kusafiria za raia wa Nigeria, Somalia, Uingereza na Botswana. Kazi yake ni kuchukua hati za wageni, kuwagongea mihuri ya uongo na kuwatengenezea hati za kughushi,” alisema na kuongeza:

“Wahusika wa hati hizi tunawatafuta na tutawapata ndani ya siku mbili. Tunafuatilia mtandao wake kujua wanafanyaje kazi hii.”

Msumule aliwataka waajiri wanaoajiri raia wa kigeni kuhakikisha wana vibali halali kabla ya kuwaajiri.

Waajiri hakikisheni mnaajiri watu wenye vibali halali si kuchukua vibali mitaani, utaratibu wetu sasa tunawakamata raia wa kigeni wanaofanya kazi bila vibali na waajiri wao.

Pamoja na waajiri, pia Msumule amewataka wamiliki wa nyumba mkoani Dar es Salaam ambao nyumba zao zina wapangaji, kuhakikisha wanakuwa na picha za wapangaji wao wote ili kuwatambua na kupunguza uwezekano wa kuhifadhi wahalifu.

Katika ziara yake ya Novemba 15 aliyoifanya katika ofisi za Idara ya Uhamiaji hapa nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, aliagiza wahamiaji wanaokiuka sheria za nchi na kuishi bila vibali, wasakwe kila kona, kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Kitendo cha mtu, ambaye si Mtanzania kuwepo nchini na kukiuka sheria na taratibu anazopaswa kuzifuata ili kuendelea kuwepo, hakuna mjadala na kwamba, akamatwe,” aliagiza.

Pia, aliagiza uongozi na watumishi wa idara hiyo nyeti, kutokumuonea mtu kwenye utekelezaji wa majukumu yao, badala yake watangulize uadilifu ili kuepuka lawama na kuchafua taswira ya ofisi hiyo.


DAVID Kafulila Ahama NCCR, Ahamia Chadema

$
0
0
Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kigoma Kusini kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila leo ametangaza kukihama chama hicho na kusema kuwa atajiunga na Chama cha Demokrasia na Manendeleo (CHADEMA).

Kafulila ambaye alijizolea umaarufu mkubwa katika bunge la kumi kwa kufichua hoja mbalimbali za ufisadi amesema kuwa ameshawasilisha barua ya kujiuzulu kwa uongozi wa chama hicho.

Akieleza sababu iliyomsukuma kujiunga na CHADEMA, Kafulila alinukuliwa akisema kuwa kikubwa ni kuhakikia wanaleta mabadiliko nchini Tanzania.

"Ili kufanya safari kuwa fupi, kuondoa vikwazo vya huyu yuko chama hiki mwingine kile nimemamua kujiunga na CHADEMA ili kurahisisha uletaji mabadiliko katika nchi yetu sababu nimeona uhitaji huo," alisema Kafulila.

Katika uchaguzi uliopita Kafulila alipoteza jimbo la Kigoma Kusini ambalo lilikwenda wa Hasna Sudi Katunda Mwilima aliyekuwa akigombea kupitia Chama cha Mapinduzi.

VIDEO:Mume wa Mtu Afumwa Akipigwa na Kahaba Guest Kwa Kutokumlipa Pesa yake

$
0
0
Kuna msemo unaosema Duniani hakuna kitu cha Bure, Huyu Mume wa mtu aliingia choo cha kike baada ya kupata mwanamke wa kupooza naye kidogo huku akiwa hana hela ya kutosha ...Kilichotokea angalia hii Video Jamaa Akichukua Kichapo kutoka kwa kahaba huyo akidai chake

VIDEO:

VIDEO: TCRA Yafunguka Kuhusu Kukamatwa Kwa Mmiliki wa Jamii Forums

$
0
0
Tazama Video Hapa Chini Mwakilishi wa TCRA Akiongea baada ya Mmiliki wa Jamii Forums Kusomewa mashtaka hiyo jana....

Bonyeza Video:

WIZARA ya Afya Yakanusha Kuwepo Kwa Virusi vya Ugonjwa wa Zika Nchini....

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amekanusha taarifa za kuwepo kwa vurusi vya ugonjwa wa zika nchini.

Katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo ametoa ufafanuzi huo na kukanusha taarifa za kuwepo kwa ugonjwa huo, huku akirejea kauli yake kuhusu ugonjwa huo aliyoitoa mwezi Februari mwaka huu kuwa ugonjwa huo haujaingia nchini.

Kuhusu utafiti uliofanywa na Taasisi ya NIMR, amesema kuwa utafiti huo ulifanyika nchini kuchunguza ubora wa kipimo kipya cha kupima magonjwa ya zika na chikungunya.

Amesema kwa utaratibu wa kitafiti hiyo ni hatua ya awali ya kuangalia ubora na uwezo wa kipimo hicho na kwamba matokeo yake bado yanahitaji kuchunguzwa kwa kina kupitia vipimo vilivyothibitishwa na Shirika la Afya Duniani.

Taarifa hiyo imesema kuwa wizara kwa kushirikiana na taasisi na ndani na nje ya nchi inaendelea na utafiti na ufuatiliaji wa kitaalamu ili kuzuia ugonjwa huo kuingia nchini na tayari imeshaandaa mkakati wa zika ambao unaelekeza utekelezaji wa ufuatiliaji wa zika.

Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu nchini, (NIMR) iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari kupitia mkurugenzi wake Dkt. Mwele Malecela ilisema kuwa Tanzania ina wagonjwa wa zika ambapo asilimia 15.6 ya watu waliopimwa kati ya mwaka 2015 na 2016 walibainika kuwa na virusi vya ugonjwa huo.

RAIS Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi NIMR Dr. Mwele Malecela

$
0
0
RAIS Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi NIMR Dr. Mwele Malecela, Taasisi NIMR aliyokuwa akiiongoza Jana ilitangaza kuwepo kwa Virusi vya ugonjwa wa Zika Nchini lakini baada Wizara ya afya kupitia Ummy Mwalimu ilikanusha Taarifa Hizo, Bado Haijaeleweka sababu hasa ya kutenguliwa kwake.....

Source:Jamii Forums
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images