Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

Aina 12 Ya Wanawake Ambao Watayafanya Maisha Yako Kuwa Magumu

$
0
0
Kila mtu hapa ulimwenguni ameumbwa na sifa tofauti tofauti. Kuna wengine wameumbwa na tabia za kuridhisha na wengine wameumbwa na tabia ambazo hazifurahishi. Hii pia inajitokeza katika wanawake. Katika mahusiano, utapata kuwa wanawake wanakuwa na tabia ambazo aidha zinawapendeza wanaume wao ama zinawachukiza.
Ok. Katika kuangalia tabia za wanawake, tumekuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanamume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.

1. Mwanamke anayekuganda nguoni
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye amekupenda kisai cha kuwa hawezi kufanya jambo lolote bila kukuhusisha wewe. Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye amekuwa amezama na penzi lako kiasi cha kuwa hakupi nafasi ya kupumua. Kila kitu atakachofanya lazima uwe karibu nayeye. Well, hii ni poa kwa mahusiano lakini itafikia mahali fulani ambapo utachoshwa na tabia zake haraka. Na pia yeye kama mwanamke atakuwa na mawazo finyu kwani kila wakati anapokumbwa na jambo fulani hawezi kulitatua bila kukuhusisha.

2. Mwanamke aliyepagawa kimapenzi
Nani hapendi mwanamke anayempenda kupindukia? Kila mtu angekuwa na mwanamke aina hii wanaume wangekuwa na furaha milele. Lakini kulingana na utafiti ni kuwa aina hii ya mwanamke ni miongoni mwa wanawake wabaya kabisa ambao wanaweza kufanya maisha yako kuwa ya taabu.
Mwanamke kama huyu ungempenda siku za kwanza kwanza lakini tatizo ni kuwa kadri siku zinavyopita mnapokuwa pamoja utagundua tatizo flani, mwanamke aina hii hangependa ufanye chochote bila yeye kuwa karibu yako. Hii inamaana kila mahali unapoenda lazima akuandame. Aidha ukiwa na marafiki zako, vilabuni, wanjani...nk, yaani kiufupi kila uendapo anataka awe hapo hapo ili akuangalie na akupende zaidi. Utamweza kweli huyu?

3. Mtumiaji
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanamume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanamume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa
urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza.

4. Mwanamke asieomba msamaha
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msahama kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

5. Mlalamishi
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.

6. Asiyejielewa
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na nirahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe unamahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuwache wewe wa kwanza.

7. Anayetawala na kutotosheka
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwegu muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.

8.Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa kwani wakisema jambo flani, bila hata kufikiria wenzao.

9. Nusa Nusa
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mindoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Owk aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana nayeye mara moja.

10. Asi na maono
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimmuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama anamalengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope
sana.

11. Mcheza ndondi
Hii ni aina ya mwanamke amabye anakasirika kwa haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake ni vita. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.

12. Mtoto wa mama
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke aina hii hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.

Hii ni baadhi ya tabia za wanawake ambazo mwanamume yeyote anafaa kuwa chonjo kwani mwishoni wanaweza kuleta taabu ambazo zitakuwa vigumu kutatua.

SHINDA Gari la Bure Kama Zawadi ya X-Mass Kutoka Kampuni ya Cars From Japan..Magari Mawili Yanashindaniwa

$
0
0
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote...Basi Hawa Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ...Fuata Maelekezo hapa chini Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi

Bonyeza Hapa : SHINDA GARI

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako

Mwisho wa Kujisajili ni 22 Dec 2016 

TOTO wa Miaka 5 Aliyebakiza Miezi Miwili ya Kuishi Dunia

$
0
0

Mtoto huyu anaitwa, Bradley Lowery, ni shabiki wa kutupwa wa klabu ya Sunderland.

Ana miaka mitano na tayari madaktari wamethibitisha kuwa amebakiza miezi miwili tu kabla kansa haijakatiza pumzi
zake na kuupeleka mwili wake futi 6 chini ya Ardhi.

Kuna kaburi liko wazi tayari likimsubiri Bradley.

Kitu chake cha mwisho kabisa alichokiomba duniani ni zawadi ya kadi ya Krismasi, kadi tu inamtosha kukifanya kifo chake kuwa na amani.

#Everybody dies but not everyone has lived..So sad

PICHA ya ALIKIBA na Mdogo Wake Zari Aitwaye Zulehah Yazua Gumzo Mitandaoni

$
0
0

Picha ambayo inaonyesha Mdogo wa Zari Akiwa na Ali Kiba imezua Maneno maneno mtandaoni huku wengine wakipongeza kitendo hicho na kusema kuwa kitapunguza bifu iliyopo katika ya Ali Kiba na Diamond huku wengine wakidai kuwa Ali Kiba ndo Amejiweka hapo kwa sasa.....

Zulehah mdogo wake na Zari baaada ya kuona maneno maneno ilibidi aweke mambo sawa kwa kuandika haya maneno hapa chini:


KIJANA Aelezea A to Z Jinsi Alivyorubuniwa na Mama Mchungaji Wafanye Mapenzi

$
0
0
KIJANA Aelezea A to Z Jinsi Alivyorubuniwa na Mama Mchungaji Wafanye Mapenzi, Bonyeza Play Hapa Chini Kusikiliza Stori hiyo ya Kusisimua: 

 VIDEO:

Nay wa Mitego Adai Nyumba ya Diamond ya South Afrika Yeye Ameijenga Tabata!

$
0
0



Jana kwenye XXL ya Clouds FM Nay wa Mitegoalikuwepo kutambulisha ngoma yake mpya ambayo ameipa jina la Sijiwezi.

Ndipo alipokutana na story ya list ya wasanii 10 wa Bongo Fleva ambao wamefanikiwa kumaliza ujenzi wa nyumba zao na ikiwa mtonyo wa kijenga nyumba hizo umetokana na music.

Diamond Platnumz alikuwa ni mmoja kati ya wasanii waliopo kwenye list hiyo ambaye yeye inasemekana amenunua nyumba yenye thamani ya zaidi ya Tsh. Million 300 huko nchini South Afrika.

Ndipo Nay wa Mitego alipoikamatia hiyo kwa juu na kudai kuwa mjengo ambao Diamond Platnumzameujenga South Africa, yeye ameujenga hapa hapa Bongo pande za Tabata. Akiwa na maana kuwa nyumba yake ambayo ameijenga Tabata ina thamani sawa na nyumba ya Diamond Platnumz ya huko South Africa (Mil 300).

NINI MAONI YAKO??

MBUNGE Sugu Anusurika ajali, mtoto afariki kwenye ajali hiyo

$
0
0
Taarifa zilizoripotiwa na kituo cha runinga cha ITV leo December 17 2016 zinasema kuwa mbunge wa Mbeya mjini ‘CHADEMA’, Joseph Mbilinyi amenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Iyunga jijini Mbeya baada ya gari lake kufeli break na kumgonga mtoto  ’15’ ambaye amefariki wakati akipelekwa hospitali.

Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa askari polisi wanne wamejeruhiwa baada ya kupata ajali wakati wakielekea kwenye ajali hiyo aliyopata mbunge Joseph Mbilinyi  ‘sugu’

Gari hilo lilikuwa  linaendeshwa na dereva wake, Gabriel Andrew (43) ambaye anashikiliwa na polisi.

Dr MWELE Malechela(Aliyetumbuliwa) : Safari Itasonga Kwa Msaada wa Mungu

$
0
0
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, NIMR, Dr Mwele Malechela, ametoa kauli yake baada ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais Dkt John Magufuli, Ijumaa hii.

Kutenguliwa kwake kumekuja siku moja tu baada ya kuzungumza na waandishi na kudai kuwepo kwa virusi vya Zika nchini. Alisema kati ya watu 533 waliopimwa wakati wa utafiti walioufanya, asilimia 15.6 waligunduliwa kuwa na virusi hivyo. Taarifa yake, ilikuja kukanushwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Akijibu tweet iliyosema, ” Pole sana @mwelentuli safari yako na isonge mbele Dada,” Dr Mwele amesema, “Ahsante na itasonga kwa msaada wa Mungu.”

Tweet nyingine alijibu: Ahsante Mathew. Nilipewa dhamana nimetumikia ninamshukuru Mungu kwa nafasi ya kutumikia WaTanzania kupitia utafiti.”

MAHAKAMA Yatupa Pingamizi la Serikali Katika Kesi ya Mbunge Godbless Lema.

$
0
0
Uamuzi wa kuongezewa muda wa kuwasilisha notisi ya nia ya kukata rufaa dhidi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, unatarajiwa kutolewa Desemba 20, mwaka huu na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Uamuzi huo utatolewa baada ya Lema jana kufanikiwa kuwasilisha maombi yake ya kuongezewa muda wa kuleta notisi hiyo ya rufaa dhidi ya dhamana yake baada ya mahakama hiyo kutupilia mbali pingamizi mbili za mawakili wa Serikali waliokuwa wakitaka maombi hayo yasisikilizwe.

Mbele ya Jaji Dk. Modesta Opiyo wa mahakama hiyo, upande wa Jamhuri ulikuwa ukiwakilishwa na Wakili Hashim Ngole, Matenus Marandu, Elizabeth Swai na Adelaide Kasala huku Lema akitetewa na Wakili Sheck Mfinanga na Faraji Mangula.

Katika maombi hayo namba 69 ya mwaka huu, baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, Jaji Dk. Opiyo alisema kuwa atatoa uamuzi huo siku hiyo saa sita mchana.

“Baada ya kusikiliza hoja za pande zote nitatoa uamuzi Jumanne ijayo saa sita mchana, msije asubuhi ili nipate muda wa kupitia hoja zenu,” alisema Jaji Dk. Opiyo.

Awali, akitoa uamuzi wa pingamizi mbili zilizotolewa Desemba 14, mwaka huu na mawakili hao wa Jamhuri, Jaji Dk. Opiyo, aliyesoma uamuzi huo kwa muda wa dakika 50 kuanzia saa 5:30 asubuhi hadi saa 6:20 mchana, alisema ameamua kuzitupa pingamizi hizo baada ya kuziona hazina mashiko ya kisheria.

Alisema kuwa hakuna maombi kama hayo yaliyoacha kusikilizwa mahakamani kwa kushindwa kuonyesha kifungu namba 392 A cha sheria ya uendeshaji wa mashauri ya jinai hivyo akalitupa pingamizi la kwanza la mawakili wa Serikali waliodai maombi hayo hayakufuata utaratibu wa kisheria ikiwemo kutoonyesha vifungu vya sheria waliyoitumia kuleta maombi hayo.

“Baada ya kupitia hoja za pande zote, mahakama imeamua kutupa pingamizi hizo za Jamhuri baada ya kuziona kuwa hazina mashiko kisheria na hata upande wa Jamhuri ulishindwa kurejea shauri lolote ambalo limewahi kufanyiwa uamuzi na mahakama za juu kuhusu suala hilo,” alisema Jaji Dk. Opiyo.

Akizungumzia hoja ya pili ambayo Jamhuri ilidai ya kiapo kinachounga mkono maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo kimekosewa hivyo hakifai kwa sababu wamejumuisha mambo yasiyotakiwa kisheria ikiwemo maoni, mabishano na hitimisho na kubeba hoja za rufaa alisema mahakama hiyo imeondoa aya ya 11 na 12.

Alisema kuwa aya nyingine za 9, 10, 13 na ile ya 17 zitabaki katika hati hiyo ya kiapo kwa sababu hazibebi hoja za rufaa, maoni, mabishano wala hitimisho hivyo mahakama hiyo haiwezi kukataa hati hiyo ya kiapo iliyoambatanishwa na maombi hayo.

Akiwasilisha hoja za maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha notisi hiyo ili rufaa hiyo iweze kusikilizwa, Wakili Mfinanga, alidai mahakamani hapo kuwa maombi hayo yamewasilishwa mahakamani hapo chini ya kifungu 361(2) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Alidai kuwa uamuzi wanaotarajia kukatia rufaa ni uliotolewa Novemba 11, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na Hakimu Desderi Kamugisha, ambapo Lema anakabiliwa na kesi namba 440 na 441 za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

Alitaja sababu mbili za msingi za kukatia uamuzi huo rufaa kuwa ni kuiomba mahakama hiyo ipitie makosa ya kisheria yaliyofanywa na mahakama ya chini na kusema kuwa uamuzi huo ulimpa mleta maombi (Lema) dhamana ila kabla hajapewa masharti ya dhamana upande wa Jamhuri ulitoa notisi ya nia ya kukata rufaa.

“Kwa msingi huo mahakama ilisema imefungwa mkono na hawawezi kuendelea na jambo lolote kuhusu suala hilo hata uamuzi wake wa kumpa dhamana haukuwezwa kutimizwa na mahakama haikueleza upande wowote ambao haujaridhika na uamuzi huo una haki ya kukata rufaa,” alidai Mfinanga na kuongeza:

“Kuna vitu muhimu na vitasahihishwa iwapo tutaleta notisi ya nia ya kukata rufaa na rufaa yenyewe kusikilizwa na mahakama yako ambayo ni msimamizi wa haki na sheria ikatoa ruksa ili tuweze kusikilizwa na rekodi ya mahakama ya chini iweze kurekebishwa, ni muhimu mahakama kuzingatia maombi haya pasipo kuzingatia mambo mengine.”

Huku akirejea mashauri mbalimbali ya mahakama za juu, aliendelea kueleza mahakama hiyo kuwa mahakama ikishasema imempa mtu haki ya dhamana lazima itaje masharti ya dhamana.

“Tunaomba mahakama itupatie muda tena mfupi ambao hautazidi hata saa 1:30 kwa ajili ya kuleta notisi hiyo ili mahakama iweze kurekebisha makosa hayo,” alisema.

Akiwasilisha hoja ya pili, Wakili Mangula, alidai mahakamani hapo kuwa tangu kutolewa kwa uamuzi huo hawajapumzika na muda wote walikuwa mahakamani.

Alidai kuwa walikuwa wanaenda mahakamani kwa njia tofauti ili kuiomba mahakama irekebishe makosa hayo ya kisheria.

Alidai kuwa baada ya uamuzi huo kutolewa muda wa kazi ulishaisha na ilikuwa Ijumaa hivyo Novemba 14, mwaka huu walipeleka barua ya malalamiko mahakamani hapo na walipoitwa pande zote mbili katika shauri namba 6 lakini walikumbana na pingamizi zilizowasilishwa na mawakili wa Serikali.

“Novemba 22, mahakama ilitoa uamuzi na kututaka waleta maombi tukate rufaa na hapo mleta maombi alipata haki yake ya kukata rufaa ambayo haikuelezwa mahakama ya chini na tulitoa notisi tukiamini tuko ndani ya muda na hatimaye rufaa ililetwa mbele ya Jaji Mfawidhi Fatuma Masengi,” alidai.

Alieleza mahakama hiyo kuwa katika rufaa hiyo namba 113, walikutana tena na pingamizi la Serikali kuwa wametoa notisi ya rufaa hiyo nje ya muda wa siku moja hivyo hizo ni jitihada walizokuwa wakifanya na si wazembe, wajinga wa sheria kama ilivyodaiwa na wakili wa Serikali.

Akijibu hoja za waleta maombi hao, Wakili Ngole, alidai kuwa ni wazembe, wajinga wa sheria na kuwa hata uamuzi wanaolalamikia mahakamani hapo ambao awali ulimpa mleta maombi dhamana, lakini kabla hajapewa masharti ya dhamana mahakama iliingiliwa mamlaka yake hawajawasilisha na maombi hayo.

Wakili huyo alidai mahakamani hapo kuwa hakukuwa na makosa yoyote ya kisheria kama inavyodaiwa na waleta maombi hao na kudai kuwa baada ya hakimu kusema mahakama inampa mshtakiwa dhamana Jamhuri kwa haki yake walisimama na kuifahamisha mahakama wana nia ya kukata rufaa.

“Ni utaratibu wa kisheria kuwa panapokuwa na notisi ya nia ya kukata rufaa mahakama haiwezi kuendelea na jambo lolote kuhusiana na kesi hiyo, hivyo hakimu asingeweza kuendelea na kesi na inafahamika notisi inasimama badala ya rufaa,” alidai na kuongeza:

“Kwa mujibu wa kifungu 359(1) na 361(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, vinaeleza mtu ambaye hajaridhika na hatua yoyote au uamuzi uliotolewa au kupitishwa anaweza kukata rufaa mahakama za juu.”

Lema anashikiliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja katika mahabusu ya Gereza Kuu  la Kisongo baada ya kukamatwa Novemba 2, mwaka huu nje ya Viwanja vya Bunge mjini Dodoma ambapo alifikishwa mahakamani Novemba 8, mwaka huu akikabiliwa na mashtaka ya uchochezi dhidi ya Rais Dk. Magufuli.


VIDEO:
KIJANA AELEZEA JINSI ALIVYORUBUNIWA NA MAMA MCHUNGAJI WAFANYA MAPENZI 

LULU Michael Ameachwa na Majay?....Ashindwa Kujibu Swali

$
0
0
Baada ya kuonekana kwenye tuzo akiwa alone na kuulizwa yupo wapi jamaa yake na kuwa mkali, wambea wamedai huenda mrembo huyo ametemwa na jamaa yake huyo, kutokana na yeye ku demand sana uwepo wake kwake wakati jamaa ni mtu wa biashara na anakosa muda wa mapenzi ya ki sekondari na ya show off....Kidding

Tazama Video:

MWANA FA Asema Wimbo "Muziki" wa Darassa Umerudisha Heshima Kwa Wasanii wa Hip Hop

$
0
0
Msanii wa muziki wa hip hop, Mwana FA amesema hatua ya mafanikio ya wimbo ‘Muziki’ wa Darassa ni hatua ambayo wasanii wengi wa muziki wa hip hop walishindwa kuifikia kwa muda mrefu.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake ‘Dume Suruali’ amesema ni muda mrefu wasanii wa hip hop walikuwa wanashindwa kutoa ngoma ambazo zitaleta ushindani mkubwa na zawasanii wa kuimba.

“Kwanza I’m happy for rap music,” FA alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Imekuwa muda mrefu hatujawahi kutengeneza nyimbo halafu zikatoka na nyimbo za waimbaji, halafu usisikie nyimbo za waimbaji na rap music ikawa vile,”

Mwana FA amesema anapenda kuona Darassa akiendelea kufanikiwa zaidi katika muziki kwa kuwa ni msanii ambaye anaujua uwezo wake katika kile anachokifanya.

Wimbo ‘Muziki’ wa Darassa umeweza kufanya vizuri kwenye chart mbalimbali za muziki. Pia kupitia channel ya mtandao wa YouTbe video ya wimbo huo imeweza kuangaliwa mara 1,787,074 katika kipindi cha wiki tatu.


VIDEO:Watu wamzushia Kifo WEMA SEPETU SIKIA AKIKANUSHA 

NAY wa Mitego Adai Ana Nyumba ya Milioni 300 Tabata...Adamu Mchomvu Ampinga

$
0
0
Wasikilize hapa Watangazaji wa Clouds FM Kina Adam Mchomvu wakibishana na Nay wa Mitego baada ya kusema anajenga nyumba ya milioni 300 inayofanana na ile ya Diamond Afrika Kusini

Bonyeza Play:

Msuva ‘on Fire’ Yanga Kileleni

$
0
0
Yanga imepaa hadi kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara mara baada ya ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya JKT Ruvu  katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili.

Ushindi dhidi ya JKT Ruvu unaifanya Yanga ifikishe jumla ya pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 pointi moja mbele ya mahasimu wao Simba ambao watacheza kesho dhidi ya Ndanda FC mchezo wao wa kwanza wa raundi ya pili ya VPL.

Deusi Kaseke alifunga goli la kwanza la Yanga dakika ya 37 kipindi cha kwanza kwa kuunganisha pasi ya Simon Msuva

Msuva akafunga bao la pili dakika ya 57 kabla ya kufunga tena dakika ya 90 na kuilaza JKT Ruvu huku Yanga ikikaa kileleni mwa ligi ikisubiri matokeo ya Simba.

Lwandamina amepata ushindi wa kwanza katika mechi yake ya kwanza VPL baada ya kupoteza mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya JKU ya Zanzibar.
Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ amepoteza mechi yake ya kwanza VPL tangu alivyoachana na Mgambo JKT ya Tanga na kuchukuliwa na TFF kuifundisha timu ya taifa ya vijana wa U-17 ‘Serengeti Boys.’
Ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa makocha wa timu zote ndani ya (Bakari Shime-JKT Ruvu na George Lwandamina-Yanga) Shime si mgeni wa VPL lakini amesimama kwa mara ya kwanza kama kocha wa JKT Ruvu wakati Lwandamina yeye ameisimamia Yanga kwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa VPL.
Ushindi wa Yanga dhidi ya JKT Ruvu ni wa nane (8) mfululizo tangu mwaka 2013, timu hizo zimecheza michezo nane tangu mwaka 2013 na Yanga imeshinda mechi zake zote kwa zaidi ya magoli mawili.
17/12/2016 JKT Ruvu 0-3 Yanga

26/10/2016 Yanga 4-0 JKT Ruvu

07/02/2016 JKT Ruvu 0-4 Yanga

19/09/2015 Yanga 4-1 JKT Ruvu

25/03/2015 JKT Ruvu 1-3 Yanga

05/10/2014 Yanga 2-1 JKT Ruvu

06/04/ 2014 Yanga 5-1 JKT Ruvu

01/11/2013 JKT Ruvu 0-4 Yanga

Yanga imeshaifunga JKT Ruvu jumla ya magoli 29 katika mechi nane zilizopita huku yenyewe ikiruhusu magoli manne tu tangu mwaka 2013.

ALIKIBA Apata Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mpira Uganda...

$
0
0
Msanii wa Bongofleva Alikiba Jumamosi ya December 17 2016 alikuwa Uganda kucheza mchezo wa Hisani kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kusaidia wa mama wajawazito ambao unajulikana kama Dorah Foundation.

Alikiba akiwa katika mchezo huo wa soka wa hisani uliyowahusisha mastaa mbalimbali, upande wake wa The Celebrity White Team waliibuka na ushindi wa goli 4-1, huku Alikiba akiwa kahusika katika upatikanaji wa goli la pili katika ushindi huo.

Upande wa timu ya Alikiba alikuwa na staa wa soka aliyetamba na Simba na Yanga Emanuel Okwi, ambapo mchezo ulimalizika na Alikiba katika mchezo huo wa hisani alipewa tuzo ya The Best Celebrity Player Award, kama hufahamu ukiachana na muziki Alikiba pia ana uwezo wa kucheza mpira.


VIDEO: KIJANA AELEZEA JINSI ALIVYORUBUNIWA NA MAMA MCHUNGAJI WAFANYA MAPENZI 

BELLE 9 Atoa Wimbo Mpya Akimshirikisha G Nako....Nimekuwekea Hapa Video Uitazame

$
0
0
Tunaofatilia bongofleva toka kitambo tunamfahamu Belle 9, ni mkali mwingine kutoka Morogoro ambapo leo hii ameshirikiana na G Nako kutuletea burudani mpya iitwayo ‘give it to me’ na ukishamaliza kuitazama hii video usiache kusema chochote kwenye comment



ULIPITWA? LULU AMEACHWA NA MAJAY AWA MKALI BAADA YA KUULIZWA


LEILAH RASHID kuachana na MZEE YUSUPH kwa Amani Ikitokea Hivyo, Tetesi za Kupata Mbwana Yemen

$
0
0
Leila Akihojiwa na Sakina lioka Amefunguka yote ikiwemo tetesi za kupata bwana Yemeni na Kuachana na Mzee Yusuph kwa amani

Tazama Video Hapa Chini:

VIDEO: Mwili wa Mwanamke Aliezikwa Akiwa Hai Wafukuliwa

$
0
0
Dunia inaelekea pabaya ..utu umepotea kabisa Embu Tazama VIDEO Mwili wa Mwanamke Aliezikwa Akiwa Hai Wafukuliwa:

NTV Kenya - Wimbo wa 'Aje' Haukustahili Kushinda Video Bora ya Mwaka EATV Awards

$
0
0
NTV ya Kenya kwenye kipindi chao cha uchambuzi wa sanaa na wasanii maarufu kama UDAKU wameongelea tuzo za Eatv na wamezisifia. 

Wakasema pia sababu za Diamond kutokuwepo kwenye tuzo hizo( hakuchukua form) ila pamoja na hayo wakasema yeye ndio alistahili video bora ya mwaka (sijui kwa wimbo gani) na kwamba video ya Aje haina sifa za kuwa video bora ya mwaka ila kuwa wimbo wa mwaka sio tatizo. 

Ila suala la mtu kuchukua form za kushiriki tuzo kwa mwaka huu kwa sababu ni mwanzo sawa ila mwakani wanapaswa kuangalia hilo.


ULIPITWE NA HII?  STORI YA KUSISIMUA Kijana Mwenye Jinsia Mbili 2 ya kike na ya Kiume


SHINDA Gari la Bure Kama Zawadi ya X-Mass Kutoka Kampuni ya Cars From Japan..Magari Mawili Yanashindaniwa

$
0
0
Umeshawahi Kufikiria Kupata Gari la Bure bila Kulipa Chochote...Basi Hawa Kampuni ya Cars From Japan Wanakupa Nafasi Hiyo ...Fuata Maelekezo hapa chini Jinsi ya Kuweza Kuwa Mshindi

Bonyeza Hapa : SHINDA GARI

Kisha Jisajili kwa Kuweka Jina na Email Yako

Mwisho wa Kujisajili ni 22 Dec 2016 

TAARIFA ya Bodi ya Mikopo kwa wadaiwa sugu kuhusu mwisho wa kulipa kwa hiari

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imeongeza muda kwa wadaiwa sugu kulipa madeni yao hadi Desemba 30, 2016.

Hatua ya Bodi inafuatia mwitikio chanya kutoka kwa wadaiwa ndani ya siku 30 za awali ambazo zinakamilika leo Desemba 14, 2016.

Akitoa taarifa ya kuongezwa kwa muda; Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi, Abdul_Razaq Badru amesema kuwa wadau wameomba kuongezewa muda kutokana na baadhi yao kukabiliana na changamoto za majukumu ya kazi na hivyo kushindwa kujitokeza ndani ya siku 30 zilizokuwa zimetangazwa awali.

Katika hatua nyingine, Bw. Badru amesema kuwa ndani ya siku za nyongeza Ofisi za Bodi ya Mikopo zilizopo Mwenge, jijini Dar es Salaam zitaendelea kuwa wazi kwa siku za Jumamosi, Disemba 17, 2016 na Jumapili, Disemba 18, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri ili kutoa fursa muhimu kwa wadaiwa wote wa mikopo ya elimu ya juu ambao hawajaanza kurejesha mikopo yao kupata taarifa kuhusu madeni yao na kulipa.

Ili kuharakisha utoaji wa muhtasari wa deni la mdaiwa; mhusika aje na Majina yake kamili, Chuo alichosoma, Mwaka wa kuanza na wa kuhitimu, anuani yake ya barua pepe (email), nambari ya simu ya kiganjani, mwajiri wake na Check Number yake iwapo ameajiriwa serikalini.
‘Kuwa Mzalendo, Rejesha Mkopo wa Elimu ya Juu’

Kwa mawasiliano zaidi piga 0763 459165 au 0767 513208

Imetolewa na:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
14/12/2016
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images