Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Sungura Amtikisa Mbatia .....Amtaka Ajiuzulu Nafasi ya Mwenyekiti NCCR-Mageuzi ili Kukinusuru Chama

0
0
Aliyekuwa  Mkuu wa Idara ya Kampeni ya Chama cha NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura, amenzisha fukuto kwa kumtaka Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia kujiuzulu nafasi yake kwa madai kuwa ameshindwa kukiongoza chama hicho tangu alipoingia madarakani.

Sungura anasema bila kufanya hivyo, atashirikiana na wanachama wengine kumwondoa, kwa sababu amekisahau chama na kujikita katika shughuli nyingine zisizo na tija, jambo ambalo limechangia chama hicho kupata mbunge mmoja kwenye uchaguzi uliofanyika Oktoba, mwaka jana.

Anasema hali ilipofikia hivi sasa, chama hicho kinaweza kufa na kubaki historia ambayo haiwezi kuwasaidia wanachama wengine wanaopigania uhuru na demokrasia ndani ya nchi yao.

“Hatumwondoi Mbatia kwa sababu tunamchukia, bali tunamwondoa kwa kushindwa kuangalia masilahi ya chama na kujikita kwenye shughuli zisizo na tija, jambo ambalo limechangia kupoteza wabunge na kubaki na mbunge mmoja ambaye ndiye yeye katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana.

“Kwa sababu nafasi ya uenyekiti si ubatizo na wala si kiungo cha mwili wake, hata tuseme tutamuumiza, hivyo basi tunaamini vijana wenye mapenzi mema na chama wataungana na mimi kuhakikisha kuwa mwenyekiti anatoka madarakani ili tuweze kukiendesha chama,”- Sungura.

Anadai  kuwa lengo lao ni kufanya siasa zenye tija, zikiwamo za kuzunguka mikoani kutafuta wanachama wapya na kuandaa viongozi ambao wataweza kukisimamia chama hadi uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

Anasema kutokana na hali hiyo, nafasi yake itakabidhiwa kwa mwanachama mwingine kama alivyonyang’anywa mwenzake na kijiti kukabidhiwa yeye ili aweze kukiongoza chama.

Sungura alijunga na chama hicho tangu mwaka 1992, akiwa mwanachama mwenye kadi N0. 00011763.

Ofisa Utawala wa chama hicho, Frolian Mbeo, alipoulizwa kuhusu kauli ya Sungura, alisema hadi jana mchana hakuwa na taarifa yoyote ya kuwapo malalamiko ya mwanachama huyo.

Alisema uamuzi wa Sungura, umekuja  baada ya kutolewa kwenye nafasi ya ukurugenzi wa kampeni, jambo ambalo limemfanya kuzunguka mikoani na kuanza kukisema vibaya chama.

AJALIi 3 Kubwa za Magari Alizopata SUGU Tangu 2013

0
0
AJALI YA KWANZA

December 17, 2016, imeripotiwa ajali ya gari kumuhusu Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la (SUGU), kwenye kivuko cha barabara (ZEBRA) na kumsababishia kifo mtoto ’15’ ambaye alifariki wakati akipelekwa hospitali.

Tukio hilo limetokea leo Desemba 17 majira ya saa mbili asubuhi huko katika eneo la Iyunga Jijini hapa, wakati gari ya Mbunge huyo ikiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege wa Songwe kwa ajili ya mapokezi ya kiongozi wa Kitaifa Freeman Mbowe.



AJALI YA PILI

January 10, 2015 ili ripotiwa kuwa Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amenusurika katika ajali ya gari eneo la Mlima Kitonga, wilaya ya kilolo mkoani Iringa.

Chanzo cha ajali hiyo kilitajwa kuwa ni kufeli kwa break hali iliyopelekea gari hilo kuanguka kichwa chini miguu juu wakati mbunge huyo akitokea Mbeya kuelekea Mikimi mkoani Morogoro kwenye mkutano wa hadhara.

Katika gari hilo aina ya Totoya Land Cruiser ambalo lilikuwa likiendeshwa na mheshimiwa Sugu, lilikuwa limebeba   watu wanne ambao wote walisalimika na kutoka salama licha ya michubuko ya mkononi aliyoipata mbunge huyo wa Mbeya Mjini.
AJALI YA TATU

Juni 19, 2013 Mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi alipata ajali katika eneo la kasheki wilayani Hanan'g akielekea Arusha mjini.

Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu alikuwa akielekea Arusha mjini kuungana na wabunge wengine wa Chadema katika shughuli ya kuaga marehemu waliolipukiwa na bomu kwenye mkutano wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika ajali hiyo hakuna mtu yoyote aliyejeruhiwa, Mbunge huyo yuko salama, gari la Sugu limeharibiwa vibaya baada ya kugongana na basi la abiria.

Maxence Melo Afunguka "Mtandao wa Jamii Forums Haujatetereka Bado Upo Ngangari"

0
0

Baada ya kuchiwa leo kwa dhamana Mwanzilishi mwenza wa JamiiForums, Maxence Melo amesema mtandao wa JamiiForums haujatetereka na bado uko ngangari na amewataka watumiaji wote wa mtandao huo waondoe hofu kwa kuwa taarifa zao za siri ziko salama.

Pia amesema hana ugomvi wowote na vyombo vya dola na ana imani na mahakama za hapa nchini kuwa zitamtendea haki katika kesi yake.

Amewataka wananchi wote bila kujali itikadi zao kuendelea kupigania uhuru wa kusema na kutoa maoni, pia amevishukuru vyombo vyote vya habari na wanahabari kwa kumuunga mkono kipindi chote alipokuwa mahabusu.


VIDEO:MCHUNGAJI WA KANISA LA ANGLIKANA ANASWA NA KAMERA AKIFANYA NGONO NA MKE WA MTU

CALISAH Afunguka....Adai Wema Sepetu ni Msichana Mwelewa na Ana Mapenzi ya Kweli

0
0

Mwanamitindo aliyejipatia jina mwaka huu kutokana na kuwa na uhusiano wa muda mfupi na Wema Sepetu, Calisah, amemwelezea muigizaji na Miss Tanzania huyo wa zamani kuwa ni msichana mzuri na mwenye mapenzi ya kweli.

“Wema ni msichana mzuri, ana upendo, ni mwelewa, ana mapenzi ya kweli, sijaona kasoro kubwa ambayo yeye anayo kubwa tofauti na wasichana wengine,” amesema Calisah. “Ni msichana anayejua kucare, ana real love, pia ana mapungufu yake lakini mazuri ni mengi,” amesisitiza.

Model huyo ameongeza kuwa kwa sasa yeye na Wema hawazungumzi tena baada ya wiki kadhaa zilizopita kusambaa mtandaoni video inayowaonesha wakibusiana kwa mahaba mazito, kitu ambacho kilimkera Wema na kuvunja uhusiano wao.

Hata hivyo Calisah amekiri kuwa uhusiano wake na Wema umemuongezea umaarufu zaidi na kumrahisishia kazi zake.

VIDEO:MANGE KIMAMBI ACHOMA MOTO KADI YA CCM 

BELLE 9: Diamond Aliniwahi ila Mimi Ndio Nilikuwa wa Kwanza Kutumia Vionjo vya Saida Karoli....

0
0
Msanii Belle 9 amekuja juu baada ya kuambiwa ameiga kuweka vionjo vya salome kwenye nyimbo yake
msanii huyo amesema wazo la ku sample wimbo huo alikuwa nalo kabla ya Diamond ajabu Diamond akatoa wimbo kabla yake

Tazama Video:

FAMILIA ya Ben Saanane Kukagua Mwili wa Mtu Uliochomwa Kwenye Kiroba Moshi

0
0

Wakati polisi wakisema kuwa wanaufanyia mchakato wa vipimo vya vinasaba (DNA), mwili wa mtu anayedaiwa kuuawa nje kidogo ya mji wa Moshi na kuwekwa kwenye kiroba na kuchomwa moto, familia ya Ben Saanane, msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye hajulikani aliko imesema inaenda kuuangalia mwili huo.

Hatua hiyo ya polisi kupima DNA ilielezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa baada ya hadi jana, mwili huo kutotambuliwa.

Mauaji hayo yaligunduliwa Ijumaa iliyopita, baada ya watu waliokuwa na gari ndogo ambao hawajafahamika, kumchoma moto mtu huyo katika Kijiji cha Ongoma na kisha kutoweka kusikojulikana.

Kamanda Mutafungwa aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mtu huyo hajafahamika na wala hakuna mtu aliyejitokeza kuutambua mwili huo hivyo kulilazimu jeshi kufanya uchunguzi huo wa kisayansi.

Kamanda Mutafungwa alitoa wito kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopotelewa na ndugu, wafike katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kuutambua mwili huo.

Kuhusu madai ya marehemu kwamba alikuwa amevaa suruali inayofanana na sare za wafungwa, Kamanda Mutafungwa alisema si kweli kwani nguo iliyoonekana ni blanketi jepesi la rangi ya chungwa.

Mzazi wa Saanane
Wakati polisi ikijiandaa kwa mchakato huo, baba wa Saanane, Focus Saanane, jana alikuwa anajiandaa kwenda KCMC kuangalia mwili huo.

Akizungumza jana mjini Moshi, Saanane alisema japokuwa mtoto wake alipotelea Dar es Salaam, watakwenda kuuangalia mwili huo ili kujiridhisha.

Juzi Saanane alikaririwa akiiomba Serikali kufanya uchunguzi wa kupotea kwa mwanaye akisema ndiyo pekee yenye vyombo vya kiuchunguzi.

Kuokotwa kwa mwili huo kunashabihiana na tukio la kupatikana kwa miili mingine saba katika Mto Ruvu mkoani Pwani ikiwa imefungwa katika viroba na kuwekewa mawe ili izame.

Miili hiyo ilizikwa na wananchi wanaoishi jirani na mto huo bila kufanyika kwa vipimo vya DNA wala kutoa tangazo la watu waliopotolewa na ndugu zao kujitokeza kutambua maiti hizo hali iliyoibua utata.

Tayari Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, alishaagiza kufanyika kwa uchunguzi wa miili hiyo na kutaka wale wote waliohusika na mauaji hayo watafutwe na kukamatwa.

ALI Kiba na Ommy Dimpoz Katika Kashfa ya Kutokumlipa Aliyewatungia Nyimbo ya Kajiandae

0
0

Zimetufikia za kunyapia nyapia kutoka shirika la wambea SHILAWADU kuihusu hitsong ya wakali wawili wa muziki hapa Bongo Ommy Dimpoz naAlikiba na ngoma yao ya Kajiandae.

Inasemekana kuna mtu  afahamikae kama Devi Zinda ambaye anadai kuwa kauandika wimbo huo na hapo awali alilipwa shilingi za kitanzania Laki 5 (500,000) na Ommy Dimpoz kama malipo ya wimbo huo na kuahidiwa kumaliziwa kitita kingine cha shilingi laki 5 ili kutimia million 1 kama ilivyokuwa makubaliano ya malipo ya uandishi wa wimbo hu

KIWANGO cha Pesa Kesi za Mafisadi Kushushwa Chini ili Kuwabana Wengi

0
0
WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema serikali inatarajia kujadili kushusha kiwango cha fedha kinachohusika katika makosa ya rushwa na uhujumu uchumi kwenye mahakama ya mafisadi ili kukomesha vitendo vya rushwa.

Mwakyembe alitoa kauli hiyo jana mara baada ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

“Nimeulizwa sana na waandishi wa habari tangu Julai hadi sasa walitegemea kungekuwa na kesi nyingi lakini kuna kesi moja katika Mahakama ya Mafisadi tumekuja kubaini kwamba uchache wa kesi ndiyo mafanikio makubwa ya hatua ya kisheria tuliyochukua,”amesema.

Aliongeza kwa sasa waliozoea kupora mabilioni wamerudi nyuma ambapo wezi hao wameonekana wakiiba fedha chini ya Sh bilioni moja iliyopo kisheria hivyo wanategemea kujadili sheria hiyo ili iwalenge hata wanaochukua kiasi kidogo.

“Sisi kama serikali tukiona wizi sasa umenza kupungua na kuenea katika viwango vya Sh milioni 400, 500, 700 tumeanza kujadiliana kuangalia uwezekano wa kushusha kiwango cha fedha ili tuweze kukomesha kabisa udokozi, ubadhilifu, wizi wa fedha au mali ya umma,”alisema.

Aidha alifafanua uamuzi wa Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda kutafuta vijana wanaojua sheria ili kusaidia wananchi kabla ya kwenda mahakamani ni mzuri.

Aliongeza kuwa tayari wamepeleka mswada wa msaada wa kisheria ambao utasaidia wananchi hasa wa vijijini na wanawake ambao ndiyo wanaumizwa na desturi zilizopitwa na muda ili kuwasaidia kupata haki na itakuwa na wasaidizi wa kisheria nchi nzima wapatao 4,900.

Makonda alisema wamejadili utoaji na upatikanaji wa haki kwa wakati kwani kuna changamoto ya watu kuwa wengi na kuchelewa kupata haki zao.

Alisema kwa kuona adha hiyo mkoa huo kwa kushirikiana na Wakuu wa wilaya watajenga Mahakama za Mwanzo 20 ili kuongeza kasi za utoaji na upatikanaji wa haki kwa wananchi endapo wanapopelekwa vituo vya polisi.

RIDHIWANI Kikwete Awaponda Diamond na Ali Kiba, Awapa Onyo

0
0
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ameponda Diamond na Ali Kiba kuwa na bifu akisema zinaweza kusababisha madhara makubwa akitolea mfano bifu ya Tupac na notorious big

Pia amesema mzee wake anapenda muziki lakini wa zamani ila wasanii wa bongo flava alikuwa akikutana nao kwa kuungabishiwa na yeye

SHIBUDA Ashinda Uenyekiti Baraza la Vyama vya Siasa, Aahidi Kuimarisha Uhusiano kati ya UKAWA na Rais Magufuli

0
0
Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, John Shibuda ametamba kuwa ataimarisha uhusiano wa kisiasa kati ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na Rais John Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa CCM.

Shibuda ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Ada Tadea, alitoa tambo hizo jana, ikiwa ni dakika chache baada ya kuchaguliwa kuongoza baraza hilo kwa kipindi cha miaka miwili katika uchaguzi uliofanyika jijini Dar  akichukua nafasi ya Peter Kuga Mziray wa APPTMaendeleo kilichofutwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Shibuda alisema atatumia fursa, uzoefu na uwezo alionao kuhakikisha vyama vyote vinakuwa na matumaini ya ushiriki wa kisiasa kupitia heshima ya baraza hilo.

“Nimepokea kwa furaha matokeo haya lakini najua nina mzigo mbele yangu. Hilo la mahusiano ninamtanguliza Mungu anisaidie ili kuhakikisha naotesha matumaini mapya katika baraza hili. Nitakunjua vizibo vyote vilivyoziba katika mahusiano haya, ushirikiano wa siasa zetu uwe kwa masilahi ya Watanzania na utaifa wetu,” alisema mbunge huyo wa zamani wa CCM na Chadema.

Shibuda aliibuka mshindi baada ya kupata kura 20 dhidi ya mpinzani wake, Mwenyekiti wa CCK, Constantine Akitanda aliyefuata kwa kura 14.

Jumla ya kura 36 zilipigwa huku mbili zikiharibika. Katibu wa CCK, Renatus Muabhi alipongeza ushindi wa Shibuda huku akitoa angalizo kuwa asikubali kutumika kulinda masilahi ya kundi la chama kilichopo madarakani.

 “Namwamini kwa uzoefu wake atasaidia kurejesha heshima ya baraza hilo ila kama atayumbishwa, sisi tuko tayari kushawishi kura ya kumwondoa madarakani,” alisema.

Wengine waliogombea kiti hicho ni Hashim Rungwe (Chaumma), Anna Mghwira (ACT), Fahmy Dovutwa (UPDP), Hassan Kisavya (NRA), na John Cheyo wa UDP ambaye alijitoa.

Baadhi ya vyama vilivyoshiriki katika uchaguzi huo ni Sauti ya Umma (Sau), CUF, CCM, DP, Demokrasia Makini, Jahazi Asilia, Ada-Tadea, CCK na Chadema.

Baraza la Vyama vya Siasa ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa kwa lengo la kuweka jukwaa la kujadiliana masuala yenye masilahi kwa Taifa na uimarishaji wa mfumo wa vyama vingi nchini.

VIDEO:MANGE KIMAMBI ACHOMA MOTO KADI YA CCM

EXCLUSIVE: ‘Ukweli sina mimba, nilifanya vile kwa sababu’ Nisha Bebee

0
0
Siku za karibuni staa wa bongo movie Salma Jabu maarufu Nisha bebee alionkana kuwa ni mjamzito kwa madai kuwa alipata mimba hiyo mara baada ya kubakwa, leo amekubali kukaa na Ayo TV katika exclusive interview na kuelezea ukweli kuwa hana mimba badi alifanya vile kwa sababu alizozitaja hapa kwenye hii video... 

VIDEO:

TAZAMA Video ya Fumanizi la Mchungaji wa Kanisa na Mke wa Mtu

0
0

TAZAMA Video ya Fumanizi la Mchungaji wa Kanisa na Mke wa Mtu 

MAMA Mzazi wa MR Nice Afunguka Baada ya Habari Kusambaa Kuwa Mr Nice Amefariki Dunia

0
0
Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba msanii wa siku nyingi wa bongofleva Mr. Nice amefariki na mwili wake upo Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Mama Mzazi wa Mr. Amesema Haya:

“Kusema ukweli hayo mambo yalisemwa lakini mimi nilizungumza na mwanangu live akasema yeye ni mzima wa afya mimi sikusikia kwenye vyombo vya habari nilisikia watu wakisema ndio nikataka anipigie simu ili niweze kujua hali yake ikoje. Alinipigia tukazungumza” – Mama Mr. Nice

VIDEO:Mwili wa Mwanamke aliezikwa akiwa hai wafukuliwa

VIDEO:Mchungaji Gwajima Aliposema Atamfufua Amina Chifupa

0
0
Tujikumbushe Gwajima Alipotoa kauli ya kumfufua Amina Chifupa, Nimekuwekea Video  kuhusu Kumfufua Amina Chifupa aliyefariki mda mrefu uliopita. Askofu Gwajima anadai Moja ya mtu aliyerudishwa kutoka kwenye msukule ndio aliesema alimwacha Amina Chifupa akiwa huko kwenye misukule

KABURI la Faru John layeyuka

0
0

Sakata na kifo cha Faru John (38), limechukua sura mpya baada ya wahifadhi wa eneo la Sasakwa Singita Grumet kueleza kuwa hakuna kaburi lake kwa kuwa hakuzikwa.

Wamesema hayo siku moja baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutangaza kuunda timu mpya kuchunguza mazingira ya kifo cha faru huyo huku akihoji mambo manne yaliyozua utata.


Mambo aliyohoji wakati akifanya majumuisho ya ziara yake mkoani Arusha ni juzi, Faru John aliumwa lini, aliumwa nini, daktari gani aliyemtibu na zilipo taarifa za matibabu yake.


Pia aliagiza mwili wa faru huyo kufukuliwa na kutazama kama vinasaba vyake vinaendana na watoto wake 26 ambao bado wapo katika Creta ya Ngorongoro.


Akizungumza na mwandishi wetu jana, mmoja wawahifadhi wa Sasakwa Grumet aliyeomba kutotajwa jina ili kutoathiri uchunguzi wa tukio hilo, alisema kitaalamu wanyama ambao wanakufa bila kuwa na magonjwa ya mlipuko katika maeneo ya hifadhi hawazikwi.


“Faru John baada ya kufa aliondolewa pembe zake na kutupwa ili kiwe chakula cha wanyama wengine wanaotegemea mizoga, lakini kuna mifupa yake,” alisema.


Alisema faru huyo aliombwa na Grumet kwenda kupanda faru waliopo katika eneo hilo, hasa baada ya dume aliyekuwapo huko kuuliwa na tembo.


“Baada ya kuonekana kuna haja ya kutafuta dume, ndipo tuliomba kupata faru dume na tukaletewa na baadaye alikufa,” alisema.


Eneo hilo la Sasakwa Singita Grumet ni mali ya mfanyabiashara mkubwa raia ya Marekani, bilionea Tudor Jones ambaye amewekeza katika maeneo kadhaa ya uhifadhi.


Akifafanua hatua zinazochukuliwa baada ya mnyama kufa katika hifadhi, mhifadhi Peter Isango alisema kwa kawaida huzikwa au kuchomwa moto pale tu wanapobainika kuwa na magonjwa kama kimeta.


“Kama mnyama ana magonjwa ambayo yanaweza kuambukiza, basi anachomwa moto au kufukiwa lakini kama anakufa kawaida na magonjwa ya kawaida huwa anatupwa ili fisi, bweha na wanyama wengine wanaokula mizoga wale na hii ndiyo ikolojia,” alisema.


Kauli hiyo iliungwa mkono na mkurugenzi mkazi wa shirika la uhifadhi la kimataifa la Frankfurt Zoological Society, Gerald Bigurube ambaye alisema kwa kawaida wanyama wanaokufa hifadhini huwa hawazikwi.


Bigurube ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) alisema kwenye kanuni za uhifadhi kitu chochote, kinachokufa ndani ya hifadhi huachwa kwa ajili ya kulinda ikolojia na bionuwai.


“Mnyama ambaye anakufa kwa kifo cha kawaida mzoga wake unapaswa kuachwa kuoza na kutumiwa na wanyama wengine,” alisema.


Alisema hata wanyama wa kawaida kama swala na wengine wanapoumwa huwa hawatibiwi tofauti na wanyama kama tembo, faru na wengine wakubwa ambao hutibiwa.


Hata hivyo, alipoulizwa kuhusu Faru John, Bigurube alisema taasisi yake haikuwahi kushiriki katika suala hilo.


Wapata dhamana


Katika hatua nyingine, Polisi imewaachia kwa dhamana maofisa watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Tanapa waliokuwa wanashikiliwa kwa tuhuma za kumhamisha Faru John kutoka Creta ya Ngorongoro na kumpeleka Sasakwa Grumet.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema jana kuwa licha ya dhamana hiyo, uchunguzi unaendelea.


Watuhumiwa hao ni Israel Naman ambaye alikuwa kaimu mkuu wa idara ya hifadhi wakati faru huyo akiondolewa, Cuthbert Lemanya aliyekuwa mkuu kanda ya Creta, Dk Athanas Nyaki ambaye ni daktari wa mifugo wa mamlaka hiyo.


Wengine ni aliyekuwa kaimu mkuu idara ya maendeleo ya jamii, Kuya Sayaleli na kaimu mkuu idara ya ikolojia, Patrice Mattey.


Kabla ya kukamatwa, maofisa hawa walikiri kushiriki kumhamisha Faru John kutoka Creta ya Ngorongoro hadi Sasakwa kwa maelezo kuwa ilikuwa ni kuendeleza uhifadhi wa faru na pia kutokana na ukorofi wa Faru John kuhodhi majike yote ndani ya Creta kuua madume wengine waliozaliwa.


Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Arusha, Waziri Mkuu alitoa taarifa za kifo cha faru John huku akiwatuhumu baadhi ya watendaji wa NCAA kuhusika na njama za kumuuza kwa Sh200 milioni ambazo alisema walishapokea malipo ya awali ya Sh100 milioni.


Baada ya maelezo hayo, Waziri Mkuu alitaka kupewa taarifa kamili za tukio hilo, pamoja na pembe za faru huyo, ambazo alikabidhiwa Desemba 8 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na kaimu mkurugenzi wa msaidizi kitengo cha kupambana na ujangili, Robert Mande ambaye alimweleza kuwa taratibu zilifuatwa katika kumhamisha.

MBUNGE wa Arumeru mashariki Joshua Nassari aifagilia serikali ya awamu ya tano

0
0
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Mheshimiwa Joshua Nassari amepongeza na kusifu jitihada kubwa zianazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea maendeleo wananchi wa maeneo mbalimbali nchini wakiwemo wa jimbo lake.
Kufuatia hatua hiyo Mheshimiwa Nassari ameahidi kushirikiana bega kwa bega na Serikali ili kuhakikisha maendeleo yanakuwa endelevu.

Mheshimiwa Nassari ametoa pongezi hizo leo mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye alikuwa katika majumuisho ya ziara yake ya siku 10 ya kikazi mkoani Arusha.

Mbunge huyo ambaye alilazimika kuja nchini kwa dharura akitokea masomoni nchini Uingereza ili kumuwahi Waziri Mkuu, amesema ameridhishwa na hatua za utatuzi wa migogoro ya ardhi zinazochukuliwa na Serikali.
Amesema ziara ya Waziri Mkuu mkoani Arusha, imesaidia kutibu majeraha na makovu makubwa yalitokana na matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana."Kama kuna kiongozi ambaye hawezi kuunga mkono jitihada hizi za kuwaletea maendeleo watu wetu, atakuwa na matatizo,” amesema.

Ameongeza kuwa kitendo cha Waziri Mkuu kuweka mikakati ya kushughulikia migogoro ya ardhi iliyodumu kwa miaka mingi ni ushahidi tosha kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwasaidia wananchi wa kawaida.

Nassari amesema mwaka 1952 wazee wa Meru walimtuma mtu kwenda Uingereza kuomba uhuru wa wananchi wa Arumeru ili waweze kujitawala na kumiliki ardhi yao kutoka kwa wakoloni.

NAY wa Mitego Adai Mpenzi Wake wa Sasa Hataki Kuuzishwa Sura Kwenye Mitandao ya Kijamii

0
0
Mwanamke ambaye amemfanya rapa Nay wa Mitego aandike wimbo ‘Sijiwezi’ hataki habari za kuuzishwa sura katika mitandao ya kijamii kama wapenzi wengine wa rapa huyo waliopita.


Akiongea na Bongo5 Jumatatu hii, Nay amedai hawezi kufanya kitu ambacho hapendi mwanamke huyo na ataendelea kuheshimu maamuzi yake huku akikiri kuwa ni jambo gumu kwake kwa kuwa alishazoea kushare picha za wapenzi wake katika mitandao ya kijamii.

“Huyu niliye naye kwa sasa hataki kusikia kuhusu masuala ya kuweka sijui picha kwenye mtandao,” alisena Nay. Ni mwanamke fulani ambaye ana msimamo wake kuhusu maisha yake, hataki masuala ya kuyumbishana yumbishana kwenye mapenzi,”

Rapa huyo amedai bado wanaendelea kuchunguzana lakini anadhani huwenda akawa ni mwanamke wa kwanza mwenye tabia za tofauti kuwa naye na huenda akafika naye mbali zaidi.

PENDEZA na Markson Beauty Products...Kukuza Makalio, Kungarisha Ngozi na Kwa Wanaume Kukuza Cassava

0
0

HABARI NJEMA
MARKSON BEAUTY
PRODUCTS

Baada ya kupata cheti cha bidhaa bora kwa mwaka 2015-2016, Sasa kampuni hii inasambaza huduma zake ndani na nje ya nchi kwa vibali maalum. Bidhaa zetu zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa. Hazina kemikali wala madhara.

DAWA ZETU NI YA:-
1. kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @100,000/=
2. Kuongeza shepu (hips na makalio) kwa/= (a)Dawa ya kunywa au kupaka @150,000/=
(b)Vidonge @170,000/=
3. Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:- (1)Mafuta @100,000/=
(11)Vidonge @150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @120,000/=
5. Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a) Gely ya kupaka @120,000/= (b) Vidonge maalum @120,000/= (c) Handsome up original @170,000
6. Kuondoa mvi milele zisiludi tena @100,000/=
7. Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito @120,000/=
8. Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a) Dawa ya kunywa au kupaka @120,000/= (b) Mkanda wa kawaida @100,000/= (c) micro-computer belt unaovaibret @200,000/=
9 .Kupunguza maziwa na kuyasimamisha @90,000/=
10. Kushepu miguu na kuwa minene @100,000/=
11. Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @90,000/=
12. kubana uke na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa mwanamke @100,000/=
13. Taiti za hips na makalio @150,000/=
NB: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii kwa bidhaa halisi.
Wasiliana nasi :-
(+255) 0767447444 na
0714335378
Google MARKSON BEAUTY.
Follow us @Markson_beauty_pr
@Markson_beauty_pr

JOH Makini Abariki Lord Eyez Kuondoka Weusi...Adai Kila Mtu Ananjia Yake Katika Maisha

0
0
Hatimaye Joh Makini amezungumza kuhusiana na taarifa za Lord Eyez kusainishwa kwenye label ambayo Barakah The Prince ameianzisha.

Joh amesema pamoja na kuwa Lord Eyez ni mshkaji wake mkubwa, ana uhuru wa kuchukua uamuzi anaodhani una manufaa kwake.

“Mimi Lord Eyez mbali na muziki ni mshkaji wangu sana, we are family. Hata ninavyoongea na wewe wiki moja nyuma kabla sijaenda South Africa tulikuwa wote usiku huo,” amesema Joh. “Mwisho wa siku unajua naheshimu sana maamuzi ya mtu binafsi na sipendi kuingilia. Kwa mfano siwezi kuongelea uamuzi wa yeye kusainiwa au kutosainiwa na Barakah The Prince sababu that’s him,” ameongeza.

“Naheshimu kila kitu ambacho yeye anakifanya kwasababu mwisho wa siku kila mtu ana njia yake, ana maisha yake, kila mtu ana maamuzi yake. Unajua huwezi kumuamlia mtu mzima.

 VIDEO:

TUNDU Lissu Ang’ang’aniwa Kisutu

0
0
LICHA ya utetezi wa kutaka kuondolewa kwa shitaka la kwanza na tano uliofanywa na wakili wake katika kesi ya uchochezi kwenye Gazeti la Mawio inayomuhusu Tundu Lissu, Jabir Idrissa, Simon Mkina na Ismail Mahaboob, mashtaka hayo wamesomewa leo,

Awali mawakili wa utetezi walitaka shitaka la kwanza na tano kutosomwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa madai kuwa, yanaupungufu kisheria ikiwa ni pamoja na kukosa kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singiuda Mashariki , Simon Mkina Mhariri wa Gazeti la Mawio, Jabir Idrissa – mwandishi mwandamizi wa gazeti hilo na Ismail Mahboob ni Meneja wa kampuni ya uchapishaji ya Flint tarehe 19, Juni 2016 walishitakiwa na Jamhuri kwa madai ya kufanya uchochezi kwa kuchapisha habari iliyobeba kichwa cha maneno “Machafuko yaja Zanzibar” tarehe 14-20 Januari 2016, Toleo Na. 182.

Tarehe 20 Septemba 2016, mahamkama hiyo ilitoa uamuzi wa pingamizi hilo ambapo upande wa jamhuri uliambiwa kuwa unauwezo wa kurudisha upya mashtaka hayo.

Leo Patrick Mwita wakili wa serikali mbele Thomas Simba Hakimu Mkazi Mkuu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amesoma shitaka la kwanza na tano.

Mwita amedai kuwa shitaka la kwanza ni la kupanga njama za kutoa chapisho la uchochezi, kosa linalodaiwa kutendwa kati ya tarehe 12 na 14 Januari mwaka huu ambapo;

Idrissa, Mkina na Lissu katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam walipanga njama za kuchapisha taarifa za uchochezi.

Katika kosa la tano, mshitakiwa namba moja (Idrissa), namba mbili (Mkina) na namba nne (Lissu), wanatuhumiwa kuchochea hofu miongoni mwa wananchi kwa kuchapisha habari “Machafuko yaja Zanzibar” na kwamba, ingeweza kuzua vita au umwagaji damu.

Mashtaka hayo yalikuwa yanapingwa na mawakili wa upande wa utetezi kwa hoja ya kuwa na upongufu wa kisheria ikiwa pamoja na kutokuwa na kibali cha mwendesha mashtaka wa serikali.

Awali upande wa Jamhuri ulilazimika kusoma mashitaka matatu ambalo ni la pili, tatu na nne.
Shitaka pili likimkabili Jabir, Mkina na Lissu, wakidaiwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika Gazeti la MAWIO, toleo Na. 182 la tarehe 14-20 Januari 2016.

Shitaka la tatu linamuhusu Ismail akidaiwa kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti hilo lenye kichwa cha Habari ‘Machafuko yaja Z’bar’.

Shitaka la nne linamkabili Ismail akidaiwa kuchapisha gazeti bila kupeleka kiapo kwa Msajili wa Magazeti.

Upande wa Jamhuri umedai kuwa, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo wameiomba mahakama ipange tarehe ya usikilizwaji wa awali. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 18 mwezi mosi mwaka 2017.
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images