Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

DIAMOND Alamba Mamilioni ya CAF, Kutumbuiza Uzinduzi wa AFCON 2017

$
0
0
Shirikisho la soka barani africa CAF limemchagua diamond platnumz na kumlipa mamilioni kutumbuiza kwenye sherehe za uzinduzi wa michuano ya mataifa africa yatakayofanyika nchini Gabon maarufu kama Afcon2017

Michuano hiyo itafanyika mapema mwakani 2017

Uganda ndo taifa pekee ya africa mashariki lililofanikiwa kufuzu
Akiongea kwenye kipindi cha Times Fm manager wa diamond sallam ameongeza kuwa diamond tayari ana booking mpaka julai 2017. Kama unamtaka inabidi usubiri hadi julai

HUU Wimbo Mpya wa Baghdad na Roma f/ Snura Unaitwa K Utata Mtupu Mwanzo Mwisho...Usikilize Hapa

$
0
0
Baghdad na Roma wameigeukia Singeli katika wimbo wao K waliomshirikisha Snura. Ni wimbo utakaokuvunja mbavu kwa ujumbe wake. Enjoy.

KUHUSU Ommy Dimpoz,Alikiba na Mr Nice,yamezungumzwa haya na Meneja wa Diamond.

$
0
0
Kuhusu Ommy Dimpoz,Alikiba na Mr Nice,yamezungumzwa haya na Meneja wa Diamond.
Times Fm imepata nafasi ya kufanya Exclusive interview na Sallam ambaye ni moja kati ya Mameneja wa Diamond Platnumz,yapo maswali yaliyohusu maisha yake,kazi yake ya kwanza na namna walivyokutana na Diamond mpaka kufanya kazi pamoja,hizi ni tweets za yote aliyoyazungumza.

‘Nimezaliwa 1980 Ocean Road Dar,Nimekulia Morogoro na kusomea huko,nilizuiliwa Forest kwa sababu ya Ukorofi so nimeishia form 4. #SallamLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Kuna kundi letu lilikua watukutu tulianzisha 1993,kati ya wasanii tuliokua tunahang nao ni pamoja na O-ten,AY alikua shabiki wangu’.#Sallam

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Kuna kundi letu lilikua watukutu tulianzisha 1993,kati ya wasanii tuliokua tunahang nao ni pamoja na O-ten,AY alikua shabiki wangu’.#Sallam

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Nilikua narap kwa fan sio kazi,nilipomaliza shule nikaingia kwenye biashara,album yangu ya kwanza nilinunua CD ya Saleh Jabri #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Tarehe 24 nitapambana na @diamondplatnumz kwenye jukwaa maana anajisifia sana anajua kurap’. – @Sallam_SK @raheemdaprince SkyTanzania

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘AY ndiye aliyenirudisha kwenye entertainment kwa sababu ya AY ana connection na wasanii wengi,tulianza na kina Prezoo na Huddah’.#SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Nilipata deal la kumleta @iam_Davido iyanya na J Martin,Diamond nilikutana nae 2012,Diamond ilikua afanye kazi na Mr Nice’. #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Mr Nice namjua siku nyingi,kipindi hicho alikua anaitwa B nice alikua ana rap na tumefahamiana nae wote tukiwa Morogoro’.- #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Nina album nzima ya Mr Nice ninayo ndani,muda wowote akiwa tayari tunaweza kuiachia tu,siwezi kuachia bila idhini yake’. – SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Msanii nilimuongoza kabisa ni Mr Nice nilifanya nae kwa miezi 6 tu’ – #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Kama hauko upande wangu lazima unichukie,mimi hata kitu sio kizuri nitalazimisha kiwe kizuri’. #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘2013 @diamondplatnumz aliniambia tufanye number one rmx na ndiyo safari yetu ilianzia hapo na ndiyo ilikua kazi yangu ya kwanza’. –#SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Ukiingia kwenye suala la muziki hapa Tanzania lazima ukutane na Fella pamoja na Tale’. #SkLive.

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Sekta yangu mwanzo WCB ilikua ni ya kupanda ndege,kidogo Mungu alinisaidia kilugha nakijua,kimesababisha nipande sana ndege’. #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Naongea lugha tatu kiswedish,Kiswahili na Kiingereza na Kiarabu nakijua jua’. #SkLive cc @Sallam_SK @raheemdaprince SkyTanzania

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Najiita Mugabe kwa sababu maamuzi yake yamenyooka,hayapindi; – #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Tuliwahi kuzinguana na @diamondplatnumz tukiwa Paris tukijiandaa kufanya Kolabo na Hayati Papa Wemba’ – #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Target yetu ni kukuza soko la muziki la ndani liwe kubwa zaidi Afrika,inabidi tupromote wasanii wote wafike mbele’. #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘WCB nina share zangu kwenye bodi ya Wakurugenzi’. #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Kolabo za kimataifa za @diamondplatnumz nazifahamu kwa sababu nyingi zinapitia kwangu,local huwa anazimaliza yeye mwenyewe’. #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Wimbo wa @QueenDarleen_tz haikua mipango kuitoa jana na tuliitoa kama zawadi kwa mashabiki wa WCB’. –#SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Kuna wasanii nje ya Tanzania tunataka kuwaongoza kama SK Entertainment sio WCB,hatuwezi kuweka kila kitu WCB,tutakua tunajifunga’.-#SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘@RichMavoko alipitia kwa @AyTanzania na mimi ndiye nikasema atafanikiwa akiwa chini ya WCB,tulimpa muda afikirie kabla ya kusaini #Sklive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Kwangu sioni utofauti wa wasanii wa WCB kwa sababu kila mmoja ana vionjo vyake’. – #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Kokoro ilianzia kwa Abydad sisi tunaangalia manufaa ya msanii na kibiashara zaidi pamoja na mafanikio’ – #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Mi sio meneja wa Diamond peke yake,namuongoza AY pia sio kila muda nionekane mtu wa WCB kuna muda inabidi nionekane wa SK Entertainment

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Niliona mapato ya @OfficialAliKiba yanapotea Kenya,nilimwambia Tale ampgie @SevenMosha na nikawatajia hadi jina la mtu anayewaibia’#SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Nilimpost @SevenMosha kwa sababu nilimaanisha ni Mrembo,mimi niko single lakini nina Familia’. –#SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Show ya Mombasa bajeti yangu ilikua kwenye hesabu ya @wizkidayo nilienda kupiga stori na rafiki yangu Sunday ambaye ni meneja wa @wizkidayo

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Kila mtu aangalie maisha yake kati ya @ommydimpoz na @diamondplatnumz so watafutane wenyewe waombane msamaha’. – #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Napokutana na @ommydimpoz @AyTanzania na @MwanaFA tunaongelea kitu kinachokuwepo hapo mezani,tunakua hatuna muda wa kudiscus watu, #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Ijumaa hii team nzima ya WCB tutakua tunauza tiketi za VIP pale Mliman City zikiisha hizo hatuna zingine,tiketi mlangoni hakuna’. #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Moja kati ya wasanii watakaoperfoam tar 24 ni pamoja na @iam_kcee tunamalizia taratibu za mwisho za usafiri kila kitu tayari’. #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Kwenye maamuzi ya WCB @ZariTheBosslady hana maamuzi tukija kutambulishwa kama Mkurugenzi mwenzetu pia sawa,kukwazana hatujawahi #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Marekani siendi kwa sababu nina matatizo yangu binafsi toka miaka ya nyuma lakini 2017 mtaniona sana’. – #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Siku namjua @diamondplatnumz kwa mara ya kwanza 2012 alikuja na @ommydimpoz ndiyo maana vitu vyao naona havinihusu’. –#SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Tulitaka kufanya kitu kama mechi kati ya team @OfficialAliKiba na team @OfficialAliKiba watu wacheze mpira halafu usiku tufanye show#SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Show ambazo @diamondplatnumz kalipwa hela nyingi ni show ya @Tigo_TZ na show zote za Kenya. – #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘@diamondplatnumz anapenda sana kununua nyumba,Nadhan hapa DAR ana nyumba 7 na ile ya South Africa ni ya 8′. – #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Team hazituumizi zaidi ya kutuongezea hela,mnapotujazia comment ndipo ubalozi unapokuja na hela ndio zinazongezeka’. #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘DSM Stand Up ya Chid Benz ndio wimbo wangu bora muda wote,@darassa_cmg anafanya vizuri sana naomba watu wamuongezee sapoti’ –#SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Ikitokea nataka kumsaini msanii wa hip hop kwenye muziki nitamsaini @FidQ ,sasa hivi kidogo kapunguza ugumu,tunaweza kufanya kazi’. -SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘@Barnabaclassic namkubali sana huyu ni FUNDI’ – #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘Kuna Online Radio tumefungua inaitwa @DizzimOnline nipo na @BabuTale ,tuna website,studio,mtu akifika akionyesha CV zake anaweza kuajiriwa’

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

‘WCB kwa sasa ina wasanii 4 na Diamond wa 5 ila kuna kijana yuko pale anaitwa LavaLava anapiga back vocal kwa @diamondplatnumz ‘. #SkLive

— DizzimOnline (@DizzimOnline) December 21, 2016

SHAHIDI wa Pili Atoa Ushahidi Kesi ya Tundu Lissu, Neno ‘Dikteta Uchwara’ Latikisa

$
0
0
Kesi ya uchochezi dhidi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana imeendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo upande wa Mashtaka umetoa ushahidi wa pili.

Lissu anakabiliwa na mashtaka ya kutoa kauli za kichochezi na maudhi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Shahidi huyo wa pili aliyetambulishwa kama ASP Kimweri, alisema kauli ya Lissu aliyoitoa June 28 mwaka huu kuhusu ‘Dikteta uchwara’, ililenga katika kufanya uchochezi na ilikuwa ya maudhi dhidi ya Rais na ililenga kuchochea wananchi kuipinga na kuichukia Serikali.

Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwampamba, shahidi huyo aliongeza kuwa kauli hiyo ya Lissu pia ililenga katika kuhatarisha usalama wa taifa kama ingesambazwa sehemu kubwa.

Naye Wakili wa Lissu, Peter Kibatala alimtaka shahidi huyo kuieleza mahakama ni nani ambaye mteja wake alikuwa anamtaja kama ‘dikteta uchwara’ na taifa analolizungumzia kwenye madai yake.

Akijibu maswali ya Wakili Kibatala, ASP Kimweli alisema kuwa hakufahamu kiuhalisia ni nani ambaye Mbunge huyo alikuwa akimrejea katika matamko yake na pia hakufahamu ni taifa gani alilokuwa akilimaanisha.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 18 mwakani itakaposikilizwa tena mahakamani hapo. Lissu yuko nje kwa dhamana.

ALIYEKUFA Muda Mfupi Baada ya Kubatizwa Azikwa Kiislam

$
0
0
Kijana Issa Juma aliyeripotiwa kufariki dunia Jumapili iliyopita, muda mfupi baada ya kubadili dini na kubatizwa katika mto mmoja kwa imani ya Kikristo akijiunga na kanisa la Efatha kwa jina la Paulo, amezikwa kwa imani ya Kiislam.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya kuwepo mvutano kati ya Kanisa la Efatha na viongozi wa dini ya Kiislam wakitaka kijana huyo azikwe kwa imani yao, lakini mwisho kauli ya wazazi wa marehemu ilikuwa na nguvu zaidi na hivyo kuzikwa kwa imani ya Kiislam.

Akizungumzia uamuzi huo, mama mdogo wa marehemu ambaye jina lake halikupatikana alizungumza kwa niaba ya mama mzazi, Rehema Juma alithibitisha kuwa walimzika ndugu yao Jumanne wiki hii kwa imani ya Kiislam.

Kifo cha kijana huyo kiliibua sintofahamu ikiwa ni saa chache baada ya kuzaliwa kwa mara pili kwa imani ya Kikristo na haikufahamika mara moja chanzo chake kama alikuwa na ugonjwa ama ni masuala ya kiimani.

MBUNGE Godbless Lema Augua Ghafla Gerezani....Ashindwa Kufika Mahakamani

$
0
0
Kesi iliyokuwa isikilizwe 21 Disemba 2016 inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema pamoja na mkewe, Neema Lema wakituhumiwa kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo imeahirishwa kutokana na hali ya Godbless Lema kuwa mbaya gerezani.

Taarifa za Godbless Lema kushindwa kufika mahakamani zimetolewa na wakili wa serikali Elizabeth Swai kwa Hakimu Mfawidhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Augustino Rwezile ambapo alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa Afisa Magereza zikieleza kuwa mbunge huyo anaumwa na amepewa mapumziko hivyo asingeweza kufika mahakamani.

Aidha, taarifa kutoka kwa kiongozi huyo wa magereza hazikueleza wazi kuwa mbunge huyo anaugua ugonjwa gani.
Kuhusu kesi hiyo inayowakabili wanandoa hao wawili leo walikuwa wasomewe hoja za awali ambapo pia shahidi wa kwanza kutoka upande wa Jamhuri, George Katabazi alikuwa atoe ushahidi
.
Godbless Lema na Neema Lema wanakabiliwa na kesi ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha kitendo wananchodaiwa kuwa walikitenda kupitia ujumbe mfupi wa simu mara baada ya Rais Magufuli kumteua Mrisho Gambo kuuongoza mkoa huo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 18 Januari 2017.


POLISI Yaomba Msaada Kumtafuta Msaidizi wa Mbowe

$
0
0
Baada ya kukaa siku 33 bila kuzungumzia kutoweka kwa Ben Saanane ambaye ni msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, jana Jeshi la Polisi lilijitokeza na kuomba msaada kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia kupatikana kwake.

Aidha, hatua hiyo ya Jeshi la Polisi imetolewa wiki moja tangu Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu atoe tamko la kuitaka Serikali kueleza kama imemkamata au inamshikilia kada huyo aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba 18.

Mbali ya kutaka Serikali ieleze mahali alipo msaidizi huyo wa Mbowe, pia mwanasheria huyo alitaka ufuatiliwe ujumbe wa vitisho aliowahi kutumiwa kupitia simu yake ya mkononi na mtu asiyejulikana.


PAUL Pogba Aonyesha Uwezo Kupiga Michano Kama Msanii Darassa

$
0
0
Kwa sasa hivi ngoma inayofanya vizuri kwenye hiphop ni Muziki wa Darassa. Wiki iliyopita nilikupa story ya kwanini Darasa alimtaja footballer Mbwana Samatta kwenye ngoma yake.

Leo hii namfananisha Pogba akiwa anachana kwenye beat kali kama vile alivyofanikiwa msanii Darasa kufunga mwaka na ngoma kali.

Sasa naomba uangalie uwezo wa Paul Pogba alivyodondoka na beat hii na uniambie uwezo wake unaonaje. Video hii ilirekodiwa wakati wapo kwenye michuano ya Euro jijini Paris. Hapo alikua na mshkaji wake Antoine Griezmann.

VIDEO: Mkuu wa Wilaya Aagiza Kukamatwa Mwandishi wa Habari wa ITV Kwa Tuhuma za Uchochezi

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti ameagiza kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa ITV wa mkoani Arusha, Khalfan Liundi kwa tuhuma za kuandika habari za uchochezi.

Kukamatwa huko kwa Liundi kumekuja siku chache baada ya kufanya mahojiano na wananchi waliokuwa na malalamiko ya maji wakidai maji yamefungwa kwa siku saba.

Wafanyakazi wenzake ambao ni pamoja na mpigapicha wake walielezea tukio hilo la kukamatwa kwa mwandishi huyo ambapo walisema kuwa Askari walifika katika ofisi zao na kusema kuwa walikuwa wanahitajika kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano. Walipofika waliabiwa kuwa wanahitajika kwa Mkuu wa Wilaya na baada ya hapo ndipo mwandishi huyo akakamatwa.

Hapa chini ni video ya mashuhuda wa kukamatwa kwa mwandishi huyo wa ITV

MENEJA wa Diamond Aelezea Zilipofikia Collabo za Diamond na Rick Ross na Rihanna

$
0
0
Hivi karibuni wakati anahojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond alitease ujio wa ngoma ambazo amewashikirisha wanamuziki heavyweight wa Marekani, Rick Ross na Rihanna.

Jumatano hii kupitia kipindi cha Campus Vibes cha Times FM, meneja wake, Sallam alifafanua zaidi kuhusu hatua iliyofikiwa ya collabo hizo. Sallam alidai kuwa collabo na Rick Ross imeshakalimika, huku ile ya Rihanna ikiwa kwenye hatua za mwisho kwakuwa tayari CV na historia ya Diamond imeshatumwa kwa uongozi wake kuweza kufikiwa maamuzi ya mwisho.

Kuhusu nyimbo alizoshirikishwa Diamond, Sallam alisema mwakwani itatoka ngoma aliyoshirikishwa na Burna Boy na Cassper Nyovest huku pia Dj Van wa Morocco akimshirikisha pamoja na msanii mkubwa wa Dubai.

Alidai kuwa kutokana na ubusy alionao hitmaker huyo wa Salome, imekuwa ngumu kupata muda wa kushoot video ya wimbo alioshirikishwa na msanii wa Jamaica, Alaine, wimbo alioshirikishwa na msanii wa Ivory Coast Serge Beynaud pamoja na kukamilisha wimbo anaoshirikishwa na rapper namba moja wa Cameroon, Stanley Enow.

Pia alidai kuwa Diamond atatumbuiza kwenye tuzo CAF 2016, Alhamis ya January 5, 2017 mjini Abuja, Nigeria na pia kwenye ufunguzi wa kombe la mataifa ya Africa (Total Africa Cup of Nations),itakayofanyika nchini Gabon kuanzia January 14.

MKUU wa Wilaya Mdogo Kuliko wote Tanzania na Sifa za Mwanaume Anayetamani Kuolewa naye

$
0
0
Zainab Abdallah, Mkuu wa wilaya ya Pangani ndiye kiongozi wa nafasi hiyo mwenye umri mdogo kuliko wote Tanzania, kwa sasa Zainab ana miaka 23 tu na bado hajaolewa lakini pia anazo sifa anazohitaji kutoka kwa mwanaume anayetamani kuolewa nae.

AYO TV na millardayo.com imempata Zainab Abdallah kwenye Exclusive na ameeleza jinsi anavyokutana na maswali mengi kuhusu lini ataolewa, nani ataolewa naye na je atakuwa na sifa zipi ili waendane.

“Nahisi nahitaji kuolewa na hata baadhi ya viongozi wameniambia Zainab utafika mbali sana lakini una mtihani mmoja tu unahitaji kuolewa, hilo ndio swali kubwa naulizwa. Unajua mimi ni binti mdogo lakini nimepanda sana kwenye siasa.”

“Kuna wakati nafikiria kuolewa na mwanaume ambaye hayuko kabisa kwenye masuala ya siasa, kwasababu tutaweza kuiweka sawa familia wakati mimi napokuwa kwenye kazi yeye atakuwa na muda na watoto, wakati mimi niko na watoto yeye atakuwa kwenye siasa, mwanaume ambaye ni mfanyabiashara labda au meneja wa taasisi fulani tena akiwa hajulikani nitakuwa salama zaidi” – Zainab Abdallah (DC Pangani) VIDEO:

LEMUTUZ Amchana Darasa...Ashangaa Kusikia Anasafari kwa Gari Badala ya Ndege

$
0
0

lemutuz_nation - LIVE STRAIGHT TALK:- Nilikuwa nasubiri baada ya ajali kwako @darassacmg najua now umepona upo sawa pamoja na kushitushwa na ajali lakini la msingi nimeshitushwa na jinsi ulivyopata ajali please sikutegemea at this stage unapopiga "WIMBO WA TAIFA" bado utaendelea kusafiri kwenye level ambazo hata mimi SOCIAL MEDIA KING nilishazipita that was a shock to me nilidhani huu ni wakati wako wa kusafirina Airbus mpaka Mwanza halafu promoters wanakukodia ndege kutoka Mwanza mpaka Kahama ukiwa na kundi la angalau watu 5 ....please kaa chini jitathmin tena enzi za Show za Vichochoroni zimeisha now it is your time kataa pesa ndogo upate kubwa huwa inaiuma sana kukataa Dola 2,000 but bila kukataa hutapata pesa kubwa na perks kubwa muamuzi ni wewe sio wanaokuzunguka nakuhakikishia kwa Miungu yangu yote wewe sasa ni wa Tsh. 15M mpaka 20M per Show ....halafu management yako inatakiwa kupigana sana kufufua miziki yako ya zamani ambayo haiku hit lakini ni mikali sana nafasi ni sasa hairudii mara mbili ikiisha imetoka pigana upate CASH CAUSE CASH IS THE KING ....anayekutaka sasa ni lazima akulipie ndege wachana na safari za magari madogo na ikibidi kama sehemu ina pesa lakini ni mbovu waachie pesa yao linda heshima ya jina lako ....niliwahi kuitwa kikazi Lindi nikakataa kwa sababu hakuna ndege Airbus na hamna Five Star Hotel nikakataa Mahela yao mengi U know so please jifunze how to play the next level game you have the juice sasa hivi kuna mahela kibao ya Kolabo unachohitaji ni Super Management ni ushauri wa bure tu na kwa nia njema sana unapotuona sisi kila wakati tunarusha picha tukiwa kwenye ndege na mahoteli makubwa kuna wanaodhani tunajiringishia tu na ujiko kumbe usichokijua ni huwa tunatuma ujumbe kwa wanaotuhitaji kibiashara kwamba itakugharimu like this hahahahaha....Darassa muziki in you hauozi kama hawataki kulipa usipige tu lakini usikubali kufa masikini na huku umepiga "WIMBO WA TAIFA"! - le Mutuz Nation

USHAURI wa Daktari Kwa Darassa Baada ya Kupata Ajali ya Gari

$
0
0
Jumapili Disemba 18 mwanamuziki Darassa akiwa na mtayarishaji wa muziki, Abbah pamoja na mtayarishaji wa video za muziki, Hanscana walipata ajali Kahama mkoani Shinyanga walipokuwa njiani kurejea Dar es Salaam.

Katika ajali hiyo ambapo Darassa ndiye alikuwa dereva, wote walinusurika kifo lakini wakiwa na majeraha machache.

Baada ya kufika Dar es Salaam, Darassa alikwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajli ya matibabu na baada ya kufanyiwa vipimo, alitakiwa kupumzika kwa muda bila kufanyama matamasha ya muziki au shughuli nyingine ngumu ili aweze kupona majeraha madogo aliyoyapata.

Picha: Mwanamuziki Darassa apata ajali Kahama
Kupitia CloudsFm leo Darassa amesema kuwa “Nipo hospitalini Muhimbili sasa hivi nawashukuru sana madaktari wa hapa wamenipokea vizuri wamenipa huduma nzuri sana, wamenicheki kwa sababu nilikuwa najisikia vibaya sana sehemu za kichwani nashukuru Mungu majibu yanaonyesha kila kitu kipo poa kabisa kuna damage ndogo wanaifanyia kazi naendelea na matibabu ila nimeshauriwa kupunguza mizunguko kwa wiki moja ili niweze kupumzika na kutibu hayo maumivu ya kichwa.”

Darassa ni mwanamuziki anayetamba zaidi kwa sasa nchini Tanzania na wimbo wake wa Muziki aliomshirikisha Ben Pol ambao umekuwa ukishangiliwa popote pale unaposikika.

POLISI Agoma Kumtaja ‘Dikteta Uchwara’ Kizimbani

$
0
0
ASP Kimweli, Mratibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi ambaye ni shahidi wa pili katika kesi inayomkabili Tundu Lissu Mbunge wa Singida Mashariki, amepata kigugumizi cha kumtaja diktekta uchwara katika ushahidi wake, anaandika Faki Sosi.

Tundu Lissu anatuhumiwa kufanya uchochezi akisema “Dikteta uchwara” anapaswa kupingwa na watu wote.

Akitoa ushahidi wake leo, ASP Kimweli mbele ya Godfrey Mwambapa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu alieleza kuwa terehe 28 Juni mwaka huu katika viwanja vya mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu alimsikia Lissu akitoa maneno ya uchochezi.

Akiongozwa na Mohammedi Salum wakili wa Serikali alidai kuwa alimshudia Lissu akitoa maneno ambayo yangeweza kuwashawishi wananchi waipinge serikali yao.

Baada ya ASP Kimweli kueleza hayo ,Peter Kibatala wakili wa upande wa utetezi alimuuliza Shahidi huyo kuwa Dikitekta uchwara ni nani? Ndipo aliposema hamjui.

Kibatala : Ni sahihi kuwa unayoyaongea Mahakamani, mliyajadili na wakili wa serikali hapo nje?
ASP Kimweli: Sio sahihi.
Kibatala: niliwasikia mkijadili kuhusu hii kesi hapo nje.
ASP Kimweli: Tumeongea mengi pamoja na masuala kesi.
Kibatala: Mpaka unaenda Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati ulijua kuwa hilo ni kosa. Je ni nani aliyetajwa kuwa ni dikteta uchwara?
ASP Kimweli: Simjui, lakini Lissu alisema kuwa hata kama amechaguliwa na wananchi.
Kibatala: Ni sahihi kuwa wapo wengi wanaochaguliwa na wananchi.
ASP Kimweli: Ndio.
Je, unajua kuwa hapa Tanzania askari wetu wanaenda kupambana vita nchi jirani kupinga utawala wa uonevu na udikteta?
ASP Kimweli: Ni kweli.
Kibatala: Ni sahihi kuwa Mwalimu Nyerere alipinga udikitekta?
ASP Kimweli: Ndio.
Kibatala: Katika maneno aliyoyasema Lissu alieleza ni nchi gani na dikteta apingwe kinamna gani?
ASP Kimweli: kimya.
Maswali magumu
Naye Jeremia Mutasebya wakili wa upande wa utetezi aliongeza maswali ambayo yalikuwa magumu kujibiwa kwa upande wa shahidi.
Mutasebya: Ni Kosa au sio kosa kwa mbunge wa upinzani kuwaalika wananchi wawapinge wanasiasa wengine kwa njia ya kupiga kura.
ASP Kimweli: sio kosa.
Mutasebya: Je kwa ufahamu wako chama cha Demokrasia na Maendeleo kipo kuhalali.
ASP Kimweli: ndio.
Mutasebya: Ni kosa au sio kosa kwa chama cha upinzani na kukiondoa kukipinga chama tawala madarakani.
ASP Kimweli: Sio kosa.
Mutasebya : Je ni sahihi kwa Mbunge wa upinzani kupinga kwa nguvu zote serikali iliyokuwepo madarakani kwa kutumia nia ya kidemokrasia.
ASP Kimweli: Kimya.
Mutasebya: Kwa ufahamu wako Tanzania ni nchi ya kidemokrasia au ya kidikteta?.
ASP Kimweli; Demokrasia.
Mutasebya: Je dikteta ni neno la kisiasa.
ASP Kimweli: Ndio.
Mutasebya: Je, siku ile kulikuwepo na waandishi wa habari na walitoa zile habari kwenye TV, redio na magazeti?
ASP: Ndio.
Mutasebya: Katika maelezo yako ulisema kuwa maneno yale yangeweza kusababisha wananchi kushawishika kuipinga serikali yao. Je tangu siku hiyo ulisikia tukio lolote linalotokana na maneno ya Lissu?
ASP Kimweli: Sijasikia.
Kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 18 Januari mwakani kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

TANGU Nimefunga Ndoa, Sioni Tabu Naona Raha tu – Mwana FA

$
0
0
Msanii wa muziki wa hip hop, Mwana FA amesema anayafurahia sana maisha ya ndoa tofauti na inavyodhaniwa na vijana wengi wenye uoga wa kuingia katika maisha hayo.

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Dume Suruali, amedai toka aingia kwenye maisha ya ndoa amekuwa ni mtu mwenye furaha zaidi.

“Ndoa siyo ngumu kama inavyofikiriwa na wengi, cha msingi muelewane, kila mtu ajue unachofanya, na kuheshimu nafasi yake ndani ya ndoa, maisha ya ndoa ni mzuri sana, tangu nimefunga ndoa, sioni tabu naona raha tu,” Mwana FA alikiambia kipindi cha FNL cha EATV wiki hii.

Mkali huyo wa wimbo ‘Bado Nipo Nipo’ aliyoitoa takriban miaka 7 iliyopita iliyokuwa ikitisha vijana kuoa, amedai aliyoyaimba katika ngoma ile ni ya kweli, na yalimsaidia kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kuingia kwenye ndoa na ndiyo maana ndoa yake haina mambo kama yale aliyoyaimba katika ngoma ile.

KRC Genk ya Samatta imepoteza mchezo dhidi ya Zulte-Waregem

$
0
0
Ligi Kuu soka Ubelgiji iliendelea usiku wa December 21 2016 kwa michezo kadhaa kuchezwa, timu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilikuwa mgeni wa timu ya Zulte-Waregem katika uwanja wa Regenboog.

KRC Genk ikiwa ugenini imekubali kupoteza mchezo kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na  Souahilo Meite dakika ya 26 ya mchezo, kwa matokeo hayo KRC Genk wanakuwa na takwimu kwa mechi zao 5 zilizopita kushinda mechi 2, kufungwa mechi 2 na kutoka sare mchezo mmoja.

Kwa upande wa Mbwana Samatta kocha wake Peter Maes ameendelea kumuamini na kumpanga kwa dakika zote 90, mchezo uliyopita Genk walilazimishwa sare ya kufungana goli 2-2 na Standard de Liege goli la pili la kusawazisha la Genk lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 78.

TUNDU Lissu Akamatwa na Jeshi la Polisi

$
0
0
TUNDU Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam

“Nashikiliwa na polisi hapa Kituo Kikuu kutokana na ile press conference (mkutano na waandishi wa habari) kuhusu kupotea kwa Ben Saanane,” alimweleza mwandishi wa habari hii kupitia simu leo.

Mwandishi alimtafuta Lissu kutaka kujua baadhi ya mambo, ndipo alipopokea simu na kueleza hivyo. Hakuna taarifa zaidi mpaka sasa.

Saanane ambaye ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa-Freeman Mbowe alipotea ghafla takribani mwezi mmoja sasa na hajulikani alipo.

Wafuasi wa CHADEMA wamekuwa wakimsaka kiongozi huyo bila mafanikio yoyote jambo ambalo limeendelea kuzua hofu kama yu hai ama ameuawa.

Tarehe 14 Desemba mwaka huu, Lissu alizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam akiomba vyombo vya ulinzi kusaidia kupatikana kwa kiongozi huyo.

Chanzo: Mwanahalisi

RAIS Magufuli Amteua Jaji Semistocles Kaijage Kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

$
0
0
Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Makamu wake(Himid Mahamoud Hamid).

Ateua majaji wengine 4 kuingia Mahakama ya Rufani

GAZETI la Guardian la UK Latoa Nyimbo Kumi Bora za Africa Mwaka 2016, Mtanzania Ashika Nafasi ya 2

$
0
0
Gazeti ya the guardian la uingereza litemtoa nyimbo kali za mwaka 2016 zilizotikisa africa.
Katika orodha hiyo tanzania imebahatika kuingia nyimbo 1 tena ikishika nafasi ya 2,
Diamond platnumz kupitia wimbo wake wa salome amefanikiwa kushika nafasi ya 2 huku, nafasi ya kwanza ikienda nigeria kwa kuchukuliwa na msanii Tekno na wimbo wake wa Pana

Orodha kamili
1. Pana -- tekno
2. Salome -- diamond ft rayvany
3. Hollup -- mr eazi ft joey B and danny krame
4. No kissing baby --- patoranking ft sarkodie
5. Wololo --- babe wodumo ft mampintsha
6. Dance for mr --- eugy ft mr. Eazi
7. Ngudu --- kwesta ft cassper nyovest
8. Koffi anan --- yemi alade
9. Soweto baby ----- dj mophorisa ft wizkid
10. Uncondionational bae --- sauti sol ft alikiba

NISHA Afunguka Sababu za Kudanganya Kuwa ni Mjamzito

$
0
0

Kila mmoja ilimsikitisha story ambayo mwanadadaNisha alikuwa akitupanga na kutuaminisha kuwa amebakwa na aliyekuwa mpenzi wake na kupelekea kupata ujauzito.

Kitu ambacho kilizua utata mkubwa sana na maswali ya sintofahamu na kupelekea wasanii ambao wamewahi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Nisha kuingizwa katika sakata hilo akiwemo Nay wa Mitego.

Siku chache zilizopita Nisha alisikika katika vyombo vya habari akifunguka ukweli kuhusu ujauzito wake na kudai kuwa ni kazi ndiyo ilimfanya kudanganya hivyo lakini yeye sio mjamzito. Kitu ambacho kiliwatoa mapovu wengi ambao walikuwa wakimfuatilia mwanadada huyo.

Soudy Brown amepiga story na mwanadada huyo kwenye U-Heard ya leo December 22 na amefunguka mengi kuhusu kitendo chake hicho cha kudanganya umma. Soudy pia alimvutia waya Nay wa Mitego ili kutaka kujua ana kipi cha kuzungumza baada ya story hizo za mwanadada Nisha.
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images