Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

TATU Bora Mchezaji Bora Afrika Zatoka

$
0
0

Mshambuliaji raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang, mshambuliaji na winga wa Algeria Riyad Mahrez na winga wa Senegal  Sadio Mané wameingia kwenye orodha ya wachezaji wattau bora wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika.

Wachezaji hao watatu wamefika hatua hiyo baada ya kupigiwa kura na makocha na wakurugenzi wa ufundi wa vyama vya soka vilivyokuwa chini ya  CAF, kamati za vyombo vya habari, kamati za soka na ufundi na wataalamu wa habari. Mohamed Salah na Slimani hawajafanikiwa kuingia katika hatua hii.

Kwa mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani, golikipa wa Uganda Dennis Onyango na Mzimbabwe Khama Billiat na mchezaji wa Zambia kiungo Rainford Kalaba wameingia.

TWashindi watatangazwa kwenye tuz hizo maarufu kama Glo-CAF Awards Gala siku ya Alhamis, 5 January 2017 jijini Abuja, Nigeria.

 

Mchezaji bora wa Afrika

Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)

Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)

Sadio Mané (Senegal & Liverpool)

 

Mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)

Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns)

Rainford Kalaba (Zambia & TP Mazembe)

VIDEO: Saida Karoli Adai Diamond Katapeliwa

$
0
0

Saida Karoli Adai Diamond Katapeliwa, Angalia Video Hii Hapa Chini:

KWANINI Wachagga Hupenda Kwenda Kwao Mwishoni Mwa Mwaka?

$
0
0
Nimeamua kuandika kipande cha waraka huu kutokana na kuwepo kwa dhana nyingi potofu juu ya wachagga kwenda kwao kipindi cha mwisho wa mwaka, maarufu kama "kwenda kuhesabiwa".
Je ni kweli wachagga huenda kuhesabiwa? Jibu ni Hapana.. si kweli. Wachagga hawaendi kuhesabiwa.
SWALI; Sasa kama hawaendi kuhesabiwa neno "kuhesabiwa" limetoka wapi na kwanini litumike kwao tu sio kwa Wasukuma, Wamasai, Wayao au Wamakonde?

JIBU; Neno "kuhesabiwa" limetoholewa kutoka neno la Kiebrania "מִפקָד אוֹכלוּסִין" linalomaanisha Wana wa Israel kurudi kwao kwa ajili ya kuhesabiwa.

Mara nyingi Waisrael walikua wanarudi kipindi cha mwisho wa mwaka wa Kiyahudi ktk mwezi uitwao "Adar Beit" ambao kwa mujibu wa Kalenda ya Kiyahudi huo ndio mwezi wa mwisho wa mwaka. Na hukaa huko hadi mwezi wa kwanza wa mwaka ambao kwa kiyahudi huitwa "Nissan".
Utamaduni huu ulitumika ktk Israel ya zamani (Ancient Jews) japo kwa sasa haupo tena. Katika kipindi hiki Waisrael walikua wakikutana nyumbani na kupanga mipango ya maendeleo pamoja na kuhesabiwa ili kujua idadi yao kutokana na kutawanyika katika mataifa mengi duniani.
Tangu enzi za Musa miaka zaidi ya 4,000 kabla ya Kristo; Waisrael walikua na utamaduni wa kurudi kwao kuhesabiwa.

Katika kitabu cha 1 Nyakati 23:2-3 Biblia inasema "Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi. Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikapata thelathini na nane elfu."

Huu ni udhibitisho wa kuhesabiwa kwa Wana wa Israel zamani hizo. Lakini pia kitabu cha Hesabu 3:14-15 kinasema "Kisha Bwana akanena na Musa huko katika bara ya Sinai, na kumwambia, Uwahesabu wana wa Lawi kwa kuandama nyumba za baba zao na jamaa zao; kila mtu mume tangu umri wa mwezi mmoja na zaidi utawahesabu."

Maandiko yanayoeleza juu ya kuhesabiwa kwa wana wa Israel ni mengi na unaweza kuyasoma baadae ktk (Kutoka 12:37, Waamuzi 20:14, 1 Samweli 11:8, Ezra 2:64).
Kwa hiyo kuhesabiwa ni agizo la Mungu na utamaduni huu wa wana wa Israel kurudi kwao kwenda kuhesabiwa ni utamaduni uliokua maagizo ya Mungu mwenyewe (Jehovah).
Sasa je ikiwa Wachagga hawaendi kuhesabiwa iweje wafananishwe na WaIsrael?
Sababu mbili hufanya wachagga kufananishwa na utamaduni huu wa Israel wa kuhesabiwa.
SABABU YA KWANZA ni kitendo cha wachagga kurudi kwao mwishoni mwa mwaka (December) na kukaa huko hadi mwanzoni mwa mwaka mpya (January). Ikumbukwe wana wa Israel nao huenda kwao mwishoni mwa mwaka wa Kiyahudi (Adar Beit) na kurejea mwanzoni mwa mwaka mpya (Nissan). Ufanano huu wa majira hufanya wachagga nao waonekane kuwa wanaenda "kuhesabiwa" kama waIsrael.

SABABU YA PILI ni mtawanyiko wa jamii hizi mbili. Wana wa Israel wametawanyika ktk mataifa mbalimbali duniani. Kutokana na ufinyu wa nchi yao wamejikuta wakisambaa nchi mbalimbali ambapo wanaishi na kufanya kazi huko. Wengine ni wahandisi, madaktari, majemadari wa vita etc. Wana wa Israel wametawanyika mataifa yote ya Ulaya, America na baadhi ya nchi za Asia na Afrika. Pamoja na kutawanyika huku lakini mwisho wa mwaka hukumbuka kurudi kwao.
Kwa upande wa wachagga nao wametawanyika sana ktk mikoa mbalimbali nchini. Mtawanyiko wao unafananishwa na ule wa wana wa Israel kwa sababu mbili. Kwanza eneo lao la makazi (Kilimanjaro) ni dogo na haliwatoshi, sawa na Israel ilivyo ndogo na isivyotosha watu wake. Pili ni "nature" ya mtawanyiko wao. Wachagga kama Waisrael wametawanyika sehemu mbalimbali za nchi na hata nje ya nchi.

Hakuna mkoa au Wilaya yeyote unaweza kwenda nchini ukamkosa Mchagga. Wametapakaa kila kona ya nchi wakifanya shughuli mbalimbali hususani biashara. Mtu mmoja aliwahi kutania kuwa "ukienda eneo la nchi hii ukakosa Mchagga ondoka haraka maana hapafai kuishi".. Hii ina maanisha Wachagga wanaweza kuishi ktk mazingira yoyote na hali yoyote.

Mtawanyiko wa Wachagga ktk maeneo mbalimbali ya nchi hufananishwa na mtawanyiko wa Waisrael ktk maeneo mbalimbali ya dunia, na hivyo basi kitendo cha Wachagga kurudi kwao mwishoni mwa mwaka hufananishwa na kitendo cha Waisrael kurudi kwao mwishoni mwa mwaka wa kalenda ya kiyahudi. Tofauti ni kuwa Waisrael huenda kuhesabiwa lakini Wachagga hawaendi kuhesabiwa.
KAMA WACHAGGA HAWAHESABIWI, WANAENDA KUFANYA NINI?
Pengine hili ndio swali la msingi ambalo wengi wanajiuliza. Ikiwa wachagga hawaendi kuhesabiwa kama ilivyo kwa waisrael, Je wanaenda kufanya nini?

Ukweli ni kwamba Wachagga wanakwenda kwao kwa sababu mbalimbali. Leo nitaainisha kwa uchache sababu 10 zinazorudisha wachagga kwao kila mwisho wa mwaka. Zipo nyingi zaidi ila kwa kifupi ni kama ifuatavyo;
1. Kuna wanaokwenda kwao kwa ajili ya kuonana na familia zao na kuwaona wapendwa wao na kujumuika nao kwa ajili ya kufurahia sikukuu za mwisho wa Mwaka huhusani "Krismasi" na "Mwaka mpya".

Kwa mfano wazazi wako (baba na mama) au ndugu zako wengine (babu, bibi, kaka, dada, shangazi, wajomba etc) hujawaona kwa kipindi cha mwaka mzima. Mmekuwa mkiwasiliana tu kwa simu. Hivyo basi December huwa ni kipindi kizuri cha kurudi nyumbani na kuwaona na kuwajulia hali.

2. Pia kipindi hiki hutumika kupanga mipango ya maendeleo ya familia kama vile kujenga. Kwa kuwa watoto wote wa familia hukutana kipindi hiki basi huweka mipango ya maendeleo kwa familia yao. Wanaweza kupanga kujenga nyumba kwa ajili ya wazazi wao ambao ni wazee, kuweka umeme, maji etc.
Uchaggani ni mojawapo ya maeneo nchini ambako kuna nyumba nyingi za kisasa vijijini na ni mkoa uliofanikiwa kupiga vita nyumba ya Nyasi tangu mwaka 1996.
Ni jambo la Kawaida kukutana na maghorofa ya kisasa kule "Machame Uswaa, Kibosho Kirima, au Mamba Komakundi".. au ukipita "Uru Mawela, Rombo Mamsera au Kilema Poffo" nyumba zote unazokutana nazo ni self-contzined za kisasa, lakini wanaishi wazee. Watoto wao wapo Shinyanga, Dar, Kigoma, Mwanza etc wanatafuta maisha. Mipango hiyo ya kujenga na kuhudumia wazazi hupangwa msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

3. Msimu huu wa sikukuu hutumika kupatanisha ndugu, jamaa au marafiki waliokosana. Wazee huitwa na kuzungumza na pande zote mbili kisha kuwapatanisha. Mkikubali kuelewana basi huchinjwa mbuzi kama ishara ya furaha ambapo jamii yote hujumuika kwa kula na kunywa.

4. Kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ndio kipindi kizuri ambacho vijana hukitumia kutambulisha wachumba zao nyumbani. Unaweza kuwa unaishi Dar na umepata mchumba wa Morogoro. Lakini ndugu zako wametawanyika. Wengine wapo Tabora, wengine Mwanza, wengine Mbeya. Huwezi kupita na mchumba wako kote huko kumtambulisha. Kwahiyo "option" nzuri ni kusubiri msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka ambapo ndugu zako wote watakuwepo nyumbani ndipo umpeleke mchumba wako kumtambulisha, na kupanga mipango ya ndoa.

5. Kuwaleta watoto wafahamu ndugu zao na wafahamike nyumbani. Unaweza kuwa unaishi Dar na familia lakini ndugu zako wanaishi na familia zao maeneo mengine ya nchi, watoto wenu hawafahamiani maana hawajawahi kuonana. Hivyo mkikutana nyumbani msimu wa sikukuu ni kipindi kizuri cha watoto wenu kufahamiana na kufahamu asili yao.
Pia ikiwa umejaliwa mtoto ukiwa huko unakofanyia shughuli zako lakini wazazi wako hawajamuona mjukuu wao, hiki ni kipindi kizuri cha kuwapelekea wazazi wako mjukuu wao wamuone na kumpa baraka.

6. Kushiriki shughuli za kijamii (charity work). Wachagga wengi ni waumini wazuri sana wa dini iwe ukristo au uislamu. Hivyo kipindi cha msimu wa sikukuu hutenga muda wa kutembelea wagonjwa, Yatima na Wasiojiweza na kuwapa misaada mbalimbali. Kwa wale Wakristo huita "sadaka ya Epifania".

7. Kipindi hiki hutumika pia kufanya usafi na kurekebisha maeneo waliyopumzika wapendwa wetu (makaburi). Wachagga kama ilivyo binadamu wengine hutenga maeneo maalumu ya kuzikia ndugu zao; na mara nyingi kila familia ina eneo lake.

Kwa hiyo ikiwa kuna ndugu amefariki na akazikwa basi msimu huu huwa ni kipindi kizuri cha kujengea makaburi kama kumbukumbu ya sehemu walipopumzika wenzetu.
Bahati mbaya wapo watu wanaohusisha utamaduni huu na matambiko. Kwanza ieleweke kujengea makaburi si dhambi na si matambiko. Hata Yakobo alipofia kule Misri alipoenda kwa mwanae Yusufu alizikwa kwenye Kaburi lililojengewa (Matendo 7:15-16). Hivyo basi ni vizuri ikaeleweka kuwa kujengea makaburi si dhambi.

Na mara nyingi uchaggani kabla ya kujengea Kaburi kiongozi wa dini huitwa na kufanya sala, kabla ya shughuli ya ujenzi haijaanza. Kwahiyo hakuna nafasi ya matambiko.
Ikiwa kuna mchagga anafanya matambiko wakati wa kujengea makaburi ichukuliwe kuwa ni tabia ya mtu binafsi na isihuhishwe wachagga wote. Kwani wapo watu wa makabila mengine hufanya matambiko pia lakini huwezi kusema jamii yote hutambika.
8. Msimu huu wa sikukuu ni kipindi kizuri ambacho wachagga hukitumia kupanga na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ya jamii yao kama vile mashule, hospitali, Maji, barabara n.k
Kwa mfano zipo barabara nyingi ambazo zimejengwa kwa nguvu ya wananchi wenyewe kwa kuamua kujichangisha bila kusubiri serikali ifanye. Barabara ya Uru Kusini ni mojawapo. Mipango hii hupangwa msimu huu wa sikukuu.

9. Msimu huu hutumika kwa ajili ya mapumziko ya familia baada ya mahangaiko ya mwaka mzima. Ni wakati wa familia kutulia pamoja kutafakari mipango ya mwaka uliopita na kuweka mipango mipya ya mwaka unaofuata.
Ndugu na jamaa hukutana pamoja na kufurahia sikukuu za "Krismasi" na "mwaka mpya" kwa kula na kunywa hasa vyakula vya asili kama "kisusio, faya, supu ya mbuzi iliyopikwa kiasili kwa kuchanganywa na majani aina ya "mahombo" na vyakula vingine bila kusahau kinywaji aina ya mbege.

10. Kipindi hiki hutumiwa kujenga na kukarabati nyumba za ibada. Ni wazi kuwa Kilimanjaro ni miongoni mwa maeneo ambayo kuna nyumba nzuri na za kisasa za Ibada.
Kanisa kubwa na la kisasa kama la KKKT Old-Moshi Rau, au La RC Kristu Mfalme, Au TAG Kilimanjaro Revival, au Msikiti wa kisasa kama wa Riadha, ni nadra kuvipata mahali pengine. Au Kanisa la kale kama la KKKT Old-Moshi Kidia lililojengwa mwaka 1843 utalipata wapi kwingine?
Mipango ya ujenzi wa nyumba hizi za ibada za kisasa na kukarabati zile za zamani hufanywa msimu huu wa sikukuu.

Pia wachagga wengi hupenda kwenda kwao kwa kuwa ibada zote ktk msimu huu huongozwa kwa kichagga. Yani kuanzia usomaji wa misa, mahubiri hadi nyimbo huimbwa kwa kichagga, wakati huo nyumba za ibada zimepambwa kwa mapambo ya asili kama "Makurera, makangachi, migomba imechimbiwa vichumini (njia za kwenda nyumbani)" etc.

Hii huongeza nakshi na kufanya mtu ajisikie kupungukiwa kitu ikiwa hatakuwepo Nyumbani msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

NB: Utamaduni huu wa Wachagga ni mzuri sana, na kuna mengi jamii nyingine zinaweza kujifunza kupitia Wachagga kama ambavyo wachagga wanaweza kujifunza kupitia jamii nyingine.
Tuukatae uzungu, tujivunie vya kwetu. Jivunie usukuma wako, jivunie Usambaa wako, jivunie Unyakyusa wako, jivunie Umasai wako, Jivunie Ungoni wako, najivunia Uchagga wangu. SI KOSA kujivunia kabila lako lakini NI KOSA kutumia kabila lako kumbagua mtu wa kabila jingine.

Henry Kilewo

HII ni Moja ya Zawadi Alizopewa Samatta Siku ya Birthday

$
0
0
Leo ni siku ambayo Mbwana Samatta anasherekea siku yake ya kuzaliwa na watu wengi wakiwemo mashabiki zake wamemuonyesha love kumtakia maisha mema na mafanikio kwenye safari yake ya soka.

Kama ilivyo desturi ya watu kupewa zawadi mbalimbali siku ya birthday zao basi imekua hivyo hivyo kwa Sama Goal. Akiwa kwenye muendelezo wa safari ya kuelekea kwenye mafanikio ya soka lazima mtu kama Samatta anahitaji inspiration ya wachezaji wakubwa waliofanikiwa kwenye soka.

Zawadi aliyopewa ya kitabu cha nguli Pirlo ni zawadi muhimu sana. Kitabu hicho ambacho kinaitwa “I Think Therefore I Play” kinaelezea maisha ya Pirlo aliyopitia hadi kufika alipofika leo. Maamuzi ya busara na makosa aliyofanya kwenye maisha yake ya soka yote kazungumzia humo.

Kwa mchezaji kama Sama Goal ambae safari yake kwenye soka la Ulaya bado changa kitampa muongozo mzuri wa kufanya maamuzi sahihi kama Pirlo au kutofanya makosa ambayo Pirlo amefanya.

Moja ya sehemu Pirlo amezungumza ni kuhusu sehemu ya maisha yake ya kisoka ambapo alisema hivi,“Sikubali kujipa pressure, natumia muda wa mapumziko kwa kulala au kucheza Playstation, nikacheza na baadae nikashinda kombe la dunia”. Hii ni sehemu ndogo ya life style ya Pirlo alivyoelezea kwenye kitabu hiki.

Happy born day Sama Goal, all the best achieve zaidi ya Pirlo.

MWASITI Anyang'anywa Benzi Alilokuwa Akiendesha, Mwenyewe Azungumza

$
0
0
Msanii mkali toka THT Mwasiti Almasi yasemekana amenyang'anywa Benz alilokuwa akitamba nalo hapa mjini baada ya kutoonekana nalo kwa muda
Akihojiwa kuhusu swala hilo amesema yeye huwa haongelei maswala yake binafsi ila baada ya kubanwa sana akasema aliyemhonga amelichukua

 VIDEO:

Nay wa Mitego Aonyesha Thamani ya Mama yake Mzazi.....Amzawadia Zawadi Hii

$
0
0
Rapa Nay wa Mitego ambaye sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya 'Sijiwezi' ameamua kumnunulia mama yake mzazi gari katika siku yake ya kuzaliwa kama zawadi ili iwe inamsaidia mzazi wake huyo na mtoto wake wa kiume kwenda sokoni.

Nay wa Mitego akiongea kwenye kipindi cha eNewz amedai mwezi uliopita ndiyo ilikuwa siku ya kuzaliwa kwa mama yake lakini yeye hakuwepo hivyo aliweza kumpa zawadi za kawaida na sasa amerudi ameona ni bora amnunulie gari.

“Yeah ni kweli nimemnunulia mama yangu gari aina ya Porte japo bado hajaiona gari hiyo rasmi lakini ipo tayari kuna baadhi ya vitu namalizia then nitamkabidhi gari hiyo aina ya Porte mama yangu amekuwa akinisaidia sana na kama unavyojua mama yangu huwa ndiye anayekaa na watoto wangu muda mwingi nimeona hata nikimpa zawadi hii itakuwa inamsaidia na kurahisisha maswala ya usafiri"

Kuhusu kuchelewa kutoa zawadi hiyo, "Unajua mama yangu alizaliwa mwezi uliopita na mimi sikuwepo nilimpa baadhi ya zawadi lakini baada ya kurudi saizi nimeona nimnunulie gari kama zawadi yangu kwake ni zawadi ndogo ila kwa sasa nadhani ni kitu kikubwa kwake ila panapo majaliwa tutafanya kikubwa zaidi"

Polisi Yanasa 200 Kwa Ujambazi Dar

$
0
0
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 200 wanaohusishwa na makosa mbalimbali.

Wanne kati ya hao, wanatuhumiwa kukutwa na gari lililoibwa hivi karibuni katika eneo la ofisi za Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania (TIRA) zilizopo Manispaa ya Ilala.

Mkuu wa Operesheni Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya, alitaja watu hao wanne wanaotuhumiwa kukutwa na gari hilo kuwa ni Leonard Said, Omary Said, Shomaly Kilobo na Adam Unemba.

Alisema katika uchunguzi wa awali, watuhumiwa wote wamekiri kuhusika katika wizi wa gari hilo, aina ya Toyota Spacio lenye namba za usajili T 398 CAE, boksi la chuma la kutunzia fedha na televisheni ya ukubwa wa inchi 32.

Alisema Desemba 5, mwaka huu alipokea taarifa kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa TIRA, Egnance Edward (53) kuwa wamekuta ofisi za mamlaka hiyo, zimevunjwa na kuibwa baadhi ya vifaa ikiwemo gari hilo.

SERIKALI Yapiga Marufuku Shule Binafsi Kufanya Mitihani ya Kuchuja Wanafunzi

$
0
0

Hiyo ni baada ya kutangaza kupiga marufuku utaratibu wa kuwachuja wanafunzi wanaotakiwa kufanya mitihani ya taifa uliokuwa unaofanywa na baadhi yao kwa lengo la kuonekana shule zao zinafaulisha vizuri.

Hivi karibuni, Nipashe iliripoti kuhusu hofu ya baadhi ya shule hizo; za msingi na sekondari ziko hatarini kubadilishwa matumizi kutokana na kukosa wanafunzi wa kutosha baada ya Serikali kuboresha shule zake na kutoa elimu bure, huku hali ya kiuchumi ikiwaumiza wananchi.

Huku udahili kwenye shule za serikali ukiongezeka na kuonekana kuwa tishio kwa ustawi wa shule za watu na taasisi binafsi, imewabana tena wamiliki wa shule binafsi kwa kuwazuia kufanya mchujo wa wanafunzi wanaoingia kwenye madarasa au vidato vyenye mitihani ya taifa.

Mmoja wa wazazi aliliambia Nipashe kuwa mwanawe anayesoma kidato cha tatu katika shule moja ya binafsi jijini Dar es Salaam, amepangiwa kuhamishiwa shule nyingine ya mmiliki huyo huyo kutokana na kufaulu kwa daraja la tatu.

Kwa mujibu wa mzazi huyo, kuna wanafunzi takribani 70 wa kidato cha tatu, wanatarajiwa kuhamishwa katika shule hiyo waliyosajiliwa tangu kidato cha kwanza, watahamishwa shule hiyo na kubaki wale waliofaulu kwa viwango vya madaraja ya kwanza na pili tu.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo, akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam juzi, alisema ni marufuku shule kumkaririsha darasa, kumfukuza, kumhamishia shule nyingine au kumsajili kama mtahiniwa binafsi (PC) mwanafunzi kwa kigezo cha kutofanya vizuri katika mitihani ya shule husika.

"Ni marufuku kabisa kufanya hivyo. Mitihani tulionayo sisi (Wizara ya Elimu) ndiyo mchujo sahihi. Na mtihani ambao unamkaririsha mwanafunzi ni mtihani wa taifa wa kidato cha pili na mtihani wa darasa la nne tu," alisema.

"Wala siyo mtihani wa shule na madarasa mengine hayana mtihani wa kumkaririsha mtoto au kumfanya aondolewe shuleni au ahamishiwe shule nyingine, hatuna utaratibu huo na serikali haiwezi kukubaliana nao," aliongeza Dk. Akwilapo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tamongosco), Benjamin Nkonye, aliiambia Nipashe jana kuwa utaratibu wanaoutumia ni kushauriana na wazazi wa wanafunzi wanaoshindwa kufanya vizuri shuleni ikiwamo kuwapeleka katika vyuo vya ufundi (Veta).

Alisema shule binafsi zinapaswa kupongezwa kwa kudahili hata wanafunzi hasa wa sekondari ambao shule za serikali huwa haziwachukui kutokana na kushindwa kufanya vizuri katika mitihani ya shule za msingi.

“Hakuna shule ambazo zinapaswa kupongezwa kama za binafsi, serikali yenyewe imekuwa ikichagua wanafunzi wote. Inatuachia ‘vilaza’, lakini sisi kwa kujitoa kuwasaidia watoto wa Kitanzania, tunakubali kuwachukua hao hao wanaoonekana wabaya, tunawafundisha na mwisho wa siku wanakuwa wazuri kuliko hata hao wanaokuwa wamethaminiwa na serikali,” alisema Nkonya.

“Na sisi hatuchuji wala kumfukuza mwanafunzi, isipokuwa kinachofanyika kwa kuwa tunapokea wakati mwingine wanafunzi ambao ni ‘vilaza’ kabisa, huwa tunawagawanya katika makundi kulingana na uelewa wao, wenye uelewa wa kwanza, wa kati na wa mwisho. Na mwisho na tunawafundisha kulingana na ‘speed’ (kasi) ya uelewa wao na wanajikuta wanafanya vizuri.

“Lakini kwa sababu sisi tunakuwa na wanafunzi ambao ni wagumu sana, inapoonekana wakatokea wachache hawawezi kabisa huwa tunashauriana na wazazi wao, kuwapeleka Veta ili kule wanapokuwa wanaendelea kujifunza, wengine wanafanya vizuri hadi wanafika vyuo vikuu, hatuwaachi kama ilivyo katika shule za serikali na vyuo vya serikali, haya maneno mengine yanayozungumzwa ni ya kisiasa tu."

HALI ILIVYO

Uchunguzi wa Nipashe uliofanyika hivi karibuni katika baadhi ya mikoa, ulibaini baadhi ya wamiliki wa shule binafsi wamekuwa na utaratibu wa kuchuja wanafunzi kila mwaka kwa lengo la kupata wenye uwezo mkubwa darasani.

Ilibainika kuwa utaratibu huo umekuwa ukifanywa kwa nia ya kuwa na wanafunzi wenye uwezo mkubwa ili shule hizo zifanye vizuri katika mitihani ya taifa, hivyo kuvutia wazazi wengi zaidi kupeleka watoto wao.

Gazeti hili lilibaini kuwa, baadhi ya shule binafsi zimekuwa zikiendesha utaratibu huo kipindi cha mitihani ya mwishoni mwa mwaka kwa kuwafukuza, kuwakaririsha darasa au kuwahamishia shule nyingine wanafunzi wanaoshindwa kufikia kiwango kinachowekwa na shule husika kwenye mitihani ya kufunga mwaka.

Nipashe pia ilibaini baadhi ya shule hizo zimekuwa na utaratibu wa kuwachuja kwa kuwasajili kama watahiniwa binafsi (Private Candidates) kwenye mitihani ya taifa wanafunzi wake wanaoshindwa kiwango kilichowekwa wanapofanya mitihani ya shule husika.

MTOTO WA PROFESA AKACHA KULA

Akizungumzia suala hilo katika mahojiano maalumu na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Masomo ya Shahada ya Kwanza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Allen Mushi, alisema haungi mkono utaratibu wa baadhi ya shule binafsi kuwafukuza wanafunzi wanaoshindwa kufikia kiwango cha alama zilizojiwekea.

Alisema: "Ni makosa kumfukuza shule mwanafunzi aliyekuwa amedahiliwa, anasoma halafu unamsitishia, unamwambia nenda katafute shule nyingine.

"Na ni kweli wana tabia hiyo. “Nina kijana wangu yuko ‘Form One’ (Kidato cha Kwanza) anasoma shule ... (anataja eneo ilipo shule hiyo), yaani anasoma kupindukia. Nilikuwa na wasiwasi hata akija likizo hawezi kula vizuri, anasoma tu."

Alisema kuwa katika shule hiyo ya jijini Dar es Salaam anayosoma mtoto wake, wameambiwa ni lazima awe na wastani wa kuanzia alama 50 katika mitihani ya shule ili aruhusiwe kuingia kidato kinachofuata, vinginevyo wakatafute shule nyingine.

"Katika utaratibu wa elimu, siyo sahihi kufanya hivyo, wewe kama wanafunzi wameshindwa, wewe siyo ndiyo mwalimu, ndiyo kazi yako ya kufanya wanafunzi waelewe," alisema na kufafanua zaidi:

“Sasa ukiwa unafanya hivyo, mwisho wa siku utakuwa unafelisha darasa zima na kujitamba kwamba unafaulisha kwa sababu umefukuza wengi na kubaki na wazuri wachache. Sasa hiyo ni biashara, siyo elimu tena. Wewe kama ni mwalimu, unatakiwa kufundisha wanafunzi wote.

“Kwa hiyo, wanasema shule za ‘private’ (binafsi) zinafaulisha wanafunzi wote, kumbe wengine mliowachuja. Mimi binafsi sikubaliani na hali hiyo kabisa."

Alisema ni muhimu wizara yenye dhamana ya elimu nchini iweke masharti kwamba ukishadahili wanafunzi, wasiondolewe shuleni kwa utaratibu wa viwango vya ufaulu katika mitihani ya shule husika isipokuwa kwa sababu za tabia mbaya na zisizofaa kwa mwanafunzi kwa mujibu wa sheria za nchi.

MAKUNDI YA UELEWA

Msomi huyo alisema wanafunzi wamegawanyika katika madaraja mawili kiuelewa darasani, la kwanza likiwa la wenye uelewa wa haraka (fast learners) na jingine likiwa la wenye uelewa hafifu (‘slow learners).

"Wote hao wanapaswa wazingatiwe katika elimu. Sasa hawa (shule binafsi) wenyewe wanaangalia 'fast learners' tu. Ni vema wote wakachukuliwa katika vigezo sawa, siyo unawachuja wengine halafu unasema unafaulisha wote," alisema Prof. Mushi.

BIASHARA

Aliyekuwa Rais wa Chama cha Walimu (CWT), Gratian Mukoba, akizungumza na Nipashe jana kuhusu changamoto hiyo, alisema si vyema kumfukuza, kumkaririsha darasa au kumhamisha mwanafunzi aliyefanya vibaya katika mitihani ya shule.

"Mtihani wa Kidato cha Pili ni mchujo sahihi tu. Shule binafsi wanakosea. Ufundishaji wa kawaida huwezi kuwa na wanafunzi wanaopata daraja la kwanza na la pili tu," alisema.

"Hao shule binafsi kuna muda wanateleza kidogo, kwa sababu hakuna mwanafunzi asiyefundishika labda kwa sababu wao wanataka suala la biashara. Ni kuonea wanafunzi, bahati mbaya akishaanza shule ya 'private' (binafsi) kidato cha kwanza, hawezi kurudi kwenye mfumo wa serikali, kwa hiyo wanafunzi wanahangaika," alisema zaidi Mukoba.

BABU Tale...Nimemsaidia Chid Benz ila Nikashindwa Kabisa Bado Hajaacha Madawa ya Kulevya

$
0
0
Jana  team nzima ya WCB Wasafi na team ya XXL walikuwa pande za limani City jijini Dar es Salaam kwenye tukio zima la kuuza tiketi kwaajili ya show ya leo pande za Jangwani Sea Breez kwenye Wasafi Beach Party.

Wakali hao waliweza kukutana na mashabiki zao ana kwa ana na kuruhusu maswali mawili matatu kutoka kwa mashabiki. Mmoja kati ya watu ambao walipokea maswali kutoka kwa mashabiki ni pamoja na meneja wa Diamond Platnumz mtu mzima Babu Tale.

Swali ambalo aliulizwa meneja huyo ilikuwa ni kuhusu rapper Chidi Benzi ambaye tetesi za kitaa zinasema amerudi tena kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya ikiwa hapo awali meneja huyo allisikika kujitolea kumsaidia rapper huyo.


“Chidi Benz nimemsaidia kwasababu mimi ni mtoto wa kiume na nimezaa watoto wa kiume, lakini wanasemaga sikio la kufa halisikii dawa. Mimi nimemsaidia lakini ikafika wakati nikashindwa kwasababu niliona mtu ndio vile vile hajaacha ikanibidi nikae pembeni.”

Hayo ni baadhi tu kati ya mengi ambayo Babu Tale amefunguka kuhusiana na Chidi Benz. Unaweza kumsikiliza yeye mwenyewe akifunguka mwanzo hadi mwisho kwa kuplay hii video hapa chini.

MBOWE Aeleza kwa nini Amekuwa Kimya Kupotea kwa Ben Saanane

$
0
0

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema amekuwa kimya muda mrefu kuhusiana na kupotea katika mazingira ya kutatanisha, msaidizi wake Ben Saanane kwa kuwa suala hilo lipo kwenye uchunguzi. 


Mbowe alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya wakati wa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho Kanda ya Nyasa inayojumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe na Rukwa. 


Alisema yeye pia ameathiriwa na tukio hilo kama ilivyo kwa wazazi wake na ndugu wengine kwa kuwa ni mtu muhimu kwake katika kutekeleza majukumu yake. 


“Ndugu zangu Watanzania msione nipo kimya, nimefanya hivi kutokana na kuwa suala hili lipo kwenye uchunguzi kwani tukizidisha kuongea ongea wale ambao wamemteka wanaweza kupoteza uhai wake kisa maneno,” alisema Mbowe. 


Alisema, “Chadema ni taasisi ambayo ina vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vinaendelea kuchunguza tukio hili la aina yake.” 


Katika hatua nyingine, Mbowe aliishitumu Serikali akidai kwamba imeendelea kuwafunga wanachama wake na kwamba mpaka sasa 180 wapo mahabusu. Alisema hizo ni jitihada za kuua nguvu za upinzani. 


Akijibu madai hayo, Kamishna wa Polisi (Operesheni na Mafunzo), Nsato Marijani alisema jeshi hilo linawashikilia watu wengi kwa makosa mbalimbali vituoni na wengine mahabusu katika magereza. Alisema polisi haimkamati mfuasi wa chama cha siasa bali mtu anayekwenda kinyume cha sheria. 


“Hayo yanayosemwa siyo ya kweli, waache kulipaka tope jeshi la polisi. Tutaendelea kuwakamata watu wote wanaovunja sheria. Hata kama akiwa mjomba wangu tutamkamata.” 


Msigwa kidedea 

Katika uchaguzi huo, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliibuka kidedea baada ya kushinda kwa kupata kura za ndiyo 62 sawa na asilimia 58.49 kati ya kura 106 zilizopigwa. 


Akitangaza matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika alisema nafasi ya makamu mwenyekiti imechukuliwa na Sadrick Malila ambaye alipata kura za ndiyo 93 sawa na asilimia 88 ya kura zilizopigwa 106 huku kura tatu zikiharibika. 

Mnyika alisema kuwa nafasi ya  mweka hazina imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Sophia Mwakagenda ambaye alishinda kwa kupata kura 91 ambayo ni sawa na asilimia 86 kura zote 106 zilizopigwa. 


Mnyika alisema katika uchaguzi huo wajumbe walipiga kura za ndiyo au hapana kwa lengo la kufanya uchaguzi wa maridhiano kwani uchaguzi wa kuweka wagombea wawili husababisha makundi na kuleta migogoro ndani ya chama. 


“Hivyo Kamati Kuu Taifa baada ya kuliona hilo tukaamua kuwaita wagombea wote na kuwaeleza nia yetu ya kufanya hivyo na hatujafanya huku tu, hata kanda nyingine tulizopita tumefanya hivyo"Alisema Mnyika

WIZARA ya Elimu yatoa ufafanuzi kuhusu ajira za Walimu

$
0
0
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imesema haihusiki na utoaji wa ajira za walimu nchini, isipokuwa inachokifanya ni uhakiki wa taarifa za walimu wenye sifa za kuajiriwa serikalini.

Akizungumza nakituo cha  EATV leo, Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa kwa sasa wizara hiyo inapitia taarifa (CV) za walimu waliohitimu ngazi ya Stashada na Stashahada, na baada ya hapo itazituma taarifa hizo katika Wizara ya Utumishi ambao ndiyo wanaohusika na kuajiri.

Akizungumzia sababu za kuwatenga wahitimu wa ngazi ya cheti, Manyanya amesema uhitaji mkubwa uliopo kwa sasa ni kwa walimu wa sekondari hususani wa masomo ya Phisics, Hisabati, Chemistry na Biolojia, hivyo inawahitaji kwa haraka zaidi walimu hao huku akisema wahitimu wengine ambao siyo wa masomo hayo na ambao siyo kwa ajili ya kufundisha sekondari, wasubiri utaratibu wa wizara inayohusika na utumishi.

"Siyo kwamba hatuhitaji walimu wa shule za msingi, lakini uhitaji mkubwa tulionao kwa sasa ni walimu wa sekondari, sisi hatuajiri, sisi tunafanya uhakiki, na sasa tunapitia CV za wahitimu waliotuma taarifa zao, tukishajiridhisha na wale ambao taarifa zao ni sahihi na wana sifa tunazohitaji, tunazipeleka Utumishi, hao ndiyo wataajiri, halafu majina yatapelekwa TAMISEMI kwa ajili ya kupangiwa maeneo ya kazi" Amesema Manyanya

Kuhusu idadi ya walimu wanaohitajika haraka, Manyanya amesema, wanahitajika walimu wengi kuliko idadi waliyoitoa mwanzo, na kuwataka wote waliotuma taarifa zao wawe na subira kwa kuwa mchako wa uhakiki bado unaendelea na majina yatatangazwa muda mfupi ujao ambao hautazidi kipindi cha miezi mitatu.

BEN Pol Ametaja Kiwango cha Pesa Utachotakiwa Kumlipa ili Upate Collabo yake

$
0
0
Inawezekana kabisa star wa BongoFlava na R&B, Ben Pol amegundua kwamba nyimbo nyingi anazoshirikiswa na wasanii wenzake zimekuwa zikiwapa mafanikio makubwa pamoja na kuwaingizia fedha za kutosha.

Kupitia Twitter, Ben Pol ametaja kiwango cha pesa ambacho msanii atatakiwa kumlipa ili apate collobo yake.

Ben Pol amesema kama kuna msanii anayehitaji kufanya naye kwazi kwasasa inabidi ahakikishe anamalizana naye kabla ya December 31, 2016 kwasababu kuanzia mwaka 2017 ili kufanya kazi naye itabidi msanii alipie kiasi cha dola 5000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 10 za Tanzania.

WASICHANA 21 wa Chibok Waachiliwa Huru

$
0
0
Wasichana 21 kati ya wasichana 276 waliotekwa nyara na Boko Haram walipovamia shule mnamo 2014 .

Wasichana 21 wa Chibok waachiliwa huru

Msemaji mkuu wa rais Garba Shehu alifahamisha kwa taarifa kuwa wasichana 21 wameachiliwa huru.

Aidha taarifa pia zafahamisha kuwa watu wasiopungua 2000 wameokolewa kutoka wilaya ya Borno nchini Nigeria .

Hata hivyo wasichana walio chini ya Boko Haram bado haijulikani walipo .

MWANAUME Ongeza Ukumbwa wa Umbile (Cassava) lako Kwa Kutumia Kifaa cha Handsome Up....

$
0
0
Handsome up ni kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa uhakika na bila madhara. Inapatikana kwa @170,000/=tu. PIA kuna Gely ya kupaka @ 120,000/= na Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa @120,000/=.
Wasiliana nasi kwa no (+ 255 ) 0767447444 au
0714335378.
Follow us @Markson_beauty_pr

FARU John Huyu Hapa, Lindo lake lilikuwa Sh215,000 Kwa Kila Siku

$
0
0
Wakati Waziri Mkuu ameagiza kaburi la Faru John lifukuliwe na kuchukuliwa vipimo vya vinasaba kuthibitisha kama pembe alizopelekewa ni zake, mabaki yanayoaminika kuwa ni ya mnyama huyo (pichani) yameonekana yakiwa porini katika eneo la Grumeti, wilayani Serengeti alipofia.

Vilevile, gazeti hili limebaini kuwa kabla ya kifo chake, Faru John alikuwa analindwa kwa gharama ya Sh225,000 kila siku.

Faru John alihamishiwa Grumeti, Desemba 17, mwaka jana na kufa Agosti 18, mwaka huu katika mazingira yanayodaiwa kuwa tata.



POLE POLE: Sasa Tunafanya Mageuzi ya Makusudi CCM

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema chama hicho kimeanza kufanya mageuzi ya makusudi ili kurejea kwenye misingi ya kuanzishwa kwake.

Katibu huyo mpya wa itikadi na uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, amesema mageuzi hayo yanakusudia kukifanya kuwa cha watu, kuwasikiliza na kusimamia masilahi ya wanyonge ili kurejesha imani kwao katika vitendo vyote vya chama.

Polepole alisema hayo jana katika mahojiano na kituo cha redio cha Uhuru FM kinachomilikiwa na chama hicho tawala.

MAPENZO yangu na Jacqueline Wolper yapo Moyoni – Harmonize

$
0
0
Msanii wa muziki kutoka WCB, Harmonize amekanusha kuachana na mpenzi wake Jacqueline Wolper baada ya hivi karibuni kuzagaa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wameachana.

Madai hayo yalichukua sura mpya wiki chache zilizopita baada ya malkia huyo wa filamu kudaiwa kufuta picha za mkali huo wa wimbo Bado katika mtandao wake wa instagram.

Akiongea jana katika kipindi cha XXL cha Clouds FM, Harmonize alidai mapenzi yao yapo moyoni na watu wasichanganywe na issue ya kufuta picha instagram.

“Wolper alifuta tu picha za instagram hakufuta mapenzi yetu yapo moyoni,” alisema Harmonize.

Pia muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Matatizo, alidai suala la malkia huyo kufuta picha instagram ni kawaida kwani anaweza kufuta na kuanza kupost mpya.

Wapenzi hao wamebadili utaratibu wa maisha yao kwani huko nyuma walikuwa wanasafiri na kula bata pamoja.

BILA Tume Huru Wapinzani Wasahau Kuingia Ikulu – Kingunge

$
0
0
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru amesema bila ya kuwa na tume huru ya uchaguzi na katiba mpya, vyama vya upinzani visahau kushinda urais katika uchaguzi mkuu ujao.



Kauli ya mwanasiasa huyo mkongwe imekuja siku moja baada Rais John Magufuli kumteua Jaji Themistocles Kaijage kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya Jaji Damian Lubuva kufikia muda wake wa kustaafu.

Kwa muda mrefu, NEC imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya upinzani kwa kutokuwa huru kwa sababu ya uongozi wake wote huteuliwa na Rais ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, huku sheria zikikataza matokeo ya nafasi ya urais kupingwa mahakamani.

Akizungumza katika mkutano wa kuwafariji vijana waliokamatwa na Jeshi la Polisi na kushtakiwa kwa makosa yaliyohusu Uchaguzi Mkuu uliopita, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana, Kingunge aliwatia moyo vijana hao, akisema hakuna ushindi unaopatikana bila kupambana.

“Yako mambo ambayo itabidi tujitahidi yaamuliwe sasa kabla ya 2020. Mambo hayo makubwa kwanza ni tume huru (ya uchaguzi). Suala hilo lazima lizungumzwe sasa, hatuwezi kwenda 2020 na tume ya sasa na Katiba ya mwaka 1977, tukienda hivyo sahau habari ya upinzani kushinda uchaguzi,” alisema Kingunge.

“Sheria inayohusu matokeo ya uchaguzi wa Rais kuhojiwa. Hivi sasa sheria inasema matokeo ya uchaguzi wa Rais hayahojiwi mahakamani. Lazima hilo suala lipate jibu sasa. Kwa hiyo Katiba na sheria iseme, matokeo ya uchaguzi wa Rais yanaweza kuhojiwa mahakamani. Tusipokuwa na hilo, tutakuwa na matatizo makubwa sana”.

AUNTY Ezekiel afunguka kuhusu mimba yake

$
0
0
Zile tetesi za muigizaji wa filamu nchini Aunty Ezekiel ni mjamzito huenda zikawa zimetimia baada ya kuficha kwa muda mrefu.

Akiongea kwenye kipindi cha FNL cha EATV, Aunty hajaweka wazi kama ni kweli ni mjamzito ila alichokisema ni kuwa anatamani tena kupata mtoto mwingine wa kike baada ya mtoto wao wa kwanza Cookie naye kuwa wa kike.

“I wish nipate mtoto wa kike tena, watoto wa kike hela ile, yaani mpaka wajae,” amesema muigizaji huyo.

Aunty Ezekiel ameongeza kuwa hataki kuweka wazi kama ni mjamzito kwa sasa ila watu watafahamu tu kwa kuwa hata mimba yake ya kwanza aliificha lakini watu waliweza kuibaini.

UTAFITI: Mitandao ya Kijamii Inaweza Kusababisha Magonjwa ya Akili

$
0
0
Je, unapenda kufungua mitandao mbalimbali ya jamii kama Facebook, Tweeter, Instagram, Google Plus, Snapchat, LinkedIn, Youtube na mingineyo kila siku?

Kama jibu ni ndiyo, basi uko hatarini kupata tatizo la msongo wa mawazo na wasiwasi.

Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Pittsburgh cha Pennsylvania nchini Marekani mwaka 2014 na kuzinduliwa mwaka huu, unaonyesha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya mitandao ya jamii yanaweza kusababisha magonjwa ya akili, ukiwamo msongo wa mawazo na wasiwasi.

Wakati kukiwa na tatizo hilo, inakadiriwa kuwa asilimia 71 ya vijana duniani kote hutembelea mitandao tofauti ya jamii kila siku huku simu za mikononi zinazowezesha kupatikana mitandao hiyo kirahisi zikizidi kubuniwa na kuboreshwa.

Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images