Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

EDWARD Lowassa Aitaka CCM isome Alama za Nyakati

$
0
0
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ameitaka CCM iache kujidanganya kuwa haiwezi kuondoka madarakani akiitaka iangalie alama za nyakati hasa mabadiliko ya uongozi yanayotokea kwingineko duniani.

Hata hivyo, Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amesema unahitajika muungano wa dhati wa vyama na uliopangiliwa vizuri katika juhudi za kuiondoa CCM madarakani.

Lowassa alisema hayo alipoombwa na mwandishi wa habari hizi kutoa tathmini ya maisha yake ya kisiasa mwaka mmoja na nusu tangu alipojiondoa CCM na kujiunga na Chadema ambako aliteuliwa kuwa mgombea urais wa chama hicho akiwakilisha muungano wa vyama vine – Chadema, CUF, NCCR - Mageuzi na NLD – Iliopewa jina la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).



MAGARI Yakifahari Yafurika Moshi.. .

$
0
0

Mji wa Moshi umekuwa na msongamano mkubwa wa magari katika barabara kuu ya kuingia mjini kutokea Dar es Salaam.

Msongamano huo wa ongezeko la magari unalosababishwa na utamaduni wa wenyeji wa Mkoa Kilimanjaro, kurejea nyumbani kutokea mikoa mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Awali, ilitarajiwa kusingekuwapo na ongezeko hilo la wageni kwa mwaka huu, kutokana na ugumu wa maisha uliotokana na kupungua kwa mzunguko wa fedha mitaani.

Hata hivyo, juzi saa 12.00 jioni hadi saa 2.00 usiku, kuliibuka msongamano wa magari kuanzia eneo la Mbwaharuki hadi Magereza Barabara Kuu ya Dar es Salaam- Moshi.

NDEGE Yapotea Angani na Abiria 91

$
0
0

Ndege ya Jeshi la Urusi, Tu-154 iliyokuwa ikielekea Syria yapotea kwenye Rada muda mfupi baada ya kupaa. Ilikuwa na abiria 91.

Asilimia kubwa ya waliokuwa kwenye ndege hiyo ni Wafanyakazi wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi

HAJI Manara Amemmisi Jerry Muro Katika Soka...Amuombea Msamahaa TFF

$
0
0

December 25 2016 mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Club ya Simba Haji Manara alitumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi kumuomba asamehewe afisa habari mwenzake wa Yanga Jerry Muro ambaye amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka.

Kwako Rais wa TFF
Kwanza nikutakie heri na baraka ktk sikukuu hii kubwa kabisa duniani kote. Nnakuandikia ujumbe huu mfupi na wa wazi
kwako, nikiamini wewe ni mtu mwelewa na mwenye huruma na upendo, pia ni kiongozi mwenye maono ya dhati kwa maendeleo ya soka nchini,

kwa vigezo hivyo na ukizingatia leo tupo ktk sherehe ya Noeli, utalikubali ombi langu binafsi ntakalokuomba.
Nimekaa nimetafakari sana, nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, nnafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake.

Ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla,
Ninafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi binafsi, lakini yale yashapita na binafasi amenihakikishia kutorudia tena, na ninaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wanasimba,

Tunamiss rikaka zake zinazoongeza ushabiki na utani wetu wa jadi. kwangu Mh Rais nina hakika utatumia mamlaka yako kumfungulia mtani wangu Jerry, au kuziomba kamati zilizomfungia kumuachia huru,
ukizingatia Jerry sio mzoefu sana wa utamaduni wa siasa za mchezo huu murua zaidi duniani.
Mwisho nikutakie mapumziko mema ya kuelekea mwishoni mwa mwaka. Wako
HAJI MANARA

UKWELI Kuhusu Lulu Diva Kutoka Kimapenzi na Barnaba Classic

$
0
0
Mwanadada ambaye ameingia kwa kasi ya aina yake kwenye game ya bongo fleva, Lulu Diva, amevunja ukimya na kufunguka kuhusu skendo za yeye kulala chumba kimoja na msanii Barnaba Classic, walipokuwa wamekwenda kufanya video nchini Afrika Kusini.


Akifunguka kwa watanzania kupitia kipindi cha FNL cha EATV, Lulu amesema taarifa hizo siyo za kweli na kwamba anamchukulia Barnaba kama kaka yake, hivyo hawezi kumvunjia heshima kwa kuwa na mahusiano naye, wakati akijua kuwa Barnaba anaye mke wake wa ndoa.

"Barnaba na mimi tunaheshimiana sana, tulipokwenda Sauzi hatukufanya chochote, yule ni kaka yangu hata tukiwa chumba kimoja hatuwezi kabisa kufanya chochote, yule ni kaka yangu, kwahiyo taarifa hizo siyo za kweli" Alisema

Kuhusiana na mahusiano yake na mke wa Barnaba amesema wanafahamiana na wanaishi kama marafiki "Mimi na mke wake tunafahamiana na ni marafiki wa karibu sana na mambo mengine tunashauriana"

Amesema kila kitu walichokifanya kule kilikuwa ni sehemu ya kazi iliyowapeleka kule na si vinginevyo
Mbali na Barnaba, Lulu alipangua pia skendo nyingine zinazomkabili za kutoka kimapenzi na wasanii wa kiume Bongo, na wote alisema ni kaka zake.

Lulu amefanya kolabo na Barnaba na tayari ameachia video ya ngoma hiyo inayokwenda kwa jina la Milele ambayo ndani ya wiki mbili ilikuwa imefikisha views zaidi ya laki 2.

PAPA Misifa Amuwashiwa Moto Upya Mavoko

$
0
0
Meneja maarufu wa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Papaa Misifa, ameibuka na kuzidi kumuwashia moto Msanii Rich Mavoko ambaye kwa sasa anafanya kazi na lebo ya Wasafi.

Misifa akiwa ndani ya FNL alisema Mavoko hana adabu na ni miongoni mwa wasanii wasiokuwa na shukrani kwa yale aliyowafanyia kwa kuwa yeye ndiye aliyewatoa na kuwang'arisha kwenye Bongo Fleva, lakini wamemtelekeza kwa kuvunja makubaliano.

Akizungumza jinsi alivyomsaidia Rich Mavoko, amesema tangu wimbo wake wa kwanza, yeye ndiye aliyegharamia studio.

"Sitamsahau Mavoko, alinifanyia vitu vya ajabu sana, mavoko hana heshima, kuanzia Mary me, one time nilikuwa nagharamia kila kitu hata kuna pesa nilitoa kwa ajili ya video Sauz, lakini akachukua"
Alipoulizwa endapo ugomvi wake na Mavoko ulisababishwa na pesa, Papaa Misifa akaruka na kusema "Tatizo siyo pesa, hata adabu hana"


Alipoulizwa kama endapo ana mpango wa kutumia 'ndumba' kumuadhibu, Misifa alisema "Hakuna uchawi ila kuna laana, hakuna uganga wowote, lakini atapata laana"
Kuhusu kumsamehe, Misifa amesema yuko tayari kumsamehe endapo atamfuata kumuomba radhi "kesi bado ipo lakini akija tuzungumze nitamsamehe".

AUNTY Ezekiel Aziponda movie zake za zamani

$
0
0
Mrembo aliyekuwa kimya kwa muda mrefu katika uga wa Bongo Movie mwanadada Aunty Ezekiel amerudi kwa kishindo na kazi mpya ambayo imemfanya aziponde kazi zake za zamani kutokana na ubora wake.


Aunty aliyekuwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV amesema movie ambayo amekuja nayo sasa ni ya viwango vya hali ya juu, na ina utofauti na movie zote alizowahi kucheza siku za nyuma kwa kuachana na mambo ambayo anadai kuwa hayakuwa na maana kwenye movie.

Movie hiyo inayokwenda kwa jina la 'Christmas Eve' ambamo Aunty anatumia jina la Salome, inazinduliwa leo na itakuwa LIVE kupitia EATV kuanzia saa 3:00 usiku, ambapo Aunty pia ameeleza sababu za kuifanyia uzinduzi movie hiyo kuwa ni pamoja na kuwaonesha mashabiki wake utofauti wa movie hiyo na kazi zake zamani

"Tumefanya kitu tofauti, siyo kama ile ya zamani ya kwenye makochi, unaingia shikamoo baba, halafu mambo yanakuwa yaleyale, tumeona tuzindue kwa kishindo ili kuwaonesha watu utofauti" Amesema Aunty.

Katika hatua nyingine Aunty alikiri kuwa yeye ni mjamzito na kwamba hicho ni kitu ambacho hawezi kuficha wala hana sababu ya kufanya hivyo kwa kuwa ujauzito haufichiki na pia kuweka wazi kuwa sasa amebadili mtindo wake wa maisha na kuachana na mambo aliyoyaita kuwa ni ya kitoto.

TANZIA:Mwanamuziki Mkongwe wa UK, George Michael Afariki Dunia

$
0
0
Mwanamuziki mkongwe wa nchini Uingereza, George Michael amefariki dunia nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 53.

Msemaji wake amedai kuwa mwanamuziki huyo aliyeanza kujipatia umaarufu miaka ya 1980s amefariki kwa amani huko Goring, Oxfordshire.

Taarifa ya msemaji wake imesema: It is with great sadness that we can confirm our beloved son, brother and friend George passed away peacefully at home over the Christmas period. The family would ask that their privacy be respected at this difficult and emotional time. There will be no further comment at this stage.

Moja ya mastaaa waliomlilia ni Sir Elton John aliyeweka picha yake kwenye Instagram na kuandika: I am in deep shock. I have lost a beloved friend – the kindest, most generous soul and a brilliant artist. My heart goes out to his family and all of his fans.”

Michael, aliyezaliwa kwa jina la Georgios Kyriacos Panayiotou, kaskazini mwwa London, ameuza zaidi ya nakala milioni 100 katika maisha yake ya muziki.

RAIS Magufuli Atoboa Siri ya Kula Christmass Mkoani Singida

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli,amefichua siri ya kusali Krismasi kwenye kanisa la Parokia ya Moyo wa Yesu, mjini Singida mwaka huu.

Ametaja siri hiyo kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, aliwahi kusali kwenye kanisa hilo na wakati akitoka, alikutana na sista mmoja (hamkumbuki jina) ambaye alimzawadia rozali, na kumwahidi kuwa itamsadia kushinda uchaguzi huo.

Rais Magufuli ametoa siri hiyo jana  wakati akizungumza kwenye sherehe ya Krismasi iliyofanyika kwenye kanisa la Porokia ya Moyo wa Yesu, na kuhudhuriwa pia na mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli.

Akifafanua, alisema kuwa rozali hiyo amezunguka nayo kwenye kampeni yake, na mwisho wa siku, alifanikiwa kupata kura za kutosha na hivyo kuwa mshindi.

“Hiyo ndio sababu kubwa au siri ya mimi kufika mjini Singida, na kuungana na wakazi wa mkoa wa Singida na Watanzania kwa ujumla, kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu kristo,” alisema na kusababisha mamia ya waumini kushangilia kwa nguvu.

Rais Magufuli alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania wote kutumia sikukuu hii ya Krismasi kuimarisha upendo, kuvumiliana na wala wasibaguane ,na kwa njia hiyo,Tanzania itaendelea kupaa kimaendeleo.

Katika hatua nyingine, alisema kuwa Watanzania na hususani wakulima, wahakikishe wanazitumia vizuri mvua zinazonyesha kwa sasa nchini kwa kuchapa kazi ya kilimo kwa nguvu zote na kulima mazao yanayostahimili ukame.

“Ndugu zangu waumini na Watanzania kwa ujumla, acheni kulialia kuwa fedha zimepotea … fedha hazijapotea isipokuwa ninyi wenyewe hamfanyi kazi. Vitabu vyote vya madhehebu ya dini vinasisitiza wajibu wa kuchapa kazi … na vinasema asiyefanya kazi na asile,” alisisitiza.

Akiijengea nguvu hoja yake ya hapa ni kazi tu, alisema kuwa Yesu kristo amezaliwa na fundi mchapa kazi kweli kweli seremala, na hivyo tunaposherehekea Krismasi Watanzania wote wenye uwezo wa kufanya kazi, wafanye kazi huku wakijua hakuna cha bure.

Aidha, Rais Magufuli, aliwataka wakazi wa mkoa wa Singida, kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti, ili kukiwezesha kiwanda kikubwa cha kukamua mafuta ya alizeti cha Mount Meru kupata mbegu za kikudhi mahitaji ya kiwanda.

Awali askofu wa kanisa katoliki jimbo la Singida, Edward Mapunda, alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wakazi wa mkoa wa Singida, kutunza mazingira, ili yaweze kuwatunza na wao.

Alisema hivi sasa hali ni mbaya kutokana na binadamu kuongeza kasi ya kuharibu mazingira, kitendo kinachochangia madhara mengi ikiwemo uhaba wa mvua.

“Mimi nashangaa sana, watu wanaendelea kuzaa huku wakiendelea kuharibu mazingira na kutishia nchi kuwa jangwa. Tuna zaa watoto waje wateseke kutokana na uharibifu wa mazingira. Kama tunaendelea kuharibu mazingira, ni vema tuache kuzaa”, alisema Mapunda.

PICHA 15: Vodacom Wasafi Festival Ilivyofanyika Dec 25 Mkoani Iringa

$
0
0
Usiku wa Dec 25, 2016  wakali wa Bongo Fleva akiwemo Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen, Q Boy, Chege pamoja na msanii kutoka Nigeria Kcee wameandika historia katika mkoa wa Iringa.

Show hiyo iliyopewa jina la Vodacom Wasafi Festival imefanyika katika uwanja wa Samora Stadium, hizi ni baadhi ya picha kutoka mahali palipofanyika tamasha hilo.

MEYA Chadema aeleza Ubungo Aitakayo

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam, Boniface Jacob amesema kuanzia mwezi ujao wataanza  oparesheni ya kukusanya mapato yatakayokwenda kwenye miradi ya maendeleo.

Jacob alitoa kauli hiyo juzi baada ya kukakibidhi msaada wa Sikukuu ya Krismasi zenye thamani ya Sh2 milioni kwa makundi mbalimbali wakiwamo watu wasiojiweza.

Miongoni mwa zawadi hizo ni mbuzi tano, mchele kilo 200, juisi na guni la viazi.

Alisema halmashauri hiyo ni mpya na bado hawajajua mapato yanayokusanywa kwa mwezi ingawa lengo ni kufikia Sh36 bilioni kwa mwaka.


TAARIFA ya Kusikitisha Kutoka Kata ya Masanze Jimbo la Mikumi.

$
0
0
OFISI YA MBUNGE Jimbo La Mikumi inalaani sana kitendo cha kinyama kilichofanywa na Ndugu zetu wa jamii ya wafugaji kwa kujichukulia sheria mkononi na kumjeruhi vibaya Ndugu Augustino Mtitu mkulima wa kitongoji cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata Ya Masanze Jimbo la Mikumi ambapo leo tarehe 25 Desemba majira ya Mchana amechomwa mkuki mdomoni na kutokezea nyuma ya shingo yake, ambapo alipelekwa hospitali ya wilayani Kilosa na baadae amekimbizwa hospitali ya mkoa Morogoro  ili kufanyiwa operesheni ya kuondoa mkuki huo na kwa matibabu zaidi.

Augustino Mtitu alishambuliwa na wafugaji wa kimasai alipokuwa akimsaidia jirani yake kufukuza Ng'ombe wasiharibu mazao shambani kwake, Kipande cha mti kinachoonekana hapo mdomoni ndiyo mkuki uliokatwa ili kupunguza urefu wa mkuki huo wakati wakimkimbiza hospitali,  Inasemekana MwenyeKiti wa kijiji na MwenyeKiti wa kitongoji hicho nao wamejeruhiwa.

WITO KWA SERIKALI.
Ofisi Ya Mbunge Mikumi inatoa wito kwa Serikali  kuwabaini wale wote waliofanya kitendo hiki cha kinyama kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria  ili kuweza kukomesha vitendo hivi vya kujichukulia sheria mkononi inayopelekea kuongezeka kwa uvunjifu mkubwa wa Amani na migogoro isiyokwisha kati ya wakulima na wafugaji wilayani KILOSA.

Imetolewa na:-
Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Mikumi.

SAKATA la Mwandishi Halfani Lihundi , Mkuu wa Mkoa wa Arusha Aingilia Kati

$
0
0
Sakata la mwandishi wa habari wa ITV Halfan Lihundi kukamatwa na kuwekwa mahabusu kwa saa 24 kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Arumeru baada ya kuandika habari ambayo haikumfurahisha mkuu huyo, limechukua sura mpya baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuingilia kati na kusema waandishi wa habari wanao uhuru wa kuandika habari mahali popote katika mkoa huo ili mradi wazingatie weledi katika taaluma.

Gambo ambaye wakati sakata hilo linatokea alikuwa safarini analazimika kukutana na wanahabari wote wa jiji la Arusha baada ya tukio hilo lililogoga vichwa vya waandishi mkoa wa huo na kusababisha kusimamisha shughuli zao ikiwemo kuweka kalamu chini kumnusuru mwenzao lakini pia wadau mbalimbali tasnia ya habari kukerwa na kitendo hicho.

Gambo amesema anatambua umuhimu wa kazi za waandishi wa habari na kuongeza kuwa kabla ya kiongozi huyo hajafanya maamuzi hayo pamoja na mamlaka aliyonayo busara ilitakiwa itumike.

Claud Gwandu ni mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa arusha na baadhi ya waandishi arusha anapaza sauti zao kuonyesha hisia zao juu ya sakata hili.

Lakini busara ya Gambo inatuliza munkari ya waandishi hawa na kumaliza mzozo huo ambao ulionekana kwenda mbali zaidi.

Na je nini kauli ya mkuu huyo kuhusiana na usalama wa waandishi hawa wakiwa katika kutekeleza majukumu yao?

Akiwa mkoani arusha katika majumuisho ya ziara yake mwishoni mwa wiki iliyopita waziri mkuu aliwapongeza waandishi wa habari kwa kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya kwani huamsha au hutoa mrejesho wa mambo muhimu ambayo huwasaidia viongozi kufanya maamuzi sahihi.

ZARI Afunguka :Hakuna Kitu Ninachokipenda Katika Maisha yangu Kama Kuzaa....

$
0
0
Wakati mabinti wengine wakijikita katika matumizi ya mikorogo na kukimbilia wanaume wenye pesa hali ni tofauti kwa mwanamama zari hassan (the boss lady ) ambaye amekiri wazi kuwa kitu anachopenda zaidi katika maisha yake ni kuzaa.

Zari ambaye ni mpenzi wa mwanamziki nyota Africa diamond platnumz amesema hayo ikiwa ni siku chache tangu apate mtoto wa kiume aliyezaa na diamond ambaye watu walimbeza kuwa anazaa bila mpangilio eti kiza tu alibeba ujauzito kabla ya mtoto wao wa kwanza tiffah hajatimiza mwaka mmoja.

Licha ya zari kuwa na watoto watano kwa sasa ameweka wazi kuwa kwa sasa yeye na diamond wana mpango wa kuzaa mtoto mwingine wa tatu na baada ya hapo hatozaa tena na badala yake watajikita zaidi katika kuwalea watoto wao.

MZEE wa Upako Afukuza Waandishi

$
0
0
MMCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi (GRC) la Ubungo jijini Dar es Salaam, Anthony Lusekelo maarufu 'Mzee wa Upako, aliwagomea waandishi wa habari kusikiliza hotuba yake ya ibada na kutuma wasaidizi wake wawaondoe waandishi hao.

“Samahani tunaomba muondoke kwani Mchungaji amesema hataki kumuona mwandishi hivyo tunaomba muende kwenye makanisa mengine,” alisema msaidizi huyo na kuhakikisha waandishi wote wanaondoka eneo hilo majira ya saa sita kasoro mchana.

Lusekelo maarufu Mzee wa Upako hivi karibuni amekuwa akirushiana maneno na baadhi ya waandishi wa habari baada ya kuandikwa akituhumiwa kuwa mlevi na kutukana hadharani.

Desemba 25 ya kila mwaka, waumini wa dini ya Kikristo nchini huungana na wenzao duniani kuadhimisha sherehe za kuzaliwa kwa Bwana wao Yesu Kristo yapata miaka 2000 iliyopita.

Wakati huohuo waumini wa dini ya Kikristo nchini wametakiwa kudumisha upendo, utii na unyenyekevu ili kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bwana na Mwokozi wao Yesu Kristo ikiwa ni pamoja na kuliombea amani taifa lao la Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ibada ya mkesha wa sikukuu hiyo, Dk Alex Malasusa, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani, aliwataka waumini wa kanisa hilo, kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa amani na upendo kwa wenzao.

Alisema siku ya Krismasi ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwana wa Mungu Yesu Kristo ambaye kutokana na upendo wake, aliwaunganisha watu na Mwenyezi Mungu.

“Tuuenzi upendo wake, lakini kubwa zaidi tukumbuke kuwa amani ndio msingi wa sikukuu hii. Hata alipokuja Yesu maneno yake ya kwanza yalikuwa ni amani,” alisisitiza. Askofu Malasusa, aliwataka wananchi katika kudumisha upendo huo, waliombee taifa pamoja na viongozi wake ili amani iliyopo iendelee kudumu.

“Ndio maana leo katika ibada yetu ya mkesha wa Krismasi tumeamua kupeana zawadi ikiwa ni ishara ya kuoneshana upendo na kudumisha amani miongoni mwetu,” alisema.

Mara baada ya ibada hiyo, waumini wa kanisa hilo, walibadilishana zawadi ambayo kila mtu alikuja nayo na kumpatia mwenzake huku Askofu Malasusa na viongozi wengine wa Kanisa hilo nao wakigawa zawadi zao kwa waumini hao.

UVUMI Juu Ya Noti Ya Shilingi 500

$
0
0
Benki kuu ya Tanzania inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa,habari inayoenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi mia tano  haitatumika tena kuanzia Desemba 31,2016; sio taarifa ya kweli na ni uvumi unaopaswa kupuuzwa.
Ukweli ni kwamba noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa wananchi. Tafadhali mpuuze taarifa hizo sio za ukweli.

Marcian Kobello.
Mkurugenzi wa Huduma za kibenki- BOT

VIDEO:Chid Benz Arudia Madawa ya Kulevya, Babu Tale Aapa Kutomsaidia Tena!

$
0
0
Chid Benz amerudia tena madawa ya kulevya na yupo kwenye hali mbaya
Mwana Fa alimuomba Babu Tale wamsaidie msanii huyo hivi karibuni lakini Babu Tale akasema hatomsaidia tena kwa kuwa Chid Benz ni kama sikio la kufa, halisikii dawa
Watu kadhaa walitabiria Chid Benz kurudia kutumia madawa kutokana na msanii huyo kukosa nidhamu na utabiri wao umetimia

SOMA Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo Katika Magazeti

KOCHA wa Mbwana Samatta Afungashiwa Virago Genk....

$
0
0

Boxing day yako imekujaje leo? basi kwa kocha Peter Maes imekua mbaya kwasababu kibarua chake kimeota nyasi kwenye club ya KRC Genk leo.

Habari kutoka kwenye tovuti maalum ya club ya KRC Genk imetoa taarifa kuhusu kumaliza ushirikiano na kocha huyu baada ya kuanza kuifundisha club hii tangu msimu wa 2015/2016.

Kocha huyu alianza majukumu ya kuifundisha club ya Genk mwaka 2015 hivyo basi ndiye kocha wa kwanza kumpokea Mbwana Samatta kwenye soka la Ulaya.

Genk wamemtakia maisha mema kwenye majukumu yake mengine na maisha baada ya Genk.

TAZAMA Picha za MKULIMA Aliyechomwa Mkuki Mdomoni na Kutokezea Shingoni

$
0
0
MKULIMA na mkazi wa kijiji cha Dodoma Isanga kata ya Masanze wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, Augustino Mtitu,amechomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni.

Umemjeruhi hivyo kulazimika kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, kufanyiwa upasuaji kuondoa mkuki huo na kuokoa maisha yake.

Mtitu na wengine wanane walijeruhiwa katika vurugu zilizohusisha jamii ya wafugaji wa Kimasai na wakulima wa kijiji hicho kilichopo wilayani Kilosa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. Alisema mpaka jana watu watatu walikuwa wanashikiliwa na Polisi, na msako unaendelea kuwasaka wale wote waliohusika katika kufanya vurugu hizo.

Tukio hilo ni la Desemba 25, mwaka huu, baada ya mtu huyo kujaribu kuzuia vurugu hizo, zilizokuwa zimetokea baada ya wafugaji hao kulisha mifugo yao katika shamba la maharage na mahindi katika kijiji hicho.

Mtitu akijaribu kuzuia vurugu hizo, aliishia kuchomwa mkuki na mmoja wa wafugaji wa jamii hiyo, ambao baada ya tukio hilo walikimbia kutoka eneo hilo.

Kutokana na tukio hilo, wananchi wenzake waliamua kumkimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya matibabu.

Lakini, alihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji na matibabu zaidi ya kuokoa maisha yake.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, muda mfupi baadaye wafugaji hao walirudi tena kijijini hapo, kwa lengo la kuokoa mifugo yao iliyokuwa imekamatwa, na ndipo walipoanzisha tena vurugu kwa kuwashambulia watu wengi wanane akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji pamoja na wa Kitongoji.

Watu watano, kati ya waliojeruhiwa, walikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kupatiwa matibabu. Diwani wa Kata ya Masanze, Bakari Pilo, akizungumza kwa njia ya simu, alisema hilo ni tukio la tatu kutokea kwenye kata yake katika kipindi kifupi.

Alisema vitendo hivyo vinaendelea kuhatarisha usalama wa wananchi, hasa wakulima, kufuatia mamlaka zinazohusika kushindwa kuwahamishia wafugaji katika eneo walilokuwa wametengewa, licha ya suala hilo kupitishwa kwenye vikao vya Baraza la Madiwani.

Stanley Andrea, ambaye ni ndugu wa Mtitu, yupo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro akimuunguza nduguye, alisema kuwa tukio hilo ni la Desemba 25, mwaka huu majira ya saa 5 asubuhi kwenye mashamba ya wakulima baada ya wafugaji kuingiza mifugo kwenye mashamba ya mahindi na maharage ili kulisha mifugo.

Alisema, wakulima wenye mashamba hayo,waliamua kuifukuza mifugo hiyo, lakini wafugaji wa jamii ya Kimasai, waliingilia kati na kuanza kuwapiga kwa fimbo wakulima na kusababisha kutokea kwa vurugu baina ya pande mbili hizo.

Alisema, mfugaji mmoja wa Kimasai alichukua mkuki na kumchoma Mtitu sehemu ya mdomoni na kutokezea shingoni na kuwajeruhi wengine wanane, akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji na wa Kitongoji, ambao baadhi wamelazwa Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.

Alisema kuwa vurugu ziliongezeka, pale wafugaji hao waliporudi kijijini hapo kwa ajili ya kuikomboa mifugo yao iliyokuwa inashikiliwa, kabla ya kufika kwa askari polisi kutoka mjini Kilosa.

Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Sanifa Mdee, alisema walimpokea mgonjwa huyo akiwa na mkuki mdomoni, ulitokea upande wa shingoni na kuanza kumpatia matibabu na kumtoa mkuki huo, ambapo amelazwa wodi namba moja hospitalini hapo.

Hata hivyo, alisema kutokana na mkuki huo kuchomwa kwa nguvu, ulijeruhi baadhi ya meno yake na kuharibu fizi, hali iliyosababisha jana madaktari kumfanyia upasuaji wa kurekebisha fizi zake, ambapo baada ya kutolewa mkuki huo, hali yake ilikuwa inaendelea vizuri.

Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images