Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104771 articles
Browse latest View live

POLISI Wapigwa Marufuku Kuvisha Mabango Madereva Walevi

$
0
0
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema wamesitisha kuwatangaza watuhumiwa katika mitandao ya kijamii  baada ya kupata malalamiko ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Hata hivyo, amesema hadi wanasitisha walikuwa wamewakamata  madereva 20 wa Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuonyesha jamii ili wengine wenye tabia hiyo wajifunze kupitia kwa wenzao na kuacha kuendesha wakiwa wamelewa.

“Kwa sababu watu wengi wapo mtandaoni ilikuwa rahisi ujumbe kuwafikia kwa wakati mmoja. Tulipata malalamiko ya haki za binadamu kuwa kufanya hivyo kunawasababishia kudhalilika katika familia zao, tukaona tusitishe,” amesema Mpinga.

Hata hivyo, amesema pamoja na kusitisha utaratibu huo, madereva wasijisahau kwa sababu vijana wapo kazini na wanaendelea kuwakamata wale wote watakaokiuka sheria za barabarani, ikiwamo hiyo ya kuendesha wakiwa wamelewa.

Awali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imelitaka Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, kuacha kuziweka hadharani picha za madereva wanaotuhumiwa kukiuka sheria, badala yake liwafikishe mahakamani kwanza.

Kauli ya Tume hiyo imetokana na utaratibu ulioanzishwa na trafiki wa kuwavisha mabango madereva wanaotuhumiwa kukiuka sheria ambayo yameandikwa makosa yao na kurushwa kwenye mitandao ya kijamii kabla hawajafikishwa mahakamani.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bahame Nyanduga amesema hayo wakati akifafanua kuhusu kusitisha kuwaanika katika mitandao ya kijamii madereva wanaokamatwa na trafiki kwa makosa ya usalama barabarani ikiwamo ulevi

MWANAFUNZI Anusurika Kifo Baada ya Kukatwa Mapanga na Mwalimu

$
0
0

MWANAFUNZI Marco Limbe(14) aliyemaliza darasa la saba mwaka huu katika shule ya msingi Yitwimila iliyoko kata ya kiloleli wilaya ya Busega mkoani Simiyu amelazwa katika kituo cha afya Busega mara baada ya kuchalangwa mapanga kichwani na mdomoni na mwalimu wake.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akirejea nyumbani kwao akitokea katika malisho ya mifugo ndipo alipokaribia katika shamba la mwalimu Pendo Gabriel ndipo mwalimu huyo alimkamata kijana huyo na kuanza kumchalanga kwa panga na kupelekea kijana limbe kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 mara baada ya kufikishwa katika kituo cha afya Busega.

“Shuhuda wa tulio hilo aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Manoga anaeleza kuwa ilikuwa kama mchezo lakini kumbe ni kweli kwani niliona mifugo ya limbe iliyokuwa ikielekea nyumbani na huku limbe akiwa nyuma ya mifugo hiyo katika barabara ambalo liko karibu na maeneo ya shule ghafla nilimuona mwalimu pendo wakishikana na kijana huyo na ndipo nikamuona akiwa na panga na kuanza kumchalanga”

Nilikimbia katika tukio na kutoa msaada kwa wote lakini mara watu walijaa na kuanza kumshambua mwalimu Pendo kwa kumpiga ingawa jaribio hilo lilikwama mara baada ya mwenyekiti wa kijiji hicho mshemas bahai.

Mwandishi alikwenda katika kituo cha afya cha Nyashimo na kujionea hali mbaya kwa kijana Limbe ambaye alikuwa amepoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 bila kujitambua na huku akiwa anaongezewa drip na kwa pembeni mwalimu Gabriel naye akipata matibabu ya jeraha lake kichwani amabolo alishambuliwa na wananchi na huku akiwa chini ya ulinzi wa jeshi la piolisi.
Akithibitisha kutokea kwa tukio mwenyekiti wa Sogesca Bahai Mshemas alisema kuwa sikukuu ya kuzaliwa kwa yesu imekuwa ni mbaya katika kijiji chake mara baada ya wananchi walio na hasira kali kufanya shambulio la kumshambulia mwalimu Pendo kwa kosa la kumchalanga na panga mwanafunzi wake aliyekuwa akitokea kwenye malisho na kupita karibu na shamba lake la mahindi.
Aliongeza kuwa alifanikiwa kuwatuliza wananchi wa kijiji chake na kuanza kufanya mikakati ya kuwapeleka kituo cha afya ili wapate huduma za matibabu.

Aidha Mshemasi aliongeza kuwa walifika polisi na kuandikiwa barua ya kwenda kutibiwa wote wawili mwalimu pamoja na mwanafunzi.
Kwa upande wake kaimu mganga mfawidhi wa kituo hicho cha afya Dk Ayubu Ismail alithibitisha kuwapokea kwa majeruhi hao na kudai kuwa kijana limbe ndiye aliyekuwa na hali mbaya zaidi kuliko mwalimu pendo.

Aliongeza kuwa kijana ameshonwa nyuzi 9 katika sehemu zake zote alizopatwa na majeraha na huku mwalimu yeye akiwa ameshonwa nyuzi 6.
“Ni kweli Limbe alikuwa ametokwa na damu nyingi sana na hivyo kumpelekea kupoteza fahamu kwa muda wa masaa 6 lakini hali yake inaendelea vizuri alisema Dk Ismail”
Chanzo: Rweyunga

MOTO Wateketeza Nyumba 50 Wamiliki Wake Wakila Krismasi

$
0
0

MOTO mkubwa umezuka na kuteketeza nyumba zaidi ya 50 katika kisiwa cha Kasalazi kilichopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa mkoani Mwanza.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 3:00 usiku, linadaiwa kuwa ni la nne kutokea kisiwani humo katika miaka ya karibuni.

Imeelezwa kuwa moto huo ulizuka na kuteketeza nyumba hizo huku wamiliki wake wakiwa kwenye shamra shamra za Krismasi.

Nyumba zilizoteketea kwa moto ni zile zilizojengwa kwa kutumia mabanzi ya miti, mbao na kuezekwa kwa maturubai, nyasi na baadhi kwa bati.Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kasalazi, Andrew Mkama, amesema  kuwa wakati tukio hilo linatokea, wakazi wengi wa kisiwa hicho walikuwa kwenye kumbi mbalimbali za starehe kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.

Mkama alisema alilazimika kupuliza filimbi kuashiria hatari na wananchi walijitokeza na kuanza jitihada za kuuzima moto huo licha ya kwamba tayari ulikuwa umeshasababisha madhara makubwa kwa kuunguza mali zote zilizokuwa ndani yake.

Hata hivyo alisema hakuna mtu aliyekufa wala kujeruhiwa kutokana na janga hilo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walisema moto huo umesababisha hasara kubwa kwao.

Mmoja wa mashuhuda hao, Raphael Bituro, anayemiliki duka la vinywaji, alisema baada ya kupulizwa filimbi kuashiria hali ya hatari, baadhi ya wateja wake walikurupuka bila kulipia vinywaji vyao na hivyo kusababisha apate hasara.

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole, alithibitisha kisiwa hicho kuungua kwa moto.

Kipole alisema ameagiza kufanyika kwa uchunguzi ili kubaini ukubwa wa madhara hayo na kuahidi kutoa taarifa zaidi atakapopewa ripoti hiyo.

Kisiwa hicho kinakadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya 2,400 ambao hujihusisha na shughuli za uvuvi na ni miongoni mwa visiwa vinane vilivyopo kwenye Kata ya Bulyaheke wilayani Sengerema.

MKULIMA Aliyechomwa Mkuki na Wafugaji Apata Nafuu Baada ya Mkuki Kutolewa

$
0
0
Maendeleo Ya Ndugu AUGUSTINO MTITU aliyejeruhiwa kwa kuchomwa na mkuki jana tarehe 25/12/2016 Kijiji cha Dodoma Isanga Kata Ya Masanze Jimbo La Mikumi na jamii ya wafugaji, hivi sasa anaendelea vizuri na matibabu baada ya kutolewa mkuki mdomoni salama salimini kwenye HOSPITALI YA MKOA MOROGORO na amelazwa wodi namba moja hospitalini hapo.

Ofisi Ya Mbunge Jimbo La Mikumi inatoa shukrani zake za dhati kwa Madaktari na wauguzi waliofanikisha zoezi hilo, Lakini pia Ofisi Ya Mbunge Mikumi itakuwa ikiwapa maendeleo ya Bwana AUGUSTINO MTITU mpaka hapo hali yake itakapokua imetengemaa.

Lakini la muhimu zaidi Mh. Mbunge amefanya mawasiliano na ngazi mbalimbali zinazohusika akiwemo Waziri wa Mambo Ya ndani Mh. Mwigulu Nchemba juu ya kile kilichotokea na waziri amesikitika sana na ameahidi kulifuatilia suala hili kwa kina na kulitolea maamuzi magumu.

Imetolewa na :- Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Jimbo La Mikumi

CHID BENZI Anastahili Kuombewa..Siwezi Muhukumu-Solo Thang

$
0
0
Msanii mkongwe wa muziki wa hip hop, Solo Thang ameposti video akiwa na rapa Chidi Benz ambaye walikutana usiku na kuongea baadhi ya mambo, lakini kutokana na hali aliyokuwa nayo Chidi Benz Solo Thang alisema hawezi kumuhukumu bali anastahili kuombewa tu.

Katika ujumbe ambao Solo Thang aliandika kwenye mtandao wake wa Instgram alisema hawezi kuhukumu na hata iweje bado Chidi Benz ataendelea kuwa mdogo wake, rafiki yake na mtu wake wa karibu.

“Met with my Young brother Chid Benz last night almost cried, I dont judge, no matter what still my hommie, tumeongea sana, tuzidi kumuombea Mola” aliandika Solo Thang

FARU John Wajanja Walishamnywa Kitambo, Pembe zilizoonyeshwa ni za Faru "Hadija"

$
0
0
Gazeti la Jamhuri limeripoti kuwa FARU John Wajanja Walishamnywa Kitambo, Pembe zilizoonyeshwa ni za Faru "Hadija"


MAJANGA:Nimeamka Asubuhi Nipo na Mama Mkwe Kitandani...Nifanyeje?

$
0
0
Heka heka la jana si mchezo kabisa, nilikata moto kama ngoma sita ilikuwa Bar moja nilienda na familia kupata burudani ya mziki live Band, sasa wife hakukaa sana na ilivyofika saa tano akasepa na watoto akaniacha na mdogo wake wa kike na mama mke ambaye ni mama mkwe.

Nikiri tu huyu mama ni mmama wa kimjini mjini na pombe nyama kwa sana tukiwa watatu pale mimi, mama mkwe na mdogo wake wife mida si mida mziki umekolea mdogo wake wife akaniamsha tukaelekea kwa Dance floor huku mama mkwe akiendelea kupiga vyombo.

Tumecheza muda si muda mama mkwe akamuita mwanae wakaongea then akasepa, Daah kuanzia hapo vitimbi vya mkwe wangu vikaanza akaniambia tuhame bar eti twende Hotel ambayo ina burudani na vyumba ikitokea mtu kazidiwa anaenda pindua, nikamuuliza Rachel yuko wapi mdogo wake sasa na wife akaniambia kuna mtu wake kamuita nikaona isiwe case japo nilianza kulalama nani ataendesha gari kuelekea huko anakotaka ile hali wote tuko chakari, akasema ni drive tu pole pole basi bana tumeelekea huko.

Ile tunapiga urabu wife kaanza kusunbua kupiga simu ikabidi mama ake ambae ni mkwe wangu apokee simu na kumtoa hofu bado wife akasisitiza muda umeenda na turudi, wakuu pombe zilinizidi na yule mama mkwe akanikokota mpaka chumbani wazee pombe kali si mchezo, nilisimamia show usiku sasa ndio nashituka usingizini na mama mkwe bado amelala pembeni hapa nimechukua simu missed calls 30 za wife.

Wakuu niko njia panda baada nifanyeje kuua msala huu, Najuta kuja ukweni huku, swala hili nitalisolve vipi ndugu zangu?

By Mwana Ukoo/JF

JINSI Punyeto Inavyoathiri Nguvu za Kiume

$
0
0
Kupiga punyeto kwa muda mrefu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya tatizo la la ukosefu wa nguvu za kiume. Asilimia kubwa ya vijana wenye tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume, linasababishwa na upigaji wa punyeto kwa muda mrefu.

JINSI PUNYETO INAVYO SABABISHA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.

Unapopiga punyeto unakuwa unaiminya mishipa ya uume ambayo ndio inaufanya uume usimame. Matokeo yake unaifanya mishipa hiyo ilegee na kutokuwa na uwezo wa kusimama tena. Mishipa ya uume iliyo legea kutokana na upigaji punyeto, huleta madhara yafuatayo :
Huondoa uwezo wa mishipa ya uume kurelax. (Unapopata wazo la kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume ina relax , mishipa iki relax husababisha mishipa ya ateri kupanuka na kuruhusu damu kuingie ndani ya mishipa ya uume na hatimaye kuufanya uume usimame na kuwa mgumu)
Mishipa ya kiume ikishindwa ku relax husababisha mishipa ya ateri kuziba
Mishipa ya ateri ikiziba, damu haiwezi kutiririka kuingia kwenye mishipa ya uume, na hata ikitokea damu imeingia ndani ya mishipa ya uume basi huingia kiasi kidogo sana tena kwa presha ndogo sana hivyo basi hata kama uume utasimama basi utasimama ukiwa legelege sana
Mishipa ya uume ikishindwa kurelax basi haitakuwa na uwezo wa kuipush na kuiziba mishipa ya vena ambayo ndio hunyonya damu kutoka kwenye mishipa ya uume ulio simama. Matokeo yake basi, damu kidogo iliyo ingia ndani ya mishipa ya uume na kuufanya uume kusimama, hunyonywa na kutolewa nje ya mishipa ya uume ndani ya sekunde chache sana na hivyo kuufanya uume usinyae ndani ya muda mfupi sana.
Mishipaya uume kulegea
Uume kurudi ndani na kusinyaa na kuwa kama uume wa mtoto.

Tatizo la unene kupita kiasi : Tatizo la unene na uzito kupita kiasi ni miongoni mwa mambo yanayo sababisha upungufu wa nguvu za kiume. Unene kupita kiasi humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na magonjwa kama vile kisukari, presha, moyo na shinikizo kuu la damu. Na magonjwa ya kisukari, moyo,presha na shinikizo la damu husababisha upungufu na ukosefu wa nguvu za kiume, na hivyo kumuweka muhusika katika hatari kuu ya kupatwa na tatizo la ukosefu/upungufu wa nguvu za kiume.
Hivyo basi kwa wewe mwenye tatizo la unene na uzito kupita kiasi , pamoja na kutumia tiba ya nguvu za kiume, ni vyema ukafanya na mpango wa kupunguza unene na uzito wako.
Matatizo Katika mfumo wa Ubongo
Uume hauwezi kusimama bila ya kuwa na ushirikiano na ubongo. Ili mtu uume uweze kusimama, mtu lazima apate wazo la kufanya tendo la ndoa (UBONGO UNA HUSIKA HAPO ), akishapata wazo, ubungo hupeleka ishara kwenye mishipa ya fahamu iliyopo katika uti wa mgongo ambayo nayo hupeleka taarifa kwenye mishipa ya uume then uume usimama. Hivyo basi ili mtu aweze kuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake ni lazima kuwa na mawasiliano mazuri na imara kati ya mishipa ya fahamu (ubongo), mishipa ya kwenye uti wa mgongo na mishipa ya kwenye uume. Bila ushirikiano kati ya vitu hivyo vitatu, uume hauwezi kusimama.

Magonjwa yanayoweza kuathiri ushirikiano kati ya mishipa ya ubongo na mishipa ya uume, yanaweza kusababisha kushindwa kusimama kwa uume.
Magonjwa hayo ni pamoja na kiharusi,kupoteza kumbukumbu (Alzheimer), multiple sclerosis pamoja na ugonjwa wa Parkinson.

Ni vyema mgonjwa akatibiwa kwanza magonjwa hayo kabla ya kuanza kutumia dawa ya nguvu za kiume.
Mambo mengine yanayo sababisha ukosefu na upungufu wa nguvu za kiume, ni pamoja na maumivu & majeraha kwenye uti wa mgongo, chango la kiume , ngiri na matatizo katika homoni.

VIASHRIA VYA MTU MWENYE TATIZO LA UKOSEFU/UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume huwa na dalili zifuatazo ;
Kushindwa kabisa kusimamisha uume wake
Uume kusimama ukiwa legelege
Kuwahi kumaliza tendo la ndoa
Mwanaume kutokuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa katika baadhi ya staili (Mara nyingi mwanaume huyu huwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa staili moja tu). Hapa mwanaume anakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa staili ya “ missionary” pekee. Ikibadilishwa staili, mwanaume anakuwa hana tena uwezo wa kusimamisha uume wake japo katika hali ya u lege lege
Uumekuto kuwa na uwezo wa kusimama wenyewe bila kushikwashikwa ama kutomaswa kwa muda mrefu.

Uume kusinyaa ukiwa ndani ya mwanamke.
Uume kusinyaa, pindi inapotokea activity yoyote ya kiungo ama ogani nyingine ya mwanaume wakati wa tendo la ndoa. Kwa mfano, wakati wa tendo la ndoa, ikitokea mwanaume amekohoa au kupiga chafya, uume nao unasinyaa.
Uume kusinyaa mara tu baada ya kutolewa ndani ya uke (Kwa mfano kama unafanya tendo la ndoa, halafu uume ukatoka nje, kitendo cha kuushika kuurudisha ndani, tayari unasinyaa)
Kutokuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa.
Kupatwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

VIASHIRIA VYA MWANAUME ASIYE NA TATIZO LA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.
Mwanaume asiye na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume, huonyesha ishara zifuatazo ;
Uume husimama ukiwa imara kama msumari.
Hukaa kifuani kwa muda mrefu (Wastani ni kati ya dakika 20 hadi 45)
Huweza kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila misuli ya uume kuchoka.
Huweza kufanya tendo la ndoa kwa staili yoyote ile.
Uume husimama wenyewe bila kushikwa shikwa wala kuwa stimulated kwa namna yoyote ile
Kwa ufupi anakuwa na uwezo wa kufanya na kukamilisha tendo la ndoa kwa uukamilifu mkubwa.
Source: Ruwehy blog

EDWARD Lowassa: CCM Isijidanganye

$
0
0
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ameitaka CCM iache kujidanganya kuwa haiwezi kuondoka madarakani akiitaka iangalie alama za nyakati hasa mabadiliko ya uongozi yanayotokea kwingineko duniani.

Hata hivyo, Lowassa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA amesema unahitajika muungano wa dhati wa vyama na uliopangiliwa vizuri katika juhudi za kuiondoa CCM madarakani.

Lowassa alisema hayo alipoombwa na mwandishi wa habari hizi kutoa tathmini ya maisha yake ya kisiasa mwaka mmoja na nusu tangu alipojiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA ambako aliteuliwa kuwa mgombea urais wa chama hicho akiwakilisha muungano wa vyama vinne – CHADEMA, CUF, NCCR - Mageuzi na NLD – Iliopewa jina la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

MADEE Awashukia Wanaompiga Picha Chid Benz na Kuposti Mitandaoni

$
0
0

Hii ni kwa ajili ya Mastaa wanaopiga video na picha na Chid Benz ambae anasubuliwa na matumizi ya madawa ya kulivya

ZITTO Kabwe na Make Wake Wapata Mtoto wa Kike

$
0
0

Ameandika ''Mimi na Mke wangu mpendwa tumebarikiwa na Allah kupata mtoto wa kike. Mtoto na mama yake wana afya njema kabisa, Mashaallah. Mtoto amezaliwa saa moja na dakika 45 asubuhi leo Disemba 27, 2016''''.

''Binti yetu ataitwa Josina - Umm Kulthum. Josina kwa heshima ya mwanamama mpigania Uhuru wa Kusini mwa Afrika, Josina Muthembi Machel wa FRELIMO. Umm Kulthum kwa heshima ya mama yangu mdogo na pia jina la binti wa Mtume Muhammad (SAW)''

''Tunamshukuru mungu kwa Baraka hizi za mtoto Josina - Umm Kulthum Zitto'' Kabwe Z. Ruyagwa Zitto

AY Amtambulisha Mchumba Wake...Ndoa Hivi Karibuni

$
0
0

Mwanamuziki Ay kwa Mara ya kwanza amemtambulisha rasmi Mpenzi wake....
Habari hii Leo imekuwa gumzo mitandaoni kwa wengi walikuwa wakijiuliza Ay mpenzi wake ni nani hasa baada ya Swahiba wake wa Karibu Mwana FA Kuoa....

WALIOFAULU Usaili wa Kazi Serikalini Watakiwa Kuomba Ajira Upya

$
0
0

Waliofanya usahili serikalini, wakafaulu lakini kabla ya kupangiwa vituo vya kazi ajira zikasitishwa; watakiwa kuomba ajira upya.

Taarifa ya Sekretarieti ya Utumishi wa Umma imesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida wa sekretarieti hiyo.

Aidha majina ya waliofaulu huhifadhiwa kwenye kanzi data (Database) kwa muda usiozidi miezi sita, na baada ya hapo majina hayo hufutwa.

ZITTO Kabwe Asimulia Alichokutana Nacho Hospitalini Mkewe Akijifungua

$
0
0
Usiku wa kuamkia tarehe 26 Desemba 2016 mke wangu alipata uchungu wa uzazi. Nikampeleka hospitali moja hapa Masaki. Hakuweza kujifungua siku hiyo bali tulikaa hospitali mpaka tarehe 27 Desemba, saa moja dk 45 asubuhi alipojifungua mtoto wetu wa kike Josina- Umm Kulthum.

Masaa ya jioni tarehe 26/12/2016 nikiwa napiga soga na Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Msafiri Mtemelwa na shemeji yangu mmoja mbele ya hospitali, wakaja watu 3. Watu hao mmoja mwanaume na wengine wanawake walikuwa na mtoto mdogo. Mwanaume huyu alikuwa amembeba mtoto akiwa na taharuki kubwa na mama mmoja mtu mzima na mwengine wa umri wa miaka 30 hivi walikuwa wakilia. Wakaingia hospitalini kwa kasi. Tukaambiana pale kuwa huyu binti atakuwa mahututi. Tukaendelea na soga. Mara kina mama wale wakatoka, wanapiga mayowe "mtoto hana damu" na ilitakiwa damu ya haraka Group A+.

Wenzangu hawakuwa group hilo au group linaloweza kupeana damu. Mimi sikuwa najua/kukumbuka Group langu. Nikawaambia kina mama wale kuwa ngoja nijaribu kupima group langu na pia kuona kama damu yangu inaweza kuokoa maisha ya mtoto yule malaika za mungu. Nikaingia maabara nikapima. Baada ya dakika 10 Hivi nikaitwa kuambiwa damu yangu ni group sawa na mtoto yule na kwamba ni safi inafaa wanitoe muda ule ule ili kumuwahi mtoto. Nikatoa nusu lita muda ule ule. Baadaye nikaenda kumjulia Hali mtoto yule, nikaambiwa anaitwa Rahma. Ana umri wa miaka 2 na miezi 3. Nikawatakia kheri wazazi wake ( kumbe yule mwanaume ndie baba wa mtoto na msichana mama yake. Yule bi mkubwa nadhani ni bibi ya Rahma, sina hakika).

Leo asubuhi, 27 Desemba 2016 baada ya mke wangu kujifungua, nikaenda kumwona Rahma wodini. Nimemkuta anaendelea vizuri, anakula na kuongea. Mola ampe umri mrefu zaidi yeye na wazazi wake. Amwondolee maradhi na akue katika maadili mema ya dini. Namshukuru mola kuniweka mahala sahihi na wakati sahihi hivyo kuweza kufanya ibada hii ya kumsaidia binti Rahma. Lau kama sikuwa nimechagua jina la binti yangu mapema, ningemwita Rahma. Hata hivyo inshallah Rahma atakuwa dada yake Umm Kulthum-Josina. Naishauri Serikali itengeneze kanuni za kuhakikisha kila hospitali inakuwa na akiba ya damu ya kutosha na mgonjwa mwenye kuhitaji apewe kwanza damu kabla ya kutafuta watu wa kuchangia kiwango husika.

Juhudi za kuchangia damu kwa hiari ziongezeke kama tufanyavyo wanachama wa ACT Wazalendo ambao kila mwaka Wiki ya kwanza ya Mwezi Mei hujitolea damu kwa hiari kwenye hospitali za umma nchini kote. Pia nimepata somo kubwa kwamba ni muhimu Sana kujua Group lako la damu na kuwa na kumbukumbu nalo kwani inaokoa muda pindi damu ikitakiwa kwa haraka. Sasa najua Group langu, ilikuwa ni makosa makubwa na uzembe wa hali ya juu kwangu kutojua ' blood group ' yangu. Nawasihi Watanzania wenzangu na mie msiojua blood group, mjue sasa kwani hatujui Siku wala Saa.


*****Heri ya mwaka mpya 2017 *****

Zitto Kabwe

PICHA za Ray C Ndani ya Muonekano Mpya wa Kihindi

$
0
0

Huenda huu ukawa ndio ujio mpya wa msanii mkongwe wa muziki wa bongofleva Rehema Chalamika aka Ray C baada ya misukosuko ya hapa na pale katika maisha yake ya muziki.


Muimbaji huyo ambaye amedaiwa kuweza kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya baada ya kushindwa kwa muda mrefu,wiki chache zilizopita aliweka kambi ndani ya studio ya Wanene kwa ajili ya maandalizi ya ujio wake mpya.


MAAJABU: Nyoka Afa na Mmiliki wake Songea

$
0
0
Mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) kufa baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi.

Komba alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo.

Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724 AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.

Akisimulia tukio hilo, alisema alipofika katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga gonga kwa nyuma, ndipo alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka mkubwa huku amesimamisha kichwa.

Haule alisema, baada ya kumuona nyoka huyo aliruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka pembeni mwa barabara na abiria wake alimwachia yule nyoka ambaye alikimbilia kwenye kalavati la maji.

Aliongeza kuwa ndipo alipopiga kelele za kuomba msaada na kundi la vijana waendesha pikipiki wenzake walifika eneo hilo la tukio kwa lengo la kumsaidia mwenzao juu ya maswahiba yaliyompata hadi kumfanya apige kelele.

Alisema kabla ya vijana hao hawajafanya jambo lolote, Komba aliwaomba vijana hao na watu wengine waliofika katika eneo hilo wasimpige nyoka wake kwani iwapo watampiga na kufa yeye pia atapoteza maisha. Kutokana na maneno hayo, Haule alimtoa nyoka huyo ndani ya kalavati na kwa kushirikiana na vijana wenzake walianza kumpiga nyoka huyo hadi kufa.

Alisema wakati wanampiga nyoka huyo, Komba ambaye ndiye mmiliki wa nyoka huyo naye alianza kulegea kisha akaanguka chini huku akitokwa na mapovu mdomoni na puani.

Habari zinasema kuwa,baada ya Komba kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu; hata hivyo juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali za kuokoa maisha yake zilishindikana kwani Komba alifariki.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa Songea.

Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma.

Aidha Kamanda Mwombeji, ametoa rai kwa wananchi kuacha mara moja kumiliki nyara za serikali zinazoweza kuwaletea madhara kama vile majeraha au vifo.

RIDHIWANIA Ainyoshea Kidole Serikali ya Magufuli. Asema Ajira Serikalini Bado zimesitishwa Hadi Sasa

$
0
0
RIDHIWANIA Ainyoshea Kidole Serikali ya Magufuli. Asema Ajira Serikalini Bado zimesitishwa Hadi Sasa

HOJA Sita za rufaa ya Mbunge Lema Kusikilizwa leo

$
0
0
Hoja sita za mawakili wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kupinga kunyimwa dhamana zinatarajiwa kusikilizwa leo mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Salma Maghimbi.

 Wakili Sheck Mfinanga anayemwakilisha Lema alisema waliwasilisha hoja hizo za rufaa kupinga uamuzi wa kunyimwa dhamana mteja wao.

 Lema aliyekamatwa Novemba 2, akiwa mjini Dodoma, tangu wakati huo anashikiliwa kwenye Gereza Kuu la Kisongo jijini Arusha ambako amekaa kwa siku 56.

 Baada ya kukamatwa na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Lema alipewa dhamana na Hakimu Mkazi Desdery Kamugisha katika kesi namba 440 na 441/2016 akidaiwa kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

 Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) alikata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama kumpa dhamana mbunge huyo.

Mawakali wa Lema nao walikata rufaa kupinga mteja wao kunyimwa dhamana ambayo imepangwa kusikilizwa leo baada ya kukwama kwa muda mrefu kutokana na kuwapo pingamizi za kisheria zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri.


FAHAMU Namna ya Kuishi na Mpenzi Anayependa Fedha...

$
0
0
HAPA tunazungumza kuhusu mapenzi kama kawaida yetu. Leo nimekuja na mada ambayo naamini itawagusa wengi. Marafiki zangu, kusaidia katika mapenzi ni jambo zuri tena lenye mantiki sana.
Suala la kusaidiana si la upande mmoja. Linaweza kuwa kwa wote, kwa mwanaume au mwanamke. Ni kati ya nguzo muhimu katika mapenzi, lakini kwa bahati mbaya kuna wale ambao
wamekuwa na tabia ya kupenda sana fedha!

Unajua wenzi wanajuana kulingana na wanavyoishi, hivyo ni rahisi sana kumgundua mwenzako kama anapenda sana fedha au ni kweli ana tatizo linalohitaji msaada wako. Hii ni kasoro, lakini haimaanishi kwamba ndiyo sababu ya kuachana.

Katika mada hii ipo dawa ya namna ya kudumu katika mapenzi motomoto na mwenzi wa aina hii. Imekuwa ni kawaida kumsikia msichana akitamba mbele ya wasichana wenzake kwa kusema: “Mimi nina kibuzi changu bwana kila ninachotaka kinanipa, kinajua kisiponipa nakitosa tu, yaani nakichuna kama sina akili nzuri.”

Umewahi kukutana na maneno ya aina hii? Bila shaka jibu ni ndiyo. Si hivyo tu, wapo wanaume pia ambao ni kero kwa wapenzi wao, yaani wamegeuka wanaume kama mabinti kwa tabia zao za kutegemea kupewa kila kitu na wapenzi wao hata kama wanao uwezo wa kuvipata vitu hivyo kama watajishughulisha.

Ninachotaka kusema leo ni kwamba, mapenzi ya kweli hayana uhusiano wowote na fedha, ukiona mpenzi wako anaweka fedha mbele na ukishindwa kumpatilizia anachokitaka anakasirika, jua penzi lake lina walakini, hakupendi bali anataka kukutumia kisha kukuacha.

Katika mapenzi hatukatai suala la kusaidiana, mpenzi wako akiwa na shida fulani akaomba umsaidie, kama unao uwezo msaidie na kama huna mueleze ukweli kisha muangalie namna nyingine ya kumsaidia.

Itakuwa siyo busara kama utakuwa na tatizo lakini ukaona kwamba ukimweleza mpenzi wako ataona unamchuna. Wapenzi wanaopendana kwa dhati hawachunani bali wanasaidiana na hili ni kwa pande zote mbili.

Kinachokera ni kutoishiwa na matatizo na wakati mwingine unakuta kuchuna kwingine ni kwa mambo ya starehe. Yaani sasa hivi umemuomba mpenzi wako vocha, hajakaa vizuri umemtaka akija akuletee chipsi mayai, baadaye unataka akutoe ‘out’, bila kujali kwamba wakati huo mpenzi wako ana fedha au laah.

Katika mazingira hayo unadhani mpenzi wako atashindwa kukuchoka? Akikuacha kwa sababu hiyo utamlaumu? Kimsingi ukiwa na mpenzi mwenye tabia ya kutaka kukuomba fedha kila wakati tena katika matumizi mengine ambayo siyo ya msingi, mbinu zifuatazo ni muhimu kuzifuata. Twende tukaone.

MWELEZE UKWELI
Kama huna fedha wakati mpenzi wako anakuomba, mueleze wazi kuwa huna na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa kuzitimiza. Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara nitakununulia hiki na kile.

Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana fedha au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea! Mwanamke akijua hilo naye ataongeza ‘mizinga’ ili afaidi.

JENGENI KUSAIDIANA
Jambo la muhimu ambalo wanaume wengi wanalisahau ni kutokuwafundisha wapenzi wao wajibu wa kutoa. Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya basi analipa, wakati mpenzi wake ana kazi yake.

Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna fedha zinavyokuwa hazitoshi na ataweza kubana matumizi.

ACHA UFUJALI
Kuna wanaume wengine tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa fedha kwa kutoa ofa na zawadi kibao. Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa unazo!

Unachotakiwa ni kudhibiti mapema matumizi yako hata kama fedha itakuwepo. Ifahamike kuwa kutoa hakushibishi uhitaji, kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji. Weka maisha yako katikati usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.

BAKI NA HILI
Katika kumalizia niseme tu kwamba, mapenzi si kukomoana, bali kusaidiana. Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku na wewe ukiwa na tatizo akusaidie.

Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kero. Kumbuka kumpiga mizinga mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi hivyo epukana na tabia hiyo.

MAPYA Yaibuka Mtoto Aliyefia Bwawani Hotelini

$
0
0

SAKATA la mtoto wa miaka 12 aliyekufa wakati akiogelea katika bwawa la hoteli ya kitalii ya Mount Meru mjini hapa, limechukua sura mpya baada ya kugundulika kuwa bwawa hilo lilijaa damu baada ya kifo chake.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha madai ya mashahidi waliokuwa eneo la tukio, waliodai kuwa bwawa la kuogelea la hoteli hiyo liligeuka kuwa dimbi la damu wakati mwili wa mtoto huyo ukiopolewa kutoka bwawa hilo, siku ya Krismasi.

“Inaaminika kuwa kichwa cha Clifford Alex kilipasukia ndani ya bwawa la kuogelea,” alisema, kamanda huyo wa Polisi wakati akitolea ufafanuzi kifo hicho kilichozua utata mjini hapa.

Kuna madai kwamba Clifford alijirusha kwenye dimbwi ili aogelee, lakini kichwa chake kilipiga kwenye ukingo wa bwawa hilo la kuogelea na hivyo kusababisha kifo chake, ingawa baadhi ya watu wanadhani kuwa alisukumwa. Uongozi wa hoteli ya Mount Meru pia haujatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo na kwa nini watoto waliruhusiwa kuogelea bila ya kuwa na msimamizi.

“Tunachunguza tukio hilo na ikiwa itabainika kuwa hoteli ilifanya uzembe basi tutaichukulia hatua,” alisema Kamanda Mkumbo.

Tukio hilo lilitokea katika siku ya Krismasi wakati mtoto huyo aliyekuwa anasoma darasa la tano katika shule ya Sekei ya mjini hapa, alipokwenda na wenzake kuogelea katika bwawa la hoteli hiyo mchana wa Jumapili.

Mama wa mtoto, Christina Michael, mkazi wa eneo la Idara ya Maji Sekei, anaeleza kuwa mwanawe huyo alitoka nyumbani majira ya mchana kwenda matembezini na wenzake, lakini ilipofika saa moja usiku, watoto wengine walirejea ila mwanawe hakuwepo.

“Nilipowauliza walisema kuwa Cliff ord amebaki kwenye maji kule Mount Meru, basi haraka nikaenda pale hotelini lakini wakaniambia kuwa ameshapelekwa Hospitali ya Arusha International Conference Center (AICC) Kijenge kwa matibabu,” alisema.

Hata hivyo, mama huyo alipofika hospitalini alikuta mwili wa mtoto huyo umefunikwa kwa shuka nyeupe na hapo hata yeye akaishiwa nguvu na kuanguka akijua Cliff ameshakufa.

Watoto wenzake walioandamana na Cliff kwenda kuogelea hotelini hapo, Kelvin Celestine na Passon Alex ambao wanasema kuwa walikuwa hawana pesa za kulipia hotelini, hapo hivyo wakamuomba mlinzi awaruhusu kuogelea bure. Mlinzi huyo aliwaruhusu kuogelea kwenye eneo maalumu la watoto.

Lakini inasemekana kuwa baadaye giza lilipoanza kuingia Cliff aliwaacha wenzake na kwenda kuogelea kwenye bwawa la wakubwa na huko ndiko mauti yalimkuta. Hata hivyo, haijulikani kama kweli alijipeleka mwenyewe au alishawishiwa kwenda kwenye bwawa hilo la wakubwa au hata kama kuna mtu asiyejulikana aliyemsukumia humo.

Babu wa marehemu, Emmanuel Magie amesema wanasuburi ripoti ya daktari kuhusu kifo cha Cliff na wameshangazwa kuona uongozi wa hoteli haukuwa na taratibu ya kuwawekewa waangalizi watoto wanaokwenda kuogelea.

Ripoti za kifo cha mwanafunzi huyo zilikuwa hazijawafikia polisi wakati tunakwenda mitamboni, lakini Mwenyekiti wa Mtaa wa Sekei, Alphayo Mollel anayesimamia eneo ambalo hoteli hiyo ilipo, anasema bado anawasiliana na uongozi waeleze kwa nini watoto waliruhusiwa kuogelea hadi usiku.
Viewing all 104771 articles
Browse latest View live




Latest Images